meya jerry slaa atekeleza ahadi alizozitoa jimbo la ukonga

2
MEYA JERRY SLAA ATEKELEZA AHADI ALIZOZITOA JIMBO LA UKONGA -Atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Ukonga MEYA wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya G Mboto, JerrySlaa ameainisha mafanikio aliyotekeleza katika kipini !ha miaka " tangia a!hag#liwe k#wa Diwani na Meya Manispaa ya Ilala ambapo pia alitimiza ahai mbalimbali alizok#wa ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala$ Slaa ali%ipatia msaaa wa feha %ik#ni %ya &I'()A ali%yok ame%iahii k#%isaiia,Genereta za k#toa nishati za k mirai kwa %ik#ni kwenye maeneo yasio na #meme,%if mi!hezo kwa %i*ana na hati za #thibitisho wa #*enzi wa bar zitakazo*engwa kwa maiwani wa kata za *imbo la +konga$ Slaa ambaye pia ni m*#mbe wa Kamati K## ya 'hama Mapin#zi alitangaza mafanikio hayo katika mk#tano wa hah #liofanyika katika sh#le ya msingi ya Kit#na iliyopo *imb +konga *ana ambapo pia alitangaza nia ya k#gombea #b#nge *imbo la +konga k#pitia 'hama !ha Mapin#zi katika Mk## #takaofanyika (ktoba mwaka h##$ )aahi ya mafanikio aliyofanikisha katika kipini !ha #on wake aliyabainisha k#wa ni katika sektaya elim# ambapo mazingira katika sh#le mbalimbali yameboreshwa,afya am %it#o %ipya %ime*engwa na %ingine k#patiwa %ifaa na awa ya ma*i na #*ezi wa barabara kwenye kata ya Gongo la Mboto kata zote za Manispaa ya Ilala$ - Kutokana na mafanikio yaliyopatikana nawaomba wanan wa jimbo la Ukonga mniunge mkono kwa kinichagua niwe Mbunge wenu katika uchaguzi mkuu ujao ili nizidi kuwatumi na kushirikiana nanyi kuleta maendeleo katika jimbo Ukonga ambalo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali za maendeleo.Alisema$

Upload: misty-collins

Post on 04-Nov-2015

3.624 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

Atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Ukonga

TRANSCRIPT

MEYA JERRY SLAA ATEKELEZA AHADI ALIZOZITOA JIMBO LA UKONGA-Atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la UkongaMEYA wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jerry Slaa ameainisha mafanikio aliyotekeleza katika kipindi cha miaka 5 tangia achaguliwe kuwa Diwani na Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo pia alitimiza ahadi mbalimbali alizokuwa ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala.Slaa alivipatia msaada wa fedha vikundi vya VICOBA alivyokuwa ameviahidi kuvisaidia,Genereta za kutoa nishati za kuendeshea miradi kwa vikundi kwenye maeneo yasio na umeme,vifaa ya michezo kwa vijana na hati za uthibitisho wa ujenzi wa barabara zitakazojengwa kwa madiwani wa kata za jimbo la Ukonga.Slaa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi alitangaza mafanikio hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi ya Kitunda iliyopo jimbo la Ukonga jana ambapo pia alitangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.Baadhi ya mafanikio aliyofanikisha katika kipindi cha uongozi wake aliyabainisha kuwa ni katika sekta ya elimu- ambapo mazingira katika shule mbalimbali yameboreshwa,afya-ambapo vituo vipya vimejengwa na vingine kupatiwa vifaa na dawa,miradi ya maji na ujezi wa barabara kwenye kata ya Gongo la Mboto na kata zote za Manispaa ya Ilala.Kutokana na mafanikio yaliyopatikana nawaomba wananchi wa jimbo la Ukonga mniunge mkono kwa kinichagua niwe Mbunge wenu katika uchaguzi mkuu ujao ili nizidi kuwatumikia na kushirikiana nanyi kuleta maendeleo katika jimbo hili la Ukonga ambalo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali za maendeleoAlisema.Alisema wakazi za jimbo la Ukonga wanahitaji Mbunge ambaye atakuwa bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. Bado tunahitaji kuboresha zaidi huduma za kijamii kama vile shule, hospitali ,maji safi,kubuni miradi ya maendeleo ya akina mama na vijana kwa kuwa naelewa matatizo ya jimbo hili na baadhi yake nilishaanza kuyavalia njuga nikiwa diwani, mkinichagua kuwa mbunge wenu nitaendeleza safari ya kuleta maendeleo.

Mkutano huo wa Meya Jerry Slaa ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wengi wa jimbo la Ukonga ambao wengi wao walipokea tamko hilo la kutangaza nia kwa furaha na baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa kiongozi huyo anaelewa matatizo ya wananchi wa Ukonga na ni mtu wa watu ambaye amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kazi kwa kujali watu wa aina zote.