mafunzo ya msingi kwa wajasiriamali wadogo
TRANSCRIPT
Mafunzo ya msingi Kwa
wajasiriamali wadogo Mwongozo huu umeandikwa Kwa ajili ya kuwasaidia watu mbalimbali ambao wangependa kupata muhtasari juu ya masuala ya biashara na Utunzaji rahisi wa hesabu za biashara.
Imeandikwa na Kheri A.Rajabu
2
YALIYOMO
Utunzaji wa kumbukumbu za fedha kwa wafanyabiashara wadogo………….…………………………03
Vitabu vya hesabu za biashara………………………………..…………………………………………………………….04
Huduma kwa wateja……………………………………………………………………………………………………….……..09
Njia rahisi kupambana na matumizi/gharama za lazima(fixed costs) katika biashara yako…......11
Jinsi ya kuuendesha Mkopo……………………………………………….…………………………………………………….12
Aina za biashara ambazo mtaji wake ni mdogo lakini faida yake ni kubwa……………….………………14
3
Utunzaji wa kumbukumbu za fedha kwa wafanyabiashara wadogo
• Utunzaji wa hesabu za fedha ni muhimu kwa kila mfanyabiashara bila kujali ukubwa wa
biashara au ukubwa wa mtaji,unapoweka hesabu zako vizuri utakuwa na uwezo wa
kujua mapato yako,matumizi yako na kukubwa zaidi ni kujua faida au hasara
unayotengeneza kutokana na biashara yako,changamoto kubwa wanayoipata
wafanyabiashara/wajasiliamali hasa wadogo ni jinsi ambavyo wanashindwa kutofautisha
biashara zao na wao wenyewe.Inabidi kufahamika kuwa mmiliki wa biashara na biashara
ni vitu viwili tofauti,inapaswa kuiheshimu biashara yako hata kama mtaji wako ni mdogo
sana,biashara ni biashara.
Misingi ya kuheshimu biashara yako
• Tofautisha biashara yako na wewe mwenyewe binafsi.
• Unapochukua fedha toka kwenye biashara kwa ajili ya mayumizi yako
binafsihaimaanishi kuwa umechukua hela yako,hii ni gharama kwa
biashara(expenditure) na inapunguza kiasi cha faida unayopata toka kwenye biashara
yako,kiasi cha fedha unachotoa kwenye biashara yako kwa ajili ya matumizi yako binafsi
hutambulika kama “Drawing”
• Iwapo una biashara na wewe mwenyewe unafanya kazi kwenye biashara hiyo badala ya
kuajiri mtu, inakupasa ujilipe mshahara kama vile ambavyo ungemlipa mtu kwa ajili ya
kufanya kazi hiyo.
• Ainisha gharama za uchukuzi hata kama unatumia usafiri wako binafsi kwa ajili ya
kuchukua mali au mzigo wa biashara yako
• Usichukue mali ya biashara kwa matumizi yako binafsi bila kulipia,iwapo huna fedha kwa
wakati huo na unahitaji kitu kutoka kwenye biashara yako ni vyema ukachukua kwa
kukopa na uhakikishe unalipa kwa wakati vinginevyo ufanye uchukuzi huo kama
‘drawing’ na kumbuka kuwa hii itakuongezea gharama kwenye biashara yako na
kukupunguzia faida pia,hivyo tafakari mara mbili kabla hujachukua mali ya biashara kwa
ajili ya matumizi binafsi.
• Iwapo unafanya biashara katika nyumba unayoishi, hakikisha unagawanya gharama ya
vitu Kama umeme na maji iwapo vinatumika na kwenye biashara yako pia.
• Iwapo utatumia fedha ya biashara Kwa ajili ya chakula, usafiri na mengineyo hakikisha
gharama hizo unaziingiza kwenye biashara ili kupata faida halisi.
4
• Ni vizuri kuhifadhi kiasi cha fedha toka kwenye faida Kwa ajili ya kuongeza mtaji (non-
distributable profit) hii itasaidia biashara kujifadhili yenyewe kifedha (sel-f finance)
badala ya kutumia mkopo au chanzo kingine cha fedha tofauti na biashara yako.
• Marekebisho yeyote unayoyafanya katika eneo la biashara yako lazima uyaingize
kwenye gharama za uendeshaji za biashara yako.
• Iwapo utachukua mkopo kwa ajili ya kuboresha biashara yako,hakikisha fedha hiyo
unatumia kwa madhumuni ya biashara tu na sio vinginevyo,utapotumia kwa ajili ya
matumizi mengine itakuja kuwa mzigo kwako kwenye kurejesha.
• Marekebisho yeyote unayoyafanya katika eneo la biashara yako lazima uyaingize
kwenye gharama za uendeshaji za biashara yako.
• Iwapo utachukua mkopo kwa ajili ya kuboresha biashara yako,hakikisha fedha hiyo
unatumia kwa madhumuni ya biashara tu na sio vinginevyo,utapotumia kwa ajili ya
matumizi mengine itakuja kuwa mzigo kwako kwenye kurejesha.
Vitabu vya hesabu za Biashara
• Yeyote anaweza kutunza hesabu za biashara yake hata Kama hana elimu ya uhasibu
mradi ajue kusoma na kuandika.Katika vitabu hivi sio lazima kununua vitabu maalum
vilivyochapishwa, unaweza kununua kitabu cha kawaida (counter book) ambapo
gharama yake si kubwa sana (inaingia pia kwenye gharama za biashara) na kuchora
mistari kulingana na mahitaji ya kitabu husika.
• Vitabu muhimu ni kama ifuatavyo
• Kitabu cha manunuzi
• Kitabu cha mauzo
• Kitabu cha biashara,Faida na hasara
• Kitabu cha mapato na matumizi
• Kitabu cha fedha
• Kitabu cha manunuzi
• Hiki utarekodi manunuzi yote unayofanya kwa ajili ya biashara yako, kitabu hiki
kitakusaidia kufahamu manunuzi yote uliyofanya kwa ajili ya biashara yako katika kipindi
fulani pengine siku, wiki au mwezi kutegemea ni kipindi gani unafunga hesabu zako.
5
• Kitabu cha mauzo
• Hiki ni kitabu ambacho kinatumika kurekodi mauzo yako ya kila siku,pia
kitakusaidia kujua kiasi cha mauzo ulichopata katika biashara yako .
Kitabu cha Biashara, Faida na hasara
• Hiki ni kitabu muhimu na ndio hutoa taarifa iwapo umepata faida au hasara
kwenye biashara yako ndani ya kipindi fulani.Huandaliwa kwa kuchukua jumla ya
manunuzi yote,unajumuisha na gharama ya manunuzi kama vile ubebaji na
kadhalika,kisha unachukua kiasi cha mauzo yote pamoja na gharama za mauzo
unajumlisha ,ukishapata jumla ya manunuzi na mauzo kisha unatoa mauzo toa
manunuzi,kama gharama za maunuzi ni kubwa kuliko mauzo hapo itakuwa ni hasara,na
iwapo mauzo ni makubwa kuliko manunuzi hapo itakuwa ni faida,faida au hasara hii
tunayopata hapa huwa ni ile ambayo si halisi,ili kupata faida halisi,inakubidi uchukue
faida isiyo halisi kisha utoe gharama nyingine mbalimbali kama vile
umeme,maji,usafiri,na gharama nyingine ambazo hutokea katika mzunguko wa
biashara,ukishatoa hizi ndo unapata faida halisi(Net Profit) na pia unaweza pata hasara
halisi(net loss) iwapo gharama nyinginezo zimekuwa kubwa kuliko faida halisi.
MIFANO YA VITABU VYA KUTUNZA KUMBUKUMBU
KITABU CHA MAUZO YA SIKU (mfano)
TAREHE MAELEZO KIASI
1.01.2016 Sukari kilo 2@1500 xxxx
02.01.2016 xxxx
03.01.2016 xxxx
xxxx
Jumla
KITABU CHA MANUNUZI YA SIKU (mfano)
TAREHE MAELEZO KIASI
1.01.2016 Sukari kilo 2@1500 xxxx
02.01.2016 xxxx
03.01.2016 xxxx
Jumla xxxx
6
KITABU CHA MAPATO NA MATUMIZI
TAREHE MAELEZO MAPATO MATUMIZI
01.01.2016 Salio la kufungulia xxxx
02.01.2016 mauzo xxxx
“ usafiri xxxx
31.01.2016 Salio la kufungia
KITABU CHA FEDHA JEDWARI MOJA (Fedha taslimu tu)
Mapato matumizi
Tarehe Maelezo Fedha Taslimu
Tarehe Maelezo Fedha taslimu
01.01.2016 Salio la kufungulia xxxxx 01.01.2016 Bili ya maji xxxx
01.01.2016 mauzo xxxxx mshahara xxxx
Mapato mengine xxxxx Jumla xxx
Salio la kufungia xxx
Jumla kuu xxxx
KITABU CHA FEDHA JEDWARI MBILI (Fedha taslimu NA Benki)
Mapato matumizi
Tarehe Maelezo Fedha Taslimu
Benki Tarehe Maelezo Fedha taslimu
Benki
01.01.2016 Salio la kufungulia
xxxxx xxxx 01.01.2016 Bili ya maji xxxx
01.01.2016 dipositi xxxx 01.01.2016 dipositi xxxx
01.01.2016 mauzo xxxxx mshahara xxxx
Mapato mengine xxxxx Jumla xxx -
Salio la kufungia xxx xxxx
Jumla kuu xxxx xxxx
7
KITABU CHA BIASHARA, FAIDA NA HASARA
Mali ya kuanzia xxxxx Mauzo xxxxx
Jumlisha: manunuzi xxxxx Jumlisha: gharama za mauzo xxxxx
Gharama za manunuzi xxxxx
Faida isiyo kamili xxxx
Jumla
Faida isiyo kamili xxxxx
Gharama za uendeshaji
Umeme xxxxx
Maji xxxxx
Matengenezo xxxxx
Mshahara xxxxx
Usafiri xxxxx
Matumizi mbalimbali xxxxx
Jumla: xxxxx xxxx
Faida Halisi xxxxxx
8
MIZANIA (balance sheet)
MALI MADENI
Mali za sasa Madeni ya sasa
Fedha taslimu xxxx Fedha utarajiazo kulipa xxxx
Fedha zilizo benki xxxx kodi utakiwayo kulipwa xxxx
Fedha utarajiazo xxxx mishahara isiyolipwa xxxx
Gharama zilizolipwa Madeni ya muda mrefu xxxxx
Kabla xxxx Mtaji wa wanahisa
Uwekezaji wa muda Mtaji xxxxx
Mfupi xxxx faida isiyogawanywa xxxxx
Jumla ya Mali za sasa xxxxx Jumla ya mtaji ya wanahisa xxxxx
Mali za kudumu
Ardhi (toa thamani ya uchakavu)
Jengo (toa thamani ya uchakavu)
Samani (toa thamani ya uchakavu)
Jumla ya Mali xxxxx Jumla ya mtaji na Madeni xxxxx
9
HUDUMA KWA WATEJA
Mteja ni ufunguo wa aina yeyote ile ya biashara iwe ni kuuza bidhaa au huduma, mteja ndio
sababu ya biashara kuwepo. Biashara yeyote ile inaanzishwa Kwa madhumuni ya kupata Mteja
ili anunue kama ni huduma aitumie na mwisho wake uweze kulipia gharama za biashara na
muhimu zaidi kupata faida kutokana na biashara unayoifanya.
Misingi ya huduma kwa wateja
Kauli nzuri
Kauli nzuri ni kitu cha Msingi sana kwa biashara yako, mara nyingi Mteja huvutiwa kuja
kwenye biashara yako kutokana na vile ambavyo unazungumza nae.Kuna baadhi ya
wateja wengine ni wakorofi, ni muhimu kujua aina ya wateja wako, iwapo wewe ni
mfanya biashara yakupasa kuongeza vizuri na Mteja wako hata kama Mteja ni mkorofi
na kauli zake si nzuri, unapozungumza vizuri na wateja itakufanya utengeneze uwigo wa
wateja wa kudumu ambao ni muhimu sana kwa biashara yako.
Uaminifu
Uaminifu kwenye biashara hapa unabeba maana kubwa sana,kwanza kama unauza
bidhaa hakikisha ya kuwa bidhaa hizo ni bora na hazijapita muda wake wa matumizi,ni
vizuri kuuza bidhaa bora hata kama bei yake ni kubwa kuliko kuuza bidhaa hafifu hata
kama bei yake ni ndogo,kamwe usiuze bidhaa ambazo ni batili(fake) au ambazo
zimepigwa marufuku na vyombo vinavyohusika hata kama unazipata kwa bei
rahisi,Mteja akigundua unamuuzia vitu visivyofaa anaweza akahama na kuamia kufanya
manunuzi yake pengine,kibaya zaidi iwapo atawataarifu watu wengine inaweza
kukusababishia kupungua kwa wateja kwenye biashara yako kwa kiasi
kukubwa.Uaminifu pia unajumuisha kurudisha chenji kwa usahihi,kama unatumia mizani
kupimia bidhaa hakikisha kuwa kipimo chako ni sahihi,pia uza bidhaa zako kwa bei ile
ambayo ni halisi bila kuweka aina yeyote ya ulanguzi.
Ushauri kwa wateja
Kutokana na dunia ya sasa kuna aina nyingi sana za bidhaa kutoka kwa watengenezaji
mbalimbali,wakati mwingine Mteja hushindwa kuchagua anunue bidhaa ipi toka kwa
mtengenezaji yupi,hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kuwashauri wateja wako,mara
nyingi wateja hupenda unafuu wa bei,ila ni muhimu kuwashauri wateja wanunue bidhaa
ambayo si nafuu tu,bali pia ni bora,vinginevyo ni Kheri kumshauri Mteja kununua bidhaa
ambayo ni bora zaidi hata kama bei yake ni kubwa kidogo,Mteja anapopata bidhaa bora
kutoka kwako,kutamfanya awe Mteja wa kudumu ambacho ni kitu muhimu kwa
biashara yako.
10
Vifungashio
Vifungashio vya bure ni muhimu pia kama sehemu ya huduma kwa Mteja, baadhi ya
wateja huwa hawapendi wajulikane wamebeba nini wanapotoka dukani au sehemu
yeyote ya kununua, ni vizuri kuwa na vifungashio vya ukubwa mbalimbali kwa ajili ya
bidhaa tofauti, hakikisha gharama ya vifungashio kama vile mifuko ya plastiki, karatasi
n.k unazijumuisha kwenye gharama zako za biashara, ili uweze kupata faida halisi pindi
unapofanya hesabu zako za biashara.
Mauzo kwa mkopo
Hii pia ni njia nzuri za kudumisha mahusiano na huduma kwa Mteja,ila ni muhimu
ifanywe kiuangalifu sana na ni kwa wale tu wateja ambao ni wa kudumu na
unawafahamu vizuri kuzingatia uwezo na sifa za ulipaji za Mteja. Mfano wateja wengi
ambao ni waajiriwa hupenda kupata mahitaji yao na kulipa gharama zote mwisho wa
mwezi,wapokeapo mshahara, hata hivyo ni vizuri kuweka ukomo wa kukopesha ili
kuepusha kutetereka au kuyumba kwa biashara yako, pia kwa wateja kama wauzao
vyakula au vitafunwa huwa ni wazuri wa kukopa na kulipa pia,ni vizuri kutoa huduma
kwa mkopo katika biashara yako,lakini hakikisha tahadhari ya hali ya juu inachukuliwa
kwenye suala hili,pia ni muhimu kutunza kitabu maalum kwa ajili ya kuhifadhi
kumbukumbu za wateja unaowadai.
Zawadi ndogondogo
Iwapo mtaji wako unaruhusu unaweza kutoa Zawadi ndogondogo Kama vile pipi au
biskuti Kwa wateja ambao wananunua zaidi Kwa siku na hii hufaa zaidi kwa watoto
ambao mara nyingi ndo hutumwa dukani hasa kwenye maduka ya rejareja.
Punguzo la bei
Wakati mwingine unaweza kuuza bidhaa fulani kwenye biashara yako kwa be3i ya
punguzo ili kuwavutia wateja, muhimu ni kuhakikisha bei hiyo ya punguzo utayouza
haitokusababishia kupata hasara, mara nyingi bei ni kigezo kukubwa katika manunuzi,
bei ikiongezeka kidogo mauzo yatashuka na ikipungua kidogo mauzo yataongezeka,
hivyo siku zote sio busara kwa mfanyabiashara kung’ang’ania kuuza vitu kwa bei ya juu
kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unajifukuzia mwenyewe wateja katika biashara yako.
11
NJIA RAHISI ZA KUPAMBANA NA MATUMIZI/GHARAMA ZA LAZIMA (FIXED COSTS)
KATIKA BIASHARA YAKO
Matumizi au gharama za lazima ni zile gharama ambazo haziepukiki katika biashara yako, vitu
hivi huwa haviepukiki na ni muhimu sana katika biashara yako,baadhi ya gharama hizo ni kama
vile; kodi ya pango(iwapo umepanga sehemu ya kufanyia biashara),kodi ya
mapato,mishahara(kama umeajiri mtu kwenye biashara yako),umeme,marejesho ya mkopo N.K
Gharama hizi huwa ni lazima zitokee kila baada ya muda Fulani katika biashara yako, gharama
hizi huwa ni mzigo sana kwa mfanyabiashara hasa kama hujafanya maandalizi ya
awali.Unachoweza kufanya ili gharama hizo zisiwe mzigo kwako ni kutenga kiasi fulani cha
fedha pembeni toka kwenye mauzo ya kila siku.Unachoweza kufanya ni kutengeneza mfumo
wa kutoa asilimia fulani ya fedha kutoka kwenye mauzo ya kila siku na kutunza pembeni.
Mfano: Mauzo ya siku ni Tsh 85,000 ambayo ni sawa na 100%
Mgawanyo:
Kodi 10% 85,000x10/100= 8,500
Mshahara 5% 85,000x 5/100 = 4,250
Marejesho ya mkopo 8% 85,000x8/100 = 6,800
Umeme 2% 85,000x 2/100 = 1700
Jumla 25% 21,850
Kwa kufanya Mgawanyo kama huo hapo juu kutegemea na mauzo yako kwa siku utakuwa na
uwezo wa kutenga fedha kwa ajili ya kulipia gharama za lazima za biashara yako bila
kukwamakwama kwa kuwa fedha utakuwa tayari umeshaiandaa hivyo ifikiapo wakati wa kulipa
ni kuchukua na kulipa tu, hii itasaidia sana kukupunguzia mzigo wa gharama kipindi mzunguko
wa biashara si mzuri na fedha fulani ni lazima ilipwe.
12
JINSI YA KUENDESHA MKOPO
Mara nyingi mahitaji ya kibiashara huweza kupelekea kuhitaji mkopo ili uweze kutimiza
malengo yako.Mkopo si mzigo kwa biashara yako kama vile ambavyo wengi hudhani,cha Msingi
ni kujua tu jinsi gani unaweza kuuendesha(manage)mkopo wako.Zipo njia kadhaa ambazo ni
rahisi sana kufanya mkopo uwe na tija kwako na si mzigo. Njia hizi ni kama ifuatavyo.
1. Malengo ya Mkopo
Hakikisha unazingatia lengo la kuchukua mkopo baada ya kupata mkopo, ni vizuri kujua ni nini
hasa unataka kufanya kwa mkopo unaochukua, ukachukua mkopo bila malengo itakufanya
ujipe mzigo mkubwa na mkopo huo kutokuwa na manufaa yeyote kwako. Hivyo zingatia
kuchukua mkopo Kwa ajili ya malengo ya kibiashara au ya kimaendeleo uliojiwekea na hakikisha
unatumia katika malengo hayohayo.
2. Fanya Mgawanyo mzuri wa fedha ya mkopo
Unapochukua mkopo Kwa ajili ya biashara yako fanya Mgawanyo mzuri wa fedha hiyo ili mkopo
uwe na tija kwako. Kwanza kabisa hakikisha unatenga Marejesho mawili au matatu kutoka
kwenye fedha hiyohiyo ya mkopo ili kuwa na hakika wa kulipa hata biashara ikiyumba,pili ingiza
hela iliyobaki katika mahitaji ya biashara ila hakikisha unabakisha kidogo kwa ajili ya dharura
kwani hali ya biashara huwa inabadilika badilika kutokana na sababu mbalimbali za
kiuchumi,iwapo utatumia hela yote ya mkopo kwa bidhaa fulani halafu bidhaa ile isiuzike
utajikuta umejipa mzigo na atakosa njia ya dharura kurekebisha hali hiyo iwapo fedha yote ya
mkopo umeshaiingiza kwenye biashara.
3. Marejesho ya Mkopo
Pigia hesabu Marejesho yako ya mkopo Ili uweze kurejesha Kwa wakati na kuondoa usumbufu
wa kushindwa kulipa kiasi cha Marejesho ya mkopo kwa wakati. Njia nzuri ni kutenga asilimia
fulani ya mapato yako ya kila siku kutoka kwenye biashara yako kwa ajili ya kulipia mkopo wako
na ikifika siku ya kurejesha usiwe na wasiwasi wa kukosa rejesho lako.
13
4. Kiasi cha mkopo kisizidi uhitaji
Jambo jingine la Msingi la kuzingatia ni kiasi cha mkopo utachochukua kilingane na mahitaji
yako halisi, Usichukue fedha zaidi ya mahitaji yako, hii itakufanya kujiingiza katika matumizi
yasiyo ya lazima na pia kujipa mzigo wa kulipa deni la mkopo wako. Watu wengi hudhani,cha
kuwa fedha nyingi ndio Msingi wa Maendeleo ya biashara,hufikia hatua mtu kuwa tayari hata
kutoa hongo ili aidhinishiwe mkopo maradufu ya ule anaoweza kupata.Kufanikiwa ni kuweka
mipango thabiti na inayotekelezeka ndo Msingi wa Maendeleo ya biashara yako, Unapochukua
kiasi kidogo cha mkopo na ukakitumia vizuri huleta tija zaidi kwa Maendeleo ya biashara kuliko
kuchukua kiasi kukubwa na kushindwa kukisimamia vizuri.
5. Gharama na masharti ya mkopo
Jambo kubwa na la Msingi la kuzingatia ni kuhakikisha unafanya chaguo sahihi la mkopo
unaotaka kuchukua, ni muhimu sana kuangalia gharama na masharti ya mkopo iwapo unaweza
kumudu au la,zingatia sana unafuu wa riba na gharama nyingine kabla hujafanya maamuzi ya
kuchukua mkopo kutoka kwenye taasisi tofauti za mikopo,pia angalia manufaa mengine
unayoweza kunufaika nayo kwa kuchukua mkopo kutoka katika taasisi fulani, Ni muhimu
kuangalia vitu kama Mafunzo, Ushauri na faida nyingine ambazo taasisi ya mkopo inaweza
kutoa,pia epuka taasisi za kitapeli za mikopo ambazo nyingi zimeanzishwa kiujanjaujanja ili
kuwatapeli wananchi,ikitokea bahati mbaya ukachukua mkopo toka taasisi kama hizo unaweza
kujikuta unaingia kwenye matatizo ya uchumi ikiwemo kufilisiwa mali zako pasipo kufuata
utaratibu halali unaokubalika.
14
AINA ZA BIASHARA AMBAZO MTAJI WAKE NI MDOGO LAKINI FAIDA YAKE NI KUBWA
Genge la chakula,mbogamboga na matunda
Biashara hii huweza kufanywa kwa kuanzia na mtaji mdogo sana na soko lake ni kubwa hasa
maeneo ya makazi ya watu, kwa kuwa hugusa mahitaji ya kila siku ya watu,na ikiwa biashara
ipo maeneo ya makazi ya watu,mfanya biashara atakuwa na uhakika wa kuuza bidhaa zake ila ni
muhimu kuzingatia usafi na mpangilio mzuri wa biashara yake ili kuvutia zaidi wateja.
Vitafunwa na vyakula vikavu
Unaweza pia kufanya biashara ya vitafunwa na vyakula vikavu katika maeneo yetu ya makazi
huwa na uhitaji mkubwa wa vitafunwa hasa nyakati za asubuhi na kidogo jioni, watu wengi
hawapendelei kutumia vitafunwa vya aina moja kila siku (mfano mkate) hivyo vitafunwa mfano
maandazi, kachori, sambusa, vitumbua, mihogo na viazi vya kukaanga, bagia, chapati n.k
vinaweza kuwa na soko kubwa mtaani na kukupatia faida nyingi mno.
Upikaji wa chakula
Wakati mwingine biashara hii ya chakula huonekana ya kawaida Kwa kuwa imezoeleka bila
watu wengi kufahamu kuwa Ina faida kubwa Sana, inaweza kufanywa na mtu mmoja au
mkajiunga kiasi cha watu wanne hivi na mkawa na sehemu maalum ya kuuzia(kama vile mama
lishe) lakini pia kiubunifu zaidi biashara hii inaweza kufanywa kwa kutafuta oda mbalimbali
mfano kupelekea maeneo ya maofisini au maeneo ya kazi,viwandani n.k hasa nyakati za
mchana,pia kuongeza thamani na ubora wa chakula hicho unaweza kukifunga kwa kutumia
vifungashio maalum(lunch box).Pia mnaweza kutafuta oda za kusambaza chakula kwenye
sherehe mbalimbali,mikutano na kadhalika.
Ung’arishaji na ukarabati wa viatu,pochi na mabegi na bidhaa nyingine za ngozi
Hii pia ni biashara nyingine nzuri sana isiyohitaji mtaji mkubwa,ukushakuwa na sehemu ya
kufanyia biashara, gharama ya kununua vifaa vya kuanzia inaweza isizidi hata hamsini
elfu(50,000)hukugharimu sana kununua rangi za viatu,nyuzi za kushonea,sindano za
kushonea,sindano za kushonea na vifaa vingine vidogodogo.Biashara hii inapokwenda vizuri
15
unaweza kuongeza vitu kama vocha,biashara ya magazeti na vitu vidogovidogo kama
sigara,pipi,karanga,kwa kuwa muda mwingi unakuwa hapo na baadhi ya wateja kama kazi
inachukua muda mrefu kusubiri huweza kuhitaji bidhaa ndogondogo kama hizo ili kusogeza
muda,mafanikio ya biashara hii yanaweza yakaonekana zaidi iwapo itafanyika sehemu zenye
mikusanyiko ya watu kama vituo vya mabasi,sokoni katikati ya mitaa yenye ofisi nyingi.
Duka la rejareja
Aina hii ya biashara hupatikana Sana kwenye maeneo tunayoishi na ni biashara iliyozoeleka
sana. Biashara hii ina gharama ndogo za uendeshaji na pia uhakika wa mauzo, pia haihitaji
taratibu nyingi za kuirasimisha kuifanya,ukipata leseni na namba ya utambulisho wa mlipa kodi
(TIN)inatosha kuifanya biashara yako iwe rasmi na pia unaweza kupata fursa za kupata mikopo
toka taasisi mbalimbali za fedha kwa ajili ya biashara yako.Ili ufanukiwe zingatia kuuza vitu
ambavyo vinahitajika zaidi na pia uwe makini kwenye udhibiti wa mzigo wako wa biashara,
bidhaa zinazohitajika kwa wingi na mzunguko wake ni mkubwa uziweke kwa wingi kuliko zile
ambazo hazihitajiki sana na mzunguko wake ni mdogo.
Ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku una faida kubwa na uendeshaji wake huitaji fedha kidogo hasa kwa kuku wa
kienyeji.Ukiwa na banda zuri lenye nafasi ya kutosha unaweza kununua kuku wadogo kwa bei
rahisi kiasi cha 3,000 hadi 4,000 na kuwalisha vizuri na kuwakuza na baada ya miezi kadhaa
ukauza kwa kiasi cha 8,000 hadi 10,000,kwa harakaharaka unaweza kuona jinsi gani unaweza
kutengeneza faida kubwa kutokana na biashara hii,uzuri ni kwamba kuku hawa huwa hawaugui
mara kwa mara na wala hawahitaji mlo maalum wenye gharama kubwa kama walivyo kuku wa
kisasa,pia mabanda yao hayana mahitaji mengi maalum na kizuri zaidi ni kwamba wanataga na
kutotoa mayai hivyo mayai inaweza ikawa ni zao lingine kwa biashara lakini pia vifaranga
ukiwatunza nao pia utakuja kuwafanyia biashara hivyo baada ya mda fulani unakuwa na
uhakika wa mzunguko mzuri wa biashara. Biashara hii ya kuku unaweza kuipeleka mbali na
kuwa ya kisasa zaidi na kuweza kukupatia kipato kukubwa sana.Mfano unaweza kuwachinja
kuku hao,kuwaandaa na kuwafunga kwenye vifungashio vizuri na kutafuta soko la jumla
16
kwenye maduka makubwa (supermarkets) au ukawa na sehemu yako ya kuuzia ukawaweka
kwenye jokofu na ukaweza kuwauza kwa urahisi kutokana na harakati nyingi za kimaisha watu
wengi hupenda vitu vya namna hii ambavyo vimeshaandaliwa .Faida nyingine kubwa ni
kwamba unaweza kupata kipato zaidi kwani unafunga kuku na kuuza peke yake na pia virigisi
unazifunga na kuuza peke yake hivyo kwenye kila kuku watano unapata mfuko mmoja wa
firigisi ambao unaweza ukauza hadi elfu tano,ila hadi kufukia hatua hizi zote inabidi uwe
umeendesha mradi huu kwa muda mrefu kidogo ili kujizalishia fedha za kuweza kufanya yote
hayo,japo pia iwapo unaweza kupata fursa ya kupata mkopo inaweza kukufikisha haraka
kwenye hatua hii.
Bustani ya mbogamboga
Bustani ya mbogamboga pia ni biashara nyingine ambayo inaweza kukuongezea kipato kwa njia
rahisi sana.Kama una eneo zuri sehemu unayoishi na kuna huduma ya maji hiyo ni fursa.
Unaweza kulima Bustani na kupanda vitu kama nyanya, vitunguu, karoti, mbogamboga, pilipili,
bamia, bilinganya na kadhalika, ukizitunza na zikamea vizuri unaweza kutafuta sehemu ya
kwenda kuuzia au ukawa na eneo lako la kuuzia au pia watu wanaweza wakaja kwako na
ukawauzia pia.Mradi huu ni mzuri kwani utakupatia kipato lakini pia utakupunguzia matumizi
kwa kujipatia mahitaji yako muhimu ya chakula toka kwenye Bustani yako na fedha utayokua
umeiokoa waweza kuifanyia mambo mengine ya Maendeleo.
*****MWISHO*****
17