maarifa ya uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki...

281

Upload: others

Post on 01-Sep-2019

423 views

Category:

Documents


4 download

TRANSCRIPT

Page 1: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema
Page 2: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Maarifa ya Uislamu

Darsa la Watu Wazima

Juzuu 5

JAMII YA KIISLAMU

Islamic Propagation Centre

Page 3: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Toleo ya Kwanza 2004

Islamic Propagation Centre (IPC)S.L.P 55105, Dar es Salaam, Tanzania.

© Hakimiliki 2005, 2004 na IPC

Maarifa ya UislamuDarasa la Watu WazimaJuzuu ya Tano

Wachapaji/WasambazajiIslamic Propagation Centre (IPC)S.L.P 55105, Dar es Salaam, Tanzania.Chapisho la kwanza, 21, April, 2004Nakala 1000Chapisho la kwanza, 27, April, 2005Nakala 1000

Kimetayarishwa na Islamic Propagation CentreP.O.BOX 55105, simu 022-2450403

Usanifu wa kurasa na Jalada: Islamic Propagation Centre.

ii

Page 4: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Neno la AwaliShukurani zote njema zinamstahiki Allah(s.w) aliye

Bwana na Mlezi wa walimwengu wote. Rehema na Amaniziwaendee Mitume wake wote pamoja na wale wanaofuatamwenendo wao katika kuhuisha Uislamu katika jamii.

Tunamshukuru Alla(s.w) kwa kutuwafikisha kutoajuzuu ya Tano ya Maarifa ya Uislamu kwa Darasa la WatuWazima. Masomo haya ya Uislamu kwa watu wazimayamejikita katika Qur’an na Sunnah ya MtumeMuhammad(s.a.w).

Juzuu hii ya Tano, imekusudiwa kuwawezesha wasomajikuyafahamu vyema Maadili ya Kiislamu na tafauti yakekimsingi,ikilinganishwa na yale ya jamii za kitwaghuuti.Misingi hii ya Maadili imedhihirishwa kwa ufafanuzi wakiutekelezaji, katika Utamaduni, sheria na hukumu, uchumina kuchuma; na hatimaye katika Siasa na uendeshaji waDola.

Hivyo basi, baada ya wasomaji kuipitia juzuu hii kwamakini, inatarajiwa watakuwa mstari wa mbele kwenyeharakati za kuhuisha Uislamu katika jamii, wakitumianeema ya mali, nguvu, vipawa na muda aliowajaaliaAllah(s.w), kama walivyofanya Mitume na watu wemawaliotangulia.

Mola wetu! Tupe rehema zinazotoka kwakona tutengenezee uongofu

katika kila jambo letu(18:10)iii

Page 5: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

iv

Yaliyomo

Sura ya Kwanza.............................................................1Misingi ya Maadili...................................................1Binadamu si mnyama.................................................1

Mtizamo wa Kikafiri juu ya Uadilifu............................5 Mtizamo wa Uislamu juu ya Uadilifu...........................11 Zoezi la Kwanza........................................................20

Sura ya Pili.................................................................21Utamaduni............................................................21

Utamaduni wa Muislamu..........................................21 Vipengele vya Utamaduni wa Kiislamu................25

Tabia njema............................................25Vazi la Kiislamu......................................28Miiko katika kula na kunywa...................37Michezo na Burdani.................................54Misiba na Maombolezo.............................65Maombi na Dua.......................................69Kumkumbuka Allah (s.w) Saa 24..............75

Zoezi la Pili...........................................................80

Sura ya Tatu.................................................................81Sheria....................................................................81Maana ya Sheria......................................................81Kazi za sheria katika jamii.........................................81

Chimbuko la sheria za Kitwaghuti..............................83 Chimbuko la Sheria ya Kiislamu.........................89

Mahakama ya Kiislamu.....................................98Haki za Mshitakiwa ..............................104Mgawanyo wa Makosa............................110

Haki za wasiokuwa Waislamu................................118 Zoezi la Tatu.........................................................121

Page 6: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Sura ya Nne................................................................122Uchumi.................................................................122Maana ya Uchumi...................................................122Nadharia ya uchumi wa Kiislamu............................123

Dhana ya mafanikio.................................124Dhana ya umilikaji mali...........................125Dhana ya bidhaa......................................126Dhana ya Matumizi..................................126Milki ya Rasilimali....................................127

Umuhimu wa uchumi katika Uislamu.....................134 Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu......138

Sera ya uchumi katika Uislamu..............................139Haki ya Serikali kuzuia Dhulma...............140

Haki na Uhuru wa kuchuma katika Uislamu...........142Biashara ................................................143Haki ya kumiliki mali...............................157Mipaka ya Umilikaji mali..........................159

Mgawanyo wa mali katika Uislamu..........................160

Zakat.....................................................160Sadakat................................................161Kodi (Jizya)............................................166Mikopo..................................................167

Mfumo wa benki (za riba) za kitwaghuti....................175Madhara ya riba katika jamii.....................177Uharamu wa Riba katika Uislamu.............179

Benki za Kiislamu..................................................187Mudharabah..........................................188Musharikah..........................................188Ijara-Uara wa Iktina................................189Murabah...............................................189Muqaradha............................................189Uzuri wa benki za Kiislamu......................190

Zoezi la Nne.........................................................191

v

Page 7: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Sura ya Tano..............................................................193Siasa...................................................................193Maana ya Siasa......................................................193Mifumo ya siasa za kitwaghutii.................................193

Ujima.............................................................194Utumwa..........................................................194Ukabaila.........................................................195Ubepari..........................................................195Ujamaa...........................................................195Udemokrasia..................................................196

Mfumo wa siasa ya Kiislamu...................................197 Dhana ya Dola.......................................................198

Dola za Kitwaghutii.................................................199Muundo na Uendeshaji wake...................199Dosari za Dola za Kitwaghutii...................204

Dola ya Kiislamu....................................................204Dhana ya Utawala....................................205Vyombo vya Dola....................................206Uraia katika Dola ya Kiislamu..................211Msonge wa Uongozi.................................213Masharti ya kuwatii viongozi (Ulul-amri)...219Siza za anayestahiki kuwa kiongozi...........223Wajibu wa kiongozi..................................230

Usimamishaji Haki katika dola ya Kiislamu...........243Haki ya Kuishi.......................................245Haki ya Usalama wa Maisha.....................246Haki ya Heshima......................................247Haki ya Uhuru..........................................248Haki ya Kuhukumiwa kwa Uadilifu............250Haki ya Usawa wa Binaadamu..................251Haki ya uhuru wa mahusiano...................252Haki za raia...........................................252Haki za wasiokuwa Waislamu...................259

Zoezi la Tano...............................................................269

vi

Page 8: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Utangulizi

Lengo la kuumbwa watu na kuwezeshwa kuishi hapaduniani ni kumuabudu Allah (sw). Qur’an, kitabukisichokuwa na shaka ndani yake, kinabainisha kuwa Al-lah (sw) anasema:

Sikuwaumba majini na wanaadamu ila waniabudu (51:56)

Ibada kwa msimamo wa Qur’an haiishii tu kwenye kusali,kufunga, kutoa zakat na sadaqat, kuhiji, kumsalia Mtume(saw), kumsifu na kumtukuza Allah (sw). Kila jamboanalofanya mtu katika binafsi yake, kifamilia au kijamii, niibada. Na ndiyo maana Allah(sw) anaamuru kuwa:

Sema: hakika sala zangu, na shughuli zangu, na uhaiwangu na umauti wangu ni kwa ajili ya MwenyeziMungu Hana mshirika (6:162-163)

vii

Page 9: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Aidha, kuna aina mbili tu za ibada kwa mujibu waQur’an. Ibada wafanyayo watu kumuabudia Allah (sw) naibada ambayo watu hufanya kumuabudu Shetani.Ushahidi uthibitishao kuwepo kwa ibada ya watukumuabudu shetani ni ile kauli ya Allah (sw) alipowaonyawanadamu mbele, kuwa siku ya kiyama atawalaumuakisema:

Je, sikukuagizeni, enyi wanadamu kuwamsimuabudu shetani? Hakika yeye kwenu ni aduialiye dhahiri . Na kwamba niabuduni mimi. Hii ndiyonjia iliyonyooka. (36:60-61)

Hivyo, watu na watahadhari amali zao zisiwe zakumuabudu shetani kwa dhamira na matendo. Maanaamali za mja, akiwa binafsi au kundi, huingia kwenyemoja ya aina hizo za ibada. Qur’an inasema kuna madaftarimawili ya amali za waja:

Kwa hakika maandishi (ya amali) za watu waovuyamo katika Sijjin.

(hilo)Ni daftari lililoandikwa (ndani yake amali zawatu wabaya). (83:7,9)

viii

Page 10: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Hakika maandishi ya watu wema yamo katika Iiyyin.

(Hilo) ni daftari ambalo zinaandikwa humo (amali zawatu wema). (83:18,20)

Kutokana na ukweli huu, unapatikana ulazima kwaWaislamu kuishi katika jamii yenye kujenga mazingiramazuri ya kutomkwaza muumini kutenda mema nakumsaidia aweze kumuabudu Allah (sw) katika kila amaliaitendayo. Jukumu hili la kujenga jamii bora,inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwamabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema Allah (sw):

Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu zote zaUislamu, wala msifuate nyayo za shetani, kwahakika yeye ni adui dhahiri (2:208)

Kwahiyo, pamoja na kutekeleza zile nguzo za Uislamukwa ukamilifu wake, yapasa zitujenge na tujengeke kuwawakweli katika amali na kauli thaabiti katika kuusimamiana kuufuata mfumo wa maisha wa Kiislamu kijamii.Tusifuate nyayo za shetani, isipokuwa sheria za Allah (sw)katika kuhukumu na kuhukumiana. Tuchume kiislamuna kuuvaa utamaduni wake, tujenge maadili ya Kiislamuna kuifuata siasa yake safi, iliyotwahara.

ix

Page 11: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

Juzuu hii, kwahiyo, inakusudia kudhihirisha mawandana msimamo wa Uislamu katika maisha ya kijamii katikasura zifuatazo:

1 Misingi ya maadili katika Uislamu2 Utamaduni katika Uislamu3 Sheria katika Uislamu4 Uchumi katika Uislamu5 Siasa na Uendeshaji wa Dola

x

Page 12: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

1

Sura ya Kwanza

MISINGI YA MAADILI

Binadamu si mnyamaMtu ni kiumbe tofauti na viumbe wengine, hata wale

waliokaribiana kimaumbile katika kundi la mamalia(mammals).Pamoja na makafiri kudai kuwa asili ya mtuni jamii ya masokwe kwa kuwa wanakaribia kufananakimaumbile, wametafautiana mno.Tofauti hii inatokanana vipawa maalum alivyotunukiwa mtu ukilinganisha navipawa vya wanyama. Vipawa hivi humfanya mwanadamuaunde au kufuata maadili fulani, jambo ambalo wanyamahawana.Vipawa hivi ni:

1.Akili yenye kumuwezesha kutafakari juu yamambo mbali mbali.2.Kujitambua (Self consciousness)kunakomuwezesha mtu kujua mahusiano yake namazingira yake.3.Elimu yenye kumuwezesha kuendesha maishayake hapa ulimwenguni kwa wepesi na kwa ufanisi.4.Uhuru wa kuchagua na kutenda alitakalo ndaniya kanuni za maumbile:

Vipawa hivi humfanya mtu mwenye akili timamuajiulize maswali mengi ya msingi kama vile, nini chanzocha ulimwengu na vyote vilivyomo, nini kusudio la kuwepowatu na maumbile yote yaliyowazunguka, ni ipi hatimaya ulimwengu na vyote vilivyomo, n.k. Mwenendo wa tabiaya mtu itategemeana na majibu atakayoyapata kutokanana maswali hayo ya msingi. Akipata majibu sahihi atawezakuishi maisha mazuri yenye kulingana na lengo lakuumbwa kwake.Kwa hakika majibu sahihi atayapata

Page 13: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

2

kutoka kwa yule aliyeMuumba yeye pamoja na maumbileyote yaliyomzunguka. Anapaswa kumtambua Muumbawake kwa kutumia vipawa hivi vya ziada alivyotunukiwakama inavyosisitizwa katika Qur-an:

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatanowa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonyesha kuwapoMwenyezi Mungu mmoja), kwa wenye akili. (3:190)

Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wimana wakikaa na wakilala. Na hufikiri umbo la mbingu naardhi (kisha) wakasema “Mola wetu! Hukuviumba hivibure. Utukufu ni wako. Basi tuepushe na adhabu yaMoto.” (3:191)

Kwa mujibu wa aya hizi, kinachofuatia baada ya mtukumtambua Muumba, ni kufuata mwongozo wake katikakila kipengele cha maisha.

Endapo binaadamu atatumia vipawa vyake vya akili,utambuzi wa ubinafsi, elimu na uhuria kwa kufuatamsukumo wa matashi yake atapotea njia na kuishi maishayasiyo na muelekeo na atakuwa na mwenendo na tabia

Page 14: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

3

iliyochupa utu inayompelekea kufanya mambo maovu naduni kuliko yale yanayofanywa na wanyama. Juu ya hiliMuumba wetu karimu anatutanabahisha:

“Na bila shaka tumewaumbia Moto wa Jahannamuwengi katika majini na watu (kwa sababu hii): Nyoyo(akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo, na machowanayo lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayolakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, baliwao ni wapotofu zaidi. Hao ndiowalioghafilika.”(7:179)

Inadhihirika bayana kuwa pamoja na maendeleomakubwa ya sayansi na tekinolojia, amani katika maishaya hivi leo chini ya mfumo wa kitwaghutii (mfumounaochupa mipaka ya utu aliyoiweka Muumba), imetowekakabisa, na dhuluma imeshamiri. Kutoa na kupokea rushwandio mtindo wa maisha; ujambazi na uporaji umeongezekakitaifa na kimataifa; familia zinavunjika na ufuskakustawi; vijana wengi wametumbukia katika unywajipombe, uvutaji bangi, utumiaji wa madawa ya kulevya nakupoteza kabisa dira ya maisha yao; ukweli na uaminifuvimekuwa vitu adimu, ambapo fitina na propaganda zauwongo uliokithiri vimeshamiri katika vyombo vya habarikitaifa na kimataifa.

Page 15: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

4

Ukatili wanaofanyiana binaadamu hivi leo ni wa kutishakiasi ambacho mwanafalsafa mmoja wa Kiingereza aitwayeBertrand Russell alifikia kusema kuwa si haki kabisakumnasibisha binaadamu na mnyama kwa sababumnyama anatabia nzuri sana kuliko binaadamu! Maranyingi mnyama akiua, huua kwa haja ya chakula chawakati huo huo na si kuzusha vita isiyo na maana yoyotena kuua mamilioni ya watu wasio na hatia.

Mauwaji ya halaiki yaliyofanywa na Majeshi yaMarekani na Washirika wake dhidi ya wananchi na raiawa Afghanistan na Iraq, pamoja na unyama wa Serikaliya Israil dhidi ya Wapalestina, ni ushahidi wa alichokisemaRussell .

Akijadili juu ya maadili ya binaadamu yalivyo katikaulimwengu huu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia,mwanafalsafa mwingine Harold H.Titus ameandika:

“Mlolongo wa matukio katika miaka ya hivi karibuniumedhihirisha wazi kuwa kuna jambo lililokwendakombo katika maisha ya binaadamu. Binaadamuamejipatia uwezo mkubwa mpya katika nyanja za sayansina tekinolojia, lakini mara nyingi uwezo huo umetumikakatika njia za uharibifu. Binaadamu amepanua upeo naubora wa ujuzi wake, lakini amepiga hatua ndogo sana,kama basi amepiga hatua yoyote, katika kujileta furahana amani”.

Aidha, mwanasaikologia aitwaye F.S.C. Northrop, nayeanaishangaa hali hii ya maadili na kuandika:

“Ulimwengu wetu ni wa kitendawili. Mafanikio ambayondio fahari yake yanatishia kuuangamiza… yaelekea kilatunapopiga hatua ya maendeleo ndivyo tunavyoshindwakudumisha ustaarabu”.

Page 16: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

5

Wanafalsafa hawa wangelikuwa Ulul-albaab (wenyeakili) na kumtambua Muumba wao, wasingeliishangaa halihii kwani imedhihirishwa na Muumba Karimu tangu karneya sita (A.D.), pale Mtume Muhammad (s.a.w)aliposhushiwa wahyi wa Qur-an:

Bila shaka TumeMuumba mwanaadamu kwa umbolililobora kabisa. Halafu tukamrudisha kuwa chinikuliko walio chini.Ila wale wenye kuamini nakutenda mema, watakuwa na ujira usiokwisha,(unaendelea maisha) (95:4-6)

Aya hizi zinatukumbusha kuwa pamoja na binaadamukuumbwa katika umbo bora na kutunukiwa vipaji alivyonavyo hawezi kuwa na mwenendo na tabia njema mpakaawe amemtambua na kumuamini Mola wake Muumba nakufuata mwongozo wake pekee katika kuendesha maishayake ya kila siku ya kibinafsi na kijamii huku akitarajiakupata radhi zake na malipo kutoka kwake katika maishaya hapa duniani na ya kesho akhera.

Mtizamo wa Kikafiri juu ya MaadiliMaadili ni mwenendo mwema unaombakisha

binaadamu katika hadhi yake na kumfikisha katika lengola kuumbwa kwake. Katika jitihada za kumfanyabinaadamu awe na tabia ya kufanya mema na kuachamaovu ili kuleta furaha na amani katika jamii, baadhi yawanafalsafa wa kikafiri wanauliza na kujaribu kutoamajibu ya maswali makuu manne yafuatayo:

Page 17: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

6

1. Ni kitu gani ambacho ndicho lengo kuu la maisha?2. Zipi chem chem, tunazozitegemea katika ujuzi wetu

juu ya mema na maovu? Yaani tutajuaje kuwajambo fulani ni baya au zuri? Tunapata kutoka wapihabari hizi za mema na maovu?

3. Ni nani msimamizi wa mwenendo wa tabia yabinaadamu? Yaani ni mamlaka ipi yenyekuhakikisha kuwa watu wanakuwa waadilifu?

4. Ni kitu gani kinachowasukuma watu wafuatemwenendo fulani wa tabia? Wanahamasishwa nanini?

Hebu tupitie majibu wanayotoa wanafalsafa na udhaifuwa majibu hayo:

1. Lengo kuu la maisha kwa mtazamo wa makafiriKatika kujibu swali la kwanza “Ni lipi lengo kuu la

maisha yetu”, wanafalsafa wa kikafiri wamegawanyikakatika makundi mengi miongoni mwa hayo ni haya matatu.

Kundi la kwanza linasema lengo kuu la maisha yetuhapa duniani ni kuishi maisha yenye furaha. Hivyo basijambo lolote linalotuongezea furaha yetu ni jema na lolotelile linalotuletea machungu, huzuni, na majonzi ni ovu.

Kundi la pili linasema lengo kuu la maisha yetu hapaduniani ni kufikia utimilifu (perfection). Hivyo kitendochochote kinachopelekea katika kukuza na kukamilishavipawa vyetu ni kitendo chema na jambo lolote linalokwazana kuviza vipawa vyetu visifikie kilele cha ukamilifu wakeni jambo ovu.

Kundi la tatu linasema lengo kuu la maisha haya nikuwa kila mtu atimize wajibu wake kwa madhumuni yakutimiza wajibu tu basi (duty for the sake of duty). Hivyojambo lolote linalomfanya mtu atimize wajibu wake bila

Page 18: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

7

ya kutarajia chochote ni jema na kila linalomzuia kutimizawajibu wake kwa madhumuni tu ya kutimiza wajibu basini ovu.

Udhaifu wa majibu hayoTukichunguza majibu ya wanafalsafa wa kikafiri juu

ya lengo la maisha, tunaona kuwa yanapwaya sana.

Tukianza na jibu la kwanza linalosema kuwa furahandio lengo kuu la maisha yetu hapa duniani, maswalikadhaa yanazuka. Ni furaha ya aina gani hiyoinayotafutwa? Ni furaha anayoihisi mtu baada yakutosheleza matamanio yake ya kimwili au ni furahainayotokana na kujifaharisha? Ni furaha itokanayo nakutathmini kazi za sanaa au furaha ya kiroho? Ni furahaya nani inayotafutwa, ya mtu binafsi au ya jamii ambamoanaishi? Au furaha ya watu wote au ni furaha ya kikundicha watu tu?

Tukichukua jibu la pili lisemalo kuwa lengo kuu nikufikia utimilifu, pia yanajitokeza maswali kadhaa. Ninimaana ya utimilifu? Ni kipi kipimo cha utimilifu? Niutimilifu wa nani unaotafutwa wa tabaka au kikundi alichomtu au wa mtu binafsi au wa jamii?

Vivyo hivyo tukichukua jibu la tatu lisemalo lengo kuuni kutimiza wajibu kwa lengo tu la kutimiza wajibu,hatuwezi kuepuka maswali haya:. Lengo hili maana yakeni nini hasa? Nani aliyeliweka? Nini hekima ya kulifuata?

2.Utambuzi wa Mema na Maovu kwa Mtizamo waMakafiri

Katika kujibu swali la pili, “zipi chem chem. (sourcesof knowledge) tunazozitegemea katika ujuzi wetu juu yamema na maovu, wanafalsafa wamegawanyika makundimatatu vile vile.

Page 19: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

8

Kundi la kwanza, linasema uzoefu wa binaadamu (hu-man experience) ndio chem chem pekee ya hakikainayomuwezesha mtu kujua lipi jema na lipi ovu. Rai hiihujulikana kama “empiricism” katika lugha ya Kiingereza.Kwa mujibu wa rai hii tunajua kuwa jambo fulani ni bayakwa sababu katika maisha yetu ya kila siku uzoefu wetuumetuonyesha kuwa jambo hilo lina madhara fulanikwetu.

Kundi la pili, linasema kinachotujulisha kuwa jambofulani ni zuri au baya ni silka zetu (intuition). Na rai hiihujulikana kama “Intuitionism” kwa lugha ya Kiingereza.

Kundi la tatu, linasema kuwa kinachotuwezeshakupambanua zuri na baya ni kipawa cha kufikiri na kuhojiau “Rationalism” kama rai hii inavyojulikana kwaKiingereza.

Udhaifu wa Makafiri juu ya Chem chem ya Ujuzi waWema na Uovu

Iwapo tutazifanya rai hizo za makafiri kuwa ndio chemchem ya ujuzi wa mema na maovu, tutajikuta katika haliya kutatanisha sana. Jema la asubuhi laweza kuwa ovula jioni na kinyume chake.

Kasoro za rai kuwa, “chem chem ya ujuzi juu ya wemana ovu ni uzoefu” ni hizi zifuatazo:

Kwanza, inabidi watu wasubiri mpaka kiyama ndiowang’amue kuwa jambo fulani lilikuwa baya au zuri iliupatikane uzoefu wa watu wote na halafu uzoefu huouchambuliwe na kutafsiriwa kwa ufasaha bila upendeleowowote. Hii ina maana kuwa watu itabidi wasubiri mpakasiku ya kiyama kabla ya kujua kuwa jambo fulani ni bayaau zuri. Na zaidi hakuna mtu anayeweza kuutafsiri uzoefuwa watu wote kwa usahihi bila ya upendeleo.

Page 20: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

9

Pili, uzoefu wowote alionao binaadamu leoumegawanyika katika fani chungu nzima za Elimu namabingwa wa kila fani wanautafsiri uzoefu wao kulinganana mwangaza wa taaluma zao. Tuchukue uzoefu wa nanikatika kuamua lipi ni jema na lipi ovu? Na kama kila mtuafuate uzoefu wake basi hapatakuwa na jambo loloteambalo tunaweza kusema ni jema au baya, kwa mfano,wizi ni jambo baya, mwizi atasema hapana, uzoefu wanguunanionesha kuwa nikiiba nakula na kustarehe bila yakuhangaika huku na huko!

Halikadhalika kutegemea hoja, akili na silka kunamatatizo kama hayo.Hapana shaka yoyote kuwa kipaji chaakili ni hazina kubwa yenye manufaa mengi na kiongozikikubwa katika maisha yetu na husaidia kuturekebishakatika namna mbali mbali. Lakini katika suala hilihaitufikishi popote. Kwanza lina zuka swali lile lile: Je,tuitegemee akili ya nani? Akili yangu au yako au ya huyuau ya yule? Au tutegemee akili ya kikundi Fulani chawatu au ya watu wote au ya watu wa kizazi hiki aukilichopita au cha baadaye?

Tatu, swali zito zaidi ni kama akili ya binaadamu pekeyake haiwezi kufanya kazi hiyo, kwa sababu lipo suala laupendeleo na chuki ambalo huipotosha akili. Athari zahisia, harara za maono, dhana za awali na sababu zakimakuzi au za kimazingira juu ya akili haziwezi kupuuzwa.Kutokana na udhaifu huu si busara kuifanya akili na silkakuwa chem chem za ujuzi juu ya mema na maovu.

3.Msimamizi wa Maadili kwa Mtizamo wa MakafiriKatika kujibu swali la tatu, “Ni nani msimamizi wa tabia

ya binaadamu?”, wanafalsafa wa kikafiri wametofautianapia.

Page 21: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

10

Kundi la kwanza linasema kuwa maadili ya jamiiyatasimamiwa na lengo tarajiwa. Yaani kama lengo kuuni “furaha” basi ni kule kupatikana kwa furaha ndikokutakako simamia maadili ya jamii.

Kundi la pili, linasema msimamizi ni kitu wanachokiita“law of practical reason”, yaani “kanuni zinazooana nahoja”. Rai hii inafanana na ile ya “Rationalism” ya kutumiaakili.

Kundi la tatu, linasema msimamizi ni serikali kwakutumia askari polisi, mahakama na magereza.

Kundi la nne, linasema msimamizi ni maoni ya watukatika jamii hiyo hiyo yaani “Social pressure”.

4.Motisha wa Kufuata Maadili kwa Mtizamo wa MakafiriKatika kujibu swali la nne, “Ni kitu gani

kinachowasukuma wawe na maadili wafuate maadili yajamii, baadhi ya wanafalsafa wanasema ni katikamaumbile ya binaadamu kutii na kuheshimu sheria. Lakinitunaona siku hizi watu wanavyoshindana kuvunja sheria!

Kundi la pili la wanafalsafa linadai kuwakinachomsukuma mtu kufuata maadili ya jamii ni kutakamalipo na kuepukana na adhabu (Reward and Punish-ment). Swali linakuja: “Ni nani anayetoa malipo au adhabuhiyo?” Wengine wanasema ni dola au serikali na wenginewanasema ni jamii anamoishi mtu.

Itadhihirika wazi kuwa majibu yanayotolewa nawanafalsafa wanaojaribu kusimamisha maadili ya jamiikwa misingi ya kikafiri yanapwaya na hutatanisha sana.Hata hivyo haina maana kuwa yote yaliyosemwa nawanafalsafa hawa ni upuuzi usiokuwa na ukweli wowote.Zipo chembe chembe za ukweli hapa na pale lakini bila

Page 22: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

11

kudhibitiwa na mfumo sahihi hoja zao zinaelea tu angani.Dosari kubwa kupita zote katika jitihada zao ni kulekumtaka binaadamu awe muadilifu bila kwanzakumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho.

Mtizamo wa Uislamu juu ya UadilifuKosa kubwa walilolifanya wanafalsafa wa kikafiri katika

jitihada za kuchunguza mwenendo wa tabia ya binaadamuni kule kuanzia utafiti wao katikati badala ya kuanziamwanzo. Kabla ya kuingia kwenye yale maswali manne,walitakiwa waulize na kuyatafutia majibu sahihi maswalimawili ya kwanza ya msingi yafuatayo:

1. Nini chanzo cha binaadamu? Yaani binaadamuametokea wapi au “Nani aliyemfanya akawepo?

2. Ni ipi hadhi na nafasi ya binaadamu katikaulimwengu huu?

Katika kujibu swali la kwanza tunajifunza katika Qur-an kuwa binaadamu ni kiumbe wa Mwenyezi Mungualiyetukuzwa:

“Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura,kisha tukawaambia malaika: “Msujudieni Adamu”Basi wakasujudu isipokuwa Ibilis hakuwa miongonimwa waliosujudu.” (7:11)

Page 23: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

12

“Na (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika,hakika Mimi nitaMuumba mtu kwa udongo mkavuunaotoa sauti; wenye kutokana na matope meusiyaliyovunda.Basi nitakapomkamilisha na kumpuliziaroho inayotokana na Mimi basi mumuangukie kwasijida (kuonyesha utii wenu)” Basi Malaikawakamsujudia wote pamoja.” (15:28-30)

Kuhusu hadhi na nafasi ya binaadamu hapaulimwenguni tunajifunza katika Qur-an kuwa yeye niKhalifa au balozi (mwakilishi) wa Mwenyezi Mungu hapaulimwenguni anayepaswa kuuongoza kwa uadilifu kwakufuata mwongozo wa yule aliyemteua kuwa balozi hapa.Kuhusu nafasi hii ya mwanaadamu Qur-aninatukumbusha:

“(Wakumbushe) wakati Mola wako alipowaambiaMalaika: ‘Mimi nitaleta Khalifa katika ardhi…” (2:30)

Ili kumuwezesha binaadamu kuchukua nafasi yakehapa ardhini, Allah (s.w) amemtunuku elimu ya mazingirayake pamoja na mwongozo utokao kwake kupitia kwa

Page 24: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

13

Mitume wake na vitabu vyake kama tulivyojifunza katikaaya zifuatazo:

“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adamu majinaya vitu vyote…” (2:31)

“Tukasema “Shukeni humo nyote, na kamaukikufikieni uongozi utokao kwangu, basiwatakaofuata uongozi wangu huo haitakuwa khofujuu yao wala hawatahuzunika.(2:38)

Lakini wenye kukufuru na kuyakadhibisha manenoyetu, hao ndio watakao kuwa watu wa motoni, humowatakaa milele.” (2:39)

Pamoja na kutunukiwa elimu na kupewa mwongozowa maisha, binaadamu pia ametiishiwa viumbe vyote,ikiwa ni pamoja na Malaika. Qur-an inazidikutukumbusha:

“Yeye (Allah) ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomokatika ardhi, ….” (2:29)

Page 25: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

14

Binaadamu kwa kupewa nafasi ya Ukhalifa nakutunukiwa elimu na vipawa vyote alivyonavyo, maishayake hapa ulimwenguni yamekuwa mtihani.

Ametukuka yule ambaye Mkononi mwake umoufalme (wote); Naye ni mwenye uweza juu ya kilakitu. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni(kukufanyieni mtihani); ni nani miongoni mwenumwenye amali nzuri. Naye ni Mwenye nguvu naMwenye Msamaha. (67:1-2)

Kwa hakika tumemuumba mtu kutokana na mbeguya uhai iliyochanganyika: (ya mwanamke namwanaume), ili tumfanyie mtihani (kwa amri namakatazo); kwa hivyo tukamfanya ni Mwenyekusikia Mwenye kuona. (76:2-3)

Binaadamu atafaulu mtihani huu kama ataishi hapaulimwenguni kama mja na khalifa wa Allah (s.w) kwakufuata na kusimamisha sheria ya Allah (s.w) ambayoitapelekea kusimamisha uadilifu katika jamii.

Page 26: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

15

Mtu, atafeli mtihani huu kama ataishi hapaulimwenguni kwa kufuata na kusimamisha sheriazilizotungwa na watu zinazopelekea ulimwengu kuwauwanja wa fujo na vurugu.

Matokeo ya mtihani huu hayatatangazwa katika maishayetu ya hapa duniani bali yatatolewa baada ya watu wotekumaliza makazi yao hapa duniani na baada ya mema namaovu yao kujidhihirisha kikamilifu. Ni katika wakati huoambapo Allah (s.w) atamhesabu kila mtu na kuamua niyupi alitimiza wajibu wake kama Khalifa wake hapaulimwenguni na yupi ambaye hakutimiza. Hisabu hiyohaitahusu jambo moja maalumu au kipengele fulani tubali itahusu maisha yote ya binaadamu ya kibinafsi nakijamii. Itahusu pia vipawa vyake vyote vya mwili na akilina amana yoyote aliyopewa juu ya watu au vitu.

Kwa mtizamo wa Uislamu, Ufalme ni wa Allah (s.w)peke yake na binaadamu ni khalifa wake tu, hivyo njiapekee ya uadilifu inayompasa binaadamu ni kutekelezawajibu aliopewa na Allah (s.w). Hana uhuru wa kuamuaapendavyo upi uwe mwenendo wake wa tabia, bali kipimocha lipi jema na lipi ovu lazima kichukuliwe kutoka kwaAllah (s.w), wajibu wa binaadamu ni kutekeleza kwaukamilifu na uaminifu wajibu aliokabidhiwa na Muumbawake.

Maadili ya jamii hayatabuniwa na binaadamu baliutachukuliwa kutoka kwa Allah (s.w) ambaye ndiyeMuumba na mpangaji wa sheria. Binaadamu hanabudikuishi na kutenda kulingana na maamrisho na sheria yaAllah (s.w). Uhusiano huu uliopo kati ya Allah (s.w) nabinaadamu utakapo eleweka, yale maswali manne yawanafalsafa wa kikafiri, kuhusiana na Maadili ya jamii,yatapata majibu yaliyowazi na yanayotua akilini.

Page 27: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

16

Majibu ya maswali manne yanavyotolewa na UislamuPindi mtu akiikubali nafasi ya uja na ukhalifa aliyopewa

binaadamu na Muumba wake, maswali makuu manne yawanafalsafa wa kikafiri, juu ya mwenendo wa tabia yabinaadamu, yanajibiwa na Uislamu kwa wepesi kamaifuatavyo:

1.Lengo Kuu la Maisha kwa Mtizamo wa UislamuKufuzu mtihani wa Allah (s.w) na kupata radhi zake ndiyo

lengo kuu la maisha ya binaadamu hapa duniani. Atafuzumtihani wa Mola wake, endapo binaadamu atajitahidi kutiisheria za Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha yakebinafsi na kujitahidi kusimamisha sheria hizo katika jamii.Yaani binaadamu atafuzu kwa kufanya biashara na Allah(s.w) kama inavyobainishwa katika aya zifuatazo:

Enyi mlioamini! Je! Nikujulisheni biasharaitakayokuokoeni na adhabu iumizayo?(Biasharayenyewe ni hii):Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtumewake na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa malizenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu; ikiwa mnajua.(61:10-11)

Page 28: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

17

(Mkifanya haya) atakusameheni dhambi zenu naatakuingizeni katika mabustani yapitayo mito mbeleyake na (atakupeni) maskani mazuri mazuri katikaBustani za milele; Huku ndiko kufuzu kukubwa”(61:12)

“Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waislamu nafsizao na mali zao ili naye awape Pepo. Wanapiganakatika njia ya Mwenyezi Mungu; wanaua nawanauawa. Hii ndiyo ahadi aliyojilazimisha(Mwenyezi Mungu) katika Taurati, Injili na Qur-an.Na ni nani atekelezaye zaidi ahadi yake kulikoMwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenumliyofanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.”(9:111)

2.Chem chem ya Ujuzi wa Wema na Uovu kwa Mtizamowa Uislamu

Chem chem za kweli anazoweza kuzitegemeabinaadamu katika kutambua mema na maovu ni Allah(s.w) kupitia kwa Mitume na vitabu vyake.

Page 29: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

18

“Kwa hakika tumewapeleka Mitume wetu kwa daliliwazi wazi na tukaviteremsha vitabu na uadilifupamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu……” (57:25)

3.Msimamizi wa Maadili kwa Mtizamo wa UislamuMsimamizi wa mwenendo wa tabia njema inayompeleka

binaadamu kwenye kusimamisha uadilifu ni Imani thabitijuu ya Allah (s.w) na Siku ya mwisho (siku ya malipo) najuu ya vipengele vingine vya nguzo sita za imani yaKiislamu. Muumini wa kweli hana hiari ya kwendakinyume na maamrisho na makatazo ya Allah (s.w) naMitume wake.

“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwamwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wakewanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao.”(33:36)

4.Motisha inayowapelekea Waislamu kusimamishaUadilifu katika jamii

Kinachowachochea Waislamu kuwa na tabia ya kufanyamema na kuacha maovu, na kisha kuamrisha mema nakukataza maovu katika jamii ni matarajio ya kupata radhiza Mwenyezi Mungu na kukhofia ghadhabu zake. Matokeoya kupata radhi za Allah (s.w) na kuepuka ghadhabu zake

Page 30: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

19

ni kuepukana na maisha ya huzuni na hofu hapa dunianina kupata maisha ya furaha na amani ya milele hukoakhera.

Majibu haya yanayotolewa na Uislamu yanatanzuautatanishi wote uliokuwepo katika majibu yaliyotolewa nawanafalsafa wa kikafiri juu ya maadili.

Page 31: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

20

Zoezi la Kwanza

1. Taja vipawa alivyotunukiwa Mwanadamuvinavyomtafautisha na wanyama.

2. Bainisha makusudio ya Allah (sw) yanayotarajiwakufikiwa na mwanadamu aliyetunukiwa vipawa hivi.

3. Ng’amua na kubainisha sababu kubwa mbili zilizopelekeamakafiri wasiafikiane, wala kufaulu kudhihirisha lengohalisi la maisha ya mwanadamu hapa duniani.

4. Eleza kwa kutoa mifano hai, upogo na udhaifu uliopokatika dhana za makafiri juu ya maadili na uadilifu katikamawanda manne.

5. Ukiondoa suala la Qadar, taja misingi mitanoiliyobainishwa ndani ya Qur’an ambayo ndiyo mihimilimikuu ya maadili mema ya Kiislamu.

6. Tumia Qur’an kujibu kwa ufasaha wa kukinaisha ,maswali manne ya makafiri juu ya misingi ya Maadili nauadilifu.

7. (a) Nini maana ya Maadili? (b) Wakati wanyama huongozwa na silka, wanadamu wana Maadili, kwanini?

8. Kwanini mtu asiyemuamini Allah na siku ya mwisho,hawezi kufanya wema muda wote au kuacha maovukabisa?

Page 32: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

21

Sura ya Pili

UTAMADUNI

Uislamu ni utaratibu kamili wa maisha uliofumwa naAllah (s.w) unaoelekeza namna Muumini anavyowezakukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kila siku ilikumuwezesha kuishi kwa furaha na amani na kufikia lengola maisha yake hapa ulimwenguni. Miongoni mwa vipengelemuhimu vya maisha ambavyo jamii ya mwanaadamu hainabudi kuviendea ni kipengele cha utamaduni au mila nadesturi za jamii. Sio kila mila na desturi za jamii zinamfikishamwanaadamu katika lengo la maisha yake hapa dunianikwa furaha na amani.

Ukichunguza tamaduni za jamii mbali mbali utagunduakuwa tamaduni hizo hazimuinui mwanaadamu nakumfikisha katika kilele cha hadhi yake, bali kinyume chakehuiteremsha hadhi yake na kuifanya duni kuliko ile yawanyama.Ni utamaduni wa Kiislamu pekee unaomuinuamwanaadamu na kumbakisha katika kilele cha hadhi yaketukufu ya Ukhalifa wa Allah (s.w), kwa vile utamaduni huuumefumwa na Mwenyewe Sub-haanahu Wata’aala, Mjuziwa kila kitu, Mwenye hekima.

Utamaduni wa MuislamuWaislamu tumehimizwa katika Qur-an kuwa tusifuate

utamaduni mwingine au mila nyingine isiyokuwa ile milaya Nabii Ibrahim (a.s) kama tunavyojifunza katika ayazifuatazo:

Page 33: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

22

Na nani atakayejitenga na mila ya Ibrahim isipokuwaanayeitia nafsi yake katika upumbavu. Na kwayakini sisi tulimchagua (Ibrahimu) katika dunia, nakwa hakika yeye katika akhera atakuwa miongonimwa watu wema kabisa. (2:130)

Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule ambayeameuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, nayeni mwema, na anafuata mila ya Ibrahim (kuwaMuislamu kweli kweli).Na Mwenyezi Munguamemfanya Ibrahim kuwa kipenzi chake. (4:125)

Mila ya Ibrahim (a.s) iliyosisitizwa katika aya hizi sinyingine zaidi ya ile ya kumpwekesha Allah (s.w) na kujitupakwake kwa utii na unyenyekevu.Yaani mila ya Ibrahimu(a.s) ni kuufuata Uislamu kwa ukamilifu kwa kutii kwaunyenyekevu maamrisho yote ya Allah (s.w) na kujitengakwa utii na unyenyekevu na yale yote aliyoyakataza (s.w).Mwenendo huu wa Nabii Ibrahiim ambao tunasisitizwatuufanye utamaduni wetu uko bayana katika Qur-an:

(Kumbukeni) Mola wake (Ibrahim) alipomwambia Silimu(jisalimishe kwa unyenyekevu), akanena:“Nimejisalimisha kwa Mola wa Ulimwenguwote”.(2:131)

Page 34: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

23

Na Ibrahim akawausia haya wanawe na Yaaqubu (piaakawausia wanawe): Enyi wanangu! Hakika MwenyeziMungu amekuchagulieni dini hii, basi msife ila nanyimmekuwa Waislamu (wanyenyekevu kwa Allah (s.w).(2:132).

Tunajifunza katika aya hizi kuwa hatua ya kwanza yakufuwata mila ya Ibrahim ni sisi wenyewe kujisalimishakikweli kweli kwa Allah (s.w) kwa kufuata maamrishoyake yote na kuacha makatazo yake yote. Hatua ya pili yakufuata mila ya Ibrahimu ni ile ya kuwahimiza ahali zetukuwa Waislamu wa kweli wenye kufuata mwenendo wamaisha anaoridhia Allah (s.w) katika kuendea kilakipengele cha maisha yao ya kila siku.

Pia aya zifuatazo zinatubainishia kwa uwazi mwenendowa Nabii Ibrahimu (a.s) ambao tunahimizwa tuuige natuufanye ndio mila yetu:

Hakika Ibrahimu alikuwa kiongozi (mfano mzuri wa kuigwa)mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu mtii kamili, walahakuwa miongoni mwa washirikina.(Alikuwa) mwenyekushukuru neema zake (Allah).(Mwenyezi Mungu)akamchagua na kumuongoza katika njiailiyonyooka.(16:120)

Na tukampa wema katika dunia; na hakika yeye katikaakhera atakuwa miongoni mwa watu wema (pia).(16:122).

Page 35: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

24

Nabii Ibrahim (a.s) alikataa kata kata mila ya jamiiyake na akawahakikishia kwa maneno na matendo kuwayeye ni Muislamu na si miongoni mwa washirikina:

Mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumbambingu na ardhi. Hali ya kuwa nimeacha dini yaupotofu. Mimi (ni Muislamu) si miongoni mwa washirikina.(6:79).Vile vile Muislamu wa kweli anayefuata vilivyo mila ya

Ibrahimu (a.s) hana budi kuuhakikishia ulimwengu kwamaneno na matendo kuwa yeye ni Muislamu katika halizote na si miongoni mwa washirikina.Msimamo waMuislamu wa kweli ni huu ufuatao:

Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu ameniongozakatika njia iliyonyooka, katika dini iliyo sawa kabisaambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliyekuwa muongofu, wala(kabisa) hakuwa miongoni mwa washirikina.”(6:161)

Sema: “Hakika swala yangu na Ibada zangu (nyinginezote) na maisha yangu na kufa kwangu (vyote) ni kwaajili ya Mwenyezi Mungu.Bwana (Rabii) wa walimwenguwote.(6:162)

Page 36: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

25

Hana mshirika wake. Na haya ndiyo niliyoamrishwana mimi ni wakwanza wa waliojisalimisha”. (6:163).

Tumejifunza kutokana na aya hizi kuwa mila yaMuislamu ni Uislamu. Yaani Muislamu wa kweli hanamila nyingine isiyo kuwa ile ya kufuata vilivyo mwenendowa kujisalimisha kwa Allah (s.w) kwa kila kipengele chamaisha.

Vipengele vya Utamaduni wa KiislamuTumejifunza kuwa utamaduni wa Kiislamu ni mwendo

wa maisha unaofuata bara bara misingi ya Uislamu kwakuchunga vilivyo mipaka ya Allah (s.w) katika kukiendeakila kipengele cha maisha. Hivyo kila kipengele cha maishaya jamii ya Kiislamu ni kipengele cha utamaduni waKiislamu.

1.Tabia njemaMuislamu wa kweli ni yule anayejitahidi kwa kadri

ya uwezo wake kujipamba na tabia njema. Tabia njemandio mwenendo wa Mitume wa Allah (s.w) ambaotumeamrishwa tuigize mwenendo wao hatua kwa hatua.Msisitizo wa kufuata mwenendo wa Nabii Ibrahim (a.s)tumeshauona na pia tusisahau msisitizo wa kuigizamwenendo wa Mtume (s.a.w) unaobainishwa na ayaifuatayo:-

Page 37: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

26

Bila shaka mnao mfano mwema (kiigizo chema) kwaMtume wa Allah, kwa mwenye kumuogopa Allah (s.w)na siku ya mwisho na mwenye kumkumbuka Allah (s.w)kwa wingi. (33:21).

Mtume (s.a.w) ambaye tunatakiwa tumuigize alikuwani mwenye tabia nzuri kweli kweli kama Mola wakeanavyomsifu katika Qur-an:

Na bila shaka unatabia njema kabisa (68:4).

Mtume mwenyewe katika kuwasisitiza Waislamukujivisha vazi zuri la tabia njema amesema:

Aliye mbora kuliko wote miongoni mwenu ni yule aliyewazidi kwa tabia njema. (Bukhari na Muslimu).

Pia Mtume (s.a.w) amebainisha ubaya wa mtu kuwana tabia mbaya aliposema:

Yule ambaye tabia yake ni mbaya na katili (harsh)hataingia Peponi. (Abu Daudi).

Vipengele vya tabia njema ambavyo kila Muislamuanahimizwa ajivishe na kujipamba kwavyo vimebainishwakwa uwazi katika Qur-an na Hadith (Rejea Juzuu ya 2 na3) na kwa muhtasari Muislamu wa kweli anatakiwa afanyekila jambo kwa ajili ya Allah (s.w) na awe mwenyekumkumbuka Allah (s.w) kila wakati awe mwema namwenye kuwahurumia wanaadamu wenziwe na viumbewengine, awe mwepesi wa kutoa msaada wa hali na mali,awe mwenye kumuheshimu kila mtu, awe mwenyekuongea maneno mazuri na kwa upole awe ni mwenye

Page 38: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

27

kujizuia na hasira na kuwavumilia wengine, awe mwenyesubira na mwepesi wa kusamehe wengine kwa ajili yaAllah (s.w), awe mwenye kutoa haki za wengine na awejasiri na mwenye msimamo katika kutetea haki za wenginena katika kusimamisha haki katika jamii, awe tayari kutoanafsi yake na mali yake kwa ajili ya kusimamisha Uislamukatika jamii, awe mwenye kukinai, awe mkarimu, awemwenye kujitahidi kujipamba na tabia njema nyinginezoambazo huzaa mahaba, furaha na amani katika jamii naawe mwenye kujiepusha na maneno na matendo yotemaovu ambayo huzaa bugh-dha, chuki, uadui na vurugukatika jamii ya mwanaadamu.

Wazazi wa Kiislamu na wahusika na taasisi zote zaKiislamu zinazohusika na malezi ya watoto, wanayodhimakubwa ya kuwalea vijana wa katika maadili haya mema.Ni vyema tukumbushane Waislamu wote kuwa suala lakuwalea vijana wetu katika maadili ya Kiislamu ni sualala msingi na la muhimu kuliko shughuli nyingine yoyoteile tutakayowafanyia vijana hawa. Amesema kweli Mtumewa Allah aliposisitiza:

Hapana zawadi yoyote atakayoitoa baba kumpakijana wake itakayozidi kumfunza tabia njema.(Tirmidh).

Waislamu, tutakapoacha kuchukua dhima hii yakuwalea vijana wetu katika mila ya Ibrahim na badalayake tukawaachia walelewe katika mila za kitwaaghutitutakuwa tumewapoteza vijana wetu na tutakosa wakuwarithisha katika uongozi wa kusimamisha Uislamukatika jamii. Tunawajibika kuwarithisha watoto wetuutamaduni wa Kiislamu kama alivyofanya NabiiIbrahim(a.s)

Page 39: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

28

Na Ibrahimu akawausia haya wanawe na Yaaqubu(mjukuu wake na kuwaambia) Enyi wanangu! HakikaMwenyezi Mungu amekuchagulieni dini hii; basi msifeila nanyi mmekuwa Waislamu”. (2:132)

Waislamu kamwe tusitarajie kuwa Uislamuutasisimama katika jamii yetu bila ya kuwalea vijana wetukatika maadili ya Kiislamu pamoja na kuomba msaadawa Allah(s.w) atuwezeshe kufanya kazi hii kamaalivyotufundisha kuomba katika Qur-an:

Mola wetu! Tupe katika wake zetu na watoto wetuyatuburudishayo macho (yetu – nyoyo zetu) na utujaalietuwe viongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu. (25:74).

2. Vazi la KiislamuVazi la Kiislamu ni sehemu ya utamaduni wa Kiislamu.Vazi la Kiislamu ni lile vazi linalositiri uchi kwa mujibuwa sheria ya Kiislamu. Lengo la vazi kwa jamii yamwanaadamu linabainishwa katika Qur-an:

Enyi wanaadamu! Hakika tumekuteremshieni nguozifichazo tupu zenu na nguo za pambo na nguo za ucha-Mungu ndizo bora. Hiyo ni katika ishara za MwenyeziMungu ili mpate kukumbuka. (7:26)

Page 40: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

29

Kama inavyobainishwa katika aya hii lengo kuu la vazila Kiislamu ni kusitiri awrah (uchi). Vazi la Kiislamu nilile linalotekeleza masharti yafuatayo:

(a) Vazi lisitiri Awrah (uchi)Awrah ya mwanamke ni mwili mzima isipokuwa uso

na viganja vya mikono kwa mujibu wa kauli ya Mtume(s.a.w) aliposema:

Mwanamke atakapofikia baleghe hataacha wazisehemu yoyote ya mwili wake isipokuwa uso naviganja (Abu Daud).

Amri ya kujisitiri kwa wanawake inabainishwa katikaaya zifuatazo:

Page 41: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

30

Na waambie Waislamu wanawake wainamishe ma-cho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirisheviungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika (uso naviganja). Na waangushe shungi zao mpaka vifuanimwao na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waumezao au baba zao, au baba za waume zao, au watotowao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wanawa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawakewenzi wao, au wale iliyowamiliki mikono yao yakuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanioau watoto ambao hawajajua mambo yaliyohusu uke.Wala wasipige miguu yao ili yajulikanewanayoyaficha katika mapambo yao. Na tubieni nyotekwa Mwenyezi Mungu, enyi Waislamu ili mpatekufaulu. (24:31).

Page 42: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

31

Ewe Mtume! Waambie wake zako na binti zako, nawanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao.Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane (kuwa niwatu wa heshima ili) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Munguni mwingi wa kusamehe (na) mwingi wa kurehemu.(33:59).

Pamoja na mwanamke kuamrishwa kujifunika mwilimzima isipokuwa uso na viganja, pia katika aya hizianaamrishwa:

- Ateremshe shungi mpaka kifuani. Shungi nikitambaa (mtandio) kinachofunika kichwa, shingona kifua.

- Asidhihirishe mapambo yake na- Asitingishe miguu yake na viungo vyake vingine kiasi

cha kujulisha aliyoyaficha katika mapambo.

Awrah ya mwanaume ni sehemu yote iliyo kati yakitovu na magoti kwa mujibu wa kauli ya Mtume (s.a.w)aliposema:

Sehemu yoyote iliyo juu ya magoti haina budi kufunikwana sehemu yoyote iliyo chini ya kitovu haina budikufunikwa. (Darqutny).

Mwanamume hana budi kufunika ile sehemu ya mwiliwake iliyo kati ya kitovu na magoti. (Al-Mabsuut).

Ni haram kwa Muislamu mwanamume kuvaa bukta aukaptura nje ya chumbani kwake.

(b) Vazi lisibaneVazi la mwanamke au mwanamume lisibane kiasi cha

kuonyesha mchoro wa sehemu za mwili zinazotakiwazisitiriwe.

Page 43: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

32

(c) Vazi lisiwe lenye Kuonyesha (transparent)Mwenye kuvaa vazi linaloonyesha rangi ya mwili

anahesabika kuwa yuko uchi kama tunavyojifunza katikaHadith zifuatazo:

Hafsa bint Abdur-Rahman, alikuja kwa Aysha (r.a) akiwaamevaa shungi inayoonyesha kichwa chake na mabega.Aysha aliichana chana na kumfunika shungi nzito. (ImamMalik)

Mtume (s.a.w) amesema: Allah amewalaani wanawakewaliovaa nguo na huku bado wako uchi.

(d) Vazi Lisiwe Lenye KuvutiaWanawake wameamrishwa kufunika mwili mzima ili

kuficha uzuri wao wa asili (natural beuty) na mapamboyao ili wasiyavute matamanio ya wanaume. Ni katikamsingi huu pia wanawake wa Kiislamu hawaruhusiwikuvaa vazi linalovutia sana nje ya nyumbani kwake. Nikatika msingi huu pia wanawake wa Kiislamuhawaruhusiwi kutoka majumbani mwao ila kwa dharurakama inavyosisitizwa katika Qur-an:

Ni mwenendo wa kitwaghuti kwa wanawake kutokatokamajumbani mwao ovyo na kuonyesha ovyo mapambo yaoikiwa ni pamoja na mavazi yanayovutia.

(e) Vazi la mwanamke lisifanane na la mwanamumena kinyume chake

Ni haramu kwa mwanamume kuvaa mavazi yawanawake na pia ni haramu kwa wanawake kuvaa mavaziya wanaume. Katika Hadith iliyosimuliwa na Ibn Abbas,Mtume (s.a.w) amewalaani wanaume wanaoigiza mavazina tabia za kike na wanawake wanaoigiza mavazi na tabiaza kiume.

(f) Vazi lisiwe kiigizo cha vazi la wasiokuwa WaislamuNi haramu kwa Muislamu kuigiza mavazi ya wasiokuwa

Page 44: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

33

Waislamu. Hii ni kwa sababu Waislamu wanao utamaduniwao ambao ni tofauti na wa watu wengine. Muislamuanatakiwa atambulikane, ili kwa mfano aweze kusalimiwana Waislamu wenziwe kwa “Assalaam Alaykum” maamkiziya Kiislamu waliyoyatumia mitume wote na wafuasi waona ndiyo yatakayo kuwa maamkizi ya Peponi. Kuamkianahuko hakutawezekana kwa mfano iwapo Waislamuwanaona haya kuvaa vazi litakalowatambulisha kuwa niWaislamu.

Matokeo yake ni kwamba utamaduni wao utapotea nawao kumezwa katika utamaduni wa kijahili. Muislamanatakiwa ajirekebishe haraka iwapo kwa mavazi yakewatu wanashindwa kumtofautisha na kafiri au mtu wautamaduni mwingine. Ni aibu ilioje kwa Muislamu kujikutaanaambiwa na mtu mwingine: “Mimi siku zote hizi sikujuakama wewe ni Muislamu”. Tunafahamishwa katika Hadithiiliyosimuliwa na Ibn Umar kuwa Mtume (s.a.w) amesema:

Atakaye waigiza watu, atahusikana nao (atakuwa pamojanao). (Ahmad, Abu-Daud).

(g) Vazi lisiwe la majivuno na kujifaharishaVazi linalompelekea mtu kwenye majivuno na

kujifaharisha ni vazi haram, na limekemewa vikali naMtume (s.a.w) kama tunavyojifunza katika Hadithizifuatazo:

Ibn Umar ameeleza kuwa atakaye ning’iniza suruali yakekwa kujifaharisha, Allah (s.w) hatamwangalia siku yakiyama. (Bukhari na Muslim).

Ibn Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:“Avaaye vaa vazi la fahari katika ulimwengu huu, Allah(s.w) atamvisha vazi la huzuni (hizya) siku ya kufufuliwa”.(Tirmidh, Ahmed, Abu Daud, Ibn Majah).

Page 45: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

34

(h) Vazi lisiwe chafu na la kudhalilishaKinyume cha kujifaharisha ni kujidhalilisha. Ni haramkwa Muislamu kuvaa vazi linalo mdhalilisha. Muislamuanatakiwa ale vizuri na kuvaa vizuri ila tu asijifaharishewala asifanye israfu. Allah (s.w) ametuamrisha kutangazaneema zake:

“Na neema za Mola wako zisimulie” (93:11).

Ni katika kushukuru na kutangaza neema za Allah(s.w) kwa mtu kuvaa vizuri na kula vizuri na kwa kadri yauwezo wake. Pia tunajifunza hili katika Hadith ifuatayo:

Amr bin Shuaib amesimulia kutoka kwa baba yake,kutoka kwa babu yake kuwa Mtume wa Allah amesema:“Hakika Allah anapenda kuona matokeo ya neema zakekwa mja wake”. (Tirmidh).

Yaani Allah (s.w) hampendi mtu ambaye ingawaamemneemesha bado anaendelea kuishi katika hali ileile duni kama kwamba hakuneemeshwa neema yoyote.Pia Waislamu wanahimizwa wajenge tabia ya usafi naumaridadi wa miili yao na nguo zao kama tunavyojifunzakatika Qur-an:

Na nguo zako uzitakase. (74:4).

“Na Mwenyezi Mungu anawapenda wajitakasao”.(9:108)

“Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu nahuwapenda wanojitakasa”. (2:222).

Page 46: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

35

Kujitakasa katika aya hizi, hakuishii kwenyekujitakasa nafsi tu bali ni pamoja na kujitakasa mwili,nguo na matendo.

Jabir anasimulia: Mtume (s.a.w) alipokuja kutuonaalimkuta mtu mwenye nywele nyingi zisizochanwa,kisha Mtume akasema: Huyu mtu hajapata kitu chakuchania kichwa chake! Na alimuona mtu aliyevaa nguochafu, kisha akasema: Huyu mtu hajapata kitu (maji) chakufulia nguo zake! (Ahmad, Nisai)

Unadhifu ni katika utamaduni wa Kiislamu. Mtume(s.a.w) amehimiza:

“Uislamu ni nadhifu, basi jinadhifisheni”.

Kwa ajili ya unadhifu Mtume (s.a.w) alipendelea sanavazi jeupe kama inavyobainika katika Hadith zifuatazo:

Abu Dard’a amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema:Hakika vazi bora ambalo waweza kuwa nalo katikakukutana na Mola wako kaburini au msikitini ni vazi jeupe.(Ibn Majah).

Samurah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Vaavazi jeupe kwa sababu ni safi na linapendeza, nalifanyeni sanda kwa ajili ya maiti wenu. (Ahmad,Tirmidh, Nisai).

(i) Vazi la hariri limeharamishwa kwa wanaumeNi haramu kwa wanaume kuvaa nguo za hariri au

mapambo ya dhahabu na fedha kwa mujibu wa Hadithzifuatazo:

Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema:“Hakika anayevaa nguo za hariri katika ulimwengu huuhatakuwa na kitu katika siku ya Malipo”.(Bukhari na Mus-lim).

Page 47: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

36

Hudhaifa amesimulia “Mtume wa Allah ametukatazakutumia vyombo vya dhahabu na fedha na piaametukataza vazi la hariri hata kukaa juu yake”. (Bukharina Muslim).

Bali wanawake wameruhusiwa kuvaa nguo za haririna kuvaa mapambo ya dhahabu na fedha ila tu wachungemipaka iliyowekwa:

Abu Mussa anaeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:“Dhahabu na hariri vimefanywa halali kwa wafuasiwangu wanawake na wamefanywa halali kwa wafuasiwangu wanaume” (Tirmidh, Nisai)

Pia vazi jekundu (sio lenye mistari au michirizimyekundu)limeharamishwa kwa wanaume.Tunafahamishwa katika Hadith kuwa:

Abdullah bin Amr amesimulia:“Mwanamume mmojaaliyevalia vipande viwili vya nguo nyekundu alipita naakamsalimia Mtume, lakini Mtume hakuitikia salam hiyo”(Tirmidh, Abu Daud).

(j) Wanaume wamekokotezwa kuvaa kofiaWanaume wamehimizwa sana kuvaa kitu cha kufunika

kichwa iwe kofia au kilemba. Katika Hadith iliyo nukuliwana Baihaq na Tirmidh, Mtume (s.a.w) amesema kuwakufunika kichwa kwa kilemba ni katika mwenendo waMalaika. Ikumbukwe kuwa kwa wanawake kufunikakichwa si jambo la kupendeza tu bali ni wajibu. Mwanamkeakiacha kichwa wazi hatakama amefunika sehemunyingine yote ya mwili atahesabika kuwa yuko uchi naakitembea hivyo mbele ya wanaume wasio maharimuwake, laana ya Allah (s.w) itakuwa juu yake.

Huu ndio utamaduni wa Kiislamu ambao kila Muislamuwa kweli analazimika kujiambatanisha nao. Utamaduni

Page 48: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

37

mwingine wowote utakaompelekea Muislamu kuvaakinyume na vazi la Kiislamu utakuwa ni utamaduni waKijahili au wa shetani. Allah (s.w) anatuhadharisha naShetani katika aya ifuatayo:

Enyi wanaadamu! Shetani asikutieni katika matata,kama alivyowatoa wazee wenu katika pepo akawavuanguo zao ili kuwaonyesha tupu zao. Hakika yeye pamojana kabila yake wanakuoneni, na hali ya kuwa nyinyihamuwaoni. Bila shaka sisi tumejaalia mashetani kuwamarafiki wa wale wasioamini. (7:27).

3. Miiko katika kula na kunywaHata kula na kunywa katika Uislamu kuna miiko yake.

Muislamu wa kweli hatakula na kunywa tu bila kuchungamiiko na kufuate utaratibu uliowekwa. Mwongozo wa kulana kunywa uko bayana katika Qur-an. Hebu turejee ayazifuatazo:

Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuriwala msifuate nyayo za shetani, bila shaka yeye kwenuni adui dhahiri. (2:168).

Page 49: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

38

Enyi mlioamini! Kuleni vizuri tulivyokuruzukuni, namumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa mnamuabuduyeye peke yake. (2:172).

“… Na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri). Lakini msipitekiasi tu.Hakika yeye (Mwenyezi Mungu) hawapendiwapitao kiasi”. (7:31).

Katika aya hizi Allah (s.w) anatuagiza kuwa:(i) Tule vilivyo halali na vilivyopatikana kwa chumo halali.(ii) Tule vizuri tuvipendavyo kwa kadiri ya uwezo wetu.(iii) Tusifanye ubadhirifu katika kula na kunywa.(iv) Tumshukuru Yeye kwa vile alivyotuneemesha, kwakufuata maamrisho yake kwa utii na kuchunga mipakayake kwa unyenyekevu katika maisha yetu ya kila siku.

Wanaokula na kunywa bila kufuata mazingatio hayawanakuwa hawatofautiani kabisa na wanyama.Qur-aninasema:

Lakini waliokufuru hujifurahisha (hapa duniani) na kulakama walavyo wanyama, na moto ndio makazi yao.(47:12)

Page 50: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

39

Vyakula vilivyo haramishwaVyakula vyote visivyo haramishwa katika Qur-an na

Hadith ni halali. Vyakula vilivyoharamishwa katika Qur-an:

Mnaharamishiwa nyamafu na damu na nyama yanguruwe na mnyama aliyechinjwa si kwa ajili ya Allah,na kilichokufa kwa kusongeka koo, na kilichokufa kwakupigwa, na kilichokufa kwa kuanguka, na kilichokufakwa kupigwa pembe (na wanyama wengine), naalichokila mnyama ila mkiwahi kukichinja. Na (piammeharamishiwa) kilichochinjwa panapo fanyiwa Ibadaisiyokuwa ya Mwenyezi Mungu (kama mizimu)… (5:3).

Aya hizi za Qur-an pamoja na (6:145) zinatupatiamafunzo yafuatayo juu ya vyakula vilivyoharamishwa:

1. Mnyama aliye kufa bila ya kuchinjwa kwa sababuyoyote iwayo (mzoga).

2. Mnyama asiyechinjwa kwa jina la Allah –Tumeamrishwa katika Qur-an:

Basi swali kwa ajili ya Mola wako na uchinje (kwa ajiliya Mola wako). (108:2).

Page 51: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

40

Kutokana na amri hii si halali kula nyama ya mnyamaaliyechinjwa na Kafiri, Mshirikina au yeyote asiye MuaminiAllah (s.w) na Upweke wake. Nyama itakuwa halali iwapomchinjaji ni Muislamu atakaye chinja kwa jina la Allah –Bismillah Allahu Akbar na atakayezingatia masharti yakuchinja ya kumkata mnyama koo (shingo) kwa kisu kikaliau kitu chochote cha kukatia kilicho kikali.

Muislamu yeyote awe mtoto, mwanamume aumwanamke katika hali yoyote anaruhusiwa kuchinja. Walahapana suala la kupewa kisu na Sheikh.

3. Mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya matambiko,mashindano, n.k. mnyama huyo maadam kusudiola kuchinjwa kwake ni kumshirikisha Allah (s.w)nyama yake ni haramu kuila hata kama mwenyekuchinja anajiita Muislamu na ametaja jina la Al-lah wakati wa kuchinja.

4. Nyama ya nguruwe.

5. Damu inayomwagika – damu inayobakia kwenyenyama si haramu.

Vyakula vilivyoharamishwa katika Hadith6. Wanyama na ndege wote wanaowinda wengine kwa

makucha na meno au midomo yao ni haramu kulanyama yao kwa mnasaba wa Hadith zifuatazo:

Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allahamesema:“Kila mnyama awindae kwa meno ni haramukuliwa” (Muslim)

Ibn Abbas ameeleza kuwa Mtume wa Allah aliharamishakila mnyama awindaye kwa meno na kila ndegeanayewinda wengine kwa kucha. (Muslim)

Page 52: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

41

Wanyama wanaowinda kwa meno na kucha ni kamasimba, chui, paka, fisi, vicheche, mbwa mwitu, n.k.

Ndege wanao winda kwa makucha ni kama tai,mwewe, kipanga, n.k.

7. Nyama ya punda wa nyumbani, farasi na nyumbuni haramu kwa mnasaba wa Hadith ifuatayo

Khalid bin Walid ameeleza kuwa Mtume wa Allahameharamisha nyama ya farasi, nyumbu na punda wanyumbani. (Abu Daud, Nisai).

Bali nyama ya punda milia ni halali kamatunavyofunzwa katika Hadithi ifuatayo:

Abu Watadah ameeleza kuwa alimchinja pundamilia(punda wa porini). Mtume (s.a.w) akamuuliza:Unachochote katika nyama yake?” Alijibu: Tuna miguumiwili ya nyuma. Kisha alichukua na kula. (Bukhari naMuslim).

8. Nyama ya wanyama wachafu wenye kuathiri mwilina utu kama nguruwe, mbwa, paka, n.k.

Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allahameharamisha nyama na maziwa ya wanyama wachafu.(Tirmidh).

9. Ni haramu kula nyama ya mjusi na jamii yote yamijusi:

Abdul-Rahman bin Shibl amesimulia kuwa Mtume (s.a.w)ameharamisha nyama ya mijusi. (Abu Daud).

Page 53: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

42

10.Nyama ya paka ni haramu:Jabir amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) ameharamishanyama ya paka na kumpiga bei.

11.Nyama ya kiungo cha mnyama kilichokatwamwenyewe akiwa yungali hai kama vile mkia wakondoo, mguu wa mnyama uliokatika kwa ajali, n.k.ni haramu kwa mnasaba wa Hadith ifuatayo:

Abu Waqidil Laysi ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alikujaMadina akawakuta wanapenda nundu za ngamia nakukata mikia ya kondoo. Mtume (s.a.w) akasema: “Kilekilichokatwa kwa wanyama wakingali hai ni mzoga. Niharamu kuliwa”. (Tirmidh, Abu Daud).

12. Ni haramu kula wadudu isipokuwa nzige kwamujibu wa Hadith ifuatayo:

Ibn Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:Mizoga ya aina mbili na damu za aina mbili, vimefanywahalali kwetu: Mizoga ya samaki na nzige na damu yamaini na wengu. (Ahmad, Ibn Majah, Darqutni).

Hivi ndivyo vyakula vilivyo haramishwa katika Qur-anna Hadith lakini Muislamu atakaposongwa na njaa ya kufana kupona na pakawa hapana njia yoyote ya kupatachakula, ameruhusiwa kula haramu kiasi kidogo chakumuwezesha kuishi na wala asile kwa kufurahia kamatunavyojifunza katika Qur-an:

“… Lakini aliyelazimika (kula kwa ajili ya njaa, n.k.)pasipokupenda wala kwa kuvuka mipaka, basi,Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na mwingiwa kurehemu. (6:145)

42

Page 54: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

43

Vinywaji vilivyoharamishwaVinywaji vyote vinavyolevya (intoxicants)

vimeharamishwa hata kuonja.

Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa(na kuombwa) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, nakutazamia kwa mishale ya kupigia ramli (na kwavinginevyo); (yote haya) ni uchafu (ni) katika kazi yashetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufaulu(kutengenekewa). (5:90)

Ulevi, kamari, kumshirikisha Allah na kutazamia nimatendo yanayoivuruga jamii na kuifarikisha:

Hakika shetani anataka kukutieni uadui na bughudhabaina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari na anatakakukuzuilieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na(kukuzuilieni) kuswali. Basi je, hamtaacha haya)? (5:91).

Vinywaji vyote vinavyolevya na vilivyo najsi kama viledamu, mkojo, n.k. vimeharamishwa kunywewa hata kwadawa kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

Page 55: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

44

Waili al-Hadhrami ameeleza: Tariqa bin Suwaidalimuuliza Mtume (s.a.w) juu ya ulevi. Mtume (s.a.w)aliuharamisha. (Tariqa) akasema hakika natengenezaulevi kwa ajili ya dawa. Mtume (s.a.w) alijibu: Huo sidawa bali ni ugonjwa. (Muslim).

Ulevi ni haramu ukinywewa kwa wingi au kwa uchachekama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

Jabir ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:“Kinacholevya ni haramu kikiwa kingi au kidogo.(Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).

Vyakula na vinywaji HalaliVyakula na vinywaji vyote vilivyo patikana kwa njia ya

halali au kutokana na chumo la halali na visivyoharamishwa katika Qur-an na Snnah, ni halali kwaWaislamu. Ni haramu mtu kuharamisha alivyovihalalishaAllah (s.w).

Mtume (s.a.w) alipoapa kutokula “asali” kwa sababu tuya kutaka kuwaridhisha wake zake, Mola wake alimuonyana kwa hiyo tunaonywa Waislamu wote:

Ewe Mtume: Mbona unaharamisha alichokuhalalishiaMwenyezi Mungu? Unatafuta radhi za wake zako? NaMwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenyekurehemu. (66:1).

Kama mtu chakula fulani kinamdhuru au hakipendiatakuwa na udhuru wa kutokila lakini asikiharamishe.

Page 56: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

45

Adabu za kulaKula kwa Muislamu ni Ibada, kwani wakati anapokula

anatakiwa azikumbuke neema za Allah (s.w) naazishukuru kwa kumuabudu Mola wake ipasavyo. Mtuanayemkufuru Allah (s.w) na kuona kuwa lengo la kuwepokwake hapa ulimwenguni ni kula na kustarehe, mbele yaAllah (s.w) anawekwa katika kundi la wanyama kamatunavyojifunza katika aya ifuatavyo:

Kwa hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walioamini nakufanya mema katika mabustani yapitayo mito mbele yake.Lakini waliokufuru hujifurahisha (hapa duniani) na kulakama walavyo wanyama, na moto ndio makazi yao. (47:12)Muislamu hatarajiwi ale kama walavyo wanyama, bali

anatarajiwa ale kwa heshima na adabu iliyobainishwa naUislamu kama tunavyojifunza katika kipengele hiki. Adabuza kula hapa tutazigawanya katika mbeya nne zifuatazo:

(a) kabla ya kuanza kula.(b) Wakati wa kula.(c) Baada ya kula.(d) Kula katika kundi.

(a) Kabla ya kuanza kula(i) Kuhakikisha kuwa chakula Muislamu anacho

kwenda kula ni halali kwani tonge moja la chakulaharamu linamfanya mtu asikubaliwe Ibada zakekwa siku 40.Pia tunafahamishwa kuwa mwili

Page 57: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

46

uliojengwa na chakula haramu umeharamishiwapepo na mahali unapojuzu kuingia ni motoni.

(ii) Kuosha mikono kabla ya kuanza kula ili kutoauchafu kwa ajili ya afya. Pia kufanya hivyo kunabaraka ndani yake kama tunavyofahamishwakatika Hadith ifuatayo:

Salman ameeleza; Nimesoma katika Taurati kuwa barakaza chakula zinapatikana kwa kuosha mikono baada yakula. Nilipolieleza hili kwa Mtume (s.a.w) alisema:Baraka za chakula zinapatikana kwa kuosha mikonokabla ya kuanza kula na baada ya kumaliza kula.(Tirmidh).

(iii) Meza au mahali pa kulia patandikwe kitambaa safi,vyema kiwe cheupe ili chakula kitakachodondokahumo kiokotwe na kuliwa kama alivyosisitizaMtume (s.a.w). Mtume (s.a.w) hakuwahi kuliakwenye meza kama tunavyojifunza katika Hadithifuatayo:

Anas (r.a) amesimulia: Kwa kadri nijuavyo, Mtume (s.a.w)kamwe hakuwahi kula chakula kwenye trei kubwa, walahakuwahi kula silesi za mkate zilizokaushwa, walahakuwahi kula mezani. (Bukhari).

(iv) Wakati wa kula mtu akae vizuri, asiweamejiegemeza wala asile huku amelala. Akaemkao ambao utamuwezesha kula kwa starehe:

Abdullah bin Amr amesimulia kuwa Mtume wa Allahhakuwahi kuonekana akila huku ameegemea mahali…” (AbuDaud)

(v) Kuweka nia ya kula ili kupata nguvu zakumtumikia (kumuabudu) Allah (s.w) inavyostahikina kuzingatia aya ifuatayo:

Page 58: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

47

Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema(mlizopewa mlizitumiaje). (102:8)(vi) Mgeni atosheke na chakula kilichotayarishwa na

wenyeji wake, badala ya kuwasumbua wenyejiwake wamtayarishie chakula kingine. Ila ikiwachakula hicho ni kigeni kwake na hawezi kula,basi itakuwa hapana budi atafutiwe chakulakingine.

(vii) Ni vyema kula chakula pamoja kuliko kula mmojammoja kwani chakula kinacholiwa kwa pamojakina baraka kama tunavyojifunza katika Hadithifuatayo:

Umar bin Khattab ameeleza kuwa Mtume wa Allahamesema: Kula pamoja na sio kwa kutengana kwanibaraka ziko kwa walio pamoja na wengi. (ibn Majah).

Pia kuwakaribisha chakula wageni, fukara, maskini,yatima na wote wenye kuhitajia ni jambo lililosisitizwasana katika Uislamu.Tunafahamishwa katika Qur-ankuwa mtu asiyejihimiza kuwalisha maskini nakuwaangalia vyema yatima amekadhibisha siku ya malipohata kama atajiita Muislamu:

Je, umemuona yule anayekadhibisha dini (asiyeaminiakhera)? Huyo ni yule anayemsukuma yatima, walahajihimizi kuwalisha maskini. (107:1-3).

Page 59: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

48

Katika Hadith iliyosimuliwa na Ibn Abbas, Mtume (s.a.w)amesema:

Baraka zinashuka haraka haraka katika nyumbaambamo chakula hutolewa kuliko kisu kinavyopita katikanundu ya ngamia(Ibn Majah)

(b) Wakati wa kula(i) Kuanza kula kwa jina la Allah kwa kusema:

“Bismillahir rahmanir Rahiim”. Muislamu kuanzakula bila ya kulitaja jina la Allah (s.w) nikumkaribisha Shetani katika chakula chake.Katika Hadith iliyosimuliwa na Hudhaifah Mtumewa Allah amesema:

Hakika Shetani anakifanya chakula kiwe halali kwakepale ambapo jina la Allah halikutajwa. (Muslim)

Kama Muislamu amesahau kuanza kwa jina la Allahwakati wa kula atakapokumbuka asema:

“Bismillahi awwalahu wa aakhirahuu” yaani “Naanzakwa jina la Allah mwanzoni mwake na mwishonimwake”. (Tirmidh, Abu Daudi).

(ii) Kula kwa mkono wa kulia. Mtume (s.a.w)amesema: “Mmmoja wenu atakapokuwa ana kula,na ale kwa mkono wa kulia na atakapokuwaanakunywa, na anywe kwa mkono wa kulia”.(Muslim).

(iii) Kumega chakula sehemu iliyo mbele yako,ukianzia chini na wala sio juu kama inavyosisitizwakatika Hadith ifuatayo:

Ibn Abbas ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) aliletewachakula kisha akasema:Anza kumega pembani mwake

Page 60: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

49

na wala isiwe katikati kwa sababu baraka zinamiminikakwenda chini kupitia katikati. (Tirmidh, Ibn Majah naDarimi).

Katika riwaya ya Abu Daud, alisema: “Wakati mmojawenu anakula, asile kutokea sehemu ya juu ya chakulabali amege kuanzia sehemu ya chini pembeni mwa sahanikwa sababu baraka zinashuka kutokea sehemu ya juu.

Pia tunakatazwa kuyumbayumba kwenye sahani wakatiwa kula kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

Amir bin Salamah ameHadithia: Nilikuwa kijana mdogochini ya malezi ya Mtume wa Allah na mkono wanguulikuwa unayumba yumba katika sahani kwa hiyoalinionya: “Kula kwa mkono wako wa kulia na megapale palipo karibu yako” (Bukhari na Muslim)

(iv) Muislamu akila anatakiwa amege tonge ndogondogo na atafune vizuri ili kurahisisha usagajiwa chakula tumboni.

(v) Ni vizuri kukata nyama kwa meno kuliko kutumiakisu kama Mtume (s.a.w) anavyotuhimiza katikaHadith ifuatayo:

Aysha ameeleza kuwa Mtume wa Allah anasema:“Usikate nyama kwa kisu kwa sababu ni jambo lawageni, lakini ichane kwa meno kwani huleta utamu zaidina ni wepesi zaidi kufanya hivyo.” (Abu Daud, Darimi).

(vi) Kama chakula ni cha moto ni vizuri kusubiri kipoena sivizuri kupoozesha chakula kwa kupuliza.

(vii) Kula kwa kiasi. Si vizuri Muislamu kujaza sanatumbo. Hiyo ni israfu na inamadhara yake kiafyana kiroho:

Page 61: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

50

Miqdam bin Maadi amesimulia: “Nimemsikia Mtume waAllah akisema: “Hapana mtu kujaza sana tumbo lake kiasicha kuchukiza. Hapana budi pawe na kipimo cha kujazatumbo kwa mwanaadamu kiasi cha kuubakisha uti wakewa mgongo katika hali ya kunyooka. Kama hawezikuweka kipimo hicho, basi theluthi (1/3) ya tumbo lakeaijaze chakula, theluthi (1/3) iliyobakia kwa ajili ya hewa.(Tirmidh, Ibn Majah).

(viii) Kuokota tonge la chakula lililoanguka kwa bahatimbaya na kula kama liliangukia kwenye kitambaamaalum kilichotayarishwa kwa ajili hiyo. Kamatonge hilo litakuwa limeanguka chini, utaondoasehemu iliyoshika chini na kula sehemu safiiliyobakia.Jitihada zote hizi ni ili kuepukana naisrafu ambayo ni njia ya Shetani. Tunajifunza hilikatika Hadith ifuatayo:

Jabir ameeleza kuwa alimsikia Mtume wa Allah akisema:Hakika Shetani anamuhudhuria kila mtu katika kila kituanachokifanya hata wakati wa chakula. Tonge la chakulalitakapomponyoka mmoja wenu na atupe sehemu iliyoshika vumbi na ale kilichobakia na asimwachie shetani.Na atakapo maliza chakula chake na alambe vidole vyakekwani hajui ni wapi katika chakula chake kuna baraka.(muslim).

(ix) Kulamba sahani na vidole ili kuhakikisha kuwahakuna hata chembe ya chakula inayotupwa, nimiongoni mwa adabu za kula kama tunavyojifunzakatika Hadith ifuatayo:

Kaab bin Malik ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alikuwaakila kwa vidole vitatu na alikuwa akilamba mkono wakekabla hajanawa. (Muslim).

Jabir amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akilambavidole vyake na sahani na akisema: Hujui ni wapi katikachakula kuna baraka. (Muslim)

Page 62: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

51

Ibn Abbas ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema:Mmoja wenu anapokula chakula hatanawa bila yakulamba mkono wake. (Bukhari na Muslim).

(c) Baada ya chakula(i) Baada ya Kulamba vidole, na sahani tunanawa

mikono kwa ajili ya unadhifu na kutunza afya zetu.Mtume (s.a.w) ametusisitiza kunawa baada ya kulakama inavyobainishwa katika Hadith:

Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:Atakayepitisha usiku na uchafu mkononi mwake kwasababu ya kutonawa (baada ya kula) ikatokea kudhurikakutokana na uchafu huo, asimlaumu yeyote ila yeyemwenyewe. (Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).

(ii) Kumshukuru Allah (s.w). Baada ya Muislamu kulaau kunywa kitu chochote humshukuru Allah (s.w)kwa kusema:“Al-hamdulillaahi Rabbila-aalamiin”yaani shukrani zote anastahiki Bwana mlezi waviumbe vyote”. Amesimulia Abu Sayyid Al-Kudriyyikuwa Mtume (s.a.w) alipomaliza kula alizoeakushukuru hivi:

Al-hamdulillaahil-ladhii atwa-amanaa wasaqaanaawajaalnaa minal muslimiina.

Yaani:Sifa zote njema zinamstahiki Allah aliyetulisha,akatunywesha na akatufanya kuwa Waislamu.(Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).

Muislamu atatakiwa akiweke kila kitendoanachokifanya katika Ibada kwa kukianza kwa jina la Al-lah, kuchunga mipaka ya Allah wakati wa kukifanya nakumaliza kwa kumshukuru Allah (s.w).

Page 63: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

52

Hivyo, kula kutakuwa Ibada endapo Muislamu ataanzakula kwa jina la Allah, kisha akawa anamkumbuka Allah(s.w). Faida zaidi ya kumshukuru Allah (s.w) baada yakula inabainishwa katika Hadith ifuatayo:

Anas ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: HakikaAllah anamfurahia mja anayekula chakula kishaakamshukuru baada yake au anayekunywa kishaakamshukuru baada yake. (Muslim).

(iii) Kumshukuru mwenyeji au mtayarishaji wa chakulakwa kumwambia “Ahsante” au “Shukran” kwaniasiye mshukuru mwanaadam aliyemtendea wema,hawezi kumshukuru Allah (s.w):

Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:Mlaji mwenye shukrani ni sawa na mfungaji mwenyesubira. (Tirmidh, Ibn Majah).

Kulinganishwa mlaji na mfungaji ni kielelezo kinginekuwa kula ni Ibada kama ilivyo kufunga kama utaratibuwa kula utafuatwa kama unavyofuatwa katika kufunga.

Pamoja na kutoa shukrani kwa mtayarishaji wachakula, ni vyema pia kumuombea dua kwa kusema:“Jazakallahu khair” akiwa mwanamume, na akiwamwanamke utamuombea kheria kwa kusema: “Jazakillahikhair” yaani “Allah akujazie kheri”.

(d) Adabu za kula katika Kundi(i) Mtu asianze kula kabla ya wengine.(ii) Asifanye haraka, ale kwa kasi inayolingana na

wengine na awafikirie wengine ili asiwapunje.(iii) Kama kila mmoja anajiwekea chakula katika

sahani yake kutoka kwenye dish kubwa, hana budikuchukua kiasi kidogo kwanza mpaka wote

Page 64: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

53

waenee, kisha akihitaji baadaye ataongeza lakinivile vile awafikirie wengine nao watakaotakakuongeza.

(iv) Asiwang’ang’anize wengine kula aina ya chakulaasichokipenda, badala yake awapendelee wenginekile anachokipenda.

(v) Asiwaangalie wengine wanavyokula wala sahanizao.

(vi) Awapendelee wengine kupata kitu kama vile majikabla ya yeye mwenyewe kupata.

(vii) Vile vile awe tayari kuwahudumia wengine kablayeye hajahudumiwa.

(viii) Asiache kula na kunawa kabla ya wengine. Hatakama ameanza kushiba, itabidi aendelee kidogokidogo mpaka wote washibe kama tunavyojifunzakatika Hadith ifuatayo:

Ibn Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Nguoya chakula inapotandikwa, hapana mtu atakayesimamampaka nguo hiyo iondolewe wala hapana mtu atakayetoamkono wake kwenye chakula hata kama ameshiba mpakawatu wote wamemaliza kula. Ikibidi aache kula kabla yawengine, na awatake radhi kwani bila ya kufanya hivyoatawavunja moyo (atawanyima raha) wenzake… (Ibn Majah).

(ix) Asikosoe chakula au kinywaji mbele ya wengine.

Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) hakuwahikubainisha ubaya wa chakula (au kukiadhiri chakula)chochote kama alikipenda chakula alikila na akamahakukipenda chakula aliacha kula. (Bukhari na Muslim).

Page 65: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

54

4. Michezo na BurdaniUislamu ni utaratibu wa maisha uliokamilika.

Umebainisha namna ya kuliendea kila jambo linalohitajikakatika kuendesha maisha ya mwanaadam ya kila sikukatika kila uwanja ili kumuinua mwanaadamu kimwili,kiutu na kijamii. Michezo ni miongoni mwa vipengele hivi.Uislamu unawataka watu wacheze na kufurahia lakinikwa kuchunga mipaka iliyowekwa na kuzingatia lengo lamaisha ya mwanaadamu hapa ulimwenguni.

Michezo iliyoruhusiwa katika UislamuMichezo yote ambayo humfanya mchezaji kupata uwezo

zaidi wa kiafya na kiakili wa kumuabudu Allah (s.w)inasisitizwa kufanywa na Uislamu. Mtume (s.a.w)amesema: “Afya kwa mtu anayemwogopa Allah (s.w) nibora kuliko utajiri”. Mara kwa mara Mtume (s.a.w) katikakusisitiza afya njema ya mwili na akili amesema:“Waumini (wacha Mungu) wote mbele ya Allah ni sawalakini aliyebora zaidi ni yule mwenye siha nzuri zaidi”.Hivyo, michezo yote isiyochupa mipaka ya Allah (s.w)itakayochezwa kwa lengo la kujenga afya ya mwili na akilihaikukatazwa katika Uislamu.

Aidha, michezo yote ya mazoezi ya kivita kama vilekulenga shabaha, kutupa mkuki, kareti, mieleka, mbio zafarasi, imesisitizwa na Uislamu. Ikumbukwe kuwaWaislamu ni askari wa Allah (s.w) ambao daimawanatakiwa wawe tayari kupigana na maadui wa Uislamuna Waislamu mara watakapoanza kuwachokoza. Kazi yakupigania dini ya Allah (s.w) haikupachikwa kwa jeshimaalum lililoandaliwa kwa kazi hiyo, bali hiyo ni Ibadainayomuhusu kila Muislamu.

Utbah bin Amir ameeleza kuwa Mtume wa Allahamesema: “Kila mchezo atakaocheza mtu ni haramu ilakutupa mishale, kumfunza farasi wake na kucheza namkewe. Hakika hii ndio michezo ya kweli (yenye faida).

Page 66: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

55

Pamoja na kwamba michezo yote hii iliyotajwa katikaHadith hii inatoa mazoezi ya mwili na kuituliza akili badokuna faida za ziada zinazopatikana. Ambapo michezo miwiliya kwanza inampa Muislamu mazoezi ya kijeshi, mchezowa kucheza mtu na mkewe chumbani au katika mazingiraya nyumbani kwao, huimarisha furaha na upendo katikafamilia.

Michezo iliyoharamishwa katika UislamuMichezo iliyoharamishwa katika Uislamu tunaweza

kuigawa katika mafungu mawili:

Kwanza, uharamu unaotokana na kuchupa mipaka yaAllah (s.w). Hata kama atacheza michezo iliyoruhusiwakwa nia nzuri ya kuupa mwili mazoezi, kujipa mazoezi yakijeshi n.k. itakuwa ni haramu michezo hiyo endapoatachupa miapaka ya Allah (s.w) katika uchezaji wakekama vile kucheza na bukta hadharani, kupita wakati waswala, kutumia lugha chafu, n.k.

Pili, kucheza michezo yote iliyoharamishwa katika Qur-an na inayofanana na hiyo. Michezo yote ya kamari au yakibahati nasibu (games of chance) na yenye mfano wahiyo imekatazwa katika Qur-an:

Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa(au kuombwa) asiye kuwa Mwenyezi Mungu, nakutazamia (kupiga ramli, utabiri, n.k.) ni uchafu na ni kaziya shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufaulu.(5:90).

Page 67: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

56

Michezo yote ya kibahati nasibu kama vile michezo yoteya pata-potea, karata, dama, bao, chess na michezo yoteya mashindano kama vile mpira riyadha, ndondi, n.k.imeharamishwa kwa sababu inaleta madhara makubwakatika jamii.Pamoja na faida inayotazamiwa katika michezohiyo, madhara yake ni makubwa zaidi. Hilianatuhakikishia Allah (s.w) katika Qur-an:

Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari, Sema: Katika hivyomna madhara makubwa na manufaa kwa (baadhi ya)watu. Lakini madhara yake ni makubwa zaidi kulikomanufaa yake…. (2:219).

Pamoja na madhara mengine mengi madogo namakubwa yanayotokana na michezo ya kikamari (kibahatinasibu), madhara makuu yamebainishwa katika Qur-ankama ifuatayo:

Hakika Shetani anataka kukutilieni uadui na bughudhabaina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari na anatakakukuzuilieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na(kukuzuilieni) kuswali. Basi, je hamtaacha (mabayahayo)?

Madhara maku bwa ya michezo yote ya kikamari kamayalivyobainishwa katika aya hii ni:

(a) Kusababisha uadui na bughudha.(b) Kuwazuilia waumini kumkumbuka Allah (s.w)(c) Kuwazuilia waumini kuswali (kwa wakati).

Page 68: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

57

Hebu tuangalie madhara haya kwa kuzingatia hali halisiya michezo ambayo imepewa nafasi kubwa na kuundiwawizara katika jamii za kitwaghuti.

(a) Michezo ya Kikamari Husababsha Uadui naBughudha

Wale wote wanaojihusisha au waliowahi kujihusishana michezo hii watakuwa mashahidi wa ukweli huu. Ilivyokawaida ni kwamba anayepata ushindi katika michezohiyo hufurahia na kujiona na yule anayeshindwa huchukiana huwa na hisia za kutaka kulipiza kisasi. Kwa ujumlakatika michezo ni furaha na ufakhari kwa mshindi na nihuzuni na chuki kwa aliyeshindwa. Ukichanganya halihizi mbili unachotarajia ni nini kama sio uadui nabughudha baina ya wachezaji wa pande mbili. Kuteta,kusengenya, matusi na utani ni lugha ya kawaida yamichezo. Uadui kati ya timu mbili za mpira na washabikiwake si jambo geni kwetu. Watu kuuana kutokana nakudhulumiana katika michezo ya kamari si jambo geni.

Utashangaa vipi dola za kitwaghuti zinaipa michezohii kipaumbele! Kisingizio chao kikubwa ni kwamba inaletaushirikiano na kujenga udugu. Hii ni kauli ya uongoinayopingana na hali halisi. Tumeelezwa kuwa michezoya kikamari na ya mashindano ni kazi ya Shetani. Nimuhali kutokea ushirikiano na upendo katika uwanja wamichezo ambapo Shetani ndiye mgeni rasmi.

(b) Michezo ya Kikamari (Games of chance)huwazuilia Waumini kumkumbuka Allah (s.w)

Kila mchezaji au aliyeshuhudia michezo ya karata, bao,chess, gudugudu, na michezo mingine yote ya kibahatinasibu (games of chance),pamoja na mchezo wa mpira,anafahamu vyema jinsi michezo hii inavyopoteza mudana kumsahaulisha mtu na majukumu muhimu ya maisha

Page 69: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

58

yake binafsi, familia na jamii kwa ujumla. Ni mara ngapitunawaona watu wazima na akili zao na wenye majukumumengi mbele yao, wakishinda kutwa wanacheza bao bilahata kula.

Ni mara ngapi tunaona wakati umetangazwa mchezokati ya timu mbili maarufu za mpira, watazamajiwakihudhuria uwanjani saa mbili asubuhi na kungojeahumo uwanjani mpaka saa kumi alasiri, mechiitakapoanza?

Ni jambo la kawaida vile vile kuwakuta watu wazimana nguvu zao na akili zao timamu wakitumia muda mrefukatika michezo ya karata na mingineyo kama hiyo.Michezo yote hii hupumbaza wachezaji na watazamajiwasiweze kufikiri mambo ya msingi ya maisha yao.Utashangaa kwa nini michezo ya aina hii inapewakipaumbele katika jamii za kitwaghuti hasa kwa vijanawa mashuleni na mitaani. Bila shaka huu ni mpango wakuwapumbaza vijana ili watawala madhalimu waendeleekuiendesha jamii watakavyo kwa maslahi yao binafsi.

Katika Uislamu michezo yote inayompumbaza mtuasitekeleze majukumu yake na kuliendea lengo lake lakuwepo hapa ulimwenguni imeharamishwa naatakayejitumbukiza humo atakuwa miongoni mwa watuwa motoni kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:

Page 70: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

59

Kila nafsi itafungika (motoni) kwa amali (mbovu)ilizozichuma. Isipokuwa watu wa kuliani, wanaulizana juuya watu wabaya: Ni kipi kilichokupelekeni motoni?Waseme:Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali,wala hatukuwa tunalisha maskini. Na tulikuwa tukizama(katika upuuzi) pamoja na waliokuwa wakizama.(74:38-45).

Lengo la maisha ya mwanaadamu ni kumtumikia Al-lah (s.w) kwa kusimamisha Ufalme wake katika jamii kwakuhakikisha kwa hali na mali kuwa utaratibu wa maishaunaofuatwa na jamii ni ule aliouweka Yeye. Ili kufikialengo hili kuu, kila wakati mwanaadamu anatakiwaakumbuke uhusiano wake na Allah (s.w) na daimaakumbuke kuwa yeye hapa ulimwenguni ni Khalifa waAllah (s.w).Mtu aliyezama kwenye michezo ya upuuziinayopoteza muda na kupumbaza ni muhali kuwa nakumbukumbu hizi hata kama atajiita Muislamu. Waislamuhasa waliofuzu mbele ya Allah (s.w) ni wale wanaojiepushana michezo yote ya upuuzi (laghwi) kama tunavyojifunzakatika Qur-an:

Hakika wamefuzu Waislamu, ambao katika swala zaohuwa ni wanyenyekevu. Na ambao hujiepusha namambo ya upuuzi. (23:1-3).

Katika suratul Furqaan tunafahamishwa kuwamiongoni mwa sifa za waja wa Rahman ni pamoja na waleambao hawajihusishi na mambo ya upuuzi, hata tu kuwawatazamaji:

Page 71: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

60

Na wale ambao hawashuhudii shahada za uwongo, nawanapopita penye upuuzi, hupita kwa heshima (zao)(25:72)

(c) Michezo ya Upuuzi huwazuilia Waumini kuswaliMichezo ya upuuzi kama vile mpira, bao, karata, n.k

huwapumbaza wachezaji na wasikilizaji kiasi cha kujengatabia ya kupuuza swala.Tumeyashuhudia haya katikamagenge ya mabao.Ni jambo la kushangaza kuwakutaWaislamu wakiendelea na bao kuanzia asubuhi mpakajioni na kupitwa na swala zote za kutwa kisha huziswalikadha wakati wa isha, jambo ambalo halimo kabisa katikautaratibu wa kusimamisha swala tano. Swala ni faradhikuswali katika wakati wake maalumu

“… Kwa hakika swala kwa Waislamu ni faradhiiliyowekewa nyakati makhususi”. (4:103).

Swala ndio zana ya kumuwezesha Muislamukumuabudu Mola wake ipasavyo na humuwezesha kuishikwa nidhamu katika jamii kama Khalifa wa Allah (s.w).Nidhamu katika jamii haipatikani pale ambapo swalaimepuuzwa.

Hivyo michezo yote inayomtoa mtu katika lengo lakuumbwa kwake ni michezo ya upuuzi na Muumini wakweli hana budi kujiepushia mbali na michezo hiyo.

(iv) Sherehe na BurdaniMaisha ya mwanaadamu yamezungukwa na furaha na

majonzi penye furaha watu hushereheka na penye msibawatu huomboleza. Katika kipengele hiki tutazingatiasherehe na burdani katika jamii ya Kiislamu ukilinganishana jamii za kitwaghuti.Katika jamii ya kitwaghuti

Page 72: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

61

iliyozunguka tunawaona watu wakijiburudisha nakujitumbuiza katika sherhe zao kwa ngoma, disco, nyimbo,mashairi, ngonjera n.k. Je, Uislamu unamtazamo upi juuya sherehe na burdani na kushereheka kwa Waislamukunatofautianaje na kushereheka kwa majahili?

Majahili hawajui halali wala haramu katika sherehezao na katika kusherehekea kwao. Kwa maana nyinginemajahili hawajali kuona nafsi ya sherehe iliyo mbele yaokuwa ni yenye kumridhisha Allah (s.w) au ni yenyekumchukiza na katika kushereheka kwao hawana habarina mipaka ya Allah (s.w) aliyoiweka.

Sherehe ya Kiislamu ni tofauti sana na hizi zakitwaghuti.

Kwanza katika Uislamu, sherehe yoyote ileinayopingana na hukumu za Allah (s.w) ni haramu nahivyo si ruhusa Waislamu kushiriki. Kwa mfano ni haramukwa Waislamu kuitika mwito wa harusi ya kumuoza bintiwa Kiislamu kwa Mkristo au kwa yeyote asiyekuwaMuislamu.Halikadhalika ni haramu kwa Waislamukujiunga na sherhe zozote zile za kidini minghairi yaUislamu. Kwa mfano, kama ilivyo haramu kwa Waislamukujitumbukiza katika sherehe za matambiko ya aina yotendivyo ilivyo haramu kwa Waislamu kusherehekeaKrismas, Mwaka mpya na Pasaka.

Jambo la pili linalozingatiwa na Waislamu katikasherehe zao ni uchungaji wa mipaka ya Allah (s.w) katikakushereheka kwenyewe. Vyakula na vinywajivitakavyotumika katika sherehe havina budi kuwa halali,vitolewe bila ya kufanya israfu na pasiwe na ubaguziwowote katika kuvigawanya.

Page 73: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

62

Imesimuliwa na Abu Hurairah kuwa Mtume (s.a.w)amesema: “Karamu ya harusi iliyo mbaya kuliko zote niile ambayo wamealikwa matajiri wakaachwa maskini”(Bukhari na Muslim).

Kwa ujumla sherehe za Kiislamu zinatakiwaziambatanishwe na kutoa sadaqa ili kuwafurahishamajirani na wenye matatizo. Maendelezo ya sherehe zaKiislamu kuanzia hatua ya mwanzo hadi ya mwishohayanabudi kuzingatia mipaka yote ya Allah (s.w). Kilelecha sherehe za Kiislamu kinafikiwa kwa kumtaja Allah(s.w) na kumtaka maghfira. Qur-an inatuongoza kuwa:

Itakapofika nusra ya Mwenyezi Mungu na kushinda. Naukawaona watu wakiingia katika dini ya MwenyeziMungu makundi makundi. Basi hapo mtakase Mola wakopamoja na kumsifu, umuombe maghufira (msamaha)hakika yeye ndiye apokeaye toba. (110:1-3).

Katika aya hizi tunakumbushwa kuwa hatuna budikukumbuka daima kuwa ushindi au furaha ya aina yoyoteanaileta Allah (s.w). Hivyo, katika hali hiyo ya furahahatuna budi kumshukuru Allah na kumsifu kwa sifa zakena kumuomba msamaha kwa makosa yetu ili furaha hiyotuliyoipata hapa duniani iwe yenye kuendelea katikamaisha ya akhera, Muislamu kamwe hatathubutukujihasirisha na kujitumbukiza katika huzuni ya milelekatika maisha yake ya akhera kwa sababu ya furahazidanganyazo za hapa duniani.

Page 74: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

63

Furaha ya kweli kwa Muislamu ni ile iliyoambatanana Radhi za Allah (s.w). Na lolote lile linalomghadhibishaAllah (s.w) ni msiba na huzuni kubwa kwa Muislamu hatakama limesherehekewa na walimwengu wote.

Hebu sasa tuanglie mtazamo wa Uislamu juu yamatumizi ya ngoma, “disco”, nyimbo na mashairi kamaburdani na kama sehemu ya sherehe.

Ngoma na “Disco”.Michezo yote ya ngoma, disco, dansi, n.k. kama

tuionavyo katika utamaduni wa jamii hizi za kijahili, niharamu kwa sababu zifuatazo:

Kwanza, ni laghwi yaani michezo ya upuuzi kwanihuwafanya watu wapoteze muda mwingi nje ya lengo lakuumbwa kwao hapa ulimwenguni. Yaani michezo hii yangoma na “disco” huwasahaulisha wachezaji nawatazamaji kumkumbuka na kumtukuza Allah (s.w). Kwahiyo michezo hii ya ngoma ni miongoni mwa kazi yashetani na Allah (s.w) ametukataza kushiriki katikashughuli zote za Shetani.

Pili, michezo mingi ya ngoma na “madisco” huchezwakatika mchanganyiko wa wanawake na wanaume na huwani vichocheo vikubwa sana vya zinaa. Katika Uislamu niharamu kushiriki katika shughuli yoyote inayochocheazinaa.

Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo ni uchafu mkubwa)na njia mbaya (kabisa).(17:32)

Page 75: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

64

Katika sherehe za harusi wanawake wameruhusiwakupiga dufu na kuimba nyimbo ambazo hazichupi mipakaya Allah (s.w) kama tunavyojifunza sunnah. Hapana kamwekatika mafundisho ya Mtume (s.a.w) ambapo dufulimetiliwa mkazo kama Waislamu wanavyolitilia leo hii.

Nyimbo na mashairiNyimbo na mashairi huwa halali au haramu

kutegemeana na madhumuni ya nyimbo au mashairi hayo.Ni wazi kuwa nyimbo au mashairi ya kimapenzi ambayoni vichochezi vya zinaa ni haramu moja kwa moja. Piamashairi au nyimbo ambazo ndani yake kuna lugha mbaya,au kuna kuitukana au kuipinga dini ya Allah (s.w), basimashairi hayo au nyimbo hizo zitakuwa ni haramu. Halikadhalika mashairi na nyimbo ambazo ziko palekumpotezea mtu muda wake ni laghwi na ni haramu.

Nyimbo na mashairi ambayo ndani yake kuna hekimana mafunzo ya aina mbali mbali ambayo hayaambatani nasauti na midundo ya ngoma za miziki, yanakubalika katikaUislamu. Nyimbo na mashairi ya Kiislamu hayana budikumuelekeza Muislamu katika kumcha Mwenyezi Munguzaidi na katika kumpa nguvu na hamasa ya kupiganiadini ya Allah (s.w). Tunajifunza katika Hadith ya Bukharina Muslim iliyosimuliwa na Jundub kuwa Mtume wa Al-lah (s.w) alijipooza kishairi alipoumia vidole vyake katikavita vya Uhud.

Alijiliwaza katika shairi hilo kuwa kutokwa na damukwake si kwa sababu nyingine ila ni kwa ajili ya Allah(s.w) na kwa ajili ya dini yake. Pia katika Hadith nyingineya Bukhari na Muslim iliyosimuliwa na Barasi, tunajifunzakuwa Mtume (s.a.w) aliimba wimbo wa kuwatia nguvuWaislamu walipokuwa katika kazi ngumu sana yakuchimba handaki katika vita vya Handaki wakatiWaislamu wapatao alfu mbili (2,000) tu walipovamiwa mjini

Page 76: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

65

mwao na jeshi la watu wapatao alfu ishirini na nne(24,000) mnamo 5 A.H. Wimbo huu umesheheni na manenoya hekima na kuwapelekea Waislamu kuwa imara kwakumtegemea Allah (s.w).Hakika Allah (s.w) aliwanusuruWaislamu katika vita hivyo.

5. Misiba na MaombolezoMisiba na maombolezo ni miongoni mwa vipengele vya

utamaduni wa jamii. Kila jamii ina namna yake ya kupokeamisiba na kuomboleza. Katika jamii za kijahili misiba yoteimeambatanishwa na mkono wa mwanaadamu au nguvuzinazotokana na maumbile asili yaliyomzingiramwanaadamu.

Maombolezo ya misiba, kama vile maombolezo ya vifo,katika jamii za kijahili huambatana na malalamiko,lawama, masononeko.Wengine, katika kupunguzamsononeko hulewa sana, huchezesha ngoma na hufanyakila jambo lingine litakalowapumbaza ili wasahau kifo.

Mtazamo wa Uislamu juu ya misiba na maombolezoyake ni tofauti kabisa na mitazamo ya kijahili, Waislamuwanamini kuwa kila jambo hutokea kwa Qadar ya Allah(s.w) pamoja na kwamba kila jambo linalotokealimeambatanishwa na sababu za kimaumbile. Kwa mfanoni kawaida kuwa ukimkata mtu shingo kwa kisukilichokikali atachinjika na atakufa lakini haitatokea hivyoiwapo kitendo hicho hakikulandana na Qadar ya Allah(s.w). Nabii Ismail (a.s) hakuchinjika pamoja na jitihadaza baba yake – Ibrahimu (a.s) za kumchinja kwa kisu kikalisana.Mwenyewe Nabii Ibrahiim (a.s) hakuungua motoalipotumbukizwa kwenye moto mkubwa na mkali kwa kuwakitendo hicho cha kumuua kwa kumchoma motohakikulandana na Qadar ya Allah (s.w). Kutokana namifano hii miwili tunaona wazi kuwa hautokei msibawowote ila uko mikononi mwa Allah (s.w):

Page 77: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

66

Haitokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ilaumekwisha andikwa katika kitabu kabla hatujaumba;hakika jambo hilo ni jepesi kwa Allah.Ili msihuzunikesana juu ya kitu kilichokupoteeni wala msifurahi sanakwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kilaajivunaye, ajifaharishaye. (57:22-23).

Kwa mtazamo wa Uislamu, furaha na huzuni ndio halihalisi ya mazingira ya ulimwengu na yote ni mitihani kwamwanaadamu. Mwanaadamu mwenye akili atakayefauluvizuri mtihani huu wa furaha ni yule anayefahamu fikakuwa furaha zote anazozipata katika ulimwengu huuzimetoka kwa Allah (s.w) ili kumjaribu kuwa atakuwa nimwenye shukurani na kutumia furaha hizo kwakumtukuza Allah (s.w) na kumuabudu inavyostahiki ikiwani pamoja na kumuomba msamaha kutokana na udhaifuwake wote uliompelekea kumkosea Bwana Mlezi (Rabb)wake.

Atakayefurahia maisha yake hapa ulimwenguni kamakwamba yeye mwenyewe binafsi au wengine katikawanaadamu ndio chanzo cha furaha hizo na kwa hiyoakafurahia atakavyo bila ya kujali mipaka aliyoweka Al-lah (s.w), basi atakuwa ni mwenye kubunda katika mtihaniwa furaha.

Page 78: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

67

Na mwanaadamu mwenye akili atakayestahiki kufaulumtihani wa misiba ni yule anayefahamu vyema kuwa mtuhawezi kufikwa na msiba wowote ila Allah (s.w) apende;kuwa hapana mtu yeyote awezaye kumletea mtu msibaiwapo Allah (s.w) hakumwandikia msiba huo na walahapana yeyote awezaye kumuondolea mtu msiba iwapoAllah (s.w) amemuandikia msiba huo.

Atafaulu mbele ya Allah (s.w) yule ambaye anapofikwana msiba hapapatiki, hanung’uniki na kulalama balihuupokea msiba huo kwa moyo mkunjufu na kuridhia kuwahuo ni utaratibu wa Allah (s.w) usio na makosa na kwambakila alilolipanga Allah (s.w) ni lenye kumnufaishamwanaadamu. Namna Waislamu wanavyotakiwa waipokeemisiba imebainishwa katika aya zifuatazo:

Na tutakutieni katika msukosuko wa (baadhi ya mambohaya); khofu na njaa na upungufu wa mali na wa watuna matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri.Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika sisi ni waMwenyezi Mungu, na kwake yeye tutarejea (atatupa jazayake)”. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Molawao na Rehema, na ndio wenye kuongoka. (2:155-157).

Page 79: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

68

Waislamu wanapopatwa na misiba wanatakiwa wasubirikama iliyobainishwa katika aya hizi na pia wanatakiwawamuombe Allah (s.w) awawezeshe kuwa miongoni mwawenye subira na awabariki na kiuwarehemu kutokana namisiba hiyo. Katika Hadith iliyosimuliwa na Abu Hurairah,Mtume (s.a.w) amesema:

Allah (s.w) atasema: “Hapana zawadi mbele yangu ilaPepo kwa mja wangu ambaye ninapomfisha kipenzichake miongoni mwa watu katika dunia huomba ujiramwema kutokana na msiba huo.” (Bukhari).

Waislamu wanawajibika kuwapa mkono wa pole nakuwaliwaza wale waliopatwa na msiba kwa manenoyafuatayo aliyotufunza mtume (s.a.w): “Hakika kilaalichokichukua Allah (s.w) ni chake na kile alichokitoa ni chakena kila kitu kitarejea kwake kwa muda maalum”. Kwa hiyokuwa mwenye subira na tarajia kupata malipo”. (Bukhari naMuslim). Tunajifunza vile vile katika Hadith kuwa, mwenyekumliwaza aliyepatwa na msiba amepata malipo sawa nayule aliyesubiri katika msiba:

Abdullah bin Masud ameeleza kuwa Mtume wa Allahamesema “Anaye mliwaza yule aliyekuwa na msiba,kuna kwake malipo sawa na yule aliyefikwa na msiba”.(Tirmidh, Ibn Majah)

Iwapo kwa njia moja au nyingine Muislamu ataonakuwa msiba uliomtokea ni matokeo ya matendo yakemaovu au kupuuza kwake mwongozo wa Allah (sw), hanabudi kujitupa kwa Allah (s.w) kwa toba ya kweli na kusubirina sio kukata tamaa. Kwani pamoja na kukosea kwake,Allah (s.w) ameahidi kumsamehe kama tunavyojifunzakatika Qur-an:

Page 80: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

69

Na misiba inayokupateni ni kwa sababu ya vitendo vyamikono yenu, na (juu ya hivi Mwenyezi Mungu)anasamehe mengi. (42:30).

6.Maombi na DuaNi katika utamaduni wa Kiislamu Muislamu

kumtegemea Allah (s.w) kwa kila jambo. Muislamu wakweli anafahamu vyema kuwa mafanikio yote hutokanana Allah (s.w). Hivyo anapopatwa na tatizo lolote hanabudi kwanza kabisa kumuelekea Mola wake na kumuombamsaada kabla hajamuelekea mtu yeyote kwa msaada. Hiindio ahadi tunayoitoa kila mara tusomapo suratul-Fatiha:

Wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiyetunayekuomba msaada. (1:5).

Hatuna budi kukumbuka kuwa matatizo na shida mbalimbali zinazotufika ni mtihani kwetu kuwa tutakuwa niwenye kusubiri na kuomba msaada wa Allah (s.w) aututapapatika na kutafuta misaada kwa wengine minghairiya Allah (s.w). anatuita Allah (s.w) katika Qur-an:

Enyi mlioamini! Jisaidieni (katika mambo yenu) kwasubira na swala bila ya shaka Mwenyezi Mungu yupamoja na wanaosubiri. (2:153).

Pia Waislamu hatuna budi kuwa na hakika, mia kwamia, kuwa Allah (s.w) ni muweza wa kila kitu na

69

Page 81: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

70

halishindikani kwake jambo na kwamba ni mwenye kusikiamaombi yetu na yukaribu zaidi kuliko tulivyo karibu namshipa mkuu wa damu wa shingoni (jangular vain) mwetu:

Na bila shaka tumemuumba mtu nasi tunajua yanayopitakatika nafsi yake, nasi tukokaribu naye zaidi kulikomshipa wa shingo (yake). (50:16)

Baada ya kuwa na uhakika wa namna hii hatuna budikuyaelekeza maombi yetu moja kwa moja kwa Allah (s.w)kwa matumaini makubwa ya kupata kila tunachokiomba.Tunajifunza katika aya zifuatazo namna ya kumuombaAllah (s.w):

Na waja wangu watakapokuuliza hakika yangu(waambie kuwa) mimi niko karibu nao. Naitikia maombiya mwombaji anaponiomba. Basi na waniitikie nawaniamini, ili wapate kuongoka. (2:186).

70

Page 82: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

71

Mwombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na kwa siri(kwa suati ndogo bila ya kufanya kelele). Yeye(Mwenyezi Mungu) hawapendi wapitao mipaka(7:55).

Katika aya hizi tunajifunza yafuatayo:Kwanza, tunatakiwa tumuombe Allah (s.w) moja kwa

moja bila ya kupitishia maombi yetu kwa yeyote yule nawala tusiombe kwa baraka za yoyote yule. KumuombaAllah kwa baraka za yeyote au kupitia kwa yeyote nikumdunisha Allah (s.w) na kukanusha Qur-an (2:186).Tunaamrishwa tumuombe Allah (s.w) na kwa baraka zakena majina yake matukufu:

Na Mwenyezi Mungu ana majina (sifa) mazuri mazuri,muombeni kwayo, na waacheni wale wanaoharibuutukufu wa majina yake. Karibuni hivi watalipwa yalewaliyokuwa wakitenda. (7:180).

Pili, tunatakiwa pia tumuombe Allah (s.w)a kwaunyenyekevu, na kwa siri sio kwa kupiga makelele. Ilituwe wanyenyekevu kwa Allah (s.w) wakati wa kuombahatuna budi kuomba kwa lugha tunayoifahamu vyema.Tukiwa ndani ya swala tutaomba kwa lugha ya Kiarabulakini hatuna budi kufahamu tafsiri au maana ya yaletunayoyaomba.

Tatu, vile vile tunatakiwa wakati wa kumuomba Allah(s.w) tuwe na khofu kwa kuzingatia Hadhi yake na Utukufuwake na papo hapo tuwe na yakini kuwa ameyasikiamaombi yetu na atatujibu kulingana na ahadi yake, kwaniyeye ni muweza wa kutujibu na si mwenye kukhalifu miadiyake.

Page 83: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

72

Nne, sharti kubwa tunalotakiwa tulitekeleze ili maombiyetu yajibiwe ni kumuitikia Allah (s.w). Kumuitikia Allah(s.w) ni kumuamini Allah (s.w) inavyostahiki nakumuabudu ipasavyo kwa kumtii kwa unyenyekevu katikakukiendea kila kipengele cha maisha yetu ya kila siku.Kuchunga mipaka yote ya Allah (s.w) kwa kutekelezamaamrisho yake yote na kujiepusha mbali na makatazoyake yote ni katika kumuitikia Allah (s.w). Hivyo ili yajibiwemaombi yetu mbali mbali tunayomuomba Allah (s.w),hatuna budi kujitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kufuatautaratibu wa maisha aliotufunulia Allah (s.w) katikakuendesha maisha yetu ya kila siku.

Waislamu hatupaswi kumuomba Allah (s.w) tukiwa nashida au tunapohitajia msaada tu wa maisha ya dunia,bali tunatakiwa tumuombe Allah (s.w) nyakati zote, tukiwakatika furaha au tukiwa katika matatizo. Tukiwa katikafuraha tunatakiwa tumuombe Allah (s.w) aijaalie furahahiyo iwe yenye kheri. Tukiwa katika matatizo tunamuombaAllah (s.w) atuondolee matatizo hayo na atulipe ujiramwema kutokana na kusubiri kwetu juu ya matatizo hayona iwe ni sababu ya kutusamehe makosa yetu. Kwamtazamo huu Muislamu katika nyakati zote na katika halizote yuko katika Ibada ya Allah (s.w) na hupata thawabu(ujira mwema mbele ya Allah (s.w)) akiwa katika dhiki aukatika furaha. Kwa ujumla tunatakiwa katika maombiyetu, tumuombe Allah (s.w) atupe mema ya hapa dunianina huko akhera na atuondolee dhiki ya hapa duniani naadhabu kali ya huko akhera.

Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema akhera,na utulinde na dhabu ya moto. (2:201)

Page 84: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

73

Dua mashuhuri ambazo tunaweza kuzitumia katikakumuomba Allah (s.w) ni zile zilizoombwa na waja wakembali mbali kama zilivyobainishwa katika Qur-an na zilealizozitumia Mtume Muhammad (s.a.w) katika kumuombaMola wake katika hali na nyakati mbali mbali kamazinavyobainika katika Hadith mbali mbali. Hapa tumejaribukubainisha aya za Qur-an mnamopatikana dua mbali mbaliwalizoomba waja wa Allah (s.w).

Dua ya Adam (a.s) na Hawa ya kuomba msamaha baadaya kumkosea Mola wao kwa kula tunda walilokatazwa:(7:23)

Dua alizoomba Nabii Nuhu (a.s):(23:26), (26:117-118), (54:10), (71:26-28), (11:41), (11:45),(11:47), (23:29).

Dua ya Nabii Swaleh (a.s): (23:39)

Maombi ya Nabii Ibrahim (a.s)(2:126-129), (14:35-41), (26:83-89), (37:99-100), (60:4-5).

Maombi ya Nabii Lut (a.s):(26:169), (29:26), (29:30).

Maombi ya Nabii Ayyub (a.s)(21:83), (38:41).

Maombi ya Nabii Yusuf (a.s)(12:33), (12:101).

Dua ya Nabii Shuayb (a.s)(7:89).

Maombi ya Nabii Mussa (a.s)(28:16), (28:17), (28:21), (28:24), (7:148), (20:25-35),(7:151), (10:88), (7:155-156), (2:67), (5:25).

Page 85: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

74

Maombi ya wafuasi wa Nabii Mussa (a.s):(10:85-86), (7:126).

Dua ya Bi Asia, Mkewe Firaun: (66:11).

Maombi ya watu wa Talut wakati walipokuwa wakipambanana Jaluti (Mfalme wa Maadui): (2:250).

Dua ya Nabii Sulaiman (a.s): (27:19), (38:35).

Dua ya Malkia wa Sheba – Bibi Bilqis: (27:44).

Dua ya Nabii Yunus (a.s) - (21:87).

Maombi ya Nabii Zakaria (a.s) – Mlezi wa Bibi Mariam:(3:38), (19:4-6), (21:89).

Maombi ya Hannah – Mama wa Bibi Maryam – (3:35-36).

Maombi ya wafuasi wa Nabii Issa (a.s): (3:53).

Dua ya Vijana wa pangoni: (18:10).

Dua ya mwenye Bustani: (68:29).

Dua ya Mume na mke kabla ya mtoto kuzaliwa – (7:189).

Dua za Malaika: (11:73), (40:7-9).

Dua ya watu wema: (7:47)Dua za Mtume Muhammad (s.a.w) na wafuasi wake:

(1:1-7), (2:156), (2:201), (2:286), (3:8-9), (3:16), (3:26-27), (3:191-194), (4:45), (5:83), (6:161-163), (9:59),(17:24), (20:114), (21:112), (23:93-94), (23:97-98),(23:109), (23:118), (25:65-66), (25:74), (39:46), (46:15),(59:10), (66:8), (113:1-5), (114:1-6).

Page 86: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

75

(vii) Kumkumbuka Allah (s.w) Saa 24Kumkumbuka Allah (s.w) muda wote wa maisha ndio

lengo lililombele ya kila Muislamu wa kweli.Lengo lakuletwa kwetu hapa ulimwenguni ni kumuabudu Allah(s.w), yaani kumtumikia Allah (s.w) kwa unyenyekevu kwamuda wote wa maisha yetu. Kumtumikia Allah (s.w) kwamuda wote wa maisha yetu kunawezekana tu endeapotutaendesha maisha yetu yote ya saa 24 kwa kuchungabarabara mipaka ya Allah (s.w) aliyotuwekea katikakukiendea kila kipengele cha maisha yetu katika kila faniya mtu binafsi, familia, uchumi, siasa, utamaduni, sheriana fani nyinginezo za maisha ya jamii. Kuchunga mipakaya Allah (s.w) kwa muda wote wa saa 24 katika kilakipengele na kila fani ya maisha ni jambo linalowezekanapale Muislamu atakapoibakisha akilini mwakekumbukumbu ya Allah (s.w) kila wakati.Ni vipi Muislamuataweza kumkumbuka Allah (s.w) kila wakati?

Kwanza, Muislamu ataweza kumbukumbuka Allah (s.w)na utukufu wake kila wakati, endapo kila maraatazichunguza neema zote zilizomzunguka alizotunukiwana Mola wake kisha akawa ni mwenye shukurani kwakekwa kumtii na kumtukuza ipasavyo. Pia Muislamu atazidikukuza yakini juu ya uwezo na utukufu wa Allah (s.w)endapo atatafakari kwa makini umbile la mbingu na ardhina vyote vilivyomo. Allah (s.w) anatuhakikishia kuwa watuwenye kushukuru neema zake na kutumia akili zao vilivyokatika kutafakari maumbile yaliyowazunguka ndio pekeewanaoweza kumkumbuka na kuuona utukufu wake kwamuda wote wa saa 24.

Page 87: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

76

Katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi na mfuatano wausiku na mchana, ziko hoja (za kuonyesha kuwepo Al-lah (s.w) na utukufu wake) kwa wenye akili.(3:190)

Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima,na wakiwa wamekaa na wakiwa wamelala.Nahutafakari juu ya umbile la mbingu na ardhi (kishahusema): Mola wetu! Hukuviumba hivi bure. Utukufu niwako. Basi tuepushe na adhabu ya moto. (3:191).

Pili, Muislamu ataweza kubakia katika kumkumbukaAllah (s.w) endapo atajitahidi kwa kadri ya uwezo wakekusimamisha swala tano za faradhi kama ipasavyo na piaakajitahidi kwa kadri iwezekanavyo kufuatilizia swala zaSunnah na hasa zile zilizokokotezwa. Kazi ya swalailiyosimamishwa vilivyo katika kumuwezesha Muislamuaweze kumkumbuka Mola wake kwa nyakati zoteimebainishwa wazi katika aya ifuatayo:

Page 88: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

77

Soma uliyoletewa wahyi katika kitabu (hiki ulicholetewa)na usimamishe swala. Bila shaka swala (ikiswaliwavilivyo) humzuilia (huyo mwenye kuswali na) mambomachafu na maovu, na kwa yakini (ndani ya swala) kunakumkumbuka Mwenyezi Mungu kukubwa. NaMwenyezi Mungu anajua mnayotenda. (29:45).

Tatu, Muislamu ataweza kubakia katika kumkumbukaAllah (s.w) nyakati zote iwapo atajitahidi kwa kadri yauwezo wake kutekeleza nguzo ya Zakat na kuwa mwepesiwa kutoa mali yake na kujitolea nafsi yake kwa ajili yaAllah (s.w) katika kusaidia na kutoa huduma mbali mbaliza kijamii.

Pia Muislamu atabakia katika kumkumbuka Allah s.w)na utukufu wake kila wakati endapo atakamilisha nguzoya funga ya Ramadhani na kuiambatanisha na funga zaSunnah kwa kadri ya uwezo wake kisha akatekeleza nguzoya Hija iwapo anauwezo. Tukumbuke kuwa, lengo la nguzotano za Uislamu ni kumtayarisha mja aweze kumtumikiaMola wake ipasavyo katika kila kipengele cha maisha yake.

Nne, kumsafia nia Allah (s.w) na kumtanguliza katikakila kitendo tunachokifanya. Kabla hatujafanya kitendochochote kile hatuna budi kukichunguza kitendo hichokuwa kitatupelekea kupata radhi za Allah (s.w) aughadhabu zake. Endapo kitendo hicho ni chema na chenyekutupelekea kupata radhi za Allah (s.w) tukifanye. Endapokitendo hicho chema kitawaudhi makafiri, washirikina,wanafiki na maadui wengine wa Allah (s.w) tusisitekukifanya maadam matarajio yetu ni radhi za Allah (s.w)tu. Endapo kitendo hicho ni kiovu na chenye kutupelekeakughadhibikiwa na Allah (s.w) tukiache na kujiepushambali nacho hata kama kufanya hivyo kutawakasirishawalimwengu wote. Hii ndiyo tabia ya Waislamu wa kwelikama inavyobainishwa katika aya zifuatazo:

Page 89: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

78

Afanyaye kitendo kizuri (kila kitendo kilichofanywa kwaajili ya Allah ni kitendo kizuri) atalipwa (mbele ya Allah )mfano wake mara kumi. Na afanyaye kitendo kibayahatalipwa ila sawa nacho tu. Nao (wote hao) hawatadhulumiwa.(6:160)

Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu ameniongozakatika njia iliyonyooka, (katika) dini iliyosawa sawakabisa ambayo ndiyo dini ya Ibrahim aliyekuwamwongofu, wala kabisa hakuwa miongoni mwawashirikina. (6:161)

Sema: Hakika swala yangu, matendo yangu yotemengine, na uzima wangu, na kufa kwangu (yote) ni kwaajili ya Mwenyezi Mungu, Muumba Mlezi wa walimwenguwote.(6:162)

Na haya ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanzawa waliojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (6:163).

Page 90: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

79

Tunajifunza katika aya hizi kuwa jambo loloteatakalolifanya Muislamu kwa ajili ya Allah (s.w) ni jambojema (amali swalihi), na kila jambo jema analolifanya mjahulipwa ujira mwema (thawabu) kutokana na kitendohicho mara kumi. Tunahimizwa kuwa katika Ibada yaAllah (s.w) katika kila kitendo chetu. Muda tutakao kuwanje ya Ibada ya Allah (s.w) tutakuwa katika Ibada (utumishiwa) ya wengine minghairi ya Allah (s.w) na bila shakawakati huo tutakuwa ni washirikina. Jambo lingine ambaloni la msaada kwetu litakalotupelekea kuyafanya matendoyetu yote yawe Ibada ni kuanza kila jambo kwa jina laAllah, yaani kuanza kila jambo kwa “Bismillahir RahmaanirRahiim – “Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema Mwenyekurehemu”. Muislamu anatakiwa ajenge tabia ya kuanzakila jambo jema kwa “Bismillah”. Miongoni mwa faida kubwazinazopatikana kwa Muislamu kwa kuanza kila jambo lakekwa “Bismillahir Rahmaanir Rahiim” huku akiwa anazingatiamaana yake ni hizi zifuatazo:

(1) Mtu anapoanza na “Bismillah” anatangulizamaombi yake ya kutaka msaada wa Allah (s.w), ilialifanikishe jambo hilo analotaka kulifanya kwa ajiliyake.

(2) Kuanza kila jambo kwa “Bismillah” kutamkingakufanya mambo machafu na maovu kwani kama niMuislamu wa kweli atamuonea haya Allah (s.w) nahatathubutu kufanya jambo ovu kwa jina lake.

(3) Kitendo cha kuanza kwa “Bismillah” ni kitendokinachompelekea Muislamu kuwa hadhiri na kileanachoanza kukifanya na humkumbusha kutia niayake ya kufanya kitendo hicho kwa ajili tu yakutafuta radhi za Allah (s.w).

Page 91: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

80

Zoezi la Pili

1. (a) Eleza maana ya utamaduni (b) Msingi wa Utamaduni wa Kiislamu ni Mila ya nani?

2. Kwanini ni muhimu kwa jamii kufuata Mila ya nabiiIbrahiim (a.s)

3. Orodhesha masharti ya vazi la Kiislamu

4. Taja mambo manne muhimu ambayo Qur’an inamtakakila Muislamu ayazingatie katika kula na kunywa.

5. Orodhesha(a) Vyakula vilivyoharamishwa kwa Muislamu.(b) Vinywaji vilivyoharamishwa kwa Muislamu.

6. Eleza kwa muhtasari adabu anazotakiwa kuzitekelezaMuislamu katika kula.

7. (a) Michezo ina umuhimu gani kwa Muislamu. (b) Ni michezo ipi isiyoruhusiwa kwa Waislamu, nakwanini?

8. Taja mambo ya Msingi yanayohitajika kuyafanya nakuyasimamia ili sherehe na burdani za Waislamu zisikiukeQur’an na Sunnah ya Mtume Muhammad (s.a.w), kamazilivyo sherehe na burdani za wasiokuwa Waislamu.

9. Muislamu anapofikwa na msiba, anatafautianaje naasiyekuwa Muislamu katika kuomboleza?

10. Soma kwa makini sura 3:190-192. Kisha oneshavipengele na mkakati wa namna ya kutekeleza maudhuiyake, na ushikamane nayo kila siku.

Page 92: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

81

Sura ya Tatu

SHERIA

Maana ya sheriaKatika lugha ya Kiarabu, neno Shariah lina maana ya

njia ya kufuatwa. Kiistilahi neno sheria linakusanyakatika maana yake, taratibu, sharti, kanuni (principles)na amri (rules) ambazo huwekwa ili kuongoza mahusianoya watu katika jamii inayohusika.

Sheria ni fani muhimu mno katika maisha ya jamii.Haijatokea jamii yoyote ile katika kipindi cha historia yamwanaadamu isiyo na sheria. Kazi ya sheria ni kuiwekajamii katika nidhamu na kulinda haki za raia ili ipatikanefuraha na amani katika jamii hiyo.

Sheria ni kanuni au amri ambazo si tu hupasa kutiiwa,bali pia zinapovunjwa, mvunjaji hudhibitiwa baada yakugundulika na kuadhibiwa na vyombo vinavyohusika nausimamiaji wa hiyo sheria. Kwahiyo, ili pawepo na sheriani lazima pia pawepo na vyombo vyenye mamlaka na nguvuya kusimamia ili kuhakikisha kuwa hiyo sheria inafuatwana iwapo itavunjwa basi hatua zitachukuliwa dhidi yamvunjaji.

Kazi ya Sheria katika JamiiKwanza sheria humlinda binaadamu binafsi dhidi ya

madhara mbali mbali yanayoweza kusababishwa namwenendo wake mbaya. Kwa mfano sheria yakulazimishwa watu kufanya kazi ina lengo la kuwaepushawatu na umaskini wa kujitakia. Sheria ya kumkataza mtukuvuta bangi na kutumia madawa ya kulevya ina lengo lakulinda afya yake. Sheria ya barabarani ina lengo la

Page 93: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

82

kumuepusha mtu na ajali. Uzoefu unaonesha kuwa sheriazinapokuwa madhubuti mwenendo na hulka ya watuhubadilika na hivyo hujiepusha na maovu.

Pili, sheria hulinda watu na mali zao. Kwa mfanosheria zinazokataza kuua (bila ya sababu inayokubalikakisheria), kumjeruhi mtu, kuiba, kunyang’anya, kulaghai,kupunja vipimo, n.k. ziko pale ili kulinda uhai na mali zawatu. Bila ya kuwepo sheria kama hizi watuwatadhulumiana na kuliana mali kwa batili.

Tatu, sheria ni muhimu ili kuhifadhi amani na usalamakatika jamii, ili jamii iweze kuishi bila ya migongano navurugu. Bila ya kuwepo amani na usalama jamii haiwezikupiga hatua za kimaendeleo bali maisha hujaa hofu navitisho.

Nne, sheria huhifadhi maadili ya jamii. Inafahamikakuwa maadili ni moja ya misingi mikuu ya mwenendo wajamii. Hivyo moja ya malengo makuu ya sheria kwakawaida huwa ni kulinda maadili ili kuhakikisha kuwajamii inaendeshwa katika mwenendo mwema.

Tano, sheria inapanga utaratibu juu ya namna yakuendesha shughuli mbali mbali zenye maingiliano yakijamii. Mfano sheria ya ujenzi wa makazi mijini, matumiziya barabara, taratibu za uendeshaji serikali na vyombovyake, uendeshaji wa masoko, uendeshaji wa biashara,utunzaji wa mazingira, ulinzi na usalama wa raia na taifa,n.k.

Kwa ujumla, kazi kuu ya sheria ni kuiweka jamii katikanidhamu na kulinda haki za raia ili ipatikane amani nafuraha katika maisha ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.Pamoja na ukweli huu, swali linakuja: “kama kazi yasheria nikuiweka jamii katika nidhamu na kuleta furaha

Page 94: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

83

na amani, mbona hivi leo, pamoja na jamii za kitaifa nakimataifa kujiwekea sheria, hatuoni dalili ya furaha naamani isipokuwa vurugu, vita, mauaji ya halaiki,ukandamizaji na unyanyasaji wa kila aina?”

Hatuna budi kufahamu kuwa si kila sheria ya jamiiinaleta furaha na amani kwa raia wote. Sheria nyingizilizotungwa na wanaadamu zina udhaifu mkubwa kamatutakavyoona. Kwa hiyo pamoja na nia njema inayokuwepowakati wa kuzitunga, katika matumizi yake hazifikii kabisalengo linalokusudiwa. Ni sheria za Allah (s.w) pekeezinazoweza kuiweka jamii ya mwanaadamu katikanidhamu inayotakikana na kuiwezesha kuishi kwa furahana amani. Sheria ya Kiislamu inaweza kuifikisha jamiikwenye lengo hilo kwa kuwa imewekwa na Muumbamwenyewe ambaye anamjua vyema mwanaadamu,matashi yake, matatizo yake, ujanja wake na udhaifu wakekwa ujumla kama Qur-an inavyotutanabahisha:

Bila shaka tumemuumba mtu, nasi tunajua yanayopitakatika nafsi yake; nasi tu karibu naye zaidi; kulikomshipa wa shingo (yake).” (50:16)

Chimbuko la sheria za KitwaghutiChimbuko la sheria zilizotungwa na wanaadamu ni

vipawa vya wanaadamu vya kufikiri na kuhoji (reason) namila na desturi zilizozoeleka. Hivyo sheria hizo ni zao laakili ya mwanaadamu na mazingira yake. Hata hivyo,pamoja na kuwa vipawa hivyo vya kuhoji, miiko na desturihizo ni nyenzo za muhimu, lakini zenyewe tu bila ya ufunuo(revelation) kutoka kwa Mwenyezi Mungu hutoa ujumbewa kubahatisha na usio na uhakika wa kudumu. Hata

Page 95: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

84

hivyo wale wakanao ufunuo hushikilia kuwa ndizochemchem za hakika katika utunzi wa sheria na kanunimbali mbali. Kwa jitihada hizo za akili (bila ya ufunuo),jamii, nchi na mataifa yote ya kitwaghuti hujitungia sheriambali mbali ambazo nazo hutokana na chimbuko kuu,ambalo ni Katiba. Katiba za nchi ndizo msingi wa sheriazote.

Page 96: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

85

Udhaifu wa sheria zilizotungwa na binadamuNi wazi kuwa kutumia akili na kufikiri ni jambo muhimu

sana kwa mwanaadamu, lakini je akili ya mwanaadamuau fikra zinaweza kutoa sheria ambazo ndio mwongozo wamaisha? Wanaadamu hutofautiana sana katika kufikirina huathiriwa sana na mazingira, wakati na matashi. Ninani mwenye fikra za kutoa sheria sahihi zenye kuwezakuwaongoza wanaadamu hapa ulimwenguni zisizoathiriwana mazingira yake; wakati na matashi yake. Ukweli nikwamba uamuzi unaotokana na fikra ya mwanaadamuhutegemea mazingira yake ambayo yako katika upeo wamilango ya fahamu ambayo tayari ina udhaifu mkubwa.Kama taarifa iliyopatikana kutokana na milango ya fahamuitakuwa na kasoro, pia uamuzi utakaotegemea taarifa hiyonao utakuwa na kasoro.

Hali kadhalika, ujuzi na uwezo wa kufahamu wamwanaadamu haumtoshi kuweza kuyazingatia mazingirayote yanayopasa kuzingatiwa katika kumpangiamwanaadamu sheria, au utaratibu unaofaa wa maisha.Watafiti wa mambo ya uwezo wa akili ya mwanaadamuwameonesha kuwa akili ya binaadamu siku zote uwezowake umefungika katika mazingira aliyomo na upeo wamaendeleo ya sayansi ambao jamii yake imeufikia. Niukweli unaokubaliwa na watu wote kuwa, mambo yoteanayoyajua mwanaadamu kuhusu nafsi na mwili wakeyeye mwenyewe na kuhusu mazingira yake ni machacheikilinganishwa na yale yote anayohitajia kuyajua ilikujitosheleza katika ujuzi alionao.

Udhaifu huu umepelekea mwanaadamu kutegemeazaidi dhana na ujuzi usiotosheleza katika kutoa maamuziya lipi baya na lipi zuri. Hii imepelekea mwanaadamukujipangia taratibu zisizomfaa kwa dhana ya kuwa hizondizo zifaazo.Hivyo, mara nyingi hata mwanaadamuanapokusudia kujipangia taratibu nzuri zifaazo ameishia

Page 97: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

86

kutunga sheria zisizofaa, na pengine zenye madhara kwakemwenyewe.Hii ndio imekuwa moja ya sababu kubwa zakubadilishwa mara kwa mara kwa sheria za kutungwa namwanaadamu. Ukizichambua vyema sheria hizo utakutakuwa mara nyingi badala ya kutimiza malengo ya kuwepokwake katika jamii, zenyewe huenda kinyume chake.Matokeo yake, kwa mfano badala ya kumkingamwanaadamu na maovu na madhara yake, zenyewehuyachochea. Na badala ya kulinda maadili zenyewehusaidia kuyabomoa. Na huchochea dhulma badala yakuzuia. Bali katika jamii nyingine, sheria huwa ndiochimbuko la ukandamizaji na uonevu wa kila hali.

Sheria kama zile zinazounga mkono mifumo ya utumwakatika jamii, ubaguzi wa rangi n.k., ni mifano ya udhaifumwingi uliopo katika mifumo ya sheria zilizotungwa nabinaadamu.

Jambo lingine ni kuwa, moyo wa mwanadamu naoumetawaliwa na matashi ambayo mara nyingihuwapelekea watungaji wa sheria wasiofuata mwongozowa Muumba kujipendelea katika sheria wanazozitunga.Hili linadhihiri katika kila kaumu ya watu wafuatao sheriazilizowekwa na wanaadamu.

Mfano wakati wa Firauni yeye mwenyewe alijikwezana kujifanya Mungu. Sheria ziliwapendelea na kuwakwezajamaa na watu wa kabila lake (yaani Wamisri):

Page 98: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

87

“Hakika Firauni alitakabari (alijitukuza) katika ardhi naakawafanya watu wa huko makundi mbali mbali.Akalidhoofisha kundi moja miongoni mwao, akiwachinjawatoto wao wanaume na kuwawacha hai watoto waowanawake.Hakika yeye alikuwa miongoni mwawaharibifu (kabisa).” (28:4).

Mifano ya namna hii ni mingi. Wagiriki wa zamanipamoja na kusifiwa kwao kuwa chimbuko la dhana yademokrasia na falsafa za kuigwa za kina Socrates, Plato,Aristotle n.k, walijitungia sheria zilizowagawa watu katiya mabwana na watumwa. Katika jamii hiyo, watumwa,wanawake na wale ambao hawakuwa wazawa walikuwahawana haki yoyote, na zaidi watumwa walikuwa ni sawana bidhaa zinazoweza kuuzwa na kununuliwa, bali hatana kuuawa na mabwana zao kama njia ya kujifurahisha!

Katika wakati huu tulionao pia udhaifu huu wa matashiya watu umetawala utunzi wa sheria. Katika sheria zakimataifa, mataifa makubwa ya Ulaya na Marekaniyamelaumiwa kwa kujipendelea. Huko Marekani, watuweusi wanakandamizwa na kubanwa sana. Hivyo sheriazilizotungwa na mwanaadamu mara nyingi haziafikianina misingi ya haki na usawa.

Pia mara nyingi sheria hizo hushindwa kuyazingatiana kuyasimamia sawasawa maslahi ya kweli yamwanaadamu. Hii inatokana na zile sifa za udhaifualizonazo huyo mwanaadamu mwenye kuzitunga hizosheria. Sifa zile tulizo zitaja juu pamoja na nyingine nyingikama vile za uongo, wivu, husuda, hila na ulaghai,ubinafsi, uchoyo, hasira, kiburi, n.k., pamoja na ile sifaya ufinyu na uwezo wa kujua mambo. Ni kwa msingi huuAllah (s.w) ametutanabahisha:

Page 99: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

88

“Na kama ukiwatii wengi katika (hawa) waliomoulimwenguni watakupoteza na njia ya Mwenyezi Munguhawafuati ila dhana tu na hawakuwa ila ni wenye kuzua(tu basi).” (6:116)

Hivyo ni makosa makubwa akili ya mwanaadamukubeba dhima ya utunzi wa sheria. Matokeo yake, badalaya sheria hizo kutimiza malengo ya kuwepo kwake katikajamii, zinakiuka na kuchochea madhara. Haweki haki nauadilifu, ila dhuluma. Na kwahivyo sheria huwa ndiochimbuko la ukandamizaji na uonevu wa kila namna.Sheria kama zile zinazoruhusu ulevi, uzinifu, utumwa,ubaguzi wa rangi, ukoloni , riba, kamari (n.k.) ni mifanoya udhaifu mwingi uliopo katika mifumo ya sheriazilizotungwa na mwanaadamu.

Matokeo ya sheria hizo kuyaruhusu mambo hayoimekuwa ni ya maafa na maangamizi makubwa kwa watuwa dunia nzima. Ulevi umekuwa ndio sababu inayoongozakwa kusababisha maafa ya ajali barabar ani na matatizomengi ya kiafya. Zinaa imesababisha magonjwa mbalimbali kama vile Kaswende, Kisonono na Ukimwi. Riba naKamari navyo vimekuwa ndio sababu kubwa ya umaskinikatika nchi za ulimwengu wa tatu. Sehemu kubwa yamzigo wa madeni ya mataifa maskini inatokana na riba.Na hali ya uchumi ilivyo kwa sasa ni kuwa nchi maskinikamwe hazitaweza kujivua mzigo wa madeni ambayohuongezeka siku zote kutokana na kukua kwa riba. Kwaujumla sheria zilizotungwa na mwanaadamu zimeshindwa

Page 100: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

89

kabisa kuiongoza jamii katika misingi ya haki na usawa.

Udhaifu katika Usimamizi wa sheria za kitwaghutiPamoja na udhaifu katika utunzi wa sheria, upo pia

udhaifu katika usimamiaji wa sheria hizo. Hii inatokanana ukweli kwamba kila anachoweza kukipangamwanaadamu, mwanaadamu anaweza kukipangua. Sheriazilizotungwa na binaadamu hazimjengei mja ile fikramuhimu sana ya utii kwa yule aliyemwekea sheria,mwenye uwezo wa kubaini pindi tu mja huyoatakapozikiuka. Vile vile watunzi wa sheria hujiweka juuya sheria daraja ambayo mwanaadamu hastahiki kuwanayo.

Sheria za kibinaadamu pamoja na kuwepo vyombo vyadola vya kusimamia kama vile polisi, vikosi vya kuzuiafujo, kamisheni za kuzuia rushwa, magereza, idara zausalama wa taifa, na kadhalika, bado inashindikanakuhakikisha kuwa zinatekelezwa. Sababu ni kuwa nivigumu binaadamu kumchunga binaadamu mwenzakekama awezavyo kumchunga mbuzi au kondoo. Ni rahisimwanaadamu kujificha mwanaadamu mwenzakeasimuone, na hivyo kufanya maovu bila taabu. Piawakiukaji sheria waweza kushirikiana na wasimamiziwake kwa kutumia rushwa, udugu, ukabila, urafiki nakadhalika.

Chimbuko la Sheria ya KiislamuMsingi wa kwanza wa sheria ya Kiislamu ni Qur-an.

Qur-an ni mwongozo utokao moja kwa moja kwa Allah(s.w) kupitia kwa Mtume Muhammad (s.a.w). Allah (s.w)ndiye Muumba wa binaadamu na vyote vilivyomzungukakatika mbingu na ardhi. Amekiumba kila kitu kwa lengona Ndiye pekee Mwenye kustahiki kutoa mwongozo,kuweka taratibu, na kanuni zitakazokiwezesha kila kiumbekuwa na nidhamu itakayokipelekea kufikia lengo lake.

Page 101: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

90

Hivyo, Allah (s.w) ndiye chimbuko la sheria zotezinazomiliki maumbile yake (natural laws)zinazoyawezesha maumbile hayo yabakie katika nidhamuinayoyawezesha kufikia lengo lake. Pia Allah (s.w) ndiyepekee anayestahiki kumuwekea binaadamu sheria (so-cial laws) itakayomuwezesha kuwa na nidhamuitakayompelekea kuishi kama mja na khalifa wa Allah(s.w) hapa ulimwenguni.

Msingi wa pili wa sheria ya Kiislamu ni Sunnah yaMtume Muhammad (s.a.w) Mtume Muhammad (s.a.w)pamoja na Mitume wengine, wameteuliwa na Allah (s.w)ili kuwa Waalimu katika jamii zao wanaoupokea nakuufundisha ujumbe kutoka kwa Allah (s.w) kinadhariana kimatendo. Si ujumbe wote kutoka kwa Allah (s.w)kupitia kwa mitume ulioandikwa na kuhifadhiwa katikavitabu vyake bali sehemu kubwa ya ujumbe wa Allah (s.w)unadhihiri katika maelekezo na utendaji wa Mitume kamaQur-an inavyotuthibitishia juu ya Mtume (s.a.w):

Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwahaya (anayosema) ila ni wahyi uliofunuliwa(kwake).(53:3-4)

Hivyo ni wajibu kwa Waislamu kumtii Mtume (s.a.w)kwa kufuata vilivyo mafundisho yake na kumuigiza tabiayake.

Vyanzo vingine vya sheria ya KiislamuTumeona kuwa vyanzo vikuu vya sheria ya Kiislamu ni

Qur-an na Sunnah. Vyanzo vya aina ya pili vya sheria yaKiislamu ni vile vinavyopatikana kwa kutumia vigezo vyaQur-an na Sunnah. Vyanzo hivi ni Al-Ijmaa, Al-Qiyaas naAl-Ijtihaad.

Page 102: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

91

Al-Ijmaa’Al-Ijmaa ni makubaliano ya kongamano la wanazuoni

(shura ya wataalamu) wa jamii, baada ya kufariki Mtume(s.a.w). Makubaliano hayo yanafikiwa kwa kuzingatiamipaka ya Qur-an na Sunnah na maslahi ya jamii. Ijmaa,haitakubalika pale itakapokwenda kinyume na Qur-an naSunnah. Allah (s.w) mwenyewe anatuhimiza kushaurianakatika mambo mbali mbali ambayo hatuyapati moja kwamoja kutoka kwake katika aya zifuatazo:

Basi kwa sababu ya rehema itokayo kwa MwenyeziMungu umekuwa laini kwao (Ewe Muhammad). Na kamaungekuwa mkali na mwenye moyo mgumu bila shakawangalikukimbia. Basi wasamehe wewe na uwaombeemsamaha (kwa Mwenyezi Mungu) na ushauriane naokatika mambo. Na ufungapo nia mtegemee MwenyeziMungu (tu ufanye hili uliloazimia). Mwenyezi Munguanawapenda wamtegemeao. (3:159)

Na wale waliomuitikia Mola wao (kwa kila amri Zake) nawakasimamisha Sala, na wanashauriana katika mamboyao na wanatoa katika yale tuliyowaruzuku. (42:38)

Page 103: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

92

Pia Ijmaa inasisitizwa katika aya zifuatazo:

Enyi mlioamini! Mtiini Allah na mtiini mtume na wenyemamlaka juu yenu walio katika nyie. Na kamamkikhitalifiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwaAllah na Mtume wake ikiwa mnamwamini Allah na sikuya mwisho. Hiyo ndiyo heri nayo ina matokeo borakabisa. (4:59)

Na atakayemuasi Mtume baada ya kumdhihirikiauwongofu na akafuata njia isiyokuwa ya Waislamu,tutamgeuza aliko geukia mwenyewe na tutamwingizakatika Jahannam; napo ni pahali pabaya kabisa pa mtukurudia.” (4:115)

Aya hizi zinasisitiza kuwa shura ya wataalamu naviongozi wa jamii ya Kiislamu itakapopitisha maamuziambayo hayapingani na Qur-an na Sunnah, Waislamuwanalazimika kutii vinginevyo watakuwa wamemuasi Al-lah (s.w) na Mtume wake.

Page 104: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

93

Naye Mtume (s.a.w) katika kusisitiza Ijmaa, amesemakatika Hadith:

“Watu wangu (waumini wa kweli wa umma wake)hawatakubaliana na yeyote anayewapoteza na njia yahaki”

Mifano mingi ya Ijmaa inapatikana katika kipindi chaMaswahaba, baada ya kufariki Mtume (s.a.w). Kwa mfano,katika Qur-an na katika Sunnah ya Mtume (s.a.w), adhabuya mlevi haikubainishwa. Lakini shura ya maswahabailikaa na kuweka adhabu ya viboko thamanini kwa mlevikutokana na ushauri ‘Ali bin Abuu Taalib aliyesema:“Anayekunywa pombe analewa; mlevi huongea ovyo (kamakichaa); anayeongea ovyo huwazulia watu uovu; naanayewazulia watu uovu adhabu yake ni viboko thamaninikwa mujibu wa Qur-an:

“Na wale wanaowasingizia wanawake watahirifu (kuwawamezini) kisha hawaleti mashahidi wane, basiwapigeni mijeledi thamanini, na msiwakubalie ushahidiwao tena, na hao ndio mafasiki”. (24:4)

Al-Qiyaas (analogical Deduction)Al-Qiyaas ni maamuzi(fat-wa)anatoa mwanachuoni

(mjuzi wa Qur-an na Sunnah) kulingana na mazingira nakwa maslahi ya jamii, pale ambapo hapana fat’wailiyotolewa na Qur-an au Hadith au Ijmaa. Suala lakutumia akili limesisitizwa mno katika Uislamu kamatunavyojifunza katika aya zifuatazo:

Page 105: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

94

“Hakika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wausiku na mchana ziko hoja (za kuonyesha kuwepo Allah(s.w) kwa wenye akili.” (3:190)

“Na bila shaka tumewaumbia Moto wa Jahannam wengikatika majini na watu (kwa sababu hii). Nyoyo (akili)wanazo lakini hawafahamukwazo na macho wanayolakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakinihawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao niwapotevu zaidi. Hao ndio walioghafilika.” (7:179)’

Suala la kutoa maamuzi kwa kutumia akili pale ambapohapana fat-wa ya Qur-an na Sunnah ameliridhia Mtume(s.a.w) kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

“Mtume (s.a.w) alimtuma Mu’aadh bin Jabal Yemenkwenda kuwa Kadh (Jaji) na mkuu wa Jimbo (Gover-nor). Kabla hajaondoka, Mtume (s.a.w) alimuuliza kuwakama atafikwa na tatizo atalitatua kwa kutumia kigezogani. Mu’aadh alijibu kuwa atatoa maamuzi kutokanana Qur-an. Mtume (s.a.w) akamuuliza: Jaalia kuwa

Page 106: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

95

hukupata ufumbuzi wa tatizo hilo katika Qur-an,utafanyaje katika kutoa uamuzi?” Mu’aadh akajibu kuwaatatafuta ufumbuzi kutokana na Sunnah ya Mtume(s.a.w). Mtume (s.a.w) akaendelea kumuuliza: “Jaaliahukupata jibu kwenye Qur-an wala Sunnah utafanyaje?”Mu’aadh bin Jabal alijibu kuwa atatoa uamuzi kutokanana akili yake. Mtume (s.a.w) alifurahi kusikia jibu hili.”

Pia tunajifunza katika Hadith kuwa Mtume (s.a.w)alimtuma Abuu Musa al Ash-a’ri kwenda Yemen nakumuagiza kuwa ahukumu kwa mujibu wa Qur-an, nakama hakupata uamuzi kutoka kwenye Qur-an, atumieHadith za Mtume (s.a.w) na akikosa kupata uamuzikutokana na Hadith, basi atoe maamuzi kutokana na akiliyake.

Al-IjtihaadIjtihaad ni neno la Kiarabu lenye maana ya kufanya

jitihada ili kufikia maamuzi binafsi. Katika masuala yakisheria, Ijtihaad, ni kutumia jitihada za kuchambua nakutoa ufafanuzi juu ya sheria.

Imamu Shafii, ameunga mkono suala la Ijitihaad, kwakurejea aya ya Qur-an ifuatayo:

“Na po pote wendako geuza uso wako kwenye msikitimtakatifu. Na popote mlipo geuzeni nyuso zenu upandeuliko (msikiti huo) …” (2:150).

Page 107: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

96

Imamu Shafii kutokana na agizo la aya hii, anasisitizakuwa si rahisi mtu kujua upande ilipo Ka’abah bila kutumiajitihada binafsi, kwa kutumia jua, ramani, dira, n.k.

Ijtihaad inakubalika kwa kuzingatia misingi ya Qur-an, Sunnah, Ijmaa na Qiyas. Mujtahidi hanabudi kuwana ujuzi wa kina juu ya Qur-an, Sunnah, Ijmaa na Qiyas.Pamoja na ujuzi wa kutosha juu ya vyanzo hivi vinne vyasheria, Mujtahidi pia hanabudi kuwa na sifa zifuatazo:

(a) Awe Muislamu mzuri wa vitendo.(b) Awe mcha-Mungu mwenye kushikamana na Qur-

an na Sunnah.(c) Asiwe mwenye kuathiriwa na misimamo ya

vikundi.(d) Awe muadilifu na muaminifu na awe ameepukana

kabisa na matendo machafu.

Halali na Haramu Katika Sheria ya KiislamuUislamu umepambanua na kuliweka wazi kila jambo.

Uislamu pamoja na kuwataka watu wafanye mema nakuacha maovu umeainisha wazi wazi yepi mema(Ma’arufaat).

Na yepi maovu (Munkaraat). Allah (s.w) peke yake ndiyemwenye mamlaka ya kuhalalisha na kuharamisha.Kuhalalisha alicho kiharamisha Allah (s.w) au kufanyakinyume chake ni kuchukua nafasi ya Allah (s.w) katikamamlaka yake na hiyo ni shirk kubwa.

Yale yote aliyohalalisha Allah (s.w) yana manufaa kwabinaadamu kibinafsi na kijamii. Katika sheria ya Kiislamumambo halali yamewekwa katika daraja tatu zifuatazo:

(i) Faradh. (iii) Mustahabu. (iii) Mubaha.

Page 108: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

97

(i) Faradh ni mambo ambayo ni halali lakini kutokanana umuhimu wake, Allah (s.w) amewaamrisha watukuyatekeleza pasina hiari. Mwenye kuacha kufanyahaya kwa makusudi atakuwa amevunja amri ausheria ya Allah (s.w), na atastahiki kughadhibikiwana Mola wake na kustahiki adhabu yake iwapohataleta toba ya kweli.

(ii)Mustahabu ni mambo ambayo sio tu kuwa ni halalikuyafanya, bali pia watu wanahimizwa sanawajitahidi kuyafanya kwa ajili ya manufaa binafsina jamii kwa ujumla. Mambo hayo yanaweza kuwayale yanayohusiana na Ibada maalumu, siasa,uchumi, utamaduni, n.k.

(iii)Mubaha, katika sheria ya Kiislamu ni jambo loloteambalo ni halali kulifanya lakini sio lazimakulifanya. Kwa mfano, iwapo mtu anapenda bustaniya maua anaruhusiwa na sheria kuwa nayo lakinisheria haimlazimishi mtu kuwa na bustani ya maua.

Yale yote aliyoyaharamisha Allah (s.w) yana madharakwa binaadamu kibinafsi na kijamii. Kufanya mamboyaliyoharamishwa ni kuvunja sheria ya Allah(s.w) nakustahiki ghadhabu zake na adhabu yake.

Kuna mambo ambayo japo sheria haijatamka waziwazikuwa ni haramu lakini uzoefu unaonesha kuwa yanamadhara kwa binaadamu kibinafsi na kijamii. Mambo yaaina hii katika sheria ya Kiislamu huitwa makruhuMuislamu analazimika kujiepusha na mambo haya.

Ukichunguza makatazo yote katika sheria ya Kiislamuutaona kuwa yamewekwa kwa manufaa ya binaadamu nayamegawanyika katika sehemu kuu tano zifuatazo:

Page 109: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

98

(i) Makatazo yenye lengo la kulinda na kuhifadhiimani.

(ii) Makatazo yenye lengo la kulinda na kuhifadhimaisha na uhai wa binaadamu.

(iii) Makatazo yenye lengo la kulinda na kuhifadhi akiliya binaadamu.

(iv) Makatazo yenye lengo la kulinda na kuhifadhiheshima na hadhi ya binaadamu.

(v) Makatazo yenye lengo la kulinda na kuhifadhi mali.

Mahakama ya KiislamuUislamu huyaratibu maisha ya jamii na hivyo kuweka

sheria zinazolinda maslahi ya mtu yasiharibiwe na mtumwingine. Sheria pia inamhakikishia usalama wake raiaanayetuhumiwa kuwa ametenda kosa fulani. Sheria yaKiislamu husimamisha haki kwa kuzingatia; maslahi yadola ya kuzuia uhalifu na kwa kuyalinda maslahi ya raiaili haki zake zidumishwe:

1. Kanuni ya uwajibikaji wa mhalifu.2. Kanuni ya uwiano wa kosa na adhabu, na3. Kanuni ya kutosogeza nyuma hukumu zinazotolewa

kwa wahalifu.

1. Kanuni ya uwajibikaji kwa mhalifuRaia hawezi kuwa salama iwapo atalazimika kujibu

mashtaka ya makosa ya mtu mwingine. Hivyo kanuni hiini msingi wa usalama wa raia.

Kanuni hii ina maana kuwa ni yule mtendaji wa kosatu ndiye ashitakiwe, na si mtu mwingine yeyote. Yaaniikiwa Juma ndiye aliyeteka nyara ndege basi yeye pekeyake (kama alikuwa peke yake) ndiye ashitakiwe.Asichukuliwe baba yake mtu au mkewe n.k.

Page 110: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

99

Kanuni hii pia maana yake ni kuwa ikiwa mtoto waRais ameiba pesa, basi asiachwe kwa sababu ni mtoto wamtu mkubwa. Kanuni hii pia ina maana kuwa mtualiyeshiriki katika kutenda kosa kama mtendaji mkuu aukama msaidizi hana budi kushitakiwa kwa mujibu wakushiriki kwake. Qur-an imebainisha katika sehemu mbalimbali juu ya kanuni hii ya uwajibikaji wa mtu binafsi:

Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya. (53:39)

Anayefanya mema anajifanyia (mwenyewe) nafsi yake,na mwenye kutenda ubaya ni juu (ya nafsi) yake (vilevile). Na Mola wako si dhalimu kwa waja wake (41:46)

Wala nafsi yoyote haichumi (ubaya) ila ni juu yake.(6:164)

Wala hatabeba mzigo wa mwingine. (35:18)

Atakayefanya ubaya atalipwa kwa (ubaya) huo. (4:123)

Hadith za Mtume (s.a.w) pia zinaithibitisha kanuni hii.Mtume (s.a.w) amesema:

Page 111: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

100

“Nafsi haitaulizwa kwa makosa ya baba, au ndugu yake.

Huko Ulaya kanuni hii ilitambuliwa baada ya Mapinduziya Ufaransa. Kanuni hii ilipitishwa katika sheria yaJanuari 21, 1790, na kuingizwa katika katiba 1791. Kablaya hapo mtu aliwajibika siyo tu kwa makosa yake bali piakwa makosa yaliyotendwa na wengine.

Kwa mfano sheria moja ya Kifaransa ya zama hizoilikuwa inasema kuwa kusema maneno yasiyopendezadhidi ya Mfalme ni kosa ambalo adhabu yake ni kifo kwahuyo msemaji na kufilisiwa mali ya familia ya mtu huyo.

2. Kanuni ya uwiano wa kosa na adhabu(a) Kanuni hii ina maana kuwa hakuna mtu anayeweza

kushitakiwa au kuadhibiwa isipokuwa kamailivyobainishwa na sheria. Kanuni hii ina maanakuwa makosa na adhabu zake lazima zitolewe naserikali.

Kanuni ya uhalali wa kosa na adhabu inalinda usalamawa raia kwa kuhakikisha kuwa mtu hanyanyaswi na dola.Kanuni hii pia inadhibiti mamlaka na uwezo wa hakimukwani hawezi kutoa adhabu isipokuwa tu kamailivyowekwa katika sheria, hata kama kosa hili limeudhiwatu namna gani.

Hivyo basi sheria ndiyo inayogawa baina ya lipi halalina lipi haramu. Hakuna mtu atakayeadhibiwa aukushitakiwa kwa jambo ambalo halikubainishwa wazikuwa ni kosa kabla ya kutendwa:

Na si wenye kuwaadhibisha (viumbe) mpakatuwapelekee Mtume. (17:15)

Page 112: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

101

(Hao ni) Mitume waliotoa khabari (kwa watu wema)wakawaonya (wabaya) ili watu wasiwe na hoja juu yaAllah baada ya (kuletwa hawa) Mitume. Allah ni MwenyeNguvu na Mwenye Hikima. (4:165).

Na Mola wako haangamizi miji mpaka ampeleke Mtumekatika mji wao mkuu, awasomee aya zetu. (28:59)

Na Qur-an hii imefunuliwa kwangu ili kwa hiyonikuonyeni nyinyi na kila imfikiayo. (6:19).

Na hakuna taifa lolote ila alipita humo muonyaji (Mtume).(35:24).

Hivyo Qur-an ambayo ndio chimbuko kuu la sheria yaKiislamu imeweka kanuni kuwa mshitakiwa hawezikuadhibiwa mpaka kwanza awe ametaarifiwa juu ya kuwajambo hili ni kosa. Haki ya kuarifiwa kosa na adhabu yakendio lengo la kanuni hii ya uhalali wa kosa na adhabu.

Page 113: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

102

3. Kanuni ya Kutosogeza nyuma hukumuzinazotolewa

Raia hawawezi kuzitumia haki zao kwa usalama iwapowanaweza kushitakiwa kwa makosa ambayo hayakuwamakosa wakati yalipotendwa. Kwa sababu hiyo Uislamuunatambua kanuni hii na kuitumia katika sheria zake.Kanuni hii ina maana kuwa sheria huanza kutumika baadaya kutangazwa na siyo kabla. Umuhimu wa kanuni hii nikulinda usalama wa raia na pia inazuia matumizi mabayaya madaraka.

Hii ni taafauti na mifumo yaa sheria za kitwaghutiambapo mtu anakamatwa kisha sheria inafuatia. Kamailivyotokea hapa nchini miaka ya themanini watuwalikamatwa kwa madai ya kuhujumu uchumi wa nchiwakati hakukuwa na sheria ya uhujumu uchumi. Baadaya watu kukamatwa ndipo ikatungwa sheria! Qur-animetaja kanuni hii katika Aya mbali mbali. Allah alikatazariba lakini hakuwaadhibu wale waliotoa au kula riba kablaya kushuka katazo hilo (taz:Qur-an 2:275). Allah piaanakataza kuwaoa ndugu wawili wakati mmoja, lakinihakuwaadhibu wale waliofanya hivyo kabla yakulidhihirisha kuwa ni kosa. (taz: Qur-an, 4:23)

Hali kadhalika, makatazo ya zinaa, wizi, ulevi namakosa mengine hayakutolewa adhabu iwapo yalifanywakabla ya kubainishwa wazi katika Qur-an.

Lengo la kanuni hii ni kutoa muda wa kutosha kwawatu juu ya makatazo ya Allah ili kuwapa fursa yakujirekebisha.

Taratibu za Mashtaka katika Sheria ya KiislamuMiongoni mwa mambo muhimu sana yanayohakikisha

usalama wa raia ni taratibu zinazotawala mwenendo wamashitaka. Taratibu hizi zina lengo la kuleta mizani ya

Page 114: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

103

haki kati ya haki ya dola ya kusimamia sheria na haki yaraia ya kuishi kwa amani bila usumbufu na kunyanyaswakinyume cha sheria.

Katika sheria ya Kiislamu watu wote ni sawa mbeleya Sheria. Taratibu zake za mashitaka zawezakugawanywa katika vipengele vikuu vinne:

1. Raia kudhaniwa kuwa hana hatia.2. Upepelezi na kuhojiwa.3. Haki za mshtakiwa wakati wa kusikiliza kesi.4. Haki za mfungwa.

Raia kudhaniwa kuwa hana hatiaKuhusu kanuni hii Mtume (s.a.w) amesema: “Kila mtoto

huzaliwa bila doa; ni wazazi wake ndio wanaomfanya aweMyahudi, Mkristo au Mmajusi.” (Bukhari) Mtume (s.a.w) piaamesema: “Msitoe adhabu ikiwa mna shaka”.

Hivyo chini ya sheria ya Kiislamu hadhi ya mshtakiwani ile ya mtu asiye na hatia. Hii ina maana kuwa jukumula kuthibitisha kosa linakuwa mikononi mwa mtuanayeshtaki. Mshatakiwa hatakiwi kutoa ushahidi wakukanusha kosa (negative evidence). Kumtaka mshtaki(mlalamikaji) atoe ushahidi wa kuthibitisha kutendekakwa kosa (positive proof) kunatokana na Hadithi ya Mtume(s.a.w) aliposema:

Lau watu wangeaminiwa kwa madai yao tu, baadhi yawatu wangedai damu na mali ya watu wengine, lakinimshtaki anawajibika kutoa uthibitisho wa madai yake.(Bukhari, Muslim, Ahmad).

Aidha matokeo mengine ya kanuni hii ni kuwa shaka(shubha) inamsaidia mshtakiwa. Katika sheria ya Kiislamuili kumtia mtu hatiani (conviction) inategemea uhakikakuwa mshtakiwa alitenda kosa na siyo uwezekano kuwa

Page 115: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

104

alitenda kosa. Ikiwa kutokana na ushahidi uliotolewahakimu bado ana wasi wasi basi itambidi aamue kuwamshtakiwa hana hatia.

Hii ni kutokana na Hadithi ya Mtume (s.a.w) aliposema:

“Msitoe adhabu ikiwa mna shaka. Mwacheni hurumshitakiwa, kwani bora kufanya kosa la kumsamehekuliko kosa la kumwadhibu.”

Haki za MshitakiwaWakati wa UpeleleziKumvamia mtu nyumbani kwake na kumpekua ni

kitendo kinachowaondoshea uhuru raia na chakumdhalilisha mtuhumiwa, hivyo sheria ya Kiislamuimeweka taratibu za kulidhibiti hili. Ikumbukwe kuwajamii itanufaika iwapo ukweli utajulikana kutokana naupelelezi utakaofanywa. Hivyo sheria ya Kiislamu imewekakanuni ya kuyaweka katika mizani yote mawili.

Sheria ya Kiislamu inazuia upekuzi wa nyumba za watupasi na sababu za kimsingi kisheria. Haki ya kila mtukuwa faragha imebainishwa katika Qur-an aliposema Al-lah (s.w):

Enyi mlioamini! Msiingie nyumba ambazo si nyumbazenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee Salaamwaliomo humo.Hayo ni bora kwenu; huendamtakumbuka.(24:27)

Page 116: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

105

Na kama hamtamkuta humo yoyote, basi msiingie mpakamruhusiwe. Na mkiambiwa “rudini”, basi rudini; hili nitakaso kwenu. Na Allah anajua mnayoyatenda. (24:28).

Hivyo kwa mujibu wa aya hizi kuingia katika nyumbaza watu kumekatazwa isipokuwa kwa idhini ya mwenyenyumba. Katazo hili halikomei katika nyumba tu, balilinahusu pia mali ya mwenye nyumba mwenyeweasipokuwapo. Mtume (s.a.w) amesema:

Mambo matatu hayaruhusiwi kwa mtu yeyote; mtuanayeongoza kundi katika swala asijiombee dua pekeyake, kwani akifanya hivyo atakuwa amewasaliti. Mtuasiangalie ndani ya nyumba ya mtu ila akipewa ruhusa.Na mtu asiswali hali amebanwa na haja hadi ajisaidiekwanza. (Muslim).

Mtume (s.a.w) pia ametumia lugha ya ishara ilikusisitiza haki ya mtu kuwa huru kutokana nakubughudhiwa faragha katika Hadithi ifuatayo:

Ikiwa mtu anakutazama (anakukodoleo macho) bilaridhaa yako na ukampiga kwa jiwe hadi ukalipofua jicholake huna hatia.

Haki hii pia inazihusu nguo zake mtu. Hakuna mtumwenye haki ya kumfunua mwingine nguo ili kuangaliakitu alichokificha bila ya idhini na bila sababu ya msingi.

Page 117: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

106

Aidha, kuilinda nyumba hakutakuwa na maana bilakumlinda mmilikaji pia. Barua zake mtu pia lazimazihifadhiwe. Hivyo ni haramu kuzisoma barua za mtu zakibinafsi baada ya kuzichukua kwa siri. Mtume (s.a.w)amesema: Mtu anayeisoma barua ya nduguye bila ruhusayake, ataisoma barua hiyo motoni.

Hata hivyo, chini ya sheria ya Kiislamu haki ya kuwana faragha na haki ya kutobughudhiwa yaweza kukiukwaikibidi ili kudumisha amani na usalama wa jamii. Vyombovya dola vyaweza kumpekua mtu kwa maslahi ya jamii.Lakini haki hiyo ya kupekua inatawaliwa na mashartiyanayohakikisha kuwa raia hanyanyaswi ovyo. Mashartihayo ni:1. Mtoaji wa amri ya kupekuwa ni mkuu anayehusika na

malalamiko (Wali-al-Muzahim). Kwa mujibu wa kanuniza mahakama za Kiislamu, hakimu hana haki ya kutoaamri ya upekuzi (search-warrant) wala si juu yakekutafuta ushahidi. Kazi yake ni kumwambiamlalamikaji kuleta ushahidi wa uthibitisho wa madaiyake.

2. Hati ya kupekua haiwezi kutolewa hadi kwanzaupatikane ushahidi wa kutosha unaoonesha kuwa upouwezekano mkubwa kuwa kosa limetendwa namshitakiwa. Kwa mfano ikiwa mtu mwadilifu anatoataarifa kuwa amemwona mtu anaingia faraghani namwanamke au kama mtu anapita nje ya nyumba naakasikia harufu ya pombe yatoka ndani na kelele zawatu waliolewa.

3. Kosa ligunduliwe kihalali, kuwa ikiwa limegunduliwakwa njia za haramu kama ujasusi (kwa mfano kwakutoboa tundu ukutani na kuchungulia ndaniaukusikliza kwa siri na kwa kuvizia. Ushahidi wakijasusi hauwezi kutumika kumtia mtu hatiani.

Page 118: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

107

Allah amesema:“Wala msipeleleze” (49:12)

Haki za Mtuhumiwa wakati wa KuhojiwaKatika sheria ya Kiislamu mahojiano siyo maana yake

mtuhumiwa kujibu maswali tu la. Bali ni fursa yakumwambia mtuhumiwa makosa yake na ushahidiuliopatikana dhidi yake, ili akiri au aukanushe ushahidihuo.

Vile vile katika sheria ya Kiislamu hakuna mtuatakayeadhibiwa mpaka kwanza mahakama ya wazi (yenyekushuhudiwa na watu) ithibitishe kosa lake. Kesi zafaragha ni haramu kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu piani haramu kumkamata mtu kwa kumshuku tu nakumsukumiza jela bila ya kufuata utaratibu wa mahakamana bila ya kumpa fursa ya kujitetea. Aidha ni haramukumtesa mtuhumiwa “ili aisaidie polisi” kuhusiana nauovu uliotendeka. Uadilifu katika kutoa hukumu, bila yaubaguzi wa aina yoyote ni jambo lililosisitizwa katikamisingi ya sheria ya Kiislamu:

“Na mnapohukumu baina ya watu hukumuni kwauadilifu”. (4:58)

Pia Mtume (s.a.w) amesisitiza:

“Nimeamrishwa kuhukumu kwa uadilifu”.

Katika sheria ya Kiislamu hairuhusiwi mtu kuwekwandani mpaka ahukumiwe kwa uadilifu, wala hapana yoyoteasiye na hatia kuadhibiwa au kutiwa ndani kwa makosaya mwingine au kwa niaba ya mwingine.

Page 119: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

108

Tofauti na sheria za kijahili ambazo humuonamtuhumiwa kuwa ana makosa kwanza mpaka aithibitishiemahakama kuwa hana makosa, sheria ya Kiislamuhumuona mtuhumiwa hana makosa mpaka mahakamaithibitishe kuwa ana makosa.

Haki za mtuhumiwa zinavyohifadhiwa1. Wanaohoji wawe wawili:

(i) Mkuu wa Malalamiko.(ii) Mwendesha mashtaka (Muhtasib).

2. Mtuhumiwa katika makosa ya Hudud na Qisas anahaki ya kutoapa.

3. Katika uchunguzi wa makosa ya Hudud anayo hakiya kukataa kuhojiwa, na anayo haki ya kukaa kimya.

4. Kimya chake hakiwezi kuwa ushahidi dhidi yake.

5. Mtuhumiwa asiteswe (au kufanyiwa ukatili).Mtume (s.a.w) amesema: Allah atawatesa siku yamalipo wale waliowatesa wenzao duniani. BwanaAudi ibn Artana alimwandikia Umar baruakumwomba ruhusa ya kuwatesa watu wanaokataakutuo Zaka. Umar akamkatalia.

6. Mahojiano yawe ya kibinaadamu, ili mtuhumiwaakiri kosa lake kwa hiari bila kulazimishwa. Mtume(s.a.w) alimwambia mtu aliyeletwa kwake kwatuhuma za wizi: “Sidhani kama uliiba; Je, uliiba? AuBwana Maaz alipokiri kuwa kazini, Mtume (s.a.w) alimpafursa ya kubatilisha ungamo lake, akamwambia, “Labdaulimbusu tu, au pengine ulimpapasa tu?” Aidhamwanamke mmoja alituhumiwa wizi, Mtume (s.a.w)akamwambia, “Je, uliiba? Sidhani kama uliiba. Semahapana” Hivyo kumpa fursa ya kufuta ungamo lake.

Page 120: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

109

7. Chini ya sheria ya Kiislamu mtuhumiwa awezakukana ungamo lake wakati wowote kabla yakutolewa adhabu. Bwana Maaz, alikana ungamolake baada ya kuanza kupigwa mawe, lakini wapigajihawakumwacha. Alipoambiwa Mtume (s.a.w)akasema, “Kwa nini hamkumwacha atubie? Allahangepokea toba yake”.

Haki za mshtakiwa wakati wa kusikilizwa kesi(1) Afunguliwe mashtaka haraka na ahukumiwe.

(2) Ushahidi katika makosa ya Hudud ni wa kisheriana si wa rai.

(3) Anayohaki ya kulipwa fidia ikiwa atahukumiwakimakosa.

(4) Ashitakiwe katika mahakama yenye mahakimuwenye ujuzi na waadilifu.

(5) Mtu yeyote pamoja na kiongozi wa nchi anawezakujibu mashitaka mahakamani.

(6) Mshitaki na mshitakiwa wote wana haki ya kumteuamtu wa kuwawakilisha mahakamani (wakili).

Haki ya Kuhukumiwa kwa UadilifuSheria ya Kiislamu ipo pale kusimamia uadilifu na lengo

lake si kuadhibu wala kukomoa bali kujenga jamii bora.Kila mtu bila ya kujali dini yake, rangi, taifa lake, uraiawake, (n.k.), anastahiki kuhukumiwa kwa uadilifu.Uadilifu katika kutoa hukumu umesisitizwa na ndiomsingi mkuu wa sheria ya Kiislamu:

Page 121: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

110

Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi (wa kupitisha haki)kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, muwe mkitoa ushahidikwa uadilifu… (5:8).

Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu,mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu;ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu au (juu ya) wazazi (wenu)na jamaa (zenu). Akiwa tajiri au maskini… basi msifuatematamanio mkaacha uadilifu… (4:135).

Mgawanyo wa MakosaSheria imeyagawanya makosa katika makundi

makubwa matatu:(i) Makosa ya Hudud(ii) Makosa ya Qisasi(iii)Makosa ya Ta’azir

Makosa ya HududMakosa ya Hudud ni yale ambayo yamekatazwa na Al-

lah na hukumu zake kutajwa katika Qur-an au Sunnah.Makosa hayo ni haya yafuatayo:

(1) Kuritadi (Ridda)Kuritadi ni Muislamu kuukanusha Uislamu kwamaneno aya yoyote ya Qur-an. Au kuukataa Uislamukwa vitendo kama vile kwa kuzini au kuyawacha

Page 122: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

111

maamrisho ya Qur-an kama vile swala na zaka. Mtuanahesabiwa amekanusha Uislamu kwa makusudina hali yakuwa anajua adhabu ya kufanya hivyo.

Mtu aliyeritadi anapewa muda wa kutubia kosa lake.Ukipita muda wa kutosha na hajatubia basi hukumuyake ni kuuliwa:Hukumu imetolewa katika Qur-an:

Basi wauweni washirikina popote muwakutapo nawakamateni mateka, na wazungukeni na wakalieni katikakila njia. Lakini wakitubu na wakasimamisha swala nawakatoa zaka, basi iacheni njia yao. Hakika MwenyeziMungu ni Mwingi wa kurehemu. (9:5).

(2) Uasi (Baghi)Baghi ni uasi dhidi ya kiongozi halali wa Kiislamu.

Uasi huo waweza kuwa hauna msingi wowote au wawezakuwa umetegemezwa katika kipengele fulani maalumambacho hao wapiganaji Waislamu wamekitegemea katikauasi wao. Kiongozi wa Kiislamu anatakiwa awasihi waacheuasi huo na ayajue madai yao ili ipatikane suluhu.Wakikataa ana haki ya kupigana nao. Hata hivyo iwapomadai yao ni ya haki na Imam ndiye aliyekwenda kinyume

Page 123: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

112

na Uislamu basi huyo kiongozi ndiye mwasi na walewanaopigana naye hawataadhibiwa. Kuhusiana na UasiAllah amesema katika Qur-an:

Na ikiwa makundi mawili katika Waislamu wanapigana,basi fanyeni suluhu baina yao; na likiwa mojawapolinamdhulumu mwenziwe, basi lipigeni lile linalooneampaka lirudie katika amri ya Mwenyezi Mungu. Na kamalikirudi basi yapatanisheni baina yao kwa uadilifu. Nahukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Munguhuwapenda wanaohukumu kwa haki. (49:9)

(3) WiziKuhusiana na wizi Allah anasema:

Na mwizi mwanamume au mwizi mwanamke, ikatenimikono yao; malipo ya yale waliyoyachuma. Ndiyoadhabu, itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na MwenyeziMungu ni mwenye nguvu na mwenye hikima. (5:38)

Hukumu ya mwizi ni kukatwa mkono wake wa kuliaiwapo yatatimia masharti yafuatayo:

Page 124: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

113

(a) Awe amekusudia kuchukua mali ya wizi pasi naidhini ya mwenye mali.

(b) Awe ameiondosha mali hiyo kutoka mahalainapowekwa.

(c) Awe amevunja sefu au kasha au kibweta cha fedha.(d) Mali iliyoibiwa iwe ni halali katika Uislamu, isiwe

mfano pombe, au nyama ya nguruwe au bangi n.k.(e) Mali iliyoibiwa iwe imefikia angalau thamani ya

kima cha chini Nisab yaani angalau tu ifikiethamani iliyo sawa kifedha na mizani moja. Juuya hili Mtume (s.a.w) analifahamisha: Mkono wamwizi usikatwe ila kama thamani ya mali iliyoibiwani sawa na thamani ya mizani.

Zipo kauli tofauti juu ya thamani ya Mizani, wenginewanasema ni robo (1/4) ya dinar ya dhahabu audinar tatu za fedha. Wengine wanasema ni dirhamkumi za fedha.

(f) Isiwepo “shubha”, yaani mazingira yatakayoruhusukutendeka kosa hilo.

TahadhariAdhabu ya mtu ambaye imethibitika kwa haki ya sheria

kuwa kaiba ni kukakwa mkono. Ndivyo Allah (s.w)alivyoamuru! Basi ole wao wale wanaochukuwa sheriamkononi kwa kuwapiga watu, kuwajeruhi, kuwachomamoto, na pengine kuwauwa kwa ajili ya kuwatuhumuuwizi. Ni vyema ikaeleweka kuwa mwenye haki yakuhukumiwa kifo, ni mtu aliyeuwa nafsi yenye haki yakuwa hai kisheria. Vinginevyo Qur-an inakataza!

Wala usiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza(kuiuwa) isipokuwa kwa haki (17:33).

Page 125: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

114

Atakayemuuwa mtu bila ya yeye kuuwa mtu, au bila yakufanya fisadi katika nchi, basi ni kama amewauwawatu wote (5:32)

(4) Ujambazi (Haraba)Adhabu ya ujambazi imefafanuliwa katika Qur-an kamaifuatavyo:

Basi malipo ya wale wanaopigana na Mwenyezi Munguna Mtume wake na kufanya uovu katika nchi ni kuuawana kusulubiwa au kukatwa mikono yao na miguu yaokwa mabadilisho, au kuhamishwa katika nchi. Hii ndiyofedheha yao katika dunia; na Akhera watapata adhabukubwa. (5:33)

Aya hii inawahusu wale wote wanaoifisidi jamii iwekijeshi au kwa kuvuruga amani na usalama wa watu namali zao, wanyama, mimea n.k. hivyo majambaziwanaotumia silaha wanaangukia chini ya sheria hii.

Page 126: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

115

Hukumu hii itatumika iwapo jambazi atakuwaamesababisha kifo au la Yaani katika hali zote nne:

(a) Iwapo raia atavamiwa bila kuporwa mali yake.(b) Iwapo raia atanyang’anywa mali yake kwa nguvu

lakini bila ya kuuliwa.(c) Iwapo raia atauliwa bila kuporwa mali.(d) Iwapo raia atauliwa na kuporwa mali.

(5) Uzinzi (zinaa)Adhabu ya zinaa ni kupigwa fimbo 100 hadharani, Allah(s.w) anasema:

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mpigenikila mmoja katika wao mijeledi mia. Wala isiwashikenikwa ajili yao huruma katika (kupitisha) hukumu hii yaMwenyezi Mungu ikiwa nyinyi mnamuamini MwenyeziMungu na siku ya mwisho. Na lishuhudie adhabu yao(hii) kundi la Waislamu. (24:2).

Sharti la kutolewa adhabu ya zinaa ni kupatikana kwamashahidi wanne walioshuhudia kitendo hicho au kukirikosa kwa mzinzi mwenyewe.

(6) Kashfa (Badhf)Kashfa (defamalion) yawezekana ikawa ni msemo (slan-der) vijembe (innuendo) au maandiko na machapisho (li-bel) yenye lengo la kutoa kejeli dhidi ya, kutusi aukushusha hadhi ya mtu. Kuhusiana na kosa hili Qur-animetoa adhabu ifuatayo:

Page 127: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

116

Na wale wanaowasingizia wanawake wataharifu (kuwawamezini) kisha hawaleti mashahidi wanne, basiwapigeni mijeledi thamanini na Msiwakubalie ushahidiwao tena, na hao ndio mafasiki. (24:4).

Kashfa katika sheria ya Kiislamu ni kumzulia mtukuwa kazini au kulawiti au kulawitiwa au kumkashifumtu muadilifu, mwenye akili timamu na uwezo wa kimwiliwa kutenda kosa alilozuliwa.

(7) Kunywa uleviQur-an imeharamisha ulevi pale aliposema Allah (s.w):

Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwaasiyekuwa Mwenyezi Mungu na kutazamia kwa mishaleya kupigia ramli ni uchafu (ni) katika kazi za shetani. Basijiepusheni navyo, ili mpate kufaulu. (5:90).

Hivyo ilipoteremka aya hii ya 90 na 91 Waislamu waliitiiiamri ya Allah kwa kumwaga ulevi wote waliokuwa nao.Mtume (s.a.w) alitoa adhabu kwa mlevi kuwa nikutandikwa viboko 40 kama alivyo amuru:

Page 128: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

117

“Yule anywaye ulevi mpigeni bakora”

Imesimuliwa na Anas bin Malik (r.a) kuwa:

Mtume (s.a.w) alimpiga mlevi kwa matawi (majani) yamtende na kwa viatu. Na Abu Bakr alimwadhibu (mlevi)kwa fimbo arobaini. (Bukhari).

Makosa ya QisasBaada ya makosa ya Hudud, kundi la pili ni lile la

makosa ya Qisas.

Neno qisasi lina maana ya “usawa” au “kufanana”. Linamaana kuwa mtu aliyetenda kosa fulani ataadhibiwa vilevile na kwa namna ile ile aliyotumia katika kumdhulumumwenzake (kulipiziwa).

Haki ya Qisasi imewekwa na Allah (s.w) katika Qur-an:

Page 129: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

118

Enyi mlioamini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katikawaliouawa – Muungwana kwa muungwana na mtumwakwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke.Naanayesamehewa na ndugu yake chochote basi ashikwekulipa kwa wema; na yeye alipe kwa ihsani. Hiyo nitahafifu itokayo kwa Mola wenu na ni rehema. Naatakayeruka mipaka baada ya haya, basi yeye atapataadhabu iumizayo. (2:178)

Kimsingi makosa ya kisasi ni ya namna mbili: Makosaya kuua na makosa ya kujeruhi. Makosa ya kisasiyanahesabiwa kuwa ni kukiuka haki ya mtu binafsi nahivyo sheria inampa fursa mtu au ndugu zake kulipa kisasiau kulipwa fidia. Kuhusu fidia tazama Qur-an 4:92. Hayani maelezo ya jumla tu. Hata hivyo kabla ya kutekelezwakwa kisasi au fidia yapo mambo kadhaa ya kuzingatiakuhusiana na ushahidi wa kosa, na adhabu.

Makosa ya Ta’azirMakosa ya Ta’azir ni yale yote ambayo Qur-an na

Sunnah havijaweka adhabu fulani maalum. Adhabu zamakosa ya aina hii hutolewa na Jaji kwa idhini ya kiongoziwa Kiislamu. Neno Ta’azir lina maana ya adhabu. KisheriaTa’azir lina maana ya adhabu ambayo haijawekwa mojakwa moja katika Qur-an bali hutegemea maamuzi ya Jajiau hakimu kwa kulinganisha kosa, mazingira ya kosa naadhabu.

Haki za wasiokuwa Waislamu (Dhimmi)

Sheria ya Kiislamu imewapa haki wasiokuwaWaislamu kama ifuatavyo:

(i) Haki ya ulinzi wa maisha na maliDamu ya Dhimmi ni haramu kumwagwa pasipo

sababu kama ilivyo damu ya Muislamu. Muislamu akimuua

Page 130: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

119

Dhimmi adhabu yake ni sawa na ile ya kumuua Muislamu.Mtume (s.a.w) amesema:

“Ni jukumu langu kusimamia haki za wanyonge”.

Vile vile mali ya Dhimmi katika sheria ya Kiislamuinathaminiwa kama ilivyo mali ya Muislamu. Muislamuakiiba mali ya Dhimmi kwa kiwango kile kilichotajwa naMtume atahukumiwa kukatwa mkono kama kawaida.

Khalifa wa nne wa Mtume (s.a.w.) baada yakumuhukumu Muislamu mmojakuuawa na warithi wa Dhimmi aliyemuua, alisisitiza:

Yeyote aliye Dhimmi wetu damu yake ni takatifu kamadamu yetu na mali yake ni takatifu kama mali yetu.

(ii) Haki katika sheria ya jinaiKatika sheria ya Kiislamu hukumu za makosa ya

jinai (penal laws) zinawahusu wadhimmi sawa nazinavyowahusu Waislamu. Makosa ya jinai ni makosayanayoathiri jamii nzima na mhalifu atakuwaanaidhulumu jamii nzima. Kwa hivyo Dhimmi akiibaatakatwa kiganja chake cha mkono wa kulia, akiziniatatandikwa viboko 100.

Ila Dhimmi hataadhibiwa kwa kosa la ulevi kamaatakavyoadhibiwa akilewa Muislamu kwa kutandikwaviboko 40,

(iii) Haki katika sheria za Madai (Civil Laws)Katika sheria ya Kiislamu hukumu za madai ni sawa

sawa kwa Waislamu na wasio kuwa Waislamu. Kilamwenye kudaiwa atahukumiwa na sheria kutoa haki yamdai bila ya ubaguzi wa dini. Pia yale yaliyo haramishwakwa Waislamu katika uchumi pia sheria inayakataza kwa

Page 131: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

120

madhimmi. Kwa mfano riba na kamari ni haramu kwaWaislamu na imekatazwa pia kwa wasiokuwa Waislamukwani riba na kamari huiathiri jamii nzima.

(iv) Haki ya heshima ya DhimmiKumvunjia heshima dhimmi kwa kumtukana, kumuita

jina baya, kumdhuru, kumuadhiri, kumteta, n.k. nimakosa makubwa sana mbele ya Allah (s.w) kama ilivyomakosa makubwa kumfanyia Muislamu. Heshima ni hakiinayomstahiki kila mwanadamu pasi na ubaguzi wa ainayoyote. Ni dhima ya serikali ya Kiislamu kulinda heshimaya kila mtu.

(v) Sheria ya Mtu binafsiKatika sheria ya Kiislamu, mambo yote yanayohusu

imani ya mtu binafsi huhukumiwa kulingana na imani yadini yake. Kama jambo lililoharamishwa kwa Waislamusi haramu kulingana na imani ya Dhimmi, sheriaitaendelea kumruhusu kulitenda jambo hilo.

Page 132: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

121

Zoezi la Tatu

1. Eleza maana ya sheria kilugha na kisheria.2. Taja na kufafanua kwa muhtasari kazi za sheria katika jamii na manufaa yake.

3. Sheria zilizotungwa na wanadamu hazizingatii umbile halisila mwanadamu, hivyo huzidisha matatizo badala ya kutatua.Jadili kwa kutoa mifano hai toka katika jamii yako.

4. Bainisha udhaifu uliopo kwenye chimbuko la sheriazilizotungwa na wanadamu kwa msukumo wa matashi namahitaji, uzoefu, sayansi, akili na fikra zao.

5. (a) Taja misingi mikubwa miwili ya sheria za Kiislamu. (b) Eleza maana ya Al-Qiyaas na Al-Ijima’a; na tafauti zake.

6. Eleza kwa muhtasari, kwanini sheria za Allah (sw) ndizozenye uwezo wa kuondoa dhulma na ukandamizaji, nakusimamisha haki na uadilifu katika jamii.

7. (a) Taja makundi mawili ya amali za waja kwa mujibu waQur’an. (b) Orodhesha daraja tatu za matendo mema.

8. Kazi ya Sheria za Kiislamu, ni kumnufaisha na kumhifadhimwanaadamu.Thibitisha kwa dondoo tano zenye maelezomafupi.

9. Bainisha (a)Kanuni tatu zenye kumtwika au kumvua mja dhima yakuhukumu au kuhukumiwa katika sheria ya Kiislamu. (b) Utaratibu wa mashitaka wa Kiislamu. (c) Tanzu za makosa katika sheria ya Kiislamu.

10. Uislamu ni mfumo wa maisha wa kiadilifu, hivyo, haunyimiwala kukandamiza haki za wasiokuwa Waislamu. Dhihirishaukweli huu kwa kurejea Qur’an na Sunnah.

Page 133: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

122

Sura ya Nne

UCHUMI

Maana ya UchumiMfumo wa maisha wa Kiislamu humuelekeza

binaadamu kujenga na kudumisha uhusiano wake na Al-lah (s.w), uhusiano wake na binaadamu wenziwe nauhusiano wake na vinavyomzunguka katika ulimwenguhuu. Aidha mfumo wa Kiislamu una lengo la kuelekezanamna ya kukiendea kila kipengele muhimu cha maishaya binaadamu uchumi ukiwa miongoni.

Uchumi hujumuisha uzalishaji, usambazaji na utumiajiwa mali na huduma. Uislamu umelipa suala la uchuminafasi muhimu kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:

“Wala msiwape wapumbavu mali zenu ambazo Allahamezijaalia kuwa msingi wa maisha yenu…” (4:5)

Uislamu umeweka utaratibu wa kiuchumiunaohakikisha kuwa haki inatendeka kwa wote ilikudumisha amani, utulivu na mshikamano wa kweli katikajamii. Katika sura hii tutaangalia uchumi katika Uislamukwa kuzingatia maeneo yafuatayo:

1. Nadharia ya uchumi wa Kiislamu.2. Umuhimu wa uchumi katika Uislamu.3. Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu.4. Sera ya uchumi katika Uislamu.5. Haki na Uhuru wa kuchuma katika Uislamu.6. Mgawanyo wa mali katika Uislamu.7. Umuhimu wa Benki katika Uchumi.8. Tatizo la Riba.

Page 134: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

123

1.Nadharia ya uchumi wa KiislamuMfumo wa uchumi katika Uislamu ni utaratibu

utokanao na Qur-an na Sunnah juu ya uzalishaji,umilikaji, usambazaji, na utumiaji wa mali na hudumapamoja na miiko yake. Kwa msingi huo, uchumi huoumejengwa juu ya fikra ya ukati na kati (Iqtisaad), hivyoumetofautiana na mifumo mingine iliyobuniwa na watu.Dhana (concept) ya ukati (Iqtisaad) katika shughuli zakiuchumi ni kule kutoa uhuru kwa mtu binafsi (sektabinafsi) kuchuma na kumiliki mali ili iwe motisha kwakeya kuchapa kazi wakati huo huo serikali ikisimamia nakutoa miongozo katika uzalishaji na ugawaji, na vile vilekuwa na sekta zake (sekta za umma) ili kila mwana jamiiapate haki za kimsingi. Mifumo iliyobuniwa na watuimeathiriwa na udhaifu wa kibinaadamu wa kuelemeaupande huu au ule.

Ipo mifumo ya kiuchumi kama vile ubepari ambaoumeelemea mno katika ubinafsi kiasi ambacho umepuuzakabisa haki za kijamii. Katika mfumo huu (ubepari) ummahauna chake; mali, huduma na shughuli mbali mbalihubinafsishwa. Wachache chini ya mfumo huu ndiohunufaika na rasilimali za Taifa. Hujilimbikizia mali, namotisha yao ya uzalishaji ni ile faida waipatayo. Serikalikuu ya mfumo huu wa kibepari hushirikiana na wachachehao waliohodhi mali, kuwanyonya walio wengi.

Pia, kuna mfumo wa uchumi wa Kikomunist au Kijamaaambao nadharia yake imeelemea mno katika “usawa” wasare kiasi cha kudhoofisha mno motisha ya watu binafsina hivyo kupelekea kukosekana kwa ufanisi katikauzalishaji. Katika mfumo huu mali na shughuli mbalimbali hutaifishwa (toka milki ya watu binafsi kuwa milkiya taifa). Ukweli ni kwamba huwa si mali ya taifa kamainavyotangazwa bali mbiu ya “usawa”, na “mali ya umma”,chini ya mfumo huu, ni mwavuli tu uliokinga kikundi cha

Page 135: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

124

watu kilichojipa mamlaka ya uendeshaji wa nchi kwa suraya chama au serikali kwa maslahi ya kikundi hicho.Kikundi hicho ndicho humiliki na kutafuna mali hukuwananchi wengi wakiendelea kudhulumiwa kwa sababumbali mbali. Hivyo hakuna usawa ulio chini ya mfumohuu bali ni ubinafsi ule ule ambao huhamishwa toka kwamtu binafsi kwenda kwenye kikundi fulani.

Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ileya Kitwaghuti

(i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio

yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupataradhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya MwenyeziMungu.Mafanikio hayapimwi kwa mali. Katika uchumi waKitwaghuti mafanikio maana yake ni mafanikio yakiuchumi. Ni kiasi gani cha mali mtu amefanikiwakukipata.Jinsi atakavyojilimbikizia mali ndivyoitakavyoonesha “mafanikio” yake. Katika Uislamu kufuzukwa kweli ni kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kufelikukubwa ni kule kukosa radhi hizo. Hivyo ili binaadamuafanikiwe hana budi kuishi kwa uadilifu.

Mtazamo huu unaathiri pia mizani yake ya wakati.Muislamu anapozitumia rasilimali zilizomo katika ardhihafikirii tu mahitaji yake ya binafsi ya sasa bali piamatokeo ya vitendo vyake kwa vizazi vijavyo.

Kwa mtazamo huu mtu anakuwa hana haki ya kufujamali au rasilimali za ardhi, kwa vile anazingatia maslahiyake katika maisha haya, huko akhera na maslahi yaviazazi vijavyo. Mafanikio katika Uislamu ni kule kulijualengo la maisha hapa ulimwenguni, kuwa na kumbukiziya kisimamo mbele ya Mola siku ya hesabu, kukinai

Page 136: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

125

moyoni na kuona kila kitu cha ulimwengu huu kuwa nicha kawaida. Kujitahidi kuyaendea mambo mema bila yakuchelea chochote na kujiepusha na yale yote yanayowezakumtoa mtu au kumkhasirisha katika maisha yajayo hatakama yana “manufaa” kwa mtazamo wa wengi katikamaisha haya. Kujali shida na matatizo ya wengine nakuweza kutoa kwa ajili ya kuwasaidia wengine kwa kadiriya wasaa uliopo.

Kuwa na huruma, mapenzi na bashasha isiyobaguataifa, kabila, nasabu wala ukoo wa mtu. Kutokuwa nachuki, majivuno, kibri, utesi, usengenyi, ulimbukeni,kujiona, kujitukuza au kujidhalilisha na kujitweza kwayeyote yule anayemulikwa na jua iwe kihali au kimali.

Aliyetajiri wa Nafsi ni yule ambaye fursa yoyotealiyonayo haiwi kero na huzuni kwa wengine bali huitumiamwisho wa uwezo wake kupambana na taratibu potofu nakandamizi zinazotawala jamii yake. Hii ndiyo Dhana yamafanikio katika Uislamu.

(ii) Dhana ya umilikaji maliKatika Uislamu mmiliki wa hakika wa mali ni Mwenyezi

Mungu, mwanaadamu kama Khalifa wa Allah hapa dunianianamiliki mali kwa dhamana tu siyo kwa hakika na kwasababu hiyo ataulizwa jinsi alivyotumia hiyo mali.

Pamoja na hivyo mali katika Uislamu si kitu kiovu balikinachosisitizwa ni kuwa ichumwe na kutumiwa kwakuzingatia maelekezo ya Mwenyezi Mungu.

Kuhusu kutafuta mali Qur-an inatueleza kamaifuatavyo:

Page 137: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

126

“Na utafute – kwa yale aliyokupa Mwenyezi Mungumakazi mazuri ya akhera wala usisahau sehemu yakoya dunia”. (28:77)

(iii)Dhana ya bidhaaKatika uchumi wa kitwaghuti kitu chochote chaweza

kuwa ni bidhaa maadamu kinaweza kutumiwa na mtu.Kwa mfano pombe pamoja na madhara yake huitwa bidhaakwa kuwa hutumiwa na baadhi ya watu.

Katika uchumi wa Kiislamu “bidhaa” huitwa ama“Atwayyibaati” au “Rizk”. Atwayyibaat ni kitu kizuri, safi,Twahara. Rizk ni neema, au hidaya itokayo kwa Allah(s.w). Hivyo katika uchumi wa Kiislamu bidhaa ni vilevitu halali tu kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu.Kisichokuwa halali si bidhaa. Kwa mfano pombe ni haramuhivyo si bidhaa.

(iv)Dhana ya MatumiziKwa kuwa Allah ndiye Muumba wa watu na rasilimalizote katika ulimwengu, sera ya uchumi wa Kiislamuhaimpi mtu fursa ya kufuja mali apendayo pamoja nauhalali atakaokuwa nao katika dhamana ya milki ya malihiyo. Kinyume chake, katika uchumi wa Kitwaghuti mtuanayo fursa ya kufuja mali apendavyo maadam ni mmilikiwa mali hiyo.

(v) Mizani ya wakati katika tabia ya mtumiajiMtu anapofanya maamuzi yoyote hujiuliza nini matokeoau matazamio ya kitendo hiki au uamuzi huu baada ya

Page 138: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

127

saa moja au wiki moja au mwezi mmoja au mwaka mmojaau miaka mitano au kumi n.k. Kipimo cha wakati katikauchumi wa Kitwaghuti na ule wa Kiislamu ni tofauti.Katika ujahili mtu hujiuliza mali kiasi gani awe amepataatakapofikia umri fulani, kinyume chake Muislamuanapofikiria jambo lolote, pamoja na masuala ya uchumi,kipimo chake cha wakati hukipa upeo mpana sana.Hujiuliza, je hiki kitendo ninachofanya kitakuwa namatokeo gani siyo tu kwa wiki hii au mwezi huu au mwakahuu au ujao bali kina matokeo gani siku ya kiyama.Muislamu anaamini kuwa ipo siku ya malipo na kwambakuna pepo na moto. Watu watahesabiwa na kulipwa kwamujibu wa matendo yao. Kila mtu binafsi atasimamishwapeke yake mbele ya Mwenyezi Mungu na kupewa hisabuyake. Imani hii ina athari kubwa kwa Muislamu namaamuzi yake anayochukuwa.

Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote

mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikiaazma hiyo. Miongoni mwa rasilimali kuu (natural re-sources) ni zile zinazohusiana na ardhi, maji na wanyama.Kwa mujibu wa Uislamu rasilimali hizo ni neema za Allah(s.w).

(a) Rasilimali za Ardhi

Page 139: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

128

“Na katika ardhi mna vipande vinavyoungana (na kuzaakwake namna mbali mbali) na mna mabustani yamizabibu, na mimea mingine, na mitende ichipuayo katikashina moja na isiyochipua katika shina moja. Vyotevinavyonyweshelezwa (vinamiminiwa) maji yale yale; natunavifanya bora baadhi yake vyengine katika kula(katika utamu). Hakika katika haya zimo ishara kwa watuwanaotia mambo akilini”. (13:4)

(b) Rasilimali za maji na mvua

“… Na unaiona ardhi imetulia kimya lakinianapoyateremsha maji juu yake, inataharaki na kukuwana kuotesha kila namna ya mimea mizuri.” (22:5)

“Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha majikutoka mawinguni. Kisha akayapitisha (chini kwa chini)yakawa chemchem katika ardhi, tena akaotesha kwayomimea ya rangi mbali mbali (na sura mbali mbali)…”(39:21).

Page 140: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

129

(c) Rasilimali za bahari na samaki

“Mwenyezi Mungu ndiye aliyekutiishieni bahari ili humozipite merikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yakena mpate kushukuru”. (45:12)

“Na yeye ndiye aliyeitiisha bahari ili humo mule daimakitoweo kipya (samaki) na mtoe humo mapambomnayoyavaa. Na utaona merikebu zikipasua humo, ilimtafute fadhila zake (kwa kufanya biashara) na ili mpatekushukuru.” (16:14)

(d) Rasilimali za wanyama

“Na (pia) amewaumba wanyama. Katika hao mnapata(vifaa vitiavyo) joto na manufaa; na wenginemnawala(16:5).

Page 141: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

130

Na mnaona raha mnapowarudisha jioni namnapowapeleka malishoni asubuhi.(16:6)

Na (wanyama hao pia) hubeba mizigo yenu kupelekakatika miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashakana taabu. Hakika Mola wenu ni Mpole sana (na) Mwenyerehema nyingi”.(16:7)

Na (amewaumba) farasi na nyumbu na punda ilimuwapande na (wawe) mapambo. Na ataumba (vipandovyingine) msivyovijua”. (16:8).

(e) Rasilimali za madiniMuhutasari wa aya hizo juu ya rasilimali unapatikana

katika aya ifuatayo:

“Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katikaardhi.” (2:29).

Page 142: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

131

Wajibu wa KufanyakaziUislamu siyo tu unawahimiza watu kufanya kazi na

kutokuwa wavivu bali kufanya kazi ni Ibada. Kila jambolenye manufaa kwa watu binafsi, familia, jamii (n.k) lawezakuhesabiwa kuwa ni Ibada kwa Allah yakitimia mashartimawili; usafi wa nia (Ikhlasi) na kutenda jambo kwakuzingatia mipaka ya sheria ya Kiislamu. Hivyo kazi niIbada. Kufanya kazi ni wajibu alionao mtu mbele yaAllah.Qur-an inawahimiza Waislamu kutenda kazi nzurizenye manufaa katika eneo lolote lile.

Na sema: Tendeni mambo (mazuri). Mwenyezi Munguatayaona mambo yenu hayo na Mtume wake naWaislamu. Na mtarudishwa kwa mjuzi wa siri na dhahiri;naye atakwambieni (yote) mliyokuwa mkiyatenda.”(9:105)

Katika aya hii Mwenyezi Mungu amefungua milangokwa watu kutenda mambo yote mema katika eneo lolotela uchumi au siasa na yeye ataliona na atalilipa.

Uchaguzi wa kaziUislamu umempa mtu uhuru wa kuchagua kazi yoyote

aipendayo maadamu kazi hiyo ni ya halali kwa mujibu washeria ya Kiislamu. Na ni wajibu wa serikali ya Kiislamukuhakikisha kuwa watu wanapata fursa ya kufanya kaziwazipendazo. Watu watafanya kazi kwa mujibu wa vipajivyao, kwani Mwenyezi Mungu amewajaalia watu vipawambali mbali:

Page 143: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

132

“Na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine darajakubwa ili akufanyieni mtihani kwa hayo aliyokupeni.”(6:165).

Kila mtu anafanyiwa mtihani kwa neema au kipawaalichopewa. Katika maisha yetu ya kila siku wanaadamuni viumbe wanaotegemeana kila mmoja ananufaika kwakazi ya mwenzake. Daktari atamhitaji Muashi kumjengeanyumba yake na Muashi atamhitaji Daktari kumtibumaradhi yake n.k. Katika Uislamu kazi hutegemea uwezotu hakuna kazi zilizotengwa kwa ajili ya watu wa ukoo aukabila au nasaba fulani.

Tofauti ya malipoTofauti ya mapato au malipo ipo kwa sababu ya utendaji,

uwingi au ubora wa bidhaa zilizozalishwa. Ni halali kwafundi aliyetengeneza mashati kumi, hasa amzidi kipatoyule aliyetengeneza matano. Au yule aliyetengeneza kitubora lazima amzidi yule aliyetengeneza kitu duni. Aidhatafauti ya mapato pia ni halali iwepo kutokana na mudamrefu wa mafunzo baadhi ya kazi zikilinganishwa nanyingine. Kwa mfano ikiwa mtu ataajiriwa kufutamavumbi katika madirisha ya ofisi atahitajia siku moja tuya kuelekezwa namna ya kuifanya kazi hiyo. Lakini mtuakiajiriwa kutengeneza madirisha hayo atahitajia mudamrefu zaidi katika kujifunza useremala hawezi kuelekezwakwa siku moja tu halafu akaweza kuunda dirisha. Hivyomalipo ya mfutaji na mtengenezaji wa madirisha hayawezikuwa sawa. Malipo yao yakiwa sawa basi watu wanaweza

Page 144: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

133

kuzikwepa kazi zinazohitaji mafunzo ya muda mrefu kamaudaktari, usanifu majengo uhandisi (n.k.) na kukimbiliazile zenye mafunzo ya muda mfupi kama utarishi,uhudumu, kufagia ofisi n.k.

Aidha malipo hayatakuwa halali iwapo shughulianayoifanya Muislamu ni faradhi. Kwa mfano; si halalikwa Imamu kupokea mshahara kwa ajili ya kusalishaswala za faradhi, si halali kupokea malipo kutokana nakumhudumia maskini, n.k.

Hifadhi ya WafanyakaziUislamu pia umeweka taratibu za kuhifadhi haki na

maslahi ya Wafanyakazi. Kwanza kila mfanyakazi lazimaawe na mkataba na mwajiri wake. Mkataba huo uwekewazi malipo yake na kazi yake na makubaliano yaomengine. Mkataba huo ni bora uwe kwa maandishi lakiniwaweza pia kuwa kwa mdomo.

Mwenyezi Mungu ameagiza katika Qur-an kuwa watuwatekeleze kikamilifu ahadi zao za halali.

“Enyi mlioamini tekelezeni wajibu …” (5:1)

Katika Hadith iliyosimuliwa na Bukhari, Mtume (s.a.w)amesema kuwa miongoni mwa watu watatu ambao Mtume(s.a.w) atawakataa siku ya Kiyama ni yule anayemwajirimfanyakazi halafu asimpe haki zake.Katika Hadithnyingine amesema;Mlipeni mtu mliyemuajiri kabla yajasho lake halijakauka. Mradi wa Hadith hii ni kuwa mtuasicheleweshewe malipo yake. Kama mapatano ni kilawiki au kila mwezi n.k. basi muda huo ukifika tu mtualipwe.Vivyo hivyo kwa mfanyakazi malipo ya kazi yatakuwa

Page 145: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

134

ni halali iwapo atatimiza kipimo walichoafikiana na mwajirikwa mshahara huo. Kutegea kazi humfanya mtu achukuesehemu ya malipo isiyo haki yake. Kwa hiyo, kipatokinachotokana na kazi iliyotegewa kimechanganyika nakipato cha haramu. Uislamu unamtaka kila muumini awemwaminifu na muadilifu katika kazi baada ya kupatanana kukubaliana na muajiri.

2. Umuhimu wa uchumi katika UislamuMwanaadamu ameumbwa na mahitajio mengi ambayo

hana budi kuyapata ili aweze kuishi kwa furaha na amanihapa ulimwenguni. Kwa kuwa mwanaadamu nimchanganyiko wa mwili na roho, pia mahitajio yakeyamegawanyika, ana mahitajio ya kiroho na kimwili.Mahitajio ya kiroho ambayo humuwezesha mwanaadamukuishi maisha ya utulivu yenye furaha na amani,hupatikana kwa kufuata kwa utii na unyenyekevumwongozo wa Allah (s.w).

Mahitajio ya kimwili kama vile chakula, mavazi, vipandona njia ya uchumi hupatikana kwa kuchapakazi chini yamazingira yatokanayo na itikadi sahihi yenye kusimamiwana viongozi wanaozingatia haki itokayo kwa Muumba.Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Allah (s.w)amejaalia mali anayoichuma mwanaadamu iwe ndiyoinayoboresha maisha yake:

“Wala msiwape wapumbavu mali zenu ambazo MwenyeziMungu amezijaalia kwa ajili ya maisha yenu …” (4:5)

Page 146: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

135

Kutokana na aya hii, kuchuma mali si jambo la hiarikwa mwanaadamu kwani kwa namna Allah (s.w)alivyokadiria, maisha ya mwanaadamu kwa hapaulimwenguni hayawezekani pasi na kuchuma.

Ni kweli kwamba vitu vyote vilivyomzungukamwanaadamu katika ulimwengu huu vimeumbwa kwa ajiliyake kwa ushahidi wa Qur-an:

“Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katikaardhi…” (2:29).

Lakini mara nyingi vitu hivi haviko katika hali yakutumiwa na mwanaadamu moja kwa moja. Balimwanaadamu analazimika kutumia elimu yake, Maarifayake, juhudi zake na vipawa vyake vingine ili ayabadilishemazingira yake yaweze kumtumikia na kukidhi haja zake.

Kwa mtazamo huu Uislamu unatuamrisha kuchumakama unavyotuamrisha kusimamisha Swala, kutoa Zakatna kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi:

Na itakapokwisha swala, tawanyikeni katika ardhimtafute fadhila za Mwenyezi Mungu na mkumbukeniMwenyezi Mungu kwa wingi, ili mpate kufaulu. (62:10)

Tunajifunza kutokana na aya hii kuwa, kuchuma niwajibu unaompasa Muislamu mara tu baada ya kutekeleza

Page 147: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

136

Ibada maalum. Hili linabainishwa katika Hadithi ifuatayo:

“Abdullah bin Mus’ud ameeleza kuwa Mtume (s.a.w)amesema: Kutafuta chumo la halali ni faradhi baada yakutekeleza faradhi nyingine.” (Baihaqi).

Pia Mtume (s.a.w) amebainisha wazi ubora wa kujizatitikatika kutafuta chumo la halali kwenye Hadith ifuatayo:

“Miqdam bin Ma’ad Yakrab ameeleza kuwa Mtume waAllah amesema: Hapana mmoja wenu aliyekula chakulakizuri kuliko kile alichokula kutokana na kazi ya mkonowake mwenyewe. Na Daud, Mtume wa Allah, alikuwaanakula kutokana na kazi ya mikono yake.” (Bukhari)

Kwa upande mwingine Uislamu unalaani uvivu nakuwategemea wengine pasi na sababu au dharura maalumkama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:

“Jubair bin Awam ameeleza kuwa Mtume wa Allahamesema: Mmoja wenu kuchukua kamba na kisha akajana mzigo wa kuni akiwa amebeba mgongoni mwake naakauuza, na kwakufanya hivyo Allah akailinda hadhiyake, ni bora kwake kuliko kuomba omba watu, wakimpachochote au wasimpe (Bukhari.)

Mpaka hapo tumejifunza kuwa kwa mtazamo waUislamu, uchumi ndio msingi wa maisha ya mwanadamuhapa ulimwenguni na Uislamu umewajibisha kuchumakwa kila mwenye uwezo.

Ni makosa katika Uislamu mtu mwenye uwezo na afyakubweteka na kuwategemea wengine katika kukidhimahitaji yake.

Page 148: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

137

3.Mazingatio muhimu katika uchumi wa KiislamuKanuni kuu za uchumi katika Uislamu ni:

(i) Kumwamini Allah kuwa ndiye Muumba na mfalmewa ulimwengu huu yaani kumtii Allah katika mamboyote.

(ii) Binaadamu ni Khalifa wa Allah hapa duniani, hivyowajibu wake ni kusimamisha amri ya Allah.

(iii) Ili kumsaidia mwanaadamu kutimiza wajibu wakekama Khalifa, Allah amemdhalilishia kila kitukatika ulimwengu huu:

“Mwenyezi Mungu ndiye aliyekutiishieni bahari ili humozipite merikebu kwa amri yake ili mtafute fadhila yakena mpate kushukuru”. (45:12).

“Je, Hukuona kwamba Mwenyezi Mungu amevitiishakwa ajili yenu vilivyomo ardhini…” (22:65)

“Je, Hukuona kwamba Mwenyezi Mungu amekutiishienivilivyomo mbinguni na ardhini na anakukamilishienineema zake zilizo dhahiri na za siri? …” (31:20).

Page 149: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

138

“Yeye ndiye aliyefanya ardhi iweze kutumika kwa ajiliyenu. Basi nendeni katika pande zake zote na kulenikatika rizki zake na kwake ndiyo marejeo.” (67:15).

Hivyo kuzitumia neema hizo za Allah si dhambi balini katika kushukuru.

(iv) Kutokana na wajibu wa Ukhalifa wa Allah,mwanaadamu ataulizwa kwa neema alizompatia naatahesabiwa kwazo, ikiwa ni pamoja na namnaalivyochuma na kutumia mali.

(v) Kuwa na mali au kutokuwa na mali nyingi au kidogosi dalili ya ubora au udhalili wa mtu. Hali zotembili ni mtihani. Anachotazama Allah ni nyoyo zawatu.

Misingi au kanuni hizo zikithibiti katika moyo wa mtuzinakuwa na athari kubwa sana katika shughuli zakiuchumi za Muislamu.

Kanuni ya kwanza kwa mfano humfanya mtu afuatemaamrisho ya Allah na hivyo atafanya kila njia ajiepushena makatazo yake.

Pili, kwa kujua kuwa yeye ni Khalifa tu atajua yeye simmilikaji wa hakika, hivyo atafuata maagizo ya huyoaliyempa ukhalifa yaani Allah.

Tatu, atajua kuwa utajiri si kitu cha kukipigania, bali

Page 150: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

139

mtu apiganie maisha bora na afya katika kutafuta radhiza Allah (s.w).

Nne, kwa kujua kuwa atahesabiwa na Allahanayeshuhudia kila kitu ataendesha shughuli zake zakiuchumi kwa kumcha Allah.

4. Sera ya uchumi katika UislamuKwanza, katika Uislamu utekelezaji wa mambo yote

hutegemea zaidi ucha-Mungu wa mtu binafsi na kuogopakwake kusimamishwa mbele ya Allah na kuhisabiwa,kuliko usimamizi wa vyombo vya dola kama sheria,mahakama, na askari polisi. Hii ni kwa sababu hisabusiku ya kiyama itakuwa kwa kila mtu binafsi. Hapana shakavyombo vya dola vipo katika Uislamu na vinafanya kazilakini msisitizo wa utekelezaji wa mambo yote upo katikauadilifu na taqwa kuliko katika kuogopa polisi namahakama.

Pili, uhuru wa watu binafsi kufanya wanalolitaka ndiosera inayofuatwa katika Uislamu. Yaani katika masualaya uchumi Uislamu umempa uhuru kila mtu afanye lileanaloliona linafaa. Na serikali ya Kiislamu haitaingiliauhuru wake huo isipokuwa tu pale ambapo hakihaitatendeka iwapo uhuru huo hautaingiliwa. Mtume(s.a.w) amelielezea kwa ufasaha sana suala hili palealipoyapigia mfano maisha ya watu katika jamii na wasafiriwaliomo chomboni baharini:

“Hebu tuchukue mfano wa meli inayosafiri baharini ikiwaimejaza abiria ambao wamekaa katika sehemu zote zachini na juu. Sasa iwapo abiria mmoja aliyekaa katikasakafu hiyo ataamua kujipatia maji kirahisi kwa kutoboapale alipoketi na iwapo abiria wengine watamzuiakufanya hivyo (na ni wajibu wa abiria wote walio juu nachini kumzuia) watamnusuru yeye na wao wenyewe na

Page 151: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

140

kufa maji. Iwapo watamwacha atoboe basi watazamawote waliochini na juu ya meli.” (Bukhari).

Mfano huu unatuonesha kuwa japo Uislamu unampakila mtu uhuru wa kufanya alitakalo lakini uhuru huouna mipaka. Iwapo mtu atafanya jambo lisilo la haki basiserikali ya Kiislamu lazima iingilie kati kwa maslahi yajamii nzima.

Tatu, wajibu mkubwa wa serikali ya Kiislamu nikusimamia haki na kuzuia dhulma katika maisha ya jamii.

Haki ya Serikali kuzuia DhulmaKwanza, serikali ya Kiislamu inao wajibu wa kuandaa

mazingira mazuri ya kihuduma na kimawasilianokuwawezesha raia kujiletea maendeleo na inao wajibuwa kuingilia kati ili kusimamia haki na kuzuia dhulma.Ni wakati gani kwa mfano ambapo serikali inawezakuingilia kati. Allah ndiye aliyeziumba rasilimali zilizopoduniani na hivyo ni wajibu wa binaadamu kuzitumiarasilimali hizo kwa manufaa ya watu na kwa ufanisi. Hivyoserikali yaweza kuingilia kati iwapo rasilimali hizozitatumiwa kuwadhulumu watu au hazitatumika kwaufanisi.

Pili, baadhi ya kazi ni haramu katika Uislamu kwasababu zimefungamana na mambo ya haramu, kama vilekamari, umalaya, uchawi, ulevi n.k. Ni wajibu wa serikalikuona kuwa mambo hayo hayapewi nafasi katika jamii.

Tatu, ni wajibu wa serikali pia kutoa fursa sawa kwawatu wote ya kuendeleza na kuvikuza vipaji vyao kwakuwapa fursa sawa za elimu na mafunzo. Ni wajibu waserikali kugharamia elimu kwa ajili ya manufaa ya watuwote. Elimu ni haki ya msingi kwa wanadamu wote.

Nne, ni wajibu pia wa serikali kuhakikisha kuwa hata

Page 152: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

141

katika zile kazi za halali kisheria zinafanywa kwa uadilifupasi na dhulma yoyote. Yaani Serikali ihakikishemathalani kuwa bidhaa zinazotolewa zimefikia ubora kwawanaoizalisha, kuona kuwa uadilifu wa kitaalamuunadumishwa, kuona kuwa Wafanyakazi wanalipwamishahara kwa haki.

Hata hivyo, Uislamu hauelemei upande mmoja tu wakumtetea mfanyakazi peke yake wala kumtetea mwajiripeke yake. Wafanyakazi pia wakileta madai yasiyo yahaki ni juu ya serikali kuingilia kati.

Tano, ni wajibu wa serikali pia kuzuia mamboyanayoweza kudhuru watu, kwa mfano kama mtu akijengakiwanda cha hatari katika makazi wanamoishi watu. Auhata mambo yanayoweza kuwatesa wanyama, kamakuwabebesha mizigo mizito sana hadi wanaanguka nakuvunjika miguu au kufa, au kuwafanyisha kazi kwamateso makubwa na kutowapa chakula cha kutosha. Halikadhalika serikali inaweza kwa mfano kuzuia magari aumeli iliyopakia abiria au mizigo kuliko uwezo wake.

Sita, katika suala la usambazaji wa bidhaa, serikaliinaweza kuingilia kati iwapo watu watahodhi vyakula nabidhaa nyingine muhimu kwa lengo la kupandisha bei.

Saba, ni wajibu wa serikali kujenga miundo mbinu (in-frastructures) na kuidhibiti, kwa mfano kujenga barabara,madaraja, reli, kusambaza maji ya bomba, kujengamitambo ya umeme, simu n.k.

Wakati wa Ukhalifa wake, Ali (r.a) alimwambia Nahri,ambaye alikuwa mkuu wa jimbo la Misri; “Usifanyeukusanyaji wa kodi ya ardhi kuwa ndiyo kazi yako kubwa;kazi yako kubwa ni kuindeleza ardhi hiyo.”

Page 153: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

142

Nafasi ya serikali katika ugawajiKatika suala la ugawaji, wajibu wa serikali ya Kiislamu

upo katika maeneo makuu yafuatayo:

(i) Kusimamia utoaji na ukusanyaji wa zaka.Serikali ndiyo yenye wajibu wa kuhakikisha kuwakila anayepaswa kutoa Zaka anatoa na serikaliinasimamia ukusanyaji wake.

(ii) Kutoza na kukusanya kodi iwapo zakahaikutosha.

(iii) Kutoza na kukusanya Jizya (aina ya kodi) kutokakwa wasiokuwa Waislamu (dhimmi) wanaoishikatika dola ya Kiislamu.

(iv) Serikali ya Kiislamu pia inao wajibu wakuchukua hatua za kupunguza tafauti kati yamaskini na matajiri, kwa kugawa Zakat nakutoa huduma muhimu bure kwa maskini.

5. Haki na Uhuru wa kuchuma katika UislamuKwa kuwa kuchuma kwa njia za halali ni wajibu kwa

kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, hapana budi kilamtu kupewa uhuru kamili wa kutumia juhudi yake navipawa vyake katika kuchuma kwa njia za halali. KatikaUislamu ni kosa kubwa kwa serikali au Dola kuwekavikwazo vya kuwazuia watu wasitumie vipaji vyao na uwezowao wote katika kuchuma kwa njia za halali. Kinyumechake, serikali au dola ya Kiislamu ina wajibu wa kuondoavikwazo vyote vinavyowazuia watu kutumia vipawa vyaovyote katika kuchuma na inawajibu pia wa kutoa motishana vishawishi vya kuwavutia watu binafsi au watuwaliojiunga katika vikundi wajiingize katika sekta mbalimbali za uchumi kwa juhudi kubwa na maarifa.

Page 154: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

143

Pamoja na uhuru kamili uliotolewa na Uislamu wakuchuma kwa njia za halali kwa kadri ya uwezo wa kilamtu, pia unampa kila mtu haki ya kumiliki kilaalichokichuma kwa njia za halali kama tunavyojifunzakatika aya ifuatayo:

“Wala msitamani vile ambavyo Mwenyezi Munguamewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine wanaumewanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma, nawanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vilewalivyovichuma. Na mwombeni Mwenyezi Mungufadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kilakitu. (4:32)

BiasharaBiashara imepewa hadhi ya juu katika Qur-an na

katika Hadith za Mtume (s.a.w) kwa sababu ya umuhimuwake katika kuwaunganisha wanaadamu na kuharakishamaendeleo yao.

Kihistoria, maendeleo ya ulimwengu yalianza palebiashara ilipopanuka na kuufanya utajiri wa ulimwenguufike katika kila kona ya dunia.

Tunafahamu kilimo na viwanda ni shughuli muhimu

Page 155: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

144

sana kwa maisha ya binaadamu, lakini mazao ya shambanina bidhaa za viwandani bila ya kusambazwa kwa watuwanaozihitaji, binaadamu bado watabakia katika hali duni.Inatokea hivyo kwa sababu binaadamu hakuumbwakujitegemea kwa kila kitu. Vipaji, bahati na fursahavikugawanywa sawa sawa kwa kila mtu au kwa kilanchi ya ulimwengu katika nyanja zote za maisha.

Kiungo kikubwa cha ushirikiano huu ni biashara katiya watu wa jamii moja au nchi moja na nyingine. Hivyobiashara ina umuhimu wake katika maisha ya binaadamuna maendeleo yake. Uhalali na msisitizo wa biashara ukobayana katika Qur-an:

“… Haya ni kwa sababu wanasema: “biashara ni kamaRiba” hali Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara nakuiharamisha riba…” (2:275)

Katika aya hii tunafahamishwa wazi kuwa Allahameihalalisha biashara na kuiharamisha riba. Hivyobiashara yoyote itakayoambatana na riba. Kuuza kwamkopo wa riba itakuwa ni biashara haramu. Katikakuonesha ubora wa biashara Mtume wa Allah amesema:

“Mfanya biashara mkweli na mwaminifu (mcha Mungu)atakuwa pamoja na Mitume, Masadiq na Mashahidi”.(Tirmidh, Ibn Majah)

Malipo haya kwa mfanyabiashara yatapatikana tu iwapoatakuwa mkweli na mwaminifu katika biashara yake.Akiwa kinyume cha hivyo atakuwa pamoja na maasi katika

Page 156: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

145

siku ya Kiyama kama tunavyofahamishwa katika Hadithnyingine inayosema:

“Ubaid bin Rafa’a kutoka kwa baba yake ameeleza kuwaMtume (s.a.w) amesema: “Wafanyabiasharawatakusanywa pamoja na wakosaji ila wenyekumuogopa Allah, wacha Mungu na wakweli.” (IbnMajah na Tirmidh).

Kwa hiyo ili biashara iweze kuleta mafanikio kwamfanyabiashara na kwa jamii kwa ujumla, hapana budikufuata miiko na taratibu zilizowekwa na Uislamu.

Kwanza, pasiwe na udanganyifu wowote katika uuzajina ununuzi. Kila mmoja kati ya muuzaji na mnunuzianatakiwa awe mkweli na mwaminifu kwa mwenzake.Hebu tuzingatie Hadith ifuatayo:

Jabir ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Allahamrehemu yule ambaye ana mahusiano mema wakatiakiuza, akinunua na wakati wa kutoa uamuzi.”(Bukhari).

Jambo muhimu la kuangalia, katika biashara niuaminifu katika upimaji kwa vipimo vya uzito, urefu, naujazo. Wafanyibiashara walio wengi huanguka kwenyemtihani huu wa vipimo na huishia katika laana ya Allah(s.w). Qur-an imesisitiza mno kuchunga haki katikavipimo:

“Na timizeni kipimo mpimapo, na pimeni kwa mizani zilizosawa. Hayo ni wema kwenu na bora mwishoni.” (17:35)

Page 157: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

146

“Kijazeni kipimo cha pishi sawa sawa wakati mnapopima;(msidhulumiane) wala msiwe miongoni mwawapunguzao. Na pimeni kwa mizani iliyo sawa (pia).Wala msiwapunguzie watu vitu vyao, wala msitembeekatika ardhi mkifisidi.” (26:181-183).

Pamoja na msisitizo huu Allah (s.w) anatufahamishakatika Qur-an kuwa aliiangamiza kaumu ya Nabii Shuayb(a.s) kwa sababu ya kukithiri kwao katika kuwapunja watukatika vipimo katika biashara. Maangamizi hayakuishiakwenye kaumu ya Shuayb (a.s) tu bali Allah (s.w) ameahidimaangamizi kwa kila mwenye kupunja katika vipimo kamainavyodhihirishwa katika aya zifuatazo:

“Maangamizi yatawathibitikia wapunjao wenziwao.Ambao wanapojipimia kwa watu hupokea (kipimo) kamili.Lakini wanapowapimia kwa kipimo cha vibaba au mizani(au vinginevyo), wao hupunguza. Je! Wao hawafikiri yakwamba watafufuliwa? (83:1-4)

Page 158: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

147

Waislamu hatuna budi kuwa macho sana katika vipimovya uzito, ujazo na urefu tunavyotumia katika biasharazetu. Kutokana na msisitizo uliopo katika Qur-an mtuhata ajiite Muislamu mwenye kusali swala zote, akatoazakat na sadaqa, akafunga, na akahiji, ataangamia nakuishia Jahannam iwapo katika biashara yake atakuwaanawapimia watu kwa ujanja ujanja.

Ugongaji wa vipimo vya ujazo na kuuza bei ya kipimokizima, utegesheaji wa mizani, ugongaji wa mizani iliishuke kabla ya kipimo kukamilika, uchanganyaji wabidhaa mbovu na nzuri na kuiuza kwa bei nzuri (n.k.) nimiongoni mwa udanganyifu katika biashara.Mfanyabiashara wa namna hii ndiye yule Mtume (s.a.w)aliyesema atafufuliwa pamoja na waovu watakaoingiamotoni. Pia tumefahamishwa katika Hadithi kuwa:

Wasikh bin Asqa’a ameeleza: Nimesikia Mtume wa Allahakisema: Anayeuza bidhaa mbovu bila kuonesha ubovuwake ataendelea kuwa katika laana ya Allah na malaikawataendelea kumlaani.” (Ibn Majah).

Pili, katika biashara pasiwe na viapo kwani hii nimiongoni mwa kuuza kwa ujanja-ujanja. Bidhaa iliyoapiwasana na mwenye kuuza, inaweza imhadae mnunuziaidhanie kuwa ni nzuri zaidi kuliko hali halisi. Mnunuziatakapogundua baadaye ataona kuwa amedanganywa kwaviapo. Hivyo viapo vingi kwenye biashara, kwa muuzaji aumnunuzi vimekatazwa kwa sababu vina hila ndani yake.Mtume (s.a.w) ameonya katika Hadith ifuatayo:

Abu Qatada ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema,“Kuwa muangalifu na viapo vingi katika uuzaji, kwasababu japo kuwa kunarahisisha uuzaji, kuna punguzabaraka. (Muslim).

Page 159: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

148

Kuapa sana katika biashara kuna hadaa, kwa sababuwanunuzi wanapogundua kuwa wamedanganywa kwaviapo, na kumbe bidhaa hiyo haikuwa nzuri kiasiwalichotarajia, hawatapendelea tena kununua kwa mfanyabiashara huyo.

Tatu, katika biashara pawe na uhuru kamili kwamnunuzi wa kuikataa au kuikubali bidhaa baada yakuiangalia. Uhuru wa kuikataa bidhaa unaendelea kwamnunuzi hata baada ya kununua, iwapo atagundua dosariyoyote katika bidhaa hiyo kabla ya kuanza kuitumia bidhaahiyo. Vile vile muuzaji anayohaki ya kukataa au kukubalikuuza bidhaa yake kwa bei anayoridhika nayo kabla yamkataba wa kununua hauja kamilika. Muuzaji hana uhuruwa kuitaka bidhaa irudishwe baada ya mkataba wa kuuzana kununua kukamilika labda kwa mapatano yaliyofanywakatika mkataba wa kuuziana. Kuhusu jambo hili la uhuruwa uamuzi wa muuzaji na mnunuzi katika kuuza nakununua bidhaa, tunafahamishwa katika Hadith ifuatayokuwa:

Ibn Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:“Mnunuzi na muuzaji kila mmoja katika wao ana uhuruwa mapatano na mwenzake ili mradi tu hawajaachanaila kwa uhuru wa uamuzi wa ununuzi (anaweza akakataabidhaa hata baada ya kuelewana).” (Bukhari na Mus-lim).

Katika maelezo ya Muslim – wakati mnunuzi namuuzaji wanauziana kila mmoja katika wao ana uhuruwa uamuzi kutokana na mauzo au manunuzi yake, ilimradi tu wawe hawajaachana au wameuziana kwamapatano. Kama kuuziana kwao ni kwa mapatano basikila mmoja atafungika (kulingana na mapatano hayo).

Biashara yoyote itakayoendeshwa kwa kumnyimauhuru muuzaji au mnunuzi ni biashara haramu ambayo

Page 160: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

149

haimnufaishi mnunuzi wala muuzaji. Kutokana na uzoefuwetu tunayaona haya katika mazingira yetu. Ni marangapi tumeona watu wakilazimishwa kununua bidhaawasizozipenda wala kuzihitaji? Kwa mfano utaona mtuakilazimishwa kununua kilo ya unga wa muhogo usiofaakula kabisa, ili apatiwe kilo ya sukari anayohitajia. Huuni uuzaji wa hila na ni uuzaji wa haramu. Kuna mifanomingi kama hii, Uislamu umetoa uhuru kwa muuzaji namnunuzi.

Kwa ujumla utaona biashara itakayoendeshwa kwamisingi ya Kiislamu iliyoelezwa hapa kwa ufupi, ndio pekeebiashara halali na ndio pekee yenye kutumainiwa kuletaushirikiano, umoja, ustawi na amani ya kweliulimwenguni. Kisiasa na kiuchumi inafahamika wazikuwa matatizo mengi yanayoukabili ulimwengu katikanyakati zote za historia yanasababishwa na kukiukamisingi ya haki ya biashara na ya uchumi, kwa ujumlaaliyoiweka Allah (s.w).

Kwa hiyo Waislamu hatuna budi kujua kuwa utatuziwa matatizo yanayoukabili ulimwengu ni kusimamishamisingi ya Uislamu katika nyanja zote za maisha, hasakatika nyanja za uongozi na uchumi ambazo ndizo roho yajamii.

Biashara haramuBiashara inaweza kuwa haramu kwa namna mbili:

kwanza kwa kutofuata misingi ya halali iliyowekwa naAllah (s.w). Pili, kuna biashara ambayo moja kwa mojaimeharamishwa hata kama misingi ya halali itafuatwa.Kwa maana nyingine kuna biashara ambazozimeharamishwa katika nafsi yake yenyewe. Katikakipengele hiki tutaorodhesha biashara ambazozimeharamishwa moja kwa moja katika nafsi yake naHadithi mbali mbali za Mtume (s.a.w).

Page 161: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

150

(i) MuzabanahNi kunufaika kibiashara kutokana na matatizo ya watu

wengine. Ni haramu kufaidi shida ya mwengine katikabiashara. Uislamu unataka mwenye shida asaidiwe nawala asikandamizwe kutokana na shida yake. Biasharaya Muzabanah imeharamishwa kwa muuzaji na mnunuzi.Uislamu unasisitiza kuwa kinachouzwa nakinachobadilishwa nacho ni lazima kifahamike kwamnunuzi na muuzaji.

(ii) Mu’awamahHuu ni uuzaji wa matunda, nafaka, na mazao mengine

ya shambani kabla ya kukomaa kiasi cha kufaa kuliwa;na ni haramu kama inavyosisitizwa katika Hadithizifuatazo:

Abdullah bin Umar ameeleza kuwa Mtume (s.a.w)ameharamisha kuuza matunda shambani mpaka yaive.Ameharamisha kwa muuzaji na mnunuzi(wamekubaliana Bukhari na Muslim). Na katika maelezoya Muslim: (Mtume) aliharamisha kuuza tende mpakaziive na nafaka mpaka ziwe nyeupe na zisiwe zenyekudhuriwa tena na madhara mbali mbali.

Jabir ameeleza kuwa Mtume wa Allah ameharamishakuuza (kwa matunda yangali mtini) kwa kipindi chamiaka, na ameamrisha kungojea kwanza yawe tayari(kiasi cha kutoweza kudhuriwa na chochote). (Muslim).

(iii) Hablul-HabalahKuuza kilichotumboni kabla hakijazaliwa. Kwa mfano

kuuza mimba ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, ngamia, n.k niharamu. Tunafahamishwa katika Hadithi ifuatayo:

Ibn Umar ameeleza kuwa Mtume Mtukufu ameharamishamauzo ya Habalul-Habalah; na ni uuzaji waliokuwawakiufanya watu majahili. Mtu alikuwa akinunua ngamia

Page 162: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

151

mpaka ngamia jike lishike mimba na mpaka hicho nachokatika tumbo la uzazi kiwe na mimba. (Bukhari na Mus-lim).

Jambo linalosisitizwa katika Hadithi hii ni kwambaimeharamishwa kuuza mimba kwani ni jambo ambalohalina uhakika kabisa. Ajuaye na mwenye uhakika wakuzaliwa au kutozaliwa kilichomo tumboni ni Allah (s.w)peke yake. Kwa hiyo uuzaji wa mimba ni uuzaji wa pata-potea (uuzaji hewa).

(iv) Uuzaji wa bidhaa kabla hazijamfikia mnunuzi niharam,

Ununuzi au uuzaji hauhusiki mpaka mnunuziashuhudie bidhaa anazouziwa. Hivyo ndivyotunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:

Ibn Abbas ameeleza: “Katika mauzo aliyoyaharamishaMtume (s.a.w) ni mauzo ya chakula mpaka yawemikononi mwa mnunuzi…” (Bukhari na Muslim).

Msisitizo wa Hadithi hii ni kwamba mtu asiuze kituambacho hajakishuhudia machoni mwake au machonimwa mwakilishi wake.

(v) Uuzaji wa bidhaa njiani kabla ya wauzaji kufikishabidhaa sokoni.

Wakati mwingine wafanya biashara hufanya ujanja kwakuteka nyara bidhaa njiani kabla hazijaingia sokoni ilikuwaghilibu na kuwapumbaza wauzaji ambao hawajajuabei halisi ya bidhaa ile sokoni.

Ununuzi wa namna hii ni ulanguzi na umeharamishwakatika Uislamu kama inavyosisitizwa katika Hadithizifuatazo:

Page 163: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

152

Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allahamesema: “Usimfuate mfanya biashara wa nafakamkakutana naye njiani kabla (ya kuingia sokoni). Naendapo atanunua kutoka kwake-atakapoingia sokoni nakujua hali halisi ya soko ana haki ya kukataa mauzianoya awali. (Muslim, Bukhari).

Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:“Usikutane (usiteke nyara) bidhaa njiani mpakazitakapofikishwa sokoni.” (Bukhari na Muslim)

Kununua bidhaa iliyonunuliwa na mwingine kwa kulipabei kubwa zaidi au kwa sababu nyinginezo ni haramu kamainavyobainishwa katika Hadithi zifuatazo:

Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:“Hapana mapatano ya atakayenunua kitu yatayofanyikabaada ya mwenzake kununua na hapanaatakayemchumbia ambaye ameshachumbiwa namwenzake (ndugu yake) mpaka apate ruhusa kutokakwake (huyo) aliyeanza na kupatana bei au aliyeanzakuchumbia.” (Muslim).

Kinachosisitizwa katika Hadithi hii ni kwamba,Muislamu haruhusiwi kununua bidhaa iliyonunuliwa namwingine. Mara nyingine kwa sababu ya husuda au urohomatajiri huweza kuwashawishi watu wenye uroho kamawao wakaamua kuvunja mkataba wa mauzo uliofanyikahapo awali ili apate bei kubwa kwa huyu mteja aliyejitokezabaada ya mauzo kwa yule mteja wa kwanza.

(vi) Kuuza maji au majani ambayo mtuhakuyagharamikia chochote imekatazwa katikaHadithi zifuatazo:

Jabir amesimulia kuwa Mtume wa Allah amekataza(ameharamisha) kuuza maji ya asili. (Muslim).

Page 164: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

153

Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:Majani ya asili hayatauzwa ili kununua malisho yaliyomo.(Bukhari na Muslim).

Hadithi hizi zinatufundisha kuwa mali asili kama maji,majani, miti ya porini (n.k.) ni haki ya kila mwanaadamukwa hiyo hapana mwenye haki ya kuzuia mali ya asili nakuifanya yake na kuwauzia watu wengie. Bali kama maliasili imeshughulikiwa ndio ifae kutumika, itajuzu mwenyekuishughulikia awe na haki ya kudai arudishiwe gharamaalizozitoa katika shughuli hiyo. Kama gharama za bomba,na mashine ya kusukumia maji na kadhalika.

Lakini kuyauza maji ya chemchem ya asili au mto niharamu.

(vii) Uuzaji wa samaki aliyeko majini, uuzaji wa ndegeanayeruka angani (ambaye hafugwi), uuzaji wamaziwa ambayo hayajakamuliwa na uuzaji wamanyoya ya mnyama yangali mwilini mwake niuuzaji haramu. Ni wazi kuwa mauzo yote hayayameharamishwa kwa sababu bidhaa hizo hazinauhakika wa kuzipata. Ili pawe na haki kati yamuuzaji na mnunuzi bidhaa hizo hazina budikupatikana kwanza mkononi ndio ziuzwe.

(viii) Uuzaji wa damu na uuzaji wa uhuru wa mtu(utumwa) uuzaji wa nywele na maziwa yabinaadamu ni biashara haramu. Vitu vyote hivi sihaki ya mwanaadamu na havipatikani kutokanana jasho lake. Hivyo hana haki ya kuviuza na walahana hata uwezo wa kukadiria thamani yake halisi.Kama hatuwezi kukadiria thamani ya mvuto mmojawa hewa au thamani ya tone moja la maji, tunawezakukadiria thamani ya damu, achilia mbali thamaniya maisha yetu?

Page 165: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

154

(ix) Mauzo ya mbwa, nguruwe, pombe, damu na mzogani biashara haramu. Pia ni haramu kuuza pichana sanamu kama tunavyofahamishwa katikaHadithi zifuatazo:

Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allahameharamisha kipato kilichotokana na kuuza damu,mbwa, na kipato cha Malaya. Na amelaani mwenyekupokea na mwenye kutoa riba, na mwenye kuchoramwili kwa chale na mwenye kuchorwa mwili kwa chalena mchoraji wa picha (za wanyama) na watu. (Bukhari).

Jabir ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allah akisemakatika mwaka wa ushindi (wa kuiteka Makka) wakatialipokuwa Makka.Hakika Allah na Mtume wakewameharamisha mauzo ya pombe; mizoga, nguruwe namasanamu. (Bukhari na Muslim).

(x) Ulanguzi (Kuhodhi bidhaa)Hili ni neno pana linalotumiwa kwa maana mbali mbali;

lakini katika kipengele hiki tutalitumia neno hilikuwakilisha kitendo cha kuteka nyara bidhaa muhimusokoni kwa kuinunua kwa wingi labda kwa bei ya juu kidogokwa madhumuni ya kuilundika (kuihodhi) na kuifanya iweadimu ili hapo baadaye itakapokosekana sokoni iuzwe kwabei ya juu sana na kutoa faida kubwa sana.

Biashara ya namna hii ni biashara haram kamatunavyofahamishwa katika Hadithi kadhaa zifuatazo:

Umar amesimulia kutoka kwa Mtume wa Allah aliyesema:“Mwenye kuleta nafaka (mjini) anazidishiwa rizki namkusanyaji na mfichaji wa bidhaa hizo amelaaniwa.”(Ibn Majah, Dirimi).

Page 166: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

155

Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema:“Anayelundika na kuzuia bidhaa za chakula kwa siku 4kwa nia ya kupata bei kubwa zaidi, anajitenga na Allahna Allah anajitenga naye.” (Razin).

Hadithi zote hizi zimedhihirisha ubaya wa kuzuiabidhaa, hasa bidhaa muhimu kama vile chakula, nakuzifanya ziwe adimu ili kuuza kwa bei kubwa itakayotoafaida kubwa sana. Biashara ya namna hii ni biaharaharamu na laana ya Allah iko juu ya walanguzi hawa:

Mu’az amesimulia: Nimemsikia Mtume wa Allah akisema:“Mbaya ni yule anayelundika bidhaa na kuifanya iweadimu. Kama Allah akifanya bidhaa kuwa rahisi, yeyeanachukia na kama Allah akifanya kuwa ghali,anafurahi. (Razin, Baihaqi).

Hadithi hii inatueleza sura hasa ya mlanguzi. Amamtu kuweka bidhaa alizozilima na alizotengenezamwenyewe au kuuza bidhaa alizozinunua kutoka masafaya mbali si haramu. Lililoharamishwa ni kule kununuabidhaa katika soko la kawaida na kuzificha ili baadayeaziuze kwa bei kubwa baada ya bidhaa hiyo kuwa adimukatika soko.

Pamoja na Uislamu kulaani ulanguzi, hauruhusukumkangandamiza mfanyabiashara kwa kumuwekea beiya bidhaa yake. Bei inatakiwa ijiweke yenyewe kulinganana hali halisi ya soko. Bidhaa zikiwa nyingi bei itakuwachini na bidhaa zikiwa chache itakuwa juu. Tunajifunzakutokana na Hadithi ifuatayo:

Anas amesimulia kuwa wakati mmoja katika wakati waMtume wa Allah bei ya vitu ilikuwa ghali. WakamuombaMtume: Ewe Mtume wa Allah panga bei kwa nafuu yetu.Mtume wa Allah akajibu: Hakika Allah ndiye anayemiliki

Page 167: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

156

bidhaa, anapunguza, anatoa kwa wingi, anatoa rizki, naananipendelea sana nikutane na Bwana wangu katikahali ambayo hapana yeyote kati yenu atakayenifanyaniwe na dhima juu ya damu (iliyomwagika kwa sababuyangu) au mali (aliyopunjwa kwa sababu yangu)!(Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).

Uislamu kama usivyoruhusu kukandamizwa nakudhulumiwa mnunuzi ndivyo hivyo hivyo usivyoruhusukukandamizwa kwa mchuuzi au muuzaji. Mtume (s.a.w)akiwa kiongozi mkuu wa serikali ya Kiislamu, hakuthubutukutumia madaraka hayo kuingilia haki za wafanyabiasharawalizopewa na Allah (s.w). Jibu lake kwa namna nyinginelilikuwa “anayepanga bei ni Allah (s.w).

Kutokana na Hadithi hii hapana yeyote aliyojitokezamwenye haki ya kukaa chini na kumpangiamfanyabiashara bei iliyo kinyume na ile iliyojitokezayenyewe sokoni. Kinachotakiwa kifanywe na nguvu za dolani kutokomeza njama zote za ulanguzi na vikwazo vyotevya uchumi. Kisha kuwaacha huru wafanyabiashara wauzebidhaa zao kwa bei halisi inayokubaliwa katika soko huru.

(xi) Kupunguza kipimo cha ujazo au kilo kwa kuharibumizani au kugonga vipimo vya ujazo ni haramu.Allah (sw) anasema :

Maangamizo yatawathubutikia wapunjao (wenzao).Ambao wanapojipimia kwa watu hupokea (kipimo) kamili,lakini wanapowapimia kwa (kipimo cha) vibaba au mizani(au vinginevyo), wao hupunguza. (83:1-3)

Page 168: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

157

Na timizeni kipimo mpimapo; na pimeni kwa mizani zilizosawa. Hayo ni wema kwenu na bora mwishoni (kwake).(17:35).

(xii) Kuficha ila (dosari) ya bidhaa inayouzwa niharamu. Katika Hadithi iliyosimuliwa naBukhari, Baihaq na Al-Hakim, Mtume (s.a.w)amesema: Muuzaji na mnunuzi kila mmojalazima atimize makubaliano. Na muuzaji akitoahabari zote juu ya bidhaa anayoiuza pamoja namfano, kama unauza maharage makavumwambie mnunuzi mathalan, uzuri wamaharage haya ni kuwa hayajatoboka lakiniyana ila moja ya kuchelewa sana kuiva. Mwachemnunuzi apime hiari ya kununua au kuwacha.

Kutokana na maelezo yote haya; juu ya vipengele mbalimbali vilivyo haramishwa katika biashara, tunaona kuwabiashara japo ni kazi halali yenye hadhi kubwa mbele yaAllah, haitamnufaisha mwanaadamu iwapo mipaka ya Al-lah (s.w) haitachungwa wakati wa kufanya shughuli hiyo.

Haki ya kumiliki maliKumiliki mali ni suala la kimaumbile na

limeshikamana na silka ya kujihami (selfpresevation).Katika historia ya binaadamu suala lakumiliki mali limekuwa likiandamana na itikadi au falsafainayotawala mahali.

Page 169: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

158

Kwa mfano katika baadhi ya jamii za kitwaghutiumilikaji wa mali uko chini ya familia au huwa chini ya“watu wote” (mali ya umma) au huwa chini ya mtu auwatu binafsi. Katika Uislamu kila kitu kipo chini ya milikiya Mwenyezi Mungu:

“Sema Ee Mola uliyemiliki Ufalme wote! Humpa ufalmeumtakaye na humuondolea ufalme umtakaye nahumtukuza umtakaye na humdhalilisha umtakaye, kheriimo mikononi mwako. Bila shaka wewe ni MwenyeUwezo juu ya kila kitu”. (3:26).

Hivyo ni dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mmilikajiwa hakika wa vitu vyote. Binaadamu anamiliki mali kwadhamana tu siyo kwa hakika na kwa sababu hiyo ataulizwajinsi alivyotumia. Katika Qur-an Allah (s.w) ameruhusuwatu binafsi au kwa vikundi kumiliki mali pale aliposema:

“Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajiliya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbeleyangu) na uwaombee dua. Hakika kuwaombea kwakokutawapa utulivu (watengenekewe); na Mwenyezi Mungundiye asikiaye na ajuaye.” (9:103)

Page 170: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

159

Hivyo Uislamu unakubali na kuheshimu haki ya mtuau watu binafsi kumiliki mali.

Mipaka ya Umilikaji mali(i) Mali hiyo iwe imechumwa kwa njia ya halali.

Uislamu unaitambua haki ya kumiliki mali nahaki ya kuilinda mali hiyo, lakini mali yenyeweiwe ya halali.

(ii) Mtu anaweza kuiuza au kuitumia mali yakeapendavyo maadamu ana akili timamu. Iwapohana akili timamu, itabidi apatikane mdhaminiwa kuingalia mali hiyo kwa niaba na manufaayake na manufaa ya jamii.

(iii) Maadamu mtu anayo mali basi anao pia wajibuwa kutekeleza majukumu yanayohusiana namali aliyo nayo.

(iv) Uislamu unakataza ubakhili na israfu(ubadhirifu) katika matumizi. Mwenyezi Munguanasema:

Wala usifanye mkono wako (kama) uliofungwa shingonimwako, wala usikunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenyekulaumiwa na kufilisika. (17:29).

Enyi wanaadamu! Chukueni mapambo yenu wakati wakila sala; na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri). Lakinimsipite kiasi tu. Hakika Yeye hawapendi wapitao kiasi.(7:31).

Page 171: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

160

Ubadhilifu ni kufanya mojawapo ya mambo matatuKwanza, kununua kitu usichokihitaji. Au kununua

kitu unachokihitaji lakini kwa kiasi kingi kulikounavyoweza kutumia. Kwa mfano kutengeneza chapatitano ilihali uwezo wako ni wa kula chapati mbili tu, halafuzile tatu ukazitupa jalalani. Pili ni ubadhilifu kununuakitu chochote kile cha haramu, hata ikiwa kwa thamanindogo namna gani. Kwa mfano hata kama masandukulaki moja ya bia yanauzwa kwa shilingi hamsini ukiitoashilingi hamsini hiyo kununua pombe hiyo unaandikiwamadhambi ya ubadhilifu. Tatu kutoa sadaka kwa ajili yakujionesha kwa watu, badala ya kuandikiwa thawabuunaandikiwa madhambi ya israfu.

(v) Uislamu unakataza rasilimali zilizo katika jamiikuachwa bila kutumiwa Mtume (s.a.w) amesemamtu akiendeleza ardhi ana haki ya kuimiliki.Lakini akiiwacha kwa miaka mitatu bila kuitumiamtu mwingine ana haki ya kuiendeleza nakuimiliki.

6. Mgawanyo wa mali katika UislamuUislamu unasisitiza kuwa zaidi ya kuchuma, kumiliki

na kusambaza mali, mgawanyo pia uwe wa haki katikajamii ili kujenga udugu, amani na utulivu wa kweli. Nakatika kuhakikisha hilo mfumo wa uchumi wa Kiislamu(Iqtisad) unatumia njia zifuatazo:

1. Zakat(i) Kilugha, neno zakat lina maana mbili: (a) Utakaso

na (b) Ustawi. Hivyo zaka ni Ibada inayochangiasana katika kuleta uadilifu na ustawi wa jamiikiuchumi na hata kisiasa.

(ii) Zakat katika Uislamu ni taasisi maalumu naimesisitizwa katika Qur-an. Aya zipatazo 80zimeitaja Zakat pamoja na Swala Zakat ina upeompana sana na ina husisha vipengele vingi kamavile:

Page 172: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

161

(a) Kijamii – Zakat ni kama bima ya jamiiinayowahakikishia wakazi hifadhi ya kiuchumiendapo watapata matatizo kama ya umaskini aumaafa. Zaka pia huondosha chuki na migogoroya kitabaka na kujenga hisia za kuwa wamoja.

(b) Kisaikilojia, Zakat inawalea watu katika moyowa kuhurumiana na kusaidiana. Inawapawanyonge na masikini moyo wa kujiamini nakujiona sawa na wengine.

(c) Kiuchumi – Zakat ni njia mojawapo yakupambana na tatizo la umaskini. Tatizo hililinazikabili nchi zote na Uislamu unalenga katikakuondoa umaskini pasi na jitihada za watubinafsi. Uislamu haupiganii usawa bandia nakuwa kipato cha kila mtu kiwe sawa na mwinginewala Uislamu hauinyamazii hali ya wenginewatumie na kusaza wakati wengine wanaendeleakutaabika kwa kushindwa kujipatia mahitajimuhimu. Tofauti za kimapato, vipaji na uwezozitakuwepo katika jamii, lakini pengo la tofautihiyo lisiwe kubwa sana.

(d) Kwa maumbile yake, Zakat huwahimiza watukuweka vitega uchumi na kuzalisha mali nakupiga vita tabia ya kuhodhi mali. Hii ni kwasababu Zakat hutozwa kwa kipato kilichokaamwaka mzima bila kutumika.Kila mtu hanabudikupata mahitaji ya msingi.

2. SadakatHisia za kuhurumiana na moyo wa kusaidiana kama

ndugu zinazomsukuma mtu kutoa Zakat kwa kutarajikupata radhi za Allah ndizo hizo hizo zinazomsukuma mtukutoa sadaka. Hivyo tofauti kati ya Zakat na sadaka haipo

Page 173: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

162

katika lengo la kutoa bali katika wajibu wa kutoa. Zakatni wajibu kutoa na sadaka ni amali iliyokokotezwa sanajapo haikuwekewa kiwango na muda wa kutoa. Hutolewakulingana na haja. Misingi ya kutoa sadaka ni ile ile yakuhurumiana na kusaidiana kama Allah alivyoagiza katikaQur’an:

Na saidianeni katika wema na ucha-Mungu, walamsisaidiane katika dhambi na uadui” (5:2).

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia yaMwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje mojailiyotoa mashuke saba; ikawa katika kila shuke panapunje mia., Na Mwenyezi Mungu humzidishiaamtakaye, na Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaamkubwa na Mwenye kujua.” (2:261).

Aidha, Mtume (s.a.w.) amesisitiza katika Hadithi nyingisana umuhimu wa kutoa sadaka. Katika Hadithiiliyosimuliwa na Bukhari, Muslim, Ahmad na At-Tirmidh,Mtume (s.a.w.) amesema mtu asiyewahurumia watuhatahurumiwa na Allah. Na katika Hadithi iliyosimuliwana Attabarani na Baihaqi, Mtume (s.a.w.) amesema: Naapa

Page 174: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

163

kwa Allah si muumini yule anayelala akiwa kashiba nailhali jirani yake kalala na njaa.

Na katika Hadithi iliyosimuliwa na Al-Hakim, Mtume(s.a.w.) amesema ikiwa wakazi wa eneo fulani (kama vilemtaa) wakiamka asubuhi na ilhali mmoja wao ana njaabasi Allah hujitenga nao.

Matukio maalum ya kutolewa kwa sadakaBaada ya kumaliza mfungo wa Ramadhani kutoa

Zakatul Fitr ni lazima. Zakatul Fitr kiwango chake ni kilo2½ za chakula kilichozoeleka katika mji huo kama vilemchele au ngano.

Na mtu hutoa kiasi hicho kwa ajili yake mwenyewe nahutoa tena kiasi hicho hicho kwa kila mtu anayemtegemeakatika familia yake. Hivyo atamtoleo pia mkewe, na wanawewote na wazazi wake iwapo anakaa nao na hawana uwezo.

Tukio la pili ni siku ya kuvuna mazao shambani,Mwenyezi Mungu ameagiza siku hiyo mtu atoe baadhi yamazao yake na awape maskini, jamaa na majirani zakealiposema katika Qur’an:

Page 175: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

164

Naye (Allah) ndiye aliyeumba miti inayoegemezwa (katikachanja) katika kuota kwake na isiyoegemezwa na(akaumba) mitende na mimea ya matunda mbali mbali,na (akaumba) mizaituni na mikomamanga inayofananana isiyofanana. Kuleni matunda yake inapotoa matunda;na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake (kwa kuwapamaskini na jamaa na majirani na wengineo) Wala msitumiekwa fujo, hakika Yeye (Allah hawapendi watumiao kwafujo.” (6:141).

Tukio la tatu ni wakati wa ndoa, Kuoana ni jambolililohimizwa sana katika Uislamu. Hivyo Uislamuunasisitiza kuwa watu wasaidiane sana katika jambo hili.Wanazuoni wengi wanasema kuwa iwapo mtu anao uwezowa kuoa lakini hapa mwanzo anakabiliwa na matatizo yakifedha Hazina ya serikali ya Kiislamu (Baitul Maal) itumikekumsaidia. Wakati wa Ukhalifa wa Umar vijana kama haowalikuwa wakisaidiwa. Katika kuonesha ubora wa ndoaAllah amesema:

Na waozeni wajane miongoni mwenu (waungwana) nawalio wema katika watumwa wenu (wanaume) nawajakazi wenu, kama watakuwa mafakiri Allahatawatajirisha katika fadhila zake; na Allah ni Mwenyewasaa” (24:32).

Tukio la nne ni iwapo mtu atapata wageni. Uislamuunamtaka mtu awakirimu wageni wake. Katika Hadithi

Page 176: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

165

iliyosimuliwa na Bukhari na Muslim, Mtume (s.a.w.)amesema: Yule anayemwamini Allah na siku ya mwishoawe mkarimu kwa wageni wake. Kwa mchana mmoja nausiku afanye takrima maalum. Kwa siku tatu zinazofuataafanye takrima ya kawaida na zaidi ya hapo ni sadaka yahiari.

Tukio la tano ni wakati wa kugawa urithi, iwapowatakuwepo watu mafakiri wakati huo wa kugawa basiwapewe chochote, kwani Allah anasema:

“Na wakati wa kugawanya wakihudhuria jamaa namayatima na maskini, wapeni kitu katika hayo (maliya urithi) na waambieni kauli njema.” (4:8).

Tukio la sita ni agizo la Allah la kusaidiana kwa halimbali mbali hasa majirani.

Tukio la saba ni wakati wa uzazi. Kama ambavyoUislamu unahimiza ndoa ndivyo pia unavyothamini maleziya watoto. Kihistoria Uislamu ndio ulioanzisha utaratibuwa kutoa malipo fulani maalum kwa familia zenye watotowachanga.

Hivi leo ziko baadhi ya serikali duniani ambazo hutoamsaada wa pesa kwa familia zenye watoto wachanga. HukoCanada kwa mfano upo utaratibu wa kutoa msaada wapesa kwa kila mtoto aliyezaliwa na kama watoto wakifikiaumri wa miaka 18 na bado wanasoma kiwango cha pesawanachopewa huongezwa.

Page 177: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

166

Utaratibu huu ulianza katika karne ya 7 wakati waukhalifa wa Umar. Umar alianzisha mfumo wa kutoadirham 100 kwa kila mtoto aliyezaliwa na kiwango hichokiliongezwa kadiri mtoto alivyokua. Hivyo mfumo wa kutoaruzuku kwa familia ni moja ya sadaqa zitolewazo katikamfumo wa uchumi wa Kiislamu.

Sadaka wakati wa dharuraKatika Hadithi iliyosimuliwa na Bukhari na Muslim,

Mtume (s.a.w.) aliwasifu sana Al-Afariyyin (watu wa ukoowa Abu Musa). Akasema watu hao walipokuwa vitani ausafarini na chakula kikapungua basi walikikusanya pamojachakula chote kilichosalia na kukigawa tena sawa sawamiongoni mwao.

Au nchi ikiingia njaa - ilitokea njaa kubwa kwa mfanowakati wa Ukhalifa wa Umar. Alichokifanya ni kutoataarifa kwa viongozi wa majimbo mbalimbali na kuwatakawalete chakula cha ziada. Na kilipokuja alikigawa bila yakujali cheo, madaraka au ukoo wa mtu bali kwa kujalimahitaji tu. Kwa bahati njema njaa hiyo ilikwishamapema. Lakini miongoni mwa maneno aliyoyasema Umarni kuwa lau njaa hiyo isingekwisha mapema, basiangewakusanya watu wote wenye njaa na angewagawakwa familia zenye chakula. Akasema hii ni kwa sababuwatu hawatakufa wakila chakula hata kama hawatashiba.

3. Kodi (Jizya)Ni njia nyingine itumiwayo na Uislamu katika

kuigawanya mali katika jamii. Tafauti na Zakat na Sadaqaambazo hupasa kutolewa na Waislamu, Jizya hutolewana wasiokuwa Waislamu (Dhimmi), wanaoishi chini yadola ya Kiislamu, kwa ajili ya kupata hifadhi na hudumambalimbali.

Page 178: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

167

4. MikopoMikopo kama njia mojawapo ya kugawa mali kwa watu

wote, Uislamu unaruhusu watu kukopeshana. Mtuanaweza kumkopesha mwingine fedha ama kwa kutumia(matumizi ya kawaida katika maisha) au kwa kumsaidiamtaji kufanya biashara.

Njia za uchumi zilizoharamishwaVipengele vya biashara haramu vilivyoorodheshwa

nyuma ni miongoni mwa hizo. Njia nyingine za uchumizilizoharamishwa ni hizi zifuatazo:

(i) WiziWizi wa aina yoyote ni kitendo cha dhulma ni haramu

katika Uislamu.

(ii) UleviUlevi wa aina yoyote kwa kiwango chochote ni

haramu. Uharamu wa ulevi hauishii kwa mnywaji tu;bali pia ni haramu kushiriki katika hatua yoyote ile yautengenezaji, uuzaji na uandazi.

Anas ameeleza kuwa Mtume (s.a.w.) amewalaani(watu) kumi kuhusiana na pombe-yule anayeikamua,yule aliyehusishwa katika kuikamua, yuleanayeinywa, yule anayeibeba, yule anayepelekewa,yule anayeiandaa, yule anayeiuza, yule anayepangabei yake, yule anayeinunua na yule anayemnunulia.(Tirmidh, Ibn Majah).

Kutokana na Hadithi hii, inatuwia wazi kuwa ainayoyote ile ya utengenezaji, uuzaji na unywajiimeharamishwa. Pato lolote mtu atakalolipata kama malipoya kushiriki katika hatua yoyote ya matayarisho na unywajiwa ulevi, litakuwa ni pato la haramu. Hebu tuangalie halihalisi. Je, hatuwaoni Waislamu wakishiriki kwa ukamilifu

Page 179: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

168

katika viwanda vya pombe kama mameneja, makarani,wakemia, madereva, n.k.? Je, hawa wataridhikakuendelea kujiita Waislamu na ili hali kila saa wakokatika laana ya Allah na Mtume wake na ibada zao zotehazikubaliwi maadam miili yao imerutubishwa na kipatocha haramu; kivazi chao ni haramu na kila walicho nachokatika mazingira yao kimepatikana kwa pato la haramu?

(iii) KamariKamari imeharamishwa pamoja na pombe kama ilivyo

katika aya ya (5:90) na (2:219). Pia Hadithi ifuatayoinatubainishia kuharamishwa kwa kamari:

Abdullah bin Amr ameeleza kuwa Mtume wa Allahameharamisha ulevi, michezo ya bahati nasibu,kamari ya karata, na gobairah (aina ya pombe) naanasema: “Kila ulevi ni haram”. (Abu Daud).

Hadithi hii inatubainishia kuwa aina zote za kamari-gudugudu, pata-potea, karata, bahati nasibu, nakadhalika,ni haramu na kwa hiyo pato lolote litakalo tokana nakamari ni pato haramu.

Ni muhimu kufahamu kuwa uharamu wa kamarihauishii kwa watu wawili au kikundi cha watu wachachebali hata kama kamari hiyo itachezwa kitaifa, itabakiakuwa haramu tu.

Kwa hiyo bahati nasibu ya taifa, Bima ya Kimataifa,na michezo yote ya kamari iliyotolewa kibali na taifa, yoteni haramu mbele ya Allah na yeyote atakayeshiriki kwanamna yoyote katika michezo hiyo ya kamari atakuwaameshiriki katika haramu na kipato chochoteatakachokipata kutokana na ushiriki wake huo kitakuwani kipato cha haramu. Katika aya tulizozirejea hapo juu(5:90 -91) kamari imeharamishwa kwa sababu kuu tatu:

Page 180: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

169

Kwanza, ni uchafu, kamari imeitwa “rijsi”. Kamariimeitwa uchafu kwa sababu pesa anazozipata mtu kwakamari ni za dhulma na haramu. Kufumba na kufumbuamtu amepata maelfu ya pesa bila jasho lolote. Hivyo nidhulma na ni haramu.

Pili, kamari inajenga chuki na uadui. Hii ni kwasababu yule aliyeliwa pesa zake kwa maelfu kwa njia hiiya dhulma huwa ana mfundo mkubwa moyoni naanamchukia sana yule aliyechukua pesa zake hata kamaajidai kuwa hajali, ukweli ni kuwa pesa zake zitamuumasana. Na mara kadhaa wacheza kamari wameishiakupigana na hata kuuana.

(iv) Kipato chochote kinachotokana na utengenezajiwa sanamu na picha za watu na wanyama ni kipatoharamu.Rejea katika Hadithi zilizotolewa chini ya“Biashara haramu”.

(v) Kipato chochote kutokana na umalaya, ngoma namuziki wa aina yoyote ni kipato haramu. Kamainavyobainika katika Hadithi ifuatayo:

Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allahameharamisha kipato kutokana na mauzo ya mbwa,na kipato kutokana na kuimba kwa wasichana (sing-ing girls) (Sharhi Sunnat).

(vi) Kipato chochote kutokana na utabiri, ramli, naupigaji bao ni kipato haramu, na yote hayo ni kazi yashetani katika Qur’an Allah (s.w.) ametuasa:

Page 181: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

170

Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi na kamari nakuabudiwa (kuombwa) asiyekuwa MwenyeziMungu, na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli(na kwa vinginevyo); (yote haya) ni uchafu (na ni)katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo ilimpate kufaulu” (5:90)

Kutokana na aya hii upigaji ramli na utazamiaji waaina yoyote ni haramu na kipato chake kitakachopatikanana kazi hiyo ni haramu pia. Utabiri wa aina yoyote niharamu, hali kadhalika kipato kinachotokana na kazi hiyoya utabiri ni haramu. Abu Bakar aliwahi kujitapisha baadaya kugundua kuwa amelishwa kutokana na malipo yautabiri. Pia kipato kutokana na uchawi ni kipato haramu.

(vii) Hongo (Rushwa)Utoaji na upokeaji wa rushwa ni haramu na pato lolote

lililotokana na rushwa ni pato haramu. Mtoaji na mpokeajiwa rushwa wote wamelaaniwa na Allah na Mtume wakekama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:

Abdullah bin Amr ameeleza kuwa Mtume wa Allahamemlaani mpokeaji rushwa na mtoaji rushwa katikakutoa hukumu. (Abu Daud, Ibn Majah).

Hongo au rushwa ni kiasi chochote anachopokeamuhudumu (mfanyakazi) zaidi kuliko malipo yake ya hakikatika kutoa huduma alizoajiriwa kwazo. Kwa maananyingine, mtu akipokea malipo yoyote, hata yawe madogokiasi gani ambayo ni ziada ya mshahara wake katikakufanya kazi ile ile na katika kiwango kile kile cha kazialiyoajiriwa kwayo, atakuwa amepokea rushwa. Turejeekwa makini Hadithi ifuatayo:

Abu Humaid as-Sayyid ameeleza Mtume (s.a.w.)alimteua mtu katika kabila la Azd aliyekuwa akiitwaIbnul Luthiyyah kama, mkusanyaji wa zakat,Aliporudi Madina, alisema: “Hii ni kwa ajili yenu na

Page 182: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

171

hivi ni vyangu (nilivyopokea) kama zawadi KishaMtume (s.a.w.) alitoa hutuba baada ya kumhimidi nakumtukuza Allah akasema: Jambo lingine nikwamba nimewateua baadhi ya watu miongonimwenu kufanya (kuongoza) shughuli ambazo Allahamenipa mamlaka kwazo. Mmoja wao anakuja nakusema: ‘Hii ni kwa ajili yenu na hii ni zawadiniliyopewa. Kwa nini basi asibakie katika nyumbaya baba yake au katika nyumba ya mama yake nakuona kuwa angalipewa zawadi au hangelipewa?Kwa yule ambaye mikononi mwake uko uhai wanguhapana yoyote atakayechukua kitu chochotekutokana na zakati awe siku ya Kiyama hakutokeahuku amebeba kitu hicho mabegani mwake. Kamaalichukua punda atakuwa analia humo begani; kamaalichukua mbuzi atakuwa analia (mee mee) humobegani. Kisha Mtume (s.a.w.) aliinua mikono yakempaka tukaona weupe wa makwapani na akasema:“Ee Allah! Nimefikisha ujumbe)? Ee Allah!Nimefikisha ujumbe)?” (Bukhari na Muslim).

Hadithi hii inatuonesha kuwa mkusanyaji hakuwana haki ya kuchukua zawadi katika kukusanya maliambayo ndiyo kazi aliyoteuliwa kwayo. Swali aliloulizwani: Je, angalikuwa nyumbani au asingalitoka kukusanyazakat, angaliletewa zawadi hizo? Jibu ni kwambaasingeletewa zawadi hizo nyumbani kwake. Kwa hiyozawadi zinazopatikana kwa namna hiyo si zawadi bali nirushwa au hongo. Hadithi hii inatupa fundisho kubwa juuya upokeaji zawadi makazini. Mara nyingi watu hupokearushwa kwa jina la “zawadi”. Hadithi hii imetuwekeampaka unaotenganisha rushwa na zawadi. Kitu cha ziadaya malipo ya kazi au ziada ya mshahara kitabainika kuwazawadi au hongo (rushwa) kutokana na jibu la swalilifuatalo: Je, kama afisa (mfanyakazi) asingelikuwa katikanafasi ya kazi aliyonayo au katika cheo alicho nacho,

Page 183: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

172

angalipata zawadi hiyo au asingelipata? Kama jibu ni“asingalipata” basi afisa huyo au mfanyakazi huyo akipokeazawadi ajuwe amepokea hongo. Kama afisa au mfanyakazihuyo amepewa zawadi isiyohusiana na nafasi yake ya kazi;na angaliweza kupata zawadi hiyo hata kama angalikuwahana kazi au angalikuwa mahali pengine, basi zawadi hiyoitakuwa ni zawadi kweli na itakuwa halali kwake.

Madhara ya rushwa yako wazi. Kwanza, mwenyekupokea rushwa (hongo) anapokea chumo la haramuambalo litamfanya asikubaliwe ibada zake zote. Pili, Mlarushwa hawezi kumsaidia mtu asiyejiweza. Kila marawatawahudumia wale wenye kitu cha kutoa hongo kwanamna nyingine mnyonge asiye na uwezo wa kutoachochote hatapata huduma muhimu za maishaanazostahiki kupata. Tatu, mla rushwa hawezikuheshimiwa au kuaminiwa katika jamii kwa shughuliyoyote ile.

Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo,

ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbalivya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekeeunaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili. Ombaomba ni kitendo kibaya sana kikiwa kimefanywa na mtubinafsi au taifa na kinashusha hadhi ya mtu binafsi nahadhi ya taifa kwa ujumla. Hivyo Uislamu ambao ndionjia sahihi pekee ya maisha, hauwezi kamwe ukapaliliaomba omba na wala Zaka na sadaka kazi yake si kupaliliaomba-omba, bali kinyume chake zaka na sadaka nimiongoni mwa silaha zinazotumiwa kutokomeza ombaomba. Uislamu unawashutumu vikali omba omba kamatunavyojifunza katika Hadithi ifuatayo:

Hubshi bin Junadah ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema: Kuomba-omba si halali kwa mwenyeuwezo wala kwa mwenye uzima wa afya na mwenye

Page 184: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

173

nguvu (za kufanya kazi) ila kwa mwenye kupigwaufakiri na mwenye deni kubwa (asiloweza kulilipa).Na yule anayeomba watu ili ajiongezee mali yakeatakuwa na mkwaruzo usoni mwake katika siku yaKiyama na atayala kwa ulafi mkubwa mawe ya motokutoka motoni. Kwa hiyo anayetaka, mwache aombekidogo, na mwache aombe kingi. (Tirmidh)

Wanaoruhusiwa kuomba kwa mujibu wa Hadith ni:(i) Mtu aliyesimama kumdhamini mtu mwingine ili

kuleta suluhu kati ya wagomvi wawili. huyu anaruhusiwakuomba hata akiwa tajiri. Kwa mnasaba huu, wauminiwa misikitini, madarasa, na shughuli mbali mbali zaKiislamu wanaruhusiwa kuomba michango ya Waislamuili kufanikisha shughuli hizo.

(ii) Mtu aliyepata ajali na kuharibikiwa kabisa na vituvyake vyote kama vile ajali ya moto, mafuriko, nakadhalika.

(iii) Mtu ambaye amepigwa na ufakiri na amekosakabisa mahitaji muhimu ya maisha kama vile chakula,malazi na makazi, lakini mtu akiwa na angalau chakulacha siku moja na malazi mkononi mwake haruhusiwikuomba kama tunavyofahamishwa katika Hadithizifuatazo:

Abdullah bin Mas’ud ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema: Anayeomba omba watu na ilhali anamahitaji muhimu ya maisha atakuja siku ya Kiyamana mikwaruzo, vidonda au majeraha usoni mwake.Iliulizwa: Ee Mtume wa Allah! Ni kiasi ganikinachomtosha mtu? Akajibu: Dirham 50 au thamaniyake. (Abu Daud, Tirmidh, Nisai, Ibn Majah).Sahl bin Haohaliyya ameeleza kuwa Mtume wa Al-lah amesema:Yeyote yule anayeomba na ilihalianajitosheleza kwa mahitaji muhimu, anaomba moto(Jahannam). Nufaili ambaye ni miongoni mwa

Page 185: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

174

wasimulizi wa Hadithi hii katika sehemu nyinginealiuliza: Ni yupi mwenye uwezo ambaye kuomba niharamu? Alijibu (Mtume s.a.w.): Yule mwenyeuwezo wa kupata chakula cha asubuhi na usiku.Mahali pengine amesema: Yule mwenye chakula chasiku moja (usiku na mchana) (Abu Daud).

Hivyo ikibidi mtu aombe, basi aombe kwa sababu hizotatu zilizotajwa katika Hadithi hii. Kuomba omba bila yasababu za msingi kumeharamishwa kwa sababu kuu tatuzifuatazo:

(i)Kuomba omba kunamfanya mtu apoteze moyonimwake ile hali ya kumtegemea Allah (s.w.) na atajengamoyoni mwake hali ya kulalamika juu ya neema za Allahzilizomzunguka kila mahali. Kwa msingi huu hatima yakuomba omba ni kumfanya mja awategemee wengine kwamahitajio yake badala ya kumtegemea Allah (s.w.) nakumfanya ashindwe kushukuru neema za Allah (s.w.).

(ii) Kuomba omba humfanya mtu awe mnyonge naajidhalilishe kwa wengine ambapo Muislamu anatakiwaajidhalilishe kwa Allah (s.w.) peke yake.

(iii) Vile vile kuomba omba kumekatazwa kwa sababukunamuweka yule anayeombwa katika hali ngumu. Wakatimwingine anayeombwa hali yake si nzuri vile vile lakinikwa kuombwa hulazimika kutoa jambo ambalo linawezakumuathiri yeye na wale anaowaangalia.

Uislamu haukuishia kwenye kukemea tu tabia ya ombaomba bali umetoa njia za kutatua tatizo hili kamaifuatavyo:

(i)Kuwasaidia wale wote wenye matatizo na dhiki mbalimbali kwa kuwapa Sadaqa na zakati kabla hawajaomba.

Page 186: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

175

(ii)Njia ya pili, ya kukomesha kuomba omba nikujitegemea kwa kufanya kazi kwa kutumia juhudi namaarifa.

7. Mfumo wa benkiMabenki ni taasisi za fedha ambazo ni muhimu sana

katika uchumi. Benki husaidia uchumi kwa kutoa hudumakuu zifuatazo:

Kwanza, Benki hutoa huduma ya kuhifadhi akiba zawatu na kuhifadhi mali zenye thamani kubwa kama viledhahabu, na mfano wake.

Pili, kutokana na akiba inazozikusanya, benki hujikutakila wakati ina fedha nyingi zisizo na shughuli yoyote.Benki hukopesha fedha hizi kwa watu wanaozihitajia iliziwe mtaji wa kuendeleza biashara, viwanda, kilimo nasekta nyingine mbali mbali za uchumi na utoaji huduma.

Tatu, benki hutoa huduma ya kurahisisha malipo kwanjia ya hundi (cheque) kuwalipa Wafanyakazi kupitia benkizao au kwa hundi, huwaepusha walipaji na hatari yakuibiwa.

Nne, pia benki hutoa huduma ya kutoa malipo ya mbalipopote pale penye matawi yake nchini au ulimwenguni.Huduma hii ni muhimu sana kwani huwapunguzia watumzigo wa kusafiri na fedha nyingi mkononi.

Badala yake benki huidhinisha malipo kwa simu aukwa njia yoyote ya mawasiliano ya haraka katika tawi laBenki hiyo popote lilipo nchini au ulimwenguni kupitiakwenye Account ya huyo anayestahiki kulipwa.

Huduma hizi muhimu na nyinginezo nyingi ambazohatukuzitaja hapa zinatudhihirishia umuhimu wa kuwepotaasisi hii ya fedha katika jamii.

Page 187: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

176

Hivyo ni dhahiri kwamba Uislamu ukiwa ni mfumokamili wa maisha unaojitegemea kwa kila kitu, hautarajiwiukapinga au ukaharamisha kuwepo kwa mabenki katikajamii.Bali Uislamu unaharamisha mabenkiyanayoendeshwa kwa kipato cha riba.

Mabenki ya RibaMabenki ya kitwaghuti (yasiyokuwa ya Kiislamu)

sehemu kubwa ya kipato chake hutokana na riba.

Mabenki ya Riba hukopesha watu wenye miradi mbalimbali ya uchumi na kuwatoza riba kubwa katika mfumowa malimbikizo (compound interest). Sehemu ndogo ya ribainayokusanywa na Benki za Riba, hutumiwa katikakuwalipa wateja walioweka akiba zao ambao ndio hasamatajiri walioifanya Benki iwepo.

Ni kutokana na unyonyaji wa namna hii utakuta,wakati wakulima na Wafanyakazi wa ngazi za chini ambaondio wanaovuja jasho ili kuchangia riba, hawajimudukatika kujipatia chakula, mavazi, na makazi bora, wenyemabenki wanagawa “bonus” kwa wafanya kazi wao na waowenyewe wanaponda starehe na anasa zilizopindukiakutokana na riba ambayo hawakuitoleo jasho lolote.

8. Tatizo la RibaRiba ni kupata chochote kile cha ziada kutoka katika

mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara.Mwenyezi Mungu anatufahamisha katika Qur’an:

Page 188: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

177

Wale wanaokula riba hawasimami ila kamaanavyosimama yule ambaye shetani kamzuga kwakumsawaa; haya ni kwa sababu wamesema, Biasharani kama riba, hali Mwenyezi Mungu amehalalishabiashara na kuiharamisha riba.(2:275)

Mwenyezi Mungu huyafutia (baraka mali ya) riba; nakuyatia baraka (mali iliyotolewa) sadaka (2:276).

Madhara ya riba katika jamii(i) Riba inachafua nafsi ya Tajiri na uchumi wake.

Tajiri ambaye hayuko tayari kukukopesha mali yake pasina riba, kamwe hawezi kutoa mali yake bure kuwasaidiawanyonge na wenye dhiki. Tajiri asiye tayari kutoa maliyake kuwasaidia wenziwe wenye dhiki na shida katikajamii huwa mchoyo, bahili, mpupiaji mali, asiyetoshekana utajiri alionao, mfujaji, muonevu na dhalimu. Tajirimwenye moyo wa namna hii hata kama atajiita Muislamuhawezi kamwe kuchunga mipaka ya halali na haramukatika kuchuma!

(ii) Riba inamkandamiza Mnyonge mwenye dhiki.Wanyonge na wenye dhiki katika jamii inayoendeshauchumi wake katika misingi ya riba, hawapati msaadawowote wa bure kutoka kwa matajiri kwa kiasi ambachowengi wa wale wasiojiweza kabisa kujitosheleza kwa

Page 189: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

178

mahitaji muhimu ya maisha yao kwa namna duni sana -wengi hujipatia chakula chao kutoka katika mapipa yataka (watoto wa mtaani), wengi hujisitiri kwa masalioyaliyookotezwa hapa na pale na wengi makazi yao nistesheni na sokoni. Hawa, kisaikolojia, hujiona ni watuduni wasio na maana yoyote katika jamii na huwaonamatajiri na watu wenye uwezo kuwa ndio wenye maana.Na hapa ndipo inapojengeka chuki baina ya wasionachokuwachukia walio nacho.

(iii) Riba inaharibu uchumi wa jamii na maendeleoyake. Riba na msingi wake wa unyonyaji imma ikitozwana tajiri mmoja au kikundi cha matajiri, imefanywa msingiwa uchumi wa taifa au wa kimataifa. Kwa bahati mbayakutokana na mazoea tuliyonayo juu ya vyombo vya uchumivya kitaifa na kimataifa vinavyoendeshwa katika misingiya Riba kama vile mabenki ya taifa na shirika la Bima laKimataifa, baadhi ya watu wamediriki kuhalalisha Ribaya mabenki na Bima. Kuhalalisha huku kwa riba yamabenki na Bima aidha kumetokana na uzoefu wa uchumiharamu katika jamii zetu au umetokana na kushindwakuona ubaya wa riba kitaifa au kimataifa.

Waislamu hatuna budi kukumbuka kuwaalichokiharamisha Allah (s.w) kinakuwa ni haramu katikawingi wake na katika uchache wake. Tukichukua mfanowa pombe Mtume (s.a.w.) amesema:

Kinacholewesha kikiwa kingi ni haramu pia hatakikiwa kichache.(Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).

Kwa hiyo kilicho haramishwa kwa mtu binafsi, pia niharamu kwa taifa na ni haramu kwa mataifa yoteulimwenguni. Kwa upande mwingine jambo la haramulitakapotendwa kitaifa litakuwa na athari mbaya zaidi kwa

Page 190: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

179

jamii kuliko likitendwa katika kiwango cha mtu binafsi,hali kadhalika jambo baya likitendwa kimataifa huwa naathari kubwa na mbaya zaidi kwa jamii ya mwanadamukuliko likitendwa katika kiwango cha kitaifa.

(iv) Riba ni mali ya dhulma inayonyakuliwa na matajirikutoka kwa wanyonge kwa njia moja au nyinginekiuchumi, pia riba inaukandamiza na kuudidimiza uchumiwa kitaifa au kimataifa. Mali ya riba kwa kuwa ni maliinayopatikana bila jasho na bila hata ya kushiriki katikamashaka ya uchumi, huwafanya matajiri na wenye uwezowa kuendesha miradi mbali mbali ya kiuchumi wakae tubila kazi wakingojea fedha zao zizae katika mabenki ambazowana kila uhakika wa kuzipata hata itokee gharka yanamna gani. Kwa hiyo kutokana na riba, jamii huwakosawatu wenye uwezo mkubwa wa kuzalisha mali ambaowangaliweza kuendesha miradi mbali mbali ya kiuchumiambayo ingaliinua uchumi wa taifa na wa kimataifa kwaujumla.

Wataalam wa uchumi wanakiri kuwa ribainaporomosha uchumi. Wamegundua kuwa kadiri kiwangocha riba kinavyokuwa kikubwa ndivyo uchumi unavyozidikushuka kwa sababu matajiri huona kuwa wanapata faidakubwa zaidi na kwa njia nyepesi isiyotoa jasho lolotewakiweka fedha zao benki kuliko kuziingiza katika miradiya kiuchumi. Hivyo utaona kuwa riba hupunguza uzalishajina huongeza gharama za uzalishaji.

Uharamu wa Riba katika Uislamu

Kwanza, Uislamu umeharamisha riba kwa sababu nidhulma (unyonyaji).Ukichukua mkopo wa ribauliochukuliwa kwa madhumuni ya kukidhi haja ya

Page 191: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

180

matumizi ya lazima ya nyumbani, utozaji wa riba unakiukalengo la Allah la kuumba (kuleta) mali kwa wanadamu.Utaratibu aliouweka Allah ni kwamba kwa kuwa maliameileta kwa wanaadamu wote:

“Yeye (Allah) Ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomokatika ardhi...” (2:29).

Ni lazima matajiri (wenye mali) wawapatie wanyongena wenye dhiki mahitaji yao muhimu ya maisha.

Pili, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababuinahamisha mali kutoka kwa maskini au wanyonge nakuipeleka kwa tajiri ambayo huzidi kuondoa usawa katikamgawanyo wa mali. Hii ni kinyume na mahitaji ya jamii.Uislamu unataka kila mtu apate mahitaji muhimu yamaisha. Hivyo wale walio na ziada ya mahitaji muhimuya maisha wanatakiwa wawape wasionacho kabisa au walewaliopungukiwa kwa upendo na udugu. Riba inakanushakabisa msimamo huu.

Tatu, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababuhufanya kundi la watu katika jamii liishi kivivu bila yakufanya shughuli yoyote ya uzalishaji, likitegemea kuishikwa riba kutokana na mali zao walizozikusanya katikamabenki, bima, na vyombo vingine vya riba. Jamii inakosamchango wa watu hawa katika uzalishaji na si hivyo tu,bali watu hawa wanakuwa mzigo na bughudha katikajamii. Ufasiki (uharibifu) wa aina zote katika ardhihufanywa na kundi hili.

Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi

ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna

Page 192: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

181

shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana. Ribaimechukuliwa kuwa kama motisha (faida) kwa mwenyekuruhusu fedha zake zitumiwe na mtu mwingine. Hivyomikopo kutoka kwa watu, makampuni, mabenki, mashirikaya bima n.k. haipatikani bila riba. Hivi sasa mikopo karibuyote duniani haitolewi bila riba. Mikopo hii kwa kawaidaimegawanywa katika makundi mawili:

(a) Mikopo ya muda mfupi(b) Mikopo ya muda mrefu

Tatizo hasa la riba linaonekana katika aina ya pili yamikopo (yaani mikopo ya muda mrefu) Hii ni kwa sababukiasi cha riba huongezeka mwaka hadi mwaka penginekuzidi hata fedha zilizokopeshwa mwanzoni. Aidha katikamikopo hii, baya zaidi ni kuingizwa kwa rahani na hatariiliyopo ya mkopeshwaji kunyang’anywa mali aliyowekarahani pindi atakaposhindwa kulipa deni kwa mudauliopangwa. Uislamu ukifuatwa vilivyo, tatizo hili haliwezikujitokeza kwani mwenye fedha analazimishwa kufanyamoja kati ya yafuatayo kwa mwenye kuhitaji fedha hizo:

(a)Kumkopesha bila riba kwa mudawatakaokubaliana. (Ama kwa kuweka au kutowekarahani mali yake).

(b)Kushirikiana katika mtaji na kugawana gharamaza uendeshaji, faida na hasara.

(a) Kukopesha bila ribaUislamu ni mfumo kamili wa maisha alioufuma Allah

(s.w.) na ni muhali kwa Allah (s.w.) kuwalazimishawanaadamu kufanya jambo wasiloliweza. Amekataza ribana kuruhusu biashara kwa sababu anafahamu kuwa ribainaweza kuepukika na biashara kufuatwa. Aidha uislamuunawaruhusu watu kukopeshana. Mtu anawezakumkopesha mwingine fedha ama kwa kutumia (matumizi

Page 193: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

182

ya kawaida katika maisha), au kwa kumsaidia mtajikufanyia biashara. Kwa hali yoyote itakavyokuwa mwenyekukopesha (mtoa fedha) analazimika kudai kiasi kile kilealichotoa kwa muda waliokubaliana bila ya kudai nyongezayoyote. Sheria iliyopo katika Uislamu katika kukopeshanani deni hilo kuandikwa (hata kama ni dogo) mbele yamashahidi waadilifu. Allah (s.w.) hata hivyo ametoaruhusa ya kukopeshana bila mwandishi kwa njia yakuweka vitu rahani. Anayathibitisha haya Mwenyezi Mungupale anaposema:

“Na kama hamkupata mwandishi basi (mdai) apewe(astakabadhishwe) (kitu kiwe) rahani mikononimwake. Na kama mmoja wenu amewekewa amanana mwenzake basi aliyeaminiwa airudishe amanaya mwenzake, na amche Mwenyezi Mungu Molawake. Wala msifiche ushahidi (japo juu ya nafsi zenu)Na atakayeficha basi hakika moyo wake ni wenyekuingia dhambini. Na Mwenyezi Mungu huyajuamnayoyatenda.” (2:282).

(b) Ushirika katika biasharaUislamu unaruhusu watu kufanya biashara kwa shirika

maadamu wanachunga sheria zilizowekwa (za Uislamu).Ushirikiano katika biashara unaweza kuwa wa watu wawiliau zaidi. Mara nyingi wanaoshirikiana huchangia katikamtaji wa biashara yao. Pindi watu wakikubaliana kufanyabiashara kwa shirika Uislamu unawalazimishakushirikiana vile vile katika gharama, faida au hasaraitakayopatikana. Hii hutegemea kiasi gani kila mshirikaamechangia katika biashara hiyo. Ushirikiano mwinginewowote usiokuwa katika mtaji utategemea makubalianoya washirika. Hebu tutazame ni kwa jinsi gani ushirikakatika mtaji wa biashara unavyoweza kutumika badala yamikopo ya rahani yenye riba.

(i)Mikopo inayopatikana kwa rahani (Mortgages).Kupata mkopo kwa kitu rahani si haramu katika Uislamu

Page 194: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

183

kama ilivyokwishabainishwa katika Qur’an. Hata MtumeMuhammad (s.a.w.) aliwahi kufanya hivyo kamatunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:

Bi Aisha (r.a) amesimulia kuwa: Mtume (s.a.w.) alinunuavyakula kwa mkopo kwa muda maalum na aliwekarahani (armour) zake kwa ajili hiyo (Bukhari).

Wanyama wafugwao vile vile wanaweza kuwekwarahani kwa ajili ya mkopo. Wanyama hawa wanawezawakatumika hata kama bado wapo rahani. Hadithi ifuatayoinatuthibitishia hayo:

Abu Hurairah (r.a) amesimulia: Mtume wa Allahamesema: “Mnyama aliyewekwa rahani anawezakutumika kuendeshwa maadamu analishwa namaziwa ya mnyama atoaye maziwa yanawezayakanyewa kulingana na kiasi mtu anagharimika juuyake. Yule anayemwendesha mnyama au kunywamaziwa yake hana budi kugharimia mahitaji yamnyama huyo”. (Bukhari).

Kinyume na utaratibu huo hivi sasa rahani hutumikakatika kupata mikopo ya muda mrefu. Mikopo hii huwezakutolewa na makampuni ya bima au makampuni ya akiba.Kitu kinachowekwa rahani huhesabiwa kama dhamanaya mkopo uliotolewa. Kwa kawaida kitu kinachowekwarahani ni kile ambacho kinaeleweka kuwa kina uwezowa kuzalisha mathalani nyumba au mashine. Mkopohulipwa na riba. Kama aliyekopeshwa atashindwa kutoariba au malipo ya fedha za mkopo basi mkopeshajihuhesabiwa kuwa ana haki ya kuchukuwa mali ya dhulmailiyo bayana kwa aliyekopeshwa.

(c) Ushirika katika mtaji badala ya mikopo ya rahaniyenye riba

Mtu anaweza kupata fedha kwa njia hii bila kutoariba. Njia hii inawezekana tu kwa kuwafanya watu

Page 195: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

184

wengine wawe wanashirika katika mali/kitu ambachokingewekwa rahani kwa kuchangia katika thamani ya kituhicho kwa njia ya kununua hisa (shared equity). Watuhawa wataridhia iwapo watafahamu hisa walizonazo katikamali/kitu hicho. Iwapo kwa mfano kitu hicho ni nyumbakodi itakayopatikana ni lazima igawanywe kwa wenye hisawote (baada ya kutoa gharama za uendeshaji). Mwenyenyumba au mwenye nyumba mtarajiwa (the owner to be)atakubaliana na washiriki hao kununua hisa zao hatuakwa hatua mpaka hisa zote zitakapokuwa zake (yaninyumba itakapokuwa mali yake). Njia hii hutekelezwakwa kufuata hatua zifuatazo:

(i) Makisio ya thamani ya kitu na idadi ya hisa. Kituambacho kilifikiriwa kuwekwa rahani ili kupata mikopohufanyiwa utafiti wa bei ambayo ingeweza kuuzwa.Hiihuchukuliwa kama thamani ya kuridhisha ya kitu hicho.Ni thamani hii ndiyo itakayogawanywa kwa watakaokuwana hisa (akiwemo atakayekuwa mwenye nyumba) Thamaniya kila hisa huamuliwa na huyo mwenye kutafuta fedhakwa wengine.

Thamani ya kitu na thamani ya kila hisa ndivyovitakavyoonesha idadi ya hisa. Iwapo thamani ya nyumba,mathalani ni shilingi 2,000,000 na thamani ya hisa mojani shilingi 100,000 idadi ya hisa itakuwa

(ii) Kutafuta mtaji wa mwanzo wa atakayekuwamwenye mali. Atakayekuwa mwenye mali lazima afahamukiasi cha mtaji au hisa atakazokuwa nazo mwanzoni kablaya kutoza hisa nyingine kwa wengine.

(iii) Kufahamu idadi ya hisa za washirika wengine.Idadi ya hisa za washirika wengine katika mali inapatikanakwa kugawa thamani ya hisa zote kwa thamani ya hisamoja.

Page 196: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

185

(iv) Kufahamu mapato (kabla ya kutoa gharama) namapato halisi (baada ya kutoa gharama za uendeshaji).wa mali. Mapato ya mali ambayo ilikusudiwa kuwekwarahani kwa ajili ya kupata mkopo lazima yafahamike.Mapato kwa ajili ya nyumba kwa kawaida huwa ni kodi yanyumba (rental charge). Thamani ya mapato hayo (gross rentalvalue) si yote yanayogawanywa kwa wenye hisa katika mali.Kuna umuhimu wa kutoa gharama zote za uendeshaji.

(v) Mapato yaliyobaki baada ya kutoa gharama zauendeshaji, hugawanywa kwa wenye hisa kulingana naidadi ya hisa mtu alizonazo katika mali ile.

Itaonekana wazi kuwa njia hii haihusu riba kwa namnayoyote ile. Tofauti zinazojitokeza kati ya njia hii na ile yakukopa kwa kuweka vitu rahani ni:

1) Mali humilikiwa na wenye hisa wote mpaka hapoatakayekuwa mmilikaji atakapomaliza kununua hisa zawengine wote.

2) Wenye hisa wote wana haki ya kugawana(kulingana na hisa mtu alizo nazo) mapato yanayotokanana mali hiyo na pia wana wajibu wa kushiriki katikagharama zote za uendeshaji.

Mali yenye kuchangiwa mtaji kwa hisaMtu akishaamua kuuza hisa (share) kwa watu wengine

kwa ajili ya mali fulani katika sheria ya Kiislamuanapoteza umilikaji wa mali wa mtu mmoja. Kuuza hisakwa wengine kwa maana nyingine ni kukaribisha watuwengine kushiriki katika umilikaji wa mali ile. Nafasi yamtu katika kumiliki mali hiyo itategemea idadi ya hisaalizonazo katika mali ile. Wenye hisa inabidi washirikianekatika faida na hasara pamoja na gharama za uendeshaji.

Page 197: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

186

Faida anazopata atakayekuwa mwenye kumiliki mali

Zipo faida kadhaa ambazo atakayekuwa mwenyekumiliki mali huzipata kwa kufuata ushirika katikabiashara, mtaji na faida (Shared Equity and rental) badalaya kupata mikopo ya biashara yenye riba. Faida kubwaatakayopata ni fadhila za Allah (s.w.) kwa kule kuepukakwake kutoa riba kwa mkopo atakaopata. Tunajifunzakatika Hadithi za Mtume (s.a.w.) kuwa laana ya Allah (s.w.)huwafikia wote wanaohusika na riba (mtoaji, mpokeaji,shahidi). Hata hivyo kuna faida nyingine ambazo anawezakuzipata:

(i) Atakayekuwa mwenye kumiliki mali kwakutochukuwa mkopo wenye masharti ya riba hujiepushakabisa na hatari ya kunyang’anywa mali yake (aliyowekarahani) akishindwa kutimiza masharti yake.

(ii) Fedha ambayo angeitoa kama riba kwa ajili yamkopo atabaki nayo na kutumia kwa shughuli nyinginekuendeshea maisha yake.

(iii) Atakuwa na uhakika wa kupata sehemu halaliya faida inayotokana na mali hiyo (kama ipo). Kadhalikakama ikitokea hasara haitamlazimu kubeba mzigo wotewa hasara kwani ushirika katika biashara huhusisha vilevile umuhimu wa kugawana hasara itokeapo.

Faida kwa wenye kununua hisaMwenye kununua hisa huchangia katika mtaji. Naye

huepuka ghadhabu za Allah (s.w.) za utoaji mkopo kwariba. Zaidi ya haya hupata faida zifuatazo:

(i) Hupata sehemu ya faida itokanayo na mali hiyokulingana na mchango wake kwenye biashara (idadi yahisa alizonazo).

Page 198: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

187

(ii) Huwa na sauti kwenye mali kwani naye pia nimwenye kumiliki mali ile mpaka atakapouza hisa zake.Isitoshe hutoa kiwango kidogo kujipatia haki ya kumilikiukilinganisha na mtaji mzima.

Kwa ujumla jamii nzima itanufaika kwa kuachamfumo wa mikopo kwa riba na kuhimiza watu kufanyaushirika katika biashara. Ilivyo waliokopeshana kwa ribahawawi katika uhusiano mzuri kiroho. Aliyekopeshwailimbidi kufanya hivyo kutokana na shida aliyokuwa nayo.Kutoa kwake riba anakufanya kwa kuwa anafahamu hatariza kutofanya hivyo (kupoteza mali yake) ingawa kitendohicho kinamuuma sana rohoni. Hivyo urafiki kati yamkopeshaji na mkopeshwaji huwa ni wa kinafiki. Jambohili ni wazi sana katika jamii ya dunia ya sasa. Hebufikiria athari za mikopo hii kwa nchi masikini duniani. Nimara nyingi nchi masikini zimekuwa zikipiga kelele aidhakupunguziwa au kufutiwa kabisa baadhi ya madeni yao.Sehemu kubwa ya madeni hayo ni limbikizo la riba lamiaka mingi.

Hivyo Uislamu unapiga vita riba kutokana namadhara yake kibinafsi, kitaifa na kimataifa. AidhaUislamu unahimiza ushirikiano katika biashara kamaufumbuzi wa tatizo la riba.

Benki za KiislamuBenki za Kiislamu ambazo hutoa huduma kama benki

nyingine zinaendeshwa katika msingi wa biashara na sioule wa riba. Benki za Kiislamu badala ya kukopesha kwariba, hutumia rasilimali zake kwa zenyewe kujihusishakatika uzalishaji kwa kufuata misingi inayokubalika katikaUislamu. Miongoni mwa misingi inayokubalika kwaMuislamu au Benki ya Kiislamu kuingiza fedha zake katikamiradi ya biashara au uzalishaji ni hii ifuatayo:

Page 199: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

188

(i) MudharabahMudharabah ni makubaliano kati ya watu wawili au

zaidi ambapo mmoja au zaidi kati ya hao anatoa mtaji namwingine hushiriki kwa ukamilifu katika kuendesha nakuongoza mradi wa uchumi. Faida itakayopatikana katikamradi huo itagawanywa kulingana na makubaliano yao.Hasara itakayotokana na mradi huo itakuwa ni ya mwenyekutoa mtaji. Wengine hawatoi chochote kusaidia hasarakwa sababu wameshatoa mchango wao wa hasara hiyokwa jasho walilolitoa katika shughuli ambayo haikuzaamatunda bali hasara.

Benki za Kiislamu zinaingiza fedha zake katika miradi yauchumi kwa njia hii ya Mudharabah ambapo benki hutoamtaji kwa ajili ya miradi mbali mbali ya uchumi kwamapatano ya kupata kiasi (asilimia) fulani cha faidaitakayopatikana na kuwa tayari kulipa hasaraitakayopatikana.

(ii) MusharikahMusharikah ni ushiriki kati ya watu wawili ambapo,

tofauti na Mudharabah wote wawili wanachangia mtaji nakushiriki katika uendeshaji wa shughuli ya kiuchumi,lakini si lazima watoe hisa sawa sawa, kwa makubalianoya kugawana faida na hasara kulingana na kiasi cha hisaalichotoa kila mmoja wao. Kwa mtindo huu wa“Musharikah” Benki ya Kiislamu inaingia katikakuchangia mtaji, kuendesha na kusimamia mradi wauchumi na watagawana (faida au hasara) kulingana nakiasi cha mtaji kila mmoja alichotoa.

(iii) Ijara-Uara wa IktinaHuu ni utaratibu mwingine unaokubalika kisheria

ambapo mtu au benki inatumia fedha zake katika kukodivitu kama vile magari, majumba, ardhi, na kadhalika,ambavyo vikifanyiwa kazi huzalisha mali na kutoa faida.

Page 200: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

189

Benki za Kiislamu hujipatia faida kubwa kutokana namtindo huu.

(iv) MurabahHuu ni utaratibu unaotumiwa katika kununua bidhaa

kwa wingi kwa ajili ya kuwauzia wafanya biashara ambaowaliofikiana kuwa bidhaa hizo zinunuliwe kwa ajili yao.Benki kutokana na uwezo wake inapanga na wafanyabiashara kuwa inunue bidhaa nyingi kutoka ndani na njeya nchi kwa jina lake kisha iwauzie wafanyabiashara haokwa bei itakayoipatia benki faida. Pia benki kwa mtindohuu inaweza kununua mazao ya wakulima na kuyauzakwa walaji kwa faida.

(v) MuqaradhaMtindo huu wa Muqaradha humruhusu mtu au benki

kununua “share” au “bonds” katika kampuni ya uzalishajikwa mapatano ya kugawana faida au hasara kulinganana kiasi cha “share”.

Kwa kufuata mitindo hii katika kuingiza fedha zakekatika miradi ya uchumi, Benki za Kiislamu hupata faidakubwa hata zaidi ya kipato cha riba kinachopatikana katikabenki za riba. Benki za Kiislamu nazo hugawa faidainayopatikana kwa wateja wake walioweka fedha zaokwenye benki.

Uzuri wa benki za KiislamuPamoja na benki za Kiislamu kutoa huduma

zinazotolewa na kila benki kama tulivyoziorodhesha hukonyuma, kuna faida za ziada zinazopatikana kutokana nabenki hizi kama ifuatavyo:

Kwanza benki za Kiislamu huiokoa jamii na uchumiwake na madhara yote yanayosababishwa na riba.

Page 201: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

190

Pili, Benki za Kiislamu huwaingiza katika uchumina kuwainua hata wale ambao hawana hata rasilimaliyoyote kwa mtindo wa Mudharabah. Hivyo ni kwamba,benki zinazoendeshwa kwa mikopo ya riba, haziwezikukopesha fedha zake kwa mtu yeyote asiye na rasilimaliyenye thamani sawa au zaidi ya mkopo ili atakaposhindwakulipa ifilisiwe rasilimali hiyo. Kwa mtindo huu wa mikopoya riba, ni matajiri tu wanaopata mikopo ya benki namasikini wasio na rasilimali yoyote huachwa hivyo hivyona umasikini wao bila ya msaada kutoka benki wakuwainua kiuchumi.

Tatu, benki za Kiislamu huinua uchumi wa jamii,kutokana na umakini na tahadhari kubwa zinazochukuakatika kuchagua na kuendesha miradi mbali mbali yauchumi. Kwa kuwa benki zenyewe zinajiingiza katikauchumi, zinahakikisha kuwa miradi zitakazoichagua niile yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha faida kubwa nayenye uwezekano mdogo wa kusababisha hasara.

Page 202: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

191

Zoezi la Nne

1. Uchumi ni nini?

2.Toa ufafanuzi mfupi namna Uislamu unavyoeleza dhanaya;

(a) Mafanikio(b) Umiliki wa mali(c) bidhaa(d) Matumizi

3. Soma kwa makini Qur’an (9:105),(5:1) na (6:165), kishatoa mafunzo ya kiuchumi.

4. Nukuu aya za Qur’an zinazoonesha umuhimu wauchumi, kisha bainisha mafunzo yake kwa muhtasari.

5. Katika uchumi wa Kiislamu, serikali ya Kiislamuinawajibu gani kwa wananchi na raia wake?

6. Taja mambo matatu yanayopaswa kuzingatiwa katikauuzaji na ununuzi wa bidhaa.

7. Bainisha biashara haramu zisizostahiki Muislamukuzifanya kibidhaa na njia au kiutaratibu.

8. Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu ni Rehema kwawalimwengu wote.

Thibitisha neema hii kwa kuonesha namna Qur’aninavyoondoa dhiki na ukata wa kiuchumi katika jamiikupitia mgawanyo wake wa mali.

9. Soma kwa mazingatio Qur’an 89:19,104:2,90:6, 68:12,89:17-18, 70:19-25. kwa mujibu wa Qur’an:

Page 203: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

192

(a) Wajibu wa kusimamia Haki za masikini na mafukarakuwezeshwa kujikimu kiuchumi katika jamii, Allah (sw)amewakabidhi akina nani?

(b) Ni akina nani wenye jukumu la kuondoa Omba-ombakatika jamii, ambao pia wanadhima ya kujibu mbele yaAllah (sw) kwa kuwepo na kushamiri tatizo hilo katikajamii.

(c) Je, katika jamii ambayo waumini wamewaachiakhatamu matwaghuti wenye mioyo ya uchoyo, unyimifu,ubakhili, kuhodhi, husda, na ubinafsi wa kutojali wengine;yafaa waumini kutowaangalia Omba-omba, ambao ni“madhuluman”?.

10. (a) Onesha tafauti zilizopo baina ya biashara na riba. (b) Riba ina madhara gani katika jamii?

11. Onesha kwa ufupi misingi ya uendeshaji benki yaKiislamu pasina riba.

Page 204: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

193

Sura ya Tano

SIASA

Maana ya siasaSiasa ni sayansi ya uendeshaji mambo ya kijamii.

Dhana kuu za siasa ni utawala (mamlaka), itikadi,matashi na maamuzi.Hivyo tunapoitizama siasahatunabudi kuzingatia kuwa ni mfumo wa utawala, itiqadi,matashi na maamuzi ya mtu au kikundi cha watu auufunuo kutoka kwa Allah (s.w).

Kumbukumbu za kihistoria zinatufahamisha kwambasiasa ilianza pale wanaadamu walipoanza kuishi pamojakama kijiji, mji, taifa hadi kufikia mataifa. Hivyo siasa nijambo kongwe kama ilivyo historia ya mwanaadamumwenyewe.

Katika jamii ya mwanaadamu kuna mfumo mikuumiwili ya siasa.

1. Mifumo ya siasa iliyobuniwa na wanadamu – siasaza kitwaghutii.

2. Mfumo wa siasa uliowekwa na Mwenyezi Mungu –siasa ya Kiislamu.

1. Mifumo ya siasa za kitwaghutiKwa mtazamo wa Kiislamu, masuala ya kijamii yenyekufuata mitindo na mipangilio iliyobuniwa na watu ndiyoyanayofahamika kama siasa za kitwaghuti. Kihistoriasiasa hizo zimepita katika vipindi mbali mbali hadi hivileo. Vipindi hivyo ni pamoja na:

(i) Ujima.(ii) Utumwa.(iii) Umwinyi.(iv) Ubepari.

Page 205: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

194

(v) Ujamaa na Ukomunisti.(vi) Demokrasia.

(i) UjimaNadharia za kitwaghutii zinamuangalia mwanaadamu

kama mnyama ambaye katika kipindi cha ujima (cha awali)hakutofautiana na wanyama wengine. Yeye pia aliishimtini, akaenda kwa miguu na mikono kwa pamoja.Hakutofautiana sana na nyani alipokuwa katika hali yausokwe-mtu. Kutokana na mabadiliko ya kimazingirabaadhi ya wanyama, miongoni mwao akiwemo sokwe-mtu,walitoka katika hali ya kuishi mitini, wakateremka chini.Hapo ndipo yalipotokea “mabadiliko” ya maumbile ya miiliyao kulingana na mazingira mapya. Lakini kutokana nauhasama uliokuwepo katika mazingira hayo mapya, kwanimisitu na wanyama wakali walienea kote, mtu wa mwanzohakuweza kuishi peke yake kiubinafsi. Hali hizo zakimazingira zilimlazimisha mtu wa mwanzo aishi kwaushirikiano na wenziwe ili aweze kupambana na mazingirahayo makali. Hapo ndipo ilipoanza siasa kwa mujibu wanadharia hii.

(ii) Mfumo wa siasa za utumwaMfumo wa siasa za kitumwa unafuatia ujima katika

siasa za kitwaghutii. Ni mfumo wa siasa za kitabakaambapo watu huishi kwa jasho la watu wenginewanaomilikiwa kama bidhaa. Watu hao wenye fursa zamali au hadhi katika jamii huishi kwa kuwatumikishawengine. Katika mfumo huu, utawala uko mikononi mwamatajiri ambao huendesha siasa za kuwatumikishawengine na wao kuishi maisha ya raha. Chini ya mfumohuu wa siasa, uzalishaji mali umewekwa migongoni mwawatu wa tabaka la chini la watwana.

Mfumo huu wa kitumwa ulianza kuyumba kwamigongano mbalimbali. Watumwa walianza kujizatiti na

Page 206: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

195

kupinga vikali sana utumwa wao. Watu ambao hapo awaliwalinyang’anywa mali zao na mabwana wenye watumwawaliungana pamoja na watumwa katika mapambano yakuufuta utumwa:

(iii) Mfumo wa siasa za UkabailaSiasa za Ukabaila ambazo zilifuatia baada ya siasa

za kitumwa nazo vile vile zilikuwa na minyororo yake.Katika mfumo huu tabaka la Kikabaila hutawala njia zoteza kijamii. Njia za kiuchumi hutawaliwa kwa kukodishamashamba halafu kutoa fungu kubwa kwa mwenyeshamba wakati wa mavuno. Wazalishaji kwenye mashambahayo chini ya mfumo huu, tofauti na utumwa, hulipwaposho kidogo kama malipo ya kazi nzito walizotumikishwa.Kwa mtazamo wa Kitwaghuti juu ya historia ya mfumohuu, inadaiwa kuwa taasisi za dini pia zimetumika“kuhalalisha” ubwana na utwana! Mfumo wa siasa zaUkabaila ulisita kuendelea baada ya wanyonywaji kujiungapamoja dhidi ya wanyonyaji.

(iv) Mfumo wa siasa za kibepariSiasa za kibepari ni moja ya mifumo ya Kitwaghuti

iliyokita mizizi katika jamii nyingi. Katika mfumo huu kilakitu kinachowezekana kufanywa ili “kuzalisha” pesahufanywa. Wachache walio na fursa za mali na hadhindiyo huendesha masuala yote ya jamii na kundi kubwala wanajamii huishi kwa kuuza nguvu, vipaji na taalumazao kwa wachache hao, na wale wasio na chochotehulazimika kufanya vitendo vyovyote ili mradi wapate pesa.

(v) Mfumo wa siasa za Kijamaa (Kikomunist)Katika mfumo huu uliodhaniwa na waasisi wake kuwa

ungelimkomboa mwanaadamu na kuleta “usawa wa sare”,chama ndicho hushika hatamu zote na “huwakilishamatakwa ya walio wengi” katika jamii. Aidha hudaiwakuwa jamii chini ya mfumo huu wa siasa watu huwa huru

Page 207: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

196

kabisa na kuwa na “demokrasia” halisi. Hata hivyo historiainaonesha kuwa chini ya mfumo huu wa siasa, jamiihupumbazwa na kudumazwa kwa njia mbalimbali. Kwakuwa chama hushika hatamu za maongozi, ni kamati yawatu wachache tu ndani ya chama hicho ndioinayoendesha masuala yote ya utawala Hudhibiti kila kitukwa kuimarisha ulinzi wa siri ambao hupenyezwa kilaeneo la jamii. Huendesha propaganda dhidi ya wale wotewenye fikra tofauti na zao. Njia zote za uchumi huwa chiniya kikundi hicho cha watu kwa sura ya “mali ya umma”.Katika Tasnifu (thesis) yake ya shahada ya udaktari wafalsafa mwaka 1946, Dk. Rafiuddiin, aliandika juu yakuporomoka kwa siasa hii kama ifuatavyo:

“Marxism (Communism), like every wrong ideal, containsthe germs of its own dissolution and must break upsooner or later”1

Umarx (ukomonist), kama ilivyo kwa itikadi yoyote ileya urongo, umebeba sumu inayoumaliza , hivyo lazimauporomoke hivi karibuni au baadae”.

Hali iliendelea kuwa ngumu katika nchi zilizokuwaviranja wa siasa hii na hadi kufikia mwaka 1989 miaka70 ya mapinduzi hayo ya kikomonist, Urusi ilisambaratikana huo ukawa ndio mwisho wa siasa hiyo.

(vi) Mfumo wa siasa za kidemokrasiaDemokrasia ikiwa na maana ya maamuzi ya wengi

katika kuweka mamlaka waitakayo ni mfumo wa maishauliobuniwa Uyunani (Ugiriki). Wataalamu wa mambo yasiasa wanafahamisha kuwa neno Democracy ni muunganowa maneno mawili yenye kuleta maana moja; Demos-nguvuya raia na cracy ni “utawala”, yaani utawala unaotokanana maamuzi ya wengi miongoni mwa raia.

Page 208: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

197

Hivi leo Demokrasia hufahamika kama ni utawala wawatu uliowekwa na watu kwa ajili ya watu (The govern-ment of the people by the people for the people). Au ni uhuruwa kujiamulia mambo vile mtu apendavyo! Kutokana natafsiri hiyo, kisiasa, kuna aina tofauti za miundo yademokrasia; zipo demokrasia za chama kimoja, demokrasiaza vyama viwili, demokrasia ya vyama vingi, demokrasiaya kiliberali ambayo ni demokrasia ya moja kwa moja (di-rect democracy) na demokrasia ya uwakilishi (representa-tive democracy), nakadhalika.

2. Mfumo wa siasa ya KiislamuMfumo wa siasa ya Kiislamu ni utaratibu na muongozo

wa masuala ya jamii ambao misingi yake ni vitabu vyaAllah (s.w) na Sunnah za Mitume wake tangu Mtume wakwanza, Adam (a.s) hadi Mtume wa Mwisho, Muhammad(s.a.w). Ni mfumo uliowekwa na Allah (s.w) kupitia kwaMitume wake wote. Mitume wote walikuja kusimamishamfumo wa maisha aliouridhia Allah (Dini ya Allah).Kuhusu Mtume Muhammad (s.a.w) tunafahamishwakatika Qur-an:

“Yeye (Allah) ndiye aliyemleta Mtume wake (NabiiMuhammad) kwa uongofu na kwa dini ya haki ili aijaaliekushinda dini zote, ijapokuwa watachukia washirikina”.(9:33, 61:9)

Kwa ujumla, mitume wote waliwalingania watu waokutambua kuwa mwenye haki ya kutoa mwongozo nakuweka utawala juu ya wanaadamu ni Allah (s.w) pekee.

Page 209: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

198

Pia waliwalingania watu wao kuwa kufuata maongoziyoyote yale ya kijamii (siasa), kinyume na Allah (s.w) nishirk. Hivyo, wale wote wanaoendesha masuala ya kijamiikwa kutumia taratibu na miongozo iliyoasisiwa na watuwanamshirikisha Allah (s.w) katika siasa na ni wazushitu kama Mwenyewe Allah (s.w) anavyotutahadharisha:

Na kama ukiwatii wengi katika (hawa) waliomoulimwenguni watakupoteza na njia ya Mwenyezi Mungu.Hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kuzua(tu basi).” (6:116).

Dhana ya DolaDola ni eneo la ardhi lenye mkusanyiko wa watu walio

huru chini ya utawala mmoja wenye uwezo wakujitosheleza kwa mahitaji muhimu na kulinda mipakaya eneo lake. Eneo hili la ardhi huitwa nchi na wakaziwake ndio wazawa au wananchi wenye haki na eneo hili.Katika ulimwengu huu kuna aina kuu mbili za Dola. Dolaza kitwaghutii na Dola za Kiislamu.

Tutaangalia kwa muhutasari miundo na uendeshajiwa dola hizi ili tuweze kulinganisha na kutofautishamifumo ya utawala iliyowekwa na wanaadamu na uleuliowekwa na Muumba.

Dola za Kitwaghuti1. Muundo na Uendeshaji wakeChombo kikuu cha kwanza katika dola za kitwaghuti

ni serikali. Kazi kuu ya serikali ni kutawala kwa kutumia

Page 210: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

199

nguvu kuhakikisha kuwa jamii husika inafuata mwenendounaotakiwa na serikali. Serikali inaundwa na sehemutatu – Kiongozi Mkuu wa Dola au Rais. Baraza la Mawazirina Majeshi. Kiongozi Mkuu wa Dola amekuwa ndiyemtendaji mkuu na muamrishaji mkuu wa majeshi (AmirJeshi Mkuu). Katika uhusiano na Dola nyingine, kiongozimkuu ndiye msemaji mkuu kwa niaba ya Dola yake.Kiongozi huyu mkuu wa dola huwa juu ya sheria na hawezikushitakiwa kwa kosa lolote analolitenda wakati wautendaji kazi wake kama kiongozi mkuu wa dola

Majeshi ya serikali za kitwaghuti ndio nguvu ya dola.Majeshi hutumika kulinda, kutetea, na kuhakikishamatakwa na maslahi ya serikali yanapatikana. Majeshivile vile hutumika katika kulinda mipaka na mamlaka yadola. Wakati mwingine hutumika kuvamia nchi nyingineili kupanua mipaka ya dola. Majeshi pia hutumiwa katikakusimamia utekelezaji wa sheria na amri zotezinazotakiwa na serikali. Majeshi yenyewe hugawanyikakatika sehemu tofauti kiutendaji. Kuna jeshi la polisi lenyevikosi vya ulinzi wa kawaida kwa usalama wa raia, vikosivya kutuliza fujo, vikosi vya usalama barabarani, nakadhalika, hivi vyote hushughulikia usalama wa raia tu.Kuna jeshi la ulinzi linaloshughulika na ulinzi wa mipakaya dola kwa ujumla likiwa na vikosi vya nchi kavu, vikosivya anga na vikosi vya majini. Kuna jeshi la magerezalinaloshughulika na wahalifu wote wanaovunja sheria.

Pamoja na majeshi zipo idara au vitengo maalumu vyausalama vilivyo chini ya ofisi ya mkuu wa dola ambavyohujishughulisha na utafiti wa habari muhimu kiutawala(Intelligence bureau) ambavyo ndani ya mipaka ya dolahuchunguza kwa mbinu mbali mbali kutafuta hisia naminong’ono ya wananchi jinsi wanavyoitazama serikali namipango yao dhidi yake.

Page 211: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

200

Kwa ujumla Idara ya usalama hujishughulisha namaeneo yafuatayo:

(1) Kupeleleza mambo mbali mbali kisha kuiarifuserikali sambamba na kupendekeza au kushaurihatua muafaka za kuchukuliwa.

(2) Kukusanya habari na taarifa muhimuzinazohitajika na serikali kiusalama.

(3) Kuingilia kati shughuli za idara au mashirikamengine ya upelelezi na ujasusi.

(4) Kueneza na kushinikiza sera na matakwa yaserikali kwa njia mbali mbali za siri vikiwamovitisho (intimidation), upotoshaji wa habari aukueneza habari zisizo zenyewe (disinformation),udhibiti wa habari, urubunifu, kufitinisha nakufarakanisha wapinzani, kuendesha propa-ganda na kuwadhibiti wapinzani wa kisiasa,kujipenyeza au kutumia watendaji (doubleagents) ndani ya makundi ya watu, taasisi aujumuiya ili kufahamu mipango yao ili wawezekuivuruga. Vile vile katika serikali kuna sehemuya utawala (Administration) iliyoundwakutokana na msururu mrefu wa urasimu.Warasimu hao waliogawanywa katika wizara,idara, na vitengo mbalimbali, husimamiashughuli za kila siku za serikali. Wanakuwa namamlaka ya kutoa amri na maelekezo ya marakwa mara. Mbali na kuwa na serikali kuu, Dolahuwa pia na serikali za majimbo (mikoa), serikaliza wilaya, miji, na za mitaa. Kila serikaliinakuwa na kiongozi wake mkuu k.v. mkuu wamkoa, mkuu wa wilaya, n.k.

Page 212: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

201

Chombo kikuu cha pili cha dola ya kitwaghutii niBunge. Bunge nalo huwa na sehemu mbili. Bunge kwamaana ya wabunge tu na Bunge Kuu kwa maana yawabunge na kiongozi mkuu wa dola (Rais). Kazi ya Bungeni kutunga sheria na kudhibiti mwenendo wa serikali.Hata hivyo katika mfumo wa serikali iliyochini ya Rais(Presidential form of government) sheria zinazopitishwana Bunge haziwi sheria mpaka akubali Rais na kuidhinishakwa saini yake.

Vile vile bunge lina kazi ya kudhibiti mwenendo waserikali kwa kujadili na kupitisha makisio ya mapato namatumizi ya serikali (Budget).

Chombo kikuu cha tatu cha Dola ni Mahakama. Kazikuu ya mahakama katika mfumo wa kitwaghutii ni kuelezana kufafanua utekelezaji wa sheria. Kuonesha namnaya kuwajibika na kuadhibu pale inapolazimu. Kwa maananyingine mahakama inayokazi ya kutoa au kusimamiautoaji wa haki. Mahakama zinaweza kuwa na mpangiliowa kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu kama vile mahakamaza mwanzo, mahakama ya wilaya, mahakama za mikoa,mahakama kuu na mahakama za Rufaa.

Kwa ujumla vyombo vyote vilivyoorodheshwahusimamiwa moja kwa moja na Dola na huwajibika kwadola. Vipo baadhi ya vyombo ambavyo sio mali ya Dolalakini hutumiwa na dola katika kutekeleza shughuli zakekama vile vyombo vya Kijasusi na vyombo vya Itikadi.

Vyombo vya KijasusiKatika mataifa makubwa ya kisekula, mbali ya vitengo

vya ndani vya upelelezi huwepo pia mashirika ya kijasusiyanayofanya ujasusi nchi nyingine kwa manufaa yamataifa hayo. Mataifa hayo yana idara za usalama namashirika ya ujasusi.

Page 213: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

202

Nchi za Marekani na Israil ni maarufu katikashughuli hii ya ujasusi. Taifa la Marekani, kwa mfano,mbali ya shirika lake la ndani la upelelezi FBI (FederalBureau Investigation) pia ina mashirika mengine kama CIA(Central Intelligence Agency), NSA (National Security Agency)na DIA (Defence Intelligence Agency). Taifa la Israel linamashirika mawili makubwa ya kijasusi, shirika la Shin-Bet likijishughulisha na upelelezi wa ndani ya Israel nashirika Ia Mossad linajishughulisha na “nje” ya Israel.Uingereza ina vitengo vikuu viwili. Kitengo cha usalama(M15) ambacho hushirikiana na idara maalum ya polisiiliyo chini ya ofisi ya waziri Mkuu vikiwajibika na usalamawa ndani. Pia kuna shirika la kijasusi la secret Intelli-gence Service (SIS) au M16, hili liko chini ya wizara yamambo ya Nje. Secret Intelligence Service hufanyaujasusi nje ya Uingereza kulinda maslahi ya nchi hiyo.Ufaransa nayo ina shirika liitwalo Service Documenta-tion Exterieure Contre Espionage (SDECE). Na Ujerumaniina kitengo kama hicho kiitwacho Bundes NachristenDienst (BND).

Vyombo vya ItikadiKatika dola za kisekula pamoja na kuwepo vyombo vya

mabavu pia huwepo vyombo vya itikadi. Baadhi ya vyombohivi huweza “kusimamiwa moja kwa moja na dola, wakativingine huwa nje ya mamlaka hiyo.

Katika suala la itikadi chombo ambacho hupewaumuhimu wa “pekee” ni elimu. Elimu hutolewa ama nadola yenyewe au na taasisi zilizosajiliwa. Kazi moja yadola ni kutoa au kusimamia utoaji na uendeshaji wa elimuna maarifa. Huunda, kutengeneza au kujenga itikadi nakuifanya iwe rasmi. Hulazimisha itikadi hiyo ikubalikena kufuatwa na watu wote. Japo itikadi hiyo hupingwa najamii nzima, lakini ukweli ni kwamba itikadi inayotawalana kuongoza dola siku zote ni itikadi ya tabaka linalotawala

Page 214: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

203

Itikadi hii hutumika kutawala matabaka yanayotawaliwakatika kipindi cha “amani na utulivu”. Mara nyingi utiina unyenyekevu wa raia huwa ni wa woga kutokana navitisho na mabavu ya watawala kwamba wotewanaokwenda, wanaoongea na wanaotenda kinyume chaitikadi rasmi hushughulikiwa na vyombo vya dola

Vyombo vya itikadi ni pamoja na shule na vyuo, dini,vyama vya siasa, miungano ya namna mbali mbali navyombo vya habari. Pamoja na mengine vyombo vyote hivihuelimisha watu kuhusu itikadi, sera au dira ya tabakalinalotawala huwashawishi watu waikubali na kuifuata.Hujitahidi kuihalalisha kuwa ni sahihi na nzuri kulikoitikadi nyingine. Tabaka linalotawala huandaa mitaalaambayo katika ufundishaji hutumika kwenye Mashule;Vyuo, Vyuo Vikuu na Taasisi za elimu, mkazo mkubwaukiwa kuifikisha itikadi ya watawala kwa wananchi, tanguwakiwa na umri mdogo kabisa hadi wanapokuwa watuwazima wenye uwezo wa kufahamu, kufikiri, kuchambua,kutathmini, kulinganisha, kuchanganua na kufikia, aukutoa “uamuzi huria”. Shule na vyuo huwalea watu waumri mbali mbali na kutoa daraja mbali mbali zaWataalamu na wanafikara ambao hutazamiwa watendekulingana na matakwa ya Watawala.

Katika mfumo wa kisekula (hasa wa kijahilia) Dini nataasisi zake kama makanisa, misikiti, shule na vyuo mbalina kueneza “imani ya dini”, pia hutumika kueneza itikadiya tabaka linalotawala hufundisha waumini wao kutii dola,kufuata itikadi yake na kuwa waaminifu kwa kiongozianayetawala

Dosari za Dola za KitwaghutiHistoria inatuonesha kuwa pamoja na umuhimu wa

uongozi au serikali katika jamii, si kila serikali iliyowezakuwashikamanisha wanaadamu pamoja na kuwaelekezakatika lengo la maisha yao. Dola yoyote iliyowekwa na

Page 215: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

204

kuendeshwa kwa kufuata matashi ya binaadamu imekuwaikiwafarakanisha binaadamu na kuwagawa katikamatabaka mbali mbali.

Matabaka ya waungwana na watwana, matajiri namaskini, wenye nguvu na wanyonge, wageni na wazawa,watawala na watawaliwa, na kadhalika. Katika kipindicha historia ya mwanaadamu, watu wa matabaka ya juudaima wamekuwa wakiwanyonya na kuwakandamiza watuwa matabaka ya chini kwa kutumia hila mbali mbali.

2. Muundo wa Dola ya Kiislamu na Uendeshaji wakeKwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, mwanaadamu

analazimika kuishi maisha ya kijamii ambayo humtakaahusiane na kushirikiana na watu wengine ili awezekufikia lengo la kuumbwa kwake na kuletwa hapa duniani.Ili wanaadamu waweze kushirikiana na kuliendea lengola maisha yao kwa pamoja hapana budi kuwa na serikaliau uongozi madhubuti.

Adam (a.s) alipokuwa peponi (bustanini) pamoja namkewe, alikuwa kiongozi. Aliposhushwa hapa dunianialiongoza familia yake (kizazi chake) kwa mwongozo utokaokwa Allah (s.w) kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:

Tukasema: “Shukeni humo nyote; na kama ukikufikieniuwongozi utokao kwangu, basi watakaofuata uwongoziwangu huo haitakuwa khofu juu yao walahawatahuzunika.(2:38)

Page 216: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

205

Lakini wenye kukufuru na kuyakadhibisha manenoyetu, hao ndio watakaokuwa watu wa Motoni, humowatakaa milele.” (2:39)

Katika sehemu hii tutaangalia dhana ya utawala katikaUislamu na muundo wa Dola ya Kiislamu na uendeshajiwake.

Dhana ya Utawala katika UislamuWataalamu wa siasa (Political scientists) wanautazama

utawala kama “uwezo wa juu kabisa wa kuamuru,kuongoza na kudhibiti vyote vilivyo ndani ya mipaka yaDola usio wajibika kwa yeyote yule ndani ya mipaka hiyo.”Kwa mtazamo huo mtu au kikundi cha watu (chama,taasisi, n.k.) kinaposhika utawala, basi neno au tamko lamtu huyo au kikundi hicho huwa ni amri au sheria yakutiiwa bila hiari.

Kwa hiyo, kwa namna dhana ya utawala ilivyo, hakunamwanaadamu mwenye sifa, uwezo na haki ya kushikanafasi ya utawala” Ni kwa msingi huu Qur-an imetoamsisitizo na maelezo yaliyo wazi kabisa kuwa utawala nihaki na milki ya Allah (s.w) pekee kwa sababu yeye:

Haulizwi (Mwenyezi Mungu) anayoyafanya (kwani yoteni ya haki) lakini wao (viumbe) wataulizwa. (21:23)

Page 217: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

206

Sema: “Ni nani mkononi Mwake umo ufalme wa kila kitu,Naye, ndiye, alindaye, na hakilindwi (chochote)kinyume Naye, kama mnajua (jambo nambieni hili).”(23:88)

Yeye, Allah (s.w), peke yake ndiye Muumba wa vyotena ndiye mtawala halisi wa ulimwengu na vyote vilivyomo.Si haki ya kiuumbe yeyote yule awaye kuamrisha, kutiiwaau kuongoza kinyume na Allah (s.w).

Vyombo vya Dola ya KiislamuSerikali ndiyo taasisikuu katika dola ya Kiislamu, nayo

imegawanywa katika sehemu kuu tatu: Yaani Bunge(Shuura), Urasimu (mamlaka ya utendaji) na Mahakama.

Kazi za Bunge la KiislamuBunge la Kiislamu, tofauti na mabunge ya mifumo

mingine, ni chombo cha Mshawara na ufafanuzi wamasuala mbali mbali ya dola. Bunge la Kiislamu si chombocha kutunga sheria kinyume na zile zilizomo ndani yaQur’an na Sunnah:

“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwamwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume Wake

Page 218: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

207

wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Namwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake,hakika amepotea upotofu (upotevu) ulio wazi (kabisa) “.(33:36).

“Hakika tuliteremsha Taurati yenye uwongozi na nuru;ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha (kwa MwenyeziMungu) waliwahukumu Mayahudi: na watawa namaulamaa pia (walihukumu kwa hiyo Taurati), kwasababu walitakiwa kuhifadhi Kitabu (hicho) chaMwenyezi Mungu; nao walikuwa mashahidi juu yake.Basi (nyinyi Waislamu) msiwaogope watu, bali niogopeni(mimi). Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamanichache (ya duniani). Na wasiohukumu kwa yalealiyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.”(5:44).

Pamoja na hivyo, Bunge la Kiislamu hufanya kazi zifuatazo:

(i) Pale ambapo Qur’an na Sunnah zimewekamaelezo na hukumu wazi, bunge la Kiislamu halinauwezo wa kufanya vinginevyo bali kuyaweka

Page 219: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

208

maelezo hayo kulingana na mazingira, kutoa tafsirina ufafanuzi wa kina na kuweka kanuni namaelekezo yatakayohimiza utekelezaji wa hukumuhizo.

(ii) Pale ambapo Qur’ an na Sunnah zina maelezoyenye tafsiri zaidi ya moja, wajibu wa bunge ndaniya dola ya Kiislamu ni kuchagua moja ya tafsirihizo na kuiidhinisha kutumika kijamii kama rejeailiyokubalika.

(iii) Pale ambapo hukumu (Qur’an na Sunna) hazikowazi, kazi ya bunge ni kujadili na kupitisha fat-waya kufuatwa na jamii. Msingi utakaozingatiwa katikamajadiliano, ni ule usemao kuwa jambo lolote lileambalo halikuharamishwa basi ni halali.

(iv) Kutoa Fat’wa kuhusiana na hali za dharurazinazojitokeza kisiasa, kiuchumi n.k.

Kazi za Warasimu (Ulul-Amri)Wenye mamlaka (Ulul-Amri) katika dola ya Kiislamu

ni wasimamizi wa utekelezaji wa maamrisho na makatazoya Allah (s.w.), kazi yao kubwa ni kuiandaa jamiikuyapokea, kuyakubali, kuyatii na kuyatekelezamaamrisho hayo katika maisha ya kila siku.

Utaratibu huu wa Urasimu wa dola ya Kiislamuunatofautiana na ule wa dola za kitwaghutii ambaohuwafanya Warasimu kuwa waheshimiwa na watawala.Amri ya Allah juu utii kwa viongozi ni:

Page 220: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

209

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtumena wenye mamlaka juu yenu, walio katika nyie(Waislamu wenzenu). Na kama mkikhitalifiana juu yajambo lo lote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu naMtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na sikuya mwisho. Kufanya hivyo ni bora kwenu na kunamatokeo mazuri(4:59).

Utii kwa wenye mamlaka ndani ya dola ya Kiislamuhutanguliza sharti la wao kwanza (Ulul-Amri) kuwa watiifukwa Allah (s.w.) na Mtume wake. Kinyume na hivyo,Qur’an ina maelekezo yafuatayo:

“Wala msitii amri za wale maasi, (wenye kupindukiamipaka ya Mungu). “ Ambao wanafanya uharibifu tukatika ardhi wala hawaitengenezi. “ (26:151-152)

Kazi za MahakamaWajibu wa Mahakama katika dola ya Kiislamu ni

kufafanua, kusimamia na kuhakikisha hukumu na sheriaza Allah zinatekelezwa ili kulinda haki; kuzuia maovu,

Page 221: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

210

ufisadi na dhulma katika jamii:

Na tumekuteremshia Kitabu kwa (ajili yakubainisha) haki, kinachosadikisha vitabuvilivyokuwa kabla yake, na kuvihukumia (kamahaya ndiyo yaliyoharibiwa au ndiyoyaliyoasalimika). Basi wahukumu baina yaokwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu,wala usifuate matamanio yao kwa kuacha hakiiliyokufikia. Na kila (umma) katika nyinyi(binadamu) tumeujaalia sheria yake na njia yake.Na kama Mwenyezi Mungu angalitakaangekufanyeni kundi moja (Ia kufuata sheriamoja), lakini anataka kukujaribuni kwa hayoaliyokupeni. Basi shindaneni kuyafikilia mamboya kheri. Nyinyi nyote marudio yenu ni kwaMwenyezi Mungu; naye atakwambieni (yote) yale

Page 222: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

211

mliyokuwa mkikhitilafiana.(5:48)

Na wahukumu baina yao kwa yale aliyokuteremshiaMwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao...(5:49)

Je, wao wanataka hukumu za Kitwaghuti? Na nani aliyemwema zaidi katika hukumu kuliko Mwenyezi Mungu;(yanafahamika haya) kwa watu wenye yakini.” (5:50).

Kuhukumu kinyume na hukumu za Allah (s.w.) nikuleta dhulma katika jamii. Ni kwa msingi huu Allah(s.w.) anatuasa:

“... Na wasio hukumu kwa yale aliyoyateremshaMwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu”. (5:45).

Uraia katika Dola ya KiislamuDola ya Kiislamu ina raia wa aina mbili ndani ya

mipaka yake:(1) Waislamu (2) Dhimmi. Qur’an inafahamishaifuatavyo:

Page 223: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

212

Hakika wale walioamini na wakahama na wakapiganiadini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao; (Naoni wale Muhajiri -Waislamu wa Makka). Na walewaliowapa (Muhajiri) mahala pa kukaa (Nao ni Ansari)na wakainusuru (dini ya Mungu); hao ndio marafiki, waokwa wao (katika kurithiana na mengineyo). Na walewalioamini, lakini hawakuhama, ninyi hamna haki yakurithiana nao (wala ya mengineyo) hata kidogo mpakawahame katika nchi ya kikafiri waje wakae nchi moja nanyinyi). Lakini wakiomba msaada kwenu katika dini,basi ni juu yenu kuwasaidia, isipokuwa juu ya watuambao kuna mapatano baina yenu na wao, (hapomsiwasaidie wao mkapigana na waitifaki wenu. Lakinijitahidini kupatanisha). Na Mwenyezi Mungu anayaona(yote) mnayoyatenda. (8: 72).

Kutokana na aya hii, sifa za kustahiki uraia ndani yaDola ya Kiislamu ni Uislamu na asili au uzawa ndani yamipaka ya Dola Kiislamu. Muislamu yoyote yule hata kamani mhamiaji ni raia anaetambulika na kukubalika na Dolabila ya kujali rangi, taifa au lugha yake. Dola ya Kiislamuinawatambua Waislamu wote kama ni raia zake na wotehao ni ndugu:

Page 224: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

213

Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu; basi patanishenibaina ya ndugu zenu, na Mcheni Mwenyezi Mungu(msipuuze jambo la kupatanisha) ili mrehemewe. “(49:10).

Kuhusiana na wale ambao si Waislamu lakini niwazawa ndani ya mipaka ya Dola ya Kiislamu, uraia waoutatambuliwa iwapo watakubali kutii maamrisho ya Dola.Raia hawa watiifu kwa Dola katika sheria ya Kiislamuhuitwa dhimmi na hustahiki hupata haki zote kama raia.

Msonge wa Uongozi katika Dola ya KiislamuMsonge wa uongozi katika Dola ya Kiislamu

umebainishwa wazi katika Qur’an na kufasiriwa vyemana Mtume Muhammad (s.a.w) katika Dola ya Kiislamualiyoiunda. Hebu turejee aya zifuatazo:

Page 225: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

214

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtiini Mtumena wenye mamlaka juu yenu walio katika’ nyie. Na kamamkikhitilafiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwaMwenyezi Mungu na Mtume; ikiwa mnamuaminiMwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hiyo ndiyo kherina ina matokeo bora kabisa.(4:59)

Katika aya hii tunajifunza kuwa aliye juu naanayestahiki kupewa utii wa kwanza au anayestahikikupwekeshwa kwa utii ni Allah (s.w.), kisha hufuatiaMtume wake ndipo hufuatia viongozi wa jamii (Warasimu)wa ngazi mbalimbali. Viongozi hawa wa jamii, kwa mujibuwa aya hii, watastahiki kutiiwa tu pindi watakapokuwa niWaislamu wanaoongoza kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah.

Msonge wa uongozi katika UislamuMsonge wa uongozi katika jamii yoyote ya Kiislamu.

Msonge wa uongozi katika jamiiyoyote ya Kiislamu.

1. Allah (s.w.) Qur’an)

2. Mtume (s.a.w.) (Sunnah)

3. Majlis Shura (Bunge)

4. Viongozi wa Jamii wa ngazi zote(Msonge wa uongozi utatiririkakuanzia Taifani hadi kwenye familia

5. Raia (wenye mchanganyiko waWaislamu na wasiokuwa Waislamu)

Msonge wa uongozi katika Dolaya Kiislamu wakati wa Mtume.

1. Allah (s.w.)

2. Mtume Muhammad (s.a.w.)

3. Shura (Sekretariati ya Mtume)

4. Viongozi wa Mikoa na viongoziwengine katika ngazi na nyanja mbalimbali.

5.Raia (wenye mchanganyiko waMayahudi, Wakristo na W ashirikina)

Page 226: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

215

Kwa nini Utii uelekezwe kwanza kwa Allah (s.w.)?Allah (s.w.) anastahiki kupewa nafasi ya kwanza na ya

juu ya Utii wa mwanaadamu kwa sababu yeye ndiyeMuumba na Mmiliki pekee wa mbingu na ardhi na vyotevilivyomo - vidogo na vikubwa na vinavyoonekana navisivyoonekana. Yeye ndiye Mfalme wa kweli mwenyeuwezo juu ya kila kitu asiyehitajia msaidizi au mshirikayeyote katika kuuendesha ufalme wake. Ufafanuzi waufalme wake tunaupata katika Qur’an. Hebu tuzingatieaya zifuatazo:

Hakika Mola wenu ni Allah aliyeziumba mbingu na ardhikwa nyakati sita. Kisha akatawalia juu ya arshi Yake.Huufunika usiku kwa mchana ufuatiao upesi upesi; (nahuufunika mchana kwa usiku ufuatiao upesi upesi). Naameliumba jua, mwezi na nyota (Na vyote) vimetiishwakwa amri Yake. Fahamuni! Kuumba (ni kwa Allah) naamri zote ni zake. Ametukuka kweli kweli Allah, Mfalme(Rabbi) wa walimwengu wote. (7:54)

Page 227: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

216

(Mwenyezi Mungu) ambaye ni wake (pekee) ufalme wambingu na ardhi, wala hakuzaa mtoto wala hana mshirikakatika ufalme (wake) na ameumba kila kitu naakakikadiria kipimo (chake)(25:2).

Allah (s.w.) amekiumba kila kitu kwa lengo naakakiwekea utaratibu (sheria madhubuti utakaokiwezeshakuwepo, kubakia na kufikia lengo lake. Hivyo ili kituchochote kibakie hakina hiari ya kutii sheria za Allah(s.w.) alizokiwekea. Hizi ni sheria za maumbile (naturallaws) ambazo hata miili yetu inazitii bila hiari. Allah (s.w)anatutanabahisha:

Je! wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, nahali kila kilichomo mbinguni na ardhini kinamtii yeyekipende kisipende? Na kwake watarejeshwa wote.(3:83)

Aya hii inamtanabahisha mwanaadamu kuwa pamojana kwamba amepewa uhuru na uwezo wa kujiamuliautaratibu wa maisha na kujiwekea sharia zitakazomuongoza katika kuendesha maisha yake ya kijamii,kwanini asitumie uhuru huo kwa busara kwa kuamuakufuata utaratibu au sheria za kuendesha maisha yakijamii alizoziweka Allah (s.w.) ambazo zinalandana nasheria za maumbile zinazofuatwa na kila kilichomombinguni na ardhini pamoja na mwili wake wenyewe Je,mwanaadamu atakapo amua kutii utaratibu wa maishakinyume na ule aliomuwekea Muumba wake; Maisha yaupinzani yatamfikisha wapi kama si katika matatizo yakijamii ya kila namna na maangamivu? Mwanaadamu

Page 228: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

217

mwenye akili na busara ni yule anayemtii Muumba wakeipasavyo kwa kuitikia wito wake ufuatao:

Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawa sawa -ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu,(yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana bara bara naumbo la binaadamu). Hakuna mabadiliko katikamaumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndiyodini ilivyo haki, lakini watu wengi hawajui. (30:30)

Kwa nini Mtume (s.a.w) achukue nafasi ya pili ya utii?Ilivyo ni kwamba, Allah (s.w.) katika utaratibu wake

wenye hikima, hawasiliani na kila mwanaadamu baliamewateua wajumbe wake miongoni mwa wanaadamukufikisha ujumbe wake kwa wanaadamu wote nakuwafundisha kwa matendo namna ya kuutekelezaujumbe huo katika kuendesha maisha yao ya kila sikukwa mtu binafsi na kwa jamii kwa ujumla.

Wajumbe hawa ni Mitume ambao walifunuliwa na Al-lah (s.w.) namna ya kuiongoza jamii katika njiaanayoiridhia. Ambayo ndiyo pekee inayomfikishamwanaadamu katika lengo la kuumbwa kwake kwa furahana amani. Mitume wa Allah (s.w.) wamethibitishwa kwawalimwengu na mwenyewe Allah (s.w) kwakuwaambatanisha na dalili mbalimbali na piaamewateremshia vitabu kutoka kwake ambavyo nimwongozo kamili wa maisha ya mwanaadamu na ni vyenyekutoa hukumu baina ya watu kwa uadilifu.

Page 229: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

218

Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili waziwazi na tukaviteremsha vitabu na uadilifu pamoja nao, iliwatu wasimamie uadilifu(57:25)

Mitume wa Allah (s.w.) ni tofauti na viongozi wakawaida ambao huongoza kwa kutumia fikra na jitihadaza kibinaadamu ambazo mara zote huathiriwa na udhaifumwingi alionao. Mwanaadamu wa kawaida anaathiriwasana na mazingira yake, matashi yake na ufinyu wa elimuyake. Kutokana na udhaifu huu si lazima kilaatakaloamua, liwe sahihi na lenye manufaa kwa jamii.Lakini Mitume hawaongozi kwa fikra na matashi yao, balihuongoza kwa ufunuo (Wahyi) kutoka kwa Allah (s.w.)ambaye ni mjuzi wa kila kitu mwenye habari ya mamboyote. Allah (s.w.) anatuthibitishia hili katika Qur’an:

Naapa kwa nyota zinapoanguka kwamba mtu wenu(huyu Nabii Muhammad) hakupotea wala hakukosa, walahasemi kwa matamanio (ya nafsi Yake). Hayakuwa hayaanayosema ila ni Wahyi (ufunuo) uliofunuliwa (kwake).Amemfundisha (Malaika) mwenye nguvu sana. (53:1-5).

Page 230: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

219

Hivyo mwanaadamu hawezi kufuata njia ya uongofuanayoiridhia Allah (s.w.) ambayo ndiyo pekee yenyekumuwezesha kupata furaha na amani katika maisha yakehapa ulimwenguni pasina na kumtii Mtume wa Allah (s.w.). Qur’ an inatubainishia:

Mwenye kumtii Mtume amemtii Allah…”. (4:80)

Sema (ewe Muhammad): ikiwa nyinyi mnampendaMwenyezi Mungu basi nifuateni (hapo) Mwenyezi Munguatakupendeni na atakughufirieni dhambi zenu. NaMwenyezi Mungu ni mwenye maghfira mwenye rehema.

Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume (wake). Nakama mkikengeuka (Mwenyezi Mungu atakutieni adabu).Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi Makafiri. (3:31-32)

Masharti ya kuwatii viongozi (Ulul-amri)Viongozi au wenye mamlaka (Ulul-amr) waliokusudiwa

katika Qur’an (4:59) ni viongozi wa aina zote na wa ngazizote katika fani zote za jamii ambao huielekeza nakuiongoza jamii kwenye kuliendea lengo la maisha. Qur’anhaituamrishi kumtii kila kiongozi au kila mwenyemamlaka juu yetu kwa sababu si kila kiongozi anawaongozavyema walio chini yake na kuwaelekeza kwenye kufikia

Page 231: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

220

lengo la maisha yao. Kuna viongozi wengine wanawatoawatu wao kwenye maisha ya furaha na amani nakuwatumbukiza kwenye maisha ya matatizo na huzuni.Viongozi tunaoamrishwa na Allah (s.w.) kuwa tuwatii niwale tu Waislamu ambao ni wacha Mungu wanaoongozakwa mujibu wa Qur’an na Sunnah. Viongozi hawatulioamrishwa kuwatii hawako juu ya sheria bali nao wakosawa na wale wanaowaongoza. Wako tayari kukosolewana kurejeshwa kwenye Qur’an na Sunnah endapowatateleza kidogo katika kufanyakazi yao. Viongozi wanamna hii ndio pekee tunaoamrishwa tuwatii kwani ndiopekee wanaotuongoza katika njia iliyonyooka:

Mwenyezi Mungu ni mlinzi (kiongozi) wa wale walioaminiHuwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru (2:257)

Kinyume chake, Waislamu tumeamrishwa tusiwatiiviongozi wanaoongoza kwa miongozo mingine kinyume naQur’an na Sunnah. Inasisitizwa katika Qur’an:

Na usiwatii makafiri na wanafiki wala usijali udhia wao,na mtegemee Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Munguanatosha kuwa mlinzi. (33:48)

Page 232: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

221

“… Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zaowakafuata matamanio yao, na mambo yao yakawayamepita mipaka (yaani makafiri). (18:28)

Tukiwatii viongozi hawa kinyume na mwongozo wa Al-lah (s.w.) tutakuwa tumewafanya miungu yetu nakuangukia kwenye shirk. Tumekatazwa kuwatii hawa kwasababu watatuelekeza kwenye maovu na kuacha maadilimema ili tu wakidhi matashi ya nafsi zao.

Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na(yale) ambayo huna elimu nayo, usiwatii lakini kaa naokwa wema hapa duniani. Shika njia ya wale wanaoelekeakwangu kisha marejeo yenu ni kwangu, haponitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda. (31: 15)

Pia Mtume (s.a.w.) ametukataza kuwatii viongoziwanaotuelekeza kwenye uovu kama tunavyojifunza katikaHadith zifuatazo:

Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a. w.) amesema:Muislamu analazimika kumsikiliza na kumtii kiongozikwa lolote lile atakalomuamrisha, likiwa linampendezaau linamchukiza alimradi hamuamrishi kufanya kitendokiovu. Atakapo amrishwa kufanya kitendo kiovu, hakunakumsikiliza wala kumtii” (Bukhari na Muslim) Ali (r.a)ameeleza kuwa Mtume (s.a. w.) amesema:Hapana utiikwenye uovu (dhambi). Hakika utii ni wa matendo mazuritu” (Bukhari na Muslim)

Page 233: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

222

Tukiwatii viongozi hawa watatutoa kwenye maisha yanuru, wema na uadilifu na kutuingiza kwenye maisha yagiza la uovu na utapeli ambayo daima huidumaza nakuihilikisha jamii. Allah (s.w.) anatutanabahisha kwakusema:

“ Na waliokufuru walinzi (viongozi) wao ni Matwaghuti(wachupaji mipaka ya Allah). Huwatoa katika nuru nakuwaingiza katika giza. Hao ndio watu wa motoni, humowatakaa milele. “ (2:257)

Matwaghuti ni wachupaji mipaka ya Allah (s.w.). Walewote wanaoiongoza jamii kwa miongozo inayochupa mipakaya Allah (s.w.) au inayopingana na Qur’an na Sunnah.Pia Allah (s.w.) anawatanabahisha Waislamu juu yaviongozi hawa walio kataa mwongozo wake:

Page 234: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

223

“ Wala (Makafiri) hawataacha kupigana nanyi mpakawakutoeni katika dini yenu kama wakiweza. Nawatakaotoka katika dini yao katika nyinyi, kisha wakafahali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zaozimeharibika katika dunia na Akhera. Na ndio watu waMotoni; humo watakaa milele” (2:217)

Ni haramu kwa Waislamu wa kweli kweli kumtii yeyotekinyume na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kumtiiyeyote kinyume na Allah (s.w.) ni kumfanya huyounayemtii kuwa Mungu wako kama tunavyofahamishwakatika Qur’an:

Wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwani Miungu badala ya Mwenyezi Mungu (9:31)

Katika aya hii Mayahudi na Wakristo wanashutumiwakuwa waliwafanya viongozi wao Miungu badala ya Allah(s.w.). Mtume (s.a.w.) katika kufafanua aya hiianatufahamisha kuwa Mayahudi na Wakristohawashutumiwi hivyo kwa kuwaita au kuitakidi kuwaviongozi wao ni Miungu, bali walishutumiwa hivyo kwakuwa walikuwa wakiwatii kinyume na maamrisho namakatazo ya Allah (s.w.)

Sifa za anayestahiki kuwa kiongoziKiongozi wa Kiislamu hachaguliwi kwa kuomba kura

na kuwahonga wapiga kura kama wachaguliwavyo viongoziwa Kitwaghutii. Mtume (s.a.w.) amekataza asichaguliwekuwa kiongozi yule anayeomba uongozi:

Abdul-Rahman bin Samurah (r.a) amesimulia kuwaMtume wa Allah amesema: “Usiombe uongozi kwasababu utakapopewa uongozi kwa kuomba utaachiwa

Page 235: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

224

peke yako jukumu la uongozi, na kama umepewa bila yakuomba, utasaidiwa katika uongozi huo” (Bukhari naMuslim)

Yeye mwenyewe Mtume (s.aw.) alikataakuwachagua wale walioomba uongozi miongoni mwamasahaba zake kama tunavyojifunza katika Hadithifuatayo:

Abu Mussa ameeleza: “Tulikwenda kwa Mtume (s.a.w.),mimi pamoja na binamu zangu. Mmoja wao akasema: “EeMtume wa Mwenyezi Mungu! Nifanye niwe gavana wanchi ambamo Allah (s.w.) amekupa mamlaka juu yake.Na yule mwingine naye akamuomba hivyo hivyo.Akasema Mtume wa Allah, “Hatumchagui kwenyeuongozi huu yeyote anayeomba wala hachaguliwi yulealiye mroho wa uongozi. “

Katika riwaya nyingine alisema Mtume: “Hatuwachaguikwenye nafasi zetu za uongozi wale wanaotaka uongozi”(Bukhari na Muslim)

Muislamu wa kweli anafahamu vyema kuwa uongozini amana nzito na mtihani mkubwa. Hawezi kamwekuomba uongozi, sembuse kuufanyia kampeni nakuununua kwa hongo! Mtume (s.a.w.) anathibitisha hivyokatika Hadith ifuatayo:

Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:“Utawaona watu hawapendi kabisa kazi ya uongozimpaka uchaguzi utakapo waangukia (kwakubebeshwa)”. (Bukhari na Muslim)

Katika jamii ya Kiislamu atachaguliwa kuwa kiongozimtu mwenye sifa zifuatazo:

Kwanza, awe Muislamu Mcha-Mungu. Hii ni tabiaanayotakiwa asifike nayo kila Muislamu wa kweli. Mcha-

Page 236: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

225

Mungu ni yule anayeishi kwa kuchunga mipaka ya Allah(s.w.) kwa kujitahidi kwa jitihada zake zote kufuatamaamrisho yote ya Allah (s.w.) na kuacha makatazo Yakeyote. Anafanya hivyo kwa sababu anahofia adhabu kali yaAllah (s.w.) isiyo na kifani endapo atatenda kinyume namaamrisho Yake na pia ana matarajio ya kupata radhi yaAllah (s.w.) na malipo makubwa yasiyo na kifani endapoataishi maisha ya kutii maamrisho Yake yote. KiongoziMcha-Mungu kwa vyovyote vile atakuwa muadilifu katikakazi yake.

Pili, awe mjuzi wa Qur’an na Sunnah na mwenye ujuzina uzoefu wa kazi anayotakiwa aifanye katika eneo lakela uongozi. Ujuzi wa kutosha wa Qur’an na Hadith nimuhimu sana kwani ndio mwongozo anaotarajiwakuutumia katika uongozi wake.

Ujuzi wa kazi ya uongozi ni muhimu pia kwani pamojana ucha-Mungu wa mtu na ujuzi wa Qur’an na Hadith,hataweza kuongoza vizuri iwapo hana ujuzi na uzoefu wauongozi. Umuhimu wa sifa ya elimu kuwa nayo kiongoziumebainishwa katika Qur’an, Taluti alipochaguliwa kuwaMfalme wa Mayahudi:

Page 237: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

226

Na huyo Mtume wao akawaambia: “Mwenyezi Munguamekuchagulieni Taluti kuwa Mfalme:. Wakasema: “Vipiatakuwa na ufalme juu yetu, nahali sisi tumestahiki zaidikupata ‘ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wamali?” Akasema: “Mwenyezi Mungu amemchagua juuyenu na amemzidishia wasaa wa elimu na kiwiliwili. NaMwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye. NaMwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, Mjuzi”. (2:247)

Tunajifunza kuwa utajiri au nasaba ya mtu siyo vituvya msingi vya kuangaliwa katika kumchagua kiongozi balivitu vya msingi vinavyoangaliwa ni uchaji wa mtu na elimuYake.

Tatu, ambayo pia imetajwa katika aya hii ni Sihanzuri na uwezo wa kimwili: Mtu mcha-Mungu, mwenyeelimu mwenye siha nzuri na mwili wenye nguvuanastahiki zaidi kuchaguliwa kuwa kiongozi kuliko mtudhaifu.

Nne, ya mtu anayestahiki kuchaguliwa kuwa kiongoziwa Waislamu ni tabia njema. Mtu mwenye tabia njema niyule anayejitahidi kwa kadri ya uwezo wake kujipambana vipengele vyote vya tabia njema. Kwa mtazamomwingine mtu mwenye tabia njema ni yule anayejitahidikuiga mwenendo wa Mtume (s.a.w.) kama inavyosisitizwakatika Qur’an:

Bila shaka mnao mfano mwema (ruwaza nzuri) kwaMtume wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuogopaMwenyezi Mungu na siku ya Mwisho na kumtajaMwenyezi Mungu sana (33:21)

Page 238: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

227

Na mwenendo wa Mtume ulikuwa ni kufuata Qur’anvilivyo. Allah (s.w.) anamsifu Mtume wake kwa tabia njemaaliyokuwa nayo:

Na bila shaka una Tabia njema kabisa (68:4)

Pia Mtume (s.a.w.) amesisitiza ubora wa mtu mwenyetabia njema kwa kusema:

“Mbora wenu ni yule aliye mbora kwenu kwa tabianjema” (Bukhari na Muslim)

Hivyo, mwenye tabia njema kuliko wengine ndiyeatakayestahiki kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Waislamu.

Hizi ndizo sifa anazotakiwa awe nazo kiongozi waKiislamu. Yeyote katika jamii ya Kiislamu atakayekuwana sifa hizi anastahiki kuwa kiongozi wa watu bila ya kujalinasaba yake, taifa lake, rangi yake, umaarufu wake auwasaa wake wa kimali. Aliowachagua Mtume (s.a.w.)kushika nyadhifa mbalimbali katika uongozi wa serikaliya Kiislamu walikuwa Waislamu wenye tabia njema kwelikweli. Katika uchaguzi wake hakujali nasaba, taifa aurangi. Kwa mfano, alimchagua Bilal (r.a) aliyekuwaMhabeshi kuwa Muadhini bila ya kujali manung’uniko yabaadhi ya masahaba wake. Pia alichaguliwa Zaid bin Harithambaye hakuwa na umaarufu wowote miongoni mwaMasahaba wake kuwa Kamanda wa jeshi pamoja namanung ‘uniko yaliyojitokeza mbele ya Mtume (s.a.w.).

lkitokea watu wenye sifa hizi za uongozi ni wengi kulikonafasi za uongozi, wale walio mstari wa mbele na uzoefuwa muda mrefu katika harakati za kuupigania Uislamuwatachaguliwa kwanza. Endapo bado watakuwa wengikuliko nafasi zilizopo, watachaguliwa wale wenye umrimkubwa zaidi. Endapo bado watakuwa wengi kuliko

Page 239: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

228

mahitaji, itapigwa kura na Waislamu wote, wake kwawaume, na watakaopata kura nyingi zaidi ndiowatakaostahiki kuwa viongozi wa jamii.

Mfano mzuri wa kuigwa ni ule wa kuchaguliwa kwaAbu Bakr (r.a.) kuwa Khalifa wa kwanza wa MtumeMuhammad (s.a.w.). Baada ya maafikiano kati ya Answarna Muhajirina kuwa kutokana na uzoefu wa kazi yakusimamisha dini ya Allah (s.w.), Muhajiriina ndiowachukue nafasi ya Ukhalifa, Abu Bakr alimpendekezaUmar (r.a) au Abu-Ubaidah (r.a.) achaguliwe kuwa Khalifa.Lakini wote wawili walikataa pendekezo hilo na kusema

“Hapana, hatuwezi kukutangulia mbele katikajambo hili. Bila shaka wewe ni mbora kulikoMuhajiriina wote (kwa kila kitu). Ulikuwa na Mtumekatika pango, Mtume alikuchagua kuongoza swalakwa niaba yake alipokuwa mgonjwa, na swala ndiyonguzo kubwa ya dini. Ni nani mwingine anayestahikikuchukua nafasi hii ya Ukhalifa kuliko wewe?Nyoosha mkono wako tukupe “Bai’at”.

Baada ya kiongozi wa Kiislamu kuchaguliwa kwakufuata utaratibu huu Waislamu hulazimika kutoa ahadiya utii - Bai’at”. Ahadi hii inafungamana na kiongozi; balipia ni ahadi kwa Allah (s.w.) kama inavyobainika katikaQur’an:

Page 240: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

229

Bila shaka wale waliofungamana nawe, kwa hakikawamefungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono waMwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Bali avunjayeahadi amevunja kwa kuidhuru nafsi yake, atekelezayealiyomuahidi Mwenyezi Mungu; (Mwenyezi Mungu)atamlipa ujira mkubwa. (48:10).

Amri ya kuwatii viongozi ipo wazi katika Qur’an (4:59).Pia msisitizo wa kuwatii viongozi unapatikana katikaHadithi ifuatayo:

Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allahamesema: “Atakayenitii amemtii Allah na atakayeniasiamemuasi Allah; na atakayemtii kiongozi amenitii naatakayemuasi kiongozi ameniasi “ (Bukhari na Muslim)

Kumpinga kiongozi aliyechaguliwa na watu kwa halalini katika uasi mkubwa. Yeyote yule anayempinga(anayempiga vita) kiongozi wa halali anayewaongoza watukatika njia ya usawa, anauchu wa madaraka na anatakakuvuruga amani, utulivu na mshikamano wa jamii. Mtuwa namna hii anastahiki kuuawa kwa mujibu wa Hadithzifautazo:

Urfajah ameeleza kuwa amesikia Mtume (s.a. w.)akasema: “Hivi karibuni patakuwa na upinzani na uasi.Anayetaka kuwagawanya watu walioungana muuenipopote pale alipo “(Muslim)

Abu Said (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a. w.)amesema: Ahadi ya utii itakapotolewa kwa Makhalifawawili kwa wakati mmoja, muueni wa pili” (Muslim)

Hadith zinaonesha uovu wa kupinga uongozi halaliunaoendesha mambo kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah.Waislamu hawawajibiki kuwatii na wanaamrishwakutowatii viongozi wanao waongoza kwenye mambo maovu.

Page 241: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

230

Katika Khutuba yake ya kwanza baada ya kuchaguliwakuwa Khalifa wa kwanza wa Mtume (s.a.w.) Abu Bakar(r.a) alisema: “Bila shaka nimechaguliwa kuwa Amir(kiongozi) wenu pamoja na kwamba mimi si mbora kulikonyinyi. Nisaidieni nikiwa katika njia ya usawa nanikosoeni nikikosea” Waislamu walifanya hivyo.Hawakumchelea kiongozi yeyote aliyechupa mipaka yauongozi wa Qur’an na Sunnah Waislamu wamekatazwakuwachagua wanawake na watoto kuchukua nafasi yauongozi wa juu katika jamii kama tunavyojifunza katikaHadith ifuatayo:

Abu Bakar (r.a) ameleeza: Mtume (s.a.w.) alipopata habarikuwa Waajemi wamemfanya binti Mfalme kuwa kiongoziwao alisema (Mtume): Hawatafanikiwa kamwewanaomchagua mwanamke kuwa kiongozi wao “(Baihaq, Ahamad)

Uongozi ni jukumu kubwa ambalo watoto na wanawakehawana uwezo wa kulibeba. Historia inashuhudia matatizoyaliyotokea katika jamii mbalimbali zilizotawaliwa nawanawake na watoto. Bila shaka hekima ya watotokukataliwa kupewa uongozi wa jamii iko wazi kwamba akilizao hazijakomaa kiasi cha kuweza kubeba dhima kubwaya uongozi. Wanawake nao kulingana na umbile lao nadhima kubwa waliyo nayo ya uzazi na malezi ya familia,itakuwa ni kuwaonea kwa kuwapachika tena hii dhimaya uongozi wajamii. Hata hivyo wanawake wanawajibikakuwa viongozi wa jumuiya na idara za wanawake na katikakuongoza shughuli zote za huduma zitolewazo kwawanawake tu.

Wajibu wa kiongozi katika dola ya KiislamuMtume (s.a.w.) ametukumbusha sote kuwa kila mtu

ajue kuwa ni kiongozi anayewajibika juu ya waleanaowaongoza na hapana shaka ya kuwepo maulizo ya

Page 242: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

231

Allah (s.w.) juu ya uwajibikaji wake juu ya waleanaowaongoza kwa mujibu wa Hadith ifuatayo.

Abdullah bin Umar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Al-lah amesema: “Kila mmoja ni mchunga (kiongozi) na kilammoja ataulizwa juu ya wale aliowaongoza.imam(kiongozi wa jamii) ni mchunga wa watuanaowaongoza na ataulizwa juu yao. Mwanamume nikiongozi wa familia yake na ataulizwa juu ya watu wafamilia yake. Mwanamke ni malkia wa nyumba ya mumewake na watoto na ataulizwa juu yao. Mtumishi nimchunga wa vitu vya mwajiri wake na ataulizwa juu yavitu hivyo. Sikilizeni! Hakika kila mmoja ni mchunga(kiongozi) na ataulizwa juu ya wale aliowachunga(aliowaongoza)” (Bukhari na Muslim)

Katika Hadith hii tunajifunza kuwa kila mtu ni kiongozina kila kiongozi anao wajibu kwa wale anaowaongoza.Katika kipengele hiki tumejaribu kubainisha wajibu waviongozi wa Kiislamu kama ifuatavyo:

1. Ucha-MunguKiongozi ajitahidi kujikurubisha kwa Allah (s.w.) zaidi

kwa kuzidisha swala za (Sunnah), funga za Sunnah, kutoasadaqa kwa wingi, kuomba dua na maghfira kwa wingi ilikupata msaada wa Allah (s.w.). Kwani kazi ya uongozi ninzito mno inayohitajia sana msaada wa Allah (s.w.). Piakiongozi wa jamii ya Kiislamu anawajibika kuzidishakusoma Qur’an na Hadith ili aweze kufanya kazi yakekwa kuchunga mipaka ya Qur’an na Sunnah na pia awezekujipamba na mwenendo mwema uliosisitizwa katikaQur’an na Hadith. Kiongozi wa Kiislamu hana budikujitahidi kuwa kiigizo kwa ucha-Mungu kwa kutekelezamaamrisho yote ya Allah (s.w.) na kujiepusha na makatazoyake yote. Ucha-Mungu ni zana muhimu sanainayomwezesha kiongozi kutekeleza wajibu wake vilivyo.

Page 243: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

232

2. HurumaKiongozi awe mnyenyekevu, mpole, mwenye huruma

anaye wahurumia wale anaowaongoza na mwenyekuwapendelea lile analolipendelea katika nafsi yake.Kiongozi anatakiwa daima kuwa yeye ni mtumishi wa walewaliomuweka katika uongozi, awaheshimu kama mtumishianavyomuheshimu bwana wake. Wakati huo huo, kiongozianatakiwa ajiweke katika nafasi ya ulezi ambayo hanabudi kuwahurumia wale anaowalea. Kiongozi wa Kiislamudaima anatakiwa azingatie usia wa Allah (s.w.) ufuatao:

Naye ndiye aliyekujaalieni kuwa Makhalifa (viongozi)katika ardhi. Na amewanyanyua baadhi yenu juu yawengine daraja kubwa kubwa ili akufanyieni mtihanikwa hayo aliyokupeni. Hakika Mola wako ni mwepesiwa kuhisabu na hakika yeye ni mwingi wa kusamehe,mwingi wa kurehemu. (6:165)

Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa kiongozianatakiwa mara zote afahamu kuwa wadhifa wa uongozialia nao ni mtihani kwake. Allah (s.w.) amemuinua darajana kumfanya kiongozi juu ya wengine ili kumfanyiamtihani kuwa atashukuru neema hiyo aliyotunukiwa naMola wake kwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo nakuchunga mipaka ya Allah (s.w.) katika kazi hiyo auatakufuru ajipe uungu kwa kuchupa mipaka ya Allah nakuwageuza watumwa wake wale waliomchagua nakumfanya kiongozi wao. Kiongozi anatakiwa awe msaadana rehema kwa wale anaowaongoza na wala asiwe mzigo

Page 244: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

233

na tatizo kwa raia zake hao. Mtume (s.a.w.) kilaalipowachagua sahaba zake kuwa viongozi wa mahalambalimbali daima alikuwa akiwausia kuwa watu wamsaada wenye huruma na upole kwa raia zao.

3. UadilifuKiongozi wa Kiislamu anatakiwa awe muadilifu. Kipimo

cha kiongozi mzuri ni uadilifu. Kiongozi wa Kiislamu akiwamuadilifu huwa Khalifa wa Allah (s. w.) na akiwa simuadilifu huwa Khalifa wa Shetani. Uadilifu unasisitizwamno katika Qur’ an kamatunavyojifunza katika ayaifuatayo:

Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamia uadilifu,mtoao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ijapokuwani juu ya nafsi zenu, au wazazi wenu, au jamaa. Akiwatajiri au masikini. (4: 135)

Kiongozi muadilifu ni yule anayechunga haki za watuanaowaongoza. Yeye ni mchunga na mgawaji wa haki.Hana budi kuhakikisha kuwa yeye mwenyewe hachukuihaki zake mpaka ahakikishe kuwa kila mtu amepata hakiyake.

Mtume (s.a.w.) aliwaamuru wale aliowapa kazi kuwawasivae kivazi kizuri zaidi kuliko wale wanaowaongoza nawasifunge milango yao wakati watu wanawahitajia hakizao, au wanataka kutoa madukuduku yao.’

Page 245: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

234

Kiongozi wa Kiislamu anatakiwa awe muaminifu namkweli na asijilimbikizie mali kwa kutumia madaraka yakeya uongozi. Amir au kiongozi wa juu wa Serikali ya Kiislamuanatakiwa achukue mshahara au posho kutoka kwenyemfuko wa serikali (Baitul-mali) kiasi kile tukinachotosheleza mahitaji muhimu ya chakula, mavazina makazi kwa yeye mwenyewe na familia yake. Kiongoziwa Kiislamu anatakiwa akumbuke daima kuwa uongozikatika Uislamu si kitega uchumi kama ulivyo uongozi waKitwaghuti. Mtume Muhammad (s.a.w.) ambaye ndiyekiongozi wa Ummah huu wa mwisho na kiigizo chetu kwamwenendo na uongozi wake bora, aliishi maisha rahisi.

Abu Bakar (r.a) alichaguliwa kushika uongozi wa Ummawa Kiislamu mara baada ya kutawafu Mtume (s.a.w.),alifuata nyayo za Mtume (s.a.w.) kwa kila kitu. MaishaYake yalikuwa rahisi mno. Umar (r.a) aliyechaguliwa kuwakiongozi wa serikali ya Kiislamu baada ya Abu Bakaralifuata vyema nyayo za uongozi wa Mtume (s.a.w.) na ulewa Abu Bakar. Pamoja na kuwa Umar alikuwa kiongoziwa Dola kubwa ya Kiislamu iliyoenea mashariki ya katiyote na kupanuka hadi Spain, aliishi maisha rahisi sana.

Umar (r.a) alikuwa na kawaida ya kuzunguka usiku ilikujua matatizo ya watu wake. Siku moja katika mizungukoyake alimkuta mama mmoja porini na watoto wake wanalia.Umar (r.a) alipomuuliza kwanini wako pale alimjibu kuwagiza la usiku na baridi kali imewafanya walazimike kulalapale. Alipomuuliza kwanini watoto wanalia, alimjibu kuwawananjaa. Umar (r.a) aliondoka mbio mpaka kwenye ghalaya Baitul-mali na kuchukua mgongoni mwake gunia la ungawa ngano na mafuta ya kupikia mpaka kwa yule mama.Umar (r.a) alisaidiana naye kupika na baada ya chakulakuiva aliwaamsha watoto na kuwalisha ndipo akarejeanyumbani kwake. Matukio ya aina hii yako mengi katikahistoria ya ukhalifa wa Umar bin Khattab (r.a).

Page 246: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

235

Kinyume chake viongozi wa Kitwaghuti, huchukuamadaraka ya uongozl wanayopewa na jamii zao kamakitega uchumi chao kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi.Huifuja watakavyo na humpa yeyote wamtakaye kwaupendeleo mali ya jamii ambayo imepatikana kwakukung’uta mifuko ya masikini. Muda mfupi baada yakiongozi wa Kitwaghuti kukabidhiwa madaraka ya uongoziwa ngazi ya juu katika jamii, utamuona ana gari zuri jipya,ana nyumba nzuri mpya, na mabadiliko ya kila namnakatika matumizi yake ya kimaisha pamoja na familia yake.

Kama mambo yenyewe ni haya, kwa nini watu wenginekatika jamii ya Kitwaghutii wasiupupie uongozi kwa halina mali au kwa kufa na kupona? Kwa nini mtu aliyeonjauongozi katika serikali ya Kitwaghuti asing’ang’aniekubakia humo kwa gharama yoyote ile?

Kwa nini mapinduzi ya mara kwa mara na mauajiyasitegemewe katika jamii za Kitwaghuti ambapo watuwanashindania uongozi kwa lengo la kujinufaisha waobinafsi? Haya yote ni matunda machungu yanayotarajiwakatika jamii kutokana na uongozi uliokosa uadilifu.

Kiongozi muadilifu hana budi kuhakikisha kuwawanyonge katika jamii wanapata haki zao na wenye maliwanatoa haki za wanyonge. Abu Bakar, katika khutubayake ya kwanza baada ya kuchaguliwa kuwa Khalifa wakwanza wa Mtume (s.a.w.) alisisitiza:

“Mnyonge miongoni mwenu ni mwenye nguvu katikauongozi wangu mpaka apate haki zake; na mwenyenguvu miongoni mwenu atakuwa dhaifu katika uongoziwangu, mpaka akipenda Allah nichukue haki za watuanazodaiwa... “

Page 247: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

236

Vile vile ni katika uadilifu kwa kiongozi kuhakikishakuwa kila mtu mkosaji anahukumiwa kwa mujibu washeria bila ya upendeleo au uonevu wowote. Kiongozihatamchelea yeyote katika kupitisha hukumu. KatikaUislamu watu wote ni sawa mbele ya sheria na hakunaaliye juu ya sheria hata akiwa Amir (Rais) wa nchi.

4. SubiraKiongozi katika dola ya Kiislamu anatakiwa awe

mwenye subira, mvumilivu na mstahimilivu. Kiongoziatekeleze wajibu wake ipasavyo na asitarajiwe kupendwana kufurahiwa na watu wote. Waumini wa kweli tu ndiowatakaomfurahia na kumsaidia atakapowaongoza kwamujibu wa Qur’an na Sunnah. Lakini wanafiki, wenyehusda, wapenda vyeo na sifa na maadui wote wa Uislamuhawawezi kamwe kumfurahia kiongozi wa Kiislamu.

Kiongozi wa Kiislamu hana budi kukumbuka kuwaanafanya kazi ile ile ya Mtume (s.a.w.). Arejee historiaajikumbushe maudhi na vitimbi vya kila namnaalivyofanyiwa Mtume wa Allah na makafiri wa Makkah naMayahudi na wanafiki wa Madina. Kisha katika uongoziwake anapokumbana na matatizo ya kutukanwa,kusingiziwa, kuupuzwa n.k. ajiulize: “Je haya yaliyonifikiayanaweza kulinganishwa na yale yaliyomfikia Mtume waAllah”.

Pia kiongozi wa Kiislamu anayejitahidi kutekelezawajibu wake kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah, hana budikukumbuka kuwa malipo ya kazi yake yapo kwa Allah (s.w.)na ndiye pekee anayewajibika kumuogopa na kutaka radhiyake.

Vyombo vya dola katika UislamuMalengo ya vyombo vya dola (State machineries) katika

dola ya Kiislamu yanatofautiana na yale ya serikali za

Page 248: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

237

Kitwaghutii. Vyombo kama usalama, polisi, mahakama,magereza n.k., vipo katika dola zote tofauti ni malengo yakazi na majina. Katika dola ya Kiislamu, jeshi la polisikwa mfano, kazi yake ni kuamrisha mema na kukatazamaovu na vile vile kuwakamata wale wote wanaofanyauhalifu:

Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri nawanaoamrisha mema na wakakataza maovu. Hao ndiowatakaotengenekewa “ (3:104)

Magereza hali kadhalika, kazi zake si kuwaadhibu tuwahalifu bali kurekebisha tabia na mienendo yao iliwanapotoka magerezani wawe raia wema na wajute kwamakosa yao ya awali.

Kinyume na Uislamu, vyombo vya dola za Kitwaghutiimalengo yake ni kama tulivyokwishaona huko nyuma, nimabavu na kulinda maslahi ya walio madarakani.Huwaonea raia badala ya kuwasaidia, aidha badala yakekurekebisha mienendo ya wakosefu huwafanya wazamezaidi katika uhalifu, bali vyombo hivyo hufanyaukandamizaji na dhulma kwa raia. Hivyo vyombo vya dolaya Kiislamu malengo yake ni tofauti kabisa na yale yaserikali za Kitwaghuuti.

Demokrasia katika Dola ya KiislamuPamoja na kuwepo uhuru kamili wa kuchagua viongozi

kushiriki katika maamuzi ya kisiasa, kushiriki katika

Page 249: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

238

kuamrisha mema na kukataza maovu ili kuhakikishakuwepo kwa amani na utulivu, dola ya Kiislamu si yakidemokrasia kwa mtazamo wa kitwaghuti. Maana yaserikali ya kidemokrasia kwa mtazamo wa kitwaghutii ni“Serikali ya watu inayoongozwa na watu kwa manufaa yawatu.”

Hivyo, watu kwa mtazamo wa kitwaghuti, ndio wenyekauli au mamlaka ya mwisho. Katika Uislamu mamlakayote ni ya Allah (s.w) pekee. Viongozi na watu wotewanatakiwa wajisalimishe chini ya sheria na amri za Al-lah (s.w). Katika dola ya Kiislamu hapana sera ya “wengiwape” hata kama ni kinyume na haki.

Katika Uislamu “haki” itabakia haki hata kamaimefuatwa na mtu mmoja au watu wachache (minority)na “dhuluma” au “batili” itabakia kuwa hivyo hata kamaimesimamiwa au imeungwa mkono na watu wengi (ma-jority).

Page 250: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

239

Tafauti ya Serikali ya Kiislamu na ile ya kidemokrasia

Serikali ya Kiislamu1. Watu wote wako chini yaUfalme au utawala wa Al-lah (s.w.) na kila mtu amekusudiwa awe Khalifa, wa Al-lah (s.w.) katikakusimamisha ufalme wakehapa ulimwenguni.

2. Itikadi na sheria zinatokakwa Allah (s.w.) kupitia kwaMitume wake. KilaMuislamu anawajibika kutiisheria za Allah na kutiimaelekezo ya Mtume.Hakuna aliye juu ya sheriawote wanahukumiwa sawa.

3.Dola ya Kiislamu iko kwamadhumuni yakusimamisha ufalme wa Al-lah na kutafuta radhi yake.

4. Kwa ujumla Dola yaKiislamu iko chini yamamlaka ya Allah (s.w.) naMtume wake, na huendeshamambo yake kwa kuchungabarabara mipaka ya Allah(s.w.) na Mtume wake.

Serikali ya kidemokrasia1. Ufalme au utawala ukochini ya watu walio wengi(popular sovereignty).

2. Itikadi, sheria na serahutungwa na Wananchi auwawakilishi wao katikabunge au kamati za vyama.Na kiongozi wa juu wa nchi(Rais) amepewa madarakamakubwa ya kuwa juu yasheria.

3. Madhumuni ya serikali nikutosheleza mahitaji namatashi ya raia “waliowengi”.

4. Dola ya kidemokrasia inamamlaka ya mwisho nauhuru wa kuendeshamambo bila ya kuwa nayeyote aliye juu yake.

Page 251: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

240

Serikali ya Kiislamu ni ya Ki-khalifaUmma wote wa Kislamu unashika nafasi ya ukhalifa

wa Allah (s.w). Yaani umma wote wa Kiislamuunamwakilisha Allah (s.w) katika kusimamisha ufalmewake hapa ulimwenguni kama tunavyojifunza katika ayaifuatayo:

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongonimwenu na kufanya vitendo vizuri, kuwa Atawafanyamakhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifawale waliokuwako kabla yao, na kwa yakiniAtawasimamishia dini yao aliyowapendelea, naatawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawewananiabudu, hawanishirikishi na chochote. Nawatakaokufuru baada ya hayo; basi hao ndio wavunjaoamri zenu. (24:55)

Hivyo, kila mmoja anayo haki na anayo mamlaka yakuiongoza jamii chini ya ufalme wa Allah (s.w). Kiongoziwa nchi, japo amechaguliwa na watu hana mamlaka yakujiamulia mwenyewe mambo ya jamii. Bali uamuzi wamwisho utapitishwa na Majlis Shura (Bunge) yenyewajumbe waliochaguliwa na watu kutokana na watuwacha-Mungu, ili wawakilishe mawazo yao kwa niaba yao.

Page 252: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

241

Kushauriana katika kuongoza jamii kunasisitizwa katikaQur-an kuwa ni miongoni mwa matendo mema ya jamiiyatakayo iwezesha kufaulu:

Na wale waliomuitikia Mola wao (kwa kila amri zake) nawakasimamisha swala na wanashauriana katika mamboyao na wanatoa katika yale tuliyowaruzuku. (42:38).

Pia Mtume (s.a.w) (na kwa hiyo viongozi wote)anaamrishwa na Mola wake:

“… Na ushauriane nao katika mambo. Na ufungapo niamtegemee Mwenyezi Mungu (kisha ufanye hilo uliloazimia bila kurudia nyuma). Hakika Mwenyezi Munguanawapenda wamtegemeao.” (3:159)

Baada ya Waislamu kuamua jambo katika Shura yao,ambalo liko katika mipaka ya Allah (s.w) na Mtume wake,hawana budi kutegemeza mafanikio yake kwa Allah (s.w)na kuanza kulitekeleza kwa umoja pasi na kurudi nyuma.Kiogozi wa Dola na viongozi wengine walio chini yake, kaziyao itakuwa kusimamia utekelezaji, wao wenyewe wakiwamfano bora, katika kutekeleza yale yaliyoamuliwa na MajlisShura. Endapo kiongozi atafanya kinyume na maamuzi yaShura, Umma unayo haki ya kumkatalia. Tujikumbushe tenamaneno ya Abu bakar (r.a) katika khutuba yake ya kwanzabaada ya kuchaguliwa kuwa Amir wa Waislamu:

Page 253: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

242

“Bila shaka mmeshanichagua kuwa Amir wenujapokuwa mimi si mbora kuliko nyinyi. Nisaidieni nikiwakatika njia ya sawa na nikosoeni nitakapokuwa ninakwenda vibaya”.

Katika Dola ya kikhalifa viongozi na wanaoongozwa wotewana nafasi sawa ya ukhalifa. Hivyo wananchi pamoja nakuwa na uhuru wa kutoa mawazo yao pia wana uhurukamili wa kuwakosoa viongozi wao na kudai haki zao kutokahata kwa Amir mkuu (Rais) wa nchi. Mfano mzuri wa uhuruwa kukosoa viongozi tumeupata katika uongozi wa Umarbin Khattab (r.a). Umar hakufurahishwa na tabia yawanawake iliyozuka ya kudai mahari kiasi kikubwa sana.Hivyo akaamua kuikomesha tabia hiyo. Akasimama katikamimbari msikitini na kuamuru kuwa kuanzia wakati ulemahari isivuke dirhamu 400. Na mwanamke atakaye daimahari yaliyozidi kiasi hicho, ziada yote itachukuliwa nakutiwa katika Baitul Maali (hazina ya dola ya Kiislamu).Papo hapo akasimama mwanamke mmoja akasema:

“Yaa Umar! Laisa laka ahalika”. Yaani “Ewe Umar!Huna mamlaka ya hilo”. Akamkumbusha aya ya Qur-an:

Na kama mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, (yaani:kumwoa mke mwingine na kumwacha wa zamani) nahali mmoja wao (naye ndiye huyo atayeachwa) mmempamrundi (tani) wa mali, basi msichukue chochote. Je,mtachukua kwa dhulma na kwa hatia iliyo wazi? (4:20)

Page 254: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

243

Aya hii inawakataza wanaume kudai mahariwanapowaacha wake zao hata kama waliwapa mali nyingi.Qintara Maana yake ni tani. Hivyo hata kama mtu ametoamahari tani za dhahabu. Yule mwanamke akamuulizaUmar: “Kwa msingi gani wewe unataka kuwanyang’anyawanawake haki waliyopewa na Allah (s.w)? Kwa kumjibu,Umar alisema kwa unyenyekevu: “Mwanamke yu sahihina Umar amekosea”. Na akaifuta kauli yake. Je, kunauhuru wa kukosoa viongozi uliopita huu?

Usimamishaji Haki katika Dola ya KiislamuLengo la dola ya Kiislamu sio kutawala bali ni kuhuisha,kudumisha na kuendeleza maadili mema ambayo Allah(s.w) amemtaka mwanaadamu ajipambe kwayo; na kuzuiana kukomesha maovu ambayo Allah (s.w) amemuamrishamwanaadamu ajitenge nayo. Yaani lengo la Dola yaKiislamu ni kuhuisha, kudumisha na kuendeleza maadilimema ambayo huwapelekea watu katika jamii kuishi kwafuraha na amani. Na papo hapo dola ya kiilsmau iko palekuzuia na kukomesha maovu ambayo huleta vurugu,mashaka na huzuni katika jamii. Furaha na amaniinapatikana katika jamii iwapo haki inasimamishwa naudhalimu unatokomezwa. Lengo hili linaelezwa vyemakatika aya ifuatayo:

Wale ambao tukiwamakinisha (tukiwapa madaraka)katika ardhi hisimamisha swala na wakatoa Zakat nawakaamrisha yaliyo mema na wakakataza yaliyomabaya, na marejeo ya mambo ni kwa Mwenyezi Mungu.(22:41).

Page 255: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

244

Uislamu ni Dini ya Haki na Serikali yake iko palekusimamisha haki kama tunavyojifunza katika Qur-an:

Yeye (Allah (s.w) ndiye aliyemtuma Mtume wake kwauongofu na kwa Dini ya Haki ili kuifanya ishinde dinizote ijapokuwa washirikina watachukia. (61:9)

Uislamu ni Dini ya Haki kwa kuwa ni utaratibu wa maishauliowekwa na Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mitume wake.Pia ni dini inayo simamia haki za binaadamu.Hawi Muislamuwa kweli yule asiyechunga haki za wengine, kuwausiawengine kusimamisha haki na kuwasaidia wengine kwahali na mali kupata haki zao. Katika Suratul Asr, Allah (s.w)anatuhakikishia kuwa wanaadamu wako hasarani katikamaisha ya duniani na akhera ila wale watakao muaminiAllah na vipengele vyote vya nguzo za imani na kufanyamatendo mema, na kusimamisha haki na kufanya subira ilikubakia katika haki. Kilicho iwezesha Dola ya Kiislamuwakati wa Mtume (s.a.w) na Makhalifa wane kuwa juu yadola zote za ulimwenguni ni msimamo wake wa kusimamishahaki katika jamii kwa hali na mali.

Waislamu hawakupigana vita vyovyote ili kuwaingiza kwanguvu watu katika Uislamu kama wanavyodai maadui waUislamu, bali walipigana na makabila na mataifa mbali mbaliili kutokomeza dhulma na unyonyaji wa kila ainaulioshamirishwa na watawala na kusimamisha haki kwakuwaondoa watawala wanyonyaji na kuwaweka viongozi waKiislamu waliokuwa watumwa wa Allah (s.w) pekee nawatumishi halisi wa watu walio waongoza. Kiongozi wa watukuwa na ulinzi mkali au “Body-Guard” ni jambo lisiloelekewakatika mtazamo wa uongozi wa Kiislamu.

Page 256: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

245

Katika dola ya Kiislamu haki za mwanaadamuzimezingatiwa kwa ukamilifu na hakuna mfano wakeunaopatikana katika dola yoyote ya kitwaghutii. Dola yaKiislamu imezigawanya haki za binaadamu katika mbeyatatu:

(a) Haki zinazomstahiki kila mwanaadamu.(b) Haki zinazowastahiki raia katika dola ya Kiislamu.(c) Haki zinazowastahiki wasio kuwa Waislamu katika

dola ya Kiislamu.

(a) Haki zinazomstahiki kila mwanaadamuNi jukumu la dola ya Kiislamu kusimamia na

kuhakikisha kuwa kila mwanaadamu awe Muislamu auasiwe Muislamu, awe raia au mgeni katika dola yaKiislamu, anapata haki zifuatazo:

(i)Haki ya KuishiKila mtu pasina ubaguzi wa aina yoyote ana haki ya

kuishi na kulindiwa maisha yake. Kumuua mtu yeyoteawaye ni kosa la jinai na muuaji ni lazima ahukumiwekwa sheria ya Kiislamu. Makemeo ya Qur-an kuhusukosa hili yanadhihirisha kwa uwazi ubaya wa kuua mtuyoyote pasi na haki:

Kwa sababu ya hayo tukawaandikia wana wa israil yakwamba atakayemuua mtu bila ya yeye kuua mtu, aubila ya kufanya fisadi katika nchi, basi ni kama amewauawatu wote…” (5:32)

Page 257: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

246

“… Wala msimuue mtu ambaye Mwenyezi Munguameharamisha (kuuwa) la ikiwa (imetokea) haki (yakuuawa)…” (6:151)

Hukumu ya muuaji ni kuuawa kama inavyobainishwakatika Qur-an:

Wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameiharamishakuuawa isipokuwa kwa haki (Akahukumu hakimu waKiislamu kuwa mtu amestahiki kuuawa na akatoa amri yakuuawa). Na mwenye kuuawa kwa kudulumiwa, basitumempa nguvu mrithi wake (juu ya muuaji huyo, akitakaataomba kwa hakimu kuwa amuue au akitaka amtoze fidiaau akitaka amsamehe). (17:33).

(ii) Haki ya Usalama wa MaishaKila mtu katika dola ya Kiislamu anayo haki ya kuokolewaau upate ulinzi utakao muweka katika hali ya usalamabila ubaguzi wa aina yoyote. Tunafahamishwa katika Qur-an kuwa:

“… Na mwenye kumwacha mtu hai (kumsaidia kuishi)ni kama amewaacha hai watu wote…” (5:32).

Page 258: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

247

Katika dola ya Kiislamu kila mtu awe mgeni au raiaana haki ya kupata mahitajio muhimu ya maishayatakayomuwezesha kuishi na kila mtu anayo haki yakupata hifadhi itakayomuhakikishia kuishi kwa usalama.

(iii) Kuheshimu Utoharifu (Utakaso) wa MwanamkeDola ya Kiislamu inalojukumu la kuhakikisha kuwa

kila mwanamke anapata hifadhi ya kutoguswa namwanamume yoyote awaye nje ya utaratibu wa ndoa.Kitendo cha zinaa au kishawishi chochote cha zinaakimekatazwa katika Uislamu bila ya kujali kuwakimefanywa na Muislamu au na asiye kuwa Muislamu aukimefanywa na raia au mgeni wa Dola ya Kiislamu.Makemeo ya Qur-an juu ya kitendo hiki ni haya yafuatayo:

Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo ni uchafu na ni njiambaya kabisa. (17:32).

Uzinifu katika Uislamu ni kosa la jinai, na mzinifuyeyote anastahiki adhabu kali ya kupigwa viboko mia moja(Qur-an, 24:2) au kupondwa mawe mpaka kufa bila yaubaguzi wa aina yoyote.

(iv) Haki ya HeshimaUislamu unatuamrisha kuwaheshimu wanaadamu nakuwathamini pasi na ubaguzi wowote na unatukatazakufanya jambo lolote litakalotupelekea kuwavunjiaheshima. Tunaamrishwa katika Qur-an kuwa:

....Wala msitukanane kwa kabila, wala msiitane majinamabaya...(49:11)

Page 259: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

248

Ni jukumu la dola ya Kiislamu kuhakikisha kuwa kilamtu anaheshimika bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

(v) Haki ya UhuruNi jukumu la dola ya Kiislamu kuhakikisha kuwa mtu

anakuwa huru na hawi mtumwa wa mwingine kimabavuau kifikra. Inasikitisha kuwa maadui wa Uislamu wanaunasibisha Uislamu na biashara ya watumwa.Wameunasibisha Uislamu na utumwa kwa kuwa etiwalioonekana kuhusika na biashara hiyo hapa Afrika yaMashariki ni waarabu. Wengi wa watu wasiokuwaWaislamu na hata baadhi ya Waislamu wasiojua vyemadini yao, wameuelewa Uislamu kuwa ni dini ya Waarabu.Hivyo kwa mtazamo wao huu, kila mwarabu ni Muislamuna kila alichokifanya Mwarabu kiwe kibaya au kizuri nikitendo cha Kiislamu. Mtazamo huu ni mtazamo potofu.Uislamu ni Dini ya Allah (s.w) isiyo na ubaguzi wa ainayoyote. Uislamu ni dini ya walimwengu wote wa nyakatizote na wamataifa yote. Wote walioikubali dini hii ni ndugu(Qur-an 49:10) na Uislamu hautambui ubaguzi wowotekatika mgawanyo wa haki za binaadamu.

Uislamu umekomesha utumwa wa fikra na mawazo,kwa kuwahimiza waumini wake wawe watumwa wa Allah(s.w) peke yake kwa kujinyenyekesha kwake kwa utii nakufuata vilivyo mwongozo wa maisha alio mfunuliamwanaadamu kupitia kwa Mitume wake.

Uislamu umekomesha utumwa uliokuwepo wakati waujahili kwa kuwahimiza Waislamu watumie mali zaokuwakomboa watumwa na katika Zakat limewekwa fungumaalumu la kuwagomboa watumwa. Katika historia yaUislamu tunajifunza kuwa Mtume Muhammad (s.a.w)mwenyewe aliwagomboa watumwa 63 na kuwaachia huru.Mkewe Bi Aysha (r.a) aligomboa watumwa 67, Abbas (r.a)aligomboa watumwa watumwa 70, Abdullah bin Umar (r.a)

Page 260: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

249

aligomboa watumwa 1000, Abdur-Rahman (r.a)aliwagomboa watumwa 30,000 na maswhaba wengine waMtume (s.a.w) waliwagomboa watumwa mamia kwamamia.

Mtume (s.a.w) amekemea vikali kitendo cha kumfanyamtu huru kuwa mtumwa wa mwingine kama tunayojifunzakatika Hadith ifuatayo:

Kuna watu wa aina tatu ambao mimi mwenyewenitasimama kuwashitaki katika siku ya hukumu;miongoni mwa hao ni yule anayemfanya mtu huru kuwamtumwa na kumuuza… (Bukhari, Ibn Majah).

(vi) Usalama na Uhuru wa Mtu binafsiUislamu umeweka utaratibu kwamba, hakuna mtu

atakayefungwa mpaka kwanza kosa lake lithibitishwembele ya mahakama ya wazi (yenye kushuhudiwa nawatu). Kesi za faragha au “IN CAMERA” ni haramu katikaUislamu. Pia ni haramu kumkamata mtu kwa kumshukutu na kumsukumiza jela bila ya kufuata utaratibu waMahakama na bila ya kumpa fursa ya kujitetea. Uadilifukatika kutoa hukumu, bila ubaguzi wa aina yoyote, nijambo lililosisitizwa mno katika Qur-an:

“… Na mnapohukumu baina ya watu hukumuni kwauadilifu…” (4:58)

Katika Dola ya Kiislamu hakuna mtu atakayetiwa ndanimipaka ahukumiwe kwa uadilifu, wala hapana yeyote asiyena hatia atakaye adhibiwa au kutiwa ndani kwa makosaya mwingine au kwa niaba ya mwingine.

Page 261: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

250

(vii) Haki ya Kuhukumiwa kwa UadilifuJukumu kubwa la Dola ya Kiislamu ni kusimamia uadilifu.Kila mtu bila ya kujali dini yake, rangi yake, taifa lake,uraia wake, n.k. anastahiki kuhukumiwa kwa uadilifu.Uadilifu katika kutoa hukumu unasisitizwa mno katikaUislamu kama tunavyojifunza katika Qur-an:

Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi (wa haki) kwa ajiliya Mwenyezi Mungu, muwe mkitoa shahada kwauadilifu. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeenikutowafanyia uadilifu…” (5:8).

Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu,mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwani juu ya nafsi zenu, au (juu ya) wazazi (wenu) na jamaa(zenu). Akiwa tajiri au maskini. Mwenyezi Munguanawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio mkaacha

Page 262: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

251

kufanya uadilifu. Na kama mkipotoa (ushahidi) aumkijitenga (na kushuhudia, Mwenyezi Munguatakuadhibuni), na Mwenyezi Mungu anazohabari za yalemnayoyatenda. (4:135).

(viii)Haki ya Usawa wa BinaadamuUislamu hauruhusu ubaguzi wa kabila, taifa, rangi,

hadhi, kipato, ubaguzi wa aina yoyote ile. Tunafahamishwakatika Qur-an:

Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule)mwanamume (mmoja – Adam) na (yule yule) mwanamke(mmoja Hawa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila(mbali mbali) ili mjuane (tu basi). Hakika aheshimiwayesana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yuleamchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini MwenyeziMungu ni Mjuzi Mwenye habari zote. (49:13)

Mtu hawi bora kwa kuwa ni tajiri, au kuwa na hadhikubwa katika jamii, au kwa kuwa anatokana na taifakubwa, bali aliye bora ziadi kuliko wote ni yule mcha-Mungu mwenye tabia njema na utu kwa wanaadamuwenziwe. Mtume (s.a.w) katika kusisitiza kwake usawawa binaadamu amesema:

Hapana Mwarabu aliye bora zaidi kuliko asiye Mwarabu,wala asiye Mwarabu si bora zaidi kuliko Mwarabu. Piamtu mweupe si bora kuliko mweusi, wala mtu mweusisi bora kuliko mweupe.Wote ni watoto wa Adam na adamameumbwa kutokana na udongo (wa mfinyanzi). (Baihaqina Bazzaaz).

Page 263: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

252

(ix) Haki ya uhuru wa mahusianoKatika dola ya Kiislamu kila mtu anayo haki ya kujiunga

na jumuia, chama au kikundi chochote katika kuhuishana kuendeleza mema kwa manufaa yake na manufaa yajamii kwa ujumla. Pia kila mmoja anayo haki ya kutojiungaau kujitoa kwenye jumuiya au chama au kikundi chochotepindi atakapoona kuwa chama hicho au jumuiya hiyohaina manufaa na wala hainufaishi umma bali huletafitina na uadui katika jamii. Mwongozo wa kushirikianana kushikamana umewekwa wazi katika Qur-an:

Saidianeni katika wema na ucha-Mungu walamsisaidiane katika Dhambi na uadui. Na McheniMwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wakuadhibu. (5:2).

(b) Haki za Raia Katika dola ya KiislamuPamoja na haki za binaadamu wote kwa ujumla

zinazotolewa na kusimamiwa na dola ya Kiislamu, kunazile haki zinazo wahusu raia tu wa Dola wakiwemoWaislamu na wasiokuwa Waislamu. Hapa tutarejea hakiza Msingi zifuatazo:

(i) Haki ya Kuendesha maisha ya BinafsiUislamu unatoa haki kwa kila raia kuwa asiingiliwe

katika maisha yake binafsi maadam haendi kinyume nautaratibu wa kibinaadamu. Tunaamrishwa katika Qur-an kuwa:

“… Wala msipeleleze (habari za watu)…” (49:12).

Page 264: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

253

Enyi mlioamini! Msiingie nyumba ambazo si nyumba zenumpaka muombe ruhusa (mpige hodi) na muwatolee Sa-laam waliomo humo.Hayo ni bora kwenu huendamtakumbuka(24:27)

Na kama hamtamkuta humo yoyote, basi msiingie mpakamruhusiwe. Na mkimbiwa “Rudini” basi rudini, hili nitakaso kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayotenda?(24:28).

Mtume (s.a.w) amekemea vikali kuchungulia nyumba zawatu kiasi cha kusema: Kama mtu atampofua macho aujicho mwenye kuchungulia nyumbani kwake, hatalaumiwawala hatakuwa na hatia”. Mtume (s.a.w) pia amekatazakusoma barua za watu.Hii ndiyo hifadhi ya maisha ya mtubinafsi inayotolewa na Uislamu. Hifadhi hii haipo katikadola za Kitwaaghuti. Ni mara ngapi twaona barua zikisomwana kuchukuliwa kopi (photocopy) kwa kisingizio cha usalamawa taifa? Vile vile katika dola za Kitwaaghuti, simu hutegwakatika nyumba za watu ili mazungumzo yao ya siriyajulikane. Kila dola ya kitwaghuti ina askari wa siri wengiambao kazi zao ni kupeleleza habari za watu.

Page 265: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

254

(ii) Haki ya Kupinga UdhalimuDola ya Kiislamu inatoa haki kwa raia wake kupinga,

kuonya au kukemea kitendo cha udhalimu kitakachofanywana dola au viongozi wake. Kila raia katika dola ya Kiislamuanayo haki ya kukosoa serikali au kiongozi wa juu waseriakli. Umar (r.a) akiwa Amir (Rais) wa dola kubwa yaKiislamu alikosolewa hadharani na mwanamke alipotakakuwadhulumu wanawake haki yao waliyopewa na Allah (s.w)ya kupanga kiasi cha mahari wanachokiridhia wao wenyewe.Pale pale mbele ya hadhara ya watu Umar (r.a) alikiri kuwaamekosa na akafuta amri yake.

(iii) Haki ya Uhuru wa Kutoa Maoni na KuamrishaMema

Uislamu unatoa uhuru kamili kwa kila raia kutoa maoniyake yanayopelekea kwenye wema. Bali maoni ya kupelekeakwenye maovu, vurugu, fitina na uhasama katika jamiihayapewi nafasi katika Uislamu. Vile vile matumizi ya lughambaya ya matusi, dharau na kejeli katika kutoa maoni sijambo linalokubalika katika Uislamu.

Pamoja na kuwa kutoa maoni au mapendekezo katikaserikali yanayopelekea kwenye wema ni haki ya kila raia,waumini wanawajibika kuamrisha mema na kukatazamaovu katika jamii kama tunavojifunza katika ayazifuatazo:

Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri nawanaoamrisha mema na kukataza maovu. Na hao ndiowatakaotengenekewa. (3:104).

Page 266: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

255

Na wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake nimarafiki wao kwa wao. Huyaamrisha yaliyo mema nahuyakataza yaliyo mabaya…. (9:71).

Kwa kulinganisha tabia hii ya waumini na ile yawanafiki Qur-an inatufahamisha:

Wanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wote ni halimoja, huamrisha yaliyo mabaya na huyakataza yaliyomazuri… (9:67).

Katika kusisitiza wajibu wa Waislamu katikakuamrisha mema na kukataza maovu Mtume (s.a.w)amesema:

“Miongoni mwenu atakayeona ovu hana budi kuliondoakwa mkono wake (kutumia nguvu) iwapo anauwezo,kama hana uwezo wa) kuliondoa kwa mkono wake hanabudi kuliondoa kwa ulimi wake (kulikemea); kama hanauwezo huo basi achukie na akilaani kitendo hicho kiovumoyoni mwake. Hali hii ya kuchukia ni kiwango chachini kabisa cha imani.” (Sahihi Muslim)

(iv) Haki ya Uhuru wa Kufuata Dini YoyoteDola ya Kiislamu inatoa uhuru kamili kwa raia wake

kutumia akili zao na vipaji vyao katika kuchagua dini

Page 267: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

256

wanayoiona kuwa ndiyo inayostahiki kufuatwa. Uislamuumekataza watu kushuruitishwa kuingia katika dini kamatunavyojifunza katika Qur-an:

Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini. Uongofuumekwisha pambanuka na upotofu. Basi anayemkufurutwaghuti na kumwamini Mwenyezi Mungu, bila shakayeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichovunjika…(2:256).

Waislamu hawaruhusiwi kutumia nguvu yoyote katikakuwaingiza watu katika dini bali wameariwa kuwalinganiawatu kwenye Dini ya Allah kwa mawaidha mazuriyanayofanana na vitendo vyao na kwa hekima kamatunavyojifunza katika Qur-an:

Wete (waite watu) katika njia ya Mola wako kwa hikimana mauidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyobora (siyo kwa kuwatukana wao au kutukana dini yao.Kwa njia hii huwezi kumvuta mtu) Hakika Mola wakondiye anayemjua aliyepotea katika njia yake. Naye ndiyeanayewajua walioongoka. (16:125)

Page 268: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

257

(v) Haki ya KuabuduPamoja na haki ya kufuata dini mtu anayoitaka,

Uislamu vile vile umetoa uhuru kamili kwa mtu kufanyaIbada ya dini yake apendavyo. Dola ya Kiislamu inajukumula kuhakikisha kuwa haki hii inapatikana kwa raia zakena inawajibu wa kuhakikisha kuwa Ibada na mahali pakuabudia panaheshimiwa. Tunaonywa katika Qur-ankuwa:

Wala msiwatukane wale wanaowaabudu kinyume chaMwenyezi Mungu, wasije wakamtukana MwenyeziMungu kwa jeuri zao bila kujua. Namna hivyotumewapambia kila watu vitendo vyao. Kisha marejeoyatakuwa kwa Mola wao. Naye atawambia (yote)waliyokuwa wakiyatenda. (6:108).Ifahamike wazi kuwa Uislamu haumkatazi mtu kuwa

na majadiliano juu ya mambo ya dini bali umesisitiza kuwamajadiliano hayo yaendeshwe kwa utaratibu mzuri bilaya kuwa na matukano, kuzozana na vurugu nyinginezo.Mabishano na mizozano imekatazwa katika Uislamu kamatuanvyokumbushwa katika aya ifuatayo:

Page 269: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

258

Wala msibishane na watu waliopewa Kitabu (kabla yenu)ila kwa yale (majadiliano) yaliyomazuri, isipokuwa walewaliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: “Tunaaminiyaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu, naMu ngu wetu na Mungu wenu ni mmoja, nasi ni wenyekunyenyekea kwake.” (29:46).

Amri hii haishii tu kwa watu wa Kitabu (wakristo naMayahudi) bali ni pamoja na wanaofuata dini nyinginezo.

(vi) Haki ya Kuwashitaki Viongozi wa Juu wa DolaKatika Dola ya Kiislamu, Wafanyakazi wote wa serikali,

akiwa kiongozi wa Dola au mfanyakazi wa kawaida, woteni sawa mbele ya Sheria. Hakuna yeyote aliye juu yasheria au asiyeguswa na sheria ya Dola. Raia yeyotekatika dola ya Kiislamu anayo haki ya kutoa madai yakeau mashitaka yake dhidi ya kiongozi yeyote, hata akiwaRais wa nchi. Tunao mfano mzuri wa kuiga kwa Mtumewa Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

Umar (r.a) amesema: Kwa macho yangu nilimuona Mtume(s.a.w) akijilipizia kisasi dhidi yake mwenyewe. Katikavita vya Badr wakati Mtume (s.a.w) alipokuwaakinyoosha mistari ya jeshi la Waislamu alilipiga tumbola askari mmoja, kwa bahati mbaya, katika kujaribukumrudisha nyuma katika mstari. Yule askariakalalamika: “Ewe Mtume! Umeniumiza na fimbo yako”.Mtume (s.a.w) pale pale alifunua wazi tumbo lake,akasema: “Samahani sana, unaweza kulipiza kisasi kwakunifanyia kitendo hicho hicho nilichokufanyia’. Yuleaskari alitoka mbele na kulibusu tumbo la Mtume (s.a.w)na kusema: “Hicho ndicho nilichokitaka”,

Mfano mwingine tunaupata katika uongozi wa Umar(la), khalifa wa pili wa Mtume (s.a.w). Wakati wa uongoziwa Umar, Muhammad mtoto wa Amr bin al-‘As, Gavana

Page 270: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

259

wa Misri alimchapa (kwa maonevu) Mmisri mmoja. YuleMmisri alifunga safari kwenda Madina kutoa malalamiko(mashtaka) yake kwa Khalifa Umar. Umar aliyapokeamashtaka na kumwita yule Gavana na mtoto wake waendeMadina. Walipofika Madina, Khalifa alimpa mjeledi yulemlalamikaji wa Kimisri na akamwambia amtandike yulemtoto wa Gavana mbele yake. Baada ya kulipiza kisasiyule Mmisri alipotaka kurudisha ule mjeledi, Umaralimuamuru “Mtandike Gavana naye kiboko kimoja, kwanimtoto wake asingali kupiga kama si kiburi alichokuwanacho kutokana na hadhi ya baba yake”. Mlalamikajialijibu: Mtu aliyenipiga nimelipiza kisasi changu kwake.Umar akasema: “Naapa kwa jina la Allah, kamaungalimtandika (‘Gavana) nisingalikuzuia kufanya hivyo,umeacha kwa hiari yako mwenyewe”. Kisha Khalifa waWaumini kwa hasira alimgeukia Gavana, na kumkemea.“Ewe Amr, umeanza lini kuwafanya watu watumwa, japowamezaliwa na mama zao wakiwa huru?”

(vii) Haki ya Kuiendesha Dola ya KiislamuWenye haki kushika hatamu ya uongozi wa dola ya

Kiislamu si watu wa cheo Fulani, au wa kabila Fulani, auwa chama fulani, bali ni wale wote wanaomuamini Allah(s.w) ipasavyo na wanaoamini Ukhalifa wa mwanaadamuhapa ulimwenguni. Uislamu unatufahamisha kuwamwanaadamu hapa ulimwenguni ni mwakilishi wa Allah(s.w), hivyo utawala wa Dola ya Kiislamu ni lazima ufuatekwa ukamilifu mwongozo wa Allah (s.w) na umshirikishekila Muislamu kwa njia ya uwakilishi na kushauriana.

(c) Haki za Wasiokuwa Waislamu katika Dola yaKiislamu

Pamoja na kuona haki zinazotolewa na dola ya Kislamukwa binaadamu wote na kwa raia zake – Waislamu nawasiokjuwa Waislamu kama ilivyobainishwa katika vipengele

Page 271: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

260

(a) na (b) tunawajibika kubainisha kwa uwazi zaidi haki zawasiokuwa Waislamu katika Dola ya Kiislamu.Kuwajibikakwetu huku kunafuatiwa na kueleweka vibaya madhumunina shabaha ya Dola ya Kiislamu kwa wasiokuwa Waislamuhasa wakristo, na hata kwa baadhi ya Waislamu wasioielewadini yao vilivyo. Kuna shutuma nyingi dhdidi ya Dola zaKiislamu zinazotolewa na maadui wa Uislamu, hasa wakristoambazo zinatoa picha kuwa Uislamu ni dini ya ukatili,inayoleta vurugu na fujo katika jamii. Hebu hapa tuangalie,kama mfano tu wa shutuma hizo, sehemu ya barua ndefuya Rev. Christopher Mtikila aliyomwandikia MakamuMwenyekiti, Halimashauri Kuu ya Chama, Dodoma (Tanza-nia) mnamo 1/2/1988. Katika kuonyesha ubaya wa UislamuRev. C. Mtikila amesema:

“Ubaya sana na hatari kubwa ya siasa ya Islamu kwa walewanaoifuata kwa kila herufi, ni kule kufika mahaliwanapoamua kwamba watu wote ambao si Waislamu (nahasa Wakristo) ni OUTLAWS au “State Criminals”, yaaniwahaini au viumbe wasiotakiwa kabisa na Mungu wao nahuwaita MAKAFIRI na kadiri wanavyoendelea, ndivyohekima ya kuwawezesha kuishi na kuchukuliana na jamiizingine alizoziumba Mungu inavyozidi kuwatoka. Asiyekubaliana na Islamu ya jinsi hiyo huwa sasa ni adui, naIslamu hiyo imeletesha mauaji ambayo wahusika kwakuharibikiwa akili zao eti kuyaita JIHAD pamoja na ukatiliwa kinyama ulionao katika SHERIA. Hushindwa kutambuakuwa Mungu wao wa mashindano, chuki, wivu, ugomvi,uadui, mauaji, unyama, uzushi, usharati, husuda n.k. niTOFAUTI KABISA na Mungu wetu wa ukweli, Upendo,furaha, Amani, Utu wema, Uvumilivu, Fadhili, Uaminifu,Upole na Kiasi! Inabidi ndugu zetu (viongozi Waislamu)mzinduke na kutambua kuwa mwapotea kwani: Islamuhiyo ni adui kabisa wa siasa yetu kwa vile humo kunaUbwana na Utwana, na hata wewe, ndugu MakamuMwenyekiti, unaitwa KAFIRI kwa vile u mweusi au wa asiliya Kiafrika na siyo ya Kiarabu!”

Page 272: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

261

Hizi ndizo fikra za Wakristo walio wengi juu ya dola yaKiislamu.Pamoja na sababu nyingine, fikra hizizimejitokeza kwa Wakristo na maadui wengi wa Uislamukutokana na sababu kubwa mbili zifuatazo:

Kwanza, kutoufahamu Uislamu na matundayanayoletwa na Uislamu katika jamii endapo misingi yaUislamu itafuatwa vilivyo.

Pili, husda na chuki iliyopandikizwa kwa Wakristo naviongozi wao ili wauchukie Uislamu ambao endapowataachwa huru kujifunza wataupenda na uwezekano wawengi kusilimu. Pia viongozi wa Makanisa wanaogopakuulizwa maswali na wafuasi wao ambayo wakiyajibuvilivyo watakuwa wanathibitisha kuwa Uislamu ni dini yahaki kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Ukristo ni diniiliyozuliwa tu na watu.

Hakuna muumini wa kweli wa Mungu wa hakiatakayeufahamu Uislamu vilivyo aache kuwa Muislamu.Kila Wakristo walipopata mwanya wa kuufahamu vizuriUkristo wao na Uislamu, wameamua kwa moyo mkunjufukusilimu na kuwa Waislamu wa kweli.

Kuhusu sababu hii ya pili ya kuuchukia Uislamu kwahusda, kwa kuwa Uislamu ni dini ya kweli yenye hojamadhubuti zinazompelekea kuielewa upesi kila mwenyekuitaka, na kwa kuwa Qur-an inabainisha kwa uwazi niwapi Wakristo na Mayahudi walipoacha njia ya uongofuna kupotea, hatuna msaada wowote wa kuwasaidia nduguzetu hawa kwani huo ni uamuzi wao wenyewe. Pia,hatustushwi na chuki zao kama zilivyojionyesha katikabarua ya Rev. C. Mtikila kwani hayo ndio mategemeo yetukwao kama Allah (s.w) anavyotutahadharisha katika Qur-an:

Page 273: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

262

Enyi mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu watuwasiokuwa katika nyinyi: “hao hawataachakukufanyieni ubaya. Wanayapenda yaleyanayokudhuruni. Bughudha (yao juu yenu)inadhihirika katika midomo yao. Na yanayofichwa navifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekubainishieni dalili(zote) ikiwa nyinyi ni watu wa kufahamu.(3:118)

Endapo fikra hizi mbaya dhidi ya Uislamu na dola yaKiislamu zimetokea kutokana na kutoufahamu Uislamuvilivyo, tunachukua fursa hii kuwaelimisha Wakristo nawengineo wasio Waislamu na hata Waislamu ambaohawajapata fursa ya kuifahamu dini yao vizuri, kuwaUislamu ni Dini ya Haki na dola ya Kiislamu lengo lakekuu ni kusimamisha Haki katika jamii kwa kuhakikishakuwa kila mtu anapata haki yake bila ya kujali dini yake.Ili kuhakikisha hili linafanyika, Uislamu umetoa msisitizomaalumu kuhusu haki za wasio kuwa Waislamu katikadola ya Kiislamu kama ifuatavyo:

(i) Haki ya Ulinzi wa maisha na MaliDamu ya Dhimmi ni takatifu kama ilivyo damu ya

Muislamu. Muislamu akimuua dhimmi adhabu yake nisawa na ile ya kumuua Muislamu. Muislamu mmoja

Page 274: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

263

alimuua dhimmi wakati wa Mtume (s.a.w). Mtume (s.a.w)alimuhukumu kuuawa akasema:

“Ni jukumu langu kusimamia haki za wanyonge”.

Wakati wa Ukhalifa wa Umar (r.a), Muislamu mmojaalimuua dhimmi. Khalifa aliamuru muuaji akamatweapelekwe kwa jamaa wa marehemu. Hili lilifanyika nawarithi wa marehemu walimuua.

Vile vile mali ya dhimmi katika dola ya Kiislamu nitakatifu kama ilivyo takatifu mali ya Muislamu. Muislamuakiiba mali ya Dhimmi atahukumiwa kukatwa mkonokama kawaida.

Khalifa wa nne wa Mtume (s.a.w) baada yakumuhukumu Muislamu mmoja kuuawa na warithi wadhimmi aliyemuua, alisisitiza:

Yeyote aliye Dhimmi wetu damu yake ni takatifu kamadamu yetu na mali yake ni takatifu kama mali yetu.

(ii)Dhimmi na sheria ya jinaiKatika dola ya Kiislamu hukumu za makosa ya jinai

(penal laws) zinawahusu madhimmi sawa nazinavyowahusu Waislamu. Makosa ya jinai ni makosayanayoathiri jamii nzima na mhalifu atakuwaanaidhulumu jamii nzima. Kwa hiyo dhimmi akiibaatakatwa kiganja chake cha mkono wa kulia, akiziniatatandikwa viboko 100 au kupigwa mawe mpaka kufaendapo amewahi kuoa au kuolewa.

Ila dhimmi hataadhibiwa kwa kosa la ulevi kamaatakavyoadhibiwa akilewa Muislamu kwa kutandikwaviboko 40.

Page 275: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

264

(iii) Dhimmi na Sheria za Madai (Civil Laws)Katika dola ya Kiislamu hukumu za madai ni sawa

kwa Waislamu na wasio kuwa Waislamu. Kila mwenyekudaiwa atahukumiwa na sheria kutoa haki ya mdai bilaya ubaguzi wa dini.

Pia yale yote yaliyoharamishwa kwa Waislamu katikauchumi, pia sheria inayakataza kwa madhimmi. Kwamfano riba na Kamari ni haramu kwa Waislamu naimekatazwa pia kwa wasiokuwa Waislamu kwani riba nakamari huiathiri jamii nzima.

Bali madhimmi wanaruhusiwa kulewa na kulanguruwe. Pia wana uhuru wa kutengeneza pombe nakufuga nguruwe katika maeneo yao ambamo hawaishiWaislamu. Hawaruhusiwi kufanya hivyo katika maeneoya Waislamu wala hawaruhusiwi kutengeneza na kuuzapombe, kufuga na na kuuza nguruwe katika sehemu zaumma zinazotumiwa na wote.

Muislamu akimuingilia dhimmi katika eneo lakeambapo anaruhusiwa na sheria kutengeneza pombe nakufuga nguruwe, kwa kuiharibu [pombe yake au kuwauanguruwe wake atawajibika kulipa vitu hivyo mbele yasheria ya Kiislamu.

(iv)Haki ya HeshimaKumvunjia heshima dhimmi kwa kumtukana, kumuita

jina baya, kumdharau, kumuadhiri, kumteta, n.k. nimakosa makubwa sana mbele ya Allah kama ilivyo makosamakubwa kumfanyia Muislamu.

Heshima ni haki inayomstahiki kila mwanaadamu pasina ubaguzi wa aina yoyote. Ni dhima ya Serikali yaKiislamu kulinda heshima ya kila mtu.

Page 276: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

265

(v) Sheria ya Mtu Binafsi (Personal Law)Katika serikali ya Kiislamu, mambo yote yanayohusu

imani ya mtu binafsi huhukumiwa kulingana na imani yadini yake. Kama jambo lililoharamishwa kwa Waislamusi haramu kulingana na imani ya dhimmi, serikaliitaendelea kumruhusu kulitenda jambo hilo. Kwa mfanokuoa bila ya kutoa mahari au kufunga ndoa wakati wakipindi cha eda ni haramu kwa Waislamu lakini kamakatika imani ya dini ya dhimmi haya hayakukatazwa, basimahakama ya Kiislamu haitamkataza dhimmi huyo kuoapasi na kutoa mahari au kuoa wakati wa eda. Kwa ufupi,katika yale mambo yanayohusu imani za dini nyingine naambayo hayaathiri jamii kwa ujumla, kama vile ndoa,talaka na mirathi, sheria ya Kiislamu imetoa haki yamadhimmi kuhukumiwa kulingana na imani za dini zao.

(vi) Haki ya Kuabudu na Kupewa Heshima Mahalipa Kuabudia

Katika dola ya Kiislamu, madhimmi wana uhuru kamiliwa kuabudu kulingana na dini yao inavyowataka. PiaWaislamu wameamrishwa kuheshimu dini za wengine –wasizitukane wala kuonyesha dharau ya aina yoyote –(Qur-an 6:108). Vile vile Waislamu wamekatazwakujiingiza katika mabishano yasiyo na msingi na watu wadini nyingine, (Qur-an 29:46).

(vii)Haki ya Kusamehewa Kushiriki JihadDhimmi katika serikali ya Kiislamu wamesamehewa

kupigana vita kwa sababu ulinzi wa serikali dhidi yamaadui zake ni jukumu la Waislamu tu. Inakuwa hivyokwa sababu ni wale tu wanaokubaliana na itikadi ya dolaya Kiislamu, ndio tu watakaoipigania dola kwa moyomkunjufu wa kufa na kupona.

Pia ni waumini tu wa Kiislamu watakaoweza kuchungakwa ukamilifu mipaka ya Uislamu iliyowekwa kuhusiana

Page 277: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

266

na vita vya jihadi. Dhimmi wanalazimika kutoa Jizya (kodimaalum) kama malipo ya ulinzi wanaopewa na Uislamu.Dola ya Kiislamu ikishindwa kutoa ulinzi kwa nchi yaDhimmi iliyojisalimisha kwa dola ya Kiislamu, nchi hiyoya Dhimmi haitalazimika kutoa Jizya.

(viii)Nafasi ya Dhimmi Katika Kuendeleza Dola yaKiislamu

Kwa kuwa serikali ya Kiislamu inaendeshwa kwamisingi ya itiqadi ya Dini ya Kiislamu, wenye kustahikikuongoza serikali ni wale tu wenye imani thabiti juu yaitikadi ya Kiislamu.Hawa pekee ndio watakaowezakuiongoza Dola kwa uadilifu mpaka kufikia lengo lake kuula kusimamisha haki na kuiwezesha jamii kuishi kwafuraha na amani.

Watu wenye itikadi nyingne wanayo haki kamili yakuchangia maendeleo ya serikali na wakipendawatashirikishwa katika sekta mbali mbali za kitaalamuna zisizokuwa za kitaalam lakini hawatapewa kazi yauongozi katika sekta yoyote au katika ngazi yoyote yauongozi wa dola.

Uongozi ni dhimma ya Waislamu kama tunavyojifunzakatika aya ifuatayo:

Page 278: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

267

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongonimwenu na kufanya vitendo vizuri, kuwa atawafanyamakhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifawale waliokuwako kabla yao, na kwa yakiniatawasimamishia dini yao Aliyowapendelea, naAtawabadilishia amani baada ya khofu yao… (24:55)

Waislamu wa vitendo wamepewa haki hii kwa sababundio pekee, kutokana na imani yao thabiti juu ya Allah(s.w) na malipo ya Akhera, watakaoweza kusimama kidetekutetea haki za watu na kuhakikisha kuwa jamiiinahuisha na kuendeleza mema na inaepukana na maovu.Waislamu hawapewi kazi hii ya uongozi kwa upendeleo,bali wamepewa kazi hii kwa kuwa wanao uwezo wakuifanya kama Allah (s.w) anavyowatukuza katika Qur-an:

Nyinyi ndio umma bora kuliko umma zotezilizodhihirishwa watu (ulimwenguni) – mnaamrishayaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, namnamwamini Mwenyezi Mungu. Na kama walewaliopewa kitabu wangaliamini ingalikuwa bora kwao…(3:110)

Waislamu wakiacha kuchukua dhima hii ya uongoziwa jamii na badala yake watu wengine wasiomwaminiAllah ipasavyo na malipo ya akhera, wakaichukua kazi

Page 279: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

268

hii ya uongozi wa jamii na kuifanya kwa kufuata matashiyao kinyume na matashi ya Mwenyezi Mungu, jamiiitatumbukia katika giza la huzuni na majuto kama ilivyohivi sasa katika ulimwengu huu wa Kitwaghuti kamatunavyojifunza katika Qur-an:

“Mwenyezi Mungu ni mlinzi (kiongozi) wa walewalioamini. Huwatoa katika giza na kuwaingiza katikanuru. Lakini waliokufuru, walinzi (viongozi) wao nimatwaghuti. Huwatoa katika nuru na kuwaingizakatika giza. Hao ndio watu wa motoni humo watakaamilele”. (2:257).

Utukufu ni wako (Allah)! Hatuna elimu isipokuwaile uliyotufundisha, bila shaka

wewe (Allah) ndiyeMjuzi na ndiyeMwenye hikima

(2:32)

Page 280: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

269

Zoezi la Tano

1. (a) Nini maana ya Siasa (b) Taja tanzu za mfumo wa siasa za kitwaghuti

2. Linganisha na kutafautisha baina ya mfumo wa Siasaza Kidemocrasia na mfumo wa Siasa wa Kiislamu

3. (a) Eleza maana ya Dola. (b) Onesha msonge wa utendaji katika dola yakitwaghuuti

4. Soma kwa makini Qur’an 27:48-49, 8:30,9:40. (a) Ni chombo kipi kinachohusika na hila hizi katika dolala kitwaghuuti?(b) Ni mambo gani yanayofanya chombo hiki kufikiamalengo yake?

5. Kuna tafauti gani kati ya kazi za bunge,mahamaka, napolisi katika dola ya kitwaghuuti na kazi za vyombo hivyokatika dola ya Kiislamu.

6. Eleza, ni mfumo upi wa Dola, kati ya ule wa kitwaghutina wa kiislamu ambao ni muhimu, na bora kwa jamiikuufuata

7. Taja na kufafanua misingi ya utii katika maongozi yadola ya Kiislamu na sababu zake.

8. Bainisha sifa na vigezo vya kumstahikisha mtu kuwakiongozi wa Kiislamu.

9.Taja, eleza na kuthibisha kwa Qur’an, njia za kumpatamtu atakaye kabidhiwa dhima ya kuwa kiongozi atakayeongoza Waislamu na jamii katika kutekeleza wajibu namajukumu yao kulingana na lengo halisi la maisha.

Page 281: Maarifa ya Uislamu - iep.or.tz · inayoongozwa kwa kanuni na sheria zenye adili (flaw-less), haki na uadilifu usio na doa la upogo, limewekwa mabegani mwa waumini, Waislamu! Anasema

270

9. Bainisha tafauti nne katika ya serikali ya Kiislamu naile ya Kidemokrasia.

10. (a) Taja aina za raia katika Dola ya Kiislamu (b) Onesha kwa ushahidi wa Qur’an na Sunnah, hakiinazopasa kusimamia serikali ya kiislamu kwa raia zake.