maadili final gpalace

14
0 TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR MUONGOZO WA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA KWA UCHAGUZI MKUU, 2015 JULAI, 2015

Upload: zanzibariyetu

Post on 03-Nov-2015

514 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR MUONGOZO WA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA KWA UCHAGUZI MKUU, 2015JULAI, 2015MUONGOZO WA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA KWA UCHAGUZI MKUU, 2015

UtanguliziKwa kuwa tunahitaji kuwa na amani, uhuru wa kampeni, na kuheshimu sheria ili kufanya uchaguzi wa huru na wa haki. Sisi vyama vya siasa tumeamua kwa hiari yetu wenyewe kutengeneza maadili haya ili yatuongoze katika shughuli zetu za uchaguzi na tunakubaliana kuwa sisi kama wananchi wa Zanzibar, tutahakikisha kuwa maadili haya yanajulikana kwa wagombea, mawakala na wafuasi wetu, na kwamba tutahakikisha vifungu vyote vinatakelezwa kikamilifu. Kwa hiyo, kwa hiari yetu tunatengeneza na kujipa wenyewe maadili yafuatayo:-Mamlaka 1. Maadili haya yanaanzishwa chini ya kifungu cha 130 cha Sheria ya Uchaguzi Namba 11 ya 1984.

Kuanza kutumika1. (1) Maadili haya yametayarishwa kwa pamoja kati ya Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2015, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na yataanza kutumika baada ya uteuzi wa wagombea na kumalizika mwezi mmoja baada ya uchaguzi.(2) Maadili haya, pia yatatumika katika Uchaguzi Mdogo pale utakapojitokeza.

Madhumuni1. Madhumuni ya Maadili haya ni kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2015, unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu kwa kuzingatia uhuru na haki ya ushiriki wa makundi yote ya kijamii yakiwemo wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, na vigezo vya kimataifa vya uchaguzi wa kidemokrasia.

Haki na wajibu wa Vyama vya siasa.1. Sisi Vyama vya Siasa, tunaoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2015, tukiwa wawakilishi wa wananchi tunaamini na kukubali kuwa:1. Kulinda usalama, utulivu na amani ya Zanzibar ni jukumu la msingi la vyama na wananchi wote.1. Vyama vitahakikisha ushiriki huru na ulinzi wa haki za wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama wapiga kura au wagombea. 1. Kufuata maelekezo ya Sheria, Kanuni, Miongozo ya Tume, Maadili na Taratibu za Uchaguzi ni muhimu katika kufanya uchaguzi ulio huru na wa haki. 1. Vyama havitatumia makundi ya wanawake, vijana na makundi mengineyo katika kufanya vurugu au uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi.1. Kujiunga na chama chochote cha siasa na kumchagua kiongozi anayemtaka ni uhuru na haki ya kila mwananchi mwenyewe. 1. Kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2015, kina haki ya kufanya kampeni kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo nchini.

Thamani, utu na haki za binadamu 1. (1) Sisi Vyama vya Siasa kwa umoja wetu :1. Tunathibitisha kwa imani yetu kwamba, utu, thamani na haki ya maisha ya mwanadamu vinastahiki kulindwa kwa nguvu zote kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Zanzibar 1984, na maazimio ya kimataifa; 1. Tunapinga kwa nguvu zetu zote hujuma dhidi ya maisha ya mwanadamu na mali zake kwa sababu ya itikadi yake ya kisiasa;1. Tutaheshimu haki ya kila Chama cha Siasa, wanachama na wafuasi wake kutoa na kueleza maoni yao ya kisiasa na kutekeleza shughuli zao na malengo ya kisiasa kwa mujibu wa Sheria; na 1. Tutaheshimu utu wa mwanamke na mtu mwenye ulemavu kama mgombea na mpiga kura katika mchakato wa uchaguzi.

Kupinga na kujiepusha na kauli za chuki, fujo, vitisho na vurugu 1. (1) Sisi Vyama vya Siasa kwa pamoja:

1. Tunakataa na kupinga matumizi ya silaha za aina yoyote kutumiwa na viongozi, mawakala, mwanachama na wafuasi wetu kwa malengo ya kufanya hujuma katika harakati za kisiasa;1. Tunakataa mbinu zozote zisizo halali kutumika na vyama katika harakati za uchaguzi.1. Tunakataa vikundi vya ulinzi vya vyama kutumiwa kwa malengo ya kuchochea fujo na kuvuruga amani wakati wa kampeni na uchaguzi1. Tunaamini kuwa ni jukumu na wajibu wetu wa kuwa na jamii yenye mahusiano mema, yasiyo ya vurugu, chuki na vitisho;1. Tunakataa kauli na vitendo vyote vinavyopelekea kuibua hisia za chuki, vitisho, fujo, udhalilishaji wa wanawake na watu wenye ulemavu na kutofahamiana katika kutekeleza malengo ya kisiasa;(2) Kwa mwelekeo huo kufanya Uchaguzi wa kidemokrasia ulioandaliwa katika mazingira ya uwazi na ukweli ni jambo muhimu sana kwa ustawi wa Zanzibar.

Sheria, Kanuni na Taratibu

1. Sisi Vyama vya Siasa tunakubali kuwa:1. Tutatekeleza shughuli zote za kisiasa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, Kanuni, Miongozo ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na taratibu zinazotawala mwenendo wa Uchaguzi Zanzibar.1. Tunakemea vitendo vya rushwa na vyengine visivyo halali, pia tunawasisitiza wafuasi wa vyama vyetu na wananchi kuepuka kutoa matangazo na matamshi yatakayochochea ubaguzi wa aina yoyote ukiwemo wa rangi, kabila, jinsia, dini, ulemavu, na itikadi za kisiasa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu;1. Tunawataka wanachama na mawakala wetu kuheshimu haki za wengine, ili kuhakikisha kuwa haki ya mtu kutoa mawazo yake inaheshimiwa.

Kampeni za utulivu, amani na heshima kwa wengine1. Sisi Vyama vya Siasa, tuko tayari kusaidia kwa uwezo wetu wote kufikia Malengo ya Uchaguzi huru na haki na tunaahidi kufanya yafuatayo;a. Kukataza matumizi ya lugha za matusi, lugha zisizofaa, vitisho na vitendo vya fujo vitavyopelekea kushawishi na kuharibu mikutano au shughuli nyingine halali za Vyama vya Siasa.b. Kupinga uchapishwaji wa vijarida, vipeperushi, mabango ya matangazo, katuni, katika mitandao ya kijamii au aina nyingine za machapisho yatayobeba ujumbe unaochochea na kuwashawishi watu kuvunja amani ya nchi au kudhalilisha wagombea kutokana na jinsia zao au ulemavu;c. Kukataza wagombea, wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa kufanya vitendo vya aina yoyote vitakavyoharibu mikutano, maandamano au mikusanyiko ya chama chengine cha siasa.d. Kukataza na kupinga vikali vitendo vyote vitakavyopelekea kuharibu picha za wagombea, kuchana matangazo na machapisho mengine yanayowahusisha wagombea wa vyama vyengine.e. Kila chama kuondosha katika maeneo ya wazi mabango, picha za wagombea na matangazo yake yahusianayo na Uchaguzi ndani ya kipindi cha siku kumi na nne baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi.f. Kukataza mawakala na wafuasi wa Vyama vya siasa kubandika picha, machapisho au matangazo ya wagombea katika nyumba za ibada na za watu binafsi na vyombo vya usafiri bila ya ridhaa za wamiliki. g. Kuhamasisha kampeni za amani na utulivu ambazo zitapelekea kila chama kujiheshimu na kuheshimiwa;

Muda wa Kampeni1. Tunakubaliana kuwa kampeni za nje zitaanza saa mbili asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni. Vipaza Sauti vitumike kwa muda uliolekezwa hapo juu.

Matumizi ya magari ya serikali na rasilimali za umma katika kampeni1. Sisi, Vyama vya Siasa tunakubaliana kutotumia:- 1. Gari za Serikali na rasilimali za umma katika kampeni.1. Majengo, watumishi na Taasisi za umma katika shughuli za kampeni za uchaguzi.

Kuheshimu Sheria za usalama barabarani

1. Sisi vyama vya siasa tunakataza wanachama na wafuasi wa vyama vyetu wanaosafiri kufuatilia mikutano ya kampeni, kujazana kupita kiasi katika gari wakati wa kwenda na kurudi katika mikutano hiyo na gari hizo hazitovunja Sheria za Usalama Barabarani.

Kuheshimu mchakato wa uchaguzi

1. (1) Sisi Vyama vya Siasa pamoja na wagombea, wanachama na mawakala wa vyama vyetu: 1. Tutashirikiana na kuisaidia Tume ya Uchaguzi, watendaji na maafisa wake katika kutekeleza majukumu na wajibu wao; tutajizuia na lugha za matusi, vitisho na vitendo vinavyochochea uvunjifu wa amani wakati wa shughuli za uchaguzi.1. Tutahakikisha wagombea, mawakala na wanachama wetu hawafanyi hila kwa njia yoyote ile katika zoezi la kupiga na kuhesabu kura. Aidha, tutawazuia kueneza uzushi kuhusiana na matokeo ya uchaguzi.1. Tutawaelekeza wagombea, mawakala na wanachama wetu kutosababisha hasara ya aina yeyote katika maeneo ya uchaguzi kwa kuondoa, kuharibu, kuchana machapisho na nyaraka mbali mbali zinazotolewa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar.

Wajibu wa Tume1. Katika kutekeleza majukumu yake, Tume ya Uchaguzi pamoja na watendaji wake itahakikisha inatekeleza majukumu yake kwa:-a. Kufuata Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu zinazoongoza mchakato wa Uchaguzi wa Zanzibar.b. Kutopendelea chama chochote cha siasa au Mgombea. c. Kushirikiana na wagombea wa vyama vyote katika kuhakikisha maelekezo ya Sheria juu ya mchakato wa uchaguzi yanafuatwa.d. Kutoa taarifa, ufafanuzi na maelezo juu ya jambo ililolifanya, inalolifanya na inalotarajia kulifanya katika hatua za uchaguzi.e. Kuweka wazi milango yake kwa chama au mgombea kwa ajili ya ufafanuzi, maelekezo au taarifa inayohusiana na utendaji wa Tume ya Uchaguzi; naf. Kushughulikia kwa upesi malalamiko ya ukiukwaji wa Sheria au maadili unafanywa na Ofisa wa Tume au wadau wengine wa uchaguzi.

Utoaji wa Taarifa za Uchaguzi 1. Tume ya Uchaguzi inaahidi kutoa habari na taarifa za mwenendo wa Uchaguzi kwa njia ya uhuru, uwazi na ukweli hatua kwa hatua hadi kukamilika hatua zote za uchaguzi.

Wajibu wa Serikali1. Serikali itahakikisha kuwa:-a. Inatoa huduma na nafasi sawa kwa vyama vyote vya siasa bila ya upendeleo wa aina yoyote;b. Inachukua hatua za kisheria kwa kiongozi yeyote wa Serikali atakayebainika kuvuruga au kuhujumu shughuli au kampeni ya chama cha siasa;c. Kupitia vyombo vya usalama inasimamia usalama wa nchi na kutoa ulinzi unaostahiki katika mikutano na kampeni na mikusanyiko yote iliyo rasmi ya vyama vya siasa;d. Majengo, watumishi na vyombo vya usafiri vya Serikali havitumiwi katika shughuli za vyama vya siasa kufanikisha kampeni za vyama vyao;e. Watendaji wa Serikali wanatoa ushirikiano kwa vyama vya siasa katika kutekeleza majukumu yao hasa kampeni. f. Watumishi wa Serikali hawatumii muda wa kazi kufanya kampeni katika Ofisi zao.

Wajibu wa Jeshi la Polisi1. Jeshi la Polisi litahakikisha:-a. linalinda usalama wa raia na mali zao, maafisa wa Tume ya Uchaguzi, mawakala wa vyama vya siasa, wapiga kura na waangalizi wa uchaguzi;

b. kuwa katika kutekeleza jukumu lake la kutunza na kulinda amani na usalama wa raia katika shughuli za uchaguzi haliingiliwi na taasisi nyengine yoyote ili kuepusha mgongano wa dhamana katika usimamizi wa ulinzi na usalama wa raia na mali zao;

c. kuwa linafuata Katiba na Sheria za nchi katika kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Kuheshimu Wagombea wengine 1. Sisi Vyama vya Siasa tutahakikisha kuwa:- a. Wagombea, mawakala au wafuasi wetu hawatowi lugha ya udhalilishaji kwa viongozi wengine wa Vyama ambao wanagombea nafasi moja au vyenginevyo. b. Wagombea, mawakala au wafuasi wetu hawatoi lugha za kuwadhalilisha wagombea wengine kutokana na jinsia zao, maumbile yao, rangi zao au sehemu wanazotoka.

Ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama1. Sisi Vyama vya Siasa tutashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika usimamizi wa sheria na kudumisha amani wakati wa kampeni, upigaji kura, utangazaji wa matokeo na baada ya matokeo ya uchaguzi.

Kukubali matokeo ya uchaguzi1. Sisi Vyama vya Siasa tunaahidi kuyakubali matokeo halali ya uchaguzi yatakayopatikana kwa mujibu fomu za matokeo ya uchaguzi zilizokusanywa kutoka katika vituo vya kupigia kura na yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambayo ndio yenye mamlaka ya kutangaza matokeo kisheria

Ukiukaji wa maadili1. Muhusika yeyote atakayekwenda kinyume kwa mujibu wa maadili haya atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa adhabu zifuatazo:-1. Onyo au Karipio;1. Kutangazwa katika jamii;1. Kutakiwa kuomba msamaha kwa jamii;1. Kumsimamisha mgombea au chama kuendelea na kampeni kwa kipindi kitakachoonekana kinafaa na kamati; na1. Faini kama zinavyoelekezwa na Tume.

Mamlaka ya usimamizi wa maadili1. Maadili haya yatasimamiwa na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi iliyopo chini ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Kamati hii itakuwa na mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa maadili haya katika ngazi zote za uchaguzi wa Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.

Uwasilishwaji wa Malalamiko1. Chama kitakachoona kuwa maadili haya yamekiukwa au kuna ushahidi wa kutosha kuwa yatakiukwa, kina haki ya kuwasilisha malalamiko kwa Kamati ndani ya saa arobaini na nane kabla au baada ya tukio la uvunjifu wa maadili kutokea.

Muda wa kusikiliza Malalamiko1. (1) Kamati mara baada ya kupokea malalamiko, itazijulisha pande zote mbili muda, siku na wakati wa kusilizwa lalamiko hilo.(2) Kamati itasikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kutoa Uamuzi ndani ya masaa sabini na mbili.

Rufaa1. (a) Chama ambacho hakitaridhika na uamuzi wa kamati kina haki ya kukata rufaa kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ndani ya siku tatu. (b) Tume itasikiliza rufaa iliyowasilishwa ndani ya kipindi cha siku tatu na kutoa uamuzi.(c) Kama Chama hakitaridhika na uamuzi wa Tume, kina ruhusiwa kupeleka lalamiko lake mahakamani.

Kuridhia utekelezaji1. (1) Sisi Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi na Serikali tunakubaliana kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maadili haya kwa madhumuni ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambayo kwa kiasi kikubwa yatasaidia kuwa na uchaguzi huru na haki. (2) Kwa uthabiti wetu tutawaagiza wagombea, wanachama na mawakala wetu na wananchi kwa ujumla kutekeleza maadili haya na tunajitolea kuchukuwa hatua za ziada kuhakikisha elimu juu ya maadili inatolewa nchi nzima na yanatekelezwa kwa vitendo.

TAMKO

SISI, vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi na Serikali kwa hiari yetu tunatia saini na kuridhia usimamizi na utekelezaji wa maadili haya.

1CHAMAAlliance for Change and Transparency - ACT

JINA

WADHIFA

2CHAMAAlliance for Democratic Change - ADC

JINA

WADHIFA

3CHAMAAlliance for Famers Party - AFP

JINA

WADHIFA

4CHAMAAfrica Progressive Party - APPT Maendeleo

JINA

WADHIFA

5CHAMAChama cha Kijamii - CCK

JINA

WADHIFA

6CHAMAChama cha Mapinduzi - CCM

JINA

WADHIFA

7CHAMAChama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA

JINA

WADHIFA

8CHAMAChama cha Ukombozi wa Umma - CHAUMA

JINA

WADHIFA

9CHAMAChama cha Ustawi Tanzania - CHAUSTA

JINA

WADHIFA

10CHAMACivic United Front - CUF

JINA

WADHIFA

11CHAMADemokrasia Makini - DM

JINA

WADHIFA

12CHAMADemocratic Party - DP

JINA

WADHIFA

13CHAMAJahazi Asilia

JINA

WADHIFA

14CHAMANational Convention for Construction and Reform - NCCR Mageuzi

JINA

WADHIFA

15CHAMANational League for Democracy - NLD

JINA

WADHIFA

16CHAMANational Reconstruction Alliance - NRA

JINA

WADHIFA

17CHAMASauti ya Umma - SAU

JINA

WADHIFA

18CHAMATanzania Democratic Alliance - TADEA

JINA

WADHIFA

19CHAMATanzania Labour Party TLP

JINA

WADHIFA

20CHAMAUnited Democratic Party - UDP

JINA

WADHIFA

21CHAMAUnion for Multiparty Democracy - UMD

JINA

WADHIFA

22CHAMAUnited People Democratic Part - UPDP

JINA

WADHIFA

Kwa niaba ya Tume ya Uchaguzi ya ZanzibarJina ___________________________________.Cheo___________________________________.Saini ___________________________________Tarehe ______/_____/20_____.

Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya ZanzibarJina ___________________________________.Cheo___________________________________.Saini ___________________________________Tarehe ______/_____/20_____.

Kwa niaba ya Jeshi la Polisi, ZanzibarJina ___________________________________.Cheo___________________________________.Saini ___________________________________Tarehe ______/_____/20_____.

CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT)

CHAMA CHA ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE (ADC)

CHAMA CHA WAKULIMA (AFP)

CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA (CHAUMMA)

CHAMA CHA PROGRESSIVE PARTY OF TANZANIA(APPT-Maendeleo)

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

CHAMA CHA HAKI NA USTAWI (CHAUSTA)

CHAMA CHA WANANCHI (CUF)

CHAMA CHA DEMOCRATIC PARTY (DP)

CHAMA CHA JAHAZI ASILIA

CHAMA CHA KIJAMII (CCK)

DEMOKRASIA MAKINI (MAKINI)

CHAMA CHA NATIONAL CONVENTION FOR CONSTRUCTION AND REFORM (NCCR- Mageuzi)

CHAMA CHA NATIONAL LEAGUE FOR DEMOCRACY (NLD)

CHAMA CHA SAUTI YA UMMA (SAU)

CHAMA CHA TANZANIA DEMOCRATIC ALLIANCE (TADEA)

CHAMA CHA NATIONAL RECONSTRUCTION ALLIANCE (NRA)

CHAMA CHA UNITED DEMOCRATIC PARTY (UDP)

CHAMA CHA UNION MULTIPARTY DEMOCRACY (UMD)

CHAMA CHA TANZANIA LABOUR PARTY (TLP)

CHAMA CHA UNITED PEOPLES DEMOCRATIC PARTY (UPDP)

0