kumjua yesu yaliyomo sura 1 - jinsi mungu anavyowapenda ... · uligeuka ukawa mbaya, tena badala ya...

128
KUMJUA YESU YALIYOMO Sura 1 - Jinsi Mungu Anavyowapenda Wanadamu VIUMBE vya ulimwengu, na jinsi Mungu alivyowafunulia wanadamu mambo yajayo, vyote huonyesha upendo wa Mungu. Baba yetu aliye mbinguni ndiye asili ya uhai, hekima, na furaha. Vitazame viumbe vyote jinsi vilivyo vizuri na vya ajabu. Fikiri jinsi vifaavyo kwa mahitaji na furaha, siyo ya wanadamu tu, bali ya viumbe vyote vilivyo hai. Jua na mvua, vinavyofurahisha na kuburudisha nchi, pamoja na vilima, bahari na mabonde, vyote hutuonyesha upendo wa Muumba wetu. Mungu ndiye anayeviruzuku viumbe vyake vyote mahitaji yao ya kila siku. Katika maneno mazuri ya Mtunga Zaburi twasoma haya, - KY 7.1 “Macho yao wote yakutazamia wewe; Nawe huwapa chakula chao majira yake. Hufunua mkono wako, Humshibisha kila hai uradhi.” KY 7.2 Zaburi 145:15, 16. KY 7

Upload: others

Post on 02-Mar-2020

48 views

Category:

Documents


7 download

TRANSCRIPT

KUMJUA YESU

YALIYOMO

Sura 1 - Jinsi Mungu AnavyowapendaWanadamu

VIUMBE vya ulimwengu, na jinsi Mungualivyowafunulia wanadamu mambo yajayo, vyotehuonyesha upendo wa Mungu. Baba yetu aliyembinguni ndiye asili ya uhai, hekima, na furaha.Vitazame viumbe vyote jinsi vilivyo vizuri na vya ajabu.Fikiri jinsi vifaavyo kwa mahitaji na furaha, siyo yawanadamu tu, bali ya viumbe vyote vilivyo hai. Jua namvua, vinavyofurahisha na kuburudisha nchi, pamojana vilima, bahari na mabonde, vyote hutuonyeshaupendo wa Muumba wetu. Mungu ndiyeanayeviruzuku viumbe vyake vyote mahitaji yao ya kilasiku. Katika maneno mazuri ya Mtunga Zaburitwasoma haya, - KY 7.1

“Macho yao wote yakutazamia wewe;Nawe huwapa chakula chao majira yake.Hufunua mkono wako,Humshibisha kila hai uradhi.” KY 7.2

Zaburi 145:15, 16. KY 7

Mungu alimwumba mwanadamu katika hali yafuraha na utakatifu kamili; na wakati nchi ilipotokamkononi mwa Muumba, ilikuwa nzuri kabisa; haikuwana dalili ya uharibifu wala ya laana ya Mungu. Taabuna mauti viliingia kwa ajili ya kuharibu amri za Mungu.Walakini upendo wa Mungu huonyeshwa hata kwamaumivu yaliyokuja kwa ajili ya dhambi. Imeandikwakwamba Mungu aliilaani ardhi kwa ajili yamwanadamu. Mwanzo 3:17. Miti yenye miiba namagugu - yaani shida na majaribu yanayompatamwanadamu katika uzima wake - yaliwekwa kuwamsaada wake, kuwa ni namna mojawapo yamafundisho yake yanayotakiwa katika mpango waMungu juu ya mwanadamu, ili apate kumtoa katikahali mbaya ya dhambi na kumrudisha katika halinjema jinsi alivyokuwa mara ya kwanza. KY 7.3

Ingawa dunia imeanguka katika hali mbaya kwa ajiliya dhambi, lakini yote yaliyomo si huzuni na mashaka.Viumbe vimekuwa kama mitume wa Mungu kutuleteamaneno ya kututia faraja na kututuliza roho zetu. Kilamti wa miiba una maua yake; yaani, katika kila shidatwaweza kupata baraka za Mungu. KY 8.1

“Mungu ni pendo” imeandikwa kila mahali. Ndegewaimbao vizuri, kila aina ya maua na miti, - yotehutushuhudia upendo na uangalifu wa Mungu, jinsiatakavyo kuwafurahisha watoto wake. KY 8.2

Neno la Mungu huonyesha tabia zake. Yeyemwenyewe ametangaza upendo wake na hurumayake visivyo na kiasi. Musa alipoomba, “Nionyeshebasi utukufu wako,” Bwana alimjibu akanena,“Nitapitisha mimi wema wangu wote mbele yako.”Huu ndio utukufu wake. Bwana alipita mbele ya Musa,akatamka, “Bwana, Bwana Mungu, mwenye rehema naneema, si mwepesi kwa hasira, na mwingi wa hurumana kweli; awawekeaye elfu huruma, mwenyekusamehe uovu, na kosa, na dhambi.” Kutoka 33:18,19; 34: 6, 7. Naye “mvumilivu, na mwenye wemamwingi,” “kwa sababu apendezwa na huruma huyu.”Yona 4: 2; Mika 7:18. KY 8.3

Mungu amejifungia mioyo yetu kwake kwa namnanyingi zinazotuonyesha upendo wake; katika viumbevya ulimwengu, na kwa upendano ulio wema wawanadamu, Mungu amejaribu kutuonyesha wemawake. Lakini hayo yote hayawezi kutudhihirishiabarabara upendo wake jinsi ulivyo, kwa kuwa adui,yaani Shetani, amepofusha macho va kiroho yawanadamu ili wawe na hofu kwa Mungu; naohumwona Mungu kama ni mkali asiye na huruma.Shetani aliwapoteza wanadamu ili wamdhanie Mungukuwa ni mkali kabisa - kama mwamuzi aliye na rohongumu asiyeweza kumwachia mtu. Aliwatiliawanadamu fikara kama Muumba wetu

huwachunguachungua watu ili apate kujua makosayao na kuwalipiza kisasi. Bwana Yesu alikuja hapaduniani na kuishi kati ya wanadamu kwa kusudikuziondolea mbali fikara mbaya hizo, na kutuonyeshaupendo wa Mungn jinsi ulivyo. KY 9.1

Mwana wa Mungu alitoka mbinguni ili awaonyeshewanadamu Baba aliye mbinguni. “Hakuna mtualiyemwona Mungu wakati wo wote; Mwana wa pekeealiye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasirihabari yake.” “Wala hakuna mtu amjuaye Baba ilaMwana, na ye yote ambaye Mwana apendakumfunulia.” Yoh. 1:18; Mattayo 11:27. Mmoja wawanafunzi wake alipomwambia, “Tuonyeshe Baba,”Yesu alimjibu, “Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zotewala hukunijua, Filipo? Aliyeniona mimi, amemwonaBaba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba?” Yoh. 14:8,9. KY 10.1

Yesu alipoeleza namna ya kazi yake aliyojiliakuifanva hapa duniani, alisema hivi, - KY 10.2

“Roho ya Bwana ni juu yangu,Kwa sababu amenitia mafuta kuwahubirimaskini habari njema.

Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo,Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa,

na vipofu kupata kuona tena,Kuwaacha huru waliosetwa.” KY 10.3

Luka 4:18. KY 10

Hiyo ndiyo kazi yake. “Naye akatembea huko nahuko, akitenda kazi njema na kuponya wotewalioonewa na Shetani.” Matendo 10:38. Katikamatendo yake yote alionyesha upendo, rehema nahuruma. Alikuwa katika hali ya kibinadamu ili apatekujua mahitaji ya wanadamu. Hakuna hata maskinikabisa aliyeogopa kumfikilia karibu. Watoto piawakavutwa kwake. KY 10.4

Yesu hakuficha neno lo lote la kweli, lakini aliyesemayote katika moyo wa upendo. Alitumia busara sana nauangalifu na huruma katika maongezi yake na watu.Hakuwafanyia watu jeuri kamwe, hakusema manenoyo yote makali yasipohusu, hakuwahuzunisha watubila maana. Hakuulaumu udhaifu wa kibi¬nadamu.Alisema kweli tupu, lakini alisema yote katika moyowa upendo. Alichukizwa sana na hali ya unafiki, nakutokuamini, na uovu; lakini kila aliposema maneno yalawama na mashtaka, aliyesema kwa masikitikomakubwa. Aliulilia Yerusalemi, mji alioupenda, ambaoulikataa kumpokea yeye aliye Njia, Kweli, na Uzima.Walimkana yeye aliye Mwokozi, lakini hata hivyoakazidi kuwahurumia. Maisha yake yalikuwa ya

kujinyima mwenyewe na kuwafikiria wengine. Kila mtualikuwa na thamani kubwa machoni pake. Ingawaalikuwa Mwana wa Mungu, hakumdharaumwanadamu ye yote; bali aliwaona wote kuwa niwenye dhambi ambao alikuja kuwaokoa. KY 11.1

Hizo ndizo tabia zake Kristo kama zilivyofunuliwakatika maisha yake. Tena hizo ndizo tabia za Mungumwenyewe pia. Yesu, Mwokozi aliye mwema, mwenyehuruma, ndiye Mungu hasa aliyedhihirishwa katikamwili wa kibinadamu. 1 Tim. 3:16. KY 11.2

Yesu aliishi, akateswa, akafa ili atukomboe. Alikuwa“mtu wa huzuni,” ili tuwe washiriki pamoja naye katikafuraha ya milele. Naye Mwana Mpendwa wa Mungu,aliyejaa neema na kweli, Mungu alimwacha atokemahali pa utukufu na kufika hapa duniani,palipoharibika kwa ajili ya dhambi, penye giza ya mautina laana. Alimkubalia atoke mahali anapopendwa naBabaye na kusifiwa na malaika, aje kuaibika,kudhiliwa, kuchukiwa, na kuuawa. “Adhabu ya amaniyetu juu yake.” Isa. 53: 5. Mwangalie jinsi alivyojangwani, katika bustani ya Gethsemane, tena juu yamsalaba. Mwana Mtakatifu wa Mungu akachukuamwenyewe uzito wa dhambi ya wanadamu. Yeyealiyekuwa na umoja na Mungu, akaona mwenyewemoyoni mwake ubaya wa hali ya kutengana na Mungu,ndiyo hali ya wanadamu kwa ajili ya dhambi. Kwa ajili

ya matengano hayo akaona uchungu moyoni nayeakalia, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbonaumeniacha?” Mattayo 27:46. Uzito wa dhambi, jinsiulivyo mbaya kupita kiasi, na jinsi unavyoletakutengana na Mungu - huu ndio uliouvunja moyo waMwana wa Mungu. KY 12.1

Lakini Yesu hakujitoa kuwa dhabihu kubwa hivimakusudi kumtilia Baba yake moyo wa kuwapendawanadamu na kuwaokoa. Sivyo! “Kwa maana jinsi hiiMungu aliupenda ulimwengu, hata akampelekaMwana wake wa pekee, ili mtu aliye yote amwaminiyeasipotee, bali apate uzima wa milele.” Yoh. 3:16.Tangu zamani Baba yetu aliye mbinguni ametupenda,si kwa ajili ya upatanisho alioufanya Yesu, ila kwakuwa Mungu mwenyewe alitupenda, naye akamkubaliYesu afanye upatanisho huo. Kristo ndiye njia ambayokwayo Mungu hutuonyesha upendo wake kwetu.“Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanishaulimwengu na nafsi yake.” 2 Wakor. 5:19. Mungualipata maumivu pamoja na Mwanawe. HukoGethsemane, na kwa kufa kwake Kalwari, Mungualijitoa kwa ajili ya wokovu wetu. KY 12.2

Yesu alisema, “Ndio maana Baba anipenda, kwasababu nauweka uzima wangu ili niutwae tena.’ Yoh.10:17. Yaani, ni kama Yesu angesema hivi: “Babayangu amewapendeni sana hata anazidi kunipenda

mimi kwa sababu ya kujitoa maisha yangu kwa ajiliyenu. Mimi nikawa ninajitoa badala yenu tena kuwakama dhamana yenu, na kwa jinsi nilivyochukuamakosa yenu na adhabu ambayo iliwapasa ninyi, kwahayo Baba yangu huzidi kunipenda mimi; kwa sababuya Dhabihu yangu, Mungu aweza kuwa mwenye hakitena kumhesabia haki yule amsadikiye Yesu.” KY 13.1

Hakuna awezaye kutuokoa, ila Mwana wa Mungu tu;kwa kuwa yeye pekee aliyekuwa pamoja na Baba,ndiye awezaye kumsifu na kueleza tabia zake. Yeye tualiyeujua upendo wa Mungu ndiye awezayekuudhihirisha upendo ule barabara. Hakuna njianyingine ya kutuonyesha jinsi Mungu anavyowapendawanadamu waliopotea, ila kwa njia hii moja tu, yaaniya Kristo alivyojitoa na kufa badala yao. KY 14.1

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akampeleka Mwana wake wa pekee.” Yoh. 3:16.Mungu alimtoa Mwanawe aishi kati ya wanadamu iliazichukue dhambi zao, apate kuadhibiwa badala yao,na kuwatolea maisha yake kama dhabihu; pia Munguakamtoa awe katika hali moja na wanadamu ambaowamepotea, na kushirikiana nao katika mambo yamaisha yao na haja zao zote. Yeye aliyekuwa mamojana Mungu amejiunga na wanadamu kwa namnaisiyoweza kuvunjwa. Yesu “haoni haya kuwaita nduguzake.” (Waeb. 2:11); yeye ndiye Dhabihu yetu,

Mwombezi wetu mbele ya Mungu, Ndugu yetu aliyekatika mfano wa kibinadamu na kushirikiana nao haoambao amekuja kuwaokoa - Yeye ndiye Mwana wamwanadamu. Alifanya hayo yote ili awakomboewanadamu katika dhambi na hali yake mbaya, nayemwanadamu apate kujua upendo wake Mungu nakushirikiana naye katika hali ya furaha na usafi. KY14.2

Tukifahamu kimo cha wokovu wetu, jinsi Mwana waMungu alivyokufa kwa ajili yetu, imetulazimukutambua jinsi tunavyoweza kuwa watu walio borakatika Kristo. Mtume Yohana alipofahamu upendo waMungu jinsi ulivyo mkubwa mno, aliona hana budikumcha Mungu na kumsujudu moyoni mwake.Upendo huo, jinsi ulivyo wa huruma na rehema, niupendo mkubwa usioweza kusemeka; naye Yohanaalisema, “Fahamuni, ni pendo la namna gani alilotupaBwana, kuitwa wana wa Mungu.” 1 Yoh. 3:1. Munguamewaona wanadamu kuwa ni wenye thamani kubwaya namna gani! Kwa kuanguka katika kufanya dhambi,wanadamu wakawa chini ya mamlaka ya Shetani.Lakini kwa kumwamini Kristo na kutolewa kwake,waweza kuwa wana wa Mungu. Kristo alikuwa katikahali ya kibinadamu ili apate kuwasaidia wanadamu.Nao wenye dhambi wakiwa wanashirikiana nayeKristo, watageuzwa hali yao, na kustahili kuitwa “wana

wa Mungu.” KY 15.1

Upendo wa ajabu huo, hauwezi kulinganishwa nakitu cho chote! Wana wa Mfalme aliye mbinguni!Ahadi ya kupendwa sana! Jambo la maana sanalifaalo kufikiriwa! Upendo usio na kifani, jinsi Mungualivyoupenda ulimwengu usiompenda! Fikara hiyohuutiisha moyo na kuutuliza ili ufungwe kwake Munguna kufanya mapenzi yake. Na jinsi tunavyozidikuzichungua tabia za Mungu, na kufahamu jinsialivyotufanyia kwa kufa kwake Kristo msalabani,ndivyo tunavyozidi kuona kama Mungu ndiye mwenyerehema na huruma, na ndiye awezaye kuwasamehewenye makosa, naye ni mwenye haki, nayehuwapenda wanadamu kwa upendo mkubwa upitaokiasi cha upendo wa mama kwa watoto wake. KY 15.2

Mapenzi ya mileleNdiyo yanipendayo;Yalinipenda mbele,Sina fahamu nayo;Sasa amani yakeTele rohoni mwangu,Ni mimi kuwa wake,Na Yeye kuwa wangu.Ni mimi kuwa wake,Na Yeye kuwa wangu.

Wake hata milele,Si kutengana tena;Hunipa raha teleMoyoni mwangu, BwanaHiyo nchi na mbinguZitatoweka zile;Ni wake, Yeye mbwangu,Milele na milele,Ni wake, Yeye mbwangu,Milele na milele. KY 16.1

Sura 2 - Jinsi Mwenye Dhambi AnavyomhitajiKristo

HAPO mwanzo binadamu alipewa uwezo bora nafikara safi. Alikuwa mkamilifu katika mwili wake, nayeakawa katika hali ya umoja na Mungu. Fikara zakezilikuwa safi na makusudi yake yakawa matakatifu.Lakini kwa ajili ya kutomtii Mungu, uwezo wakeuligeuka ukawa mbaya, tena badala ya upendo akawaakijifikiria nafsi yake mwenyewe. Dhamiri yakeikapungua nguvu kwa sababu ya kufanya dhambi, hatayeye mwenyewe kwa nguvu zake peke yake alikuwahawezi kushindana na maovu. Alikuwa chini yamamlaka ya Shetani, naye mwanadamu angalikuwakatika hali hiyo milele kama Mungu asingaliondoka nakumsaidia. Ilikuwa nia ya mshawishi, yaani Shetani,kuyapinga maazimio mema ya Mungu katikakumwumba binadamu, na kujaza dunia ubaya naukiwa. Na hatimaye angesema kwamba mabaya hayoyote yalitokea kwa ajili ya kazi ya Mungu katikakumwumba binadamu. KY 17.1

Katika hali yake ya kutokuwa na dhambi mwanzoni,mwanadamu akawa na furaha katika kuzungumza naYule “ambaye ndani yake zimo hazina zote za hekimana maarifa.” Wakol. 2:3. Lakini baada ya kufanyadhambi mwanadamu hakuweza kufurahishwa na hali

ya utakatifu, naye alitaka kujificha mbali na macho yaMungu. Hata sasa hiyo ndiyo hali ya moyousioongoka. Haupatani na Mungu, tena hauna furahakatika maongezi naye. Mwenye dhambi asingewezakuwa na furaha mbele ya Mungu; angewaepukawatakatifu. Kama angeweza kuruhusiwa kuingiambinguni, asingekuwa na furaha huko. Nayeasingeweza kushirikiana nao walio mbinguni katikahali ya kuwa na roho inayopatana na Mungu, yaaniroho isiyofikiria nafsi yake yenyewe, bali huwa yakuwafikiri wengine kwa upendo. Fikara zake, mamboanayoyapenda, na maazimio yake yote, vyote hivivingemfanya mwenye dhambi kuwa mgeni kabisa katiya wateule wa Mungu; angekuwa hawezi kulingananao. Angeona mbinguni kama ni mahali pabayakwake; angetaka kujificha mbali na uso wake yeyealiye nuru na furaha ya watakatifu wa Mungu. Wabayahawatazuiliwa kuingia mbinguni kwa sababu ya amrikali ya Mungu isiyo na maana, bali watazuiliwa kwakuwa wenyewe hawana tabia inayopatana na hali yambinguni. Utukufu wa Mungu ungekuwa kama motowa kuwateketeza, nao wangetaka kufichwawasimwone uso wake yeve aliyekufa kuwakomboawatu. Ufunuo 6:15-17. KY 17.2

Sisi wenyewe kwa nguvu zetu hatuwezi kujiokoakatika shimo la uovu ambamo tumeangukia. Mioyo

yetu mibaya kabisa, nasi hatuwezi kuigeuza. “Awezayenani kutoa kilicho safi katika kisicho safi? si hatammoja.” “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu yaMungu, kwa maana haitii sheria za Mungu walahaiwezi.” Ayub 14:4; Warumi 8:7. Elimu, ustaarabu,kujitawala nia, kujibidisha, hivi vyote vinafaa, lakinikatika kazi hii ya kuugeuza moyo haviwezi kitukamwe. Pengine vyaweza kumfanya mtu awe namwenendo mzuri mbele ya watu; lakini haviwezikuigeuza asili yake na moyo wake. Nguvu isiyokuwayake mwenyewe lazima itumike moyoni mwake iliapate uzima mpya utokao juu, hapo ndipo binadamuatakapoweza kugeuza hali yake ya kufanya dhambi nakuwa katika hali ya usafi. Nguvu hiyo ndiyo Kristo. Niyeye tu ambaye anaweza kuwavuta watu kwa Munguili wawe safi. Mwokozi alisema, “Mtu asipozaliwamara ya pili,” yaani kuzawa na Roho, “hawezi kuuonaufalme wa Mungu.” Yoh. 3:3. Maana yake, isipokuwaamepata moyo mpya, nia mpya, maazimio mapya, nakuishi katika uzima mpya, “hawezi kuuingia ufalme waMungu.” Yoh. 3:5. Tusifikiri kwamba inatoshakuziongeza zile tabia njema ambazo amezipata mtutangu asili. “Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokeimambo ya Mungu; maana kwake ni mapumbavu, walahawezi kuyajua, kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsiya rohoni.” Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamnabudi kuzaliwa mara ya pili.” 1 Wakor. 2:14; Yoh. 8:7.

Imeandikwa juu ya Kristo, “Ndaniyake ndimoulimokuwa uzima, nao uzima ulikuwa nuru ya watu,”tena “hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewawanadamu litupasalo kuokolewa nalo.” Yah. 1:4;Matendo 4:12. KY 19.1

Haitoshi kujua namna ya upendo, na neema yaMungu. Haitoshi kutambua tu namna ya amri zake,jinsi zilivyo za haki. Mtume Paulo aliyajua haya yote,akasema, “Nakiri ya kuwa sheria ile ni njema.” “Toratini takatifu, na ile amri takatifu na ya haki na wema.”Warumi 7:16,12. Naye akazidi kusema kwa uchunguwa moyo, “Mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini yadhambi.” Warumi 17:14. Alitamani sana kuwa na usafina uadilifu kamili, ambavyo yeye mwenyewe kwanguvu zake hakuweza kuvipata, naye akalia, “Olewangu mimi binadamu! nani atakayeniokoa na mwilihuu wenye kunifisha.” Warumi 7:24. Kila anayelia hivyohujibiwa neno moja tu. “Tazama, Mwana-Kondoo waMungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” Yoh. 1:29.KY 20.1

Kwa njia nyingi na mifano mingi Roho Mtakatifuamejaribu kuwafundisha watu mambo hayo, nakuwaeleza dhahiri wale watakao kuokolewa katikadhambi. Yakobo alipokimbia baada ya kumdanganyaEsau, aliona moyoni mwake kuwa ana hatia; nayeakaogopa akifikiri labda makosa yake yamemtenga

mbali na Mungu, naye akawa na huzuni moyonimwake. Alipolala usingizi usiku ule, akaota ndoto;aliona ngazi iliyotoka chini mpaka mbinguni; tenamalaika wa Mungu wakawa wakipanda na kushuka;tena kutoka mahali patakatifu juu akasikia sauti yaMungu ikimwambia maneno ya kumtia moyo. Mambohayo yakamjulisha Yakobo kwamba yuko Mwokozi,tena aliona jinsi alivyoweza kurudishwa tena kupatanana Mungu. Ile ngazi ya ndoto ilikuwa mfano wa Yesu,ambaye ni njia ya pekee kwa wanadamu kuwezakumfikia Mungu. KY 21.1

Huu ndio mfano Yesu alioutaja alipozungumza naNathanael, akisema, “Mtaziona mbingu zimefunguka,na malaika wa Mungu wakipanda, wakishuka juu yaMwana wa Adamu. Yoh. 1:51. Katika maasi yake,binadamu alijitenga mbali na Mungu; wanadamuwalikuwa hawawezi kuzungumza nao wa mbingunikama walivyokuwa wamezoea kufanya zamani. Lakinikwa ajili ya Kristo tumepata njia ya upatanisho.Malaika waweza kuja kusema na wanadamu nakuwasaidia. Tena hata kama binadamu wamekuwawabaya kwa ajili ya dhambi, katika Kristo wawezakupata nguvu ya kushindana na maovu. “Kila kutoakwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, chatokajuu,” kwa Mungu. Yakobo 1:17. KY 21.2

Binadamu hawawezi kuwa na sifa njema ya kweli

bila Mungu. Tena Kristo ndiye njia ya pekee kwakumfikia Mungu. Asema, “Ndimi niliye njia, na kweli, nauzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.” Yoh. 14:6.Moyo wa Mungu huwafikiria watoto wake duniani kwaupendo mkubwa mno. Alipomtoa Mwanawe wa pekeekwa ajili yetu, alikuwa kama anatoa kwetu ubora wotewa mbinguni. Maisha ya Mwokozi hapa duniani, kufakwake, na maombezi yake huko mbinguni, msaada wamalaika, maombezi ya Roho Mtakatifu mioyoni mwetu- hivyo vyote hutuonyesha jinsi Baba yetu aliyembinguni awapendavyo wanadamu, tena hutumia njianyingi ili awakomboe. KY 22.1

Heri tufikiri sana habari za Mwokozi wetu, jinsialivyojitoa kama dhabihu kwa ajili yetu! Ajabu sana,mambo haya! Imetupasa kufahamu kwamba katikaKristo tumepewa thawabu kubwa kupita kiasi, ili apatekutuokoa na kuturudisha kwa Mungu. Tufikiri tenayote ambayo Mungu amewaahidia waaminifu wake!Ameahidi thawabu kubwa kwao wanaofanya haki:kufurahishwa mbinguni, kukaa na malaika na kuwa naumoja nao, kuongea uso kwa uso na Mungu naMwanawe, na kujua upendo wao hasa jinsi ulivyo, tenakuzidi kuelimishwa milele. Je, hivyo vyote havitoshikutuonyesha kuwa ni lazima tumtolee Mwokozi wetumioyo yetu kwa upendo wetu, ili tuwe watumishi wakemilele? KY 22.2

Bali, hukumu ya Mungu imetangazwa jinsiitakavyokuwa juu ya dhambi na wenye dhambi, kupataadhabu isiyoepukika, kuwa katika hali ya udhilifu, nauharibifu wa mwisho; hivyo vyote vimetangazwakatika Neno la Mungu kutuonya tusiwe watumishi waShetani. KY 23.1

Laiti tungefikiri sana rehema ya Mungu! Angewezakufanya nini tena zaidi ya hivyo vyote? Heri tulinganenaye ambave ametupenda sana kwa upendo waajabu. Heri tufuate njia yake, tena tutumie nguvu zakeili tupate kugeuka kuwa katika mfano wake, tuingietena katika hali ya kushirikiana na malaika kamawalivyokuwa wanadamu mwanzoni, hali ya umoja naBaba aliye mbinguni na Mwanawe pamoja. KY 23.2

Sura 3 - Kutubu

BINADAMU awezaje kuhesabiwa kuwa ana hakimbele ya Mungu? Mwenye dhambi awezajekusahihishwa na kuwa kama asiye na makosamachoni pake? Kristo ndiye njia tu ya kutupatanishana Mungu na kutuweka katika hali ya usafi. Lakinitwawezaje kufika kwake Kristo? Watu wengi wangaliwakisema kama walivyosema wengine siku ile yaPentekote: “Tufanyeje?” Jibu la Petro lilikuwa hivi:“Tubuni.” Pengine pia alisema hivi, “Tubuni basi,mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.” Matendo 2:38; 3:19.KY 24.1

Kutubu maana yake ni hivi: kuhuzunika kwa ajili yadhambi. tena kujitenga mbali nayo. Hatuwezi kuachakufanya makosa mpaka tumetambua ubaya wake:tena hali yetu katika maisha yetu haitabadilika kamwempaka tumeitenga dhambi mbali na mioyo yetu. KY24.2

Kuna watu wengine ambao hawafahamu asili yakutubu jinsi ilivyo halisi. Wengi huhuzunika kwa ajili yamakosa yao, tena hujaribu kuongoka katikamwenendo wao mbele ya watu, kwa kuwa wanaogopaadhabu ambayo watajipatia kwa ajili ya matendomabaya. Lakini huku si kutubu kama Mungu

anavyotaka. Wao hufikiria adhabu zaidi ya ubaya wamakosa yao. Hivyo ndivyo alivyofanya Esau alipoonaya kwamba amepotewa kabisa na urithi wake. Balaampia, alipotiwa hofu sana kwa ajili ya kumwona malaikaaliyesimama mbele yake na upanga mkononi,akakubali kutiwa hatiani asije akauawa; walakinihakutubu kwa kweli, hakugeuka moyo, hakuchukizwana maovu. Yudas Iskarioti, alipomsaliti Bwana,alisema, “Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.”Mattayo 27:4. KY 24.3

Alishurutishwa kukiri makosa yake alipoona moyonimwake jinsi alivyostahili kuhukumiwa na Mungu kwakosa lake. Lakini kitu kilichomtia hofu kilikuwahukumu na adhabu ya Mungu; hakuhuzunika sanamoyoni na kuingiwa na majuto kwa kuwa amemsalitiyule mtakatifu Mwana wa Mungu, au kwa kuwaamemkana Mtakatifu wa Israeli. Farao pia; alipoonamaumivu ya Mungu alikiri makosa yake ili apatekuepuka adhabu; lakini mapigo yalipokoma, alizidikufanya kiburi. Watu hao wote walililia mamboyaliyotokea kwao kwa ajili ya makosa yao, lakinihawakuwa wakihuzunika na kujuta kwa ajili yamakosa yenyewe na ubaya wake. KY 25.1

Lakini kama mwenye dhambi anajitoa kuwa chini yautawala wa Roho Mtakatifu, ndipo dhamiri yakeitakaposafishwa, ataona barabara jinsi alivyo katika

hali ya kufanya dhambi, atafahamu maana ya usafi waamri za Mungu ambazo ndizo msingi wa utawalawake. “Kulikuwako nuru halisi, imtiayo nuru kila mtuajaye katika ulimwengu.” Yoh. 1:9. Nuru ile, ndiyeKristo, humtia mtu nuru moyoni, mambo ya sirihufunuliwa, na yule mwenye dhambi hujiona jinsialivyo na hatia machoni pa Mungu mwenye hakikabisa. Pia huelewa na upendo wa Mungu na uzuri wakuwa katika hali ya usafi na utakatifu; hutamanikusafishwa na kupatana nao walio mbinguni. KY 25.2

Sala ya Daudi baada ya kuanguka kwake dhambinihutudhihirishia vizuri namna ya kweli ya kuhuzunika nakujutia maovu. Hakutaka kulipunguza kosa lake, walakuepuka hukumu ilivyokuwa stahili yake. Daudi alionakosa lake jinsi lilivyokuwa kubwa mno; aliona unajisiwa moyo wake; akachukizwa sana na kosa lake.Hakuomba ili apate kuachiliwa tu, akaornba pia apatekusafishwa moyoni mwake. Akatamani kuingia katikahali ya usafi na kuwa mmoja na Mungu. Akaomba hivi:- KY 26.1

Heri aliyesamehewa makosa, aliyestirikiwadhambi,Heri mwanadamu, Bwana asiyemhesabia hatia,Rohoni mwake isipokuwa hila.” KY 26.2

Zaburi 32:1, 2.

KY 26

Unirehemu, Ee Mungu, kwa jinsi ulivyo mwema:Rehema zako zilivyo kuu, ufute makosa yangu.Unioshee kabisa hatia yangu, unitakasie dhambizangu.Kwani nayajua makosa yangu: na dhambi yangumbele yangu daima . . . .Unisafishe kwa ezobu, nami nitakuwa safi;Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. . . .Uniumbie moyo safi, Ee Mungu,Ufanye ndani yangu roho aminifu.Usinitupe usoni pako;Usiniondolee roho yako takatifu.Unirudishie furaha ya wokovu wako:Unichukue kwa roho bora . . . .Uniponye kwa damu, Ee Mungu, Mungu wa wokovuwngu;Na ulimi wangu utaiimba haki yako.” KY 26.3

Zaburi 15:1-14. KY 27

Kutubu kwa namna ile hakuwezekani kwetu sisi kwauwezo wetu wenyewe; kunawezekana katika Kristo tu.Hapo ndipo wengi hupotea katika kudhani kwambahawawezi kuja kwake Kristo isipokuwa kwanzawamekwisha kutubia dhambi zao. Ni kweli mtu lazima

kutubia dhambi zake kwanza, ndipo Munguatamwachilia; kwani bila masikitiko moyoni kwa ajiliya makosa, mwenye dhambi hawezi kufahamu jinsianavyomhitaji Mwokozi. Je, mwenye dhambi hanabudi kungoja kumfikia Kristo mpaka ametubu? KY27.1

Katika Biblia, Neno la Mungu, hatusomi kwambamwenye dhambi hana budi kutubu kabla ya kukubalimwito wa Kristo aliyesema, ” Njooni kwangu, ninyinyote msumbukao na wenye mizigo, naminitawapumzisha.” Mattayo 11: 28. Ni uwezo wa Kristounaowezesha watu kutubu kwa kweli. Petro ameelezamambo haya dhahiri aliposema, “Mtu huyo Munguamemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuuna Mwokozi, awape Waisraeli toba na masamaha yadhambi.” Matendo 5:31. Kwa kadiri tusivyowezakusamehewa dhambi bila Kristo, ndivyo tusivyowezakutubu pasipo nguvu za Roho ya Kristo mioyonimwetu. Kristo ndiye asili ya kila fikara njema. Yeye tundiye awezaye kuutia moyo fikara ya kushindana namaovu. Kila aonaye moyoni mwake haja ya kuwa nakweli na usafi, kila asadikiye hali yake ya dhambi,huwa anashuhudia kwamba Roho Mtakatifu yumomoyoni mwake. KY 27.2

Yesu amesema, “Nami nikiinuliwa juu ya nchinitavuta wote kwangu.” Yohana 12:32. Mwenye

dhambi hana budi kumwona Yesu kama Mwokoziwetu aliyekufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu; nasitukimwona msalabani kwa macho ya kiroho, tutazidikufahamu mambo ya wokovu, tena wema wa Munguutatuongoza ili tutubu. Hatuwezi kufahamu barabaraupendo wa Kristo jinsi ulivyomshurutisha afe kwa ajiliyetu; lakini upendo huo huivuta mioyo yetu kwake. KY28.1

Pengine watu huona aibu kwa ajili ya matendo yaomabaya, nao huacha kufanya maba- ya mengine, kablahawajajua kwamba Kristo Yesu ndiye anayewavutakwake. Naye akizidi kuwavuta macho ili wamwangaliemsalabani na jinsi alivyopata maumivu kwa dhambizao, wao nao huzidi kufahamu ubaya wa mwenendowao wenyewe, na kujua namna ya haki yake Kristo.Nao huwa wanaanza kusema, “Je, dhambi ni kitu gani,ikiwa imetakiwa dhabihu kubwa namna hii kwakumwokoa mwenye dhambi? Je, upendo wa namnahii, maumivu haya yote, udhilifu huu, hivi vyote vilikuwani lazima ili sisi tusipotee mbali, bali tupewe uzima wamilele?” KY 28.2

Isipokuwa mtu amekataa kuvutwa kwake Kristo,Roho yake itazidi kuugeuza moyo wake mpakaametubu na kuongoka moyo. Mambo ya kiduniahayawezi kutuliza moyo wa binadamu. Furaha yakweli hupatikana katika kumjua Kristo tu. Kwa njia

nyingi, zinazojulikana na zisizojulikana, Mwokozianawavuta watu kwake ili waitoe mioyo yao mbali naanasa ya kidunia na kujua mibaraka ya Mungu isiyo namwisho. Wewe ambaye umetamani moyoni mwakokupata kilicho bora zaidi ya vyote vya kidunia, heri ujuekwamba kutamani huko ni ile sauti ya Munguanayosema kwako. KY 29.1

Pengine tumejisifu kwamba maisha yetu yamekuwasafi, dhamiri yetu imekuwa barabara, hatuna haja yakujitweza moyo mbele ya Mungu kama wabayawengine; lakini nuru ya Kristo ikituangaza roho zetu,tutaona hali yetu halisi, jinsi tunavyokuwa na unjisimachoni pake; ndipo tutakapofahamu jinsi haki yetuinavyokuwa kama vitambaa vichafu, tena ni damuyake Kristo peke yake ambayo huweza kutusafishamioyo unajisi wa dhambi, na kute ngeneza mioyo yetutena kuwa katika hali ya kufanana naye. KY 29.2

Mwonzi mmoja wa nuru ya utukufu wa Munguukiupenya moyoni, umetosha kutudhihirishia hali yetukatika dhambi, udhaifu wetu na upungufu wetu. Hivyotwatambua tamaa zetu zisizo safi, jinsi tunavyomkanaMungu mioyoni mwetu, na jinsi midomo yetuinavyotoa maneno yasiyofaa. Roho ya Munguikiupenya moyo ndani, na kumjulisha mtu hali yake yakumwasi Mungu, hapo ndipo hujichukia sanaakijilinganisha na Kristo jinsi alivyo safi bila mawaa yo

yote. KY 30.1

Nabii Daniel alipouona utukufu wa Mungualiyetumwa kwake, akabaini moyoni mwake, jinsiudhaifu na ukosefu wake ulivyokuwa mkubwa.Akasema, “Hazikusalia nguvu ndani yangu: kwaniuzuri wangu umebadilika mwangu kuwa uharibifu,wala sikuwa na nguvu.’ Danieli 10:8. Mtu akijiona hivyokuwa si safi, ndivyo atakavyotaka kuwa na moyo safina kuingia katika hali ya kupatana na amri za Munguna kufanana naye Kristo. KY 30.2

Paulo alipojichunguza aliona kwamba ka- tikamatendo ya nje, alikuwa, hana makosa; (Wafil. 3:6);lakini alipotambua matakwa ya sheria kwa njia yakiroho, alijiona kuwa ni mwenye dhambi kabisa.Alipojipima kwa maneno ya sheria za Mungu jinsiwanavyopima binadamu kwa matendo ya nje, Pauloalijiona kwamba amekuwa katika hali ya kutofanyamakosa, hakuwa na hatia; lakini alipoichunguza nakujua maana hasa ya sheria, akajiona jinsi Mungualivyomwona yeye, kuwa ni mwenye dhambi kabisa,naye akajishusha moyo na kuungama makosa yake.Alisema, “Na mimi nalikuwa hai hapo kwanza bilasheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, na miminikafa.” Warumi 7:9. Alipoona asili ya sheria, jinsiilivyokuwa ya kiroho, ndipo alipoona dhambi jinsiilivyokuwa ya uovu, naye hakujiona tena kuwa ni bora.

KY 30.3

Mungu hazioni dhambi zote kuwa ni sawa;zinakadirika mbalimbali machoni pa Mungu kama vilezinavyokadirika mbalimbali machoni pa binadamu pia.Lakini tendo baya liwalo lote, ingawa linaonekanakuwa ni dogo machoni pa binadamu, halihesabiwidogo machoni pa Mungu. Hukumu ya kibinadamu sikamili, kwa kuwa huona sehemu moja tu; hawezi kujuania ya ndani ya mtu; walakini Mungu hujua moyo tenahukadirisha mambo jinsi yalivyo halisi. Mlevihudharauliwa na wenziwe na kuambiwa kwambadhambi yake itamzuia asiingie mbinguni; lakini maranyingi makosa kama kufanya kiburi, kujifikiriamwenyewe bila kufikiri wengine, kuwa na choyo, namengineyo kama hayo hayakadiriwi na binadamu.Lakini makosa kama hayo yanachukiwa sana naMungu; kwa kuwa yamekuwa kinyume kabisa cha sifayake Mungu mwenyewe. Yule ambaye hufanyadhambi zinazohesabiwa na binadamu kuwa ni mbayasana - yaani ulevi, kuiba uzinzi na zingenezo - mtukama huyo huona aibu na namna anavyomhitajiKristo; lakini mwenye kufanya kiburi haoni lazimayake, naye humfungia Kristo asiingie moyoni mwake,na kwa hivyo hukosa kupata mibaraka yake. KY 31.1

Yule mtoza ushuru aliyeomba, “Mungu uniwie radhimimi mwenye dhambi,” alijiona kwamba yu mtu

mbaya sana, na wengine pia wakamwona hivyo; lakiniyeye alijua shida yake, naye alimletea Mungu mzigowake mzito wa dhambi kwa haya, ili Munguamrehemu na kumtoa katika utumwa wa dhambi.Luka 18:13. Yule mfarisayo aliyefanya kiburi nakujifanya mwenye haki katika sala yake, akaonyeshakwamba amemfungia Roho Mtakatifu mlango wa rohoyake, asiingie. Kwa hivyo hakujiona jinsi alivyo naunajisi; hakuona jinsi anavyouhitaji msada wa Kristo,naye hakupata kubarikiwa kamwe. KY 32.1

Ukitambua hali yako jinsi ulivyo katika dhambi,usingoje kumwendea Kristo mpaka umejaribumwenyewe kujitengeneza kuwa safi. Wengi hufikirikwamba hawawezi kumfikia Kristo kwa kuwa niwabaya. Je, unafikiri utapata kuwa mwema kwauwezo wako mwenyewe? “Aweza Mkushi kubadilingozi yake, au chui madoadoa, ndipo nanyi mtawezakutenda mema, mliofundishwa kutenda mabaya.” Yer.13:23. Hakuna msaada kwetu ila kwa Mungu tu. Sisiwenyewe hatuwezi kitu. Imetulazimu kwenda kwakeKristo kama tulivyo. KY 32.2

Hata hivyo tusijidanganye katika kufikiri kwambaMungu, kwa neema yake, atawaokoa hata walewanaotupilia mbali neema yake na rehema zake.Afikiriye hivyo, afadhali aitazame Kalwari. Kwa kuwahakuna njia nyingine ya kuwaokoa watu, kwa kuwa

bila dhabihu aliyoifanya Kristo katika kufa kwakemsalabani, binadamu asingeweza tena kuwa katikahali ya kupatana na watakatiu wa mbinguni - kwahivyo Kristo alichukua mwenyewe dhambi za wakosaji,akaadhibiwa kwa ajili yao. Upendo wa Mwana waMungu, maumivu yake, na kufa kwake, hivi vyotehushuhudia jinsi dhambi inavyokuwa kubwa mnomachoni pa Mungu; pia mambo hayo yatudhihirishiakwamba hakuna njia ya kuokoka na kutoka katikautawala wa uovu, hakuna matumaini ya uzima bora wamilele, ila kwa kujiweka chini ya mamlaka yake Kristona kumtii. KY 33.1

Wenye mioyo migumu wasiotubu, penginehujisingizia wakisema hivi juu yao wanaojidai kuwa niWakristo, “Hata mimi ni mtu mwema kwa kadiriwanavyokuwa wema wale. Wao hawajinyimi zaidiyamimi; mimi najiweza jinsi wafanyavyo. Wao piahupendezewa na anasa ya kidunia kamanipendezewavyo mimi.” Hivyo watu kama haohujisingizia kwa ajili ya makosa ya wengine iliwasifanye wajibu wao. Lakini kujisingizia hivyo haifaikitu; kwa kuwa Bwana ametuwekea mfano usio wakibinadamu: Mwana wa Mungu, asiye na hila walakosa lo lote, yeye ndiye mfano wetu. Wale ambaohunung’unika kwa ajili ya mwenendo mbaya wawengine wanaojidai kuwa ni Wakristo, imewapasa

kufuatisha maisha na matendo ya Kristo, nakuwatolea wengine namna ya mfano ulio bora.Wamejua namna iwapasavyo Wakristo kufanya; hivyowakikosa wenyewe kufanya yaliyo mema, makosa yaoni makubwa zaidi. KY 34.1

Tuangalie tusifanye usiri. Tusichelewe kuziachadhambi zetu na kutaka usafi wa moyo katika Yesu.Watu wengi hukosa katika jambo hilo; hukawia katikakujitoa kuwa wa Kristo; wafanyao hivyo wanaehaguakuishi katika hali ya kufanya dhambi. Kitu ambachotunakosa kukishinda, kitatushinda sisi nakutuangamiza. KY 34.2

Adamu na Hawa walijidanganya kwamba kulamatunda yaliyokatazwa si kosa kubwa linalowezakuadhibiwa kama Mungu alivyosema. Lakini katikajambo hilo dogo walihalifu amri takatifu ya Mungu,amri isiyobadilika; kwa hivyo binadamu akatengwambali na Mungu, tena kifo na taabu viliingia dunianimwetu. Kufa kwake Yesu katika Kalwari, kamadhabihu, kulikuwa njia ya pekee ya kufanya upatanishotena kati ya Mungu na binadamu. Tusidhanie dhambikwamba ni kitu kisicho na maana sana. KY 34.3

Kila tendo baya, kila mara unapoidharau na kuitupiliambali neema ya Kristo, moyo wako huzidi kuwamgumu, nia yako huzidi kuwa mbaya, nawe huzidi

kuwa katika hali ya kutosikia maombezi ya RohoMtakatifu moyoni mwako. KY 35.1

Watu wengi huwa wakijituliza dhamiri na mawazoyanayowasumbua, wakidhani kwamba watawezakugeuza mwenendo wao mbaya wakati wo wotewatakapo; wao hufikiri kwamba waweza kuacha nakutosikia wito wa Roho wakati mwingine, wakitumainiwatachomwa moyoni mara kwa mara baadaye. Lakinisivyo. Hata tabia mbaya moja tu, ama namna moja yatamaa isiyofaa, ikidumu moyoni itathibitisha moyokatika kutompenda Mungu. Kwa maonyo yote katikaBiblia juu ya kuchezacheza na maovu, lile la kututishazaidi ndilo hili, linalosema, “Maovu yake yatamkamatamwovu mwenyewe, naye atashikwa kwa kamba yadhambi yake.” Methali 5: 22. KY 35.2

Kristo amekuwa tayari kutuweka huru kwa dhambi,lakini halazimishi watu kwa nguvu; kama mtuamekusudia kufanya dhambi, naye hataki kupatauhuru katika Kristo, asitake kupokea neema yake,Kristo angefanya nini tena? Mtu akifanya hivyoamejiharibu mwenyewe kwa ajili ya kukana upendowake Kristo. Tumeambiwa, “Sasa ndio wakatiuliokubalika sana; tazama, sasa ndio siku ya wokovu.”“Leo, kama mtasikia sauti yake, msifanye migumumioyo yenu.” 2 Wakor. 6:2; Waeb. 3:7,8. KY 36.1

“Wanadamu hulitazama umbo la nje, lakini Bwanahutazama moyo.” 1 Sam. 16:7. Mungu huutazamamoyo wa kibinadamu jinsi ulivyo mkaidi, panapokuwaunajisi na udanganyifu. Mungu hutujua kabisa, moyowetu, dhamiri yetu, makusudi yetu na maazimio yetu.Nenda kwake jinsi ulivyo na moyo usio safi,ukamwambie, “Unitafutetafute, Ee Mungu, unijuemoyo; unijaribu, unijue mawazo; utazame kama njia yakukasirisha mwangu, unichukue kwa njia ya milele.”Zaburi 139:23, 24. KY 36.2

Watu wengi hukubali dini katika akili zao tu, nakufanya matendo matupu ya nje tu, bila kugeuzwamoyo. Imekupasa kuomba hivi, “Uniumbie moyo safi,Ee, Mungu; ufa- nye ndani yangu roho aminifu.” Zaburi51:10. Ni heri ujitahidi ili usipotewe na uzima wamilele, kwa jinsi watu wafanyavyo kujiokoa maisha yasasa wakiwa hatarini. Ni heri ufanye bidii katikakusoma Neno la Mungu pamoja na kuomba. KatikaNeno hilo, kwa njia ya amri za Mungu na maisha yaKristo, tumeonyeshwa asili ya utukufu, “ambaohapana mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao.”Waeb. 12:14. Neno lile husadikisha watu kuwa niwenye dhambi, tena huonyesha njia ya kupatawokovu. Ni heri ulisikilize kama sauti ya Munguinayosema nawe moyoni mwako. KY 36.3

Kama umefahamu dhambi jinsi ilivyo mbaya sana,

na kujiona mwenyewe jinsi ulivyo katika hali yakufanya dhambi, usikate tamaa. Kristo alikuja iliawaokoe wenye dhambi. Si juu yetu kufanya patanishokati ya Mungu na sisi, lakini katika Kristo, Mungumwenyewe alifanya patanisho. “Mungu alikuwa ndaniya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.” 2Wakor. 5:19. Hakuna hata mzazi wa kibinadamuambaye angefanya saburi juu ya makosa ya mwanawejinsi Mungu anavyofanya kwa wale atakao kuwaokoa.Ahadi zake zote, hata na maonyo yake yote, ni kwa ajiliya upendo wake tu, upendo usioelezeka hasa jinsiulivyo. KY 37.1

Kama Shetani anakuambia kwamba wewe nimwenye dhambi, mwangalie Mwokozi wako nakuongea juu ya tabia na sifa zake. Ziungame dhambizako na mwambie adui kwamba “Kristo Yesu alikujaulimwenguni, awaokoe wenye dhambi.” 1 Tim. 1:15.Yesu alimwuliza Simon swali juu ya wadeni wawili.Mmoja alikuwa anamwia bwana wake pesa kidogo, namwingine mapesa mengi, naye bwana yulealiwaachilia wote wawili; na Kristo akamwuliza Simonni nani atakayempenda bwana wake zaidi. Simonalimjibu, “Nadhani ni yule aliyesamehewa nayemengi.” Luka 7:43. KY 37.2

Sisi tumekosa sana, lakini Kristo alikufa ili tupatekuachiliwa dhambi. Wale ambao amewaachilia zaidi,

wao ndio watakaompenda zaidi na kukaa karibu naye,tena kumsifu zaidi katika ufalme wake kwa ajili yaupendo wake na dhabihu aliyoifanya kwa ajili yao. KY38.1

Tukifahamu sana upendo wa Mungu jinsi ulivyo,ndipo tutakapozidi kufahamu dhambi jinsi ilivyombaya mno. Na jinsi tunavyozidi kufahamu kamaKristo alivyojinyima kwa ajili yetu, ndivyo tutakavyozidikuchomwa moyo na kujitoa kwake kuwa watu wakekabisa. KY 38.2

Sura 4 - Kuungama Dhambi

MWENYE kusetiri makosa yake hatasitawi: kilaaziungamaye na kuziacha atarehemiwa.” Methali28:13. KY 39.1

Masharti yanayompasa mtu kufanya ili apaterehema ya Mungu si magumu, ni ya haki na ya maana.Bwana Mungu hataki tufanye mambo mazito ilitusamehewe dhambi; hasemi tufanye malipomakubwa kwa ajili ya dhambi zetu; asema tu kwambaanayeungama dhambi zake na kuziacha, ndiyeatakayerehemiwa. KY 39.2

Mtume Yakobo asema, “Ungameni makosa yenuninyi kwa ninyi, na kuombeana: mpate kuponywa.”Yak. 5:16. Ungama dhambi zako hasa kwa Mungu,ambaye yeye tu ndiye awezaye kuzisamehe; lakinimakosa ambayo umewafanyia wanadamu, basiuyaungame mbele ya wanadamu. Hivi ikiwaumemfanyia fulani yasiyofaa na kumchukiza kwa njiayo yote, nenda kwake na kuungama kosa lileulilomfanyia, naye amepasiwa kulisamehe kabisa.Nyuma yake imekupasa kuomba msamaha kwaMungu, kwa sababu huyo mwenzako ni kiumbe chaMungu, na kumfanyia mwanadamu mako- sa nikufanya makosa machoni pa Mungu pia. Hivyo kwa

njia ya kuomba, mambo hufika mbele ya Mwombeziwetu, Kuhani Mkuu wetu ambaye “alijaribiwasawasawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi,”naye awezaye “kuyachukua mambo yetu ya udhaifu,”huweza kutusafisha uchafu wote wa dhambi. KY 39.3

Wale ambao hawajajishusha moyo mbele ya Munguna kuziungama dhambi zao na kukiri kwambawametiwa hatiani, hao nao hawajafanya bado jambola kwanza lipasalo ili wapate kukubaliwa na Mungu.Isipokuwa tumemtubia Mungu kwa kweli, nakuchukizwa kabisa na maovu yetu, tumekuwa katikahali ya kutoomba kweli kwa kupata kusamehewadhambi zetu; hivyo hatujapata kweli amani ya Mungurohoni mwetu. Mtu akikiri dhambi zake, kukiri kwakelazima kuwa kwa moyoni; mtu akimtupia Mungu rohoyake yote, Mungu atamhurumia kweli. “Bwana yukokaribu yao wenye moyo uliovunjika, wenye rohoiliyopondeka huwaokoa.” Zaburi 34:18. KY 40.1

Katika kuungama kwa kweli, imepasa kukiri dhambiau kosa hasa jinsi lilivyo. Pengine ni dhambi ambazozimefaa kukiri wa kwa siri mbele ya Mungu tu; pengineni tendo baya lifaalo kukiriwa kwa mtu mmoja tu, yulealiyehasiriwa kwa tendo lile; au pengine ni kosa lifaalokukiriwa kwa wazi hadhara ya watu; hata ni dhambi aukosa la namna gani, mwenye kufanya kosa lazimakukiri kosa lile lile ambalo amelifanya. KY 40.2

Zamani wakati wa Samweli, Waisraeli walimwasiMungu; tena waliona taabu kwa ajili ya dhambi zao.Walikuwa hawamwamini Mungu jinsi alivyokuwa nauwezo na akili kwa kuwatawala vizuri. WalimtupiaMfalme Mkubwa kisogo, nao walitaka kutawaliwa kwajinsi yalivyotawaliwa mataifa mengine yaliyokuwakaribu nao. Na kabla ya kukubaliwa tena na Mungu,wakakiri hivi: “Tumeziongeza dhambi zetu kwa uovuwa kututakia mfalme.” 1 Sam. 12:19. Kosa lile ambalokwalo walitiwa hatiani, liliwalazimu kulikiri hasa. KY41.1

Kukiri kutupu hakutakubaliwa na Mungu bila kutubukwa kweli na kugeuka moyo na matendo na maisha;kila kitu kinachomchukiza Mungu lazima kutolewa ilimwenendo uwe safi machoni pake. Kazi iliyo wajibuwetu imeelezwa dhahiri hivi: “Osheni, safikeni; wekeenimbali uovu wa matendo yenu toka machoni pangu;acheni kutenda maovu; jifunzeni kutenda mema;takeni hukumu, msaidieni mwenye kuonewa,mhukumieni yatima, mteteeni mjane.” Isa. 1:16,17.“Mwovu atakaporudisha amana, akitoa tena aliyoitwaakwa unyang’anyi, akiendea sheria za uzima,asipotenda maovu; kuishi ataishi hatakufa.” Ezek.33:15. Mtume Paulo alisema hivi juu ya kutubu:“Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele zaMungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu:

naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, nahofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, nakisasi. Kwa kila njia mmejionyesha kuwa safi katikajambo hilo.” 2 Wakor. 7:11. KY 41.2

Kama maovu yametia giza macho ya kiroho,mwenye dhambi hawezi kutambua hali yake jinsialivyo na upungufu, na jinsi makosa yakeyanavyokuwa mabaya sana; tena isipokuwa atajitoa iliRoho Mtakatifu afanye kazi moyoni mwake, basiatadumu kuwa na giza la kiroho. Kukiri kwake si kwakweli wala kwa haki. Anapoungama kosa lakehujisingizia akisema kwamba laiti mamboyasingalikuwa hivi na hivi, asingalifanya hivi na hivi, nahivyo asingalipata kukaripiwa. KY 42.1

Adamu na Hawa walipokwisha kula matundayaliyokatazwa, waliona haya na hofu kuu. Mara yakwanza walifikiri namna ya kujitetea kosa lao, iliwaepukane na hukumu ya kifo. Mungu alipowaulizahabari za kosa lao, Adamu akawa kama anamlaumuMungu, akisema, “Mwanamke uliyenipa kuwa nami,ndiye aliyenipa ya mti, nikala.” Yule mwanamkealimshtaki nyoka akisema, “‘Nyoka alinidanganya,nikala.” Mwanzo 3:12,13. Inaonekana kwamba wotewawili walikuwa wanamsingizia Mungu, Adamu kwakuwa Mungu alimpa mwa- namke; tena Hawa kwa ajiliya kumwumba nyoka na kumwacha aingie katika

bustani ya Aden. Ile roho ya kujifanya kuwa na hakiilianzishwa na yule baba wa uwongo, nayo huonekanakwa wanadamu wote. Kukiri namna hii na kujisingizialiaifai kitu, wala hakukubaliwi na Mungu. Katika kutubuna kukiri kwa kweli, mtu hukubali kwamba ametiwahatiani bila kujisingizia wala kutaka kujifanya mwenyehaki. Huomba kama yule mtoza ushuru alivyoomba,na kusema, “Mungu uniwie radhi mimi mwenyedhambi;” asitake hata kuinua macho yake mbinguni.Hao nao wanaokiri makosa yao kwa namnawalivyotiwa hatiani, watapata msamaha, kwa kuwaYesu atawaombea kwa ajili ya damu yakealiyomwagika kwao wenye kutubu. KY 42.2

Katika Neno la Mungu twasoma habari juu yawengine wenye kutubu kwa kweli, na kujishushamioyo na kuziungama dhambi, wala hawakuwa namoyo wa kujisingizia ama kujifanya wenye haki. Fikirijinsi alivyosema Paulo, asitake kamwe kujiteteeamakosa yake;“Niliwafunga wengi miongoni mwawatakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amrina makuhani wakuu; na walipouawa nalitoa. idhiniyangu. Na mara nyingi katika masunagogi menginaliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaoneahasira kama nina wazimu, nikawaudhi hata katika mijiya ugenini.” Matendo 26:10, 11. Lakini hakuogopakusema, “Yesu Kristo alikuja ulimwenguni, awaokoe

wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.” 1 Tim. 1:15.Alijiona kuwa ni mwenye dhambi zaidi ya wenginewote. KY 43.1

Yule mnyenyekevu mwenye kupondeka moyo nakutubu kwa kweli, yeye atafahamu kidogo upendo waMungu, na dhabihu iliyofanywa Kalwari jinsi ilivyo nathamani kubwa sana. Tena jinsi mtotoatakavyoungama makosa yake mbele ya baba yakeanayempenda, hivyo ndivyo mweye kutubnatakavyomletea Mungu dhambi zake zote; kamailivyoandikwa, “Tukiziungama dhambi zetu, yu aminina wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafishaudhalimu wote. Yoh. 1:9 KY 44.1

Ninaye Rafiki, naye alinipenda mbele;Kwa kamba za pendo zake nimefungwa milele;Aukaza moyo wangu, nisitengane naye:Mimi wake, Yeye wangu; ndimi naye milele.

Ninaye Rafiki ndiye aliyenifilia;Alimwaga damu yake kwa watu wote pia;Sina kitu mimi tena, nikiwa navyo tele;Pia vyote ni amana, ndimi wake milele.

Ninaye Rafiki, naye yuna na moyo mwema:Ni Mlwalimu, Kiongozi, Mlinzi wa daima;Ni nani wa kunitenga na Mepnzi wa mbele?

Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele. KY 44.2

Sura 5 - Kujitoa Kuwa wa Mungu

MUNGU ameahidi hivi: “Nanyi mtanitafuta, na kuona,mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” Yer. 29:13.KY 45.1

Isipokuwa moyo mzima umetolewa kuwa wa Mungu,mtu hawezi kugeuzwa kuwa katika hali ya kufananana Mungu. Kwa hali yetu ya kibinadamu tumetengwambali na Mungu. Roho Mtakatifu ameeleza hali yetukuwa ni hii: “wafu kwa sababu ya makosa yenu nadhambi zenu;” “kichwa chote kigonjwa, moyo woteumezimia;” “hamna uzima.” Waef. 2:1; Isa. 1:5, 6.Mungu hutaka kutuponya na kutuweka huru. Kufanyahivyo ni kugeuza hali yetu kabisa, na kuifanya dhamiriyetu yote kuwa mpya; tena hayawezekani hayo ila sisitukijitoa kabisa kuwa wake Mungu. KY 45.2

Kupigana kule ambako mtu hupigana na nafsi yakemwenyewe, ni vita vikubwa kuliko vyote. Kujitoa hivyona kujisalimisha mkononi mwa Mungu, hakuwezekanibila mashindano moyoni; lakini isipokuwa mtuamejitoa na kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu,hawezi kabisa kusafishwa na kuwa katika hali yautakatifu. KY 45.3

Mungu hawashurutishi watu wamtii, bila kwanza

kuwaonyesha sababu ya maana yake, ili tupime kwaakili zetu jinsi ilivyo na kuchagua sisi wenyewe namnaya kufanya. “Njooni, tufanyane huja, asema Bwana.”Isa. 1:18. Mungu halazimishi watu. Anataka tumtii nakumcha kwa hiari yetu wenyewe, si kwa lazima.Anataka tujitoe kwake sisi wenyewe, ili kwa Roho yakeafanye kusudi lake mioyoni mwetu. Imekuwa juu yetusisi kuchagua kwa hiari yetu ili tuondolewe katikautumwa wa dhambi, na kuwekwa huru kuwa wana waMungu. KY 46.1

Na pia, tukijitoa kwa Mungu, hivyo imetupasa kuachavyote vinavyotaka kututenga mbali na Mungu.Mwokozi asema, “Kila mmoja wenu asiyeviacha vituvyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu.”Luka. 14:33. Hata jambo gani, liwalo lote, linalotuvutamacho kutoka kwa Mungu, lazima tuliache kabisa.Kupenda mali, kutaka fedha, ni kama minyororoinayofunga wengine kwa Shetani. Wengine hupendasifa na heshima ya watu, na mambo na anasa yadunia. Imekuwa ni lazima kuikatakata minyororo hiyoyote. Hatuwezi kumpenda Mungu kwa moyo nusu, nanusu kuipenda dunia na mambo yake. Hatuwezikuitwa watoto wa Mungu mpaka tutakapokuwa wakekabisa. Kuna wengine wanaosema kwambawanamtumikia Mungu, na huku hujitegemea nguvuzao wenyewe kwa kufuata sheria za Mungu na

kujipatia sifa njema na wokovu. Hawawi wakiamshwamioyoni na kufahamu upendo wa Kristo kamainavyopasa; bali hujaribu kufuata mambo ya kikristowakidhani kwamba kwa njia hiyo wataweza kujipatiamahali mbinguni. Dini ya namna hiyo haifai kitu. KY46.2

Inapokuwa Kristo anakaa rnoyoni, roho inajaaupendo wake, hupenda kuongea naye, huambatananaye; hivyo pia mtu anajisahau nafsi yake kabisa natamaa zake. Wale ambao hubidishwa moyoni kwa ajiliya upendo wa Kristo jinsi alivyojitoa kabisa kwa ajiliyao, hawafikiri kumtii Mungu kwa kad ri ya kutoshakukubaliwa naye; bali hutaka kufikilia kile kipeo chaKristo kwa kufuata matakwa yote ya Mwokozi wao. KY47.1

Je, umeona ya kwamba kujitoa kwa Kristo nikujinyima kupita kiasi? Jiulize hivi: “Kristo amefanyanini kwa ajili yangu?” Mwana wa Mungu alijitoa kabisa- maisha yake, kupendwa kwake, na kupata maumivu -ili apate kutukomboa. Na sisi je, wabaya wasiofaakupendwa sana hivi, twawezaje kumkataa mioyonimwetu? Tangu mwanzo wa maisha yetu tumepatamibaraka yake. Tungewezaje kumwangalia Yulealiyeumizwa kwa ajili ya dhambi zetu, na hukukutokubali upendo wake na dhabihu yake? Tukifikiri nakufahamu jinsi Yesu alivyojishusha kwa ajili yetu, sisi

tungewezaje kunung’unika kupata uzima kwa njia yakushindana na kujinyima na kujishusha mioyo? KY47.2

Kosa la wengi wanaojisifu mioyoni mwao ni kusemahivi: “Mbona imenipasa kutubu na kujishusha moyo ilinijue kwa yakini kwamba nimekubaliwa na Mungu?”Mtazame Kristo. Yeye alikuwa mahali pasipo dhambikabisa, tena zaidi ya hayo, alikuwa Mfalme wambinguni; lakini kwa ajili ya binadamu alihesabiwakuwa ni mwenye dhambi. Alihesabiwa “pamoja nawakosao: ila dhambi za wengi akazichukua yeye,akawaombea wakosao. Isa. 53:12. KY 48.1

Lakini sisi je, hata tukijitoa kabisa kwa ajili ya Kristo,tumetoa nini? Moyo uliochafuka kwa dhambi, ili Yesuautengeneze na kuusafisha kwa damu yake, nakutuokoa kwa upendo wake mkuu. Hata hivyowanadamu huona kwamba ni vigumu kujitoa kwakekabisa. Kusema hivyo ni haya tupu. KY 48.2

Mungu hataki tuache kitucho chote ambachokingekuwa na faida kwetu. Katika mambo yote, Munguanataka tu ili tuwe na hali njema. Wote ambaohawajamchagua Kristo bado, laiti wangefahamu yakwamba mambo ya dunia wanayoyataka, hayafai, kituyakilinganishwa na vitu vizuri ambavyo Kristo anatakakuwapa. Yule afuataye njia iliyokatazwa na Mungu,

hawezi kabisa kupata furaha ya kweli. Njia ya kufanyadhambi ni njia ya taabu na uharibifu. KY 48.3

Si vizuri kufikiri ya kwamba Mungu hupenda kuonawatoto wake wakipata kuumizwa na kuona uchungu.Anataka ili watoto wake wapate furaha tu. Baba yetualiye mbinguni anataka tuache kujaribu kujifurahishana anasa za dunia, ambazo huleta maumivu nakulegea moyo kwa ajili ya kutopata raha na furahajinsi inavyotazamiwa; na pia anasa zile zitatufungiamlango wa furaha ya mbinguni. Mwokozi hukubaliwatu jinsi walivyo, pamoja na mahitaji yao, upungufuwao, na udhaifu wao; tena pamoja na kuwasafishamoyo na kuwakomboa kwa damu yake, piaataridhisha mioyo ya wote watakaomjia kwa ajili yamkate wa uzima. Matakwa yake ni haya; tufanyemambo hayo tu yatakayotuongoza katika njia ya kweli,ili tufikilie kipeo cha furaha kisichoweza kufikiliwa nawale wasiomtii Mungu. Na kama Kristo anakaa ndani,hivyo ndivyo moyo huwa na furaha ya kweli. KY 49.1

Wengi wanauliza hivi: “Nawezaje kujitoa kwakeMungu?” Kweli umetaka kujitoa kwake, lakiniumekuwa dhaifu katika dhamiri yako, una mashakamoyoni, umefungwa na mazoezi na matendo yadhambi. Huwezi kutimiza ahadi na maazimio yako.Huwezi kutawala fikara zako, nia yako, wala mapenziyako. Tena kama unafikiria hayo yote, unashuka moyo

na kudhani ya kwamba hutakubaliwa na Mungu; lakiniusikate tamaa. Jambo kubwa la kufahamu ni hili:Mungu ametupa sisi uwezo wa kuchagua kwa hiarizetu jinsi tutakavyofanya. Wewe mwenyewe huwezikugeuza moyo wako; huwezi kwa nguvu zako mpakaMungu upendo wa moyo wako; lakini wawezakuchagua kama unataka kumtii Mungu na kufanyamapenzi yake. Mpe nia yako na dhamiri yako ili apatekuitawala; ndipo Mungu atakapoweza kufanya kaziyako moyoni mwako, ili kutaka kwako na kutendakwako kupatane na kusudi lake jema. Hivyo utajiwekachini ya mamlaka ya Kristo; upendo wako utavutwakwake, utapatana na Kristo katika fikara zako. KY 49.2

Kutaka mema na usafi ni vizuri; lakini kutaka tuhaifai kitu. Wengi watapotea wakiwa wanatamani tukuwa Wakristo, kwa kuwa wanakosa kujiweka chini yamamlaka ya Mungu katika dhamiri zao; huchelewakuchagua kabisa ya kwamba watakuwa Wakristosasa. KY 50.1

Ukitumia nia na dhamiri yako kwa njia ya kweli, haliya maisha yako itageuka kabisa. Kama ukijiweka chiniya mamlaka ya Kristo, unajiunga na uwezo wa kupitauwezo mwingi- ne wo wote. Utakuwa na nguvu itokayojuu iwezayo kukuimarisha kabisa; tena kwa njia yakujitoa na kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu kilasiku, utajaliwa kushi maisha mapya, maisha ya

kumwamini Mungu daima. KY 50.2

Naendea msalaba, miye mnyonge na mpofu,Yapitayo naacha, nipone msalabani.

Nakulilia sana: nalemewa na dhambi;Pole Yesu asema: “Nitazifuta zote.

Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,Roho yangu na mwili viwe vyako milele.

Kwa damu yake sasa nimegeuka roho,Nikaziacha tamaa, nimtafute Yesu tu.

Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu;Nainamia kwako; niponye Mponya wangu.

Yesu yuaja tena! Nimepevuka kwake,Kila chembe kamili; msifuni yeye Mponya. KY 51.1

Sura 6 - Kumwamini Mungu na KukubaliwaNaye

KWA jinsi dhamiri na roho yako vilivyohuishwa naRoho Mtakatifu, hivyo unazidi kufahamu ubaya wadhambi, nguvu zake, na jinsi inavyoleta taabu; tenaunazidi kuchukizwa nayo moyoni. Huona kwamba kwaajili ya dhambi umepata kutengwa na Mungu, naweumekuwa umefungwa na uovu. Huwezi kamwekujisaidia mwenyewe. Nia yako si safi, tena moyowako huwa najisi. Umefahamu kwamba maisha yakohujaa dhambi na mambo ya kujipendeza nafsi yakomwenyewe. Wataka sana kusamehewa makosa yako,ili upate kutakaswa na kuwekwa huru kutoka utumwawa Shetani. Kupatana na Mungu, na kufanana naye, nakuwa salama moyoni, - waweza kufanya nini ili uwekatika hali hiyo? KY 52.1

Hali hii haiwezi kununuliwa kwa fedha, piahaipatikani kwa ajili ya akili wala elimu; tena huwezikutumaini kuwa katika hali hiyo kwa juhudi yakomwenyewe. Bali utaipata bure mkononi mwa Mungukama karama yake, “pasipo fedha na pasipo thamani.”Isa. 55:1. Ni juu yako tu kuichukua. Mungu asema,“Dhambi zenu zikiwa kama bendera (nyekundu),zitakuwa nyeupe kama theluji; zikiwa nyekundunyekundu mno, zitakuwa kama sufu.” Isa. 1:18. “Nami

nitawapa ninyi moyo mpya, roho mpya nitatia ndaniyenu.” Ezek. 36:26. KY 52.2

Basi, umeziungama dhambi zako na kuziweka mbalina moyo wako. Pia umeazimia kujitoa kuwa mtu waMungu. Sasa nenda kwake, na kumwomba iliakusafishe dhambi zako zote, akupe moyo mpya.Ndipo usadiki kwamba amefanya hivyo kwa kuwandivyo alivyoahidi. Yesu alipokuwa hapa duniani, alitoafundisho lile, kwamba imetulazimu kusadiki ya kuwatumepata upaji wa Mungu aliotuahidi, ndivyoutakavyokuwa wetu. Yesu aliwaponya watu maradhiyao walipouamini uwezo wake. Aliwasaidia katikamambo waliyoweza kuyaona na macho ya kimwili, iliwapate kumtumainia juu ya mambo wasiyowezakuyaona, yaani, wapate kusadiki uwezo wake katikakuwasamehe dhambi zao. Hivyo ndivyo alivyosemadhahiri katika kumponya yule mgonjwa wa kupooza:“Ili mjue ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlakakatika dunia kuondoa dhambi, (amwambia yulemgonjwa wa kupooza), Ondoka, ujitwike kita- ndachako, ukaende nyumbani kwako.” Mattayo 9: 6.Mtume Yohana pia, aliposema juu ya miujiza ya Kristo,alisema hivi: “Hizi zimeandikwa mpate kuaminikwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwakuamini mwe na uzima kwa jina lake.” Yoh. 20: 31. KY53.1

Hivyo tukisoma habari katika Biblia jinsi Yesualivyoponya wagonjwa wa kimwili, twawezakufundishwa na kufahamu namna ya kumsadiki kuwakweli anaweza kuachilia na kuondoa dhambi. Tusomejuu ya yule mgonjwa wa kupooza. Alikuwa hoi kwaugonjwa tangu miaka thelathini na minane, asiwezekwenda kwa miguu. Walakini Yesu alimwambia,“Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende.” Yulemgonjwa angaliweza kusema: “Bwana, kamautaniponya, nitafanya usemavyo.” Lakini sivyo.Alikubali neno la Kristo, alisadiki kwamba amepona,akajitahidi mara moja; alifanya jinsi Kristoalivyomwamuru, ndipo Mungu akamtolea nguvu zake,naye mgonjwa akapona mara, akawa mtu mzima. KY54.1

Hivyo ndivyo ilivyo kwako mwenye dhambi. Huwezikulipia ukosefu wako, huwezi kugeuza moyo wako nakujitakasa mwenyewe kuwa safi. Lakini Munguameahidi kwamba atakufanyia hivyo katika Kristo.Unakubali hivyo? Na kwa jinsi unavyoziungamadhambi zako, na kujitoa kwa Mungu na kuazimiakumtumikia, ndivyo Mungu atakavyotekeleza ahadiyake, nawe utaachiliwa dhambi na kutakaswa; nautakuwa mtu mzima jinsi yule mgonjwa wa kupoozaalivyowezeshwa na Kristo kwenda kwa miguu maraaliposadiki kwamba amepona. Ikiwa unaamini kama

yule, ndivyo utakavyopata kupona katika dhambi. KY54.2

Yesu asema, “Yo yote myaombayo mkisali, amininiya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Marko11:24. Lakini kuna masharti juu yetu ili ahadi hiiitimizwe, - tuombe kama vile apendavyo Mungu. Tenani mapenzi ya Mungu kutuondolea dhambi zetu nakututakasa, ili tuwe watoto wake na kuishi maishayaliyo safi kwa uwezo wake Mungu. Kwa hivyotwaweza kumwomba Mungu mibaraka hii, na kuaminikwamba tumeipata, na kumshukuru Mungu kwa kuwakweli tumeipata mibaraka yake. Ni jambo linalotuhusu,kwenda kwake Yesu na kutakaswa, na kuhesabiwakuwa ni safi bila lawama, na pasipo kuaibishwa “Sasa,basi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu,wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili balimambo ya Roho. “Warumi 8:1. KY 55.1

Toka sasa mwili wako si wako mwenyewe;umenunuliwa na bei kubwa. “Hamkukombolewa kwavitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu, . . . bali kwadamu ya thamani, kama ya mwana kondoo asiye nahila, na asiye na waa, ya Kristo, aliyejuliwa tanguzamani.” 1 Petro 1: 18-20. Kwa kumwamini Mungu tu,Roho Mtakatifu ameanzisha, uzima mpya moyonimwako. Sasa umekuwa kama mtoto aliyezaliwa kwakiroho kuwa katika watu wa nyumba ya Mungu, naye

anakupenda namna ampendavyo Mwana wake. KY55.2

Sasa kama umejitoa kuwa wa Yesu, usirudi nyumatena kutoka mkononi mwake. Kila siku heri useme,“Mimi ndimi wake Kristo; nimejitoa kwake;” tenaumwombe Roho yake akulinde kwa neema yake.Ulipata kuwa mtoto wa Mungu kwa njia ya kujitoakwake na kumwamini; hivyo ndivyo utakavyofanya kilasiku ili uishi katika Kristo. “Basi, kama mlivyompokeaKristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye.”Wakol. 2:6. KY 56.1

Wengine hufikiri kwamba ni lazima kuwa na wakatiwa kujaribiwa na kumdhihirishia Mungu ya kuwawameongoka kabla ya kuweza kupata mibaraka yake.Lakini sivyo. Waweza kupata mbaraka wa Mungumara. Lazima wawe na Roho ya Kristo mioyoni mwao,kuwasaidia udhaifu wao katika kushindana na maovu.Yesu apenda ili tumwendee jinsi tulivyo, - wenyedhambi, wadhaifu, wasioweza kujiokoa wenyewe.Hata kama tumefanya mabaya ya namna gani,tusiogope kufika kwake. Atatupokea kwa moyo waupendo, naye anakubali kututakasa makosa na unajisiwo wote. KY 56.2

Wengi huanguka katika neno hili; hawaaminikwamba Yesu anawasamehe wao wenye- we hasa.

Hawakubali ya kuwa jinsi Mungu asemavyo, ndivyoilivyo. Ni haki ya watu wote wanaoyatimiza mashartiya Mungu, kujua kwa hakika kwamba kuna masamahakwa kila dhambi. Ahadi za Mungu ni kwa kila mkosajimwenye kutubu. Hata mwenye kufanya dhambi iwayoyote, hakuna asiyeweza kupata nguvu, na usafi, nakuwa mwenye haki katika Kristo Yesu aliyekufa kwaajili yetu. Huwaambia waishi, na wasife. KY 56.3

Mungu hatutendei jinsi binadamu wanavyowatendeawenzao. Yu mwenye rehema, upendo, na huruma.Asema, “Aache mwovu njia yake, na mtu mbayamawazo yake; akamrudie BWANA, naye atawarehemu;na kwa Mungu wetu, kwani mkarimu kuachilia.”“Nimefuta, kama wingu zito, makosa yako, na, kamawingu, dhambi zako.” Isa. 55:7; 44:22. KY 57.1

“Kwani sikifurahii kifo chake afaye, anena BwanaMungu: basi geukeni, mkaishi.” Ezek. 18:32. Shetani yutayari kila mara kutudanganya ya kwamba ahadi zaMungu si kwa watu kama sisi. Lakini tusisikilizemaneno yake, bali tuseme hivi moyoni: Yesu alikufakwa ajili yangu, niwe na uzima. Anipenda mimi; atakanisife. Baba yangu aliye mbinguni ni mwenye huruma;na ingawa nimemtendea vibaya, na ingawanimepoteza mibaraka yake kwa siku zilizopita, kwavile anavyonipenda nitaondoka na kwenda kwa Babana kusema, “Baba, nimekosa juu ya mbingu, na mbele

yako; sistahili kuitwa mwana wako baada ya hayo;unifanye kuwa kama mmojawapo wa watumishiwako.” Mfano ule wa Mwana Mpotevu kuonyeshanamna Mungu anavyowapokea wanaokuja kwake;“Alipokuwa angali mbali, baba yake akamwona,akamhurumia, akapiga mbio, akamwangukia shingoni,akambusu sana.” Luka 15: 18-20. KY 57.2

Na hata mfano huu umepungukiwa kuonyesha sawanamna ya upendo na huruma ya Baba aliye mbinguni,kwa kuwa huruma yake haina kifani. Mungu asema,“Kupenda nimekupenda mapenzi ya milele; kwa hiyo nawema nimekuvutia.” Yer. 31:3. Mwenye dhambiingawa angali mbali na Baba yake, yuleBabaanamhurumia moyoni mwake na kumtaka sana.Na kila mpotevu asikiaye moyoni mwake kwambaanataka kumrudia Mungu, ameona hivyo kwa kuwaRoho Mtakatifu anamvuta kwa Baba ampendaye sana.KY 58.1

Kama umezijua ahadi njema za Mungu zilizoandikwakatika Biblia, wawezaje kuona mashaka moyoni?Wawezaje kudhani kwamba Mungu angemkataamwenye kumfikilia na kutubu? Fikara kama hiziziondolewe mbali kabisa! Katika kumdhania Baba yetuhivi, unajihatarisha moyo wako mwenyewe. Ni kwelikama Mungu huchukizwa na maovu, lakini humpendamwanadamu mpotevu, hata akajitoa pamoja na Kristo,

ili aliye yote amwaminiye apate kuokoka na kurithiurithi wa milele katika ufalme wake mtukufu.Angeweza kusema nini tena zaidi ya hayoaliyoyasema kwa kuonyesha jinsi anavyotupenda sisi?Asema, “Aweza mwanamke kusahau mtoto wakeanyonyaye, asimrehemu mwana wa tumbo lake? hatawaweza hawa kusahau, ila siwezi mimi kukusahauwewe.” Isa. 49:15. KY 58.2

Inueni macho, ninyi mlio na mashaka na wenyekuogopa; Yesu ndiye Mwombezi wetu. MshukuruMungu kwa ajili ya Mwanawe Mpendwa, nakumwomba msaada wake ili isionekane kwamba kufakwa Yesu kumekuwa bure kwako. Roho Mtakatifuanakuita hivi leo. Mtolee Yesu moyo wako mzima, iliupate mbaraka wake. KY 59.1

Nawe ukisoma ahadi zake, kumbuka kwamba yotehusemwa kwa upendo na huruma. “Katika yeye tunaukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi kwawingi wa neema yake.” Waef. 1:7. Ndiyo, usadiki tu yakuwa Mungu ni msaidizi wako. Anataka kuwarudishawanadamu katika hali yao ya kwanza, kwa jinsialivyowaumba kwa mfano wa Mungu. Naweukimkaribia Mungu na kuziungama dhambi zako nakutubu, yeye pia atakukaribia kwa moyo wa rehema namasamaha. KY 59.2

Sura 7 - Dalili ya Kuwa Wanafunzi wa Kristo

MTU akiwa ndani ya Kristo, ni kiumbe kipya; vya kalevimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.” 2 Wakor.5:17. KY 61.1

Pengine mtu hawezi kutaja siku wala mahali hasaalipoongoka kuwa mfuasi wa Kristo; lakini kukosakufanya hivyo si kama kusema kwamba yulehakuongoka kweli. Kristo alimwambia Nikodemo,“Upepo huenda utakako, na sauti yake waisikia, lakinihujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na kilamtu aliyezaliwa kwa Roho.” Yoh. 3:8. Upepo hauwezikuonekana, lakini twasikia na kuona matendo yake; navilevile Roho ya Mungu inajulikana kwa namna yamatendo yake mioyoni mwa wanadamu. Uwezo wake,usionekane na macho ya kibinadamu, huanzishamaisha mapya moyoni; humwumba mtu kuwa mpyakwa mfano wa Mungu. Ijapokuwa kazi ya Rohoinatendeka kwa kimya, tena haionekani; matokeo yakeyamekuwa waziwazi. Kama Roho Mtakatifuametengeneza moyo kuwa mpya, jambo hilolitaonekana katika maisha yake aliyeongoka moyo.Ingawa sisi wenyewe hatuwezi kugeuza mioyo yetu,ama kuzifanyiza nia zetu kupatana na Mungu; tenahaifai kabisa kujitegemea wenyewe kwa matendo yetuyaliyo mema; walakini, kwa namna ya maisha yetu,

itajulikana kama tunayo neema ya Mungu mioyonimwetu. Itaonekana kwamba tabia zetu, desturi zetu,mazoea yetu, na mambo yetu yote yamegeuka kuwambalimbali na yale ya zamani. Tabia na desturi za mtufulani zinajulikana si kwa matendo mema au mabayaya siku moja moja tu, ila kwa maelekezo ya matendoyake na maneno yake, na mazoea yake ya siku zote.KY 61.2

Ni kweli ya kuwa kuna watu ambao mienendo yao nimyema machoni pa wenzao, bila kuongoka moyo kwaajili ya Kristo. Kwa sababu ya kupenda kusifiwa nakuwa kama waongozi kati ya wengine, hivyo hujilindaili waonekane kuwa ni wenye adabu. Kwa ajili yakujistahi nafsi zao, huyaepuka matendo mabaya yanje. Hata mwenye kuzoea kujifikiria nafsi yakemwenyewe na kujipendeza, pengine anafanya mema.Ikiwa ni hivyo, twawezaje kuyakinisha kama tumekuwaupande wa Kristo, au sivyo? KY 62.1

Ni nani anayeutawala moyo? Fikara zetu ni juu yanini? Tunazoea kuzungumza juu ya nani? Ni naniambaye tunampenda zaidi na kumtumikia? Ikiwa tuwatu wa Kristo, fikara zetu ni juu yake. Tunajitoakwake pamoja na vyote tulivyo navyo. Twatakakufanana naye, kuwa na Roho yake mioyoni, kufanyamapenzi yake na kumpendeza kwa mambo yote. KY62.2

Wale wanaokuwa wapya katika Kristo Yesu, hao naowatazaa matunda ya Roho, yaani, “upendo, furaha,amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole,kiasi.” Wagal. 5:22, 23. Hawatafuata tamaa zao zazamani, bali watamwamini Mwana wa Mungu nakufuata nyayo zake; tabia zake zitaonekana katikamaisha yao, watatakaswa kuwa safi kama yeye alivyomtakatifu. Mambo waliyochukizwa nayo zamani, sasawanayapenda; na vile walivyopenda zamani, sasahuchukizwa navyo. Yule aliyefanya kiburi, sasa huwampole na mnyenyekevu. Mlevi huacha ulevi wake,mwasherati na mzinzi huachana na matendo yao yazamani, na kuwa watu safi. Mkristo hafuati anasa namvao na mambo ya kidunia. Hataki kufanana na watuwa dunia kwa “kujipamba kwa nje,” “ila mtu wa moyoniasiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho yaupole na utulivu iliyo ya thamani kuu mbele yaMungu.” 1 Petro 3:3, 4. KY 63.1

Toba si ya kweli isipokuwa imeonekana dhahirikwamba mtu huongoka moyo na kufanya yaliyomema. Kama mtu anarudisha amana yake, na kutoatena aliyoitwaa kwa unyang’anyi, kuziungama dhambizake, kumpenda Mungu na wenziwe, yule aliyemwenye dhambi anaweza kutumaini kwamba“amepita toka mauti hata uzima.” Yoh. 5:24. KY 63.2

Sisi wanadamu ambao tungali wabaya, tukimfikilia

Kristo na kupata kusamehewa dhambi zetu, hali yetuinageuka kabisa. Upendo huonekana moyoni.Twapata furaha katika kufanya yaliyo wajibu wetu sisiWakristo; twapenda kujinyima kwa ajili yake Kristo.Zamani tulikuwa gizani, na sasa tuko katika nuru yakealiye “Jua la haki.” KY 64.1

Tabia za Kristo zitaonekana katika wafuasi wake.Yeye alijitoa kufanya mapenzi ya Mungu kwa kuwaalimpenda Mungu. Mungu ni upendo. Upendo wakweli hutoka kwa Mungu; pia unapatikana katika moyoule tu ambao Yesu huutawala. Haupatikani kamwekatika moyo usioongoka na kujitoa kuwa wa Mungu.“Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupendasisi.” 1 Yoh. 4:19. Upendo wa Mungu ukiwa humomioyoni mwetu, maisha yetu yatakuwa safi, hatawengine katika jirani zetu watavutwa moyo na kutakakutengeneza maisha yao kuwa safi, hasa kwa ajili yamfano mwema wao walio Wakristo wema. KY 64.2

Kuna makosa mawili ambayo watu wa Munguhawana budi kujihadhari nayo. La kwanza,kujitumainia matendo mema yao wenyewe iliwapatane na Mungu. Hakuna awezaye kujitakasamwenyewe ila kwa njia ya kuamini neema na msaadawa Kristo. KY 64.3

Kosa la pili litupasalo sisi kuwa na hadhari nalo ni

kinyume cha lile la kwanza, ndilo kufikiri kwambahatuna haja kuzishika sheria za Mungu; wenginehufikiri ya kuwa kama tumewekwa haki kwa neema yaKristo tu, basi hakuna inayotakiwa juu yetu ili tupatewokovu katika Kristo. Lakini sivyo kabisa. KY 65.1

Angalia ya kwamba kumtii Mungu siyo kwa matendoya nje yanayoonekana tu, bali kwa mambo ya moyo naupendo. Kumpenda Mungu ni asili ya kumtii.Mwanadamu awapo na upendo moyoni na kuwakatika mfano wa Yule aliyemwumba, ndipoinapotimizwa ahadi ya Agano Jipya ya Mungu jinsiinavyoandikwa, “Nitatia sheria zangu mioyoni mwao,na katika akili zao nitaziandika.” Waeb. 10:16. Nasheria ikiwamo moyoni, itakuwa inaongoza katikamambo yote ya maisha ya mwanadamu. KumtiiMungu kwa sababu ya kumpenda, hiyo ndiyo dalili yakweli kama mtu fulani ni mfuasi wake, Imeandikwahivi katika Biblia, “Huku ndiko kumpenda Mungu,kuzishika amri zake.” “yeye asemaye, Nimemjua, nayehazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndaniyake. 1 Yoh. 5:3;2:4, Hivyo twaona ya kwambaimetakiwa ili tumtii Mungu na kuzishika amri zake;lakini kwa kumwamini Kristo tu tutaweza kumtii kwanjia ya kweli. KY 65.2

Hatuwezi kustahili wokovu kwa ajili ya utii wetu;wokovu ni thawabu ya Mungu iliyotolewa bure, nasi

tunaipokea kwa kumwamini Mungu. Na kumtii Munguhufuatana na kumwamini. “Mnajua ya kuwa yeyealidhihiri ili aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimondani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi;kila atendaye dhambi hakumwona, walahakumtambua.” 1 Yoh. 3:5, 6. Hiyo ndiyo dalili ya kweliinayodhihirisha kama mwanadamu ni mfuasi waKristo. Kama tunakaa ndani ya Kristo, na upendo waMungu hukaa mioyoni mwetu, ndipo mawazo namatendo yetu yatakapopatana na mapenzi ya Mungujinsi yanavyonenwa katika amri zake takatifu.“Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyaye haki yunahaki; kama yeye alivyo na haki.” 1 Yoh. 3:7. Namna yahaki inayotakiwa na Mungu imeelezwa kwa kipimocha sheria yake, jinsi inavyonenwa katika zile amrikumi zilizotolewa na Mungu katika mlima wa Sinai. KY66.1

Kusema ya kuwa tunamwamini Kristo, na hukukusema kwamba hatuna haja kumtii Mungu kwamambo ya amri zake, hiyo si kuamini kwa kweli, bali nikama kufanya kiburi tu, maana “mmeokolewa kwaneema, kwa njia ya imani.” Waef. 2:8. Lakini “imaniisipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake.” Yak.2:17. Na Yesu, kabla ya kuja kwake duniani, alisema,“Kufanya mapensi yako, Ee Mungu wangu, ndio furahayangu; na sheria yako imo ndani ya moyo wangu.”

Zab. 40:8. Tena kabla ya kurudi kwake mbingunialisema, “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendolangu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu,na kukaa katika pendo lake.” Yoh. 15:10. Tena katikaMaandiko imeandikwa hivi: “Na hivi twajua ya kuwatumemjua, ikiwa tunashika amri zake. . . Hivi twajua yakuwa tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwaanakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewevilevile kama yeye alivyoenenda.” “Maana Kristo nayealiteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuatenyayo zake.” 1 Yoh. 2:3-6; 1 Petro 2:21. KY 66.2

Sharti la kupata uzima wa milele limekuwa mojatangu zamani, - jinsi lilivyokuwa katika bustani ya Adenkabla Adamu na Hawa hawajaanguka na kufanyadhambi, - ndilo hili, kumtii Mungu kwa ukamilifu katikamambo yote ya amri zake, kuwa na haki kamilifukatika Kristo. Sisi peke yetu hatuna haki kabisa, ilakwa Kristo tu. Yesu alikaa hapa duniani, akajaribiwakama sisi. Akaishi maisha yaliyo makamilifu pasipodhambi. Akafa kwa ajili yetu; akajitoa badala yetu;alikubali kuzichu- kua dhambi zetu ili sisi tupatekupewa haki kwake. Kama unajitoa kwake, uakumkubali kuwa ni Mwokozi wako, ijapokuwaumekuwa mwenye dhambi kabisa, utahesabiwa kuwamwenye haki katika Kristo. Sifa njema ya Kristoitahesabiwa kuwa ni yako, nawe utakuwa katika hali

ya kukubaliwa na Mungu kana kwamba hukufanyadhambi kabisa. KY 67.1

Zaidi ya hayo, Kristo huigeuza hali ya moyo jinsiilivyo. Hukaa ndani ya moyo wako kwa njia ya kuamini.Nawe imekupasa kuendelea kumwamini Kristo nakumtolea nia yako siku zote ili upate kumshiriki Kristodaima; na kwa kadiri unavyoendelea kufanya hivyo,ndivyo atakavyotenda kazi ndani yako, ili kutakakwako na kutenda kwako vipatane na kusudi lakejema. Ndipo utaweza kusema, ‘‘Uhai nilio nasa katikamwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungualiyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.”Wagal. 2:20. Ndivyo Kristo alivyowaambia wanafunziwake: “Kwa kuwa si ninyi msemao, bali Roho ya Babayenu asemaye ndani yenu.” Mattayo 10:20. Na kamaKristo atenda kazi ndani yako, utakuwa na nia sawa nania iliyokuwamo ndani ya Kristo na kutenda matendokama vile alivyotenda yeye - matendo yaliyo ya kaki, nakumtii Mungu. KY 68.1

Basi, hatuna kitu chema ndani yetu cha kujisifunacho. Hatuna sababu ya kujitukuza. Tumaini letupekee ni katika haki ya Kristo: ya kwamba itahesabiwakwetu kama ni yetu wenyewe: tena katika haki hiyo,ikitendeka ndani yetu kwa kazi ya Roho Mtakatifu. KY68.2

Tukisema juu ya imani, lazima tufahamu ya kwambakuna tofauti kati ya kusadiki tu ya kuwa Mungu yu hai,na kumwamini kabisa katika moyo. Hata Shetani namalaika wabaya huamini ya kuwa Mungu yuko;huamini uwezo wake, na maneno yake jinsi yalivyo yakweli: ni mambo wasiyoweza kuyakana. Bibliainasema, “Mashetani nao waamini na kutetemeka,”Yak. 2:19; lakini hiyo siyo imani ya kweli. Mwarninifuwa kweli hujitoa kabisa kuwa wa Mungu na kufanyamapenzi yake. Kwa imani ya kweli moyounatengenezwa kuwa mpya kwa mfano wa Mungu.Moyo na nia ya mwili, iliyo katika hali ya zamani, haitiisheria ya Mungu wala haiwezi; bali yule aliyeongokamoyo, sasa hupata furaha katika amri zake, nakusema “Nimeipendaje sheria yako! Ndio fikara yangumchana kuchwa.” Zab. 119:97. Na hivyo “wemauagizwao na torati unatimizwa ndani yetu,”tusioenenda “kwa kufuata mambo ya mwili, balimambo ya roho.” Warumi 8:4,1. KY 69.1

Kuna wengine ambao wamejua upendo wa Kristo najinsi anavyowasamehe dhambi zao, nao wanatakasana kuwa watoto wa Mungu; walakini wanaona yakwamba sifa yao si kamili, na maisha yao si sawa.Hao wamekaribia kuona shaka kama kweli mioyo yaoimefanywa mipya na Roho Mtakatifu. Na wote wanamna hiyo nawaambia hivi: Msife moyo ninyi, wala

kurudi nyuma. Mara kwa mara tutalazimishwakumwendea Yesu tukihuzunika kwa ajili ya makosayetu; lakini haifai kushushwa moyo. Ingawatumeshindwa na adui, Mungu hatatuacha nakututupilia mbali. Sivyo; mtume Yohana aliandika, “Naijapo mtu akatenda dhambi, tuna Mwombezi kwaBaba, Yesu Kaisto mwenye haki.” 1 Yoh. 2:1. Tenatusisahau maneno yake Kristo: “Baba mwenyeweawapenda ninyi.” Yoh. 16:27. Mungu anatakakukurudisha kwake mwenyewe, na kuona mfano wakendani yako jinsi Yeye alivyo safi na mtakatifu. Endeleakuomba kwa moyo wa bidii zaidi; na kumwaminiMungu kabisa. Na kwa jinsi tunavyopunguakujitegemea uwezo wetu wenyewe, tuzidi kutegemeana kutumainia uwezo wa Mwokozi wetu na kumsifu.KY 69.2

Na kwa vile unavyozidi kumkaribia Yesu, hivyoutazidi kujiona mwenyewe kuwa u mwenye makosazaidi; kwa kuwa macho ya kiroho yatazidi kuwa safi yakufahamu namna ya ukosefu na upungufu wako, kwavile unavyomtazama Yesu na kujilinganisha naye jinsialivyo mkamilifu. KY 70.1

Mtu asiyefahamu hali yake jinsi alivyo mbaya namwenye dhambi, yule hawezi kumpenda Yesu sanamoyoni mwake; bali yule ambaye ameongoka moyokwa neema ya Kristo, yeye atamheshimu Kristo

kwaajili ya sifa yake njema. Lakini isipokuwatumefahamu hali yetu katika dhambi, tunabainisha yakwamba hatujaona bado uzuri na ubora wa Kristo. KY70.2

Kwa jinsi tunavyopungua kujiona tu bora wenyewe,ndivyo tutakavyozidi kumheshimu Mwokozi wetu kwawema na utakatifu wake. Mtu anapofahamu udhaifuwake na kumtaka Kristo, Kristo naye atamsaidia nakumjulisha uwezo wake. Na kwa vile tunavyozidikuona ubora na sifa ya Kristo, ndivyo tutakavyozidikuwa katika mfano wake. KY 71.1

Yesu kwetu ni Rafiki, hwambia haja pia;Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia;Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya;Kwamba tulimwomba Mungu, dua angesikia.

Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia?Haifai kufa moyo, dua atasikia.Hakuna mwingine M wema, wa kutuhurumia;Atujua tu dhaifu; maombi asikia.

Je, hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,Uja podharauliwa, ujaporushwa pia.Watu wangekudharau, wapendao dunia,Hukwambata mikononi, dua atasikia.

Bwana Yesu unitazame sasa,Unifanye niwe dhabihu hai;Najitoa kwako, moyo, na vyoteUnioshe sasa niwe mweupe. KY 71.2

Sura 8 - Kukua Katika Kristo na Kuwa WatuWake Wakamilifu

KULE kuongoka moyo ambako kunatufanya tupatekuwa watoto wa Mungu, kumenenwa katika Bibliakama ni kuzaliwa. Pengine tena kumelinganishwa nakuota kwa mbegu njema zilizopandwa na mlimaji.Vivyo hivyo wale ambao wameongoka moyo nakuanza kumfuata Kristo ni kama “watoto wachanga,” (1 Petro 2:2 ), tena lazima wakue hata wawe kamawatu wazima katika Kristo Yesu. Kadiri zinavyotakiwambegu njema kwa mimea mizuri, basi pia imewapasawatu wawe na mbegu njema moyoni ili watoematunda mema ya kiroho. Isaya asema juu yao,“Wapate kuitwa miti ya haki, miche ya BWANA,atukuzwe.” Isa. 61:3. KY 72.1

Akili zote na ustadi wote wa binadamu haviwezikamwe kuhuisha kitu cho chote ulimwenguni. Hatawanyama wala mimea, vyote hupata kuhuishwa naMungu tu. Hivyo wanadamu hawapati kuzaliwa marapili na kupata uzima mpya wa kiroho ila katika uzimautokao kwa Mungu. Mtu asipozaliwa mara ya pili,hawezi kushiriki uzima ule ambao hutolewa na Kristo.KY 72.2

Na jinsi ilivyo katika kupata uzima, ndivyo ilivyo

katika kuendelea kukua. Mimea haipati maua namatunda yake ila kwa uwezo wa Mungu tu. Yeye ndiyeanayeziotesha na kukuza mbegu, “kwanza jani, tenasuke, kisha ngano pevu katika suke,” Marko 4:28.Mimea haikui kwa kuhangaika kujitahidi yenyewe, ilakwa kuvipokea vile inavyopewa na Mungu kwakuendesha uzima wake. Hivyo pia mtoto hawezikuongeza urefu wake kwa kujitahidi mwenyewe. Nawewe pia, kwa kujishughulisha na kuhangaika kwakohuwezi kuendelea kukua katika mambo ya kiroho.Mmea au mtoto hupata kukua wakipokea vilevinavyoweza kusaidia na kuendesha uzima wao, -hewa, na chakula. Na kwa kadiri vitu vile vinavyosaidiakwa kuendesha uzima wa sasa, ndivyo alivyo Kristokwa wale waaminifu wake. Yeye ndiye “nuru ya milele”kwao, “ndiye jua na ngao.” (Isa. 60:19; Zab. 84:11).“Atakuwa kama umande kwa Israel.” “Atashuka kamamvua juu ya majani yaliyokatwa.” ( Hosea 15:5, Zab.72:6 ). Yeye ndiye maji ya uzima, “mkate wa Mungu . . .ushukao kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.Yoh. 4:14; 6:35,33. KY 73.1

Yesu mwenyewe hufundisha mambo haya hayaanaposema, “Kaeni ndani yangu na mimi ndani yenu.Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaandani ya mzabibu, kadhalika na ninyi, msipokaa ndaniyangu . . . Maana pasipo mimi hamwezi kufanya

neno.” Yoh. 15:4,5. Tawi lazima lifungamane na mtiwenyewe ili lipate kukua na kuzaa matunda; basi,wewe pia imekulazimu kumtegemea Kristo ili upatekuishi maisha safi. Pasipo yeye huna uzima kabisa.Peke yako huwezikuyakinga majaribu, wala kukua kwanamna ya kiroho na kuwa mtu mwenye usafi.Unapokaa ndani yake utasitawi. Kama unaishi kwake,huwezi kunyauka wala kutozaa matunda. Bali utakuwakama mti uliopandwa mtoni penye maji. KY 73.2

Wengi hudhani kwamba ni wajibu wao kufanyasehemu ya kazi ile wenyewe. Wamemtumainia Kristokwa kusamehewa dhambi, lakini sasa wanaona yakwamba ni heri wajitahidi wenyewe ili waishi maishayaliyo sawa. Kujitahidi hivyo hakutafaulu kamwe. Yesuasema, “Pasipo mimi hamwezi kufanya neno.” Tena nikwa njia ya kushiriki naye na kuongea naye, kwa kukaandani yake kila siku saa zote, tunavyopata kukua kwanamna ya kiroho. Yeye si mwanzo tu wa imani yetu, ilamwisho wake pia; yaani, imetupasa kumtumainiaKristo tangu mwanzo mpaka mwisho. Imetupasa iliKristo akae nasi, siyo tu kwa siku zile tuanzapokumjua na siku za mwisho wa maisha yetu, ilakini kwamwenendo wetu wote katika maisha yetu yote. Daudialisema, “Nimeweka BWANA siku zote mbele yangu:kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,sitatikisika.” Zab. 16: 8. KY 74.1

Pengine unauliza, Nawezaje kukaa ndani ya Kristo?”Kama vile ulivyompokea moyoni mara ya kwanza.“Kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendenivivyo hivyo katika yeye.” “Mwenye haki ataishi kwaimani.” Wakol. 2:6; Waeb. 10:38. Ulijitoa kwa Mungukuwa mtu wake kabisa, kumtii na kumtumikia tenaulimtumaini Kristo kama Mwokozi wako. Wewemwenyewe hukuweza kujiondolea dhambi zako nakugeuza moyo wako; lakini ulipokuwa umejitoa kuwawa Mungu, ndipo uliposadiki kama Mungu ndiyealiyekutendea haya yote kwa ajili ya Kristo. Kwa njia yakumwamini Kristo, ulikuwa wake; tena kwa kumwaminihivyo utazidi kukua naye - kwa kujitoa na kumpokea.Lazima ujitoe kwake kabisa, - moyo wako, nia yako, nautumishi wako; jitoe kwake na kuzishika amri zake namatakwa yake yote. Hivyo pia imekupasa kuvipokeavyote vinavyotoka kwa Kristo, ili akuwezeshe kumtiisawa sawa; umkubali Kristo mwenye mibaraka yoteakae moyoni mwako, awe uwezo wako, na haki yako,na msaidizi wako daima. KY 75.1

Jitoe kwake Mungu kila asubuhi, kabla hujafanyakitu cho chote. Omba hivi: “Bwana wangu, unichukue,niwe wako kamili. Nia yangu na maazimio yangu yotenayaweka mbele yako. Unitumie leo, niwe mtumishiwako. Ukae nami ili kazi yangu yote itendeke kwauwezo.” Hili ni jambo lipasalo kwa kila asubuhi, kujitoa

kuwa wa Mungu kwa siku ile. Makusudi yote na miradiyako yote uweke mbele yake ili kuyafanya au kutofayakwajinsi atakavyokuonyesha. Hivyo ndivyo maishayako yatakavyokuwa mkononi mwa Mungu kila siku,na maisha yako yatazidi kuwa kwa mfano wa Kristo.KY 75.2

Kukaa ndani ya Kristo ni kukaa raha mustarehemoyoni, na kutulizwa roho. Matumaini yako si juu yakomwenyewe, ila kwa Kristo. Udhaifu wakoumefungamana na ujinga wako na kutojua kwakohufungamana na akili zake, na nguvu zake, uhafifuwako umefungamana na uwezo wake. Hivyo haifaikujiangalia nafsi na kujiwazia sana; yapasakumwangalia Kristo tu, na kufikiri sana juu ya upendowake na sifa yake jinsi ilivyo njema na timilifu. JinsiKristo alivyojinyima, na udhilifu wake jinsialivyoaibishwa, jinsi alivyo safi na mtakatifu, upendowake usio na kifani, - hayo ndiyo mambo vafaayokufikiriwa moyoni. Kwa njia ya kumpenda Yesu,kumfuatisha kwa namna ya matendo yake na tabiazake, kumtegemea na kumtumainia kabisa, utapatakugeuka kuwa katika mfano wake. KY 76.1

Yesu asema, “Kaeni ndani yangu.” Maneno hayayatufikirisha juu ya kukaa mustarehe na imara, nakuwa na matumaini. Asema tena, “Njooni kwangu,nami nitawapumzisha.” Mattayo 11:28,29. Mtunga

Zaburi alisema hivi: “Umnyamalie BWANA,ukamngoje.” Zab. 37:7. Na Isaya pia hutuambia, “Kwakunyamaza na kutumaini zitakuwa nguvu zenu.” Isaya.30:15. Kustarehe huku hakupatikani kwa kukaa burekatika hali ya kutofanya kazi; kwa kuwa katika manenoyale ya Mwokozi wetu, ahadi ya kupata rahaimeungamana na wito wa kufanya kazi. “Jitieni nirayangu, . . . nanyi mtapata raha.” Mattayo 11:29. Yuleanayemtegemea Kristo zaidi na kukaa raha kwakemoyoni, ndiye atakayekuwa mtu wa moyo na juhudikwa kumtumikia Mungu. KY 77.1

Kama mtu anajifikiria nafsi na kujipendezamwenyewe tu, roho yake hugeuka na kutoka kwaKristo ambaye ni uwezo na uzima wake. Kwa hivyoShetani huwa anafanya bidii kuvuta watu nakuwapotosha, ili kuwazuia wasimshiriki Kristo. Anasaza dunia, fadhaa na mashaka, na ama huzuni, makosaya wengine, makosa na upungufu wako mwenyewe -Shetani hutumia hayo yote kwa kupotosha fikara zawatu. Tujiangalie tusidanganywe na hila zake. Wengiwanaotaka kufanya yapasayo na kuishi maisha safimachoni pa Mungu, mara nyingi huvutwa kwa Shetanikatika kufikiri sana juu ya makosa yao na udhaifu waompaka wamejitenga mbali na Kristo. Tusifikiri nafsizetu sana, na kuhangaika na mashaka moyoni kamatutaokoka au sivyo. Mambo kama hayo hugeuza moyo

kutoka kwa Kristo aliye asili ya nguvu zetu. Weka rohoyako mkononi mwa Mungu kama amana, nakumtumainia. Mazungumzo yako na fikara zako ziwejuu ya Yesu. Usiwe na shaka wala hofu moyoni. Sernakama alivyosema mtume Paulo: “Ni hai; wala si mimitena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio naosasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana waMungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajiliyangu.” Wagal. 2:20. Ukae na kustarehe kwa Mungu,ukasadiki kwamba aweza kukilinda kile ulichokiwekaamana kwake. Kama unajiweka mkononi mwake,atakuwezesha kushinda, na zaidi ya kushinda, kwayeye aliyekupenda. ( Soma Warumi 8:37). KY 77.2

Kristo alipoutwaa mwili wa kibinadamu, alijifungiamioyo ya wanadamu kwake kwa upendo wake, nakufungamana huku hakuwezi kuharibika ila kwa hiariya mwanadamu mwenyewe. Shetani hufanya bidii sikuzote kuvuta roho zetu na kutushawishi ili tujitengembali na Kristo. Kwa hivyo imetupasa kujilinda, nakuomba kwa bidii ili tusishawishiwe na jambo lo lotena kuchagua kutawaliwa na Shetani. Tumkazie Kristomacho yetu, yeye awezaye kutulinda. TukimtazamaYesu, tutakuwa salama; wala hakuna awezayekutupokonya katika mkono wake. TukimwangaliaYesu na utukufu wake daima, “tunabadilishwa nakufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hata

utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwanaaliye Roho.” 2 Wakor. 3:18. KY 78.1

Hivyo ndivyo wanafunzi wake wa zamaniwalivyopata kufanana naye. Walikuwa nayewakafundishwa kwake. Wakamwangalia, kamawatumishi wanavyomwangalia bwana wao, ili wapatekujua yaliyo wajibu wao. Walikuwa wanadamu wenye“tabia moja na sisi.” Yak. 5:17. Wakawa wakishindanana maovu sawa na sisi. Iliwapasa kusaidiwa kamasisi, ili wapate kuishi maisha yaliyo safi na matakatifu.KY 79.1

Na hata Yohana, mwanafunzi mpendwa wa Yesu,aliyefanana naye zaidi ya wengine, hakuwa na sifanjema kwa desturi. Alikuwa mtu wa kujitokeza mbelena kutaka makuu. Naye alipozidi kufahamu namna yasifa ya Yesu jinsi ilivyo bora, alizidi kuona upungufuwake mwenyewe na kushushwa moyo. Siku kwa sikumoyo wake ukazidi kuvutwa kwa Yesu Kristo, nakujisahau nafsi yake mwenyewe. Moyo wakeulitengenezwa kuwa mpya kwa Roho Mtakatifu, nahata tabia zake hasa ziligeuka kufanana na Kristo.Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa kila ashirikianayenaYesu. Kristo akaapo ndani ya moyo, na kuutawala,ndipo yule mwanadamu anapogeuzwa tabia zakehasa; sasa fikara zake na tamaa zake ni juu ya Munguna mambo ya mbinguni. KY 79.2

Siku ya kupaa kwake mbinguni, Yesu aliwaambiawanafunzi wake, “Tazama, mimi nipo pamoja nanyisiku zote, hata mwisho wa dunia.” Mattayo 28:20.Akapaa mbinguni na umbo la kibinadamu. Walijua yakwamba alikwenda kuwaandalia makao, na kuruditena baadaye, kuwapeleka kwake alipo. KY 80.1

Walipokutana walikumbuka ahadi yake jinsialivyosema, “Mkimwomba Baba neno kwa jina languatawapeni. Mpaka leo hamkuomba neno kwa jinalangu; ombeni, na mtapata, furaha yenu iwe timilifu.”Yoh. 16:23,24. Pia walitumaini ya kwamba “Kristondiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka,naye yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiyeanayetuombea.” Warumi 8:34. Na siku ya Pentekotewakapata kujazwa Roho Mtakatifu, yule Mfarijiambaye Kristo ailsema juu yake, “Naye atakaa ndaniyenu.” Alisema pia, “Yawafaa ninyi niondoke; kwamaana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; balinikienda zangu, nitampeleka kwenu.” Yoh. 14:17; 16:7.Tangu siku hiyo, kwa njia ya Roho Mtakatifu, Kristoamekuwa anaweza kukaa mioyoni mwa watu wakesiku zote, Sasa waweza kumshiriki Kristo zaidi kulikowalivyomshiriki siku zile alipokuwa nao katika umbo lakibinadamu. Upendo na uwezo wa Kristo vikaonekanakwao, hata wengine walipotambua hivyo,“wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa

pamoja na Yesu.” Matendo 4:13. KY 80.2

Kwa kadiri Kristo alivyowasaidia wanafunzi wake wazamani, ndivyo apendavyo kuwasaidia watu wake wasasa; kwa kuwa katika kuomba kwake alisem. “Wala sihao tu ninaowaombea, bali na wao watakaoniaminikwa sababu ya neno lao.” Yoh. 17:20. KY 81.1

Yesu alituombea sisi, ili tuwe katika umoja ndaniyake, kama Yeye na Baba yake walivyo katika umoja.Huo ni umoja wa namna gani! Mwokozi alisema juuyake mwenyewe, “Mwana hawezi kutenda neno kwanafsi yake, ila lile amwonalo Baba analitenda;”akasema tena, “Baba akaaye ndani yangu huzifanyakazi zake.” Yoh. 5:19; 14:10. Ikiwa Kristo anakaamioyoni mwetu, atatenda kazi yake ndani yetu, ilikutaka kwetu na kutenda kwetu kupatane na kusudilake jema.Wafil. 2:13. Tutafanya kama alivyofanyayeye; tutakuwa na nia ndani yetu iliyokuwamo ndaniyake; hivyo kwa kumpenda Yesu na kukaa ndani yake,tutakua “mpaka tumfikie yeye katika yote, aliyekichwa, ndiye Kristo. Waef. 4:15. KY 81.2

Sura 9 - Kazi na Maisha, JinsiVinavyohusiana

MUNGU ndiye asili ya uzima na mwanga na furahakwa ulimwengu wote. Mibaraka inatoka kwake kwaviumbe vyake vyote. Na mahali po pote ukiwapouzima wa Mungu mioyoni mwa wanadamu, itakuwakama mito ya maji ya uzima ule, kuwatokea nakuwasaidia na kuwabariki wengine. KY 83.1

Ilikuwa furaha ya Mwokozi wetu kuwainua nakuwakomboa wanadamu wapotevu. Kwa hiyohakuyahesabu maisha yake kuwa ni kitu cha thamanikwake, lakini “kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbeleyake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu.” Waeb.12:2. Hivyo pia malaika hushughulika katika kazi yakufurahisha wengine. Hiyo ndiyo furaha yao. Kazi ileambayo wengine hudhani ni kazi ya namna yakuwavunjia heshima na cheo, yaani kuwahudumia nakuwasaidia walio chini yao na wenye hali mbaya, ndiyokazi wanayoifanya malaika wakaao mahali pasipodhambi kabisa. Ile nia ya Kristo ya kutojipendeza nafsiyake, bali kufikiria na kusaidia wengine, ndiyo niainayoenea kote mbinguni, tena ni asili ya furaha yaowa mbinguni. Hiyo ndiyo nia watakayokuwa nayowafuasi wa Kristo, na namna ya kazi watakayoifanya.KY 83.2

Upendo wa Kristo ukiwamo moyoni, hauwezikufunikika, bali utatambulika kwa wote tunaokutananao. Kumpenda Yesu kutabainishwa katika kutamanikutenda kama alivyotenda yeye, kwa kusaidia nakubariki walimwengu wengine. Tutakuwa na moyo waupendo, na huruma, na kushiriki katika hali ya wenginewote walio viumbe vya Baba yetu aliye mbinguni. KY84.1

Mwokozi alipokuwa hapa duniani, hakukaa rahamustarehe na kujipendeza mwenyewe; bali alifanyabidii kuwaokoa wanadamu wapotevu. Tangu kuzaliwakwake mpaka kusulubiwa kwake Kalwari, alifuata njiaya kujinyima. Alisema ya kwamba Mwana wa Adamuhakuja “kuhudumiwa, bali kuhudumu, na kutoa rohoyake kuwa dia ya wengi.” Mattayo 20:28. Hilo ndilokusudi kuu la maisha yake, kufanya mapenzi yaMungu na kumaliza kazi yake. Hakufikiri kamwe juu yakujipendeza nafsi yake mwenyewe. KY 84.2

Vivyo hivyo wale wanaomshiriki Kristo watakuwatayari kujinyima ili wengine wapate kujua jinsi Yesualivyokufa kwa ajili yao, nao pia washirikiane naye.Hiyo ndiyo roho inaooynekana kwa yule anayeongokakweli. Mara anapomjua Kristo, husikia moyonikwamba ameshurutishwa kuwajulisha wengine kuwaYesu ni rafiiki wake mwema. Ikiwa tumesikia wemawa Bwana wetu, basi, tuwaonyeshe wenzetu, ili wao

pia wavutwe kwa Yesu, na kumjua “Mwana Kondoowa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yoh.1:29. KY 84.3

Tukijitahidi hivyo kusaidia wengine tutabarikiwa sisipia. Mungu alikusudia hivi alipotupa sisi sehemu yakazi ya kuokoa watu. Kuwa watenda kazi pamoja naMungu ni heshima iliyo kuu na furaha iliyo kubwa zaidiya yote wanayoweza wanadamu kupewa na Mungu.KY 85.1

Mungu angaliweza kuwapa malaika kazi yakuwahubiria wanadamu Injili. Lakini kwa upendo wakealituchagua tuwe watenda kazi pamoja naye, pamojana Kristo na malaika, ili tushiriki mibaraka, furaha, nakuchangamshwa roho kwa jinsi inavyopatikana katikahuduma hii. Tena kila tendo la kujinyima kwakuwasaidia wengine, humzidishia moyo wa ukarimuyule mwenye kujinyima, naye huzidi kupatana nakushirikiana na Mwokozi; “maana mmejua neema yaBwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwaajili yetu, alipokuwa tajiri, ili ninyi mpate kuwa matajirikwa umaskini wake.” 2 Wakor. 8:9. Tena kwa kadiritunavyotimiza kusudi la Mungu juu yetu, ndivyotutakavyopata furaha na baraka katika maisha yetu.KY 85.2

Kama utafanya kazi kama Kristo alivyokusudia

wafuasi wake wafanye, na kuwavuta watu kwake,utaona haja ya kuzidi kumjua Mungu moyoni mwako,na kuzidisha maarifa katika mambo ya Mungu, naweutaona “njaa na kiu ya haki.” Utaendelea kumwombaMungu, tena kuamini kwako kutazidi kuthibitika. Kamaunapata kujaribiwa utashurutishwa kusoma Neno laMungu na kumwomba zaidi. Hivyo utazidi kumjuaKristo, na kupata neema yake na kuwa mwaminifuwake katika maisha yako; hasa utazidi kufanana naKristo, tena utapata raha na furaha zaidi moyonimwako. KY 86.1

Wale wanaojaribu kuwa Wakirsto na kupatamibaraka yake bila kumfanyia kazi yo yote, hufananana watu wanaotaka kupata chakula na kukaa bure bilakufanya kazi. Mtu anayekataa kuvinyosha viungovyake kwa kutenda kazi, atapotewa na nguvu ile aliyonayo. Vivyo hivyo Mkristo anayekataa kuutumia uwezoule aliopewa na Mungu, hukosa kukua na kuwa kamamtu mzima katika Kristo, hata na yeye pia atapotewana uwezo wa kiroho aliokuwa nao zamani. KY 86.2

Mungu ameweka kanisa la Kristo kuwa kama wakiliwake kwa kuwaokoa watu. Kazi yake: ni kueneza Injiliduniani pote. Sharti hiyo imekuwa juu ya Wakristowote. Kama tumejua upendo wa Kristo, basi tunawiwadeni na wote wasiomjua Kristo. Mungu ametupa nuru,si kwa kujisaidia sisi wenyewe tu, ila pia tumulikie

wale wengine wasiomjua. KY 86.3

Wafuasi wa Kristo wangaliamka na kufanya wajibuwao, kungekuwako watu elfu wa kuhubiri Injili mahalipalipo na mhubiri mmoja tu sasa. Na hata walewasioweza wenyewe kuwa watenda kazi wa Mungu,wangesaidia kazi kwa fedha zao na maombi yao. Tenakazi ya kueneza Injili na kuwajulisha watu kuwa Kristondiye Mwokozi wao, ingeendelea na kufanywa kwamoyo wa bidii sana. KY 87.1

Si lazima twende katika nchi ngeni za makafiri,kumfanyia Kristo kazi, ikiwa wajibu wetu uko hukokwetu. Twaweza kumtumikia Kristo nyumbani mwetu,kanisani kwetu, kwa wenzetu, majirani zetu, hata nawale tunaokutana nao katika kazi yetu. KY 87.2

Katika maisha yake hapa duniani, Yesu alipitishamiaka mingi katika kufanya kazi ya useremala pamojana babake mjini Nazareti. Tena alimwamini Mungukatika kufanya kazi ile kama alivyokuwa akiwaponyawagonjwa na kutembea juu ya maji ya Galilaya. Hivyona sisi pia, hata ikiwa tumehesabiwa kuwa tu watuduni na kufanya kazi iliyo chini, twaweza kutembea naYesu na kumtumikia. KY 87.3

Mtume Paulo asema, “Kila mtu . . . na akae katikahali hiyo hiyo aliyoitwa.” 1 Wakor. 7:24. Mfanyi

biashara anaweza kufanya kazi yake kwa namnaawezavyo kumtukuza Mungu kwa ajili ya uaminifuwake. Ikiwa yu mfuasi wa kweli wa Kristo, dini yakeitaonekana katika mambo yake yote, naatawadhihirishia watu namna ya roho ya Kristo.Mwashi, au mfanyi kazi yo yote, inampasa kuwamwenye bidii tena mwaminifu katika kazi yake, nahivyo atakuwa mjumbe mwaminifu wa Kristo. Kila mtuanayejiita kwa jina la Kristo inampasa kutenda kazikwa namna iliyo sawa, ili wengine wapate kuyaonamatendo yake mema wakamtukuze Mungu aliyeMuumba tena Mwokozi wetu. KY 87.4

Wengi hujisingizia wasitumie akili zao katika kufanyakazi ya Kristo, kwa sababu kuna watu wengine wanayoakili iliyo bora zaidi. Watu wengi hudhani ya kwambawale tuwenye akili nyingi ndio ambao wametakiwakujitoa na akili zao katika kumtumikia Mungu. Piawengi hudhani ya kwamba ni baadhi tu va watu, yaaniwanaopendelewa zaidi na kuwa Katika hali nzuri,ambao hupewa akili na talanta; na wenginewametengwa mbali, hao nao hawapati kutiwa kushirikikazi ya Mungu na neema yake. Lakini haikuelezwahivyo katika mfano uliotolewa na Kristo. Bwana wanyumba alipowaita watumishi wake, alimpa kilammoja kazi yake. KY 88.1

Kwa moyo wa kupenda, twaweza kuifanya hata kazi

iliyo chini kabisa na kuifanya “kama kwa Bwana.”Wakol.3:23. Upendo wa Mungu ukiwamo moyoni,utaonekana katika maisha. KY 89.1

Usingojee jambo lililo kuu wala kutumaini kupataakili nyingi kabla ya kumtumikia Mungu. Tena usifikirijuu ya wengine jinsi watakavyokudhania. Kamamaisha yako na matendo yako ya siku zotehuushuhudia wema wako na uaminifu wako, nakuwasadikisha wengine ya kwamba unatakakuwatendea valiyo mema, kazi yako haitapotea bure.Hata na wafuasi wa Yesu wanaohesabiwa kuwa niwatu duni, wanaweza kusaidia wengine na kuwaleteabaraka. Kama wanaendelea kufanya kwa uaminifukazi ile wanayopewa na Mungu, maisha yaohayatakuwa bure. Watazidi kufanana na Kristomioyoni mwao; huwa wafanyi kazi pamoja na Mungukatika maisha ya sasa, na vivyo hivyo wanatayarishwakumhudumia Mungu mbinguni, na kupata furaha kuukatika uzima ujao. KY 89.2

Sura 10 - Kumjua Mungu

KWA njia nyingi Mungu anajaribu kutujulisha tabiazake, ili tupate kumjua na kushirikiana naye. Viumbevya ulimwengu vyatuonyesha wema na upendo wakemilele. Moyo unaofunuliwa utaona upendo na utukufuwa Mungu jinsi unavyoonekana katika matendo yakena katika kazi za mikono yake. Tukiona na kufikiri juuya miti na maua, mazao ya mashamba, mawingu,mvua, mito, nyota na uzuri wote wa mbingu, hatunabudi kuvutwa moyoni kumjua yeye aliyeviumba vyote.KY 90.1

Mwokozi wetu alitoa mafundisho mengi juu yaviumbe vya ulimwengu. Akasema juu ya miti, maua,ndege, vilima, maziwa ya maji, na vitu vya mbinguni,pamoja na mambo yanayotukia kwa watu katikamaisha yao siku zote; na watu walipoviona vitu vile namambo hayo mara kwa mara iliwalazimu kukumbukamafundisho yake. KY 90.2

Tukifunua roho zetu na kusikiliza sauti ya Mungukatika viumbe vyake, tutapata kufundishwa namna yakumtii na kutawakali kwa Mungu. Viumbe vyote, tangunyota zinazofuata njia zao mbinguni, hata na viduduvidogo, vyote hufuata mapenzi ya Mungu. TenaMungu huangalia kila kitu alichokiumba.

Huzitegemeza nyota katika mahali pakubwa mbinguni,na hata ndege wadogo wa anga huangaliwa naye.Wanadamu wakiondoka asubuhi kwenda kazini, nawakati waombapo, wakati wanapokwenda kulalausiku; tajiri katika jumba lake, hata na maskini katikakibanda chake, Baba yetu aliye mbinguni huangaliawote kwa huruma na upendo. Mtu akitoka machoziama akiwa na furaha, Mungu huona yote. KY 90.3

Kama tungesadiki hivyo kabisa, mahangaiko yoteyasiyofaa yangeondolewa mioyoni mwetu; kwasababu mambo yote, makubwa hata madogo,tungekuwa tunayaacha mkononi mwa Mungu; nasitungeona raha mioyoni mwetu. KY 91.1

Na kama unapendezwa machoni kwa kuona uzuriwa dunia hii, fikiri juu ya ulimwengu mpya ujao, ambaohuko uharibifu wa dhambi na mauti hautaonekanakamwe. Tena ukumbuke ya kwamba fahari yake nautukufu wake havina kifani. Imeandikwa, “Mamboambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu, mamboambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” 1 Wakor.2:9. Wale tu watapata furaha katika kutambua uzuriwa viumbe vya ulimwengu, ambao wanafahamu yakwamba vyote hutangaza upendo wa Mungu kwawanadamu. KY 91.2

Mungu husema nasi katika matendo yake, pia katikauongozi wake, tena katika mvuto wa Roho yakemioyoni mwetu. Katika mambo yanayotukia kwetu, nakatika hali yetu, twaweza kupata mafundisho yake,ikiwa mioyo yetu imekuwa wazi kuyatambuamafundisho yu Mungu. Mtungu Zaburi alisema, “Nchiimejaa wema wa Bwana.” “Mwenye hekimautayaangalia haya, nao watazijua rehema za Bwana.”Zaburi 33:5; 107:43. KY 92.1

Mungu husema nasi tena katika Neno lake. Hapoimefunuliwa dhahiri sana namna ya sifa zake na tabiazake, jinsi anavyowatendea wanadamu, na kazi yakekubwa katika kuwakomboa wanadamu. Hapozimesimuliwa habari za wazee wakuu na manabii nawengine wa zamani waliokuwa watu wa Mungu. Haonao wakawa watu wenye “tabia moja na sisi.” Yakobo5:17. Twasoma juu yao jinsi walivyoshindana namambo ya kulegeza moyo kama sisitunavyolazimishwa kushindana; walijaribiwa nakuvutwa na mabaya kama sisi tunavyopata kuvutwa;hata hivyo walijitia moyo tena, wakashinda kwa uwezona neema ya Mungu; na sisi pia tukijua hivyoimetupasa kujitia moyo na kuendelea kujitahidi katikakuyanyosha maisha yetu ili yawe na haki ma- choni paMungu. Kama tunaona namna ya kazi ya wale watuwa zamani waliyofanya kwa neema na msaada wa

Mungu, na jinsi walivyobarikiwa na kupata furahakatika kufanya kazi ile, sisi pia twatamani kufanananao katika sifa zao na kuendelea pamoja na Mungukama wao. KY 92.2

Maandiko Matakatifu hutoa habari za Kristo, jinsialivyosema, “na hayo ndiyo yanayonishuhudia.” Yoh.5:39. Biblia nzima hutoa habari za Kristo. Tangu habariza mwanzo juu ya kuumbwa kwa ulimwengu kwakuwa “pasipo yeye hakikufanyika cho chotekilichofanyika,” Yoh. 1:3 - mpaka ahadi ya mwisho,“Angalieni, naja upesi,” Uf. 22:12, twasoma juu yamatendo yake tena twasikiliza sauti yake. Kamaunataka kumjua yule aliye Mwokozi, heri ufanye bidiikatika kuyachunguza maneno ya Biblia, yaaniMaandiko Matakatifu. KY 93.1

Ujaze moyo mzima maneno ya Mungu. Hayo ndiyomaji ya uzima, na mkate wa uzima utokao juu. Yesualisema, “Msipoila nyama yake Mwana wa Adamu nakuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.”Akazidi kueleza maana yake hivi: “Manenoninayowaambieni ni roho, tena ni uzima.” Yoh. 6:53,63. Kadiri miili yetu inavyokuwa mizima na kupataafya njema kwa ajili ya vile tulavyo na tunywavyo, basivivyo hali yetu ya kiroho itazidi kuwa njema nakuongezeka nguvu kwa vile tunavyofikiri na kuwazamambo ya kiroho. KY 93.2

Jambo la ukombozi wa watu katika Kristo ndilojambo ambalo malaika wanatamani kulichungulia;tena litakuwa jambo kuu katika kuelimisha wateule waMungu katika ufalme wake hata milele. Je, si jambolifaalo kufikiriwa hata na sisi katika siku hizi?Imetupasa kufikiri sana juu ya rehema na upendo waYesu, na jinsi alivyojitoa maisha yake kwa ajili yetu.Imetupasa kuchunguza sifa na tabia za Mwokoziwetu. Ni wajibu wetu kufikiria kazi yake katikakuwaokoa watu katika dhambi zao. Na tunapowazamambo matakatifu, imani yetu na upendo wetuvitaongezeka kwake, tena kwa hiyo maombi yetuyatazidi kukubaliwa na Mungu. Tutazidi kumtegemeana kumtumainia Kristo na uwezo wake “kuwaokoakabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye.” Waeb. 7:25.KY 94.1

Na tunapofikiri juu ya Mwokozi jinsi alivyo mkamilifuna mwenye sifa bora, tutatamani kugeuka moyo kuwawapya na hufanana naye hasa katika usafi wake. Tenatukizidi kumfikiria Kristo, tutazidi kumshuhudia kwawengine. KY 94.2

Biblia haikuandikwa kwa ajili ya wenye elimu nyingitu; bali ilikusudiwa kuwa ya watu wote, hata na akinasisi. Mafundisho makubwa juu ya wokovu yamekuwadhahiri kabisa, na mtu ye yote aweza kuyafahamu;hakuna awezaye kukosa njia ya haki ila yeye afuataye

nia yake mwenyewe badala ya kufuata mapenzi yaMungu. KY 94.3

Tusikubali neno lo lote la binadamu juu yamafundisho ya Biblia, bali tujifunze wenyewe manenoya Mungu na kuyachunguza hata tufahamu maanayake. Tukifanya bidii katika kujifunza mambo ya Biblia,tukilinganisha sehemu fulani ya Biblia na sehemunyingine, na mambo ya kiroho, kwa mambo tutaona yakuwa akili zetu zinaongezeka. KY 95.1

Hakuna njia nyingine ya kuzidisha akili zaidi ila yakujifunza na kuyachunguza maneno ya Biblia.Mafundisho yake yaweza kuadilisha fikara nakuzidisha akili kwa namna isiyowezekana kwakusoma kitabu kingine cho chote. KY 95.2

Kama wanadamu wangejifunza na kulichunguzaNeno la Mungu kama inavyostahili, wangekuwa namaarifa mengi na sifa bora, na kuimarishwa mioyoni.KY 95.3

Lakini hakuna faida katika kusoma Biblia ovyo ovyokwa haraka. Kwa kusoma namna hiyo tungewezakuisoma Biblia nzima bila kutambua uzuri wake walakufahamu maana yake, hasa maana ya siri ya ndani.Yafaa kuisoma sehemu moja na kuichunguza sanampaka maana yake imekuwa dhahiri, na kuona jinsi

inavyohusiana na mpango wa Mungu kwa kuwaokoawanadamu; kufanya hivyo kwa kila sehemu ya Bibliakutakuwa na faida sana kuliko kusoma tu sura nyingibila kusudi la kujifunza hakika yake. Biblia yako iwekaribu nawe kila mara. Kila upatapo nafasi, isome;jifunze mafungu yake kwa moyo. Hata wakatiutembeapo, waweza kulisoma fungu fulani na kufikirimaana yake, na kulitia moyoni. KY 95.4

Hatuwezi kupata kuelimishwa bila kujitahidi nakukaza moyo kwa kujizoeza kusoma pamoja nakuomba. Kuna sehemu nyingi za Biblia ambazomaana yake imekuwa dhahiri kabisa; lakini kunasehemu zingine tena ambazo maana yake si rahisikufahamiwa mara moja. Yafaa kulinganisha sehemumoja na sehemu nyingine, na kuzifikiri na kuzichunguasana pamoja na kuomba. Tusifungue kabisa Biblia nakuyasoma maneno yake bila kuomba. Kabla yakuifungua Biblia heri tusali ili tupate mwangaza waRoho Mtakatifu, ndipo tutaupata. Nathanaelalipomwendea Yesu, Mwokozi alisema, “Tazama, huyuni Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.”Nathanael akamwambia, “Umepataje kunijua?” Yesuakamjibu, “Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini yamtini, nalikuona.” Yoh. 1:47, 48. Tena Yesu ataonananasi katika mahali pa siri pa sala, ikiwa tutamwombaili tupate kuelimishwa na kujua yaliyo ya kweli.

Malaika watokao mbinguni watawasaidia walewatakao kuongozwa na Mungu. KY 96.1

Roho Mtakatifu humtukuza na kumsifu Mwokozi.Kazi yake ni kutuonyesha Kristo, na hali yake jinsiilivyo yenye haki na usati, na kutudhihirishia habari zawokovu tupatao kwake. Yesu alisema, “Atatwaa katikailiyo yangu, atawapasheni habari.” Yohana 16:14. Rohoya kweli ndiye mwalimu wa pekee awezaye kutujulishabarabara yaliyo kweli ya Mungu. Ni dhahiri ya kwambaMungu huona wanadamu kuwa wa thamani kubwa,kwa kuwa alimkubali Mwanawe afe kwa ajili yetu, tenaameweka Roho wake Mtakatifu kuwa mwalimu nakiongozi wa wanadamu daima. KY 97.1

Nataka nimjue Yesu,Na nizidi kumfahamu;Nijue pendo lake, naWokofu wake kamili.

Nataka nimwone Yesu,Na nizidi kusikiaAnenapo kitabuni,Kujidhihirisha kwangu.

Nataka nifahamu, naNizidi kupambanuaMapenzi yake, nifanye

Yale yanayompendeza.

Nataka nikae naye,Kwa mazungumzo zaidi,Nizidi kuwaonyeshaWengine wokofu wake. KY 97.2

Sura 11 - Kuomba ni Faradhi Yetu

MUNGU hutumia njia nyingi kwa kusema nasi, yaanikwa viumbe vyake, kwa kuwafunulia wanadamumambo yajayo, kwa maongozi yake, na kwa mvuto waRoho yake Mtakatifu. Lakini hata njia hizi zotehazitoshi; hata na sisi pia imetupasa kumtolea Munguyote yaliyomo mioyoni mwetu. Imetulazimu kuongeana Baba yetu aliye m binguni, ili tupate uzima na nguvuza kiroho. Na kama twataka kuongea na Mungu, shartituwe na mambo ya kumwambia, hasa juu ya maishayetu. KY 98.1

Katika kuomba tunamfunulia Mungu mioyo yetu nakuongea naye kama tunavyoongea na rafiki wa kweli.Si lazima kufanya hivyo ili kumjulisha Mungu hali yetuilivyo, bali kuongea naye kunatuwezesha kumpokeamioyoni mwetu. Sala hazimlazimishi Mungu kushukakwetu, bali ni sisi ambao tunainuliwa mpaka kufikakwake. KY 98.2

Yesu alipokuwa hapa duniani, aliwafundishawanafunzi wake kusali. Aliwaagiza waweke mbele yaMungu upungufu wao na mahitaji yao ya kila siku, nakumtupia mashaka yao na mahangaiko yao yote. Tenakama alivyowaahidi wanafunzi wake ya kwambamaombi yao yatakubaliwa, basi ahadi ile imekuwa

yetu pia; yaani anatuahidi ya kuwa sala zetuzitakubaliwa. KY 98.3

Yesu mwenyewe, alipokaa na wanadamu, aliombakwa kawaida. Mwokozi wetu alijishirikisha mahitajiyetu na udhaifu wetu; kwa hivi akawa mhitaji namwombaji, akimwomba Baba yake ili apate nguvu zakufanya kazi yake na kuyashinda majaribuyatakayompata. Yeye ndiye mfano wetu katikamambo yote. Ni ndugu yetu ashirikiye udhaifu wetu,“alijaribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote;”lakini kwa sababu alikuwa safi bila dhambi,akayaepuka maovu nafsini mwake. Katika hali yake yakibinadamu, kuomba kulikuwa ni faradhi yakeiliyomhusu, naye tena akapata faraja na furaha katikakuongea na Baba yake. Na ikiwa Mwokozi wetu, aliyeMwana wa Mungu, aliona ya kwamba anahitajikuomba, basi sisi, tulio wanadamu dhaifu wenyedhambi, tunahitaji zaidi kufanya bidii katika maombiya kawaida. Baba yetu aliye mbinguni huwa anangojakutubariki. Mungu yu tayari kusikiliza maombi ya kweliya kila mtoto wake, walakini sisi hatuna moyo sana wakumwambia Mungu haja zetu. KY 99.1

Giza ya Shetani huzunguka wale wasiofanya bidiikatika kuomba. Adui wao, Shetani, huwashawishi iliwafanye maovu, nao kwa sababu ya kuacha kuombahawana nguvu za kushindana naye. Mbona watu wa

Mungu hutupilia mbali faradhi yao ya kuomba,ijapokuwa kuomba ni kama ufunguo mikononi mwawaaminifu wa Mungu wa kuwafungulia msaada wotena mibaraka yote ya Mungu isiyo na kiasi.Tusipoomba siku zote na kukesha kwa uangalifu,tutajitia katika hatari ya kuwa walegevu wa mambo yakiroho na kupotewa na njia ya haki. KY 100.1

Kuna masharti mengine juu yetu ambayo ni wajibuwetu, ili tuweze kutumaini ya kuwa Mungu atatusikiana kutujibu maombi yetu. Shart moja ni hili; lazimatufahamu jinsi tunavyohitaji msaada wake. Ameahidi,“Nitamimina maji juu yake mwenye kiu, na mito juu yapakavu.” Isa. 44:3. Wale wenye njaa na kiu ya haki,wamtakao Mungu sana, watashiba. Lakini baraka zaMungu haziwezi kupatikana ila kwanza moyo uweumefunguliwa na Roho Mtakatifu kuingia. Bwana wetuhujua haja zetu, lakini imetupasa kutambua haja zetusisi wenyewe na kumwomba Mungu mambo hayo.Asema, “Ombeni na mtapewa.” Mattayo 7:7. Tena“Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoakwa ajili yetu sisi sote. atakosaje kutukarimia na vituvyote pamoja naye?” Warumi 8:32. KY 100.2

Tukiwa tunaangalia maovu moyoni na kuyashikilia,Mungu hawezi kusikia maombi yetu; lakini mwenyekutubia kosa lake, maombi yake yanakubaliwa maramoja. Hatuwezi sisi kujistahilisha machoni pa Mungu

kwa matendo yetu mema; ustahilifu wa Yesu ndioutakaotuokoa, na damu yake ndiyo itakayotutakasa;hata hivyo kuna masharti juu yetu pia ili tukubaliwe naMungu. KY 101.1

Sharti jingine juu yetu ni kuwa na imani. “Pasipoimani haiwezekani kumpendeza (Mungu): kwa maanamtu ampendezaye Mungu lazima aamini kwambayuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”Waeb. 11:6. Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwambamnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Marko 11:24. Je,twayasadiki maneno yake? KY 101.2

Kama tunakosa kupata mambo yale yaletuliyoyaomba, kwa wakati ule ule tuombao, hata hivyotukubali ya kwamba Mungu hutusikia, tena atatujibumaombi yetu. Kwa ajili ya ujinga wetu, penginetwamwuliza Mungu mambo yasiyotufaa, naye Babayetu wa mbinguni hutujibu na kutupa mambo yaleyanayokuwa bora kwetu, - ambayo sisi wenyewetungeyataka kama tungeweza kuona mambo yote jinsiyalivyo kama Mungu aonavyo. Hata kama inaonekanakwamba maombi yetu hayajibiwi, tutazidi kuendeleakutumaini ahadi yake; kwa kuwa bila shaka atatujibubaadaye, nasi, tutapata mbaraka ule ule unaotupasa.Lakini kusema ya kwamba Mungu hana budi kutujibumaombi tunayoomba na kutupa sisi yale yale

tunayoyataka, - ni kama kujidai bila haki na kumfanyiaMungu kiburi. Mungu ni mwenye busara asiyewezakufanya kosa, tena yu mwema; kwa hivyo hawanyimiwaaminifu wake jambo jema lo lote. Ni heri tutegemeeahadi yake ya kweli, “Ombeni na mtapewa.” KY 101.3

Tunapomwendea Mungu na kumwomba msamahana mbaraka wake, imetupasa kuwa na moyo waupendo na kusamehe wengine. Twawezaje kuombahivi, “Utusamehe makosa yetu, kama sisitunavyowasamehe waliotukosea.” Na sisi katika rohozetu tungali hatujakubali kuwasamehe wengine?Tukitumaini kujibiwa maombi yetu, sharti tuwe na rohoya kuwasamehe wengine kama vile sisi tunavyotarajiakusamehewa. KY 102.1

Kudumu katika kuomba ni sharti jingine juu yakujibiwa maombi. Kama tunataka kuongeza imani nakuwa watu wazima katika Kristo, imetupasa kuombasiku zote; “katika kusali, mkidumu;” “dumuni sanakatika kuomba, mkikesha katika kuomba huku nashukrani.” Warumi 12:12; Wakol. 4:2. Petro awausiaWakristo, “Mwe na akili, mkakeshe katika sala.” 1Petro 4:7. Mtume Paulo awaagiza hivi, “Katika kilaneno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru,haja zenu zijulike kwa Mungu.” Wafil. 4:6. Na Yuda piaasema, “Ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenuiliyo takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu,

jilindeni katika upendo wa Mungu.” Yuda 20, 21.Tukidumu katika kuomba, roho zetu zitafungamanakuwa moja na Mungu, ili tupate uzima utokao kwake;na maisha yetu yatakuwa safi machoni pake. KY 102.2

Sharti tufanye bidii katika kuomba; tusikubali kitucho chote kutuzuia kuomba. Shika kila nafasi yakwenda mahali ambapo watu huzoea kuomba. Walewatakao kushirikiana na Mungu kweli, wataonekanakila mara kwenye mkutano wa kusali; watakuwawaaminifu katika kufanya iliyo wajibu wao, piawatakaza mioyo yao kupata msaada wote wa Munguunaowahusu. KY 103.1

Sharti tuombe pamoja na watu wa nyumbani; nazaidi ya yote tusiwe wavivu katika kuomba faraghanipeke yetu, maana kufanya hivyo ndio asili ya uzima waroho. Kusali hadhara ya watu peke yake hakutoshi.Yatupasa kumfunulia Mungu mioyo yetu katikafaragha, ambapo maombi yetu yatasikiwa na Mungubila shaka; maana hapo tuna nafasi kumwonyeshamambo yetu yote. Katika sala ya upweke roho zetuhupata nguvu ya kustahimili katika kushindana naShetani. Mungu ndiye nguvu zetu. KY 103.2

Omba faraghani; tena katika kufanya kazi yako,umwinulie Mungu moyo wako. Hivyo ndivyo Enokalivyopata kuendelea pamoja na Mungu. Shetani

hawezi kamwe kumshinda yule ambaye moyo wakehumtegemea Mungu hivi. KY 104.1

Hakuna wakati wala mahali pasipofaa kumwombeaMungu. Hakuna kinachoweza kutuzuia tusimwinuliemioyo yetu katika kusali. Kati ya watu njiani, hatakatika kufanya kazi yetu, twaweza kumwomba Mungumsaada wake na uongozi wake, kama alivyofanyaNehemia alipomtolea mfalme Artashashta haja yake.Ni heri tumkaribishe Yesu aje akae mioyoni mwetudaima. Wale ambao mioyo yao i wazi kwa kupatamsaada na mbaraka wa Mungu, hao wamoulimwenguni kweli, lakini si watu wa ulimwengu kwasababu hawapendi kufuata mambo na anasa zadunia. Hao nao hupatana na mambo ya mbinguni nakushirikiana na Mungu. KY 104.2

Mwonyeshe Mungu mahitaji yako, furaha yako, uzitowako, mashaka yako na hofu zako. Huwezi kumwudhiMungu wala kumchosha. Yeye ambaye huhesabunywele za kichwa chako, hawezi kuwa na kutojali kwamahitaji ya watoto wake. “Bwana ni mwenye rehemanyingi, mwenye huruma.” Yak. 5:11. Moyo wake waupendo huingiwa na huruma kwa ajili ya huzuni nauzito wetu. Mwambie mambo yote yanayofadhaishamoyo. Hakuna msiba uwezao kumpata hata mtotowake aliye mdogo, wala jambo linalomhangaisha aukumfurahisha, wala hakuna maombi yatokayo moyoni

mwa mmojawapo wa watu wake, bila Baba yetu aliyembinguni kuyaona yote na kusikia mara moja.Huyaangalia na kuyajali mambo yote yanayohusika nawatu wake. “Huwaponya waliopondeka moyo,huziganga jeraha zao.” Zab. 147:3. Mungu humfikiriana kumwangalia kila mtu kana kwamba hakuna mtumwingine wa kumshughulikia ila yeye tu ambayeMwana wake Mpendwa alikufa kwa ajili yake. KY104.3

Yesu alisema, “Mtaomba kwa jina langu: walasiwaambii ya kwamba mimi nitawaombea Baba: kwamaana Baba mwenyewe awapenda ninyi.” Yoh. 16:26,27. “Mimi niliyewachagua ninyi, . . . ili lo lotemmwombalo Baba kwa jina langu, awapeni.” Yoh.15:16. Na kuomba kwa jina la Yesu, maana yake siyokulitaja tu jina lake katika mwanzo na mwisho wa sala.Maana yake ni hivi: katika kuomba kwetu tuwe na niana roho ndani yetu iliyokuwamo ndani ya Yesu nakuziamini ahadi zake, kutegemea neema yake, nakutenda matendo ya namna yake. KY 105.1

Maisha yetu lazima kufanana na maisha ya Kristo,kwa kuomba na kufanya kazi pia. Yeye aombaye tukila mara bila kufanya kazi yo yote, hatimaye maombiyake yatakuwa yasiyo na maana. Wale wasiomtumikiaYesu aliyewatumikia wao sana, hawana mamboyafaayo kuombwa, wala hawana sababu ya kusali.

Watu kama hao hujifikiria nafsi zao wenyewe tu.Hawawezi kuwaombea wengine na kufikiri mahitajiyao, wala kuendesha ufalme wa Kristo na kupatanguvu za kumtendea kazi yake ya Injili. KY 105.2

Tunaona hasara tukikosa kushirikiana kwakuimarishiana katika kumtumikia Mungu. Katikakushirikiana na kuongea kwetu sisi Wakristo twapataupungufu mkuwa sana kwa ajili ya kutokuwa nahuruma sisi kwa sisi kama inavyotupasa. Lakinitukiandamana na watu na kufanya urafiki wa kwelinao, na kujua mambo yao, tunapata kuwahurumiawengine katika haja zao na misiba yao; pia ni njia yakusitawisha mambo ya kiroho na kupata nguvu sisiwenyewe kwa kumtumikia Mungu. KY 106.1

Kama Wakristo wangekuwa wanashirikiana sawasawa, na kuongea juu ya upendo wa Mungu namambo yanayohusiana na ukombozi, mioyo yaowenyewe ingeburundika, pia wangewaburudishawengine mioyo yao. Kama tungezidi kumfikiria Yesuna kuongea juu yake, na kutojifikiria sana nafsi zetu,Yesu angezidi kuwapo pamoja nasi. KY 106.2

Kama tungemwaza Mungu kila mara kama vileMungu anavyotuonyesha uangalifu wake kwetu,angekuwa katika fikara zetu milele. Twazoea kuongeajuu ya mambo ya dunia hii kwa kuwa tunahusika nayo

na kupendezwa nayo. Twaongea juu ya rafiki zetu kwasababu twawapenda. Tunafikiri sana juu ya mambo yamaisha ya kila siku, kama ni ya furaha au ya huzuni.Lakini imekuwa wajibu wetu kumpenda Mungu zaidi,kwa kuwa ametufanyia mema mno; ingefaa kuwadesturi na kawaida yetu kumfikiria Mungu zaidi yawengine wote, na kuongea juu ya wema wake nauwezo wake. KY 106.3

Ni wajibu wetu kumshukuru Mungu zaidi kwa ajili ya“rehema zake na miujiza yake kwa wanadamu.” Zab.107:8. Asili ya kumwabudu Mungu si kutaka na kupatamahitaji yetu hasa. Tusifikiri juu ya haja zetu tu, bilakufikiri mibaraka tunayoipata. Sisi hatuombi zaidikupita kiasi, lakini tunakosa kumtolea Mungu shukranikwa kiasi kipasacho. Twapata rehema zake daima,walakini tunamshukuru kwa machache tu katika yoteambayo ametutendea. KY 107.1

Katika siku za zamani, Waisraeli walipokutanikakatika mkutano wa dini, Mungu aliwaagiza hivi: “Ndipomtakapokula mbele ya Bwana Mungu wenu, nanyimtafurahia kila mtakazotia mikono, ninyi na nyumbazenu, alizokubarikia Bwana Mungu wako.” Kumbu. 12:7. Yote yatendwayo kwa kumtukuza Mungu yafaakutendwa kwa furaha, na shangwe, na shukrani, siyokwa huzuni na moyo mzito. KY 107.2

Mungu wetu ndiye Baba mwenye huruma narehema. Imewapasa watu wake kumfurahia katikakumwabudu na kumtumikia. Yeye ambayeamewawekea watoto wake wokovu mkuu, hatakiwamtumikie kama vile angalitaka msimamizi wawatumwa aliye mkali, na asiye na huruma. Mungundiye rafiki yao aliye bora zaidi; na wanapomwabudunaye hutumaini kuwa pamoja nao, kusudi awabariki nakuwafariji, akijaza mioyo yao furaha na upendo.Mungu ataka watoto wake waburudike moyo katikahuduma yake, tena wasione kazi yake kuwa ni ngumusana, bali wapate kupendezewa katika kumtumikia.Hata na wale wanaokutanika kumwabudu, Munguhutaka wapate kufikiri juu ya uangalifu na upendowake, ili wachangamshwe moyo katika mambo yoteya maisha yao, na kufanya yote kwa haki na uaminifu.KY 108.1

Kristo naye amesulubiwa, na hili ni jambo lakufikiriwa sana, lipasalo kuwa jambo kubwa katikamaongezi yetu. Imetupasa kukumbuka mibaraka yotetunayoipata mkononi mwa Mungu; na kamatunafahamu upendo wake mkubwa usio na kifani, basitukubali kumwekea amana mambo yetu yote, yulealiyesulubiwa kwa ajili yetu. KY 108.2

Huko mbinguni Mungu husujudiwa kwa nyimbo nashangwe. Nasi tunapomtolea Mungu shukrani yetu,

tunamtukuza kama vile anavyotukuzwa na majeshi yambinguni. “Atoaye za kushukuru, ndiye anitukuzaye.”Zab. 50:23. Hivyo tufike mbele zake “kwa zaburi natenzi na nyimbo za roho, mkiimba na kumshangiliaBwana mioyoni mwenu; mkimshukuru Mungu Babasiku zote kwa mambo yote.” Soma Isa. 51:3; Waef5:19. KY 109.1

Tafuta daima utakatifu;Fanya urafiki na Wakristo tu;Nena siku zote na Bwana wako:Baraka uombe kwa kila jambo.

Tafuta daima utakatifu;Uwe peke yako ukimwabudu;Ukimwangalia Mwokozi wako,Utabadilishwa kama alivyo.

Tafuta daima utakatifu;Kiongozi wako awe Yesu tu;Katika furaha au huzuniDumu kumafuata Yesu Mwokozi.

Tafuta daima utakatifu;Umtawaze Roho moyoni mwako;Akikuongoza katika haki,Hufanywa tayari kwa kazi yake. KY 109.2

Sura 12 - Yatupasayo Kufanya Tukiwa naMashaka Moyoni

WATU wengi, hasa walio Wakristo wapya, sikuzingine huwa na mashaka moyoni juu ya mambomengine katika Biblia ambayo hawawezi kuyaelezaama kuyafahamu. Naye Shetani huyatumia mamboyale kwa kuwapunguzia imani yao katika kukubalikwamba Biblia ni ufunuo wa Mungu. Wanasema,“Nawezaje kujua njia iliyo ya haki? Kama kweli Biblia niNeno la Mungu, nawezaje kuondolewa mashaka hayamoyoni, nisije nikashikwa na fadhaa?” KY 110.1

Kila jambo atakalo Mungu tulisadiki, hakosikutubainishia sababu ya kuwa na imani juu ya jambolile. Jinsi Mungu mwenyewe alivyo hai, namna ya tabiazake, na ukweli wa Neno lake, mambo haya yoteyamehakikishwa kwetu kwa namna nyingi. Hata hivyoMungu haoni ni afadhali kutuondolea nafasi ya kuwana shaka. Imetupasa kumwamini Mungu kwa viletunavyobainishiwa mioyoni mwetu juu ya mamboyasiyoonekana, siyo kwa ajili ya mambo yaliyo dhahirikatika macho yetu ya kibinadamu. KY 110.2

Haiyamkiniki kwa nia ya kibinadamu kufahamukabisa namna ya tabia za Mungu wala kazi yake. “Kwakutafuta utampata Mungu? Utampata Mwenyiezi

Mungu alivyo bora? Juu kama mbingu; utafanyaje?Chini kupita ahera; utajuaje?” Ayub 11:7, 8. KY 111.1

Mtume Paulo alisema, “Ee ajabu ya utajiri na hekimana maarifa ya Mungu; hazina hata kiasi! hukumu zakehazichunguziki, na njia zake hazitafutikani!” Warumi11:33. Na hata “mawingu na giza yamemzunguka,”“haki na hukumu maweko ya kiti chake.” Zab. 97:2.Katika matendo yake juu yetu twaweza kufahamumakusudi yake kwa kutosha kuona upendo wake nahuruma yake isiyo na kiasi, na jinsi uwezo wake ulivyomkuu kupita cheo. Twaweza kutambua makusudiyake kwa kadiri inavyotufaa; zaidi ya hayo imetulazimukumtawakali Mwenyiezi Mungu, ambaye moyo wakeumejaa upendo. KY 111.2

Katika Neno la Mungu, vile vile katika sifa yake, kunamambo ya siri wasiyoweza wanadamu kuyafahamu.Jinsi dhambi ilivyoingia ulimwenguni, jinsi Kristoalivyojifanya kuwa na umbo halisi la binadamu, uzaziwa pili jinsi ulivyo, ufufuo, na mengineyo katika Biblia,ni mafumbo makubwa sana kushinda akili zakibinadamu kuyaeleza, wala kufahamu maana yakevizuri. Lakini hatuna sababu ya kuwa na shaka juu yaNeno la Mungu kwa ajili ya kutofahamu mafumbo yauongozi wake na majaliwa yake. Hata katika mamboya ulimwengu na viumbe vyake twaona mafumbomengi tusiyoweza kuyafahamu. Wenye akili sana

wameshindwa kueleza habari za uhai jinsi ulivyo, hatauhai wa vidudu vidogo. M.ahali pote pana maajabutusiyoweza kuyafahamu. Kwa hivyo mbonatunastaajabu tukiambia kuwa kuna mambo ya kirohoyasiyowaza kufahamiwa na kuelezwa na binadamu?Shinda imekuwa kwa ajili ya udhaifu na akili chache zabinadamu. Katika Maandiko yenyewe Munguametuhakikishia jinsi Maandiko haya yalivyo yake,tusione shaka moyoni juu ya Neno lake kwa sababu yakutofahamu mafumbo yake yote. KY 111.3

Mtume Petro amesema kwamba katika Maandiko“yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; namambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara,huyapotoa . . . kwa upotevu wao wenyewe.” 2 Pet.3:16. Wengine husema ya kwamba mafumbo ya Bibliani sababu ya kutosadiki maneno yake: lakini kwa kwelimafumbo haya ni ushahidi mkuu kuwa yametoka kwaMungu. Kama ingekuwa Biblia haina habari za Munguila tu mambo yawezavo kuelezwa kwa urahisi nakufahamiwa na binadamu, Biblia isingekuwa na hakikakwamba ni ya Mungu kweli. KY 112.1

Mafundisho ya Biblia juu ya wokovu, yametolewakwa namna ifaayo kwa mahitaji na matakwa ya moyowa binadamu; watu wastaarabu na wenye elimu nyingiwamevutwa na uzuri wa maneno yake; na hata watuduni waweza kuelewa na kufahamu njia ya wokovu.

Hata hivyo twaweza kuyasadiki hivi tu, kwa kuwaMungu ndiye anayetujulisha mambo hayo. Mpango waMungu juu ya ukombozi wa wanadamu umebainishwavizuri kwetu, ili mtu ye yote ajue la kufanya katikakutubu kwa Mungu, na kuwa na imani kwa Bwanawetu Yesu Kristo, ili apate kuokoka kwa njia aliyoiwekaMungu. Walakini ndani ya mambo haya kunamafumbo ya Mungu yasiyofunuliwa ila kwa yuleanayeyachunguza kwa moyo na bidii. Na kwa jinsianavyozidi kuyachunguza maneno ya Biblia, ndivyoanavyozidi kusadikishwa kwamba ni Neno la Mungualiye hai. KY 113.1

Wenye kumkana Mungu hutupilia mbali Neno lakekwa sababu hawawezi kufahamu mafumbo yake yote.Hata na wengine wanaojidai kuwa wanasadiki Biblia,huona mashaka moyoni juu ya jambo hilo. Mtumeamesema, “Angalieni, ndugu zangu, usiwe katikammoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwakujitenga na Mungu aliye hai. Waeb. 3:12. Ni vizurikujifunza mafundisho ya Biblia, na kuchunguza “hatamafumbo ya Mungu,” (1 Wakor. 2:10 ), kwa kadiriyana- vyofunuliwa katika Maandiko. Ingawa ni “kwaBwana Mungu wetu yaliyo ya siri,” ni kwetu sisi“yaliyofunuliwa,” Kumbu. 29:29. Lakini ni kusudi laShetani kuipotoa njia ya binadamu kama anatakakuyachunguza mambo. Kwa ajili ya ufundi wanaojiona

kuwa nao katika kuchunguza mafundisho ya Biblia,watu wengine huwa wepesi wa kuchukizwawasipoweza kueleza maana ya kila sehemu yaMaandiko kwa namna ya kutosheleza nafsi zaowenyewe. Ni aibu kwao kukiri ya kwambahawayafahamu vizuri. Hawataki kumngojea Munguhata atakapowafunulia maana ya hakika. Huonakwamba akili za kibinadamu zimetoshakuwafahamisha Maneno ya Mungu; nao wakishindwakufanya hivi, basi huyakana kuwa si ya Mungu. Kunamaelezo na mafundisho mengi ya dini yanayodhaniwatu ya kuwa asili yake ni maneno ya Biblia, lakini maanayake ni kinyume cha ukweli wa Biblia. Kwa ajili yamambo hayo watu wengi hushikwa na fadhaa nakuona shaka mioyoni mwao. Lakin imekuwa hivyo sikwa ajili ya Neno la Mungu hasa, ila kwa kuwawanadamu wamepotoa maneno yake. KY 113.2

Kama wanadamu wangeweza kupata kufahamu jinsiMungu alivyo hasa, pamoja na matendo yake, basi,wasingekuwa na jambo jipya la kuvumbua,wasingezidi kuelimishwa tena, wasingepata kuzidishamaendeleo yao ya kiroho. Hapo Mungu asingekuwaMwenye enzi; tena kwa vile ambavyo binadamuangekuwa amefika mwisho wa elimu na maarifa yote,asingepata maendeleo yo yote tena. TumshukuruMungu kwa kuwa si hivyo. Mungu ni mewnye uwezo

wote, mwenye kujua yote; “ndani yake zimo hazinazote za hekima na maarifa.” Wakol. 2:3. Maisha yamilele wanadamu watakuwa wanachunguza nakuendelea kufahamu akili za Mungu, wema wake, naenzi yake, bila mwisho. KY 114.1

Kuna njia moja tu kwa kupata kuelimishwa nakuendelea kufahamu Neno la Mungu, - kama Roho yaMungu inang’aa mioyoni mwetu na kutumuliki.“Mambo ya Mungu hakuna ayajuaye ila Roho yaMungu;” “maana Roho huyachunguza yote, hatamafumbo ya Mungu.” 1 Wakor. 2:11,10. TenaMwokozi aliwaahidia wafuasi wake hivi: “Ajapo yeye,Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli; . .. atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni habari.”Yoh. 16:13, 14. KY 115.1

Mungu ataka binadamu atumie akili zake.Kuchunguza na kujifunza Biblia kunaimarisha rohozetu kwa jinsi isivyowezekana katika kujifunza mamboyo yote mengine. Ili tupate Kufahamu Maandiko, namioyo yetu isifadhaisnwe, imetupasa kuwa na imanina moyo mmoja kama watoto, tuwe tayarikufundishwa ua kumwomba Roho Mtakatifu msaadawake. Tukiona uwezo wa Mungu na akili zake jinsivilivyo kuu zaidi pasipo kiasi, na kuelewa hali yetu yakutoweza kufahamu namna ya utukufu wake, hapobasi imetupasa kunyenyekea; na tunapofunua katabu

cha Neno lake, imetupasa kuwa na heshima naunyenyekevu moyoni kama tupo mbele yake hasa. KY115.2

Kuna mambo mengi ya fumbo, ambayo Munguatawadhihirishia wale watakao kweli kuyafahamu.Lakini bila uongozi wa Roho Mtakatifu binadamuhuelekea kupotoa maneno ya Biblia na kueleza maanaisiyo ya kweli. Masomo mengi ya wanadamu katikaBiblia yamekuwa bure bila faida. Kama kitabu chaNeno la Mungu kinafunuliwa bila heshima na maombi:mtu asipomkazia Mungu fikara zake na upendo wakena kufanya mapenzi ya Mungu, bila shaka atashikwana fadhaa. Ndipo Shetani atayatawala mawazo yake,na kumtilia moyoni mwake maelezo ya Biblia yayasiyo ya kweli. Kila mara wanadamu wasipopatanana Mungu katika maneno na matendo yao, ingawa niwenye maarifa ya namna gani, bila shaka watakosakufahamu Maandiko, tena haifai kuyaamini maelezoyao. Wengi wao walio na mashaka moyoni, asili yakushuku kwao ni kupenda dhambi. Masharti na vizuizivya Neno la Mungu havipendezi wenye moyo wakujisifu; na wale wasiokubali kufanya matakwa yaBiblia yake huwa wepesi kutosadiki kuwa ni Neno laMungu halisi. Bali, wote watakao kwa moyo kujuamatakwa ya Mungu na huyafanya, hao naowatabainishiwa kuwa Biblia na Maneno ya Mungu

yawezayo kuwapa hekima hata wapate wokovu. KY116.1

Kristo asema, “Mtu akipenda kuyatenda mapenziyake, atajua habari ya elimu hii kwamba yatoka kwaMungu.” Yoh. 7:17. Badala ya kubishana bure juu yamambo msiyoweza kuyafahamu, ni heri mfanye kilawajibu wenu kwa vile mnavyofahamu na kuelewa nao,ndipo mtasaidiwa kuyafahamu na kuyafanya yaleambayo sasa mnayaonea mashaka. KY 117.1

Mungu ataka tujihakikishie ukweli wa Neno lake naahadi zake. Asema, “Onjeni mwone BWANA ndiyemwema.” Zab. 34:8. Tusitegemee neno la wengine, ilatuonje sisi wenyewe na kuona wema wake. Asematena, “Ombeni, na mtapata,” Yoh. 16:24. Ahadi zakezitatimia. Haziwezi kuwa na upungufu. Na kwa viletunavyomkaribia Yesu, na kufurahishwa na upendowake, ndivyo nuru yake itakavyong’aa mioyoni mwetu,tena mashaka na giza vitaondolewa. Mtume Pauloasema ya kwamba Mungu alituokoa “na nguvu zagiza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme waMwana wa pendo lake.” Wakol. 1:13. Kila ambaye“amepita toka mauti hata uzima” anaweza kutia“muhuri wake kwamba Mungu ni wa kweli.” Yoh. 5:24;3: 33. Awe- za kushuhudia, “Nimepata msaada kwakeYesu; naye ameniruzuku mahitaji yangu yote,nimeshibishwa njaa ya moyo wangu; tena sasa Biblia

inakuwa kwangu ufuno wa Yesu Kristo. Waniulizambona namwamini Yesu? - Kwa kuwa ni Mwokoziwangu. Kwa nini nasadiki Biblia? Kwa sababu nimeonakuwa ni sauti ya Mungu moyoni mwangu.” Twawezakuwa na ushuhuda ndani yetu kuwa neno la Biblia nikweli, tena Kristo ni Mwana wa Mnngu. Twajuakwamba hatufuati hadithi zilizotungwa kwa werevu. 2Petro 1:16. KY 117.2

Petro awaamuru Wakristo walio ndugu zake, “Kaenikatika neema, na katika kumjua Bwaua wetu, Mwokoziwetu Yesu Kristo.” 2 Pet. 3:18. Watu wa Munguwakikaa katika neema yake, watazidi kudhihirishiwaNeno lake. “Matembezi yao wenye haki kama nurunyeupe, iangazayo ikizidi hata mchana utimiapo.”Methali 4:18. KY 118.1

Kwa imani twaweza kutazama mbele hata mpakaufalme wa Mungu, na kutumaini ahadi ya Mungu juuya kutuzidisha akili, na jinsi uwezo wetu woteutakavyoungamana na uwezo wa Mungu. Twawezakufurahi kwa kuwa yote ambayo sasa tumeshikwa nafadhaa nayo, hapo ndipo yatadhihirishwa kwetu;mambo yanayokuwa magumu kufahamiwa, wakatihuo yataelezwa dhahiri. “Wakati wa sasa tunaona kwakioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso;wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ulenitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.” 1

Wakor 13:12. KY 118.2

Kumtegemea Mwokozi,Kwangu tamu kabisa;Kukubali Neno lakeNina raha moyoni.

Kumtegemea Mwokozi,Kwangu tamu kabisa;Kuamini damu yakeNimeoshwa kamili.

Kumtegemea Mwokozi,Kwangu tamu kabisa;Kwake daima napataUzima na amani.

Nafurahi kwa sababuNimekutegemea;Yesu, Mpendwa na RafikiUwe nami dawamu. KY 119.1

Sura 13 - Kufurahia Mungu

WATU wa Mungu wameitwa wajumbe wa Kristo, kwakutangaza wema wa Bwana na rehema zake. Kwa vileYesu alivyotudhihirishia sifa za Baba, hivyo na sisiimetupasa kuwadhihirishia wengine wasiomjua Kristojinsi alivyo mwenye upendo, na mwenye huruma. Yesualisema, “Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, namivivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni.” Mimi ndaniyao, na wewe ndani yangu,. . . . ili ulimwengu ujue yakuwa ndiwe uliyenituma.” Yoh. 17:18, 2, 3. MtumePaulo huwaambia wanafunzi wa Yesu,Mnadhihirishwa kuwa ni barua ya Kristo,”inavyojulikana “na kusomwa na watu wote.” 2 Wakor.3:3, 2. Kila mmoja wa watoto wake ni kama baruaYesu anayoipeleka ulimwenguni. Kama wewe nimfuasi wa Kristo, u barua yake anayoipeleka kwajamaa zako, mji wako na mtaa unaokaa. Yesu akaapondani yako, anataka kusema kwa mioyo yaowasiomjua. Pengine hawasomi Biblia na kusikia sautiyake humo; hawatambui upendo wa Mungu kwakuumba kwake. Lakini kama wewe ni mjumbe wakewa kweli, pengine kwa sababu ya mwenendo wakomwema na matendo yako mema, wataongozwawapate kujua kidogo wema wake ua kuvutwa kwakeYesu, hata kumpenda na kumtumikia. KY 120.1

Wakristo wamewekwa kuwaangazia wengine njiaiendayo mbinguni; kuwaonyesha nuru itokayo kwaKristo. Mienendo yao na sifa zao vyapasa kuwa safi,kuwajulisha wengine hakika ya Kristo na namna yakumhudumia. KY 121.1

Nasi tukiwa wajumbe wa Kristo kweli tutakuwa watuwa furaha. Wakristo ambao huzoea kuwa na mioyomizito, wagunao na kunung’unika, huonyesha wenginemfano usio wa kweli juu ya Mungu na maisha yakikristo. Wale ambao mienendo yao na desturi zaozinafanya wengine kudhani kwamba Munguhapendezwi kama watu wake wanafurahi, hao naowanamshuhudia uwongo Baba yetu aliye mbinguni.KY 121.2

Shetani husimanga sana anapoweza kuwatilia watuwa Mungu fikara za kutoamini na kufa moyo. Hufurahisana tukiona mashaka mioyoni juu ya Mungu jinsianavyotupenda na kuweza kutuokoa. Ni kazi yaShetani kumtangazia Mungu kuwa hana huruma narehema. Hujaribu kuutia moyo wa binadamu fikara zauwongo juu ya Mungu; nasi mara nyingi twasikilizahabari zile za uwongo, na kutomheshimu Mungu kwaajili ya kutomwamini na kumnung’unikia. Shetanihujaribu kuwatia watu fikara kuwa njia ya kikristo ni yataabu na shida. Tena Mkristo kama anaonyeshamashaka haya katika maisha yake, ni kama kusema

yu pamoja na Shetani. KY 121.3

Wengi hufikiri sana juu ya makosa yao, upungufuwao na dhiki zao, hao nao mioyo yao hujaa huzuni nauchungu. Je, katika maisha yako hujapata mamboyafaayo kuyafurahia? Hata nyakati zingine hujaonafuraha moyoni mwako kwa ajili ya mvuto na uongoziwa Roho ya Mungu? Hata hujaona uzuri wa ahadi zaMungu? KY 122.1

Kudumu kufikiri mambo haya yanayoutia moyouchungu na kukata tamaa, ni kama kukusanya miibana viwavi vinavyotuchoma na kutuuma, bila kuonamaua na matunda jinsi yalivyo mazuri na yakufurahisha moyo. Yule ambaye amekata tamaa,moyo wake umekufa ganzi, haoni nuru ya Mungumoyoni mwake, pia huwatia wengine giza njianimwao. KY 122.2

Tumshukuru Mungu kwa vile ambavyoametuhakikishia upendo wake kwa njia nyingizitupasazo kuzifikiri mara kwa mara; Mwana waMungu jinsi alivyoacha utukufu wake, na kuwa katikamfano wa kibinadamu ili apate kutuokoa katikamamlaka ya Shetani; jinsi alivyomshinda Shetani, nakuinua binadamu toka katika hali ya uhalifu ambaoaliuangukia kwa ajili ya dhambi, na kutupatanisha tenana Mungu; naye binadamu akivumilia na kustahimili

hata mwisho kwa kumwamini Mwokozi, jinsiatakavyovikwa nguo nyeupe, yaani haki itokayo kwaMungu, kwa imani - hayo ni mambo ambayo Munguataka tuyafikirie. KY 122.3

Ikionekana kwetu kana kwamba tuko katika hali yakutosadiki upendo wa Mungu na ahadi zake,tunamdharau Mungu na kumhuzunisha Roho wakeMtakatifu. Mama fulani angeonaje kama watoto wakewangemnung’unikia mara kwa mara kama asiyetakakuwatendea vizuri, naye hudumu kuwakifiri nakuwatendea mema? Na sisi je, Baba yetu aliyembinguni ataonaje kama tunamdharau kwa upendowake jinsi alivyomtoa Mwana wake wa pekee ili tupateuzima? Mtume Paulo alisema, “Yeve asiyemwachiliaMwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi,atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja naye?”Warumi 8:32. Hata hivyo kuna wengi ambao kwamatendo yao, si kwa maneno hasa, huwa wanasema,“Maneno haya ya Mungu hayanihusu mimi. Pengineawapenda wengine, lakini si mimi.” KY 123.1

Katika kufanya hivyo unajihatarisha moyo wakomwenyewe; kwa kuwa kila mara unaposema manenoya kushuku na kutoamini, unazidi kujithibitisha katikakutoamini; tena si wewe mwenyewe tu ambayeunajihatarisha kwa tendo hili; hata na wale ambaowanasikia maneno yako watavutwa kuwa na shaka

pia, tena pengine haitawezekana kubatilisha matokeoya maneno yako jinsi yatakavyokuwa mwishowe.Wewe mwenyewe labda utaweza kuokoka katikamtego wa udanganyifu wa Shetani, lakini walewaliovutwa nawe, pengine hawataweza kuondolewamawazo yale uliyowatilia mioyoni mwao. Hivyoinatupasa sana kusema mambo yale tuyatakayozidisha nguvu na uzima wa kiroho! KY 123.2

Watu wote hupata majaribu: mambo ya kutiamajonzi na huzuni, ambayo ni vigumu kuyastahimili;na mivuto ya Shetani, ambayo ni vigumu kuipinga.Tusiwasimulie wanadamu wenzetu taabu zetu namambo ya kuwatilia mashaka mioyoni mwao; ilatumwonyeshe Mungu shida zetu zote katika sala zetu.Kwa namna ya maisha na maneno yetu, wenginewaweza kutiwa moyo na kuzidishiwa nguvu, amawaweza kuingiliwa na mashaka na kuzuiliwawasimtake Kristo na ukweli wake. KY 124.1

Ni kweli Mwokozi wetu alikuwa mtu wa huzuni,ajuaye taabu, kwa kuwa alichukua huzuni zote zawanadamu. Lakini ijapokuwa hivyo, moyo wakeulikuwa mtulivu, nao ulikuwa kama chemchemi yauzima; po pote alipokwenda, aliwatilia watu raha,amani, furaha na shangwe mioyoni mwao. Alikuwamtu wa moyo wa juhudi, asiye na chuki, wala mwenyeuso mzito kamwe. Maisha yao wanaomfuata Mwokozi

yatakuwa na kusudi jema; watafaha- mu jinsi walivyona mzigo wa kuwa mfano wake mbele ya wengine.Hawatatoa ubishi na upuzi au kufanyiza mzaha, kwakuwa dini ya Yesu ni yenye adibu na ya utaratibu: nidini ya amani. Dini hii haizimi furaha wala kuzuiaukunjufu au vicheko vya upendo. Kristo hakujakuhudumiwa bali kuhudumu; upendo wake ukiwamomoyoni tutafuata mfano wake. KY 124.2

Tukifikiri sana juu ya makosa ya wengine, ukali waona matendo yao yasiyo na haki, haitawezekana kwetukuwapenda jinsi Kristo alivyotupenda sisi. I lakinitukifikiri zaidi juu ya pendo la ajabu na hurumaambayo Kristo anatuonyesha, haitakuwa vigumukwetu kuonyesha roho ile ile kwa wengine.Tungependana na kuheshimiana ingawa tunajuanakuwa tunayo makosa. Tungejifunza kujidhili na kuwana unyenyekevu na kuyavumilia makosa ya wenginekwa upole mwingi. Hivyo nia ya kujipendeza nafsi zetuitaondolewa na tutajawa na ukarimu wa moyo. KY125.1

Mtunga Zaburi asema, “Umwamini Bwana, ukatendemema; ukae kwa nchi, ukaishike amini.” Zab. 37:3.“Umwamini Bwana.” Kila siku inaleta taabu namahangaiko yake; nasi tu wepesi kuzungumza nawenzetu juu ya shida zetu na majaribu yetu, kanakwamba hatuna Mwokozi atupendaye, aliye mwepesi

kusikia haja zetu zote, naye yu karibu sana kutusaidiakatika shida. KY 125.2

Wengine huzoea kuwa na hofu na kutazamia shidaisiyokuwapo bado. Siku zote sisi huzungukwa na vituvinavyoonyesha upendo wake; kila siku hufurahishwana wingi wa majaliwa ya Mungu; lakini wengine wetuhusahau mibaraka ya sasa hivi, na huzoea kufikirimabaya wanayodhani labda yatakuja. KY 126.1

Je, imetupasa kutokuwa na shukrani na amini hivi?Yesu ndiye rafiki yetu. Wa mbinguni wote hutufikirisisi. Tusife moyo; tumtwike Bwana taabu zetu zote,nasi tuwe na amani na uchangamfu. TumwombeMungu hekima na akili katika kufanya shughuli zetu, ilitusipate hasara na misiba. Yesu ameahidi msaadawake, lakini inatupasa pia tufanye juhudi sisiwenyewe. Mungu hapendi ili tutaabike. Bwana wetuhatudanganyi. Hasemi, “Msiogope; hamtapatakuhatarishwa kamwe.” Si kusudi lake kuwatoa watuwake katika dunia palipo dhambi na maovu, lakinihuwaonyesha mahali pa kukimbilia kwa kupatamsaada. Aliwaombea wafuasi wake hivi: “Siombiuwatoe katika ulimwengu, bali uwalinde na yulemwovu.” Alisema pia’ “Ulimwenguni mtapata shida:lakini jipeni moyo: mimi nimeushinda ulimwengu.”Yoh. 17:15; 16:33. KY 126.2

Katika mafundisho yake mlimani, Kristoaliwafundisha wafuasi wake kwamba ni lazimakumtumaini Mungu. Mafundisho haya yali- kusudiwakusaidia watu wa Mungu siku zote hata siku hizi iliwajipe moyo. Mwokozi aliwaonyesha ndege za anga,jinsi waimbavyo bila kufadhaika moyo; “hawapandi,wala hawavuni.” Lakini Baba aliye mbinguni awalisha.Ndipo Mwokozi anauliza, “Ninyi je! si bora kupita hao?”Mattayo 6:26. Baba mkuu hufunua mkono wake,huviruzuku viumbe vyake vyote mahitaji yao. Ndegehawana budi kudonoa punje za nafaka na vituvinginevyo vinavyokuwa chakula chao. Imekuwa juuyao kuokota vitu vya kutengeneza viota vyao.Wamelazimishwa kuwalisha watoto wao. Hao naohuondoka kufanya kazi yao na wimbo kwa kuwa “Babayenu wa mbinguni awalisha hao.” Na “ninyi je! si borakupita hao?” Naye alituumba sisi katika mfano wakemwenyewe, naye angekosa kuturuzuku mahitaji yetukama tunamtumainia? KY 126.3

Kristo alielekeza nia za wafuasi wake kwa maua yamashamba, jinsi yameavyo. Alisema kwamba “hataSulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kamamoja la hayo.” Naye Yesu auliza, “Lakini Munguakiyavika hivi majani ya mashamba, yaliyopo leo, nakesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavikaninyi, enyi wa imani haba?” Mattayo 6:28, 30. Fundisho

hili la Kristo linakaripia masumbufu na mahangaiko yamoyo usio na amani. KY 127.1

Mungu ataka watu wake wote wawe na moyo wafuraha na utulivu, na usikivu. Yesu alisema, “Amaninawaachieni; amani yangu nawatolea; si kamaulimwengu utoavyo, mimi nawatolea. Msifadhaikemioyo yenu, wala msiwe na woga.” “Hayanimewaambieni, ili furaha yangu iwe ndani yenu, nafuraha yenu itimizwe.” Yoh. 14:27; 15:11. KY 127.2

Furaha inayotakiwa na mtu fulani kwa ajili yakujipendeza mwenyewe tu, bila kufanya yanayompasa,hiyo ndiyo furaha isiyofaa, isiyo na faida, furahaisiyodumu. Lakini katika kumhudumia Mungu, Mkristoaweza kupata furaha na kuridhishwa moyo. Ingawatunakosa anasa za maisha haya, twaweza kuonafuraha moyoni katika kutumainia maisha yajayo yamilele. KY 128.1

Lakini hata hapa duniani Wakristo waweza kufurahikatika kumshiriki Kristo na kuongea naye; wawezakujua upendo wake, na kufarijiwa moyoni. Kila sikukatika maisha haya ya sasa twaweza kuzidikumkaribia Yesu na kuzidi kujua upendo wake jinsiulivyo kwetu. Tusiutupe ujasiri wetu; bali tushikamanesana “na ujasiri wetu, . . . kwa kutumaini mpakamwisho.” Waeb. 10:35; 3:6. “Hata sasa Bwana

ametusaidia,” pia atatusaidia mpaka mwisho. Ni heritudumu kufikiri mambo yaliyo ukumbusho kwetu, jinsiBwana alivyotusaidia na kutuokoa mkononi mwakealiye mharabu. Tukizoea kukumbuka jinsi Mungualivyotuhurumia - machozi ambayo ameyafuta katikamacho yetu, maumivu yetu aliyovatuliza, jinsialivyotuondolea fadhaa na hofu mioyoni mwetu, jinsialivyoturuzuku mahitaji yetu, na mibaraka yakeambayo tumeipata - tutajipa moyo kwa kujiwezakustahimili yote yatakayotupata katika siku zijazo. KY128.2

Katika mashindano ya yule mwovu yatakayokuwakwa siku zijazo, twajua ya kwamba tutafadhaikamoyoni; lakini kwa vile tunavyofikiri mambo yaliyopitana kusema, “Hata sasa Bwana ametusaidia,” twawezakutazamia mambo yatakayokuja na kujua hivi: “Nakadiri ya siku kadhalika nguvu zako.” 1 Sam. 7:12;Kumbu. 33:25. Majaribu hayatakuwa makali kushindanguvu tutakayopewa kuyastahimili. Kwa hiyo tushikekazi yetu jinsi ilivyo, na kutumaini kwamba tukipatwana jambo lo lote, bila shaka tutapewa nguvu kwa kadiriya jaribio lile ili tuweze kustahimili. KY 129.1

Hatimaye milango ya mbinguni itafunguliwakuwakaribisha wana wa Mungu, naye Mfalme wautukufu atawaambia, “Njooni, mliobarikiwa wa Babayangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa

ulimwengu.” Mattayo 25:34. KY 129.2

Ndipo waliokorabolewa watakaribishwa hapo Yesuanapowaandalia. Hapo majirani zao hawatakuwawaovu wa dunia, waongo, makafiri, wasio na usafi nawenye kutoamini; bali watashirikiana naowaliomshinda Shetani, wenye kufanana na Mungu nakuwa na sifa kamili. Kila tamaa ya dhambi, kilaukosefu na hila ambavyo tunavyo katika hali yetu yasasa, vitakuwa vimefutwa na damu ya Kristo; hao naowatapata uzuri usio na kiasi na kuwa na utukufu waKristo. Watakuwa na sifa kamilifu kwake; watasimamambele ya “kiti cha enzi, cheupe, kikubwa,” wakiwahawana hila na mawaa. KY 129.3

Kwa sababu ya utukufu wa urithi uliowekwa kwake,“mtu atatoa nini badala ya roho yake?” Mattayo 16:26.Hata amekuwa maskini, mwana wa Mungu huwa nautajiri na heshima ambavyo haviwezi kupatikana kwadunia. Moyo uliokombolewa na kusafishwa dhambi,na kujitoa kumtumikia Mungu, umekuwa wa thamanikubwa isiyokadiriwa; iko furaha mbele ya Mungu namalaika zake kwa mwenye dhambi mmoja atubuye,furaha inayoonyeshwa kwa nyimbo za shangwe. KY130.1

Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;Siku ile shangwe tele nikimwona Mwokozi.

Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;Na kwa utukufu wake nitamwona milele.Sasa siwezi kujua jinsi alivyo hasa;Bali atakapokuja, nitamwona halisi.Mbele yake yafukuzwa machozi na huzuni;Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.Uso kwa uso! Hakika palepale furaha;Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi. KY 130.2