katiba yetu miss demokrasia tanzania

58
KATIBA YETU www.missdemocrasiatz.com ,http://www.ustream.tv/channel/miss- demo-tz Balozi wa Demokrasia Tanzania MISS DEMOKRASIA TANZANIA &ENTERTAINMENT COMPANY LIMITED- MIDETA P.O BOX 8017 DAR ES SALAAM, TANZANIA Tel: +255-767/713- 869133/ FAX: +255 (22)767869133 12/6/2012 BALOZI WA DEMOKRASIA TANZANIA [email protected] [email protected] www.missdemokrasia.blogspot.com www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.

Upload: mpalule-shaaban

Post on 17-Feb-2017

200 views

Category:

Education


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

KATIBA YETU

www.missdemocrasiatz.com,http://www.ustream.tv/channel/miss-demo-tz

Balozi wa Demokrasia Tanzania

M I S S D E M O K R A S I A T A N Z A N I A & E N T E R T A I N M E N T C O M P A N Y

L I M I T E D - M I D E T A

P . O B O X 8 0 1 7 D A R E S S A L A A M , T A N Z A N I A

T e l : + 2 5 5 - 7 6 7 / 7 1 3 - 8 6 9 1 3 3 /

F A X : + 2 5 5 ( 2 2 ) 7 6 7 8 6 9 1 3 3

1 2 / 6 / 2 0 1 2

BALOZI WA DEMOKRASIA TANZANIA

[email protected]

[email protected]

www.missdemokrasia.blogspot.com

www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com

www

Page 2: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

SEHEMU YA KWANZA

BALOZI wa Demokrasia nchini Tanzania ni shindano maalumu kwa ajili ya kuwapata wawakilishi wa Demokrasia kila mwaka, linafanyika katika mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Kati na Vyuo Vikuu Katika Michezo na Elimu. Lengo kuu ni kuwajenga Vijana kujiamini katika masuala mbalimbali ya kiutendaji na ambao wataiwakilisha Tanzania Kitaifa na Kimataifa.

SEHEMU YA PILI

Utangulizi

Baada ya miaka 50 ya Uhuru, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukuza demokrasia na utawala bora. Kumekuwa na mabadiliko makubwa katika kutambua -Haki za binadamu, na hasa haki za wanawake. Idadi ya wanawake wanaoshiriki katika shughuli za serikali imeongezeka, msingi wa haki za binadamu pamoja na utamaduni wa kisiasa na kijamii.

Kwa nini Tanzania kumsaka Balozi wa DEMOKRASIA?

"Ambassador of Democracy in Tanzania"

Balozi wa Demokrasia Tanzania ni mkakati mkubwa unaolenga kukuza demokrasia Tanzania. Lengo ni kuwainua na kuwaimarisha wanawake kisiasa ambao katika miongo kadhaa wamekuwa wakisahaulika katika nyanja hii. Mpango huu ni mahususi katika kuchagiza agenda yetu ya kisiasa, katika kuimarisha demokrasia yetu ikiwa ni pamoja na kuendeleza mshikamano, Uhuru, Amani, Utamaduni na siasa, katika kuijenga Tanzania iliyo bora.

Balozi wa Demokrasia Tanzania, ni maadhimisho ya demokrasia tuliyonayo hapa

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 3: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

nchini, kupitia idadi kubwa ya Wanafunzi Vijana ambao ni wasomi wa Vyuo vya elimu ya kati na elimu ya vyuo Vikuu Tanzania. Dhumuni la maadhimisho haya ni kuleta changamoto kwa viongozi wetu kwa njia ya Mitandao, miadhara, Mikutano, Makongamano, na midahalo mbalimbali.

Demokrasia Kama falsafa ya kisiasa inalenga kuleta maendeleo ya binadamu, kutambua thamani ya mtu binafsi na kuwaleta watu wote pamoja katika masuala mbalimbali kama jamii moja ya binadamu kwa njia ya demokrasia, ili isifike wakati watu wakakata tamaa ya malengo imara waliyojiwekea kutokana na mfumo wowote wa utawala kisiasa, bila kusaidiwa.

Demokrasia ya kudumu ni zao linalo chagizwa na wananchi wenye uwezo wa kutambua mipango na matarajio katika mikakati (sera) za nchi yao. Demokrasia ya kweli lazima ihakikishe uhuru kutoka katika utumwa wa aina yoyote ile, unyonyaji na ubaguzi (rangi na kijinsia) kwani mambo haya yote hudhoofisha maendeleo ya wanawake, kwa kuyapa kipaumbele maslai ya watu wachache.

Haki ya kushiriki katika mipango kisiasa ina maana zaidi ya uchaguzi huru na wa haki, na pia inahusisha ushiriki na taarifa za wanawake ambao mara nyingi wameachwa katika maamuzi ya sera.

Utulivu wa kisiasa ni hali ambayo inawezesha jamii nzima ikiwa ni pamoja na wanawake wa taifa husika kufikia malengo yao wenyewe, watu kuwa na maadili mema na kwa ajili ya wao kuwa na sababu ya kushirikiana na kila mmoja.

Ni katika mawazo na ubunifu huu kwamba "Balozi wa Demokrasia Tanzania" ndiyo pekee inayokuja kwa taswira ya:-

* Kujenga uelewa mkubwa wa dhana na kutekeleza Demokrasia miongoni mwa wanawake vijana.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 4: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

* Ili kuongeza ushiriki wa wanawake vijana katika michakato ya kisiasa.

*Kuwapa wanawake vijana sauti katika kuchagiza Tanzania kisiasa (landscape).

* Kuandaa wanawake vijana kwa ajili ya uongozi makini wa baadaye.

*Kuchunguza vipaji, ubunifu wa wanawake vijana.

*Kutoa mazingira mazuri kwa ajili ya kujieleza binafsi na utambuzi wa ndoto zao.

* Zinazozalishwa ujasiri na kujiamini katika wanawake vijana na hamu ya kukabiliana na changamoto ya maneno ya umma.

*Kuendeleza roho ya urafiki na uzalendo miongoni mwa wanawake vijana.

*Kuendeleza mabadiliko chanya katika hali ya hewa Tanzania kisiasa.

* Kujitokeza Kuhifadhi na kulea Demokrasia yetu.

*Kuimarisha Demokrasia yetu na kujenga utulivu wa kisiasa.

Malkia wa Demokrasia Tanzania watakuchukua nje ya baadhi ya miradi ambayo ni pamoja na:

* Safari nchini kote, na kufanya mechi ya umma na kufanya mahojiano na vyombo vya habari

* Kufanya ziara za utetezi wa Viongozi wa jamii na Bunge katika ngazi zote za Serikali.

* Kushirikiana na Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Ushirika wa Umma, Benki, Makanisa, Misikiti, Balozi, NGOs, CBOs, Vombo vya habari nk kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo ya jamii na matendo ya upendo.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 5: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

* Ziara za kutembelea Watoto wanaoishi katika mazingira magumu, yatima na Wajane.

* Kuandaa warsha za uwezeshaji kwa wanawake na vijana

* Kuandaa mipango ya kuyawezesha makundi chini (priviledged) na wanyonge katika jamii

* Kufanya mipango ya kutetea kuhusika zaidi wanawake katika utawala.

SEHEMU YA TATU

DEMOKRASIA NI

Utawala wowote wa Demokrasia ni ule unaotokana na ridhaa ya wananchi, ambao kutokana na utaratibu waliojiwekea hufanya maamuzi ya kuwapata viongozi wao. Raia kila mmoja kwa nafasi yake anayo haki ya kushiriki kutoa maoni ya kuwapata wawakilishi, kwa mantiki hiyo wananchi ndio waajiri wa viongozi walioko madarakani.

Kama ilivyo ada wananchi ndio hufanya maamuzi ya kuwapata viongozi wao wa dola ambao huwajibika kwa raia na raia wanathibitisha imani kwa viongozi hao wakati wa uchaguzi.

Kama ilivyo kauli mbiu kuwa binadamu wote ni sawa na kila mtanzania anayo haki kuishi mkoa wowote Tanzania isipokuwa asivunje sheria na taratibu za nchi, kuchagua ama kuchaguliwa ni tendo linalotarajiwa kwa kila mtanzania, ili mradi tu awe ametimiza matakwa yanayohitajika, hivyo kila mmoja ana haki sawa kushiriki katika kufanya maamuzi, na kusimamia ustawi wa watu wote kwa manufaa ya watu Katika kuzingatia Demokrasia kila wanachokifanya na si kile wanachofanyiwa katika kukuza uhuru, usawa na haki kwa wote katika kusimamia

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 6: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

ukuzaji wa ushiriki wa moja kwa moja katika kuwakilisha jamii ikijidhihirisha kwa njia ya kushiriki katika chaguzi.

Demokrasia ina thamani kubwa katika kuendeleza Elimu, kulinda na kuthamini Afya na Katiba, Sheria za nchi na Mazingira, Jamii katika kukuza uchumi, kuendeleza Burudani Utamaduni na Michezo, mtawala na mtawaliwa, pamoja na maeneo ambayo ni muhimu katika kuleta maendeleo kwa jamii.

B: LENGO LA MASHINDANO

Lengo la mashindano ni kuibua vipaji kwa vijana, kuwapa uzoefu katika uongozi na utawala, kujenga misingi ya Utawala Bora, kurekebisha mmomonyoko wa Maadili yasiyofaa, kutangaza Tanzania Kitaifa na Kimataifa, kuondoa ubaguzi wa aina yoyote, kuhamasisha jamii katika kutunza mazingira ya haki za mwanadamu, kuelimisha jamii katika mavazi, kuwapa mafunzo vijana juu ya elimu ya kutambua misingi ya Demokrasia na Historia ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na Kutoa changamoto kwa Viongozi, Msukumo wa Uwajibikaji katika kuleta Maendeleo.

Shindano litasaidia kukuza na kupata Vijana wa Taifa makini na watawala wa taifa la kesho wakiwa na vipaji mbalimbali kulingana na mahitaji ya Nchi Tawala na Tawaliwa, kulinda na kusimamia Demokrasia kwa misingi yake yote, kusaidia kukuza tasnia ya Elimu ya Kisasa ya Teknolojia endelevu.

Kutoa mwamko kwa Makampuni kusaidia na kutunza vijana ikiwa ni pamoja na kujenga moyo wa ushirikiano na mshikamano kwa uzalendo na upendo, amani, umoja wa taifa na mataifa nchi na wananchi wa nchi na nchi.

Kuwaandaa vijana kuwa viongozi kitaifa na kimataifa ambao watakuwa na majukumu ya kuhamasisha maelewano, ushirika na umoja miongoni mwa nchi na mabara yote ulimwenguni kwa kutangaza Uhuru wa mtu kwa jamii pamoja na

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 7: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

kutembelea vijiji katika kuratibu na kufuatilia masuala ya uzingatiaji haki za binadamu, misingi ya utawala bora, kutoa elimu ya Uraia, kuhamasisha katika kupata viongozi watakaochaguliwa kwa haki bila kutumia Rushwa, kusaidia kueneza elimu ya haki za binadamu kwa jamii.

Kumbuka kuwa -Balozi wa Demokrasia Tanzania - ni Ubunifu ambao utasaidia kuongeza kiwango cha ushiriki wa raia katika chaguzi na kuongeza hamasa na idadi ya wapiga kura, kwa kuwa Demokrasia huanzia majumbani.

Mashindano yanalenga kudumisha haki, Usawa, Umoja, Upendo, Uhuru, Uzalendo na Amani, kwa jamii na watu wote kupanua uelewa juu ya Demokrasia na kupanua mtandao wa Elimu ya demokrasia kupitia washiriki na mashindano haya,“ Taifa lisilo na Demokrasia ni Taifa Mfu”

Shindano hili la Balozi wa Demokrasia Tanzania , Fainali na matukio yake ni sehemu ya mafunzo na maboresho katika maisha ya mwanadamu ikiwa ni nyenzo na mahitaji kidunia katika kutambua haki, Usawa, Umoja na kutangaza sera na Misingi ya Utawala bora, uhuru, wakati wa kujiburudisha, katika kutembea na wakati wa kusafiri katika kubadilishana mawazo bila kujali rangi, taifa, nguvu za kiuchumi pamoja na Imani ya Kidini jukwaani na hata nje ya jukwaa.

Mikoa yote na Kanda zote za Tanzania zikiwemo kanda Maalum za Vyuo Vikuu vya Tanzania Kanda hizo ni kanda ya Kaskazini (Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara) kanda ya ziwa (Bukoba, Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga), Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma, Katavi na Rukwa) Kanda ya kati (Dodoma na Singida) kanda ya mashariki (Pwani, Dar es Salaam na Morogoro) Kanda ya kusini (Mtwara na Lindi) na kanda ya nyanda za juu kusini (Iringa, Njomba, Songea na Mbeya) na kanda ya Zanzibar (Unguja na Pemba) itafanya fainali za Taifa za Kupata Balozi mwakilishi wa Demokrasia katika kuwania taji kubwa Zaidi la Demokrasia

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 8: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Tanzania kila Mwaka.

Shindano hili ndilo pekee linaweza kuwaweka karibu Wanasiasa na wananchi, wakionyeshwa kwa Mifano mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambua Utawala Bora, Kampeni bila Rushwa, Misingi ya Uongozi, Chaguzi za Kidemokrasia, Elimu ya Uraia, Uchaguzi na Kura, Umuhimu wa Chaguzi za Kidemokrasia, Mfumo wa Chaguzi Tanzania, taarifa za msingi juu ya taasisi zinazosimamia chaguzi, mchakato wa Uchaguzi, Umuhimu wa Ushiriki wa watu katika Demokrasia, Ushiriki wa Wote ndani ya Demokrasia, Uongozi na Uraia, Vikwazo vya Chaguzi za Kidemokrasia, Utawala wa Kidemokrasia, Utawala na Taasisi za Utawala, Njia za Kuimarisha Utawala bora, Misingi ya Katiba, Haki za Raia na Utawala bora, maana ya haki na kazi za katiba,Mgawanyo wa Madaraka, Utawala wa Sheria, Haki na wajibu wa Raia.

MFUMO WA SHINDANO

Shindano hili ni tofauti na Mashindano Mengine.

Fainali kubwa za mashindano haya zitafanyika kila baada ya miaka mitano ikiwa ni baada ya kukusanya taarifa mbalimbali za maoni baada ya kumalizika mchakato mzima wa uchaguzi ambapo washiriki baada ya kufanya ziara ya kutembelea wananchi watawasilisha tathmini ya makusanyo ya Maoni ya wananchi kwa njia ya maswali, kujibu mada, kuhusiana na mchakato mzima kutoka kwenye Majimbo yao.

Kabla ya Fainali hiyo kuu ya taifa, kwa kipindi chote mashindano haya yatafanyika kuanzia kwenye majimbo yote ya Uchaguzi Tanzania kwa lengo la kupata wawakilishi watakaoshiriki kuwania Tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Balozi wa Demokrasia Tanzania, Miss Demokrasia Tanzania, Mr. Demokrasia Tanzania

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 9: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

kwa lengo la kuwapata Wawakilishi wa Demokrasia Tanzania, kwa pamoja itatajwa kwa majina ya Majimbo, Wilaya, Mikoa na Tanzania- Balozi wa Demokrasia(Ambassador of Democracy)ambapo itashirikisha wasanii mbalimbali katika kupamba onyesho mahala husika.

Shindano litashirikisha Wasichana na Wavulana kulingana na idadi waandaaji watakayopendekeza- chini ya Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment Co LTD, huku washiriki wakiwa ni :-

(a)- Vijana wenye upeo wa kuelewa na kuelewesha jamii kuhusu masuala yatokanayo na Demokrasia, hususani wasomi wa vyuo vikuu ngazi za mikoa katika kupata wawakilishi bora wa Kitaifa, bila kuendana na itikadi za Chama, Dini, Kabila, Rangi na jimbo analotoka, hivyo washiriki watashindana katika kutembea, Debate -kujibu maswali yatakayoulizwa na majaji na Mavazi stahiki katika Demokrasia.

(b)- Washiriki lazima wawe wamehitimu elimu ya Sekondari hivyo kuwa katika Chuo au Kuhitimu Elimu ya Chuo na wananchi wa kawaida watashiriki katika kuibua vipaji kuanzia ngazi za vijiji, Majimbo na Wilaya ambapo kupitia Mawakala watachujwa kupata wawakilishi wenye uwezo wa kujieleza mbele ya jamii na kuwa na ushawishi kwa majaji ambapo wataungana na wenzao wa vyuo vikuu.

(c)-Mchujo wa kuelekea Fainal kuu za Taifa zitajumuisha washindi wa Vyuo Vikuu ndani ya nchi na Washindi ambao ni Watanzania Vyuo Vikuu kutoka nje ya Mipaka ya nchi, Mikoa na Wilaya ya Tanzania Bara na Zanzibar.

d)-Fainali kuu ya kupata Balozi wa Demokrasia Tanzania, washindi watachaguliwa na wananchi kwa njia ya maoni kupitia vyombo vya habari, kwa kushirikiana na BASATA, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mwenyekiti wa Vyuo Vikuu Tanzania, Majaji,

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 10: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

na kamati kuu ya Miss Demokrasia Tanzania ambao ndio waandaaji wa Mashindano, Kabla ama baada ya Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani kutegemeana na waandaaji watakavyopendekeza.

E)-Pia kutafanyika Mashindano ya Vyuo kwa Vyuo, Hii itahusisha Viongozi wa Serikali za Wanafunzi katika Debate ambayo kila kiongozi atajielezea kulingana na Ufahamu wake kuhusu Uongozi na Mambo mbali mbali yanayohusiana na Demokrasia, Utawala, ili kupata Chuo Bora ambacho kitawasilisha mada nzuri kwa jamii, ambayo itawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kujengewa hoja na kujadiliwa na Wabunge na kuweza kutumiwa na Serikali.

F)-Ili kupata wawakilishi wa Chuo inapendekezwa kila Chuo kifanye mashindano yake Chuoni na kuchuja kisha kuleta wawakilishi watakaoitajika kulingana na idadi itakayotajwa isipokuwa siku ya Mwisho ya Mchujo Chuo au Mwandaaji wa Chuo anapaswa kuwashirikisha waandaaji wa Taifa kwa lengo la kusaidia kupata wawakilishi bora na wenye Vigezo vinavyokubalika.

MAJUKUMU YA WASHINDI WA TAIFA

Mshindi wa kwanza atapata fursa ya kufanya kazi na Utawala kama Mjumbe wa sauti ya Demokrasia jukwaa la vijana na Balozi wa Demokrasia Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Mshindi wa pili atapata fursa ya kuwa mwakilishi wa Balozi wa Demokrasia Tanzanioa (Bunge) kwa kipindi cha miaka mitano.

Mshindi wa tatu atapata fursa ya kuwa mwakilishi Balozi wa Demokrasia (Tume ya Taifa ya uchaguzi) kwa kipindi cha miaka mitano.

Mshindi wa nne atapata fursa ya kuwa mwakilishi wa Elimu ya Juu (Vyuo Vikuu Tanzania) na Balozi wa Elimu kwa kipindi cha miaka mitano.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 11: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Mshindi wa Tano atapata fursa ya kuwa mwakilishi Balozi wa Tume ya Haki za Binadamu kwa kipindi cha miaka mitano.

Mshindi wa Sita atapata fursa ya kuwa mwakilishi Balozi wa Taasisi ya Kuzuia na kuapambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kipindi cha miaka mitano.

Mshindi wa Saba atapata fursa ya kuwa mwakilishi Balozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kipindi cha miaka mitano.

Mshindi wa nane atapata fursa ya kuwa mwakilishi Balozi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo (Mawasiliano) kwa kipindi cha miaka mitano.

Mshindi wa Tisa atapata fursa ya kuwa mwakilishi Balozi wa Upinzani Bara, na Visiwani kwa kipindi cha miaka mitano katika kuleta changamoto jukwaa la vijana kujifunza.

Mshindi wa Kumi atapata fursa ya kufanya kazi na waandaaji wa Fainal kuu za Taifa za Balozi wa Demokrasia Tanzania katika Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o LTD, kwa miaka mitano.

C: KALENDA YA MASHINDANO:

Kalenda ya mashindano itaendana na mabadiliko ya mfumo wa Chaguzi na Utawala, isipokuwa kila mwaka utaratibu wa kuwapata wawakilishi utaanza katika Majimbo yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi chote kuelekea miaka mitano ya Uchaguzi Mkuu kwa lengo la kutoa Elimu ya Mpiga Kura na Uraia kwa wananchi, na tarehe za mashindano itategemeana na mabadiliko kidunia, isipokuwa itatangazwa miezi mitatu kabla ya tarehe husika ikiambatana na matukio muhimu ya Kihistoria Kitaifa na Kimataifa.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 12: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

SEHEMU 4:

TARATIBU ZA MASHINDANO.

A: WASHIRIKI

Balozi wa Demokrasia Tanzania ni shindano jipya lililoanza kufana katika nchi mbalimbali zikiwemo CANADA, na NIGERIA.

linalowahusu zaidi Vijana, wenye tabia, maadili na mwenendo mwema, Wakiwa raia halali wa taifa, kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kimataifa, washiriki wa fainali za Taifa ni wenye uraia wa Taifa na washiriki wa Fainali za Dunia ni washindi wa fainali za Taifa husika.

B: SIFA ZA WASHIRIKI:

1.1-Umri wa washiriki

Kulingana na sheria za mataifa mbalimbali ulimwenguni kutofautiana, umri wa washiriki utategemeana na sheria za mataifa husika, hata hivyo umri wa chini unaopendekezwa ni miaka (18) na umri wa juu ni miaka thelathini (30).

1.2-Wasifu wa washiriki

Washiriki wa mashindano ni wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania na Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaosoma Nje ya Tanzania. Ambao awajawahi kuolewa, kuoa, wala si wajawazito.

Washiriki wa mashindano haya watatumia lugha wanayoweza kuzungumza kwa ufasaha zaidi ni vyema pia wakajua kuzungumza japo lugha nyingine moja ya kimataifa zaidi ya lugha yao, isipokuwa wanashauriwa kutumia lugha ya Kiswahili

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 13: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

kwa lengo la kueleweka na Watanzania walio wengi pia ikiwa ni njia ya kuenzi lugha yetu ya Taifa, isipokuwa wakati wa kushiriki mashindano ya Kimataifa lugha ya kigeni itakuwa wajibu ili kuweza kueleweka na wengi.

C: MAVAZI YA WASHIRIKI:

Mavazi ya heshima yasiyo mzalilisha mvaaji, jamii wala mtazamaji wakati wote yawe ya heshima yenye kuzingatia Demokrasia kidunia na Taifa wenyeji wa Mashindano.

Washiriki wawapo kambini wanatakiwa kuja na mavazi yakutosha kwa muda wote watakao kuwa kambini kwa matumizi mbalimbali kama Mazoezi, michezo, kuogelea, kukimbia, kushindia, kutokea, kuendea katika maeneo ya burudani na dhifa za kitaifa na kimataifa.

-Mavazi yote ya mashindano haya ni lazima yawe ni kielelezo cha Utukufu katika jamii ikiwa ni pamoja na vazi la Uongozi, Ofisini, Utawala pamoja na vazi la Nyumbani.

1. Vazi la Ofisini.

Mavazi haya yatakuwa maridadi, nadhifu, kulingana na Mhusika kuwakilisha Idara yake.

2. Vazi la Nyumbani.

Mavazi haya yatakuwa ni mfano wa kuigwa vijana kwa lengo la kujenga taifa lenye maadili yanayostaili na kupendeza machoni pa watu, huku likiwa halimzalilishi mvaaji na mtazamaji.

3. Vazi la Uongozi / Utawala

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 14: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Mavazi haya yatakuwa ni kielelezo na yanayostahiki kutumiwa na wakuu mbalimbali wa Idara ama Mamlaka kuu tawala za Serikali na za falme, yakiwa ni mavazi nadhifu, Maridadi, yenye muonekano wa heshima kwa mvaaji.

D: SHINDANO LA VIPAJI:

Kwa lengo la kuvumbua vipaji zaidi vya Uongozi, Kila mshiriki wa mashindano haya atashiriki katika shindano la awali la vipaji, hapa kila mshiriki atabuni Sera na Hotuba kulingana na hali halisi katika kipaji husika atakachoonyesha, ni vyema kila mshiriki akaonyesha kipaji cha zaidi ikiwa kama mafundisho kwa jamii husika.

E: KAMBI NA MAZOEZI:

Waandaaji walioteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi wa Shindano hili katika kila Jimbo, Mkoa, Kanda, Mkoa na nchi watasimamia kambi na mazoezi ya mashindano ya Balozi wa Demokrasia katika maeneo yao, kwa ushirikiano wa karibu na waandaaji wa Taifa wa mashindano. Katika ngazi ya fainali za Dunia, Bodi ya Wakurugenzi ya (BDD) waandaaji wa dunia, watasimamia kambi na mazoezi kwa muda wote wa mashindano.

Wakati wa kambi au mazoezini washiriki watafundishwa jinsi ya kutembea jukwaani, mbinu na namna ya kujieleza, kujiheshimu, kujithamini na kujitambua, uzalendo, masuala ya kijamii, namna ya kujikinga na Magonjwa, Mazingira, uchumi, michezo, Utawala na Uongozi, Demokrasia na upigwaji wa picha.

Washiriki watafundishwa pia kujitambua, nafasi yao na majukumu yao katika jamii. Maana na malengo ya mashindano, na historia yake. Historia na jografia ya Dunia. Washiriki wote katika mashindano ya Balozi wa Demokrasia Tanzania, Afrika, na Dunia Wanapaswa kutii masharti yote kinyume cha hivyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu, kisheria, zikiwemo kufukuzwa kambini na

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 15: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

mashindanoni.

F: MASHARTI YA KAMBI- Washiriki wote watatakiwa kulala katika sehemu walizopangiwa kwa wakati na utaratibu uliopangwa na waandaaji, Washiriki wote watakuwa chini ya uangalizi wa wasimamizi watakaoteuliwa na waandaaji wa mashindano.

Katika kipindi chote washiriki hawataruhusiwa kuzungumza na watu wasio wahusu au kuondoka katika kambi bila ya ruhusa kutoka kwa waandaaji, Washiriki wote watatakiwa kuwa vyumbani mwao mara wasimamizi watakapoamuru, Tabia nzuri, ucheshi, ushirikiano, bidii katika kipindi chote cha mazoezi vitasiaidia kujenga ushindi.

Si ruhusa kuzungumza na waandishi wa habari bila ya idhini ya waandaaji. Waandaaji hawatahusika na uharibifu au uvunjwaji wowote wa sheria za nchi za mshiriki ikiwemo wizi, kuharibu mali ya hoteli au mtu yeyote sehemu yeyote, Upotevu wa mali za washindani washiriki (vitu vya thamani kama pesa, dhahabu n.k vinaweza kuhifadhiwa kwa mtunza hazina wa hoteli).

Gharama za simu, bia na sigara, zitalipwa na mshiriki iwapo mshiriki atashindwa kulipia gharama za matumizi hayo waandaaji watakuwa na haki ya kuzuia zawadi au kukata pesa zake kufidia gharama hizo.

(viii) Washiriki wote wanapaswa kuzingatia na kutambua kuwa:

Washiriki wote watahudumiwa sawa sawa bila ubaguzi.

Chakula kitatolewa kwa wakati uliopangwa tu, Washiriki wote watavishwa Mavazi na wataalamu watakaochanguliwa na waandaaji tu, Mshiriki anayo haki ya kuelezea namna atakavyotaka kuvaa / (Smart), Kila mshiriki atalazimika kuwa na nidhamu ya hali ya juu.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 16: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

(b)Ngazi ya Taifa;

kambi wakati wa maandalizi itakuwa si chini ya siku 15 na si zaidi ya siku 100 katika hoteli ya nyota tatu, baada ya Siku kumi za mwanzo za kambi washiriki wakiambatana na waandishi wa habari wata tembelea Vyuo Vikuu, Bunge, Wizara na Idara za Serikali, Tume ya Taifa, Balozi na IKULU kwa Lengo la kujifunza masuala yanayohusiana na Vitengo Vya Demokrasia katika kujifunza masuala ya Utawala, Uongozi pamoja na maeneo mbali mbali ya kihistoria,

(c)Wakufunzi wa Washiriki:

-Vyuo Vikuu mbalimbali chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Political science Departiment) watatoa mafunzo Kwa washiriki, na Wakufunzi wa ngazi za mikoa na kanda watapangwa au kuthibitishwa na Bodi ya wakurugenzi wa Balozi wa Demokrasia TANZANIA (Taifa).

-Wasomi na wadau wa POLITICAL SCIENCE DEPARTIMENT ngazi zote, -Mkufunzi mkuu wa ngazi za mashindano, atafundisha washiriki wa fainal za taifa akishirikiana na Bodi ya wakufunzi watakaoteuliwa na kamati ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment co ltd, wakiwemo wakufunzi wa kimataifa na Balozi wa miaka ya nyuma wa mashindano haya.

-Aidha wakati wa kambi, mafunzo na semina juu ya upigaji vita Rushwa ,kujikinga na Ukimwi, Elimu ya Uraia, Elimu ya Mpiga kura, Uchaguzi na Elimu juu ya Demokrasia itatolewa na wadau wa mamlaka husika kwa kushirikiana na waandaaji.

Washindi wa Balozi wa Demokrasia Tanzania wa sehemu husika kila mwaka watakuwa ni miongoni mwa waangalizi wa washiriki, na wanawajibika kukabidhi mataji kwa washindi wapya siku ya Fainali.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 17: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

SEHEMU YA 5

MAJAJI WA MASHINDANO

A: Utaratibu wa Uteuzi wa Majaji:

1. Kutakuwa na majaji katika kila ngazi ya mashindano haya.

2.majaji wote watateuliwa na mamlaka za sanaa za Serikali katika kila ngazi,(Utamaduni na BASATA).

Waandaaji wa ngazi husika watapeleka Mapendekezo ya majina ya watu wenye sifa za kuwa majaji kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano haya kwa maafisa utamaduni kwa ngazi za majimbo, Wilaya, Mikoa, na Kanda na BASATA kwa ngazi ya Taifa na Kimataifa, nao watateua majaji.

(a)- Katika kulinda haki za ushindi kwa waandaaji wa ngazi husika na kukwepa lawama za matendo ya kupendelea washindi na kwa kuzingatia taratibu za kimataifa za mashindano haya na mengineyo duniani, kwa upande wa Majimbo, Wilaya, mwandaaji wa kila eneo husika ndiyo atakuwa mwenyekiti wa jopo la majaji na atatangaza jina la Balozi wa eneo husika.

Majaji hawaruhusiwi kufanya mawasiliano ya namna yoyote baina yao na washiriki wakati wakiwa katika zoezi zima la kumpata mshindi.

B: Idadi ya majaji:

Katika kila ngazi idadi ya majaji itakuwa ni namba tasa yani isiyo gawanyika kwa mbili, ili kuondoa kufungana au kupanga matokeo na mvutano miongoni mwa majaji.

Katika ngazi ya Majimbo na Wilaya, idadi ya majaji itakuwa si chini na si zaidi ya

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 18: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

watano (5), wa nne wa kuteuliwa na wa tano mwaandaaji.

Mwandaaji atapendekeza kwa Afisa Utamaduni si chini ya majina 7 na si zaidi ya tisa kwa ajili ya uteuzi.

Katika ngazi ya mkoa na kanda idadi ya majaji itakuwa si chini na zaidi ya saba (7), waandaaji watapendekeza BASATA si chini ya majina 9 na si zaidi ya 11 kwaajili ya uteuzi.

Katika ngazi ya Taifa idadi ya majaji itakuwa si zaidi ya tisa (9).waandaaji watapendekeza si chini ya majina kumi na tano na si zaidi ya kumi na tisa kwa uteuzi majina mawili yatatoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi akiwemo mwenyekiti wa jopo la majaji ambaye ni mkufunzi mkuu(Chief Corographer) wa Taifa.

C: Semina Elekezi za Majaji wa Mashindano:

Waandaaji wa kila ngazi wataandaa na kugharamia semina za majaji wa mashindano ya ngazi husika kwa kushirikiana na mamlaka zausimamizi wa sanaa, katika ngazi ya Taifa waandaaji watashirikiana na kushirikisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kurugenzi ya Sanaa na Utamaduni. Mada kuu ya semina hizo itakuwa ni kuwaelimisha majaji husika juu ya sheria, taratibu na kanuni za mashindano haya na pale itapowezekana wadau kutoka mamlaka ya Demokrasia na Rushwa watahusishwa katika utoaji wa mada.

D: Sifa za majaji wa mashindano:

Majaji wa mashindano haya ndiyo hubeba jukumu la kumteua mshindi kwa niaba ya umma na jamii kwa ujumla.

Kutokuwa watenda au wapenda haki kutaathiri uthamani wa shindano katika jamii na miongoni mwa washiriki, mashindano haya na hata heshima ya majaji

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 19: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

wenyewe. Hivyo suala zima la kuwa na majaji wenye hulka na tabia ya kupenda kutenda haki ni la muhimu sana. Hivyo suala la kuwa na majaji wenye hekima, busara na wenye kuchukia hongo ya namna yoyote halikwepeki.

• Jaji awe ni mwanamichezo au mwana sanaa, Anaweza pia kuwa mfanyabiashara au taaluma yoyote ya kuheshimika katika jamii.

• Jaji awe ni mwenye uwezo wa kuelewa na kugundua tabia na vipaji.

• Jaji awe na ufahamu na uwezo wa kupokea na kuvielewa vigezo vitumikavyo kupata washindi

• Jaji asiwe na tabia ya upendeleo na mpokeaji au mtoaji hongo.

SEHEMU YA 6

WASHINDI WA MASHINDANO.

A: Sifa za Mshindi:

Kila mshiriki wa mashindano haya aliye fika ngazi ya fainali za Mikoa anasifa na vigezo vya kushinda Taji la Fainali kuu ya Taifa ya Balozi wa Demokrasia, Majaji wakati wote wanatakiwa kuangalia kasoro za kila mshiriki ili kumwondoa nafasi ya kushinda, yule mwenye kasoro chache ndiye atakaye ibuka mshindi, majaji wanatakiwa kutafuta sifa za ziada za mshiriki ukilinganisha na wengine, ili kuona au kujua anawazidi nini wenza hata awe mshindi, majaji wakumbuke kuwa washindi watawakilisha taifa katika mashindano ya dunia na mengineyo ya kimataifa, Tabia, hulka na mwenendo wa kila mshiriki ni moja ya mambo ya kuzingatia katika kumpata mshindi.

B: MAJAJI WATAZINGATIA VIGEZO NA SIFA ZIFUATAZO: -

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 20: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

(a) Mvuto wa umbile na ushupavu unaokubalika wa mshiriki.

(b) Umbo zuri la mshiriki si unene wala si wembamba, bali ni uwiano unao kubalika wa umbo na kimo cha mshiriki.

(c) Tabasamu zuri, uchangamfu na ushirikiano mzuri wa mshiriki

Miondoko na muonekano wa hesima wa mshiriki.

Ufahamu wa mshiriki uwezo wa kujieleza na kuelewesha.

(g) Kipaji cha kujiendeleza kitaaluma na matarajio yenye kutia

Matumaini ya mshiriki, Kipaji cha juu cha mshiriki ili akishinda taji katika ngazi husika aweze kuwa Balozi bora kabisa wa Wilaya, Mkoa, Taifa na Dunia akiwa mwenye Elimu na Maarifa ya kiwango cha juu kabisa duniani, ukazingatiwa na majaji katika ngazi zote.

Nidhamu ya hali ya juu binafsi katika jamii na mwenendo wa kukubalika, kuheshimika, kwa Umma.

C: Washindi wa Taifa:

Washindi wa Taifa wa kila mwaka wa Balozi wa Demokrasia:

• Watawakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya Afika Mashariki, Afrika Magharibi, Arika Kusini na DUNIA.

• Watapeperusha Bendera ya TANZANIA, yenye ujumbe wa Demokrasia Kitaifa na Kimataifa.

Washindi watapangwa katika majukumu kulingana na vigezo vya uwakilishi ikiwa ni kushindana au kushiriki kutokana na mahitaji na waandaaji husika.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 21: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Na endapo itatokea kwa namna moja ama nyingine, msichana ama mvulana atakayekuwa anashikilia taji kubainika kujihusisha na masuala yatakayokuwa ni kinyume na taratibu za mashindano ikiwa ni pamoja na kufanya vitendo visivyokuwa na maadili, vitampelekea kupoteza sifa ya kuendelea kutumikia taji, hivyo kuvuliwa ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa zawadi ambazo

Waandaaji wa taifa watakabidhi kwa mshindi wa pili kulingana na sifa za mshindi.

c) Idadi ya wawakilishi wa nchi itaongezeka kila itakapowezekana kutegemeana na Idadi ya Eneo na viwango vya wawakilishi, malengo ya awali ni kupeleka wawakilishi 1-6 na wa tuzo za vipaji, kwa kuanzia washindi wa 1-4 na mshindi wa tuzo za vipaji kila mwaka anakuwa ni miongoni mwa wawakilishi wa taifa na kimataifa.

E: Washindi wa Mikoa, Wilaya na Majimbo:

Washindi wa kwanza wa kila mkoa watawakilisha mkoa katika Fainali za Taifa, hata hivyo waandaaji wa taifa wanaweza kuongeza Idadi ya wawakilishi wa mkoa katika fainali za Taifa kama watakavyoona inafaa kutokana na mahitaji ya Idadi ya washiriki kwa lengo maalum likiwemo la kupanua Elimu ya Demokrasia, katika mkoa husika. Kila wilaya itawakilishwa na washindi1- 5 na mshindi wa tuzo za vipaji katika fainali za mkoa na kwa Idadi hiyo hiyo kwa wawakilishi wa majimbo katika fainali za wilaya.

Washindi wa Mikoa, wilaya na majimbo ya mashindano haya watajulikana kwa mpangilio ufuatao: - Jina la Shindano, Jina la Mkoa, Wilaya/Jimbo (Mfano; Balozi wa Demokrasia Tanzania- Ukerewe 2010).

c) Mikoa ambayo itawakilishwa katika fainali za Taifa za kila mwaka ni yote ya Tanzania bara, Zanzibar na Vyuo vikuu itawakilishwa kama mkoa hivyo kuwa na

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 22: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

jumla ya mikoa ya mashindano 26, Wilaya zote na Majimbo ya ubunge ili kila mkuu wa mkoa, wilaya na Mbunge awe na balozi wake wa Demokrasia. Idadi ya mikoa, wilaya na majimbo itabadilika kulingana na Idadi itakayowekwa kisheria na serikali.

Kuanzia ngazi ya mikoa majina ya Tuzo hizo itatajwa kwa jinsi ya majina ya Lugha ya Kigeni (Kiingereza) kwa Kuwa Kati ya Wageni Waalikwa wengi watakuwa ni pamoja na Mabalozi wawakilishi wa Balozi mbalimbali Duniani.

-Kwa sasa mikoa hiyo ni:

Ambassador of Democracy Tanzania -Arusha

Ambassador of Democracy Tanzania -Dar es Salaam

Ambassador of Democracy Tanzania -Dodoma

Ambassador of Democracy Tanzania -Iringa

Ambassador of Democracy Tanzania -Kigoma

Ambassador of Democracy Tanzania -Kilimanjaro

Ambassador of Democracy Tanzania -Kagera

Ambassador of Democracy Tanzania -Lindi

Ambassador of Democracy Tanzania - Mara

Ambassador of Democracy Tanzania - Morogoro

Ambassador of Democracy Tanzania -Mbeya

Ambassador of Democracy Tanzania -Mwanza

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 23: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Ambassador of Democracy Tanzania -Mtwara

Ambassador of Democracy Tanzania -Manyara

Ambassador of Democracy Tanzania - Pwani

Ambassador of Democracy Tanzania -Ruvuma

Ambassador of Democracy Tanzania -Rukwa

Ambassador of Democracy Tanzania -Singida

Ambassador of Democracy Tanzania -Shinyanga

Ambassador of Democracy Tanzania -Tabora

Ambassador of Democracy Tanzania -Tanga

Ambassador of Democracy Tanzania - Simiyu

Ambassador of Democracy Tanzania -Njombe

Ambassador of Democracy Tanzania - Katavi

Ambassador of Democracy Tanzania -Zanzibar

Ambassador of Democracy Tanzania -University

Kufanyika kwa fainali za Wilaya na Majimbo kutategemea mazingira ya mkoa husika,lakini kwa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ambazo kwa sasa ni Mikoa ya kanda maalumu ya Kipolisi ni lazima ifanye fainali zake, kulingana na Idadi yake zitakazo kuwepo kwa mujibu wa sheria. Kwa sasa ambazo hizo ni:

Ambassador of Democracy Tanzania -Kinondoni

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 24: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Ambassador of Democracy Tanzania - Ilala

Ambassador of Democracy Tanzania -Temeke

Washindi 1-5 na wa Tuzo za vipaji watakuwa chini ya uangalizi wa waandaaji wa ngazi husika (Wilaya, Mikoa, Taifa) kwa msimu wote wa ushindi isipokuwa wale watakaotwaa ushindi kama huo kwa ngazi za taifa, mkoa na Wilaya watakuwa chini ya waandaaji wa ngazi husika na kwa wale watakao twaa nafasi hizo katika ngazi za Taifa ngazi za chini hazitahusika nao moja kwa moja.Msimu wa ushindi au kukaa na taji kwa ngazi zote ni kwa kipindi cha msimu mmoja kamili.

F: HAKI NA MAJUKUMU YA WASHINDI

a) Haki za washindi:

Kupewa zawadi mara baada ya washindi kutangazwa kwa Ngazi za Mikoa, Wilaya na Majimbo. Kufahamishwa na kuonyeshwa mikataba ya shughuli zinazowahusu Kupata huduma zote muhimu wawapo kambini, mazoezini na mashindanoni Kusafirishwa kwenda kituo cha mashindano au cha shughuli za kijamii na kurudishwa na kugharamiwa malazi, vyakula,vinywaji baridi (Maji,soda) Kutangaziwa na kujulishwa zawadi kabla ya shindano na kusaini mikataba Kupata nakala za mikataba aliyosaini na waandaaji / Wakala wa ngazi husika, Kuheshimiwa na kujiheshimu, Kujikosoa na kukosolewa Kila mshiriki / mshindi analo jukumu la kuelezea na kutetea, Demokrasia kwa makini na ufasaha.

b) Majukumu ya Washindi:-

Washindi wa mashindano haya wanamajukumu yafuatayo: -

Kuelewa vyema na kutetea siasa za wananchi, uchumi, uongozi na utawala, Tanzania na masuala mbalimbali ya kijamii, kitaifa na kimataifa katika

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 25: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Demokrasia.

Kuelewa Bendera ya Taifa, rangi zake na maana zake, wimbo wa Taifa na lugha ya Taifa.

Kuzingatia kujivunia na kuuenzi utaifa wake (Tanzania), Kuelewa jografia ya Tanzania, Afrika, na Dunia katika Utawala Bora na misingi ya kidemokrasia, Kuhamasisha jamii katika kutangaza Sera za Taifa, ikiwa ni pamoja na kufundisha maana ya Uchaguzi katika Utawala wa Kidemokrasia na kuelimisha zoezi la Upigwaji kura ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya Uraia.

Kuhamasisha watu na makundi mbalimbali katika Jamii kusaidia wenye kuhitaji na wanaoishi katika mazingira magumu kama Walemavu, Yatima, Maskini, Waathirika wa Ukimwi na vita dhidi ya uaharibifu wa Mazingira hususani jamii inayo zunguka Maliasili za Taifa.

Kuhamasisha jamii na jumuiya kupambana na Rushwa, Ubaguzi wa Kijinsia, Uvaaji wa Mavazi yenye kudhalilisha, Utumiaji wa madawa ya kulevya, kufanya mapenzi kabla ya ndoa n.k.

Kuhamasisha jamii, hususani vijana na kizazi kipya, kudumisha na kuthamini Demokrasia, Uongozi na Utawala, Maendeleo, Utamaduni na haki ya kupiga Kura.

Kuwa mfano bora wa kuigwa na tegemeo kwa watu wengine na jamii kwa ujumla kitabia na mwenendo mwema.

Kuhamasisha kufuata na kufundisha maana na kanuni muhimu za kidemokrasia Kutii na kufuata sheria za nchi, mamlaka za Uongozi na Utawala na kushiriki katika hatua zinazofuata za mashindano haya. Kushirikiana na wakurugenzi (Wakala) wa ngazi husika na waandaaji wa Taifa kuendeleza Demokrasia,Utamaduni Kuitika wito wa waandaaji na kushiriki katika shughuli zozote zinazohusiana na Sauti ya

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 26: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Demokrasia kama watakavyo pangiwa au kutakiwa na waratibu wa ngazi husika

Kuheshimu na kutii viongozi wa Mashindano, Serikali na Mamlaka za Sanaa katika jamii, Kitaifa na Kimataifa.

Kufikisha Ujumbe katika kukosoa, kusifia na Tathmini ya zoezi zima la mchakato wa uchaguzi mkuu wa Rais kila baada ya miaka mitano, ambapo ujumbe huo utatolewa wakati joto la vuguvugu la Uchaguzi linapokuwa ndani ya mwezi baada ya uchaguzi.

G: KUTENGULIWA USHINDI, USHIRIKI:

Ushindi au ushiriki utatenguliwa na waandaaji wa Taifa baada ya kuridhika na taarifa au ushahidi juu ya ukiukwaji au uvunjwaji wa kanuni za mashindano haya na utovu wa nidhamu utakaokuwa umefanywa na mshiriki au mshindi ambapo ni pamoja na:

Ikithibitika kwamba mshiriki ni mwanafunzi wa shule ya msingi au hakumaliza elimu ya sekondari ama umri wake ni chini ya miaka 20 au zaidi ya 30.

Ikithibitika kwamba, mshiriki au mshindi alitiwa hatiani na mahakama kwa kutenda kosa la jinai.

Ikithibitika kuwa mshindi ameshiriki zaidi ya mara moja katika msimu mmoja wa mashindano, Ikithibitika kwamba mshiriki si raia wa Tanzania, Ikithibitika kuwa mshindi si mkazi/ mzaliwa wa eneo husika, Kutoshiriki mashindano ya ngazi inayofuata bila ya sababu ya msingi itakayo kubaliwa na waandaaji wa ngazi husika na Taifa, Kuchelewa kuripoti mashindanoni au kambini bila ya taarifa na idhini ya waandaaji wa ngazi husika.

Ikiithibitika kwamba katika msimu wa ushindi, mshindi katenda matendo yoyote

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 27: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

yenye kudhalilisha jamii na maana nzima ya Demokrasia kwa ujumla kwa makusudi.

Kujifungua, kuolewa, kuchukua ujauzito kabla ya msimu wa ushindi kwisha na ikithibitika kutumia madawa ya kulevya.

Mshindi kutokutekeleza wajibu na majukumu yake kikamilifu ama kuwa na mwenendo mbaya katika jamii.

Ukiukaji wa namna yoyote wa kanuni na taratibu za mashindano haya na sheria za nchi.

Mshiriki kutofanya na kuzingatia Mafunzo na maelekezo ya walimu kwa uzembe au kutokujali.

SEHEMU YA 7:

WAKURUGENZI / MAWAKALA WA WILAYA NA MAJIMBO

Ili kuondokana na ukiritimba wa madaraka na kupanua uwajibikaji wa pamoja na mfumo wa kitaasisi zaidi, kutakuwa na wawakilishi wa mashindano haya katika ngazi za kanda, Mikoa, Wilaya, na Majimbo, Hawa watajulikana kama mawakala au wakurugenzi wa ngazi husika, hawa watakuwa wakifanya kazi kwa niaba ya waandaaji wa taifa (BDT) na watawajibika moja kwa moja kwa waandaaji wa Taifa (Principle and Agency), Watakuwa na mamlaka kamili ya kiutendaji kwa mujibu wa kanuni ya mashindano haya.

B: WAJIBU WA WAKURUGENZI / WAKALA:

1.1 Kugharamia na kusimamia mashindano katika ngazi husika mkoa/wilaya kutangaza washindi baada ya mashindano na kutoa zawadi jukwaani.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 28: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

1.2 Kuhakikisha kuwa kanuni na taratibu zote za mashindano haya zinafuatwa kama zilivyotolewa na waandaaji wa Taifa na kupitishwa na BASATA

1.3 Sifa na uwezo wa kuhakikisha hakuna upendeleo.

1.4 Kuhakikisha washiriki wana sifa na viwango vya juu vinavyotakiwa kwani ngazi hizo ni nyenzo na ni msingi wa demokrasia bora kwa Taifa na Dunia.

1.5 Kuhakikisha kuwa washindi wote wanashiriki mashindano ya ngazi inayofuata na kuhakikisha kwamba washiriki wote hawana vikwazo wala pingamizi za kushiriki.

1.6 Kuhakikisha kuwa wanawasafirisha na kuwagharamia hadi katika kituo cha ngazi inayofuata kwa muda uliopangwa wakiwa na mavazi yote yanayotakiwa na wakiwa na nauli ya kurudi katika kituo pamoja na pesa za matumizi.

1.7 Kuhakikisha kuwa washindi hawafanyi au kutumiwa katika matangazo ya biashara, hadi baada ya mashindano ya ngazi inayofuata kwisha.

1.8 Kuhakikisha kuwa fomu za kuthibitisha uraia na kiwango cha elimu zinapelekwa katika ngazi inayofuata ya mashindano.

1.9 Kuandaa shindano kwa kuzingatia kalenda iliyo tolewa na waandaaji wa Taifa, kutozingatia kalenda kutapelekea mashindano ya mkoa husika kufutwa au Wakala kufutiwa kibali au waandaaji wa Taifa kuchukua hatua zozote za kufaa kunusuru Shindano.

1.10 Kuhakikisha kuwa wanashirikiana na vyombo na taasisi za Sanaa za Serikali katika ngazi husika kwa mujibu wa sheria na taratibu za mashindano haya na za Nchi.

1.11 Wakala atalipa ada itakayokubaliwa na waandaaji wa Taifa, na ataleta

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 29: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

mapendekezo kwa waandaaji wa Taifa na Wakala wa ngazi za chini yake kwa uteuzi, Atashirikiana na waandaji wa Taifa kusimamia mashindano ya ngazi za chini yake.

1.12 Wakala watawasimamia washindi/ washiriki wa ngazi zao katika kuendeleza, kuhamasisha Demokrasia na majukumu kama ya mshindi wa Taifa na kuingia mikataba na washiriki wote kabla ya Shindano ili kulinda haki za washiriki na waandaaji.

1.13 Kugharamia malazi, Chakula na usafiri wa ndani ya wasimamizi wawili kutoka ngazi ya Taifa na wakati wa mashindano Malazi yawe katika hoteli yenye hadhi na kuheshimika.

1.14 Kushirikisha na kushirikiana na mamlaka za sanaa za ngazi husika , ikiwa ni Pamoja na kutoa heshima zote za kiprotokali kwa viongozi wa Sanaa na Serikali katika ngazi husika.

1.15 Kushirikiana na vyama, vyombo vya wanahabari katika kupromoti na kutoa Taarifa Sahihi za Shindano kwa jamii kupitia Vyombo vya Habari.

1.16 Kutoa ripoti ya maandishi kwa waandaaji wa Taifa Pamoja na nakala ya mkanda wa video na picha za washindi wakiwa mmoja mmoja katika mavazi yote na picha moja moja ya full Saizi Paspoti Saizi za Shindano ndani ya wiki moja tangu Tarehe ya Shindano.

1.17 Kulipa ada ya leseni ya uwakala kwa waandaaji wa Taifa kabla ya kuandaa Shindano.

C: SIFA ZA MAWAKALA

a) Lazima awe amesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 30: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

b) Awe na ofisi ya kudumu katika eneo husika.

c) Awe na uwezo wa kuwapata washiriki wenye sifa.

Awe tayari kushirikiana na vyombo vya serikali katika ngazi husika katika kuendeleza, Elimu, sanaa, michezo na utamaduni

Awe na kibali cha kuendesha Shindano kutoka Taasisi zinazosimamia sanaa katika ngazi husika.

Awe na uwezo wa kutafsiri na kuzingatia kanuni na taratibu za Shindano hili.

Atambue na kukubali kuwa Ubunifu huu ni Mali ya Mpalule Shaaban, ambaye ameweka kwenye kampuni ya MISS DEMOKRASIA TANZANIA & ENTERTAINMENT CO LTD, kwa ajili ya kuandaa na kuendesha mashindano haya ya Balozi wa Demokrasia Tanzania- (Ambassador of Democracy Tanzania) isipokuwa Mabadiliko ya Kampuni Katika Kuratibu Itategemeana na Mabadiliko ya Kila Siku.

Awe na uwezo wa mtaji au kupata wadhamini wa kugharamia uendeshaji wa mashindano ya ngazi husika na kutoa zawadi kwa washindi.

I) Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa haraka na waandaaji wa taifa na mamlaka husika katika ngazi za mashindano yake.

Awe na uwezo wa kuandika na kutoa ripoti ya maandishi ya mashindano yake kwa waandaaji wa Taifa ndani ya siku saba tangu Tarehe ya kufanyika kwa Shindano lake.

Awe na uwezo wa kumsafirisha mshindi / washindi wa ngazi za Shindano lake, kwenda katika mashindano ya ngazi inayofuatia na iwapo mshindi kwa sababu zozote hataweza kushiriki basi mshindi aliye mfuatia ata wakilisha.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 31: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

l) Awe na uwezo wa kuhakikisha kuwa washiriki katika ngazi inayofuatia ni wale walioshinda au kushiriki fainali za mwaka husika katika ngazi hiyo.

m) Kwa kushirikiana na mamlaka husika na waandaaji wa Taifa na majaji ,awe na uwezo wa kusimamia uamuzi wa haki wa kuwapata washindi na kutangaza matokeo sahihi ya washindi kama yalivyoamuliwa na jopo la majaji.

n)-Awe na uwezo wa kuwaandalia washindi na washiriki shughuli za kijamii na za kutangaza DEMOKRASIA kwa eneo husika kila mwezi au angalau kila baada ya miezi miwili.

o) Awe na uwezo wa kujenga na kuimarisha mahusiano mema na ushirikiano na jamii, Serikali, Mamlaka za Sanaa, Sekta Binafsi na za Umma wakiwemo wana Habari na Vyombo vya Habari.

p) Awe ni mwenye upeo wa kutosha juu ya masuala mbalimbali ya kijamii,kitaifa na kimataifa, pia uwezo wa kuelewa,kuelewesha na kujieleza hususani katika masuala ya Ufundishaji wa Elimu ya Chaguzi, Demokrasia,Historia jographia,Utamaduni,Sanaa, Desturi ya Tanzania.

q) Awe na uwezo wa kutayarisha na kuwasilisha kwa waandaaji wa Taifa mchanganuo wa namna atakavyo fanikisha Shindano la ngazi yake.

D: HAKI ZA MAWAKALA

Kupendekeza Tarehe ya mashindano kwa waandaaji wa Taifa kabla ya kalenda ya kitaifa ya mashindano haya kutolewa, kuzuia na kutatua utata wowote utakao jitokeza katika mashindano na washiriki wa ngazi husika pia kufahamu na kurekebisha kasoro yoyote itakayotokea

Uamuzi wa majaji ni wa mwisho, rufaa zote za kupinga uamuzi wa majaji,

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 32: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

haziruhusiwi, isipokuwa kwa sababu maalum zitakazokubaliwa na waandaaji wa Taifa.

Kuruhusu na kutambua kuwa waandaaji wa Taifa wanayohaki ya kushauri, kusimamia, kurekebisha kasoro au mapungufu yoyote katika mashindano ya ngazi yoyote na shughuli yoyote inayohusiana na mashindano haya.

Kuhakikisha kuwa washiriki wote ni wale wenyesifa za kushiriki mashindano haya kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano haya na sheria za nchi.

Kuwasimamia washindi na kuhakikisha hawafanyi matendo yenye kudhalilisha jamii na Demokrasia,sanaa na urembo kwa Taifa, kutoa taarifa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya washindi wanao kiuka Taratibu na kanuni za mashindano zikiambatana na ushahidi kwa waandaaji wa taifa.

Kupewa si chini ya tiketi mbili za kuingia bure katika fainali za Taifa na kuingia bure katika Shindano au shughuli yoyote ya ngazi zote nchini.

Kupongezwa au hata kuzawadiwa na waandaaji wa Taifa pale watakapokuwa wamefanya au kutekeleza majukumu yao vyema zaidi. Kwa kushirikiana na waandaaji wa ngazi husika kuwatumia washindi wa ngazi zao na hata ngazi za taifa katika kutekeleza malengo na madhumuni ya mashindano haya.

E : MKATABA BAINA YA WAKURUGENZI /WAKALA/ NA WAANDAAJI WA TAIFA

Mawakala wote watathibitisha kukubaliana na kanuni na taratibu zote za mashindano haya kama zilivyotolewa na waandaaji wa Taifa kwa kutia saini fomu na kila ukurasa wa kanuni na taratibu za mashindano haya na kuzifuata bila ya kukosa ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya leseni ya uwakala kwa waandaaji wa taifa.Mikataba ya mawakala na waandaaji wa Taifa itakuwa ni ya msimu mmoja wa mashindano na kurudiwa kila msimu kulingana na utendaji wa mkurugenzi

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 33: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

/Wakala.

Ukiukwaji wa aina yoyote utasababisha: -

a) Washindi wa mkoa/wilaya kutokubaliwa kushiriki ngazi ya Taifa/ Mkoa Kubatilishwa kwa mashindano ya Wilaya, Mkoa / Taifa

b) Kutopewa tena kibali cha uwakala na kushtakiwa kwa kuvuruga mashindano na kuwafidia washiriki kwa uzembe wa wakurugenzi/wakala Mawakala na waandaaji wa Kitaifa kupewa adhabu yoyote na Serikali.

F: ZAWADI NA WADHAMINI.

Zawadi zote zinapaswa kuwasilishwa kwa wasimamizi wa Sanaa au Serikali katika ngazi zote za Wilaya/ Mkoa zawadi za ngazi ya Taifa zitakabidhwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) juma moja (week moja) kabla ya mashindano.

Wakala wa Wilaya, Mikoa/ waandaaji wa ngazi husika wataingia mikataba ya maandishi na washiriki kabla ya kuanza mashindano.

Wakala atakayeshindwa kutoa zawadi atafungiwa kufanya shughuli za Sanaa nchini na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria.

Wakala/ Mkurugenzi ataingia mikataba ya maandishi na wadhamini wa mashindano ya ngazi yake kabla ya kuwatangaza, na kwamba udhamini wote ukabidhiwe angalau si chini ya wiki mbili kabla ya kuanza kambi au mazoezi ya washiriki.

G : MAJUKUMU NA WAJIBU WA WAANDAAJI WA TAIFA

Kuteua, kusimamia na kuthibitisha mawakala wa ngazi zote.

Kuandaa na kuendesha mashindano ya Balozi wa Demokrasia Tanzania na kutoa

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 34: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

zawadi kwa washindi wa Taifa Kugharamia malazi, chakula, usafiri wa ndani na nje mpaka wanarudi mikoani washiriki wote waliofuzu kushiriki ngazi ya Taifa kwa kipindi chote hadi siku ya kurudi makwao, ikiwa ni pamoja na mahitaji mengine muhimu kama matibabu na usalama kwa washiriki wakati wote wa kambi na mashindano.

kutangaza washindi siku ya mashindano, Kuwagharamia washindi wa Taifa katika mashindano ya ngazi inayofuata, zikiwemo za mavazi ya mashindano, viatu nauli ya kwenda na kurudi mashindanoni, na pesa za matumizi kwa muda wote atakaokuwa mashindanoni na kusimamia maandalizi na kumuandaa kwa mashindano ya ngazi inayofuata.

Kusimamia washindi wa Taifa na kimataifa waliopo nchini au watakapokuja nchini kwa niaba ya waandaaji wa mashindano husika.

Kusimamia shughuli zote za washindi na washiriki zinazohusisha mashindano haya, ushindi wao, ushiriki wao, wadhamini, mamlaka za Umma na Binafsi, Mikataba na Matangazo na mengineyo yenye kuhusisha mashindano, ushiriki au ushindi wa Balozi husika.

Kushirikiana na washindi wa Taifa kupata wadhamini wa mavazi ya mashindano ya Kitaifa na Kimataifa, Viatu , nauli ya kwenda na kurudi mashindanoni, pesa ya matumizi kwa muda wote atakaokuwa katika mashindano pamoja na kusimamia maandalizi kwa kumuandaa katika mashindano ya Kimataifa na Dunia.

H: MFUMO WA ONYESHO NA NGAZI ZA MASHINDANO.

Mashindano ya kumpata “Balozi wa Demokrasia Tanzania” yatafanyika katika ngazi na mfumo ufuatao: -

Ngazi za Mashindano:

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 35: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Yataanzia ngazi za majimbo (Majimbo ya uchaguzi) Ngazi za Wilaya, Ngazi za Mikoa, Ngazi ya Kanda, Ngazi za Taifa, Ngazi za Mabara, Ngazi za Dunia na Kimataifa.

Mfumo wa Onyesho (Show Parten):

Washiriki katika ngazi zote watapanda katika steji kuwania Taji na Tuzo za ngazi husika katika awamu mbalimbali wakionyesha umahili katika Mitindo wakiwa wamevalia mavazi ya Nyumbani, Ofisini, Utawala na Uongozi, Washiriki wataingia na kutembea jukwaani kwa nyimbo za kumbukumbu, ukiwemo wimbo waTaifa ambapo pia watahusika kwenye DEBATE kama sehemu ya Shindano.

Mpangilio wa onyesho la Balozi wa Demokrasia Tanzania utakuwa ifuatavyo:

2.3 (a) Balozi wa Demokrasia Tanzania-Kipaji:-

Washiriki wote watapita jukwaani kwa mara ya kwanza kuwania Taji la tuzo ya vipaji kwa kuigiza moja ya Tendo lililomo ndani ya Demokrasia kwa mfumo wa kuigiza kama mtawala, kiongozi, katika Jimbo, Wilaya au Mkoa anaowakilisha, hapo kila mshiriki atavaa vazi kuendana na igizo lake, Onyesho hili linaweza kufanyika juma moja kabla ya fainali za ngazi husika ama siku hiyo hiyo ya shindano kutegemeana na waandaaji na mshindi atatangazwa siku ya fainali sambamba na washindi wa jumla wa ngazi husika.

1) Vazi la Nyumbani

Vazi la kwanza litakuwa ni vazi linalovaliwa wakati muhusika akiwa eneo la nyumbani.

2) Vazi la Utukufu (Taifa).

Vazi la pili litakuwa ni vazi la Utukufu, Washiriki watapita na mavazi halisi ya

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 36: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Tanzania, hii imetokana na kuenzi na kuendeleza Taifa letu ili kudumisha na kukuza Rangi za Bendera ya Tanzania, Desturi, na hapo Ualisia wa shindano utatimia kwa kuzingatia Demokrasia na Ushiriki wa watu.

3). Vazi la tatu litakuwa ni la Utawala na Uongozi.

Washiriki wote watapita katika jukwaa wakiwa katika mavazi ya Uongozi na Utawala, ambapo kila mshiriki ataonyesha mavazi yanayopaswa kutumiwa na Viongozi, Watumishi, pamoja na watawala, pasipo kuzalilisha jamii kwa kuzingatia Demokrasia.

Baada ya hapo washiriki wote watajibu mada zitakazoulizwa na majaji husika, ili kupata washindi watakaoingia hatua ya kumi bora, tano bora, tatu bora na kisha kupata mshindi.

Mavazi na uvaaji ni Utamaduni wa jamii husika, kwa mujibu wa Utamaduni wetu wa Tanzania, Kila mshiriki atavaa mavazi ya heshima yasiyo mdhalilisha mvaaji, jamii wala mtazamaji.

Kumi na Tano Bora :- Washiriki walioingia hatua hii ya nusu fainali, watapewa dakika tano kila mmoja kuonyesha uwezo wake wa kuchanganua mada na kuonyesha uwezo wake wa kujieleza, kuelewesha na kuelewa. Mada hizo zitahusu Uchaguzi na Kura, Umuhimu wa chaguzi za Kidemokrasia, Mfumo wa Uchaguzi Tanzania, Ukaguzi wa Chaguzi, vyama vya siasa na Chaguzi, Mchakato wa Uchaguzi na Kupiga Kura, Demokrasia na Ushiriki wa Watu, Demokrasia na Ushiriki wa Wote, Uraia na Uongozi, Vikwazo vya Chaguzi za Kidemokrasia, Utawala wa Kidemokrasia, Utawala na Taasisi za Utawala, Njia za Kuimarisha Utawala Bora, Misingi ya Katiba,Haki za Raia na Utawala Bora, Haki na Kazi za Katiba, Misingi ya Katiba, Mgawanyo wa Madaraka, Utawala wa Sheria, Haki na Wajibu wa Raia, Uongozi na Utawala, Demokrasia TANZANIA.

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 37: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

-Tano Bora:-

Washiriki watano kati ya 15 watatangazwa kuingia katika hatua ya fainali.Washiriki watapewa dakika tano kila mmoja kuonyesha uwezo wa kuchanganua mada inayofanana kuhusiana na Uchaguzi na Kura, Umuhimu wa chaguzi za Kidemokrasia, Mfumo wa Uchaguzi Tanzania, Ukaguzi wa Chaguzi, Vyama vya Siasa na Chaguzi, Mchakato wa Uchaguzi na Kupiga Kura, Demokrasia na Ushiriki wa Watu, Demokrasia na Ushiriki wa Wote, Uraia na Uongozi, Vikwazo vya Chaguzi za Kidemokrasia, Utawala wa Kidemokrasia, Utawala na Taasisi za Utawala, Njia za Kuimarisha Utawala Bora, Misingi ya Katiba,Haki za Raia na Utawala Bora, Haki na Kazi za Katiba, Mgawanyo wa Madaraka, Utawala wa Sheria, Haki na Wajibu wa Raia, Uongozi na Utawala, Demokrasia TANZANIA.

Washindi kutangazwa:-

Wakurugenzi / Wakala wa kila ngazi atatangaza washindi 1-5 na mshindi wa tuzo ya vipaji na katika ngazi ya Taifa Mwenyekiti wa mashindano haya atatangaza washindi 1-5 na mshindi wa tuzo za vipaji ambapo Mpangilio wa kutangaza matokeo utakuwa kama ufuatao:

Ambassador of Democracy Tanzania …4th Runner Up

Ambassador of Democracy Tanzania …3rd Runner Up

Ambassador of Democracy Tanzania …2nd Runner Up

Ambassador of Democracy Tanzania …Talent Award

Ambassador of Democracy Tanzania

Ambassador of Democracy Tanzania …1st Runner Up

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 38: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

Zawadi na Tuzo kwa washindi (Prizing and Awarding):

Baada ya matokeo kutangazwa washindi watakabidhiwa zawadi zao na vifuta jasho kwa washiriki wote wa ngazi za Mkoa, Wilaya na Majimbo, na katika ngazi ya Taifa zawadi kwa washindi wa jumla na wa tuzo zitatolewa siku ya pili baada ya Shindano katika hafla maalum itakayo andaliwa na waandaaji wa Taifa ambapo kwenye ngazi ya taifa hakuna kifuta jasho kwa washiriki, isipokuwa tuzo mbalimbali zitakazoshindaniwa.

MWISHO:

Msimamizi Mkuu, Mtunzi na mwandishi wa Ubunifu- Mpalule Shaaban.–

1. WANACHAMA NI: Violety Timoth, Peter Mziray 0715665506, Fredy njeje

0654221465, lucy Kiwelo, Leila Banji, Agatha Mkama 0718195052,

Nyakasagani Masenza 0784296263, Celine Junju, Paulo Siboka-

0715094209, Angel Gaudence,`Aika Gasper Munisi, Mariana Lawrence,

Mamadou Shaaban-0652897852, Basomingera Varia, Jeremia Bomani,

Leila Bhanji, . HALIMA BAKARI- 0753 411 893, . MAYUNGA JUMANNE –

0756 862 812, GETRUD WINFRED -0653 605 021, IBRAHIM MUSSA -0654

848 154, NEEMA COSTANTINE -0769 988 198, ALEX VALLERIUS – 0762 000

179, GABRIELA FAITH -0712 194 123, AGATH SWAI – 0755 773 610,

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 39: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

SUZAN JOSEPH -0766 435 984, ALAN MWASUBILA-0718 762 674,

Zuhura Masoud-0657745589/0767448688, Upendo Laban

Morento-0715560177/0755900185, Stephano Stefan 0766241185,

Jazminy Terry -0654200401.

HALIMA BAKARI- 0753 411 893 MAYUNGA JUMANNE – 0756 862 812

GETRUD WINFRED -0653 605 021 IBRAHIM MUSSA -0654 848 154

NEEMA COSTANTINE -0769 988 198 ALEX VALLERIUS – 0762 000 179

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 40: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

GABRIELA FAITH -0712 194 123 AGATH SWAI – 0755 773 610

SUZAN JOSEPH -0766 435 984 ALAN MWASUBILA-0718 762 674

Haki zote zimeifadhiwa

C O S O T A

Copyright society of Tanzania

Ref No. CST/APP/REG/WORKS/VOL.XV/86 -ACT, NO. 7 (CAP 218 RE

Balozi wa Demokrasia Tanzania

Page 41: Katiba yetu  miss demokrasia tanzania

2002)

Dar es Salaam-TANZANIA.

Balozi wa Demokrasia Tanzania