islamic banking lecture-dodoma university

46

Upload: kakasule

Post on 02-Jul-2015

1.638 views

Category:

Documents


12 download

DESCRIPTION

DARSA HILI LILITOLEWA UDOM TAREHE 11 N0VEMBER 2010, COLLEGE YA SOCIAL SCIENCE

TRANSCRIPT

Page 1: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY
Page 2: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• Utangulizi• Historia ya kanuni za fedha za kiislamu• Hali ya Mfumo wa fedha wa Kiislamu Duniani• Taasisi za Kimataifa za Usimamizi wa Kifedha• Tofauti za Shughuli za kibenki zilizojengwa katika

misingi ya Riba na Shughuli za Kibenki za kiislamu• Faida za Mfumo wa Fedha wa Kiislamu• Uzoefu Wetu Absa Islamic BankingUzoefu Wetu Absa Islamic Banking• Sababu za NBC kuanzisha Huduma za Kibenki za Sababu za NBC kuanzisha Huduma za Kibenki za

KiislamuKiislamu• Huduma za Kibenki za Kiislamu za NBCHuduma za Kibenki za Kiislamu za NBC

Page 3: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

3

Utangulizi:

• Idadi ya Waislamu duniani inakadiriwa kufikia zaidi ya watu Bilioni Moja na Nusu

• Uislamu ni njia kamili ya maisha, yenye misingi yake maalumu ya Kijamii, Kisiasa na Kiuchumi.

• Misingi ya Utaratibu wa Fedha wa Kiislamu ipo ndani ya Qur’an Tukufu na matendo ya Mtume (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ya karne 14 zilizopita

Page 4: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Historia ya Kanuni za Fedha za Kiislamu

• Biashara ya kukopeshana fedha, mali na bidhaa pasina riba (Qardh) ilitumika kugharimia miamala ya walaji (consumers) na hata biashara ya masafa marefu katika ulimwengu wa Kiislamu. Mfumo huu ulifanya kazi vizuri sana kwa kipindi chote cha ustawi wa waislamu katika dola ya mashariki na ile ya magharibi (Andalusi) hadi kufikia kuanguka kwa dola ya mwisho ya waislamu chini ya Waturuki (Ottoman empire) mwaka 1920.

• Mwanahistoria wa uchumi aitwaye Udovitch anauzungumzia mfumo huu kama ifuatavyo;- "These Islamic mode of financing were able to mobilize the "entire reservoir of monetary resources of medieval Islamic world for financing agriculture, crafts, manufacturing and long-distance trade". (Udovitch, 1970, uk.180 na 261)

Page 5: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• Tafsiri: "Miamala hii ya ukopeshaji ya Kiislamu iliweza kukusanya hazina ya rasilimali fedha ya ulimwengu wa Kiislamu katika zama za kati, ikiwezesha uwekezaji katika kilimo, uhunzi, utengenezaji wa bidhaa na biashara ya masafa marefu".

• Udovitch anazidi kuuelezea mfumo huu wenye kufuata kanuni za kiislamu za Kifedha kwamba;- "They were used not only by Muslims but also by Jews and Christians to the extent that interest bearing loans and other overly usurious products were not in common use.” (Udovitch, 1981, p.257; angalia pia uk.268).

• Tafsiri: “Mifumo hii ilitumika si tu na waislamu bali ulitumiwa na wayahudi na wakristo kwa kiasi kwamba mikopo yenye riba na miamala mingine ya kiriba haikuwa jambo la kawaida wakati huo".

Page 6: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

6

• Katika Dunia, Utaratibu wa Kibenki wenye kufuata mafundisho ya Kiislamu (Global Islamic Finance) ni wenye kukuwa zaidi ya asilimia 29% kila mwaka na makadirio ya rasilimali zake ni USD 2.8 Trillion (“Islamic Finance: Overview and

Policy Concerns”, CSR Report for Congress, July 2008)

• Utaratibu wa Fedha wa Kiislamu sio tishio kwa utaratibu uliopo wa Kibenki bali sehemu nyingi duniani unakuwa ni nyongeza yenye kutoa fursa za ziada kwa wenye kutaka miamala yenye kufuata maadili.

• Kimataifa, asilimia kubwa ya wateja wa mabenki yenye kufuata Mfumo wa fedha wa Kiislamu sio Waislamu, bali ni watu wa dini nyingine wanaohitaji huduma mbadala za kifedha.

Hali ya Mfumo wa fedha wa Kiislamu Duniani

Page 7: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• Kuna takribani taasisi za Kifedha zaidi ya 600 zinazotoa huduma hizi na zinazidi kuongezeka.

• Taasisi hizi za Kifedha zimetawanyika katika nchi zaidi ya 75, zikiwemo za Kiislamu na zisizo za Kiislamu

• Nyingi zipo Mashariki ya kati (Middle East) na Asia ya Kusini Mashariki (Southeast Asia)

• Sasa hivi zishaingia Ulaya na Marekani.

• Ukuwaji wa rasilimali (Asset growth) wa sekta hii ni kati 20pc–30pc katika karne iliyopita – na inaelekea kuwa mara tatu zaidi katika mwaka 2015 kufikia $10 Tn

• Taasisi za kifedha za kimataifa zinazotoa huduma za fedha zenye kufuata taratibu za Kiislamu zipo, Morgan Stanley, Citigroup, HSBC, UBS, Standard Chartered, Deutsche Bank, Goldman Sachs, Lloyds na Barclays na zinginezo

Page 8: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY
Page 9: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Source: Shari‘ah Fortune

Page 10: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Baadhi ya Mabenki Makubwa Duniani yenye Kutoa Huduma zenye Kufuata Mfumo wa Fedha wa Kiislamu

New Entrants

Angalizo:

Benki nyingi zisizo za Kiislamu zinatoa huduma za fedha zenye kufuata taratibu za Kiislamu

Page 11: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

AAOIFI inatengeneza, inaandaa na kutoa kwa ajili ya utekelezaji Kanuni na Taratibu za Kifedha za Kibenki

IFSB inaandaa kanuni za Udhibiti na Viwango vya Kisheria vinavyoendana na vyenye hadhi ya Kimataifa

IIFM inajishughulisha na kuanzisha, kuendeleza na kushajihisha Masoko ya Kiislamu ya Mitaji na fedha (Islamic capital and money markets)

IIRA, ni Islamic rating agency ya pekee, inayotoa tathmini ya viwango kwa masoko ya Mitaji na katika Sekta ya Kibenki katika nchi za Kiislamu

IDB inajenga na kushajihisha maendeleo ya kiuchumi na kijamiii kwa kufuata Misingi ya Sharia’h.

GCIBFI ina malengo ya kuongeza muonekano wa Sekata ya mfumo wa fedha wa kiislamu katika maeneo makuu ya masoko ya fedha ya kimataifa

General Council of Islamic Banks and

Financial Institutions

Taasisi za Kimataifa zenye Kusimamia Masuala ya Kifedha yenye Kufuata Mfumo wa Kiislamu Duniani

Page 12: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Adabu za Mfumo wa Fedha wa Kiislamu

• Ni zipi? Baadhi ya Adabu hizo ni:-– Hakuna utoaji au upokeaji riba.– Faida inaendena na biashara ya kweli. (Al Kharaaj bi dhamaan).– Hakuna kuuza usichokimiliki.– Hakuna kujihusisha na biashara ambazo ni haramu.– Hakuna kudhuru mazingira na binadamu – Hakuna Israfu.– Tabia bora ndio juu ya kila kitu.– Tabia bora juu ya Faida.– Hakuna Kamari.

Page 13: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Tofauti Iliyopo kati Mabenki yenye kufuata kanuni za kiislamu za kifedha na mabenki ya kawaida

• Benki zenye kufuata kanuni za kifedha za Kiislamu zimejengwa katika misingi ya kiimani.

• Benki zenye kufuata kanuni za Kifedha za Kiislamu zinafuata misingi ya kutotoa riba na kutopokea riba.

• Benki zenye kufuata kanuni za fedha za Kiislamu miamala yake yote imejengwa katika shughuli za kiuchumi halisi.

• Uwekezaji haufanywi katika sekta ambazo kinyume na maadili ya Uislamu na ubinadamu, sekta za Picha za ngono, Cinema, Pombe, Sigara, Makasino n.k

• Benki za Kiislamu ni zenye kufanya biashara, kugawana faida, na kugawana faida na hasara na wateja. Fedha zikiwekezwa katika baadhi ya miamala badala ya kupata riba ya kila mwezi fedha zinaweza kupata faida kufuatana na mgawo waliokubaliana kati ya benki na mteja.

Page 14: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• Benki za Kiislamu hazijajifunga katika kuwa kiungo tu cha kifedha Bali zinafanya kazi za ziada za kuwa muwekezaji, mfanya biashara, na Mshauri katika mambo ya fedha.

• Zina Wasimamizi ambao ni Wanazuoni waliobobea katika Fiqhil Maswrafi.

• Uhusiano wa benki na wateja wake ni ule uhusiano wa Mdai (creditor) na mdaiwa (Debtor). Uhusiano wa Benki na wateja wake ni uhusiano wa ubia, uwekezaji, mjasiriamali, muuuzaji, mnunuzi, mkodishaji na mkodishwa.

• Mikataba yote ni yenye uzito wa kipekee kulingana na mafundisho ya dini.

• Dini zote kuu nne duniani (Judaism, Christianity, Hinduism na Islam), zenye wafuasi zaidi ya theluthi mbili za watu duniani zimeharamisha Riba. (For the Judaic and Christian views on interest see Johns, et. al., and Noonan (1957);and for the Hindu view, see Bokare (1993), p. 168). Uislamu umeharamisha riba (2:278-279)

• Pia angalia Biblia, Deuteronomy 23: 19; Leviticus 25:36; Exodus 22:25; Ezekiel 18:5-9. Luke 2:34-35.

Page 15: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• Hivyo, mchakato wa kuanzisha shughuli za kibenki zenye kufuata maadili ya Kiislamu ni katika juhudi za kuondoa riba katika jamii ya wanaadamu. Juhudi hizi zinaendana na mafundisho ya Uislamu na yale ya dini kuu duniani, Ukristo, uyahudi, na Uhindu.

Page 16: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Faida za Mfumo wa Fedha wa Kiislamu

Page 17: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

1. Kuheshimiwa kwa maadili ya Biashara ya Kiislamu

Cone-demned ... 'spinning whirl' ice creams look similar to the world Allah written in Arabic script

  Ice creams are being withdrawn from Burger King — because a design on the lid looks like the word Allah. 

http://www.thesun.co.uk/article/0,,2-2005430136,,00.html

Page 18: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Nike apologized to Muslims for any unintentional offense, agreed to recall all products carrying the design, introduced training for Nike designers in 

Islamic imagery and agreed to investigate how the design came about. http://www.cnn.com/US/9811/21/nike.islamic/

Page 19: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Vatican offers Islamic finance system to Western Banks.

The Vatican says Islamic finance system may help Western banks in crisis as

alternative to capitalism. The Vatican offered Islamic finance principles to Western

banks as a solution for worldwide economic crisis. Daily Vatican newspaper,

'L'Osservatore Romano, reported that Islamic banking system may help to overcome

global crisis.

2. Ulimwengu kutambua Uzuri na Ubora wa Sharia za Kiislamu

Page 20: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• The Vatican said banks should look at the ethical rules of Islamic finance to restore confidence amongst their clients at a time of global economic crisis.

"The ethical principles on which Islamic finance is based may bring banks closer to their clients and to the true spirit which should mark every financial service," the Vatican's official newspaper Osservatore Romano said in an article in its latest issue late yesterday.

• Author Loretta Napoleoni and Abaxbank Spa fixed income strategist, Claudia Segre, say in the article that "Western banks could use tools such as the Islamic bonds, known as sukuk, as collateral". Sukuk may be used to fund the "'car industry or the next Olympic Games in London," they said.

Page 21: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

3. Faida na Umuhimu wa Shughuli za Kibenki zenye Kufuata mfumo wa fedha wa Kiislamu

• Ni zenye kuangalia mahitaji ya waislamu kama sehemu ya Jamii. Mabenki nchini kutambua kuwa huduma walizokuwa wanatoa zilikuwa hazikidhi mahitaji ya jamii ya Kiislamu. Walikuwa wanalazimisha watu kufanya shughuli za Kibenki kinyume na Imani zao.

• Mabenki kugundua kuwa walikuwa wanapoteza fursa ya kuhudumia sehemu kubwa ya jamii ya Watanzania. (Unbankable)

• Sasa zinafanya kazi kama chombo cha kujaza ongwe kwa kukusanya rasilimali fedha kwa malengo ya uzalishaji, hasa kwa jamii ya Kiislamu. Fursa kwa Watanzania.

Page 22: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

4. Faida na Umuhimu wa Shughuli za Kibenki zenye Kufuata mfumo wa fedha wa Kiislamu

– Zimethibitishwa kuwa ndio shughuli bora za kifedha zenye kusaidia ukuwaji wa uchumi duniani.

– Zinakidhi mahitaji sio ya Waislamu peke yao bali na dini nyingine.

– Ni njia nzuri ya kufikisha maadili mema kwa jamii kwa kutumia sekta ya kibenki.

Page 23: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Huduma za NBC Islamic Banking Huduma za NBC Islamic Banking

• Islamic Savings Account (Akaunti ya Akiba) Islamic Savings Account (Akaunti ya Akiba)

• Islamic cheque Account (Akaunti ya Hundi)Islamic cheque Account (Akaunti ya Hundi)

• Bidhaa zote mbili zinafuata utaratibu wa Kiislamu wa Bidhaa zote mbili zinafuata utaratibu wa Kiislamu wa QardhQardh

Page 24: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Utaratibu wa Utaratibu wa QardhQardh

• QardhQardh – Mkopo – Mkopo

• Mteja anaipa mkopo Benki, na Benki itarudisha fedha kamili Mteja anaipa mkopo Benki, na Benki itarudisha fedha kamili kwa mteja atakapozihitaji bila ya kulipa riba, au kumpa baadhi kwa mteja atakapozihitaji bila ya kulipa riba, au kumpa baadhi ya faida au hasara tuliyoipata katika kufanyia biashara.ya faida au hasara tuliyoipata katika kufanyia biashara.

• Miamala ya Akaunti za Kiislamu za NBC za Kuweka na za Miamala ya Akaunti za Kiislamu za NBC za Kuweka na za Hundi zimeegemea katika utaratibu wa Hundi zimeegemea katika utaratibu wa QardhQardh. .

Page 25: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

PROFITS

LOSSES

1

1

4

3

4

2

5

Page 26: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Manufaa ya Akaunti ya AkibaInayofuata Kanuni za Kiislamu ni Yapi?

• Kupata huduma za kibenki saa 24 kupitia mtandao wetu wa ATM zaidi ya 300 zilizosambaa nchi nzima.

• Kupata huduma kwa saa 24 kwenye akaunti yako kwa njia ya Mtandao wa Intaneti wa Kibenki wa NBC.

• Kutokuwepo kwa idadi ya ukomo wa uchukuaji fedha kwenye kaunta, na bila ya kuwa na kiwango cha mwisho cha uchukuaji fedha.

• Kuruhusu malipo kwa maelekezo maalum na uhamishaji wa fedha kielektroni.

• Malipo kwenye akaunti yanaweza kufanywa kwenye tawi lolote lile la NBC nchini.

Page 27: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• Mwenye akaunti atalipwa Takaful ya Mazishi ya kiasi cha Shilingi 500,000. Takaful hii ni mchango wa Mazishi, wenye kufuata utaratibu wa Kiislamu, ataolipwa Mwenye Akaunti baada ya kufariki. NBC Takaful ya Mazishi ni bima ya Kiislamu iliyojengwa katika misingi ya kusaidiana na kushirikiana.

• Kufuata kiukamilifu utaratibu wa kifedha wa Kiislamu, Fiqhi Muamalat.

Page 28: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Manufaa ya Akaunti ya HundiInayofuata Kanuni za Kiislamu Ni Yapi?

• Kupata huduma kwa saa 24 kupitia mtandao wetu wa ATM zaidi ya 200 zilizosambaa nchi nzima

• Kupata huduma za akaunti yako kwa saa 24 kwa njia ya huduma za kibenki kupitia mtandao wa Intaneti wa NBC.

• Kutokuwepo kwa idadi ya ukomo wa uchukuaji fedha kwenye kaunta, na bila ya kuwa na kiwango cha mwisho cha uchukuaji fedha.

• Kuruhusu malipo yanayofaa kwa maelekezo yaliyopo na uhamishaji wa kielektroni.

Page 29: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• Malipo kwenye akaunti hii yanaweza kufanyika kupitia tawi lolote lile la NBC nchini. Mwenye akaunti anaweza kuomba kitabu cha Hundi kama ziada ya kadi ya ATM.

• Kufuata kiukamilifu utaratibu wa kifedha wa Kiislamu, fiqhi Muamalat.

Page 30: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Masharti ya kushiriki katika Masharti ya kushiriki katika Mfuko wa Mfuko wa WaqfWaqf wa Takaful wa Takaful

Lengo la Mfuko wa Waqf wa Takaful

• Lengo la mfuko huu ni kumpa msaada mwenye akaunti aliyefariki atakapokuwa amefuata kikamilifu masharti ya masharti ya mfuko huu.mfuko huu.

Mchango katika mfuko wa Mchango katika mfuko wa WaqfWaqf wa wa TakafulTakaful

• Kwa kukubali kujiunga, utakuwa umekubali kutoa sadaka Kwa kukubali kujiunga, utakuwa umekubali kutoa sadaka yako kwenda kwenye mfuko huu. Fedha zote zinazoingia yako kwenda kwenye mfuko huu. Fedha zote zinazoingia katika mfuko zitakuwa ni mali ya mfuko na zitasimamiwa katika mfuko zitakuwa ni mali ya mfuko na zitasimamiwa kulingana na masharti yanayosimamia taratibu za mfuko kulingana na masharti yanayosimamia taratibu za mfuko wa wa WaqfWaqf. .

Page 31: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Ziada (Surplus) katika Mfuko wa Waqf wa Takaful

• Kama kutathibitika ziada katika Mfuko wa Waqf, 5% ya ziada zitagawiwa na mfuko kama sadaka kwa taasisi inayostahiki ya Kiislamu au ya Kijamii.

• 95% zilizobakia zinaweza kurejeshwa kwa wenyewe wenye akaunti, au kutolewa sadaka, au kuwekwa kama akiba kwa ajili ya kufidia hasara zinazoweza kutokea katika mfuko.

• Wadhamini wa Mfuko, kwa idhini ya Bodi ya Sharia’h ya NBC, ndio watakaokuwa na mamlaka ya mwisho ya kutoa maamuzi ya namna ya ugawaji.

Page 32: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Upungufu (Deficit) katika Mfuko wa Waqf wa Takaful

• Kama kutatokea upungufu wa fedha katika mfuko wa Waqf wa Takaful, Wadhamini wa mfuko, kwa mamlaka na maamuzi yao wataomba mkopo kutoka African Life Assurance (T) Ltd, kwa lengo la kuondoa huo upungufu. Mkopo huu utakuwa kwa utaratibu wa Qardh, ambao utalipwa baada ya kupatikana ziada katika Mfuko wa Waqf wa Takaful

Page 33: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

33

Awamu zetu zingineAwamu zetu zingine

•Huduma hizi zimeanza kupatikana toka 3 May 2010

•Tunajiandaa kuleta katika masoko huduma zingine za kifedha.

•Tutaendelea kuhamasisha jamii kwa njia ya Semina na makongamano yanayohusu Utaratibu wa kibenki wenye kufuata mafundisho ya Kiislamu

•NBC itafuata sheria zote za Tanzania katika utoaji wa huduma hizi.

Page 34: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Hitimisho

• Dharura ya Kuweka Pesa katika utaratibu wa Riba haipo.

• Wajibu kwa Waislamu kuamka na kushiriki kikamilifu katika shughuli za Kibenki zinazofuata taratibu za Kiislamu.

• Fursa adhimu ya kufata mafundisho katika sekta ya fedha na biashara.

Page 35: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Ahsante

Page 36: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Habari• "UK Islamic bank gets foothold in France.

LONDON-BASED Gatehouse Bank, the latest Islamic bank to be authorized by the UK’s Financial Services Authority (FSA), has become the first Islamic bank to join Paris Europlace, an organization that promotes Paris as a financial center. Paris Europlace has over the last two years also started to focus on the Islamic finance sector and established an Islamic Finance Commission in December 2007 (Arab News-19 October, 2009).

Tafsiri:• "Gatehouse Bank, benki yenye makao yake makuu London, benki ya hivi 

karibuni itoayo huduma za Kiislamu kuruhusiwa na Mamlaka ya Huduma za kifedha ya Uingereza (FSA), imekuwa benki ya kwanza ya Kiislamu kujiunga na taasisi inayopigania Paris kuwa kitovu cha biashara Ulaya iitwayo Paris Eurospace. Taasisi hiyo ya Paris Eurospace, imekuwa ikitupia jicho sekta ya huduma za kifedha za Kiislamu kwa takriban miaka miwili sasa na imeanzisha Kamisheni ya Huduma za Kifedha za Kiislamu mnamo mwezi Desemba, 2007".

Page 37: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Hoja za Kukubali Mabenki kujishughulisha na miamala ya kiislamu

Maulamaa wanaounga mkono uhalali wa kuanzishwa "Islamic Windows" katika benki zisizo za kiislamu alimradi taratibu na kanuni za Shari'ah ziwe zimewekwa na kusimamiwa na waislamu, wanasema;-

1. Kufanya miamala ya kifedha au kibiashara inayoendana na Shari'ah si suala linalowahusu waislamu peke yao bali binadamu wote. Kwa hoja hii, ni inajuzu, na pia ni jambo zuri, kwa yeyote yule awe Muislamu au vinginevyo kufanya miamala kwa mujibu wa kanuni na maelekezo ya Shari'ah.

2. Ikiwa haiwezekani kufuata Shari'ah katika miamala yote basi mtu aanze na kile kinachowezekana kwake kwa msingi wa maelekezo ya Qur'an "Mchehi Allah kadiri ya uwezo wenu" na kanuni ya Usuulul fiq-h "ما ل يدرك كله ل يترك كله "kwamba "Lile lisilodirikika lote haliachwi lote".

Page 38: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Hoja za Kukubali Mabenki kujishughulisha na miamala ya kiislamu-1

Maulamaa wanaounga mkono uhalali wa kuanzishwa "Islamic Windows" katika benki zisizo za kiislamu alimradi taratibu na kanuni za Shari'ah ziwe zimewekwa na kusimamiwa na waislamu, ni hawa wafuatao:

1. (Fatawa mbalimbali za aliyekuwa) Mufti Mkuu wa Saudi Arabia Sheikh Ibn Baz (Mungu Amrehemu) aliulizwa kuhusu kufungua Akaunti katika Mabenki ya riba alijibu, ‘kufungua akaunti bila kupokea au kulipa riba ni halali’ (Ibn Baz, majmau’l fatawa 9:413). 

2. Sh. Dr Bakr Abu Zaid, Sh Abdulaziz Al sheikh, Sh. Salah al-Fouzan na Sh. Ibn Baz (Fatawa allajnaa Addaimah 13: 374).

3. Sh. Prof. Ali Qurra Daghi (Profesa wa Sharia chuo Kikuu cha Qatar), anaona vitengo vya shughuli za Kibenki za Kiislamu ni alama ya mvuto wa Uislamu duniani.

4. Dr S’ad b. Turkey al-Khathlan, Profesa wa Usulul fiqhi chuo Kikuu cha Imam (Saudi Arabia)

Page 39: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

5. Sh Dr. Abdullah b. Sulaiman al-Manee.

6. Sh Dr. Abdullah b. Abdul aziz Al-Muslih.

7. Maulamaa wengi wakubwa wa zama zetu hizi. 

Baadhi ya Hoja zao kuu ni kama zifuatazo;-

1. Kufanya miamala ya kifedha au kibiashara inayoendana na Shari'ah si suala linalowahusu waislamu peke yao bali binadamu wote. Hivyo basi shughuli hizi za kibenki zinajuzu, na pia ni jambo zuri, kwa yeyote yule awe Muislamu au vinginevyo kufanya miamala kwa mujibu wa kanuni na maelekezo ya Shari'ah.

2. Ikiwa haiwezekani kufuata Shari'ah katika miamala yote basi mtu aanze na kile kinachowezekana kwake kwa msingi wa maelekezo ya Qur'an "Mchehi Allah kadiri ya uwezo wenu" na kanuni ya Usuulul fiq-h "ما ل يدرك كله" kwamba "Lile lisilodirikika lote haliachwi lote".ل يترك كله

Page 40: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

3. Kwa mujibu wa mafundisho ya Shariah miamala na mikataba yote inaruhusiwa isipokuwa ile ambayo iliyokatazwa. (Maqdisi, Al-Furu’h 4:323, mirdawi, al-Insaaf 6:31; Ibn qayyim A’lamul Muwaqqieen 1:344)  Ibn taymiyya amesema, “Miamala yote imeruhusiwa kwa waislamu isipokuwa ile iliyoharamisha katika qur’an na Sunnah.” Majmu’ al-fatawa 28:386  

4. Kujishughulisha na Vitengo vya miamala ya Kibenki ya Kiislamu inachukuliwa katika katika wema na uchamungu. (Suratul maidah: 2)

5. Ni njia nzuri ya kufikisha maadili mema kwa jamii kwa kutumia sekta ya kibenki.

6. Kiislamu, ni ruhusa kufanya biashara na wenye kujishughulisha na haramu, kwa sharti kuwa miamala yako hiyo inaruhusiwa na sharia’h. Imepokewa kwa mama Aisha (r.a) kwamba "Mtume (s.a.w) alinunua chakula kutoka kwa myahudi na akatoa vazi lake la vita kama rehani", katika hadithi nyingine akataja "Swa'ah thelathini za shayiri“ badala ya kusema chakula. (Bukhari, 3, uk. 15 na 231).

Page 41: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• 2373 -  إبراهيم بن مسلم حدثنا قتادة، عن: حدثنا هشام: حدثنا:أنس رضي ا عنه قال

ولقد رهن النبي صلى ا عليه وسلم درعه بشعير، ومشيتإلى النبي صلى ا عليه وسلم بخبز شعير وإهالة سنحة، ولقد

ما أصبح لل محمد صلى ا عليه وسلم إل: (سمعته يقول).صاع، ول أمسى، وإنهم لتسعة أبيات

[1963 ].من رهن درعه: باب2 -

ا عبد الواحد: حدثنا مسدد2374 - ا العمش قال: حدثن :حدثنبراهيم الرهن والقبيل في السلف، فقال إبراهيم :تذاكرنا عند إ

ا السود، عن عائشة رضي ا عنها :حدثنلنبي صلى ا عليه وسلم اشترى من يهودي طعاما إلى أن ا

.أجل، ورهنه درعه1962 ][

Page 42: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

7. Abdul razzaq, Al-Musannaf 6:74; Ibn Hajar, ad Dirayah 2:162; Ibn Qudamah, Al-Mughni 9:279. Abu Ubaid, Kitabu Amwal p. 62. Khalifa Umar Bin Khattab (r.a) maelekezo yake kwa wakusanyaji wa kodi kuhusu mali za haramu.

8. Maulamaa wameruhusu kuwepo kwake kwa masharti maalumu.

Page 43: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

FATWA YA KAMATI YA KUDUMU YA FATWA YA SAUDI ARABIA JUU YA KUTAAMALI NA BENKI

ZINAZOJISHUGHULISHA NA RIBA.

فتاوى اللجنة الدائمة( 16013 )السؤال السادس من الفتوى رقم

( : 375)، الصفحة رقم: 13الجزء رقم فما الحكم في التعامل مع. هناك بعض البنوك لها فروع إسلمية، ولكن البنك الرئيسي يتعامل بالربا6: س

هذا الفرع؟ ل بأس بالتعامل مع البنك أو فرعه إذا كان التعامل ليس فيه ربا؛ لن ال سبحانه أحل البيع وحرم6 : ج

. الربا، ولن الصل في المعاملت الحل، مع البنك أو غيره؛ ما لم تشتمل المعاملة على حرام. وبال التوفيق وصلى ال على نبينا محمد وآله وصحبه وسلم

اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والفتاء

الرئيس نائب الرئيس عضو عضو عضو

عبد العزيز بن عبد ال بن باز عبد الرزاق عفيفي صالح الفوزان عبد العزيز آل الشيخ أبو زيد بكر

Page 44: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

TAFSIRI:Swali la sita (6) katika Fatwa nambari 16013, Juzuu ya  13 ukurasa wa 375.Swali la sita (6): 

"Kuna baadhi ya mabenki yana kitengo cha kiislamu lakini benki ya asili inataamali na riba, basi ni pi hukumu katika kutaamali na kitengo hicho?

Jawabu la sita (6): "Hapana ubaya kutaamali na benki hiyo au kitengo chake pindi itakapokuwa kuamiliana huko hakuna riba ndani yake. Kwa sababu Allah Subhaanahuu amehalalisha biashara na ameharamisha riba. Na ni kwa sababu asili ya miamala yote ni uhalali, iwe na benki au kitengo vinginevyo alimradi muamala huo usiwe katika haramu"

Wabillaahi t-tawfiiq, na rehema na amani ziwe juu ya bwana wetu Muhammad na ali zake na swahaba zake.

Kamati ya kudumu ya uchunguzi wa kiilmu na kutoa fatwaMwenyekiti:  Mufti Sheikh Abdulaziz Ibn Abdallah Ibn Baaz Makamu Mwenyekiti: Sheikh Abdurazaaq Al 'afiyfiiMjumbe:  Sheikh Swalih Al FawzaaniyMjumbe:  Abdulaziz Aali Sheikh (Mufti wa sasa wa Saudia)Mjumbe:  Sheikh Bakr Abuu Zayd

Page 45: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

• Fatawa al-Lajnah daima 13:405. Kuhusu Uhalali wa Mikopo inayotolewa na Nasser Bank.

• Fatawa al-Lajnah daima 13:404. Kukopa katika Vitengo vyenye kufuata kanuni za Kiislamu.

• Fatawa al-Lajnah daima 13: 19 Miamala kati ya waislamu na wasio kuwa waislamu inaruhusiwa inapofuata Shariah za Kiislamu.

Page 46: ISLAMIC BANKING LECTURE-DODOMA UNIVERSITY

Tubaddalu sababul Milki Ka-iman maka-ma Tabadduli Ddhat

Kubadilika sababu ya kumiliki kunasimama mahali pa kubadilika dhati (yenyewe).

225: Maana ya kanuni na sababu zakeItakapobadilika sababu ya kumilikii kitu Fulani, basi  kitu hicho 

kitazingatiwa ni kubadilika hukumu japokuwa hicho hakikubadilika ki uhakika. Na msingi wa kanuni hii ni hadithi sahihi alioitoa Bukhari na Muslim, na katika riwaya ya Muslim toka kwa Anas bin Malik (r.a.) amesema: Bariirah alipeleka nyama aliopewa yeye sadaka kwa Mtume (s.a.w.) na Mtume akasema “kwake ni sadaka. Na kwetu ni hadiya” (zawadi).

Na Imamu Nawawiy amesema:Katika kuieleza hadithi hii  na mifano yake. Mlango wa kuhalalisha hadiya kwa Mtume (s.a.w.) Na Banii Hashim na Banii Muttwalib. Iwapo anayeitoa ameimiliki kwa njia ya sadaka. Na kubainisha kuwa sadaka akishaipokea aliyepewa sadaka, tayari ile sifa yake ya usadaka imeondoka. Na kitakuwa halali kwa kila mtu miongoni mwa waliokuwa ni haramu kwao kula sadaka.