injilikamaalivyoiandika markomtakatifu · tuangamiza? najua wewe ni nani: wewe ni mtakatifu wa...

47
MARKO MTAKATIFU 1:1 1 MARKO MTAKATIFU 1:15 INJILI KAMA ALIVYOIANDIKA MARKO MTAKATIFU 1 Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2 Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeye atakutayarishia njia yako. 3 Sauti ya mtu imesikika jang- wani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni mapito yake.” 4 Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba ni lazima watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao. 5 Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani. 6 Yohane alikuwa amevaa vazi lililofumwa kwa manyoya ya ngamia, na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. 7 Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. 8 Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.” 9 Siku hizo, Yesu alifika kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, akaba- tizwa na Yohane katika mto Yordani. 10 Mara tu alipotoka majini, aliona mbingu zimefunguliwa, na Roho akishuka juu yake kama njiwa. 11 Sauti ikasikika kutoka mbinguni: “Wewe ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe.” 12 Mara akaongozwa na Roho kwenda jangwani, 13 akakaa huko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa huko pamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawa wanamtumikia. 14 Yohane alipokwisha fungwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya, akahubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, 15 “Wakati umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema!”

Upload: others

Post on 08-Feb-2020

5 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 1:1 1 MARKO MTAKATIFU 1:15

INJILI KAMA ALIVYOIANDIKAMARKO MTAKATIFU1 Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

2 Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:“Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeyeatakutayarishia njia yako. 3 Sauti ya mtu imesikika jang-wani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni mapitoyake.” 4 Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubirikwamba ni lazima watu watubu na kubatizwa ili Munguawasamehe dhambi zao. 5 Watu kutoka sehemu zote zaYudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea,wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mtoYordani. 6 Yohane alikuwa amevaa vazi lililofumwa kwamanyoya ya ngamia, namkandawa ngozi kiunonimwake.Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. 7Nayealihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye uwezozaidi kulikomimi, ambayemimi sistahili hata kuinama nakufungua kamba za viatu vyake. 8Mimi ninawabatiza kwamaji, lakini yeye atawabatiza kwa RohoMtakatifu.” 9 Sikuhizo, Yesu alifika kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, akaba-tizwa na Yohane katika mto Yordani. 10Mara tu alipotokamajini, aliona mbingu zimefunguliwa, na Roho akishukajuu yake kama njiwa. 11 Sauti ikasikika kutoka mbinguni:“Wewe ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe.”12Mara akaongozwa na Roho kwenda jangwani, 13 akakaahuko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa hukopamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawawanamtumikia. 14 Yohane alipokwisha fungwa gerezani,Yesu alikwenda Galilaya, akahubiri Habari Njema yaMungu, akisema, 15 “Wakati umetimia, na Ufalme waMungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema!”

Page 2: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 1:16 2 MARKO MTAKATIFU 1:3216 Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaonawavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivuasamaki kwa wavu. 17 Yesu akawaambia, “Nifuateni naminitawafanya ninyi wavuvi wa watu.” 18Mara wakaziachanyavu zao, wakamfuata. 19 Alipokwenda mbele kidogo,aliwaona Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Nao piawalikuwa ndani ya mashua yao wakizitengeneza nyavuzao. 20 Yesu akawaita mara, nao wakamwacha babayao Zebedayo katika mashua pamoja na wafanyakazi,wakamfuata. 21 Wakafika mjini Kafarnaumu, na marailipofika Sabato, Yesu akaingia katika Sunagogi, akaanzakufundisha. 22 Watu wote waliomsikia walishangazwana mafundisho yake, maana hakuwa anafundisha kamawalimu wao wa Sheria, bali kama mtu mwenye mam-laka. 23 Mara akatokea mle ndani ya sunagogi mtummoja mwenye pepo mchafu, 24 akapaaza sauti, “Unanini nasi, wewe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja ku-tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifuwa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtokemtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu akamtikisatik-isa mtu huyo, kisha akalia kwa sauti kubwa, akamtoka.27 Watu wote wakashangaa, wakaulizana, “Ni mambogani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyuanayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, naowanamtii!” 28 Habari za Yesu zikaenea upesi kila mahalikatika wilaya ya Galilaya. 29 Wakatoka katika sunagogi,wakaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simonina Andrea; Yakobo na Yohane walikwenda pamoja nao.30Basi, mamammoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandaniana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.31 Yesu akamwendea huyo mama, akamshika mkono,akamwinua. Na ile homa ikamwacha, akaanza kuwatu-mikia. 32 Jioni, jua lilipokwisha tua, wakamleteaYesuwag-

Page 3: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 1:33 3 MARKO MTAKATIFU 2:2onjwa wote na watu waliopagawa na pepo. 33Watu wotewa mji ule wakakusanyika nje ya mlango. 34 Naye Yesuakawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbal-imbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusukusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.35 Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka,akaenda mahali pa faragha kusali. 36 Simoni na wenzakewakaenda kumtafuta. 37 Walipomwona wakamwambia,“Kila mtu anakutafuta.” 38 Yesu akawaambia, “Twendenikatika miji mingine ya jirani nikahubiri huko pia, maananimekuja kwa sababu hiyo.” 39 Basi, akaenda kila mahaliGalilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo.40Mtu mmoja mwenye ukoma alimwendea Yesu, akapigamagoti, akamwomba, “Ukitaka, waweza kunitakasa!”41 Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake,akamgusa na kumwambia, “Nataka, takasika!” 42 Maraukoma ukamwacha mtu huyo, akatakasika. 43 KishaYesu akamwambia aende zake upesi na kumwonya vikali,44 “Usimwambie mtu yeyote jambo hili, ila nenda uka-jionyeshe kwa kuhani; kisha utoe sadaka kwa ajili ya ku-takasika kwako kama alivyoamuru Mose, iwe uthibitishokwao kwamba umepona.” 45 Lakini huyo mtu akaenda,akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusemamambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katikamji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pafaragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kilaupande.

21Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu

wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani. 2 Basi,wakaja watu wengi sana hata nafasi yoyote ikakosekanamlangoni. Yesu alikuwa akiwahubiria ujumbe wake,

Page 4: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 2:3 4 MARKO MTAKATIFU 2:163 wakati mtu mmoja aliyepooza alipoletwa kwake akiwaamechukuliwa na watu wanne. 4 Kwa sababu ya huoumati wa watu, hawakuweza kumpeleka karibu naYesu. Basi, wakatoboa sehemu ya dari iliyokuwa juuya mahali alipokuwa Yesu. Walipokwisha pata nafasi,wakamteremsha huyo mtu akiwa amelala juu ya mkeka.5 Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtualiyepooza, “Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.”6 Baadhi ya walimu wa Sheria waliokuwa wameketihapo wakawaza mioyoni mwao, 7 “Anathubutuje kusemahivyo? Anamkufuru Mungu! Hakuna mtu awezayekusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake.” 8 Yesualitambua mara mawazo yao, akawaambia, “Mbonamnawaza hivyo mioyoni mwenu? 9 Ni lipi lililo rahisizaidi: kumwambia mtu huyu aliyepooza, Umesamehewadhambi zako, au kumwambia, Inuka! Chukuamkekawakoutembee? 10 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtuanayo mamlaka ya kuwasamehe watu dhambi duniani.”Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, 11 “Nakwambiasimama, chukua mkeka wako uende nyumbani!” 12Mara,watu wote wakiwa wanamtazama, huyo mtu akainuka,akauchukua mkeka wake, akaenda zake. Watu wotewakashangaa na kumtukuza Mungu wakisema, “Hatu-japata kamwe kuona jambo kama hili.” 13 Yesu alik-wenda tena kando ya ziwa. Umati wa watu ukamwen-dea, naye akaanza kuwafundisha. 14 Alipokuwa akipita,akamwona Lawi mwana wa Alfayo, ameketi katika ofisiya ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate!” Lawi akasi-mama, akamfuata. 15 Baadaye, Yesu alikuwa amekaamezani, nyumbani kwa Lawi, kula chakula. Watozaushuru wengi na wenye dhambi walikuwa wamemfuataYesu na wengi wao wakawa wamekaa mezani pamojanaye na wanafunzi wake. 16 Basi, baadhi ya walimu

Page 5: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 2:17 5 MARKO MTAKATIFU 2:26wa Sheria ambao walikuwa Mafarisayo walipomwonaYesu akila pamoja na watu wenye dhambi na watozaushuru, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini anakulapamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?” 17 Yesualipowasikia, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitajidaktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikujakuwaita watu wema, ila wenye dhambi.” 18Wakati mmojawanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo wa-likuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwulizaYesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayowanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” 19 Yesuakajibu, “Walioalikwaharusiniwanawezaje kufunga kamabwana harusi yupo pamoja nao? Wakati wote wawapopamoja na bwana harusi hawawezi kufunga. 20 Lakiniwakati utafika ambapo bwana harusi ataondolewa katiyao; wakati huo ndipo watakapofunga. 21 “Hakuna mtuanayekata kiraka kutoka katika nguompya na kukishoneakatika nguo kuukuu. Kama akifanya hivyo, hicho ki-raka kipya kitararuka kutoka hilo vazi kuukuu, nalo lita-haribika zaidi. 22 Wala hakuna mtu atiaye divai mpyakatika viriba vikuukuu. Kama akifanya hivyo, divaiitavipasua hivyo viriba, nayo divai pamoja na hivyoviriba vitaharibika. Divai mpya hutiwa katika viribavipya!” 23 Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapitakatika mashamba ya ngano. Walipokuwa wanatem-bea, wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke yangano. 24 Mafarisayo wakawaambia, “Tazama! Kwa niniwanafanya jambo ambalo si halali kufanya wakati waSabato?” 25 Yesu akawajibu, “Je, hamjapata kusoma juuya kile alichofanya Daudiwakati alipohitaji chakula? Yeyepamoja na wenzake waliona njaa, 26 naye akaingia ndaniya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbeleyaMungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa

Page 6: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 2:27 6 MARKO MTAKATIFU 3:12Kuhani Mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwawameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tenaakawapa na wenzake.” 27Basi, Yesu akawaambia, “Sabatoiliwekwa kwa ajili ya binadamu na si binadamu kwa ajiliya Sabato! 28Kwa hiyo, Mwana wa Mtu ni Bwana hata waSabato.”

31 Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani

mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza. 2Humobaadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo sikuya sabato ili wapate kumshtaki. 3 Yesu akamwambiahuyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, “Njoo hapakatikati.” 4 Kisha, akawauliza, “Je, ni halali siku yaSabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya;kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao hawakusema neno.5Hapo akawatazamawote kwa hasira, akaona huzuni kwasababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambiahuyo mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyoshamkono wake, ukawa mzima tena. 6 Mara Mafarisayowakatoka nje, wakafanya shauri pamoja na watu wakikundi cha Herode jinsi ya kumwangamiza Yesu. 7 Yesualiondoka hapo pamoja na wanafunzi wake, akaendakando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata. Watuhao walikuwa wametoka Yerusalemu, Yudea, 8 Idumea,ng'ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu haowengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambomengi aliyokuwa ameyatenda. 9 Yesu akawaambia wana-funzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wawatu usije ukamsonga. 10 Alikuwa amewaponya watuwengi, nawagonjwawotewakawawanamsonga ili wapatekumgusa. 11 Na watu waliokuwa wamepagawa na pepowachafu walipomwona, walijitupa chini mbele yake nakupaaza sauti, “Wewe ni Mwana wa Mungu!” 12 Lakini

Page 7: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 3:13 7 MARKO MTAKATIFU 3:29Yesu akawaamuru kwa ukali wasimjulishe kwa watu.13Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi,wakamwendea, 14 naye akawateua watu kumi na wawiliambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri15 na wawe na mamlaka ya kuwafukuza pepo. 16 Basi,hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni(ambaye Yesu alimpa jina, Petro), 17 Yakobo na Yohane,wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jinaBoanerge, maana yake “wanangurumo”), 18 Andrea naFilipo, Batholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwanawa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanani na 19Yuda Iskariotiambaye alimsaliti Yesu. 20 Kisha Yesu alikwenda nyum-bani. Umati wa watu ukakusanyika tena, hata Yesu nawafuasi wake wasiweze kupata nafasi ya kula chakula.21Basi, watu wa jamaa yake walipopata habari hiyo waka-toka kwenda kumchukua maana walikuwa wanasemakwamba amepatwa na wazimu. 22 Nao walimu wa She-ria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “AnaBeelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuuwa pepo.” 23 Hapo Yesu akawaita, akawaambia kwamifano, “Shetani anawezaje kumfukuza Shetani? 24 Ikiwautawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanay-opigana, utawala huo hauwezi kudumu. 25 Tena, ikiwajamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopin-gana, jamaa hiyo itaangamia. 26 Ikiwa basi, utawala waShetani umegawanyika vikundivikundi hauwezi kudumu,bali utaangamia kabisa. 27 “Hakuna mtu awezayekuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kum-nyang'anya mali yake, isipokuwa kwanza amemfungahuyo mtu mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kum-nyang'anya mali yake. 28 “Kweli nawaambieni, watuwatasamehewa dhambi zao zote na kufuru zao zote;29 lakini anayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu,

Page 8: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 3:30 8 MARKO MTAKATIFU 4:10hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambi ya milele.”30 (Yesu alisema hivyo kwa sababu walikuwa wanasema,“Ana pepo mchafu.”) 31 Mama yake Yesu na nduguzake walifika hapo, wakasimama nje, wakampelekeaujumbe kutaka kumwona. 32 Umati wa watu ulikuwaumekaa hapo kumzunguka. Basi, wakamwambia, “Mamayako na ndugu zako wako nje, wanataka kukuona.”33 Yesu akawaambia, “Mama yangu na ndugu zanguni kina nani?” 34 Hapo akawatazama watu waliokuwawamemzunguka, akasema, “Tazameni! Hawa ndio mamayangu na ndugu zangu. 35Mtu yeyote anayefanya anay-otaka Mungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yangu namama yangu.”

41 Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa.

Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidiaingie katika mashua na kuketi. Watu wakawa wamekaakatika nchi kavu, kando ya ziwa. 2 Aliwafundishamambo mengi kwa mifano, na katika mafundisho yakealiwaambia, 3 “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupandambegu. 4Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani,ndege wakaja wakazila. 5 Nyingine zilianguka penyemawe pasipokuwa na udongo mwingi. Mbegu hizo zil-iota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina. 6 Jualilipochomoza, zikachomeka; na kwa kuwa mizizi yakehaikuwa na nguvu, zikanyauka. 7 Nyingine ziliangukakwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazohazikuzaa nafaka. 8 Nyingine zilianguka katika udongomzuri, zikakua na kuzaa: moja punje thelathini, mojasitini na nyingine mia.” 9 Kisha akawaambia, “Mwenyemasikio na asikie!” 10 Yesu alipokuwa peke yake, baadhiya wale waliomsikia walimwendea pamoja na wale kumi

Page 9: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 4:11 9 MARKO MTAKATIFU 4:25na wawili, wakamwuliza juu ya hiyo mifano. 11 Nayeakawaambia, “Ninyi mmejaliwa kujua siri ya Utawala waMungu, lakini wale walio nje wataambiwa kila kitu kwamifano, 12 ili, Watazame kweli, lakini wasione. Wasikiekweli, lakini wasielewe. La sivyo, wangemgeukia Mungu,naye angewasamehe.” 13 Basi, Yesu akawauliza, “Je, ninyihamwelewi mfano huu? Mtawezaje basi, kuelewa mfanowowote? 14 Mpanzi hupanda neno la Mungu. 15 Watuwengine ni kama wale walio njiani ambapo mbegu zil-ianguka. Hawa hulisikia hilo neno lakini mara Shetanihuja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao.16Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penyemawe. Mara tu wanapolisikia hilo neno hulipokea kwafuraha. 17 Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndaniyao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakatitaabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo nenomara wanakata tamaa. 18 Watu wengine ni kama zilembegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfanowa wale wanaolisikia hilo neno, 19 lakini wasiwasi waulimwengu huu, anasa za mali na tamaa za kila namnahuwaingia na kulisonga hilo neno, nao hawazai matunda.20Lakini wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa katikaudongo mzuri. Hawa hulisikia hilo neno, wakalipokea,wakazaa matunda: wengine thelathini, wengine sitinina wengine mia moja.” 21 Yesu akaendelea kuwaambia,“Je, watu huwasha taa wakaileta ndani na kuifunikakwa pishi au kuiweka mvunguni? La! Huiweka juuya kinara. 22 Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, nakila kilichofunikwa kitafunuliwa. 23 Mwenye masikio naasikie!” 24 Akawaambia pia, “Sikilizeni kwa makini mna-chosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine,ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa. 25 Aliye nakitu atapewa zaidi; asiye na kitu, hata kile alicho nacho

Page 10: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 4:26 10 MARKO MTAKATIFU 4:41kitachukuliwa.” 26 Yesu akaendelea kusema, “Ufalmewa Mungu ni kama ifuatavyo. Mtu hupanda mbegushambani. 27 Usiku hulala, mchana yu macho na wakatihuo mbegu zinaota na kukua; yeye hajui inavyofanyika.28 Udongo wenyewe huiwezesha mimea kukua na kuzaamatunda: kwanza huchipua jani changa, kisha suke, namwishowe nafaka ndani ya suke. 29 Nafaka inapoiva,huyo mtu huanza kutumia mundu wake, maana wakatiwa mavuno umefika.” 30 Tena, Yesu akasema, “Tuu-fananishe Utawala wa Mungu na nini? Tuueleze kwamifano gani? 31 Ni kama mbegu ya haradali ambayoni ndogo kuliko mbegu zote. 32 Lakini ikisha pandwa,huota na kuwa mmea mkubwa kuliko mimea yote yashambani. Matawi yake huwa makubwa hata ndege waangani huweza kujenga viota vyao katika kivuli chake.”33 Yesu aliwahubiria ujumbe wake kwa mifano minginemingi ya namna hiyo; aliongea nao kadiri walivyowezakusikia. 34Hakuongea nao chochote bila kutumia mifano;lakini alipokuwa pamoja na wanafunzi wake peke yaoalikuwa akiwafafanulia kila kitu. 35 Jioni, siku hiyohiyo,Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvuke ziwa, twendeng'ambo.” 36Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakam-chukua Yesu katika mashua alimokuwa. Palikuwapo piamashua nyingine hapo. 37 Basi, dhoruba kali ikaanzakuvuma, mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikaanzakujaa maji. 38Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua,amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamshana kumwambia, “Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tu-naangamia?” 39 Basi, akaamka, akaukemea ule upepo nakuyaamrisha mawimbi ya ziwa, “Kimya! Tulia!” Hapoupepo ukakoma, kukawa shwari kabisa. 40 Kisha Yesuakawaambia wanafunzi wake, “Mbona mnaogopa? Je,bado hamna imani?” 41 Nao wakaogopa sana, wakawa

Page 11: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 5:1 11 MARKO MTAKATIFU 5:15wanaulizana, “Huyu ni nani basi, hata upepo namawimbivinamtii?”

51 Basi, wakafika katika nchi ya Wagerase, ng'ambo

ya ziwa. 2 Mara tu Yesu aliposhuka mashuani, mtummoja aliyepagawa na pepo mchafu alitoka makaburini,akakutana naye. 3 Mtu huyo alikuwa akiishi mak-aburini wala hakuna mtu aliyeweza tena kumfungakwa minyororo. 4 Mara nyingi walimfunga kwa pinguna minyororo lakini kila mara aliweza kuikata hiyominyororo na kuzivunja hizo pingu, wala hakuna mtualiyeweza kumzuia. 5 Mchana na usiku alikaa mak-aburini na milimani akipaaza sauti na kujikatakata kwamawe. 6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia,akamwinamia 7 akisema kwa sauti kubwa, “Una shaurigani nami, wewe Yesu Mwana wa Mungu aliye juu? Kwajina la Mungu, nakusihi usinitese!” 8 (Alisema hivyokwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia, “Pepo mchafu,mtoke mtu huyu.”) 9 Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lakonani?” Naye akajibu, “Jina langu ni Jeshi, maana sisi tuwengi.” 10 Kisha akamsihi Yesu asiwafukuze hao pepokatika nchi ile. 11 Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwemalishoni kwenye mteremko wa mlima. 12Basi, hao pepowakamsihi, “Utupeleke kwa hao nguruwe, tuwaingie.”13Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka,wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwewapatao elfu mbili likaporomoka kwenye ule mteremkomkali mpaka ziwani, likatumbukia majini. 14Wachungajiwa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilomjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliy-otukia. 15 Wakamwendea Yesu, wakamwona na mtuyuleyule aliyekuwa amepagawa na jeshi la pepo ameketi

Page 12: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 5:16 12 MARKO MTAKATIFU 5:30chini, amevaa nguo na ana akili yake sawa, wakao-gopa. 16Watuwalishuhudia tukio hilo wakaeleza wenginemambo yaliyompata huyo mtu aliyekuwa amepagawana pepo na juu ya wale nguruwe. 17 Basi, wakaanzakumwomba aondoke katika nchi yao. 18 Yesu alipokuwaanapanda mashuani, yule mtu aliyekuwa amepagawa napepo akamwomba amruhusu kwenda naye. 19 LakiniYesu akamkatalia. Badala yake akamwambia, “Nendanyumbani kwa jamaa yako, ukawaambie mambo yoteBwana aliyokutendea na jinsi alivyokuonea huruma.”20 Basi, huyo mtu akaenda, akaanza kutangaza hukoDekapoli mambo yote Yesu aliyomtendea; watu wotewakashangaa. 21 Yesu alivukia tena upande wa pili waziwa kwa mashua. Umati mkubwa wa watu ukaku-sanyika mbele yake, naye akawa amesimama kando yaziwa. 22Hapo akaja mmojawapo wa maofisa wa sunagogi,jina lake Yairo. Alipomwona Yesu, akajitupa mbele yamiguu yake, 23 akamsihi akisema, “Binti yangu mdogoni mgonjwa karibu kufa. Twende tafadhali, ukamwekeemikono yako, apate kupona na kuishi.” 24 Basi, Yesuakaondoka pamoja naye. Watu wengi sana wakamfu-ata, wakawa wanamsonga kila upande. 25 Mmojawapoalikuwa mwanamke mwenye ugonjwa wa kutokwa damukwa muda wa miaka kumi na miwili. 26 Mwanamkehuyo alikuwa amekwisha sumbuka sana kuwaendea wa-ganga wengi. Na ingawa alikuwa amekwisha tumia maliyake yote, hakupata nafuu bali hali yake ilizidi kuwambaya. 27 Alikuwa amesikia habari za Yesu, na hivyoakaupenyamsongamanowawatu kutoka nyuma, akagusavazi lake. 28 Alifanya hivyo, maana alijisemea, “Nikigusatu vazi lake, nitapona.” 29 Mara chemchemi ya damuyake ikakauka, akajisikia mwilini mwake kwamba ame-ponywa ugonjwa wake. 30 Yesu alitambua mara kwamba

Page 13: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 5:31 13 MARKO MTAKATIFU 6:2nguvu imemtoka. Basi akaugeukia ule umati wa watu,akauliza, “Nani aliyegusa mavazi yangu?” 31 Wanafunziwake wakamjibu, “Unaona jinsi watu wanavyokusonga;mbona wauliza nani aliyekugusa?” 32 Lakini Yesu akaen-delea kutazama amwone huyo aliyefanya hivyo. 33 Hapohuyo mwanamke, akifahamu yaliyompata, akajitokezaakitetemeka kwa hofu, akajitupa chini mbele ya Yesuna kusema ukweli wote. 34 Yesu akamwambia, “Binti,imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisaugonjwa wako.” 35 Yesu alipokuwa bado anaongea, watuwalifika kutoka nyumbani kwa yule ofisa wa sunagogi,wakamwambia, “Binti yako amekwisha kufa. Ya ninikuendelea kumsumbua Mwalimu?” 36 Lakini, bila ku-jali walichosema, Yesu akamwambia mkuu wa sunagogi,“Usiogope, amini tu.” 37Wala hakumruhusu mtu yeyotekufuatana naye ila Petro, Yakobo na Yohane nduguyeYakobo. 38 Wakafika nyumbani kwa ofisa wa sunagoginaye Yesu akasikia makelele, kilio na maombolezo mengi.39 Akaingia ndani, akawaambia, “Mbona mnapiga kelelena kulia? Msichana hakufa, amelala tu.” 40 Lakini waowakamcheka. Basi, akawaondoa wote nje, akawachukuababa namamaya huyomsichana nawalewanafunziwake,wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana. 41Kishaakamshika mkono, akamwambia, “Talitha, kumi,” maanayake, “Msichana, nakwambia, amka!” 42 Mara msichanaakasimama, akaanza kutembea. (Alikuwa na umri wamiaka kumi na miwili.) Hapo watu wakashangaa kupitakiasi. 43 Yesu akawakataza sana wasimjulishe mtu jambohilo. Kisha akawaambia wampe huyo msichana chakula.

61 Yesu aliondoka hapo akaenda katika kijiji chake, ak-

ifuatwa na wanafunzi wake. 2 Siku ya Sabato ilipofika,alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia

Page 14: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 6:3 14 MARKO MTAKATIFU 6:17walishangaa, wakasema, “Je, ameyapata wapi mambohaya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendajemaajabu haya anayoyafanya? 3 Je, huyu si yule sere-mala mwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo, Yose,Yuda na Simoni; Je, dada zake si wanaishi papa hapakwetu?” Basi, wakawa namashaka naye. 4Yesu akawaam-bia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake,kwa jamaa zake na nyumbani mwake.” 5 Hakuwezakutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwawachache, akawaponya. 6Alishangaa sana kwa sababu yakutoamini kwao. Kisha Yesu alivitembelea vijiji vya palekaribu akiwafundisha watu. 7 Aliwaita wale wanafunzikumi na wawili, akaanza kuwatuma wawiliwawili. Ali-wapa uwezo wa kuwatoa pepo wachafu, 8 na kuwaamuru,“Msichukue chochote mnapokwenda isipokuwa fimbo tu.Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni.9Vaeni viatu lakini msivae kanzumbili.” 10Tena aliwaam-bia, “Popote mtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humompaka mtakapoondoka mahali hapo. 11 Mahali popoteambapo watu watakataa kuwakaribisheni au kuwasik-iliza, ondokeni hapo na kuyakung'uta mavumbi miguunimwenu kama onyo kwao.” 12 Basi, wakaondoka, wakahu-biri watu watubu. 13 Waliwafukuza pepo wengi wabaya;wakawapaka mafuta wagonjwa wengi, wakawaponya.14 Basi, mfalme Herode alisikia juu ya hayo yote, maanasifa za Yesu zilienea kilamahali. Baadhi ya watuwalikuwawakisema, “Yohane Mbatizaji amefufuka kutoka wafu,ndiyomaananguvu zamiujiza zinafanya kazi ndani yake.”15 Wengine walisema, “Mtu huyu ni Eliya.” Wenginewalisema, “Huyu ni nabii kama mmojawapo wa man-abii wa kale.” 16 Lakini Herode alipopata habari hizialisema, “Huyu ni Yohane! Nilimkata kichwa, lakiniamefufuka.” 17 Hapo awali Herode mwenyewe alikuwa

Page 15: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 6:18 15 MARKO MTAKATIFU 6:31ameamuru Yohane atiwe nguvuni, akamfunga gerezani.Herode alifanya hivyo kwa sababu ya Herodia ambayeHerode alimwoa ingawaje alikuwa mke wa Filipo, nduguyake. 18 Yohane alikuwa amemwambia Herode, “Si halalikwako kumchukua mke wa ndugu yako.” 19 Basi Hero-dia alimchukia sana Yohane, akataka kumwua, asiweze.20Herode alimwogopa Yohane kwa maana alijua kwambayeye ni mtu mwema na mtakatifu, na hivyo akamlinda.Herode alipenda kumsikiliza Yohane, ingawaje baadaya kumsikiliza, alifadhaika sana. 21 Ikapatikana nafasi,wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode. Herodealiwafanyia karamuwazee wa baraza lake, majemadari naviongozi wa Galilaya. 22 Basi, binti yake Herodia aliingia,akacheza, akawafurahisha sana Herode na wageni wake.Mfalme akamwambia huyo msichana, “Niombe chochoteutakacho, nami nitakupa.” 23Tena akamwapia, “Chochoteutakachoniomba, nitakupa: hata ikiwa ni nusu ya ufalmewangu.” 24 Hapo huyo msichana akatoka, akamwulizamama yake, “Niombe nini?” Naye akamjibu, “Kichwacha Yohane mbatizaji.” 25 Msichana akamrudia mfalmembio akamwomba, “Nataka unipe sasa hivi katika siniakichwa cha Yohane mbatizaji.” 26 Mfalme akahuzunikasana, lakini kwa sababu ya kiapo chake, na kwa ajiliya wale wageni wake karamuni, hakutaka kumkatalia.27 Basi, mfalme akamwamuru askari kukileta kichwa chaYohane. Askari akaenda, akamkata kichwa Yohane mlegerezani, 28 akakileta katika sinia, akampa msichana nayemsichana akampa mama yake. 29 Wanafunzi wa Yohanewalipopata habari, walikwenda wakachukua mwili wake,wakauzika kaburini. 30 Wale mitume walirudi, wakaku-sanyika mbele ya Yesu wakamwarifu yote waliyotendana kufundisha. 31 Alisema hivyo kwa kuwa kulikuwa nawatu wengi mno walikuwa wanafika hapo na kuondoka

Page 16: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 6:32 16 MARKO MTAKATIFU 6:46hata Yesu na wanafunzi wake hawakuweza kupata nafasiya kula chakula. Basi, Yesu akawaambia, “Twendenipeke yetu mahali pa faragha kula chakula, mkapumzikekidogo.” 32 Basi, Wakaondoka peke yao kwa mashua,wakaenda mahali pa faragha. 33 Lakini watu wengi wali-waona wakienda, wakawatambua. Hivyo wengi waka-toka katika kila mji, wakakimbilia huko Yesu na wana-funzi wake walikokuwa wanakwenda, wakawatanguliakufika. 34Waliposhuka pwani, Yesu aliona umati mkubwawa watu, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kamakondoo wasio na mchungaji. Akaanza kuwafundishamambo mengi. 35 Saa za mchana zilikwisha pita. Basi,wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwambia, “Hapani nyikani, na sasa kunakuchwa. 36 Afadhali uwaagewatu waende mashambani na katika vijiji vya jirani,wanunue chakula.” 37 Lakini Yesu akawaambia, “Wapenininyi chakula.” Nao wakamwuliza, “Je, twende ku-nunua mikate kwa fedha dinari mia mbili, na kuwapachakula?” 38 Yesu akawauliza, “Mnayo mikate min-gapi? Nendeni mkatazame.” Walipokwisha tazama,wakamwambia, “Kuna mikate mitano na samaki wawili.”39 Basi, Yesu akawaamuru wanafunzi wawaketishe watuwote makundimakundi penye nyasi. 40 Nao wakaketimakundimakundi ya watu mia moja na ya watu hamsini.41 Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samakiwawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu,akaimega mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawiewatu. Na wale samaki wawili pia akawagawia wote.42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Wakaokota mabakiya mikate na samaki pia, wakajaza vikapu kumi na viwili.44 Nao waliokula hiyo mikate walikuwa wanaume elfutano. 45MaraYesu akawaamuruwanafunziwakewapandemashua, wamtangulie kwenda Bethsaida, ng'ambo yaziwa, wakati yeye anauaga umati wa watu. 46 Baada ya

Page 17: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 6:47 17 MARKO MTAKATIFU 7:5kuwaaga watu alikwenda mlimani kusali. 47 Ilipokuwajioni, mashua ilikuwa katikati ya ziwa, naye alikuwa pekeyake katika nchi kavu. 48 Basi, akawaona wanafunzi wakewakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwaunawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendeaakitembea juu ya maji. Alitaka kuwapita. 49 Lakiniwalimwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu,wakapiga yowe. 50Maana wote walipomwona waliogopasana. Mara Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msio-gope!” 51 Kisha akapanda mashuani walimokuwa, na up-epoukatulia. Naowakashangaa sana. 52maanahawakuwabado wameelewa maana ya ile mikate. Akili zao zilikuwabado zimepumbazika. 53 Walivuka ziwa, wakafika nchiya Genesareti, wakatia nanga. 54 Walipotoka mashuani,mara watu wakamtambua Yesu. 55 Basi, kwa harakawakazunguka katika nchi ile yote, wakaanza kuwachukuawagonjwa wamelala juu ya mikeka yao, wakawapelekakila mahali waliposikia Yesu yupo. 56 Kila mahali Yesualipokwenda, vijijini, mijini, au mashambani, watu wali-waweka wagonjwa uwanjani, wakamsihi waguse walaupindo la vazi lake. Nao wote waliomgusa walipona.

71Baadhi yaMafarisayo na walimuwa Sheria waliokuwa

wametoka Yerusalemu walikusanyika mbele ya Yesu.2 Waliona kwamba baadhi ya wanafunzi wake walikulamikate kwamikononajisi, yaani bila kunawa. 3MaanaMa-farisayo na Wayahudi wengine wote huzingatia mapokeoya wazee wao: hawali kitu kabla ya kunawa mikonoipasavyo. 4 Tena hawali kitu chochote kutoka sokonimpaka wamekiosha kwanza. Kuna pia desturi nyinginewalizopokea kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuriana vyombo vya shaba. 5 Basi, Mafarisayo na walimu

Page 18: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 7:6 18 MARKO MTAKATIFU 7:21wa Sheria wakamwuliza Yesu, “Mbona wanafunzi wakohawayajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu, balihula chakula kwa mikono najisi?” 6 Yesu akawajibu,“Wanafiki ninyi! Nabii Isaya alitabiri ukweli juu yenualipoandika: Watu hawa, asema Mungu, huniheshimukwa maneno matupu, lakini mioyoni mwao wako mbalinami. 7 Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanay-ofundisha nimaagizo ya kibinadamu tu. 8Ninyimnaiachaamri ya Mungu na kushikilia maagizo ya watu.” 9 Yesuakaendelea kusema, “Ninyimnajua kuepa kwa ujanja she-ria yaMungu kwa ajili ya kufuatamapokeo yenu. 10MaanaMose aliamuru: Waheshimu baba yako namama yako, na,Anayemlaani baba au mama, lazima afe. 11 Lakini ninyimwafundisha, Kama mtu anacho kitu ambacho angewezakuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasemakwamba kitu hicho ni Korbani (yaani ni zawadi kwaMungu), 12 basi, halazimiki tena kuwasaidia wazazi wake.13 Hivyo ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa ajiliya mafundisho mnayopokezana. Tena mnafanya mambomengi ya namna hiyo.” 14 Yesu aliuita tena ule umatiwa watu, akawaambia, “Nisikilizeni nyote, mkaelewe.15 Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu toka nje am-bacho chaweza kumtia mtu najisi. Lakini kinachotokandani ya mtu ndicho kinachomtia mtu najisi.” 16Mwenyemasikio na asikie! 17Alipouacha umatiwawatu na kuingianyumbani, wanafunzi wake walimwuliza maana ya huomfano. 18Naye akawaambia, “Je, hata ninyi hamwelewi?Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu tokanje hakiwezi kumtia unajisi, 19 kwa maana hakimwingiimoyoni, ila tumboni, na baadaye hutolewa nje chooni?”(Kwa kusema hivyo, Yesu alivihalalisha vyakula vyote.)20Akaendelea kusema, “Kinachotoka ndani yamtu ndichokinachomtia najisi. 21 Kwa maana kutoka ndani, katika

Page 19: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 7:22 19 MARKO MTAKATIFU 8:1moyo wa mtu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi,uuaji, 22 uzinzi, uchoyo, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu,kashfa, kiburi na upumbavu. 23Maovu hayo yote yatokandani ya mtu, nayo humtia mtu najisi.” 24Yesu aliondokahapo, akaenda hadi wilaya ya Tiro. Huko aliingia katikanyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza ku-jificha. 25 Mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwana pepo, alisikia habari za Yesu. Basi, akaja akajitupachini mbele ya miguu yake. 26 Mama huyo alikuwaMgiriki, mwenyeji wa Sirofoinike. Basi, akamwomba Yesuamtoe binti yake pepo mchafu. 27 Yesu akamwambia,“Kwanza watoto washibe; kwa maana si vizuri kuchukuachakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” 28 Lakinihuyo mama akasema, “Sawa, Bwana, lakini hata mbwawalio chini ya meza hula makombo ya watoto.” 29 Yesuakamwambia, “Kwa sababu ya neno hilo, nenda. Pepoamemtoka binti yako!” 30Basi, akaenda nyumbani kwake,akamkuta mtoto amelala kitandani, na pepo amekwishamtoka. 31 Kisha Yesu aliondoka wilayani Tiro, akapitiaSidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.32Basi, wakamletea bubu-kiziwi, wakamwomba amwekeemikono. 33Yesu akamtenga na umati wawatu, akamtia vi-dole masikioni, akatema mate na kumgusa ulimi. 34Kishaakatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia,“Efatha,” maana yake, “Funguka.” 35 Mara masikioyake yakafunguka na ulimi wake ukafunguliwa, akaanzakusema sawasawa. 36 Yesu akawaamuru wasimwambiemtu juu ya jambo hilo. Lakini kadiri alivyowakataza,ndivyo walivyozidi kutangaza habari hiyo. 37 Watu wal-ishangaa sana, wakasema, “Amefanya yote vyema: ame-wajalia viziwi kusikia, na bubu kusema!”

81Wakati huoumatimkubwawawatuulikusanyika tena,

Page 20: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 8:2 20 MARKO MTAKATIFU 8:18na hawakuwa na chakula. Basi, Yesu akawaita wana-funzi wake, akawaambia, 2“Nawahurumiawatu hawa kwasababu wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu, walahawana chakula. 3Nikiwaacha waende nyumbani wakiwana njaa watazimia njiani, maana baadhi yao wametokambali.” 4 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Hapa nyikaniitapatikana wapi mikate ya kuwashibisha watu hawawote?” 5 Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?”Nao wakamjibu, “Saba.” 6 Basi, akawaamuru watu wakaechini. Akaitwaa ile mikate saba, akamshukuru Mungu,akaimega, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu,nao wakawagawia. 7Walikuwa pia na visamaki vichache.Yesu akavibariki, akaamuru vigawiwe watu vilevile.8Watu wakala, wakashiba. Wakaokota mabaki yaliyosaliawakajaza makapu saba. 9 Nao waliokula walikuwa watuwapatao elfu nne. Yesu akawaaga, 10 na mara akapandamashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda wilaya yaDalmanutha. 11 Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadil-iana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka awafanyieishara kuonyesha anayo idhini kutoka mbinguni. 12 Yesuakahuzunika rohoni, akasema, “Mbona kizazi hiki ki-nataka ishara? Kweli nawaambieni, kizazi hiki haki-tapewa ishara yoyote!” 13Basi, akawaacha, akapanda tenamashua, akaanza safari kwenda ng'ambo ya pili ya ziwa.14 Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate;walikuwa na mkate mmoja tu katika mashua. 15 Yesuakawaonya, “Angalieni sana! Jihadharini na chachuya Mafarisayo na chachu ya Herode.” 16 Wanafunziwakaanza kujadiliana wao kwa wao, “Anasema hivyokwa kuwa hatuna mikate.” 17 Yesu alitambua hayo,akawaambia, “Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa namikate? Je, bado hamjafahamu, wala hamjaelewa? Je,mioyo yenu imeshupaa? 18 Je, Mnayo macho na ham-woni? Mnayo masikio na hamsikii? Je, hamkumbuki

Page 21: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 8:19 21 MARKO MTAKATIFU 8:3319 wakati ule nilipoimega ile mikate mitano na kuwapawatu elfu tano? Mlikusanya vikapu vingapi vya mabakiya makombo?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.” 20 “Nanilipoimega ile mikate saba na kuwapa watu elfu nne,mlikusanyamakapumangapi ya makombo?” Wakamjibu,“Saba.” 21 Basi, akawaambia, “Na bado hamjaelewa?”22Yesu alifika Bethsaida pamoja nawanafunziwake. Hukowatu wakamletea kipofu mmoja, wakamwomba amguse.23 Yesu akamshika mkono huyo kipofu, akampeleka njeya kijiji. Akamtemea mate machoni, akamwekea mikono,akamwuliza, “Je, unaweza kuona kitu?” 24 Huyo kipofuakatazama, akasema, “Ninawaona watu wanaoonekanakama miti inayotembea.” 25 Kisha Yesu akamwekea tenamikono machoni, naye akakaza macho, uwezo wake wakuona ukamrudia, akaona kila kitu sawasawa. 26 Yesuakamwambia aende zake nyumbani na kumwamuru,“Usirudi kijijini!” 27 Kisha Yesu na wanafunzi wake wa-likwenda katika vijiji vya Kaisarea Filipi. Walipokuwanjiani, Yesu aliwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasemamimi ni nani?” 28 Wakamjibu, “Wengine wanasemawewe ni Yohane Mbatizaji, wengine Eliya na wenginemmojawapo wa manabii.” 29 Naye akawauliza, “Na ninyije, mnasema mimi ni nani?” Petro akamjibu, “Wewendiwe Kristo.” 30 Kisha Yesu akawaonya wasimwambiemtu yeyote habari zake. 31 Yesu alianza kuwafundishawanafunzi wake: “Ni lazima Mwana wa Mtu apatwena mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhaniwakuu na walimu wa Sheria. Atauawa na baada ya sikutatu atafufuka.” 32 Yesu aliwaambia jambo hilo wazi-wazi. Basi, Petro akamchukua kando, akaanza kumke-mea. 33 Lakini Yesu akageuka, akawatazama wanafunziwake, akamkemea Petro akisema, “Ondoka mbele yangu,Shetani! Fikira zako si za kimungu ila ni za kibinadamu!”

Page 22: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 8:34 22 MARKO MTAKATIFU 9:934 Kisha akauita umati wa watu pamoja na wanafunziwake, akawaambia, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasiwangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalabawake, anifuate. 35Maanamtu anayetaka kuyaokoamaishayake mwenyewe, atayapoteza, lakini mtu atakayepotezamaisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema,atayaokoa. 36 Je, kuna faida gani mtu kuupata ulimwenguwote na kuyapoteza maisha yake? 37Amamtu atatoa kitugani badala ya maisha yake? 38 Mtu yeyote katika kizazihiki kiovu na kisichomjali Mungu anayenionea aibu mimina mafundisho yangu, Mwana wa Mtu atamwonea aibumtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wa Babayake pamoja na malaika watakatifu.”

91 Yesu akaendelea kuwaambia, “Kweli nawaambieni,

wako wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla yakuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa enzi.” 2 Baada yasiku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohanejuu ya mlima mrefu peke yao. Huko, Yesu akageukasura mbele yao, 3mavazi yake yakang'aa, yakawa meupesana, jinsi dobi yeyote duniani asingeweza kuyafanyameupe. 4 Eliya na Mose wakawatokea, wakazungumza naYesu. 5Petro akamwambia Yesu, “Mwalimu, ni vizuri sanakwamba tuko hapa. Basi, afadhali tujenge vibanda vitatu:kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya.”6 Yeye na wenzake waliogopa hata hakujua la kusema.7 Kisha likatokea wingu likawafunika, na sauti ikasikikakutoka katika hilo wingu, “Huyu ni Mwanangumpendwa,msikilizeni.” 8 Mara wanafunzi hao wakatazama tena,lakini hawakumwona mtu mwingine, ila Yesu peke yakepamoja nao. 9 Walipokuwa wakishuka mlimani, Yesualiwakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliy-oyaona, mpaka Mwana wa Mtu atakapokuwa amefufuka

Page 23: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 9:10 23 MARKO MTAKATIFU 9:24kutoka wafu. 10 Basi, wakashika agizo hilo, lakini wakawawanajadiliana wao kwa wao maana ya kufufuka kutokawafu. 11 Wakamwuliza Yesu, “Mbona walimu wa Sheriawanasema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza?” 12 Nayeakawajibu, “Naam, Eliya anakuja kwanza kutayarishayote. Hata hivyo, kwa nini basi imeandikwa katikaMaandiko Matakatifu kwamba Mwana wa Mtu atapatwana mateso mengi na kudharauliwa? 13 Lakini nawaambi-eni, Eliya amekwisha kuja, naowakamtendeawalivyotakakama ilivyoandikwa juu yake.” 14 Walipowafikia walewanafunzi wengine, waliona umati mkubwa wa watuhapo. Na baadhi ya walimu wa Sheria walikuwa wana-jadiliana nao. 15 Mara tu ule umati wa watu ulipom-wona, wote walishangaa sana, wakamkimbilia wamsal-imu. 16Yesu akawauliza, “Mnajadiliana nini nao?” 17Hapomtu mmoja katika ule umati wa watu akamjibu, “Mwal-imu, nimemletamwanangu kwako, ana pepo aliyemfanyakuwa bubu. 18 Kila mara anapomvamia, humwangushachini na kumfanya atokwe na povu kinywani, akisagameno na kuwamkavumwili wote. Niliwaombawanafunziwako wamtoe huyo pepo lakini hawakuweza.” 19 Yesuakawaambia, “Enyi kizazi kisicho na imani! Nitakaa nanyimpaka lini? Nitawavumiliampaka lini? Mleteni kwangu.”20 Wakampeleka. Mara tu huyo pepo alipomwona Yesu,alimtia mtoto kifafa, naye mtoto akaanguka chini, aka-gaagaa na kutoka povu kinywani. Yesu akamwuliza babayake huyo mtoto, 21 “Amepatwa na mambo hayo tangulini?” Naye akamjibu, “Tangu utoto wake. 22 Na maranyingi pepo huyo amemwangusha motoni na majini,ili amwangamize kabisa. Basi, ikiwa waweza, utuhuru-mie na kutusaidia!” 23 Yesu akamwambia, “Eti ikiwawaweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye naimani.” 24 Hapo, huyo baba akalia kwa sauti, “Naamini!

Page 24: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 9:25 24 MARKO MTAKATIFU 9:39Lakini imani yangu haitoshi, nisaidie!” 25Yesu alipouonaumati wa watu unaongezeka upesi mbele yake, alimke-mea yule pepo mchafu, “Pepo unayemfanya huyu mtotokuwa bubu-kiziwi, nakuamuru, mtoke mtoto huyu walausimwingie tena!” 26 Hapo huyo pepo alipaaza sauti,akamwangusha huyomtoto chini, kisha akamtoka. Mtotoalionekana kama maiti, hata wengine walisema, “Amek-ufa!” 27 Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua, nayeakasimama. 28Yesu alipoingia nyumbani, wanafunziwakewalimwuliza kwa faragha, “Kwa nini sisi hatukuwezakumtoa?” 29Naye akawaambia, “Pepo wa aina hii hawezikutoka isipokuwa kwa sala tu.” 30Yesu nawanafunzi wakewaliondoka hapo, wakaendelea na safari kupitia wilayaya Galilaya. Yesu hakupenda watu wajue alipokuwa,31 kwa sababu alikuwa anawafundisha wanafunzi wake.Aliwaambia, “Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watuambao watamuua; lakini siku ya tatu baada ya kuuawaatafufuka.” 32 Wanafunzi hawakufahamu jambo hilo.Wakaogopa kumwuliza. 33 Basi, walifika Kafarnaumu.Na alipokuwa nyumbani, aliwauliza, “Mlikuwa mnajadil-iana nini njiani?” 34 Lakini wao wakanyamaza, maananjiani walikuwa wamebishana ni nani aliye mkuu katiyao. 35 Yesu akaketi chini, akawaita wale kumi na wawili,akawaambia, “Yeyote anayetaka kuwa wa kwanza lazimaawe wa mwisho na kuwa mtumishi wa wote.” 36 Kishaakamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha kati yao,akamku mbatia, halafu akawaambia, 37 “Anayempokeamtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; naanayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokeayule aliyenituma.” 38 Yohane akamwambia, “Mwalimu,tumemwona mtu mmoja akitoa pepo kwa kulitumia jinalako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa yeye si mmojawetu.” 39 Lakini Yesu akasema, “Msimkataze, maana

Page 25: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 9:40 25 MARKO MTAKATIFU 10:4hakuna mtu anayefanya muujiza kwa jina langu, na papohapo akaweza kusema mabaya juu yangu. 40 Maana,asiyepingana nasi, yuko upande wetu. 41 Mtu yeyoteatakeyewapeni kikombe cha maji ya kunywa kwa sababuninyi ni watu wake Kristo, hakika hatakosa kupata tuzolake. 42 “Mtu yeyote atakayemfanya mmoja wa hawawadogowanaoniamini atende dhambi, ingekuwa afadhalikwa mtu huyo kufungiwa shingoni mwake jiwe kubwa lakusagia na kutupwa baharini. 43Mkono wako ukikukose-sha, ukate! Afadhali kuingia kwenye uzima bila mkonommoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katikamoto wa Jehanamu. 44 Humo, wadudu wake hawafi namoto hauzimiki. 45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate!Afadhali kuingia katika uzima bila mguu mmoja, kulikokuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto waJehanamu. 46Humo, wadudu wake hawafi na moto hauz-imiki. 47 Na jicho lako likikukosesha, ling'oe! Afadhalikuingia katika utawala wa Mungu ukiwa na jicho mojatu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwakatika moto wa Jehanamu. 48Humowadudu wake hawafi,namoto hauzimiki. 49“Maana kilammoja atakolezwa kwamoto. 50 Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake,itakolezwa na nini? Muwe na chumvi ndani yenu nakudumisha amani kati yenu.”

101 Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea na hata

ng'ambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendeatena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturiyake. 2Basi, Mafarisayowakamwendea, na kwa kumjaribuwakamwuliza, “Je, ni halali mtu kumpa talaka mkewe?”3 Yesu akawajibu, “Mose aliwapa maagizo gani?” 4 Naowakasema, “Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati

Page 26: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 10:5 26 MARKO MTAKATIFU 10:22ya talaka na kumwacha.” 5 Yesu akawaambia, “Mosealiwaandikia amri hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyoyenu. 6 Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu al-iumba mwanamume na mwanamke. 7 Hivyo mwana-mume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana namkewe, 8 nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo,wao si wawili tena bali mwili mmoja. 9 Basi, alichoun-ganishaMungu, binadamu asitenganishe.” 10Walipoingiatena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juuya jambo hilo. 11 Naye akawaambia, “Anayemwachamkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe.12 Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewana mwingine anazini.” 13 Watu walimletea Yesu wa-toto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawake-mea. 14 Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia,“Waacheni haowatotowaje kwangu, walamsiwazuie, kwamaana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kamawatoto hawa. 15 Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiye-upokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hataingiakatika Ufalme huo.” 16 Kisha akawapokea watoto hao,akawawekea mikono, akawabariki. 17Yesu alipoanza tenasafari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magotimbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyejeili niupate uzima wa milele?” 18 Yesu akamjibu, “Mbonaunaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu pekeyake. 19 Unazijua amri: Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoeushahidi wa uongo; Usidanganye; Waheshimu baba namama yako.” 20 Naye akamjibu, “Mwalimu, hayo yotenimeyazingatia tangu ujana wangu.” 21 Yesu akam-tazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa nakitu kimoja: nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwapemaskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoounifuate.” 22 Aliposikia hayo, alisikitika, akaenda zake

Page 27: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 10:23 27 MARKO MTAKATIFU 10:35akiwa na huzuni, kwa maana alikuwa na mali nyingi.23 Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunziwake, “Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajirikuingia katika Ufalme wa Mungu!” 24 Wanafunzi wal-ishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena,“Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalmewa Mungu! 25 Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katikatundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalmewa Mungu.” 26 Wanafunzi wake wakashangaa sanawakaulizana, “Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?”27 Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa binadamu hai-wezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungumambo yote huwezekana.” 28 Petro akamwambia, “Nasisi je? Tumeacha yote, tukakufuata!” 29 Yesu akasema,“Kweli nawaambieni, kila mtu aliyeacha nyumba, aundugu, au dada, au mama, au baba, au watoto aumashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya HabariNjema, 30 atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasanyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashambapamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokeauzima wa milele. 31 Lakini wengi walio wa kwanzawatakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wakwanza.” 32 Basi, walikuwa njiani kwenda Yerusalemu,na Yesu alikuwa anawatangulia. Wanafunzi wake wal-ijawa na hofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesuakawachukua tena kando wale kumi na wawili, akaanzakuwaambia yale yatakayompata: 33 “Sikilizeni! Tu-nakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atak-abidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria,nao watamhukumu auawe na kumkabidhi kwa watuwa mataifa. 34 Nao watamdhihaki; watamtemea mate,watampiga mijeledi na kumwua. Na baada ya siku tatuatafufuka.” 35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo,walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka

Page 28: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 10:36 28 MARKO MTAKATIFU 10:51utufanyie kitu tutakachokuomba.” 36 Yesu akawauliza,“Mnataka niwafanyie nini?” 37 Wakamjibu, “Uturuhusutuketi mmoja upande wako wa kulia na mwingineupande wako wa kushoto katika utukufu wa Ufalmewako.” 38 Yesu akawaambia, “Hamjui mnachoomba!Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa, au ku-batizwa kama nitakavyobatizwa?” 39 Wakamjibu, “Tu-naweza.” Yesu akawaambia, “Kikombe nitakachokunywamtakinywa kweli, namtabatizwa kama nitakavyobatizwa.40 Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu siwajibu wangu kupanga, bali nafasi hizo watapewa walewaliotayarishiwa.” 41Walewanafunzi wengine kumiwali-posikia hayo, walianza kuchukizwa na Yakobo na Yohane.42 Yesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwamba walewanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawalawatu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watuwao. 43 Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwamkuu kati yenu, sharti awe mtumishi wenu. 44Anayetakakuwa wa kwanza, sharti awe mtumishi wa wote. 45MaanaMwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila alikuja kutumikia,na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.” 46 Basi,wakafika Yeriko, naye Yesu alipokuwa anatoka katika mjihuo akiwa na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwawa watu, kipofu mwombaji aitwaye Bartimayomwana waTimayo alikuwa ameketi kando ya barabara. 47Aliposikiakwamba ni Yesu wa Nazareti aliyekuwa anapita mahalihapo, alianza kupaaza sauti, “Yesu, Mwana wa Daudi,nihurumie!” 48 Watu wengi walimkemea ili anyamaze,lakini yeye akazidi kupaaza sauti, “Mwana wa Daudi, ni-hurumie!” 49 Yesu alisimama, akasema, “Mwiteni.” Basi,wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo!Simama, anakuita.” 50 Naye akatupilia mbali vazi lake,akaruka juu, akamwendea Yesu. 51 Yesu akamwuliza,

Page 29: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 10:52 29 MARKO MTAKATIFU 11:13“Unataka nikufanyie nini?” Huyo kipofu akamwambia,“Mwalimu, naomba nipate kuona.” 52Yesu akamwambia,“Nenda, imani yako imekuponya.” Mara huyo kipofuakaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.

111 Walipokuwa wanakaribia Yerusalemu walifika

Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni.Hapo aliwatuma wawili wa wanafunzi wake,2 akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbeleyenu. Mtakapokuwa mnaingia humo, mtakuta mwanapunda amefungwa ambaye bado hajatumiwa na mtu.Mfungueni mkamlete. 3 Kama mtu akiwauliza, Mbonamnafanya hivyo? Mwambieni, Bwana anamhitaji naatamrudisha hapa mara.” 4 Basi, wakaenda, wakamkutamwana punda barabarani amefungwa mlangoni.Walipokuwa wakimfungua, 5 baadhi ya watu waliokuwawamesimama hapo wakawauliza “Kwa nini mnamfunguahuyo mwana punda?” 6 Wanafunzi wakajibu kama Yesualivyokuwa amewaambia; nao wakawaacha waende zao.7Wakampelekea Yesu huyo mwana punda. Wakatandikamavazi yao juu ya huyomwana punda, na Yesu akaketi juuyake. 8Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani;wengine wakatandaza matawi ya miti waliyoyakatamashambani. 9 Watu wote waliotangulia na walewaliofuata wakapaaza sauti zao wakisema, “Hosana!Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana! 10 UbarikiweUfalme ujao wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni!”11Yesu aliingia mjini Yerusalemu akaendamoja kwamojampaka Hekaluni, akatazama kila kitu kwa makini. Lakinikwa vile ilikwisha kuwa jioni, akaenda Bethania pamojana wale kumi na wawili. 12 Kesho yake, walipokuwawanatoka Bethania, Yesu aliona njaa. 13 Basi, akaona

Page 30: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 11:14 30 MARKO MTAKATIFU 11:26kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea iliaone kama ulikuwa na tunda lolote. Alipoufikia, aliukutabila tunda lolote ila majani matupu, kwa vile hayakuwamajira ya mtini kuzaa matunda. 14 Hapo akauambiamtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matundakwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.15 Basi, wakafika Yerusalemu. Yesu akaingia Hekaluni,akaanza kuwafukuza nje watu waliokuwa wanauzana kununua vitu humo ndani. Akazipindua meza zawale waliokuwa wakibadilishana fedha na viti vya walewaliokuwa wakiuza njiwa. 16 Hakumruhusu mtu yeyotekupitia Hekaluni akichukua kitu. 17Kisha akawafundisha,“Imeandikwa: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya salakwa ajili ya mataifa yote! Lakini ninyi mmeifanya kuwapango la wanyang'anyi!” 18Makuhani wakuu na walimuwa Sheria waliposikia hayo, walianza kutafuta njia yakumwangamiza. Lakini walimwogopa kwa sababuumati wa watu ulishangazwa na mafundisho yake.19 Ilipokuwa jioni, Yesu na wanafunzi wake waliondokamjini. 20 Asubuhi na mapema, walipokuwa wanapita,waliuona ule mtini umenyauka wote, hata mizizi.21 Petro aliukumbuka, akamwambia Yesu, “Mwalimu,tazama! Ule mtini ulioulaani, umenyauka!” 22 Yesuakawaambia, “Mwaminini Mungu. 23Nawaambieni kweli,mtu akiuambia mlima huu: Ng'oka ukajitose baharinibila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwambamambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambohilo. 24 Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuombakitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa.25Mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakoseachochote, ili Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyimakosa yenu. 26 Lakini msipowasamehe wengine, hataBaba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa

Page 31: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 11:27 31 MARKO MTAKATIFU 12:7yenu.” 27Basi, wakafika tena Yerusalemu. Yesu alipokuwaakitembea Hekaluni, makuhani wakuu, walimu wa Sheriana wazee walimwendea, 28 wakamwuliza, “Unafanyamambo haya kwa mamlaka gani? Nani aliyekupamamlaka ya kufanya mambo haya?” 29 Lakini Yesuakawaambia, “Nitawaulizeni swali moja; mkinijibu, napia nitawaambieni ni kwa mamlaka gani ninafanyamambo haya. 30 Je, mamlaka ya Yohane ya kubatizayalitokambinguni ama kwawatu? Nijibuni.” 31Wakaanzakujadiliana, “Tukisema, Yalitoka mbinguni, atatuuliza,Basi, mbona hamkumsadiki? 32 Na tukisema, Yalitokakwa watu...” (Waliogopa umati wa watu maana wotewaliamini kwamba Yohane alikuwa kweli nabii.) 33 Basi,wakamjibu Yesu, “Sisi hatujui.” Naye Yesu akawaambia,“Nami pia sitawaambieni ninafanya mambo haya kwamamlaka gani.”

121 Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja

alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, nakatikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai,akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwawakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali. 2 Wakati wamavuno, alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulimaakamletee sehemu ya mazao ya shamba lake. 3 Walewakulima wakamkamata, wakampiga, wakamrudishamikono mitupu. 4 Akatuma tena mtumishi mwingine;huyu wakamuumiza kichwa na kumtendea vibaya.5 Mwenye shamba akatuma mtumishi mwingine tena,na huyo wakamuua. Wengine wengi waliotumwa, baadhiyao walipigwa, na wengi wakauawa. 6 Alibakiwa badona mtu mmoja, yaani mwanawe mpendwa. Mwishoweakamtuma huyo akisema, Watamheshimu mwanangu.7 Lakini hao wakulima wakaambiana, Huyu ndiye mrithi,

Page 32: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 12:8 32 MARKO MTAKATIFU 12:22basi, tumuue ili urithi wake uwe wetu! 8 Kwa hiyowakamkamata, wakamuua na kumtupa nje ya lile shambala mizabibu. 9 “Basi, mwenye shamba atafanya nini?Atakuja kuwaangamiza hao wakulima na kulikodisha hiloshamba la mizabibu kwa watu wengine. 10 Je, hamjasomaMaandiko haya? Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwajiwe kuu la msingi. 11 Bwana ndiye aliyefanya jambohili, nalo ni la ajabu sana kwetu.” 12 Makuhani wakuu,walimu wa Sheria na wazee walifahamu ya kwambamfano huo ulikuwa unawahusu. Kwa hiyo walijaribukumtia nguvuni, lakini waliogopa umati wa watu.Basi, wakamwacha wakaenda zao. 13 Basi, baadhi yaMafarisayo na wafuasi wa kikundi cha Herode walitumwaili wamtege Yesu kwa maneno yake. 14 Wakamwendea,wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe nimtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjalimtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakiniwafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halalikulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”15 Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbonamnanijaribu? Nionyesheni sarafu.” 16Wakamwonyesha.Naye akawauliza, “Sura na chapa hii ni ya nani?”Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” 17 Basi, Yesu akawaambia,“Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari na Mungu yaliyo yakeMungu.” Wakashangazwa sana naye. 18 Masadukayowasemao kwamba hakuna ufufuo walimwendea Yesu,wakamwuliza, 19 “Mwalimu, Mose alituagiza hivi: Mtuakifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazimaamchukue huyo mamamjane amzalie watoto ndugu yakemarehemu. 20 Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanzaalioa, akafa bila kuacha mtoto. 21Ndugu wa pili akamwoahuyo mjane, naye pia akafa bila kuacha mtoto; na nduguwatatu hali kadhalika. 22Wote saba walikufa bila kuacha

Page 33: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 12:23 33 MARKO MTAKATIFU 12:35mtoto. Mwishowe yule mama mjane naye akafa. 23 Basi,siku watu watakapofufuka, mama huyo atakuwa mke wanani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.” 24 Yesuakawaambia, “Ninyi mmekosea sana, kwa sababu hamjuiMaandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu. 25 Maanawafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwakama malaika wa mbinguni. 26 Lakini kuhusu kufufuliwakwa wafu, je, hamjasoma kitabu cha Mose katika sehemuinayohusu kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto?Mungu alimwambia Mose, Mimi ni Mungu wa Abrahamu,Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. 27 Basi, yeyesi Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai. Ninyimmekosea sana!” 28 Mmojawapo wa walimu wa Sheriaalifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwambaYesu aliwajibu vyema, akajitokeza akamwuliza, “Katikaamri zote ni ipi iliyo ya kwanza?” 29 Yesu akamjibu,“Ya kwanza ndiyo hii: Sikiliza, Israeli! Bwana Munguwetu ndiye peke yake Bwana. 30 Mpende Bwana Munguwako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwaakili yako yote na kwa nguvu zako zote. 31 Na ya pilindiyo hii: Mpende jirani yako kama unavyojipendamwenyewe. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kulikohizi.” 32 Basi, yule mwalimu wa Sheria akamwambia,“Vyema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Munguni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye. 33 Na nilazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwaakili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yakekama anavyojipenda mwenyewe. Jambo hili ni muhimuzaidi kuliko dhabihu na sadaka zote za kuteketezwa.”34 Yesu alipoona kwamba huyu mtu alimjibu kwaujasiri, akamwambia, “Wewe huko mbali na Ufalme waMungu.” Baada ya hayo, hakuna mtu aliyethubutu tenakumwuliza kitu. 35 Wakati Yesu alipokuwa akifundisha

Page 34: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 12:36 34 MARKO MTAKATIFU 13:3Hekaluni, aliuliza, “Mbona walimu wa Sheria wanasemaya kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 36 Daudimwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema:Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wanguwa kulia, Mpaka nitakapowaweka adui zako chini yamiguu yako.” 37 “Daudi mwenyewe anamwita KristoBwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanae?” Umati wa watuulikuwa ukimsikiliza kwa furaha. 38 Katika mafundishoyake, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa Sheriaambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu nakusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketimahali pa heshima katika masunagogi, 39 na kuchukuanafasi za heshima katika karamu. 40Huwanyonya wajanehuku wakijisingizia kusali sala ndefu. Siku ya hukumuwatapata adhabu kali!” 41 Yesu alikuwa ameketi karibuna sanduku la hazina. Akawa anatazama jinsi watuwengi walivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katikahazina ya Hekalu. Matajiri wengi walitoa fedha nyingi.42Hapo akaja mama mmoja mjane maskini, akatoa sarafumbili ndogo za fedha. 43 Yesu akawaita wanafunzi wake,akawaambia, “Kweli nawaambieni, huyu mama mjanemaskini ametoa zaidi kuliko wengine wote waliotiafedha katika sanduku la hazina. 44 Maana wote walitoakutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawani maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitualichohitaji kwa kuishi.”

131 Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wana-

funzi wake alimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi mawehaya na majengo haya yalivyo ya ajabu!” 2 Yesuakamwambia, “Je, unayaona majengo haya makubwa?Hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kilakitu kitabomolewa.” 3 Yesu alipokuwa ameketi juu ya

Page 35: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 13:4 35 MARKO MTAKATIFU 13:17mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro, Yakobo,Yohane na Andreawakamwuliza kwa faragha, 4“Twambiemambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonye-sha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?” 5 Yesuakaanza kuwaambia, “Jihadharini msije mkadanganywana mtu. 6 Maana wengi watakuja wakilitumia jinalangu, wakisema, Mimi ndiye! nao watawapotoshawatu wengi. 7 Mtakaposikia juu ya vita na fununu zavita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakinimwisho wenyewe ungali bado. 8 Taifa moja litapiganana taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawalamwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko yaardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu yakwanza ya kujifungua mtoto. 9 “Lakini ninyi jihad-harini. Maana watu watawapelekeni mahakamani, nakuwapigeni katika masunagogi. Mtapelekwa mbele yawatawala na wafalme kwa sababu yangu ili mpate kun-ishuhudia kwao. 10 Lakini lazima kwanza Habari Njemaihubiriwe kwa mataifa yote. 11 Nao watakapowatieninguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasijuu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semenichochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema,bali Roho Mtakatifu. 12 Ndugu atamsaliti ndugu yakeauawe; baba atamsaliti mwanae; watoto watawashambu-lia wazazi wao na kuwaua. 13Watu wote watawachukienininyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumiliampaka mwisho ndiye atakayeokolewa. 14 “MtakapoonaChukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake,(msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu waliokoYudea wakimbilie milimani. 15 Mtu aliye juu ya paa lanyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukuakitu. 16 Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazilake. 17 Ole wao waja wazito na wanaonyonyesha siku

Page 36: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 13:18 36 MARKO MTAKATIFU 13:35hizo! 18 Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati zabaridi. 19 Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayohaijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpakaleo, wala haitatokea tena. 20 Kama Bwana asingepunguzasiku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakinikwa ajili yawateulewake, Bwana amezipunguza siku hizo.21 “Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa!au Yupo pale! msimsadiki. 22 Maana watatokea kinaKristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya isharana maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kamaikiwezekana. 23 Lakini ninyi jihadharini. Mimi nime-waambieni mambo yote kabla hayajatokea. 24 “Basi, sikuhizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hau-taangaza. 25 Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvuza mbingu zitatikiswa. 26 Hapo watamwona Mwana waMtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.27Kisha atawatuma malaika wake; atawakusanya wateulewake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wadunia mpaka mwisho wa mbingu. 28 “Kwa mtini jifunzenimfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa lainina kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangaziumekaribia. 29Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambohayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yukokaribu sana. 30 Nawaambieni kweli, kizazi hiki haki-tapita kabla ya mambo hayo yote kutukia. 31 Mbingu nadunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.32 “Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakujalini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba pekeyake ndiye ajuaye. 33 Muwe waangalifu na kesheni,maana hamjui wakati huo utafika lini. 34 Itakuwa kamamtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachiawatumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake;akamwambia mlinzi wa mlango awe macho. 35 Kesheni,

Page 37: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 13:36 37 MARKO MTAKATIFU 14:12basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini;huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asub-uhi. 36 Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.37Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote: Kesheni!”

141 Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na

ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na wal-imu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesunguvuni kwa hila wamuue. 2 Lakini walisema, “Tusimtienguvuni wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya gha-sia.” 3 Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni,Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula, mama mmojaaliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya nardosafi ya thamani kubwa alikuja, akaivunja hiyo chupa,akammiminia Yesu marashi hayo kichwani. 4 Baadhi yawatu waliokuwa hapo walikasirika wakajisemea, “Kwanini kupoteza ovyo marashi haya? 5Yangaliweza kuuzwakwa fedha kiasi cha denari mia tatu, wakapewa mask-ini!” Wakamkemea huyo mama. 6 Lakini Yesu akawaam-bia, “Mwacheni; kwa nini mnamsumbua? Ameniten-dea jambo jema. 7 Maskini mnao daima pamoja nanyi;mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaopenda. Lakinimimi sitakuwapo pamoja nanyi daima. 8 Yeye ame-fanya alivyoweza; ameupaka mwili wangu marashi ku-utayarisha kwa maziko. 9 Nawaambieni kweli, popoteulimwenguni Habari Njema itakapohubiriwa, kitendohiki alichofanya kitatajwa kwa ajili ya kumkumbuka.”10 Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na waw-ili, alienda kwa makuhani wakuu ili kumsaliti Yesu.11 Makuhani wakuu waliposikia habari hiyo, walifu-rahi, wakaahidi kumpa fedha. Basi, Yuda akaanzakutafuta nafasi ya kumsaliti Yesu. 12 Siku ya kwanza

Page 38: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 14:13 38 MARKO MTAKATIFU 14:25ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wakati am-bapo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunziwake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamuya Pasaka?” 13 Basi Yesu akawatuma wawili wa wana-funzi wake akiwaambia, “Nendeni mjini, nanyi mtaku-tana na mtu anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni14 mpaka katika nyumba atakayoingia, mkamwambiemwenye nyumba, Mwalimu anasema: wapi chumbachangu ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunziwangu? 15 Naye atawaonyesha chumba kikubwa gho-rofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalienihumo.” 16 Wanafunzi wakaondoka, wakaenda mjini,wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa ame-waambia. Wakaandaa karamu ya Pasaka. 17 Ilipokuwajioni, Yesu alifika pamoja na wanafunzi wake kumi nawawili. 18 Walipokuwa mezani wakila, Yesu alisema,“Kweli nawaambieni, mmoja wenu anayekula pamojanami, atanisaliti.” 19 Hapo wanafunzi wake wakaanzakuhuzunika, wakamwuliza mmojammoja, “Je, ni mimi?”20 Yesu akawaambia, “Ni mmoja wenu ninyi kumi nawawili, anayechovya mkate pamoja nami katika bakuli.21Kweli Mwana wa Mtu anakwenda zake kama MaandikoMatakatifu yanavyosema juu yake; lakini, ole wake mtuyule anayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhalikwa mtu huyo kama hangalizaliwa!” 22 Walipokuwawanakula, Yesu alitwaa mkate, akashukuru, akaumegana kuwapa wanafunzi wake akisema, “Twaeni; huu nimwili wangu.” 23 Kisha akatwaa kikombe, akamshukuruMungu, akawapa; nao wote wakanywa katika kikombe hi-cho. 24 Akawaambia, “Hii ni damu yangu inayothibitishaagano la Mungu, damu inayomwagwa kwa ajili ya watuwengi. 25 Kweli nawaambieni, sitakunywa tena divai yazabibu mpaka siku ile nitakapoinywa upya katika Ufalme

Page 39: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 14:26 39 MARKO MTAKATIFU 14:43wa Mungu.” 26 Kisha wakaimba wimbo, wakaondoka,wakaenda katika mlima wa Mizeituni. 27 Yesu akawaam-bia wanafunzi wake, “Ninyi nyote mtakuwa na mashakanami; maana Maandiko Matakatifu yasema: Nitampigamchungaji nao kondoo watatawanyika. 28 Lakini nik-isha fufuka, nitawatangulieni kule Galilaya.” 29 Petroakamwambia “Hata kama wote watakuwa na mashakanawe na kukuacha, mimi sitakukana kamwe!” 30 Yesuakamwambia, “Kweli nakwambia, usiku huu, kabla jogoohajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” 31 LakiniPetro akasisitiza, “Hata kama ni lazima nife pamoja nawe,sitakuacha kamwe.” Wanafunzi wote pia wakasema vivyohivyo. 32 Basi, wakafika katika bustani iitwayo Gethse-mane. Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapawakati mimi nasali.” 33Kisha akawachukua Petro, Yakobona Yohane; akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.34 Akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyoni hata karibukufa. Kaeni hapa mkeshe.” 35 Akaenda mbele kidogo,akajitupa chini kifudifudi, akasali kwamba, kama in-gewezekana, asiipitie saa hiyo ya mateso. 36 Akasema,“Baba yangu, kwako mambo yote yanawezekana. Union-dolee kikombe hiki; lakini isiwe kama nitakavyo mimi,bali utakavyo wewe.” 37 Kisha akarudi kwa wanafunziwale watatu, akawakuta wamelala. Basi, akamwulizaPetro, “Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hata saamoja?” 38 Kisha akawaambia, “Kesheni na kusali ili msijemkaingia katika majaribu. Roho i radhi, lakini mwili nidhaifu.” 39Akaenda kusali tena akirudiamaneno yaleyale.40 Kisha akarudi tena, akawakuta wamelala. Macho yaoyalikuwa yamebanwa na usingizi. Hawakujua la kumjibu.41 Alipowajia mara ya tatu aliwaambia, “Mnalala bado nakupumzika? Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana waMtu anakabidhiwa kwa watu waovu. 42Amkeni, twendenizetu. Tazameni, yule atakayenisaliti amekaribia.” 43Yesu

Page 40: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 14:44 40 MARKO MTAKATIFU 14:60alipokuwa bado anasema, Yuda, mmoja wa wale kumina wawili, akafika pamoja na umati wa watu wenye ma-panga na marungu. Watu hao walikuwa wametumwa namakuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee. 44MsalitiYuda alikuwa amewapa ishara: “Yule nitakayembusundiye; mkamateni, mkampeleke chini ya ulinzi.” 45 Yudaalipofika tu, alimwendea Yesu moja kwa moja, akasema,“Mwalimu!” Kisha akambusu. 46Basi, haowatuwakamka-mata Yesu, wakamtia nguvuni. 47 Mmoja wa walewaliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesu akau-chomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa KuhaniMkuu, akamkata sikio. 48Yesu akawaambia, “Je, mmekujanamapanga namarungu kunikamata kana kwambamimini mnyang'anyi? 49 Kila siku nilikuwa pamoja nanyinikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini sasalazimaMaandikoMatakatifu yatimie.” 50Hapo wanafunziwote wakamwacha, wakakimbia. 51 Kulikuwa na kijanammoja aliyekuwa anamfuata Yesu akiwa amevaa shuka.Nao wakajaribu kumkamata. 52 Lakini yeye akaponyoka,akaiachilia ile shuka, akakimbia uchi. 53 Basi, wakam-peleka Yesu kwa Kuhani Mkuu ambapo makuhani wakuuwote, wazee na walimu wa Sheria walikuwa wameku-tanika. 54 Petro alimfuata Yesu kwa mbali, akaingiandani ya ya wa Kuhani Mkuu, akaketi pamoja na wal-inzi akiota moto. 55 Makuhani wakuu na Baraza lotewakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu wapate kumwua,lakini hawakupata. 56 Watu wengi walitoa ushahidi wauongo juu ya Yesu, lakini ushahidi wao haukupatana.57Kishawenginewalisimama, wakatoa ushahidiwauongowakisema: 58 “Tulimsikia mtu huyu akisema, NitaliharibuHekalu hili lililojengwa kwa mikono, na kwa siku tatunitajenga lingine lisilojengwa kwa mikono.” 59 Lakinihata hivyo, ushahidi wao haukupatana. 60 Basi, KuhaniMkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, “Je,

Page 41: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 14:61 41 MARKO MTAKATIFU 15:1hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidiyako?” 61 Lakini yeye akakaa kimya; hakusema hataneno moja. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, “Je, wewendiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?” 62 Yesuakajibu, “Naam, mimi ndiye. Tena, mtamwonaMwanawaMtu amekaa upande wa kulia wa Mwenyezi, akija katikamawingu ya mbinguni.” 63 Hapo Kuhani Mkuu akararuajoho lake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi?64 Mmesikia kufuru yake! Ninyi mwaonaje?” Wotewakaamua kwamba anastahili kuuawa. 65Basi, baadhi yaowakaanza kumtemeamate, wakamfunika uso, wakampigana kumwambia, “Bashiri ni nani aliyekupiga!” Hatawatumishi wakamchukua, wakampiga makofi. 66 Petroalipokuwa bado chini ukumbini, mmoja wa wajakazi wakuhani Mkuu alikuja. 67 Alipomwona Petro akiota moto,alimtazama, akamwambia, “Hata wewe ulikuwa pamojana Yesu Mnazareti.” 68 Lakini Petro akakana, “Sijui, walasielewi unayosema!” Kisha Petro akaondoka, akaenda njeuani. Hapo jogoo akawika. 69 Yule mjakazi alipomwonatena Petro, akaanza tena kuwaambia watu waliokuwawamesimama hapo, “Mtu huyu ni mmoja wao.” 70 Petroakakana tena. Baadaye kidogo, watu waliokuwa wames-imama hapo wakamwambia Petro, “Hakika wewe nimmoja wao, maana wewe ni Mgalilaya.” 71 LakiniPetro akaanza kulaani na kuapa akisema, “Mimi simjuimtu huyu mnayesema habari zake.” 72 Hapo jogooakawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbuka jinsi Yesualivyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika marambili, utanikana mara tatu.” Petro akabubujika machozi.

151Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri

pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote,

Page 42: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 15:2 42 MARKO MTAKATIFU 15:20wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhikwa Pilato. 2 Pilato akamwuliza Yesu, “Je, wewe nimfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe ume-sema.” 3 Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambomengi. 4 Pilato akamwuliza tena Yesu, “Je, hujibu neno?Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako.” 5 LakiniYesu hakujibu neno, hata pilato akashangaa. 6 Kilawakati wa sikukuu ya Pasaka, Pilato alikuwa na desturiya kuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka. 7 Basi,kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwaamefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababishauasi na mauaji. 8 Watu wengi wakamwendea Pilatowakamwomba awafanyie kama kawaida yake. 9 Pilatoakawauliza, “Je, mwataka niwafungulieni Mfalme waWayahudi?” 10 Alisema hivyo kwa sababu alijua wazikwamba makuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwake kwasababu ya wivu. 11 Lakini makuhani wakuu wakawa-chochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba.12 Pilato akawauliza tena, “Basi, sasa mwataka nifanyenini na mtu huyu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?”13 Watu wote wakapaaza sauti tena: “Msulubishe!”14 Lakini Pilato akawauliza, “Kwa nini! Amefanya kosagani?” Lakini wao wakazidi kupaaza sauti, “Msulubishe!”15 Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi,akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesuapigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe. 16 Kisha askariwalimpeleka Yesu ndani ukumbini, katika ikulu, wakaku-sanya kikosi kizima cha askari. 17Wakamvika vazi la rangiya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamwekeakichwani. 18 Wakaanza kumsalimu, “Shikamoo Mfalmewa Wayahudi!” 19 Wakampiga kichwani kwa mwanzi,wakamtemea mate; wakampigia magoti na kumsuju-dia. 20 Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho,

Page 43: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 15:21 43 MARKO MTAKATIFU 15:36wakamvika nguo zake, kishawakampeleka kumsulubisha.21 Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja ait-waye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa babawa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitokashambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalabawa Yesu. 22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahalipalipoitwa Golgotha, maana yake, “Mahali pa Fuvu laKichwa.” 23 Wakampa divai iliyochanganywa na mane-mane, lakini yeye akaikataa. 24 Basi, wakamsulubisha,wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura waamuenani angepata nini. 25 Ilikuwa saa tatu asubuhi walipom-sulubisha. 26 Na mshtaka wake ulikuwa umeandikwa:“Mfalme wa Wayahudi.” 27 Pamoja naye waliwasulu-bisha wanyang'anyi wawili, mmoja upande wake wa ku-lia na mwingine upande wake wa kushoto. 28 Hapoyakatimia Maandiko Matakatifu yanayosema, “Aliwekwakundi moja na waovu.” 29 Watu waliokuwa wanapitamahali hapo walimtukana, wakitikisa vichwa vyao nakusema, “Aha! Wewe mwenye kuvunja Hekalu na kuli-jenga kwa siku tatu! 30 Sasa, shuka msalabani ujiokoemwenyewe!” 31Nao makuhani wakuu pamoja na walimuwa Sheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoa wengine,lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! 32 Eti yeye ni Kristo,Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuonena kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja nayewalimtukana. 33Tangu saa sitamchanampaka saa tisa ku-likuwa giza nchini kote. 34 Saa tisa alasiri Yesu akalia kwasauti kubwa, “Eloi, Eloi, lema sabakthani?” Maana yake,“Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”35 Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hivyo,walisema, “Sikiliza! Anamwita Eliya!” 36 Mtu mmojaakakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juuya mwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuone kama

Page 44: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 15:37 44 MARKO MTAKATIFU 16:2Eliya atakuja kumteremsha msalabani!” 37Yesu akapaazasauti kubwa, akakata roho. 38 Basi, pazia la Hekalu lika-pasuka vipande viwili toka juu mpaka chini. 39 Jemadarimmoja aliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsiYesu alivyolia kwa sauti na kukata roho, akasema, “Kwelimtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!” 40 Walikuwakopia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwaoakiwaMaria tokamjiwaMagdala, Salome, naMariamamawa kina Yakobo mdogo na Yose. 41 Hawa walimfuataYesu alipokuwa Galilaya na kumtumikia. Kulikuwa nawanawake wengine wengi waliokuja Yerusalemu pamojanaye. 42 Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyoilikuwa siku ya Maandalio, yaani siku inayotanguliaSabato. 43 Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya,mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye piaalikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi,alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili waYesu. 44 Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu alikuwaamekwisha kufa. Basi, akamwita jemadari, akamwulizakama Yesu alikuwa amekufa kitambo. 45 Pilato alipoari-fiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwishakufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake. 46HapoYosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huomwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburilililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirishajiwe kubwa mbele ya mlango. 47Nao Maria Magdalene naMaria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa.

161 Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome

na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato iliwakaupake mwili wa Yesu. 2Basi, alfajiri na mapema sikuya Jumapili, jua lilipoanza kuchomoza, walienda kaburini.

Page 45: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 16:3 45 MARKO MTAKATIFU 16:183Nao wakawa wanaambiana, “Nani atakayetuondolea lilejiwe mlangoni mwa kaburi?” 4 Lakini walipotazama,waliona jiwe limekwisha ondolewa. (Nalo lilikuwakubwa mno.) 5 Walipoingia kaburini, walimwona kijanammoja aliyevaa vazi jeupe, ameketi upande wa kulia;wakashangaa sana. 6 Lakini huyo kijana akawaambia,“Msishangae. Mnamtafuta Yesu wa Nazareti aliyesu-lubiwa. Amefufuka, hayumo hapa. Tazameni mahaliwalipokuwa wamemlaza. 7 Nendeni mkawaambie wana-funzi wake pamoja na Petro ya kwamba anawatangulienikule Galilaya. Huko mtamwona kama alivyowaambi-eni.” 8 Basi, wakatoka pale kaburini mbio, maanawalitetemeka kwa hofu na kushangaa. Hawakumwambiamtu yeyote kitu, kwa sababu waliogopa mno. 9 Yesualipofufuka mapema Jumapili, alijionyesha kwanza kwaMaria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa peposaba. 10 Maria Magdalene akaenda, akawajulisha walewaliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwawanaomboleza na kulia. 11 Lakini waliposikia ya kwambaYesu yu hai na kwamba Maria Magdalene amemwona,hawakuamini. 12 Baadaye Yesu aliwatokea wanafunziwawili akiwa na sura nyingine. Wanafunzi hao walikuwawanakwenda shambani. 13Nao pia wakaenda wakawaam-bia wenzao. Hata hivyo hawakuamini. 14 Mwishowe,Yesu aliwatokea wanafunzi kumi na mmoja walipokuwapamoja mezani. Akawakemea sana kwa sababu ya ku-toamini kwao na ukaidi wao, maana hawakuwaaminiwale waliokuwa wamemwona baada ya kufufuka. 15 Basi,akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiriHabari Njema kwa kila mtu. 16 Anayeamini na kubatizwaataokolewa; asiyeamini atahukumiwa. 17 Na ishara hizizitaandamana na wale wanaoamini: kwa jina langu wata-toa pepo na watasema kwa lugha mpya. 18 Wakishika

Page 46: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

MARKO MTAKATIFU 16:19 46 MARKO MTAKATIFU 16:20nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hak-itawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao wat-apona.” 19 Basi, Bwana Yesu alipokwisha sema nao,akachukuliwa mbinguni, akaketi upande wa kulia waMungu. 20 Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali.Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbehuo kwa ishara zilizoandamana nao.

Page 47: INJILIKAMAALIVYOIANDIKA MARKOMTAKATIFU · tuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!” 25 Yesu akamkemea, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu

47Biblia Takatifu

Portions of the New Testament in the Swahili Language of Kenya,Mozambique, Somalia, and Tanzania, translation by Dr. Johann

Ludvig Krapf completed in 1850Public DomainLanguage: Kiswahili (Swahili)Dialect: KimvitaTranslation by: Dr. Johann Ludvig Krapf

2014-08-25PDF generated using Haiola and XeLaTeX on 11 Jan 2020 from source files dated 30 Dec201962071dc0-70e6-5b86-b569-c1b45e7771bd