ifahamu biblia katika ubora wake. - wordpress.com · biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na...

186
1 IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. Na Ngowi Dennis. "*Natazamia Mbingu mpya na Nchi mpya*

Upload: others

Post on 30-Dec-2019

272 views

Category:

Documents


23 download

TRANSCRIPT

Page 1: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

1

IFAHAMU

BIBLIA

KATIKA

UBORA

WAKE.

Na Ngowi Dennis.

"*Natazamia Mbingu mpya na Nchi mpya*”

Page 2: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

2

YALIYOMO:

SHUKRANI: ............................................................................................................................................................ 5

UTANGULIZI KWA WASOMAJI WA BIBLIA! .............................................................................................. 6

AGANO LA KALE .............................................................................................................................................. 7

AGANO JIPYA .................................................................................................................................................... 8

USOMAJI WA BIBLIA NA UCHAMBUZI WA MAANDIKO. ........................................................................ 9

HISTORIA YA BIBLIA KATIKA KUTAFSIRIWA KATIKA LUGHA MBALIMBALI! ............................. 11

VITABU VYA APOKRIFA. ...................................................................................................................................... 14

MUHTASARI WA KITABU CHA MWANZO. ............................................................................................... 19

MUHTASARI WA KITABU CHA KUTOKA .................................................................................................. 23

MUHTASARI WA KITABU CHA MAMBO YA WALAWI! ......................................................................... 25

MUHTASARI WA KITABU CHA HESABU: .................................................................................................. 27

MUHTASARI WA KUMBUKUMBU LA TORATI......................................................................................... 29

MUHTASARI WA KITABU CHA YOSHUA. ................................................................................................. 31

MUHTASARI WA KITABU CHA WAAMUZI. .............................................................................................. 33

MUHTASARI WA KITABU CHA RUTHU. .................................................................................................... 37

USHUHUDA WA RUTHU KWA KANISA LA LEO! ................................................................................................... 38

MUHTASARI WA KITABU CHA KWANZA CHA SAMWELI. ................................................................... 39

MUHTASARI WA KITABU CHA PILI CHA SAMWELI. ............................................................................. 41

DAUDI MTU SHUJAA NA MASHUJAA WAKE! ...................................................................................................... 43

MUHTASARI WA KITABU CHA WAFALME. ............................................................................................. 46

HABARI ZA MFALME SULEMANI! ........................................................................................................................ 48

UFALME WA ISRAELI. .......................................................................................................................................... 51

UFALME WA YUDA. ............................................................................................................................................. 55

MANATI YA MFALME UZIA.................................................................................................................................. 59

MAOVU YA MFALME MANASE. .......................................................................................................................... 61

HEKALU. .............................................................................................................................................................. 63

MUHTASARI WA KITABU PILI CHA WAFALME. ..................................................................................... 65

TAIFA (DOLA) LA ASHURU.(KINGDOM OF ASSYRIA.) .......................................................................................... 67

MUHTASARI KITABU CHA MAMBO YA NYAKATI. ................................................................................ 69

MUHTASARI WA KITABU CHA MAMBO YA NYAKATI WA PILI. ........................................................ 72

MUHTASARI KITABU CHA EZRA! .............................................................................................................. 74

Page 3: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

3

MUHTASARI WA KITABU CHA NEHEMIA! ............................................................................................... 76

MUHTASARI WA KITABU CHA ESTA ......................................................................................................... 78

MUHTASARI WA KITABU CHA AYUBU. ................................................................................................... 81

MUHTASARI KITABU CHA ZABURI! .......................................................................................................... 84

MUHTASARI: KITABU CHA MITHALI! ....................................................................................................... 87

MUHTASARI: KITABU CHA MHUBIRI!....................................................................................................... 89

MUHTASARI WA KITABU CHA WIMBO ULIO BORA .............................................................................. 91

KATIKA UBORA WAKE! ................................................................................................................................ 91

MUHTASARI KITABU CHA ISAYA! ............................................................................................................. 94

MUHTASARI KITABU CHA YEREMIA ........................................................................................................ 96

MUHTASARI, KITABU CHA MAOMBOLEZO. ............................................................................................ 98

MUHTASARI WA KITABU CHA EZEKIELI. .............................................................................................. 100

MUHTASARI WA KITABU CHA DANIELI. ............................................................................................... 102

MUHTASARI KITABU CHA HOSEA! .......................................................................................................... 104

MUHTASARI WA KITABU CHA YOELI! ................................................................................................... 106

MUHTASARI WA KITABU CHA AMOSI. ................................................................................................... 107

MUHTASARI WA KITABU CHA OBADIA! ................................................................................................ 108

MUHTASARI KITABU CHA YONA! ........................................................................................................... 109

MUHTASARI KITABU CHA MIKA! ............................................................................................................ 110

MUHTASARI WA KITABU CHA NAHUMU. .............................................................................................. 111

MUHTASARI WA KITABU CHA HABAKUKI. .......................................................................................... 112

MUHTASARI WA KITABU CHA SEFANIA. ............................................................................................... 113

MUHTASARI WA KITABU CHA HAGAI. ................................................................................................... 114

MUHTASARI WA KITABU CHA ZEKARIA! .............................................................................................. 116

MUHTASARI WA KITABU CHA MALAKI. ................................................................................................ 118

KATI YA MALAKI NA MATHAYO NINI KILIENDELEA. ....................................................................... 120

MUHTASARI WA KITABU CHA MATHAYO. ........................................................................................... 125

MUHTASARI WA KITABU CHA INJILI YA MARKO. .............................................................................. 127

MUHTASARI WA KITABU CHA LUKA...................................................................................................... 130

MUHTASARI WA KITABU CHA INJILI YA YOHANA! ........................................................................... 132

MUHTASARI WA KITABU CHA MATENDO YA MITUME!.................................................................... 135

MUHTSARI WA KITABU CHA WARUMI. ................................................................................................. 137

Page 4: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

4

MUHTASARI WA KITABU CHA 1.WAKORINTHO .................................................................................. 138

MUHTASARI WA WAKORINTHO 2:........................................................................................................... 140

PAULO WA TARSO!: .......................................................................................................................................... 142

MUHTASARI WA WARAKA WA WAGALATIA. ...................................................................................... 144

MUHTASARI WA KITABU CHA WAEFESO. ............................................................................................. 145

MUHTASARI WA WARAKA KWA WAFILIPI. .......................................................................................... 147

MUHTASARI WA WARAKA WA WAKOLOSAI. ...................................................................................... 148

MUHTASARI WA WARAKA KWA WATHESALONIKE 1: ...................................................................... 149

MUHTASARI WA WARAKA 2 WATHESALONIKE! ................................................................................. 150

MUHTASARI WA TIMOTHEO WA KWANZA! .......................................................................................... 151

MUHTASARI WA KITABU CHA 2 TIMOTHEO!........................................................................................ 153

MUHTASARI WA KITABU CHA TITO! ...................................................................................................... 154

MUHTASARI WA WARAKA KWA WAEBRANIA. ................................................................................... 155

MUHTASARI WA WARAKA WA YAKOBO. ............................................................................................. 157

MUHTASARI WA WARAKA WA FILEMONI ............................................................................................ 159

MUHTASARI WA WARAKA WA KWANZA WA YOHANA! ................................................................... 161

MUHTASARI WA WARAKA WA PILI WA YOHANA!. ............................................................................ 163

MUHTASARI WA WARAKA WA TATU WA YOHANA!. ........................................................................ 164

MUHTASARI WA WARAKA WA PETRO WA KWANZA! ...................................................................... 165

MUHTASARI WA WARAKA WA PETRO WA PILI!. ................................................................................. 167

MUHTASARI WA WARAKA WA YUDA. ................................................................................................... 169

MUHTASARI WA KITABU CHA UFUNUO WA YOHANA! ..................................................................... 171

RATIBA YA KUISOMA BIBLIA. .................................................................................................................. 174

VITABU REJEA! ............................................................................................................................................. 186

Page 5: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

5

SHUKRANI:

Page 6: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

6

UTANGULIZI KWA WASOMAJI WA BIBLIA!

Biblia ina mweleza Mungu pande zote kwa wanadamu. Biblia ni ufunuo wa Mungu ulioandikwa

kuhusu mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Biblia ni kitabu zaidi ya, kuliko kitabu kingine

chochote. Biblia ni kitabu cha ajabu!

Ni kitabu cha Vitabu,kitabu kilichovuviwa,ni kitakatifu kwa sababu kina maneno ya mwandishi

mkuu ambae ni mtakatifu.Ni kitakatifu kwa sababu mjumbe wake ni mtakatifu,maandiko yake ni

matakatifu! Ni kitakatifu kwa sababu maudhui yake ni kutufanya kuwa watakatifu.

Biblia ina vitabu 66 vilivyo­andikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani

kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi ya vizazi 40, katika mazingira tofauti,wakati

tofauti,nyakati tofauti,ktk mabara 3(asia,ulaya na Afrika) ktk lugha 3( kiebrania,kiaramu na

kiyunani)Karibu Agano la Kale lote liliandikwa kwa lugha ya Kiebrania isipokuwa mafungu

machache kwenye kitabu cha Danieli yaliyoandikwa kwa lugha ya Kiaramu. Agano Jipya

limeandikwa kwa lugha ya Kigiriki\kiyunani.

Sasa, mwanzoni mwa mwaka 2007; Biblia nzima tayari imekwi­shatafsiriwa kwa lugha tofauti

yaani. 429 Na Agano Jipya au Agano la Kale tu zimekwishatafsiriwa kwa lugha tofauti 1144. Na

Biblia nzima tayari imekwishatafsiriwa kwa lugha za Afrika mia moja sitini. (160)

Steven Lagton (1228) Aliigawanya Biblia ktk sura. R Nathan (1488) aliigawanya agano la kale

ktk aya na Robert Stephanus(1551) aliigawaya Agano jipya katika aya. Biblia ilikuwa kitabu cha

kwanza kuchapishwa na machine mwaka 1455 na Johann Gutenberg

Vitabu vingine huchakaa lakini kitabu hiki Biblia hupita juu ya karne zote. Vitabu vingine

lazima vibadilishwe kufuatana na umri. Bali wazee kwa vijana huipenda Biblia. Vitabu vingi ni

kwa ajili ya sehemu ndogo ya watu na huwavutia watu wa lugha ile tu, lakini kitabu hiki Biblia,

sivyo.

Katika Biblia kuna vitabu 66. Katika Agano la Kale kuna vitabu 39 na katika Agano Jipya 27.

Katika Biblia kuna sura 1,189; Agano la Kale kuna sura 929.Na Agano Jipya 260.

Katika Biblia ya kiswahili kuna mistari 31,102. Ambazo ni mistari 23,145 katika Agano la Kale.

Na mistari 7,957 katika Agano Jipya.

Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2 Petro 1:21).

Page 7: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

7

AGANO LA KALE

Kuna vitabu 5 vya Sheria( Pentatuki);

Mwanzo, Kutoka, Mambo ya walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati.

Vitabu 12 vya historia.

Yoshua,Waamuzi,Ruthu,I Samweli, II Samweli,I Wafalme,II Wafalme,I Mambo ya Nyakati,II

Mambo ya Nyakati, Ezra,Nehemia na Esta.

Vitabu 5 vya mashairi;

Ayubu,Zaburi,Mithali,Mhubiri na wimbo ulio bora!.

Vitabu 17 vya unabii

Manabii wakubwa 5:

Isaya,Yeremia,Maombolezo,Ezekieli na Danieli.

Manabii wadogo 12;

Hosea,Yoeli,Amosi,Obadia,Yona,Mika,Nahumu,Habakuki,Sefania,Hagai,Zekaria na Malaki

Kwa maelezo zaidi ni kuwa;Katika Agano la Kale.

Kitabu cha katikati ya Biblia : Mithali; Sura ya katikati : Ayubu 29; Aya ya katikati : II Mambo

ya Nyakati 20:17; Aya ndefu zaidi : Esta 8:9; Aya ya katikati katika Biblia nzima : Zaburi 118:8;

Sura ndefu zaidi : Zaburi 119; Sura fupi na ya katikati mwa Biblia : Zaburi 117.

Tunaweza kuwaza kwamba Agano la Kale ni kama msingi. Na Agano Jipya ni kama jengo juu

yake. Msingi haufai kama jengo halijengwi juu yake. Jengo haliwezekani kama msingi haupo.

Kwa hiyo Agano la Kale na Agano Jipya hutegemeana.

Kama unasoma Agano la Kale tu au Agano Jipya tu, ni sawa na kuruka kwa mguu mmoja.

Agano la Kale ni kama mguu mmoja na Agano Jipya mguu mwingine. Ikiwa unatembea kwa

miguu miwili, basi unakwenda vizuri.

Page 8: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

8

AGANO JIPYA

Vitabu : 27; Sura :260; Aya : 7,957 ; Waandishi : 8 ; Kitabu cha katikati : 2Thesalonike

Sura ya katikati: Warumi 13: Aya ya katikati : Matendo 17:17: Aya fupi?

Kitabu kirefu : Luka; Kitabu kifupi : 2Yohana.

Kitabu vya mwanzoni kabisa kuandikwa NI II Thesalonike,Yakobo,Wagalatia, cha mwisho NI

ufunuo Wa Yohana.

Vitabu vya Agano Jipya tunaweza kuvipanga hivi: Injili

Vitabu 4 – MATHAYO, MARKO, LUKA na YOHANA.

Historia – kitabu 1, MATENDO YA MITUME.

Nyaraka 21.

Paulo aliandika nyaraka 13 ama 14,

Warumi,I Korintho,II Korintho,Wagalatia,Waefeso,Wafilipi,Wakolosai,I Thesalonike,II

Thesalonike,I Timotheo,II Timotheo,Tito,Filemoni ( Waebrania);

Nyaraka nyingine 7; Yakobo, I Petro,II Petro,I Yohana,II Yohana,III Yohana, Yuda.

Hatujui, ni nani hasa aliandika waraka wa WAEBRANIA (pengine ni Paulo),

Kitabu cha unabii – kimoja – UFUNUO. .

ANGALIZO:

Biblia ya kiyahudi INA vitabu 51 tu! Agano la kale 24 na Jipya 27. Kwanini.?, @vitabu vya

manabii wadogo12 vimekusanywa na kuwa kitabu kimoja,vivyo hivyo kwa Ezra-

Nehemia,Mambo ya Nyakati,wafalme na Samweli zote mbili,

Biblia ya Roman Catholic(Vulgate) INA vitabu 72 kutokea vitabu 80 vya awali,vitabu 46 Agano

la kale na 27 agano jipya..hii NI kutokana na kuvikubali vitabu vya apokrifa;

Tobithi,Judithi,Hekima ya Yoshua bin Sira,Baruku,Makabayo Wa 1&2, na hekima za Sulemani

pia Danieli sura 13&14,Esta sura za mwishoni.

Hivyo maandiko katika Biblia zanaweza kuwa sawa kasoro itaonekana kwenye vitabu nyongeza

na sura nyongeza!

Page 9: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

9

USOMAJI WA BIBLIA NA UCHAMBUZI WA MAANDIKO.

NI mengi yaliyoandikwa duniani,mamilioni ya vitabu,magazeti,majarida, na masomo mbalimbali

yahusuyo mambo mbalimbali katika dunia yetu. Biblia NI Neno la Mungu lililovuviwa na kuleta

tofauti kubwa kati ya kitabu Biblia na vitabu vingine vyote. Ndani ya kitabu hiki Biblia kuna

maneno makuu mawili yanayo eleza moja ya sifa kuu ya Biblia yaani Neno la Mungu.

1. Neno la kiyunani " logos"

2. Neno la kiyunani " Rhema"

Maneno haya hutumika sana katika usomaji na kuelewa uzito Wa andiko,uvuvio wake na ukuu

wake. Neno " logos" humaanisha yaliyoandikwa! yaani kumbukumbu fulani juu ya kila

unachotaka kujua,habari zake zilisha andikwa. mfano; Yesu akamjibu shetani " imeandikwa,

MTU hataishi kwa mkate tu!( logos).Neno la pili " rhema" humaanisha lililokusudiwa,vuviwa

kwa majira na kwa wakati huu! mfano; "Bali kila neno litokalo kinywani mwa BWANA!( rhema)

ndio maana tangu enzi na Torati hadi na leo,Biblia imekuwa ikisomwa na Neno likihubiriwa ama

kufundishwa lakini ujumbe wake haujaisha,hauja chakaa,hajapitwa na wakati,unawafaa watu

wote,maususi kwa kila jambo,tukio na kuwa na nguvu ya kuathiri jamii,MTU na taifa

unaposikilizwa!

Wahubiri wakubwa waliowahi kuhubiri sana, mfano; Billy Graham,Catherine Kuhlman,

Bonke,Myles,Benny,Maxwell nk, hata ikatokea wakakutembea Leo nyumbani kwako,

utashangaa atasoma Mathayo ama Hosea sura na aya/mistari ile ile usomayo kila siku!

Nitakushangaa sana ikiwa kwa kujiona unajua,unaelewa sana maandiko,umekomaa kiroho,wewe

NI mshirika Wa Siku nyingi kanisani; hutaki kuonywa,kusahihishwa,kupewa ushauri eti kwa

sababu hilo andiko wanalokusomea unalijua,'nilijua tu utanisomea hilo andiko' (logos). Hii NI

sawa na kusema umefikia level ya kuipita Biblia hivyo hakuna jipya usilolijua!

" Neno la Mungu li hai...." (rhema)

Uchambuzi Wa Biblia/maandiko!

Shule za sekondari wanafundisha juu ya tahakiki,yaani uchambuzi Wa vitabu vya

Riwaya,Tamthilia na ushairi. Kwa namna kwamba mwanafunzi hupaswa kukisoma kitabu

fulani,kisha akakielezea kwa kuchambua NANI mhusika mkuu,hadhira yake,maudhui

yake,dhima kuu ya kuu,mada mbalimbali Ndani yake nk. Hivyo NI sawa na kueleza

alivyokielewa kwa muhtasari kitabu hicho!Kadhalika kwa Biblia njia kama hii unaweza

kuitumia kuielewa na kuvielezea vitabu vya Biblia!

Kuoanisha na kuonesha nini wazo kuu katika kitabu cha mwandishi,sura hii na nyingine katika

Biblia. Kutafsiri/kufasiri maandiko hakuji kwa namna tunavyo taka sisi bali atakavyo Mungu!

Epuka kujilisha/kuwalisha watu tango pori!

Page 10: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

10

Kuna kanuni zenye kubeba funzo kuu( Doctrine) za maandiko na kuna kanuni za mahubiri ya

kawaida Mfano: mafunzo juu ya utakatifu huhusisha toba ya kweli,kuonya juu ya dhambi! nk.

Kwa upande wa mahubiri juu ya mafanikio! Huusisha mambo kama utoaji, panda na uvune

Baraka yako. Hivyo lazima mkazo uwe kwenye kanuni kuu za mafundisho ili MTU/watu

waelimike sio kumsisimua. Biblia Neno la Mungu lina kina,urefu,upana na kimo ambacho

mpaka sasa bado hatujakifikia pengine hata robo yake!

Soma sana, soma tena,tafakari,chambua,fafanua na ishi(direct application) ya

ulichojifunza"Nataka nimjue Yesu,na nizidi kumfahamu,

Mapenzi yake nifanye Yale yanayompendeza!"

BWANA MUNGU NA AKUBARIKI KWA KUDHAMIRIA

KWA MAKUSUDI KUMFAHAMU YEYE!!!Amen.

Page 11: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

11

HISTORIA YA BIBLIA KATIKA KUTAFSIRIWA KATIKA LUGHA

MBALIMBALI! "Gombo la chuo" NI neno lililotumika sana katika Agano la kale,likimaanisha maadiko

matakatifu.Sehemu ama jumla ya maandiko ya nabii Fulani ama torati! Huitwa chuo,."Chuo" ni

neno lingine lililokuwa likimaanisha maandiko yaliyokuwa yanaandikwa katika ngozi laini,na

kusokotwa kwa kuviringisha wakati unasoma ama unafunga ili kuhifadhi maandiko hayo!.

Mfano; chuo cha nabii Isaya. Biblia NI mkusanyiko Wa chuo mbalimbali,yaani

torati,manabii,Injili, na nyaraka. Hivyo wakati mwingine wako waliozoea kusema Gombo la

chuo akimaanisha kitu kilekile! Lakini vitabu vyote 39 vya Agano la kale viliandikwa kwa

kiebrania! Na vile 27 vya Agano Jipya viliandikwa kwa kiyunani! Je ikawaje sasa Biblia

ikatafsiriwa kwa lugha mbalimbali hadi za makabila ya watu?

Ooh! Haikuwa kazi ndogo hata kidogo,wako waliochomwa kama nyama za mshikaki wakafa.

kisa na mkasa wametafsiri Biblia kwa lugha isiyoruhusiwa!

Sasa tuone ilivyokuwa hapo zamani za kale!

Mnamo mwaka 250 K.K pale Alexandria Misri,jopo la watu 72 lilikusanyika kutafsiri Biblia

kutoka kiebrania kwenda kiyunani! Waliongeza vitabu 14 vya Apokrifa kwenye vitabu vile 39

vya Agano la kale. Mwaka 382 B.K Jerome alitafsiri Biblia kwenda Kilatini akiviweka na vitabu

vile visivyo rasmi,vitabu 14 vya Apokrifa hivyo Biblia aliyoitafsiri(Vulgate) ikawa na vitabu 80.

Chini ya utawala Wa Mapapa Wa kanisa la Roman Catholic walipiga marufuku kufasiri/kutafsiri

Biblia kwenda lugha zingine isipokuwa kilatini tu. Mwaka 1384 John Wycliffe Profesa wa

Oxford,mwana zuoni na mtheologia! akamwa MTU Wa kwanza kuitafsiri Biblia kwenda lugha

ya kiingereza! Alinakili mkono kwa mkono,yaani teknologia ya kuchapisha ilikuwa bado

haijavumbuliwa.Miaka 44 baada ya kifo chake,nakaza kadhaa za maandiko yake yakamfikia

Papa,alikasirika sana, kusikia kuna MTU mmoja aliyetafsiri Biblia kwenda kiingereza! Aliamuru

kaburi lake lifukuliwe,mifupa yake ipondwepondwe kisha itupwe mtoni. Mtu yeyote

aliyekutwa,ama kukamatwa na nakala zozote za Biblia zisizokuwa kwa kilatini,walihukumiwa

hukumu ya kifo. mwaka 1415 B.K, kama vile utani,mwanafunzi Wa John Wycliffe,John Hus

alikamatwa akiwa na nakala kadhaa ambazo zilitumika kumchoma kama mwizi mbele ya

kadamnasi ya watu. kabla hajafa akasema maneno haya ! Namnukuu..

""Kwa miaka 100 ijayo Mungu atamwinua MTU, ambae wito wake kwa mageuzi hauwezi

kuzuiliwa!""" .mwisho Wa kumnukuu!

Kama alivyotabiri mwaka 1517 B.K, Martin Luther akaanzisha mageuzi ya wazi dhidi ya kanisa

Katoliki kwa kugongelea mlangoni mwa kanisa,wakati kabla ya misa/ibada kuanza,mambo 95

kinyume na Neno la Mungu yanayofanywa na Kanisa katoliki mjini Wittenberg! kitabu cha Foxe

kilichokuwa kikiandika mashahidi Wa Imani(wafia dini) waliouwawa kwa kosa la kulipinga,ama

Page 12: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

12

kwenda kinyume na kanisa Katoliki;kilieleza mwaka huo Wa 1517 watu 7 walichomwa

hadharani kwa kosa la kuwafundisha watoto wao kusali sala ya Bwana kwa lugha ya

kiingereza/kimombo badala ya kilatini. Martin Luther alienda mbali zaidi katika kuitafsiri Biblia

kwenda kijerumani huku akihimiza kila MTU asome Biblia mwenyewe! Asisubiri kusomewa

kanisani. Mwaka 1450 huko Mainz,Ujerumani Johann Gutenberg akawa MTU Wa kwanza

kutengeneza mashine ya kuchapisha Biblia! Ikarahisisha Biblia kunakiliwa kwa haraka,na

kusambazwa kwa kasi,tofauti na hapo kabla! ambapo nakala za Biblia zilikuwa chache na

ziliuzwa ghali sana! Matajiri tu ndio walioweza kununua. William Tyndale,mwana

zuoni,mbobevu tena kapteni Wa jeshi la mageuzi alikuwa anazungumza lugha 8 tofauti kwa

ufasaha kana kwamba ndizo alizozaliwa nazo! Alichapisha Biblia(Agano Jipya) kwa lugha ya

kiingereza. Alitumia karibu miaka 11 kuikamilisha Agano Jipya kwa lugha ya

kiingereza,akinakili kutoka kwa Erasmus aliyewahi pia kutafsiri Agano Jipya kutoka Kiyunani

kuja kilatini!

Mwaka 1530 kazi yake ilipata soko sana kwa sababu kila MTU alitaka apate nakala yake! Hivyo

zilifichwa kwenye mabarota ya pamba na magunia ya unga kama bidhaa za magendo ili

ziwafikie Wateja wake! Ambao wengi walikuwa watumishi Wa Mfalme. Kila aliyekamatwa na

kopi/nakala hizo alihukumiwa kufa,la sivyo aiteketeze kwa moto kabla hajakamatwa!

Maparoko,mapadri walizitafuta nakala hizo kwa waumini wao ili kuwazuia wasizisome kwa

madai zilikuwa na makosa mengi! na ndugu Tyndale alitafutwa kwa udi na uvumba,Mwisho

nakala hizo zilifika hadi chumbani mwa Mfalme Henry VIII Wa Ungereza. Mwaka 1536

William alikamatwa baada ya kusalitiwa na rafiki yake,akafungwa kwa siku 500,kisha

akanyongwa na akachoma moto hadi kuwa majivu.

Kabla hajafa akasema " Ee Bwana naomba ufungue macho ya Mfalme Wa Ungereza"!. Mwisho

Wa kumnukuu. Miaka 3 baadae Mfalme Henry VIII akatoa amri,akaidhinisha mchakato Wa

kuitafsiri Biblia yote kwa kiingereza iliyopewa jina la 'Biblia kubwa' chini ya Askofu Thomas

Cranmer Wa jimbo la canterbury alimteua Myles Coverdale kuichapisha biblia hii iliyokuwa na

kimo cha inchi 14! Kuanzia April 1539 hadi Desember 1541 yalichapishwa matoleo 7 ya Biblia

hii. John Calvin mwana zuoni,mthelogia,mwenye fikra za mageuzi, huko Geneva uswizi

alianzisha chuo cha Biblia na John Knox Wa Scotland walisimamia mpango Wa Biblia iliyoitwa

"Geneva study Bible" ilikusudiwa kuwafundisha watoto wao wakati wao wako uhamishoni,ama

kifungoni! Ilikuwa Biblia ya kwanza kutumia Sura/mlango na aya/mstari kila ukurasa ukiwa na

mistari 42! kwa kipindi cha miaka 100 iliongoza kuwa bora zaidi ya nyingine! Ilikuwa ya

kwanza kupelekwa bara la Amerika.

Mwaka 1560-1644 matoleo 144 yalichapishwa katika juhudi ya kuboresha na kuihakiki maana

halisi ya kila neno likilotumika kuitafsiri. Mwaka 1611 NI mwaka Wa historia kubwa katika

Biblia kwani mfalme James VI alifadhili mpango Wa kuchapisha Toleo la Bibli litakalomaliza

ubishi na kuwa bora kuliko yote yaliyopita. Miaka 6 ilitumika kuikamilisha! Mwaka 1605-1606

utafiti ulifanyika, 1607-1609 uchambuzi na kuikusanya 1610 kuichapisha, 1611 ilikamilika

Page 13: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

13

yenye urefu Wa kimo inchi 16 kwa ukubwa. Ndio hadi Leo inatumika kama standard ya

nyingine zinazotafsiriwa!

Zingine zilizochapishwa 1885 ilichapwa tena

1971 new American standard Bible(NASB)

1973 new international version(NIV)

1982 new king James version (NKJV)

2002 English standard version (ESV)

Biblia kwa lugha ya kiswahili, Union Version(SUV) ilichapwa kwa mara ya kwanza mwaka

1952, 1997: na lugha iliyotumika inajulikana kama kiswahili cha kimvita!na Kiunguja . Ndio

maana maneno kama "maseyidi,"mashehe," yametumika! Na sinagogi wakitafsiri kama sinagogi

la wayahudi!

Japokuwa Mbingu na nchi zitapita! Neno la Mungu ladumu hata milele!

Page 14: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

14

VITABU VYA APOKRIFA.

Je umewahi kuisoma/kusikia Biblia yenye vitabu 72?

Je vitabu nyongeza 7 vimeingiaje na vina nini?

Mnamo mwaka 250 K.K( kabla ya Kristo) kufuatiwa na kutafsiriwa kwa sheria(Pentateuch)

yaani vitabu 5 vya Musa huko Alexandria(Misri) na vitabu vingine kwa jopo la waandishi

70,kulipelekea kutolewa na kuchapishwa kwa toleo la Septuaginta(lxx) la Biblia lililotowewa

zamani kwa ajili ya wayahudi wa mataifa,lililoandikwa kwa kiyunani.Lilianza kusomwa katika

masinagogi ya wayahudi wamataifa.lilikuwa pia limekusanya vitabu 14 visivyo rasmi. Hivyo

kufanya Biblia toleo kwanza (katoliki) LA kilatini lililotafsiriwa na Jerome kuwa na vitabu 80!

Baadae walivipunguza hadi 72.Apokrifa=imefichwa!

MAJINA YA VITABU VYA APOKRIFA.

1.Tobithi

2.Judithi

3.Hekima ya Yoshua bin Sira

4.Baruku

5.I Makabayo

6.II Makabayo

7.Hekima ya Sulemani

Page 15: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

15

1. TOBITI.

Uandishi: 400-200 K.K. mbali na Palestina labla Misri.

Toleo la kwanza liliandikwa kwa lugha ya kisemitiki likapotea. Kinasimulia habari za jamaa za

Tobiti,kina tafsiri nyingi zinazohitafiliana. Ni simulizi za kale zisizo na msingi wa neno la

Mungu wala maandiko.mfano jini asmodeo,malaika Rafaeli.Kutukuza wafu,kuhimiza watu

kuwashughulikia marehemu. mfano, kuwaombea.Tobiti anasimuliwa kama mtu aliyeishi baada

ya kifo cha mfalme Sulemani na kugawanyika kwa ufalme.

Kitabu hiki hakikupokelewa na wayahudi na waporestanti katika orodha ya vitabu rasmi.

2. YUDITHI.

Uandishi: 100 K.K. Inaonekana kitabu hiki kimetungwa katika Palestina kati ya miaka 120-80

K.K. Mwanamke Yudithi anasimuliwa kuwakomboa wayahudi kutoka kwa jemedari Holofene

aliyetumwa na Nebukadreza huko Betulia.Tafsiri zinatofautiana kati ya Vulgata na

nyingine,historia ya geografia haikuzingatiwa.Kitabu hiki hakikupokelewa na wayahudi na

waporestanti katika orodha ya vitabu rasmi.

I MAKABAYO

Uandishi : 100 K.K. Kitabu kinasimulia vita vya wayahudi na wafalme waseleusidi,vita vya

kupata uhuru wa dini na siasa. Yuda(Makabayo) alikuwa kama shujaa mkuu(mhusika mkuu) na

ndugu zake/wenzake, kama Matathia,Yonathani na Simoni. Tukio la mfame Epifani IV, alipotoa

sadaka ya nguruwe katika madhabahu ya hekalu la wayahudi(Chukizo la uharibifu ilikuwa Des

8,167 K.K.) Kitabu hiki hakikupokelewa na wayahudi na waporestanti katika orodha ya vitabu

rasmi.

4. II MAKABAYO.

Uandishi :120 K.K.,baada ya mwaka 124 K.K. Tabia ya utungaji wa kitabu wa Makabayo wa

kwanza,ni tofauti sana na na kitabu cha pili,kinaandikwa kwa lugha ya kiyunani. Ni muhutasari

wa wa vitabu 5 vilivyoandikwa na Yasoni mtu wa Kirene. Ni kwa ajili ya wayahudi wa

Iskanderia(Misri).Sala kwa ajili ya marehemu(sura ya 12:41-46)

Dhima kuu ni kuwafurahisha wayahudi/kuwaimarisha watu na kuwavuta wayahudi wa Misri ili

kushikamana zaidi na wayahudi wa Yerusalemu.

5. YOSHUA BIN SIRA.

Uandishi : 190-132 K.K. Kiliandikwa/kutungwa huko Misri na kufasiriwa mwaka 38 wa mfalme

Ptolomeo VII Evergete.Kinahimiza watu kutumia kileo ilimradi mtu asilewe:(sura 31:25-31).

Kutokana na tafsiri ya Septuaginta,waporestanti walikihesabu miongoni mwa Apokrifa.

Page 16: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

16

Vingine ni :Hekima ya Sulemani,Baruku n.k.

Nyongeza nyinginezo.

Waraka wa Yeremia, Danieli sura ya 13-14,Wimbo wa Azaria katika tanuru, Wimbo wa vijana

3,Suzana na hukumu ya Danieli,Belina na Joka.Baadhi ya sura ktk Kitabu cha Esta;ndoto ya

Mordekai,nakala ya barua ya mfalme Artashata,sala ya Mordekai,sala ya Esta na amri mpya ya

mfalme Muunganiko wa Ezra na Nehemia(Esdras)

UMUHIMU WA BAADHI YA VITABU.

Kitabu cha 3 Esdras na Makabayo 1.

Katika taaluma ya historia ya Biblia na theolojia vinasaidia wanazuoni(wasomi) kufahamu

mambo yafuatayo;

Nini kilikuwa kinaendelea katika dini na taifa la kiyahudi katika miaka ile ya giza (400) kati ya

Malaki na Mathayo.

Kufahamu mazingira(context) ya siasa,dini,tamaduni aliyozaliwa Yesu.

Kujua taifa,historia,siasa na taasisi za dini ya kiyahudi zilizoanza au kukubalika katika kipindi

hiki cha miaka 400;mfano mafarisayo,masadukayo,n.k

Je kazi ya umisheni ya kumtangaza Yehova kwa mataifa iliendeleaje katika kipindi hiki?(inter-

testimonial period).

Kujua chanzo cha ibada za wafu katika kanisa Katoliki na viongozi wakuu walioanzisha.

SABABU ZA KUKATALIWA KATIKA BIBLIA

Havikukubaliwa na Waebrania na dini yao hata wakati mmoja,Talmud-kitabu cha mapokeo ya

wayahudi kinasema baada ya malaki, Roho Mtakatifu aliondoka Israel.Hii ina maana unabii au

uandishi wowote baada ya Malaki ulikuwa hauna uvuvio wa Mungu.Maneno yaliyomo katika

Apokrifa hayakutajwa katika Agano Jipya.

Josephus na Philo(Yosefu na Filo) wana falsafa wataalam waliobobea katika historia ya wakati

ule walivikataa vitabu hivi.

Havikuwamo na haviko katika orodha yeyote ile ya maandiko matakatifu kabla ya mwaka 400

k.k

Page 17: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

17

Jerome mwandishi na mtaalam anayeheshimika katika historia ya kanisa,alikuwa pamoja na

kanisa Katoliki alivikataa kabisa vitabu hivi.

Waandishi wenyewe wa vitabu hivi vya Apokrifa hawakudai hata mara moja kuwa ni vya

Mungu.

Havina unabii wa kweli wala havisemi “hili ndilo neno la BWANA” au “asema BWANA wa

majeshi”

Vina makosa mengi ya usahihi wa historia,vinapingana,havipatikani katika mambo makuu

muhimu ya historia(theologia).

Havina mafundisho ya kiroho kwa viwango vya ki-Biblia.

Maneno mengi ni ya hadithi,ya kigeni,yakuchekesha na yaliokosa dhima kuu ya ujumbe.

Yesu hakuwahi kunukuu katika vitabu hivi.

Mitume na manabii pia hawakuwahi kunukuu toleo,kifungu katika vitabu hivi.

Vilianza kutumika(kutumiwa) rasmi na kanisa Katoliki mwaka 1546 B.K. Katika kukabiliana na

matengenezo yaliyokuwa yakifanywa na Martin Luther na wenzake.

Ni baraza kuu la Katoliki lililoitwa (council of trent) lililovunja kanuni za Biblia na kuingiza

rasmi vitabu hivi.

Chini ya Papa Paul III,wa wakati huo vitabu hivi vilikubalika na wajumbe wachache na wasio na

taaluma.

Waliokuwa wajumbe katika baraza hili walibishana sana,na sio wote waliokubali jambo hili.

Baraza hili ndilo lililopitisha kuwa yeyote anayekataa vitabu hivi na alaaniwe! “anathema”!

Vitabu hivi havifai kutumika katika kanisa wala kusomwa wakati wa ibada.

Vitabu visivyokubaliwa na yeyote.

Kitabu cha Henoko,Siri za Henoko,Ufunuo wa Baruku,Kuchukuliwa kwa Musa,Ufunuo wa

Musa,Kupaa kwa Isaya,ufunuo wa shija,wosia wa Adam,Mausia ya Ibrahim na Isaka na Yakobo,

ufunuo wa Ibrahimu,Maisha ya Asenati(mke wa Yusufu),kitabu cha Nuhu.

Page 18: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

18

Utangulizi wa Agano la Kale.

Vitabu 5 vya Musa

Vitabu vitano vya kwanza vya Biblia ambavyo katika utamaduni wa kidini wa Wayahudi

vilijulikana kwa jina moja: “Torah” jina lenye maana ya Sheria au Mwongozo. Wayahudi

waliozungumza lugha ya Kigiriki waliviita vitabu hivyo vyote vitano “Pentateuko” yaani

“Kitabu katika sehemu tano.” Vitabu hivyo vinajulikana pia kama Vitabu vya Musa, na tafsiri

nyingine huvitaja kama Kitabu cha kwanza cha Musa (Mwanzo), Kitabu cha pili cha Musa

(Kutoka) n.k.

Page 19: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

19

MUHTASARI WA KITABU CHA MWANZO.

Kina sura 50:

Kina mistari 1,533.

Mwandishi: Musa.

Mwaka Wa Uandishi: 1450-1410 k.K

Matukio ya kitabu hiki yalimalizika karne 3 kabla ya kuzaliwa kwa Musa.

Matukio ya kitabu hiki yamechukua muda mrefu sana kuliko kitabu kingine chochote! Hivyo

Musa aliandika kwa kifupi tu baadhi ya matukio makuu muhimu yaliyokuwa yakionesha

mpango Wa Mungu kwa mwanadamu kama alivyooneshwa na Mungu juu ya mlima Sinai.

Neno “Mwanzo” (Kitabu cha Mwanzo) linamaanisha: Chimbuko, chanzo, asili; nalo linatumiwa

kukitaja kitabu hiki cha kwanza cha Agano la Kale kwani chenyewe kinasimulia hasa juu ya jinsi

ulimwengu ulivyoanza kuwako, asili au chimbuko la binadamu na asili ya Waisraeli.

Jina la kitabu kwa Kilatini ni GENESIS, maana yake ni kuzaliwa, mwanzo. Tafsiri zingine

zinatumia majina ya Ki­latini: GENESIS. Na zingine: KITABU CHA KWANZA CHA MUSA.

Biblia ya Kiswahili inatumia jina: MWANZO. Kiebrania kitabu hiki kinaitwa BERE´SHIT.

Maana yake ni Mwanzoni. Kuandikwa; mwaka wa 1807 K.K.

Kitabu kinatueleza mwanzo wa mambo yote isipokuwa Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu. Wao

hawana mwanzo. Ndani ya kitabu hiki kuna mianzo mingi. Kwa mfano: kuna mwanzo wa

uli­mwengu, mwanzo wa taifa la wana­damu, mwanzo wa dhambi ulimwe­nguni. Kuna mwanzo

wa ahadi ya ukombozi. Na pia mwanzo wa maisha ya familia. Mwanzo wa ustaarabu wa

wanadamu na mwanzo wa mataifa ya ulimwengu. Na pia mwanzo wa taifa la Wayahudi yaani

mwanzo wa taifa la Waebrania.

Kitabu hiki ni historia ya kushindwa kwa mtu. Lakini tunaona kwamba kila mara mtu

ali­poshindwa Mungu alikuwapo kumwo­koa. Yeye ni Mwokozi wa ajabu!

Kitabu cha Mwanzo chaweza kugawanyika katika sehemu mbili kuu:

Sura 1–11:

Historia ya awali ya kale juu ya ulimwengu na binadamu. Simulizi hili linatokana na imani

thabiti kwamba ulimwengu wote uliumbwa na Mungu na kwamba watu walitokana na wazazi

wa kwanza walioumbwa na Mungu, kwamba uovu, mateso na kifo duniani chanzo chake ni watu

wenyewe.

Page 20: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

20

Baada ya historia hiyo ya awali ya kale tunasimuliwa jinsi Mungu alivyowaadhibu watu kwa

gharika kuu na jinsi Nuhu alivyookolewa katika maangamizi hayo. Kisha tunafahamishwa juu ya

asili ya mataifa na lugha tofauti katika simulizi la Mnara wa Babeli (Sura 11.)

Sura 12–50:

Historia ya kale ya Waisraeli. Mungu alijichagulia watu wa Israeli ili kwa kupitia kwao mataifa

mengine yamjue Mungu na kubarikiwa. Kwa hiyo, Mungu alimwita Abrahamu (12:1–25:18)

ambaye anasifika kwa imani yake na utii wake kwa Mungu, kisha mwanawe wa pili, yaani Isaka,

halafu Yakobo (25:19-37:1) ambaye alipewa jina ambalo limekuwa jina la taifa hilo Mungu

alilochagua – Israeli. Yakobo alikuwa na wanawe kumi na wawili ambao walikuwa chanzo cha

makabila kumi na mawili ya Israeli. Mmoja wao, Yusufu, (37:2–50:28) alikuwa baba wa

makabila mawili: Efraimu na Manase.

1. Simulizi la awali kuhusu ulimwengu na mtu,

Sura 1–11

(a) Kuumba ulimwengu (1–2)

(b) Uasi na kuanguka kwa mtu (3)

(c) Uasi unaongezeka (4–5)

(c) Nuhu na gharika (6–9)

(d) Mnara wa Babeli (10–11)

2. Historia ya awali ya Waisraeli, Sura 12–50

(a) Habari za Abrahamu na watoto wake (12–24)

(b) Habari za Yakobo (25–36)

(c) Habari za Yusufu (37–50)

Huo ndio utangulizi mfupi juu ya kitabu cha Mwanzo!

Kwa maelezo zaidi soma kitabu cha mwandishi huyu huyu: SIMULIZI ZA MPANGO WA

MUNGU TOKA ADAMU HADI WEWE!

Page 21: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

21

UTANGULIZI WA KITABU CHA KUTOKA!

Tangu mwaka wa 1807 K.K. hadi mwaka wa 1558 K.K. ilikuwa katikati ya MWANZO na

KUTOKA na ilikuwa miaka 250. Biblia haisemi mambo yaliyotokeo hapo katikati. Wakati huo

wana wa Israeli waliongezeka huko Misri. Waliishi kwenye jimbo la Gosheni. Waliongezeka

kwa kasi sana na waka athiri mambo yote kuanzia siasa,uchumi,biashara,tamaduni na mambo ya

kijamii ya wamisri! Wakatapakaa kila kona ya maamuzi! Wamisri wakaona kama vile wachaga

walivyo kila kona ya inchi ila bora wachaga NI watanzania! Wayahudi/waebrania sio wamisri!

Jamii ya kifalme Babeli wa kwanza ilitawala. (1894-1595) Hammurabi, mwanasheria maarufu,

alikuwa mfalme (1792-1750 K.K.).

Kwenye mwaka wa 1730 kabila la Hyksos liliwatawala Wamisri. Lilikuwa na magari ya farasi

ya kivita na hivyo Wamisri hawakuweza kitu. Kabila la Hyksos lilitawala Misri miaka 150.

Kabila la Hyksos lilitoka kaskazini na lilikuwa jamaa ya Shemu. Huko Misri, katika mji wa

Thebe farao Sekenenre (1600 K.K.) alipigana na kabila la Hyksos lakini aliuawa katika

mapigano. Inawezekana aliuawa wakati wa vita. Fuvu la kichwa chake kilichojeruhiwa liko

katika jumba la makumbusho huko Kairo. Kijana wake farao Ahmose (aliyetawala 1580-1558

K.K.) pamoja na ndugu yake Kamose walifaulu na kuwafukuza wa Hyksos toka Misri.

Farao Amenhotepi I (alitawala 1558-1525 K.K.) aliyemfuatia farao Ahmose, alianza kuwatesa

sana wana wa Israeli. Aliogopa kwamba Waisraeli watakapopata nguvu zaidi watawatawala

Wamisri na kuwaweka chini ya utawala wao, kama watu wa Hyksos walivyofanya kabla.

Waebrania wala wazo la kurudi kwao kaanani jalikuwepo vichwani mwao! Raha mustarehe

ziliwafanya kuona Gosheni NI inchi yao halali,sasa ili watoke Misri acha mateso yaanze! Ule

msemo usemao "akufukuzae hakiambii toka"..

1558-1447 K.K.

KUTOKA. Ilichukua miaka 111.

Farao= Nyumba kubwa.

1558 K.K. Farao Amenhotepi I (1558-1525) alichukua utawala. (KUT 1:8)

1531 K.K. Haruni alizaliwa.

1529 K.K. Farao Amenhotepi I alitoa amri: "Watoto wa Waisraeli wote wakiume watupwe mtoni,

mto Nile." (KUT 1:22)

1528 K.K. Musa alizaliwa. Binti wa farao Amenhotepi I (jina lake Hatsepsuti) alimchukua mtoto

Musa. (KUT 2)

Page 22: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

22

1525 K.K. Farao Amenhotepi I alifariki na farao Tho times I I (1525-1508) alichukua utawala.

Musa alikuwa na miaka 3.

1508 K.K. Farao Thotmesi I alifariki na farao Thotmesi II (1508-1504) alichukua utawala. Musa

alikuwa na miaka 20.

1504 K.K. Farao Thotmesi II alifariki. Musa alikataa kuwa farao. (EBR 11:24) Hatsepsuti, mama

yake wa kambo alichukua utawala (1504-1492).

Wakati huo alizaliwa Thotmesi III, mtoto wa dada au wa kaka yake Hatsepsuti.

1497 K.K. Yoshua alizaliwa.

1487 K.K. Musa alianza kuwatetea Waebrania waliokuwa watumwa Misri. Musa alikuwa

kinyume cha Wamisri.

Farao Hatsepsuti akaogopa kwamba Musa, atakapokuwa mfalme, angehamisha utawala kutoka

Misri kwenda kwa Waebrania yaani wa Waisraeli.Ili mambo hayo yasifanyike, Hapsepsuti alitoa

amri Musa auawe.

Musa akakimbia mpaka Midiani. (KUT 2:11-15)

1482 K.K Farao Thotmesi III (1482-1450) alichukua utawala.

1450 K.K. Farao Amenhotepi II (1450-1425) alichukua utawala.

1448 K.K. Musa mbele ya kijiti cha moto. (KUT 3)

Musa alirudi Misri

Page 23: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

23

MUHTASARI WA KITABU CHA KUTOKA

Kina sura 40

Kina mistari 1,213.

Mwandishi: Musa.

Mwaka Wa Uandishi: 1445-1405 k.K

Kuzaliwa kwa taifa la Israeli kwa uchungu Na kumalizia kwa ukombozi Wa kutoka

Misri.Katikati ya MWANZO na KUTOKA kuna miaka 250-300 Wakati huo Biblia imenyamaza

kimya. Wakati huo taifa la Israeli waliongezeka huko Misri toka watu kama mia moja hadi watu

milioni mbili hadi tatu.

Kitabu cha KUTOKA kinaitwa Kilatini: EXO­DUS. Maana yake: Kuondoka, Toka nje, Kwenda,

Maandamano wa kuondoka. Tafsiri zingine zinatumia jina: EXODUS, au KITABU CHA PILI

YA MUSA, au kama tafsiri ya Kiswahili: KUTOKA.

KUTOKA ni kitabu cha ukombozi kinachotueleza kuokoka kutoka wapi, ina­wezekanaje na

mwanadamu anaokoka kwenda wapi? Anaokoka kutoka utumwa wa Misri anatoka kupitia damu

ya mwanakondoo wa pasaka, anapita Bahari ya Shamu. Ni mfano: mtu anaokoka kutoka dhambi.

Kupita Bahari ya Shamu ni mfano wa ubatizo. (1KOR 10:1,2). Ni mifano ya mambo ya Agano

Jipya. Na baadaye mtu anatembea jangwani kue­lekea nchi ya ahadi.

Mungu alitaka akae kati ya watu wake na kwa ajili ya hii akawaamuru wajenge Hema ya

kukutania.

Taarifa za kutoka!

Katika utawala Wa 18 Wa mafarao waliowahi kuitawaka Misri: ndipo Mungu akamtuma Musa

kuwatoa wana wa Israeli Misri. Ilichukua mda wa siku moja Mungu kuwatoa Wana wa Israeli

Misri lakini ilichukua miaka 40 Misri kutoka ndani ya mioyo ya wana wa Israeli! Kutoka

kunaonesha mwanzo wa taifa la Israeli,mwanzo wa Kalenda yao,walianzia katika utumwa

wanamalizia katika ukombozi! Maisha ya Musa yamechukua 1/7 ya Biblia nzima! Aliishi, ikulu

miaka 40,akaishi jangwani(midiani)miaka 40 na akawaongoza wana wa Israeli kwa miaka 40!

“Egypt is a type of the world. Moses is a type of Jesus Christ. Passover is a type of the death of

Jesus Christ. The Exodus is a type of salvation. The crossing of the Red Sea is a type of victory

over the world. The pillar of cloud and of fire is a type of the presence of God in the believer.

God had Israel spoil the Egyptians to provide for the Tabernacle.”

Page 24: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

24

Mgawanyo wa Sura katika kitabu cha Kutoka

Kitabu cha Kutoka ni kitabu cha pili katika orodha ya vitabu vya Agano la Kale, cha kwanza

kikiwa Kitabu cha Mwanzo.

Jina la kitabu hiki KUTOKA ni tafsiri ya jina la Kigiriki “eksodos” ambalo lahusu tukio

maalumu kabisa katika historia ya Waisraeli: Kutolewa kwao utumwani Misri, kuvuka bahari ya

Shamu na safari yao jangwani hadi mlima Sinai.Kule mlimani Sinai, Mungu alijijulisha kwao,

akaratibisha uhusiano wake nao kwa kuwawekea agano lake na mwongozo utakaoimarisha

uhusiano huo, yaani amri kumi na maagizo mengine kuhusu namna ya kuishi.Mhusika mkuu

katika kitabu hiki ni Musa. Musa aliitwa na Mungu kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri. Yeye

anaonekana katika kitabu hiki kuwa msemaji wa Mungu kwa watu wa Israeli. Aliwaongoza

safarini kwa niaba ya Mungu na kuwajulisha matakwa ya Mungu.

Kwa jumla, kitabu hiki chatuonesha hasa juu ya uhuru wa kweli, uhuru ambao Mungu

anawapatia watu wake wapate kuwa na uhusiano mwema naye, na baina yao wenyewe.!

Page 25: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

25

MUHTASARI WA KITABU CHA MAMBO YA WALAWI!

Kitabu kimeandikwa mara baada ya mwanzo wa safari jangwani, hema ya kukutania

ilipokamilika. Hema ya kukutania ilikamilika mwaka (1447). Kabla ya Kristo. Jina la kitabu

kwa Kilatini ni LEVITICUS, maana yake ni: Kinawahusu Walawi.

Tafsiri zingine zinaitwa: KITABU CHA TATU CHA MUSA.

Au MAMBO YA WALAWI, kama tafsiri ya Kiswahili.

Kina sura 27 ; mistari/aya 659.

Kitabu hiki kimeandikwa 1445-1444K.K

Mazingira ya uandishi; chini ya mlima Sinai

Wahusika wakuu!

Walawi na namna ya kuwaongoza watu katika kumwabudu,kumtumikia na kumtii Mungu!

Dhima kuu:

Utakatifu! Kutengwa kwa ajili ya Mungu! Waisraeli walipaswa kutengwa na wanadamu (kukaa

jangwani) ili waweze kumwakilisha na kuwasilisha Sera, ilani na tabia ya Mungu kwa mataifa

mengine! Katika kabila zote 12 za Israeli, kabila la Lawi lilitengwa kwa ajili ya kazi ya

utakatifu,wao hawakupewa urithi,wale na kuishi madhabahuni,wahudumu madhabahuni,waishi

kwenye miji yao iliyotengwa!

Ndani yao kulikuwa na koo 3 ambazo NI Merari, Kohathi na Gersoni.

Kohathi walitoka makuhani na watu cream/mahususi waliotakaswa zaidi kwa ajili ya patakatifu

pa patakatifu,mfano Musa na Haruni;

Merari alifuatia kwa nafasi ya patakatifu na Gersoni kwa nafasi ya ua wa nje,hema na vifaa

vyake,ulinda lindo nk!

MAMBO YA WALAWI ni kitabu cha uta­kaso.

Maana ya utakaso au kutakasa ni kufanya takatifu au kutangaza au kutambua hali ya utakatifu.

Neno Utakatifu limetumika mara 87 katika kitabu hiki! Shule ya utakaso inaanza kwa kujifunza

dhabihu.Bila dhabihu huwezi kujita­kasa.

1. Bwana akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia,

Page 26: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

26

2. Nena na wana wa Israeli, uwaambie, mtu wa kwenu ata­ka­pomtolea Bwana matoleo, mtatoa

matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng´ombe na ka­tika kondoo. (LAW 1:1,2)

Mwanzoni mwa kitabu hiki kuna dhabihu kuu tano:

Sadaka ya kuteketezwa. Sadaka ya kuteketezwa ni mfano wa Kristo, ambaye ...

alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa. (Ebr 9:14).

Sadaka ya Unga ni mfano wa Yesu Kristo aliyechu­kua ubinadamu mbele ya watu na

ya Mungu.

Sadaka za amani ni mfano kwamba ku­pitia Yesu sisi tuna mawasiliano na Mungu.

Sadaka ya dhambi. Sadaka ya dhambi ni sadaka kwa Wakristo wanyonge. Na

anayejua yeye si Mkristo mkamilifu bali dhambi ikaayo ndani yake.

Sadaka ya hatia ni mfano kwa Kristo kwa wasioa­mini, anayetafuta wokovu. Na

sadaka ya hatia ni pia Kristo kwa Mkristo aliyeanguka dhambini lakini anayetaka

kurudi..

" Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na

mmoja kwa mwungwana.

Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.

Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka

mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko

Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto."

NI maneno ya Paulo kwa kanisa la Leo tujifunze kiini cha utakatifu tupate kuhesabiwa haki

baada ya kutengwa kama vile Ibrahimu alivyotengwa mbali na inchi yake kwa yeye Sera,

ilani,wokovu ukatufikia sisi tuliokuwa mbali na Mungu! Haleluya!!!

UTAKATIFU, MTAKATIFU ,UTUKUFU UNA YEYE LEO,SASA NA HATA MILELE!

AMINA!

Page 27: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

27

MUHTASARI WA KITABU CHA HESABU:

Katika kitabu cha Hesabu ambacho kimeandikwa na Musa eneo kubwa la kitabu hicho

kimeandikwa kuhusu sensa ambazo Mungu aliruhusu zifanywe pia tunasoma kuhusu wapelelezi

waliotumwa kuipeleleza nchi ya Kaanani. Jambo linaloonekana kugusa mahusiano ya

mwanadamu na Mungu katika kitabu hichi ni jambo hasi linaroharibu mahusiano. Jambo hilo ni

manunguniko. Kinatokana na hesabu za sensa 2 zilizofanyika jangwani!

Mwandishi: Musa

Mwaka Wa uandishi: 1450-1410 K.K

Idadi ya sura : 36

Idadi ya aya/mistari :1288

Kitabu cha manunguniko!

Kitabu cha misafara( msafiri na mpitaji) Kimechukua miaka 39 katika matukio yake. Hesabu

1:1-10:11 imechukua nafasi ya siku 21. Hesabu 10:1- 33:38 imechukua miaka 38. Hesabu 33-38

katika Kumbukumbu 1:3 imechukua miezi 6: Safari ya kutoka Misri baada ya miezi 13 ndio

kitabu cha Hesabu kinaanza! Safari ya siku 11 inageuka na kuwa safari ya miaka 40!

Kadesh barnea kilikuwa NI kituo cha mwisho kuikaribia Kaanani NI maili 150 toka Sinai na NI

maili 50 kufika Beersheba mji Wa kusini Wa Yuda! Taarifa ya wapelelezi 12 waliokwenda

kuipeleleza Inchi ya ahadi kwa siku 40 wale 10 wakasababisha safari yao ya upelelezi Wa siku

40 iwe adhabu ya miaka 40 kuifikia kaanani! Kadesh barnea ilikuwa 75% ya safari yao ikageuka

ikawa 7% ya safari yao maana walitumia miaka 38 kutoka Kadesh barnea kufika Kaanani!.

HESABU YA MATUKIO YA MANUNG'UNIKO!

Kutoka mlima Sinai [nyika ya Sinai] walisafiri hadi kufika Tabori ambako moto uliteketeza

hema za waliokuwa wananungunika. Wakazidi kwenda mbele hadi Kibroth-hataava walikopewa

Kware baada ya hapo wakafika Haserothi;Miriam na Haruni wakamnena vibaya Musa.

Kutoka Haserothi wakasafiri hadi Rithma wakafika Rimon-peresi kisha Libna wakatokea Risa na

kufika Keheletha wakapanda mlima Sheferi na kushukia Harada wakapita tambarare ya

makelothi na tahathi na tera na mithka wakatua Hashmona wakazidi kwenda mbele wapitia

moserothi kuingia beneyakani hadi hor-hagidgad na kisha wakafika gudgotha[nchi ya vijito vya

maji]. Kutoka godgoda hadi yotbatha na abrona wakaingia mlima seir[esion-geberi] na kuanza

kuuzunguka mlima huu ambako Miriam alikufa

Nyika ya Sini(Kadesh –Barnea); Mateto mengine ya wana wa Israeli juu ya maji ya

meriba.Upelelezi wan chi ya kaanani …kwa siku 40. Matokeo ya taarifa mabaya ya wapelelezi

Page 28: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

28

ilipelekea adhabu ya watu wote kufa jagwani na safari yao kuwa ya miaka 40…..(miaka 38

kutoka Kadesh barnea hadi Kaanani). Walitaka kwenda kwa hasira na haraka wakapigwa na

Wakaanani.Ndipo uasi wa Kora,Dathani na Abiramu na watu 250 wateule wakamezwa na ardhi.

Watu 14,700 walikufa kwa tauni. Kutoka Kadesh-Barnea hadi mlima Hori(Edomu);Haruni

alipanda,mlimani akafa huko. (Akiwa na miaka 123).Mfalme wa kaanani alipigwa mbele ya

Israeli(Aradi)Negebu aliyesikia habari..Horma. Walianza kuzunguka zunguka nchi ya

Edomu(milima ya Seyiri) kwa miaka 38. Kutoka mlima Hori hadi Salmona wakaenda

Punoni(alipotengeneza nyoka wa shaba) wakaendelea mbele hadi Obothi kisha Iye

abarimu(moabu) safari yao ikazidi kwenda mbele mpaka Dibon

gadi(zeredi),almoni,diblathaimu,milima Abarimu kuikabili

Nebo,beeri,matana,Nahalieli,Bathmoth (kilele cha Pisga)Milima Abarimu kwenda

Shitimu(tambarare za moabu;kisa cha balaki na balaam)baal-peori wakafika Yeriko ngambo ya

Yordani.

Sensa ya 2 ya wana wa Israeli. Kifo cha Musa&kurithi kwa Yoshua.Tohara kwa wana wa

Israeli.Habari za Balaki na Balaam,Pigo la Baal Peori (watu 24000 kufa)

Hotuba za Musa: mwaka 40 mwezi 11 siku ya 1

Walikuwa wengi kuanzia Beth-yeshimothi hadi abeli-shitimu kama mchanga Wa bahari! Kutoka

horebu/Sinai walijifunza utakatifu (mkazo Wa kitabu cha Mambo ya Walawi) lakini

walimchokoza Mungu na Musa kadiri walivyoweza! Hadi Musa akapoteza nafasi ya kufika

Kaanani pia! Inawezekana nawe NI miongoni mwa wale waliookoka vizuri lakini kumsumbua

na kumpa mawazo mchungaji wako NI jambo la kawaida sana! Pengne Mchungaji/viongozi

wako Wa kiroho wamefikia mahali pa kuikosa mbingu kwa sababu yako! Je hili NI Jema?

Tafakari!

Page 29: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

29

MUHTASARI WA KUMBUKUMBU LA TORATI.

Mwandishi:Musa

Mwaka Wa uandishi: kati ya 1408-1405 K.K

Maana ya jina: sheria ya pili,torati iliyojirudia

Idadi ya sura: 34

Aya/mistari: 957

Kitabu hiki huitwa ; kitabu cha kumbukumbu!

Matukio yake yamechukua kipindi cha mwezi mmoja!

Safari ya wana Wa Israeli sasa imefikia karibu kabisa na nchi ya ahadi!,kwenye tambarare za

moabu ng'ambo ya Yordani!

Kimezaliwa kizazi kipya cha jangwani,wengine wamezaliwa baada ya kuondoka mlima Sinai

hivyo hawajui chochote wala kushuhudia matendo makuu ya Mungu kama;kuvushwa bahari ya

shamu,amri 10,mwamba kutoa maji na mengineyo! kizazi kile kilichopewa amri 10 katika mlima

Sinai baada ya kutoka Misri kimekufa chote jangwani! Kutokana na uasi wao juu ya Mungu!

Miaka ile 40 kama adhabu inafikia ukingoni!wapo wachache walio pata NEEMA ya kuishi hadi

wakati huo; nao NI Musa,Joshua na Kalebu. Sasa Musa anatoa habari,taarifa,hotuba kwa hiki

kizazi kipya! Akiwausia kwa kuwasomea kumbukumbu la Torati kabla ya Yeye kufa!

HOTUBA KUU 3 ZA MUSA!

Hotuba ya kwanza: sura 1:1 - 4:3

historia fupi ya taifa la Israeli tangu walipotoka mlima Sinai,uasi uliotokea Kadesh

Barnea,manung'uniko ya jangwani,wosia Wa Musa.

Hotuba ya pili : sura ya 4:44 - 26:19

Nini dhima kuu ya agano!

Amri na sheria zote zihusuzo mambo mbalimbali.

Hotuba ya tatu: sura ya 27-34

Kutoa toleo jipya, kuliboresha toleo lile la agano, maonyo ya Musa, ahadi ya Baraka kwa

kutii,na laana kwa kukaidi, Musa kumsimika Yoshua kuwa kiongozi baada Yake,wimbo Wa

Musa, mausia ya Mungu kwa Musa, baraka za Musa kwa kabila 12 za Israeli

Page 30: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

30

Kifo cha Musa!

Inawezekana sura ya mwisho iliandikwa na Yoshua akimtolea sifa nabii,mtu

mpole,mzee,mwenye miaka 120,kiongozi maarufu asiye taka utukufu wakati harufu za kifo

zinavyomzunguka anapopanda kwenye safu ya mlima akiiona kwa mbali Nchi ya ahadi

akiishangilia nafsini moyoni mwake!.

"Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso;

katika ishara zote na maajabu yote, ambayo BWANA alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri,

kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote; na katika ule mkono wa nguvu

wote, tena katika ule utisho mkuu wote, alioutenda Musa machoni pa Israeli wote."

Je unakumbuka? Je una kumbukumbu yeyote kwa kizazi kijacho?

Tangu unafundishwa Neno la Mungu hadi sasa hatua gani umepiga?

Dua yangu!

Ee BWANA,MUNGU MWENYEZI fufua kazi yako katika kizazi hiki cha zinaa na dhambi!

Wakati wengine wanaongeza viwango vya uovu na iwapo NEEMA ya kuwawezesha wengine

kuongeza viwango vyao vya utakatifu!

Page 31: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

31

MUHTASARI WA KITABU CHA YOSHUA.

Kwa hiyo imesemwa katika chuo cha Vita vya BWANA,

Yoshua: wokovu! "Mungu huokoa"

Alizaliwa kama mtumwa Misri,akawa shujaa Wa kuipeleleza Kaanani akiwa na miaka 50,akawa

kiongozi baada ya Musa akiwa na miaka 85 akaingia Kaanani kama shujaa na majeshi ya Israeli!

Akatawala kwa kuendesha vita miaka 25 akafa akiwa na miaka 110.alikuwa Wa kabila la efraim

mwana Wa Yusufu! Kama vile babu yake alivyokufa na miaka 110 nae aliifikia miaka hiyo!

Aliwasomea torati yote kila baada ya miaka 7 kwenye sikukuu ya vibanda! Hivyo enzi ya uhai

wake walisomewa Mara 3! Torati yote!

Kitabu kina sura 24

Kitabu hiki kina mistari 658.

Kuitwa nchi ya Kaanani ilihusisha vita ktk maeneo makuu 3!

Katikati ya Kaanani: Yoshua 6-8

Kusini mwa Kaanani: Yoshua 9-10

Kaskazini mwa kaanani: Yoshua 11-12

Mambo yaliyomo katika sura za kitabu hiki!

maagizo ya Mungu kwa Yoshua!

Makabila 3; Reubeni,Gadi na 1/2 ya Manase walishapewa urithi ng'ambo ya Yordani baada ya

kuwapiga Waamori; Ogu mfalme Wa Bashani na Sihoni mfalme Wa heshboni ila waliahidi

watavuka mto kupigana kwa ajili ya ndugu zao kisha watarudi kazi ya utekaji ikimalizika!.

Habari za Rahabu kahaba na wapelelezi,

kuvuka MTO Yordani,

Tohara kwa wana Wa Israeli,

Kuanguka kwa ng'ome ya Yeriko,

dhambi ya Akani,

Kuharibiwa kwa Ai,kutoa dhabihu,kusomewa torati na kuandikwa kwenye mwamba huko Ebali

na Gerizimu,

Page 32: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

32

Udanganyifu Wa Wagibeoni,Jua na mwezi kusimama, vita kaskazini mwa kaanani, orodha ya

wafalme 31 waliouwawa na Yoshua, kutomalizika kwa utekaji maeneo, ugawanyo Wa urithi Wa

makabila, miji ya makimbilio,miji ya walawi, zile kabila 3 kurudi ng'ambo ya Yordani,

Mausia ya Yoshua na kifo cha Yoshua na Eliazeri.

Miaka na Matukio!

1408-1387 K.K.

KITABU CHA YOSHUA. Matukio yalichukua miaka 21.

1408 K.K.

Chini ya uongozi wa Yoshua wana wa Israeli waliingia nchini Israeli. Kutekwa kwa Yeriko.

(Yos 6)

1402 K.K.

Nchi iligawanywa kati ya makabila ya Israeli.(Yos 13-21)

1401 K.K.

Hema ya kukutania ilisimimishwa Shilo. (Yos 18:1)

1400 K.K.

Makabila ya Reubeni, Gadi na 1/2 ya kabila la Manase walirudi mashariki ya Yordani. (Yos 22)

1387 K.K.

Yoshua alifariki akiwa na miaka 110. (Yos 24:29)

Kumalizika kwa kitabu cha YOSHUA.

Yoshua = Yesu = Yehova anaokoa. Yehova ni wokovu

The English and Hebrew title is based on the name of the central character, Joshua. His original

name was Hoshea (“Salvation”) before Moses changed it to Yehoshua (“The Lord is Salvation”).

It is tranditionally spelled “Joshua” in English while in the Greek language it is “Jesus”. The

“captain of the Lord’s army” (5:15)

Jesus took the same name meaning the one who saves people from their sin, Christ is "Messiah"

Page 33: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

33

MUHTASARI WA KITABU CHA WAAMUZI.

Utangulizi. Sehemu ya 1!

Kina sura 21:

Kina aya/mistari 618

Mwaka Wa uandishi 10043 -1004!

Dhima kuu: dhambi na madhara ya dhambi!

WAAMUZI 1387-1070. K.K. (Kilichukua miaka 317/335)

Miaka ya Giza! Wakati mwingine Giza tororo!

Matukio ya kitabu hiki yalifanyika 138O-1045 K.K. Matukio ya KITABU CHA WAAMUZI

yalichukua zaidi ya miaka mia tatu. Matu­kio katika kitabu hiki hayako katika mpangilio wa

miaka, kwani sura za mwisho zilifanyika kabla ya yale yaliyotangu­lia. Sura za nyuma zinaeleza

jinsi anguko lilivyowapeleka wana wa Israeli mbali mapenzi ya Mungu.

Ujuzi wa Wayahudi wanafikiri nabii Samweli amekuwa mwandishi wa kitabu cha Waamuzi.

Biblia ina mifano ya aina mbali mbali. Katika vitabu vya Musa mifano hiyo inatu­eleza namna

ya kutoka katika utumwa wa Misri (yaani - kuokoka), tunavyovuka bahari ya Shamu (ni -

ubatizo). Tunavyosafiri jangwani kuelekea nchi ya ahadi (maana yake - safari ya imani).

Mfano katika kitabu cha Yoshua ni tofauti. Inatueleza kuhusu kutekwa kwa nchi ya Kanaani. Ni

mfano kwetu kwamba baada ya kuo­koka tuna­anza safari ya maisha ya rohoni na ahadi za

Mungu zinavyotimizwa kwetu kadri tunavyozidi kusonga mbele.

Kitabu cha Waamuzi kinaendeleza kitabu cha Yoshua. Jina la kitabu hiki kinatokana na kujazwa

roho wale viongozi 12, walio­itwa na Mungu kuwasaidia wana wa Israeli. Hekalu lilikuwa huko

Silo, lakini watu wa­lipomkataa Mungu walishindwa kuka­taa kuingia kwa maadui.

Mahakimu waliwakomboa kwanza Waisra­eli na baadaye wa­kaanza kazi zao za utawala.

Walishughulika sehemu mbali mbali na sehemu zingine walitawala kwa pamoja.

Kitabu cha waamuzi kinaelezea kipindi cha giza ndani ya maisha ya Israeli katika nchi ya ahadi.

Shindi zilizoko katika kitabu cha Yoshua ziligeuka hasara na uhuru ukawa utumwa na badala ya

amani wakaanza kukosa imani. Kuendelea kukaanza kupungua wakapoteza macho ya kiroho na

badala yake watu walianza kuwaza kiulimwengu. Uaminifu kwa Mungu ukapungua badala ya

furaha huzuni ikaingia, na badala ya nguvu kukaja unyonge. Umoja ukatoweka na kuzorota.

Zamani dhambi ilihukumiwa lakini sasa dhambi ilikubaliwa. Watu walianza kumwacha Mungu

naye aka­waacha mikononi mwa maadui. Israeli ilipoanguka lakini walipojuta na kumlilia

Page 34: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

34

Mungu yeye akawainulia mwamuzi/ha­kimu aliyewakomboa.Kitabu kinaeleza kuhusu nyakati 7

za ku­jiuzulu, nyakati 7 za utumwa na 7 za kuwekwa huru.

Waisraeli walianza kumsahau Mungu polepole. (Amu 3:12-14)

Farao Amenhotepi IV, yaani Ekhnaton, alitawala nchi ya Misri (1370-1352).

Mama malkia Teje. Mke Nefertiti.

1368 K.K.

Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia aliwatesa wana wa Israeli. (AMU 3:8)

1360 K.K.

Kijana wa ndugu yake Kalebu, Othnieli aliwapa uhuru Waisraeli. (AMU 3:10) Othnieli akiwa

mwamuzi.

Amani miaka 40.

Waamuzi walitawala sehemu mbali mbali za Israeli, na wachache kwa wakati moja.Ndiyo maana

miaka inalaliana na hata hivyo hatuna uhakika na miaka kamili. (AMU 3:10)

1320 K.K.

Egloni mfalme wa Moabu aliwatesa wana wa Israeli. Na aliteka mji wa Mitende, yaani Yeriko.

(AMU 3:12-14)

1302 K.K.

Ehudi Mbenyamini mwenye mkono wa kushoto, aliwapa uhuru Waisraeli, na alimwua mfalme

Egloni. (AMU 3:15-30) Ehudi akiwa mwamuzi na baada yake Shamgari. Wakati wa amani

ulichukua miaka 80. (AMU 3:31)

1222 K.K.

Mfalme aliyetawala kaskazini mwa Palestina mfalme wa Kanaani Yabini pamoja na mkuu wa

jeshi Sisera, waliwatesa wana wa Israeli. (AMU 4:1-3)

1202 K.K.

Baraka aliondoka kwenda kupigana na Sisera baada ya kuambiwa na hakimu wa kike nabii

Debora. Israeli ilipata uhuru. (Amu 4:4-24) .Wimbo wa Debora. (Amu 5).Amani ilikuwepo

miaka 40. (Amu 5:31)

1162 K.K.

Page 35: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

35

Wamidiani waliwatesa Waisraeli. (Amu 6:1-6), Gideoni, yaani Yerubaali, aliwashinda

Wamidiani akiwa na wanajeshi 300. (Amu 6:11-7:25), Abimeleki, mwana wa Gideoni, alikuwa

mfalme. (Amu 9). Tola alikuwa mwamuzi miaka 23. (Amu 10:1,2). Yairi alikuwa mwamuzi

miaka 22. (Amu 10:3-5) Wana wa Israeli walimkosea tena Mungu. Waliabudu Baali na

Ashtorehti na miungu mingine. Mungu akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamori kwa

miaka 18. Waisraeli walimlilia Mungu. (AMU 10:6-18)

Waamuzi 12 Wa Israeli!

1. OTHINIELI

Mwana wa Kenazi,ndugu mdogo wa kalebu.

2. EHUDI

Mwana wa Gera,mbenjamini;mtu wa shoto

3. DEBORA+BARAKA

Nabii mke;mwana wa Abinoamu

Yaeli, mkeni, shemeji Wa mbari ya Musa aliyemuua Sisera!

4. GIDEONI

(Yuribaali);kabila ;manase.

5. YEFTHA

Mgileadi;mtoto wa nje!( mama Wa nyumba ndogo)

6. SAMSONI

Kabila;Dani.

7. SHAMGARI

Mwana wa Anathi

8. TOLA

Mwana wa Pua,mwana wa Dodo;kabila Isakari

9. YAIRI

Mgileadi

Page 36: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

36

10. IBZANI

Bethlehemu

11. ELONI

Zabuloni

12. ABDONI

Mwiefraimu

Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya yaliyokuwa ni mema machoni

pake mwenyewe.

Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi

kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua BWANA, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa

ameitenda kwa ajili ya Israeli.

hakikisha unasoma,kwa ajili ya kizazi baada yako! Unawarithisha kumjua Mungu zaidi yako!

ikiwa wewe ulifanya 10% kwa kumtumikia Mungu,yeye ajae baada yako afanye 100%, na yule

amfuatae afanye 1000% !nakutakia maandalizi mema ya mpango huu!

Page 37: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

37

MUHTASARI WA KITABU CHA RUTHU.

Kina sura 4.

Kina aya/mistari 85

Mwandishi:

Mwaka Wa uandishi:

Ruthu maana yake ni Urafiki,ushirika!

habari za Bibi Wa Mfalme Daudi.

Kuna vitabu viwili katika Biblia wahusika wake wakuu wakiwa wanawake ambayo NI Ruthu na

Esta. Japo 👇Ndani ya Biblia kuna habari nyingi zihusuzo wanawake mashujaa,waliofanya vitu

vya ajabu hadi kuishangaza dunia ya wakati wao,wanawake hawa Ruthu na Esta wamepewa

upendeleo maalum kwa vile walivyokuwa! Mfano Esta alikuwa yatima akilelewa na Mjomba

wake Mordekai,Esta akiwa katika nchi ya ugeni yaani Uajemi,Ruthu alikuwa mjane akilelewa na

mamamkwe wake Naomi,akiwa nchi ya ugeni Israeli.

Tukio hili lilitokea kipindi cha mwishoni cha waamuzi Wa Israeli,walipokuwa wanarudia rudia

kumwasi Mungu na kuabudu miungu mingine Mungu aliruhusu madhara kama kuchukuliwa

utumwani,kutawaliwa kwa mabavu na kutokea kwa baa la njaa!

Mambo yalikuwaje?

Pengine Elimeleki ( Mungu wangu ni mfalme)na mkewe Naomi (utamu wangu) watu wa

betlehemu ya Yuda, pamoja na watoto wao 2, Maloni (ugonjwa) na Kilioni (wakupotea)

Walifikiri hukumu ya Mungu aliyoikusudia kuwatenda Isreali kwa kuwapiga kwa njaa baada ya

kumwasi na kwenda kuabudu miungu ya wakaanani,wanaweza kuiepuka kwa kwenda inchi ya

jirani[Moabu] yenye chakula wakaishi bila shida.

Tutambue kuwa dawa ya dhambi ni kutubu sio kuikimbia adhabu; baada ya kufika huko

Elimeleki, akafa Naomi akawa mjane kisha Maloni akaoa mke wa nchi ile,Orpa(shingo ngumu)

akafa akaacha mjane,naye Kilioni akaoa vilevile mmoabu,Ruthu(rafiki) naye akafa kabla ya

kupata mtoto.

Hivyo miaka yote 10 Naomi aliyoishi inchi ile hakupata jema lolote bali madhara tu.Hatimaye

habari njema zikamfikia Naomi kuwa Israeli BWANA amewapa chakula,akaazimu kurudi Israeli

akawaaga wakwe zake 2 wajane;Orpa akakubali kubaki katika nchi yake na kuwarudia wazazi

wake lakini Ruthu akataa kabisa. Akamtaka Mungu wa Israeli kuwa Mungu wake na watu wa

Israeli kuwa watu wake na akifa na atazikwa alipozikwa Naomi. Kitabu cha Ruthu kina sura 4 tu,

na sura ya 4 ikionyesha mibaraka ya wazee Wa mji wakimbariki Boazi,nasaba ya Daudi mfalme!.

Page 38: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

38

Wanawake walioonekana kama hawafai kumbe kwa Mungu NI Wa kipekee!

Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu yule aliyekuwa kahaba!; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu;

Obedi akamzaa Yese;Yese akamzaa mfalme Daudi.Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa

Uria;.....akamzaa Yusufu aliyemposa Mariamu, mamae Yesu Kristo!

USHUHUDA WA RUTHU KWA KANISA LA LEO!

Palitokea mama aliyejikuta mjane katika uchanga Wa ndoa yake! Hakika alikuwa akimpenda

mumewe tena sana! Je afanyaje? (Wamoabu)Watu wa inchi yake sio wenye moyo mzuri kama

watu wa inchi ya marehemu mumewe(Israeli)! Hatimaye habari njema zikamfikia Naomi,kuwa

Israeli BWANA amewapa chakula,akaazimu kurudi Israeli akawaaga wakwe zake 2

wajane;Orpa akakubali kubaki katika nchi yake na kuwarudia wazazi wake lakini Ruthu akataa

Kata katu kabisa.! Akajipiga moyo konde akaazimia kuondoka na mama mkwe(Naomi)kurudi

inchi ya Israeli!

"Naye Ruthu akasema,Usinisihi nikuache,Nirejee nisifuatane nawe;Maana wewe uendako

nitakwenda,Na wewe ukaapo nitakaa.Watu wako watakuwa watu wangu,Na Mungu wako

atakuwa Mungu wangu;" akaongeza kwa kusema huku machozi ya uchungu yakimlengalenga

usoni!

"Pale utakapokufa nitakufa nami,Na papo hapo nitazikwa;BWANA anitende vivyo na kuzidi,Ila

kufa tu kutatutenga wewe nami."

Mungu akayasikia maombi ya Ruthu akamjalia kuhurumiwa! Akafika inchi ya Israeli akapata

kibali cha kupata mume mpya yaani Boazi akampa na shamba umasikini wake ukamtoka! na

zawadi ya mtoto, akapata yaani Obedi (alikuwa baba wa Yesse) na aliyekuwa babu yake Daudi

mfalme. Jina lake likapanda chati! Sasa NI mama Obedi! Akaandikwa kwenye Biblia!

Kutoka taifa lisilo kubalika hadi kuingia kwenye orodha ya wanawake waliomleta Yesu duniani!

Wengne akiwa NI Rahabu,.

Ujumbe mkuu Wa Kitabu chake!

Mwanamke uliye yatima,ewe Wanawake mjane,nanyi mliodhulumiwa haki zenu,masikini na

wahitaji! msihofu,msichoke, Mungu yu upande wenu!

Ruthu anamaliza ushuhuda wake kwa kusema wanawake wanaweza wakiwezeshwa na Roho

mtakatifu........!

Page 39: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

39

MUHTASARI WA KITABU CHA KWANZA CHA SAMWELI.

Vitabu vifuatavyo vyatokana na vitabu vikuu 3 kabla ya kugawanya:

I Samuel

II Samuel

I Wafalme

II Wafalme

I Mambo ya Nyakati

II Mambo ya Nyakati

Andiko:

1. Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Mwana lilikuwa adimu

siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri. (1Sam 3:1)

Kiliandikwa mwaka : 1015 K.K

Sura : 31

Aya : 810

WASIFU WA NABII SAMWELI!:

Alikuwa nabii Wa kwanza katika Israeli,Alianzisha chuo cha manabii ktk Israeli

Aliwatia mafuta wafalme 2 Wa Israeli. Alikuwa mwamuzi Wa mwisho ktk Israeli

Alikufa akiwa na miaka 90. mwana Wa Elkana MTU Wa kabila la lawi aliyeishi nchi ya kabila

la Efraimu.(1Sam 1:19-20).Alikuwa kuhani japo Yeye hakutokana Na ukoo Wa Haruni.

Alikuwa nabii. Alikuwa mtawala Wa kisiasa Wa taifa la Israeli. Alitembea Na kuishi kwa muda

katika miji mikubwa 4 ya Israeli akaitisha mikutano huko Na kutatua matatizo yao.(1 Samw

7:15-17) Alianzisha chuo cha manabii,mjini Rama.Na baadae Betheli,Yeriko Na Gilgali.(1Samw

19:18-20). Aliwatia mafuta wafalme 2 ; Sauli Na Daudi. Sauli akiwa bado hajaachia madaraka!

Alikuwa ni MTU pekee aliyekuwa Na huduma 3 kwa wakati mmoja! Mwamuzi,nabii Na kuhani.

Alikuwa Na watoto 2; Yoeli Na Abia walioshindwa kusimama vizuri katika nafasi zao! Kama

waamuzi walipendelea watu Na kupokea rushwa!. Hermani mwana Wa Yoeli,mjukuu Wa

Samweli ndie mwandishi Wa Zaburi ya 88. Aliitwa pia muonaji.

Alipokufa aliamshwa katika roho ili azungumze Na Sauli. Katika vitabu vya Samweli kuna

wahusika wakuu watatu: Samweli, Sauli na Daudi.

Page 40: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

40

Samweli alikuwa kiongozi wa mwisho wa­kati wa mahakimu na pia nabii wa kwanza

aliyejulikana. Sauli alikuwa mfalme wa kwanza Israeli na Daudi mfalme mkubwa na mpendwa

zaidi. Samweli alipopata wito, hali ya kiroho huko Israeli ilikuwa mbaya. Ukuhani wa kiroho

ulikuwa umezorota, sanduku la agano limeibiwa lakini baa­daye likawa limerudishwa tena.

Makuhani waliacha kazi zao na watu walikaa katika hali ya kusikitikia hasara yao. Anguko la

watu lilisababishwa na­kumwacha Mungu kama mfalme na walitaka wanadamu badala yake

kuwao­ngoza. Walimpata Sauli. Hivyo miaka mia 500 ya utawala wa ki­falme ulianza Israeli.

Sauli pia alimwacha Mungu, ndipo Mungu alimwita Daudi badala yake. Wakati wa Daudi hali

ya watu kiroho ilianza kuinuka tena. Ndani ya vitabu kuna maelezo mengi ya kihisto­ria na

matukio lakini zaidi pia kuna mifano na mafundisho. Mwandishi Samweli ali­kusanya sehemu

ya maelezo na walio­kuwepo wakati wa Daudi walikusanya baadhi.

Matukio yalichukua miaka 103 hivi!

Watoto wawili wa Eli waliokuwa waovu sana ni:Hofu/Hophni na Finehasi/Phinehas. Sanduku la

Agano lilikaa Kwa wafilisti miaka 20.Wafalme 3 waliotawala Israeli kabla ya kugawanyika kwa

muda Wa miaka 40 kwa kila mmoja ni Sauli, Daudi, na Sulemani. I Samweli ameonesha namna

Israeli walivyokataa utawala wa Mungu theocracia kuja monarchy/utawala Wa kifalme!

Maana ya majina

Samweli: "aliyesikiwa/alieulizwa kwa Mungu"

Ikabod - Utukufu umeondoka

Eben-ezeri = Jiwe la msaada.hata sasa Bwana ametusaidia!

Hana = Aliyerehemiwa

Sauli = Aliyeombwa

Eli = Mungu

Swali kuu!

1. Wana Wa Israeli walikua na kosa gani walipodai mfalme?

2. Je inawezekanaje mganga Wa jadi amfufue Samweli?

Soma kwa tafakari ya kina!

Page 41: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

41

MUHTASARI WA KITABU CHA PILI CHA SAMWELI.

Kina sura 24

Kina aya/mistari 695

Mhusika mkuu akiwa Mfalme Daudi.

Kitabu cha 2 cha Samweli kinaeleza wa­kati wa utawala wa mfalme Daudi, yaani 1012-972 K.K.

1012-972 K.K.:Kilichukua miaka 40.

Mwamaleki kijana alimwua Sauli, aliyeumia wakati alipojaribu kujiua. (2SAM 1:5-10)

Daudi alifanywa mfalme wa Yuda. (2SAM 2:4)

Ishboshethi mwana wa Sauli akawa mfalme juu ya sehemu ingine ya Israeli. (2SAM 2:8-10)

Wasifu Wa Daudi:

Alitawala kwa miaka 40; miaka 7 na nusu alitawala Yuda wakati huo mji mkuu ulikuwa

Hebroni,miaka 33 alitawala Israeli yote, mji mkuu ukiwa Yerusalemu! Sauli alifanya vita vya

kujilinda( defensive) na Daudi alifanya vita vya mashambulizi(offensive) ili kuongeza himaya ya

mipaka yake! Alisimama katikati kati ya Ibrahimu na Masihi.Daudi ndie mfalme pekee

aliyempendeza Mungu kutoka Ndani ya moyo wake! Ametumika kama standard ya Wafalme

wote waliotawala Yuda na wale waliotawala Israeli. Mungu alifanya nae agano kuwa hatakosa

mzao wa kukikalia kiti cha ufalme hadi waliporudi kutoka Babeli,Yuda hawakutawaliwa tena na

wafalme Bali na mataifa kama Umedi na Uajemi,Uyunani na Rumi.

Aliandika na kutunga Zaburi nyingi ktk Biblia.

Jifunze kuongozwa na kumtegemea Mungu!

Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Niupandie mji wo wote wa

Yuda? BWANA akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema,

Hebroni.

Chagua kumkimbilia Mungu hata kama anakuadhibu!

Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika

mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa

wanadamu.

Page 42: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

42

Moyo Wa Daudi !

Daudi, alipomwoma malaika aliyewapiga watu, akanena na BWANA, akasema, Tazama, ni

mimi niliyekosa, ni mimi niliyepotoka; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako na

uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya baba yangu.

Kumbukumbu!

1010 K.K.

Ishboshethi aliuawa. Daudi aliwaadhibu wauaji.

1005 K.K.

Daudi aliwekwa kuwa mfalme juu ya Israeli yote. Yerusalemu ikawa mji mkuu. (2Samweli 5:3,

1NYA 11:1-3)

980 K.K.

Absalomu mwana wa Daudi alijaribu kuchukua utawala kwa njia ya vurugu.(2Sam 15-18)

973 K.K.

Rehoboamu, mwana wa Sulemani alizaliwa. (2Nya 12:13)

972 K.K.

Sulemani alikuwa mfalme. (1Falme 1, 1Nya 29:28)

Daudi alikufa. (1Falme 2:10, 1Nya 29:26-28)

KITABU CHA PILI CHA SAMWELI kilimalizika.

Page 43: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

43

DAUDI MTU SHUJAA NA MASHUJAA WAKE!

FURAHA YA KULITIMIZA KUSUDI.

Utangulizi.

"Hakuna jema kupita kufurahi na kufanya mema kwa kupatia! maadamu tunaishi"

Daudi pamoja na kumiminiwa mafuta kuwa Mfalme wakati ule Samweli alipomtawaza mbele ya

Yese na ndugu zake,mambo hayakwenda kwa mstari ulionyooka,Bali kwa kupindapinda sana!

Ooh! Kumbe alitakiwa kwanza aingie darasa la Mungu ili afuzu kuwa Mfalme yule Mungu

amtakae! Sauli alipokufa,Daudi alitawazwa kuwa Mfalme Wa kabila la Yuda huko Hebroni kwa

miaka 7 na nusu!

Wakati huo Ishiboshethi mwana Wa Sauli alikuwa Mfalme miaka 2 pande mwingine Wa Israeli!

Huku kukiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi pale Abneri jemedari wa Sauli,na

Ishiboshethi walipouwawa!.(Kwa maana; Ishiboshethi alimkemea Abneri kwa kumuoa suria wa

babae{Sauli},Abneri akachukia,akamwasi Ishiboshethi,Abneri akamuua Asaheli nduguye

Yoabu,kwenye vita ya Gibeoni, Yoabu akamuua Abneri)

Israeli wote wakamfanya Daudi kuwa Mfalme. Kulikuwa na upako Wa uhakika!,wingu la

kukubalika(kibali) juu ya Daudi tangu ujana wake lakini hakufanya haraka kuutwaa ufalme!

"Naye Daudi akaendelea, akazidi kuwa mkuu; kwa maana BWANA wa majeshi alikuwa pamoja

naye".

Hebu tuangalie kikosi kazi; Bwana alichompatia Daudi na jinsi kilivyokuwa cha kipekee yaani.

Ni balaa! Mashujaa wa Daudi na Ushindi wao!

Yoabu mwana wa Seruya,

alikuwa jemedari mkuu wa majeshi ya Daudi.Alikuwa mtoto wa dada yake Daudi (alimwita

Daudi mjomba).Ndiye aliyeuteka mji Wa Yerusalem uliokuwa na ngome imara ya wayebusi,

isiyowezekana kushambuliwa kirahisi.Yashobeamu, Mhakmoni, mkuu wa maakida; aliuinua

mkuki wake juu ya watu 300,(maadui) akawaua pamoja.Aliinua shoka lake juu ya watu

800,(maadui)akawauwa kwa pamoja!

Kama hiyo haitoshi vita vya mashambulizi na kujihami,watu Wa kazi maalum za unyeti,wenye

vifua vya kutunza uaminifu na siri za taifa!. Hawa ndio! Alikuwa na watu maalumu mashujaa 3

ambao ni;

Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi,

mmojawapo wa mashujaa 3.

Page 44: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

44

Aliwapiga wafilisti hadi mkono wake ukachoka na mkono wake ukaambatana na upanga! Maana

Israeli waliowagopa wafilisti wakakimbia wakamwacha peke yake! Ikabidi warudi kuja kuteka

nyara tu!

Abishai, nduguye Yoabu, alikuwa mkuu wa hawa 3;

kwa kuwa aliuinua mkuki wake juu ya watu 300, akawaua;

Benaya, mwana wa Yehoyada,

mtu hodari,alifanya mambo makuu, aliwaua simba wakali 2 wa Moabu; alimwua simba katikati

ya shimo wakati wa theluji. alimwua Mmisri, mtu mrefu sana, aliyekuwa wa dhiraa 5 urefu

wake;(Jitu) huyo Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi; lakini yeye

akamshukia na gongo la mti, akautwaa ule mkuki mkononi, akamwua kwa mkuki wake

mwenyewe.!.....NI shidaa! Mambo haya ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada,

akawa na jina kati ya hawa mashujaa 3 .

Aliwekwa kuwa mkuu wa walinzi wake!

hawa walimfuata Daudi pangoni,alipokuwa anawindwa na Sauli,walipenya ngome hatari ya

wafilisti wakaenda hadi kisima cha Bethlehemu kumchotea Daudi maji ya kunywa japo Daudi

alipoyapokea alikataa kuyanywa!

Baada ya hao mashujaa 3 alikuwa na kikosi cha kuogopwa na wafalme wote Wa nchi jirani. Kwa

kuwa Alikuwa na mashuja 30 wenye kuvijua vita na wepesi Wa mashambulizi za ghafla kwa

adui!

Wakiwemo

Asaheli nduguye Yoabu ambaye Abneri alimuua.

Uria Mhiti ambaye Daudi alimfanya afe vitani ili amchukue mke wake!

ndio maana ilimpasa kulipwa kisasi Mara 4 (watoto wake:Amnoni,Absalomu,Adonia na mtoto

yule wa kwanza kabla ya Sulemani) kutokana na damu ya Uria.

Jumla ya mashujaa wote walikuwa 37. (2 Sam 23:39)

Zaidi ya hao 30 bado Mungu alimpatia askari hodari na wenye uwezo mkubwa juu ya vita

vyovyote vile!

Wa Benyamini. Walikuwa wenye kupinda upinde, walikuwa hodari wa kutumia mkono wa

kuume na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, kwa kupiga mishale ya upinde; Walikuwa na

uwezo wa kuutupia unywele mawe kwa teo, ( kwa kombeo) wala asikose. Watu wa kabila la

Page 45: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

45

Gadi,waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; nyuso zao

zilikuwa kama nyuso za simba, walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;

walikuwa maakida wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa

mkuu, na elfu.Wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli

wayatende; vichwa vyao walikuwa watu 200 ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.

Wa Zabuloni,

watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita za kila

namna, askari wastadi wasiokuwa na moyo wa kusita-sita.watu wa vita, 50,000; askari

wastadi,(1Nyakat 11-12)wakaja Hebroni wenye moyo mkamilifu, ili kumtawaza Daudi awe

mfalme juu ya Israeli wote; tena wote waliosalia wa Israeli nao walikuwa na moyo mmoja

kwamba wamtawaze Daudi kuwa mfalme kwa miaka ile 33 na nusu. aliyoitawala Israeli yote!

Miaka yote Daudi aliyotawala ilikuwa miaka 40 yaani kuanzia mwaka 1010-970 K.K

Je wewe NI shujaa katika jambo gani?

Je wewe u hodari katika lipi?

Ikiwa kuna kusudi uliloumbiwa kabla ya kuzaliwa hilo ukilifahamu ndilo hasa utakuwa shujaa,

ukifanikiwa kulitimiza!

Kumbuka!

Amelaaniwa aifanyae kazi ya Bwana kwa ulegevu!

Lolote mkono wako ulipatalo kulifanya Fanya kwa bidii! Maana kila jambo lina majira yake,na

kila kusudi lina wakati wake! Tafadhali okoa muda! ufalme Wa Mungu unatekwa na wenye

nguvu! Na wenye nguvu huutwa kwa fujo. Nakuona sifa zako zikivuma kwa siku zijazo!

Mungu na atufadhili na kutubariki,Na kutuangazia uso wake.! Amina!

Page 46: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

46

MUHTASARI WA KITABU CHA WAFALME.

VITABU VYA WAFALME

Kuna vitabu viwili ambavyo kwa wayahudi kilikuwa kitabu kimoja cha Wafalme!. Kitabu cha

kwanza cha WAFALME na Kitabu cha pili cha WAFALME.

Vitabu vya Wafalme ni endelezo ya vitabu vya Samweli. Kadri ya jina vitabu vinaeleza kuhusu

uta­wala wa Daudi, Sulemani na wa­falme wa Yuda na Israeli. Utawala ulichukua kipindi cha

miaka 400 na inaeleza kukua na kuanguka kwa utawa­la.

Wayahudi wanamfahamu nabii Yeremia kama mwandishi wa vitabu hivi.

Kina sura 22.

Mistari/aya 816.

Mwaka Wa uandishi: 561-538 K.K

Mwandishi; Yeremia,na kundi la manabii!

Wahusika wakuu:

Kifo cha mfalme Daudi,uasi wa Adonia,utawala Wa Sulemani,Rehoboamu,Yeroboamu,Eliya na

matengenezo.

Wakati wa Kitabu cha kwanza cha WAFALME ni 971-851K.K.

Wakati wa matukio haya ulichukua kama miaka 120.

Kuanzia utawala Wa Sulemani hadi utawala Wa Ahazi.

Sura 11 za mwanzoni zikimweleza mfalme Sulemani,ujenzi Wa hekalu,jumba lake na hekima

yake!

Mnamo mwaka 931 K.K utawala Wa Rehoboam mwana Wa Sulemani uligawanyika na kuwa

ufalme mbili!

Ufalme Wa kaskazini (Israeli) wenye makabila 10.

Ufalme Wa kusini(Yuda) wenye makabila 2.

Pia tunaona Yuda na Israeli walivyo pe­lekwa uhamishoni. Utawala wa kusini, yaani Yuda,

ulikuwa na wafalme 20 na utawala wa kaska­zini, yaani Israeli, walikuwepo 19 kutoka koo 9

tofauti. Uhamisho ulitokana na kutokutii. Eliya na Elisha pia wanapatikana kama manabii wenye

nguvu.

Page 47: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

47

BWANA akamwambia Eliya;

mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu.Japo NI taifa hilo sio taifa teule,Mungu ana kazi ya

kuganya kupitia mtumishi wake Hazaeli.Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme

wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.

Nabii Eliya ni nabii pekee aliyewatia mafuta wafalme 2 wasio uzao Wa kifalme kuwa wafalme!

Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa

Yehu, Elisha atamwua.Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu 7,000, kila goti

lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu. Ufalme Wa Israeli ulichukuliwa utumwani

na mfalme Shalmanesa Wa Ashuru mwaka 722 K.K baada ya kuunusuru Samaria miaka 3. Na

baada ya miaka 135 hivi ufalme Wa Yuda ukachukuliwa utumwani Babeli chini ya Nebukadreza

mwaka 586 K.K.

Muda wa Kitabu cha pili cha WAFALME: 853-562 K.K. Ilichukua muda kama miaka 291.

Jumla ya miaka Vitabu vya WAFALME ni kama miaka 410.

Hata mwezi wa 5, siku ya 7 ya mwezi, ndio mwaka wa 19 wa mfalme Nebukadreza, mfalme wa

Babeli, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia

Ye­rusalemu.

Akaiteketeza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam,

kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.

Na jeshi lote la Wakalda­yo, waliokuwa pamoja na huyo amiri wa askari walinzi, wakazibomoa

kuta za Yerusalemu pande zote. (1Falm 25:8-10)

Vitabu vya WAFALME vinaanza kwa ujenzi wa hekalu na kunamali­zika kwa kuchomwa

kwake.!

Page 48: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

48

HABARI ZA MFALME SULEMANI!

Yeyedidia( rafiki wa Bwana)lilikuwa jina la kwanza alilopewa Sulemani na nabii Nathani,Bath-

sheba alikuwa ndie mamae,Daudi alimwita, Sulemani maana yake "Utulivu" baba yake Wa

kambo alikuwa Uria,Mhiti,askari Wa Daudi. Aliyeuwawa kwa mkono wa Daudi ,vitani.

Alianza kutawala kama mfalme Wa 3 kwa miaka 40 juu ya Israel,Daudi babae yuko ukingoni

kumaliza safari yake ya maisha! Alifundishwa utoaji na akapewa mausia yote ya kuwa mtawala

bora Wa millennia! Kama sio karne!,alianza vema kwa kuomba hekima! Akapewa

hekima,utajiri,heshima na amani,hakuwa na adui yeyote!

Utukufu wa Utawala wa Sulemani

Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi wao huku wakila, na

kunywa, na kufurahi.alikuwa na amani pande zake zote. Yuda na Israeli wakakaa salama, kila

mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za

Sulemani.

vyakula vya Sulemani vya siku 1: yaani menyu yake ya siku, ilikuwa kori/pipa 30 za unga mzuri,

na kori/pipa 60 za ngano,ng’ombe 10 walionona, na ng’ombe 20 za malisho, na kondoo 100,

pamoja na ayala, na paa, na kulungu, na kuku walionona!

alikuwa na mabanda ya farasi 40,000 kwa magari yake, na wapandao farasi 12,000.

Kulikuwa na zamu ya akida 1, kwa kila maakida 12 kwa kati ya majimbo 12 wakuleta chakula

kwa mfalme na kwa wageni wote walioalikwa kuja kula mezani mwa mfalme, kila mtu katika

mwezi wake, kisipunguke kitu.

Shayiri na majani kwa farasi, na kwa wanyama wenye mbio, wakaleta mahali walipokuwapo,

kila mtu kwa kadiri ya kazi yake. Na walimletea tunu!

Sifa za Hekima ya Sulemani

Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko

pwani.Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote

yaliyozunguka.

alinena mifano 3,000, na nyimbo 1005.aliandika vitabu 3 katika Biblia yaani Mithali,Mhubiri na

wimbo ulio bora pamoja na moja ya zaburi.Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko

Lebanoni hata hisopo umeao ukutani;(macro to micro organisms) akanena habari za wanyama,

na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. Katika kitabu chake cha MITHALI,tunaweza kuona

baadhi ya mifano yake iliyojaa busara

Page 49: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

49

mfano; "jiwe ni zito na mchanga hulemea,lakini hasira zake mpumbavu huvizidi hivi vyote

viwili".

malkia Wa Sheba alipokuja kuisikiliza hekima ya Sulemani na kuona kwa macho yake mawili

maajabu haya akazimia palepale!enzi za ujana wake akampenda mwanawali, na akiwa katika

uchumba na katika fungate la ndoa yake akaandika wimbo maridadi kabisa ulioitwa WIMBO

ULIO BORA katika ubora wake! Yaani wimbo unaoeleza kwa kina na mapana ya upendo wa

wapenzi 2 waliopendana! alipokuwa katika uzee wake akaona namna alivyofanya

upumbavu,wazimu na kuifanya siku zake kukosa maana baada ya kumwacha Mungu! Akaandika

kitabu cha mausia yaani MHUBIRI!

UJENZI WA HEKALU.

Mnamo mwaka 1446 K.K wana Wa Israeli walitoka Misri,wakafika mlima sinai wakatengeneza

na kujenga Hema ya kukutania(hekalu la kuhamishika) sasa wanajenga hekalu la lisilo

hamishika!

Ilipita 430 baada ya wana Wa Israeli kutoka Misri,ktk mwaka Wa 4 Wa utawala Wa Sulemani

mwaka ule Wa 966 K.K mwezi Wa 2 (Zivu) siku ya 2 juu ya kilima cha moria, alianza Kulijenga

hekalu lililochukua miaka 7 kumalizika!

Akaliweka wakfu kwa kutoa hotuba ndefu ya hali ya juu huku akitoa sadaka maelfu za

kuteketezwa!ndie anayefanya wayahudi wasalipo wasali kuelekea Yerusalemu ilipo!Alijenga

jumba lake la kifahari lililochukua miaka 13 kumalizika! Kujenga hekalu na jumba lake

ilichukua miaka 20!

UMAARUFU WA BIASHARA YA SULEMANI.

Uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani kwa mwaka mmoja, ndio talanta 666; yaani tani 23.

Ilizidi faida za wachuuzi, na bidhaa ya wafanya biashara,za wafalme wote kwa ujumla wao, na

za maliwali wa nchi. Alifanya ngao 200 za dhahabu iliyofuliwa; kila ngao moja ilipata shekeli

600(kilo 3.5) za dhahabu.Na vigao 300 vya dhahabu iliyofuliwa; kila kigao kimoja kilipata mane

3 (kilo 1.7) za dhahabu. aliviweka katika nyumba ya mwitu wa Lebanoni.

na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, hesabu yake

ya mwaka kwa mwaka.Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, magari na wapandao

farasi; naye alikuwa na magari 1400, na wapandao farasi 12,000, aliowaweka katika miji ya

magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. fedha humo Yerusalemu ilikuwa kama mawe,

mierezi akaifanya kuwa mingi kwa wingi wake, farasi aliokuwa nao wakapewa wafanya biashara

wake mfalme kwa makundi, kila kundi na thamani yake. Vyombo vyote vya kunywea,vilikuwa

vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu

iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani. Alikuwa na

Page 50: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

50

merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara 1, katika miaka 3 huja

merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.

Biashara ilikuwa kati gari 1, kutoka Misri kwa shekeli 600 za fedha, na farasi 1, kwa shekeli 150;

kiti chake cha enzi kilifanywa kwa dhahabu safi.,kilikuwa na daraja/ngazi 6; na mikono huko na

huko mahali pa kuketi, mfano wa simba 2 wakisimama kando ya hiyo mikono. Zaidi sana

kulikuwa na mfano wa simba 12 juu ya daraja 6 huko na huko, wakati ukishuka/kupanda kwenye

ngazi hizo!

Alijenga miji mingi, alijenga ukuta Wa Yerusalemu akaongeza eneo lake la mraba!,

Kulikuwa na watumwa/shokoa (forced labour) Wa kuijenga hekalu, na ikulu, na Milo, na ukuta

wa Yerusalemu, na miji ya Hazori, na Megido, na Gezeri. Maakida wakuu, 550, walikuwa juu ya

kazi, waliwaamuru watu watende kazi.

MAMBO YA BINAFSI.

Alijenga Milo, jumba la kifahari la mke wake,binti Wa farao! (nyumba ya mwitu wa Lebanoni)

alikuwa na wake 700 na Masuria(nyumba ndogo) 300. Jumla wake 1,000 je hakuvunja Torati?

Ni majina 3 tu ya watoto wake yametajwa katika Biblia,Pengine wingi Wa watoto wake

walikosa vigezo na umuhimu wao katika maandiko,ila inawezekana wake zake walikuwa watoto

Wa wafalme,vigogo,watawala maarufu Wa nyakati zile hawakuishi wote, Yerusalemu Bali kwa

nchi hizo walizotoka!

SABABU KUSHINDWA KWA SULEMANI.

Hakutumia hekima yake kila eneo la Maisha yake. Aliruhusu tamaa imwendeshe,alikosa

kujizuia,kuwa na nidhamu binafsi juu ya starehe. Hakuishi kwa busara kama watu wengine

waaminifu kwa Mungu kama Daudi, Samweli, Ibrahimu.

Bora mwisho Wa jambo kuliko mwanzo Wa jambo! Unajifunza nini juu ya Maisha ya Sulemani?

utajiri Wa Sulemani?,Anasa na starehe alizosifanya? Je nini maana ya andiko hili?

"Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia ktk ufalme Wa Mungu"!

Je Sulemani kuwa tajiri sana NI kosa?....lakini utauwa na kuridhika NI faida kubwa sana!

Yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo

yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani? Historia ndefu ya hayati marehemu

Mfalme ikaisha!

Sulemani akafa, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala

mahali pake.!

Page 51: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

51

UFALME WA ISRAELI.

Utawala Wa Sulemani ulimalizika kwa kugawanyika taifa la Israeli lililokuwa limeshaongozwa

na wafalme 3(Sauli,Daudi, Sulemani) kwa kipindi cha miaka 40 kila mmojawao! Mtoto Wa

Sulemani Rehoboamu aliharibu mambo alipowakwaza wananchi wake!,akabakiwa na makabila

2 kati ya 12; makabila 10 yakajianzishia utawala wao! Mfalme Sulemani katika uzee wake

akasema!

"Kwa hiyo nikageuka kukata tamaa moyoni mwangu juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha

nayo chini ya jua. Maana kuna mtu ambaye kazi yake ni kwa hekima, na kwa maarifa, na kwa

ustadi; naye atamwachia mtu asiyeshughulika nayo kuwa sehemu yake. Hayo tena ni ubatili,

nayo ni baa kuu.(Mhubiri 2:20-21). Mungu hatazami kama mwanadamu,hatazami kwamba ni

mzaliwa Wa kwanza ama Wa mwisho!,hutazama moyo! Utaratibu Wa kutawala wafalme kwa

kurithi kiti cha ufalme kizazi hadi kizazi ulishindwa kutoa suluhu ya matatizo ya

kiutawala,alipotawala mfalme mzuri,haikusababisha mwanae awe mzuri!

Rehoboamu aliharibu mambo mazuri aliyoyafanya watangulizi wake(kile Sulemani alichokuwa

anakiogopa kikampata!). ila kutokana na ahadi ya Mungu kwa Daudi, na kazi za Sulemani

zikamfanya apate neema ya kubaki na makabila 2 ( Yuda na benjamini).

Utawala uligawanyika:

Israeli ya Kaskazini, na Israeli ya Kusini, yaani Yuda.

Ufalme Wa Israeli uliongozwa na wafalme 19 kutoka koo 9 tofauti,sehemu yao ya

kuabudu(ndama) ilikuwa Betheli.

931-722 K.K.

Wafalme wa Israeli ya Kaskazini:

1.Yeroboamu I, (931-910 K.K.)

alikuwa mfalme Israeli ya kaskazini miaka 22. Alifanya mabaya. (1FAL 12:20-14:21)

Manabii wakati wa Yeroboamu: Mtu wa Mungu (Yeddo?) (1FAL 13:1-32). Ahia. (1FAL 14:2-

18).

2.Nadabu, (910-909 K.K.)

mwana wa Yeroboamu, alikuwa mfalme miaka 2. Alifanya mabaya. (1FAL 14:20, 15:25-28)

3. Baasha, (909-886 K.K.)

Mwisakari, alimwua Nadabu, akawa mfalme miaka 24. Alifanya mabaya. (1FAL 15:27-16:6)

Nabii alikuwa Yehu.

Page 52: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

52

4. Ela, (886-885 K.K.)

mwana wa Baasha, alitawala miaka 2. Alifanya mabaya. (1FAL 16:6-10,13,14) Nabii alikuwa

Yehu.

5. Zimri, (885 K.K.)

alikuwa mfalme siku saba. Alimwua Ela. Aliua jamaa yote ya Baasha. Alifanya mabaya.

Alijiunguza na moto hadi akafa. (1FAL 16:9-20)

6. Omri, (885-874 K.K.)

alitawala miaka 12. Alianzisha/mwasisi wa Samaria. Alifanya mabaya zaidi ya wale

waliotangulia.

(1FAL 16:16-28)

7. Ahabu, (874-853 K.K.)

mwana wa Omri, alitawala miaka 22. Mke wake Yezebeli. Ahabu aliabudu Baali. Alifanya

mabaya. (1FAL 16:28-22:40) Wakati wake, nabii Eliya alitabiri.

8. Ahazia, (853-852 K.K.)

mwana wa Ahabu, alitawala miaka 2. Alifanya mabaya. (1FAL 22:51-53)

9. Yoramu, (852-841 K.K.)

mwana wa Ahabu, alitawala miaka 12. Alifanya mabaya.

Manabii Mikaya mwana wa Imla na Elisha walikuwa manabii wakati wa Yoramu.

(2FAL 3:1-, 6:26-7:20, 8:28-, 29, 9:15-24)

10. Yehu, (841-814 K.K.)

alitawala miaka 28. Aliteketeza jamaa ya Ahabu. Akafutilia mbali kuabudu Baali.

Nabii alikuwa Elisha. (2FAL 9-10)

11. Yehoahazi, (814-798 K.K.)

mwana wa Yehu, alitawala miaka 17. Alifanya mabaya. (2FAL 13:1-9)

12. Yehoashi, (Yoashi) (798-782 K.K.)

mwana wa Yehoahazi, alitawala miaka 16.

Page 53: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

53

Alipigana na mfalme wa Yuda Amazia na alimshinda. Alifanya mabaya.

(2FAL 13:9-25, 14:8-16)

13. Yeroboamu II, (782-753 K.K.)

mwana wa Yehoashi , alitawala miaka 41. Alifanya mabaya.

(2FAL 14:16, 23-29) Manabii walikuwa Yona, Amosi na Hosea.

14. Zekaria, (753-752 K.K.)

mwana wa Yeroboamu alitawala nusu mwaka. Alifanya mabaya. (2FAL 15:8-11)

Nabii alikuwa Hosea.

15. Shalumu, (752 K.K.)

alitawala mwezi 1. Alimwua Zekaria. (2FAL 15:10-15) Nabii alikuwa Hosea.

16. Menahemu, (752-742 K.K.)

alitawala miaka 10. Alimwua Shalumu. Alifanya mabaya. (2FAL 15:14-22) Nabii alikuwa Hosea.

17. Pekahia, (742-740 K.K.)

mwana wa Menahemu, alitawala miaka 2. Alifanya mabaya. (2FAL 15:23-26).Nabii alikuwa

Hosea.

18. Peka, (740-732 K.K.)

alitawala miaka 20. Alimwua Pekahia. Alifanya mabaya. (2FAL 15:25-30) Nabii alikuwa Hosea.

19. Hoshea (732-723/722 K.K.)

alikuwa mtawala wa mwisho wa Israeli ya kaskazini. Alitawala miaka 9. Alimwua Peka.

Alifanya mabaya. Alichukuliwa mateka Ashuru. (2FAL 15:30, 17:1-6) Nabii alikuwa Hosea.

722 K.K.

Kumalizika kwa Waisraeli walihamia Ashuru.

Angalizo

*Ni vigumu kujua miaka kamili ya utawala wa wafalme wa Israeli ya kaskazini na Yuda pia,

kwani mara nyingi mtoto alianza utawala hata kabla ya kifo cha baba. Hivyo hatuna uhakika na

miaka.

Page 54: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

54

Mwisho Wa historia ya Israeli inaishia ;2 Wafalme sura 17 na 18: inabaki historia ya Yuda.

Mwaka 722: Kuanguka kwa Samaria,mji mkuu Wa Israeli.baada ya kunusuriwa(kuzingirwa)

miaka 3;nabii Eliya,Elisha,Amosi,Hosea na Mika walitoa unabii juu ya hukumu ya mji huo

inayokuja!.

Utumwani kwa Waashuru chini ya mfalme Shalmanesa V (727-722) walipelekwa miji ya

Hala,Habori,Karibu na mto Gozani na ktk miji ya wamedi, wakaletwa watu toka

Babeli,kutha,Ava,Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka ktk miji ya Samaria kujaza nafasi

iliyoachwa wazi baada ya Israeli kuondoka, watu hawa kutokana na kutokumcha BWANA

Mungu aliwapeleka na wanyama mwitu(Simba) wawatafune kama kitoweo!

Mwanzo kizazi chotara, Watu Wa Wasamaria ambao Yesu aliwakuta wasiochangamana na

wayahudi.mfano mwanamke kisimani.

Mnamo 612K.K nabii Nahumu alitoa unabii juu hukumu inayokuja ya taifa la Ashuru, baada ya

Yona kutoa unabii wa mji mkuu Wa Ashuru(Ninawi) ilipita miaka 135 ndipo ufalme Wa Yuda

nao ukapelekwa utumwani Babeli walikokaa miaka 70 na wengine walibaki huko miaka zaidi ya

70.

baada ya dola la waashuru kukosa nguvu na kuanguka,iliinuka dola mpya ya Umedi,ilifuatiwa na

Babeli( Nebukadneza),kisha Umedi na Uajemi(Koreshi),kisha wayunani(Alexanda mkuu),na

mwisho warumi(Pilato& Herode)! Wakati huo Yesu anazaliwa!

Maswali

Je Israeli ya sasa imeundwa na makabila yote 12 au la?

Je enzi za Yesu kulikuwa na kabila zote 12?

Page 55: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

55

UFALME WA YUDA.

Kama misingi ikiharibika,Mwenye haki atafanya nini?

Ni masikitiko na huzuni kubwa pale misingi imara ya waliotangulia inapovunjwa na kizazi

kilichopo kwa maneno rahisi rahisi hujitia moyo bado tunaweza kufanya vizuri kuliko uongozi

uliopita. Mfalme Sulemani alimwacha BWANA akaambatana na miungu migeni,mwanae

Rehoboamu aliyeanza kutawala akiwa na miaka 41, akaoa wake Wachache sana na kwa

waamoni,akaoa, akawa na wake 18,wana Wa kiume 28 Wa kike 60. Akakataa ushauri Wa

wazee,akachukua ushauri Wa vijana! Akalitumbukiza taifa zima la Israeli kwenye dimbi la

kugawanyika kuwa mataifa 2, na vita ya wenyewe kwa wenyewe!

Je Mungu aliposema wasiwe na wake wengi, wasifanye fedha yao kuwa nyingi sana hakuwa

sahihi?Na mambo yote yaliyosalia ya Sulemani,na hekima yake yote je hayakuandikwa kwenye

kitabu cha tarehe cha mambo ya wafalme? Akalala na babaze akazikwa mji Wa Daudi,mwanae

Rehoboamu akatawala mahali pake!

Nabii Ahiya akalishika lile vazi jipya alilokuwa amelivaa, akalirarua vipande kumi na viwili.

Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana BWANA, Mungu wa Israeli,

asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe

kabila kumi, (lakini yeye atakuwa na kabila moja kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi, na kwa

ajili ya Yerusalemu mji ule niliouchagua katika miji yote ya kabila za Israeli);

Ndipo mfalme Rehoboamu akampeleka Adoramu, aliyekuwa juu ya shokoa, nao Israeli wote

wakampiga kwa mawe hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda katika gari, ili

akimbilie Yerusalemu.Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi hata leo.

wafalme 20 Wa ukoo 1 kwa zaidi ya miaka 345. Leo tutaangalia ufalme Wa Yuda!

Wafalme wa Israeli ya Kusini, yaani Yuda: 931-587 K.K.

1. Rehoboamu (kuongezeka kwa watu), (931-914)

mwana wa Sulemani, alikuwa mfalme wa Yuda kwa miaka 17. Alifanya mabaya. (1FAL 12:1-24,

14:21-31, 2NYA 10-12) Nabii alikuwa Shemaya. (1FAL 12:22-24)

925 K.K. Farao Shishaki alitawala Yerusalemu na aliwaibia.Ikawa, mwaka wa tano wa mfalme

Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; akazichukua hazina za

nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao

zote za dhahabu alizozifanya Sulemani.( 1FAL 14:25,26)

2. Abiya(Yehova ni baba yangu), (913-911) k.K

Page 56: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

56

mwana wa Rehoboamu alitawala miaka 3. Alifanya mabaya. (Fal 15:1-8, 2Ak 13:1-14:1) Nabii

alikuwa Iddo.

3. Asa (Mponyaji), (911-870) k.K

Mwana wa Abiya alitawala miaka 41. Alifanya mema. Manabii walikuwa Asaria na Hanani.

(1FAL 15:8-24, 2Ak 14-16)

3. Yehoshafati (Yehova NI mwamuzi),(870-848) k.K

mwana wa Asa,alikuwa na miaka 35 alipoanza kutawala alitawala miaka 25. Mama yake

alikuwa Azuba. Alifanya amani na Israeli. Alifanya mema. (1FAL 22:41-51)

4. Yehoramu/Yoramu(Yehova ametukuzwa), (848-841)k.K

mwana wa Yehoshafati alitawala miaka 8. Mkewe binti wa Ahabu mfalme Wa Israeli.

Alifanya mabaya. (1FAL 22:51, 2FAL 8:16-24) Nabii alikuwa Obadia.

5. Ahazia, (841) mwana wa Yehoramu mwaka 1.

Mama yake alikuwa (Athalia) binti Wa Omri,(baba Wa Ahabu),mfalme Wa Israeli.

Yehu mfalme wa Israeli alimwua. Ahazia alifanya mabaya. (2FAL 8:25-29, 9:16-29)

6. Athalia, (841-835) k.K

Mamaye Ahazia alitawala miaka 6. Alikuwa mtawala mbaya sana. (2FAL 11:1-20)

7. Yoashi (Yehova ametoa), (835-796) k.K

Mwana wa Ahazia alitawala miaka 40. Alifanya mema. (2FAL 12:1-21) Manabii walikuwa

Yoeli na Zekaria.

8. Amazia (Yehova ana nguvu), (796-767) k.K

Mwana wa Yoashi. Alitawala miaka 29. Alifanya mema. (2FAL 14:1-20) Alijiamini sana baada

ya kuwashinda waedomu, akajaribu kupigana na Yehoashi mfalme Wa Israeli akashindwa

vibaya.

Nabii alikuwa Zekaria, Amosi

9. Azaria, yaani Uzia (Yehova ni nguvu zangu), (767-740) k.K

Mwana wa Amazia alitawala miaka 52. Alifanya mema. Aliugua muda mrefu, hakuweza

kutawala mwishoni. (2FAL 4:21,22,15:1-7) Nabii alikuwa Isaya.

Page 57: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

57

10. Yothamu, (750/740-735) k.K

Mwana wa Azaria alitawala miaka 16. Alifanya mema. (2FAL 15:32-38) Manabii walikuwa

Isaya na Mika.

11. Ahazi (anayemiliki) (732-716) k.K

Mwana wa Yothamu miaka 16. Hakufanya mazuri. (2FAL 15:38-16:20) Manabii walikuwa

Isaya na Mika.

722 K.K.

Israeli ya Kaskazini ilihamishwa Ashuru. Israeli ya Kaskazini haikuwepo tena. (2FAL 17)

12. Hezekia (Yehova ameimarisha), (716-687 K.K.)

Mwana wa Ahazi alitawala miaka 29. Alifanya mazuri. Alitakasa hekalu kwa kuanzisha upya

ibada. Aliugua lakini aliongezewa maisha miaka 15. (2FAL 18:1-20:21) Manabii walikuwa Isaya

na Mika. 710 K.K Yerusalemu ilinusuriwa!

13. Manase (ya kusahau), (687-643 K.K.)

Mwana wa Hezekia alitawala miaka 55. Alifanya mabaya. Baadaya alinyenyekea. (2FAL 21:1-

18).Nabii alikuwa Isaya.

14. Amoni (Mtu Wa kazi mkuu), (643-641 k.K.)

Mwana wa Manase alitawala miaka 2. Alifanya mabaya. (2FAL 21:18-26) Nabii Yeremia.

15. Yosia (Yehova na atoe), (641-609 K.K.)

Mwana wa Amoni alitawala miaka 31. Alifanya mema. Aliimarisha ibada. Ulikuwa wakati wa

Uamusho Yuda. Farao-neko alimwua. (2FAL 22:1-23:30) Manabii walikuwa Nahumu, Habakuki,

Sefania, Yeremia na Hulda walitabiri wakati wa Yosia.

16. Yehoahazi (Yehova ameshika), (609 K.K.)

Mwana wa Yosia alitawala miezi 3 tu. Alifanya mabaya. Farao-neko alimweka kifungoni na

akampeleka Misri. (2FAL 23:30-34) Manabii walikuwa Yeremia na Habakuki.

17. Yehojakimu (Yehova hupanga= Eliakimu)(609-598 K.K.)

Mwana wa Yosia, ndugu wa Yehoahazi alitawala miaka 11. Alifanya mabaya. (2FAL 23:34-24:6)

Nabii alikuwa Yeremia.

604 K.K.

Page 58: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

58

Danieli pamoja na wengine wa jamii ya kifalme walihamishiwa katika uhamisho wa lazima

Babeli. (Dan 1:1-6)

18. Yekonia/Yehoyakini (Yehova huanzisha), (598/597 K.K.)

Mwana wa Yehoyakimu alitawala miezi 3 tu. Alifanya mabaya. Nebukadreza aliteka

Yerusalemu na kuchukua vitu vya Hekalu na sehemu kubwa ya watu wa Yerusalemu

akawapeleka Babeli. Uhamisho Wa kwanza kwenda babeli (2FAL 24:6-15) Nabii Yeremia.

Ezekieli(Yehova ametia nguvu) alipelekwa Babeli. Alitabiri miaka 593-570 K.K.

19. Sedekia (Yehova ana haki), = Matania (597-586 K.K.)

Ndugu ya baba yake Yekonia alitawala miaka 11. Alifanya mabaya. (2FAL 24:17-25:7)

Uhamisho Wa pili kwenda babeli. Nabii Yeremia.

588 K.K.

Nebukadreza alianza kuizunguka Yerusalemu. (2FAL 25:1)

586 K.K.

Yerusalemu ilitekwa. Mji na Hekalu viliteketezwa. Sedekia na watu na sehemu kubwa

walipelekwa Babeli. Uhamisho Wa tatu kwenda babeli. (2FAL 25:2-4)

582 K.K.

Sehemu ya mwisho ya wafungwa walihamishiwa Babeli. Miaka hii kuna Dini kubwa mbili

ziliibuka huko Asia. 560-480 K.K.:Budha (Bara-Hindi) na 551-478 K.K.:Konfutse (Uchina)

539 K.K.

Koreshi alitawala Babeli. Dola/Utawala wa Babeli uliangushwa!. (2NYA 36:21-)

Uajemi ikawa dola/utawala wa dunia nzima mpya.

538 K.K. Wayahudi kama 50,000 walirudi Yerusalemu kufuatia wito wa Zerubabeli. (2NYA

36:22,23)

515K.K Ujenzi Wa hekalu la pili kumalizika na kulitakasa!

Manabii Hagai,Zekaria na Malaki.

445K.K Nehemia aliwasili Yerusalemu!

448** Ezra awasili Yerusalemu. Kama misingi ikiharibika,Mwenye haki atafanya nini?

Page 59: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

59

MANATI YA MFALME UZIA.

Akafanya katika Yerusalemu mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu wastadi, iwekwe juu ya

minara na juu ya buruji, ili kutupa mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana;

kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.(2 Nyakati 26:15)

Mfalme Uzia.

Alianza kutawala akiwa na miaka 16,akatawala juu ya Yuda miaka 52, wafalme wawili

waliopata NEEMA ya kutawala muda mrefu NI : Uzia na Manase!, Uzia alianza vizuri

akamaliza vibaya!. Manase alianza vibaya sana akamaliza vizuri! Nabii isaya anatuambia siku ile

Mfalme Uzia,alipokufa ndipo alipoanza Huduma yake ya unabii. Enzi za Mfalme Uzia kulitokea

tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha watu kukimbia kwa hofu sana!

Uzia aliujengea Yerusalemu minara, penye lango la pembeni, na penye lango la bonde, na

ugeukapo ukuta, akaifanya kuwa imara. Alijenga minara nyikani, akachimba mabirika ya

kusindika zabibu mengi ya kutosha, alikuwa na ng’ombe wengi; Alikuwa mkulima mzuri sana

na alipenda kilimo!

Alikuwa na mashamba ya mizabibu na wafanyakazi Wa kutosha! Alikuwa na Mfalme

maarufu,maana sifa zake zilienea mpaka Misri.Aliletewa zawadi na wafalme Wa nchi jirani.

Aliwapiga wafilisti, akajenga miji ya maboma,(akaweka vituo vyake vya kijeshi kwao)! Katika

wafalme waliofanikiwa sana na kuwa na nguvu kiuchumi, kiutawala na kijeshi alikuwa Mfalme

Sulemani na Uzia.

Uzia alikuwa na jeshi la watu wa kupigana, waliokwenda vitani vikosi vikosi, watu mashujaa,

ilikuwa 2600. Na chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la askari, 307,500 ambao walipigana

vita kwa nguvu nyingi, kumsaidia mfalme juu ya adui.

Uzia aliwafanyizia jeshi lake,lote ngao na mikuki, na chapeo, na deraya za madini, na nyuta, na

mawe ya kupiga kwa teo. Alikuwa na watu wabunifu hodari!,waliobuni manati zilizowekwa juu

ya minara zenye uwezo Wa kutupa mawe makubwa kwa adui na kuvunja kuta na malango ya

mji!.

alikuwa na mitambo ya kutupa mishale,mataifa jirani wakati wote Wa enzi yake walimwogopa!

Utukufu Wa wanadamu!

Chakusikitisha! Aliwewa sifa za wanadamu!,akawa na kiburi!, Kiburi cha mafanikio na ukuu

kikamsumbua. Siku moja akaingilia fani isiyo yake! Akataka nafasi ya ukuhani! Akajiona

anastahili kufanya chochote atakacho. Tukumbuke kuwa Enzi za Agano la kale kulikuwa na

Vipawa vya aina 3 tu! Yaani ufalme, ukuhani na unabii!

Page 60: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

60

Ikiwa Mfalme hana kipawa cha ukuhani hawezi na haruhusiwi kutoa dhabihu ama kufanya ibada

ya kufukiza uvumba, akasahau kilichomkuta Sauli. Mfalme Uzia aliingia hekaluni hadi

patakatifu,akachukua chetezo ili afanye dhabihu ya uvumba! Makuhani 80, wakaingia ndani kwa

haraka ili wamzuie lakini waliishia kuonekana duni kwake!

Akakasirika,akafanya kwa nguvu! Kabla hajatimiza azma yake! Mungu akampiga kwa ukoma

palepale!

Akapokea laana badala ya Baraka! Hasara baada ya hasira, Jamani! Ilikuwa huzuni sana.

Akatengwa asikae ikulu maana atawaambukiza wakuu wake ugonjwa wa ukoma! Akaishi kama

mfungwa Wa kifungo cha nje! Hadi kufa kwake zaidi sana akazikwa kwa kutengwa mbali na

makaburi ya Mfalme!

Mungu anapogawa vipawa,karama na vipaji,hutufanya tupate sifa,heshima na kutaminika kwa

hizo! Ila tumapojimilikisha kana kwamba tuna hati miliki kumbe NI mawakala tu! Mwakilishi

tu,mjumbe tu Wa hizo,! Tunafanya makosa makubwa sana!

Kumbuka,Musa kilichomzuia kuingia Kaanani NI hikihiki!,Paulo ili asifanye makosa yaleyale

akapewa tatizo la kuumwa na tumbo Mara kwa Mara!

Manati ya Mfalme Uzia ilifanya mengi mazuri ila ilimfanya ajione ana hati/haki, miliki ya

kufanya yasiyomhusu! angalia manati yako isikukoseshe mbingu,maana ni bora kumaliza vizuri

kuliko kujivunia manati!

Page 61: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

61

MAOVU YA MFALME MANASE.

Manase maana yake "mwenye kusahau" Manase = Yeye (Mungu) amenifanya kusahau!

Manase alikuwa mtoto pekee kwa Hezekia,mama yake aliitwa Hefsiba,binti Wa nabii Isaya!

Alipewa mafundisho yote ya Sundayschool (shule ya torati na maadili) akakua akijua vema haki

na uovu!

Ooh! Yawezekana yale mapambio ya kusifu&kuabudu aliyajua kuyaimbisha kwa

ustadi!,kushukuru kwa ajili ya chakula,kuomba kabla ya kulala, aah! NANI kama yeye? Akiwa

na miaka 12 tu! akakabidhiwa ufalme! inawezekana baba yake (Hezekia) alikuwa bado miaka 3

afe, ama alikuwa amekwisha kufa! Maana alipewa kuishi miaka 15 kama bonus!

Manase huyu! Alianza kutawala akiwa na miaka 12,akatawala kwa miaka 55,ndani ya hii miaka

ipo ya aliyofanya maovu na miaka aliyotengeneza kwa kumrudia Mungu. Ndie aliyetawala kwa

miaka mingi akifuatiwa na Mfalme Uzia. Ndie aliyefanya maovu zaidi ya wafalme wote

waliowahi tawala Yuda!

Ndie aliyemuua nabii Isaya. Kwa ubaya sana akamuua,Babu yake (Isaya) kwa kumpasua na

msumeno,miaka kama 7 tu, kupita tangu Hezekia kufa. Aliujaza Yerusalemu damu,za wasio na

hatia hadi watoto wake Wa kuwazaa aliwateketeza kama dhabihu kwa mungu( Moleki)

"Alipajenga tena mahali pa juu alipopabomoa Hezekia babaye; akazisimamisha madhabahu za

mabaali, akafanya na sanamu za maashera, akaabudu jeshi lote la

mbinguni(jua,mwezi,nyota,vimondo,malaika) na kulitumikia."

Kama hiyo haitoshi;

Alijenga madhabahu ya miungu ( kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika nyua 2 za helalu.),

akalipamba hekalu kwa salamu ya kuchonga, mahali alipopanena BWANA, Katika Yerusalemu

litakuwako jina lake milele. Aliwapitisha wanawe motoni katika bonde lile la mwana wa

Hinomu; kana kwamba NI sadaka ya kuteketezwa, alitazama bao, alibashiri, akafanya uganga,

alijishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; tunguri zikawa sehemu ya

Maisha yake! Kama ni dhambi, hakuna aliyoiacha bila kuifanya! Mtoto Wa madhabahuni,kawa

mhuni kuliko wahuni!

Manase akawakosesha Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, wakazidi kufanya mabaya kuliko

wakaanani, waamori na wayebusi, aliowaharibu BWANA mbele ya wana wa Israeli.

Mungu kumwonya, alimwonya sana tu! Ikafika kikomo! Mungu akamtumia watu wakuu

makatili Wa Mfalme Wa Ashuru,wakamkamata,wakamfunga pingu,wakampeleka

Babeli,wakamtesa mateso makali,akasema mpaka siri zisizokuwepo! Bado wakaendelea kumtesa

kwa ukatili, wakatoboa puani na kati ya mishipa ya kisigino kwa kumfungia pingu,na mateso

yasiyofaa kuneneka! Akawa hoi bin taabani!

Page 62: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

62

Akatubu dhambi zote,akaomba rehema,akalia siku nyingi,Mungu Wa Israeli amsamehe! Maana

alijiona kama yupo Jehanum ya mateso! Jasho likamtoka!

"Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za

Mungu wa baba zake."

Akamwomba Mungu; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamsamehe uovu wake!

Mungu akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba

BWANA ndiye Mungu. Mungu alimfanyia hikihiki,Nebukadneza,akashika adabu ya kucheza na

Mungu; kutoka kuwa na uovu hadi kuwa na wokovu. Manase akaisafisha Yerusalemu,na

kulitakasa hekalu,hadi wakuu wake wakamshangaa! Kulikoni? kwa mwendo Wa kasi akaigeuza

miungu yote kuwa majivu! Jamani !

"Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama!

Yamekuwa mapya".(2Wakorintho 5:17)

Sasa Manase ni kiumbe kipya! Waliokuwa barazani mwa Mfalme walipobisha haiwezekani!

Ooh! Kumbe walisha chelewa, Roho Mtakatifu akazishuhudia nafsi zao!, "Amin nawaambia,

watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa

Mungu."(Mathayo 21:31) hivi Mungu akisamehe amesamehe?...nawaza tu! Mfano! ikitokea

Obama akamstukia Osama yuko mbinguni je atatoka nje?

lini na wapi mwovu huyu alitubu,anajua mwenyewe na Mungu peke yake!

Nabii Ezekieli (18:20-28),anawaambia nini wanadamu?

Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu

zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda

hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. MTU mwovu

Mungu anasamehe na kufuta maovu yake yote! Pale anapotubu na kuacha uovu wake!

Naiona dawa ya makosa, ..hiyoo damu yake Yesu! Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha

haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je,

ataishi?

Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa

lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa. Mcha Mungu anapoacha wokovu

na kufanya maovu,Yale yote mema aliyowahi kufanya! (Ikiwa NI kujenga kanisa,kuimba

Kwaya,kusomesha Mchungaji wake) Mungu atafuta yote! Hivyo siku atakapotubu ataanza upya!

Na rekodi mpya!

Page 63: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

63

HEKALU.

Eneo lile,kilima kile ambacho Ibrahimu alijaribiwa kumtoa Isaka kwa Imani,kuwa dhabihu ya

kuteketezwa. Daudi alikinunua kiwanja cha Arauna eneo lilelile ili kuja kumjengea Mungu

hekalu. Palikuwa na hekalu la kuhamishika jagwani, lililoanzia mlima Sinai,likiitwa hema ya

kukutania,likakaa Mispa enzi za Samweli,kilima cha Gibeoni kilitumika kama mahali pa juu pa

kumtolea Bwana dhabihu!

Mfalme Sulemani akajenga hekalu!

Lilianza mwaka Wa 4 Wa utawala Wa sulemani( 966K.K)baada ya miaka 7 na miezi 6,hekalu

likakamilika!(959 K.K)

Nebukadreza alilibomoa hekalu hili mwaka 586 K.K,

Ezra na Zerubabeli akalijenga, (536 K.K.- 515 K.K.)baada ya uhamisho Wa Babeli,

Mfalme wa Uyunani,Antioko Epiphanes IV,(169 K.K) akalinajisi, alipoweka hapo Sanamu ya

mungu wa Kigiriki Zeus. Hatua hiyo ilisababisha upinzani wa Wamakabayo, waliorudisha ibada

ya Kiyahudi hekaluni na hadi leo, sherehe ya "Hanuka" inakumbusha kutakaswa kwa hekalu.

mwaka 167 K.K na Yuda Mmakabayo (164 K.K.) Mwaka 21K.K,Herode mkuu,akalijenga zaidi,

Mwaka (19 K.K,)wayahudi wakalipamba kwa kuliboresha!. mwaka 30 B.K ,wanafunzi Wa Yesu

wakalisifia! Lakini Yesu akatoa unabii,kuwa "hakuna jiwe juu ya jiwe ambalo

halitaporomoshwa" mwaka 64 BK Jemedari Tito, akalibomoa vipandevipande! tarehe ileile

lilipobomolewa mara ya kwanza.

Kuta za msingi tu zilibaki na ukuta mkubwa wa magharibi unasimama hadi leo, ukijulikana

kama "ukuta wa maombolezo" na ni Patakatifu, kwa Wayahudi

Hadi hivi Leo,tokea mwaka 70 B.K, halijajengwa lingine! Upo tu ule msingi,na sehemu fulani ya

ukuta ndio wayahudi huenda kuabudu apo, sadaka zinazodaiwa na Torati hadi sasa ni nyingi

sana! ,haziwezi kutolewa kwa muda wa miaka 2000 hivi!

Juhudi za kujenga hekalu,hazikuzaa matunda hadi Leo! Hekalu la sasa litajengwa lini?

Tangu wakati wa uhamisho hadi leo Wayahudi wanaendelea kukusanyika katika majengo

yanayoitwa masinagogi (yaani "mkutano").

Waislamu walipovamia Yerusalemu walikuta mlima wa hekalu kama mahali pa maghofu,

wakajenga hapo misikiti miwili: "msikiti wa Al Aqsa" pamoja na "kubba ya Mwamba".(rock of

dome)

Ipo siku watalijenga tena! Ila unabii waeleza kuwa,mpinga Kristo ndie ayakayewezesha ujenzi

huo kuanza! (Ufunuo sura 11)

Page 64: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

64

Japo ibada zake zitadumu kwa miaka 3 na nusu,(miezi 42)tu! maana Mpinga Kristo atawajeuka

baadae na kuanza kuwaua!

"Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa

na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale malaika

saba."(Ufunuo15:5-8)

Utawala Wa Kristo Wa millennia,yaani miaka 1000, utahusisha hekalu lenye utukufu kuliko la

Sulemani! Cha ajabu,Mbingu mpya na nchi mpya hapatakuwa na hekalu! (Ufunuo 21:22)

Kumbe mambo ya hekalu NI kwa mbingu na nchi za sasa tu. Kuna hekalu mbinguni,lenye

sanduku la Agano ndani yake!,Musa alioneshwa ili ajenge kwa mfano wake,(Kutoka 24:16-28)

Isaya aliona hekalu hilo!

Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho

juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.

(Isaya 6:1), Yohana nae aliona hekalu!(Ufunuo 11:19)

MASWALI:

1.Je katika utawala Wa miaka 1000 ya Kristo hapa duniani,dhabihu za wanyama zitatolewa tena?

2.Je kwa nini mbingu mpya na nchi mpya hapatakuwa na hekalu?

3. Ina maana wayahudi mpaka Leo hawatoi sadaka? Na hawafanyi ibada?

"Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo

tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu,

huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe,

lile jipya".!(Ufunuo 3:12)

Page 65: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

65

MUHTASARI WA KITABU PILI CHA WAFALME.

"Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote."(Mith 14:34)🙈

Sura: 25

Aya/mistari: 719.

Mwandishi: inawezekana akawa Yeremia,kundi la manabii.

Mwaka Wa uandishi: 560-550 K.K

Sura 2 za mwisho zimeandikwa baada ya kipindi cha uhamisho Wa Babeli kumalizika.

Historia ya kitabu cha 2 cha wafalme imegawanyika katika enzi kuu 2;

1. historia ya falme zote kabla ya kuanguka kwa Israeli mwaka 722.K.K sura ya 1-17 matukio

yake yalichukua miaka 131 tangu enzi za mfalme Ahazi Wa Israeli,853-hadi utumwani 722 K.K

2. Historia ya Yuda baada ya Israeli kuchukuliwa utumwani hadi kuanguka kwa Yuda mwaka

586 K.K sura ya 18-25.matukio yake yalichukua miaka 155 tokea enzi za Hezekia 715-560.K.K

Manabii Amosi na Hosea walitabiri katika Israeli na katikati ya ukengeufu Wa kutisha Wa

wafalme Wa Israeli Mungu alimwinua Eliya na Elisha kuwataka taifa na viongozi wake

wamrudie Mungu na Agano lake!

Yoeli,Isaya,Mika,Nahumu,Habakuki,Sefania,Hagai,Zekaria na Yeremia walitabiri ktk Yuda!

ufalme wa Israeli ulidumu kwa miaka 210,{931-721} kwa kutawaliwa na wafalme 19 toka koo 9

tofauti.

Ufalme wa Yuda ulidumu kwa miaka 345,{931-586}

Kwa kutawaliwa na wafalme 20 kutoka ukoo mmoja wa Daudi,na wafalme 8 kati ya 20

walifanya yaliyo mazuri..japo malkia Athalia binti wa Yezebeli alikusudia kuua uzao wote lakini

alishidwa!.Yoashi akanusurika!

Jumla ya falme zote toka Sauli hadi sedekia/Mathania ni miaka 467,(1053-586).

KITABU CHA WAFALME 2. Na sura zenyewe!

Sura 1: Hukumu ya Mungu juu ya Ahazia. Alituma wajumbe kwa baal-zebubu miungu ya

Erkoni,Eliya awarudisha. Majeshi ya vikosi 2[askari 100 na wakuu 2] waliteketea kwa moto

Page 66: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

66

Sura 2-4: Eliya kuchukuliwa mbinguni. Uasi wa moabu na vita juu yake. Mwanamke mjane na

mafuta; mshunemu kupata mtoto,kufufuliwa alipokufa.

Sura 5: Jemedari Naamani kuponywa ukoma. Elisha awapiga upofu majeshi ya shamu,

Sura 6-8: Ben-hadad kuusuru Samaria. Wakoma 4 waleta muujiza Israeli. Shamba la mshunemu

larudishwa,Hazael kumwua Ben-hadad. Kutawala kwa Yehoramu na Ahazia wafalme wa Yuda.

Sura 9: Kutawazwa kwa Yehu kuwa mfalme. Yehu Awauwa Yoramu na Ahazia,Yezebeli

auwawa

Sura 10: Kuuwawa kwa kizazi chote cha Ahabu,na watumishi wote wa mabaali.

Sura 11: Uasi wa Athalia kutaka kuua uzao wote wa kifalme wa Ahazi,washindwa.

Sura 12-14: Utawala wa mfalme Yoashi wa Yuda na kurakabati hekalu. Utawala wa mfalme

Yehoahazi, Yehoash wafalme wa Israeli, Kifo cha Elisha. Utawala wa Amazia mfalme wa Yuda

afanya vita na Yehoash, Yeroboam II.

Sura 15: Azaria mfalme wa Yuda kutawala, na kufa. Zekaria,Shallum, Menahem,Pekalia,

Peka(Israeli).Na Yotham mfalme wa Yuda.

Sura 16-17: Kutawala kwa mfalme Ahazi. Hosea mfalme wa mwisho wa Israeli, kwenda

utumwani,samaria wakaliwa.

Sura 18: Kutawala kwa Hezekia mfalme wa Yuda, Sennakerub kuvamia Yeruslemu.

Sura 19: Ukombozi wa Yerusalem watabiriwa, maombi ya Hezekia, nabii Isaya.

Sura 20: Ugonjwa wa Hezekia, ujumbe toka babeli.

Sura 21: Manase mfalme wa Yuda, Amoni mrithi wake.

Sura 22-23: Mageuzi ya Yosia na torati, Yehoahazi, Yehoiakimu.

Sura 24: Uvamizi wa Nebukadneza juu ya Yuda.

Sura 25: Kuanguka kwa Yerusalemu na kuchukuliwa mateka babeli.

Page 67: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

67

TAIFA (DOLA) LA ASHURU.(KINGDOM OF ASSYRIA.)

Ashuru mwana Wa Shemu,mwana Wa Nuhu ndie mwasisi. Katika mto Hidekeli,kaskazini

magharibi ya Mesopotamia. Mji mkuu wa kwanza ulikuwa Ashuru, kisha Kala na mwisho

ukawa ni Ninawi. Kuna taifa (ufalme) Wa Shamu/Syria upande wa kusini,na kusini zaidi lipo

taifa la Israeli. Wako manabii 2 waliotumwa kutoa unabii juu ya taifa hili, Yona na Nahumu.

Mungu aliihifadhi taifa hili baada ya toba iliyotokana na mahubiri ya Yona ili alitumie kama

chombo chake cha kuadhibia mataifa kama Israeli kwa wakati uliokusudiwa. Baada ya kutimiza

kusudi lenyewe la kuharibu samaria na kuwachukua mateka Israeli mwaka 722 k.K

Nabii Nahumu akatoka kutoa unabii wa kuangamia kwa taifa hili na mwaka 612 k.K Ninawi

iliangushwa chini kabisa.

Wafalme waliotawala Ashuru ni kama ifuatavyo.

Adadi-Ninari III (810-783)k.K

Asurdani (833-775) k.K

1. Tiglath-pileseri III (Pul) mwaka 745-727

Menahemu alimpa hongo ili asiishambulie Israeli.

Nabii Hosea(10:5-8)na Amosi(7:17)walionya dhidi ya mwendelezo Wa dhambi ya Israeli.

Mwaka 732k.K . Peka Mfalme Wa Israeli na Resini Mfalme Wa Shamu walitaka Yuda aungane

nao ili wampige Ashuru,lakini Yuda alipoona anashambuliwa,aliomba msaada kwa Ashuru.

Ikawa maafa makubwa kwa Israeli na Shamu.

2. Shalmanesa V (727-722)k.K

Alivunja na kuzima uasi wa mataifa ya Shamu na Israeli pale walipoungana ili kumpiga vita!

Aliuhusuru(aliuzingira) mji mkuu Samaria! Kwa mda mrefu miaka 3 walioko ndani walikufa

kwa njaa!

3. Sargoni II (722-705)k.K

Aliuharibu kabisa mji huu wa Samaria na kuwachukua mateka Israeli mwaka 722 k.K

Mfalme wa Mwisho kutawala Israeli; Hosea.aliasi kwa kugoma kumlipa kodi mfalme wa

Ashuru,na kuunda jeshi la vita!.Na ikawa mwisho wa utawala wa kifalme Israeli.

2 Wafalme sura 17,18: ndio mwisho Wa historia ya Israeli katika Biblia.

Page 68: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

68

Mateka Wa Israeli wakapelekwa miji ya wamedi, Hala, Habori, karibu na mto Gozani.

Sehemu yao wakaletwa watu wa mataifa mengine( Babeli,kutha,Ava,Hamathi na Sefarvaimu)

waishi huko,ila kutokana nao hawakumcha Mungu,wakawa waovu! Mungu aliwatuma simba

wakawa wanakula wakazi wavamizi wa Samaria!

Ndio maana mpaka kipindi cha Yesu bado watu wa Samaria walikuwa wanabaguliwa,wana

nyanyapaliwa kwa kuwa sio wayahudi,na wengine waliochanganya damu pia hawakuhesabiwa

kama wayahudi.

Wasamaria na yule mwanamke kisimani walimwamini ✋Yesu kwa kuwa wokovu umeyafikia

sasa mataifa yote! Na kuabudu sasa ni katika roho na kweli.

4. Senakeribu (705-681) k.K

Aliuzingira Yerusalemu baada ya Mfalme Hezekia Wa Yuda kugoma kumpa kodi mwaka 701

k.K Alichukua mateka kama 200,150. Utumwani.

Ilimbidi Hezekia kulipa faini kubwa sana ili kumzuia asiupige vita Yerusalemu!

Mungu alikuwa kazini,akamsaidia Hezekia,askari wake kama1850,000 waliuwawa na malaika

kwa usiku mmoja tu,Senakerubu aliopofika nyumbani kwake akauwawa na mwanae! (2

Wafalme 18:13)

5. Esar- hadoni (681-669)k.K

Alifanya mapatano na wakaldayo na akaujenga Babeli. Na alikuwa na ufalme pamoja na Babeli

(745-636) k.K .“Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki

na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe

akatawala mahali pake". (2 Wafalme 19:36-37)

6. Ashur-banipal (669-627) k.K

Aliwahamisha watu wa mataifa kuja kuishi samaria. Aliifanya Misri kuwa sehemu ya milki yake.

Mwaka 612 k.K mji Wa Ninawi ukaanguka,mateka wale Wa Israeli waliokuwa chini ya

Waashuru sasa wakawa chini ya Umedi. Wayahudi wapockukuliwa mateka na Nebukadneza

walipofika Babeli, waliwakuta baadhi ya ndugu zao(Israeli) huko waliotapakaa majimbo baadae

yaliyojulikana kama Umedi&uajemi!

Chini ya utawala Wa Koreshi/Dario wayahudi pamoja na wale wenzao Wa Israeli waliruhusiwa

kurudi kwa awamu awamu nchi yao!

Baadhi yao bado walibaki huko kipindi kile cha Malkia Esta na Mfalme Ahausuero!

Page 69: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

69

MUHTASARI KITABU CHA MAMBO YA NYAKATI.

Kitabu cha 1 cha MAMBO YA NYAKATI.

Kwa mtazamo Wa kikuhani,Ezra mwana "mambo ya nyakati" aliona jinsi wayahudi waliotoka

uhamishoni Babeli,walivyokosa tumaini la upekee wao wa kuwa watu wa agano,taifa teule

akavisoma vitabu,akafanya upembuzi yakinifu,wapi wametoka, kuanzia Adamu,wapi

wamepita(Ibrahimu-Daudi-uhamisho-mabaki/mateka),wapi walipopotoka,na sasa wako wapi,

kuelekea wapi!

Akaja na kusudi moja la kuwaunganisha tena mateka, kujiona sasa ni raia halisi,bado historia ya

ahadi ya Masihi inandelea mbele,umuhimu wa kurudisha uhusiano na Mungu kupitia

hekalu,torati,na Makuhani kurejea nafasi zao!

Madhumuni ya mwandishi hayakuwa kuchunguza maisha ya watu binafsi,Bali kuonesha jinsi

ufalme Wa Daudi ulivyoimarishwa pamoja na mpango Wa dini na maisha ya kitaifa ya Israeli

kuwa mambo yasiyoweza kutenganishwa!,ameongeza mambo mengi yasiyopatikana katika

vitabu vya Samweli na Wafalme!

Hamu yake kubwa ni watu waishio katika Israeli baada ya kifungo cha Babeli waishi maisha yao

ya kitaifa juu ya misingi ya Mungu. Kwa sababu hiyo walawi,ukuhani Wa uzazo wa Haruni

pamoja na hekalu ambao hawakutajwa sana katika wafalme walitajwa Mara nyingi katika kitabu

hiki.

Kitabu chenyewe!

Kina Sura: 29

Kina Mistari: 941

Mwandishi: Ezra alirejea na mateka mwaka 457

Mwaka Wa uandishi:450-420 K.K

Eneo la uandishi: Yerusalemu.

Somo/dhima kuu: Historia inayoendelea ya UKOMBOZI Wa Israeli.

Sura za mwanzo wa MAMBO YA NYAKATI ni elimu ya ukoo(nasaba ya vizazi). Ni vizuri

tuichunguze! Roho Mtakatifu atakapotufunulia elimu ya ukoo, tutapata hazina nyingi.

Page 70: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

70

Sura hizi zinatueleza kwamba Yesu ni mrithi wa kiti cha utawala wa Daudi. Elimu ya ukoo pia

inatueleza watu wali­potokea. Wayahudi wanathamini sana sura hizo kwa sababu wanamsu­biri

Masihi wao. Katika nasaba hizi za vizazi tunaweza jifunza juu ya ukoo Wa kikuhani kuanzia

kwa Lawi.

Ethani Wa uzao Wa Merari,kizazi cha 14 kwa Lawi. mwandishi Wa Zaburi ya 89.

Asafu mwandishi Wa zaburi ya 50, 73-83 jumla zaburi 12 aliziandika,nae ni wa kizazi cha 14

cha lawi kwa Gersoni.

Hermani mjukuu Wa Samweli,kizazi cha 23 kutoka kwa Lawi kupitia Kohathi.mwandishi Wa

Zaburi ya 88.

Wana Wa Kora,waandishi pia Wa Zaburi kadhaa!

Ezra (Yehosadaki) mwandishi Wa kitabu hiki,mtu Wa kizazi cha 25 kutoka kwa Lawi kupitia

Kohathi,Amramu,na Haruni.

Tunajua: Yesu ni Masihi. Lakini bado kuna Wayahudi ha­waamini Yesu ni Masihi.

Kitabu kinatueleza kuhusu Daudi vivyo hivyo kama Kitabu cha pili cha SAMWELI

kinavyotueleza.

Elimu ya ukoo inaanzia Adamu.

Tangu 1012-972 K.K. Kilichukua miaka 40, (Miaka inahesabiwa tangu sura ya 10)

UTANGULIZI WA KITABU CHA MAMBO YA NYAKATI WA PILI.

972-538 K.K. (Kilichukua miaka 434)

Kitabu hiki kinaendeleza mambo ya Nyakati wa Kwanza. Kitabu kinaanza na utawala wa

Sulemani na kueleza zaidi kuhusu Israeli ya kusini yaani wafalme wa Yuda.

Historia yao kwa sehemu kubwa ni jinsi wali­vyoanguka na baada ya yote hekalu liliteketezwa

hata watu wakapele­kwa uhamishoni Babeli.

Hekalu lilikuwa limetumika miaka 375 na liliteketezwa mwaka wa 586 K.K. Danieli na Ezekieli

walikuwa miongoni mwa wale waliohamishwa kwa nguvu Babeli.

Kitabu kinamalizika kwa Wayahudi ku­pewa ruhusa na Koreshi kurudi nchini kwao. Kitabu

kinaanza kwa matukio ya mwaka wa 972 na kumalizika kwa matukio ya mwaka wa 538 K.K.

"Yatosha kwa siku maovu yake."

Page 71: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

71

Ikiwa tumetambua wapi tumetoka,wapi tumeharibu,wapi tunaelekea.Sasa inatosha,tusiongeze

makosa mengine,badala ya kutubu, na baada ya kutubu na kutibu; kwa kukata tamaa!, wala

tusilalamike itakuaje sasa! Bali tutazame mbele, tumtazamie Mungu wetu mwenye rehema Yeye

ataponya, ataimarisha, atajenga tena!

Kuhani Ezra anaeleza kwa kinaganaga uamsho Wa pekee na kurejeshwa upya kwa aina zote za

ibada wakati Daudi alipolileta sanduku la Agano huko Yerusalemu (sura 15-16) na kusisitiza juu

ya Agano la Mungu na Daudi kama(sura 17) tumaini la Israeli kwa Masihi aliyehaidiwa.!

Page 72: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

72

MUHTASARI WA KITABU CHA MAMBO YA NYAKATI WA PILI.

Kitabu hiki NI mwendelezo Wa Kitabu cha Nyakati Wa kwanza ambavyo vilihesabika kama

kitabu kimoja. Kiliandikwa miaka mingi baada ya Israeli na Yuda kupeleka utumwani Babeli.

Watu wengi zaidi kati ya wale waliorudi kutoka utumwani Babeli baada ya miaka ile 70 na

wengine zaidi ya hiyo! Hawakuitazama nchi ya Palestina kwa mtazamo ule Wa kwanza,maana

walijua kidogo sana juu ya hekalu na Yerusalemu,walijiona kama wahamiaji na sio kama taifa

teule linalorejea nyumbani! ☝Mwandishi huyu kwa mtazamo wa kikuhani, alitaka kuwaonesha

wao, NI zaidi ya ujuzi ule Wa mazingira waliyokuwa wanayaona!

Kina Sura 36.

Kina Mistari 822.

Dhima kuu: Ibada ya kweli na mageuzi!

Mwaka Wa uandishi: 450-420 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Ezra!

Kuhani Ezra mwenye elimu ya nyakati, ana ainisha nyakati zile za wafalme kabla na baada ya

uhamisho kumalizika.

Utawala wa Sulemani(970-930) K.K: na ufalme uliogawanyika mwaka (930-586)K.K na hatma

ya Yuda. Hekalu la Yerusalemu na ibada ya kweli. Wafalme toka uzao Wa ki-MASIHI Wa

Daudi. Kabila la Yuda lililokuwa kubwa kati ya wayahudi.Mabaki ya waliorudi na kurejeshwa

upya urithi Wa kiroho!

Kitabu kimegawanyika sehemu kuu 2:

Sura 1-9 :

Utawala Wa Sulemani,kipindi kizuri cha amani,nguvu,mafanikio na fahari kwa Israeli.

Kujengwa,kuwekwa wakfu kwa hekalu!. Utajiri hadi kifo cha Sulemani. Yaani mwaka 971-931

K.K (miaka 40.)

Sura 10-36 :

Wafalme Wa Yuda tangu Rehoboamu hadi wakati Wa uhamisho! Ilichikua miaka 393 yaani

(931-538 K.K) Asilimia 70% sura hizi zinaeleza habari za wafalme 8 Wa Yuda kati ya 20

waliofanya mazuri. Asilimia 30% ya sura hizi NI Maelezo ya wafalme 12 waliyofanya mabaya

Page 73: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

73

walivyotawala Yuda. Baadhi ya wafalme waliostahili kusifiwa katikati ya kuanguka kiroho kwa

Yuda na kukengeuka!

Sura 14-15: Asa

Sura 17:19-20: Yehoshafati

Sura ya 24: Yoashi

Sura ya 29-32: Hezekia

Sura ya 34-35: Yosia

Sura ya 36: uhamisho, mfalme Koreshi kuruhusu urejesho!

UAMSHO!

Nabii Habakuki aliona hitaji la uamsho miaka 70 kabla ya taifa la Yuda kupelekwa utumwani

Babeli akimsii Mungu kwa maombi akisema!

"Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka;Katikati ya miaka tangaza habari yake;

Katika ghadhabu kumbuka rehema."

Kuhani Ezra akamaliza Nyakati zake kwa kulirudia hitaji lile la Habakuki ! Juu ya UAMSHO!

Petro kwa kufahamu umuhimu Wa Uamsho kwa kanisa, akatanguliza kutoa wito Wa toba,

akitamani kila nafsi ipate kuburudishwa kwa uwepo Wa Roho Mtakatifu!

Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako

kwake Bwana;

Pakitokea matatizo,na mapito yasababishwayo na kupoa kiroho kwa kanisa, kazi NI moja, yaani

Ni uamsho uletao urejesho na kupandisha joto la upako,!kwa kumpa Roho Mtakatifu nafasi!

Page 74: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

74

MUHTASARI KITABU CHA EZRA!

Kina Sura :10

Kina Mistari : 280.

Dhima kuu: KUREJESHWA KWA MABAKI!

Mwaka Wa uandishi: 450-420 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Ezra

Ezra =maana yake, "Mungu msaada"

Kuporomoka kwa Yuda na kupeleka Babeli kulitokea kwa vipindi 3 tofauti.

1. Mwaka 605 K.K vijana waadilifu wakiwemo Danieli walipelekwa uhamishoni

2. Mwaka 597 K.K ,walipelekwa uhamishoni wengine akiwemo Ezekieli watu zaidi ya 11,000.

3. Mwaka 586 K.K ,Yuda wote waliobakia isipokuwa Yeremia na watu waliokuwa maskini sana!

Vile vile urejesho baada ya miaka 70,Babeli, ulifanyika awamu 3 .

1. Mwaka 538 K.K ,

Ezra sura 1 hadi sura 6:

Wahusika wakuu; Zerubabeli,Yoshua,Koreshi.

Mateka 50,000 walirejea, wakiongozwa na Zerubabeli na Yoshua aliyekuwa kuhani.

2. Mwaka 457 K.K ,

Ezra sura 7 hadi sura 10: Wahusika wakuu; Mfalme Dario, Jina "Ezra" linaanza kuonekana ktk

sura ya 7. Wanaume zaidi ya 1,700 ukijumlisha na wanawake na watoto inafikia wayahudi

5,000-10,000.

Walirejea chini ya uongozi Wa Ezra.Ilikuwa ni baada ya miaka 81 kupita tangu ujio Wa

Zerubabeli na ujio huu wa Ezra. Kuna pengo la karibu miaka 60 linajitokeza kati ya sura ya 6 na

7, kipindi ambacho Esta alitawala kama malkia Wa Uajemi pamoja na Mfalme Ahausero I.

Majimbo 127 toka bara Hindi(India) hadi Kushi(Ethiopia)

Page 75: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

75

Ilipita miaka 30 ndipo Nehemia akaongoza kurejesha mateka wengine na kujenga kuta za

Yerusalemu.

3. Mwaka 444 K.K,

Nehemia sura 1-13: Artashasta!

Nehemia alirejea!(Nehemia 2:1-10)

Wahusika wakuu!

Wafalme 3 Wa uajemi Koreshi,Dario, na Artashasta.

Zerubabeli nasaba ya uzao wa kifalme Wa Daudi, aliyeongoza kujenga upya hekalu.

Yeshua kuhani mkuu,mchaji Wa Mungu

Nabii Hagai,Zekaria na Malaki.

Kulingana na mapokeo ya kiyahudi, Ezra ndiye aliyevikusanya vitabu vyote vya Agano la Kale

pamoja na kuvifanya kitu kimoja(Torati na manabii).

Alianzisha utaratibu Wa ibada uliotumika katika masinagogi!

Wakati Ezra akihimisha uamsho,Zerubabeli akijenga Hekalu,Hagai akihimisha kazi ya ujenzi

iendelee mbele baada ya kusimama kwa miaka 16,Nehemia alikuja kujenga kuta za Yerusalemu!

Page 76: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

76

MUHTASARI WA KITABU CHA NEHEMIA!

Kina Sura :13

Kina Mistari : 406

Dhima kuu: Kujenga upya kuta za Yerusalemu!

Mwaka Wa uandishi: 430-420 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Ezra na Nehemia

Maana ya Nehemia =" Yehova hufariji"

Kitabu hiki kingepaswa kiwekwe cha mwisho! Yaani kiwe badala ya Malaki ikiwa tutavipanga

vitabu vya Biblia kulingana na mtiririko wa matukio!

Malaki na Nehemia waliishi kipindi kimoja!

Maana kinahitimisha historia ya Agano la Kale!.

Kitabu hiki na Ezra kilikuwa kitabu kimoja! Kikiendeleza yale yalikoishia ya Ezra!.

Nehemia aliyekuwepo wakati Wa Ezra alikuwa mnyeshaji Wa Mfalme Artashasta I ,mfalme Wa

Uajemi

Alipopata habari kuwa wayahudi waliorejea kutoka uhamishoni Babeli na Uajemi wako katika

dhiki na ya kwamba kuta za mji Wa Yerusalemu zimebomoka Nehemia alipewa ruhusa na

mamlaka ya kurudi Yerusalemu na kutumika kama Gavana na akazijenga tena kuta za

Yerusalemu.

Nehemia anasema kuwa;

"Ikawa tokea wakati huo, nusu ya watumishi wangu walitumika katika kazi hiyo, na nusu yao

wakaishika mikuki, na ngao, na pinde, na dirii; na maakida walikuwa nyuma ya nyumba yote ya

Yuda.

Watu wale walioujenga ukuta, na wale waliochukua mizigo, walijitweka wenyewe, kila mtu

alifanya kazi kwa mkono mmoja, na kwa mkono wake wa pili alishika silaha yake;".

Kama kiongozi aliyehuishwa,aliwatia moyo watu wake katika kuujenga ukuta kwa siku 52 tu,

licha ya upinzani mkali, uliokuwa juu yao!

Page 77: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

77

Ilikuwa mwezi Abib(July/Agost) hadi Elihu(Agist/Sept) 445 K.K

Alitumika kama Gavana kwa miaka 12 kabla ya kurudi uajemi! Yaani mwaka 445-433 K.K

Muda mfupi tena akatimika tena kipindi cha 2, kama liwali Wa Yuda.(2:1; 13:6-7a)

Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda

mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.!

Siku za Leo bado kuna wakina Sanbalati na Tobia makanisani,sehemu za kazi,nyumbani,kazini

pengine kwako walishakufa, kuhama,ama walishaokoka vizuri, mshukuru Mungu! La sivyo

jasho litakutoka!

Hutoa maneno mazuri ya kuvunja moyo,wanajua namna ya kuhurumia,kukosoa hadi makosa

kabla ya kosa kutendeka!

Baada ya kupokea ushauri wao!;Yale maono mazuri ya kuwa kiongozi,huishia kuwa hadithi za

kale!..,

MTU hodari aliyekusudia kufanya makubwa!,anahairisha anakuwa MTU Wa kawaida kabisa!

Jifunze kufanya kazi hata katikati ya Sanbalati na Tobia!

Page 78: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

78

MUHTASARI WA KITABU CHA ESTA

"Hadassah"=Hadasa NI jina la Esta kwa lugha ya kiebrania,kwa kiajemi alijulikana kama Esta

yaani "nyota"= 'mungu wa kike'

"...Naye alikuwa amemlea Hadasa, yaani, Esta, binti wa mjomba wake, kwa kuwa hana baba

wala mama. Naye msichana huyu alikuwa wa umbo mzuri na uso mwema; nao walipokufa baba

yake na mama yake, yule Mordekai alimtwaa kuwa binti yake yeye."(Esta 2:7)

Mordekai alikuwa Mjomba kwa Esta.

Mwaka Wa uandishi: 464-435 K.K

Kitabu cha Esta kinafaa kiwekwe katikati ya Kitabu cha Ezra sura ya 6 na ya 7. Maana tukipanga

mtitiriko Wa matukio NI kwamba wayahudi waliokuwa uhamishoni Babeli waliporejea nchi yao

kwa msafara Wa kwanza Wa Zerubabeli mwaka wa 538 K.K; kuna miaka 81 hivi, ndipo msafara

Wa pili Wa Ezra ukafuata,kitabu hiki kinachukua matukio ya miaka 10, kati ya matukio ya

miaka 58 ya kitabu cha Ezra!

Kitabu cha Esta kina sura 10,

mistari/aya 167

Mwandishi hajulikani.

Matukio yalitokea wakati wa Kitabu cha EZRA.

Yaani mwaka wa 486-465 K.K. Esta alibaki mjane akiwa na umri chini ya miaka arobaini

alikuwa ameolewa na Ahasuero kwa muda wa miaka 14!

Habari zilizoandikwa katika Kitabu cha ESTA zilitokea Uajemi wakati Wa utawala Wa mfalme

Ahasuero,aliyejulikana pia kwa jina la Xerxes 1.alitawala kuanzia 486 K.K mpaka mwaka 465

K.K. wengi Wa wayahudi baada ya kuhakikishiwa usalama na Uhuru katika nchi ile waliamua

kubaki kule kuliko kujitwisha wasiwasi na ugumu Wa maisha mapya kule Yerusalemu.

shughuli za ibada zinatajwa kwa uchache wakati Wa mfungo Wa siku 3,Mungu anaonesha

uaminifu wake japokuwa Ndani yake jina Mungu hatajwi!.

Ruthu alikuwa MTU wa mataifa aliyeolewa na mwisraeli,Esta alikuwa mwebrania aliyeolewa na

MTU Wa mataifa!

Page 79: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

79

Mgawanyo Wa kitabu hiki!

Sura 1:1 - 2:23 kuinuliwa kwa Esta kuwa Malkia

Sura 3:1 - 7:10 Mipango ya kuwaangamiza wayahudi

Sura 8:1 - 10:3 Ushindi na shagwe kwa wayahudi.

swali: ewe mwanamke! nini unaweza kujifunza kutokana na kitabu hiki?

SHEREHE YA MFALME AHASUERO : Kitabu cha Esta!

Akiwa na miaka 3 madarakani tangu atawazwe kuwa mfalme! Mambo yake yalimnyokea sana!

Akafanikiwa kwa haraka akajikuta anatawala juu ya majimbo 127 toka Kushi/Ethiopia hadi bara

hindi ( India). Makao makuu take yalikuwa Shushani mji ulioko Irani ya Leo!

Kiutawala alikuwa vizuri,mkarimu,mwenye kutamini watu wake! Akaona NI vyema

awapongeze maakida Wa majimbo yake,wakuu wenye cheo na watu Wa nyumba ya mfalme!

Akaandaa karamu/sherehe ya ukweli,iliyosheheni vyakula na vinywaji,ukumbi ulirembwa na

mawe ya marumaru,nguzo zilikuwa za dhahabu kulikuwa na mapazia ya rangi za zambarau na

samawi,bafta kwa ubora,yenye kamba za kitani,Pete za fedha,sakafu ya marumaru.

Vyumba walikolala ilikuwa balaa,vitanda vya dhahabu na fedha, chini kulirembwa kwa mawe ya

mekundu,meupe,meusi na manjano !

Ikatolewa kanuni! Kuwa MTU anywe kama uwezo wake ulivyo! Kama anavyojisikia

Vyombo vya dhahabu ndivyo vilitumika kunyea divai na mvinyo! Watu wakafurahi kweli kweli!

Wakampenda Mfalme wakamsifu,mioyo yao ikasema "mwemere mwemere" ! Huku

vifijo,nyimbo na michezo vilitumika kutoa sifa kwa mfalme. Mfalme alifurahi sana namna

alivyowapendezesha maakida wake akaamuru waongezewe wiki moja zaidi ya kusherekea!

Mwisho Wa siku ile,akakumbuka kando ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke!

Akaazimu amwite ampongeze mbele ya wakuu wake!

Cha kuvutia zaidi, mke wake(malkia) alikuwa ameumbika,mwenye sura ya kuvutia,macho ya

upendo,vishimo penye mashavu yake wakati akitabasamu,akigeuka wanaume wanarudiarudia

kumtazama! Acha mchezo! Ama kweli mfalme alijaliwa kuwa na kifaaa!

Page 80: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

80

Akaamuru watu 7 wenye sifa na cheo Wenye kusimamia nyumba 7 za mfalme wakamlete

Malkia aje ukumbini,pengne akahitimishe sherehe zile zilizofana sana kuliko kifani!

Malkia pia yeye aliwafanyia wanawake wenzake karamu! Pengne ilikuwa siku ya wanawake

duniani!

"wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili kuwaonyesha watu na

maakida uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso.Bali Vashti, malkia, alikataa kuja kwa amri ya

mfalme kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na

hasira yake ikawaka ndani yake."

Akawauliza wenye hekima, wenye elimu ya nyakati,mahakimu wenye kujua sheria na hukumu!

Je amfanyeje Malkia?

Maamuzi yakafikiwa! Japo NI mzuri kuliko peremende,mrembo kuliko miss Tanzania, ana

mwendo mzuri kama wa twiga! Avuliwe umalkia wake,aondolewe nafasi yake apewe

mwanamke mwingine mwenye adabu na heshima kuliko yeye!

Kama ilivyo Pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe ndivyo alivyo mwa'mke mzuri asiyekuwa

adabu kwa mumewe. Ni kweli kuwa wanawake wanaweza wakiamua, NI kweli mnatafuta

madaraka,cheo, kuthaminiwa katika jamii! Ila kabla ya kuheshimiwa hutangulia unyenyekevu,

adabu, nidhamu,moyo usio na wivu,kujiona,kuona wengine kama nyanya mbichi!

mwanamke wenye adabu ndiye atakayesifiwa!

Yaimarishe Yale mambo ya msingi hasa Yale ya moyoni, ya nje yanafuatia!

Esta akapata nafasi,Vasti akaondolewa ikulu!

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani! Kuna wengine watajenga nyumba/ndoa zao ila

wengine wataishia kubomoa ndoa,maisha yao!

Page 81: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

81

MUHTASARI WA KITABU CHA AYUBU.

Ayubu=(kiebrania)"aliyeudhiwa"/"aliyetubu"(kiarabu)

Aliishi kipindi cha mababa"Patrach"

Inawezekana mambo haya yalitokea wa­kati kabla ya Ibrahimu. aliishi miaka 142 baada ya

majaribu yake hivyo yawezekana alikufa na miaka kama 284 hivi.

Mwandishi: hajulikani, pengine Ayubu mwenyewe

Kitabu hiki ni cha zamani zaidi ndani ya Biblia.

Maana aliishi kabla ya Musa kuandika vitabu 5 vya torati(Mwanzo,kutoka,walawi, hesabu na

kumbukumbu la Torati).

Ayubu hakuwa mwisraeli/mwebrania! Maana aliishi kabla ya familia ya agano la Israeli

halujapata kuwapo!

Kina sura 42,

Kina aya/mistari 1,070

Mwaka Wa tukio: Wakati wa Ibrahimu (2168-1993 K.K.)

Inawezekana katikati ya Mwanzo sura ya 11 na 12.

Mada kuu: Kitabu kinajadili: Kwanini mwenye haki wanateseka?.

Ugawanyo wa kitabu!

Ayubu sura 1-3, kisa cha Ayubu kilivyokua

Ayubu sura 4-37, mazungumzo ya marafiki zake

Ayubu sura 38-42, Majibu na mahojiano na Mungu

kiliandikwa namna ya shairi, na swali lake hasa ni: Mbona Mungu aliye mwema anaruhusu

mateso?

Wahusika Wakuu: Ayubu,na

1.Elifazi Mtemani,

2.Bildadi Mshuhi,

3.Sofari Mnaamathi,

Page 82: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

82

4. Elihu wa kabila la Buzi.

" Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake ali­kuwa akiitwa Ayu­bu; mtu huyo alikuwa

mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kue­pukana na uovu". (AYU 1:1)

Marafiki zake Ayubu watatu wana­mlaumu Ayubu kwamba anateseka kwa ajili ya dhambi zake.

Ayubu alielewa mambo hayo tofauti. Sura ya mwisho Mungu anasema kwamba marafiki zake

Ayubu wali­ongea vibaya.

MAJARIBU YA AYUBU.

KABLA YA MAJARIBIO. BAADA YA MAJARIBIO!

WANA 7 NA BINTI 3, Wana 7(Yemima, Kesia,

Keren-hapuhu.,)

Binti 3 waliokuwa wazuri

kuliko wenyeji Wa nchi ile.

KONDOO 7,000, Kondoo 14,000,

NGAMIA 3,000, ngamia 6,000,

JOZI ZA NG'OMBE 500, jozi za ng'ombe 1000

PUNDA 500. punda 1000.

Miaka ya ziada 140 na kuona hadi kizazi cha 4.

Kitabu hiki kimewafariji wengi katika matatizo yao.

Wakati shetani anajaribu kuangamiza imani ya watakatifu,Mungu huwa kazini kuhakikisha

neema ipo ya kuiongeza imani hadi ushindi upatikane!

Majaribio yapo ya aina kuu 2;

majaribio ya mafanikio na Yaliyompata Sulemani.

majaribio ya mateso.Yakobo anasema tufurahi

Ikiwa wametenda haya katika mti mbichi( kipindi cha neema ) je itakuaje juu ya mti

mkavu( dhiki kuu)

Page 83: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

83

Je Mungu atathibitishaje kuwa tunampenda?

Je Mungu hutusafishaje juu ya kuwa safi kama dhahabu?

Je atatuvishaje taji kwa mbio gani tuliozipiga?

Yeye huachilia NEEMA na roho ya maombi kwa watu wake!

ikiwa Ayubu alimudu ktk enzi zisizo na Biblia,tenzi za rohoni,kuhani yeye mwenyewe!

Akastahimili vishindo! Je dhiki kuu hali ikiwa zaidi ya hii utaweza kuimudu?

subira yake inakufundisha nini?

Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona

mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.( Yakobo 5 : 8,11)

Page 84: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

84

MUHTASARI KITABU CHA ZABURI!

Kina Sura 150

Kina Mistari 2,461

Dhima kuu: NYIMBO ZA SIFA NA MAOMBI !

Mwaka Wa uandishi: hasa karne ya 10 hadi karne ya 5.

Mahali :

Mwandishi : Daudi, na wengine

"Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi.Daudi, mwana wa Yese, anena,Anena huyo mtu

aliyeinuliwa juu,Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye

kupendeza;"(2Sam 23:1)

Kwa kiebrania jina hili "Tehillim"="sifa",psalmoi="zaburi"

NI kitabu kirefu kuliko vyote ktk Biblia!

Kilicho na sura ndefu kuliko zote ktk Biblia (119:1-176)

Chenye sura fupi kuliko zote( 117:1-2)

Chenye mistari ya katikati yaani inaigawa Biblia,nusu kwa nusu (118:8)

Kama kitabu cha nyimbo cha kiebrania na cha ibada na sala.

Urefu na upana Wa kiroho huzifanya Zaburi kusomwa zaidi,na kukifanya kuwa na thamani zaidi

kwa waumini wengi.

Neno "HALLELUYA" yaani Msifuni Bwana,limetokea mara 28 ktk Biblia na kati ya hizo 24

zimo ktk Zaburi.

Na zaburi ya 150 ilimaliza kwa kutoa sifa kamili ktk hisia kamilifu ya kumsifu Bwana!

Daudi aliandika zaburi 73 ama na zaidi.

Asafu(walawi wenye kipaji cha uimbaji na unabii)aliandika zaburi 12.

Yaani Zaburi ya 50,73 hadi 83

Wana Wa Kora(familia yenye kipaji cha uimbaji)waliandika zaburi 10.

Page 85: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

85

Mfalme Sulemani aliandika 2

Hemani aliandika 1 zaburi ya 88

Ethani aliandika 1. Zaburi ya 89

Musa aliandika 1.(Zaburi ya 90)

Jumla ya zaburi 50 waandishi wake hawajulikani moja kwa moja! Mfano Daudi,Hezekia,na Ezra!

Ukiondoa Musa,Daudi na Sulemani, waandishi wengine wote waliotajwa walikuwa makuhani au

walawi wenye vipaji vya mambo ya muziki enzi za Daudi.

Zaburi imegawanyika katika vitabu 5 kama ifuatavyo!

1.Kitabu cha 1: Zaburi 1-41

Kiasi kikubwa NI Daudi! mf. Zab 3 : Daudi alipokuwa anamkimbia mwanae Absalomu.

Zab 32: Maskil=" shairi la kuelimisha"

2. Kitabu cha 2: Zaburi 42-72

Daudi na wana Wa Kora(mf. Zab 47)

3. Kitabu cha 3: Zaburi 73-89

Kiasi kikubwa NI Asafu(mf. Zab 79)

4. Kitabu cha 4: zaburi 90-106

Mfano Zaburi ya 90 ni ya Musa.

5. Kitabu cha 5: Zaburi 107-150

Zaburi ya 8.

Wewe, MUNGU, Bwana wetuJinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!👋Wewe umeuweka

utukufu wako mbinguni;

Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,Na binadamu hata umwangalie?

Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu;Umemvika taji ya utukufu na heshima;

Page 86: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

86

Mtume Paulo akaandika juu ya Zaburi,akiona faida ya kuimba pale walipokuwa wamefungwa

gerezani yeye na Sila! Gereza lilitikiswa,minyororo ikalegea malango ya chuma yalifunguka bila

ufunguo wala kusukumwa!

Kuimba NI kuzuri,kuimba kwapendeza sikia hii....

"Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana

kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni

mwenu."

Yakobo anamaliza kwa kusema mausia haya muhimu!

"Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe

zaburi.".

Page 87: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

87

MUHTASARI: KITABU CHA MITHALI!

Sura 31

Mistari 915

Dhima kuu: HEKIMA YA KUISHI KWA HAKI !

Mwaka Wa uandishi:950-931

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Sulemani,Aguri ,Lemueli

"Mashal "=" Mithali"="mafumbo"

Mwasisi ni Mfalme Sulemani.

Aliandika mithali 3,000. Alitunga nyimbo 1,005 enzi ya Maisha yake!

Sura ya 25-29 zilikusanya na Mfalme Hezekia baada ya miaka 230 kupita!

Aguri aliandika sura ya 30

Mfalme Lemueli. aliandika sura ya 31

Ni mithali 800 za Sulemani zilizomo katika kitabu hiki

Hivyo kuna mithali 2300 sisizomo ktk kitabu hiki.

Tafakari hekima hii je unaweza ngamua nini?

Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Usije ukafanana naye.

Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

(Mithali 26:4-5)

Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa

ufahamu.(Mithali 17:28)

Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika

upumbavu wake. (Mithali 17:12)

Page 88: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

88

Turudi kwenye wazo kuu!

Hebu tutazame kwa muhtasari hekima za Sulemani.!

1. Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.

2 Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu;

3 kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili.

4 Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari;

5 mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye

njia.

6 Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.

7 Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Hii inatuonesha namna Sulemani alivyokuwa na hekima, aliwafundisha wengi, alipendwa na

wengi,wengi walikuja toka mbali kuisikia hekima hii!.

Je mambo yanakuwaje pale mwandishi, mhubiri, mchungaji, na mwalimu anashindwa kukiishi

kile alichofundisha?

Kweli Sulemani kwa hekima alifanikiwa,ila pale alipoiweka kando na kuruhusu hisia,na

matamanio yake kupata nafasi zaidi. Alijikuta amefanya upumbavu mwingi sana! Hadi

kumfanya kuona kila kitu alichokifanya, NI ubatili na kujilisha upepo! ...hii ni katika kitabu

chake cha pili cha Mhubiri.

Page 89: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

89

MUHTASARI: KITABU CHA MHUBIRI!

Kina Sura 12

Kina Mistari, 222

Dhima kuu: maisha kutokuwa na maana bila Mungu !

Mwaka Wa uandishi: 935-931K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Sulemani

"Goheleth"="MTU mwenye kutawala na kuhutubia mkutano"="Mwalimu"= ekklesiastes=

Mhubiri.

Katika desturi za wayahudi,katika Hagiographa yaani "maandiko matakatifu" walikisoma kitabu

hiki haswa walipokuwa wanaadhimisha sikukuu ya vibanda.

Mfalme Sulemani sasa NI mzee,anatoa ushuhuda wake wenye majuto, anakumbuka siku za

ujana wake alipoomba Hekima,akajaliwa hadi mambo ya ziada! Akaandika kitabu chake cha

kwanza cha Mithali,wakati alipoingia katika mahusiano ya ndoa,akaandika wimbo ulio bora

katika ubora wake, sasa mvi zimetanda kichwani pake,anaegemea mkongojo, anategemea

msaada Wa wengine ili kuweza kuishi vizuri. wingi wa mali,wake 1000 aliokuwa nao na ukuu

wa sifa zilimpelekea kuporomoka kiroho,kuishi Maisha ya anasa na dhambi.

Akitathimini haoni furaha kabisa kwa Maisha aliyoishi.

maisha chini ya Jua*(29) ni ubatili,ubatili mtupu nasema ubatili mtupu! (neno linaojirudia mara

37 katika kitabu hiki)! Kuishi Maisha nje ya mpango Wa Mungu! NI ubatili,sawa na kufukuza

upepo!

mfalme Sulemani anawaonya vijana,wanaopenda umaarufu,kujulikana,wanaopenda kuoa

wanawake wengi,wenye uchu na mafanikio,utajiri Wa kupindukia wajifunze kutoka kwake!

ndio maana akausia kwa kusema....

" Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,Wala

haijakaribia miaka utakaposema,Mimi sina furaha katika hiyo."

Akaongeza kwa msisizo!

".. Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu

vingi; na kusoma sana huuchosha mwili."

Page 90: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

90

"Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa;Mche Mungu, nawe uzishike amri

zake,Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa

baya".

Mwisho Wa kumnukuu!

Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi,

tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.(1Korintho 10:11-12)

Page 91: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

91

MUHTASARI WA KITABU CHA WIMBO ULIO BORA

KATIKA UBORA WAKE!

Kina Sura 8

Kina Mistari 117

Dhima kuu: UPENDO KATIKA NDOA!

Mwaka Wa uandishi: 971-960 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Sulemani.

Maneno kama..

"Nakupenda",Nimeanguka kukupenda(am fall in love),my honey,my sweet, my every thing! Sio

mageni kwa ulimwengu wa watu wanaopendana!

Nyimbo za mapenzi hazikuanzishwa na bongo flavor, blues,reggae,hip hop,taarabu na kadhalika!

Alianza Mfalme Suleman na mpenzi wake hapo kale kwa mistari ya mashairi yenye uzito Wa

mapenzi ya kweli! Sio mipasho!

"'Mashavu yako ni mazuri kwa mashada,Shingo yako kwa mikufu ya vito. Tazama, u mzuri,

mpenzi wangu,U mzuri, macho yako ni kama ya hua."

"Wimbo Wa nyimbo"

NI wimbo Wa mapenzi kwa wanaopendana!

Katika zile nyimbo 1,005 alizozitunga huu ukawa bora! Wimbo Wa arusi ulio bora kuliko zote

zilizowahi kuandikwa!

Sura ya 8 kuna aina 15 za wanyama,aina 21 za mimea.

ilikuwa Kabla ya kuoa wake 700 na Masuria 300.

Wayahudi Wa ki- Orthodox waliweka sheria kuwa MTU atakapofikisha miaka 30 ndipo

ataruhusiwa kukisoma kitabu hiki.

"Bustani iliyofungwa"(4:12)= ubikira Wa bibi arusi

Mwanamke Mshulami!

Page 92: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

92

Mazingira ya kitabu!

Kuna majina ya maeneo tofauti tofauti 15 kuanzia kusini mwa Misri hadi kaskazini mwa

Lebanoni.

Mfano; Kuanzia mashambani,mjini na mlimani, kaskazini mwa Yerusalemu.

Matukio ya harusi,fungate na Maisha ya mwanzoni yanaonekana zaidi Yerusalemu ( sura 3:6 -

7:13)

Kuna wahusika wakuu 3:

1. Sulemani ametajwa mara 7 (Bwana Arusi)

2. mwanawali Mshulami(bibi Arusi)

3. Na binti za Yerusalemu.(wageni waalikwa)

Inawezekana Mwanawali Mshulami alikuwa na asili ya Afrika...Mimi NI mweusi lakini ninao

uzuri,.

Alikuwa chaguo na mke Wa kwanza kwa Sulemani.

Usafi na ubora Wa kuwa na subira katika mapenzi ya watu wawili wanaopendana wakati

watapooana! Na kuishi pamoja kama Mme na mke!.

Inakosoa vikali, kuwaka tamaa na kujitia unajisi kwa kuingia katika mapenzi ya ndoa,kabla ya

wakati wake na nje ya ndoa.

"Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwa paa na kwa ayala wa porini,Msiyachochee mapenzi,

wala kuyaamsha,Hata yatakapoona vema yenyewe."(2:7)

Ndio maana maandiko yakaonya mapema kuwa!!!

Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi,

Mungu atawahukumia adhabu.(ebrania 13:4)

Page 93: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

93

Mgawanyo Wa kitabu!

1. Maisha ya uchumba..(1:2-3:5)

Mistari/aya 32 kati ya 39 inazungumzwa na mwanawali Mshulami,akimkumbuka

mchumba(mpendwa) wake,na anavyomngoja aje amchukue ili wakafunge ndoa Yerusalemu..

mazungumzo yake yanakatishwa katishwa na binti za Yerusalemu na Mpendwa wake!

2. Tukio la kufunga ndoa(harusi)

Bwana Arusi(mfalme Sulemani) 3:6-11

Harusi na usiku ule Wa kuwa pamoja 4: 1-5

3. Maisha ya ndoa (sura ya 5:2-8:4)

Jambo la kwanza la kutokuelewana likitokea.(5:2-6:3)

"Tukamatie mbweha,Wale mbweha wadogo,Waiharibuo mizabibu,Maana mizabibu yetu

yachanua." anatoa wito kuwa kuna mambo/matatizo(mbweha wadogo) wanaoharibu penzi la

wanaopendana!

Mbweha huaribu ndoa changa na kuzifanya zisiwe na matunda mazuri kwa jinsi ilivyokusudiwa!

Usiruhusu waharibu ndoa yako! Kwa kudharau kuwa NI wadogo! Hata kama mlipendana zaidi

ya sumaku na sumaku hawa jamaa wataharibu tu!

mbweha hawa wameharibu ndoa zenye miaka 20,50..familia kutawanyika na kuleta majanga

katika jamii.

Kupatana tena.(6:4-8-4)

BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana,

angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.

Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; (Malaki 2:14,16)

Kuendelea kukua katika ndoa yao.(8:5-14)

"Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake"

Page 94: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

94

MUHTASARI KITABU CHA ISAYA!

Kina Sura 66

Kina Mistari :1292

Dhima kuu: HUKUMU NA WOKOVU!

Mwaka Wa uandishi: 740*/700-680

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : ISAYA

Nabii Wa injili.alitabiri kwa miaka 40 ama na zaidi,alikufa mwaka 680 K.K

Paulo Wa Agano la kale,Injili kama ilivyoandikwa na nabii Isaya, ni wasifu wa nabii Isaya na

jina lake lenye maana ya "Bwana anaokoa" ni moja kati ya manabii wakubwa 5 wa Agano la

kale!. aliandika kwa kirefu unabii wake wenye sura 66 sawa na Vitabu 66 vya Biblia!

Sura 39 sawa na Vitabu 39 vya Agano la Kale,zikieleza hukumu ya Mungu kwa Israeli,kutokana

na kukiuka Torati,hukumu juu ya mataifa jirani.

Sura 27 sawa na Vitabu 27 vya Agano Jipya zikitabiri ukombozi/wokovu Wa Israeli na ujio Wa

Masihi kama vile Agano Jipya NI ukombozi kwa ulimwengu wote!

Waliofanya Huduma ya kinabii enzi zake walikuwa nabii Hosea na nabii Mika.

jina refu kuliko yote katika Biblia NI jina la mtoto Wa pili wa Isaya "MAHAR-SHALAL-

HASH-BAZI" lenye maana ya "mwepesi kuteka nyara,mwepesi kuchukua mateka"(8:1)lenye

kutabiri kuanguka kwa Aramu kwa Waashuru na Israeli kwa Babeli.

"SHEA-YASHUBU" Ni jina la mwana Wa kwanza Wa Isaya lenye maana ya "mabaki watarudi"

akionesha kuwa Mungu atahifadhi uzao kwa ajili ya kutimiza mpango wake!.

Kitabu cha Isaya kinamzungumzia Ma­sihi zaidi. Kina ufunuo juu ya Masihi zaidi kuliko vitabu

vingine vya manabii.

Neno "wokovu" limetumika mara 26 katika kitabu chake ukiinganisha na mara 7 katika jumla ya

Vitabu vya manabii wengine!

Page 95: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

95

Wafalme wakati wa Isaya walikuwa ni Uzia, Yothamu, Ahazi, Hezekia na Manase.

1.Azaria, yaani Uzia(Yehova ni nguvu zangu), Mwaka (767-740) mwana wa Amazia alitawala

miaka 52. Alifanya mema. Aliugua muda mrefu, hakuweza kutawala mwishoni. Alipokufa ndipo

Isaya alimwona Bwana! Sura ya 6.

2.Yothamu, (750/740-735) mwana wa Azaria alitawala miaka 16. Alifanya mema.

3.Ahazi:(anayemiliki) (732-716) mwana wa Yothamu miaka 16. Hakufanya mazuri.

722 K.K.Israeli ya Kaskazini ilihamishwa Ashuru. Israeli ya Kaskazini haikuwepo tena. (2FAL

17)

4. Hezekia(Yehova ameimarisha), (716-687 K.K.)

Mwana wa Ahazi alitawala miaka 29. Alifanya mazuri. Alitakasa hekalu kwa kuanzisha upya

ibada.Aliugua lakini aliongezewa maisha miaka 15.

710 K.K Yerusalemu ilinusuriwa!

5. Manase(-ya kusahau), (687-643 K.K.)

mwana wa Hezekia,miaka 7 tu tangu baba yake kufa,alifanya mabaya mengi! alitawala miaka 55.

Alifanya mabaya. Ndie aliyemuua nabii Isaya kwa kumkata na msumeno vipande viwili.

Japokuwa mama yake(Hefsiba) alikuwa binti Wa Isaya sawa na kusema; alimuua Babu yake

kwa ukatili kabisa!.

Isaya anatangaza hukumu tangu sura ya 1-39. Na anatangaza faraja(tumaini la wokovu) kwanzia

sura ya 40-66.

ameeleza namna vita vile vilivyomfurumusha Shetani na malaika zake kutoka mbinguni,alitoa

unabii wa mfalme Koreshi atakayekuja kuwaruhusu israeli kurudi nchi yao,kwa kumtaja kwa

jina kabisa!.

Alitabiri juu ya kuja kwa Yohana mbatizaji, alitabiri juu ya Masihi na kifo chake msalabani (sura

53),ametabiri juu ya miaka 1000 ya utawala Wa Kristo hapa duniani, ametabiri juu ya

kuharibiwa kwa dunia hii,ametabiri juu ya mbingu mpya na nchi mpya!

Page 96: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

96

MUHTASARI KITABU CHA YEREMIA

Kina Sura 52.

Kina Mistari 1364.

Dhima kuu: Hukumu isiyopingika/Epukika

(Unpingikable judgement)!

Mwaka Wa uandishi: 586-580 K.K

Mwaka Wa tukio: 627-586 K.K

Hadhira: ufalme Wa Yuda uliokuwa umebakia!

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : YEREMIA

Katibu: Baruku.

Wasifu Wa Yeremia!

Maana ya jina Yeremia= "Yehova Bwana Atukuzwe" Au, Yeremia = Mungu ni Mkuu. Mungu

anainua.Mwana Wa kuhani Hilkia,alizaliwa na kulelewa katika kijiji cha kikuhani cha Anatothi,

kama maili 4 kaskazini mashariki mwa Yerusalemu. Alizaliwa kipindi cha mfalme mwovu

Manase.

Alianza huduma yake ya unabii katika mwaka Wa 13 Wa mfalme mzuri Yosia.

Alitoa unabii wake kwa miaka 40; (626-586) K.K huku akiwa shahidi Wa mwisho Wa historia

ya ufalme Wa Yuda. Kama vile kuharibiwa kwa Yerusalemu,na Hekalu.

Moja kati ya manabii wakubwa katika Biblia. Wengi walimchukia kwa sababu hakutabiri mazuri

Bali mabaya tu, nabii huyu hakuoa! (16:1-9)

Alifungwa Mara kadhaa,alichapwa bakora,alitupwa kwenye shimo la matope,alishinda na

njaa,alidhihakiwa,aliitwa nabii mwombolezaji.

alikuwa MTU mwenye ujumbe mkali sana,(heartbroken message)lakini mwenye moyo mwepesi

sana kuhurumia,kuumia na kuomboleza kwa ajili ya taifa lake!

moyo mwepesi lakini roho ya chuma katika kutekeleza mapenzi ya Mungu.

Page 97: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

97

Mfano; dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma! Linganisha na-Maombolezo makuu

katika Rama! Yaani Bethehemu!

aliyahubiria masikio yenye uziwi na kuvuna chuki kama malipo ya upendo kwa wayahudi

wenzake! baada ya kutoa unabii kwa miaka 20,Mungu alimwagiza autie unabii wake katika

maandishi..alikuwa na Katibu wake Baruku aliyemsaidia kuandika (36:1-4)

misukusuko mikali mfano, Gombo la chuo chake lilikatwakatwa na kutupwa motoni na mfalme

Yehoyakini (36:22-23).Baruku akikamilisha sehemu ya unabii Wa Yeremia pengine baada ya

kifo cha Yeremia (sura ya 52).

unabii ulitolewa kwa wafalme Yosia,Yehoahazi,Yehoiakini na Zedekia! Miaka 70 ya utumwa

ilikuwa inawasubiri(inafuatia) baada ya adhi kukosa sabato zake (miaka 490)tangu enzi za kina

Sauli hadi Zedekia. Manabii waliokuwepo kipindi hicho walikuwa Sefania,Habakuki,Danieli na

Ezekieli japo wengine walikuwa bado hawajaanza unabii wao.

Kitabu chenyewe!

Ni kitabu cha 2 kwa ukubwa(kwa maneno) katika Biblia,kikiwa na maneno mengi zaidi baada ya

Zaburi(sio sura).

matumizi ya lugha ya picha mfano "ufito Wa mlozi" ukimaanisha!..

'Mti Wa mlozi ni mti Wa kwanza kuchipua wakati wa majira ya kuchipua'

hivyo unabii Wa Yeremia unafanya haraka kutimia!

Ndio maana baada ya unabii wake akaandika waraka (kitabu) wake Wa 2 Wa Maombolezo.

ni unabii Wa kung'oa, kuharibu na kuponda pia ni unabii Wa kupanda,kujenga na kukuza.

Je wewe ni rungu la Bwana??

Page 98: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

98

MUHTASARI, KITABU CHA MAOMBOLEZO.

Kina Sura 5.

Kina Mistari 154.

Dhima kuu:Huzuni na Matumaini ya baadae !

Mwaka Wa uandishi: 586K.K

Hadhira: watu Wa Yuda.

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : YEREMIA

Kitabu cha pili cha Yeremia,

Kwa mapokeo ya kiyahudi ni sehemu ya Hagiographa(maandiko matakatifu);

Ruthu,Esta,Mhubiri,Wimbo ulio bora na Maombolezo.

Mara nyingi kilisomwa siku ya 9 ya mwezi Abib (karibia katikati ya Julai)

Mafungu 5 ya kitabu hiki,ni mashairi 5 yanayoomboleza juu ya kubomolewa kwa Jerusalem Na

wababeli mwaka 587k.K mateso Yale yaliyotokana Na kuzingirwa kivita,watu wakafa njaa

mjini,tauni ikawaua Na upanga pia ukawaua pale walipojaribu kutoroka! Mali zao ziliporwa Na

nyingine kuchomwa moto!

Katika mashairi 3 kati ya Yale 5 aya zote 22 za kila shairi zinaanza kwa mfunulizo Wa herufi 22

za alfabeti ya kiebrania. Shairi moja lina aya 66 zilizopangwa katika vifungu 22 vyenye aya tatu

tatu. Katika shairi lile ambalo pia ni katikati ya mkusanyo Wa Yale 5 ,aya zote 3 za kila kifungo

zinaanza kwa herufi ile ile, Na herufi ya kwanza za vifungu vile zinafuata mfunulizo Wa alfabeti

ya kiebrania tena. Shairi la mwisho pia lina aya 22.

Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa,Huo uliokuwa umejaa watu!Jinsi alivyokuwa kama mjane,Yeye

aliyekuwa mkuu kati ya mataifa!Binti mfalme kati ya majimbo,Jinsi alivyoshikwa shokoa!

(Maombolezo 1:1)

wakati wasemapo kuna amani ndipo uharibifu unapotokea! Nabii Yeremia alitabiri kipindi cha

amani,watu walimchukia sana maana alikuwa anawavunja moyo askari waliokuwa tayari

kuulinda mji Wa Yerusalemu kwa ulinzi Wa uhakika.

Page 99: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

99

alipoona unabii wake unakosa wasikilizaji, kwa masikio ya kufa,alianza kuomboleza kabla ya

wakati,maana alijua siku ya msiba wao hatakuwa na nguvu ya kuomboleza tena.!

Wakaldayo waliuzingira mji Wa Yerusalemu kwa miaka 2 na miezi 5, hivyo juhudi zao

zikadhoofika kwa njaa, tauni ikawapata, mahitaji yao yakawalazimu kutoboa sehemu ya ukuta,ili

wakaziokoe nafsi zao.!Lakini Mfalme Sedekia alipotoroka kupitia tundu lile ,alikamatwa na

kufungwa hadi Babeli,alipotobolewa macho yake yote baada ya kuuwawa kwa watoto wake

mbele ya macho yake!.kisha akatiwa kifungoni.

ipo siku utaomboleza! Kwa mazuri ama mabaya! Jipatie moyo wa hekima! Maana Kwa kufiwa

na MTU umpendae,ama kwa kupatwa na jambo baya lazima kuomboleza!

lakini pia IPO siku ya kiama! Kulia na kusaga meno! Japo utaomboleza! Yatakuwa maombolezo

ya milele!

Jiepushe na maombolezo yasio ya msingi! MPE Yesu maisha! Chagua UZIMA! Amua kuishi

maisha matakatifu! Omboleza kwa wenye dhambi wasiomjua Mungu lau kwamba Neema

iwaangukie watubu waokolewe!.

Yapo majira ya dhiki kuu,kuomboleza hakuepukiki!

Fanya maamuzi ya milele!

Page 100: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

100

MUHTASARI WA KITABU CHA EZEKIELI.

"Ikawa katika mwaka wa 30, mwezi wa 4, siku ya 5 ya mwezi, nilipokuwa pamoja na watu

waliohamishwa, karibu na mto Kebari, mbingu zilifunuka, nikaona maono ya Mungu."

Kina Sura 48.

Kina Mistari 1,273.

Dhima kuu: Hukumu na utukufu Wa Mungu!

Mwaka Wa uandishi: 590-570K.K

Mahali : Babeli.

Mwandishi : Ezekieli.

Wasifu Wa Ezekieli.

Maana ya jina Ezekieli: "Mungu ataimarisha", "Mungu hutia nguvu"

Alikuwa mwana Wa Buzi. Mwenyeji Wa Yerusalemu

Ezekieli alikuwa kuhani,

alikuwa na miaka 17 hapo aliposhuhudia kundi la kina Danieli na wenzake wakichukuliwa

mateka mwaka 605 K.K.

mwaka 597 K.K. alikuwa na miaka 25 alipochukuliwa mateka zaidi ya watu 10,000 kwenda

Babeli.

Julai, 593 K.K alipokea wito Wa kinabii akiwa na miaka 30,alitoa unabii wake kwa wayahudi

walioko utumwani Babeli.

Miaka 8 ama 9 ilipita tangu Danieli achukuliwe mateka,na miaka 11 ama 12 kabla ya mji Wa

Yerusalemu haujabomolewa!

wakati Danieli akihudumu mjini Babeli,Ezekieli alikuwa akihudumu vijijini mwa Babeli.

Aprili, 571K.K. Huduma yake ya unabii ilifikia mwisho.

Alioa mke; mke akiwa sehemu ya unabii kutimizwa! Na siku alipokufa aliambiwa asilie wala

kuomboleza.

Mke wa Ezekieli alifariki siku ile ile jeshi la Babeli lilipoanza kuzunguka mji wa Yerusalemu,

Page 101: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

101

Januari 15, 588 K.K na baada ya miaka 2 na miezi 5, ya kuzingirwa ndipo ukateketezwa kwa

moto na wengi kuchukuliwa mateka 586.K.K.

Ni kitabu chenye tarehe nyingi kuliko kitabu kingine chochote cha unabii katika Agano la Kale.

Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la

BWANA. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu,

nanyi mtaishi.

(Ezekieli 37: 4-5)

Kila penye huzuni lipo neno jema lenye kuganga upya! Tabiria tatizo lako!

Page 102: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

102

MUHTASARI WA KITABU CHA DANIELI.

Kina Sura 12.

Kina Mistari 357.

Dhima kuu:Ukuu Wa Mungu katika Historia !

Mwaka Wa uandishi: 536-530K.K

Mahali : Babeli

Mwandishi : Danieli.

Muundo:

Sura 1-6 Historia

Sura 7-12 Unabii

Kimetumia lugha ya mafumbo,kuelezea falme(dola) mashuhuri kuu 4 zitakazo tawala,kuinuka na

kuanguka hadi atakapokuja Masihi kusimika utawala wake Wa Milenia(jiwe liliojaza limwengu

mzima).

Lugha mbili zimetumika

Sura 1-2:4a kiebrania

Sura 2:4b-7 kiaramu

Sura 7-12 kiebrania

Kwa Biblia zile zenye vitabu vya Aprokrifa zinazotumika hasa na Wakatoliki,kitabu cha Danieli

kina nyongeza ya sura 2 yaani sura ya 13-14.

Maana ya jina Danieli="Mungu ndie mwamuzi WANGU"

Mungu alikuwa mwamuzi wake, pale viongozi wenzake waandamizi walipomfanyia fitina

kutokana na wivu Wa madaraka wakamtia katika shimo la simba lakini simba hawakumwesabu

miongoni mwa kitoweo(hawakumdhuru.)

Katika mwaka Wa 3 Wa kutawala kwake Yehoyakimu mwana Wa Yosia,Mfalme Wa 18 Wa

Yuda aliyetawala kati ya 608-597 k.K Danieli na wengine wengi pamoja na vyombo vya hekalu.

alikuwa miongoni mwa kundi la kwanza lililochukuliwa mateka na Mfalme Nebukadneza

kwenda Babeli.(605 k.K) na alikuwa Wa ukoo Wa kifalme!.aliyetoka familia iliyoelimika ya

Page 103: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

103

tabaka la juu katika Yerusalemu.na akiwa Babeli alitumika katika serikali za wafalme

kadhaa(Nebukadneza,Belteshaza,Koreshi(Dario). kwa miaka 70. na zaidi.

Alishughulika Babeli kwa muda mrefu.

Aliendelea hadi mwaka wa 530 kabla ya Kristo.

Huenda alifanywa kuwa towashi,maana hakuoa

Na huenda alikuwa Wa uzao Wa Mfalme Hezekia.

" Na baadhi ya wanao watakaotoka kwako, utakaowazaa, watawachukulia mbali; nao watakuwa

matowashi jumbani mwake mfalme wa Babeli".

(2 Wafalme 20:18)

Kitabu cha Danieli kiliandikwa uhamishoni Babeli.

Wakati wa Danieli walikuwepo pia Ye­remia na Ezekieli. Yeremia ali­hubiri Israeli, na Ezekieli

katika vijiji vya Babeli na Danieli katika mji wa Babeli. Danieli alipokuwa amekaa Babeli karibu

miaka 20 hekalu la Yerusalemu lilibomolewa. Ilitokea mwaka wa 586 K.K (kabla ya Kristo) na

wakati huo Wayahudi wengi walipelekwa Babeli.

Kitabu cha Danieli kina unabii mwingi tofauti. Mengine yalitokea kabla ya Kristo, mengine bado

hayajatimia.

Ni kitabu kifupi kinachosomwa zaidi kati ya Vitabu 4(Isaya,Yeremia,Ezekieli,Danieli) vya

unabii vya agano la kale.

Ndio ufunuo Wa Agano la kale! Kikieleza mafunuo ya kabla ya Kristo na Nyakati za mwisho

zitakazoupata ulimwengu huu!

abari za Danieli na rafiki zake 3 zinatoa faida za vijana walioishi bila kuyumbishwa(Non-

compromised) na mazingira mageni katika kuitetea imani yao katika Mungu.

Oooh Yale maandishi ya Mungu mwenyewe! "MENE MENE TEKELI NA

PERESI"yanaendelea kuzipima tawala za mataifa ya sasa na kuyaambia kuanguka yataanguka na

kupisha ufalme Wa Yesu Kristo kutawala.!

Nakutakia usomaji mzuri kabisa Wa kitabu hiki kizuri cha Ufunuo Wa Danieli. Utajifunza mengi.

Usilegeze msimamo wa imani yako.!

Page 104: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

104

MUHTASARI KITABU CHA HOSEA!

Kina Sura 14.

Kina Mistari 197.

Dhima kuu: hukumu na Upendo Wa kukomboa Wa Mungu!

Mwaka Wa uandishi: 715-710 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Hosea

Hosea=" wokovu" mwana Wa Beeri.

Ni nabii Wa kaskazini aliyeitwa na Mungu kutoa unabii kupitia Maisha ya ndoa yake!

Kama vile Mungu alivyofanya Agano na Israeli kadhalika Hosea alifanya agano na Gomeri.

Israeli walimwacha Mungu wao na kwenda kuabudu miungu mingine,mabaali japo Mungu bado

alikuwa anawapenda!

Gomeri mke Wa Hosea alianza ukahaba,kisha akanunuliwa kuwa mjakazi kwa MTU mwingine!

Hosea alikwenda kumkomboa kwa fedha na kumrudisha tena kuwa mke wake! Kadhalika

Mungu atawapeleka Israeli utumwani kama adhabu,kisha atawakomboa!

Alikuwa na watoto 3 wenye unabii ufuatao!.

Yezreeli= Mungu hutawanya

Lo-Ruhama= asiyependwa

Lo- Ami = sio watu wangu!

Hivyo hukumu ya Israeli ni ya uhakika!

Mwaka 753 alianza unabii na 715 unabii ukakamilika.

Ni moja kati ya manabii wadogo 12 aliyeitwa kutoa unabii kwa makabila 10 ya Israeli.

Hosea na Yona ni manabii wadogo pekee wanaoitwa kutoa unabii wakiwa Wa ufalme Wa Israeli.

Alianza unabii wake mwishoni Wa kipindi cha utawala wenye mafanikio Wa Mfalme

Yeroboamu II,

Kwa muda kama Wa miaka 45,kwa kipindi cha wafalme 7 Wa Israeli na 4 Wa Yuda,

Page 105: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

105

Hii ilikuwa baada ya Yona na Amosi kutoa unabii wao (Israeli) na Obadia,Yoeli huko Yuda.

wakati huo kulikuwa na matabaka!,

walionacho na wasio nacho!

Walionacho waliwaonea na kuwanyonya wasio nacho!.

Uchoyo na magendo ya hali ya juu!

Kunyanyaswa kwa watu Wa tabaka la chini.

Mahakimu walihongwa kupotosha haki.

Page 106: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

106

MUHTASARI WA KITABU CHA YOELI!

Kina Sura 3.

Kina Mistari 73.

Dhima kuu: Siku ya Bwana iliyokuu na ya kutisha!

Mwaka Wa uandishi: 830 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Yoeli.

Yoeli="Bwana NI Mungu"

Mwana Wa Pethueli. Alitabiri juu ya Yuda.

Nabii Yoeli ambaye jina lake lina maanisha Yehova ni Mungu alianza kutabiri juu ya Israeli

mnamo mwaka 835 K.K

kwa kusema SIKU YA BWANA ILIYO KUU INAKUJA akionya hukumu ya Mungu kwa Yuda

kama vile baa la nzige,tauni,njaa,moto na majanga ya kushambuliwa yanakuja juu ya taifa

hilo;hivyo akihimiza kila mtu atubu amrudie MUNGU naye atawarehemu watu wake,na

kusamehe uovu wao. Maafa makubwa ya uharibifu uliotokana na nzige ulisababisha njaa juu ya

wakulima na wenyeji Wa Yerusalemu!

Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na

yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.(1:4)

Hakuna aliyeweza kutoroka njaa ile,na kama alifanikiwa tauni ilimuua na kuteketezwa kwa moto,

Yerusalemu wengi walikufa kwa upanga!

Sasa anatoa unabii wa matengenezo!

Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi

langu kubwa nililotuma kati yenu.(2:25)

Akaongeza na unabii juu ya kuzaliwa kwa kanisa duniani!

Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na

wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona

maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho

yangu.(2:28)

Page 107: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

107

MUHTASARI WA KITABU CHA AMOSI.

Kina Sura 9.

Kina Mistari 146.

Dhima kuu: uadilifu,haki na adhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi !

Mwaka Wa uandishi: 755 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Amosi

Amosi="mbeba mzigo" .Nabii Wa karne ya 8 k.K

Nabii Amosi jina lake likimaanisha mbeba mzigo alikuwa mkulima, alipoitwa na Mungu kutoa

unabii juu ya Israeli na Yuda mnamo mwaka 755 K.K

akiubeba mzigo wa unabii mzito wa hukumu ya Mungu itakayokuja juu ya Taifa lake kwa

sababu ya maovu yao mengi kama kuwaonea maskini, kuabudu sanamu,kupokea

rushwa,kupotosha haki,na kufanya anasa.

Akitokea Tekoa mji ulioko maili 12 kusini mwa Yerusalemu,alikokuwa mchungaji wa kondoo,

Amosi alikuwa mchunga mifugo aliye­lima mizabibu mwitu. Alitabiri vikali juu ya ubaya wa

Israeli. Hali ya watu kiroho ilikuwa mbaya la­kini kimwili ilikuwa nzuri. Akaja kutoa unabii

wake Betheli(maili 12 kaskazini mwa Yerusalemu). hii ilikua Baada ya Obadia,Yoeli na Yona na

kabla ya Hosea,Mika na Isaya.kutoa unabii wao!

Kitabu hiki kina sura 9 zenye ujumbe mkuu wa hukumu ya Mungu kwa watu na mataifa

yatendayo uovu.

Ni katika Kipindi cha Mfalme Yeroboam II, Wa Israeli.

Page 108: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

108

MUHTASARI WA KITABU CHA OBADIA!

Kina Sura 1.

Kina Mistari 21,

Dhima kuu: Hukumu kwa Edomu!

Mwaka Wa uandishi: 845 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Obadia

Obadia="mtumishi Wa Mungu"

Nabii Obadia jina lake likimaanisha anayemwabudu Yehova alikuwa nabii pekee aliyetumwa na

Mungu kutoa unabii wa hukumu itakayokuja ya maangamizo ya Edomu[esau] kwa sababu ya

kuwachokoza Yuda. ☝Kumbukumbu la Amaleki lilifutwa chini ya jua! Sasa ni zamu ya Edomu!

Maana kipindi kile wametoka utumwani Misri wakaomba wapite katika nchi yao, kama njia

kufika kaanani,Amaleki, mbali na kukatalia ombi lao bado aliwaonea njiani na kuwanenenea

mabaya!

Kosa la Edomu; ni pale Nebukadneza alipoteketeza Yerusalem na vilivyomo na kuchukua

wengine mateka! Waedomu walipiga panda wakifurahia kutekwa kwa Yuda,wakawapora mali

zao,wakawasifu wakaldayo kuwashambulia zaidi. Sasa kibao kinajeuka! Shimo waliowachimbia

wengine linakuwa mtego kwao, mwisho wa unabii Obadia ni kuwa Taifa la Edomu halitainuka

tena!Mungu anaahidi marejesho ya Taifa lake Israeli.

Kitabu hiki kina sura 1 tu,katika Agano la kale! Wenye ujumbe mkuu wa hukumu ya Mungu juu

ya Waedomu. Taifa la Edomu lilipoteza uwepo wake kama taifa mwaka 150 k.K na jina lao

likapotea wakati Pompey Mrumi alipoitwaa Yerusalemu.

Herode alikuwa Wa uzao Wa Edomu kwa hila na kujipendekeza akapewa idhini ya kuwa

mtawala Wa koloni jipya la Rumi yaani Yudea. Herode kikawa ni cheo! Moja ya uzao wa

Herode,alikuwa herode Yule aliyeliwa na chango akafa kutokana na majivuno yake!.

MAANA YA HUKUMU:

Ni kupatikana na hatia inayostahili adhabu,na kuvuma kile ambacho mtu atakuwa amekipanda

kwa wema au kwa ubaya.

"Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika

kilima cha Esau? Asema Bwana ." Obadia 1:8

Page 109: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

109

MUHTASARI KITABU CHA YONA!

Kina Sura 4.

Kina Mistari 48.

Dhima kuu: Upana Wa Rehema ya Mungu iokoayo !

Mwaka Wa uandishi: 780-760 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Yona

Yona="hua" mwana Wa Amitai.

Alikuwa anatoka Gathi Hefa, maili 2-3 kaskazini mwa Nazarethi katika Galilaya. Alianza

huduma yake muda mfupi tu baada ya ile ya Elisha,(2Fal 13:14-19),ilikuja juu ya ile ya Amosi,

na kufuatiwa na ile ya Hosea.

Kwa kadri ya Wayahudi inawezekana Yona alikuwa kijana wa mjane wa Sa­repta aliyefufuliwa

na Eliya. (1FAL 17:17-22). Yona anajulikana kama mmi­sionari wa wapagani na kwa sababu ya

mahu­biri yake watu wa Ninawi walimge­ukia Mungu.

Hii ni wakati wa mfalme Yeroboamu II mwaka 793-753)k.K

Nabii Yona jina lake likiwa sawa na njiwa alitumwa na Mungu kwenda kutoa unabii kwa mji wa

Ninawi uliokuwa ukiongoza jeshi lote la Waashuru;ambalo lilikuwa katili na adui mkubwa kwa

taifa la Israeli[wakati anatawala mfalme Yeroboamu 2]; hivyo Yona kwa sababu alikuwa

anawachukia na anajua Mungu mwenye rehema anaweza kuwasamehe alikaidi akaukimbia uso

wa BWANA kwa kwenda magharibi, Tarshishi(Hispania),kama maili 2500 kutoka Israeli.

Ninawi ilikuwa kama maili 500 kaskazini mashariki mwa Galilaya.ulikuwa na wakazi zaidi ya

120,000.

Kitabu hiki kina ujumbe mkuu wa rehema kwa watu ikiwa watatubu. Ukuu na upana Wa rehema

ya Mungu iokoayo kwa njia ya kuhubiri toba!

Tambua kama Mungu amekuita hata kama utakuwa na sababu 100 za kukataa wito wake! Epuka

kujiletea hasara na kuwaletea wengine hasara! Amka na kuwa tayari wakati ufaao na usiofaa!

Yasijekukuta ya Yona!

Page 110: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

110

MUHTASARI KITABU CHA MIKA!

Kina Sura 7.

Kina Mistari 105

Dhima kuu: Hukumu na wokovu Wa Masihi!

Mwaka Wa uandishi: 735-710 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Mika.

"Nani kama Bwana?" ndio tafsiri ya jina la Mika!

Anatokea mji mdogo Wa Moresheth-Gathi kusini mwa Yuda.kama maili 25 hivi kusini

magharibi mwa Yerusalemu.

Mika aliwahubiria watu wa kawaida wa Samaria na Yerusalemu. Alizungumza juu ya hukumu

ijayo, uta­wala wa Masihi na neema ya mwisho kwa Waisraeli.

Wakati Wa utawala Wa wafalme 3 Wa Yuda,Mika alitoa unabii wake.

Yothamu (751-736) k.K

Ahazi (736-716) k.K

Hezekia (716- 687) k.K

Alitabiri juu ya kuanguka kwa Israeli na mji wake mkuu; Samaria na alitabiri juu ya Yuda na mji

mkuu wake Yerusalemu.

Isaya na Mika walishughulika na ufalme Wa Yuda,Vitabu vyao vina mambo mengi

yanayofanana na watu wengine walihisi kwamba huenda Mika alikuwa mwanafunzi mmojawapo

Wa Isaya! (Isa 8:16) Maovu mengi kama rushwa,dhuluma,zinaa viliongezeka kadiri watu

walivyofanikiwa! Maskini wakatabishwa zaidi,wahitaji wakadhulumiwa zaidi! Mahakamani

ikawa sehemu rahisi sana kwa matajiri kupendelewa na kunufaika na hukumu zisizo za haki!.

Nabii Mika anamalizia kwa kusema!!

Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA

atakuwa nuru kwangu.Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata

atakaponitetea teto langu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki

yake. (Mika 7:8-9)

Page 111: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

111

MUHTASARI WA KITABU CHA NAHUMU.

Kina Sura 3.

Kina Mistari 47.

Dhima kuu: kukaribia kwa maangamizi ya Ninawi !

Mwaka Wa uandishi: 661-612 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Nahumu

Maana ya jina Nahumu="mfariji"

Watu walikuwa wamerudia ukatili na ukandamizaji na kuabudu sanamu,Waashuru walikuwa

wameuteka ufalme Wa Kaskazini(Israeli) sasa walikuwa wanateka nyara sehemu za Yuda.

Nahumu anawafariji watu Wa Mungu kuwa Mungu anakwenda kuliangamiza taifa la Ashuru.

Mungu anatamani kuwapa muda wenye dhambi watubu lakini kuna mpaka Wa uvumilivu na

wema wake! Ukifikia mwisho hakuna tena nafasi ya toba Bali hukumu.

Nahumu mwenye hukumu ya Ashuru, alitumika wakati wa mfalme Yosia, yaani mwaka wa 640-

609 kabla ya Kristo. Yeye alitabiri maangamizi ya Ninawi.

Ninawi ilikuwa (mji)Jiji kuu la Ashuru. Umoja wa jeshi la Wamedi na Babeli uliangamiza

Ninawi, ilitokea mwaka wa 612 k.K. Nabii Yona alikuwa ametabiri, kwamba Ninawi

itaangamizwa. Ufunuo wa Yona ulitokea miaka 200 baadaye.

Nahumu anaeleza hukumu ya Mungu ilivyo Kali!

BWANA ni Mungu mwenye wivu, BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; juu ya

adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira. BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza

mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; (Nahumu 1:2-3)

Page 112: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

112

MUHTASARI WA KITABU CHA HABAKUKI.

Kina Sura 3.

Kina Mistari 56.

Dhima kuu:Bado Mungu anatawala kwa haki japokuwa Uovu unaonekana kama

hautazami.(Maisha ya Imani)

Mwaka Wa uandishi: 609-606 K.K,ndani ya(612-588)k.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : habakuki

Habakuki="kumbatia"

Nabii Habakuki jina lake humaanisha kukumbatia,Alikuwa miongoni mwa walawi waliohudumu

hekaluni,ndipo akaitwa kutoa unabii. Alitoa unabii wake mnamo miaka ya 610K.K

Akiwa ana maswali mengi.

[sura 1] akimuuliza Mungu kwanini maovu yanazidi kuongezeka na kama Mungu hayaoni na

hatoi hukumu yake kwao wayatendayo?

Analalamika ingawa anahubiri,bado Wayuda hawaoneshi dalili za maendeleo ya toba!.

Habakuki anauliza kama Mungu ni Mtakatifu na Yuda ni watu wake,inakuwaje awatumie

Wababeli wenye dhambi kuliko Yuda, kuadhibu Yuda?

[Sura ya 2] Mungu anamjibu kwa kumuonesha hukumu yake juu ya taifa la Yuda ipo tayari

mlangoni na Babeli itatumika kama fimbo kuiadhibu Yuda, kwa miaka 70 Yuda walikaa

utumwani Babeli. Uovu wowote ukiwa ni Wa Wababeli ama Wayuda utakuwa na adhabu stahili!

Ila aliye haki hana sababu ya kuogopa kitu.

[sura 3] Nabii Habakuki anaomba Rehema na toba juu ya taifa lake,akimsii Mungu katika

ghadabu akumbuke rehema. Kitabu hiki kina sura 3 tu zenye ujumbe mkuu wa hukumu ya

Mungu juu ya YUDA.

Nabii Habakuki anamaliza unabii wake kwa kuomba maombi haya!

"Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya

miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema." (Habakuki

3:2)

Page 113: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

113

MUHTASARI WA KITABU CHA SEFANIA.

Kina Sura 3.

Kina Mistari 53.

Dhima kuu: Siku ya Bwana !

Mwaka Wa uandishi: 635-630 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi :

Sefania=" Bwana huhifadhi"

Nabii Sefania jina lake humaanisha Yehova huifadhi,

Ni unabii kuwa Bwana anakwenda kuhifadhi mabaki ya taifa lake kwa siku ya Bwana inayokuja

ya kutisha!

Kimpangilio kati ya manabii wadogo 12! Ni nabii wa mwisho kabla ya watu wa Yuda

hawajapeleka utumwani Babeli. Na manabii wadogo 3 waliobaki yaani Hagai,Zekaria na Malaki

walitabiri baada ya kurudi kutoka Babeli.

Sefania alikuwa kitukuu Wa Mfalme Hezekia; alitoa unabii wake mnamo miaka 640 na 612K.K.

Alikuwa mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia-mfalme

wa Yuda[715-686K.K]; katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda,

Alitoa unabii wakati Wa Mfalme Yosia, akiwa NI Mfalme Wa mwisho mcha Mungu kutawala

Yuda. Sefania alitumika mwaka wa 638-608 k.K.

Alikuwepo wakati wa Yeremia na ali­kuwa sababu ya uamsho uliofanyika wakati wa Yosia.

Aliongea juu ya hukumu ya Yuda na makabila mengine na kuhusu Israeli itakavyostawi wakati

wa utawala wa Masihi.

Nabii huyu anakumbuka kuwa Mungu aliichafua lugha pale kwenye mnara wa Babeli,kila taifa

likawa na lugha yake lakini sasa lipo tumaini ya kurudishiwa lugha kama hapo kabla ya uasi wa

Babeli.

Maana hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliitia jina la BWANA,

wamtumikie kwa nia moja. (Sefania 3:9)

Hii ni kipindi cha kurudi mara ya 2 kwa Kristo na kusimika ufalme wake hapa duniani.

Page 114: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

114

MUHTASARI WA KITABU CHA HAGAI.

Kina Sura 2.

Kina Mistari 38.

Dhima kuu: Kujenga upya hekalu!

Mwaka Wa uandishi: 520 K.K

NI mwaka Wa 2 Wa Mfalme Dario Wa Uajemi.

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Hagai

Historia rejea!

Mwaka ule 539 k.K Mfalme Koreshi Wa uajemi aliporuhusu wayahudi warudi nchi yao! Pia

aliwaruhusu kujenga upya hekalu na kuendelea na ibada zao! Chini ya uongozi Wa Zerubabeli

na Yoshua kuhani mkuu,waliongoza watu kujenga hekalu lakini kutokana na ubinafsi Wa watu

wakuangalia tu mambo yao na uvivu.

walipopata upinzani kwa watu wengine waliokuwa wanaishi nchi yao walisitisha ujenzi ule!

Mwaka 536K.K walijenga kwa muda wa miaka 2, kisha wakaacha kuendeleza ili hekalu

likamilike wakajiendea kila mtu kwenye kazi zake kazi ya kujenga hekalu ikasimama kwa miaka

14 na

Miaka 16 ikapita pasipo ujenzi wowote kuendelea!

Mungu aliwaadhibu kwa njia zifuatazo;

1. Walipanda mbegu nyingi wakavuna kidogo!

Walitumia nguvu kubwa kufanikiwa,wakafanikiwa kidogo tu!

2. Fedha zao walizitia katika mifuko iliyotobokatoboka!

Kila walipofanikiwa, baraka zao zilipeperushwa!

3. Walikula chakula kingi lakini hawakushiba!

Walipofanikiwa hawakutoshelezwa na mahitaji yao!

Page 115: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

115

Mnamo Tarehe 1,(Eluli) yaani Agosti 29 mwaka 520 k.K

nabii Hagai alitoa ujumbe wake Wa kwanza Wa "maliza kujenga hekalu!"

Nabii Hagai jina lake humaanisha "sikukuu/sherehe"

mwaka 520 K.K kazi ikaendelea baada ya unabii wa Hagai na Zekaria kuwahimiza kwa

msisitizo ikafanyika kwa miaka 4 hadi hekalu likamalizika.

Alikuwa na umri Wa miaka 70-80 wakati akiandika kitabu hiki.

Ni kitabu cha 2 kwa ufupi baada ya kile cha obadia katika Agano la Kale!

Kitabu hiki kina taarifa 4 ambazo zote zilitolewa kwa mda wa miezi 6.

1. Ujumbe Wa namna Mungu alivyowa adhibu ukaleta matokeo mazuri,baada ya majuma 3 kazi

ya ujenzi ikaanza tena!

2. Kuwatia moyo,kuandaa mazingira ya kuja kwa Masihi.

3. Hukumu ingefuata uasi na baraka zingefuata utii kutokana na maonyo waliyopewa!

4. Ujumbe Wa kumtia moyo Zerubabeli.

Page 116: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

116

MUHTASARI WA KITABU CHA ZEKARIA!

Kina Sura 14.

Kina Mistari 211.

Dhima kuu:Ujenzi Wa Hekalu na Ahadi za Masihi !

Mwaka Wa uandishi: 520-470 K.K

Sura ya 1-8 mwaka 520-518 K.K

Sura ya 9-14 mwaka 480- 470 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Zekaria.

Hadhira: Wayahudi waliokuwa wamerejea Yerusalemu.

Historia rejea.

Mwaka 586 K.K hekalu lilibomolewa na kuteketezwa kwa moto.

Mwaka 516 K.K kumalizika kujengwa upya kwa Hekalu na kuwekwa wakfu. Hii ni baada ya

miaka 70. Tangu libomolewe!.

Wasifu Wa Zekaria.

Alikuwa Kuhani na nabii, Maana ya Zekaria ni "Yehova hukumbuka". Mwana Wa Berekia

mjukuu Wa Ido. Alikuwa mkuu Wa familia ya kikuhani. Aliuwawa kati ya patakatifu na

madhabahu yaani mahali pakufanyia maombezi. (Math 23:35)

"Katika mwezi wa 8 , mwaka wa 2 wa Dario, neno la BWANA lilimjia Zekaria, mwana wa

Berekia, mwana wa Ido, nabii, kusema,....."

Ilikuwa Novemba mwaka 520 K.K . Mungu alipomwinua Zekaria kuwa nabii. Kwanza amsaidie

Hagai kuwatia watu moyo kujenga upya hekalu.

Pili, kutabiri juu ya masihi atakayekuja.

Mfano "vipande 30 vya fedha" = kima cha mshahara Wa mtumwa.

Sura 6 za kwanza zina mfunulizo Wa maono 8 ya usiku aliyopewa katika miaka 2 ya kwanza ya

kujenga upya hekalu.

Page 117: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

117

Sura zilizobaki, unabii juu ya kuja kwa Kristo(Masihi) kwa Mara ya kwanza na ya pili .

Zekaria aliona maono maku­bwa, zaidi kuhusu Masihi na wakati wake. Sura za mwisho

zinaeleza kuhusu yata­kayoto­kea baadaye. Kuhusu kuja kwa Kristo na mambo ya­nayohusu

hayo.

"Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na

kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea,

kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake,

kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza". (Zekaria 12:10)

Page 118: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

118

MUHTASARI WA KITABU CHA MALAKI.

Kina Sura 4.

Kina Mistari 55.

Dhima kuu: Mastaka ya Mungu dhidi ya watu wake!

Mwaka Wa uandishi: 430-420 K.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Malaki

Malaki=" mjumbe WANGU" NI ufupisho Wa Malakia, ambayo humaanisha "mjumbe Wa

Bwana".

Manabii wadogo 3. baada ya Uhamisho(Post-Exilic prophets)

1. Haggai 520 k.K

2. Zekaria 520 – 518 k.K

3. Malaki 450 – 400 k.K

Nabii Wa mwisho Wa Agano la Kale!

Inafuatia miaka 400 ya ukimya pasipo sauti ya kinabii tena katika Israeli hadi kuja kwa Yohana

Mbatizaji aliyevunja ukimya huo! ambae Malaki alimtabiri.

Yeye alitabiri juu ya atayekuja kabla ya Masihi, yaani Yohana mbatizaji. Malaki aliona mbali na

aliona siku ya Bwana inayokuja juu ya Taifa lake! yaani siku ya ghadhabu ambapo Israeli

itakombolewa.

Muundo:

Mahojiano kati ya Mungu na watu wake kwa njia ya MASWALI na majibu (23) yaliulizwa kati

ya Mungu na watu wake. Alitabiri kipindi kimoja na Nehemia. Neno la Mungu lilikosa uzito

mioyoni mwa watu,kutokana na wingi wa maisha ya dhambi waliyokuwa wanaishi.

Mfano;

Makuhani walikuwa waovu,kiasi cha kuona sawa tu watu wakimtolea Mungu sadaka za

wizi,gonjwa na vilema! Kama ile aliyotoa Kaini,bado wanamwibia Mungu,japo wanajua hizo

sadaka zao wakimpelekea Katibu kata,diwani ama mkuu Wa wilaya hawezi kuzipokea bado

walitoa tu! Ilimradi watoe!

Page 119: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

119

Kisingizio kuwa wao ni taifa la Mungu kikawaponza kutokumtii Mungu ipasavyo katika Ukuu

wake wengine wakaoa watu wa mataifa,talaka likawa jambo la kawaida tu. Wengine wakaona

kumtumikia Mungu ni hasara tu! Jamani!Na Neno la Mwisho katika Agano la kale likawa ni

"Laana" (3:14)

MASWALI:

Hivi wasio haki wanafanikiwa vizuri kuliko wenye haki? Hapo inakuaje?????

Wasiotoa Zaka na sadaka wanastawi kuliko wale wanaozitoa??

Wengi wameacha kumtolea Mungu zaka na sadaka ili nao wafanikiwe!

Je haya madai yao ni ya kweli??

Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza,

akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha

BWANA, na kulitafakari jina lake. (Malaki 3:16)

Hebu sasa tukasome!

Page 120: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

120

KATI YA MALAKI NA MATHAYO NINI KILIENDELEA.

Nabii Malaki anafunga unabii wake kwa kusema

" angalieni nitawapelekea Eliya nabii,kabla haijaja Siku ile ya BWANA iliyo kuu Na kuogofya!"

Baada ya miaka hii 400 ya ukimya kupita. sauti ya Mungu yenye unabii ilisikika tena alipotokea

Yohana mbatizaji nyikani akisema " watu watubu maana ufalme Wa Mungu umekaribia".

ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote

waliyotaka.

Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji. (Mt

17:12-13)

ALESKANDA/ISKANDA MKUU!

Mwaka 334-323k.K. Mwana Wa Philip, mtu Wa Makedonia. Ugiriki. Mtu Wa mkono Wa

kushoto! Hodari Na shujaa mwenye roho mithili ya Duma! Aliueneza ufalme wake kwa kasi

kuliko utawala uwao wowote ule uliowahi kutawala. Aligenga mji Wa Iskaderia(Alexandria)

ukiwa mji Wa bandari ya kati Mediterania,huko Misri.

Aliubadilisha ulimwengu kiasi kwamba baada yake hakuna kitu kingeliweza kuwa kama

kilivyokuwa kabla.Kwa miaka 10 aliiteka Asia ndogo,Huko Shamu aliutwaa Tiro baada ya

kuunusuru miezi 7,Palestina,Misri. Kwa kifupi ni kutoka makedonia hadi India.

Alipokufa ufalme wake uligawanywa kwa majemedari wake 4; Maana hakuwa Na watoto

wakuwarithisha. Na baada ya muda majemedari 2 walikuwa Na nguvu kuliko wengine!

Ufalme Wa kusini ulikuwa ni Misri Na Palestina! Na walijulikana kama Ptolomayo. Israeli

ilikuwa sehemu ya ufalme huu.

Agano la kale la kiyunani chini ya Tolemayo II [Filadelfi]wayahudi wa Iskanderia[Misri]

walitafsiri Agano la Kale la Kiebrania kwa kiyunani!,watafsiri walikuwa wayahudi 70,6 kutoka

kila moja ya makabila 12. Septuaginta LXX.

Ufalme Wa kaskazini ulijulikana kama Waseluki,

Nasaba yao maarufu ni Antioko.

Shamu ya kaskazini,Babeli,na Asia ndogo.

Antiokia ya Shamu ulikuwa makao makuu.

Israeli ikamezwa Na utawala huu mwaka 198 k.K

Page 121: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

121

Hellenists

Kutokana Na neno Hellas yaani Uyunani/ugiriki. Utamaduni,ustarabu,falsafa Na lugha ya

kiyunani vilienea katika sehemu zote za mashariki ya kati!

Wayahudi wengi waliacha lugha yao ya kiebrania Na kiaramu Na kupokea utamaduni mpya

hivyo mafarakao yakatokea kati yao kwa wale wanaokubaliana Na tamaduni za kigeni Na wale

wanaozipinga!,

Ujenzi Wa majengo ya kisasa, elimu ya hali ya juu Na michezo iliwafanya jamii kuwa sehemu

kuu mbili,waugwana Na wenye hekima,washenzi Na wasio Na hekima! (Rumi 1:14)

MFALME ANTIOKO IV EPIFANIA

Alikuwa mtawala mkatili aliyewatendea wayahudi ukatili mkubwa kuliko Mfalme yeyote kabla

ya hapo!

Mpinga Kristo Wa Agano la Kale! Aliyetimiza sehemu ya unabii Wa Danieli.

Alikomesha uzao Wa utawala Wa ukoo Wa kikuhani tangu Haruni,yaani Onias Wa III.

Akamteua kuhani mwingine Yasoni.ndugu yake Menelaus akamlaghai akautwaa ukuhani

mkuu,akauza vyombo vya dhahabu za hekaluni,Kama kodi.

Antioko alipokuwa Misri akipigana huko,uvumi ulienea Yerusalemu kuwa ameuwawa katika

vita!,hivyo wayahudi wakamwasi Menelaus Na kujitangazia Uhuru Wao! Ghafla Antioko

akatokea ghafla kama kimbunga akawaua kwa makali ya upanga!

Ndani ya siku 3 watu 40,000 walichinjwa,kuta za Yerusalemu zikabomolewa,hekalu likanajisiwa

kwa kuteketezwa juu yake vitu vilivyo najisi, akasimamisha juu ya madhabahu ya kuteketezea

sadaka sanamu ya mungu Jupiter Olympus. Wanawake Na watoto wakauzwa kama watumwa!

Akapiga marufuku dini ya kiyahudi,sadaka za kuteketezwa zikakoma!

Page 122: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

122

UASI WA YUDA (MAKABAYO)

Yuda - Makabayo yaani 'nyundo' mwana Wa Matatia kuhani mzee aliyekuwa Na wana 5

miongoni mwao ni Yuda alianzisha vita vya msituni kwa miaka 3 kupinga Na kupindua utawala

Wa Antioko ili kutakasa hekalu Na kupata Uhuru kamili Wa Israeli.

Yuda alianzisha vita hivi,Yonathani akaendeleza,Simoni akazidisha makali yake!

Tarehe 25 mwezi Wa 12 wakatakasa hekalu Na kuifanya siku hii kuwa sikukuu ya kutabaruku.

Maana waliupindua utawala Wa kikuhani uliopendelea mambo ya kiyunani.Na utawala mpya

Wa kikuhani uliojulikana kama Wahasmonayo ukaanza! Baada ya hayo yakatokea makundi

mawili kati yao,wako waliotaka Uhuru Wa dini tu,wakaridhika kuwa chini ya wayunani hawa

waliunda chama chao maarufu kama Mafarisayo,(walitunza mapokeo ya dini,walipinga

siasa,walikuwa maskini Na walijipendekeza kwa maskini wengi.) Na wako waliokuwa Na

misimamo mikali waliotaka Uhuru kamili Wa kisiasa pia hawa walikuwa maarufu kama

Masadukayo!( walikuwa matajiri,mamlaka,viongozi Wa makuhani)

143 k.K Baada ya miaka 20 walipata Uhuru kamili Wa kisiasa.

Kwa miaka 80 mafarakano yao yaliwadhoofisha Wao kwa Wao Na kurahisisha maadui Wao

kupata nguvu!

Kundi la mafarisayo lilipojaribu kufanya vita ya miaka 6 kupindua uongozi uliokuwa

unapendelewa Na masadukayo waliambulia kipigo cha kusulubiwa waasi 800 juu ya mti!. Na

kushindwa azma zao walimtafuta Pompey akida Wa kirumi iliyokuwa inapata nguvu kijeshi kila

kukicha,Na mwenye Kambi yake ya kijeshi huko Dameski aje awasaidie! Jirani yao Gavana Wa

Idumea Antipater na wafalme 2, walinyemelea kuwavamia ili kutwaa madaraka ya ukuhani Na

kisiasa!.

Pompey aliunusuru hekalu la Yerusalemu kwa miezi 3 akaitwaa Na kuingia hadi patakatifu pa

patakatifu!,akawachinja makuhani.

Mwaka 63 k.K Yerusalemu ikawa chini ya Rumi,koloni la Rumi. Pompey Na baraza la

Rumi(senate) wakamteua Antipater kuwa liwali Wa Yudea. Antipater kwa ushawishi wake kwa

Rumi, akawarithisha watoto wake 2 ufalme wake!

Herode mkuu akawa juu ya Yudea Na ndugu yake kuwa juu ya Galilaya.

Herode mkuu alitawala kwa miaka 33 toka (37-4 k.K)

alijitahidi kufanya mengi mazuri ili wayahudi wamkubali lakini walimchukia tu!.

Page 123: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

123

Kwa sababu alifanya udanganyifu Na uuaji ili kupata madaraka,Na alimuua mtu yeyote yule

aliyehatarisha cheo chake! Ndio maana hakuona shida kuwauwa watoto wote chini ya miaka 2

Wa Bethlehemu (Mt 2:1-5) wakati Yesu alipozaliwa!.

Aliendesha miradi mikubwa ya ujenzi ya miji kama Yerusalemu,Samaria (sebaste),Kaisaria,

Akajenga hekalu kubwa zuri sana nae akajijengea ng'ome yake binafsi. Alipokufa alimteua

mwanae Arkelau kuwa herode Wa Yudea lakini kutokana Na ukatili,asiyejali sheria na ufidhuli

wake hakupewa ridhaa Na Rumi,hivyo Rumi wakamteua Pilato kuwa liwali Wa Yudea Na

Galilaya ilitawaliwa Na mmoja ya mtoto wake Herode Antipa. Huyu alimuua Yohana mbatizaji

Na pia alipitisha kuuwawa kwa Yesu Kristo.

Herode Agripa mjukuu wa Herode mkuu,alichukua nafasi ya Pilato huyu! alimfunga

Petro,akamuua Yakobo. Alipoendelea Na kujipendekeza kwa wayahudi kwa kulitesa kanisa,

aliliwa Na chango akafa!.alipojitwalia utukufu Wa Mungu..

Mwisho.

Lugha ya uandishi Wa Agano Jipya ni kiyunani,japokuwa walikuwa chini ya dola la Rumi,bado

lugha ya kimataifa ilibakia kiyunani!.

Sifa zinazofanana kati ya Eliya Na Yohana mbatizaji.

Wote waliwageuza maelfu kumrudia Mungu!

Eliya aliigeuza Israeli kumwabudu Mungu Wa kweli!

Yohana aliitengeneza njia ya Israeli kwa Bwana!

Wote waliishi Maisha ya dhiki Na shida!

Njaa,kunguru kumlisha mikate

Njaa, asali mwitu,nzige

Mavazi singa za ngamia

Wote walitishiwa Na wanawake

Yezebeli,Herodia.

Page 124: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

124

Wote walikatishwa tamaa,walivunjwa moyo Na matengenezo madogo tu kuliko walivyokuwa

wanadhania.

Eliya alitazamia israeli wote wamuunge mkono!

Yohana alitazamia Yesu amsaidie kutoka gerezani.

Warithi Wao walikuwa Na upako zaidi.

Aliyemrithi Eliya,Elisha alikuwa Na upako Mara dufu,

Aliyemrithi Yohana,Yesu Wa Nazareti alikuwa Na upako zaidi.

Wote hawakuoa!

Wote walifanya kazi sio chini ya miaka 3 Na nusu!

Page 125: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

125

MUHTASARI WA KITABU CHA MATHAYO.

Kina sura 28.

Kina aya/mistari

Mwandishi: Mathayo

Mwaka Wa uandishi:

Eneo la uandishi:Antiokia ya shamu.

Hadhira: Wayahudi.

Jina lake humaanisha " karama ya Mungu"

Mtoza ushuru Wa mji Wa kapernaumu aliyeitwa Na Yesu akaacha vyote akamfuata Yesu.

Ametumia "mwana Wa Daudi" Mara 9 katika Injili yake.tofauti Na Injili zingine kwa pamoja

wametumia Mara 6 tu! Ameonesha nabii 25 za Agano la kale zikitimia kuwa Yesu ni Masihi.

Ametumia "ufalme Wa Mbinguni" Mara 55 akionesha mkazo Wa ufalme Wa kiti cha Daudi

yaani "Messiah" mpakwa mafuta Wa Bwana ndivyo anavyoanza kuandaa ufalme wake.

WASIFU WA MATHAYO.

Mtoza ushuru aliyeitwa Lawi. (Mk 2:14-17).

Asiyekuwa anastahili,sasa anastahili ( Lk 6:15)

Alipokubali wito wa Yesu kudhalilika kukakoma

Alikuwa miongoni mwa wanafunzi 12 wa Yesu.

Alikuwa akiishi na kufanya kazi Kapernaumu,pwani ya ziwa Galilaya.(Mk 2:1,13-14)

Alikuwa na mshahara mzuri( Mt 9:9)

Alikuwa na nyumba kubwa ya kuwakaribisha wageni ( Lk 5:2a)

Injili yake hamtaji mwandishi wake mahali popote!

Ilitokea mwaka 70 b.K

Hadhira: wakristo wa kiyahudi waliokuwa wanazungumza kiyunani.

Eneo: Antiokia ya Shamu.

Page 126: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

126

Alipanga habari zake kwa uangalifu sana

Inawezekana aliandika baada ya injili ya Marko na Luka

Kuonesha jinsi Agano la kale lilivyotimizwa katika Agano Jipya,kuja kwa Masihi mwana wa

Daudi.

Mafundisho zaidi kuliko matendo.

Habari zake hazifuati mfunulizo wa muda na matukio.

Injili 3 yaani Mathayo,Marko Na Luka huitwa Injili mfanano! Kwa sababu zinakuwa kama

zinaangaliana! Zikiorodhesha miujiza kama 35 hivi Na mifano ya Yesu 40 katika Injili hizi.

Injili ya Yohana ni ya kipekee kidogo maana miujiza yeye anaita Ishara,Na baadhi ya matukio,

machache tu ndio ameshiriki Na Injili zingine. Matukio mengine ameyaandika kwa umuhimu

mkubwa ili kuonesha namna gani Yesu ni Mungu.

Page 127: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

127

MUHTASARI WA KITABU CHA INJILI YA MARKO.

Marko ambaye aliitwa Yohana Marko a lifuatana na Mtume Paulo katika safari zake za kitume.

Yohana Marko ni mtoto wa Maria ambaye nyumbani kwao kulikuwa Yerusalemu, ambako

kunaonekana kuwa kituo kikuu cha Ukristo

(Mdo. 12: 12). Marko alisafiri na Barnaba ambaye ni mjomba wake mpendwa, kolosai. 4:10

(Mdo. 4:36 -37 )kwenda Antiokia ya Syria

(Mdo 12:25) ambako walifuatana na Paulo kwenye safari yake ya kwanza ya kitume.

Marko hata hivyo aliwaacha Barnaba na Paulo huko Kipro na kurudi Yerusalemu (Mdo 13:13)

safari ya pili ya Marko inaanza kwa kutengana kati ya Barnaba na Paulo

Baadaye Barnaba na Marko walielekea Kipro wakati Paulo akienda Asia. Miaka kumi baadaye

( 60 B.K)

Marko kwa miaka kadhaa alimsaidia Petro kueneza Injili majimbo ya Asia ndogo, (Mdo 15: 6-

8,1Petro 1:1)walifanya pia huduma Rumi.

Marko alikuwa pamoja na Paulo huko Rumi (2Tim.4:11; Kol.4:10.)

Shabaha ya Marko ilikuwa ni kukusanya pamoja ujumbe wote wa Injili.Petro anamtaja Marko

kama “mwanawe.” (1Pet..5:13),

Hatimaye aliishi Rumi ambako aliandika kumbukumbu za Mtume Petro.

Petro alipoondoka Rumi wakristo wa huko wakamwomba Marko aandike habari za Yesu kama

walivyozisikia kutoka kwa Petro.Kwa hiyo Injili ya Marko inawakilisha maneno ya

mtu(PETRO)aliyeshuhudia kwa macho yake mwenyewe juu ya maisha ya Yesu yanayoelezwa

katika Injili hii.

Kwa sababu hii,

Injili ya Marko inakazia zaidi matendo ya Yesu kuliko maneno Yake. Pia Injili hii inatumia

nafasi kubwa kueleza matukio ya juma la mwisho la maisha ya Bwana Yesu.

Marko anaanza kwa kueleza habari za huduma ya Bwana Yesu hadharani na juu ya kuhubiri

Kwake kuhusu Habari Njema ya Ufalme wa Mungu. Kisha anatoa unabii wazi kuhusu

matazamio ya kifo cha Bwana Yesu

(Mk. 8:31;9:31;10:33-34,45).

Page 128: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

128

Hatimaye anaeleza jinsi Bwana Yesu alivyosulibiwa msalabani kwa ajili ya dhambi za

ulimwengu,

kufufuka Kwake kutoka kwa wafu, kuonekana Kwake nawanafunzi Wake baada ya kufufuka,

maneno na maagizo Yake ya mwisho na kupaa Kwake kwenda mbinguni. Tarehe Inawezekana

ni katika wakati huu wa uhai wa Petro, au muda mfupi tu baada ya kifo chake (55-65 B.K.),

ambao Marko aliandika Injili hii yenye kuchukua jina lake.

Tabia ya Petro ya kutoka kwa haraka tukio moja kwenda jingine. Kutafsiri maneno mengine ya

kiebrania/kiaramu mk 3:17,15:22,34)

Aya 12 za mwisho hazimo katika maandishi ya kale ya asili kabisa!

Wazo Kuu

Marko anamdhihirisha Bwana Yesu kuwa ni Mtumishi wa Mungu, Mtu wa vitendo, aliyekuja

kutimiza mapenzi ya Mungu. Marko anaonyesha waziwazi huduma ya Yesu na utendaji Wake

wa miujiza, uponyaji Wake, mamlaka Yake juu ya pepo wachafu na nguvu Zake, Bwana Yesu

alithibitishwa kuwa si mtumishi wakawaida bali kwamba kwa hakika alikuwa Mwana wa

Mungu.Ufufuo wa Yesu ulithibitisha yale yote aliyotenda na sasa tunangojea kurudi

Kwake kwa utukufu, kutoka mbinguni.

Marko aliandika Injili hii ili pia kuwatia moyo Wakristo walioishi Rumi wakati wa mateso.

Marko NI injili fupi kuliko zote!.na ni injili ya kwanza kuandikwa

Marko hakuwa mtume!.

Amerekodi nabii 11 zilizotabiriwa juu ya Yesu kutimia

Aina ya uandishi wake: msimuliaji!

Hadhira : Wakristo wa Rumi

Paulo alimsifu sana Marko sasa anamfahamu vizuri, amekomaa anaweza kumsaidia kanisa la

Kolosai (kol 4:10)

Mgawanyo wa Sura.

Yohana Mbatizaji na ubatizo wa Bwana Yesu (1:1-13)

Huduma ya Yesu Galilaya (1:14-9:50)

Safari ya kwenda Yerusalemu na kuingia mjini (10:1-11:25[26])

Page 129: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

129

Matatizo mjini Yerusalemu (11:27-12:44)

Unabii kuhusu mambo yajayo (13:1 -37)

Kufa kwa Yesu na kufufuka kwake. (14:1-16:8[9-20])

Mark is considered the Gospel of action.

There are 3 things missing from this Gospel because they are not important for a servant - a

genealogy, birth, and childhood.

Mark summarizes John the Baptist, Christ's baptism and temptation in the first 13 verses, and

immediately goes on to the work of Christ.

Page 130: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

130

MUHTASARI WA KITABU CHA LUKA.

Maana ya jina' Luka '= Mwanga. "Kuangaza"

Mwandishi ni daktari Luka. Yeye aliwaandikia Wagiriki/wayunani namna gani Yesu ni mtoto

wa mwanadamu.

Wagiriki walimwelewa Luka vizuri. Luka aliwahoji waliokuwepo mfano Mzee Simeoni (Lk

2:25),Zakaria baba Wa Yohana mbatizaji na kuandika maelezo yao,alifanya utafiti Wa kina

tarehe za nyakati zile na akaandika kwa kirefu kuliko Injili zote 4. Yeye Alieleza mambo kwa

mpangilio, jinsi MTU asiye myahudi angeliweza kumwelewa; Inawezekana aliandika huko

Kaisaria wakati Paulo alipokuwa amefungwa mwaka wa 58 baada ya Kristo. Luka aliandika

Vitabu viwili: Injili ya Luka na matendo ya mitume

Aliviandika kwa kumwandikia Theofilo;

Maana ya Theofilo = "Rafiki wa Mungu"; Alikuwa mrumi mtawala mwenye cheo kikuu

Mwaka Wa uandishi: 60-63 B.K

Sura: 24

Mistari/aya : 1,151

Wasifu Wa Daktari Luka.

Kitaaluma: luka alikuwa daktari.mwenyeji Wa Antiokia ya Shamu,jina lake likitajwa Mara 3

katika Agano Jipya

Alikuwa mwana Theologia na mwana Historia na mwinjilisti. Aliandika huku akiwawaza watu

Wa mataifa kama wayunani na warumi, akionesha kwa umaridadi kabisa Wa ufundi Wa

kusimulia, "mfano wa Mwana Mpotevu"

Utambuzi Wa kiroho,mwenye kiasi katika maneno yake,alieleza kwa mvuto habari za Yesu

alivyowapenda maskini,alivyokula na wenye dhambi,akienda nyumbani kwa Zakayo,Yesu

mwenye huruma,mwenye kumwomba Baba daima,mwenye kuleta furaha kuu!

Uandishi Wa Luka ungali unatutibia, wenye kuleta afya kwa Roho na mwili.

Luka hakuwa miongoni mwa wanafunzi 12 Wa Yesu. Luka hakuwa myahudi alikuwa MTU Wa

mataifa. Luka alifanya kazi na Paulo, alitembea katika misafara yake,na kuandika kitabu cha

Matendo.

Kumbukumbu za kale zinaonesha kuwa Luka hakuoa!

Page 131: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

131

Alikufa akiwa na miaka 84. Ameandika Injili ya kina na marefu akitafiti chanzo/ukoo Wa Yesu

hadi kwa Adamu,namna alivyokua hadi utu uzima,kifo chake na kukufuka kwake!

Kwa sababu wengi wangetaka kujua ikawaje baada ya hapo! Luka akatuletea sehemu ya 2( part

2) ya Injili yaani matendo ya Roho Mtakatifu kupitia mitume wale aliowaacha Yesu!

Mkanda wa filamu ya Yesu ulitengenezwa mwaka 1979 ambao unachukua uhalisia wa maisha

ya Yesu kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Luka ndani ya kitabu cha Biblia.

Maneno yalivyotumika katika Injili ya Luka!

"Mwana Wa Adamu": Mara 23

"Mwana Wa Mungu ": Mara 7

"Ufalme Wa Mungu": Mara 32

Ameonesha nabii 9 ukitimizwa Wa Agano la kale:

Mgawanyo Wa kitabu cha Luka.

Mwokozi kuzaliwa: sura ya 1 - 2

Maadalio ya Huduma: sura 3 - 4:13

Huduma katika Galilaya: sura ya 4:14 - 9:50

Njiani kwenda Yerusalemu: sura 9:51 - 19:10

Kifo na kufufuka/kushinda: sura 19:11-24:53

DHIMA KUU/LENGO KUU.

Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale

yaliyotimizwa katikati yetu, kama walivyotuhadithia wale wa­liokuwa masha­hidi wenye

kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, nimeona vema mimi nami, kwa kuwa

nime­jitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo

mtukufu, upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa. (LK 1:1-4)

Daktari Luka anamalizia sehemu ya kwanza ya Injili yake kwa kutuambia! Yesu alivyomaliza

kazi yake kwa ushindi na kuwaaga wanadamu.

50. Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. 51. Ikawa katika

kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. 52. Wa­kamwabudu; kisha wakarudi

Yerusalemu wenye furaha kuu. 53. Nao wa­likuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.

(LK 24:50-53)

Page 132: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

132

MUHTASARI WA KITABU CHA INJILI YA YOHANA!

"Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa

Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli."(Yohana 1:14)

Kuna Sura: 21

Kuna Mistari:876

Eneo la uandishi: Efeso

Mwandishi: Yohana mwana Wa Zebedayo

Yohana= "Mungu ni Wa rehema/neema"

Mwaka Wa uandishi:60-90 K.K

Wasifu Wa Yohana.

zamani alikuwa mwanafunzi Wa Yohana mbatizaji( Yohana 1:19-61)

Mama wa Yohana alikuwa Salome.

Yohana alikuwa binamu Wa kwanza Wa Yesu!

Yohana mbatizaji alikuwa binamu Wa pili Wa Yesu.

Kazi ya Yohana zamani ilikuwa uvuvi, kama ndugu yake Yakobo. Wao waliitwa wana wa

Ngurumo. Yohana alikuwa mmoja wa wanafunzi 3 wa Yesu. Waliokuwa karibu na

Yesu(Petro,Yohana na Yakobo)

Alikuwa anampenda sana Yesu,na Yesu alimpenda sana!

alikuwa mwanafunzi Wa mwisho kufa!

Yohana anamwelezea Yesu kama Mungu kamili.

Yohana ameandika vitabu 5:

Injili ya Yohana,

I Yohana,

II Yohana,

III Yohana, na

Ufunuo Wa Yohana.

Page 133: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

133

Baada ya Miaka 50 hivi kupita baada ya Yesu kupaa kwenda mbinguni,aliufahamu Upendo

vizuri,

Alieleza jinsi Pendo la Mungu lilivyo kuu kwa wanadamu! aliandika neno"kuamini" (kama mara

100)juu ya Yesu Kristo ili kuupokea Upendo huu Wa Kristo;hii ikiwa lengo kuu la injili yake!

"Amini, amini" limetumika mara 25 kwenye injili yake tu!.

Lengo/dhima kuu!

Yeye aliandika kwamba Yesu ni Mungu.

Injili ya Yohana ni rahisi zaidi kuielewa kwani yeye aliwaandikia watu wote.

Watu wanaotaka kuokoka, wana­elewa zaidi Injili ya Yohana.

Barua alizoziandika ni rahisi kuzielewa.

Ni injili ya kiroho(Spiritual Gospel)

Kwa namna nyingine NI ngumu kuielewa( kuna mazingira wayahudi wakataka kumpiga mawe

mara 2,wengine wakarudi nyuma wasiandamane nae tena maana aliongea maneno magumu) japo

NI rahisi kwa sababu inatafuta kujua kwa nini? Nini maana ya maandiko/matukio hayo,kanuni

na misingi ya kuyaelewa inahitajika!

Yeye amekazia "uzima" mara 19 "UZIMA WA MILELE" mara 17, tofauti na Mathayo

aliyekazia "ufalme Wa Mungu".

Yeye ameziita ishara badala ya miujiza,

Hotuba zake NI ndefu na mifano ya Yesu imepungua(10)

Ameonesha visa/ishara 7 ! Ambazo hazipatikani kwenye Injili zingine

Maneno Yenye shuhuda " Mimi NI" yaani ile nafasi ya Mungu "NI Mimi " hii NI kuonesha

uungu wake. NI katika Injili yake ameeleza neno la mwisho "IMEKWISHA"

Injili ya Yohana imeandikwa ili mpate kua­mini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa

Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Kwa ajili ya hii watu wengi wameokoka, kwa sababu Yohana alia­ndika Injili yake kwa wengi ili

waweze kumwamini Yesu. Japo Yohana hakuweka mambo haya(4) ktk injili yake kama baadhi

ya Injili zingine, inatupa kusudi la kimafunuo!

Hakuweka nasaba ya ukoo Wa vizazi- kwa sababu Yesu NI Mungu hana mwanzo wala mwisho.

Page 134: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

134

Hakuweka namna ya kibinadamu alivyozaliwa- kwa sababu yeye NI Neno alikuwapo tokea

mwanzo.

Hakuweka namna alivyojaribiwa - kwa sababu Mungu hawezi kujaribiwa!.

Hakuweka alivyobadilika sura katika mlima - kwa sababu hakuna aliyemuona Mungu wowote - I

Yohana 4:12.

"Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa

katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo,

Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. (YN 20:30,31)

Page 135: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

135

MUHTASARI WA KITABU CHA MATENDO YA MITUME!

Maana ya jina' Luka '= Mwanga. "Kuangaza"

Mwandishi ni daktari Luka. Yeye aliwaandikia Watu wote wajue kuja KRISTO alileta ukombozi

kwa wanadamu wote na namna Ukristo ulivyokuwa unashamiri kwa Nguvu za Roho Mtakatifu!

Inawezekana aliandika huko Kaisaria wakati Paulo alipokuwa amefungwa mwaka wa 58 baada

ya Kristo. Luka aliandika Vitabu viwili: Injili ya Luka na matendo ya mitume

Aliviandika kwa kumwandikia Theofilo;

Maana ya Theofilo = "Rafiki wa Mungu"; Alikuwa mrumi mtawala mwenye cheo kikuu

KITABU CHENYEWE!

Kina Sura 28

Kina Mistari 1,007

Dhima kuu: KAZI ZA ROHO MTAKATIFU KUPITIA MITUME !

Mwaka Wa uandishi: 64- 75 B.K

Mahali : Rumi

Mwandishi : Luka

Matendo 1:1-8:4 Yerusalemu

Kukua na kuongezeka kwa kanisa!

Mateso yalivyoshindwa kuzuia kazi za Roho Mtakatifu

Mhusika mkuu alikuwa Petro!

Matendo 8:5-12:25 Yudea na Samaria!

Mashahidi walivyoihubiri Samaria na Yudea

Sauli aliyelitesa kanisa,kuokoka!

Herode kulitesa kanisa!

Matendo. 13-28 Mwisho Wa nchi!

Page 136: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

136

Mhusika mkuu alikuwa Paulo

Tunaona safari 3 za Paulo, hadi kufungwa miaka 2 ya Paulo huko Rumi. Mwaka 62.B.K

1. Safari ya kwanza ya Paulo

Matendo 13:1 - 14:28 ilikuwa ya miaka 2,

alisafiri takribani maili 1,235

2. Safari ya pili ya Paulo

Matendo 15:36 -18:23,ilidumu kwa miaka 3,

alisafiri zaidi ya maili 2,703.

3. Safari ya tatu ya Paulo

Matendo 18:23 - 21:16

Ilidumu kwa miaka 4

Alisafiri takribani maili 2,515

Kitabu cha matendo ni kitabu cha historia katika Agano Jipya kikiunganisha vitabu vya Injili na

Nyaraka. kinaonesha kwamba Baada ya wayahudi kumuua Yesu hawakufanikiwa kama

walivyofikiri kuua mwasisi ni kuua kanisa! Na matunda ya ukombozi yamedhihirika kuanzia

hapa! Kinaonesha historia ya kanisa kwa miongo 3, baada ya Yesu kupaa kurudi mbinguni,yaani

kwa miaka ile 30-35 ya mwanzoni.(30-63)B.K

Stefano wakati anapondwa kwa mawe! Jiwe jingine linamjia mwelekeo wa kichwa! Akajitahidi

kutoa maneno ya mwisho,huku damu zikitiririka

Akasema, "Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa

kuume wa Mungu."

Mungu alikuwa akimdhihirishia waziwazi tumaini lenye baraka! Akamfungulia mlango wa

mbinguni!

Upendo Wa Mungu ukamfanya asamehe wakosaji,

Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, "Bwana, usiwahesabie dhambi hii." Akiisha kusema haya

akalala.

Page 137: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

137

MUHTSARI WA KITABU CHA WARUMI.

Kina Sura 16

Kina Mistari 433

Dhima/somo kuu: HAKI YA MUNGU IMEDHIHIRISHWA

Mwaka Wa kuandikwa :56-58 B.K

Mahali : Korintho

Mwandishi : Paulo

Barua ya 6 ya Paulo.

WARAKA/BARUA YENYEWE!

Barua hii ya kitheologia zaidi,yenye kuvutia na ndefu kuliko zote anaonesha shauku yake ya

kutaka kuufikia ulimwengu wote,kwa kufika hapa Rumi mji mkuu Wa dola la Rumi iliyokuwa

inatawala ulaya yote,kaskazini mwa Afrika na pande za Asia.

Alipotimiza azma yake, bado Paulo alitamani kufika hadi Uspania!

Wakati Wa kuandika kuelekea mwisho Wa safari yake ya 3 ya kimisionari,Paulo alikuwa

Korintho kama mgeni katika Nyumba ya Gayo,alipokuwa akiandika Waraka huu kwa njia ya

msaidizi wake Tertio.

Paulo anaandika waraka wake kwa muundo Wa maswali na majibu au mtindo Wa majadiliano

akijadili "haki" ya Mungu,asili ya dhambi,akitoa nukuu kadha Wa kadha Agano la kale

akilinganisha na maana sahihi ya Agano Jipya.

Kwenye kitabu hiki anaongelea dhambi na haki kupitia maana zenye kina na mapana ya

ufafanuzi za agano la kale kuanzia: Abrahamu,Daudi,Adamu,Sara,Rebeka, Yakobo na

Esau,Farao na pia ahadi alizopewa Israeli na namna gani Wakristo wanaweza kue­nenda katika

imani.

Paulo aliandika kwa mji mkuu bila kutambua kuwa alikuwa akiuandikia ulimwengu mzima na

vizazi vyote vya wanadamu!

Page 138: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

138

Historia inaonyesha kuwa kupitia waraka kwa warumi...."mwenye haki ataishi

imani"........Martin Luther,Kavini,Wesley waliwasha moto wa mageuzi na

uamsho(Reinnances&Reformation) huko ulaya baada ya kipindi kirefu cha Giza, Kuikumba

ulaya

MUHTASARI WA KITABU CHA 1.WAKORINTHO

Sura 16

Mistari 437

Dhima kuu: matatizo ya kanisa na ufumbuzi wake!

Mwaka Wa uandishi:55 B.K

Mahali : Efeso

Mwandishi : Paulo

Barua ya 4 ya Paulo.

Mji Wa Korintho upo kusini mwa nchi ya Ugiriki,kama maili 45 magharibi mwa Athens.

Kwa kushirikiana na Prisila,Akila pamoja na timu yake ya kitume,Paulo alianzisha kanisa la

Korintho Ndani ya miezi 18 ya Huduma yake,katika safari yake ya pili ya umisheni, alipokuwa

Korintho.

Paulo akiwa hapa Korintho mwaka 51-52 B.K

Alipofukuzwa katika sinagogi la wayahudi aliingia mtaani na kuhiubiri injili,Tito Yusto

akaokoka,Krispo mkuu Wa Sinagogi aliamini,(mdo 18:8) na baadae mkuu mpya Wa sinagogi,

Sosthene aliamini pia.(mdo 18:17)

Akiwa hapa Korintho aliandika kwa Mara ya kwanza barua/waraka wake kwa Wathesalonike 1

na 2. Katika safari yake ya 3 ya umisheni akiwa pale Efeso kwa miaka 3 alipokea habari mbaya

za matatizo ya kanisa la Korintho hivyo akaandika waraka huu kutoa ufumbuzi wa matatizo hayo!

Paulo alituma barua hii kupitia kwa Ste­fana, Fortunato na Akaiko. (1Kor 16:17). mji Wa

korintho japo ulikiwa na maendeleo makubwa,kutokana na bandari yenye biashara na

usafiri,ulijaa anasa nyingi na uovu mwingi sana!

Ilikuwa MTU akionekana mhuni sana anaambiwa anatabia za kikorintho! Ama kumwita

mkorintho!

Page 139: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

139

Wakorintho walikuwa wachanga kiroho na wenye tabia ya mwi­lini.mfano walikuwa na ugomwi

wao kwa wao uliopelekea kuwa na makundi kadhaa Ndani ya kanisa,wengine wakijiita wao NI

Wa mtume Petro,wengine Apollo,wengine Paulo na wengine Kristo.!

Barua hii ya Paulo pamoja na ufafanuzi juu ya karama za Roho ziliwasaidia kurekebi­sha

mambo pole pole. Hadi pale walipopata tena barua ya pili.

Waraka wenyewe!

Sura 1:1-9 utangulizi na salamu.

Sura 1:10 - 4:21 mafarakano katika kanisa

Sura 5:1 - 6:20 Zinaa katika kanisa👙

Sura 7:1 - 40 Ndoa ya Kikristo 💑

Sura 8:1 - 11:1 Chakula kilichotolewa sadaka kwa miungu

Sura 11:2 - 14:40. Vipawa na karama za Roho Mtakatifu

Sura 15:1-58 mafundisho juu ya ufufuo Wa wafu!

Sura 16:1-24. Maagizo ya mwisho!

Sura ya 13! Imebeba kusudi zima la Waraka huu yaani UPENDO! hakika Paulo alifunuliwa

kuandika sura hii maridadi kabisa juu ya Pendo la Mungu lililomiminwa Ndani ya wakristo!

Page 140: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

140

MUHTASARI WA WAKORINTHO 2:

Kina Sura 13

Kina Mistari 257

Dhima kuu: utukufu kupitia mateso

Mwaka Wa kuandikwa :56 B.K

Mahali : Makedonia(Filipi)

Mwandishi : Paulo

Barua ya 5 ya Paulo.

Majira ya majani kupukutika,akiwa pale makedonia. alipata taarifa nyingine ya kumhuzunisha

kuwa Ndani ya kanisa la Korintho wameibuka wapinzani,wakimshambulia yeye,na mamlaka

yake ya kitume! Kuwa Paulo hakuwa miongoni mwa wanafunzi 12 wa Yesu;huku wakiikosoa

barua yake ya kwanza,Na wanaendelea kushawishi wengine wamkatae Paulo.

Alipowaandikia barua ya kwanza aliwaeleza wazipime kazi wafanyazo wanaojiita walimu na

mitume kama wanatenda kama kwa BWANA na si kwa wanadamu! Ama kujenga juu ya msingi

Wa MTU mwingine .baadae alikwenda Korintho akaa nao miezi 3 na kutokea hapo akaandika

waraka kwa Warumi.

Kanisa la Korintho lilimpa maumivu sana na kuwasumbua washirika wengine, waliokuwa

waaminifu kwa Paulo. Aliiandikia barua Kali sana! Kabla ya hii ya Pili,ambayo inadaiwa kwa

miaka ya baadae ilipotea! Maana aliwakemea kwa ukali wale wazushi waliokuwa wanaharibu

kanisa na akaamuru kanisa la Korintho liwatenge kabisa.

Kwa kuwa alitazamia kuwatembelea,alisubiri kwanza majibu ya barua hiyo kutoka kwa Tito na

baada ya kupata majibu mazuri ya kutia moyo kuwa wamebadilika. Ndipo alipowaandikia barua

hii.

Ni barua aliyoeleza udhaifu wake,huzuni zake,machozi,hatari,dhiki,faraja,majivuno,huduma na

kweli Wa dhamiri yake!. Ili tu kuwasaidia hawa wakristo wamuelewe!

Page 141: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

141

Bado anawaonya wale siku za Leo wanajiita mitume,hawajitumi wala hawafungui makanisa

mapya wao NI kusubiri MTU mwingine afungue kanisa,wao waende kuchunga kondoo wasio

wao na kujivuna kuwa wao NI bora sana!

Paulo mara nyingi alikuwa anaanza kwa kusema mtumwa na mtume,ila wale wazushi walidiriki

kujiita mitume,manabii na walimu.

Ikiwa mtume anaishi tu mjini hana hata makanisa 3 aliyoyafungua ama kuanzisha Yeye

mwenyewe atakuwa mtume kwa sifa IPI?

"Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa

maana andiko huua, bali roho huhuisha."(2Korintho 3:6)

Si kwa kutumia andiko Fulani ndiko kunampa MTU mamlaka Bali Roho aliyempa Huduma ya

kitume Ndani yake!

Page 142: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

142

PAULO WA TARSO!:

Alizaliwa mnamo 5.BK pale Tarso,mji Wa Silicia kusini mwa uturuki ya Leo! Aliuwawa

Rumi,mwaka 67 B.K.

Akiwa gerezani aliandika hivi...

"Nalitahiriwa siku ya 8, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa

Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo."

Akitokea katika familia ya kitajiri,yenye uwezo!

Msomi sana,mwenye uwezo Wa kujenga hoja na kushinda! Farisayo aliyeokoka !,oooh sasa NI

mnenaji Wa Hali ya juu ya lugha za ulimwengu Wa Roho,mtume Wa Injili ya wasiotahiriwa

anaonekana kama; Myahudi mfupi,mnyonge,mshonaji Wa mahema aliyekuwa amepanga

nyumba ndogo,vichochoroni mwa mji Wa Koritho. Alipokuwa akiandika barua yake kwa

warumi!

Kila alipopita alipindua miji na kuteka mateka kwa ajili ya Kristo! Si mchezo!!! akaja hadharani

kwa ujasiri Wa hasira za rohoni akinena kuwa!"

"Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila

aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia."

Akasisitiza zaidi huku akinukuliwa matamshi yake!

"Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama

ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani."

mwisho Wa kumnukuu!

Alihubiri injili kwa miaka 35 !

Paulo(kiyunani/kirumi),Sauli(Kiebrania);

Alikuwa Wa kabila la benjamini(Fil 3:5)

Alikuwa na uraia Wa nchi 2 myahudi/mwebrania na mrumi

Page 143: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

143

Alizaliwa Tarso katika nchi ya uturuki ya sasa!(Mdo 9:11)

Alijifunza elimu ya dini; torati toka kwa mwalimu mahiri/rabi Gamalieli(Mdo 22:3)

Gamalieli alikuwa mjukuu wa Hillel (mmojawapo wa walimu maarufu wa Kiyahudi), alikuwa

rais wa baraza la Sanhedrin.

Alikuwa farisayo Wa mafarisayo tena mwenye msimamo mkali (Mdo 23:6,Fil 3:5)

Alifurahia kushuhudia kuuwawa kwa Stefano!

Alihakikisha anawatesa wakristo kadri alivyoweza akawatafuta hadi dameski! Kama maili 130

toka Yerusalemu.

Aliokoka baada ya kupigwa mweleka na upofu Wa siku 3 ikifuatiwa na maombi ya kufunga siku

3, akabatizwa na Anania baada ya kuongozwa sala ya toba!Alikaa jangwani miaka 3

akitengenezwa na Mungu kwa kazi maalum ya Injili ya mataifa(international evangelism)

(Galatia 1:11-17)

Alijifunza zaidi juu ya injili ya Kristo kwa miaka 14 pale antiokia, akaja Yerusalemu kupewa

Baraka za mitume(Petro na Yakobo) ili kuanza umisheni kwa wasio Wa tohara!(Galatia 2:9)

Alifanya safari kuu 3 za kimeshenari!

1. Safari ya kwanza; mnamo mwaka 45-49.B.K (mdo sura 13-14) yaani Matendo 13:1 - 14:28

ilikuwa ya miaka 2,alisafiri takribani maili 1,235.

Paulo,Barnaba,Marko

Kypro kwanza kisha Galatia,Biblia zilizo nyingi zenye ramani nyuma zitakuwa zinazoonyesha

safari hizi.Baadaye Paulo aliandika waraka wake kwa Wagalatia kwa waumini walioishi katika

eneo hili.

2. Safari ya pili ya Paulo; mwaka 50-54.B.K (Mdo sura 15) yaani Matendo 15:36 -18:23, ilidumu

kwa miaka 3, alisafiri zaidi ya maili 2,703.

Paulo na Sila.

Kutoka Galatia hadi Troa na kuvuka hadi Filipi na kushuka Athene na halafu kuendelea hadi

Korintho.Safari ya kurudi Yerusalemu iliwapitisha Efeso halafu kwa mashua hadi Yerusalemu!

3. Safari ya tatu ya Paulo; Mwaka 54-58.B.K Mdo sura 18. Yaani Matendo 18:23 - 21:16

Ilidumu kwa miaka 4. Alisafiri takribani maili 2,515

Page 144: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

144

Paulo alisafiri kupitia Galatia na kuendelea hadi Efeso ambapo alikaa miaka 3!. Kutoka hapo

injili ilisambaa hadi Asia yote ikasikia Injili hadi Ugiriki kabla ya kurudi Yelusalemu.

Alisafiri na Barnaba,Marko,Sila,Timotheo,Tito na Luka kama watendakazi! Mfano wakati Paulo

akihubiri,Luka alikuwa akiandika kumbukumbu ya Yale yaliojiri.

Aliandika nyaraka 13 ama zaidi.alishitakiwa na kufungwa gerezani kama Mara 3!

Aliuwawa rumi mwaka 66 B.K chini ya kaisari Nero!.Alikuwa na katibu wake Tertio (Rum

16:22).

MUHTASARI WA WARAKA WA WAGALATIA.

Una Sura 6

Una Mistari 149

Dhima kuu: Wokovu kwa NEEMA kwa njia ya Imani.

Mwaka Wa kuandikwa :48-49* (53-56)B.K

Mahali : Antiokia

Mwandishi : Paulo

Ni barua ya 3:

Katika safari zake za mwanzoni Yeye na Barnaba walianzisha kanisa hili,lakini kutokana na

wivu Wa wayahudi waliwachanganya wagalatia kwamba ili kupata wokovu kamili NI lazima

wafuate na kushika sheria za wayahudi kama vile tohara.

Martin Luther alikiita kitabu hiki "Magna carta of Christianity liberty."

Pale Injili inapoenea toka tamaduni hadi tamaduni,na jamii moja hujiona wenye haki,bora zaidi,

nini hutokea?

Nguvu ya Injili ya kubadilisha Maisha ya MTU hupokea tafsiri potofu kuwa wokovu NI

kubadilisha tamaduni iliyo duni kwenda tamaduni yenye heshima ya jamii Fulani.

Wayahudi walipoona wagalatia wameikubali Injili,na kuwa imani juu ya Yesu Kristo,wakawa na

nia ya kutaka kuwabadilisha kuwa wayahudi kwa torati.

Walimyahudisha Petro mpaka akakosa msimamo,Paulo akamkemea kwa kuwa kigeugeu!

Iweje katikati ya waamini wasio wayahudi anakula nao wakitokea wale wayahudi,anajitenga

kuonesha kana kwamba hawafungamani na WaKristo wasio Wa torati.

Page 145: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

145

Hapa Paulo anatetea Injili ya neema kwa sababu wahubiri wa sheria waliku­wa wameharibu kazi

ya Mungu kanisani huko Galatia. Pia Paulo anake­mea watu wa Galatia, wa­lipoiacha Injili ya

neema.

Lakini Tito aliyekuwa pamoja nami, naye ni Myunani, hakulazimishwa kutahiriwa. Bali kwa

ajili ya ndugu za uongo walioingizwa kwa siri; ambao waliingia kwa siri ili kuupeleleza uhuru

wetu tulio nao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani; ambao hata saa moja hatukujitia chini

yao, ili kwamba kweli ya Injili ikae pamoja nanyi. (Galatia 2: 3-5)

MUHTASARI WA KITABU CHA WAEFESO.

Kina Sura 6

Kina Mistari 155

Dhima kuu: KRISTO NA KANISA.

Mwaka Wa kuandikwa :60-62 B.K

Mahali : Rumi

Mwandishi : Paulo

Ni barua ya 7,

Paulo akiwa gerezani,akisubiri rufaa yake kwa Kaisari,alipewa Uhuru Wa kutembelewa na

kuandika,akaandika waraka huu akamtuma Tikiko aipeleke Efeso.tukumbuke kuwa Paulo alikaa

Efeso miaka 3 kabla ya kuendelea na safari yake.

Mji wa Efeso ulikuwa mji mkuu wa jimbo la kirumi la Asia ndogo,uliokuwa hekalu la mungu

Diana(Artemi),wafua vinyago vya shaba (Demetrio) biashara ya miungu sanamu ilishamiri eneo

hili,hapa ndipo wana 7 wa Skewa walipotolewa mbio wakiwa uchi na pepo waliomjua Paulo.

Luka katika Matendo ya Mitume sura 18-20,sura 3 anatuhabarisha namna Injili ilivyohubiriwa

pale Efeso.

Akila na Priscila walikuwa waamini wa kwanza waliosimama hadi kanisa hili kusimama.

Mwinjilisti mbobevu Apolo alikuwa maarufu katika mitaa ya Efeso akihutubia kwa ujasiri Injili

ya ubatizo wa Yohana. Ndipo Paulo akaja kuimarisha kwa kuwapa semina kwa miaka 3 mizima.

Paulo hakupendezwa na kanisa lililosambaa kilometa za mraba 20 na huku kina kikiwa inchi 3 tu!

Hivi ni sawa na kusema hawakuwa na mizizi kabisa.

Page 146: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

146

Inawezekana yale makanisa 7; yaani Efeso,Laodikia,Smirna,Pergamo,Thiatira,Sardi na Filadelfia

yalizaliwa na kanisa mama la Efeso.

Tikiko katibu wa Paulo alipokea barua mbili, waraka kwa waefeso na kwa wakolosai awapelekee

akitokea Rumi. Ni katika waraka huu Paulo anaeleza wazo la Mungu ambayo ilikuwa ni siri

anayowafunulia kufahamu mpango wa MUNGU ulivyokusudiwa. Efeso 1:4

Kitabu chenyewe:

Sura 1: 1-23 Maisha yenye uzima tele na nguvu katika Kristo.

Sura 2: 1- 3:21 Mpango wa Mungu kwa kanisa.

Sura 4:1- 6:24 Maisha ya kila siku ya mwamini na kanisa.

“Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au

tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na

katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.” [Waefeso 3:20-21]

Page 147: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

147

MUHTASARI WA WARAKA KWA WAFILIPI.

Kina Sura 4

Kina Mistari 104

Dhima kuu: Furaha katika kumwishia Kristo.

Mwaka Wa kuandikwa :60-62 B.K

Mahali : Rumi,gerezani.

Mwandishi : Paulo

Kiongozi: Epafrodito.

Barua ya 10 ya Paulo.

BARUA YENYEWE!

Kanisa la filipi lilikuwa katika mji Wa Filipi ulioko mashariki ya makedonia,maili 10,toka bahari

ya Aegea,ulipewa jina hilo kufuatia Mfalme Filipo Wa II(356.K.K) ,Wa makedonia ambae NI

baba Wa Alexanda Mkuu,(Alexander the Great)mji Wa heshima na kituo cha kijeshi cha warumi.

Paulo akiwa na timu yake ya watenda kazi (Sila,Timotheo na Luka) ktk safari yake ya 2, ktk

kuitikia maono na Mungu akiwa Troa(mdo 16:9-40) alianzisha kanisa hili.

Ilipita miaka 11 baada ya kuanzisha kanisa hili alipoliandikia barua sio ya kuwaonya kama

zingine zilivyo Bali kuwashukuru kwa jinsi walivyokuwa watoaji kwake binafsi,na kwa kanisa la

Yerusalemu.

Page 148: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

148

Ujumbe wa barua hii unahusu zaidi nia ya Kikristo na jinsi ya kutosheka Kikristo katika hali

mbali mbali. Kitabu kinaonyesha kwamba tunaweza kufurahi wakati wa mapungufu, mata­tizo

na hata mateso.

"Furahini katika Bwana tena nasema furahini."

MUHTASARI WA WARAKA WA WAKOLOSAI.

Una Sura 4.

Una Mistari 95.

Dhima kuu: Mamlaka ya juu kabisa ya Kristo.

Mwaka Wa kuandikwa: 60-62 B.K

Mahali: Rumi,gerezani.

Mwandishi : Paulo

Aina ya Ujumbe: mafundisho

Hadhira: wakristo Wa pale Kolosai na viunga vyake!

Maudhui: utukufu Wa Kristo katika kanisa.

Kiongozi: Epafra

Mji Wa kolosai ulikuwa maili 100 mashariki mwa Efeso,karibu na Laodokia

NI Moja ya Nyaraka/barua 4 za gerezani alizoziandika Paulo akiwa Rumi kifungoni kwa miaka 2.

Zingine zikiwa Wafilipi,Waefeso,na Filemoni. Ni Barua ya 8, ya Paulo.

Paulo alikuwa hajaenda Kolosai. Yeye aliku­wa na wasi wasi juu ya mafu­ndisho ya pembeni

yaliyotaka kuingia kanisani. Mafundisho ya elimu ya unostiki (mafundisho ya wanikolai)

Page 149: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

149

yaliwataabisha wakristo wale. Ndio maana alimtuma Epafra huko Ko­losai pamoja na barua kwa

kanisa.

Pengine Paulo aliandika barua nyingine kwa kanisa la Laodikia ili wabadilishane na ile ya

Kolosai zisomwe zote katika makanisa yao lakini haikupatikana kuingizwa katika katika

maandiko matakatifu(2:1,4:13)

"Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana

kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni

mwenu." (Kol 3:16)

MUHTASARI WA WARAKA KWA WATHESALONIKE 1:

Una Sura 5.

Una Mistari 89.

Mwaka Wa kuandikwa :50-51 B.K

Mahali : Korintho

Dhima kuu: Kurudi kwa Kristo.

Mwandishi : Paulo

Barua ya 1 ya Paulo.

Ni mji ulioko maili 100 magharibi ya mji Wa Filipi.

Kutokana na Thessalonika,Dada Wa Alexanda mkuu.

Paulo alilianzisha kanisa hili kwenye safari yake ya 2 na alikaa Thesalonike kwa mda kama

mwezi 1 hivi.

Hapa ndipo ule usemi ukatoka kuwa ;"wale walioupindua ulimwengu wamefika mpaka huku"

wayahudi walimpinga vikali akaenda Beroya akafurahishwa na wakristo wale waliopenda

kuyachunguza,na kuyaelewa maandiko!

Page 150: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

150

Baada ya kutoka Filipi alifika hapa Thesalonike,kisha akaenda Beroya,kisha Athene ambako

alimtuma Timotheo Thesalonike,akaimarishe kazi huku yeye akivuka kuingia Korintho ndipo

Timotheo akamletea habari za kanisa la Thesalonike.

Paulo aliandika waraka huu kuhusiana na kurudi kwa Yesu Mara ya pili.

NI Moja ya barua ya kwanza ktk uandishi wake nyingine ikiwa NI 2 Wathesalonike.

Kanisa la Thesalonike lilikuwa mfano mzuri kwa makanisa mengine. Paulo alitaka kulitia moyo

kanisa changa na pia kueleza mambo ya nyakati za mwisho.

Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya

malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana

hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.(4:16-17)

MUHTASARI WA WARAKA 2 WATHESALONIKE!

Una Sura 3.

Una Mistari 47.

Mwaka Wa kuandikwa :50-51 B.K

Dhima kuu: Kurudi kwa Kristo

Mahali : Korintho

Mwandishi : Paulo

Barua ya 2 ya Paulo.

Hapa ni katikati ya Vitabu vya Agano Jipya.

Ni mji ulioko maili 100 magharibi ya mji Wa Filipi.

Paulo alilianzisha kanisa hili kwenye safari yake ya 2 na alikaa Thesalonike kwa mda kama

mwezi 1 hivi.

Page 151: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

151

Baada ya barua yake ya kwanza kuleta maswali,migongano, na wazushi kutaka kulipotosha

kanisa,aliwaandikia barua hii kuwafahamisha zaidi pia akiwaonya wale wasiokwenda kwa

utaratibu wasipewe ushirikiano.

wao walifikiri Unyakuo utatokea mapema sana,wakasitisha kufanya kazi,wakingoja kunyakuliwa!

Na wengine wakahuzunika kwa wao waliokwisha kufa kabla ya unyakuo.

Kanisa liliishi katikati ya mateso na wa­lifikiri wameingia kwenye ghadhabu(dhiki kuu),ama

Kristo alisharudi bila ya wao kujua. Paulo aliwatolea wasi wasi wao na ali­taka kuhimiza kanisa

liweze kuendelea mbele.

"Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote." (2 The3:18)

MUHTASARI WA TIMOTHEO WA KWANZA!

Maana ya Timotheo= "kumwabudu Mungu"

Barua ya kichungaji.

Kina Sura 6.

Kina Mistari 113.

Mwaka Wa kuandikwa :62-63 B.K

Dhima kuu: Mafundisho sahihi na utauwa.

Mahali : Makedonia

Mwandishi : Paulo

Barua ya 11 ya Paulo.

NI moja ya barua za mwishoni za Maisha ya Paulo kumwandikia Timotheo.(binafsi)

Page 152: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

152

Timotheo aliokoka na Kumwamini Kristo wakati Wa safari ya kwanza ya Paulo akiwa

Listra,ambako alipigwa mawe nusu afe,katika safari yake ya Pili alimpitia Timotheo na kuanza

kufanya nae Huduma.(Mdo16:1-3) hasa Galatia ya kusini!

Baba Wa Timotheo alikuwa Myunani na mama alikuwa myahudi(Eunice) bibi yake alikuwa

Loisi,Paulo alimfanyia tohara Timotheo, ili aweze kufanya nae kazi katikati ya wayahudi,ktk

miji ya troa,Berea,Thesalonike,efeso,korintho,na Rumi

mambo muhimu katika barua yalikuwa ni mpangilio ndani ya kanisa,imani,tahadhari dhidi ya

wapotoshaji na tabia ndani ya kanisa.

Baada ya kuanzishwa kwa kanisa ilikuwa lazima kute­ngeneza mambo ya maka­nisa. Paulo

alimfundisha Timotheo mambo haya.

Timotheo mchungaji Wa kanisa la Efeso anaambiwa!

" Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na

mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo; amba­yo wengine wakiikiri hiyo wameikosa

Imani. Neema na iwe pamoja nanyi." (1Tim 6:20,21)

Page 153: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

153

MUHTASARI WA KITABU CHA 2 TIMOTHEO!

Kina Sura 4.

Kina Mistari 83.

Mwaka Wa kuandikwa :63-64 B.K

Dhima kuu: Uvumilivu thabiti.

Mahali : RUMI

Mwandishi : Paulo

Barua ya 13/13 au14* ya Paulo.

Hii ni barua ya Paulo ya mwisho. Barua ya kuaga maisha, kwa sababu alijua baada ya muda

mfupi atakufa, atau­awa. Alipelekwa tena mara ya pili mbele ya kaisari Nero mwaka wa 67. Na

Paulo aliuwawa.!

Makanisa mengine yalikuwa yalipotea kiimani na kuingia chini ya sheria. Paulo alimwomba

Timotheo kufanya kazi ya uinjilisti vizuri. Paulo alimhimiza Timotheo aendelee kufanya chini ya

neema.

Mtume Yohana aliyekuwa amebakia peke yake aliandika juu ya Pendo,na Mungu katika

kuudhirisha Pendo hili akampa ufunuo Wa makanisa 7 ili kuyaonya waishindanie imani,.

Kazi ya Petro,Paulo,Timotheo zikaimarishwa na unabii Wa Yohana juu ya kanisa!

Page 154: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

154

MUHTASARI WA KITABU CHA TITO!

Barua ya kichungaji!

kina Sura 3.

Kina Mistari 46.

Mwaka Wa kuandikwa :62-63 B.K

Dhima kuu: Mafundisho na wajibu wa kazi njema

Mahali : Makedonia/Korintho

Mwandishi : Paulo

Barua ya 12 ya Paulo.

Tito alikabidhiwa kanisa la Krete(Malta) aliongoze na kulichunga.Paulo alilianzisha wakati

alipoachiwa kifungo cha mara ya kwanza huko Rumi.

Inawezekana aliiandika barua hii akiwa Korintho akamtumia Zena na Apolo ili waifikishe kwa

Tito.

Tito myunani,inaonekana alikuwa kaka Wa Luka.

Tito alikuwa ameachwa kisiwa cha Krete kufanya mipangilio ya kanisa. Paulo aliandika kuhusu

mipangi­lio ya ka­nisa na utawala wa kanisa.

"Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yali­yopunguka, na kuwe­ka wazee katika

kila mji kama vile nilivyokuamuru;" (Tito 1:5)

Unapotaka kujifunza juu ya utauwa,tahadhari dhidi ya imani potofu,uzushi! Na mambo ya kanisa

soma waraka wa Tito na nya­raka za Timotheo.

Page 155: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

155

MUHTASARI WA WARAKA KWA WAEBRANIA.

Una Sura. 13

Una Mistari 303.

Dhima kuu:Agano lililo bora zaidi. !

Mwaka Wa uandishi: 60-70

Mahali : Rumi, Ebrania (13:24)

Mwandishi : Paulo ama mwanafunzi wake!

Hadhira: wayahudi waliookoka.

Mwandishi mmoja asiyejulikana kwa jina,akaandika waraka(barua) maarufu! Akitoa maana ya

Kanuni na taratibu zilizotumika katika Torati . Neno kubwa ndani ya barua ni "Afa­dhali".

Ba­rua iliandikwa kabla ya mwaka wa 70 wakati huo bado hekalu halijabomo­lewa. Waliopokea

hiyo barua ni Wayahudi waliyookoka, waliona hekalu kubwa na ibada zilizofanyika humo.

Walijivunia hekalu lao na dini yao!

Wakristo walianza kuchoka kwa kumwa­budu Yesu asiyeonekana. Walianza kuyumba ndani ya

imani yao.

Neno "Wayahudi" humaanisha zaidi wale Wa ufalme wa Yuda na wenyeji Wa

Yerusalemu,"waebrania" humaanisha wote Wa agano la Ibrahimu, Isaka na Yakobo

ambao,walikuwa wakingoja ahadi ya Masihi. Wengi walipotoshwa na kuamini kuwa Masihi

atakuja kutawala kama Mfalme Wa wayahudi.

hivyo walipoona anazungumza habari tofauti na utawala Wa kisiasa,walikuwa na mashaka kama

walifanya vizuri kujiunga na Ukristo!,wakaacha kweli waliyokuwa wamefundishwa,wakaacha

kuhudhuria mikusanyiko ya kanisa,kwa sababu hekalu halikuwa bado halijabomolewa,dhabihu

zilikuwa zikiendelea kutolewa.wengi walitupilia mbali imani yao wakarudia dini ya kiyahudi.

Kuzuia na kurekebisha ukengeufu huo haja ya kutoa waraka wenye kuonesha mapungufu ya

kanuni zote za kiyahudi; ukatokea. Ingawa Agano la kale lilitolewa na Mungu halikukusudiwa

kamwe kuwa jambo la kudumu milele.kusudi lake lilikuwa kuwaandaa watu kwa ajili ya kuja

kwake Kristo.

Barua iliwahimiza na kuwakumbusha kwamba kumfuata Yesu ni afadhali kuliko ibada

zinazofanyika hekaluni.

Mwandishi ametoa maana za kiroho kwa yale yaliyopo kwenye torati, hasa kitabu cha kutoka na

mambo ya walawi.

Page 156: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

156

Kwa maneno mengine twaweza kusema torati iliyopo katika Agano Jipya.

Hali ya kutukuza kanuni,taratibu za kiyahudi kuliko Kristo hakutafaidia MTU kitu,wala

hakumwengezei utakatifu.

Sura ya imani yenye mistari 40, ikiwa imesheheni habari za mababa Wa imani walivyohesabiwa

haki! Ili imani zetu Leo zile endelevu!.

Page 157: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

157

MUHTASARI WA WARAKA WA YAKOBO.

Kina Sura 5.

Kina Mistari 108.

Dhima kuu: Imani katika matendo!

Mwaka Wa uandishi: 45-49 B.K

Mahali : Yerusalemu

Mwandishi : Yakobo. "Yakobo mwenye haki"

Hadhira: wayahudi Waliookoka.

Yakobo alikuwa ndugu yake Yesu, (Math 13:55,Galatia 1:19)na pia kiongozi wa kanisa la

Yeru­salemu na alithaminiwa katika baraza(mdo 15).

Wakati wa utoto alijuana na ndugu yake Yesu na Yuda. Lakini sasa anasema, mimi ni mtumwa

wa Bwana Yesu Kristo.

Inaonekana barua hii ni ya zamani zaidi kuliko barua zote za Agano Jipya.

Barua nyingine zinazofanana na hii ni.

Waraka kwa Wagalatia, Paulo anatumia baadhi ya matatizo ya Wakristo Wa kiyahudi kama

nukuu rejea kuwasaidia wayahudi waliokuwa wanawasumbua Wakristo Wa Galatia.

Waraka Wa Waebrania bado ukawahusu sana wayahudi hawa waliokuwa kwazo kwa

Kuwasumbua Wakristo wengine.

Barua Ya Yakobo iliandikiwa Wayahudi. Inasemekana kwamba hakuna barua nyingine ya

Kiyahudi kama hii.

Wayahudi waliokuwa wakristo walikuwa na matatizo makuu 2.

1. Mvuto Wa kutaka kuishi kwa kuishika torati.

iliwapelekea kuwa na imani iliyopoa,na dhaifu na mengi yaliwachanganya!

Mfano Je Wakristo Wa mataifa wanapaswa kupitia tohara?,kanuni zipi za torati zifuatwe na zipi

ziachwe?

Page 158: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

158

2. Mvuto Wa kuonyesha Uhuru wao mbali na utumwa Wa Torati.

walijikuta wakifuata hadi mwenendo mwovu,Wa watu wasioamini walioishi kati yao!...Uhuru

usio na mipaka.

Ilifika mahali wakawaona wakristo Wa mataifa hawana haki na utakatifu kama Wa myahudi

aliyeamini.

Namna Yakobo alivyoyashughulikia matatizo haya! Kwa haki pasipo upendeleo watu

wakawaida,walimwita "Yakobo mwenye haki".

Yakobo NI mithali ya Agano Jipya!

Aliuwawa Yerusalemu, kama Yakobo Wa jina wake mwana Wa Zebedayo alivyokufa.

" Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;

jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho

na mauti, na kufunika wingi wa dhambi. "(Yak 5:19,20)

Page 159: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

159

MUHTASARI WA WARAKA WA FILEMONI

Idadi ya sura: Sura 1

Idadi ya mistari: Mistari 25

Mwaka Wa kuandikwa: 60-62 B.K

Dhima kuu: Upatanisho

Mahali : Rumi

Mwandishi : Paulo

Barua ya 9 ya Paulo.

NI Moja ya Nyaraka(barua 4) za gerezani alizoziandika Paulo akiwa Rumi kifungoni. Zingine

zikiwa Wafilipi,Waefeso,na Wakolosai.

NI moja ya barua binafsi 4 alizoziandikwa Paulo kwa watu binafsi kama vile 1&2 Timoteo,Tito

na Filemoni.

Onesmo : " mwenye manufaa"

Filemoni alikuwa MTU Wa mji Wa Kolosai,alikuwa mwamini mwenye uwezo aliyemiliki

nyumba waliyokuwa wanafanyia ibada. mke wake alikuwa Afia.

Katika nyumba yake kanisa la Kolosai lilikuwa likikutana.

Alikuwa na mtumwa Onesmo aliyemtoroka kwa kumwibia Mali/pesa na kukimbilia Rumi

alipokutana na Paulo,akaokoka!, baada ya kuokoka Paulo akaanza kazi nyingine ya upatanisho

kati ya Onesmo na Filemoni.

Maana mtumwa aliyemtoroka bwana wake alistahili kuadhibiwa vikali hata kuuwawa! Na

isitoshe alimwibia vitu bwana wake. Wakati ule barua zilipotumwa kwa makanisa ya Efeso na

Kolosai. Paulo aliijua sana tabia ya Filemoni,iliyokuwa yenye upendo na kuelewa mambo

yalivyo! Hivyo hakutaka kutumia mamlaka yake ya kitume kumshurutisha, bali hiari ya moyo

wake ipelekee kumsamehe Onesmo. Kwa hiyo alimwandikia barua aliyoipeleka Onesmo kwa

Filemoni.

Paulo aliandika ndani ya barua yake kuhusu Onesimo. Alimtetea Onesimo.

Onesimo alirudi kwa bwana wake File­moni. Na Paulo alimwandikia Filemoni katika mstari wa

16: tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa ! (Filemoni 16)

Page 160: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

160

MAMBO YA KUJIFUNZA!

Wakati mshirika,muumini anaporubuniwa na mtumishi Fulani,je huyo mtumishi anaujenga

ufalme Wa Mungu?

mshirika akitenda kosa ama dhambi na kukimbilia kujificha kanisani kwako,ukampokea bila

kutaka kupata taarifa za atokako! Huku unampa huduma,na vyeo ili asitoroke je unafanya vema?

dawa baada ya kutenda dhambi sio kuhama kanisa,kumkimbia mlezi wako Wa kiroho na kwenda

kwa mwingine Bali ni kutubu!.

Kama mchungaji ananyanganya mchungaji mwenzie kondoo(washirika) je anafanya kazi ya

Mungu pia?

Yapasa kutumia hekima na kufanikiwa!

Page 161: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

161

MUHTASARI WA WARAKA WA KWANZA WA YOHANA!

Una Sura 5.

Una Mistari 105.

Dhima kuu: kweli na haki !

Mwaka Wa uandishi: 85-95.B.K

Mahali : Efeso

Mwandishi : Yohana

Barua ya 1 ya Yohana, waraka Wa ushirika.

Aliandika kuhusu Upendo,alifundisha Upendo,alihimiza Upendo,aliuishi Upendo! Alitoa mausia

ya Upendo! Neno kuu ni "upendo" limetumika mara 46..

"Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na

Mungu, naye anamjua Mungu. (1 Yohana 4:7)!

Yohana aliandika barua hii kati ya mwaka wa 85 na 90. Mafundisho ya pembeni yaliingia

kani­sani ambayo Yohana anayapinga ndani ya barua yake. Aliendelea kuandika kuhusu dhambi

na upatanisho.

MTU mmoja aliyeitwa Kerintho,alikuwa amejaa mafundisho ya unostiki,alikuwa akieneza

mafundisho ya uongo kuwa elimu na ujuzi ni bora sana! badala ya mwenendo safi,na kutii amri

za Mungu.

Wasifu Wa Yohana

Jina lake humaanisha “Mungu ni wa neema”(whom the Lord graciously)

Alikuwa mwana wa Zebedayo, kaka wa Yakobo,wana wa Boanerge(ngurumo).

Ndiye ambaye Yesu alimpenda,miongoni mwa wanafunzi 3 wakaribu kabisa na Yesu.

Mwandishi wa Injili ya Yohana,nyaraka 3 za Yohana na Ufunuo wa Yohana.

Yesu msalabani alimwambia amtunze mama yake.

Alikufa akiwa ukimbizini kama mfungwa katika kisiwa cha Patmo

Alikuwa mwanafunzi wa mwisho kufa 100 A.D

Alichukua nafasi ya kuongoza kanisa baada ya Petro,Yakobo wote kufa.

Page 162: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

162

Yohana ni mtume Wa upendo!

Paulo ni mtume Wa Imani!

Petro ni mtume Wa Tumaini!

Page 163: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

163

MUHTASARI WA WARAKA WA PILI WA YOHANA!.

Una Sura 1.

Una Mistari 13.

Dhima kuu: Kutembea katika kweli !

Mwaka Wa uandishi: 85-95 B.K

Mahali : Efeso

Mwandishi : Yohana

Barua ya 2 ya Yohana.

Ni kitabu kifupi kuliko vyote katika Biblia.

Yohana alitaka kumtahadharisha mama(kanisa) kwa sababu walimu wanao­kosesha walijaribu

kuja kanisani. Jina la huyu mama halijulikani na hatu­jui kwamba alikuwa ndani ya kanisa gani.

Lakini alikuwa mtendaji kanisani.

Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye

katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.

Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe

salamu.( II Yohana 1:9-10)

Gayo : alieneza Injili.

Diotrefe : aliizuia Injili.

Demetrio : aliiacha Injili.

Vitabu 5; vyenye sura 1 ni Obadia,Philemoni,Yohana II,Yohana III, na Yuda.

Page 164: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

164

MUHTASARI WA WARAKA WA TATU WA YOHANA!.

Una Sura 1.

Una Mistari 14.

Dhima kuu: Kufanya kwa uaminifu!

Mwaka Wa uandishi: 85-95 B.K

Mahali : Efeso

Mwandishi : Yohana

Barua ya 3 ya Yohana.

Yohana alimwandikia Gayo na kumhi­miza atoe msaada kwa wahubiri wana­osafiri.

"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako

ifanikiwavyo."(1:2)

Uchu Wa madaraka ya uongozi Wa kanisa ulimfanya Diotrefe awakatae na kuwazuia walimu

wema waliokuja kufundisha kweli!.

Hakuwapatia mahitaji yao kama mitume walivyofanya!

Yohana alimtia Moyo Gayo,na kumsaidia asitetereke!

Ikiwa Diotrefe.. Akileta kiburi na kuendelea na upumbavu wake! Yohana angekuja na

rungu( mamlaka) yake. Na kumshukia Hapo!.

Page 165: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

165

MUHTASARI WA WARAKA WA PETRO WA KWANZA!

Una Sura 5.

Una Mistari 105.

Mwaka Wa uandishi: 62-64 B.K

Dhima kuu: kuteswa kwa ajili ya Kristo

Mahali : Rumi(babeli*)

Mwandishi : Petro

Barua ya 1 ya Petro.

akisaidiwa na Silwano(Sila) kama katibu wake,

Wasifu wake!

Alikuwa miongoni mwa wanafunzi 3 Wa karibu zaidi (wengine wakiwa Yohana na Yakobo) kati

ya wanafunzi 12 Wa Yesu.

Alimkana Yesu mara 3,akatubu kwa machozi, pia alimkiri kwamba anampenda Yesu mara 3.

Alikabidhiwa dhamana ya kuliongoza kanisa,alipewa funguo za ufalme Wa Mungu!

Aliwafungulia wayahudi kuingia (Mdo 2.)

Aliwafungulia mataifa kuingia (Mdo 11.)

Alikuwa ameoa,mama mkwe wake aliponywa na Yesu,na wakati mwingine alisafiri nae (1 Kor

9:5), ameandika nyaraka 2!

Aliandika kuwatia moyo kanisa wakati wayahudi wanalipinga na sasa watawala-Warumi

wanataka kuwaangamiza!

Alisulubiwa (kichwangombe)kichwa chini miguu juu kwenye msalaba Wa (X) huko Rumi

mwaka 68 B.K na kaisari Nero.

Petro anaeleza kuhusu Yesu aliyemwona kwa macho. Barua inaeleza juu ya mateso na baraka

zilizomo ndani ya mateso.

Page 166: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

166

HALI YA MAZINGIRA ILIVYOKUWA!

Baada ya Barnaba na Marko kumaliza kazi yao Kipro,Marko alifuatana na Petro. Hawa wawili

walifanya kazi pamoja kwa miaka mingi,wakihubiri na kufundisha kaskazini mwa majimbo ya

Asia ndogo ambapo Paulo hakuruhusiwa kuingia.(Mdo 16:7-8)

Kisha walisafiri hadi Rumi, ambako Petro aliwafundisha wakristo Wa kule,na alipoondoka Rumi,

Marko alibaki huko,ndipo wakristo wale walimwomba Marko aandike habari za Bwana Yesu

kama walivyozisikia kwa Petro! Na Marko alipoziandika ndipo tukapata Injili kama

iivyoandikwa na Marko. Paulo alikuja Rumi kama mfungwa! Na alipofikiri kufa kwakwe

kunakaribia alituma ujumbe ili Marko na Timotheo waje kuonana nae.

Kwa sababu dini ya kiyahudi ilitambuliwa rasmi na serikali ya Rumi,pale ilipobainika kuwa

ukristo sio tawi wala sehemu ya dini hiyo ulipigwa marufuku! 🙈kaisari Nero alianzisha mateso

makali dhidi ya wakristo! Yakobo,ndugu yake Yesu aliuwawa Yerusalemu,Paulo aliuwawa

Rumi,na sasa Petro yuko Rumi akisubiri wakati wowote! Ahukumiwe ! Hivyo aliwajibika

kuwatia moyo wakristo Wa majimbo ya Asia ndogo. Huku akiutaja mji Wa Rumi kwa mafumbo

kama Babeli.kutokana na vitisho vilivyokuwa vinaukabili ukristo.

Page 167: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

167

MUHTASARI WA WARAKA WA PETRO WA PILI!.

Una Sura 3.

Una Mistari 61.

Mwaka Wa uandishi: 66-68 B.K

Dhima kuu: kweli halisi dhidi ya walimu Wa uongo.

Mahali : Rumi

Mwandishi : Petro

Barua ya 2 ya Petro.

Wazo kubwa ni: Mtu anapokua kiroho analindwa katika wokovu.

Petro aliuwawa kwa tamko la kaisari Nero,Juni,mwaka 68 B.K aliyekuwa mkatili sana.

WASIFU WA PETRO.

Simeon-Petro.Kefa,jiwe,Mwamba.

Mtu wa galilaya, wenyeji wa mji wa Bethsaida (nyumba ya mvuvi). Maili 6 kutoka kapernaum,

Mji uliopo kaskazini mwa pwani ya ziwa Galilaya

kaka wa Andrea,wavuvi wa samaki, mwana wa Yohana(Jonah)

Alikuwa miongoni mwa wanafunzi 3 wa karibu sana na Yesu,ndiye aliyekuja kuwa kiongozi wa

wote 12.

Alikuwa na mke aliyefuatana naye katika umisheni(1 Kor 9:5)

Aliwahi kutembea juu ya maji,kutambua uungu wa Yesu,kumkana Yesu mara 3.

Aliandika nyaraka(barua) 2 akiwa Rumi.

Aliuwawa kwa kusulubiwa kichwa chini miguu juu wakati wa utawala wa Nero.

Page 168: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

168

HALI YA MAZINGIRA!.

Baada ya mwaka mmoja hivi,tangu kuandika barua yake ya kwanza kwa makanisa ya Asia

ndogo!, habari za kuhuzunisha zilimfikia! Kuwa katika yale makanisa kumeibuka walimu Wa

uongo,walieneza mafundisho ya uongo..mfano wao walidai MTU akisha okoka tu! Anaweza

kuishi Maisha kama apendavyo! Kwa sababu kinachotakiwa ni kumwamini Kristo tu! Pia

walifanyia mzaha juu ya kurudi Mara ya pili kwa Kristo.

Petro pasipo kupoteza muda,aliwaandikia waraka huu Wa pili,ili kupingana na mafundisho yale

ya uongo.

Waraka huu unafanana kwa sehemu na waraka Wa Yuda,inawezekana tatizo la walimu hawa Wa

uongo lilikuwa likienea kama chachu katika makanisa mengi!

Hivyo pengine Yuda aliazima maandishi Yale yale ya Petro,ama walitumia chanzo kimoja

kinachofanana kulionya kanisa na mafundisho potofu!.

Hadi Leo hii kanisa lina maadui wakuu 3!

1. Shetani(kanisa kukosa uwepo Wa Mungu)

2. Dunia.(udunia kuingia kanisani)

3. Walimu Wa uongo.

(watu ndani ya kanisa kama magugu)

Bado nyaraka hizi za nusu ya pili ya karne ya 2 zinatuonya kanisa la sasa la karne ya 21 maana

Roho Wa Mungu alitangulia kuona mwisho tokea mwanzo.

Page 169: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

169

MUHTASARI WA WARAKA WA YUDA.

Una Sura 1.

Una Mistari 25.

Dhima kuu: kuishindania imani ya mara moja tu!

Mwaka Wa uandishi: 70-80 B.K

Mahali :

Mwandishi : Yuda

Barua ya 1.

WASIFU WA YUDA.

Yuda alikuwa nduguye Yakobo na ndu­guye Yesu.

Yaani ndugu Wa kambo Wa Yesu.

Yuda alimkumbuka Yesu vizuri, walikaa miaka mingi pamoja nyumbani. Yakobo alikuwa

kiongozi wa kanisa la Yerusalemu,na aliandika waraka mmoja wa Yakobo,(Imani katika

matendo).

Yuda aliandika kuhusu Yesu vi­zuri sana. Yuda aliandika kuhusu kujilinda na kumfuata Kristo.

Yuda anatoa Mashutumu makali ya Moja kwa moja dhidi ya walimu Wa uongo na mafundisho

potofu.

“Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja

nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo;

⚡ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa; ni

mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo,

ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.” (Yuda 1:12-13)

Yuda anatangaza hukumu ya Mungu juu ya walimu Wa uongo

kwa sababu walidai kwamba Maisha machafu na matendo kinyume na maadili hayakuwa kosa

kwa MTU mwenye ujuzi Wa hali ya juu zaidi kuhusu mambo ya kiroho.

"Uhuru kamili kutokana na ujuzi Wa hali ya juu"

Ni mafundisho ya unostiki yaliyokuwa yanasumbua kanisa.

Page 170: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

170

Yuda anaenda mbali zaidi hadi kunukuu Vitabu vya kale (habari za unabii Wa Henoko) ili

walimu hawa Wa uongo waelewe iliyo kweli.

Inawezekana aliazima sehemu ya maandishi ya waraka Wa pili Wa Petro (2Petro 2:1-3:4) kutia

mkazo juu ya mafundisho yale potofu.

"Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi

sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani

waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu". (Yuda 1:3)

Page 171: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

171

MUHTASARI WA KITABU CHA UFUNUO WA YOHANA!

Kina Sura 22.

Kina Mistari 404.

Dhima kuu: Mapambano na ukamilisho !

Mwaka Wa uandishi:95-100 B.K

Mahali : kisiwa cha patmo huko Efeso!

Mwandishi : Yohana Mtume wa Bwana Yesu,aliyekua akipendwa sana Yesu.

Wasifu Wa Yohana.

Yeye ndie aliyeandika:

1. Injili ya Yohana,

2. Yohana Wa Kwanza

3. Yohana Wa Pili

4. Yohana Wa tatu

5. Ufunuo.

Ndiye mtume wa mwisho kufa,historia yatueleza kuwa;alichemshwa kwenye mafuta na

kufanyiwa kila ukatili( kukatwa mkono,kesho yake anakutwa ana mikono yote) ili afe lakini

hakufa Ndipo mfalme Domitian wa Rumi(wakati Warumi walipokua wakitawala sehemu kubwa

ya dunia na Mfalme Domitian akitawala baada ya mfalme Nero) alipoona ni vema atupwe

kwenye kisiwa Patmo kilichokuwa kimetengwa maalum kwa ajili ya wafungwa sugu,hapakuishi

mtu yeyote katika kisiwa hicho wala hapakua na namna ya kuishi isipokua kusubiri kufa tu.

Yohana aliandika barua hii akiwa kisiwa cha Patmo, ambapo Kaisari Domitiani alipomfunga.

Kaisari Domitiani alitawala mwaka wa 81-96.

Ndie Kaisari pekee aliyedai kuabudiwa akiwa hai,tofauti na makaisari wengine waliabudiwa

wakiwa marehemu tayari!.

Wakati Ukristo ulipokuwa unaonekana kama sehemu ya dini ya kiyahudi ulikuwa salama lakini

pale ilipobainika kuwa Ukristo sio dini ya kiyahudi ulihesabika kuwa batili na ulipigwa

marufuku!

Neno kuu la kitabu ni 'kilele cha Uovu na Hatima ya historia’(mwisho wa dunia).

Page 172: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

172

Kuna sababu 3 za kuandikwa kwa kitabu hiki.

1. Kuyaonya yale makanisa 7 ya Asia yaliyoandikwa pamoja na mengineyo ya wakati ule juu ya

kuacha kwao msimamo uliokuwa umetolewa na mitume na kuanza kufanana na dunia kitabia na

katika upotofu wa imani.

2. Kuyatia moyo makanisa ya wakati ule na kuyafariji kwa sababu ya mateso waliyokua

wakiyapitia kutokana na utawala wa Kaisari Domitian.

3. Kusudi kuu ya yote ni kuwafahamisha wanadamu wa vizazi vyote”MAMBO AMBAYO

HAYANA BUDI KUWAPO UPESI”

Uandishi wa kipekee wa ki-apocalpse hutumia vielelezo vya fumbo ili kutoa ujumbe kwa njia ya

picha. Ujumbe wake huja kwa kuonyeshwa zaidi kuliko kuelezwa.

MIGAWANYIKO YA KITABU CHA UFUNUO WA YOHANA!

Ufunuo sura 1-3..

mambo yaliyopita na yaliyopo;

habari ya makanisa 7 na maono yao,

unyakuo wa kanisa utatokea wakati huu

Sura 4; sura ya muonekano wa mbinguni na majeshi ya mbinguni

Sura ya 5;Yesu anayestahili kudhiirisha hukumu za nyakati za dhiki kuu!

Kuanzia sura ya tano[5] hadi sura mwisho, dhima kuu ni wayahudi tu!

Sura ya 6-19;habari za dhiki kuu.

Sura ya 12: habari za shetani,wakati uliopita,uliopo na ujao

Sura ya 13:habari za mpinga kristo;wakati ujao

Sura ya 17:habari za hukumu ya dini ya uongo,mfumo utakao haribiwa na mpinga Kristo

Sura ya 18:hukumu ya mji mkuu wa mpinga Kristo.

⚪Sura ya 20;utawala wa Yesu duniani kwa miaka 1000

Page 173: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

173

Sura ya 21;mbingu mpya na nchi mpya

Sura ya 22;mazingira ya mbingu mpya nan chi mpya na mausia ya mwisho kwa Yohana na

wasomaji

Aina ya maono ya unabii:

Lugha ya picha;mfano nywele nyeupe,mkanda wa dhahabu,miguu kama shaba.

Lugha ya fumbo;mfano asomaye na afahamu..666.

Lugha ya kawaida;mfano mpinga Kristo,jua kuwa Giza.

Kisiwa cha patmo kilichopo kwenye bahari ya Aegean, kina urefu Wa maili 10 na upana Wa

maili 6.kipo maili 24 mashariki ya Asia ndogo!

Yohana alikuwa na miaka 90 alipotupwa huku!

Shetani na dunia kamwe hawawezi kushinda! Utawala Wa ufalme Wa Mungu kupitia Kristo na

kanisa vitadumu milele!.

Page 174: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

174

RATIBA YA KUISOMA BIBLIA.

Je, ungetaka kuisoma Biblia yote? Itachukua kama masaa 80. Utumie dakika 15 kila siku na hivi

utaweza kusoma Biblia tangu MWANZO mpaka UFUNUO kwa muda wa mwaka 1. Siyo kazi

ngumu bali ni rahisi. Dakika 15 kila siku. Hii NI kwa aliye na ratiba iliyokaza sana! Na NI

standard ya kimataifa! Yaani asilimia moja(1%).tu.

MWEZI: JANUARI.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Mwa 1, 2, 3 Mt 1 17. Mwa 37 Mt 9

2. Mwa 4, 5, 6, 7 18. Mwa 38 39 40

3. Mwa 8, 9, Mt 2 19. Mwa 41 Mt 10

4. Mwa 10, 11, 12, 13 20. Mwa 42 43 44

5. Mwa 14, 15, Mt 3 21. Mwa 45 46 Mt 11

6. Mwa 16, 17, 18 22. Mwa 47 48 49

7. Mwa 19, Mt 4 23. Mwa 50 Mt 12

8. Mwa 20, 21, 22, 23 24. Kut 1 2 3 4

9. Mwa 24, Mt 5 25. Kut 5 Mt 13

10. Mwa 25, 26 26. Kut 6 7 8

11. Mwa 27, Mt 6 27. Kut 9 10 Mt 14

12. Mwa 28, 29 28. Kut 11 12

13. Mwa 30, Mt 7 29. Kut 13 14 Mt 15

14. Mwa 31, 32 30. Kut 15 16 17

15. Mwa 33 Mt 8 31. Kut 18 19 Mt 16

16. Mwa 34 35 36

Page 175: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

175

MWEZI: FEBRUARI.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Kut 20 21 22 17. Law 15 16

2. Kut 23 24 Mt 17 18. Law 17 18 Mt 25

3. Kut 25 26 27 19. Law 19 20 21

4. Kut 28 Mt 18 20. Law 22 Mt 26

5. Kut 29 30 31 21. Law 23 24

6. Kut 32 33 Mt 19 22. Law 25 Mt 27

7. Kut 34 35 23. Law 26 27

8. Kut 36 37 Mt 20 24. Hes 1 2 Mt 28

9. Kut 38 39 40 25. Hes 3 4

10. Law 1 2 Mt 21 26. Hes 5 Mk 1

11. Law 3 4 5 27. Hes 6 7

12. Law 6 7 Mt 22 28. Hes 8 Mk 2

13. Law 8 9 10 29. Hes 9 10 11

14. Law 11 Mt 23

15. Law 12 13

16. Law 14 Mt 24

Page 176: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

176

MWEZI: MARCH.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Hes 12 13 Mk 3 17. Kum 6 7 Mk 11

2. Hes 14 15 18. Kum 8 9 10

3. Hes 16 17 Mk 4 19. Kum 11 Mk 12

4. Hes 18 19 20 20. Kum 12 13 14

5. Hes 21 Mk 5 21. Kum 15 16 Mk 13

6. Hes 22 23 22. Kum 17 18 19 20

7. Hes 24 Mk 6 23. Kum 21 Mk 14

8. Hes 25 26 27 24. Kum 22 23 24 25

9. Hes 28 Mk 7 25. Kum 26 27 Mk 15

10. Hes 29 30 31 26. Kum 28 29

11. Hes 32 Mk 8 27. Kum 30 31 Mk 16

12. Hes 33 34 35 28. Kum 32 33

13. Hes 36 Mk 9 29. Kum 34 Lk 1

14. Kum 1 2 30. Yos 1 2 3 4

15. Kum 3 Mk 10 31. Yos 5 6 Lk 2

16. Kum 4 5

Page 177: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

177

MWEZI: APRILI.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Yos 7 8 9 17. Amu 17 18 Lk 10

2. Yos 10 Lk 3 18. Amu 19 20

3. Yos 11 12 13 14 19. Amu 21 Lk 11

4. Yos 15 16 Lk 4 20. Rut 1 2 3 4

5. Yos 17 18 19 21. 1Sam 1 Lk 12

6. Yos 20 21 Lk 5 22. 1Sam 2 3 4 5

7. Yos 22 23 24 23. 1Sam 6 7 Lk 13

8. Hes 25 26 27 24. 1Sam 8 9 10 11

9. Amu 1 2 Lk 6 25. 1Sam 12 13 Lk 14

10. Amu 3 4 5 26. 1Sam 14 15

11. Amu 6 Lk 7 27. 1Sam 16 17 Lk 15

12. Amu 7 8 28. 1Sam 18 19 20

13. Amu 9 Lk 8 29. 1Sam 21 22 Lk 16

14. Amu 10 11 12 30. 1Sam 23 24 25

15. Amu 13 Lk 9

16. Amu 14 15 16

Page 178: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

178

MWEZI: MEI

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. 1Sam 26 27 Lk 17 17. 1Fal 8 Yn 1

2. 1Sam 28 29 30 31 18. 1Fal 9 10

3. 2Sam 1 2 Lk 18 19. 1Fal 11 Yn 2

4. 2Sam 3 4 5 6 20. 1Fal 12 13

5. 2Sam 7 8 Lk 19 21. 1Fal 14 Yn 3

6. 2Sam 9 10 11 12 22. 1Fal 15 16 17

7. 2Sam 13 Lk 20 23. 1Fal 18 19 Yn 4

8. 2Sam 14 15 16 24. 1Fal 20 21

9. 2Sam 17 18 Lk 21 25. 1Fal 22 Yn 5

10. 2Sam 19 20 26. 2Fal 1 2 3

11. 2Sam 21 Lk 22 27. 2Fal 4 Yn 6

12. 2Sam 22 23 24 28. 2Fal 5 6 7

13. 1Fal 1 Lk 23 29. 2Fal 8 Yn 7

14. 1Fal 2 3 30. 2Fal 9 10 11

15. 1Fal 4 5 Lk 24 31. 2Fal 12 13 Yn 8

16. 1Fal 6 7

Page 179: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

179

MWEZI: JUNI.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. 2Fal 14 15 17. 2Nya 1 2 3 4 5

2. 2Fal 16 17 Yn 9 18. 2Nya 6 7 Yn 17

3. 2Fal 18 19 19. 2Nya 8 9 10 11

4. 2Fal 20 21 Yn 10 20. 2Nya 12 13 14 Yn 18

5. 2Fal 22 23 21. 2Nya 15 16 17 18

6. 2Fal 24 25 Yn 11 22. 2Nya 19 20 Yn 19

7. 1Nya 1 2 3 4 23. 2Nya 21 22 23

8. 1Nya 5 6 Yn 12 24. 2Nya 24 25 Yn 20

9. 1Nya 7 8 9 25. 2Nya 26 27 28 29

10. 1Nya 10 11 Yn 13 26. 2Nya 30 31 Yn 21

11. 1Nya 12 13 14 15 27. 2Nya 32 33 34

12. 1Nya 16 17 Yn 14 28. 2Nya 35 36 Mdo 1

13. 1Nya 18 19 20 21 29. Ezr 1 2 3

14. 1Nya 22 23 24 Yn 15 30. Ezr 4 5 Mdo 2

15. 1Nya 25 26 27

16. 1Nya 28 29 Yn 16

Page 180: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

180

MWEZI: JULAI.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Ezr 6 7 8 17. Ayu 12 13 14 15

2. Ezr 9 10 Mdo 3 18. Ayu 16 17 18 19 Mdo 11

3. Neh 1 2 3 19. Ayu 20 21 22

4. Neh 4 5 Mdo 4 20. Ayu 23 24 25 26 Mdo 12

5. Neh 6 7 8 21. Ayu 27 28 29 30

6. Neh 9 Mdo 5 22. Ayu 31 Mdo 13

7. Neh 10 11 23. Ayu 32 33 34 35

8. Neh 12 13 Mdo 6 24. Ayu 36 37 Mdo 14

9. Est 1 2 3 25. Ayu 38 39 40

10. Est 4 Mdo 7 26. Ayu 41 42 Mdo 15

11. Est 5 6 7 8 27. Zab 1 2 3 4 5 6 7 8

12. Est 9 10 Mdo 8 28. Zab 9 10 11 12 Mdo 16

13. Ayu 1 2 3 4 29. Zab 13 14 15 16 17 Mdo 17

14. Ayu 5 6 Mdo 9 30. Zab 18 19 20 Mdo 18

15. Ayu 7 8 9 31. Zab 21 22 23 24 Mdo 19

16. Ayu 10 11 Mdo 10

Page 181: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

181

MWEZI: AGOSTI.

TARE

HE

ASUBUHI JIONI TA

RE

HE

ASUBUHI JIONI

1. Zab 25 26 27 28 29 Mdo 20 17. Zab 89 90 91 Rum 8

2. Zab 30 31 32 Mdo 21 18. Zab 92 93 94 95 96 97 98 Rum 9

3. Zab 33 34 35 Mdo 22 19. Zab 99 100 101 102 103 Rum 10

4. Zab 36 37 38 Mdo 23 20. Zab 104 105 Rum 11

5. Zab 39 40 41 42 Mdo 24 21. Zab 106 107 Rum 12

6. Zab 43 44 45 46 Mdo 25 22. Zab 108 109 110 111 112 113 Rum 13

7. Zab 47 48 49 50 Mdo 26 23. Zab 114 115 116 117 118 Rum 14

8. Zab 51 52 53 54 Mdo 27 24. Zab 119

9. Zab 55 56 57 58 Mdo 28 25. Zab 120 121 122 123 124 125

126 127 128 129 130 131

Rum 15

10. Zab 59 60 61 62 63

64

Rum 1 26. Zab 132 133 134 135 136 137

138

Rum 16

11. Zab 65 66 67 68 Rum 2 27. Zab 139 140 141 142 143 144 1Kor 1

12. Zab 69 70 71 Rum 3 28. Zab 145 146 147 148 149 150 1Kor 2

13. Zab 72 73 74 75 76 Rum 4 29. Mit 1 2 3 1Kor 3

14. Zab 77 78 Rum 5 30. Mit 4 5 6 7 1Kor 4

15. Zab 79 80 81 82 Rum 6 31. Mit 8 9 10 11 1Kor 5

16. Zab 83 84 85 86 87

88

Rum 7

Page 182: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

182

MWEZI: SEPTEMBA.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Mit 12 13 14 15 1Kor 6 17. Isa 10 11 2Kor 6

2. Mit 16 17 18 19 1Kor 7 18. Isa 12 13 14 2Kor 7

3. Mit 20 21 22 1Kor 8 19. Isa 15 16 17 2Kor 8

4. Mit 23 24 25 1Kor 9 20. Isa 18 19 20 21 2Kor 9

5. Mit 26 27 28 1Kor 10 21. Isa 22 23 2Kor 10

6. Mit 29 30 31 1Kor 11 22. Isa 24 25 26 2Kor 11

7. Mhu 1 2 3 1Kor 12 23. Isa 27 28 2Kor 12

8. Mhu 4 5 6 1Kor 13 24. Isa 29 30 2Kor 13

9. Mhu 7 8 9 1Kor 14 25. Isa 31 32 33 Gal 1

10. Mhu 10 11 12 1Kor 15 26. Isa 34 35 36 Gal 2

11. Wim 1 2 3 4 1Kor 16 27. Isa 37 38 39 Gal 3

12. Wim 5 6 7 8 2Kor 1 28. Isa 40 41 Gal 4

13. Isa 1 2 2Kor 2 29. Isa 42 43 Gal 5

14. Isa 3 4 5 2Kor 3 30. Isa 44 Gal 6

15. Isa 6 7 2Kor 4

16. Isa 8 9 2Kor 5

Page 183: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

183

MWEZI: OKTOBA.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Isa 45 46 47 Efe 1 17. Yer 14 15 1The 2

2. Isa 48 49 Efe 2 18. Yer 16 17 1The 3

3. Isa 50 51 52 Efe 3 19. Yer 18 19 20 1The 4

4. Isa 53 54 55 Efe 4 20. Yer 21 22 1The 5

5. Isa 56 57 58 Efe 5 21. Yer 23 2The 1

6. Isa 59 60 Efe 6 22. Yer 24 25 2The 2

7. Isa 61 62 63 Flp 1 23. Yer 26 27 28 2The 3

8. Isa 64 65 Flp 2 24. Yer 29 30 1Tim 1

9. Isa 66 Flp 3 25. Yer 31 1Tim 3 1Tim 2

10. Yer 1 2 Flp 4 26. Yer 32 1Tim 4

11. Yer 3 4 Kol 1 27. Yer 33 34 1Tim 5

12. Yer 5 Kol 2 28. Yer 35 36 1Tim 6

13. Yer 6 7 Kol 3 29. Yer 37 38 39 2Tim 1

14. Yer 8 9 Mdo 9 30. Yer 40 41 42 2Tim 2

15. Yer 10 11 Kol 4 31. Yer 43 44 2Tim 3

16. Yer 12 13 1The 1

Page 184: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

184

MWEZI: NOVEMBA.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Yer 45 46 2Tim 4 17. Eze 21 22 Ebr 12

2. Yer 47 48 Tit 1 18. Eze 23 24 Ebr 13

3. Yer 49 Tit 2 19. Eze 25 26 Yak 1

4. Yer 50 Tit 3 20. Eze 27 28 Yak 2

5. Yer 51 Flm 1 21. Eze 29 30 Yak 3

6. Yer 52 Ebr 1 22. Eze 31 32 Yak 4

7. Omb 1 2 Ebr 2 23. Eze 33 34 Yak 5

8. Omb 3 4 5 Ebr 3 24. Eze 35 36 1Pet 1

9. Eze 1 2 3 Ebr 4 25. Eze 37 38 1Pet 2

10. Eze 4 5 6 Ebr 5 26. Eze 39 40 1Pet 3

11. Eze 7 8 Ebr 6 27. Eze 41 42 1Pet 4

12. Eze 9 10 11 Ebr 7 28. Eze 43 44 1Pet 5

13. Eze 12 13 14 Ebr 8 29. Eze 45 46 2Pet 1

14. Eze 15 16 Ebr 9 30. Eze 47 48 2Pet 2

15. Eze 17 18 Ebr 10

16. Eze 19 20 Ebr 11

Page 185: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

185

MWEZI: DESEMBA.

TAREHE ASUBUHI JIONI TAREHE ASUBUHI JIONI

1. Dan 1 2 2Pet 3 17. Yon 1 2 3 4 Ufu 8

2. Dan 3 4 1Yn 1 18. Mik 1 2 Ufu 9

3. Dan 5 6 1Yn 2 19. Mik 3 4 5 Ufu 10

4. Dan 7 8 1Yoh 3 20. Mik 6 7 Ufu 11

5. Dan 9 10 1Yoh 4 21. Nah 1 2 3 Ufu 12

6. Dan 11 12 1Yoh 5 22. Hab 1 2 3 Ufu 13

7. Hos 1 2 3 4 2Yoh 1 23. Sef 1 2 3 Ufu 14

8. Hos 5 6 7 3Yoh 1 24. Hag 1 2 3 Ufu 15

9. Hos 8 9 10 Yud 1 25. Zek 1 2 3 Ufu 16

10. Hos 11 12 13 14 Ufu 1 26. Zek 4 5 6 7 Ufu 17

11. Yoe 1 2 Ufu 2 27. Zek 8 9 Ufu 18

12. Yoe 3 4 Ufu 3 28. Zek 10 11 Ufu 19

13. Amo 1 2 3 Ufu 4 29. Zek 12 13 14 Ufu 20

14. Amo 4 5 6 Ufu 5 30. Mal 1 2 Ufu 21

15. Amo 7 8 9 Ufu 6 31. Mal 3 Ufu 22

16. Oba 1 Ufu 7

Hongera kwaNajua utajifunza mengi sana!

Pole sana pia ikiwa tu hapa umeshachoka kuisoma!

Waweza kusave kwenye email,word,aka ukaprint na kubandika ukutani!

Page 186: IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE. - WordPress.com · Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 40, kwa muda usiopungua miaka 1500; (yaani kuanzia 1400 K.K hadi 100 B.K). zaidi

186

VITABU REJEA!

Fimbo ya Mchungaji;World Map, 1996 Ralph Mahoney

Biblia inasema. Donald C Fleming. Kanisa la Biblia.

Ifahamu Agano Jipya :AM Hunter 1992 Central Tanganyika Press.

Kamusi ya Biblia Don Fleming.kanisa la Biblia Publishers.2012.

New Geneva study Bible,bringing the light of reformation to scripture. 1995 NKJV Thomas

Nelson Publishers.

Agano Jipya lasema.Donald C Fleming. Kanisa la Biblia.1989 Toleo la 2.

Kauli Tata za Bwana Yesu : Isaac Edward Challo @ 2009

The Zondervan Pictorial Bible Dictionary. Merrill C Tenney pg 189

www. Biblecharts.org.

Biblia maandiko matakatifu. Union version 1952.