hotuba ya maalim seif - january 9 2016

Upload: anonymous-x8qgwff

Post on 17-Feb-2018

320 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    1/27

    1

    MAELEZO YA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CUF,

    MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, KWENYE MKUTANO NA

    WAANDISHI WA HABARI SERENA HOTEL, DAR ES SALAAM,

    TAREHE 11 JANUARI, 2016

    KIINI CHA MZOZO WA KIKATIBA NA KISHERIA ZANZIBAR

    ULIOTOKANA NA KUFUTWA ISIVYO HALALI KWA UCHAGUZI

    MKUU, CHANGAMOTO ZAKE NA NAMNA YA KUUTATUA

    N!"! #$%"! W$$%&'(& )$ H$*$+&,

    Awali ya yote, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu

    Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima wa afya na tukaweza kukutana

    hapa asubuhi hii ya leo. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu pia kwa

    kuijaalia nchi yetu kuendelea kubaki katika hali ya amani na utulivu licha

    ya changamoto nyingi zinazotukabili. Tunapoona watu wa nchi nyengine,

    zikiwemo nchi jirani, wanateseka kwa kukosa amani ndipo tunapozidi

    kutambua umuhimu wa neema hii ya amani katika nchi yetu.

    Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki nchi yetu na watu

    wake na atujaalie hekima na busara katika kuendesha mambo yetu ilituendelee kuitunza neema hii aliyotupa.

    Pili, nichukue fursa hii kukushukuruni nyinyi wahariri na waandishi wa

    habari kwa kuitikia wito wetu na kuja kutusikiliza. aamini mtatusikiliza

    kwa makini, hususan kutokana na uzito wa suala tulilowaitia, na kisha

    mtawafikishia !atanzania yale ambayo tumekuja kuwaeleza.

    Tumewaita leo hii ili kuzungumzia kwa kina suala la "chaguzi Mkuu wa

    #anzibar wa tarehe $% &ktoba, $'(% na matukio yaliyofuata, ikiwemohatua isiyo halali kikatiba na kisheria ya Mwenyekiti wa Tume ya

    "chaguzi ya #anzibar )#*+, -echa alum -echa, kudai kwamba amefuta

    uchaguzi huo na matokeo yake, mgogoro uliosababishwa na kitendo

    hicho haramu, mazungumzo yanayoendelea kutafuta ufumbuzi wa suala

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    2/27

    2

    hilo, pamoja na njama za kuhujumu jitihada zinazoendelea za kutafuta

    ufumbuzi kwa njia ya amani.

    aomba mnivumilie wakati nasoma maelezo haya niliyoyaandaa kwani

    kwa faida yenu na kwa faida ya !atanzania nimeona kuna haja ya kutoamaelezo ya kina kidogo ili suala hili liweze kufahamika kwa ukamilifu

    wake.

    1 UTANGULIZI

    /itendo cha Mwenyekiti wa Tume ya "chaguzi #anzibar, -echa alum

    -echa kutoa tamko lisilo halali kikatiba na kisheria la kuufuta "chaguzi

    Mkuu wa #anzibar pamoja na matokeo yake kumeitumbukiza #anzibar

    katika mzozo mkubwa wa kikatiba na kisheria. Aidha, kitendo hichokimeifedhehesha sana #anzibar na -amhuri ya Muungano wa Tanzania

    mbele ya -umuiya za kikanda na kimataifa. Mzozo huo pia umeiweka

    #anzibar katika njia panda sio tu kwa hali ya sasa lakini kwa mustakbala

    wake wa baadaye na kuirejesha nyuma sana katika jitihada za kujenga

    umoja wa kitaifa unaozingatia misingi ya utawala wa sheria, demokrasia

    na mfumo wa utawala bora.

    /ubwa zaidi, mzozo huo umeleta fadhaa kubwa sana kwa wananchi wa

    mirengu yote ya kisiasa. "chumi na ustawi wa #anzibar nao umeathirikasana. !ananchi wako taaban huku hali ya maisha ikizidi kuwa ngumu na

    bidhaa zikipanda bei kwa kasi wakati mzunguko wa fedha ukiwa

    umepotea.

    /atika hali hii, hapana budi juhudi za kuutatua mzozo huu zikamilishwe

    kwa haraka kwa kuzingatia misingi ya kikatiba, kisheria na pia

    mustakbala utaowafanya wananchi wa #anzibar waamini kwamba

    mfumo uliopo wa kikatiba, kiutawala na kisheria ambao umechukua

    muda kuujenga unaweza kufanya kazi na pale penye kasoro unaweza

    kuimarishwa hatua kwa hatua kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwamiaka kadhaa sasa.

    2 YALIYOJITOKEZA KATIKA UCHAGUZI

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    3/27

    3

    1- H$.& /$ U($"!#&

    "chaguzi Mkuu wa #anzibar uliofanyika tarehe $% &ktoba, $'(% kama

    zilivyo chaguzi nyengine unakwenda sambamba na "chaguzi Mkuu wa

    -amhuri ya Muungano wa Tanzania. +haguzi hizo mbili zinafanyika

    katika vituo sawa kwa kutumia utaratibu, ulinzi na usimamizi ulio sawa.

    /wa hivyo, siku ya uchaguzi mkuu mwananchi wa #anzibar ndani ya

    kituo kimoja anapiga kura tano )% badala ya tatu )0 anazopiga

    mwananchi aliyepo Tanzania 1ara. /ura ambayo mwananchi wa

    #anzibar anapiga ni2

    a /ura ya 3ais wa #anzibar4

    b /ura ya Mjumbe wa 1araza la !awakilishi4

    c /ura ya 5iwani4

    d /ura ya 3ais wa -amhuri ya Muungano wa Tanzania4 nae /ura ya Mbunge

    /wa jumla uchaguzi ulifanyika katia njia ya amani, utulivu na bila ya

    kutokea vurugu. !aangalizi wa uchaguzi wa ndani na wa nje ya nchi katika

    taarifa zao za awali walisifu na kupongeza jinsi uchaguzi ulivyofanyika.

    2- K!$%"$#)$ M$34 /$ W$5!*4 )$ B$+$#$ .$ W$)$3&.&'(&

    %$ M$&)$%&

    /wa mujibu wa heria ya "chaguzi ya #anzibar amba (( ya (678, kama

    ilivyo kwa heria ya "chaguzi ya -amhuri ya Muungano wa Tanzania,matokeo ya !ajumbe wa 1araza la !awakilishi na Madiwani unatangazwa

    na Msimamizi wa "chaguzi wa -imbo husika )3eturning &fficer. /ifungu

    cha 77 cha heria ya "chaguzi kinaeleza kama ifuatavyo2

    baada ya matokeo ya uchaguzi kuthibitishwa Msimamizi wa Uchaguzi:

    (a)Atamtangaza mgombea aliyepata kura nyingi mshindi hapo hapo;

    (b)Atampatia aliyechaguliwa taarifa ya kuchaguliwa kwa maandishi;

    (c)Atatuma taarifa ya uchaguzi kwa ume ya Uchaguzi kwa ajili ya

    kuchapishwa katika Gazeti rasmi la Serikali.

    /ifungu cha ($0 cha heria ya "chaguzi kinaeleza wazi kuwa uchaguzi wa

    Mjumbe wa 1araza la !awakilishi hautahojiwa isipokuwa kwa njia ya /esi

    ya "chaguzi mbele ya Mahkama /uu. /ifungu cha ((9 cha heria ya

    "chaguzi kinaeleza watu ambao wana haki ya kufungua /esi ya "chaguzi.

    Mwenyekiti wa Tume wala Tume yenyewe haimo katika orodha ya

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    4/27

    4

    wanaoruhusiwa kufungua kesi ya uchaguzi kuhoji matokeo ya uchaguzi

    yaliyotangazwa na Msimamizi wa "chaguzi.

    7- K!3$&.&3$ 3)$ U($"!#& )$ W$)$3&.&'(& %$ M$&)$%&

    :adi kufikia asubuhi ya tarehe $9 &ktoba, matokeo ya majimbo yote %0

    ambayo yalifanya uchaguzi wa !ajumbe wa 1araza la !awakilishi

    yalitangazwa na !asimamizi wa "chaguzi na kuwapatia shahada za

    kuchaguliwa wale wote walioshinda. Aidha, uchaguzi wa madiwani

    ulikamilika na kupatiwa shahada katika !adi zote zilizofanya uchaguzi.

    /wa maana hiyo, kufikia tarehe $9 &ktoba, uchaguzi wa !ajumbe wa1araza la !awakilishi na Madiwani ulishakamilika. Aidha, uchaguzi wa

    !abunge nao ulishakamilika na washindi kukabidhiwa vyeti vyao vya kuwa

    wamechaguliwa.

    heria ya "chaguzi ya #anzibar, kifungu cha ($0 kimeeleza wazi kwamba

    baada ya uchaguzi kukamilika, unaweza kuhojiwa tu kwa njia ya /esi ya

    "chaguzi sio vyenginevyo.

    8- M$34 /$ U($"!#& )$ R$&' )$ Z$%#&*$+

    :adi kufikia tarehe $9 &ktoba, asubuhi kazi ya kuhesabu kura za urais na

    kukusanya matokeo katika Majimbo yote ya #anzibar ilishakamilika. heria

    ya "chaguzi kifungu cha 8$ kinaelekeza ifuatavyo2

    Baada ya kukamilika kuhesabu kura katika vituo vyote vya uchaguzi

    katika jimbo (a ikihitajika kazi ya kuhesabu tea kura) !simamizi wa

    "chaguzi wa #imbo atawasilisha kwa $ume ya "chaguzi a kwamgombea urais au wakala wake%

    a) &dadi ya kura za urais zilizopigwa katika #imbo'

    b) &dadi ya kura alizopata kila mgombea'

    c ama mgombea urais i mmoja tu idadi ya kura zilizomchagua

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    5/27

    5

    Baada ya hapo $ume itajumlisha kura zote za "rais kutoka kila #imbo.

    heria ya "chaguzi, kifungu cha 8$)$ inaeleza kwamba Tume inaweza,ikiwa itakuwa na sababu za msingi, kabla ya kutangaza matokeo kuagiza

    kura katika majimbo au jimbo fulani kuhesabiwa upya.

    1aada ya kujumuisha matokeo ya urais kutoka katika Majimbo, heria ya

    "chaguzi kifungu cha 8$)0 kinaelekeza kwamba Tume itamtangaza

    mshindi.

    Tume ilifanya kazi ya kujumlisha matokeo ya "rais kutoka katika Majimbo

    kama inavyoagizwa na heria. 1aada ya majumuisho hayo, hakuna pahala

    ambapo Tume iliagiza kura zihesabiwe upya kama heria inavyoagiza ikiwakutakuwa na sababu ya kufanya hivyo. 1ila ya shaka kwa vile hakukuwa na

    kasoro iliyopelekea haja ya kuhesabiwa upya Tume haikuchukua hatua hiyo.

    :adi kufikia tarehe $7 &ktoba, Tume ilishatangaza matokeo ya kura za

    "rais kutoka katika majimbo 0(4 na ilishakamilisha kujumlisha matokeo ya

    majimbo mengine 6 )ambayo ilikuwa bado haijayatangaza. /wa maana

    hiyo, kazi ya kujumlisha na kuhakiki matokeo ya majimbo 8' kati ya

    majimbo %8 ilikuwa imeshakamilika. /wa mujibu wa heria ya "chaguzi

    kifungu cha 8$)9 Tume inatakiwa itangaze matokeo ndani ya siku 0 tokeasiku ya kupiga kura. :ivyo, tarehe $7 &ktoba ilikuwa ndiyo siku ya mwisho

    ambayo Tume ilitakiwa itangaze matokeo ya "rais.

    :ata hivyo, majumuisho ya matokeo ya "rais kupitia taarifa ambayo Tume

    iliwapatia mawakala wa wagombea au wagombea wenyewe chini ya kifungu

    cha 8$)( cha heria ya "chaguzi baada ya kujumuishwa yalikuwa

    yanaonyesha kwa ufupi kama ifuatavyo2

    MGOMBEA KURA ZA

    MGOMBEA

    ASILIMIA

    DR ALI

    MOHAME

    D SHEIN

    (7$,'(( 89.$7;

    MAALIM $'

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    6/27

    6

    SEIF

    SHARIF

    HAMAD

    =5A5= >A/"3A :A?A?=

    060, 0$0

    :apa hatukuorodhesha matokeo ya wagombea wengine kwani hakuna hata

    mmoja aliyefikisha angalau asilimia ( ya kura zilizopigwa.

    7 KUFUTWA KWA UCHAGUZI NA MWENYEKITI WA TUME

    1- M)4%4% )$ M)4%/43&& )$ T!4 %$ Y$.&/5&34#$ 3$*.$

    /$ K!9!$ U($"!#&

    /abla ya Mwenyekiti wa Tume kutoa tamko lake peke yake la kufuta

    uchaguzi alionesha dhahiri kuwa alikuwa na ajenda ya siri. /wanza,

    alichelewesha kwa makusudi zoezi la kujumuisha matokeo kwa visingizio

    mbali mbali ikiwemo kuchelewa kufika kwenye kituo cha majumuisho

    kilichokuwepo :oteli ya 1wawani, kuondoka mapema na kusingizia

    anaumwa. /wa mfano siku ya tarehe $< &ktoba aliahirisha zoezi hilo kwa

    madai ya kuwa na tatizo la sindikizo la damu. iku ya tarehe $7 &ktobaambayo kwa mujibu wa heria ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kutangaza

    matokeo, Mwenyekiti hakuonekana kabisa katika kituo cha kutangaza

    matokeo katika :oteli ya 1wawani. 1aada ya !ajumbe waliobaki wa Tume

    kuona wanachelewa na siku hiyo ilikuwa ya mwisho, waliamua kwamba

    Makamu Mwenyekiti wa Tume, -aji Abdulhakim Ameir =sssa aendelee

    kuongoza Tume kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya "rais kwa vile

    kifungu cha ((6)(' cha /atiba ya #anzibar kinaruhusu kufanya hivyo.

    !akati zoezi hilo likiendelea mambo matatu makubwa yalijitokeza2

    a /ituo cha 1wawani kilizingirwa na -eshi la "linzi la Tanzania

    )-!T# wakitoa amri ya kuzuia kila aliyekuwemo ndani asitoke na

    aliyekuwa nje asiingie katika eneo hilo4

    b Makamu Mwenyekiti wa Tume ya "chaguzi, -aji Abdulhakim Ameir

    =ssa alipewa taarifa ya wito muhimu na mmoja wa watumishi wa

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    7/27

    7

    Tume na alipotoka nje ya ukumbi wa kikao cha Tume alichukuliwa na

    askari Polisi na kupelekwa Makao Makuu ya -eshi la Polisi, /ilimani4

    c Televisheni ya hirika la "tangazaji #anzibar )#1+ na redio ya

    hirika hilo yalitoa matangazo ya tangazo la Mwenyekiti wa Tumekufuta uchaguzi na matokeo yake4

    1aada ya hapo Tume haikuitishwa tena hadi tarehe ( ovemba, $'(%

    ambapo Mwenyekiti aliwaarifu !ajumbe wa Tume yafuatayo2

    i. /wanza alitangulia kuomba radhi !ajumbe kwa vile baada ya

    kukutana na vyombo )bila ya kutaja vyombo gani alilazimika

    kusema baadhi ya mambo ya uongo katika taarifa yake na kufuta

    uchaguzi ili kuokoa hali4ii. Alitaka !ajumbe wamuunge mkono kwa kitendo alichofanya4

    Tarehe ($ ovemba, Mwenyekiti wa Tume alitoa Tangazo rasmi amba (0'

    la kufuta uchaguzi )matokeo kupitia @azeti 3asmi la erikali

    lililochapishwa tarehe 9 ovemba. :ata hivyo, Tangazo hilo lilikuwa na

    kasoro za wazi za kisheria ambazo nitazieleza hapo mbele.

    2- U($.$.& )$ M)4%/43&& )$ T!4 3!9!$ U($"!#&

    Mbali ya kwamba kitendo cha Mwenyekiti wa Tume kimedhihirika kuwa ni

    njama za wazi za kisiasa ambazo zilipangwa na kutekelezwa na Mwenyekiti

    wa Tume, vyombo vya ulinzi na viongozi wa kisiasa ambao sasa

    wanamtetea, uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume kufuta uchaguzi hauna

    uhalali wowote kwa sababu zifuatazo2

    a "chaguzi ukamilika: "chaguzi wa !ajumbe wa 1araza la

    !awakilishi na Madiwani kwa mujibu wa heria ya "chaguzi

    ulishakamilika. /wa upande wa uchaguzi wa 3ais naoulishakamilika isipokuwa hatua ya kutangaza matokeo ambayo

    nayo kwa mujibu wa sheria ilitakiwa iwe imeshakamilika.

    /ama ilichelewa ilicheleweshwa makusudi na Mwenyekiti

    katika juhudi zake za kutafuta visingizio vya kuharibu uchaguzi

    ili mshindi halali asitangazwe. Tume haina mamlaka ya

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    8/27

    8

    kuahirisha, kutengua matokeo au kufuta uchaguzi uliokwisha

    kamilika. :*3=A >A "+:A@"#= imeeleza wazi mamlaka

    ya Tume baada ya kazi ya kuhesabu kura kukamilika. Mamlaka

    pekee ni ya kurudia kuhesabu kura kwa majimbo yote au kwa

    -imbo moja iwapo itaridhika kwamba ipo sababu ya msingi yakufanya hivyo. /ifungu cha 8$)$ cha heria ya "chaguzi

    imeeleza wazi juu ya uwezo huo wa Tume. /uipa mamlaka

    Tume kutengua uchaguzi uliokwisha kamilika ni sawa na

    kuingilia kazi za mhimili wa Mahkama. :ata Mahkama

    yenyewe inafungwa na heria ya "chaguzi. /ifungu cha ($0

    kimeeleza watu ambao wanaweza kuhoji matokeo ya uchaguzi

    baada ya kutangazwa na 3eturning &fficer. Mwenyekiti wa

    Tume au Tume hawamo katika orodha ya wanaoweza kuhoji

    uchaguzi baada ya kutangazwa matokeo. Aidha, chini yaheria ya "komo, Mahkama haiwezi kusikiliza tu shauri lolote

    lazima izingatie muda unaokubalika kusikiliza shauri4

    b !amlaka ya !weyekiti:i wazi kuwa Mwenyekiti alivunja

    /atiba. Alikwenda kinyume na kifungu cha ((6)( cha /atiba

    na alikiuka kifungu cha ((6)(' cha /atiba juu ya utaratibu wa

    Tume kufanya maamuzi kwa kuamua kufuata uchaguzi bila ya

    kuitisha kikao cha Tume wala kushauriana na Tume. /ifungu

    cha ((6)( cha /atiba ya #anzibar kinaeleza muundo wa Tumeambayo imeshirikisha wadau wakuu wa uchaguzi na watu

    wengineo huru. /ifungu cha ((6)(' kinaweka utaratibu wa

    Tume kufanya maamuzi na kimeeleza kwa maelezo ya wazi

    kama ifuatavyo2

    ;3&)$%" ($ &3!$% /$ T!4 /$ U($"!#& %&

    M)4%/43&& $! M$3$ M)4%/43&& %$ W$5!*4 )$%%4

    %$ kila!$!#& )$ T!4 i lazima!!%")4 3% %$

    W$5!*4 )$.& )4%"&a kwanza ni suala la 3ais kumaliza

    muda wake kikatiba. /atiba ya #anzibar chini ya kifungu cha $7)$

    kimeeleza wazi kwamba muda wa 3ais kushikilia wadhifa huo ni miakamitano. /ifungu cha $6 kinaeleza masharti ya kuongeza muda huo wa

    miaka mitano ambayo ni magumu na yenye ukomo maalum. :ata hivyo,

    washauri wa 3ais kwa kutumia tafsiri isiyo sahihi ya /atiba wamemshauri

    kwamba kwa kutumia kifungu cha $7)()a anaweza kuendelea kuwa 3ais

    hadi 3ais mpya atapoapishwa. /wa ufupi tunaangalia athari ya tafsiri hiyo2

    M&=$3$ /$ K&9!%"! ($ 2>?1-?$-

    /ifungu cha $7)()a kinachoruhusu 3ais aendelee mpaka 3aisanayefuata ale kiapo kina mipaka ya wazi katika /atiba. Mpaka wa

    kwanza unahusu muda wa "rais. /atiba chini ya kifungu cha $7)$

    kimeweka bayana kuwa muda wa "rais ni miaka mitano. :ili ni sharti

    mahsusi na ndio maana /atiba haijaruhusu suala la kuongezwa muda wa

    miaka % lifanywe kiholela au kwa mlango wa nyuma. /ifungu cha $6

    cha /atiba kimeweka bayana sababu na utaratibu wa kuongeza miaka

    mitano. ababu hizo ni nzito na muda kuongezwa ni mahsusi. /ifungu

    cha $6 kinaeleza2 ikiwa #amhuri ya !uugao wa $azaia imo

    katika vita a ikiwa *ais aaoa kuwa i muhimu kuzuia uchaguzi,Baraza la -awakilishi liaweza kwa kupitisha azimio, kuzidisha muda

    wa miaka mitao uliotajwa kweye kijiugu cha () cha kiugu cha

    / katika kipidi hadi kipidi lakii hakua kipidi kitachozidi miezi

    sita mululizo.

    Mpaka wa pili unaoonesha ni kwa kiasi gani /atiba haitoi mwanya wa

    kujiongezea miaka mitano, ni ile ya ukomo wa vipindi viwili vya miaka

    mitano chini ya kifungu cha 0')()b. /atika kuonesha jinsi /atiba

    ilivyo strictkatika ukomo wa miaka mitano, tafsiri ya miaka mitano chiniya kifungu cha 08)iv imefanywa kwa namna ambayo /atiba inaruhusu

    miaka mitano ipungue kuliko kuzidi. /ifungu hicho kinaeleza2 Cbila

    kujali masharti ya viugu vya /(0) a 01(2) (b) vya atiba, edapo

    mtu aayemuata *ais kwa madaraka atashika kiti cha *ais kwa

    kipidi kiachopugua miaka mie ataruhusiwa kugombea aasi ya

    *ais mara mbili lakii kama atashika kiti cha *ais kwa muda wa

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    13/27

    13

    miaka mie au zaidi ataruhusiwa kugombea aasi ya *ais mara

    moja tu.

    /ama /atiba ingekuwa imelichukulia kipindi cha miaka mitano kwa

    wepesi kama alivyotaka kutuaminisha aliyetoa ushauri basi isingechukuashida ya kutafsiri maana ya miaka mitano kwa namna iliyofanywa na

    kifungu cha 08)iv.

    :ivyo tafsiri yoyote ya /atiba inayotoa mwanya wa kuongeza kipindi

    cha "rais cha miaka mitano kwa njia nyepesi, ya kiholela na ya kiujanja,

    tafsiri hiyo haiwezi kuwa sahihi. /atika kutafsiri /atiba Profesa +rabe

    ametoa angalizo muhimu kwa kusema kuwa2 Cits 3the costitutio4

    provisios are ot mere rules o coduct or the guidace o society,

    but also commads to be obeyed. &t is ot a e5uatio i mathematicsto be iterpreted by reerece to umbers, it is, i a sese, orgaic6.all

    the duties, obligatios, powers, privileges ad rights must be e7ercised

    i accordace with the letter o the costitutio. !ore tha that, they

    should be e7ercised ad eorced i accordace with the spirit o the

    costitutio

    M"%"$% )$ T$9'&+& %$ K&9!%"! ($ 2>?2- %$ 2@

    "shahidi mwengine wa wazi kuwa tafsiri inayotolewa ya kifungu cha$7)( )a kuwa sio sahihi ipo katika /anuni za tafsiri ya sheria. Moja ya

    /anuni za msingi ni kuwa tafsiri yoyote ya sheria au kifungu cha sheria

    inayopelekea kufanya kifungu chengine cha sheria kisiwe na maana

    (irrele"ant)au kisiwe na haja ya kuwepo (redundant)basi tafsiri hiyo ni

    ya kituko (absurd)# a tafsiri yoyote ya kituko basi sio sahihi. Tafsiri

    inayotolewa kumruhusu 3ais aendelee inakifanya kifungu cha $7)$

    kinachoweka muda wa "rais kuwa miaka mitano kisiwe na maana.

    Aidha, inakifanya kifungu cha $6 cha /atiba kinachoeleza sababu na

    utaratibu wa kuongeza huo muda wa miaka mitano kisiwe na haja yakuwepo. ?akini pia inafanya mfumo mzima wa kuvunjwa 1araza la

    !awakilishi na kuitishwa uchaguzi mkuu ndani ya muda maalum na

    muda wa ukomo wa vipindi vya "rais vyote visiwe na maana. /ifungu

    cha $7)( )a hakizungumzii muda wa "rais bali kinazungumzia wakati tu

    mahsusi ndani ya hiyo miaka mitano ambapo kiti cha 3ais atakabidhiwa

    mtu mwengine.

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    14/27

    14

    /ifungu hicho kinaweza tu kutumika kuongezeka kwa miaka mitano

    iwapo itatokea dharura halali kwa mujibu wa sheria )eDigency by

    operation of the law kama vile "chaguzi katika jimbo au majimbo fulani

    unapotokea kuharibika kwa sababu inayokubalika na ambayo sheriaimeiruhusu Tume kuakhirisha uchaguzi na kuitisha siku nyengine. :ii ni

    dharura ambayo sheria imeshaiwekea misingi yake. Au dharura

    isiyotazamiwa na inayokubalika )unforeseeable legitimate eDigency.

    Mfano mzuri hapa ni pale mgombea anapofariki kabla tu ya uchaguzi au

    kabla ya kuapishwa. :izi ni dharura ambazo mifumo yote ya kisheria

    inazitambua na hata Mahkama imezitambua.

    A($+& #$ T$9'&+& &'&/3!)$ '$(&(&

    Tafsiri isiyo sahihi iliyotolewa ina athari kubwa zifuatazo2

    $wanza%/atiba haikuweka muda maalumu wa kufanya uchaguzi

    uliofutwa katika mazingira yasiyokuwa halali. /isheria uchaguzi

    uliofutwa katika mazingira hayo hauitwi kwamba ni uchaguzi

    uliofutwa bali ni uchaguzi unaodaiwa umefutwa )purported

    nullification of election. /atiba imeweka muda kwa chaguzi

    zinazoitishwa kihalali tu ama kwa kuvunjwa 1araza, kufariki

    mwenye wadhifa au matokeo kulingana. /wa tafsiri iliyotolewa ina

    maana kuwa 3ais aliyepo anaweza kushika wadhifa huo hadi Tume

    ya "chaguzi itapoamua kuitisha uchaguzi. /wa vile hakuna ukomo

    wala muda maalum uliowekwa ndani ya /atiba wala heria

    uchaguzi unaweza kuitishwa hata baada ya mwaka mmoja au miwili

    kwa vile hakuna ukomo wa kikatiba wala wa kisheria. Athari ya

    jambo hili ni sawa na kuisimamisha sehemu ya /atiba4

    &ili%tafsiri hiyo ya /atiba inatoa mwanya kwa 3ais kutosimamia

    /atiba kwa kutomchukulia hatua Mjumbe wa Tume aliyekwenda

    kinyume na /atiba au sheria iwapo tu Mjumbe huyo amefanya

    hivyo kwa manufaa ya 3ais. /ifungu cha ((6)9 )

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    15/27

    15

    "chaguzi ipo juu ya /atiba na heria za nchi kwa vile 3ais ana hiari

    ya kusimamia vifungu vya /atiba vinavyosimamia nidhamu yao.

    /ubwa zaidi kuliko yote ni kujiuliza iwapo mwendo huo wa 3ais

    hauendani kinyume na masharti ya kifungu cha 0

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    16/27

    16

    (678, tokea awali ilipotungwa mwaka (678 dhana hizi mbili

    zilitenganishwa na ziliwekewa masharti tofauti juu ya uhai wa 1araza.

    5hana ya 1araza kuvunjwa na athari zake iliwekwa chini ya kifungu cha

    6')( na ile ya 1araza kumaliza muda iliwekwa chini ya kifungu cha 6$sawa na /atiba ilivyo sasa hivi. Tofauti yao ni neno tu ambalo

    limetumika4 chini ya Toleo la mwanzo la /atiba neno lililotumika ni

    C1araza litapo"un*ikaG na Toleo la $'(' neno linalotumika ni C1araza

    litapo"un*waG. Tofauti hii ya maneno ilifanywa na kifungu cha $% cha

    heria ya Marekebisho ya /umi ya /atiba, amba $ ya $''$. :ata

    hivyo mabadiliko haya ya maneno hayakubadili dhana hizi mbili kwa

    namna yoyote ile.

    /atiba ya #anzibar imeweka dhana mbili katika uhai wa 1araza. /wanza1araza linavunjwa. Madhumuni ya kuvunjwa ni kutoa fursa ya kuandaa

    uchaguzi mkuu. /atiba imetoa siku 6' kufanyika maandalizi ya uchaguzi

    hadi 1araza na 3ais mpya kuapishwa. /atika kipindi hicho ndipo

    ambapo Mawaziri wanaendelea kuwa Mawaziri. /ifungu cha 87)b

    kimetumia maneno ya wazi kwamba nafasi ya !aziri itakuwa wazi2

    Ciwapo mjumbe ameacha kuwa mjumbe wa 1araza la !awakilishi kwa

    sababu yegie zaidiya kuvujika kwa 1araza hiloG. :ivyo, 1araza

    kumalizika muda )lapse or eDpiration of tenure ni wazi haingii katika

    dhana ya 1araza kuvunjika )dissolution. 1araza likimalizika mudalinakuwa halipo na ndio maana hata /atiba, kifungu cha 6$)( kimetumia

    maneno ;!aisha/$ B$+$#$ .$ W$)$3&.&'(& /$$4%4.4$ 3)$ !$ )$

    &$3$ &$%

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    17/27

    17

    viwili tofauti, ndio maana /atiba ya baadhi ya nchi wameweka bayana

    dhana hizi mbili katika suala la kuendelea nafasi ya uwaziri baada ya 1unge

    kuvunjwa au kumaliza muda. /atiba ya Hiji kwa mfano, katika kifungu cha

    ('%)$ inaeleza2 Csub*ect to subsection (+)% appointment of a Ministerterminates if;

    (a),

    (d) the Minister ceases to be a Member of &arliament

    (+) if a Minister ceases to be a Member of &arliament because of the e7piry

    or dissolutio o the +ouse o *epresetatives% he or she continues in office

    as Minister until the ne-t appointment of a &rime Minister#

    /atiba ya #anzibar imeruhusu kwa maneno ya wazi kuwa !aziri aendeleena uwaziri katika kipindi ambacho 1araza limevunjwa tu na sio wakati

    ambao 1araza limemaliza muda. /wa hivyo tokea 1araza kumaliza muda

    wake tarehe ($ ovemba, #anzibar haina mawaziri. :ata hivyo baadhi ya

    waliokuwa mawaziri wamefanywa kama bado ni mawaziri na wanaendelea

    kufanya maamuzi makubwa jambo ambalo ni la hatari.

    - K!3!)4= B$+$#$ .$ W$)$3&.&'(&

    1araza la !awakilishi limemaliza muda tokea tarehe ($ ovemba. :oja

    kuhusu suala hili yameelezwa kwa kina katika aya )b hapo juu inayohusu

    kutokuwepo mawaziri. Aidha, pika wa 1araza hilo amethibitisha kwamba

    1araza halipo ingawa jambo la kushangaza naye amedai yeye na aibu

    wake wanaendelea kushika madaraka yao mpaka pika mpya atapoapishwa.

    /atiba ya #anzibar imeeleza wazi chini ya kifungu cha %A mgawanyo wa

    kazi baina ya mihimili mikuu ya erikali. Miongoni mwa mihimili hiyo ni

    1araza la !awakilishi. /azi muhimu ya 1araza ni kuisimamia erikali.

    /utokuwepo chombo hicho huku erikali ikiendelea na kazi zake ni jambo

    la kuvunja katiba kwa kiasi kikubwa.

    2- H5$ /$ K!+!&)$ U($"!#&

    :oja ya kurudiwa uchaguzi ambayo imeshikiwa bango na +hama cha

    Mapinduzi, #anzibar ni ya kutafuta manufaa ya kisiasa baada ya +hama cha

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    18/27

    18

    Mapinduzi kushindwa katika uchaguzi. Mbali ya matokeo ya uchaguzi ya

    "rais wa #anzibar ambayo yanaonyesha wazi kuwa ++M imeshindwa kwa

    kura nyingi sana kwa kiwango na uzoefu wa #anzibar, hata kura za "rais wa

    -amhuri ya Muungano kwa upande wa #anzibar zinaonyesha hivyo hivyo nakwa hiyo kuthibitisha kuwa ++M ilipoteza uchaguzi huo. /wa muhtasari

    matokeo ya "rais wa Muungano kwa upande wa #anzibar ni kama

    yafuatavyo2

    MGOMBEA KURA HALALI ASILIMIA

    DR JOHN

    POMBE

    MAGUFULI

    (68,0(< 89.%;

    EDWARD

    NGOYAYE

    LOWASSA

    $((,'00 %'.%';

    =5A5= >A /"3A

    :A?A?=

    8(

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    19/27

    19

    /iini cha mzozo uliozushwa katika uchaguzi ni uamuzi batili wa

    Mwenyekiti wa Tume. /urejea uchaguzi bila kupatia ufumbuzi juu ya

    uhalali wa uamuzi wa Mwenyekiti ni sawa na kuhalalisha kitendo cha

    Mwenyekiti na kutoa ruhusa kuwa huko mbele anaweza kufanya tena

    kitendo kama hicho au Tume inaweza kufanya kitendo kama hicho. :iini kujenga msingi wa kuwa na chaguzi zisizokwisha na mizozo isiyo na

    mwisho. ?azima mipaka ya Mwenyekiti na Tume iwekwe bayana ili

    hapo baadaye ijulikane nini ukomo wa mamlaka yao.

    - K!54%"$ I$%& /$ W$=&"$ K!+$

    "chaguzi ni wa wapiga kura na sio wa vyama au wagombea. ?azima

    wapiga kura waridhishwe kuwa uchaguzi ulikuwa na tatizo la kiasi cha

    kuufanya matokeo yake yasionyeshe dhamira na uamuzi wa wapiga kura.:adi sasa hakuna mwelekeo unaonyesha kuna ukweli katika tuhuma za

    kasoro za uchaguzi. Moja ya madai ya ++M ni kwamba eti Pemba watu

    waliopiga kura walikuwa ni zaidi ya walioandikishwa lakini ukweli ni

    kwamba takriban watu $6,''' walioandikishwa hawakupiga kura

    kisiwani humo. /atika mazungumzo yanayoendelea =kulu, #anzibar

    baina ya viongozi, ++M imetakiwa mara kadhaa kuleta ushahidi wa

    tuhuma zake kwamba kulikuwa na hujuma lakini imeshindwa kufanya

    hivyo. Matamko ya !aangalizi wa "chaguzi na namna tuhuma za

    kasoro za uchaguzi zilivyoibuliwa na Mwenyekiti wa Tume haziwezikuwashawishi wapiga kura kwamba kulikuwa na kasoro katika uchaguzi.

    :oja ya kurudiwa uchaguzi inaonekana wazi kuwa ni ajenda ya kisiasa

    ya chama kilichoshindwa. :ali hii ni sababu tosha ya kuleta fujo iwapo

    hatua yoyote ya kurudia uchaguzi itachukuliwa.

    - C($%"$ #$ K!!%$ T!4 M=/$ /$ U($"!#&

    i dhahiri kuwa uchaguzi wa #anzibar umehujumiwa na Mwenyekiti wa

    Tume kwa sababu ya sindikizo la kisiasa. /wa vyovyote vile yeye hafaitena kuendelea kuiongoza Tume hiyo katika kazi yoyote ya Tume

    iliyobaki. i lazima akae pembeni.

    /urejea uchaguzi ni sawa na kuihukumu Tume nzima kuwa ina makosa

    wakati makosa hayo yalifanywa na mtu mmoja tu. :ivyo, kwa vyovyote

    vile, kama uchaguzi utarudiwa, haitawezekana kwa Tume iliyopo na

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    20/27

    20

    ekretarieti kusimamia uchaguzi wa marudio. /ufanya hivyo ni

    mgongano mkubwa wa maamuzi kwamba Tume iliyokiri kuharibu

    uchaguzi isimamie tena uchaguzi wa marudio. :ivyo, kama Tume na

    ekretarieti itabidi iondoke na kuunda Tume na ekretarieti mpya, bado

    kutakuwa na changamoto kubwa zaidi ya kuunda Tume mpya yauchaguzi. Miongoni mwa changamoto kubwa ni kama zifuatazo2

    & uodolewa -ajumbe waliopo: kwa mujibu wa kifungu cha

    ((6)9,)

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    21/27

    21

    sababu ya 1araza kumaliza uhai wake, hawezi kutumia

    masharti ya kifungu cha 87)d kwa vile tayari ameshaondokewa

    na sifa chini ya kifungu cha 87)b ambayo ni sifa ya lazima

    chini ya kifungu cha 06)9 ya kuwa /iongozi wa hughuli za

    erikali ndani ya 1araza. :ivyo haitowezekana kuwapata!ajumbe $ wa Tume kutokana na kutokuwepo msingi halali wa

    kikatiba wa kuwapata4

    &&& !uda wa kujega uwezo wa kiutedaji a wa kitaasisi%:ata

    kama changamoto zilizotajwa hapo juu zitapatiwa ufumbuzi,

    changamoto kubwa ni ile ya muda utaohitajika kujenga uwezo

    wa kiutendaji kwa ekretarieti na wasaidizi wao katika ngazi ya

    Mikoa na !ilaya na !ajumbe wa Tume ili waweze kusimamia

    uchaguzi kwa ufanisi wa viwango vinavyokubalika.+hangamoto nyengine ni ya muda utaohitajika wa Tume

    kuhakiki na kujiridhisha na daftari la wapiga kura ambayo ndio

    nyenzo kuu ya uchaguzi. /wa vyovyote vile muda utaohitajika

    kwa Tume mpya kujiandaa hadi kufanya uchaguzi mwengine

    kwa kiwango cha chini kabisa ni angalau mwaka mmoja. uala

    muhimu ni kwamba nchi itawezaje kwenda wakati hakuna

    1araza la !awakilishi wala hakuna 1araza la Mapinduzi.

    /utokuwepo kwa 1araza la Mapinduzi kwa maana ya mawaziri

    kutaathiri sana utendaji kwa vile mawaziri wana mamlakamakubwa ya kisheria chini ya heria mbali mbali kama vile za

    fedha hivyo kutokuwepo kwao au uwepo wao usiokuwa halali

    kisheria kuna athari kubwa katika utendaji wa erikali.

    +hangamoto kubwa zaidi ni suala la bajeti ya erikali ambayo

    ni lazima iandaliwe na ipitishwe ndani ya muda maalum.

    /wa kuzingatia sababu zote hizo, ni wazi kuwa :oja ya kurudiwa uchaguzi

    haina uhalali, haina msingi na ni chachu ya kuiweka nchi katika utawala

    usiokuwa halali na kusababisha fadhaa kubwa kwa wananchi. i hoja

    ambayo inaweza kuzaa fujo na vurugu katika nchi na kupelekea mzozo

    mkubwa zaidi wa kikatiba na kisheria. idhani kama tunataka tuifikishe

    huko nchi na tuwafikishe huko wananchi tulioapa kuwatumikia na

    kuwalinda.

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    22/27

    22

    MAZUNGUMZO YANAYOWAHUSISHA WAGOMBEA URAIS

    WA CUF NA CCM PAMOJA NA MARAIS WASTAAFU WA

    ZANZIBAR

    /ufuatia jitihada kubwa nilizozifanya kwa njia ya simu na hatimaye

    kufikisha maombi yangu kwa maandishi kumtaka 5k. Ali Mohamed hein

    akutane na mimi, hatimaye alikubali na kupendekeza tuwashirikishe

    viongozi wengine wastaafu wa #anzibar.

    :adi sasa tumeshafanya vikao vinane, cha kwanza kikiwa ni kile cha tarehe

    6 ovemba, $'(%.

    !engi wenu mmehoji kwa nini nikakubali kushiriki vikao ambavyo niko

    peke yangu kutoka +"H wakati ++M wako watano. ilikubali hivyo kwakutumia msingi wa kuwashirikisha Marais wastaafu wa #anzibar lakini pia

    nikiamini kwamba tungeongozwa na busara na kuheshimu /atiba na heria

    badala ya utashi wa vyama vyetu.

    Tokea mazungumzo hayo yaanze, wananchi wengi wamekuwa wakitaka

    tuwaeleze kinachoendelea. Mimi binfasi niliamua kubaki kimya kwa

    kuheshimu msingi tuliojiwekea kwamba taarifa ya mazungumzo hayo

    itolewe kwa pamoja baada ya mazungumzo kukamilika. :ata hivyo,

    inasikitisha kuona wakati mimi nikiheshimu hilo na kuwa kimya kipindi

    chote hicho, viongozi wenzangu kutoka upande mwengine wamekuwa

    wakiliuka hilo na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikiwachanganya

    wananchi.

    /utokana na mwenendo huo, nimeona kuna haja na mimi kuwaeleza

    wananchi ukweli wa kile kinachoendelea.

    3ais -ohn Pombe Magufuli amefanya kazi kubwa ya kututia moyo ili

    tukamilishe mazungumzo hayo kwa ufanisi na kwa kuzingatia matakwa ya

    /atiba na heria. Alikutana na mimi na baadaye akakutana na 5k. Ali

    Mohamed hein. :ata hivyo, inasikitisha kwamba hata yeye 3ais Magufuli

    hakuachwa kufitinishwa na wananchi wa #anzibar pale 1alozi eif Ali =ddi

    alipodai hadharani kwamba eti Mheshimiwa 3ais wa -amhuri ya Muungano

    wa Tanzania katutaka turudi #anzibar tukakamilishe taratibu za kurudia

    uchaguzi, jambo ambalo si kweli.

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    23/27

    23

    "kweli ni kwamba katika vikao hivyo vinane bado 5k. Ali Mohamed hein

    na 1alozi eif Ali =ddi wananIganIgania kurudia uchaguzi huku wakimtetea

    kwa nguvu zote -echa alum -echa, na mimi nimesisitiza haja ya kuheshimu

    matakwa ya kikatiba na kisheria na maamuzi ya wananchi wa #anzibarwaliyoyafanya tarehe $% &ktoba, $'(% katika uchaguzi ambao waangalizi

    wote wa ndani na nje na hata Mwenyekiti wa Tume ya "chaguzi ya

    #anzibar walisema kwamba ulikuwa huru, wa haki na uliofanyika katika hali

    ya amani.

    /wa hakika hadi jana, ukiangalia tovuti ya Tume ya "chaguzi ya #anzibar

    utaona taarifa zinazosema kwamba uchaguzi hadi hatua ya kuhesabu kura

    ulifanyika kwa utulivu nchi nzima.

    /utokana na kutofikia muafaka pamoja, tulikubaliana kuandaa taarifa ya

    pamoja ambayo ilielezwa kwamba ingeandaliwa na /atibu wa vikao hivyo

    lakini sasa ni zaidi ya wiki mbili, hakuna kikao kilichoitishwa. imeandika

    barua kuhimiza kikao cha kupokea taarifa hiyo na kuipitisha lakini bado 5k.

    hein anasema wanahitaji muda.

    i wazi kwamba 5k. Ali Mohamed hein hakuwa na nia njema katika

    mazungumzo haya na amepoteza sifa ya kuongoza vikao hivyo.

    6 NJAMA ZA CHINI KWA CHINI ZA KUHUJUMU UTAFUTAJI

    WA UFUMBUZI WA HAKI

    !akati 5k. Ali Mohamed hein akikwepa kwa makusudi kuitisha kikao cha

    kupokea taarifa ya mazungumzo hayo, tumegundua kwamba lengo halisi ni

    kuisindikiza Tume ya "chaguzi ya #anzibar kutangaza tarehe ya uchaguzi

    wa marudio ili baadaye itolewe hoja kwamba suala hilo limeshaamuliwa.

    Tunazo taarifa za uhakika kwamba Tume ya "chaguzi ya #anzibar

    imetakiwa kukutana tarehe (8 -anuari, $'(9 kwa lengo la kutangaza tareheya uchaguzi wa marudio ambao unatajwa kuwa umepangwa ufanyike tarehe

    $7 Hebruari, $'(9.

    Taarifa hizo zinaeleza kwamba lengo la hatua hiyo ni kukwamisha juhudi

    zinazofanywa na 3ais wa -amhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    24/27

    24

    5k. -ohn Pombe Magufuli, za kutaka kuona ufumbuzi wa haki na

    unaozingatia matakwa ya kikatiba na kisheria unapatikana.

    Tukiruhusu hatua hiyo maana yake ni kuwaruhusu kikundi cha watuwachache wanaotumia nafasi zao kujifaidisha kibinafsi na bila ya kujali

    maslahi mapana ya nchi na watu wake na wasiojali amani na utulivu wan chi

    kututumbukiza katika balaa kubwa sana.

    :ivi tunavyozungumza wananchi wa #anzibar wako taaban na

    wamekumbwa na fadhaa baada ya kushuhudia maamuzi yao waliyoyafanya

    tarehe $% &ktoba, $'(% kupitia uchaguzi huru, wa haki na wa wazi yakiwa

    yanakanyagwa. !amesubiri kiasi cha kutosha kwa sababu sisi viongozi wao

    tunaojali amani ya nchi tumewataka wasubiri. asa umefika wakati

    uvumilivu na subira zao zinafikia kikomo. !anahitaji kuona "1=3A zao

    zinazaa :A/=.

    i vyema tukaweka wazi wazi hapa kwamba kurudiwa uchaguzi sio

    suluhisho na HAKUKUBALIKI. /wani kama nilivyoonesha, hakuna hoja

    wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi kurudiwa.

    NAMNA BORA YA KUTATUA MZOZO ULIOPO

    /utokana na maelezo ya hapo juu, ni dhahiri kwamba mzozo huu wa

    kikatiba na kisiasa ambao umetokana na hujuma zilizofanywa katika

    uchaguzi wa #anzibar haukuwa wa lazima na unaweza kutatuliwa kwa

    haraka kama utakuwepo utashi na utayari wa dhati wa kisiasa na wa

    kiuongozi ambao unazingatia maslahi mapana na endelevu ya #anzibar na

    ya -amhuri ya Muungano wa Tanzania. =li kufikia utatuzi huo wa haraka na

    unaozingatia na kuheshimu /atiba na sheria ziliopo na misingi ya utawala

    bora njia zifuatazo ndizo zitakazotukwamua hapa tulipokwama2

    ( =li kulinda misingi ya /atiba ya #anzibar inayoelekeza utaratibu waTume ya "chaguzi ya #anzibar kufanya maamuzi kama inavyoelezwa na

    kifungu cha ((6)( na )(' na ili kujenga uhalali na heshima ya Tume

    katika kutekeleza kazi zake, ni lazima Mwenyekiti wa Tume ya "chaguzi

    ya #anzibar atakiwe kukaa pembeni kwa kujiuzulu au kusimamishwa

    kazi hiyo kwa vile amefanya makosa makubwa yafuatayo2

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    25/27

    25

    a. >eye kama Mwenyekiti wa Tume hakuwa na mamlaka ya kufanya

    uamuzi kwa jambo lolote linalohusu Tume bila ya kupitia vikao

    halali vya Tume kinyume na maelekezo ya wazi ya kifungu cha

    ((6)(' cha /atiba ya #anzibar4

    b. Akiwa Mwenyekiti wa Tume ametoa Tangazo amba (0' katika

    @azeti 3asmi la erikali linalodaiwa kuwa ni uamuzi wa Tume la

    kufuta matokeo ya uchaguzi huku akijua kwamba Tume ya

    "chaguzi haikufanya kikao tarehe $7 &ktoba kupitisha uamuzi

    huo4

    c. Akiwa Mwenyekiti wa Tume ametoa tangazo la kufuta uchaguzi

    huku akijua kwamba hana mamlaka ya kufanya hivyo na akijua pia

    kwamba hata Tume ya "chaguzi haina mamlaka ya kufanya hivyo4

    d. Akiwa Mwenyekiti wa Tume amesema uongo hadharani ili

    kuhalalisha kitendo chake cha kutoa tamko la kufuta uchaguzi

    kama alivyokiri yeye mwenyewe katika kikao cha Tume cha tarehe

    ( ovemba, $'(%4

    Mambo yote haya ni ukiukaji wa /atiba, heria na Maadili ya dhamana

    aliyokabidhiwa4

    $ Tume ya "chaguzi ya #anzibar chini ya Makamu Mwenyekiti naMakamishna waliobaki wamalizie kutangaza matokeo ya "rais kwa

    majimbo 6 ambayo yalishahakikiwa na kumalizia kuhakiki matokeo ya

    "rais kwa majimbo (8 yaliyobaki na kutangaza matokeo. :atimaye

    wamtangaze mshindi wa "rais wa #anzibar. :atua hii ni halali na sahihi

    chini ya kifungu cha ((6)(' cha /atiba ya #anzibar. Aidha, chini ya

    kifungu cha 8$)9 cha heria ya "chaguzi, hatua hiyo ni halali kwa vile

    kifungu hicho kinataka matokeo ya "rais yatangazwe ndani ya siku 0

    ama ikiwa kutakuwa na matatizo basi ndani ya siku 0 baada ya matatizo

    haya kutatuliwa4

    0 /wa kuwa suala hili ni kubwa na limeathiri taswira ya nchi yetu mbele

    ya jumuiya ya kimataifa kwa kiasi kikubwa, na hasa kwa vile 3ais wa

    -amhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa 5k. -ohn Pombe

    Magufuli, wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya

    kukutana na mimi =kulu 5ar es alaam alisisitiza haja ya kukamilisha

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    26/27

    26

    mazungumzo na kulipatia ufumbuzi wa haraka, tunaona wakati umefika

    yeye mwenyewe aongoze juhudi zenye lengo la kufanikisha hatua

    zilizopendekezwa hapo juu4

    8 "ongozi wa juu wa yama vya +"H na ++M ufanye mazungumzo yaharaka ya kukamilisha taratibu za kuunda erikali ya "moja wa /itaifa

    #anzibar chini ya mshindi wa uchaguzi wa "rais wa #anzibar aliyepewa

    ridhaa na !azanzibari kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe $% &ktoba,

    $'(%. /upitia vikao hivyo, kama kuna mambo yoyote yanayohitaji

    kujadiliwa na kupata muafaka juu ya uundwaji wa erikali hiyo

    yajadiliwe na kupata muafaka4

    % Mambo yoyote yanayohitaji kurekebishwa katika mfumo wa uchaguzi

    wa #anzibar ili kuondoa kasoro ziliopo kwa nia ya kuimarisha mfumohuo kwa ajili ya chaguzi zozote za baadaye ni vyema yakawekewa muda

    maalum wa kujadiliwa na kupata muafaka.

    HITIMISHO

    #anzibar imepita katika siasa za dhoruba na machafuko kwa zaidi ya miaka %'.

    5horuba na machafuko hayo yalifikia hadi kugharimu maisha ya watu. i kwa

    sababu ya kuchoshwa na siasa za aina hiyo na migogoro isiyokwisha ndiyomaana mwaka $''6, mimi na 3ais mstaafu wa #anzibar, 5k. Amani /arume,

    tulichukua maamuzi ya kijasiri ya kuleta MARIDHIANOambayo yaliituliza

    #anzibar. /ila mmoja wetu ni shahidi kwamba kwa miaka sita iliyopita -amhuri

    ya Muungano wa Tanzania ilipumua kujibu hoja zisizokwisha kuhusu hali ya

    kisiasa #anzibar na badala yake tukawa tunapongezwa kwa kuleta maridhiano

    na kuanzisha muundo wa erikali ya "moja wa /itaifa. :atukutegemea

    kwamba baada ya kazi ile kubwa, sasa kutazuka kikundi cha viongozi

    waliopewa dhamana ya kuwaunganisha watu wafanye kazi ya kuyabomoa

    Maridhiano yetu na kuturudisha kwa nguvu kule tulikotoka. !atu hawahawapaswi kupewa nafasi kufanikisha dhamira yao hiyo ovu. a !azanzibari

    hawatowapa nafasi hiyo. i kwa sababu hiyo tumeamua kuzungumza na

    !atanzania na kuwajuvya haya ili kuzuia nchi yetu isivurugwe na kurudishwa

    tulikotoka.

  • 7/23/2019 Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016

    27/27

    27

    Tunaamini kwamba ufumbuzi wa mgogoro uliopo lazima uzingatie /atiba,

    heria na misingi ya utawala bora. Mapendekezo yaliyotolewa hapo juu ndio

    njia pekee ya kuutatua mzozo huo kwa kuzingatia misingi iliyotajwa. "tatuzi

    wowote nje ya hapo utakuwa ni wa nguvu na wa utashi wa kisiasa ambaohautaleta ufumbuzi endelevu na badala yake unaweza kuwa sababu ya mzozo

    mkubwa ambao hautaweza kutatuliwa kwa miaka mingi ijayo. Tumuombe

    Mwenyezi Mungu tusifike huko.

    Mimi na wenzangu tumefanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi wa #anzibar

    na kuwataka watoe nafasi kwa mazungumzo yanayoendelea huku

    kuwahakikishia kwamba suluhisho lolote litakalofikiwa litaheshimu maamuzi

    yao ya kidemokrasia waliyoyafanya tarehe $% &ktoba, $'(%. Tumefanya hivyo

    kwa kutambua wajibu wetu kama viongozi kuhakikisha kwamba #anzibar na-amhuri ya Muungano wa Tanzania inabaki kuwa salama. i bahati mbaya sana

    kwamba wengine wanauchukulia uungwana na ustaarabu wetu kwamba labda

    ni dalili ya udhaifu na wanadhani labda wanaweza kutuburuza. /wa hilo,

    nawaambia wazi kwamba !AA:A". ataka niwahakikishie kwamba sisi si

    dhaifu ila tunaongozwa na uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu na wananchi

    wenzetu. ?akini uzalendo huo huo na mapenzi hayo hayo kwa nchi yetu na

    wananchi wenzetu yanatutaka tusimame kuitetea na kuilinda /atiba na heria

    za nchi yetu, haki za raia na maamuzi yao ya kidemokrasia.

    #anzibar kuna tatizo kubwa ambalo halipaswi kuendelea kupuuzwa. !akati

    umefika kwa mamlaka zinazohusika kutokwepa wajibu wao kwa wananchi wa

    #anzibar.

    Mimi na wenzangu, kama viongozi twenye dhamana kwa wananchi wa

    #anzibar ambao walitupa ridhaa yao, tunawahakikishia kwamba tutakuwa

    tayari kushirikiana nao kuitetea haki yao na maamuzi yao ya kidemokrasia kwa

    nguvu zetu zote.

    awashukuru kwa uvumilivu wenu na kwa kunisikiliza.

    Ahsanteni sana.