fomu ya opras sio ya kuuza.pdf

Upload: imma

Post on 09-Mar-2016

390 views

Category:

Documents


3 download

TRANSCRIPT

  • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS

    Anwani ya simu: UTUMISHI, DSM. Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Simu Nambari: 2118531/4 Jengo la Utumishi, Nukushi: 2125299 8 Barabara ya Kivukoni Barua pepe: [email protected] S.L.P. 2483, Unapojibu tafadhali taja: 11404 DAR ES SALAAM. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

    FOMU YA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI (OPRAS) HAIUZWI

    Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inawaelekeza waajiri wote

    nchini kuhakikisha watumishi katika sehemu zao za kazi wanapata Fomu ya Wazi ya Mapitio na

    Upimaji Utendaji Kazi (OPRAS) kwa utekelezaji bila usumbufu.

    Fomu za OPRAS zinapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa

    Umma yenye anuani, www.utumishi.go.tz. Waajiri wote wanaelekezwa kutembelea tovuti hii na

    kutoa nakala za kutosha kwa idadi ya watumishi katika maeneo yao ya kazi. Kwa watumishi

    wanaoweza kutoa fomu hizi wenyewe wanaruhusiwa kufanya hivyo.

    Imebainika kuwa katika baadhi ya Taasisi za Umma watumishi wanaelekezwa kununua fomu za

    OPRAS kutoka kwa watu binafsi. Kitendo hiki ni kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na

    Taratibu zilizopo na pia ni usumbufu kwa watumishi. Fomu za OPRAS haziuzwi na watumishi

    hawatatakiwa kuzinunua. Endapo Mtumishi atashawishiwa au kulazimishwa kununua fomu za

    OPRAS atoe taarifa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ili hatua stahiki zichukuliwe. Waajiri

    wote wanakumbushwa kuwa ni wajibu wao kuwapatia watumishi walio chini yao fomu hizi na

    kuzihifadhi baada ya utekekelezaji na si vinginevyo.

    Serikali ilianzisha matumizi ya Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi

    (OPRAS) Mwezi Julai 2004, kupitia Waraka wa Utumishi Na. 2 wa mwaka 2004. Hivyo kutoka

    wakati huo, OPRAS ilifuta mfumo wa zamani wa kupima utendaji kazi wa mtumishi kwa njia ya

    siri.

    Mabadiliko ya kutathmini utendaji kazi wa Watumishi wa Umma kwa uwazi yanakwenda

    sambamba na Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1998 kama

    ilivyorekebishwa mwaka 2008 ambazo zote zinasisitiza uwekaji wa mifumo ya menejimenti ya

    utendaji bora wa kazi inayojali matokeo.

    Utekelezaji wa OPRAS katika taasisi za Umma ni hatua muhimu kwa Serikali katika kuboresha

    utendaji kazi na utoaji huduma kwa Umma. Hivyo ni wajibu wa kila mwajiri kusimamia na

    kuhakikisha kuwa watumishi wote walio chini yao wanajaza fomu hizo na kuwasilisha taarifa za

    utekelezaji katika Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora bila kukosa.

    IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI Kny: KATIBU MKUU OFISI YA RAIS-UTUMISHI

    03/02/2016