ejat 2019 yazinduliwa - mct€¦ · mct yaonya kuhusu habari za chuki wahariri watahadharishwa...

20
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 146, Oktoba, 2019 ISSN 0856-874X MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka Uk5 Uk 15 Uk 9 EJAT 2019 Yazinduliwa

Upload: others

Post on 19-Oct-2020

5 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 146, Oktoba, 2019ISSN 0856-874X

MCT yaonya kuhusu habari za chuki

Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha

Uvumi ushughulikiwe haraka

Uk5 Uk 15Uk 9

EJAT 2019 Yazinduliwa

Page 2: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Uangalifu na Uvumilivu upewe kipaumbele Uangalifu na uvumilivu ni muhimu yakawa maneno

muhimu katika kipindi hiki ambapo taifa linaelekea katika chaguzi – uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 na ule wa Uchaguzi

Mkuu mwakani. Hiki ni kipindi muhimu na kama uangalifu na

uvumilivu havitapewa kipaumbele, nchi yetu inaweza kuingia katika hali inayoweza kusababisha kujiangamiza.

Ni muhimu katika kipindi hiki vyombo vya habari vikawa makini na vinachochapisha na vikae mbali na kauli za uchochezi – ziwe zimetolewa na wanasiasa , viongozi wa dini ama wa kijamii ama wapambe wao.

Hii ndiyo sababu kubwa kwanini neno uangalifu ni muhimu na lizingatiwe kwa ukaribu mno.

Tunasema haya kwa kuwa vipo vyombo vya habari - magazeti pamoja na vya mtandaoni, ambavyo vimepachikwa jina la kuwa vyombo vya habari vya ‘kimkakati’ ambavyo tunashuhudia aina ya uandishi wake ambao haujawahi kuonekana hapa nchini..

Ni uandishi mbaya kwa kuwa lugha chafu na uongo zinatumika na vyombo hivyo ambavyo vinalenga kuchafua watu mashuhuri na walio kwenye upinzani.

Kama uandishi wa aina hii utaruhusiwa kuendelea na vyombo vingine zaidi vikauendeleza, tutalipua moto wa kisiasa na kijamii ambao utakuwa vigumu kuuzima.

Ni muhimu tukajifunza katika nchi kama Somali ambayo haitawaliki kwa miongo kadhaa sasa na pia uzoefu wa Kenya na Rwanda nao si mzuri hata kidogo.

Lazima tuchukulie kwa makini na umuhimu mkubwa kwamba kutangaza na kuhubiri chuki ni mambo ya mwisho kabisa Watanzania wayahimize, kwani nchi yetu imekuwa ikitambulika kuwa kisiwa cha amani.

Vyombo vya habari lazima vikatae kutumiwa kusambaza chuki kama Baraza la Habari Tanzania lilivvoeleza kwa usahihi katika mwito wake wa hivi karibuni.

Kuhusu uvumilivu, walio kwenye ngazi za juu za madaraka wakubali maoni mengine kama hatua ya afya kwa maendeleo ya nchi yetu.

Kwa kuwa nchi hii ina mfumo wa siasa wa vyama vingi, wanasiasa wa pande zote wawe na nafasi ya kufanyakazi, kuwe na uwanda sawa wa kufanyakazi kwao pamoja na vyombo vya habari na tunasisitiza wenye madaraka wavumilie hoja mbadala kwani ni kawaida ya binadamu kuwa maoni hayawezi kuwa sawa.!

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT), Kajubi Mukajanga ( wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Mfuko wa Maendeleo ya Ubunifu (HDIF), Hannah Mwandoloma (kushoto) ,Mwenyekiti wa Umoja wa Hedhi Salama , Wilhlmina Malima (kulia)na Meneja wa Programu wa MCT, David Mbulumi (wa pili kutoka kulia) wakionyesha fomu za kuwania tuzo hizo wakati wa uzinduzi wa EJAT.

Page 3: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

3

Habari

Toleo la 146, Oktoba, 2019

Na Mwandishi wa Barazani

Ni msimu mwingine wa mash-indano ya kipekee na makubwa kwa wanahabari yanayokwenda kwa jina la

Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT).

Wanahabari watakaoandika kazi zitakazoonekana kuwa bora wataibuka washindi ama wateule.

EJAT 2019 ilizinduliwa na Mwenyekiti wa Maandalizi hayo Kajubi Mukajanga, akiwa pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Mfuko wa Ubunifu (HDIF), Hannah Mwandoloma , mwenyekiti wa Hedhi Salama Wilhlmina Malima na Meneja Programu wa MCT, David Mbulumi kwa kufungua bahasha kubwa zilizokuwa na fomu za kuwasilisha kazi mbele ya wanahabari Oktoba 11, 2019.

Uzinduzi huo uliashiria kuanza kwa mashindano ya waandishi nchini kote kuwasilisha fomu za kuwania Tuzo kuanzia Oktoba 11, 2019. Siku ya mwisho ya kuwasilisha kazi hizo ni Januari 31, 2020.

Tuzo hizo zimekuza wanahabari kutoka katika vyombo vikubwa vya habari na hata kutoka vyombo vidogo kama vya kijamii, Mukajanga alisema wakati wa uzinduzi huo.

Tuzo hizo pia zimewakuza

wanahabari wanawake ambapo kwa miaka mitatu mfululizo wanawake kutoka vyombo vikubwa vya habari viwili na mmoja kutoka redio za jamii wameibuka washindi wa jumla wa Tuzo hizo.

Florence Majani wa Mwananchi alikuwa mwanamke wa kwanza kuibuka mshindi wa jumla na kuvunja umaarufu wa wanaume katika Tuzo hizo 2016 akifuatiwa na Vivian Pyuza wa CG FM mwaka 2017 na mwaka 2018 ilikuwa zamu ya Salome Kitomari wa Nipashe.

Kwa miaka 10 iliyopita mamia ya wanahabari ama wameshinda Tuzo hizo ama wamekuwa washindi wa pili na wa tatu.

Mwaka huu , mashindano hayo yatakuwa na makundi 20 ambapo matatu ni mapya.

HDIF inadhamini kundi la Ubunifu Maendelo ya Binadamu ambapo Hedhi Salama wanadhamini kundi la Hedhi Salama.

Kundi la Afya ya Uzazi linadhaminiwa na Marie Stopes, Umati na Pathfinder.

Makundi mengine ni Biashara na Fedha, Utamaduni na Michezo, Kilimo na Biashara ya Kilimo, Utalii na Uhifadhi, Elimu, Uandishi wa Habari za Uchunguzi, Uandishi wa Habari za Data, Utawala Bora, Mpiga Picha Bora , Mpiga Video Bora, Mchora Vibonzo

Bora, Uandishi wa Jinsia, , Mafuta, Gesi na Usimamizi wa Madini, Usalama wa Barabara na kundi la wazi.

Mashindano ya mwaka huu ni ya 11 ambapo washirika wanayoyasimamia ni Baraza la Habari Tanzania, Wakfu wa Habari (TMF) Taasisi ya habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA_Tan), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), HakiElimu, AMREF, SIKIKA, Agriculture Non-State Actors Forum (ANSAF), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Mukajanga alisema pia katika uzinduzi wa EJAT kuwa mwaka huu Tuzo ya Mafanikio ya Maisha ya Uandishi wa Habari (LAJA) itatolewa.

Wanaowania Tuzo hii ni wenye rekodi ya umahiri wa uandishi wa habari na kuunga mkono taaluma na kuwa na ari na dhamira kutetea uhuru wa habari .

Hakuna kazi inayotumwa kuwania Tuzo hiyo ambayo inaweza kutolewa kw amtu aliye hai ama aliyefariki ama mstaafu.

Waliotunikiwa Tuzo hiyo huko nyuma ni Fili Karashani (2011), Hamza Kasongo (2012), Mariam Mohamed Hamdan (2013), Jenerali Ulimwengu (2014) na Rose Haji Mwalimu (2015).

EJAT 2019 yazinduliwa kwa staili Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT), Kajubi Mukajanga, akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo.

l Tarehe ya mwisho kuwasilisha kazi za kushindanisha Januari 31, 2020

Page 4: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

4

Utaratibu

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

16

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Baraza la Habari Tanzania ni chombo huru kilichoundwa na wadau wa vyombo vya habari kusimamia weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Je! Una malalamiko juu ya habari au makala iliyotoka gazetini au kipindi chochote kilichorushwa hewani na radio au luninga?

Kama una malalamiko, basi wasiliana na mhariri wa gazeti au chombo husika cha habari. Ikiwa hutaridhika na hatua za chombo hicho cha habari, basi peleka malalamiko yako Baraza la Habari Tanzania. Baraza litashughulikia shauri lako haraka kwa misingi ya maridhiano na uungwana.

Jinsi ya kupeleka shauri katika Baraza• Kabla ya kuleta shauri katika Baraza dhidi ya chombo cha habari chochote au

mwandishi wa habari yeyote, mlalamikaji ajiridhishe kuwa juhudi za kuleta maelewano na kupata upatanishi kati yake na walalamikiwa zimeshindikana.

• Mlalamikaji anapaswa kuhakikisha kwamba wakati malalamiko yanaletwa kwenye Baraza habari zinazolalamikiwa hazikuchapishwa au kutangazwa zaidi ya wiki 12 zilizopita.

• Malalamiko yoyote yaletwayo kwenye Baraza sharti yawe katika maandishi na yaonyeshe tarehe, jina la chombo cha habari kilichochapisha au kutangaza habari zinazolalamikiwa. Baraza linaweza kukiamuru chombo cha habari au gazeti kumuomba radhi mlalamikaji na, au kumpa nafasi ya kujibu, au kutoa amri yoyote itakayoona inafaa na ambayo ipo ndani ya mamlaka yake.

• Iwapo mlalamikaji hataridhika na uamuzi wa Baraza anaweza kutafuta njia nyingine za kutatua shauri lake ikiwemo kulipeleka mahakamani. Hata hivyo, hatatumia uamuzi wa Baraza kama ushahidi Mahakamani. Hata hivyo, Mahakama inaweza kulialika Baraza wakati wowote kama “rafiki wa mahakama” (Amicus Curiae’) pale itakapohitaji ushauri wa kitaalamu kuhusu mambo ya habari.

Kwa mawasiliano na Baraza:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzania,Josam House, Kitalu B, Ghorofa ya Kwanza, Upande B, S.L.P 10160, Simu+255 22 2775728/ +255 22 2771947,Nukushi +255 22 2700370, Simu ya Kiganjani +255 732 998310Barua Pepe: [email protected]: mct.or.tz

BARAZA LA HABARI TANZANIA

Page 5: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetahadharisha vi-kali vyombo vya habari kutu-mika kueneza chuki, uongo

na kutumia lugha isiyo na staha. Katika taarifa kali iliyotolewa na

Baraza Oktoba 23 na kusainiwa na Katibu Mtendaji wake Kajubi Mukajanga, Baraza limekumbusha vyombo vya habari kuzingatia maadili na weledi vinaporipoti kauli ama zimetolewa na viongozi wa kisiasa, kidini ama na wapambe wao na kwamba visitumike kuwa vipaza sauti za kauli za chuki.

Baraza limeonya vyombo vya habari vinavyojulikana kuwa ni vya ‘kimkakati’ ambavyo vinalenga zaidi kutoa habari zisizo za kweli ambazo zinajenga chuki nchini.

Vimekuwa vikitumia lugha ya matusi kinyume na utamaduni wa nchini na matakwa ya kitaaluma bila kujali matokeo hasi ya muda mfupi na mrefu wa uandishi wa aina hiyo. Baraza limeonya kuwa kama tatizo hili halitashughulikiwa linaweza kusababisha uhasama mkubwa kati ya viongozi na wananchi, vyama vya siasa, wanachama wa vyama vya siasa ama makundi mbalimbali ya kijamii kama ilivyowahi kutokea katika nchi za Kenya na Rwanda.

MCT imeowaonya wahariri wasiingie katika mtego wa kuwa wasambazaji wa kauli na taarifa za chuki ambazo wenyewe hawawezi kuthibitisha kuwa kweli.

“Taarifa za chuki ziripotiwe kwa uangalifu na kuepuka kuzikuza kuhofia matokeo ya kauli kama hizo”,

MCT ilionya katika taarifa yake. Baraza limekumbusha wahariri kuwa sio kazi ya vyombo vya habari kutoa taarifa zisizo za ukweli ama kuwachafua watu na badala yake vyombo vya habari vizingatie maadili na kudhibiti madhara ya habari kabla ya kumfikia msomaji ama msikilizaji.

Ikielezea Kanuni ya Maadili ya

Taaluma ya Habari

ya mwaka 2016

iliyoandaliwa na Baraza, kauli za chuki

ni shambulio kwa mtu ama kundi kwa

misingi ya rangi, dini, itikadi na muonekano ikiwa

pamoja na maumbile na utaifa na uwezo

wa kuchochea chuki, kutoelewana na ghasia.

Pia ni mawasiliano yanayolenga kudhalilisha hadhi,

kuchochea ghasia ama kumshughulikia mtu

mwingine kwa misingi ya rangi, kabila, utaifa, dini, jinsia ama udhaifu

mwingine wowote.“Tunalaani hii hasa

wakati huu wakati taifa linaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa

mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani”, MCT imesisitiza katika taarifa

yake.Vyombo vya habari vya Tanzania,

imeeleza taarifa hiyo vijiepushe kushiriki katika kampeni yoyote ya kusambaza uongo, matusi, vitisho na chuki.

5

Habari

Toleo la 146, Oktoba, 2019

MCT yaonya vyombo vya habari kueneza chuki

Gazeti la Jamvi la Habari - uandishi aina huu unaweza kujenga chuki

miongoni mwa jamii.

Page 6: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

6

Fursa

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

This is an opportunity provided by the Sport and Society programme: Find out more

With revelations about FIFA, the IAAF and other sporting bodies‎ hitting the headlines regularly, the world is now turning a critical eye to how sport is governed.

But the governance of sport is not just about the huge, global bodies that have been the focus of so much attention. Within every country and at every level, sport must be governed. Sometimes it is run as a business, at other times it is state funded – but it should always have effective oversight. Strong, insightful media coverage is a vital part of this.The Thomson Reuters Foundation's programme for journalists in Africa who want to report on how sport is run in their own country or wider region.

Participating journalists will work on a specific story idea and develop this during an intensive workshop in Nairobi. The workshop will also cover investigative techniques, storytelling approaches, and more. They will then receive editorial guidance and mentoring support to help them make their story solid and engaging.Participating journalists will also be eligible to apply for modest funding to help cover the costs of reporting their story.

ELIGIBILITYJournalists with a proven interest in how sport is run. You do not need to be a sports correspondent – we are also interested to hear from business reporters and investigative journalists for example.Journalists must be based in an African country and working for a domestic media outlet.Journalists working in any medium may apply – print, radio, TV, online

FUNDINGWe will cover all transport and subsistence costs of journalists participating in this programme.

SUBMISSIONSYou can apply using the application form below. You will be asked to upload

2 work samples (maximum file size 5 MB) A letter from your editor consenting to your participation in the programme and committing to publish/broadcast resulting storiesYou will also be asked to provide a story idea. This might be an investigation, a feature, or a series of stories. While we welcome ideas for investigations, your idea does not need to be investigative, provided it is giving fresh insight on the topic chosen.

INVESTIGATIVE SPORTS REPORTINGDates: 16 December 20 December | Location: Nairobi, Kenya

Application deadline: 28 October | Programme: Sport and Society

Page 7: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Waandishi wa habari wan-awake wanapuuzwa ka-tika vyombo vya habari kwa kuwa na fursa

chache za kuendelea? Matatizo yao yanakuzwa kutokana na kunyan-yaswa kijinsia, kimwili na kutakiwa kingono.

Utafiti kuhusu Wanawake katika vyumba vya habari Tanzania uliofanyika katika vyombo vya habari zaidi ya 20 na kujumuisha waandishi wa habari wanawake 40 unaelekea kuthibitisha unyanyasaji wa wanawake. Wanawake waliohojiwa walitoka kwenye magazeti, redio, runinga na vyombo vya habari vya mtandaoni.

Utafiti huo ulifanyika kati ya Juni na Agosti 2019 katika vyombo vya habari 23 – Redio, Runinga na Magazeti Bara na Visiwani.

Taarifa zilizotakiwa katika utafiti huo zilikuwa ni pamoja na uendeshaji wa habari, nafasi kazini, mishahara, ajira na sera za kupanda

vyeo, mafunzo, upangaji wa utafutaji habari na masuala kadhaa yanayohusu waandishi wa habari wanawake kwenye vyumba vya habari.

Pili Mtambalike, Mtafiti kiongozi katika utafiti huo alisema wakati wa uchambuzi wa utafiti huo kwamba walipata matatizo kadhaa katika vyombo vya habari kwa kuwa idadi yake iliongezeka kutoka vyombo vitano vya awali vya Visiwani na tisa vya Bara hadi vyombo 30, lakini ukafanyika kwa vyombo 23.

Alisema licha ya kuongezeka kwa idadi ya vyombo, ni vichache tu, hasa runinga Bara vilijibu. Mtafiti mwingine ni Hawra Shamte kutoka Zanzibar.

Ikitoa mfano wa Shirika la Utangazaji Zanzibar, ripoti hiyo imeeleza kuwa ingawa shirika hilo lina vyombo – ZBC Radio, ZBC Television na Spice FM lilitoa maelezo ya jumla badala ya chombo kimoja kimoja.

Tatizo lingine ambalo uchunguzi huo ulikabiliana nalo ni baadhi ya wahojiwa hawakujibu maswali yote

yaliyohitaji ufafanuzi ama masuala ya kufuatilia. Kwa mfano kama mwanamke amejibu ‘ndiyo’ kama amebaguliwa ama kunynaswa kigono, baadhi yao hawajibu suala linalofuata kuhusu nani mhusika ama nani wahusika na hatua gani zimechukuliwa baada ya kuripotiwa tukio hilo..

Mambo Muhimu ya utafiti huo ni kama ifuatavyo:

• Wanawake wanashikilia ngazi za chini na za kati katika vyumba vya habari na inakuwa vigumu kufikia ngazi za kufanya maamuzi, hata kama wako vizuri kielimu na wana uzoefu kuliko wenzao wanaume.

• W anawake bado wanapangiwa kuripoti habari nyepesi kama vile burudani, masuala ya familia na afya kuliko wanaume ambao wanapangiwa kazi kama vile siasa za ngazi za juu, uchumi, habari za uchunguzi na maeneo nyeti.

• Wanawake katika vyumba vya habari wanabaguliwa katika kupanda vyeo na wanaweza kulipwa

7

Habari

Toleo la 146, Oktoba, 2019

Utafiti walenga kuboresha wanahabari wanawake

Endelea Ukurasa wa 8

Washiriki wa kikao cha upitiaji wa Utafiti kuhusu Wanawake katika Vyumba vya Habari Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.

Page 8: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

kiwango cha chini kuliko wanaume wenye sifa sawa ama hata chini na uzoefu.

• Wanawake kwenye vyuma vya habari wanakabiliwa na unyanyasaji wa kingono na ghasia za kijinsia ambazo zinaathiri hata maendeleo yao kitaaluma.

• Majukumu ya kiasili ya wanawake na majukumu ya nyumbani yanapunguza fursa zao kushiriki katika kazi zenye changamoto na inawakwaza mno katika maendeleo yao kitaaluma.

• Kutojiamini kunakwaza wanahabari wanawake kupata mafanikio.

• Kuna wanahabari wachache wanawake katika vyumba vya habari kulinganisha na idadi ya wanawake wanaohitimu kutoka vyuoni.

• Wasiwasi wa hatari kunakwaza fursa za kujikuza.

• Vyombo vingi vya habari havina sera ya jinsia na hata vile ambavyo vinayo sera hiyo hawaitumii.

Utafiti unajumuisha mifano halisi iliyoelezwa na wanawake wanahabari ikiwamo pamoja na kutopandishwa cheo kwa miaka kadhaa, mishahara ya chini kulingana na wenzao wanaume ambao wakati mwingine wako chini yao kwa sifa. Pia kuna suala ka unyanyasaji wa kingono.

Majadiliano katika uchambuzi Katika uchunguzi huo

uliodhaminiwa na Shirika la Maendeleo ya Vyombo vya Habari la Finland (VIKES), ilielezwa kuwa wanawake wanaweza kuwa na majukumu makubwa katika vyombo vya habari ikiwa wataendelezwa na wakipewa fursa nzuri.

Juhudi zichukuliwe na vyama husika vya habari, hasa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania kuhimiza wanahabari wanawake kufanya juhudi kujiinua kielemu.

“Hali sasa ni mbaya kutokana na wanawake wengi wanahabari kuwa na kiwango cha chini cha elimu ”, Mtambalike alisema wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo.

Unyanyasaji wa kingono ni kikwazo kingine kwa maendeleo ya wanahabari wa kike. Ilidaiwa kuwa baadhi ya wahariri wanadai kuwa na mahusiano ya kingono kabla ya kuruhusu habari ichapishwe na hata kuwapangia kazi wanahabari hao wa kike.

Wanawake wanaokataa mara nyingi huachwa hawapangiwi kazi na wanaishia kutokuwa na habari zilizochapishwa ama kutangazwa.

Waandishi wanawake pia hupata matatizo ya kushawishika kuwa washirika kingono na watoa habari.

Ilidaiwa katika mkutano wa mapitio ya ripoti hiyo ya utafiti kuwa wanahabari wa kike hawalazimiki kukubali kudhalilishwa ama kunyanyaswa kwa kuwa makini, wenye msimamo na kuandika habari ambazo hakuna mhariri atakayediriki kuacha kuzitumia.

Mtazamo huo wa wahariri wa kiume kunyanyasa wanawake ulipingwa kwa maelezo kuwa baadhi ya wanahabari wanawake wanapendelea zaidi kufanyakazi na

wahariri wa kiume kuliko wanawake wenzao. Ushauri ukatolewa nalo hili lichunguzwe.

Suala la mavazi nalo lilizungumzwa na ilielezwa kuwa baadhi ya nguo zinasisimua kingono na hivyo kuweza kushawishi matendo yanayopingwa.

Hata hivyo pamoja na ripoti kuonyesha hali mbaya ya wanawake katika vyumba vya habari, ilielezwa kuwa wanawake wamepiga hatua katika vyombo vya habari.

Kwa mfano ilielezwa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu - 2016, 2017 na 2018, waashindi wa jumla wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) walikuwa wanawake. Hata Washindi wa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha katika uandishi wa habari, kati ya watano waliopata Tuzo hiyo, wawili ni wanawake.

Michango iliyotolewa wakati wa majadiliano hayo yatajumuishwa kwenye ripoti ya mwisho, alifahamisha Pili Mtambalike.

Taarifa zilizokusanywa katika utafiti huo ni pamoja na za uendeshaji wa habari kwa kuangalia uwiano wa wanawake na wanaume - kwa mishahara, vyeo, kupandishwa ngazi, sera na taratibu mbalimbali za kikazi.

MapendekezoMapendekezo ya utafiti huo

yanahusu ngazi ya kitaifa na

8

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Endelea Ukurasa wa 10

Inatoka Ukurasa wa 7

Utafiti walenga kuboresha wanahabari wanawake

Mtafiti kiongozi wa Utafiti kuhusu Wanawake katika Vyumba vya Habari Tanzania, Pili Mtambalike, akizungumza wakati wa mkutano wa kupitia wa utafiti huo.

Page 9: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani,

Wahariri na waandishi wa habari wametakiwa kuchukua tahadhari katika matumizi ya picha za watu binafsi.

Akizungumza wakati wa usuluhishi wa malalamiko dhidi ya gazeti la Mtanzania lililotumia picha ya mkazi mmoja wa Dar e s Salaam bila idhini yake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania, Jaji mstaafu Juxon Mlay amesema picha za aina hiyo zitumike zikiwa na maelezo yanayojitosheleza.

Maria Agostino Eliasi, Mkazi wa Magomeni Kagera ambaye shughuli zake ni mama lishe, aliwasilisha malaamiko MCT, baada ya kupigwa picha akiwa amebeba watoto wake wawili na maelezo yakiwa “Kulea ni kazi”.

Aliiambia kamati hiyo kuwa baada ya kutoka tu picha ile, alipata usumbufu mkubwa na kudhalilika jinsi. baadhi ya watu wake wa karibu walivyozungumzia picha hiyo.

Wengine alisema walimuona kuwa amezidiwa kimaisha na alikuwa anatafuta msaada hali ambayo kwake si

ya halisia.Alisema kuwa alikuwa anajitegemea

na kuendelea na maisha na wanawe bila shida.

Mhariri wa gazeti hilo Kulwa Karedia alijitetea kuwa matumizi ya picha hiyo yalilenga kuonyesha adha wanazopata akina mama katika kulea watoto.

Alisema aliona kuwa badala ya gazeti

kulaumiwa, lingesifiwa.Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Jaji

mstaafu Mlay alisema matumizi ya picha hiyo yanakinzana na kanuni za maadili zilizoandaliwa na Baraza la Habari .

Alisema kanuni hizo zinatahadharisha kuhusu faragha na kwamba picha aina hiyo kabla ya kutumika ingepatikana ridhaa ya aliyepigwa picha.

Mbaya zaidi picha hiyo imewaonyesha watoto ambao nao kutumika kwao kunalindwa na kanuni hizo za maadili.

Katika uamuzi wa shauri hilo, kamati iliamuru gazeti la Mtanzania kuomba radhi na kumlipa mlalamikaji gharama za kushughulikia shauri hilo.

Wakati huo huo katika shauri jingine, gazeti la Tanzania Daima limeagizwa kutoa fursa kwa uongozi wa Parokia ya Mikaeli Kawe kuzungumza nao na kuandika kwa usahihi masuala yatakayozungumzwa katika mahojiano hayo.

Pamoja na kuandika mahojiano hayo gazeti hilo limetakiwa kuomba radhi kutokana na habari ambayo uongozi huo wa Parokia umeona umechafuliwa.

Mahojiano kati ya gazeti hilo na uongzi huo wa parokia utakaojumuisha waumini wawili yatafanyika Ijumaa Novemba 1, na habari yake itachapishwa gazeti la Jumapili Novemba 3, 2019.

Katika shauri hilo gazeti la Tanzania Daima liliwakilishwa na Mhariri wake, Martin Malera ambapo uongozi wa Parokia uliwakilishwa na Charles Lupiliya ambaye ni Mwenyekiti wa Walei wa Parokia hiyo.

Paroko wa Parokia, Nicholas Kundy hiyo akiwa na viongozi wengine wa Paroko hiyo pia walihuruidhuria kikao hicho cha usuluhishi.

Shauri hilo awali lilisuluhishwa katika ngazi ya Sekretariati lakini uongozi wa Parokia ya Kawe haukuridhika na utekelezaji wa gazeti hilo na hivyo Baraza kulazimika kuitisha kikao kamili cha Kamati ya Maadili.

9

Toleo la 146, Oktoba, 2019

Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha

Habari

Maria Agostino (kushoto) akipena mkono na Mhariri wa gazeti la Mtanzania, Kulwa Karedia baada ya usuluhishi wa shauri lao na Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari (MCT) chini ya Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Juxon Mlay (wa pili kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Edda Sanga (katikati).

Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, Martin Malera (kulia) akipeana mkono na Paroko wa Parokia ya Mikaeli ya Kawe, Nicholas Kundi. Katikati ni Mwenyekiti wa Kama ya Maadili ya Baraza ha Habari, Jaji mstaafu Juxon Mlay.

Page 10: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

10

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

majukumu ya serikali na vyombo vingine vya usimamizi na katika vyombo vya habari na wanahabari wenyewe mmoja mmoja.

Kwa serikali imehimizwa isiache jukumu lake la kutoa sera na miongozo kukabili matatizo ya vyombo vya habari yanayowakabili wanahabari wanawake kwa kuimarisha sera ya sasa ya habari na utangazaji ya mwaka 2003. Ikumbukwe kwamba katika kuandaa sera hiyo serikali ilijumuisha mapendekezo yote ya wadau wa habari na kuacha matatu tu - moja likiwa kuhusu serikali kumiliki vyombo vya habari, suala la umiliki wa vyombo mbalimbali na suala la jinsia.

Vyombo vya habari vihitajike kwa sera na sheria kuhakikisha vinashughulikia masuala yote, kama tofauti za mishahara, unyanyasaji wa kingono na ubaguzi dhidi ya wanawake katika utoaji maamuzi. Hii inaweza kufanyika kwa

kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia ni sehemu muhimu ya kupata leseni ya kuendesha chombo cha habari.

Sera ya JinsiaVyombo vya habari vilazimike

kuwa na sera ya jinsia na kuzitumia. MCT na TAMWA watoe mwongozo na kusaidia vyombo vya habari kutayarisha sera hizo za jinsia ambazo zitalinda wafanyakazi na kuhakikisha kuwepo usawa.

Sera ya jinsia itasaidia kuondoa tatizo la mabosi kuomba ngono kwa wanahabari wanawake walio ngazi za chini. Sera hiyo lazima iweke utaratibu wa kuripoti unyanyasaji wa kingono na kuweka taratibu za nidhamu dhidi ya wahusika. Sera hiyo pia ni muhimu kuwezesha vyombo vya habari kufuatilia maendeleo ya wanahabari wa kike na kuondoa hali ya sasa.

Waandishi wanawake mmoja mmoja

Kwa wanahabari wanawake mmoja

mmoja mapendekezo yanaelekeza wanaweza kuboresha hali zao kwenye vyumba vya habari kwa kuwa na msimamo na kukataa kuwa wahanga wa unyasasaji wa kingono. Wanaweza kusaidia kufichua masuala hasi mbalimbali katika sehemu zao za kazi ikiwemo ubaguzi wa mapato, vyeo na hata kupangiwa kazi. Chama kihamasishe na kutetea nafasi na haki za wanawake katika vyumba vya habari.

Wajibu wa MCT na mashirika mengine ya habari

Mashirika ya habari kama Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na TAMWA wana dhima kubwa ya kuimarisha usawa wa jinsia katika vyumba vya habari. Kukosekana kwa chama imara cha Wafanyakazi waandishi wa Habari cha kutetea haki zao ni kikwazo kikubwa katika kupigania haki za waandishi. Ni muhimu kwa wanahabari kuungana kutetea na kulinda haki zao.

Utafiti walenga kuboresha wanahabari wanawake Inatoka Ukurasa wa 8

Mshauri wa masuala ya habari, Dk. Joyce Bazira, akizungumza wakati wa upitiaji wa ripoti ya utafiti kuhusu Wanawake kwenye Vyumba vya Habari nchini Tanzania. Kulia ni Maimuna Msangi wa Pangani FM na Najjjat Omar CG FM Tabora.

Page 11: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Sera ya jinsia katika vyombo vya habari itakayosimamia taratibu na uendeshaji vyombo vya habari,

wanahabari, wamiliki wa vyombo vya habari, wachapishaji na na hata vyombo vya mitandaoni nchini Tanzania inaandaliwa.

Sera hiyo inayolenga zaidi Wanachama wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) inalenga kuweka mazingira mazuri na salama ya kufanyakazi katika vyombo vya habari.

Miongoni mwa malengo ambayo sera hiyo inalenga kudhibiti ni unyanyasaji wa kijinsia kwa kuanzisha taratibu za malalamiko, kutoa mafunzo, kushughulikia madai ya wanawake kwenye vyombo vya habari na vikwazo vya kimila na fursa sawa.

Sera hiyo inayopendekezwa inavitaka vyombo vya habari kutoa fursa sawa kwa wanawake na wanaume katika kufuatilia na kuandika habari za kisiasa,

kiuchumi ama vita na kwamba sauti za wanawake lazima zisikike.

Vyombo vya habari lazima vichukue hatua madhubuti za kupata maoni ya wanawake na wanaume bila kujali nyadhifa na nafasi zao katika jamii.

Upendeleo unapingwa kabisa kwa kuwa vyombo vya habari vinatakiwa kutopendelea upande wowote na kujiepusha na matamshi na misimamo ama taasisi.

Kwa upande wake, MCT itaongeza programu za jinsia na kuwezesha wanawake wengi zaidi kushiriki katika uandaaji wa programu hizo.

MCT itatumia uwezo wake kama chombo cha kujisimamia kushirikiana na taasisi za mafunzo kujumuisha mafunzo ya jinsia katika mitaala yao.

Sera hiyo ya jinsia inayopendekezwa inajumuisha masuala kama uwajibikaji, uwiano na kutotegemea upande wowote, kudhibiti madhara, , lugha, masoko, matangazo na usalama.

Ni muhimu, kulingana na sera ya Raslimali watu inayozingatia

jinsia, kuhakikisha kuwepo usawa katika ajira na taratibu za uteuzi kuhakikisha uwakilishi sawia wa wanawake katika ngazi zote za maamuzi.

Kuendeleza watumishi ni suala lingine muhimu linalosisitizwa katika mipango ya wafanyakazi katika vyombo vya habari ambapo ni muhimu vihakikishe wafanyakazi wanapata nafasi za mafunzo ambayo ni kwa ajili ya wote -wanawake na wanaume, mkazo zaidi ukiwa kwa wanawake.

Aidha miongozo kuhusu unyanyasaji kijinsia lazima uwepo kuondoa unyanyasaji kazini na umwamba. Umuhimu wa vyombo vya habari kuwa na sera ya jinsia ulielezwa pia katika utafiti kuhusu wanawake katika vyombo vya habari. Utafiti huo ulifanyika Tanzania Bara na Zanzibar ambapo zaidi ya vyombo vya habari 20 vilihusika na wanahabari wanawake 40 walishiriki.

Utafiti huo uliofanyika kwa uangalizi wa MCT ulidhaminiwa na Shirika la Maendeleo ya Vyombo vya habari la Finland – VIKES.

11

Habari

Toleo la 146, Oktoba, 2019

Sera ya Jinsia kwa vyombo vya habari yaandaliwa

Waandishi wakiwa kwenye mojawapo ya vyumba vya habari nchini.

Page 12: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

12

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Kitabu

Kitabu hiki ni muhimu na cha lazima kwa waandishi wa habari na wahariri kukisoma ili kuelewa takwimu na jinsi ya kuzitumia kwa usahihi katika habari

Page 13: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Kwa miaka mitatu mfululizo, wanawake watatu wamefanya mabadiliko kwa kuibuka

washindi wa jumla katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT).

Waliwashinda wanaume na kutwaa ushindi wa juu wa Tuzo hizo ambazo lengo lake ni kutambua wanahabari kwa kufanya kazi nzuri.

Tangu 2009, Tuzo hizo zilipoanza washindi wa jumla walikuwa wanaume, ingawa kiukweli walikuwa wanawasilisha kazi nyingi zaidi za kushindanisha

kuliko wanawake. Florence Majani wa gazeti la

Mwananchi alikuwa wa kwanza kuibuka mshindi wa jumla mwaka 2016.

Alishindwa kujizuia baada ya jina lake lilipotajwa na mgeni rasmi wa Tuzo kwa mwaka huo, mwanahabari veterani na mshindi wa Tuzo ya Maisha ya uandishi wa Habari, Jenerali Ulimwengu.

Ilimchukua muda kujiweka sawa kukubali ukweli kuwa ameweka historia kwa kuibuka mshindi wa jumla wa Tuzo za EJAT.

Haikuwa kazi rahisi kwa Majani. Alishinda Tuzo yake ya

kwanza ya EJAT mwaka 2010 lakini mwaka uliofuata aliteuliwa tu lakini hakushinda. Hiyo haikumkatisha tamaa kwani mwaka 2012 aliibuka mshindi katika makundi mawili – Kuripoti watu wenye ulemavu na Sayansi na Teknolojia.

Kwa ushindi huo yeye na mfanyakazi mwenzake wa kampuni hiyo ya Mwananchi Communications anayeandikia gazeti la The Citizen, Lucas Liganga walifadhiliwa na iliyokuwa Mfuko wa Vyombo vya Habari kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa habari za uchunguzi Rio de Janeiro, Brazil.

13

Toleo la 146, Oktoba, 2019

Habari

Wanawake watatu walioibuka washindi wa jumla mfululizo EJAT

Endelea Ukurasa wa 14

Washindi wawili wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2016 Florence Majani na Vivian Pyuza wa EJAT 2017.

Page 14: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

14

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Wanawake watatu walioibuka washindi wa jumla mfululizo EJAT

Mwaka 2013 hakushinda lakini alikuwa mteule. Mwaja 2014 alishinda katika makundi mawili - Kuripoti watu Wenye Ulemavu na Afya ya Uzazi na mwaka 2015 alishinda tena katika makundi mawili - Kuripoti watu wenye ulemavu na Afya ya mama na Mtoto.

Mwaka 2016,akaibuka mshindi wa jumla – alishinda katika Michezo na Utamaduni na Utawala Bora. Katika kinyang’anyiro cha ushindi wa jumla aliwashinda - Peninah Kajura wa HHC Radio, Projestus Binamungu wa Star TV na Sauli Giliard wa The Citizen.

Vivian Pyuza wa CG Fm Radio alikuwa mwanamke wa pili

kuibuka mshindi wa jumla mwaka 2017. Alisema wakati huo kuwa “ siamini” baada ya jina lake kutajwa na mgeni rasmi katika Tuzo hizo, Profesa Issa Shivji.

Alikuwa ameshinda katika makundi mawili – Kuripoti Afya na Jinsia na Vijana na hakukuwa na mshindi mwingine aliyepata tuzo katika makundi mawili.

Pyuza, ambaye ni mhitimu wa Chuo cha Royal College Jijini Dar es Salaam aliwashinda - Salome Kitomari wa Nipashe, Tumaini Msowoya wa Mwananchi na Gerald Kitabu wa The Guardian.

Hiyo ilikuwa mara ya tatu kushiriki katika Tuzo hizo. Mwaka 2015 alishinda tuzo ya Kuripoti Watoto na mwaka 2016 alishinda Tuzo ya Kuripoti Afya.

Salome Kitomari, aliibuka mshindi wa jumla mwaka 2018.

Kitomari, ambaye alifika katika hatua ya mwisho ya kuwania taji hilo mwaka 2017 alisema kuwa hakukata tamaa aliposhindwa kupata nafasi hiyo lakini aliweka juhudi zaidi na kuibuka mshindi wa jumla 2018.

Kitomari aliwashinda Yohan Gangway wa Radio SAUT na Jackton Manyerere wa Jamhuri.

Kitomari alishinda katika kundi la habari za uchunguzi kwa habari yenye kichwa “ Jinsi masoko yanavyopoteza mamilioni” na nyingine katika kundi la wazi -“ Hivi ndivyo mafao ya pensheni yatakavyokuwa”.

Kwa kuwa pazia la EJAT 2019 limefunguliwa, wanawake wataendelea kushinda?

Inatoka Ukurasa wa 13

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga akimkabidhi hundi ya sh. milioni 3 Salome Kitomari mshindi wa jumla EJAT 2018.

Page 15: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

15

Maoni

Toleo la 146, Oktoba, 2019

Na Gervas Moshiro

Wiki ya tatu ya mwezi Oktoba mwaka huu mitandao ya kijamii ilisheheni taarifa

mbalimbali kuhusiana na afya ya Rais Dk. John Pombe Magufuli. Wengine wakidai anaumwa na anatibiwa mahali pasipojulikana na wengine kuashiria kuwa sio mzima.

Kufuatia taarifa hizo, kuna wananchi waliosikitika na kumwombea kwa Mungu apone haraka na kuna wengine hawakuamini taarifa hizo. Kilichonishangaza ni baadhi ya wananchi walioandika kufurahia hali hiyo wakisema kuwa hatimaye haki imetendeka. Nilijihisi kama nimepigwa radi.

Mfadhaiko ulinizinga nikatamani kujua ukweli wa hali kujituliza. Nikaabiri vyombo vikubwa vya habari nchini kuona kama kuna taarifa yoyote kuhusiana na afya ya Rais. Sikuona.

Wananchi wengine wakazidi kuandika kwenye mitandao wakisikitika au kufurahia hali hiyo. Nilijawa na huzuni pamoja na mawazo mengi nilipotafakari hatma ya tukio hilo. Ni nini kitatokea ikiwa tetesi za msiba zitakuwa za kweli? Machozi yakanilengalenga na msongo mkubwa moyoni. Nikawaza, huu si wakati mzuri wa kumpoteza kiongozi huyo kwani agenda tunazosubiri kwa hamu ili tufaidi ujasiri wake bado hazijatimilika. Mungu apitishie mbali.

Hata hivyo nikafarijika na wazo kuwa walioweka taarifa hizo mtandaoni si waandishi wa habari. Waandishi wa habari hawabuni uzushi.

Kwa mshangao zaidi, hadi siku nasoma uzushi huo – Jumapili na Jumatatu - kama siku tatu hivi toka kuvuma kwake , hakuna mwandishi wala ofisa habari aliyekuwa amejishughulisha na suala hilo.

Nikakumbuka video moja niliyotazama siku ya Jumapili kwenye moja ya runinga za

mtandaoni iliyohusu Rais akiapisha maafisa mbalimbali aliokuwa ameteua karibuni. Hii ikanipa mfadhaiko zaidi: inawezekana vipi Rais aonekane akifanya kazi Ikulu na huku awe amegonjeka yuko kitandani kwa wakati huo huo?

Baada ya kiapo, Peter Msigwa aliyekuwa anaratibu hafla hiyo akatangaza kuwa kungekuweko na kikao cha picha ya pamoja ya Rais na walioapishwa. Hata hivyo akamwomba Rais kusema lolote, kama alikuwa nalo kabla ya tukio hilo la picha.

Kama kawaida, baada ya kuwajulia hali na kuwatambua kiprotokali viongozi mbalimbali, akiwemo Makamu wa Rais, aliwakumbusha wajibu wao wa kuwahudumia wananchi kwa uzalendo na uadilifu mkubwa, hasa wajitahidi kutatua changamoto za wananchi za maendeleo kwa kuzingatia sheria na utaratibu unaokubalika.

Niseme kweli kwamba video niliyoona ilimwonesha Rais akiwa mtaratibu na uso uliokosa ule uchangamfu tuliozoea. Hii haikujalisha sana kwa kuwa kila mtu, bila kujali wadhifa wake, kuna siku ananyon’gonea na kupooza kutokana na sababu mbalimbali.

Licha ya ukweli ule wa Rais kuweko kazini, bado baadhi ya mitandao iliendelea na kuandika kuhusu Rais mgonjwa. Nyingine zilisema kuwa Rais kasafirishwa ng’ambo kwa matibabu, na hata kuonesha bao moja lililoelekeza hospitali ilipo, japo lugha ya maandishi juu ya bango lile sikuielewa.

Kwa mashabiki wa mitandao lazima walichanganyikiwa wakihaha kutafuta ukweli wa taarifa zile kutoka mamlaka husika bila mafanikio kwa siku mbili tatu.

Kwa wale waliomwona Rais na bado wakawa wanaona wengine wanazidi kuweka mtandaoni uongo kumhusu, lazima wawe na shaka na utimamu wa akili za watu hawa wa mtandao.

Uzushi ulioanzishwa na mkorofi au mpuuzi mmoja, sasa ulikuwa unavuruga mioyo ya maelfu, kama si mamilioni ya wananchi. Hasira zitapanda kwa kuwa Rais yu timamu lakini bado kuna watu wanashikilia tu kuwa ni mgonjwa, au hata katutoka kutokana na uvumi wa dhahiri. Hii inaweza kuparaganyisha taifa. Kutafutana kutaanza, sio Rais atakayefanya hivyo, bali mashabiki na wapenzi wake wengine, jambo ambalo halitakuwa jema sana kwani haliendani na utulivu na ustawi wa jamii tunayodhamiria kujenga.

Turejee sasa kwenye uandishi wa habari na usambazaji uzushi. Uzushi upo kwenye jamii zote duniani, na ni jambo la kijamii. Kwa mwandishi wa habari uzushi ni fursa muhimu sana kwani hutoa fununu ya kitu kilichomo lakini si dhahiri bado, au ni uongo tu unaohitaji kukataliwa kwa kueleza ukweli. Mwandishi hufuatilia uzushi na kutafiti chanzo chake, mwishoni hupata taarifa ya kina inayotosheleza shauku na kuondoa dukuduku za watu.

Uzushi ni mbaya kama hauelezwi. Mara nyingi unakataliwa kijuu kijuu bila maelezo. Watu hubaki na shaka. Kama ilivyo kwenye sheria, uzushi ni shutuma zinazohitaji ushahidi ili kuwa halali na kuweza kushawishi watu wakubali mrengo uliotajwa. Kadhalika unapokataliwa, lazima uendane na maelezo ya kina kuonesha uongo huo ulivyo.

Vyombo vya habari huongeza saikolojia ya kihalaiki kwenye uzushi usioelezwa na unaposambazwa kwa watu wengi huonekana kuwa ni kweli. Kuna sababu mbili: moja ni kuwa baadhi ya watumiaji wa vyombo vya habari hapa kwetu si waelimika sana wenye kuweza kuchambua baadhi ya masuala ya kijamii na pili, ile tabia iliyojengeka zamani ya kuamini kuwa taarifa inayotoka kwenye vyombo vya habari ni

Uvumi ushughulikiwe haraka

Endelea Ukurasa wa 16

Page 16: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

ya kweli na ina baraka za uongozi wa juu.

Tetesi nyingine ni haribifu kimajanga. Saddam Hussein wa Irak alisingiziwa kuwa ana silaha za maangamizi na Kanali Muamar Qhadafi wa Libya akahisiwa kuwa anataka kuangamiza himaya ya kiuchumi ya Wafaransa na nchi za Ulaya barani Afrika. Raia wa nchi hizo wakalishwa uzushi huo na kuamini kiasi cha kuwaunga mkono waliokuwa wanatoa uongo huo hadi kuishia kupigana wao kwa wao na sasa mataifa hayo yamesambaratika. Hakuna aliyewahi kukanusha mapema kwa ushahidi uongo huo na kuweka wazi ukweli wa uzandiki wa mataifa vamizi.

Ndio maana vyombo vya habari ni muhimu sana kuhakikisha kuwa umbea hauachiliwi kutamba.

Kwa bahati mbaya mitandao imezaa utamaduni wa kila mtu kujiwekea huko chochote bila kuhakikiwa au kama inavyosemwa, maudhui yanayozalishwa na mtumiaji, jambo linaloonekana kuhalalisha maudhui yasiyodhibitiwa, ukiwemo uongo mtandaoni. Ni jambo la ajabu sana, na serikali nyingi zimeanza kushughulikia dhana hii ili mitandao iwe ya manufaa kwa jamii.

Mimi ni muumini sana wa haki za kuzaliwa za binadamu, uhuru wa habari ukiwemo, lakini pia naamini kwenye usemi wa wanafalsafa wa zamani kuwa binadamu huzaliwa huru lakini akiwa kwenye jamii anakuwa amefungwa minyororo. Haki na uhuru wetu unaishia pale unapoanza wa mwingine.

Sheria yetu ya mokosa ya mtandaoni iko wazi kabisa na inakataza yeyote kutoa umbea au kuendeleza umbea mtandaoni. Ni kosa la jinai lenye faini na kifungo.

Ni jukumu la mamlaka za usimamizi wa sekta kuhakikisha kuwa sheria

inaheshimiwa ili taaluma ya habari itende ipasavyo dhima yake ya kulinda na kuiendeleza jamii.

Katika tukio hili la uvumi kuhusu afya ya Rais, taasisi mbili zapashwa kuwajibika: Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na Idara ya habari ya Serikali, MAELEZO.

Kila binadamu kuna wakati ataugua na hakuna sababu ya kuficha ukweli huo hadi kufikia mahasimu wanasherehekea masaibu hayo. Rais wa nchi si raia wa kawaida – anabeba roho, mioyo na matarajio ya taifa zima na ni rais wa wote. Wananchi tuliomkabidhi dhima hii kubwa tuna haki pia ya kujulishwa lolote – baya na zuri linaloathiri utendaji wake.

Bahati nzuri ni kwamba hakuna baya lililomtokea Rais na wale waliosherehekea wana ajenda zao.

Tunatarajia watumia mitandao kufuata sheria na kuzingatia vigezo vinavyofanya taarifa kustahili kutolewa na kuwekwa kwenye chombo cha habari.

Nilieleza mwanzoni kuwa uvumi ni sehemu ya maisha yetu, haukwepeki. Nina mapendekezo kadha ya namna waandishi wa habari wanavyoweza kugeuza tetesi au uvumi kuwa fursa za habari.

Uvumi wa mtandaoni mara nyingi huletwa na watu tunaowajua na sisi huwashirkisha watu tunaowajua pia, au hata maswahiba wetu na hivyo kuongeza uenezi wa taarifa hizo.

Fanya utafiti hiyo tetesi kukisia au kufahamu chanzo chake au ni nini kinafanya ipate mashiko wakati huu. Kama hutafahamu chanzo au kiini cha tetesi hiyo au ushahidi wa kuinjika tetesi hiyo, basi iache – usiichapishe wala kushirikisha watu wengine kuifahamu.

Kwenye mitandao ya kijamii, mara nyingi majina yanayotumiwa ni ya bandia na

tunaweza tukawa tunawafahamu.

Kadhalika yawezekana tukawa tunafahamu hata nia na tamaa zao pamoja na malengo yao kisiasa au misimamo yao kuhusiana na masuala mbalimbali. Misimamo hii huathiri uadilfu wa taarifa, hivyo yabidi kujihadhari.

Mara nyingi tunasahau pia kuwa uongo katika sura ya uvumi au tetesi unaweza kutumiwa kama silaha ya kufanikisha malengo ya mtu. Kujihusisha katika uvumi huo, maana yake ni kusaidia kueneza uongo. Waandishi wa habari hawatarajiwi kueneza uongo.

Niliangalia majina ya wale walioeneza uvumi wa afya ya Rais na kugundua kuwa ni majina yale yale ambayo katika fani nyingi wamekuwa wakikinzana na utawala wa Dr. Magufuli. Hii inafanya madai yao kuwa na matatizo kwa sababu yanakosa uhuru wa msimamo au uadilifu wa mawazo.

Kabla ya kukumbatia uvumi wowote, jaribu kutafiti ni nani mwingine wa heshima na mwadilifu anayeshirikishwa au kuonesha kuunga mkono, la sivyo waweza kujikuta unacheza mchezo wa wengine bila kujua.

Moja ya sababu kubwa ya kuwa na vitengo vya habari katika taasisi yoyote ni kupunguza uwezekano wa wananchi kuamini uvumi au tetesi za uongo zinazoweza kuharibu taswira ya mtu au taasisi na hivyo kuathiri umadhubuti na utendaji wake. Popote penye wasi wasi, uoga, ukandamizaji, kukosa usawa, chuki na hasa zaidi penye kukosa taarifa sahihi kwa wakati, basi kwa vyovyote uvumi utashamiri.

Inahitaji ubunifu kuhakikisha uvumi unadhibitiwa na kupungua na wanaotakiwa kufanya kazi hiyo ni wanahabari na watu walio kwenye utendaji maofisini.

Uvumi ushughulikiwe haraka Inatoka Ukurasa wa 15

16

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Habari

Page 17: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Na Tumbi Kiganja

Katika Mkutano Mkuu (NGC) wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) uliofanyika Zanzibar

Oktoba 5, 2018 Rais wa Baraza Jaji mstaafu Thomas Mihayo, alionya kuhusu kuwaonyesha watuhumiwa kuwa wahalifu.

“Unawasikia polisi wanadai kuwa mtuhumiwa amekiri kufanya kosa”, Jaji alisema. “Wacheni polisi waseme hivyo, lakini ninyi ni wanataaluma”, aliongeza.

Wakati Kamanda wa Polisi wa Mkoa akiwaonyesha watu mbele ya vyombo vya habari, watu hao ni watuhumiwa, alisema.

Licha ya tahadhari na ushauri huu, vyombo vya habari vimekuwa vikiendelea kuelezea msimamo unaochukuliwa na polisi kuhusu watuhumiwa na kuwaita kuwa

wahalifu hata kabla ya kutiwa hatiani na mahakama.

Sasa mwaka mmoja umepita, Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro, amerudia kusema yale jaji Mihayo alichowaambia wanahabari kwenye Mkutano Mkuu ambao ni chombo cha juu cha MCT.

Aliwatahadharisha Polisi kutozingatia kanuni na taratibu za polisi ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Alipinga vikali tabia ya polisi kuonyesha wahalifu.“Mnataka kupata nini…mnataka kusifiwa”, IGP Sirro alishangaa alipokutana na makamanda wa polisi.

“Huyu ni mtuhumiwa, si mhalifu”, alisema na kuonya hatari ya watu wa aina hiyo kwamba baadaye wanaweza kuwafungulia mashtaka makamanda kwa kuwaonyesha na kuwatangaza kwa makosa kuwa wao ni majambazi ili wathibitishe madai yao.

Wengine katika jamii ambazo polisi wanazingatia taratibu zao watashangazwa jinsi tunavyofanyakazi.

“Huko hukuti watuhumiwa wakionyeshwa, inakuwa nadra”, alisema na kuwahimiza polisi kuzingatia taratibu na kanuni zao.

Alichosema IGP, ingawa hakuwaambia wanahabari, lakini kinatia doa kwa wanahabari kwa kutozingatia taratibu na kanuni za habari kuhusu jinsi ya

kuwachukulia watuhumiwa.

17

Habari

Toleo la 146, Oktoba, 2019

IGP Sirro asema alichowahi kuonya Rais wa MCT kuhusu watuhumiwa

Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji mstaafu Thomas Mihayo.

Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro

Page 18: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

18

ambalo mara nyingi huendeshwa na hisia zaidi hivyo ni vyema suala la maadili ya uandishi wa habari mkalipa kipaumbele ili vijana hawa wabaki katika misingi iliyo sahihi,” alisema Jaji Mlay

Nae Edda Sanga ambae ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, licha ya kuwapongeza e-media pia aliwasisitizia kutowasahau waandishi wa habari wa kike. “Nimeona mna waandishi wengi vijana lakini nawaomba muongeze pia idadi ya waandishi na wafanya kazi wa kike ili kupata usawa wa

kijinsia katika vyombo vyetu”.Meneja vipindi wa e-fm radio,

Dickson Ponela alisema kuwa wanajitahidi kuwa makini sana na suala la maadili katika maudhui ya vipindi kwani wanajua kuwa chombo cha habari kinaweza kujenga au kubomoa jamii kwa haraka sana.

“Maadili ni kipaumbele chetu maana unapokuwa na waandishi vijana lazima uwe makini kwa kuwa wao wanajali zaidi hisia zao na umaarufu hivyo ni rahisi kufanya makosa ya kimaadili. Kuna wakati inabidi ukimbilie studio haraka

na kwenda kuweka mambo sawa pindi unapohisi mwelekeo wa mtangazaji fulani unaenda tofauti na ndio maana unaona hata ofisi yangu ipo karibu kabisa na studio”.

Kwa upande wa Meneja Mkuu wa e-fm Mohamed Lukwili alishukuru ujio wa Kamati ya Maadili na kusema kuwa ujio huo umewafungua masikio na kuahidi kuwa wanachama wa Baraza ili kuweza kunufaika na huduma za uanachama. Kuhusu suala la maadili, Lukwili alisema ni kweli wanakutana na hizo changamoto japo wanajitahidi kukabiliana nazo. “Licha ya kuzingatia taaluma ya mtu, lakini pia tumejikita zaidi katika vipaji ili kuendana na soko la burudani”.

Lukwili aliongeza kuwa changamoto kubwa ambayo inawakabili ni kupokea vijana ambao hawajaiva kitaaluma hivyo wakifika kwao wanalazimika kuanza kuwafundisha ulimwengu wa kazi ulivyo ili waachane na nadharia za darasani. ”Kama uongozi tumeamua kujikita katika kuwalea wale wenye vipaji na taaluma kwa muda fulani kisha watakaoonyesha mwelekeo tunawachukua moja kwa moja” Awali akielezea madhumuni ya ziara hiyo, meneja programu wa Baraza David Mbulumi alisema kuwa ni utaratibu wa kawaida wa Baraza kuwa karibu na wadau wake ili kuwakumbusha kuhusu masuala ya maadili na pia shughuli ambazo Baraza linafanya na kusikiliza pia changamoto ambazo wadau wamekuwa wakikutana nazo kila siku ili kuona ni namna gani wanaweza kushirikiana katika kuzitatua.

Kamati hiyo pia ilitembelea Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mahusiano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (SJMC) ikiwa ni mwendelezo wa kutembelea wanachama wake na pia kujadiliana kuhusu mpango wa kuwahusisha wanafunzi katika kuripoti makosa mbalimbali ya kitaaluma watakayokuwa wanakutana nayo katika runinga, redio na magazeti ili

iwe ni sehemu mojawapo kwao ya kufanya mazoezi ya vitendo.

Mkuu wa Shule kuu-SJMC, Michael Andindile alisema kuwa wanashukuru sana kwani Baraza limekuwa karibu na wao na mara kadhaa limekuwa likisaidia katika maeneo mbalimbali ya kimafunzo hasa ya maadili.

“Baraza limekuwa likitusaidia sana katika mafunzo ya walimu wetu na hata wanafunzi, hivyo kuwajenga kitaaluma”. Kuhusu mpango wa kuwahusisha wanafunzi kushiriki katika ufuatiliaji wa makosa ya kimaadili katika vyombo vya habari, Andindilile alisema ni jambo zuri kwani litawaongezea wanafunzi uelewa hivyo, wao kama shule, wataendelea kuwasiliana na Baraza kuona ni jinsi gani sasa utaratibu utakavyokuwa.

Andindilile pia aliongeza kuwa “Wanafunzi wanahitaji kufanya mafunzo kwa vitendo hivyo kuanzisha utaratibu wa aina hii kutawasaidia kuongeza ufahamu na kujua mambo kwa uhalisia na mapana yake”

Kwa upande wa Afisa Programu wa Baraza, Saumu Mwalimu alisema kuwa Baraza litaandaa utaratibu ambao wanafunzi wataelezwa maeneo gani watapaswa kuyafanyia kazi au kuyaangalia zaidi wakati wa zoezi hilo. Pia alitoa shukurani kwa uongozi wa vyombo vya Mlimani redio na runinga kwa ushirkikiano wanaoutoa kwa Baraza.

Mapema mwaka huu Baraza lilikutana na wahariri na baadhi ya walimu kutoka vyuo mbalimbali vinavyotoa kozi za uandishi wa habari kwa lengo la kujadiliana jinsi ya kuanzisha utaratibu utaowawezesha wanafunzi wanaosoma kozi husika kuwa wanapitia magazeti, runinga na kusikiliza redio kisha kuripoti kwa Baraza makosa ya kimaadili watayokutana nayo. Hii itawasaidia wanafunzi kujifunza aina ya makosa hayo kwa vitendo kabla hawajaingia sokoni. Lakini pia itakuwa ni sehemu mojawapo ya kupatia alama za kitaaluma toka kwenye vyuo vyao.

Vyombo vya habari vizingatie MaadiliInatoka Ukurasa wa 20

Nimeona mna waandishi wengi

vijana lakini nawaomba muongeze pia idadi ya waandishi na wafanya kazi wa kike ili kupata usawa

wa kijinsia katika vyombo vyetu

Page 19: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Habari

Toleo la 146, Oktoba, 2019

19

Na Mwandishi wa Barazani

Rais wa Tanzania ametakiwa ku-hakikisha wanahabari, watu wa mtandao na watumiaji, watafiti, watetezi wa haki za binadamu na

wapinzani watakuwa na haki zao za kibin-adamu ikiwemo haki ya kujieleza, kuju-muika na kukutana bila woga.

Rais anatakiwa kutoa kauli ya wazi kwa maofisa wa serikali kulaani na kuwataka wasifanye maovu ikiwamo vitisho, kupiga watu , kukamata na kuwatishia kuwakamata wanahabari na kuwashitaki, wanaharakati, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wanachama wa upinzani.

Miito hiyo imo katika Ripoti maalum kuhusu Tanzania zilizotolewa na mashirika ya kimataifa ya – Human Rights Watch na Amnesty International zilizotolewa Nairobi, Kenya Oktoba 28, 2019.

Ripoti hizo mbili zimeeleza kuwa tangu Rais wa sasa alipoingia madarakani mwaka 2015, Tanzania imeporoka katika haki na uhuru wa kukutana, kujieleza na utawala wake unakwaza vyombo vya habari na vyama vya kiraia.

Kazi ya vyombo vya habari inabinywa kwa sheria mbalimbali mpya na kuimarishwa nyingine za zamani ambazo zinabana uandishi huru. Ripoti hizo zinatolea mfano wa sheria kama Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016, Takwimu , Makosa ya Mtandaoni, sheria ya 2018 ya vyama vya siasa na kanuni za mtandaoni zinazobana waendesha mitandao.

Ripoti hizo pia zinatumia mfumo wa sheria kunyanyasa wanahabari zikitolea mfano wa karibuni wa kukamatwa mwandishi Erick Kabendera kwa tuhuma ambazo ripoti zote zinaona ni za kutungwa.

Usimamishaji magazeti, vituo vya redio na kutoza faini kubwa vituo vya runinga kwa tuhuma za kukiuka kanuni limekuwa jambo la kawaida.

Serikali imetakiwa kuheshimu na kutekeleza hukumu ya mahakama kama ya Afrika Mashariki ambayo iliamuru serikali kuchukua hatua za kurekebisha vifungu kadhaa vya Sheria ya Huduma ya

Vyombo vya habari iendane na makubaliano ya Mkataba wa Afrika Mashariki.

Mahakama hiyo ilitoa hukumu hiyo Machi 28, 2018 kufuatia shauri lililofunguliwa mahakamani hapo na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kito cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Umoja wa Kulinda haki za Binadamu

Serikali pia imetakiwa kuondoa vikwazo vinavyohujumu kuheshimu haki za binadamu kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na ule mkuu wa 2020 ikiwemo kufuta au kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Takwimu, Sheria ya Makosa ya Mtandaoni, Sheria ya Asasi Zisizokuwa za Kiserikali na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Ripoti mbili zimetoa mapendekezo kwa taasisi mbalimbali za kitaifa ikiwemo Bunge na mawaziri kuchukua hatua za kuboresha hali ya haki za binadamu nchini.

Kwa mfano Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ameombwa kuhakikisha vyombo vya habari vinafanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa, vina uhuru wa maoni na kufanya kazi bila hofu ya kusakamwa.

Ukiacha vyombo hivyo vya kiserikali vilivyolengwa kuchukua hatua, pia walitoa mapendelezo kwa vyombo vingine akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika waliyemtaka alaani wazi wazi kwa nguvu zote uvunjifu wa haki za binadamu unaofanyika Tanzania na kuwa na wasiwasi

kuhusu vitendo wanavyofanyiwa watu binafsi na watendaji wa serikali.

Orodha hiyo inajumuisha Kamisheni ya Afrika ya haki za Watu na Binadamu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Washirika wa Maendeleo Tanzania, Umoja wa Ulaya na washirika wengine wa kimataifa wa maendeleo.

Ripoti hiyo ya Uangalizi wa Haki za Binadamu inayoitwa kwa tafsiri isiyo rasmi: ”Kadri nilivyo kimya, niko salama” – Tishio la Vyombo Huru vya Habari na Vyama vya Kijamii Tanzania “ As long as Iam quiet, Iam safe” Threats to Independent Media and Civil Society in Tanzania inatokana na mahojiano na wananchi 80 yaliyofanyika Julai hadi Septemba 2018 na Januari 2019 na inaonesha ushahidi wa mazuio na manyanyaso Tanzania Bara na Zanzibar.

Mahojiano yalihusisha waandishi habari, wahariri wa magazeti, wafanyakazi katika asasi za kiraia zilizopo Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha Lindi na Mwanza Ripoti ya Amnesty International inayoitwa – The Price we pay – Targeted for dissent by, the Tanzanian State, (Gharama Tunayolipa – kwa Kutofautiana, Ilivyo Tanzania), inatokana na mahojiano 68 yaliyofanywa Tanzania kati ya Februari na Machi 2019 na kwa mbali Serikali, maofisa wasiokuwa wa serikali, wanasheria, wanataaluma, viongozi wa dini na wanadiplomasia pamoja na kupitia ushahidi kutokakumbukumbu mbalimbali.

Amnesty International inasema kwenye ripoti yake kuwa Oktoba 3, 2019 ilipeleka barua kwa Inspekta Mkuu wa Polisi, Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mashitaka, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano, Waziri wa

Sheria na Katiba, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa

na Michezo ikielezea kwa muhtasari ripoti yake hiyo na kuomba wahusika wajibu orodha ya maswali ya kina lakini haikupata jibu lolote hadi taarifa hii ilipoandikwa.

Ripoti za kimataifa zalalamikia serikali Tanzania

Mwandishi Erick Kabendera.

Page 20: EJAT 2019 Yazinduliwa - MCT€¦ · MCT yaonya kuhusu habari za chuki Wahariri watahadharishwa matumizi ya picha Uvumi ushughulikiwe haraka ... September-Oktoba, 2010 3 Habari Toleo

Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) walipotembelea E FM Radio na E TV.

20

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Tumbi Kiganja

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) jaji Mstaafu Juxon Mlay

amevitaka vyombo vya habari ku-fanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma hiyo.

Rai hiyo ilitolewa Oktoba 9, 2019 jijini Dar es Salaam wakati Kamati hiyo ilipotembelea ofisi za e-media, ambao ni wamiliki wa vituo vya e-fm na tv-e vilivyopo Barabara ya Mwai Kibaki jijini Dar es Salaam.

Kamati ya Maadili ya Baraza inaundwa na Mwenyekiti, Jaji Mstaafu Juxon Mlay, na Makamu Mwenyekiti Edda Sanga. Wajumbe wengine ni Wallace Mauggo, Bernadina Chahali na Anna Henga.

Katika msafara huu Anna Henga hakuweza kushiriki kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kazi. Msafara huu pia uliwahusisha wajumbe kutoka sekretarieti ya Baraza ambao ni Meneja Programu – David Mbulumi na maafisa programu wawili- Saumu Mwalimu na Tumbi Kiganja.

Baada ya mapokezi yaliyoongozwa na Meneja Mkuu wa e-fm Redio, Mohamed Lukwili, Kamati ilitembezwa maeneo mbalimbali ya ofisi za e-media kujionea jinsi vituo hivyo vilivyosheheni vifaa vya kisasa na teknolojia ya hali ya juu.

E-Media ilionekana kuwa na imani kubwa na kundi la vijana ambao wengi wamekuwa wabunifu na wenye vipaji vya hali ya juu kuendana na tekinolojia ya habari na mawasiliano ingawa pia ndio kundi ambalo

hukabiliwa na changamoto za mihemko ya ujana na hivyo wakati fulani hujikuta wakifanya kazi kwa kufuata hisia zao na kusahau maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Hali hiyo iliwafanya wajumbe wa Kamati ya Maadili kusisitiza uongozi wa e-media kuwapa mafunzo ya mara kwa mara ya maadili kwa waandishi wao hasa nyakati hizi ambako nchi inaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule Mkuu mwakani.

“Kwanza niwapongeze sana uongozi wa e-media kwa kufanya uwekezaji wa mitambo ya kisasa ya utangazaji na kuleta ushindani katika tasnia ya habari nchini, pia kwa kuweza kuwaamini vijana na kutengeneza ajira kwa kiwango kikubwa. Najua vijana ni kundi

Vyombo vya habari vizingatie Maadili

Endelea Ukurasa wa 18