Wasaidizi wa misa Jumapili 20/01/ 2019
01.15 asubuhi: BLESSED IRENE STEFANI
3.00 asubuhi: YOUTH
05.30 asubuhi: ST. FRANCIS DE SALES
11.30 Jioni: Wahusika
Masomo: 1. Is: 62: 1 –5 ; Zab: 96
2. 1 Wak: 12: 4—11; Injili: Yn: 2: 1—11
Wasimamizi wa PPC 20/01/ 2019
Cynthia Tororey
Carolyne Ouko
Alfred Kandara
Elizabeth Litswa
SHRINE OF MARY HELP OF CHRISTIANS - UPPER HILL
Mandhari: ....“Kweli mimi nawabatiza kwa
maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho
Mtakatifu na kwa moto”. ..”
Mungu Baba wa mbinguni, tunasadiki na kukiri kuwa utabaki Mungu uliye
daima mwaminifu na kweli, unayerudisha na kuponya watu wako. Tunapoad-
himisha Jubilei ya miaka ishirini na tano, ya kutabarukiwa kanisa la hija la
Maria msaada wa wakristo, ambalo ni zawadi yako, tunakushukuru na kuku-
sifu wewe.
Ewe Bwana Yesu Kristo, uliyepakwa mafuta na kuteuliwa na Baba kuleta
habari njema kwa maskini, kuwahubiri wafungwa kufunguliwa kwao, vipofu
wapate kuona, waliogandamizwa wawe huru, na kutangaza mwaka wa Bwana
kwa watu wake, uturejeshe katika neema.
Uje Roho Mtakatifu na ukae katika jumuiya yetu, katika mwaka huu wa Jubi-
lei. Tunakuomba uunde ndani yetu familia kwa ajili yako, na kwa ajili ya utu-
kufu wa jina lako. Katika neema, upole na upendo wako, tuopoe kutoka yote
yawezayo kututenganisha na ibada ya kweli.
Ewe Utatu Mtakatifu, kwa maombezi yaWatakatifuYohane Bosko, Maria
Domenika Mazzarello, Dominic Savio na watakatifu wote, katika familia ya
Wasalesiani, na Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, na aliye mlinzi na
msaada wetu, tunaweka nia yetu kwako (............) Kwa njia ya Kristo Bwana wetu…..
Amina.
Nakala ya Jumapili
UBATIZO WA BWANA
13 January, 2019
Mwaka C
Sala ya Mwaka wa Jubilee
Unaombwa kuzima simu yako
Chukua nakala moja kwa kila familia.
Ubatizo wa watoto wachanga
1. Chukua na kujaza fomu ya Ubatizo kabla ya mtoto kuingizwa kwenye orodha ya wanaobatizwa. 2. Mafundisho kwa wazazi na wasimamizi wa watoto wachanga wa Ubatizo ni Jumatano tarehe 13 Februari, 2019, kwenye Ukumbi wa mkutano. Saa 11.30 jioni 3. Ritriti kwa watakaobatiziwa watoto itaku-wa Jumamosi tarehe 16, Februari, 2019, saa 3.30 asubuhi. 4. Ubatizo wa watoto utakuwa tarehe 23 Februari, 2019
MATANGAZO
1. Sikukuu ya St. John Bosco huadhimishwa tarehe 31 Januari kila mwaka. Mwaka huu, tutaadhimisha sikukuu tarehe 27 Januari. Hii ni maadhimisho ya siku yetu kama familia kama parokia. Misa itakuwa moja siku hiyo, saa nne
asubuhi.
2. Usajili wa Mafundisho ya Ubatizo kwa watoto wa zaidi ya miaka mitano unaendelea katika ofisi ya
Shrine.
3. Mafundisho ya Katekesi (Watu wazima na wato-to) na Sunday school yatarejea tarehe 13 Januari,
2019.
4. Shajara zenye masomo ya Biblia mwaka huu zinzuzwa kwenye Bookshop; Kiingereza Ksh, 700,
Swahili, Ksh. 600 /-.
5. Toleo la Kipindi Krisimasi la Shrine Digest linazwa hapo nje ya kanisa na katika bookshop.
Tafadhali jichukulie nakala.
6. Shajara maalum za Mwaka wa Silver Jubilee ya Kanisa lute za 2019 zinapatikana kwa Ksh 700/-.
Jipatie shajara yako kutoka Bookshop.
7. Kwa Wanaume wote, Chama cha Kitume CMA Don Bosco, kinaanzisha Batalion ya 24 ya Man Enough Jumamosi 19 Januari, 2019 saa 1 asubuhi. Jisajili kwenye hema nje ya kanisa baada
ya Misa.
8. “Mothers of Sons” msimu wa 5 iliaanza tarehe 12 Januari, 2019 kwenye Conference Hall 1:30 asubuhi hadi 3:30 asubuhi. Jisajili kwa kutuma
ujumbe mfupi kwa 0721469260.
9. Wiki ya Maombi kwa Umoja wa Wakristo itaanza Jan 18 hadi 25. Kutakuwa na sala maalum kwa
lengo hili katika kila Misa.
Salesians of Don Bosco, Upper Hill Road, P.O. Box 62322
00200,City Square, Nrb.Tel: 2714622,
Office No: 0722 331 662, E-mail:
Parish Priest/Shrine Director: 0716 876 680
Website www.donboscochurch.org,
Mpesa Pay bill: 331 662
Shrine of Mary Help of Christians
Je, umejiandikisha katika Parokia yoyote?
Jiandikishe kwenye Parokia mojawapo. Wale wa-
takaojiandikisha kama wanaparokia, wataanza
kupata huduma kama wanaparokia miezi 3 baada
ya kupata kadi.
MISA ZA JUMUIYA 12.30 jioni
Yatatolewa baadaye
SOMO LA KWANZA Isa. 40: 1-5, 9-11
Somo katika kitabu cha Nabii Isaya.
Watulizeni, wapeni tulizo watu wangu, asema
Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusa-
lem, utangazieni ya kwamba; Huduma yake
ngumu imekwisha, dhambi yake imeondole-
wa, Maana kwa mkono wa BWANA amepokea
adhabu maradufu kwa maovu yake yote.
Mtu analia: Tengenezeni jangwani njia ya
BWANA! Nyosheni nyikani barabara kwa Mun-
gu wetu! Kila bonde lifukiwe, kila mlima na
kilima kishushwe, Njia zenye kupotoka
zinyoshwe, na njia zenye mashimo zisawa-
zishwe. Hapo utukufu wa BWANA utafunuliwa,
na watu wote watauona mara; maana kinywa
cha BWANA kimenena haya. Panda juu ya mli-
ma mrefu, uutangaziye Sioni habari njema!
Paza sauti kwa nguvu, uutangaziye Yerusal-
emu habari njema! Paza sauti, usiogope!
Sema kwa miji ya Yuda: Tazama, Mungu
wenu! Yupo hapa BWANA Mungu: anakuja
kwa uwezo, na mkono wake unatawala; Tuzo
la ushindi wake linamsindikiza, mateka yake
yanamtangulia. Kama mchungaji, ana-
chunga kundi lake; mkononi mwake anawa-
kusanya wanakondoo, Anawachukua kifuani
mwake, anawaongoza kondoo wenye kun-
yonyesha.
Neno la Bwana
SOMO LA PILI Tit. 2:11—14; 3:4—7
Somo katika waraka wa kwanza wa Paulo
kwa Tito.
Maana neema ya Mungu imetoka kwa ku-
waokoa watu wote. Nayo inatuongoza
kuzuia yasiyo ya Mungu, na kupinga tama za
kidunia, tupate kuishi duniani hapa kwa kiasi,
kwa haki na kwa uchaji wa Mungu tukingoja
heri tunayoitazamia na ufunuo wa utukufu wa
Maungu mkuu na wa Mwokozi wetu Yesu
Kristo. Yeye amejitoa mwenyewe kwa ajili
yetu, ili atukomboe katika uovu wote, na
ajitakasie watu walio mali yake ya pekee na
wenye bidii kutenda mema. Lakini wema wa
Mwokozi wetu Mungu na hisani yake kwa
Wanadamu zilipotokea, ametuokoa, lakini si
kwa sababu ya matendo maadilifu tuliyoten-
da sis, isipokuwa kwa Huruma yake akitu-
osha tupate kuzaliwa tena na kutengenezwa
upya na Roho Mtakatifu. Mungu
amemweneza huyo ndani yetu kwa wingi
kwa ajili ya Yesu Kristo, Mwaokozi wetu, tu-
pate kuthibitishwa kwa neema yake na hivyo
kufanywa warithi wa uzima wa milele tunao-
tumaini.
Neno la Bwana
Wimbo Wa Katikati
Zab. 104
K) Umsifu BWANA, ee roho yangu!
Ee BWANA, Mungu wangu u mkuu sana!
1. Ee Bwana Mungu wangu u mkuu sana,
Umejivika fahari na adhama; Umejivika
mwanga kama vazi; Umetandaza anga kama
hema. (K)
2. Umeweka nguzo za ghorofa zake juu ya
maji. Umefanya mawingu kuwa gari lako;
Umekwenda juu ya mbawa za upepo Ume-
fanya pepo kuwa wajumbe wako; Na ndimi za
moto, kuwa watumishi wako. (K)
3. Ee BWANA, jinsi gani zilivyo nyingi kazi
zako! Zote umezifanya kwa hekima; Dunia
imejaa viumbe vyako Bahari iko kule, kubwa
na pana sana, Ndimo mlimo viendavyo bila
idadi, Viumbe hai vidogo na vikubwa. (K)
4. Hao wote hukutazamia wewe, Uwape
chakula chao kwa wakati wake Wewe hu-
wapa, nao wanakiokota; Wewe unakunjua
mkono wako, nao wanashiba mema (K)
5. Ukiuficha uso wako, wanafadhaika,
kiondoa pumzi yao, wanakufa Na kuyarudia
mavumbi yao Ukiipeleka roho yako wanaumb-
wa, Na unafanya upya uso wa nchi. (K)
SHANGILIO
Aleluya, aleluya,
mbingu zilifunguka na sauti ya Bwana
ikasikilika, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa
wangu, msikieni yeye.”
Aleluya.
INJILI Lk. 3: 15-16, 21-22
Somo katika Injili ilivyoandikwa na Luka.
Siku ile: watu walipokuwa wakingoja yataka-
yotokea, wote wakiwaza-waza mioyoni
mwao habari za Yohane, kama labda yeye
ndiye Kristo, Yohane alijibu akawaambia
wote, “Kweli mimi nawabatiza kwa maji;
lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi,
ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya
viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho
Mtakatifu na kwa moto”. Ikawa, watu wote
walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye
amebatizwa, naye anaomba, mbingu zili-
funuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake
kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti
ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu,
mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
Injili ya Bwana