dola ya kiislamu - hizbhizb.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/5.dolayakiislamu.pdf · "dhihirisha...
TRANSCRIPT
-
Page 1 of 125
بسم هللا الرحمن الرحيمDOLA YA KIISLAMU
Amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake na aali zake, تكون النبوة فيكم ما شاء هللا أن تكون, ثم يرفعها هللا إذا شاء أن يرفعها. ثم تكون الخالفة على على منهاج النبوة, فتكون ما شاء هللا «
ن يرفعها. ثم تكون ملكاً عاضاً, فيكون ما شاء هللا أن تكون, ثم يرفعها إذا شاء هللا أن يرفعها. ثم تكون أن تكون, ثم يرفعها إذا شاء أ ملكاً جبرياً, فتكون ما شاء هللا أن تكون, ثم يرفعها إذا شاء هللا أن يرفعها.
.»ن الخالفة على على منهاج النبوة ثم تكو"Utume utakuwepo kati yenu kwa muda anaotaka Allah uwepo, kisha Allah atauondosha
pindi anapotaka kuondosha, kisha kutakuwepo na Khilafa juu ya mfumo wa utume,
utakuwepo muda anaotaka Allah uwepo, kisha atauondosha pindi anapotaka kuondosha.
Kisha kutakua na ufalme wa kunyanyasa utakuwepo kwa muda Allah anaotaka uwepo,
kisha Allah atauondosha pindi Allah anapotaka kuuondosha. Kisha kutakuwepo na ufalme
wa kilazima, utakuwepo kwa muda Allah anaotaka uwepo, kisha atauondosha pindi
anapotaka kuuondosha,
kisha kutakua na Khilafa juu ya mfumo wa Utume"
UTANGULIZI
Kizazi kilichoko hakitambui serikali ya Kiislamu ambayo inaotabikisha Uislamu, na wale
ambao wameishi mwisho wa serikali ya Kiislamu (dola ya kiuthmani) ambayo ilimalizwa na
umagharibi walioona tu humo mabaki ya utawala wa Uislamu, na kwa sababu hiyo Muislamu
hupata shida zaidi ya kuiweka karibu picha ya utawala wa Kiislamu katika bongo ambalo
limetawaliwa na waqiah, na wala haliwezi (bongo) kutafakari utawala isipokuwa katika
vipimo vya kile kinachoona katika nidhamu ya kidemokrasia iliyo fisidifu, iliyolazimishwa juu
ya biladi ya Kiislamu kiulazima. Na wala ugumu sio katika hilo pekee, bali lilio gumu zaidi ni
katika kuyabadilisha mabongo hayo (yaliochorwa) kwa thaqafa ya kimagharibi. Bila shaka
thaqafa hii ya kimagharibi imekua ni silaha ambayo mmagharibi alioitumia katika uso wa
serikali ya Kiislamu, na akaidunga mdungo ambao ulimaliza uhai wake, na akaibeba
kuwapelekea watoto wa serikali silaha yake hiyo ikitona damu ya mama yao alieuwawa, na
akasema kuwaambia huku anajigamba: "nimemuua mama yenu, mzee ambae alikuwa
anastahiki kuuwawa kwa uovu wa malezi yake kwenu, na nimewafungulia malezi kwangu
ambayo mutapata ndani yake maisha mazuri na neema za milele) na wakanyosha mikono yao
wakimkumbatia katili, huku bado silaha inatona damu ya mama yao, hakika amewatendea
kitendo cha fisi katika wanaoyaona wakati anapokifanya kiwinja chake kinasepetuka na
hakiridhiki illa kukutana nae, na hakikubali illa kipigo kitakacho toa damu yake, au fisi
kumfikisha katika bonde na kuumla.
Basi ni kina nani kati ya watu hawa walio na mabongo yaliochorwa kuwa wajue kuwa silaha
hii ilioua sumu ndio ambayo imeangusha serikali yao ya Kiislamu, ndio hiyo hiyo daima
inaomaliza (muda watakao shikamana nayo) uhai wao na mipaka yao, na kua fikra hizi
wanazozibeba za kizalendo na kutengamanisha dini na serikali na baadhi za rai za kuutukana
Uislamu, ndizo baadhi za sumu ambazo zimeletwa kwao na thaqafa hii, na (uvamizi wa
kikiristo) kifungu cha kitabu hiki serikali ya Kiislamu na yote hayo ya kihakika na hisabu za
wazi zinatuonyesha katili muovu, na zinatuonyesha sababu ambazo zilimfanya atekeleze
maovu haya, na zinatuonyesha mbinu ambazo alizozitumia kutekeleza ukatili huu, na hamna
-
Page 2 of 125
sababu isipokuwa alikusudia kuumaliza Uislamu, na hamna mbinu kuu illa thaqafa hii
ambayo imekuja na uvamizi wa kimishenari.
Hakika Waislamu wameghafilika na hatari ya thaqafa hii, na wamekuwa wanapigana na
mkoloni na huku wanachukua kutoka kwake thaqafa yake, pamoja na kuomba ndio sababu ya
kukoloniwa kwao, na kwao anakita mkoloni katika biladi yao, na watizame baada ya hayo
vipi utakuwa mwelekeo wao unaogongana mgongano wa pamoja na wakuchekesha, na huku
wanataka kumshinda mgeni wanadai kumpiga vita na huku wanaomnyoshea mikono yao
kwa nyuma wakichukua kwa mikono miwili sumu yake inaouwa na kuigugumia, na
waanguka mbele yake wakiangania, mjinga atawadhania ni mashahidi. Sio chochote
isipokuwa ni kisunzi cha kughafilika na upofu.
Ni kipi wanacho Kitaka? Je, wanataka serikali juu ya msingi usiokuwa wa Kiislamu? Au
wanataka vijiserikali vingi katika biladi ya Kiislamu? Basi bila shaka mmagharibi amewapatia
hilo tangu mambo yameingia katika mikono yake, vijidola vingi, ili atekeleze mipango yake ya
kuuepusha Uislamu na utawala, na katika kuigawa biladi ya Waislamu, na katika
kuwalewesha na utawala, na bado anawapatia kila wakati serikali ili aendelee katika
kuwapotosha na azidi kuwagawanya, na huku amejitayarisha kuwapatia zaidi kwa sababu ni
wafuasi wake.
Suala lenyewe sio kusimamisha vijidola, bali ni kusimamisha serikali moja katika ulimwengu
mzima wa Kiislamu, na wala sio kusimamisha serikali yoyote, na wala sio kusimamisha
serikali inaoitwa serikali ya Kiislamu na inahukumu kinyume na aliyoyateremsha Allah, na
wala sio katika kusimamisha serikali inaoitwa serikali ya Kiislamu inaohukumu kwa kanuni
za Kiislamu tu, bila ya kuubeba Uislamu kama fikra kiongozi. Hakika suala lenyewe sio tu
kusimamisha serikali, bali ni kusimamisha serikali itakaoyarudisha maisha ya Kiislamu
kutokamana na aqeeda yake na kuutabiikisha Uislamu katika mujtama, baada ya kuwa
unatokota katika wafusi uliomakinika katika akili na kuubeba ujumbe wa Kiislamu
ulimwenguni.
Na dola ya Kiislamu sio tu ni mawazo ya kindoto, kwani historia yake imeenea kwa muda wa
karne kumi na tatu, hivyo basi ni uhakika. Ilikuwepo masiku ya kale, na itakuwepo hivi
karibuni, kwani sababu za kuwepo kwake ni zenye nguvu zaidi kuliko zama kuikataa, au
kutilia nguvu, na leo hii imejaa katika akili zinazo nawiri, nao ni ummah wa Kiislamu ulio na
kiu ya utukufu wa Uislamu.
Na dola ya Kiislamu sio mapenzi yanaoathiri hawa za nafsi, bali ni faradhi alioifaradhisha
Allah juu ya Wasilamu, kua akawaamrisha waisimamishe, na akawatahadharisha na adhabu
yake iwapo watadharau katika utekelezaji wake. Na atawakuwa vipi radhi Mola juu yao ilihali
izzah katika biladi zao sio kwa Allah na wala sio kwa Mtume wake na wala sio kwa waumini,
na watawezaje kuiepuka adhabu yake na huku wao hawaisimamishi dola inayoandaa jeshi na
kulinda mipaka, na kutekeleza hudud za Allah, na kuhukumu na kile alichokiteremsha Allah?
Hivyo basi imekua ni wajibu juu ya Waislamu kusimamisha serikali ya Kiislamu, kwani
Uislamu hautakua na athari isipokuwa kupitia serikali, na kwa sababu biladi yao haizingatiwi
-
Page 3 of 125
kuwa ni Darul-Islam isipkuwa tu itakopohukumiwa na dola ya Uislamu. Na dola ya Kiislamu
– pamoja na hayo - sio sahali kwa namna wataikejeli wanaofanya kejeli iwe ni watu binafsi au
vyama, na wakawa ni mawaziri wamekaa kukunja miguu katika viti vya utawala. Hakika njia
yake imejawa na miba, imezungukwa na hatari, iliojawa na vizuizi na matatizo. Mbali na
ugumu wa thaqafa isiokuwa ya Kiislamu, na mawazo hayo, na kwa tawala hatari zinazo
nyenyekea umagharibi.
Hakika wanoichukua njia ya ulinganizi wa Kiislamu ili kurudisha serikali ya Kiislamu, hakika
wao wanafanya kazi ya kufikia utawala ili waifanye kuwa ndio njia ya kuyarudisha maisha ya
Kiislamu katika biladi ya Kiislamu, ya kuubeba ujumbe wa Kiislamu katika ulimwengu, hivyo
basi utawakuta hawakubali utawala kipande hata kama zitatofautiana mbinu za kughuri, na
wala hawa kubali utawala kamili Isipokuwa iwapo watakua n aimani nayo ya kutabikisha
Uislamu utabikisha wa kimapinduzi.
Na baada yahayo hakika kitabu (serikali ya Kiislamu) hiki hakikusudii kuelezea historia ya
serikali ya Kiislamu, bali imekusudiwa kuwaonyesha watu vipi Mtume alivyosimamisha
serikali ya Kiislamu, na vipi kafiri mkoloni alivyoivunja serikali ya Kiislamu na namna gain
Wasilamu wataisimamisha serikali ya Kiislamu, ili ulimwengu urudi na nuru itakao mulika
njia ya uongofu katika giza lilioenea.
NUKTA YA KIANZIO
Pindi alipotumwa Mtume (SAW) alimlingania mkewe Khadija naye akaamini, kisha
akamlingania mototo wa ammi yake Ali nae akaamini, na akamlingania aliekuwa mtumwa
wake Zeid nae pia akaamini, na akamlingania rafiki yake Abubakar nae akaamini, kisha
akawa anawalingania watu akaamini alieamini na akakanausha aliyekanusha. Na pindi
aliposilimu Abubakar (ra) alidhihirisha Uislamu wake kwa yule alie na imani nae na
akaligania kwa Allah na Mtume wake. Na Abubakar alikua ni mtu mwenye ushirikiano na
kipenzi kwa watu wake na ahli, na watu wake walikuwa wanakuja kwake kwa kutaka ushauri
katika zaidi ya jambo moja, kwa sababu ya ujuzi wake na biashara yake na uzuri wake na
kukaa na watu, wakasilimu kupitia mkono wake Athman bin Affan, Zubeir bin Al-Awam,
Abdurahman bin Auf, Saad bin Waqqas na Twalha bin UbeidAllah, na akawaleta kwa Mtume
(SAW) wakti walipomkubalia na wakasilimu na wakaswali kisha akasilimu Abu Ubeidah na
jina lake ni Amir bin Al-Jarrah, Abu salama na jina lake ni Abdallah bin Abu Asad, na Arqam
bin Al-Arqam, Athman bin Madhu'un na wengineo, kisha watu wakawa wanaingia katika
Uislamu wake kwa waume, mpaka ikaenea habari za Uislamu katika Makkah na watu
wakawa waizungumza. Na alikuwa Mtume (SAW) anawazungukia watu katika mwanzo
majumba yao akiwaambia: Hakika Allah amewaamrisha mumabudu yeye na wala
musimshirikishe na chochote" na alikuwa anawalingania watu katika Uislamu katika
Makkah wazi akitekeleza amri ya Allah, amesema Ta'ala: ثُِّر قُْم َفأَنِذْر } -{ يَاأَيَُّها اْلُمدَّ
"Ewe uliejifunika funika - simama uonye" [TMQ Al-Muddathir: 1-2] na alikuwa analingnia watu
akiwaeleza dini yake na anawaunganisha nae juu ya msingi wa dini hii kwa siri, na
maswahaba na Mtume (SAW) wakijificha na watu wao. Na Mtume (SAW) alikuwa anatuma
mtu aliyesilimu mbeleni kuenda kuwafundisha waliosilimu karibuni Quran na dini, kwani
alimtuma Khabbab bin Al-Arat akawafunze Quran Zeinab bint Al- Khattab na mumewe Said,
-
Page 4 of 125
Khabbab aliwafunza Quran, na akasilimu Umar kupitia halaqa hiyo. Na wala hakusimama
hapo bali alijiwekea nyumba akiwafundisha watu Uislamu na akaifanya kama kitovu cha
kikundi hiki cha waumini, na madrasa ya ulinganizi huu mpya, nyumba yenyewe ikiwa ni
nyumba ya Al-Arqam bin Abi Al-Arqam, kwani alikuwa anawakusanya Waislamu ndani yake
akiwasomesha Quran na akiwabainishia, na akiwaamrisha kuidhirisha na kuifahamu, na kila
anaposilimu mtu anamuunganisha na nyumba ya Al-Arqam. Na akakaa miaka mitatu huku
anawajenga Waislamu hawa, na akiwasalisha na akiswali Tahajjud, na akiweka mazingara ya
kiroho kupitia swala na kusoma, na akiwapatia fikra ya kuzingatia juu ya aya ya Allah na
kuzingatia juu ya viumbe vyake, na akiwajenga akili zao kwa maana ya Quran na matamshi
yake, na ufahamu wa Uislamu na fikra zake na kuwahimiza kusubiria maudhio, na kuwajenga
katika kumtii Allah na kuwa wanyenyekevu, ili wamtakasie Allah alie tukuka mweza. Na
Mtume akaendelea kuficha yeye na Waislamu katika nyumba ya Al-Arqam na hatimae
ikashuka kauli yake Allah Ta'ala: }اْصَدْع ِبَما تُْؤَمُر َوأَْعِرْض َعِن اْلُمْشِرِكيَن َف {
"Dhihirisha yale ulioamrishwa nayo na wapuuze washirikina" [TMQ Al-Hijr: 94]
MSHIKAMANO WA MASWAHABA
Na alikuwa rehma na amani ziwe juu yake mwanzo mwanzo alimlingania yule aliye na
matumaini nae kuwa yupo tayari kuukubali ujumbe huu bila ya kujali umri wake na nafasi
yake, na bila ya kujali jinsi yake na asili yake. Na wala hakuwa anabagua watu ambao
anaowalingania katika Uislamu kiubaguzi, bali alikuwa anawalingania watu wote, na
anafuatilia utayarisho wao wa kukubali, na wengi wakasilimu. Na alikuwa na pupa ya
kuwajenga wote ambao wanaoingia Uislamu na hukmu za dini na anawahifadhisha Quran.
Na akawa anashikamanisha hawa na akawabebesha ujumbe, (na ilifika idadi yao tangu
kutumilizwa kwake Mtume (SAW) mpaka alipoamrisha kudhihirisha ujumbe wake kiasi cha
watu arubaini) wakiwemo waume na wake wa mazingara tofauti na miaka, wengi wao
wakiwa ni mashabbab wadogo, na kati yao walikuwemo dhaifu na mwenye nguvu, tajiri na
masikini. Na katika waliomuamini (SAW) na kuwa nae na Kubeba ujumbe pamoja nae
walikuwa ni: -
1:- Ali bin Abi Talib na umri wake ulikuwa ni miaka 8
2:- Zubeir bin Al-Awwam umri wake ulikuwa ni miaka 8
3:- Twalha bin Ubeid Allah nae alikuwa ni mtoto wa miaka 11
4:- Al-Arqam bin Abi Al-Arqam alikuwa ni mtoto wa miaka 12
5:- Abdalla bin Masoud alikuwa ni mtoto wa miaka 14
6:- Said bin Zeid alikuwa chini ya miaka 20
7:- Saad bin Abi Waqqas alikuwa na miaka 17
8:- Masoud bin Rabiah alikuwa na miaka 10
9:- Jaafar bin Abi Twalib alikuwa chini ya miaka 18
10:-Zeid bin Harith akiwa na miaka 20
11:-Athman bin Affan takriban miaka 20
12:- Tuleib bin Umeir takriban miaka 20
13:- Khabbab bin Al-Arat takriban miaka 20
14:- Amir bin Fuheirah akiwa ni mtoto wa miaka 20
15:- Musa'ab bin Umeir akiwa na miaka 23
16:- Musaab bin Umeir akiwa na miaka 24
-
Page 5 of 125
17:- Miqdad bin Al-Aswad akiwa na miaka 24
18:-Abdallah bin Jahash akiwa na miaka 25
19:- Umar bin Al- khatab akiwa na miaka 26
20:- Abu Ubeida bin al-jarrah akiwa na miaka 27
21:- Utbah bin Ghazwan akiwa na miaka 27
22:- Abu Hudhaifa bin Utbah akiwa takriban miaka 30
23:- Bilal bin Rabah takriban miaka 30
24:- Ayyash bin Rabiah takriban miaka 30
25:- Amir bin Rabiah takriban miaka 30
26:- Naim bin Abdallah katika miaka ya 30
27:- Athman takriban miaka 30
28:- Abdallah takriban miaka 17
29:- Qudama takriban miaka 19
30:- As-saib mtoto wa Madhuun bin Habib miaka 20
31:- Abu salama Abdallah bin Abdul Asad al Makhzumiy katika miaka ya 30
32:- Abdurrahman bin Auf takriban miaka 30
33:- Ammar binYassir takriban miaka 30
34:- Abubakar As-Siddiq akiwa na miaka 37
35:- Hamza bin abdul Muttalib akiwa na miaka 42
36:- Ubeida bin al Harith akiwa na miaka 50
Vilevile waliamini wanawake kadhaa, na pindi walipoiva hawa maswahaba katika kuwajenga,
na akliya zao kuwa ni akliya za Kiislamu na nafsiyah zao kuwa ni nafsiyah za Kiislamu kwa
muda wa miaka mitatu, Mtume akaweka matumaini yake juu yao na kuwa na yakini katika
kuiva kwao katika akili zao, na katika kunyanyuka katika nafsiyah zao na akaona kudiriki
kwao na mafungmano na Allah ni yenye kuonekanwa athari yake katika matangamano yao,
nafsi yake ikatulia sana kwa hilo, na kukifanya kikundi cha Waislamu wote hapo
akadhihirisha pindi Allah alipomuamrisha.
KUJITOKEZA KWA ULINGANIZI
Ulinganizi wa Kiislamu ulikuwa wazi tangu siku ya kwanza ya kutumilizwa kwake (SAW) na
katika Makkah watu walikuwa wanajua kua Mohammad analinganiya dini mpya, na wanajua
kua wamesilimu wengi pamoja nae, na wanajua kua Mohammad anawajumuisha maswahaba
wake na kukesha nao, na wanajua kua na kuingia kwao katika dini mpya, yote haya yalikuwa
yanafanya watu walihisi kua kuna ulinganizi mpya na wanahisi kuwepo wanaoamini,
ingawaje walikuwa hawajui ni wapi wanakutana na ni kina nani hao wanaokutana katika
waumini hivyo basi kujitokeza wazi kwa Mtume (SAW) kwa Uislamu haikua ni kitu geni kwa
makafiri wa Makkah, bali kitu kipya kilikuwa ni kudhihirika kwa hichi kikundi cha waumini.
Kwani alisilimu Hamza bin Abdulmuttalib kisha akasilimu Umar bin Al-Khattab, baada ya
kusilimu Hamza kwa masiku tatu, nguvu za Waislamu zikaongezeka na ikamshukia Mtume
(SAW) Kauli Yake Ta'ala: } الَِّذيَن يَْجَعلُوَن َمَع هللاِ إَِلًها آَخَر َفَسْوَف َيْعَلُمونَ - إِنَّا َكفَْيَناَك اْلُمْستَْهِزئِينَ - فَاْصَدْع ِبَما تُْؤَمُر َوأَْعِرْض َعِن اْلُمْشِرِكينَ {
"Dhihirisha yale ulioamrishwa nayo na wapuuze washirikina, bila shaka sisi Tutakutosheleza na wale
wanao kukejeli, wale ambao wanaweka kijungu mwengine pamoja na Allah bila shaka watakuja kujua"
[TMQ Al-Hijr: 92-94]. Hapo Mtume (SAW) akadhihirisha amri ya Allah, na akadhihirisha wazi
-
Page 6 of 125
kikundi kwa watu wote, ingawaje baadhi ya Waislamu walibakia wamejificha, kati yao kuna
waliojificha mpaka Fathi Makkah. Na mbinu ya Mtume (SAW) ya kudhihirisha muungane
huu ni kuwa alitoka na maswahaba wake katika vikundi viwili cha kwanza kikiongozwa n
Hamza bin Abdulmuttalib na cha pii kikiongozwa na Umao bin Al-Khattab, na Mtume
akaenda nao mpaka Al-Kaaba kwa nidhamu ya hali ya juu ambayo waarabu hawajawahi
kuona kabla ya hapo, na akatufu nao Al-Kaaba, na kupitia hilo Mtume (SAW) alihama na
maswahaba wake katika hali ya kujitokeza na katika hali ya maiingiliano ya yule amabaye alie
na matumaini nae kuingia katika hali ya kuwazungumzia watu wote, hapo ikaanaza
mgongano kati ya imani na ukafiri katika mujtama na yakaanza malumbano kati ya fikra
swahihi na fikra fisidifu, na ikaanza safari ya pili nao ni safari ya mvutano na mapambano. Na
makafiri wakaanza kupinga ulinganizi na kumuudhi Mtume (SAW) na maswahaba wake kwa
kila aina ya udhia. Na kipindi hiki kipindi cha mvutano na mapambano ndicho kipindi
kigumu zaidi kinacho julikana katika zama zote, kwani nyumba ya Mtume (SAW) ilipigwa
mawe, na Umm Jamil mke wa Abu Lahab alikuwa anaweka najisi Mbele ya nyumba yake, na
Abu Jahal alikuwa anaweka utumbo wa Mbuzi aliechinjwa kwa ajiliya masanamu na alikuwa
anavumilia udhia na akienda kwa binti yake Fatima alimsafisha na kumtahirisha, hayo
hayakumzidishia ila subra na kudumu katika ulinganizi, na Waislamu walikua wanatishiwa
maisha na kuudhiwa, kwani imethubutu kuwa kila kabila wakiwaadhibu na wakiwafitinisha
Waislamu katika dini yao miongoni mwao, kiasi ambacho mmoja wao alimuweka mtumwa
wake wa kihabashi Bilal juu ya mchanga kwenye jua linalochoma na akaweka jiwe juu ya
kifua chake na kumuacha ili afe sio kwa jingine isipokua kwa sababu alidumu juu ya uislamu,
na katika hali hii haikumzidishia kitu Bilal isipokua ni kukariri neno ahad (mmoja) huku
akisubiria adhabu hiyo katika njia ya Mola wake, na akaadhibiwa mwanamke kwa sababu
hakuridhia kuacha Uislamu kurudia dini ya mababa zake, na walikua Waislamu kwa jumla
wanapigwa na wanaelekezwa njia mbaya zaidi ya unyonge, na walikua wanasubiri yote hayo
kwa ajili ya kutaka radhi za Allah Taala.
KUUPINGA ULINGANIZI
Pindi alipotumilizwa (SAW) na Uislamu watu wakaanza kumzungumza yeye na kuhusu
ulinganizi wake, na makureishi walikua ndio wachache wao katika kuzungumzia, kwa sababu
hawakuwa wanajali ulinganizi na wakidhania kuwa mazungumzo yake hayatazidi
mazungumzo ya makasisi na wasimulizi, na kuwa watuwatairudia dini ya mababa zao na
mababu za, hivyo basi hawakumkimbia na wala hawakumkataza, na pindi alipokua anapita
katika katika mikao yao walikua wanasema kijana huyu wa Abdul Muttalib anazungumziwa
kutoka mbinguni, na akiendelea hivyo, isipokua baada ya kupita muda mchache wa ulinganizi
wake na wakaanza kuhisi khatari ya hunu ulinganizi walikubaliana wote juu ya kumpinga na
kumfanyia uadui na kumpiga vita, na mwanzoni walonelea akumpiga vita kwa kupinga tu
ulinganizi wake juu ya kile anacho dai kuhusu utume wake, baadae wakamuendea kumulizia
miujiza yake ambayo kwayo atathibishia utume wake, na walikua wanasema ni kwa nini
Muhammad haigeuzi milima ya Swafaa na Marwa kuwa ni dhahabu, na wala haiteremshi
kitabu kilicho andikwa kutoka mbinguni kinachozungumza kuhusu yeye, na ni kwa nini Jibril
hajitokezi ili awazungumzie wao kuhusu Muhammad, na ni kwanini hafufui wafu,na wala
hayapeperushi majabali ili Makkah isiwe ni yenye kuzingirwa nayo, na ni kwanini hapasui
maji ya chemchem yaliyo matamu kuliko maji ya zamzam ilhali yeye anajua watu wa mji
wanavyohitajia maji, na ni kwanini Mola wake hamfunulii yeye bei za bidhaa ili tuzikimbilie
-
Page 7 of 125
siku za usoni, na hivi ndivyo wakawa wanampiga mtume na ulinganizi wake kwa mbinu za
kijinga, na hali ikaendelea hivyo, lakini hilo halikumzuia Mtume (SAW) kuendelea na
ulinganizi wake bali aliendelea kuwalingania watu katika dini ya Allah na huku anayakashifu
masanamu kuyaaibisha na kuyakejeli kuzisafihi akili za wanavoviabudu na ndoto zao
wanaoyatukuza, ikawa zito juu yao hilo na hivyo basi wakatumia mbinu zote ili wamzuie na
ulinganizi wake na wala hawakufaulu, na miongoni mwa mbinu muhimu walizozitumia za
kupambana na ulinganizi huu ni mbinu tatu;
1) Kuadhibu 2) Uvumi wa kindani na wa kiinje 3) Vikwazo
Aina za adhabu zilikuwa zikimfikia Mtume rehma na amani ziwe juu yake pamoja na kwamba
ameshikamana na kaumu yake, na juu ya Waislamu wote, kwani zilizotofautiana na mbinu za
kuwaadhibu lakini waliwaadhibu vikali ili waiache dini yao lakini hilo halikuwazidishia ila
uthabiti na imani, na Mtume (SAW) alipita na huku wanaadhibiwa na akawaambiya »يئاً صبراً آل ياسر فإن موعدكم الجنة إني ال أملك لكم من هللا ش «
"Subirini jamii ya Yassir hakika makao yenu ni peponi mimi similiki chochote kutoka kwa
Allah" na hakika jawabu yoyote kutoka kwa Sumayya mke wa Yassir pindi alipowaambiya
hakika makao yenu ni peponi, isipokuwa alisema: "Mimi naiona mbele yangu, ewe Mtume wa
Allah." Na hivi ndivyo makureshi waliendelea kumuadhibu Mtume na maswahaba wake.
Makureishi walipoona kuwa hilo halikufaa wakatumia silaha nyengine nao ni silaha ya
propaganda ya dhidi ya Uislamu dhidi ya Waislamu katika kila sehemu, katika mji wa Makaa
kindani na katika mji wa Habashi kiinje, na wakatumia propaganda katika kila sehemu na kwa
kila kinacho hitajika nacho kama mjadala na huja na kueneza uvumi, na wakatumia
propaganda dhidi ya aqeeda, na kumtuhumu nayo na kuituhumu dhati yake, na wakawa
wanakanusha Mtume, na wakawa wanajiandaa na kila propaganda watakuitumia dhisi ya
Muhammad katika mji wa Makka na nje ya Makka na khususan propaganda katika msimu wa
hijja na makuireishi waliona umuhimu wa kupanga propaganda dhidi ya Mtume (SAW) kiasi
ya kuwa walikusnayika kikundi cha makuresihi kwa Walid bin Mughaira wakishauriana ni
yapi watakaoyasema kuhusu Muhammad kuwaambia waarabu wanao kuja Makkah katika
msimu wa hiujja, baadhi yao wakashauri kuwa waeme kuhusu yeye kua ni kuhani, Al-Walid
akaipinga rai hiyo kuwa anaoyasema Muhammad hayana mfanano wa kuhani, wakashauri
baadhi yao wengine wadai kua Muhammad ni mwandazimu, Al-Walid pia akapinga rai hiyo
kwa sababu hamna ishara kuwa Muhammad anaonyesha ishara ya uendawazimu wake, na
wengine wakaonelea kuwa wamtuhumu Muhammad na uchawi Al-Walid akaipinga rai hiyo
kwa kusema kuwa Muhammad hapigi ramli na wala hafanyi jambo lolote linalihusiana na
uchawi. Na baada ya majadiliano na mvutano, walikubaliana kumtuhumu Muhammad (SAW)
juu ya sihr ul-bayan (uchawi wa maneno). Kisha wakatawanyika katika makundi ya mahujaji
waarabu wakiwatahadharisha kumsikiza Mtume (SAW) kwa sababu yeye ni mchawi wa
maneno na anayosema ni uchawi unaomtenganisha mtu na kakake na mamake, na babake na
familia yake, na inaogopewa kwa yoyote atakae msikiza kurogwa na akatengana na watu
wake. Lakini uvumi huu haukufaa, na wala haikuwa ni kizuizi kati ya watu na ulinganizi wa
Uislamu. Kisha wakamuendea An-Nadhr akawa killa alipokuwa amekaa Mtume (SAW) katika
-
Page 8 of 125
kikao anapolinganiwa katika dini ya Allah nae huja akisimuliya hekaya za mafursi na dini yao,
na anasema, ni kwa lipi Muhammad awe na hadithi nzuri zaidi kuliko mimi. Si yeye anasoma
maandiko ya kale kama ninayosema mimi? Na makuresihi walikuwa wakizichukua hadithi
hizo na kuzieneza kwa watu, vile vile walikuwa wakiyasambaza anayosema Muhammad
kuwa yeye (Muhammad) anafundishwa na kijana wa kinasara aliyekuwa akiitwa Jabr na kua
hayatoki kwa Allah, na wakaeneza sana uvumi huo mpaka Allah akawarudi kwa kusema: } ولُوَن إِنََّما يُعَّلُِمهُ َبَشٌر ِلَساُن الَِّذي يُْلِحُدوَن إِلَْيِه أَْعَجِميٌّ َوَهذَا ِلَساٌن َعَرِبيٌّ ُمبِينٌ َولَقَْد َنْعَلُم أَنَُّهْم يَقُ {
"Hakika Tunajua kuwa wao wanasema:'Yeye anafundishwa na mwanadam'. Ulimi wa yule
wanaemsingizia ni wa kiajemi na huu ni ulimi wazi wa kiarabu" [TMQ An-Nahl 103] na hivyo
ndivyo uliendelea uvumi wa makureishi ndani ya bara arabu. Na wala hawakukoma hapo bali
wakti waliposikia kuwa Waislamu wamegura kwenda Habash waliwatuma wajumbe wao
wawili ili waeneze uvumi dhidi ya Waislamu kwa Najashi ili awatoe katika biladi yake. Na
wajumbe hao wawili walikuwa ni Amru bin Al-Aas na Abdallah bin Rabiah. Hivyo basi
walifika Habash na wakampelekea zawadi generali wa Najash ili awasaidie kuwarudisha
Waislamu Makka, na wakakutana na Najashi na wakamwambia, " Ewe mfalme wamekuja
katika biladi yako vijana masafihi kutoka kwetu waliojitenga na dini yao ya kaumu yao na
wala hawakuingia katika dini yako na wamekuja na dini waliozusha, hatuijui sisi wala wewe,
na tumekuja kwako na watu wao watukufu miongoni mwao mababa zao maami zao na
familia zao ili uwarudishe kwani sisi tutawaangalia wao zaidi na twaelewa zaidi kasoro yao".
Najashi akataka kuwasikia Waislamu wanaoyasema kuhusiana na hayo, na akutamana
wakaitwe na walipoitwa aliwaulizwa, "Ni dini ipo hiyo amabo mumetengana na kaumu yenu
na wala hamukuingia katika dini yangu wala katika dini nyengineo"? Akajibu Jaafar bin Abi
Twalib, akaielezea hali zao katika zama za kijahiliyya na tabia walizo kuwa nazo, na kisha
akaelezea uongofu ambao Uislamu umekuja nao, na hali ilivyogeuka baada ya kusilimu kwao,
kisha akaeleza kuadhibiwa kwao na makureshi (na walipo tushinda nguvu na kutudhulumu
na kututia dhiki na wakawa ni kizuizi kati yetu na dini yetu, tukatoka kuja katika biladi yako,
na tukakuchagua wewe na kuwawacha wengine na tukapendelea kuwa jirani yako na
tukatarajia tusiwe ni wenye kudhulumiwa hapa kwako) Najashi akasema kumuambia Jaafar,
"Je, kuna kitu alichokuja nacho mjumbe wenu kutoka kwa Allah unisomee? Jaafar akasema,
"Ndio" Jaafar akasoma sura ya Maryam kwanzia mwanzo wake mpaka katika kauli yake
Ta'ala ]ُم َم]ْن َك]اَن ِف]ي اْلَمْه]ِد َص]بِيZا{ َوَجعَلَِن]ي ُمبَاَرًك]ا أَْي]َن َم]ا ُكن]ُت -َق]اَل إِّنِ]ي َعْب]ُد اَل]ِه آتَ]اِنَي اْلِكتَ]اَب َوَجعَلَِن]ي نَبِيZ]ا - فَأََشاَرْت إِلَْيِه قَالُوا َكْي]َف نَُكّلِ
َكاِة َما ُدْمُت َحيZا الَِة َوالزَّ }َوالسَّالَُم َعَليَّ يَْوَم ُوِلْدُت َويَْوَم أَُموُت َويَْوَم أُْبَعُث َحيZا -ا بَِواِلَدِتي َوَلْم يَْجعَْلِني َجبَّاًرا َشِقيZا َوبَرZ -?َوأَْوَصاِني بِالصَّ"Maryam akaashiria kwake (Motot) wakasema itawezekanaje kuzungumzia na mtoto mchanga-akasema
(motto) hakika mimi ni mja wa Allah amenipatia Kitabu na akanijaalia Utume na akanijaalie ni mwenye
popote ulipo na akanuusia na swala na zake madamu ni hai na nimtendee wema mamangu na wala
hakunifanyia jabari muovu na amani iwe juu yangu siku siku nilio zaliwa na siku nitakao kufa na siku
nitakaofufuliwa kuwa hai" (TMQ Maryam 29:33) Na aliposikia generali haya maneno, alisema
"maneno haya yanatoka katika chimbuko lile ambalo yalipotoka maneno ya bwana wetu yesu
masihi na Najashi akasema: "Haya na hayo aliokuja nayo Issa yanatoka mshumaa mmoja."
Kisha akawaelekea wajumbe wawili wa kikureishi na kuwaambia: "Nendeni, Wallahi
sitowasalimisha kwenu." Na wakaondoka wajumbe wawili katika ikulu ya Najashi na wakawa
wanafikiria njia nyengine, na ilipofika siku ya pili Amru bin Al-Aaas alirudi kwa Najahi na
akawambia: "Waislamu wanasema maneno maovu kuhusu Issa mwana wa Maryam". Najashi
akatumana Waislamu waitwe na kuwauliza, Jaafar akasema: "Tutasema kuhusu yeye yale
aliokuja nayo Mtume wetu, anasema: "Mja wa Allah na Mtume wake na roho yake na neno
-
Page 9 of 125
lake aliyoiweka kwa Maryam bikira aliebarikiwa." Najashi akaishika fimbo na akachora nayo
mstari juu ya ardhi na kumwambia Jaafar "Hapana kati ya dini yenu na dini yetu zaidi ya
mstari huu." Na wakaondoka wajumbe wa kikureishi na wakarudi kwao mikono mitupu.
Hivyo ndvyo zilivyoanguka propaganda na nguvu ya haki ambayo Mtume rehma na amani
zimshukie anailingania ilikuwa katika sura ya wazi ambayo inaotoka katika ulimi wake
inaolea juu ya uvumi wote, na nuru ya Uislamu inaoaangaza inazima diaya zote na uvumi. Na
wakaanza makuresihi kutumia silaha ya tatu nao ni silaha ya vikwazo, na wote
wakakubaliana kumwekea vikwazo Mtume (SAW) na familia yake na wakaandika mkataba
waliokubaliana ndani yake juu ya kuiweka vikwazo baina Hashim na Banu Abdul-Muttalib
kuwatenga kamili wasiolewe wala wasiozeshwe kusinunuliwe kwao na wala wasiuziwe. Na
wakabandika mkataba huo kwenye ukuta wa Kaaba, kwa kusisitizia na kuwakumbusha, na
wakadhania kua siasa hii ya vikwazo itakuwa ni yenye athari zaidi kuliko ya kuadhibu na
uvumi. Na wakaendelea vikwazo hivyo kwa muda wa miaka miwili au miaka matatu, na
huku wakiwa wanangoja banu Hashim na Banu Abdul-Muttalib wamwache Muhammad
(SAW) na Waislamu wauuache Uislamu wao ili Muhammad (SAW) abakie pekee, nae imma
arudi nyuma na ulinganizi wake au kusiwe na tishio lolote la ulinganizi wake juu ya
makureshi na juu ya dini zao, na hili halikumzidishia Mtume (SAW). Isipokuwa ni mwenye
kushikamana na kamba ya Allah na ni menye kushikamana na dini ya Allah na kumzidishia
hamasa katika njia ya ulinganizi kwa Allah, na wala hawakuzidi waumini walio kuwa pamoja
nae Isipokuwa ukakamavu na nguvu na wala hawakuwa ndio kizuizi cha kuenea ulinganizi
wa Uislamu katika Makka na nje ya Makka, na habari ya vikwazo vya makuresihi kumuekea
Muhammad ikawafikia waarabu nje ya Makka na habari ya ulinganizi ikaenea kwa makabila,
na habari ya Uislamu ukawa unaenea katika bara arabu. Na wasafiri wakawa wanazungumza,
Isipokuwa vikwazo viliendelea na maumivu ya njaa iliendelea, na mkataba ambao uliowekwa
na makureshi ni wenye kuendelea. Na akabakia na watu wake katika vichaka vya Makka
wakiwa wanumizwa na njaa na ukosefu na ufukara. Na mara nyingi hawakuwa ni wenye
kupata kinacho tosheleza mahitaji yao, vile vile hawakuwa na fursa ya kutangamana na watu
na wenye kuwazungumzisha, isipokuwa katika miezi mitukufu Mtume (SAW) alikuwa
anakwenda upande wa Al-Kaaba akiwalingania katika dini ya Allah na kuwapa biashara ya
thawabu zake na kuwaonya na adhabu zake, kisha anarudi vichakani. Na hili lilikuwa likileta
sikitiko kwa waarabu juu yao na miongoni mwao walikuwa wakikubali ujumbe wake, na
miongoni mwao walikuwa wakiwapeleka chakula na kinywaji kwa kujificha, Hisham bin
Amru alikuwa anachukua ngamia aliebebeshwa chakula na ngano na anakwenda nae kati kati
ya usiku mpaka anapofika vichakani, hapo anawachilia kamba yake kisha anampiga ubavuni
mwake ili aende vichakani na wanachukua alichobeba, na kumchinja na kula nyama yake, na
wakendelea katika hali hiyo kwa muda wa miaka matatu mfufulizo mpaka dunia ikawa ni
dhiki kwao mpaka Allah alipoileta faraja yake na vikwazo vikaisha. Na hayo ni kutokamana
na vijana watano wa kikureshi nao ni Zubeir bin Abi Umayya na Hisham bin Amru na Mutim
bin Adiq na Abu Bukhtiriy bin Hisham na Zama'a bin Al-Aswad walikusanyika na
kuzungumzia kuhusu mkataba na suala la kikwazo, na miongoni mwao wakalipinga na
kudhihirisha chuki zao kwa baadhi yao, na wakakubaliana na kuweka ahadi ya kufanya jambo
ambalo litapeleka kuvunjika kwa mkataba na kuurarua, siku ya pili walikwenda hadi Al-
Kaaba akaja Zuheir akatufu mara saba kisha akawaita watu "Enyi watu wa Makka sisi
tunakula na tunavaa na huku Banu Hashim wanaangamia hawauzi wala hawauziwi, wallahi
-
Page 10 of 125
sitokaa mpaka uraruliwe huu mkataba wa vikwazo wa kidhalimu. Hakuwacha kusema mpaka
Abu Jahl akasikia na akampigia mayowe" Umedanganya wallahi usirarue, kwa upande wa pili
Kaaba walikuwepo Zama'a na Abu Al-Bukhtiriy na Mutim na Hisham wote hawa wakapiga
makelele huku wakimghadhabisha Abu Jahl na kumtia nguvu Zuheir. Abu Jahl akafahamu
kuwa hili limepangwa usiku na kuwa watu wanakubaliana nao na kuwa khalifu kwaweza
kuzua shari hivyo basi nafsi yake ikaingiwa na uoga na hapo akarudi nyuma. Na Mutim
akasonga Mbele ili auraruwe mkataba, na akaupata kuwa umeliwa na mchwa isipokuwa
ufunuzi wake (Kwa jina lako ewe Mola – Bismika Allahumma) na hilo likampatia nafsi Mtume
(SAW) na maswahaba wake warudi Makka kutoka vichakani na vikwazo visitishwe, hapo
wakarudi na Mtume akaendelea na ulinganizi wake, hivi ndivyo zilivyo anguka mbinu za
makureishi katika kuadhibu na uvumi na vikwazo na wala hazikuweza kufitini Waislamu na
dini yao, wala kumrudisha Mtume na ulinganizi wake na hatimae Allah Ta'ala akaifanya ni
yenye kudhihiri pamoja na vizuizi vyote na vizingiti.
MAINGILIANO YA ULINGANIZI
Mapambano ya makureishi na ulinganizi wa Kiislamu ilikuwa ni jambo la kawaida, kwa
sababu yeye Mtume (SAW) alibeba ulinganizi na kudhihirisha kikundi ambacho kinabeba
ulinganizi pamoja nae kwa sura ya mapambano na mvutano, juu ya hayo ulinagnizi wenyewe
kwa dhati yake ililazimisha kupambana na makuresishi na mujtama katika mji wa Makka kwa
sababu ilikuwa inalingania kumpwekesha Allah na kumuabudu yeye tu pekee, na kuwacha
kuabudu masanamu na kuingoa nidhamu fisidifu ambayo wanaishi nayo, hivyo basi
ikagongana na makureishi mgongano kamili, na jee yawezekana kwa Mtume (SAW) asiwe ni
mwenye kugongana na makureishi ilhali yeye anazisafihi ndoto zao na kudharau miungu yao
na kukejeli maisha yao ya kirahisi, na kukashifu njia yao kimaisha ya kidhalimu. Inamshukia
Quran ikiwahujumu na huku ikiwaambia parwanja: }إِنَُّكْم َوَما تَْعبُُدوَن ِمْن ُدوِن هللاِ َحَصُب َجَهنََّم {
"Nyinyi na munaoviabudu kinyume na Allah ni kuni za moto" [TMQ Al-Anbiyaa: 98]. Kisha
anaihujumu riba ambayo kwao wanaishi nayo akiwahujumu kwa ukali kutokamana na msingi
wake. Amesema Ta'ala katika sura ya Al-Rum: }َوَما آتَْيتُْم ِمْن ِربًا ِليَْربَُوا ِفي أَْمَواِل النَّاِس فَالَ يَْربُوا ِعْنَد هللاِ {
"Na kile mnacho kitoa ili kuchukua riba katika mali ya watu basi hakiongezeki Mbele ya Allah" [TMQ
Ar-Rum: 39]. Na anawakemea wale ambao wanaopanga katika uzito na mizani. Amesema
Ta'ala: َوإِذَا َكالُوُهْم أَْو َوَزنُوُهْم يُْخِسُروَن } -الَِّذيَن إِذَا اْكتَالُوا َعلَى النَّاِس َيْستَْوفُوَن -َوْيٌل ِلْلُمَطّفِِفيَن
"Ole wao hao wanaopunja ambao wanaponunua kwa watu wanatimiza na wanapopima hupunguza"
[TMQ Al-Mutafiffin: 1-3]. Na kwa sababu hiyo wakawa wanampinga na wakimuudhi yeye na
maswahaba wake mara kuwaadhibu, na mara nyengine kuwawekea vikwazo na kwa kueneza
uvumi dhidi yake na dini yake. Isipokuwa yeye aliendelea kuwahujumu na aliendelea
kugonga rai potofu, na kuvunja aqeeda fisidifu na kufanya juhudi katika njia ya kueneza
ujumbe. Na alikuwa anaulingania Uislamu kwa uwazi wala harudi nyuma na wala
kutaradhilia na wala kuhadaa, juu ya yale yalimkumba aina za adhabu kutoka kwa
makureishi, pamoja n mashaka yaliomsibu, juu ya kuwa alikuwa ni pekee mnyonge hana
msaidizi wala mwenye kumnusuru, hana chochote wala silaha kwani yeye alikuja kwa njia
wazi na mapambano, akilingania dini ya Allah kwa nguvu na Iman, wala hakuingiwa na
udhaifu wowote wa Kubeba majukumu ya ulinganizi na kutekeleza majukumu makubwa kwa
ajili yake, yote hayo yakawa ndio sababu kwa ajili yake, hayo yakawa ndio sababu za kuvuka
-
Page 11 of 125
vizingiti vyote ambavyo makureishi walivyomuekea mbele yake ili kumzuia yeye kuwafikia
watu. Na Mtume (SAW) aliweza kuwafikia watu na akawafikishia, na wakakaikubali dini ya
Allah, na nguvu ya haki ikawa ipo juu ya batili, na nuru ya Uislamu ukawa unazidi kila siku
kuenea kati ya waarabu, wakasilimu wengi waliokuwa wakiabudu masanamu na katika
manasara, bali mabwenyenye na kikureishi wakawa wanaisikiza Qur'an na mioyo yao
kuhuzunika.
Tufail bin Amru Ad-Dawsi alikuja Makka na alikuwa ni mtu mtukufu mwenye akili,
makureishi wakamuendea kumtahadharisha kuhusu Muhammad na kua maneneo yake ni
kama uchawi yanyomtenganisha mtu na watu wake na kuwa wao wanamroga na kaumu yake
mfano ya wale waliowapata wao Makka, na kuwa bora asiwe ni mwenye kumzungumzisha na
wala asimsikize. Siku moja Tufeil alikwenda katika Al-Kaaba na Mtume (SAW) alikuwa hapo
na hatimae akasikia maneno yake nayakawa ni maneno mazuri na akaiambia nafsi yake
"Wallahi mimi ni mtu mwenye akili mshairi, mimi siwezi kuchanganyikiwa na kizuri katika
kibaya basi ni kipi kinacho nizuia kumsikiza mtu anaoyasema, iwapo ni mabaya nitayawacha"
na akamfuata Mtume (SAW) mpaka nyumbani kwake kisha akajitambulishe na akaeleza
yaliomo moyoni mwake, hapo Mtume (SAW) akamuelezea kuhusu Uislamu na akamsomea
Quran hapo akasilimu na kutammka shahada ya haki, na akarudi kwa kaumu yake
akiwalingania Uislamu.
Na Mtume (SAW) alipokuwa Makka alijiwa na watu ishirini wa kinasara wakati walipofikiwa
na habari zake, na wakakaa nae na wakamsikiza, na wakamuitikia na wakamuamini na
wakasadiki jambo lililowaudhi makureishi mpaka wakawatukana na kuwaambia: "Allah
awaangamize ni watu aina gani nyinyi, watu wenu wamewatuma ili muwaletee habari za mtu
huyu na pindi tu mlipokaa nae mukaiwacha dini yenu na mkayaamini aliyoyasema". Na
hawakurudishwa nyuma na maneno waliyoyasema makureishi katika kufuata Mtume na wala
hawakurudi nyuma na Uislamu bali liliwazidishia imani kwa Allah juu ya imani yao. Na
hivyo ndivyo ilivyo dhihiri ulinganizi wa Mtume na ikazidi shauku ya watu ya kusikiza
Quran kiasi ambao hata wale ambao ni maadui zaidi wa kikureishi wakawa wanaulizana, "Je,
ni ukweli analingania dini ilionyoka na anayowaahidi na kuyaonya nayo ni sahihi? Maswali
haya yakawapelekea kunyanyapa na kuenda kuisikiza Quran. Alitoka usiku mmoja Abu
Sufyan bin Harb, Abu Jahl, Amri bin Hisham na Akhnas bin Shariq ili wamsikize Muhammad
(SAW) akiwa nyumbani mwake, na Muhammad (SAW) alikuwa anasimama usiku Isipokuwa
analala kidogo akisoma Quran huku wakisikia aya za Allah, mioyo yao na nafsi zao
zikaathrika, na wakawa wamenyamaa mpaka alfajiri, na wakaondoka kurudi nyumbani
mwao, wakakutana njiani na wakaanza kulaumiana na wakaambiana musirudie kwani
mukionekanwa na wengine walio wajinga mambo yenu yatadhoofika mbele yao na
Muhammad atawashinda, na ilipofika usiku wa pili, kila mmoja alijiskia kwenda ile sehemu
aliukuwepo jana ni kana kwamba miguu yake pasi na yeye kuweza kujizuia kufika pale
alipokuwepo usiku wa jana, na ili amsikize Muhammad tena upya, na wala haikuwa kizuizi
kulaumiana kwao ya kuenda usiku wa tatu na walipofahamu udhaifu wao kwa ulinganizi wa
Muhammad waliahidi wasirudie waliofanya, na wakawacha kwenda kumsikiza Muhammad
(SAW) lakini walioyasikia usiku tatu yaliwacha athari katika nafsi zao iliwafanya waulizane
baina yao kuhusu yale walioyasikia, na wote wakaingiwa na wasiwasi katika nafsi, na
anahofia asije akadhoofika na yeye ni kionozi wa watu wake wakamfuatia Muhammad
-
Page 12 of 125
(SAW). Na hivi ulienea ujumbe kila sehemu pamoja na kwamba vizingiti walivyoviweka
mbele yake, hilo liliwaudhi sana makureishi na ikazidi hofu yao ya kuenea ujumbe kati ya
makabila ya kiaarabu baada ya kuenea Makka, na wakazidi kuwaudhi maswahaba wake, na
wakawa wanaendelea kuzidi kuwaudhi, na kuongeza hasira zao kwa maswahaba mpaka
ikawa dhiki kwao. Hapo akatoka kuelekea Taif na kutarajia Uislamu wao, lakini
wakamrudisha kwa jawabu ilio mbaya zaidi, na wakatoa vijana wao na wandazimu wao na
kumtukana na wakampiga kwa mawe mpaka miguu yake yakaloa damu, akawatoroka na
kurudi mpaka alipofika kwenye bustani la zabibu la Utbah na Shaibah watoto wa Rabiah
akawa anafikiria kuhusu nafsi yake na ulinganizi wake, kwani alikuwa hawezi tena kurudi
Makka Isipokuwa chini ya ulinzi wa mmoja wa mabwenyenye wa Makka mushrikina, na wala
hawezi kwenda Taif baada ya mateso yaliomkumba, na wala hawezi kubakia hapo kwa
sababu bustani ni la watu wawili washirikina, hapo wasiwasi ukazidi na akanyanyua kichwa
chake mbinguni akimshtakia Allah katika hali ya maumivu makubwa, na katika hali ya imani
na kutaka radhi zake, na akawa anaomba dua hii: أللهم إليك أشكو ضعف قوتي وقلة حيلتي وهواني على الناس, يا أرح]م ال]راحمين أن]ت رب المستض]عفين وأن]ت رب]ي, إل]ى م]ن تكلن]ى, «
إن لم يكن بك علي غضب فال أبالي, ولكن عافيتك هي أوس]ع ل]ي. أع]وذ بن]ور وجه]ك أل]ذي إلى بعيد يتجهمني, أم إلى عدو ملكته أمري,ى ترض]ى, وال ح]ول وال ليه أمر الدنيا وآلخرة, من أن تنـزل بي غضبك, أو يحل علي سخطك, لك العتبى حتأشرقت له الظلمات, وصلح ع
»قوة إال بك "Ewe Mola kwako wewe nalalamikia udhaifu na nguzo zangu na uchache wa maarifa yangu
na unyonge wangu kwa watu, ewe mwingi wa rehma mwenye kurehemu wewe ndie Mola
wa wanyonge na wewe ndie Mola wangu, waniegemeza kwa nani, kwa wa mbali, atake
nihujumu, au kwa adui ulemilikisha mambo yangu, iwapo huna ghadhabu juu yngu basi
mimi sijali, lakini msamaha wako ndio mkunjufu kwangu. Najilinda kwa nuru ya dhati
yako ambayo imeangazia kiza, na kutengea kwao mambo ya dunia na akhera isije
ikanishukia mimi ghadhabu zako au kufikiwa na hasira zako, ni wewe wa kufanyiwa
mpaka uridhike, wala hamna uwezo wala nguvu Isipokuwa kupitia wewe". Kisha akarudi
Makka katika ulinzi wa Muti'im bin Adiy, na makureishi walijua yaliyomfikia Muhammad
katika mji wa Taif, hivyo basi wakazidisha mateso na wakazidisha vitimbi vyao juu yake, na
wakawa wanawakanya watu kumsikiza, na watu wa Makka wakawa wanajiepusha nae na
kumpuuza, hilo halikumfanya kuwacha kulingania dini ya Allah, na akawa anazungukia
makabila ya waarabu katika msimu wa hijja anawlaingania katika Uislamu, na anawaeleza
kuwa yeye Mtume aliiyetumwa, na kuwataka wamuamini, isipokuwa ammi yake Abdul-
Uzzah bin Abdul-Muttalib, Abu Lahab hakuwa akimwacha bali alikuwa anamfuata
anakoenda na akiwahimiza wasiwe ni wenye kumsikiza, hilo likawaathiri na wakawa
wajiepusha kumsikiza Mtume (SAW) akawa anayaendea makabila katika majumbani mwao,
na kuwaelezea, na akawaendea Kinda katika majumba yao na akawaendea Kalb katika
majumba yao na akawaendea Bani Hanifa na Bani Amir bin Saa' saa', hamna kati yao,
aliemsikiza na wakamrudisha kusiko kuzuri, bali Bani Hanifa walimrudisha kwa ubaya. Ama
Bani Amir bin Saa' Saa' wakafanya tamaa iwapo atashinda utwala uwe kwao baada yake, na
pindi alipo waambia, utawala ni wa Allah anauweka anapotaka, wakamgeuzia nyuso zao na
wakamrudisha kama walivyomrudisha wengine. Na hivi ndivyo Makka ilipuuza Uislamu na
watu wa Taif kumpuuza Mtume (SAW) na makabila walivyo urudisha ujumbe wa Mtume
(SAW) na makabila ambayo yanaokuja Makka kuhiji yaliona ule upweke aliokuwa nao
Muhammad na namna makureishi walivyomzingira na uadui, ilifanya kila msaidizi kuwa ni
adui kwake na wasaidizi kwao, na wakazidi kumpuuza na hilo lilimzidisha Mtume (SAW)
-
Page 13 of 125
upweke, na ulinganizi ukwa mgumu katika Makka na pambizoni mwake na kujtamaa wa
Makka ukajitokeza kwa ukafiri na inadi, jambo ambalo linalofanya matarajio kudhoofika.
MIZUNGUKO MIWILI KATIKA MIZUNGUKO YA ULINGANIZI.
Katika mji wa Makka Mtume (SAW) alifuata mizunguko miwili mfululizo, dori ya kwanza ni
kufundisha na kujenga na matayarisho ya kifikra na ya kiroho, na dori ya pili ikiwa ni dori ya
kuzihamisha hizi fikra kwa nguvu za msukumo katika mujtama itakao usukuma ili
wazitabikishe katika nyanja za kimaisha kwa sababu fikra hubakia kuwa ni malumati
madamu hazijatabikishwa, na hamna tofauti hizi fikra ziwe katika vitabu au katika mabongo
kwani zitakuwa zimefungika katika sehemu, hivyo basi fikra hazitakuwa na thamani iwapo
hazitatabikishwa katika maisha. Na fikra ili ziweze kutabikishwa ni lazima zipitie dori ya
kuzibadilisha kutoka katika fikra na kuingia katika nguvu itakao wasukuma watu, ili watu
jumla waziamini na kuzifahamu na kuzibeba na kupambana ili zitabikishwe, na wakati huo
utabikishaji wake itakuwa ni jambo lisilo na shaka na la kikawaida. Na hivi ndivyo Mtume
(SAW) aliupeleka ujumbe katika Makka katika dori hizi mbili, ama dori ya kwanza ni
kuwalingania watu katika Uislamu, na kuwajenga kwa fikra na kuwafunza hukmu zake na
kuunganishwa yule anaeweza kuunganishwa juu ya aqeeda ya Kiislamu na dori hii ni ni dori
ya kuunganisha kisiri katika dawah. Na hilo ni kwa saabu Mtume (SAW) alikuwa hadharau
ulinganizi na kuwa na bidii ya kumjenga kifikra kila anaeingia katika Uislamu, na
anawakusanya katika nyumba ya Al-Arqam, na kumtuma yule aliemjenga kujenga katika
halaqa, na wakajumuika Waislamu katika majumba yao kisiri na majabalini kwa siri na katika
nyumba ya Arqam kwa siri na wakajengwa, na kila siku kuzidi imani yao na kuongezeka
maingiliano yao, na kila siku kuzidi kufahamu umuhimu ambao wanaobeba, na kujitayarisha
kujitolea katika njia hiyo mpaka dawah ikakita katika nafsi zao, na Uislamu ukawa unatembea
ndani yao kama damu katika viwiliwili vyao, na wakawa ni Uislamu unatembea katika
mabarabara. Na kwa ajili hiyo haukuweza ujumbe kubakia umefungwa katika nafsi zao
pamoja na kujificha kwao pamoja na kujengwa kwa kisiri na kufanya bidii ya kuficha
kujumuika kwao, na wakawa wanawazungumzia wanaowaamini na kwa kila yule
wanaomtarajia kuwa yuko tayari kuukubali ujumbe, na kwa sababu hiyo watu walihisi
ulinganizi wao, na kujua kuwepo kwao, na kwa hila ukatambulika ujumbe kama nukta ya
kianzio, na ikawa hamna budi kutoka, na yakapatikana majaribio ya kuingiza na
kuwazungumzia watu wote, na kwa hilo lilimalizika dori ya kwanza ikiwa ni dori ya
kuwaunganisha kisiri na kuwajenga ambao umejenga muungano huu, na ikawa hamna budi
kuingia katika dori ya pili ikiwa ni dori ya mapambano na mvutano kwa kuwafahamisha watu
Uislamu ili waviitikie pamoja nao na kuukubali na kutangamana nao, au waukatae na
waubebe na kugongana kwa fikra zake, na yatapatikana kwa mgongano huu ni kuwa ukafiri
na usidifu vishindwe na itulie imani na matengeneo, na fikra sahihi kushinda, kwa sababu
akili namna zitakavyo kanusha lakini haitoweza kufungika mbele fikra sahihi, wala haziwezi
kuzikataa, hata kama walijaribu kuzitoroka ili zisiathiriwe. Na hivi ndivyo ilivyoanza dori ya
mapambano na kwao kuanza mvutano baina ya fikra mbili, baina ya Waislamu na makafiri,
lilionekana kwa hilo muungano wa kichama pindi alipotoka Mtume (SAW) pamoja na
maswahaba wake katika mpangilio ambao waarabu hawajauonapo kabla yake, na katika
mshikamano mmoja, na akatufu nao Al-Kaaba na kudhihirisha ujumbe wake. Na kuanzia
wakati huo Mtume (SAW) akawa anaeneza ujumbe baina ya watu wote parwanja mchana kwa
njia ya kupambana na kuwachalenji. Na zikawa aya zinamshukia Mtume (SAW)
-
Page 14 of 125
zinazolingania Tauhid, na kukanusha masanamu na shirki na kuyahujumu na kukemea
kufuata mababa na mababu pasi na muelekeo, na zikawa zinashuka kuhujumu maamiliano
fisidifu na zikihujumu riba, na kuhujumu biashara chafu na kufanya hila katika kupima na
mizani, na Mtume akawa anawazungumzia watu Uislamu kwa makundi, alikuwa anawaalika
chakula watu wake nyumbani kwake na akiwazungumzia waote kwa pamoja, na anawataka
wasilimu na kumuunga mkono na wakamkataa vibaya, kisha wanawakusanya watu juu ya
safaa na anawazungumzia, na mabwenyenye wa kikureishi wanakasirika na Abu Lahab
kumrudi vibaya mno, na chuki ya makureishi kuongezeka, na kwa Mtume Muhammad (SAW)
vile vile kuongezeka chuki baina yake na waarabu wengine wasiokua Makuresihi, na hivi
ndivyo ulinganizi inavyojumuisha kujenga kupitia halaqa katika majumba na katika majabali
na katika nyumba ya Al-Aqram kujengwa kijumla, na kutoka kulingania yule anaetarajiwa
kuwa yuko tayari na kuingia kulingania watu wote, na ulinganizi huu wa jumla na kujenga
kwa pamoja ulikuwa na athari katika makureishi, kwani ilizidisha chuki yao na kuhisi hatari
inaokuja, na wakaanza kuchukua hatua mpya Muhammad wala ulinganizi wake, na wakazidi
kumuudhi na kumkaandamiza Mtume (SAW) na maswahaba wake. Lakini hunu ulinganizi
wa kijumla ulikuwa na athari katika ulinganizi wenyewe, kwani wote walisikia neno Uislamu
na ukaenea ulinganizi kwa dini ya Allah kati ya watu wote wa Makka, na wala hamna siku
isipokuwa alisilimu mmoja wao kwa ajili ya Allah na radhi zake, na akaamini kila maskini na
kila mnyonge na kila fakiri, na kila ambae habaishwi na biashara wala hababaishwi na kuuza
na kudhrau kwa anaowalinhania kwao Mtume (SAW), na wakaamini baadhi ya wafanyi
biashara wa Makka na watukufu wake na viongozi wao, katika wale ambao nafsi zao
zilitambua usafi, hima na ukweli na kujiepusha na kiburi na kujigamba, hawa walisilimu kwa
ajili ya Allah kwa ujua tu ukweli wa ulinganizi na ukweli wa mlinganizi, na Uislamu ukaenea
Makka na watu wakaingia katika Uislamu waume kwa wake. Na ulinganizi wa jumla ulikuwa
na athari pana, japo liliwapelekea katika mashaka na adhabu na kuwaka katika nafsi za
mabwenyenye wa kikureishi kwa sababu Mtume kuhujumu dhulma na uovu na kumtenga
ambao ulikuwa umeenea Makka kukashifu kwake hali za makafiri na mambo yao. Na ikaanza
baina ya Mtume wa mswahaba wake na baina makafiri wa kikureishi marhala uilio mgumu
zaidi na dori ilio mbaya zaidi. Japokuwa ilikuwa ni kuingia katika dori ya mapambano kutoka
kwa dori ya kujenga japo ni dori nyembamba zaidi kwa sababu inahitaji hikma subra na
umakini wa utekelezaji, hivyo basi dori ya mapambano ndio dori ngumu zaidi kwa sababu
inahitaji uwazi wa kujitolea bila ya kujali natija na matokeo, kwani itapatikana kufitini kwa
makafiri kwa Waislamu juu ya dini yao, na pia hudhihirika imani nguvu ya kustahamili na
kudhihirika yaliomo katika nafsi kama ukweli wa kukutana, na hivi ndivyo alipitia Mtume
(SAW) katika dori hii yeye pamoja na mswahaba wake wakivumilia aina ya majabali
makubwa ya dhulma maonevu kunyanyaswa na kukandamizwa, miongoni mwao waliougura
Habash ili kuhifadhi dini yao, miongoni mwao waliouwawa kwa kuadhibiwa na miongoni
mwao waliovumilia aina kali za adhabu, na walioendelea hivyo kwa muda mrefu waliokuwa
unatosha kuathiri mujtama wa Makka kwa nuru ya Uislamu na kuondosha dhulma pamoja n
akwa Mtume (SAW) alikaa miaka matatu katika nyumba ya Al-Arqam na kumaliza dori ya
kwanza ikiwa ni dori ya kuunganisha na kujenga kisiri kwa muda wa miaka hii mitatu pia,
aliishi Mtume (SAW) miaka minane mengine huku anapambana na (miujiza ikiidhihirikia
watu) juu ya hayo haikusahilisha njama za makureishi za kuadhibu Waislamu wala
kusahalisha hamasa zao katika kuupinga Uislamu, naam hayo yalikuwa kutokamana na
Waislamu kuvutana na makureishi mpaka bara arabu nzima ikasikia kuhusu Uislamu, na
-
Page 15 of 125
mazingira ya dawah yakaenea katika sehemu zote za bara arabu, ilipopelekwa na mahujaji na
wakawa wanaizungumza, lakini hawa waarabu walikuwa wamesimama msimamo wa
watazamaji, na wala hawakuchukua hata hatua moja kusongelea iman, bali walikuwa
hawataki kuwaudhi makureishi, na wajiepushe na Mtume (SAW) ili makuresihi wasikasirike.
Likawa zito hilo kwa Mtume (SAW) na mswahaba wake na kudhihirika kwa dori ya
kujitokeza ina dori ya tatu nao ni utabikishaji wa Uislamu hauna budi nao, lakini uovu wa
mujtama katika Makka hauoneshi dalili ya uwezekano wa kutabikisha, na kuendelea
maudhuijuu ya Waislamu liliwazuia wao kujitolea kamili kwa ajili ya Dawah bali kuwa
kizuizi baina yao na baina yake, na watu kupuuza dawah hayo yaliwazidisha maumivu na
huzuni.
KUUPANUA UWANJA WA DAWAH
Yaliongezeka mateso ya makuresihi kwa Mtume (SAW) kwa kuwa Waislamu mpaka ikawa ni
dhiki kwao, na hapakubakia na matarajio ya makabila kumnusuru yeye baada ya Thaqif
kumrudisha na majibu mabaya, na baada ya kurudishwa na Kinda na Kalb na Banu Amir na
Banu Hanifa wakati alipowaendea katika msimu wa hijja, na hapakuwa na matumaini ya
kuingia katika Uislamu katika makureishi na yaliona makabila yasiokuwa ya kikuresihi
ambayo wanaishi jirani na Makka na yale ambayo yanaokuja kutoka sehemu tofauti kutoka
biladi za waarabu ili kuhiji, yale yanaomkumba Muhammad (SAW) kama kutengwa, na
namna makureishi walivyo mzingira na uadui ilimfanya killa msaidizi kuwa adui juu yake na
wasaidizi wao, hivyo basi wakazidi kumpuuza. Na Mtume (SAW) akaona ujumbe wa Mola
wake katika mzunguko kuanzia kufuata kwake mpaka leo, na yakarefuka masiku na Mtume
(SAW) anazidi kutengwa na watu wake, na makuresihi wanazidisa juu yake chuki, na watu
wanazidi kumpuuza, Isipokuwa yeye (SAW) pamoja na yote hayo aliendelea yeye na
maswahaba wake waliokuwa karibu nae katika hali ya imani kali zaidi juu ya nusra ya Allah
na kunyanyua dini yake juu ya dini zote na akawa anawalingania watu kila anapopata wasaa,
na msimu wa hijja unapofika wa watu wakikusanyika katika mji wa Makka kutoka bara arabu
alikuwa anawaendea na kuwalingania katika Uislamu bila ya kujali iwapo makabila hayo
watapuuza ujumbe wake au kumpuuza au kumrudisha na majibu yasio mazuri. Baadhi ya
wajinga wa kikureishi walikuwa wanamfuata na kumuudhi wakati aipokuwa anawaendea
watu kuwafirishia ujumbe wa Mola wake, na wala hayo maudhui hayakumuondoshea
matamanio na matumaini yake. Hakika Allah ndie aliemtumiliza na Uislamu hivyo basi
hamna shaka atamnusuru na atamsaidia na mwenye kuifanya dini yake idhihiri. Na akawa
anasubiri nusra ya Allah hali ya kuwa siku hizo yupo katika maumivu ya kusimama
ulinganizi wake, na katika shida na dhiki ya makureishi, na wala hakusubirii sana hatimaye
dalili ya kufuzu ikawa inakuja kutoka Madina, hilo ni kuwa watu katika Khazraj walitoka kuja
Makka katika msimu wa hijja Mtume (SAW) akakutana nao na akawazungumzia na
akawauliza kuhusu wao, na akawalingania kwa Allah na wakaanza kuangaliana na
wakasema: Wallah huyu ni Mtume ambaye mayahudi wanaahidi basi wawatangulia na
wakakubali ujumbe na Mtume na wakasilimu na wakakuambia: Sisi tumewacha kaumu yetu
(yaani Aws na Khazraj) na wala hamna watu wenye uadui kati yao kama uliopo baina yao na
huenda Allah akatuunganisha kupitia wewe na iwapo Allah atatuunganisha kupitia wewe
basi hamna mtukufu zaidi yako". Na watu hawa wakarudi Madina na wakawaeleza watu wao
kuhusu kusilimu kwao, na wakaziunganisha mioyo iliyo wazi na nafsi zilizo kunjufu katika
-
Page 16 of 125
dini mpya, na wala haikubakia nyumba ya Aws wala Khazraj ila kuna utajo wa Muhammad
(SAW).
BAYAH YA KWANZA YA AQABAH
Mwaka ulipozunguka na kuingia msimu wa hijja walikuja watu kumi na mbili mwaka huo
katika watu wa Madina na wakakutana na Mtume (SAW) katika Aqabah na wakambayiisha
bayah ya kwanza ya Aqabah, walimbajiisha juu ya asiyemshirikisha Allah na chochote na wala
assibe wala wasizini na wala asiue watoto wake na wala asieneze uvumi atakautunga Mbele
ya mikono yake na miguu yake na wala asimuasi katika jema na iwapo atatekeleza hayo basi
atapata pepo na iwapo atalaghai katika hayo chochote basi mambo yake ni kwa Allah akitaka
atamuadhibu na akitaka atamsamehe. Na baada ya kuikamilisha bayah na msimu wa hijja
kumalizika walirudi Madina.
ULINGANIZI KATIKA MADINA
Amesema ibn Ishaq: wau walipokuwa wanaondoka, Mtume (SAW) alimtuma Musa'ab bin
Umeir pamoja nao, na akamuambia awafunze Quran na awafundishe Uislamu na
awafundishe dini, na Musa'b akawa anaitwa Muqri (msomaji) katika Madina. Na makao yake
yalikuwa kwa Asaad bin Zurarah. Na akawa anawaendelea watu katika maskani zao na
makabila yao na kuwalingania katika Uislamu, na anawasomea Quran na anamsilimisha mtu
na watu wawili mpaka Uislamu ukaenea katika maskani zote za Answar isipokuwa maskani
ya Khatamah na Wail na Waqif, na Musa'b akawa anawasomea Quran na kuwafundisha, na
akamuandikia barua Mtume (SAW) kumtaka ruhusa ili awakusanye na akamruhusu na
akamuandikia: "Ama baad: subiri siku ambayo mayahudi watajitayarisha kwa zaburi kwa
ajili ya jumamosi yao…mchana unapoingia basi jikurubishe kwa Allah kwa Rakaa mbili na
uwakhutubie, Musaab bin Umeir akawakusanya katika nyumba ya Saad bin Khaithamah
wakiwa ni watu kumi na mbili na hakuwachinjia siku hiyo ispokuwa mbuzi mmoja, kwani
yeye ndie wa kwanza kuanzisha jumaa katika Uislamu. Musa'ab akaendelea kuzunguka
Madina kuwatembelea watu na akiwalingania katika Uislamu na kuwafundisha. Siku moja
Asaad bin Zurara alitoka na Mus'ab bin Umeir akiwa amekusudia nyumba ya bani Abdul
Ashhal na nyumba ni mtoto wa khalati ya Asaad bin Zurarah na akaingia nae kupitia bustani
katika mabustani ya bani Dhafr karibu na kisima kilichoitwa Marq, na wakakaa katika bustani
na watu waliokuwa waliosilimu wanaanza kujumuika. Na Saad bin Muadh na Useid bin
Khudheir siku hizo walikuwa ni mabwana kwa watu wao wakiwa ni bani Abdul Ash-hal, na
wawili hawa walikuwa wakishirikiana wakifuata dini ya watu wao, wa walipo wasikia Saad
bin Muadh akimuambia Useid bin Khudeir" Twende kwa watu wale wawili ambao wamekuja
kwetu kuwasafihi wajinga tuwafukuze na tuwakataze wasije kwetu, kwani lau kama Asaad
bin Zurarah hahusiani na mimi na mimi basi wajua mimi natosheleza, yeye ni motto wa
khalati yangu na mimi siwezi kumfanya lolote, Useid bin Khudheir akachukua mkuki wake
kisha akamwendea na pindi Asaad bin Zurarah alipomuona alimuambia Musa'ab bin Umeir
huyu anakujilia ni bwana kwa watu wake hivyo basi kuwa mkweli kwa Allah Mbele yake,
Musa'ab akasema "Iwapo atakaa nitazungumza naye" akasema: akawasimamia kwa ukali na
akasema "ni yapi ywaletani kuja kusafihi wajinga. Ondokeni iwapo mwazithamini nafsi zenu"
hapo Musa'ab akasema "Hukai ili usikie iwapo utaridhika utayakubalina iwapo utayachukia
tutawacha yanaokuudhi" akasema "umefanya uadilifu" kisha akakita mkuki wake na akakaa,
Musa'ab akamzungumzia kuhusu Uislamu na akamsomea Quran wakasema kulingania na
-
Page 17 of 125
waliyosema wallahi tuuliona Uislamu katika uso wake kabla hajazungumza kwa amani yake
kuunga kwake. Kisha akasema: "ni mazuri yalioje maneno haya, ni yapi munaoyafanya iwapo
munataka kuingia katika dini hii?" wakamuambia: "utaoga, ujitahirishe nguo zako kisha
utapiga shahada ya haki kisha utasali rakaa mbili. Akasimama na akaswali Rakaa mbili kisha
akawaambia "nyuma yangu kuna mtu iwapo atawafuata hamna hata mmmoja atakae
mkhalifu katika watu wake na nitawaletea sasa hivi Saad bin Muadh kisha akauchukua mkuki
wake na akaenda kwa Saad na watu wake wakiwa wamekaa na watu maskani yao, pindi Saad
bin Muadh alipomuona anavyokuja akasema "Naapa kwa Allah Useid bin Khudheir
anawajilia na sura taofauti na ile aliowaondokea nayo, na walipo simama katika maskani Saad
akamuambia" Umefanya nini" akasema "Nimezungumza na watu wawili na wallahi sikuona
ubaya wowote kwao na niliwakataza na wakasema tutafanya unachokipenda. Na
nimeambiwa kua bani Harith wametoka kuenda kwa Asaad bin Zurarah ili wamvuwe, na hilo
ni kuwa wamejua kuwa yeye ni mototo wa khalati yako ili wakuchimbe, Saad akasimama kwa
hasira na haraka kwa huku alioelezwa kuhusu basi Harith akashika mkuki mkononi mwake
kisha akasema: "Walla nimekuona hutoshi" kisha akawatokea na Saad alipomwona makini
alijua kuwa Useid alichotaka ni yeye awasikie na akawasimamia kwa hasira kisha
akamuambia Asaad bin Zurakah "Ewe Aba Umamah lau kama hamna kilichoko baina yangu
na yako uhusiano usingelinifanyia hayo, munatulaghai hapa kwetu kwa yale
yanayotuchukiza, na Asaad ameshangulia kumuambia Musa'ab, yaani Musa'ab amekujilia
mtu Wallah ni bwana wa watu wake iwapo atakufuata hamna atakaye kuenda kinyume yako
wawili wao. Musa'ab akamuambia: "Kwani hukutusikia iwapo utadhihirika na utapendelea
utayakubali, na iwapo utayechukia tutayawacha yanaokuchukiza." Saad akasema: "Umefanya
uadilifu" kisha akaukita mkuki wake na akakaa. Akaanza Musa'ab na kumueleza Uislamu na
akamsomea Quran, wakasema"Tukaona Uislamu usoni mwake kabla hajasema kwa sababu ya
kungaa kwake na amani yake, kisha akawaambia" munafanya nini iwapo mutasilimu na
kuingia katika dini hii?" wakasema"utajitahirisha na kutahirisha nguo zako kisha utapiga
shahada kisha utaswali rakaa mbili." Kisha akauchukua mkuki wake akaondoka kuelekea
maskani na watu wake wakiwa na Useid bin Khubeir na watu wake walipomuona anakuja
wakasema: "Tunaapa kwa Allah Saad anawarudia na sura tofauti na ile ambayo
amewaondokea nayo" na akawasimamia na akasema: "Enyi bani Abdul Ash-hal nyinyi
munachukulia vipi kwenu?' Wakasema Kiongozi wetu na mwenye ushauri bora zaidi kwetu
na kiongozi shupavu" akasema "maneno ya wanaume wenu na wanawake wenu ni haramu
mpaka mutakapo amini Allah na Mtume wake" wakasema"Basi wallah hakukutwa katika
nyumba ya bani Abdul Ashhal mwanamume na mwanamke illa Muislamu." Musa'ab akarudi
nyumbani kwa Asaad in Zurarah na akaishi kwake akiwalingania watu katika Uislamu, hata
ikafikia haikubakia nyumba katika majumba ya Answar isipokuwa wanaume na wanawake
Waislam. Musa'ab akakaa Madina pamoja na Aws na Khazraj kwa muda wa mwaka
anawafundisha dini yao huku anaangalia kwa furaha kuongezeka kwa watakao nusuru dini
ya Allah na neno la haki na alikuwa radhi za Allah zimshukie Musa'ab anawabishia milangoni
watu kwa kumkimbilia ili kuwalingania nao na akawafikishia ulinganizi wa Allah, na alikuwa
anaingia mashambani ili kuingilia na wakulima na katika shughuli yao akiwalingania katika
Uislamu, na alikuwa anakutana na viongozi anawalingania katika dini ya Allah, na alikuwa
anafanya mambo aliyokusudia kama alivyofanya pamoja Asaad bin Zurarah katika kutumia
mbinu ya kuwafikia watu ili waweze kuwasikilizisha sauti ya haki mpaka mji wa Madina
kutoka kwa ushirikina, upotofu na kutoka katika miito miovu (kuwapeleka katika tauhid na
-
Page 18 of 125
imani na miito ya Kiislamu) iliojengwa juu ya shirki na kunguza katika uzito na uzani. Hivyo
ndivyo ulivyokuwa ukakamavu wa Musa'ab na ulivyokuwa ukakamavu ya wale ambao
waliosilimu pamoja mpaka waliweza Kuibadilisha Madina katika mwaka mmoja kutoka hali
ya ushirikina mpaka katika hali ya Uislamu.
BAY'AH YA PILI YA AQABAH
Bay'ah ya kwanza ya Aqabah ilikuwa ni kheri na baraka, kwani waliosilimu juu ya uchache
wa idadi yao walitosheka na mtu mmoja miongoni mwa maswahaba wa Mtume nae ni
Mus'aab kuweza kuiadilisha Madina na kugeuza mawazo na miito iliokuwepo katika mujtama
wao, pamoja na kwamba kuwa jumla ya watu wamejitenga nao hivyo basi jumla
hawakuamini, na mujtama usiweze kuathirika kwa fikra na miito ya Kiislamu, kinyume na
Madina kwani waliuingia katika Uislamu jumla ya watu, na mujtama ukaathiri na miito
ikaathiri na hii ni dalili wazi imani ya watu fulani waliotengwa na mujtama waliotengwa na
jumla ya watu haikuathiri katika mujtama wala katika watu jumla namna iwavyo uwezo wa
watu hawa kadha. Na kwa mahusiano yaliopo kati ya watu iwapo zitaathiri kwa kuathiri fikra
na miito mageuzi yatapatikana na mapenduzi namna iwavyo uchache wa idadi ya wanaobeba
ulinganizi. Na yaonyesha pia kuwa mujtama pindi utakuwa umeganda juu ya ukafiri kama
mujtama wa Makka inakuwa ni vigumu zaidi kuliko mujtama ambao haujaongozwa na rai
fisidifu mfano wa mujtama wa Madina hata kama zipo rai hizo ndani yake, kwa sababu hiyo
uliathiri mujtama katika Madina kwa Uislamu kuliko wa Makaa, kwani watu wa Madina
walikuwa wanahisi upotofu wa fikra ambazo wanazozibeba na walikuwa wanatafuta fikra
nyengine na nidhamu nyengine kwa ajili ya maisha yao, ilhali mujtama na Makka ulikuwa
umetulia kwa yale waliokuwa nayo, na kuwa hamu ya kuendeleza hasa mabwenyenye wa
ukafiri mfano wa Abu Lahab na Abu Jahl na Abu Sufyan, kuwa sababu hiyo hakukawia
Mus'aab katika Madina muda mfupi hatimae kulipatikana mageuzi ya ulinganizi na kuweza
kuitikiwa kwa haraka na akashuhudia kukubali kwa watu Uislamu na kukubali kujifunza
hukmu zake na kumfurahisha sana, na anaona kuongzeka idadi ya Waislamu na Uislamu
kuenea Madina, anafurahishwa kwa hila na inaongezeka uchangamfu katika kufundisha na
kueneaza ujumbe, na ulipoingia msimu wa hijja alirudi Makka na akamueleza Mtume (SAW)
habari za Waislamu na nguvu zao na habari za Uislamu na kuzidi kuenea kwake, na
akamuelezea namna mujtama wa Madina umekuwa hazungumzi isipokuwa Uislamu, na
kuwa nguvu za Waislamu na uwezo wao huko una taathira na kuufanya Uislamu ndio ambao
unaolea juu ya kila kitu, na kua mwaka huu watakuja baadhi ya Waislamu walio na imani
kubwa zaidi kwa Allah na wako tayari Kubeba ujumbe wa Allah na kuihami dini ya Allah,
akafurahia sana Mtume (SAW) habari ya Mus'aab akawa anafikiria kwa urefu na akawa
analinganisha kati ya mujtamaa wa Makka na mujtama wa Madina, kwani Makka amelingania
watu kwa Allah kwa muda wa miaka kumi na mbili mfululizo na watu hakuchoka kufanya
daw'ah na wala hakuacha fursa isipokuwa alitumia kila anachoweza kama juhudi na
kuvumilia killa aina za adhabu, pamoja na hayo mujtama umejifunga na iimekosekana njia ya
kuupenyeza ujumbe kutokamana na uovu uliopo katika mioyo ya watu wa Makaa na ugumu
uliopo katika nafsi zao, na mgando wa kale uliopo katika akili zao, na kwa sababu hiyo
mujtama wa Makka muovu na dhaifu wa kukabili daw'ah kutokamana na ushirikina wa
masanamu uliokita katika nafsi za wakazi wake ambao Makka ilikuwa kama kitovu chake.
Ama mujtama wa Madina baada ya kupita mwaka ilikuwa ni kusilimu kwa watu wachache na
Khazraj, kisha bay'ah ya watu kumi na mbili na juhudi ya Mus'aab bin Umeir kwa muda wa
-
Page 19 of 125
mwaka mwengine, hayo yalikuwa yanatosha kuleta mazingara ya Kiislamu katika Madina na
watu kuingia katika dini ya Allah kwa haraka hii ya kushangaza, na iwapo Makka ujumbe
umesimama kwa wale ambao tu waliosilimu pamoja na yanaowakumba Waislamu katika
mateso na maudhi ya makureshi, basi Madina ujumbe wa Allah umeanza kuenea haraka
hivyo na wala mateso ya washirikina na hayo ni katika yanaoumakinisha Uislamu katika nafsi,
na kuwafungulia njia Waislamu, hivyo ndivyo ilivyo bainika kwa Mtume (SAW) kuwa
Madina inafaa zaidi kwa daw'ah ya Uislamu kuliko makaa na mujtama wa Madina unafaa
zaidi kueneza nuru ya Uislamu kuliko wa Makka. Na kwa sababu hiyo akafikiria kuguria na
wakagura maswahaba wake kwenda kwa ndugu zao Waislamu ili wapate amani kwao na ili
wasalimike na mateso ya makureshi na ili wajitolee kwa ajili ya daw'ah kuiingiza katika
marhala ya kivitendo nao ni utabikishaji wa Uislamu na Kuubeba ujumbe wake na nguvu za
serikali na utawala wake, hiyo ndio sababu pekee ya kuguria na wala sio nyengine.
Na ni lazima ieleweke kuwa Mtume (SAW) hakufikiria kugura Makka kwa sababu ya vizuizi
vilivyo kuwepo Mbele ya daw'ah pasi na kusubiria au ili aviepuke vizuizi hivi, kwani yeye
Mtume (SAW) alisubiri miaka kumi katika Makka, na wala haipurukushi daw'ah na alikuwa
anafikwa mateso katika njia ya daw'ah yeye na wafuasi wake na wala mateso ya makureshi
hayakudhoofisha chochote katika nafsi yake na kudhoofisha azma yake ya mapambano yao,
bali yalimzidisha mani katika daw'ah ambayo kwao imeleta utukufu kuto kwa Allah, na
kumzidisha yakini kwa nusra ya Allah kumzidisha umakinifu na uthabiti, lakini aliona baada
ya majaribio hayo uovu ulio katika mujtama wa Makka kama fikra finyo na ugumu na upotofu
mambo yanaodhoofisha matarajio na kuendeleza ujumbe inahitajia juhudi zaidi, ndio ikawa
hamna budi kutoka mujtama huo na kuingia katika mujtama mwengine na ndio maana
akafikiria kuigura Makka, na hilo ndilo ambalo limempeleka kufikiria kuguria Madina, na
wala sio mateso yaliomfikia yeye na yaliowafikia maswahaba wake. Ndio tume (SAW)
aliamrisha maswahaba wake wagurie habasha kukimbia mateso, kwani inajuzu kwa waumini
kugura sehemu za fitna kuhifadhi dini yao, japo mateso yanaongeza imani kukandamizwa
kuzidisha ikhlasi na mapambano yanalenga matarajio, na imani humpelekea alie nayo
kupuuza kila kitu na kujitolea katika njia yake kwa mali, cheo, raha na maisha, ndio hata kama
imani juu ya Allah humfanya muumin aitangulize nafsi yake katika hatari kwa ajili ya Allah
lakini kuendelea kwa mateso na kudumu katika kujitolea humfanya muumin kujishughulisha
na subra juu ya mateso na kuzidi kujitolea kutampuepusha kutafakari jambo ambalo
litamzidisha muumin upana wa kudiriki haki, hivyo basi imekuwa namna budi kwa muumin
kugura sehemu za fitna. Isipokuwa hilo linalingania na kugura kwa aislamu na kwenda
habash. Ama kuguria kwa Madina ilikuwa ni kwa ajili waweze kumakinika kuugurisha
ujumbe wao katika hali ambayo ni hai katika mujtama wao mpya, na kuueneza katika
ulimwengu ili wanyanyue neno la Allah. Na hapa ndipo Mtume (SAW) aliamrisha
maswahaba wake kiasi hicho. Na kabla hajawaarimsha kuguria Yathrib na kabla hajaamua
kuguria ni lazima aonane na mchujaji kutoka Madina, na akutane na Waislamu waliokuja
kuhiji na kujionea upeo wa maandalizi yao ya kuhifadhi ujumbe na upeo wa maandalizi ya
kujitolea kwa ajili ya Uislamu na kuona iwapo watambayiisha yeye bay'ah ya vita, bay'ah ya
vita ndio jiwe msingi ya kusimamisha serikali ya iislamu na akasubiria kuingia kwa mahujaji,
na hiyo ilikuwa katika mwaka wa kumi na mbili ya kutumilizwa sawa na 622 miladi na
mahujaji walikuwa ni wengi na miongoni mwao walikuwa Waislamu sabiini na tano: sabiini
na tatu wanaume na wanawake wawili wakiwa ni Nuseibah bint Kaab Umm Ammarah
-
Page 20 of 125
mmoja kati ya wanawake wa bani Maziu bin Najjar na Asmaa bint Amru bin Adiy kati ya
wanawake wa bani Salamah nae ni Umm Mani'i, Mtume (SAW) akakutana nao kwa siri na
akawazungumzia katika bay'ah ya pili kuwa haimaliziki katika ujumbe tu na kusubiria bali
inapita hayo inasonga mbele kiasi hawezi kuwapitia nguvu Waislamu kujihami nafsi zao, bali
inakwenda mbali zaidi ya hayo pia kiasi ya kuweka kiungoambacho kitakuwa jiwe msingi la
kusimamisha serikali ya Kiislamu, ambayo utatabikishwa katika mujtama na kuubeba ujumbe
wake kiulimwengu kwa watu wote, na Kubeba pamoja nao nguvu ambazo zitauhami na
kuondosha njiani mwaka kila kizuizi inaosimama katika njia ya kuweza kwake na utabikishaji
wake. Aliwazungumzia hayo na akatambua uzuri wa maandalizi yao na akaagana nao
wakutane nae Aqabah usiku wa manane katikati ya siku za Tashriq. Na akawaambia
wasimwamshe alielala, wala musimngoje asiekuwepo. Na siku ya maagano maalum baada
kupita thuluthi ya kwanza wa usiku wakaanza safari yao wakinyapanyapa na wakijificha,
wakiogopea kujulikanwa na yeyote na wakaenda Aqabah na wote wakapanda jabali na
wakapnda wanawake wawili pamoja nao na wakawa wanamsubiri Mtume (SAW) na akawajia
akiwa na Abbas na wakati huo hakuwa amesilimu bali amekuja kumpa nguvu motto wa
kakake. Na ndie aliekuwa wa kwanza kuzungumzia akasema: "Enyi kongamano la Khazraj,
bila shaka mwajua hali ya Muhammad hapa mwetu, na tumemhifadhi kutokamana na watu
wetu ni kama hivi tumuonavyo, yeye ni mtukufu kwa watu wake na amehifadhiwa katika mji
wake na yeye hataki illa kuungana na nyinyi na kuwa pamoja na nyinyi na iwapo mwaona
mutatekeleza munayomuahidi na kumhifadhi na maadui wake basi nyinyi na mlioyabeba na
iwapo mwaona mutamsalimisha na kumuuza baada ya kutoka kuja kwenu basi muachane
hivi sasa". Na pindi waliposikia maneno ya Abbas walimuambia "tumesikia uliyoyasema"
Kisha wakasema "Zungumza ewe Mtume wa Allah tumia ulimi wako kuizungumzia nafsi
yako na Mola wako unaoyapenda". Mtume (SAW) akajibu baada ya kusoma Quran na kutia
motisha katika Uislamu »مما تمنعون منه نساءكم وأبناءكم يعكم على أن تنمنعوني أبا «
"Nawabayiisha juu ya kunihifadhi mimi kama munavyohifadhi wake zenu na watoto
wenu". Baraa akaunyosha mkono wake ili ambayiishe kwa hayo akasema "Tumekubayiisha
ewe Mtume wa Allah wallahi sisi ni watu wa vita na watu wa silaha na tumezirithi kutoka
kwa mababu na mababu". Na kabla Barra hajamaliza maneno yake, Abu Haitham bin Tayhan
akamkatiza kwa kusema "Ewe Mtume wa Allah kati yetu na watu (yaani mayahudi) kuna
mkataba na sisi tutauvunja, na iwapo sisi tutafanya hilo na kisha Allah akakupa ushindi
utarudi kwa watu wako na kutuacha? Mtume (SAW) akatabasamu na akasema: »رب من حاربتم, وأسالم من سالمتمبل الدم الدم, والهدم الهدم أنا منكم, وأنتم مني, أحا «
"Bali damu yenu ni damu yangu na kitukufu chenu ni kitukufu kwangu mimi ni katika
nyinyi na nyingi katika mimi, utapigana na yeyote mutake pigana nae na nitaweka amani
na yule mulieweka nae amani". Na watu wakataka kufanya bay'ah Abbas bin Ubada
akawakatiza kwa kusema "Enyi Khazraj mwajua ni kuwa lipi munalo mbayiisha nalo mtu
huyu nyinyi muambayiisha juu ya kupigana na watu wekundu na weusi iwapo nyinyi
mwaona mutapoteza mali yenu na watukufu wenu kuuwawa na baadae kumsalimisha basi
bora sasa, kwani mukifanya basi hizaya ya dunia na akhera itawafika, na iwapo mwaona
mutatimiza kwa yale munaomwtia nayo ya kuharibu mali na watukufu kuuwawa basi
mchukuweni kwani wallah yeye ni kheri ya dunia na akhera. Watu wakajibu sisi tutamchukua
juu ya mali kuaribiwa na watukufu kuuwawa, kisha wakasema "Tutapata nini ewe Mtume wa
Allah iwapo tutatimiza hayo". Mtume akawajibu huku ametulia kwa kusema: »الجنة «
-
Page 21 of 125
"Pepo" Wakainyosha mikono yao nae akawanyoshea mkono wake na wakambayiisha huku
wakisema: بايعنا رسول هللا صلى هللا عليه وسلم على السمع والطاعة في عسرنا, ويس]رنا, ومنش]طنا, ومكرهن]ا وأث]رة علين]ا وأن ال نن]ازع األم]ر «
»كنا, ال نخاف في هللا لومة الئم أهله, وأن نقول بالحق أينما "Tulimbayiisha Mtume (SAW) juu ya kusikiza na kutii katika mazito yetu na mepesi yetu
na yanayotuchangamsha na yanaotuchukiza na tusiwe ni wenye kujipendelea na wala
tusizozane kuhusu utawala na wanao husika, na tuwe tunazungumza ukweli popote
tutakapo kuwepo tusiogope katika njia ya Allah lawama za mwenye kulaumu" na walipo
maliza Mtume (SAW) akasema: »كونوا على قومهم بما فيهم كفالء اثني عشر نقيباً, لي أخرجوا إلي منكم «
"Nitoleeni watu kumi na mbili kati yenu ili wawe ni wasimamizi juu ya watu wao" watu
wakachagua watu tisa kutoka Khazraj na watatu kutoka Aws, na Mtume akawaambia hawa
Manaqibu: »سى بن مريم, وأنا كفيل على قومي لى قومكم بما فيهم كفالء, ككفالة الحواريين لعيأنتم ع «
"Nyinyi ni wasimamizi wa watu wenu mfano wa wanafunzi wa Issa ibn Maryam na mimi
ni msimamizi juu ya watu wangu" wakasema "Ndio". Kisha wakarudi katika malazi yao, na
wakabeba mizigo yao na kurudi Madina. Na baada ya hayo Mtume (SAW) aliwaamrisha
Waislamu wakaamua kugura mmoja au vikundi vidogo, na makureshi walikuwa washajua
kuhusu bay'ah na ndio maana walijaribu kumrudisha Makaa wanaemweza. Na wakawa ni
pingamizi kwa Waislamu kugura mpaka kuwa pingamizi kati ya mtu na mkewe. Na wala hilo
halikuathiri katika Hijra bali Waislamu waliendelea kuguria Madina na huku Mtume (SAW)
bado anaishi Makka, na wala hamna ajuwae kama ameazimia kuguria Madina au ameamua
kubakia Makka? Lakini lile ambalo linaonekana ni kua anataka kuguria Madina, kwani
Abubakar alimtaka ruhusa ili agurie Madina na akasema Mtume (SAW): » تعجل لعل هللا يجعل لك صاحباً ال «
"Usifanye pupa huenda Allah akakujaalia rafiki" Abubakar akajua kuwa anataka kugura. Na
makureshi walikuwa wnaipigia mahisabu Hijra ya Mtume (SAW) kuenda Madina mahisabu
elfu baada ya kukithiri Waislamu huko uwingi ambao umewafanya kuwa na mkono wa juu
katika Madina na imewapatia wao nguvu kubwa pamoja na wale waliogura kutoka Makka, na
iwapo Mtume atakuwa pamoja nao wakiwa katika nguvu hizi, basi hilo litakuwa maangamizo
kwao. Hivyo basi wakafikiria kumzuia Mtume (SAW) kuguria Madina na wakati huo huo
wakiogopea kubakia kwake Makka hilo litawaudhi Waislamu katika Madina na kuja kumaliza
baada ya kupata nguvu hizo na watakuja kumkinga Mtume (SAW) wale waliomuamini yeye.
Hivyo basi wakafikiria kumuua ili asikutane na Waislamu Madina ili kusiwepo kile kitakacho
sababisha wao kupambana na watu wa Madina kwa ajili ya Uislamu na kwa ajili ya
Mohammad (SAW). Na imekuja katika kitabu cha sera imepokewa kutoka hadithi ya Aisha na
Abi Umamah bin Salmi "Na wakati walipoondoka watu sabiini nafsi yake ilitulia kwani Allah
amemjaalia nusra kutoka kwa watu wa vita na nguvu". Na mateso yakawa yanaongezeka juu
ya Waislamu kutoka kwa makafiri kwa kudhihirisha kwao kutoka na wawadhiki maswahaba
wake na wafuasi wake na akifikiwa yale ambayo hawajawahi kufikiwa katika matusi na
mateso kutoka kwa makureishi, na wakamlalamikia Mtume (SAW) na akasema: »ة قد أريت دار هجرتكم سبح «
"Nimeonyeshwa nyumba yenu mutakaohamia" Kisha akakaa masiku kisha akatoka akiwa na
furaha na kusema: »راد منكم أن يخرج فليخريج إليها قد أخبرت بدار هجرتكم وهي يثرب, فمن أ «
-
Page 22 of 125
"Nimejulishwa nyumba yenu mutakaoihamia nayo ni Yathrib, kwa hivyo yoyote anaetaka
kwenda basi aende huko". Na wakawa wanajitayarisha na kusuhubiana na kukutana na
wanaotoka na wakajificha, walitoka vipute na vikundi vidogo vidogo, huku Mtume (SAW)
bado yupo Makka akisubiria kupewa ruhusa ya kutoka, na Siddiq mara nyingi alikuwa
anamuomba ruhusa Mtume (SAW) ili agurie Madina baada ya kua Waislamu wameanza
kuguria na akimuambia: » تعجل لعل هللا يجعل لك صاحباً ال «
"Usifanye pupa huenda Allah akakujaalie rafiki" Abubakar akawa anatarajia kuwa atakuwa
ni yeye. Na pindi makureishi walipoona kugura kwa maswahaba na kujua katika Dar An-
Nadwah wakashauriana kile watakachofanya kuhusu Mtume (SAW) na wakakubaliana
wamuue na wakatawanyika juu ya uamuzi huo. Kisha Jibril akamjia Mtume akamuamrisha
asilale kwenye kitanda chake anachokilalia na akamuelezea kuhusu vitimbi vya watu, usiku
huo hakulala nyumbani kwake na hapo Allah akamruhusu atoke.
Juu ya hayo kuwepo kwa nguvu za Kiislamu katika Madina, Madina kuandaa kumpokea
Mtume (SAW) na kuisimamisha serikali ya Kiislamu huko ndio mambo ambayo yalimpeleka
Mtume (SAW) kugura, na hiyo ndio sababu za moja kwa moja za kugura. Hivyo basi
amekosea kila anayedhania kua Mtume (SAW) aliguria Madina kwa sababu ya uoga na
kuogopa makureishi wasije wakamuua, na kutoroka. Kwani yeye Mtume (SAW) hakuyapigia
mateso hisabu yoyote, na wala hakuwa akiyajali mauti katika njia ya kulingania Uislamu na
wala haikumshughulisha nafsi yake wala uhai wake, na wala haikuwa kuguria Madina
Isipokuwa kwa ajili ya ulinganizi wa Kiislamu na kwa ajili ya kusimamisha serikali ya
Kiislamu. Bali makureishi walipanga njama ya kumuua kwa kuogopea kuguria kwake
Madina, na kupata nguvu, lakini Mtume (SAW) akawashinda na akaguria Madina pamoja na
kuchukiwa kwao, na wala wasiweze kumzuia pamoja na njama walizomfanyia. Hivyo basi
Hijra imekuwa ndio kipambanuo katika Uislamu baina dori ya kulingania na kuhamisha
mujtama na serikali itakao hukumu na kuitabikisha, na kulingania kwa hijja na dalili, na kwa
nguvu ambazo itaohifadhi hunu ujumbe kutokamana na nguvu za shari na upotofu.
KUSIMAMA KWA SERIKALI YA KIISLAMU
Mtume (SAW) aliwasili Madina na akapokelewa na idadi kubwa ya wakaazi wake, wakiwemo
Waislamu na mushrikina na mayahudi, na Waislamu wakawa wamemzunguka. Na wote
walikuwa na hamu ya kumtumikia na kumfurahisha, wana hamu ya kuitolea nafsi zao kwa
ajili ya ujumbe wa Kiislamu. Na kila mmoja wao alikuwa na hamu ya kumweka Mtume
nyumbani mwake, lakini Mtume (SAW) aliachia kamba ya ngamia wake na hatimae akapiga
magoti katika kiwanja cha Sahl na Suheil watoto wa Amru, na akakinunua na akajenga msikiti
juu yake na ubavuni mwake akasimamisha nyumba yake. Na ujenzi wa msikiti na nyumba
haikua ni ya kumumiza yeyote kwani ulikuwa ni wa sahali kiasi ambacho haikuhitajika
mapesa mengi wala kazi kubwa. Msikiti ulikuwa ni ukumbi, kuta nne zilizojengwa na matofali
na udongo, na sehemu ya sakafu ilikuwa imefinikwa na matawi ya mitende na sehemu
maalum ya mafuqara ambao hawakuwa na makao na msikiti haukuwa ukiwaka mataa
Isipokuwa wakati wa suala ya ishaa, kwani ilikuwa unang'arishwa na nyasi kavu
zilizochomwa kando kando, na nyumba ya Mtume (SAW) haikuwa zaidi ya msikiti kiujuzi
isipokuwa ilikuwa inamuangaza zaidi kuliko misikiti mengine. Na Mtume (SAW) alikaa
katika nyumba ya Abu Ayyub Khalid bin Zeid Al-Answariy wakati wa ujenzi wa msikiti na
-
Page 23 of 125
nyumba mpaka ilipomalizika kujengwa kwake, na akahamia na kutulia Mtume (SAW) na
huku anatafakari kuhusu maisha mapya alioyafungua na ambayo yamemhamisha yeye na
kuhamisha ujumbe wake katika uwanja mpana kutoka katika dori moja hadi dori nyengine,
imetoka kutoka katika dori ya kujenga na katika dori ya mapambano na kuingia katika dori
kutabikisha hukumu za Uislamu juu ya watu katika mahusiano yao. Na kutoka katika dori ya
kulinganiwa isitoshe na kusubiria mateso kwa ajili yake na kuingia katika dori ya utawala na
uongozi na nguvu ambazo zitaihami ujumbe huu. Kwani Mtume (SAW) pindi alipowasioli
Madina aliamrisha kujengwa kwa msikiti kama sehemu ya kuswali kukutana na kushauriana
na kusimamia mambo ya Waislamu na kuhukumu baina yao, na akamfanya Abubakar na
Umar kama wasaidizi wake, amesema Mtume (SAW): »وزيراي في األرض أبو بكر وعمر «
"Mawaziri wangu katika ardhi ni Abubakar na Umar" na Waislamu wakawa
wamemzunguka na kumrudilia na akawa anatekeleza shughuli za kiongozi wa serikali na
hakimu na amiri jeshi, na yeye Mtume (SAW) alikuwa anachunga mambo ya Waislamu na
kuondosha husuma baina yao, na alikuwa anaviweka vikosi nje ya Madina. Na kwa hayo
alisimamisha serikali katika Madina kuanzia siku ya kwanza alioingia, na akawa
anaimaikinisha serikali hiyo kwa kujenga mujtama juu ya msingi thabiti, na kuandaa nguvu za
kutosha zitakazoweza kulinda serikali na kueneza ujumbe. Na baada ya kuwa na matumaini
na hayo yote alianza kuondosha vizuizi vya kimada ambayo vinasimama katika njia ya
kueneza Uislamu.
KUUJENGA MUJTAMAA
Allah amemuumba mwanadamu na umbile la kuhifadhi maisha na katika madhihirisho yake
kujumuika mwanadamu, hivyo basi ni jambo la kimaumbile kukutana kwa watu wao kwa
wao, na kuwepo mujtama baina yao ni jambo la kimaumbile, isipokuwa kukutana tu kwa
watu hakuwafanya kuwa ni mujtama, bali inawafanya wao kama kundi, na watabakia kundi
iwapo watakomea juu ya kukutana tu kwao na iwapo yataanza baina yao mahusiano ya
kupata maslahi yao na kujiondosha madhara, basi mahusiano hayo yatakifanya kikundi hicho
kuwa ni mujtama, isipokuwa mahusiano hayo haitawafanya wao ni mujtama moja isipokuwa
iwapo mitazamo yao itaungana wa kuunganisha fikra zao, kuungana mapenzi yao na
machukivu yao kwa kuunganisha hisia zao, na kuungana utatuzi wa mahusiano hayo kwa
kuunganisha nidhamu ambayo itakaotatua, hivyo basi hamna budi ya mtazamo wa fikra na
hisia na nidhamu wakati wa kuangalia mujtama, kwa sababu ndio jambo ambalo linaofanya
kuwa ni mujtama maalum ulio na rangi maalum. Na juu ya msingi huu tutauangalia mujtama
katika Madina wakati wa kuingia kwake Mtume (SAW) ili tujue mwelekeo wake.
Wakati huo Madina ilikuwa kunaishi vikundi vitatu: cha kwanza Waislamu wakiwemo
Muhajirun Answar na walikuwa ni wengi. La pili mushrikina katika Aws na Kazraj ambao
bado hawajasilimu na hawa walikuwa wachache. Na la tatu ni mayahudi nao ni vigawanyiko
vinne: kimojawapo wanaishi ndani ya Madina na vitatu nje ya Madina. Ama wale waliokuwa
ndani ya Madina walikuwa ni Banu Qainuqa'a na wale waliokuwa nje ni Banu adhir na
mayahudi wa Khaibar na Banu Qureidhah. Na mayahudi kabla ya Uislamu walikuwa ni
mujtama mbali na mujtama wa Madina, kwani fikra zao zilikuwa ni tofauti na hisia zao tofauti
na utatuzi, hivyo basi mayahudi hawachukuliwi kuwa ni sehemu