bunge la tanzania mei 2019.pdf · mheshimiwa spika, nakushukuru, kwa niaba ya waziri wa nchi ofisi...

252
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 13 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Tono, leo ni Kikao cha Ishirini na Sita. Katibu! NDG. ATHUMANI HUSSEIN – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka 2019/2010. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri, Viwanda na Biashara kwa kutuletea hiyo Randama mezani. Katibu!

Upload: others

Post on 31-Oct-2019

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA________

MAJADILIANO YA BUNGE_________

MKUTANO WA KUMI NA TANO

Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 13 Mei, 2019

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. WaheshimiwaWabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Tono,leo ni Kikao cha Ishirini na Sita.

Katibu!

NDG. ATHUMANI HUSSEIN – KATIBU MEZANI:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:

Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka 2019/2010.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri,Viwanda na Biashara kwa kutuletea hiyo Randama mezani.Katibu!

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

NDG. ATHUMANI HUSSEIN – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

SPIKA: Maswali, swali la kwanza litaulizwa naMheshimiwa Mbunge wa Kondoa Mjini, Mheshimiwa EdwinMgante Sannda.

Na. 210

Posho za Vikao vya Madiwani Nchini

MHE. EDWIN M. SANNDA aliuliza:-

Kwa muda mrefu tumepigania kuboreshwa kwamaslahi ya Madiwani ikiwepo posho za vikao na Serikaliimekuwa ikisisitiza kuongeza mapato ili halmashauri ziwezekuwalipa Madiwani vizuri kadri ya uwezo, wito ambaoumeitikiwa vizuri, mwezi Februari, 2019 tumepokea barua tokaTAMISEMI ikielekeza Madiwani walipwe posho za vikao shilingi40,000 na si vinginevyo.

Je, kwa nini Serikali isiache halmashauri kulipa poshokadri ya uwezo kama ambavyo msisitizo umekuwa tokaawali?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriTAMISEMI, Mheshimiwa Mwita Mwikabe Waitara, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziriwa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge wa KondoaMjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali imetoa ufafanuzikupitia barua Kumb. Na. CCB. 215/443/01 ya tarehe 02Januari, 2019 juu ya ulipaji wa posho mbalimbali za Madiwani

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

ikiwemo posho za kuhudhuria vikao. Sheria ya Serikali za MitaaSura Namba 288 Kifungu cha 42 na Sura ya 287 Kifungu cha70, inamtaka Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaakupitisha viwango vya posho za Madiwani. Hivyo posho hizozinapaswa kulipwa kwa kuzingatia miongozo na maelekezoya Waziri mwenye dhamana wa Serikali za Mitaa. Maelekezoyanayotolewa yanasaidia kuweka usawa wa viwango vyaposho za Madiwani katika halmashauri zetu nchini, hivyokuondoa malalamiko kutoka wa Waheshimiwa Madiwani.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuimarishamifumo ya ukusanyaji na udhibiti wa mapato na itendeleakuongeza posho na maslahi ya Madiwani kulingana nakuimarika kwa uwezo wa halmashauri kwa kukusanyamapato yake ya ndani.

SPIKA: Mheshimiwa Sannda nilikuona, swali lanyongeza.

MHE. EDWIN M. SANNDA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana na nashukuru kwa majibu ya Serikali. Ninamaswali mawili ya nyongeza, kwanza fursa za vyanzo vyamapato na uwezekano wa kuongeza mapato inatofautianabaina ya halmashauri na halmashauri. Hili suala la malalamikolina kosa msingi linabaki kuwa dhana.

Sasa je, Serikali huwezi kulinganisha kati ya Kondoaau Geita au hata Dar es Salaam fursa za mapato zilizopo, naMadiwani ni sehemu ya wanaoweka nguvu ya kukusanyamapato na kuongeza mapato. Serikali haioni umuhimu wakuwaruhusu walipe kadiri ya uwezo wa halmashauri zao ilipia iwe sehemu ya motisha? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, lini sasa maana tulipataWaraka wa kutuambia tulipe 40,000 na hapa tunazungumziaposho za vikao peke yake, lini sasa maslahi menginetunaendelea kuruhusu kadiri ambavyo inafanya kazi. Lini sasatutapata Waraka wa kufafanua ili ule Waraka uliotolewamwezi Januari uweze kupitwa maana Serikali inafanya kazikwa maandishi?

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri, tafadhali.

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA, (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, ni kweli kwamba Waheshimiwa Madiwani wanafanyakazi kubwa sana ya kusimamia mapato, kwa kukusanya lakinipia na ndiyo maana fedha nyingi hapa tunapelekahalmashauri Waheshimiwa Madini kupitia vikao vyao naKamati mbalimbali ndiyo wanapaswa kusimamia na kwakweli tunawashukuru sana wamekuwa wakifanya hivyo.Majibu yangu ni kwamba ni kweli Mheshimiwa Waziri wa Nchiwakati anamalizia hoja yetu hii ya bajeti ya TAMISEMI, aliahidimbele ya Bunge lako Tukufu kwamba jambo hili linafanyiwakazi na naomba niwaahidi kwamba, Waheshimiwa Wabungewote na Waheshimiwa Madiwani popote walipo wavutesubira ndani ya wiki hii Mheshimiwa Waziri atatoa maelekezona jambo hili litafikia mwisho ambapo tunaamini kwambautakuwa ni mwisho mwema, ahsante.

SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Cecil Mwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, sualalinaloulizwa na Mheshimwa Sannda na sisi pia watu wahalmashauri ya Masasi linatuletea shida. Halmashauri yaWilaya ya Masasi ilipanga kulipa posho Madiwani na stahikizao nyingine kutokana na makusanya yaliyokuwayanakusanywa kutoka kwenye ushuru wa korosho ambaoMheshimiwa Rais amesema hatapeleka tena. Sasa swalilangu, ni je, Serikali haioni umuhimu wa kuwalipa Madiwanihawa posho moja kwa moja kutoka kwenye Mfuko Mkuu waSerikali?

SPIKA: Majibu ya swali hilo moja Mheshimiwa NaibuWaziri, tafadhali.

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA, (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, kama ambavyo nimeeleza kwenye majibu yangu ya

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

msingi kwamba suala la posho za Madiwani, kwanza kimsingiyanatokana na mapato ya ndani na suala lingine ni uwezowa halmashauri yenyewe na Mheshimiwa Rais alishatoamaelekezo kwa Wilaya hizi ambazo zilikuwa zinakusanyamapato kupitia korosho wajipange kwa msimu mwingine wakorosho wafanye kazi vizuri ili waweze kupata mapato hayo.Sisi maelekezo yetu ni kwamba tutatoa maelekezo nahalmashauri italipa Madiwani kulinga na uwezo wao wandani, ahsante.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Zitto Kabwe.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwahalmashauri ambazo zinalima korosho maamuziyanayohusiana na ununuzi wa korosho ndiyo yaliyopelekeawao kupoteza mapato. Kuna halmashauri ambazomakusanyo yake sasa hivi ni 6% tu kwa sababu fedha zakezote walikuwa wanategemea korosho, Serikali haioni nibusara kufanya compensation ya fedha hizi ili halmashaurihizi ziweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida ikiwemokuwalipa Madiwani? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo la compensation,compensation yenyewe siyo kwa korosho tu hata wenginewana….

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA, (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, nadhani jambo hili kila halmashauri inapanga mipangoyao na kilichofanyika na Serikali ni kwamba ilikuwa ni lazimatuchukue hatua kuwawezesha watu wetu waweze kuuzakorosho zao, lakini halmashauri zenyewe maelekezo ya Serikalini kwamba kwa kuwa hiki kilikuwa ni kipindi cha mpitotunaamini kwamba msimu ujao watajipanga vizuri wawezekukusanya kwa kuzingatia Sheria na miongozo yao. Kwa sasasuala la compensation halitakuwepo kwa sababu hiyo bajetihatuna, ahsante.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, nawaonaWaheshimiwa Wabunge swali hili ni gumu, tuokoe muda

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

tuende mahali pengine, ndiyo Waheshimiwa halmashaurinyingi sana mapato yake ya ndani si makubwa kihivyo. Hayomapato yakishapatikana utoe asilimia 40 iende kwenyemaendeleo, utoe asilimia 20 irudi kwenye vijiji, utoe asilimia10 ya lishe tayari hapo sijui imeshakuwa asilimia ngapi, utoerunning ya halmashari, huwezi ukawa na fedha ya kulipaMadiwani, Never, huwezi. Kwa hiyo, inatakiwa iangaliwe vizurikabisa, hii posho ya Madiwani labda iwe pledged Serikali Kuuau la sivyo sijui nini kifanyike lakini ni disaster, ndiyo maananikasema ni swali gumu. (Makofi)

Mheshimiwa Khatib Said Haji wa Konde, MheshimiwaKhatib.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Sijui ni namba ngapi.

SPIKA: Swali namba 211.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsantesana, naomba swali langu namba tatu lipatiwe majibu.(Kicheko)

SPIKA: Swali namba tatu halipo tunaendelea na swalilingine.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, namba 213samahani, 211, samahani. (Kicheko)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriTAMISEMI, Mheshimiwa Khatib leo sijui ameamkia wapi leo,inaelekea ameamkia Mtera. (Kicheko)

Na. 211

Kuongeza Fedha za Mfuko wa Jimbo

MHE. KHATIB SAID HAJI aliuliza:-Fedha za kuchochea Maendeleo ya Jimbo (CDCF),

zimekuwa msaada mkubwa katika kusaidia MaendeleoMajimboni.

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza viwango vyafedha hizi ili kuleta ufanisi zaidi?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziriwa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Khatib Said Haji, Mbunge Konde kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Kuchochea Maendeleoya Jimbo yaani Constituency Development Catalyst Fund,ulianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 16 ya Mwaka 2009yaani The Constituency Development Catalyst Fund Act,2009. Lengo la Mfuko ni kuhakikisha miradi ambayo nivipaumbele vya wananchi katika Jimbo husika na ambayohaikupata fedha katika bajeti inapata fedha za utekelezaji.Kwa tafsiri ya Sheria iliyoanzisha Mfuko, fedha za Jimbo nikwa ajili ya Majimbo ya uchaguzi ambayo yameanzishwana Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia Ibara ya 75 yaKatiba ya Jamhuri ya Muungao wa Tanzania. Vigezovinavyotumika kugawa fedha ni ukubwa wa eneo, idadi yawatu na kiwango cha umasikini katika Jimbo husika.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiongeza fedhahizi kwa kadri ya upatikanaji wa fedha ambapo mwaka 2018/2019, Serikali iliongeza kiasi kinachotolewa kutoka shilingibilioni 10 zilizokuwa zikitolewa kipindi cha nyuma mpakashilingi bilioni 12.5 na Serikali itaendelea kuongeza kiwangocha fedha kinachotolewa kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kutumia fedha zaMfuko wa Jimbo umeainishwa katika Sheria ya Mfuko KifunguNa. 10(1) kwamba kutakuwa na Kamati ya Mfuko waKuchochea Maendeleo ya Jimbo katika kila halmashauriambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Jimbo husika.Miongoni mwa majukumu ya msingi ya Kamati hii nikuchambua miradi inayowasilishwa kutoka kwenye jamii nakuidhinisha miradi itayotekelezwa na jukumu la Mkurugenzi

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Mtendaji ni kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Kamatihii. Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Khatib.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante,kuna baadhi ya halmashauri hufanya matumizi ya fedha hizibila kumshirikisha Mheshimiwa Mbunge, na hayo yako hasakwa upande wa Zanzibar. Je, Serikali inatoa kauli gani iliwaache tabia hiyo mbaya na kujua kama Mbunge ndiyomhusika mkuu na msimamizi wa Mfuko huo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, sijui huku Bara lakinikwa upande wa Zanzibar Mheshimiwa Mbunge baada yakupitisha matumizi ya fedha hizi, halmashauri inakuwahaimshirikishi katika suala lolote tena. Je, mamlaka yaMbunge katika kusimamia fedha zile kwa upande waZanzibar ni ya halmashauri au ni Mbunge anahusika mwanzohadi mwisho? Ahsante sana.

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriTAMISEMI, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, swali la kwanza, anataka kujua kama fedha hii inawezaikatumika bila Mbunge kuhusika. Kama ambavyo nimeelezakwenye jibu langu la msingi ni kwamba Mwenyekiti wa fedhahii ya Mfuko wa Jimbo ni Mbunge mwenyewe na wametajwavizuri wajumbe wa Mfuko wa Jimbo, Madiwani wawili kwakuzingatia jinsia, Watendaji wawili wa Kata au Viti Maalumlakini na mtu mmoja ambaye anakuwa ni kutokana na NG’Okatika Jimbo husika, halafu anaongeza na Katibu wa Mfukohuu anakuwa ni Mchumi katika halmashauri husika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kama kuna fedhainataka kutumika, kwa vyovyote vile hata kama Mbungehatakuwa Jimboni ni lazima Mkurugenzi wa halmashauri hiyoafanye consultation na Mbunge wa Jimbo kama Mwenyekitina kama hatakuwepo maana yake Mbunge ataridhia labda

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

Diwani miongoni mwa wale Madiwani kwa sababu shughulihaziwezi kusimama ili aweze kufanya kazi hiyo. Miradiinapopitishwa Mkurugenzi kazi yake ni kwenda kupitishafedha ikatumike na siyo kupanga kwamba ongeza, punguzahiyo hairuhusiwi kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili linafanana na lakwanza, kama nilivyosema na naomba nirudie tumepatamalalamiko kwa kweli karibu Wabunge wengi hapawanalalamika. Wakurugenzi wa halmashauri hawanamaamuzi katika fedha hizi, hizi fedha zinaenda kwenye vikaona Wabunge ambao ni Wenyeviti wenyewe wanajadili, nainawezekana Mbunge akaenda kwenye eneo A au Kijiji Bakasikiliza kero za wananchi au Mwenyekiti wa Mtaa auMheshimiwa Diwani au wananchi wa kawaida wakalalamika,Mbunge anaweza akasema napeleka shilingi laki tano hapa.Kwa hiyo Mkurugenzi hawezi kubadilisha haya maelekezo yaMbunge kwa sababu ndiyo uwezo wake. Ndiyo maanainaitwa Fedha ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo, kwa hiyo,wale Wakurugenzi ambao wana tabia ya kutumia fedha bilaMbunge tunaomba majina yao tutawashuhulikia kwa sababuSheria imetaja vizuri namna ambavyo wanapaswa kufanya.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumeelekeza, ukishapitisha fedhahizi kwenda kutumika ni lazima Kamati ya Mfuko wa Jimboiende kufanya ziara ikakague hiyo miradi kama kweli ipo nakama imetekelezwa na anayetajwa pale ni Mbunge. Hii nifedha ya Serikali, lazima isimamiwe vizuri na Sheria imeelekezakwamba Mbunge inawezekana hana fedha mfukoni kutoalakini kupitia Mfuko huu unaweza ukatamka neno kwawananchi na roho za wananchi zikapona, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Wabunge mkumbuke neno moja tu, kunaKamati ambayo wewe ni Mwenyekiti usije ukafikiri weweMbunge ndiyo Kamati. Ukaanza tu dish out na fedhaunavyotaka, lazima Kamati ipitishe maana yake ni Sheria.Waziri wa Nchi nimekuona Mheshimiwa. (Kicheko)

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika,makofi kwa majibu ya Serikali kutoka kwa Wabungeyanaashiria kwamba yako matatizo katika uendeshaji namatumizi na usimamizi wa Mfuko wa Jimbo ambao lengolake mahsusi ni kuhakikisha kwamba Wabungewanachochea shughuli za maendeleo katika Majimbo yao.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaomba Serikali sisi mtuachie piatwende tukashauriane na Waziri mwenye dhamanaikiwezekana Serikali itoe waraka wa maelekezo tena kusudikila halmashauri iweze kusimamia utekelezaji wa kisheria wamfuko huo, lakini vilevile tuwaombe Waheshimiwa Wabungekama Wenyeviti wa Mifuko hiyo, waone kwamba wanawajibu pia wa kuhakikisha kwamba matumizi ya fedha yaMfuko wa Jimbo yanafanyika kwa kuzingatia Sheria. (Makofi)

SPIKA: Hilo litasaidia sana, litasaidia sana ukitoa hiyonanii. Mheshimiwa Neema William Mgaya, uliza swali lakotafadhali.

Na. 212

Fedha za “On call Allowance” kwa MadaktariHospitali za Wilaya

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali italeta fedha za on call allowancekwa madaktari wanaofanya zamu hasa katika hospitali zaWilaya na vituo vya afya ambavyo mapato yake ni madogokwani sasa ni zaidi ya miaka miwili fedha hiyo haijaletwa naSerikali?

SPIKA: Bado tuko TAMISEMI, majibu ya swali hiloMheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Naibu WaziriTAMISEMI tafadhali. On call allowance ya madaktari.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisiya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa NeemaWilliam Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hapo awali Serikali i l iwekautaratibu wa kulipa fedha za on call allowance kupitia Hazina,ambapo halmashauri ziliwasilisha orodha za madaktari nawataalamu wote wanaostahili kulipwa fedha za on callallowance. Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo hupeleka madaihayo Wizara ya Fedha na Mpipango. Hata hivyo utaratibuhuo ulipelekea baadhi ya wataalam wasiyo waaminifu kutoataarifa ambazo siyo sahihi na hivyo kusababisha madenimakubwa kwa Serikali.

Mheshimiwa Spika, ili kuondokana na hali ya kuwana madeni makubwa yasiyo na uhalisia, halmashaurizilielekezwa utaratibu wa kuweka fedha za on call allowancekwenye mipango na bajeti zao ili kuweza kulipa stahiki hizi.Pamoja na kuweka fedha za on call allowance kwenyemipango na bajeti, ilibainika kuwa zipo halmashauri zenyeuwezo mdogo wa kimapato hivyo maelekezo yaliyotolewahospitali na vituo vya afya kutenga asilimia 15 kutoka kwenyemapato yatokanayo na uchangiaji wa huduma za afya kwaajili ya kulipa motisha kwa wataalam ikiwa ni pamoja na oncall allowance.

SPIKA: Swali la nyongeza Mheshimiwa Neema Mgaya.

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante.Kwanza niipongeze Serikali kwa kuweza kudhibiti mianya yaupotevu wa fedha ya Serikali. Lakini Mheshimiwa Waziripamoja na kwamba mmeelekeza ile asilimia 15 ya mapatokutoka kwenye hospitali na vituo vya afya ziende kulipa oncall allowance kwa madaktari hawa, lakini bado kunachangamoto kwa sababu kuna halmashauri ambazo ni nyingizina mapato madogo sana.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Sasa je, nyie kama Wizara mmejipangaje kuhakikishakwamba zile halmashauri ambazo mapato yake ni madogomtumie njia gani nyingine ambayo itakuwa muafaka ilikuweza kuhakikisha kwamba madaktari hawa wanapatastahiki zao? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa badokumekuwa na changamoto za kupandishwa vyeo kwamfano kutoka clinical officer kwenda kuwa daktari lakini vilevile kutoka mkunga kwenda kuwa muuguzi na vile vilepromotion zao bado tumeziona zikiwa zina suasua. Je, nyiekama Wizara mmejipanga vipi kuhakikisha kwambamnatatua changamoto hii pia? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriTAMISEMI, Mheshimiwa Kandege tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, kwanza naomba uniruhusu kipekee nitumie fursa hiikumpongeza Mheshimiwa Neema, amekuwa mstari wambele katika kuhakikisha kwamba wananchi wa Mkoa waNjombe wanapata huduma nzuri ya afya. Binafsiameonekana akichangia mifuko ya saruji lakini pia nikimuonaamepeleka mashuka kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya pongezi hizo, katikaswali lake la kwanza anaongelea namna ambavyouwezekano mdogo kwa baadhi ya halmashauri. Kwanzakatika kuimarisha tumeajiri wahasibu zaidi ya 350 ambaokatika vituo vya afya wameenda kusimamia na mapatoyameongezeka. Hakika fedha hii ikiweza kusimamiwa vizurihakuna uwezekano wa kwamba madaktari na wauguziwanaweza wasilipwe on call allowance. Nilienda kituo chaafya Kisosora pale Tanga nimekuta katika fedha ambazozinapatikana mpaka wanafanya na ukarabati katika vituovya afya. Kwa hiyo, ni suala tu la kusimamia vizuri na hakikamaeneo yote ambayo yanasimamiwa vizuri, fedha inatoshana hatujapata malalamiko hivi karibuni.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili anaongeleasuala zima la kuwapandisha vyeo. Hizi n afasi zinategemeanana ujuzi kwa hiyo si rahisi kwamba mtu atapanda bila kwendakuongeza ujuzi na ni matarajio ya Mheshimiwa Mbungekwamba asingependa akapandishwa cheo mtu ambayehana ujuzi mahsusi na ndiyo maana zimekuwa zikitolewa fursaza wao kujiendeleza na pale anapojiendeleza na kuhitimuakirudi huwa anapandishwa cheo.

SPIKA: Tunaendelea na Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki. Swali la Mheshimiwa Ussi SalumPondeza. Mheshimiwa Ussi tafadhali.

Na. 213

Viongozi wa Kimataifa Wanaotembelea NchiniKutokufika Zanzibar

MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:-

Viongozi wa Kitaifa wanaofanya ziara Tanzaniawalikuwa wakifika Zanzibar na kuonana na Rais wa Zanzibar:-

(a) Je, kwa nini katika siku za karibuni viongozi haowamekuwa wakiishia Tanzania Bara?

(b) Je, ni viongozi wangapi wa Kimataifa ikiwemoMarais ambao wamefanya ziara Tanzania katika kipindi cha2016/2017 na nchi wanazotoka?

(c) Je, kati ya viongozi hao wangapi wamefikaZanzibar na wangapi hawakufika na kwa sababu gani?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa William TateOlenesha, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI alijibu:-

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, napenda kujibu swalila Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza Mbunge wa Chumbunilen ye kipengele (a), (b) na (c) kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika, kwa kawaida viongozi wa Kitaifawanapokuja nchini wanakuwa na ratiba ya maeneoambayo wameyaainisha kuyatembelea kulingana na mudawaliopanga kuwepo nchini. Pamoja na hilo Wizara imekuwaikiwashauri viongozi hao kuzuru maeneo m balimbali ya nchihususan Zanzibar ili pamoja na mambo mengine kukutanana kufanya mazungumzo rasmi na viongozi wa Serikali yaMapinduzi Zanzibar na kutembelea vivutio mbalimbali vyautalii vilivyopo Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha kuanzia mwaka2015 hadi Aprili, 2019 jumla ya viongozi 21 wa Kimataifawalitembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Viongozihawa walitoka katika nchi za Afrika Kusini, Burundi, Chad,Cuba, Ethopia, India, Jamhuri ya Democrasia Congo, Jamhuriya Korea, Msumbuji, Morocco, Mauritius, Misri, Malawi,Rwanda, Uturuki, Uganda, Vietnam, Sudan Kusini, Sri Lanka,Switzerland, Zambia na Zimbabwe.

Mheshimiwa Spika, kati ya viongozi hao wa Kimataifawaliotembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tisawalifika Zanzibar na 12 kati yao hawakufika Zanzibar. Sababuzinazopelekea kutofika kwao ni kutokana na aina ya ziara,ratiba ya ziara husika na ufinyu wa muda katika ziara. Sababunyingine ni vipaumbele na malengo ya ziara za viongozi haopamoja na utashi wa kiongozi husika. Serikali kupitia Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikiimeendelea kushauri viongozi wa Kitaifa kutoka nchi za kigeniwanaozuru nchini kutembelea Zanzibar katika ratiba zao.Aidha, Wizara kupitia Idara ya Mambo ya Nje Zanzibarimekuwa ikifanya maandalizi stahiki ya kiitifaki ili kurahisishaviongozi hao kutembelea Zanzibar.

MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Nashukuru sana kwa majibu hayo mazuri ya

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

Mheshimiwa Waziri lakini je, Serikali ya Muungano au Wizarahii ya Mambo ya Nje inazishauri zile nchi wakati zina mpangowa kuja kutembelea Tanzania kuziarifu kuwa nchi yetu yaTanzania ina sehemu mbili za Muungano na kila sehemu inamahitaji yake ya kiuchumi. Hivyo basi, Wizara ingekuwainazishauri kwa sababu ukiangalia nchi tisa tu ambazozimekuja Zanzibar naamini zingekuja na hizi nchi nyingine 12kuna fursa nyingi ambazo ziko Zanzibar ambazo bara hakunana kuna fursa ambazo ziko bara ambazo Zanzibar hakuna.

Mheshimiwa Spika, tunaiomba Wizara iwezekuzishawishi wakati nchi za nje zinapoweza ku-engage kujaZanzibar kuja kutembelea Tanzania. Basi iziambie kuwaTanzania ina nchi mbili na nchi hizo mbili kila upande unavipaumbele vyake vya kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ambalo natakaniliseme, Wizara inafanya jitihada gani kuwashawishi waleviongozi ambao hawakuja Zanzibar kutembelea wakati waziara zao lakini kufanya ushawishi wakutane na viongozi waZanzibar huku Tanzania Barai ili wale viongozi wa Zanzibarwaweze kutoa haja zao na kuweza kutoa ushahwishi waowa kuiona Zanzibar nayo inanufaika na ugeni ule. Ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Hivi Mheshimiwa Ussi ungependa kazi hiyowewe, watu wametoka nchi za nje wanakuja halafu unaanzakuwaambia Tanzania ina nchi mbili, watakuelewa kweli?Wataelewaje? Haya matatizo yenu wenyewe bwana hayo!Wao wanakuja kwenye nchi moja inaitwa Tanzania weweunaanza tena kusema Tanzania ina nchi mbili unamwambiamtu wa nje, majibu tafadhali. Tanzania ni nchi moja bwana.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Spika, nchi yetu ni nchi mojakwa mujibu wa Ibara ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania ya mwaka 1977. Na masuala ya nje ni sual alaMuungano kwa m ujibu wa Ibara ya 4 nyongeza ya kwanzaya Katiba. Kwa hiyo, uhusiano wetu na mambo ya nchi zanje unachukulia maanani suala la kwamba ni nchi moja.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mahusiano yetu maranyingi tukiwasiliana wanafahamu kwamba kuna nchi mojainaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pamoja na hayo,Serikali na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje imekuwa ikifanyajitihada kubwa sana kuhakikisha kwamba kwa sababu yahistoria ya Muungano wetu na hali halisi kwamba niMuungano ambao umetokana na nchi mbili tunahakikishaya kwamba wakati viongozi hao wanapokuja nchini,tunajenga ushawishi mkubwa ili watembelee Zanzibar nandiyo maana kuanzia 2015 mpaka sasa viongozi 21waliotembelea nchini kwetu. Tisa kati yao wametembeleaZanzibar, vile vile ifahamike kwamba kuna wengine vile vileambao wametembelea Zanzibar tu wala hawajatembeleaupande mwingine wa Jamhuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba tu nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba kati ya masuala ambayoyanapewa kipaumbele sana katika uhusiano wa Kimataifani Muungano wetu ndiyo maana hata kwenye Wizara yaMambo ya Nchi za Nje kuna Idara maalum inahusika namambo ya Zanzibar. Mualiko wowote au kiongozi yeyote akijaushawishi mkubwa unafanyika ili aweze kutembelea pandezote mbili za Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa mara nyingi kamanilivyosema kwenye jibu langu la msingi mara nyinginelinakuwa ni suala la utashi wa kiongozi mwenyewe nahauwezi kumlazimisha. Kwa hiyo, nimueleze tu kwanmba kwakweli Serikali inajitahidi sana kuhakikisha kwamba viongozihawa wanapata fursa ya kutembelea maeneo yote na hasakujaribu vile vile kuelezea kuhusu fursa za kiuchumi na za kitaliizilizopo Zanzibar.

SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Ally Saleh, swali lanyongeza tafadhali.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante,nchi hizi zilipoungana tulikubaliana kwamba tutakuwa naSerikali mbili na tutakuwa na nchi mbili, Taifa ndiyo moja,Tanzania lakini nchi ziko mbili na hali hii ya viongozi wa nje

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

kwenda ina historia ndefu kwenda Zanzibar kama AbdulNassor, Nelson Mandela, Fidel Castro, Indira Gandhi nawengine wengi wamekwenda.

Mheshimiwa Spika, lakini hivi karibuni miaka kama 10nyuma ulizuka utata kwa sababu wanapigiwa mizinga naikaja hoja kwanini wapigwe mizinga Dar es Salaam na kishawapigiwe mizinga Zanzibar.

Swali langu linakuja hapa, je, hamuoni kwamba kwakutowaambia wageni wanaokuja hapa kwamba kuna Taifamoja na kuna nchi mbili kunaleta mzozo na kunaletasintofahamu kubwa kwamba kunaonekana Zanzibarhawapewi hadhi ambayo inastahiki? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh kabla hujakaa, tupereference ya Katiba hilo unalolisema. Mahali gani kwenyeKatiba imeandikwa Taifa moja nchi mbili.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, nimesemakwamba kutakuwa na Serikali mbili na Zanzibar ni nchi ndaniya Tanzania hata katika Katiba ya Warioba ilisema kwamba…

SPIKA: Nimesema tupe reference ya Katiba iliyokosasa wapi maneno haya yanasemwa, ili swali lako liwe swali,vinginevyo sio swali.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, hakuna mtuyeyote aliambiwa atoe reference akiuliza swali.

MBUNGE FULANI: Ally acha uchochezi huo bwana.

SPIKA: Hakuna swali, huo ni uchochezi, tunaendelea!Huwezi kuzua mambo tu ya kichwani kwako ukafanya ndiyosera za nchi. Wewe ni Mwanasheria bwana, tupe Katiba wapiinasema haya maneno, haya ni maneno ya mtaani haya.

Wizara ya Maji, swali la Mheshimiwa Lathifah HassanChande, Tanzania ni nchi moja, Taifa moja.

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

Na. 214

Mradi wa Maji Liwale

MHE. CECIL D. MWAMBE (K.n.y MHE. LATHIFAH H.CHANDE) aliuliza:-

Serikali iliahidi Mji wa Liwale Kufanyiwa usanifu wamradi wa maji:-

(a) Je, ni lini mradi huo uliofanyiwa usanifu utakamilikana kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa Liwale?

(b) Je, ni kata zipi zilizopo katika Wilaya ya Liwaleambazo zitanufaika na mradi huo wa maji?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa ruksa yako kwanza naombanitoe pole kwa wananchi wa Pangani na Chama chaMapinduzi na wanaCCM wote kwa kuondokewa na Mzeewetu ndugu Hamis Mnegerwa ambaye ni Mwenyekiti wachama chetu Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Pangani.Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Amin.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lathifah Chande,Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu (a), (b) na (c) kwapamoja kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamotoya upatikanaji wa maji katika Mji wa Liwale ili kutatuachangamoto hiyo, Serikali inatekeleza mipango ya mudamrefu na muda mfupi. Kwa upande wa muda mfupi katikamwaka wa fedha 2018/2019 Serikali imekamilisha mradi wauboreshaji wa huduma ya maji katika Mji wa Liwale.

Mheshimiwa Spika, kazi zilizotekelezwa katika mradihuo ni ukarabati wa kituo cha kusukuma maji, ununuzi naufungaji wa pampu, ununuzi na ulazaji wa mabomba,

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

usambazaji maji umbali wa kilometa 16 pamoja na ununuziwa dira za maji 200 kwa gharama ya shilingi milioni 264.Kukamilika kwa mradi huo kumeongeza hali ya upatikanajiwa huduma ya maji kutoka masaa matano kwa siku hadimasaa 12 kwa siku.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa muda mrefu,Serikali imepanga kufanya upembuzi yakinifu, usanifu wa kinana uandaaji wa vitabu vya zabuni ambazo kazi hiyoimepangwa kufanyika mwaka wa fedha 2019/2020.Kukamilika kwa kazi hiyo kutatoa gharama halisi ya utekelezajiwa mradi mkubwa katika Mji wa Liwale pamoja na kuainishakata zitakazonufaika na mradi huo.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi ili niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, utakumbuka wakati MheshimiwaRais, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli analihutubia Bungehili wakati wa ufunguzi wake alisema asingependa tenakusikia tena hili neno la upembuzi yakinifu likiendelea kutumikakwa sababu linaonesha ni ambalo limekuwa liki-roll onmambo yaani ni utaratibu tu wa kutaka kuchelewesha. Sasatunafahamu Serikali ina mipango yake na hapa unasemaspecifically kwamba itafanyika kwenye Mwaka wa Fedha2019/2020. Sasa je, Serikali iko tayari kutueleza ni lini specificallymradi huu utaanza kufanyika ili kuondoa kero ya watu waLiwale? Swali langu la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, ni kwambamatatizo yaliyoko Liwale yanafanana kabisa na matatizoyaliyoko Jimbo la Ndanda hasa kwenye Kata ya Nanganga.Kata ya Nanganga kuna mradi ambao ulikusudiwa upelekemaji kwenye vijiji vya Chinyanyila, Nanganga A na B, Mkweramoja na Mbili pamoja na Mumburu 1 na 2 pamoja na vijijivya Chipite. Mpaka sasa hivi tunaonge ahapa mradi uleulitekelezwa chini ya kiwango na inasemekana kwambamkandarasi amekimbia hajaukamilisha na hajaukabidhikufanya commissioning kama ambavyo ilikusudiwa.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Sasa nimuulize Mheshimiwa Waziri, je, yuko tayarikupeleka wataalam wake kutoka Makao Makuu ya Wizaraya Maji wakauchunguze mradi huu na kutoa majibu stahikikwa wananchi wale?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriMaji, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaSpika, napenda kumjibu Mheshimiwa Mbunge, moja; Wizarayetu ya Maji jukumu lake ni kuhakikisha Watanzaniawanapata maji safi na salama lakini katika kuhakikishatunatatua tatizo la maji katika Mji huu wa Liwale, kuna miradiambayo inaendelea. Moja, mradi wa Kipure pamoja naMangilikiti na Nanyungu yote ni katika kuhakikisha tunatatuatatizo la maji na hata katika bajeti hii yetu ya 2019/2020tumetenga zaidi ya 699,000,000 katika kuhakikisha tunatatuatatizo la maji. Kubwa, Mhandisi wa Mkoa, wahandisi wawilaya wahakikishe fedha hizi zinatumika kuweza kutatuatatizo la maji.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu mradiambao ameuelezea nataka nimhakikishuie, sisi kama Wizaraya Maji hatutakuwa kikwazo kutuma wataalam kwendakuukagua mradi huo na mimi kama Naibu Waziri niko tayarikuongozana na wewe katika kuhakikisha tunaenda kuchukuahatua nzitio. Ahsante.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Chatanda naMheshimiwa Mbunge wa Liwale.

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Spika,nashukuru, naomba kuuliza swali la nyongeza, Korogwe Mjituna kijiji kinaitwa Mahenge, kiko nje kabisa ya Mji waKorogwe na katika mpango wa miji 28, sina hakika kamakinaweza kikafikiwa na ule mradi wa maji.

Je, mtakuwa tayari kukipatia maji kijiji hicho kwakuwapa kisima cha maji kirefu? (Makofi)

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

SPIKA: Majibu ya swali hilo ni majirani zako hawanatumaini unapafahamu Mahenge.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaSpika, kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza MheshimiwaMbunge anafanya kazi kubwa sana katika Jimbo lake walahaina haja ya kulalamika sana kwa sababu ukimuona mtumzima ujue kuna jambo. Labda tuwaagize watu wa DDCIwaende kuchimba kisima haraka pale ili wananchi wakewaweze kupata maji safi na salama. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Kuchauka, Mbunge wa Liwale.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Katika mradi wa kutafuta chanzo cha pili cha mbadala chamaji ya Wilaya ya Liwale palitolewa shilingi milioni 300 naDDCIA walishaanza kufanya kazi hiyo lakini wamechimbavisima viwili ambavyo vina uwezo wa kutoa maji lita 5,000lakini visima vile vimetelekezwa mpaka leo.

Je, Serikali iko tayari kutoa fedha kwa ajili ya kwendakufanya uendelezaji wa visima vile ambavyo viko katika Kijijicha Makata na kijiji na Mikunya?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. Visima hivyovya Makata na Mikunya.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaSpika, kwanza labda kwa nia njema kaisa katika kuhakikishavisima hivi vinakuwa endelevu labda baada ya saa sabanikutane na Mheshimiwa Mbunge na tuweze kufanyamawasiliano na wenzetu ili tangalie ni namna gani tunawezatukasaidiana naye. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Kwa sababu ya muda Waheshimiwa Wabungetuvumialne. Bado tupo Wizara ya Maji. Swali la MheshimiwaMethusalah Mbunge wa Kilolo.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Na. 215

Ujenzi wa Mabwawa Kilolo

MHE. VENANCE M. MWAMOTO aliuliza:-

Je, Serikali imetenga fedha kiasi gani ya ujenzi wamabwawa ya maji ili kupunguza matatizo ya maji katikaWilaya ya Kilolo.

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji,

naomba kujibu swali la Mheshimiwa Venance Mwamoto,Mbunge wa Jimbo la Kilolo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma yamaji katika Halmashauri ya Kilolo kw aupande wa Vijijini niasilimia 71. Kilolo Mjini ni asilimia 80 na Ilula ni asilimia 47.5.Aidha, halmashauri ya Wilaya ya Kilolo imekamilisha ujen ziwa miradi ya vijiji 10 kupitia Programu ya Maendeleo ya Sektaya Maji pamoja na Ujenzi wa vijiji vitano kupitia ufadhili waTaasisi isiyo ya Kiserikali ya WARIDI.

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019,Halm ashauri ya Wilaya ya kilolo inatekeleza miradi ya majikatika vijiji vitatu vya Lundamatwe, Kitelewasi na Ilambo. Piamiradi miwili katika miji midogo ya Kilolo na Ilula. Aidha,Halmashauri ya Kilolo kwa kutumia fedha za ndani inakarabatimabwawa matatu yaliyopo katika vijiji vya Uhambingeto,Image na Mgowelo kwa ajili ya binadamu na mifugo.

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachanngamoto ya uhaba wa maji kwa mwaka huu wa fedha2018/2019 Halmashauri ya Kilolo imepokea jumla ya shilingibilioni 1.7 ili kuhakikisha miradi ya maji inatekelezwa nakukamilika na kuwapunguzia keri ya maji wananchi wa wilayahiyo.

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge wa Kilolo nilikuonatafadhali.

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naombaniulize maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Wazirialifanya ziara katika Mji wa Ruaha Mbuyuni baada yakuonekana kuna shida kubwa sana ya maji na kipindupindukinatokea kila mara na akaahidi pale kwamba kichimbwekisima kwa tahadhari ili wananchi waanze kupata maji. Lakinikwa masikitiko makubwa wale wataalam wamepuuzwahakuna aliyefika pale. Sasa Mheshimiwa Naibu Waziriatakubali tena kwenda kuona hali ilivyo na wananchiwanazidi kuteseka?

Swali la pili, kwa kuwa Serikali kuna wahisani ambaohuwa wanansaidia Serikali, kuna tatizo kubwa katika Kijiji chaUdekwa na Mlafu, tayari Serikali ya Italy, kupitia Shirika linaitwaWAMAKI liko tayari kusaidia, lakini linataka commitment yaSerikali, yenyewe litasaidia kiasi gani, ili na wao wawezekusaidia fedha. Je, Serikali sasa itakuwa tayari kusaidia iliWAMAKI waweze kutoa maji safi na salama kwa kata mbili.(Makofi)

SPIKA: Majibu maswali hayo Mheshimiwa Naibu WaziriMaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaSpika, kwanza nikiri kabisa nilifika Kilolo na nimeona kazi nzuriambayo inafanywa na Mheshimiwa Mbunge VenanceMwamoto katika Jimbo lake. Lakini kikubwa tulifika kweliRuaha Mbuyuni na tukaona changamoto ile na tukatoaagizo, watu wa Bonde walikwenda walishafanya tafiti yaupatikanaji wa maji. Labda nimuagize sasa Mhandisi waMkoa, ahakikishe kabisa kile kisima kinachimbwa ili wananchiwale waweze kupata maji na anipatie taarifa.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu suala lake la pili,pamoja Serikali imekuwa ikitatua tatizo la maji, imekuwaikishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo. Natakanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Serikali tupo

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

tayari kukaa nao, tuangalie ni namna gani tunawezatukashirikiana katika kuhakikisha tunatatua changamoto hii.Ahsante sana.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri ahsante sana,tunahamia Fedha na Mipango, swali la Mheshimiwa JumaOthman Hija, Mbunge wa Tumbatu.

Na. 216

Malengo ya Benki ya TPB

MHE. JUMA OTHMAN HIJA Aliuliza:-

Miongoni mwa malengo ya Benki ya TPB ni kupelekahuduma ya kibenki kwenye maeneo ya vijijini na pembezoniambayo hayafikiwi na huduma hizo:-

Je, ni kwa kiasi gani lengo hilo limefikiwa mpaka kufikiamwaka 2018?

SPIKA: Ahsante sana Juma, majibu ya swali hiloMheshimiwa Naibu Waziri Fedha na Mipango, MheshimiwaDkt. Ashatu Kachwamba Kijaji.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha naMipango, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Juma OthmanHija, Mbunge wa Tumbatu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, miongoni mwa malengo ya Benkiya TPB ni kupeleka huduma za kibenki na pembezoni mwamiji, kuongeza wigo na mtadao wa biashara ya benki yakutumia teknolojia ya kisasa.

Katika kutekeleza malengo haya, Benki ya TPBimefanikiwa kuboresha huduma za kibenki kupitia mtandaowa ofisi 200 za Shirika la Posta Tanzania zilizopo katika kilawilaya na baadhi ya tarafa na kutumia teknolojia ya habari

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

na mifumo ya kisasa kutoa huduma za kibenki ikiwemo simuza kiganjani (TPB POPOTE), mawakala wa kampuni za simu,mashine za POS pamoja na ATM katika maeneo mbalimbalihapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Benki ya TPB imefanikiwa piakuongeza idadi ya matawi makubwa kutoka 30 kwa mwaka2017 hadi 36 mwaka 2018 na matawi madogoyaliyoongezeka kutoka 37 mwaka 2017 hadi kufikia 40 mwaka2018. Idadi hii ya matawi inahusisha matawi ya iliyokuwa Benkiya Twiga na Benki ya Wanawake Tanzania. Matawi yoteyameunganishwa kwenye mfumo wa TEHAMAunaowawezesha wateja kupata huduma za kibenki bilakutembelea matawi walipofungulia akaunti zao.

Mheshimiwa Spika, vituo vya huduma ndani ya Ofisiza Shirika la Posta viliongezeka kutoa 40 mwaka 2017 hadikufikia 45 mwaka 2018. Aidha mashine za ATM ziliongezekakutoka 51 mwaka 2017 hadi kufikia 72 mwaka 2018. Vilevile,mawakala wa SELCOM POS waliongezeka kutoka 225 kwamwaka 2017 na kufikia 670 Desemba, 2018. Vituo vyote vuahuduma ndani ya Ofisi za Shirika la Posta vimeunganishwapia kwenye mtandao na mfumo wa TEHAMA wa benki nahivyo kutoa fursa kwa wateja wa vijijini na pembezoni mwamiji kupata huduma kwa wakati kama ilivyo kwa watejawengine wanaohudumiwa na matawi makubwa namadogo.

Mheshimiwa Spika, jumla ya akaunti 227,052zilifunguliwa na wananchi wa vijijini na pembezoni mwa mijikwa kutumia mfumo wa kutoa huduma za kibenki kwa njiaya simu za kiganjani, ujulikanao kama TPB POPOTE. Mfumohuu wa TPB POPOTE unasaidia wananchi kufanya malipombalimbali kama kuhamisha salio, kutuma fedha, kulipaankala za maji, kununua umeme wa luku na kununua vochaza simu bila kulazimika kwenda katika matawi ya benki yaTPB. Wateja wanaweza pia kuhamisha salio kwenda katikaakaunti nyingine, kuhamisha fedha kwenda katika akauntizao za M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na Halopesa nahatimaye kuchukua fedha kupitia mawakala.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge wa Tumbatu nilikuona,swali la nyongeza.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika,ahsante, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yakemazuri na ya kutoshereza kabisa, lakini nina swali moja lanyongeza.

Majibu yake yamejikita sana kwenye maeneo ya miji,swali langu ni kwamba Serikali ina mpango gani, hudumahizi kuzipeleka katika visiwa vidogovidogo kama vileTumbatu? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri,Benki ya Posta Tumbatu kule inafika?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, kama nilivyosema huduma zetu za TPB zimeongezekakwa kiwango kikubwa na tumeweza kuwafikia wananchiwalio wengi na kwa visiwa vyetu kwa Zanzibartumeshafungua matawi tayari na sasa tunajipanga kwendakufungua katika visiwa hivi vidogo, wakati huo tukiendeleakuwahudumia kwa kupitia mfumo wa kidigitali.

SPIKA: Tunaendelea na swali linalofuata, bado tukoWizara hiyohiyo, swali la Mheshimiwa Asha Abdullah.

Na. 217

Kuwasaidia Waliokuwa Wateja wa FBME Bank

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA (K.n.y. MHE. ASHAABDULLAH JUMA) aliuliza:-

Je, Serikali inachukua hatua gani kuwasadiawananchi walioweka amana zao katika Benki ya FBME.

SPIKA: Majibu ya swali hilo bado tuko Wizara ya Fedhana Mipango, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji tafadhali.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha naMipango, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Asha AbdullahJuma, Mbunge Vitib Maalumu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Mabenkina Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 kifungu cha 39(2) na (3),amana au akiba za wateja katika benki au taasisi ya fedha,zina kinga ya bima ya amana ya kiasi kisichozidi shilingi zakitanzania 1,500,000 tu. Endapo mteja hana salio la amanala kiasi kilichozidi shilingi 1,500,000 atapata fidia ya asilimia100.

Mheshimiwa Spika, wateja walio na amana zaidi yashilingi 1,500,000, wanalipwa shilingi 1,500,000 kama fidia yabima ya amana, na kiasi kinachobakia kinalipwa kwa mujibuwa sheria na taratibu za ufirisi. Aidha malipo kwa mujibu washeria na taratibu za ufirisi yanategemea makusanyo yafedha kutoka kwenye mauzo ya mali pamoja na fedhazilizowekezwa na benki katika taasisi mbalimbali za fedha zandani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, zoezi la kukusanya mali na fedhazilizokuwa zimewekezwa na za benki ya FBME katika taasisimbalimbali za fedha, hususan nje ya nchi, limekumbwa nachangamoto za kisheria kati ya Tanzania na nchi ya Cyprusambako benki ya FBME ilikuwa na tawi lililokuwa linaendeshasehemu kubwa ya biashara zake, na hivyo kusababishaucheleweshaji wa ukusanyaji na ugawaji wa fedha za ufilisi.Hivyo basi tarehe ya kuanza kulipa fedha zinazotokana naufilisi haijulikani kwa sasa kutokana na uwepo wa kesizinazokwamisha zoezi la ukusanyaji mali na madeni ya benkiya FBME. Serikali kupitia Bodi ya Bima ya Amana, Benki Kuuya Tanzania pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikaliipo katika mazungumzo na Serikali ya Cyprus ili kulipatia sualahili ufumbuzi.

SPIKA: Mheshimiwa muuliza swali Mheshimiwa AshaJecha.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Spika,ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri, nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa tatizo hili siomara ya kwanza kutokea hapa nchini, je, Serikali ina mkakatigani wa makusudi kuzuia jambo hili lisitokee tena kupunguzausumbufu kwa wananchi wetu? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri,Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, Serikali mikakati iliyonayo ni kusimamia sheria yamabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 kamainavyoelekeza kuhusu unazishwa na usimamiaji wa uanziswajiwa taasisi za kifedha ndani ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, na Serikali mmeona kwa sasaimekuwa, imeweka udhibiti wa hali ya juu kuhakikisha taasisizote za kifedha zinafanya kazi kulingana na sheria ili kuzuiachangamoto hizi wanazozipata wateja wetu.

SPIKA: Ahsante sana, nilikuona Mheshimiwa Nape,swali la nyongeza.

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Kutokana na majibu ya Serikali, kuna mkanganyiko mkubwana mlolongo mrefu kwa watu hawa kupata haki zao.

Sasa kwa kuwa Benki Kuu ndiyo guarantor wa hizibenki, kwa nini Serikali isimalizane na hawa wateja kwa niabaya hii benki halafu Serikali sasa ibaki ikishughulika na benki hiiwakati wananchi wakiwa wanaendelea na shughuli zao,hasa ikizingatiwa kuwa ziko taarifa kwamba, wamiliki wabenki hii wametushitaki, wameishitaki Serikali kutokana nahatua walizochukua?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu WaziriFedha, tafadhali.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, kama nilivyosema kwenye majibu yangu ya msingi,benki inapofilisika, benki inaponyang’anywa leseni yake yakufanya kazi, hatua zote za ulipaji wa wateja wa beki hiyoau taasisi hiyo ya kifedha, imetajwa katika sheria ya mabekina taasisi za fedha kifungu cha 39(2) na (3), ambako kunamaeneo mawili.

Mheshimiwa Spika, kwa wale ambao wana amanazilizo chini ya 1,500,000 hulipwa fedha zao zote, kwa waleambao amana zao ni zaidi ya hiyo, hulipwa kwa kutumiasasa sheria ya ufilisi baada ya kujiridhisha na madeni na malihalisi ya benki hiyo au taasisi ya kifedha kama ilivyoelezwa.

Mheshimiwa Spika, lakini naomba niliambia Bungelako Tukufu kwamba, siyo kwamba wamiliki wa benki ndiyowalioishitaki Serikali, hapana, waliostopisha mchakato huuni Central Bank ya Cyprus, ambayo wao wanaona wanamandate ya kuweza kulipa wateja wote wa benki hii,wakisahau kwamba kulingana na sheria ya uanzishwaji wamabenki, wanaotakiwa kulipa ni kule ambako benki hiyoilikuwa na makao makuu, na makao makuu ya benki hii yaFBME yalikuwa Dar es Salaam lakini shughuli zake nyingizilikuwa zinafanyika nchini Cyprus.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibulangu la msingi, mwezi wa nne tarehe 5 mwaka 2019, Serikalimbili zimekutana nchini Cyprus na tayari makubalianoyamefikiwa ya jinsi gani ya kuhakikisha wateja wote wailiyokuwa benki ya FBME Tanzania na FBME Cyprus wanapatahaki zao bila kupoteza chochote katika mchakato huu.

SPIKA: Hiyo ni habari njema, Waheshimiwa bado mnamaswali! Uliza swali lako Mheshimiwa.

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi, wananchi wengi wameathirikakwa kukosa fedha zao ambazo waliziweka katika benki hiina Benki Kuu inapotoa leseni au kibali kwa ajili ya kufunguabenki, wao wanakuwa ndiyo dhamana.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

Mheshimiwa Spika, na kuna methali inasemadhamana ndiyo mlipaji, lakini hata mahakamaniunapomchukulia mtu dhamana, akikimbia wewe ndiyounakamatwa unahusika na suala lile. Kwa nini Benki Kuuisiwalipe hawa watu fedha zao, halafu wao wakaendeleana huo, kwa sababu watanzania wanaathirika na hili.(Makofi)

Sasa maana ya ninyi kuwa dhamana ni nini?

SPIKA: Swali zito hilo. Mheshimiwa Naibu Waziri Fedhana Mipango, Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji, ninyi ndiyoguarantor.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, nimesema kwenye majibu yangu ya msingi, uendeshajiwa taasisi za kifedha yakiwemo mabenki imeelezwa wazikwenye sheria ya mabenki na taasisi za kifedha ya mwaka2006. Benki Kuu haiwezi kuwa dhamana na kuchukua jukumula kulipa wateja wote ndiyo maana ikaanzishwa Bodi yaAmana, kama nilivyoeleza, ambayo ina dhamana kubwa yakuwalipa wateja ambao wanamiliki amana chini ya1,500,000.

Mheshimiwa Spika, na niseme kwamba, asemawateja wengi wamepoteza, kwa experience tuliyonayondani ya Taifa letu, iknapofungiwa benki yoyote au taasisiyoyote ya kifedha, zaidi ya asilimia 90 ya wateja wa benki autaasisi husika ya kifedha, huwa ni wale wenye amana ya1,500,000 kurudi chini.

Kwa hiyo, hawa asilimia 10 iliyobaki, ndiyo nimesemakwamba, Serikali mbili zimeshakutana, mwezi Aprili, tarehe 5,2019 na tayari tumeshakubaliana jinsi ya kuliendea jambohili ili wateja wateja wote sasa waliobaki ambao ni zaidi,waliokuwa na amana ya zaidi ya 1,500,000, waweze kulipwaamana zao.

SPIKA: Mheshimiwa Turky, nilikuona, swali la mwisho lanyongeza eneo hili.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

MHE. SALIM HASSAN ABDULLAH TURKY: MheshimiwaSpika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Ukiangalia juhudiza Serikali ya kukuza uchumi huu, sasa hivi jinsi hizi benkizinavyokwenda tunaanza kupata mshituko kidogo. FBMEimezama, M Bank nayo imezama, M Bank kama ninafahamuni benki ya Tanzania hatuwahitaji Ma-Cyprus kuja kutujibu,lakini bado zile dhamana ambazo ni za Serikali, naomba sanakwamba Serikali itoe tamko rasmi kwa sababu wateja niwengi ambao wanahangaika na Serikali iko hapahapa nahii benki iko hapahapa, na sasa hivi imechukuliwa na benkinyingine ya Serikali yetu.

Kwa hiyo, tunaomba sana tujulishwe hii hatma yakudai fedha za M Bank, tunazipata vipi kwa uharaka wake?Ili watu waamini kuweka fedha benki maana sasa hivi sasawatu kuweka fedha benki tunaanza kuogopa, tunaonahizooo, zinazama. (Makofi)

SPIKA: Na ukiweka benki maana yake usiweke zaidiya milioni moja na nusu. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Waziri Fedha na Mipango tupe re-assurance, kuna usalama nchini hapa kuweka fedha benkizaidi ya 1,500,000! M Benk. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, kuna usalama mkubwa sana ndani ya Taifa letu,kwenye taasisi zetu za kifedha kwa sababu Benki Kuuu yaTanzania iko macho na iko makini kusimamia sheria yakuazisha benki hizi na taasisi za kifedha.

Mheshimiwa Spika, na niliombe sana Bunge lakoTukufu, tunapokuja na sheria ya kusimamaia hizi taasisi zakifedha, muwe mnatuunga mkono, ni kwa sababu tunaonawengi wa wateja wetu wanapoteza fedha kwa kuingia katikamifumo ambayo siyo sahihi na nilishukuru Bunge lako Tukufukwa kuturuhusu kwenye Bunge letu la mwezi wa 11 kupitishasheria ya huduma ndogo za fedha na sasa tunawafikia wotekule walipo ili kuhakikisha wateja wetu wote wanakuwasalama.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Mheshimiwa Spika, na niseme, hili la M Bank, kamaalivyosema muuliza swali, M Bank imechukuliwa na benkinyingine. Kwa maana hiyo, M Bank siyo kwanza wataja wakewanatakiwa kusubiri mchakato kwa sheria ya ufilisi, hapana.Benki iliyoichukua M Bank, ina jukumu na dhamana kubwaya kuhakikisha wateja wote wanalipwa na wanalipwaamana zao zote pale wanapozihitaji.

Mheshimiwa Spika, lakini niwaambie watanzaniakwamba, kuweka fedha zao kwenye benki zetu ni salamana benki ambayo M Bank imeunganishwa inafanya vizuri naniwaombe waendelee kuacha amana zao huko kwa sababufaida ni kubwa ya kuacha fedha zao kwenyeakaunti zao.

SPIKA: Tunahamia Wizara ya Nishati, ahsante sanaMheshimiwa Naibu Waziri Fedha kwa majibu mazuri sana.Swali la Mheshimiwa Mary Deo Muro, Mheshimiwa Mary.

Na. 218

Fidia kwa Wananchi Waliopisha Ujenzi wa Njia yaUmeme Pwani

MHE. MARY D. MURO aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwalipa fidiaWananchi wa Kiluvya, Madukani, Mwanalugali na Mikongeniambao wamepisha ujenzi wa njia ya umeme?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri Nishati, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mary Deo Muro, Mbungewa Viti Maalumu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCOinatekeleza mradi wa kujenga njia ya kusafirisha umeme wa

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

msongo wa kilovot 400 kutoka Kinyerezi (Dar es Salaam) naRufiji (Pwani) kupitia Chalinze hadi Dodoma kupitia maeneoya Kiluvya, Madukani na Mwanalugali. Mradi huu unalengakuongeza upatikanaji wa umeme katika ukanda waMashariki, Kati na Kaskazini mwa nchi kutoka katika mitamboya kuzalisha umeme ya Kinyerezi na mradi wa Rufiji.

Mheshimiwa Spika, upimaji wa njia na uthamini wamali za wananchi watakaopisha mradi ulikamilika mwaka2018. Jumla ya shilingi bilioni 21 na milioni 600 zinatakiwakulipwa kama fidia kwa wananchi katika maeneo yaHalmashauri za Kisarawe, Kibaha Mjini na Kibaha Vijijiniikiwemo wananchi wa Vijiji vya Chalinze, Kiluvya madukanina Mwanalugali. Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Serikaliimetenga fedha shilingi bilioni 50 kwa ajili ya malipo ya fidiakwa wananchi wa maeneo hayo baada ya kukamilishauhakiki wa madai hayo.

Mheshimiwa Spika, Serikali inawaomba wananchiwavute subira wakati Serikali inaendelea kukamilisha taratibuza malipo haya, ahsante sana.

SPIKA: Mheshimiwa Mary nimekuona swali lanyongeza.

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwakunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, swali la kwanzakwa kuwa wananchi wa Mkoa wa Pwani especially sehemuhizo zilizotajwa, walisitishiwa tangu 2014 wakati wa Awamuya Nne, na anasema kwamba watalipa fidia kwa uthaminiwa 2018 watu hawa walikuwa wanajenga wakaacha ujenzina gharama zimepanda.

Je, Serikali iko tayari kulipa hasara ambayomaongezeko ya gharama za ujenzi watakapokuwawanalipa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa Serikaliimekaa kimya muda wote huu.

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Je Waziri yuko tayari kufuatana na mimi baada yaBunge ili akaweze kuongea hayo ambayo ameyaeleza hapawananchi waweze kumuelewa kwa urahisi? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Nishati,Mheshimiwa Subira Hamisi Mgalu tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwanzanimshukuru kwa kufuatilia ili suala hili ni swali lake la pili, lakinipamoja naye niwashukuru Waheshimiwa Wabunge waMajimbo ya Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Chalinze kwakufuatilia hili swali kwa karibu.

Mheshimiwa Spika, lakini nataka nimuelezeMheshimiwa Mbunge na na wananchi wa Mkoa wa Pwaniwakati wa mwaka 2014/2015 Serikali ilipo design mradi huuwa Kinyerezi, Chalinze, Segera Tanga ulikuwa kablahaujafanywa maamuzi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa RufijiHydro Power.

Kwa hiyo, Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingiamadarakani na kuamua kutekeleza mradi huu kwa nia yakufanya nchi iwe na umeme wa kutosha ilibidi ifanyeutaratibu wa kuuisha upembuzi yakinifu kwa sababu mradihuu sasa wa Rufuji Hydro Power kuna njia mpya ambayoitajengwa ya KV 400 kutoka Rufiji, Chalinze ambayo inaelekeaDodoma.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndiyo suala ambalolimepelekea fidia hii kuchelewa kwa sababu lazima iuishwe,lakini tunatambua fidia inalipwa kwa mujibu Sheria na Kanuni.Kwa hiyo, malipo ya fidia hii kwa wananchi wa Mkoa waPwani yatazingatia Sheria na Kanuni za nchi ambazozinapeleka malipo haya ya fidia.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili amesema je, nipotayari?, nataka nimualifu Mheshimwa Mbunge na mimi piani mdau ni Mbunge wa Mkoa wa Pwani hivi karibuni tunilifanya ziara Kata ya Pera Jimbo la Chalinze na niliongeana wananchi suala hili.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo namkubalia kwambabaada ya Bunge hili au wakati wowote tunaweza tukafanyaziara katika maeneo ya Kibaha, maeneo ya Jimbo laSegerea, maeneo ya Kibaha Vijijini, maeneo ya Chalinzekuzungumza na wananchi na kwamba kwa kweli kamanilivyosema wakati wa bajeti yetu wataona tumedhamiliakabisa kulipa hii fidia kwa sababu mradi huu unaanzamapema Julai, 2020 na kukamilika Desemba, 2022, ahsantesana.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Salm Kikwete swali lanyongeza tafadhali.

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana, kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, mradiwa kuchakata gesi wa LNG Likong’o Lindi. Ni muda mrefusana wananchi wa eneo la Likong’o hawafanyi shughuli zaoza kilimo ili kujipatia mahitaji yao ya msingi na kuongezauchumi wao binafsi na mradi huu ni muhimu sana kwawananchi wa Lindi kwa ajili ya kuongeza uchumi wao, lakinisi hilo tu bali ni Taifa kwa ujumla kwa sababu ni mradi mkubwasana, Mheshimiwa Waziri.

Je, ni lini wananchi hawa wa Lindi hasa Likong’owatalipwa fidia zao kwa ajili ya kuinua vipato vyao na kuachaeneo hilo liendelee na kazi iliyokusudiwa? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo zuri la wananchi wa Lindi,eneo la Likong’o Mheshimiwa Naibu Waziri NishatiMheshimiwa Subira Hamis Mgalu tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwaniaba ya Waziri wa Nishati nakushukuru kwa kunipa fursa yakujibu swali la Mheshimiwa mama Salma Kikwete Mbungewa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais juu ya suala la fidia la eneola Likong’o ambalo tunatarajia kutekeleza mradi mkubwawa kujenga kiwanga cha kuchakata gesi asilia ambayoimegundulika kwa wingi katika Mikoa ya Mtwara kwa kiasicha trilioni cubic feet 55.

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Mheshimiwa Spika, nataka nimtaarifu MheshimiwaMbunge mama Salma na wananchi wa Mkoa wa Lindi Serikaliinatambua umuhimu wa mradi huu na ndiyo maanaMheshimiwa Rais alitoa maelekezo ya kukwamua mkwamoambao uliokuwepo kwa Wabia wale wa mradi wa kutakakila mmoja tuzungumze naye kwa wakati tofauti namazungumzo hayo yameanza kati ya kampuni ya BP SHELLpamoja na STATOIL ambayo kwa sasa hivi inajulikana kamaequinor.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mazungumzo hayayameanza kwa kwa kuwa sasa hivi kuna kila dalili ya mradihuu kufanyika na taratibu zinaendelea na Kamati yaWataalam wameshakaa suala la fidia kwa eneo hililimeshafanyiwa kazi na naomba nimualike MheshimiwaMama Salma Kikwete na Wabunge wote wa Mkoa wa Lindikwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati kwenye mkutanowa tarehe 21 mwezi huu wa 5 wa ku-raise awareness ya mradihuu na ambapo pia taarifa na uhakika wa ulipaji wafidiabaada ya tathimini kukamilika itatolewa.

Mheshimiwa Spika, tunawashukuru wananchi waMkoa wa Lindi kwa uvumilivu wao tunakuja tarehe 21 nakwamba kila kitu Serikali imekiweka vizuri, ahsante sana.

SPIKA: Ahsante, swali la mwisho kwa siku la leolinaulizwa na Mheshimiwa Agness Mathew Marwa, Mbungewa Viti Maalum, Kwa niaba yake Mheshimiwa Chacha.

Na.219

Nyumba Ambazo Bado Hazijapata Umeme wa REA

MHE. MARWA R. CHACHA (K.n.y. MHE. AGNESS M.MARWA) aliuliza:-

Nyumba nyingi za Vijijini hazikuwekewa umemewakati wa usambazaji japo baada ya kuweka umemekumekuwa na ongezeko la ujenzi wa nyumba na uzalishajimali kama ujasiriamali.

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha nyumbazote zilizobaki zinapata umeme kabla mradi wa REAhaujamaliza muda wake?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriNishati na Madini, Mheshimiwa Subira Hamis Mgalu tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishatinapenda kujibu swali la Mheshimiwa Agnes Mathew MarwaMbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, lengo la Serikali kupitia Wakala waNishati Vijijini (REA) ni kupeleka umeme katika Vijiji vyoteTanzania Bara ifikapo Juni, 2021. Ili kutekeleza azma hiyo,Serikali imeweka kipaumbele kwa kusambaza miundombinuya umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa namiundombinu ya umeme na katika Taasisi zinazotoa hudumaza kijamiii kama vile Shule, Zahanati, Makanisa, Misikiti, Vituovya Afya, Nyumba za Makazi na Biashara na Miradi ya Maji.Utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya III mzunguko wakwanza ulianza kutekelezwa mwezi Julai, 2018 na unaendeleakatika maeneo yote nchini ambapo utekelezaji wakeutakamilika ifikapo mwezi Juni, 2019. Maeneo yatakayobakiikiwa ni pamoja na nyumba za makazi, Taasisi, miradi ya majina biashara yatapelekewa umeme kupitia mradi wa REA IIIMzunguko wa pili utakaoanza kutekelezwa mwezi Julai, 2019na kukamilika mwezi Juni, 2021.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mpango huo, Serikaliimebuni miradi ya ujazilizi (Densification) kwa lengo lakujaziliza katika mapungufu kwa miradi iliyotangulia. Miradihii ya ujazilizi inalenga hasa kuhakikisha nyumba zote katikakila Kijiji na Kitongoji zinaendelea kupata umeme. Shirika laUmeme nchini (TANESCO) nalo linaendelea kusambaza nakuunganisha wateja mara kwa baada ya miradi ya REAkukamilika. I l i kuhakikisha wananchi wote wa Vij i j iniwanaunganishiwa umeme kwa gharama nafuu ya shilingi27,000, ahsante sana.

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

SPIKA: Mhehsimiwa Mbunge wa Serengeti nilikuona.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Spika, ahsantenaomba kwanza nichukue nafasi, nimshukuru MheshimiwaWaziri, na Naibu wake Waziri wanafanya kazi nzuri sana, nani kazi ambayo itaisaidia sana CCM 2020 tunakoenda kwenyeuchaguzi.

Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza,swali la kwanza Mheshimiwa Waziri wa Nishati alipokujaSerengeti mwaka huu mwanzoni alihaidi maeneo yayafuatayo yatapa umeme; shule ya Sekondari Inagusi ilipoKata ya Isenye, Kijiji cha Nyamatoke na Mosongo vilivyopoKata ya Mosongo pamoja na Kiyakabari Kata ya Stendi Kuu.(Makofi)

Ni lini maeneo haya yatapata umeme ambaoulihaidiwa na Mheshimiwa Waziri?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni lini TANESCO au REAwatapeleka umeme Kata ya Morotonga katika Vitongoji vyaMutukura na Romakendo?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriMorotonga iko Mugumu Mjini pale pale.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwanzatupokee pongezi zake, lakini naamini pongezi ni kuhitaji zaidihuduma. Kwa hiyo, tumepokea kwa ahadi kwambatutaendelea kufuatilia hiyo miradi. La pili pia nimpongezeyeye Mheshimiwa kwa namna ambavyo anavyofuatiliamasuala ya nishati katika Jimbo lake na sekta mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, lakini masuala yake mawiliyamejielekeza kwanza kwenye ziara ambayo imefanywa naMheshimwia Waziri wa Nishati katika Jimbo la Serengeti naahadi aliyoitoa katika shule ya Sekondari Nagusi na maeneoya Kiyabakari. Nataka nimthibitishie Mheshimiwa Mbungekwamba Mheshimiwa Waziri wa Nishati alipotoa ahadi hiialikuwa na uhakika wa utekelezaji wa mradi wa REA Awamu

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

ya III mzunguko wa kwanza unaoendelea na kwambamkandarasi Derm wa Mkoa wa Mara ni miongoni mwawakandarasi wanaofanya vizuri tulivyo wa-rank na kwambainatarajiwa itakamilisha kazi kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, maeneo aliyoyatajamara tu Julai 2019 mradi wa REA Awamu ya III unaanza nakazi ndiyo itafanyika. Kwa hiyo nimthibitishie MheshimiwaMbunge kwa kipindi hiki cha kuendelea 2019 maeneo hayayote ataiona kazi inaanza na nguzo zitapelekwa naninaomba nimuelekeze mkandarasi Derm azingatiemaelekezo ya Mheshimiwa Waziri pamoja na Meneja waTANESCO wa Mkoa wa Mara na msimamizi wa mradi wa REAkatika Mkoa wa huo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili Mheshimiwa Mbungeameulizia masuala la kwa mfano Marotonga na eneoambalo umelitaja Mgumu Mjini, yanaonyesha haya maeneoni ya ujazilizi. Kama nilivyosema kwenye jibu la msingiMheshimiwa Agnes Serikali baada ya kuona panachangamoto baada ya miradi ya REA kukamilika na kwakuwa lengo lake Serikali ni kusambaza umeme palikuwa nachangamoto ya gap ya usambazaji wa umeme. Na ndiyomaana ikabuni mradi wa ujazilizi na bahati nzuri Mkoa waMara ulikuwemo katika ujazilizi Awamu ya kwanza ambaoulikuwa kama mradi wa majaribio.

Mheshimiwa Spika, na Serikali imekuja na mradi waujazilizi Awamu ya pili, Awamu ya II(a) ambayo itakuwa naMikoa tisa na Awamu ya II(b) itakuwa na Mikoa 16, ikiwemoMkoa wa Mara na kwa kweli tunauhakika Awamu ya II(a)utafadhiliwa na Serikali za Norway, Sweden na Umoja waUlaya na hela zake tunazo bilioni 197 na Awamu ya II ya ujazilizitwo (b) itafadhiliwa na Serikali ya Ufaransa mpaka sasatunauhakika wa kiasi cha bilioni 270 kati ya bilioni 400 ambazozitaanzia kazi na mchakato tupo hatua ya manunuzi na mradihuu utaanza 2019/20 kwa ajili ya kufikisha umeme katikamaeneo ya Vitongoji i l i kuweza kusambaza umeme,nikushukuru sana.

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

SPIKA: Ahsante sana kwa sababu ya mudaWaheshimiwa Wabunge inabidi tuendelee, lakini mradi huowa ujazilizi ni mradi muhimu mno ili kusahihisha makosa yoteyale yaliyofanyika kule nyuma, tunasubiri sana kwa hamu hiyoDensification.

Wageni waliopo katika Jukwaa la Spika leo asubuhini viongozi wa Benki ya DCB ambao ni Mwenyekiti wa Bodiya Wakurugenzi Profesa Lucia Msambichaka, ProfesaMsambichaka, Mkurugenzi wa Benki Godfrey Ndalama,Mkurugenzi wa Biashara James Ngaluko, Mkuu wa Kitengocha Masoko Rahma Ngasa huyo hapo, Meneja wa TawiJoseph Njile na Afisa Uhusiano Nuru Ashraf, ahsante sanakaribuni sana. (Makofi)

Wageni wa Wahaeshimiwa Wabunge wageni nanewa Mheshimiwa Stella Ikupa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuuanayeshughulikia masuala ya Watu Wenye Ulemavu ambaoni viongozi wa shirikisho la Vyama vya wenye Ulemavu(SHIVYAWATA) wakiongzwa na Katibu wao ndugu RamadhanMrisho, (SHIVYAWATA) karibuni sana wale pale.

Wageni nne wa Mheshimiwa Elias Kwandikwa NaibuWaziri Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambao ni familia yakewakiongozwa na mke wake Dkt. Marcelina Mumbee, karibusana, karibuni sana.

Pia kuna wageni wengine 24 wa MheshimiwaKwandikwa ambao ni Viongozi wa CCM na Madiwani kutokaUshetu Mkoani Shinyanga wakiongozwa na Katibu Mweneziwa CCM wa Wilaya ya Kahama ndugu Joachim Simbila, walewa kutoka Kahama wale haya karibuni sana Wasukuma woteDodoma ni Jiji muwe munaangalia magari barabarani huko.(Makofi)

Wageni 29 wa Mheshimiwa Daimu Mpakate ambaoni Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi kutoka TunduruMkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Katibu wa Chama chaMsingi ndugu Ally Jafari Ally, karibuni sana wageni wetu

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

kutoka Tunduru, mmesafiri masafa marefu karibuni sanaDodoma.

Wageni tatu wa Mhehsimiwa Joseph Haule ambaoni wapiga kura wake kutoka Jimboni kwake Mikumiwakiongozwa na Ndugu Philemon Nyalusai, karibuni sanawako pale. Mgeni wa Mheshimiwa Sophia Mwakagendaambaye ni rafiki yake kutoka Jijini Dar es Salam ndugu KweziMwakapala, karibu sana Kwezi yule kule. (Makofi)

Kuna wageni kwa ajili ya mafunzo ni wanafunzi 24toka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaowamelitembelea Bunge kujifunza namna linavyofanya kazi,wageni wa kutoka (UDOM) wengi wao watakuja mchanataarifa nilizonazo, ahsante sana.

Tangazo ni moja tu kutoka kwa Idara ya Utawala naRasilimali watu hapa Bungeni wanawaomba niwatangazieniWaheshimiwa Wabunge wote kwamba zoezi la usajili wa kadiza simu kwa kutumia alama za vidole l inatarajiwakuhitimishwa leo kwa upande wa hapa Bungeni.

Hivyo Waheshimiwa Wabunge wote ambao badohamjasajili kadi zenu za simu kwa kutumia mfumo huumnakumbushwa kukamilisha usajili huo.

Aidha, Waheshimiwa Wabunge wote mnatakiwakupatiwa chanjo ya homa ya ini kwa awamu ya tatu, piamnakumbushwa kuwa zoezi hilo bado linaendelea nalinatarajiwa kuhitimishwa wiki hii.

Hivyo Waheshimiwa Wabunge wote ambao mlikuwammepata chanjo hiyo inatakiwa iendelezwe kwa maana yaAwamu ya III mnapaswa kufika pale kituo cha afya ili kuwezakupata huduma hiyo, Katibu.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

NDG. ATHUMANI HUSSEIN - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

(Majadiliano Yanaendelea)

SPIKA: Majadiliano yanaendelea, atakayetufunguliani Mheshimiwa Peter Serukamba, atafuatiwa na MheshimiwaSecil Mwambe na Mheshimiwa Andrew Chenge ajiandae,atafuatiwa na Mheshimiwa Ally Saleh. MheshimiwaSerukamba tafadhali!

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru wka kunipa nafasi niwe wa kwanza leo, nianzekwa kumpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilianona wafanyakazi wa wote wa Wizara kwa kazi nzuriwanayofanya. Naanza, nina mambo matatu kwa kweli, mojani suala la barabara ya kwangu kule Mwandiga kwendaKabunga ni barabara mpya barabara ambayo MheshimiwaRais aliahidi kwenye kampeni, ningetamani sanatutakapoenda kwenye kampeni mwaka kesho hilo lisiweswali, naomba sana waziri tujitahidi barabara hii tuwezekuimaliza na barabara hii ina faida zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, barabara hii ikiisha maana yakeGombe watu hawataenda kwa njia ya boti; barabara hiiikiisha TPA wamejenga bandari kule Kagunda ili bandari ileiwe na maana lazima barabara hii iishe TPA na halmashauriwanajenga soko Kagunga ili soko lile liwe na maana kwabiashara ya Burundi na Uvira, lazima barabara hii iishe, niombesana Wizara tujitahidi barabara hii iishe kwa kweli ni barabaraya kiuchumi ni barabara ya kiulinzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, ni suala la PPP. Nimesomakitabu hiki cha Waziri sijaona popote tunapoongeleabarabara za PPP au mradi wowote mkubwa wa PPP. (Makofi)

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Mheshimiwa Spika, hili ningeomba sana watu waSerikali watusaidie. Mimi naamini tunapoongelea barabaraTanzania, Rais Nyerere alijenga barabara, Mwinyi alijengabarabara, Mkapa alijenga barabara, Kikwete alijengabarabara, Magufuli anajenga barabara. Mimi leo natakatumtenganishe Magufuli na Marais wote waliopita kwenyebarabara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili tuweze kumtenganisha lazimatuje na mawazo mapya. Umefika wakati barabara za nchihii tuanzishe super high way ambazo hatutumii fedha zetu.Tutajenga barabara ambazo tutalipa kwa road toll. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wako watu fulani Serikaliniwanasema kwa kujenga standard gauge barabara hainamaana, siyo kweli.

MBUNGE FULANI: Siyo kweli.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika,Dodoma Jiji, ili Dodoma iwe accessible lazima tujenge superhigh way from Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.Maana yake ni nini? Kama kuja Dodoma ni saa nane, maanayake Dodoma haiwezi kukua kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nasema reli hata ikiisha kaziyake ni mizigo. Kama mnadhani tunajenga reli kwa ajili yakusafirisha watu nadhani siyo sahihi. Kwa hiyo, tunasematujenge barabara na hizi barabra duniani kote wanatumiahela za PPP, Malaysia, Marekani na China wanatumia PPP,tatizo letu ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi na wewe tulikwenda kwenyemkutano wa IPU, Urusi. International Airport ya Urusi (Moscow)ni ya mtu amejenga, siyo Serikali lakini service zinapatikana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, najua sana mambo ya barabarakwa sababu na mimi nimekulia humo ndani, naombenitumfanye Magufuli awe tofauti na wenzake. Namna bora

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

ya kuwa tofauti ni moja tu: Amekuwa tofauti kwenye reli, wotehawakujenga reli yeye anajenga reli; amekuwa tofautikwenye umeme wa Stiegler’s wote hawakufanya yeyeanafanya, naombeni tumpe na utofauti wa barabara,tujenge super high way nchi nzima ambazo watu watakujakwa kulipa. Chalinze high way tumeiondoa, why? Ukiwaulizawatu wa Serikali wanasema Chalinze high way tumeiondoakwa sababu kuna standard gauge, hapana, havinamahusiano hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siyo lazima watu wote watapandareli. Haiwezekani kilometa 100 tunakwenda saa tatu, kiuchumisiyo sawa. Kwa sababu infrastructure ndiyo inayoleta uchumi,ndiyo enabler wa economy. Sasa kama infrastructure ndiyoenabler wa economy lazima tufanye vitu ambavyovitasababisha goods zifike mapema, tuweze kwenda kwenyemaeneo yetu mapema, twende kwenye biashara tuwahikurudi. Sielewi kwa nini Serikali haitaki miradi ya PPP. Naaminikama tunataka twende haraka lazima twende kwenye PPP.Wenzetu wote wanatumia fedha za watu, hii kwamba lazimatufanye wenyewe siyo sawa.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya kufanya wenyewe nihaya yafuatayo. Barabara ya kutoka Nyakanazi kwendaKabingo Kilometa 50 tunajenga huu mwaka wa 10. Barabaraya kutoka pale Kidahwe - Kasulu huu mwaka wa 10. Maanayake ni nini? Tuna shida nyingi sana tunataka kufanya yote.Namna bora ili tuweze kwenda kwa kasi, maeneo menginetuwaachie wengine wafanye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naamini Watanzania hawawezikushindwa kulipa road toll, hawawezi. Kama natoka na basiKigoma saa 12.00 asubuhi, nina uhakika nitakuwa Dar esSalaam saa 10.00 kuna shida gani ya kuweka toll? Naniatakataa kulipa toll? Sielewi kuna nini Serikalini. Sielewi whySerikali hawataki miradi ya PPP, sielewi.

Mheshimiwa Spika, napenda Waziri atakapokujaatuambie hivi sisi ni tofauti na watu wengine? (Makofi)

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Mheshimiwa Spika, leo ukienda Marekani hata uki-google, mtu pekee anayekumbukwa kwenye barabaraMarekani ni Rais Franklin Roosevelt? Kwa sababu gani? Baadaya vita kuu ya pili ya Dunia aliamua kuunganisha states zote50 kwa super high way na watu wanalipa kwenye toll. Kwanini hatutaki kufanya hivyo? Kwa hiyo, mimi ningeomba sanaSerikali, najua jambo hili linawawia ugumu lakini sioni ugumuwake ni nini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni viwanja vya ndege.Mimi hili naleta ushauri Serikali mlitafakari upya, nadhaniumefika wakati viwanja vya ndege viachiwe kazi ya kujengana kuendesha. Habari ya kuchukua viwanja vya ndegeunapeleka TANROADS, inawezekana ni nia ya kudhibiti lakinikuna ucheleweshaji. TANROADS wana kazi kubwa, wanamadaraja, barabara na kila kitu. Ningeomba suala la viwanjavya ndege tuvirudishe. Pale tumepeleka CEO mzuri sana,Engineer Ndyamkama is one of the best, tumpe kazi hiiataifanya na kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia tuweke taa kwenyeviwanja vyetu. Tumenunua ndege lakini ili ziweze kufanya kazimara nyingi tunahitaji taa. Hii kusubiri jua tu maana yakendege zetu hazifanyi kazi at its capacity. Kwa hiyo, naombasana hili nalo liangaliwe.

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la bandari.Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza sana viongozi wabandari kwa kazi kubwa wanayofanya. Hata hivyo, kazikubwa inayofanyika bandarini naomba tuwasaidie tuondoevizingiti barabarani.

Mheshimiwa Spika, kwenye transit trade, biashara hiitupo na wenzetu sasa kama kila baada ya dakika tano kunaPolisi, tunaifanya bandari yetu isiwe attractive. Kwa sababugani? Bandari itafanya kazi vizuri, inatoa mizigo kwa wakatilakini lori likishaingia mpaka kufika Tunduma ni shughuli yasiku nne au tano. Wafanyabiashara wanataka waendeharaka warudi, hii ndiyo maana ya biashara. (Makofi)

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Mheshimiwa Spika, hapa kwetu kuna point nyingi zakukaguliwa unapotoka Dar es Salaam mpaka Kigoma naunapokwenda kwenye mipaka yetu nawahurumia walewanaoendesha haya malori kwa sababu wanasimamishwakila baada ya kilometa 3 au 4, trafiki wapo. Rais amesemajamani eeh, Polisi haiwezekani mkasema kutoka Dar esSalaam mpaka Morogoro kuna point mbili za kukagua, hukukwingine kote wanasimamishwa, biashara haiwezi kutusubiri.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana sasa bandari yetuinapambana na ushindani wa Mombasa na Beira kwasababu bandari ina-perform lakini kama wale wenginehatuisaidii itaonekana imeelemewa. Kwa hiyo, naomba sanawatu wa Serikali tuwasaidie sana watu wa bandari kwamaana ya ku-enable ili kazi yao iweze kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho ni suala la fedha zabarabara hasa za GOT. Naomba sana Serikali, ukiangaliatrend yetu, barabara ambazo zinajengwa na GOT zinatumiamuda mrefu sana. Maana yake ni nini? Zikitumia muda mrefu,interest rate, idle time, kwa barabara ambayo ungeijengakwa shilingi bilioni 50 unaijenga kwa shilingi bilioni 100, siyosawa. Atakuja mtu siku moja tutapata shida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombana mimi niunge mkono hoja, nakushukuru sana.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Peter Serukamba.Nilikuwa nimeshakutaja Mheshimiwa Cecil Mwambe naMheshimiwa Andrew Chenge ajiandae.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangia kwenye Wizarahii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, kimsingi, nataka tu niongeemambo matatu, kwanza, ni suala linalohusiana na Reli yaKusini kwa maana ya Mtwara-Mbambabay. Pili, ni sualalinalohusiana na masuala ya barabara ya uchumi ya Mtwara

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

– Newala – Masasi - Nachingwea lakini tunaombaikiwezekana iongezwe Liwale -Morogoro kwa sababutunafahamu sasa hivi Makao Makuu ya nchi yetuyamehamishiwa Dodoma. Sisi wakazi wa Mtwaratunakwenda Dar es Salaam kufauata huduma na siyo lazimatufike pale, tungeweza moja kwa moja kutokea hukotunakokutaja tukaja hapa Dodoma straight. Kwa hiyo,tunataka na hii Serikali nayo tuishauri.

Mheshimiwa Spika, suala la mwisho kabisa, nitapendapia niihoji Serikali kwa sababu mpaka sasa kwenye Wizara hiina idara zake mbalimbali wameshatengewa na pesazimeshatumika almost trilioni 18 lakini hatujaona kimsingi athariyake kiuchumi ndani ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze na suala la barabara hiiniliyoitaja ya Mtwara – Mnivata -Newala – Masasi. Ukisomakwenye hotuba ya Waziri, ukurasa wa 278, kipengele chatano, wanasema: “Ujenzi wa barabaraya Mtwara –Newala -Masasi”.

Mheshimiwa Spika, barabara hii ina jumla ya kilometa221. Kama ambavyo Mheshimiwa Serukamba pale amesematuangalie value for money. Barabara yenye urefu wa kilometa221 imetengewa shilingi bilioni 3.4 tu. Kwa wastani wa sasawa kilometa 1 ya barabara kutengenezwa kwa shilingi bilioni1, wanatuambia kwamba katika mwaka huu wa fedhawatakwenda kujenga barabara hii kwa kilometa 3 tu. Sasatunampa mkandarasi barabara ya kilometa 221.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ameikaguabarabara hii akasema tunaomba hii barabara ijengwe kwaharaka sana kwa sababu ni barabara ya uchumi lakini katikahali ya kushangaza Wizara wanatenga shilingi bilioni 3.4 pekeyake, wanamkwamisha sana Mheshimiwa Rais. Hawawasaidizi wake wakati fulani wanashindwa labda kumpaushauri unaotakiwa.

Mheshimiwa Spika, kimsingi barabara hii ni ya uchumina ni ndefu, hauwezi kutenga shilingi bilioni 3.4 pekee kwenye

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

barabara yenye urefu wa kilometa 221. Kwa hiyo, tuiombeWizara ikiwezekana warekebishe fungu hili au waone namnaya kufanya ili kuweza kutekeleza ile ahadi ya Rais.

Mheshimiwa Spika, Rais alipokuja alisema barabarahii atahakikisha wanawekwa wakandarasi watatu mpakawanne kwa urefu wa kilometa hamsini hamsini kila mmoja.Mpaka sasa barabara inayojengwa ni Mtwara -Mnivata lakinini asilimia 36 tu ambazo zimeshatekelezwa na sasa ni mwakawa tatu. Kwa hiyo, tunaiomba Wizara itusaidie, kero yabarabara hii ni kubwa sana na nia yetu sisi ni kusafirisha watu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine hapa,suala la Reli ya Kusini. Kwa muda mrefu sana tumeongea namaeneo mengi watu wanadai fidia ikiwemo maeneo yaMtama, Ndanda, Masasi na sehemu kubwa sana ya Jimbola Mtwara Vij i j ini kwa maana ya kule anapotokeaMheshimiwa Mama Hawa Ghasia.

Mheshimiwa Spika, tatizo lililopo kwenye mradi huu,mpaka sasa haueleweki kwamba ni lini utaanza au Serikalinao wameamua kujiondoa kwenye huu mradi kamawalivyofanya miradi ya barabara ya kutoka Dar es Salaamhigh way mpaka kufikia Chalinze. Kama ni hivyo basi wasemewazi ili wale wananchi waendelee kufanya shughuli zao zakiuchumi kwenye maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika miradi mikubwa ambayoSerikali ilikuwa inaipangilia ni pamoja na mradi wa Ligangana Mchuchuma. Hakuna mwekezaji yeyote atakayekujahapa kama hatujaboresha hii miuondombinu.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani chuma kisafirishwekutoka Liganga kuletwa Bandari ya Mtwara kwa kutumiabarabara, siyo reliable na hasara ni kubwa na hii mizigo nimizito. Barabara hizi tuache watumie watu kama ambavyowengine wamesema lakini hii miradi mikubwa ya kipaumbeleitekelezwe tuweze kuona sasa manufaa ya chumatulichonacho sisi. (Makofi)

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Mheshimiwa Spika, sisi tuliishauri Serikali hata kwenyeKamati yetu ya Viwanda Biashara, kwa nini wasifanyeuwekezaji mkubwa pale ili kuokoa forex? Pesa ambayoingepatikana Mchuchuma ingekwenda kujenga hiyo Reli yaKati ya Standard Gauge. Chuma ambacho kingepatikanaMchuchuma kingekwenda kusaidia kujenga kwenye reli hiyopia lakini matokeo yake tunaagiza chuma, tuna viwandavyetu hapa vya nondo vinaweza kutengeneza lakini bidhaakaribia asilimia 90 zinazotumika kwenye standard gauge niimported. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huko ndiko tunakomalizia pesazetu za kigeni na tunashindwa kufanya miradi midogo midogohii ya kuwasaidia wananchi. Tunaona Wizara ya Majiwanalalamika lakini mpaka sasa hivi nguvu kubwa sanainapelekwa kwenye hii miradi mikubwa ambayo utekelezajiwake nao ni wenye kutia shaka kwa sababu hakujafanyikadue diligence wala kuonyesha impact assessment kwenyehii miradi mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli hii ni muhimu sana kwawatu wa Kusini kama ilivyo kwa watu wa upande waMagharibi na kwingine kwenye reli hii ya standard gauge.Sasa Serikali ituambie hapa wazi, wana mpango wowote wakufanya kazi hapa kwa sababu kwenye hivi vitabuhawaonyeshi waziwazi wanataka kwenda kufanya nini. Kwahiyo, waje watueleze kama kuna mpango huo na kamahaupo basi tuwaeleze wananchi wetu waweze kufanyashughuli zao za kiuchumi kwenye maeneo haya. Hii itakuwani failure kubwa sana kwa sababu hakuna mwekezajiatakayekuja kufanya kazi Liganga kama miundombinu hiiwezeshi hatujaitekeleza na tunajinasibu kwamba sisi ni nchiya viwanda na mambo mengine. Kwa hiyo, tuanze kwanzana msingi wa usafirishaji kutoka kule Liganga kuja kuletaBandarini Mtwara ambayo ni Reli ya Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Reli ya Kusini ilijengwa mwaka1949, mwaka 1963/1964 ilindolewa, kwa vyovyote vileinatakiwa pale kufanyike uwekezaji mkubwa. Ni jambo jemakujenga hii standar gauge railway lakini malengo ya Reli ya

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

Kusini iwe ndiyo ya kipaumbele na malengo yake ni makubwakwa sababu ni sehemu ambako tutakwenda kuongezauchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mweyekiti, nigusie kidogo suala labarabara, tukitaja barabara inayoishia Masasi. Ukisoma piakwenye hiki kitabu, barabara inayotokea Masasi kuelekeaNachingwea na yenyewe ina kilometa 45 wametenga shilingibilioni 1.3 tu. Tuiombe Wizara itueleze, tunapotenga shilingibilioni 1.3 kwenye barabara yenye urefu wa kilometa 45tunakwenda kufanya kazi gani na pesa hizi? Pale Masasi sasahivi kuna ajali nyingi sana kwa sababu kuna round aboutkubwa, barabara inayounganisha kwenda Songea, Newala,Nachingwea na kurudi Mtwara Mjini, tunaomba pale katikatiikiwezekana ziwekwe taa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili jambo sisi tumelijadili hatakwenye vikao vyetu ya RCC na Road Board kwambatunahitaji pale kupata taa kwa sabbau ni junction kubwa nawatu wengi sana wamekufa akiwemo Afisa Mkuu wa Majiwa Wilaya yetu sisi ya Msasi, alifia pale na ajali nyingizinatokea, tunaziona. Kwa hiyo, tunaomba pale ziwekwe taa.

Mheshimiwa Spika, hii barabara tunayoitajainayokwenda Nachingwea pamoja na pesa ndogomlizozitenga tuishauri sasa Serikali, tunaomba Mkoa waMtwara kupitia Wilaya ya Masasi ifunguliwe sasa isiishieNachingwea peke yake iende mpaka Liwale, ikitoka Liwaleiende mpaka upande wa Morogoro, Malinyi. Safari hii ni fupisana kutoka Masasi mpaka kufika Morogoro, Malinyi siyo zaidiya kilometa 300 lakini tunalazimika kutembea kilometa 600kwanza kufika Dar es Salaam ili tuweze kuondoka Dar esSalaam tuje Makao Makuu ya nchi na wakati mwingineunalazimika kusafiri siku mbili mfululizo. Kwa hiyo, niombeWizara hii wakafanye kazi kwenye barabara hii waone namnaya kuunganisha Wilaya hizi mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine niligusia kidogokuhusiana na uwekezaji mkubwa uliofanyika kwenye Wizarahii. Mpaka sasa hivi Wizara hii na Idara zake wametumia

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

almost 18 trillion kwa maana ya kununua ndege, kutengenezahivyo viwanja vya ndege na kufanya shughuli mbalimbalizinazohusiana na miundombinu ya hivyo vitu ninavyovisema.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana sisi tulikuja hapatukasema tunataka tuone manufaa ya moja kwa mojayanayopatikana kwa wananchi kutokana na miradi hiimikubwa inayofanywa na Wizara hii. Sasa utakapokujaMheshimiwa Waziri tueleze ni namna gani uwekezaji huumkubwa mlioufanya umenufaisha wakulima wa maeneo yetuwakiwemo wakulima wa korosho na wengine? Ni namna ganiuwekezaji huu mkubwa uliofanywa kwenye Wizara hiyoumenufaisha uwekezaji nchini kwetu? Ni namna ganitumewavutia wawekezaji kwa kununua ndege na ni namnagani tumewavutia wawekezaji kwa kufanya huo uwekezajimkubwa tunaoutaja hapa, Mheshimiwa Waziri uje hapautueleze. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mtueleze ni namna ganisekta ya kilimo imenufaika na uwekezaji huu mkubwaunaofanywa. Otherwise na yenyewe tutakuwa tunasemabad timing, hatuna proper value for money. Tuiombe Serikalimwisho kabisa ikubali kufanya utafiti wa kina (impactassessment) i l i kuweza kujua uwekezaji huu mkubwauliofanyika pale umenufaisha wananchi kiasi gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa tumewekeza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

Waheshimiwa Wabunge, kwa idadi ya Wabungenilionao na hasa upande wa Chama Tawala hatuwezi kupata

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

dakika 10, baadhi itakuwa dakika tano watakaopata nyingini dakika saba kwa sababu nina wachangiaji wengi na kwakweli haiwezekani. Kwa hiyo, ukipata nafasi yaani nendamoja kwa moja unachotakiwa useme.

Sasa tunaendelea na Mheshimiwa Chenge dakikasaba atafuatiwa na Mheshimiwa Ally Saleh dakika saba.

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Spika,nikishukuru sana kwa kunipatia nafasi hii ili nami nichangiekwa ufupi tu.

Mheshimiwa Spika nipongeze kazi nzuri inayofanywana Wizara hii kwenye maeneo muhimu ya ujenzi wa barabara,mawasiliano na uchukuzi. Hongereni sana, naelewa rasilimalifedha ndiyo zinatusumbua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jana nimetoka Bariadi kujaDodoma nimeona kazi nzuri inayofanywa kati ya Bariadi naMaswa, mkandarasi anaendelea na pesa imetengwa tena.Tungependa tukamilishe barabara hii ikiwezekana mapemamwaka huu au mwaka kesho tuweze kutoka moja kwa mojaDar es Salaam – Dodoma – Shinyanga – Mwigumbi –Bariadi –Lamadi – Musoma – Sirari - Nairobi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Bariadi imekaa katikati kwaukanda wa Kaskazini Mashariki mwa Tanzania na ndiyomaana tunasema sana barabara, tulitegemea katika Mwakahuu ujao wa fedha angalau kipande cha Bariadi kujaMoboko-Mwanuzi mpaka Sibiti kingeliweza kufanyiwafeasibility study yaani upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.Lakini naona siioni kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri hatakwenye majedwali yale ya kipande hiki hakipo, tunaendeleakuiomba Serikali kwamba tuunganishwe na mikoa jirani yaSingida na Arusha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine mkisoma hotuba za Wizarahii kwa miaka mitatu iliyopita barabara ya Kolandoto, Munze,Lalago mpaka Thibiti ilikuwa inaenda mpaka Matala -Mang’ola na Odiang Junction. Sasa hivi tunaongelea

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

kasehemu kadogo tu, tumeanzisha mradi mzuri tu huu wakutoka Karatu, Mbulu, Haydom, Sibiti, Lalago Maswa.Ningependa Serikali ituambie kwa kazi iliyofanyika kwakipande cha kutoka Sibiti, Matala, Mang’ola na OdiangJunction ile sehemu tunaiacha au tunaendelea nayo?Ningependa nipewe majibu na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nije kwenye upande wa barabara,mimi kuna barabara nasema kwa sababu tunajua hali yaTanzania iliyvyo kuna maeneo mengine ni ukame, mengineyana hali nzuri ya barabara, naendelea nashukuru Serikalinimeona upande wa barabara ya Kidatu – Ifakara - Tupilokuelekea Malinyi - Londo mpaka Lumecha Songea nashukurusana kwa sababu tukiweza kukamilisha barabara hiitunafungua njia ambayo eneo lenye utajiri mkubwa sana wachakula na hali nzuri ya hewa. Lakini ningependa tuangaliepia uwezekano wa kutoka Ifakara twende Kihansi, twendeMlimba, twende Taweta, twende mpaka Madeke, twendempaka Lupembe maana tukiyabeba haya yote unaifunguasehemu hiyo yenye utajiri na kuweza kupeleka chakula kwaharaka katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho naomba tunafanya kazinzuri katika kupanua Bandari ya Dar es Salaam, napongezaSerikali lakini nasema mwaka jana nilishauri reli yetu ya katihii tunayoijenga sasa hivi ni afadhali tukachukua mkopo wamuda mrefu kuliko hii ya mikopo ya masharti ya muda mfupiambayo yatakuja kutuumiza, maana hata kabla hatujaanzakuitumia reli hii tutaanza kulipa madeni haya. Lakinitukichukua madeni ya muda mrefu na kwa masharti nafuutunajenga reli hii tukamilisha yote kwa wakati mmoja ili tuwezekupata faida ya uamuzi mzuri huu unaofanywa na Serikali.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa bandari ya Dar esSalaam itatusaidia kwa muda mfupi tu. Duban na Bellair nasasa Nakala lakini upande wa Lam na Mombasa wenzetuhawa wanaangalia mbali sana, tungependa na sisi Bandarihizi Mungu ametupa nafasi nzuri sana, Bandari ya Mtwara,Bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Bagamoyo Mbegani

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

narudia kuishauri Serikali na Mwambani hizi kwa upande wetuwa Tanzania zikiweza hizi zikajengwa, hii ndio future yaTanzania kuunganisha na nchi za Maziwa Makuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ningependa sana Bunge lakotuendelee kuishauri Serikali waone faida ya haya. Najuamuda wangu ndio huo lakini nikushukuru sana kwa nafasiuliyonipa, naishukuru Serikali kwa haya wanayoyafanya,niungane na Mheshimiwa Serukamba kwamba tuangaliekwa haraka na sio kupoteza muda, sekta binafsi ishirikianena sekta ya Umma kwa PPP katika kuyafanya mengi hayana tusiogope. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Chenge huo ndiouchangiaji wa masenetor sio unachangia Jimboni kwako tuohoo kataja Bariadi, kataja Malinyi huko, Ifakara, Bandarinakadhalika tunachangia kama nchi inakuwa inasaidia zaidikuisaidia Wizara kuwa na uono wa mbali na kapigia mstaribandari ya Bagamoyo, kwa kweli Bandari ya Bagamoyo niukombozi mkubwa sana tungeipata ile ingefungua nchi yetu.Mheshimiwa Ally Saleh dakika saba anafuata na MheshimiwaLolesia Bukwimba dakika saba. (Makofi)

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kweli sehemu yangu kubwa ya mchango wanguutakuwa ni kuhusu bandari ya Bagamoyo ambayo umeitajahapo. Lakini kwanza nitapitia in passing tu. Kuhusiana na ATCLnakubaliana 100 kwa 100 na mchango wa MheshimiwaKapteni Abbas Mwinyi wa wiki iliyopita ametusemea wengina amesema mengi na amesisitiza yale ambayo oppositiontumekuwa tukisema lakini Serikali ilikuwa haitusikilizi naaminikwa kuwa yametoka kwao sasa labda pengine utasikiliza.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pil i ni kuhusiana na relinakubaliana na wengi ambao wanaosema kwamba reli nimuhimu lakini haiondoshi kuwepo na taratibu nyingine zausafiri. Marekani mizigo mingi inasafirishwa kwa magari

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

makubwa hata kuliko reli, reli ni ya pili, pia kutegemea relikwa abiria ni makosa makubwa sana, reli ni mizigo, yupo mtualisema hapa kuna haja ya kuwa na drive ports kila baadaya eneo ili kurahisisha mizigo kuwa collected ili kwendasehemu nyingine ya nchi au nchi jirani. Kwa mfano kuwa nadrive port Dodoma au kuwa na drive port Morogoro ili mizigoinatuliwa pale kisha reli inabeba. India mizigo ni 80 percentya reli inatia faida kwa 80 percent. Abiria ni less labda 15percent, mizigo mingine midogo ndio percent iliyobakia, kwahiyo tusijidanganye reli ni mizigo bila mizigo hakuna reliitakuwa hasara tupu.

Mheshimiwa Spika, la tatu nataka kuzungumzia juuya suala la mabaharia, nchi yetu mwaka jana tuliridhiamikataba miwili Maritime Law Conventional na Seafarers ID.Lakini hatukwenda mbali zaidi kuleta sheria kuibaidilisha ilesheria ya meli ili iweze kufaidika. Kwa hivyo kwa maananyingine tumeridhia conventional lakini hali ya mabahariawetu 5,276, iko mbovu vilevile bila kitambulisho, bila sheriaya kupitishwa hapa haiwezekani mabaharia wetu wakafaidimalipo mazuri ambayo wanaweza kulipwa na wanaendeleakupunjwa kwa sababu tu kwamba sheria haikufuatiliwadomestication I mean mkataba wa Kimataifa hawakufuatiliadomestication ya sheria ili mabaharia wetu wawe na hadhikamili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo nakwendakwenye Special economic zone ya Bagamoyo, na naanzakwa kusema kwamba tunafanya makosa kama Bunge nakama nchi kuachia miradi mikubwa kama hii ikafutwa bilakuwepo na public discussion. Vilevile nataka nikushawishihata wewe kwa nafasi yako unaweza kuunda vyombo aukuunda namna ambayo ya kuweza kuchunguza kwa ninikama nchi tunaacha mradi huu ambao tutauelezea leohapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mradi huu kwanza tunaondokanena dhana kwamba ni bandari, ni zaidi ya bandari ni mji, niajira ni kufunguka kwa uchumi wa Tanzania. Kutakuwa aukungekuwa na viwanda 800 ambavyo tayari viko pale pale

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

katika eneo kwa hivyo mzigo unachukuliwa unatiwa katikameli unapelekwa nje au mwingine unatoka pale unakwendaSilama unaunganishwa na reli hii mpya ya SGR inakwendakwingine inakwenda kuuzwa. Pia utajenga Mji wa KisasaBagamoyo kwa maana mbili, kwa maana ya kupata watukuishi lakini pia Dar es Salaam itapumua, Dar es Salaamikipumua watu wanakwenda kule kuishi Bagamoyo kwa hivyonchi inatononoka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu kutakuwa na logistic la tantrade ambayo itafanyika itakuwa kubwa sana bandari yaBagamoyo kama ingejengwa au kama itajengwa itawezakuchukua makontena milioni 420 kwa mwaka. Sasa hivibandari kubwa duniani Rotterdam inachukua milioni 11.87,kwa maana nyingine bandari ya Bagamoyo ingebakia kuwakubwa pengine kwa miaka 100 ijayo kwa Dunia nzima.Rotterdam wanaingiza meli 3,613,315 kwa mwaka kwamaana ya meli 110, hapa ndipo unaweza kuona suala lalocally country linaweza kuwa pana. Imagine meli 100zinakuja kwa siku wanataka maji, wanataka matunda,wanataka toilet paper, sijui wanataka kitu gani imagine faidaambayo ingepatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia Bandari hii au eneo hililingeweza kuzalisha ajira zaidi ya 120,000. Eneo la Dar esSalaam kusema una forfeit kule ambako mkopo unatokaChina na Oman marafiki zetu wakubwa tuseme pia suala lademokrasia katika hili wanatuunga mkono katika mambomengi lakini unasema na kuna Dar es Salaam, tayari kunaBanana unatka uje na fourth generation meli ambazo nikubwa zinashusha zinapakia wenyewe haziwezi tena kuingiaDar es Salaam, pengine kina cha bandari cha Dar es Salaamkitagoma kupokea meli hizo za fourth generation natukaenda itakuja fifth na sixth generation. Meli moja ya sasainaweza kuwa na tani milioni 100 inaleta mzigo wa tanipengine milioni mbili, pengine Dar es Salaam isiweze kubebatena. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa pale Dar es Salaampameshajaa...

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh bahati mbaya dakikasaba zimeisha, lakini kwa hatua hii kwa alichokuwaanakichangia Mheshimiwa Ally Saleh, niongeze sentensi mbilikwa dakika moja tu. Sielewi binafsi sielewi nini kimekwamishamradi huu wa Bagamoyo labda Mheshimiwa Waziri kamaatapata muda anaweza akatufafanulia vizuri yeye yukokwenye nafasi nzuri zaidi ya kuelezea jambo hili. (Makofi)

Lakini niliwahi kwenda China mwaka juzi kwa jambojingine kabisa katika Jiji la Shenzhen, nikiwa na baadhi yaujumbe wa baadhi ya Wabunge humu ndani na kumbebahati nzuri Makao Makuu ya wale China Merchants ambaowalikuwa wajenge bandari ya Bagamoyo yako Shenzhenpale. Kwa hiyo, baada ya ziara yangu kuisha MheshimiwaBalozi wetu akasema ni vizuri tukawapitia hawa jamaatukasikia kidogo wanachokisema, wakatufanyia presentationkubwa nzuri sana, ndio maana nasema sijui upande waSerikali kuna nini. Lakini ukisikiliza ile presentation huwezikuacha kuunga mkono ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.(Makofi)

Ni mradi mkubwa mno na wale jirani zetuwanatukaba pale juu sitaki kuwataja majina mnawaelewatutakuwa tumewabana vizuri, kwa kifupi Wachina walisematunawashangaeni sana Watanzania nyinyi rafiki zetu nduguzetu sijui kwa nini inapofika mambo mazuri makubwa kamahaya mnavuta miguu, hamuamui na wakasema kwenyekampuni yao ile bodi wameshabadilika sana ile turnover yaoni kubwa, hasa waliobakia ambao ni watu wazima na wana-soft touch na Tanzania katika ile bodi yao walikuwa ni wawilitu na wenyewe walikuwa kama wana miaka miwili naowataondoka, kinakuja kizazi ambacho hakijui hii maneno.Wakati nasema msipo- take advantage ya sisi tunaoondokasasa hivi mkafanya maamuzi shauri yenu. (Makofi)

Lakini mwisho akasema nimwambie MheshimiwaWaziri, tunakushangaeni eti mjenga reli ya kisasa SGR, kwamaoni yao wao ni marafiki zetu wanasema kama rafiki overlounge wanasema ni kama kugeuza mkokoteni si kunang’ombe na lile nani… wanasema mnachofanya mnaweka

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

ule mkokoteni mbela halafu ehee! Wanasema kwa sababuunaanza kujenga bandari ndio unajenga reli, nyinyi mnaanzareli kabla ya bandari wanasema kwa hiyo, tunakuangalienimarafiki zetu, kwa kweli sijui kinachokwamisha labda kunavitu viwili lakini si mradi wa kuacha jamani chonde chondena hawa wafanya maamuzi wakae waamue yaani is grandproject bandari kubwa ya kisasa hakuna Afrika Masharikihapa mpaka Msumbiji hakuna, viwanda kama alivyosemayule bwana vingi ni Mji wa viwanda yaani ni halafu karibuhela zote wanatoa wao.(Makofi)

Kwa hiyo narudia tena sijui kulichoko serikaliniinawezekana kuna mambo ya msingi sana wa kuyatazamalakini ni kitu ambacho ni vizuri tukakipa macho mawilitukaacha mambo mengine yote mradi kama huu ni uchumimkubwa tukafungua uchumi mkubwa sana tukambana jiraniyetu yule anatukaba kila wakti yule jiarni yule. MheshimiwaLolesia nilishakutaja dakika saba. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, hongera sanakwa kuchangia.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Wizarahii muhimu kabisa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Manaibu Waziripamoja na watumishi wote wa Wizara kwa kazi nzuriwanayoifanya tunashuhudia jinsi ambavyo kazi kubwainafanyika katika Taifa hili, barabara zinajengwa, flyoverzinajengwa lakini barabara mbalimbali za mikoa zinajengwa.Nichukue nafasi hii kipekee kupongeza kwa kazi nzuriinayofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze na barabara muhimukabisa katika Mkoa wetu wa Geita barabara ya kutokaKahama kwenda Bukoli mpaka Geita, ni barabara muhimusana kiuchumi, kumbuka katika Mkoa wa Geita na Mkoa waShinyanga ni mikoa ambayo imebobea katika masualamazima ya madini, na kwa sababu hiyo tunahitaji barabarahii iwe ya lami ili iwezeshe shughuli za uchiumbaji wa madini

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

ziende vizuri zaidi usafirishaji wa mizigo mbalimbali. Kwa hiyoniseme tu kwamba barabara hii ni muhimu sana na kila bajetibarabara hii huwa inakuwepo kwenye bajeti lakini kwenyeutekelezaji sijawahi kuiona. Kwa hiyo nitumie fursa hii kuiombaSerikali iwekeze fedha sasa nimeona kwenye bajeti imewekafedha kiasi fulani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ninaomba barabara hiiianze kujengwa sasa kwa kiwango cha lami, barabara hii nibarabara ya kiuchumi, barabara hii imekuwepo kwenyebajeti kuanzia wakati wa Awamu ya Nne ya Mheshimiwa RaisKikwete katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi barabara hiiimekuwepo kila Ilani inakuwepo barabara hii kuwekewakiwango cha lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sasa Serikali awamu hiibarabara hii ianze kujengwa kwa kiwango cha lami kwakuanzia Geita kwenda Bukoli mpaka Kahama. Kwa kuwatunafahamu kuna mradi mkubwa mgodi mkubwa wa Geitalakini pia kuna mradi mkubwa mgodi wa Bulyang’huru,ambao wote hawa wanafanya shughuli za uchumbaji wamadini katika mikoa yetu, kwa hiyo, tukiimarisha barabarahizi nina uhakika shughuli hizi za uchimbaji zitaweza kunufaishaTaifa letu kwa kiwango kikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna barabara muhimukabisa ya kutokea Katoro - Bukombe ambapo barabara hiipia ni muhimu sana kiuchumi katika Mkoa wetu wa Geitaniombe Serikali pia iangalie uwezekano wa kuiwekeabarabara hii lami ili kuwezesha uchumi ndani ya Mkoa kuwamchumi mzuri. Ninafahamu sera yetu ya Taifa inasemakwamba mikoa yote itaunganishwa kwa kiwango cha lami,jambo ambalo ni la msingi sana na ndio maana ninatoleamsisitizo kwamba tuunganishe Mkoa wa Geita na Mkoa waShinyanga ili hatimaye uchumi wetu uweze kwenda vizurizaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile katika upande wabarabara ziko barabara ambazo zimekuwa ni muhimu sanakuchumi kwa mfano, kuna barabara ya kutokea Katoro

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

kwenda Nyang’wale kupitia Kamena - Nyalwanzaja-Busanda ni barabara ambayo kwa muda mrefu tumeiombaiwe barabara ya mkoa imekuwa ni barabara ya halmashaurilakini sasa hivi naiombea iwe barabara ya mkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kwa bahati nzuri mwaka janakuna watu walitoka Wizara ya Ujenzi walikuja kuikaguabarabara hii lakini kwenye bajeti si jaweza kuionahaijapandishwa hadhi mpaka sasa. Niombe barabara hii piakwa umuhimu wake niombe ipandishwe hadhi iwe barabaraya Mkoa ili hatimaye iweze kuwahudumia wananchiwaliowengi kwa sababu tunatambua kabisa vijijini wananchitunahitaji barabara nzuri ambazo ziwezeshe katika kuimarishauchumi wa wananchi katika maeneo yote kwa ajili yausafirishaji wa mizigo mbalimbali, mazao, kupeleka katikaviwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba sana Serikaliiangalie barabara hii ni muhimu kuweza kuipandisha kutokahalmashauri kwenda kwenye kuwa barabara ya Mkoa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna barabara zingineambazo tunaishukuru Serikali kwamba imeweza kupandishahadhi barabara ya kutokea Mbogwe kupitia Bukoli kwendampaka Bujula kuwa barabara ya Mkoa ninaishukuru sanaSerikali na naipongeza kwa hatua hiyo niombe sasa mwakahuu barabara hii ianze kutengenezwa vizuri ili wananchiwaweze kunufaika zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni kuhusiana na sualala mawasiliano. Mawasiliano ni jambo la msingi na ni sualamuhimu sana kwa ajili ya wananchi hasa waishio vijijini.Nitumie fursa hii kuiomba Wizara iangalie sana maeneo yavijijini. Natambua kwamba Mheshimiwa Waziri alituambiatupeleke majina ya kata zote ambazo hazina mawasilianoya simu. Na mimi nilipeleka majina ya kata mbalimbaliikiwemo Kata ya Nyamalimbe, ikiwemo Kata ya Bujuraambazo zina matatizo makubwa sana ya mawasiliano.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nitumie fursa hii kuiombaSerikali iangalie maeneo haya. Najua kibiashara penginehayalipi sana, lakini kwa kuwa kuna Mfuko ule wa UCAFnaiomba Serikali iwekeze zaidi vijijini kupeleka mawasiliano ilihatimaye kuimarisha zaidi wananchi waweze kufanya kazizao kwa mawasiliano. Tunatambua mawasiliano ni kitumuhimu. Kupitia mawasiliano tunarahisisha biasharambalimbali na zinaweza kufanyika bila shida yoyote. Kwahiyo, naiomba Serikali iangalie sana katika suala hili lamawasiliano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ziko kata mbalimbali ambazozinahitaji mawasiliano kama ambavyo nimezitaja kwenyeJimbo la Busanda, lakini pia na maeneo mengine ya vijijini,kwani maeneo ya vijijini mengi yanahitaji mawasiliano ya simuili kuweza kuimarisha na kuwezesha kustawisha zaidi hali yauchumi katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, natumia fursa hiikuiomba Serikali iwekeze zaidi katika Mfuko wa UCSAF ilihatimaye kuweza kuyafikia maeneo mengi ya vijijini ambayoyamekuwa na changamoto kubwa sana ya mawasiliano.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile katika upande huo wamwasiliano napenda kuomba Serikali iangalie minara. Minaramingi ambayo imesimikwa katika maeneo mengi wanakuwahawalipi kwenye vijiji wanapochukua yale maeneo kwa ajiliya kusimika minara. Kuna changamoto kubwa, watu wengiwanafuatilia sana, lakini hawapati haki zao. Kwa hiyo,naomba Serikali iangalie pia suala hili hasa wananchi ambaoni wanyonge ambao wame… (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Lolesia Bukwimba.Mheshimiwa…

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Spika, baadaya kusema hayo naunga mkono hoja. Nashukuru sana kwanafasi hii. (Makofi)

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. ShukuruKawambwa, atafuatiwa na Mheshimiwa Hussein Bashe.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa hii kuchangia katika hotubahii nzuri ya Mheshimiwa Waziri. Nitaenda moja kwa mojakatika hoja ya Bandari ya Bagamoyo.

Mheshimiwa Spika, mradi huu wa uwekezajiumeorodheshwa na Serikali katika bajeti ya mwaka huuambayo inamalizika 2018/2019 ikiwa ni mradi mkuu wakielelezo ambao Serikali mlitaka kuutekeleza kwa ajili yamaendeleo ya nchi hii. Mradi huu unajumuisha ujenzi wabandari, lakini pia unajumuisha ujenzi wa viwanda. Eneo hilimaalum la uwekezaji ni kichocheo kikubwa sana chamaendeleo ya nchi yetu, maendeleo ya viwanda namaendeleo ya uchumi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa yaleambayo umeyasema kwa maana kwamba, umeendanakabisa na mawazo ambayo nilikuwanayo mimi kamaMbunge wa Bagamoyo. Imekuwa faraja sana kupata haowawekezaji; China na Serikali ya Oman, marafiki zetu kamaWaheshimiwa Wabunge walivyosema. Lazima tutumie fursahizi za marafiki ambao tumehangaika nao sana kwa miakamingi ambapo sasa fursa hizi wanatumia watu wengine sisihatuzitumii, ni muhimu sana tutumie fursa hizi.

Mheshimiwa Spika, China na Oman wamekubalikuwekeza jumla ya dola bilioni 10 ama takribani trilioni 23 zaKitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bandari na ujenzi waviwanda. Mwanzoni wamekubali kwamba watajengaviwanda vikubwa 190 vya kuanzia. Maana yake kwa ajili yaujenzi huu, vitatoa fursa za ajira takribani 270,000.

Mheshimiwa Spika, kazi kubwa imefanyika na viongoziwetu na wataalam katika nchi hii, kwa miaka mingi iliyopita,tumeanza na mwaka 2012 ambapo MOU ilisainiwa, Machi,2013 Framework Agreement imesainiwa; Desemba, 2013Implementation Agreement imesainiwa; Oktoba, 2015

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Tripartite MOU imesainiwa; na Septemba, 2015 jiwe la msingila ujenzi wa bandari limewekwa na Rais Mstaafu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Pande na Mlingotiniwamejitolea ardhi yao kwa ajili ya maendeleo haya ya ujenziwa bandari pamoja na viwanda katika hali ngumu sana, lakiniwakasema potelea mbali acha tutoe maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, nasikitika sana kwambainavyoelekea sasa juhudi hizi zote hazikuzaa matunda.Nimesoma ukurasa wa 99, aya ya 136 ya Hotuba ya Waziri,inaelekea kwamba bandari hii sasa haipo.

Mheshimiwa Spika, China Merchant wakati tunasainiMoU ya 2012 wamesaini pia MoU na nchi ya Djibout kwa ajiliya ujenzi wa bandari. Hivi sasa wameshajenga multipurposeport inayoitwa Doraleh kule Djibout. Bandari hii sasa inafanyakazi. Kama vile haitoshi mwezi Machi mwaka huu wamesainitena na China Merchant ujenzi wa Special Economic ZoneDjibout kwa mtaji wa dola bilioni tatu na nusu, takribani shilingiza Tanzania trilioni nane; kwamba, 2012 wamesaini kama sisina wameongeza tena sasa hivi wanajenga Special EconomicZone.

Mheshimiwa Spika, kama vile haitoshi, katika kipindihiki sisi tunaongea tangu 2012, China Merchant weamesainina kujenga bandari Nigeria, Tin Can Ireland; wamejengaLome, Togo; wamejenga Abidjan, Ivory Coast, wamejengaColombo – Sri-Lanka.

Mheshimiwa Spika, kipindi hiki cha miaka hii karibusaba sisi tunafanya maongezi, nchi tano nil izozitajazimekamilisha maongezi. Djibout imekamilisha maongezi nawamejenga bandari, Nigeria wamekamilisha maongezi nawamejenga bandari, Togo wamekamilisha maongezi, IvoryCoast wamekamilisha maongezi, Sri-Lanka wamekamilishamaongezi na wamejenga bandari isipokuwa Tanzaniatumeshindwa kwa muda wote huu kukamilisha maongezi.Tuna tatizo gani? Tuna shida gani? (Makofi)

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Mheshimiwa Spika, wataalam wa nchi hizi tanonilizotolea mfano ni bora zaidi wanaweza wakakamilishamaongezi isipokuwa sisi nchi yetu ya Tanzania hainawataalam wa kuweza kukamilisha maongezi.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani 2025 nchi hii kuwanchi ya uchumi wa kati ni miaka sita ijayo. Hatuna muda tenahata kidogo wa kusubiri katika jambo hili. Mtaji wenyewe unawakati, kwa sababu sasa hivi China wanatekeleza mradi waowa Belt and Road Initiative nao uko time bound, tukiuachahuo maana yake watakwenda kuwekeza mahali pengine.Huwezi kupata mtaji mkubwa kama huu unasubiri nchi mojatu ifanye maongezi miaka saba haikamiliki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, atakapokuja Mheshimiwa Waziri,kama ulivyoweka msisitizo, atuambie kwa kina. Tanzania tunawataalam, Watanzania ni mahodari, Watanzania hatuna faniambayo iko nyuma. Haiwezekani nchi hizi zikawezakukamilisha, bandari zikajengwa, sisi tunaendeleakuzungumza kila siku. China wana usemi wao, manenomatupu ni hatari kwa Taifa. Na sisi tunataka kukumbatiakuzungumza tu na kuzungumza tu na kuzungumza tu kila siku,tutaliangamiza Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naunga mkonohoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Nilishakutaja MheshimiwaHussein Bashe, utafuatiwa na Mheshimiwa Charles Tizeba naMheshimiwa Saada Mkuya atafuata, dakika saba saba.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa na vilevile nikushukuru kwadhati kabisa kwa maamuzi uliyofanya ya kuchangia kuhusuBagamoyo. Ni jambo muhimu sana. Investiment ya SpecialEconomic Zone ya Bagamoyo ilikuwa inatuletea inflow ya 10billion US Dollar kwenye uchumi wetu na ni jambo ambalo nivizuri Serikali wakati Waziri anakuja kufanya wind-upwatueleze kinagaubaga kwa nini mradi huu unasimama?

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Mheshimiwa Spika, nataka niongelee SGR. Kumekuwana mjadala mkubwa sana na last week kulikuwa kunamjadala mkubwa hapa ndani ya Bunge kwamba mradi wetuwa SGR kwa nini hauonekani kama unatuletea impact namzunguko wa fedha kwenye uchumi?

Mheshimiwa Spika, nilitaka nije niombe kwambawakati Waziri anakuja kufanya wind-up na hasa Waziri waFedha, the financing model ya SGR ya Dar es Salaam –Makutupora: Je, itaendelea kuwa hiyo hiyo model yafinancing kutoka Makutupora kwenda Tabora; Tabora –Mwanza, Tabora – Kigoma, Uvinza – Msongati? Kwa nininasema hivyo?

Mheshimiwa Spika, the financing model tunayofanya,which is very good, mimi sipingani nayo katika hatua hii yaawali, kwamba tunatumia fedha zetu kujenga reli hii. Sionikama tukiendelea hivi mpaka mwisho itatusaidia ndani yauchumi wetu. Kwa sababu tunakusanya shil ingi natunapomlipa huyu Mkandarasi ni ratio ya 65:35. 35% ya fedhazake analipwa kwa shilingi. 65% analipwa kwa dola.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kinachotokea nikwamba shilingi inakuwa converted into dollar, halafu dolaanalipwa Yapi nje, halafu Yapi anarudisha ndani dola ai-convert into shilling kuwalipa local contractors. Kinachotokeaile process ya kuhamisha shilingi kwenda kwenye dola thereis a cost, kwa sababu we are losing money in that process.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili kuna tatizo kubwa laMkandarasi wa Yapi kulipa local contractors. Hili nalo ni tatizo,ni vizuri Wizara ikaliangalia. Hili ni jambo muhimu sana.Tuangalie financial model ya ku-finance mradi wa SGRkuanzia Makutupora kwenda mbele ubadilike. Bila hivyo,uchumi utaendelea ku-suffocate.

Mheshimiwa Spika, sitaki kujadili takwimu za IMF, hizoni kazi za zao, lakini ninachotaka niwaulize, ukiangalia trend,toka mwaka 2014 construction sector in general, 2014/2015

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

ili-grow by 16.8%, leo ina-grow katika wastani wa asilimia 13.What is the problem? Shida ni nini wakati tunapeleka fedhanyingi sana za development budget kwenye constructionsector? Kuna nini? Hili ni jambo ambalo lazima tujiulizeSerikalini.

Mheshimiwa Spika, tuangalie 2014 to date, averagegrowth yetu ya GDP ni asilimia sita point something, imekuwanamna hiyo mpaka leo. Kuna nini wakati tunapeleka fedhanyingi sana kwenye construction? Hili ni jambo moja.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo nataka nitoeushauri, Mheshimiwa Waziri Kamwelwe, TRC wako pale,washauriane hili. Sisi tunajenga SGR kwenda Mwanza. Ourcash cow kwenye reli ni mizigo na ni nchi ya Uganda, Congo,Zambia na Malawi.

Mheshimiwa Spika, nashauri, TAZARA inasuasua, TRCikodi infrastructure ya TAZARA halafu wanunue wagon kwaajili ya kuhudumia Zambia na Malawi. Wakati huo tutakuwatunalipa fee kwa kutumia infrastructure hiyo, TRC wanunuemabehewa na vichwa ambavyo vinaweza kupita kwenyereli ya TAZARA ili wabebe mizigo ya Zambia na Malawi,tutapata revenue.

Mheshimiwa Spika, la pili, leo sisi tunataka kumpelekeahuduma Mganda ambaye ana-constitute aslimia 30 ya mzigowetu. Tujenge kipande cha Port Bell kwenda Kampalaambacho ni kilometa 11, tuweke meli kubwa, mzigo utokeDar es Salaam mpaka Mwanza, uingie kwenye hiyo melikubwa ibebe mizigo tupeleke Port Bell. Tutakuwa nacompetitive age. Kinachotokea, tunaye-compete naye leoambaye ni Mombasa anamjengea bandari kavu Mganda,Naivasha ili kupunguza distance iliyoko ambayo sisi kwetu nicompetitive age. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu, kwenda Msongati nikilometa 200, ninawashauri achacheni na reli ya kwendaRwanda, wekeni fedha kujenga Msongati kuja Uvinza.Tujenge kwa SGR. Tukijenga kwa SGR kutoka Msongati kuja

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Uvinza mzigo utabebwa kutoka Msongati kuja Uvinza kwaStandard Gauge. Kutokea pale tutatumia meter gauge kujaDar es Salaam. Kwa hiyo, tutaanza kupata fedha kabla yareli kufika Mwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la nne, we only have 30 kilometerskuhudumia Eastern Congo ambayo ina population ya 22million people. Ushauri, shaurianeni na Serikali ya Congotufanye joint effort tujenge gati upande wa Congo tuwezekubeba mizigo kutokea Kigoma kwenye meli kubwa tuvushekwenda Kalemii ili tuanze kuwahudumia hawa wakatitunasubiri ku-generate revenue. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, this is a question of where to getmoney. Kwa nini nasema hivi? Leo Mozambique wamejengareli kwenda Zambia, ili…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

SPIKA: Bahati mbaya dakika saba ndiyo hizo.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, naombaSerikali waangalie maeneo ambayo wanaweza kupatafedha. Ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Mjadala huu unaisaidia sanaSerikali katika kupata mawazo mbalimbali kutoka kwaWaheshimiwa Wabunge. Waheshimiwa Wabunge ni wajibuwetu kushauri. Kwa hiyo, tutumie fursa hii vizuri.

Mheshimiwa Spika, nilimtaja Mheshimiwa SaadaMkuya na Mheshimiwa Tizeba. Tuanze na Mheshimiwa Saada.Baada ya Mheshimiwa Tizeba, Mheshimiwa Turky.

MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia hojaambayo iko mbele yetu. Naunga mkono hoja na nitakwendakwenye maeneo mawili matatu specifically.

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Spika, kwanza naanza na Shirika letu laNdege, Air Tanzania. Naipongeza sana Serikali kwa uamuzihuu ambao umekuja kuwa implemented katika awamu hii,lakini tumeanza mazungumzo muda mrefu na tumeanzamipango ya kufufua hili shirika katika awamu zilizopita.Mkurugenzi Mkuu wa shirika anafanya kazi nzuri, lakinitunaomba aangalie utaratibu mzuri zaidi wa kupunguzaunnecessary delays, hususan katika safari ambayo tunafanyakutoka Dar es Salaam kuja Dodoma.

Mheshimiwa Spika, ukipanda ndege mara saba,nadhani mara tano tunapata delays; na tunaambiwa maranyingi kwamba kunakuwa kuna operational problems, lakinikunakuwa kuna delays. Kwa hiyo, hiyo kidogo inapunguzaufanisi wa shirika letu la ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kiukweli ni kwamba shirika hili ni laJamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini toka kuanzishwashirika hili hatujawahi kuwa na Mjumbe wa Bodi anayetokaupande wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamaana ya Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nataka Mheshimiwa Waziriatakapokuja hapa, asije akaniambia napandikiza,namwambia kwamba hakujawahi kuwa na Mjumbe wa Bodina hili ni shirika letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Nataka tu anijibu kwa nini hakujawahi kuwa na huyo Mjumbewa Bodi na kuna matatizo gani hasa? Kwa nini asikuwepo?Lini atakuwepo Mjumbe huyu wa Bodi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, tunaipongeza sanaMamlaka ya TCRA kwa kuendesha zoezi hili la usajili wa lineza simu. Hoja yangu kubwa hapa ni kwamba hili ni zoezi zurina litatusaidia kama Taifa, hususan kupunguza uhalifu kwanjia ya mitandao, lakini wakati zoezi hili linaendelea,kitambulisho kikanachotakiwa ni kitambulisho cha NIDA. KuleZanzibar wengi tuna vitambulisho vya Mzanzibari (Zan ID),hivi kwa nini TCRA haikubali mtu asajili line yake kwa kutumiaZan ID ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetumiapesa nyingi sana kuwekeza? (Makofi)

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Mheshimiwa Spika, kule Zanzibar sisi huwezi kuishi,maisha yako hayatakwenda kama huna Zan ID. Sasa tukijakwenye TCRA ambayo tunajua ni Mamlaka ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, kwa nini haitambui Zan ID kwa mtuambaye hana kitambulisho cha NIDA? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba atakapokujaMheshimiwa Waziri atuambie ni kwa sababu gani TCRAhaikubali mtu asajili line yake kwa kutumia kitambulisho chakecha Mzanzibari ambacho kwetu katika miamala yote, katikamatukio yote, katika kila unalofanya Zan ID lazima iwepo?Kwa hiyo, naomba hilo lizingatiwe na tuje kupata majibu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, tunapongezaMfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuendeleakabisa kuona kwamba inatekeleza kazi zake kwa ufanisi. Kunamaeneo kadhaa ambayo katika mwaka 2019/2020itaendelea kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuendeleakutekeleza mradi wa kuanzisha vituo 10 vya TEHAMA.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri atakapokujaatuambie hivi huu mradi wa vituo 10 vya TEHAMA, wapi nawapi utatekelezwa na tuone kwamba kwa upande waZanzibar vituo hivyo vitajengwa wapi au vitatekelezwa wapi?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ambalo natakakuzungumzia ni kuhusiana na ndege zetu hizi ndogo. Maranyingi sisi wa visiwani tunatumia sana ndege hizi ndogo, lakinitunachokiona mara nyingi ni kwamba, badala ya kuwepomarubani wawili kunakuwa kuna rubani mmoja.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2018 au mwaka 2017wakati lilitokea tatizo kupitia ndege hii ya Coast Airline,nakumbuka Serikali i l itoa tamko kwamba, ni lazimatuhakikishe kwamba ndege zetu hizi ziwe na marubani wawili,lakini umekuwa utaratibu wa kawaida, hata kamatunapanda hizo ndege, tunatoka Dar es Salaam tunakujaDodoma, rubani anakuwa mmoja.

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

Mheshimiwa Spika, sasa tunaomba Serikali i-literateyale mazungumzo yake ama tamko lake, tuone kwamba hizindege ndogo zinapunguza sana matokeo ambayohatutarajii, lakini sababu isiwe kwamba kunakuwa kunarubani mmoja. Hili jambo lipo na limezungumzwa, lakini sasahivi naona linatoweka na halipewi msisitizo ambaounahitajika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, otherwise nashukuru sana kwakupata nafasi hii. Naomba sana Bodi ya Shirika la Air Tanzaniatuone Zanzibar na yenyewe inakuwepo. Nashukuru. (Makofi)

MHE. DKT. CHARLES J. TIZEBA: Mheshimiwa Spika,nikushukuru sana kwa kunipa nafasi nami ya kuchangia hojailiyopo mbele yetu. Kwa sababu ya muda, mengineniliyopanga kusema nitaya-skip na nijikite katika mambomatatu hivi ambayo naamini kwamba yana umuhimumkubwa Serikali kuyapima na kuona kama inawezakuyafanyia kazi kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, moja, ume-pre-emptymazungumzo niliyotaka kufanya ya Bandari ya Bagamoyo,lakini kwa vile na wewe uliamua kuchangia siyo mbaya.Bandari hii ndiyo itakayokuwa pekee ya kupokea mzigoutakaosafirishwa na SGR, Dar es Salaam haina huo uwezo.Amesema vizuri sana Mheshimiwa Ally Saleh kule, Bandari yaDar es Salaam tutake, tusitake, hata tuki-dredge namna ganipale Magogoni, turning base inayoweza kupatikana haiweziku-accommodate post panamas na forth na fifth generationya meli zinazotengenezwa sasa, lakini Bagamoyo ndiyoilikuwa jibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya mambo yaangaliwe upyatu, yaani tusifike mahali tukalikatia tamaa hili jambo. NaishauriSerikali yangu na naipenda, wafanye kuangalia upya sualala Bagamoyo haraka iwezekanavyo kwa sababututakamilisha ile SGR, hatutakuwa na mahali pa kushushiamzigo, tutaonekana kituko. (Makofi)

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Mheshimiwa Spika, jambo la pil i ni Mfuko waBarabara; Mfuko wa Barabara wameusema wengi katikakuchangia hotuba ya TAMISEMI, lakini mahali penyewe nihapa kwa sababu Act ya Mfuko wa Barabara ipo chini yaWizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na ulemgawanyo wa 70 kwa 30 umepitwa na wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitasema neno moja tu, mtu akiwana matatizo ya mishipa ya damu, mishipa mikubwa huwahai-clot/haipati obstructions, inayopata obstructions nimishipa midogo midogo (arteries) na hiyo ndiyo husababishakifo. Sasa sisi tuki-concentrate sana na barabara kuutukasahau kwamba barabara kuu hazina maana kamabarabara ndogo hazifikishi watu na mizigo kwenye barabarakuu na lenyewe hili tunakosea. Iangaliwe upya tu, waangaliekwamba kama sasa ni 50 au 60, 40 lakini kuna kila haja yakuongeza fedha kwa upande wa TARURA; sasa hivi ilivyoTARURA haiwezi ku-function. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, natakakuzungumzia watoa huduma wanaitwa DSTV. DSTV hawawanatoa huduma kama ving’amuzi vingine, wanatoahuduma kama kampuni za simu, kama umeme na kadhalika.Software ya kumfanya mtu aliyelipia atumie kadiri anavyolipiazipo lakini ndugu zetu hawa wao wana-charge kwa mwezi,ukishalipia ile subscription hata ukafunga king’amuzi, baadaya mwezi ukienda kimekwisha unatakiwa ulipe tena. Sasamimi sitaki kuuita wizi kwa sababu tunalipa kwa halali, lakinihuo ni wizi. Hizi simu tuna-recharge vocha, mbona waohawatuambii uki-recharge baada ya siku 5 imekwishaautomatically, wao kitu gani kinashindikana kwamba nikiwanimezima king’amuzi maana yake mita haisomi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nimemaliza hayo, naombanizungumzie jimbo langu kidogo. Ukurasa wa 300 katika kitabucha hotuba ya Waziri, imetajwa barabara ya Sengerema-Nyehunge-Kahunda. Hii barabara natarajia inapaswakufanyiwa upgrading na siyo feasibility study na detaileddesign, namwomba Mheshimiwa Waziri aangalie hayomaneno yaliyo kwenye mabano yanatofautiana na uhalisia

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

uliopo kwa sababu hiyo hatua ya feasibility study na detaileddesign imekwishapita na huku ameweka katika miradi kwahiyo, hawawezi kurudia mradi huo ambao tayariumekwishakamilika. Naamini ni typo tu, kinachotakiwa hapakuwepo na naomba hili katika kuhitimisha anifafanulie yaanianihakikishie kwamba ni upgrading na siyo habari yafeasibility study na detail design. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho; naomba kuzungumziavivuko; nimesoma kitabu vipo vivuko vinajengwa, lakini kunakivuko cha Kome – Nyakalilo, zimeenda tume mbalimbalipale. Sitaki na mimi kubashiri vifo, ndugu yangu MheshimiwaMkundi alibashiri ajali kule Ukara na ikatokea, sasa mimi hayomaneno sitaki kuyasema, itoshe tu kusema kwamba hichokivuko hakitoshi watu ni wengi. Kome leo ina watu karibia120,000 wanavushwa na kivuko cha tani 35, ukiuliza kwa ninikivuko kingine hakijengwi? Fedha hakuna, fedhatunayozungumzia ni shilingi bilioni mbili au tatu, watu palewakiteketea sijui nani ataulizwa.

Mheshimiwa Spika, nil imweleza MheshimiwaKamwelwe tulipokuwa Ukara kwamba hicho kivuko hakifai,Mheshimiwa Kwandikwa amefika mwenyewe; tumeiliyoundwa na Serikali baada ya MV Nyerere kuzama imefikapale Nyakalilo, nimeshangaa kweli kwamba humu ndanihakuna mazungumzo ya eneo hilo, halafu nikisimamakupinga bajeti nionekane mkorofi? (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, usipinge bajeti inakutosha Dkt.Tizeba, Mheshimiwa Waziri ataangalia hayo maneno.(Kicheko)

Mheshimiwa Salim Turky atafuatiwa na MheshimiwaLucy Magereli, Mheshimiwa Mlinga na Mheshimiwa Zungumjiandae.

MHE. SALIM HASSAN TURKY: MheshimiwaSpika,ahsante sana. Kwanza nichukue nafasi hii kumpongezasana Rais wetu hasa kwa kufikiria vitu vikubwa na katika vituhivyo, hivi viwili ni vya kiuchumi kabisa na leo hapa mimi na

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mheshimiwa Bashe tunakaa pamoja lakini fikra zetu tofautikabisa. Mimi nasema uchumi wetu tunatoka kwenye reli nakwenye ndege, tujipangeni; tunajipanga namna gani?Naomba sana, pesa ziko nje nje kwa kuendesha reli hii nandege. Naomba Serikali itazame namna ya ku-float bondskatika national na international market. Tukitoa share hizitukaziweka katika stock exchange yetu, tayari watuwatanunua sharesnashares hizi ndiyo pesa unazipata harakaharaka. Tena hili litakuwa na nguvu zaidi hata keshoMheshimiwa Rais akimaliza muda wake maana yake sasatunaingia partnership ya private na Government, tupopamoja sasa. Kwa hivyo, hata ile management keshoitasimamiwa vizuri sana, mambo haya makubwa hayatofelimaisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, naomba sana hilitulipokee kwa nguvu zote Mheshimiwa Waziri alifanyie kazi.Halafu reli ni moja ambayo haina hata mshindani,Government peke yake, ni monopoly yao, hakuna mtuanayeweza akajenga reli. Kwa hivyo, hii naamini akisemakesho tu atawapata shareholders sisi wengine wote humututanunua shares na watu wa nje wengine watakujawatajiunga pesa nje nje, hilo tumemaliza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili; nashukuru sana bandariinafanya kazi vizuri sana hasa ninavyozungumza Bandari yaDar es Salaam pale, lakini kuna kitu ambacho kinatakiwakiboreshwe, nacho ni mizigo inayotoka Zanzibar. Baina yaBara na Zanzibar ni biashara ya tangu mababu na mababu,japo siku hizi imepewa majina ya ajabu ajabu lakini huweziukaamini ukweli kwamba Zanzibar ni kisiwa cha biashara nabiashara hii itadumu sisi kama tupo hata tukiondoka naaminibiashara hii itaendelea.

Mheshimiwa Spika, pale Dar es Salaam sasa hivi kunacongestion kubwa sana sana ya mizigo ya Zanzibar,nashukuru kwamba tumetoa ushauri kwa bandari kulikuwana banda lilijengwa ukuta, namshukuru sana pale PortDirector tumempa ushauri na ameufanyia kazi mara mojana jana nimepigiwa simu kwamba upo ukuta wa bati pale

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

wa kuweka magari ya godauni umeshaondoshwa na watuwanashusha mizigo yao. Hata hivyo, bado kuna ukiritimbammoja mkubwa sana ambao unafanyika; nao ni kwambakuna ZFA, TBS na TRA wanagongana pale, mizigo haitokindani ya warehouse. Naomba hili lisimamiwe kwa nguvu sanachini ya bandari yake kwa sababu hawa wote hawana ofisiisipokuwa yeye mwenye bandari ndiyo anawakaribisha mle.Kwa hivyo, wakubwa wa bandari waangalie hilo nawalisimamie kwa nguvu zote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu; Mheshimiwa Rais wetuanataka nchi hii ikue kiuchumi, mimi nashangaa sanamnapokuja na mawazo ya kudumaza uchumi kwa kusemamtu mmoja awe na line moja ya simu au line mbili za simu,akitaka ya pili apate kibali; vitu hivi vya ajabu vinatoka wapijamani? Huu uchumi leo sisi tunao mobile operators karibuwatano kwa sita, kila mmoja anataka aingie sokoni; hapakuna ajenda gani? Tunataka kumpandisha mtu mmoja, kamailikuwa wana nia kila mtu awe na simu moja, basi hawaoperators ilikuwa tuwanyime leseni hizo. Leo kila mmojaanataka soko, kwa nini anatubana tusiwe na simu?

Leo mimi nataka simu ya jimboni kwangu na ya ofisinikwangu; hizi ni simu lazima kila mmoja apewe uhuru wake,huwezi ukanibania mimi ooh uwe na laini moja, kwa nini?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi uchumi huu unatakiwaukue kwa kasi, huwezi ukabana hizi simu; simu nyingine miminapokea simu za nje tu, sasa leo unaniambia aah usiwe. Hiyonazungumza mimi kama Mbunge lakini kunawafanyabiashara nje, wakulima na watu wote wanatakasimu. Naomba hii sera ya kusema kwamba mtu mmoja lainimoja, akitaka laini ya pili special pass sijui iende wapi, hiyokitu inadumaza uchumi wa nchi hii. Naamini Rais akilisikiahili, hawezi akalikubali hata siku moja, tutakuja kuumbuliwahapa bora tujiumbueni wenyewe, tujiwekeni sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya haya, sina la zaidi ilanaipongeza sana Wizara na naunga mkono hoja na pia

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

maendeleo yote yanatofanyika katika nchi hii nayapongezakwa nguvu sana na naamini 2020 CCM itatisha sana.Ahsanteni sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Turky. NilishakutajaMheshimiwa Lucy Magereli.

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa nafasi ya kuchangia. Naomba nianze kwa kueleza tatizola kwanza kabisa la nchi hii kwamba ni matatizoyanayohusiana na sera na mipango. Tuna changamoto yakupanga nini tunataka, tuna changamoto ya kuamua ninitutekeleze na tunapoamua kutekeleza basi ni kwa manufaaya nani na kwa kipindi gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niishauri Serikali tuwewaangalifu sana nini tunapanga, nini tunatekeleza, kwawakati gani na kwa maslahi ya nani. Tuangalie mipango yetuya maendeleo na vipaumbele tuvipange kadri tunavyowezakutekeleza. Tumekuwa na vipaumbele vingi kuliko uwezowetu wa kutekeleza, badala yake tunakuwa na orodhandefu sana ya miradi ambayo hatuwezi kui-fund, tunatumiamikopo kutoka nje, pesa zinaingia kwenye miradi mikubwa,hiyo miradi haikamiliki, haiondoki ilipo wala haitunufaishi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri ni huu wa Bandari yaBagamoyo ambayo watu wengi wameizungumzia, ukurasawa 99. Ziko kazi nyingi sana ambazo zimeshafanyika pale napesa nyingi sana za walipa kodi zimeingia pale, leo yanakujamaelezo mepesi kweli kweli yanayosema eti wameshindwakuelewana majadiliano na wawekezaji, ukurasa wa 99,naomba ninukuu inasema:

“Mradi umeshindwa kwa sababu wawekezaji haokuweka masharti yasiyokuwa na maslahi kwa Taifa, mashartihayo ni pamoja na wawekezaji hao kudai kuachiwa jukumula kupanga viwango vya tozo na kutoruhusu wawekezajiwengine katika eneo la kati ya Bagamoyo na Tanga.”

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Mheshimiwa Spika, haya ni mambo ambayoyangeweza kujadiliwa, haya ni maelezo ya kitoto kabisakwamba eti tumeahirisha utekelezaji wa mradi wa Bagamoyokwa sababu eti wawekezaji wameweka masharti, hatunawataalam wa kujadili mambo hayo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nishangae pia kwambasasa Serikali inarudi kushika hatamu za huduma zakimiundombinu wakati ni kati ya eneo ambalo lingewezakuvutia wawekezaji na ni miradi ambayo ingewezakutekelezwa kwa mfumo kama alivyosema Mheshimiwa Turkyhapa aidha wa hisa ama kupata wadau na wachangiajiwengine katika maeneo hayo ili kuboresha huduma zetu zakimiundombinu ili moja, tuweze kutanuka, lakini pili, tutoehuduma, tatu, tuweze kutoa ajira. Kwa nini Serikali sasa ndiyommiliki wa SGR, ndege za Serikali, Serikali ndiye sasa hivimjenga Stiegler’s Gorge, kwa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niende kwenyedanadana za ATCL. Mwaka jana nilisimama nikashauri,nikasema miaka michache ijayo of course nilitaja mitano,nafurahi kwamba hata hatufiki mitano tunakaa tena hapaleo kujadiliana namna ambavyo ATCL haisaidii nchi hii, haipigihatua na imeshindwa kabisa ku-perform. Nilishauri kwambatuanze kwanza na kuimarisha mtandao wa ndani wa ndege,mpaka sasa hivi hatua zilizochukuliwa ni dhaifu mno.Tunang’ang’ana kufikiria kwenda Uchina kuchukua abiriakatika mipango ambayo siyo ya kudumu, si endelevu na walahaitaisaidia nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndege ambazo tumezinunuatulizinunua kwa maana ya lengo la kufufua ATCL, lakini kwabahati mbaya hizo ndege zilipewa Wakala wa Serikali na sasahivi tunavyozungumza kwa bahati mbaya nyingine tena,ndege hizo zimehamishiwa Ikulu. Sasa sielewi kwamba Ikuluimedhamiria kufanya biashara na bahati mbaya nyinginezaidi ni kwamba bado suala la ndege za Serikali tunazipafedha kupitia bajeti ya Vote 62 lakini zinakwendakuhudumiwa na Vote 20; pana kizungumkuti hapo tunaombaWaziri mhusika atatusaidia kuchambua jambo hilo ni kitu gani.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Mheshimiwa Spika, nirudi Dar es Salaam; suala lamsongamano wa Dar es Salaam ni mkubwa, imekuwa shidana tabu. Sasa hivi Dar es Salaam mvua inanyesha ninyi nyoteni mashahidi, ule mji hautembei. Mradi wa mwendokasituliofikiria kwamba ungetupa suluhisho nao umekuwa shida,umekuwa tatizo sugu; mwendokasi hau-perform, lakini kibayakuliko vyote kumekuwa na changamoto ya ununuzi na uuzajiwa tiketi. Scanner za pale hazifanyi kazi kwa hiyo, pesazinatolewa na kuhifadhiwa kiholela na sijui zinakuwa reportednamna gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine kibaya kuliko vyote, sasahivi pale kwenye mradi wa mwendokasi hakuna chenji, ukidaichenji ya 200, 150 hupati. Kwa hiyo, kuna makusanyo mengineya mapato yamezaliwa pale katika mradi wa mwendokasina kuwanyang’anya wananchi na abiria wa Dar es Salaamfedha zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala la ujenzi wa gati namaegesho eneo la abiria Ferry ya Kigamboni. Mwaka 2016/2017 na mwaka 2017/2018 tuliizungumza, tukalipangia fedhana 2018/2019 vilevile, lakini mpaka ninavyozungumza hadileo pale Ferry ya Kigamboni hakuna kinachoendelea, abiriawetu bado wanarundikana kama mizigo, utaratibu wahuduma kama vyoo na huduma nyingine pale badohaujakamilika, utaratibu wa utoaji magari ndani ya vivukona kuondosha eneo la ferry na kuingia bado ni changamoto.

Mheshimiwa Spika, kibaya kingine sawa kama ilivyokwenye mwendokasi na zile scanner za tiketi pale ferry nazohazifanyi kazi, kwa hiyo, sasa hivi tiketi unanunua inapita bureikiwezekana yule anayekusanya akaamua kuzirudisha tenakule zikauzwa upya, zinauzwa upya; hicho ni chanzo kinginecha wizi wa fedha za Watanzania kupitia ule mradi wa malipoya ferry pale Kigamboni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala la bajeti ya Wizara yaUjenzi. Mwaka 2016/2017 tuliwapa jumla ya asilimia 40.3 yafedha zote za maendeleo sawa na shilingi trilioni 11.8, mwaka2017/2018 tumewapa asilimia 40.8, mwaka 2018/2019

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

tumewapa asilimia 34.8, lakini bado unaweza kuona kabisakwamba Wizara hii haijaleta matokeo tarajiwa ukilinganishana kiasi cha bajeti kubwa ya maendeleo tunayowapatia.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante ingawa nilikuwa nadakika kumi, umenipa pungufu ya hapo. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, mbio mbio kidogo; MheshimiwaMlinga atafuatiwa na Mheshimiwa Zungu dakika tano tano.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Naomba nianze na barabara ya Kidatu –Ifakara; barabara hii ilizinduliwa tarehe 5/5/2018, tulizinduanikiwemo na mimi na Mheshimiwa Waziri na Wabunge wotewa Morogoro. Rais alizindua ujenzi na barabara ikaanzakujengwa, lakini baada ya muda mfupi mkandarasiakaondoa vitu site; mpaka sasa hivi ninavyoongea ni mwakammoja sasa barabara hii haijawekwa hata kilometa mojaya lami.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais alitoamwongozo kwa Wizara ya Fedha na Wizara ya Ujenzi watatuetatizo la mgogoro wa kikodi wa VAT lakini mpaka leo hiiMheshimiwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Ujenziwanaogopana kama mtu na baba mkwe wake. MheshimiwaRais ameshawaambia wakae watatue huu mgogoro lakiniwanaogopana; kama wameoleana si wamwambieMheshimiwa Rais awahamishe Wizara waje Mawaziri wenginewatatue huo mgogoro kama wao wanashindwa? (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, la pili, ni barabara ya Ifakara –Mahenge. Barabara hii ina urefu wa kilometa 74. Sasa hiviUlanga tuna deposit kubwa ya graphite na kuna kampunikubwa tatu tayari zimeshaanza uwekezaji na kwa mwakatutatoa tani zaidi ya laki tano.

Mheshimiwa Spika, kwa hali ya barabara ile hiibiashara haiwezi ikafanyika. Endapo barabara hii itakuwatayari Serikali ina uwezo wa kuingiza zaidi ya shilingi bilioni

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

400 kwa mwaka. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri wakati ana-wind up atuambie mkakati uliofikiwa kwa ajili ya barabarahii.

Mheshimiwa Spika, barabara nyingine ni ya Liwale –Ulanga. Ukiacha ahadi ya Mheshimiwa Rais, ni mkakati waSerikali kuunganisha barabara za mikoa na ni muhimu sanakatika uchumi wa Wanaulanga. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziriatuambie amefikia wapi kuhusiana na ujenzi wa barabarahii umefikia.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni la viwanja vyandege. Naipongeza Serikali kwa umaliziaji wa Terminal III lakiniwasisahau na viwanja vingine kwa vifaa, maanatumeshuhudia ndege zikisukumwa na watu. Bahati mbayaikatokea wafanyakazi wa airport wakawa na miili kama mimiwatasukumaje hizo ndege? (Kicheko)

Suala lingine ni uhalifu wa mitandaoni, hii naongeleakuhusu TCRA. Uhalifu wa mitandaoni umegawanyika katikasehemu tatu: Udhalilishaji, wizi na upotoshaji.

Mheshimiwa Spika, tumeshuhudia udhalil ishajimkubwa na TCRA wamekuwa wakikaa kimya. Wameanziakwa viongozi wa siasa sasa hivi wamekuwa wakitengenezapicha za ngoni za viongozi wa dini. Hali imekuwa mbaya naTCRA wamekaa kimya.

Mheshimiwa Sika, suala lingine ni la wizi wa mitandao.Wizi huu makampuni ya simu yanahusika. Tumeona meseji zatafadhali tuma pesa kwenye namba hii, waganga feki,unaweza ukatumiwa meseji ukaambiwa mtoto wakoameanguka shuleni, hizo meseji ni za uongo. Meseji nyingizinatoka Kampuni ya Vodacom na baada ya uchunguziwangu nikakuta wafanyakazi wanahusika.

Kwa hiyo, makampuni ya simu walipeni vizuriwafanyakazi wenu na wekeni mfumo ambao mtaangaliahawa wafanyakazi wasiwe wanashiriki katika wizi wamitandaoni. (Makofi)

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na taarifa nyingi zaupotoshaji. Taarifa hizi nyingine zinatolewa na Wabungewakiwa wanapotosha taarifa za Serikali katika mitandao nawanafahamika lakini TCRA wanashindwa kuwachukuliahatua. Naomba suala hili lishughulikiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la ATCL nanitaongelea kwenye nauli. Nauli za ATCL zimekuwa kubwatofauti na matarajio ya Watanzania. Kwa mfano, kutokaDodoma kwenda Dar es Salaam nauli hadi Sh.600,000. Sasamimi nakuwa nimepanda nalipa nauli au nimekodishandege? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, napenda kuongeleausafiri wa Noah. Enzi zenu kipindi hicho kulikuwa na mabasitu, sasa hivi kuna usafiri wa Noah ambao umesaidia kwa kiasikikubwa. Sasa hivi kuna Noah zaidi ya 16,000 zinasafirishaWatanzania zaidi ya milioni 115 kwa mwaka. Hizo Noah 16,000zimeajiri makondakta na madereva 32,000. Ukichukulia kilakondakta mmoja na dereva mmoja akiwa anahudumia watuwanne, kuna wananchi zaidi ya 128,000 wanahudumiwa nawatu hawa. Bado wanalipa kodi, TRA, SUMATRA, bima nawanatumia mafuta lakini kumekuwa na sintofahamu yahawa madereva wa Noah na huu usafiri wa Noah Serikaliimekuwa ikiwasumbua hasa SUMATRA…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,ahsante, siungi mkono mpaka niambiwe suala la VATlinaishaje.

SPIKA: Ahsante. Tunaendelea, Mheshimiwa Zungu,dakika tano.

MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa dakika hizo.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

Mheshimiwa Spika, mchango wangu utajielekezakwenye masuala ya infrastructure na hasa Bagamoyo kamaulivyosema wewe na baadhi ya Wabunge.

Mheshimiwa Spika, ombi langu kwako, sasa hivi lazimatuwe na new thinking kwenye economic corridor nchiniTanzania. Bila kuweka new thinking tutaendelea kuwa waogawa kufanya maamuzi, kutoa ushauri na kuirudisha nyumbahii. Uzalendo haimaanishi kukataa kila kitu, lazima tuwe nacalculated risk. Risks hizi zinapimwa na zinaweza zika-workTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ombi langu kwako; negotiatingteam hii ya Tanzania ipate fursa ya kuja kwenye Bunge lako,ikae na Wabunge wajaribu ku-brainstorm na kusaidia nchiyetu iweze kwenda mbele na hasa kwenye mradi huu waBagamoyo. Infrastructure za nchi nyingi sana zimeendeshwana gold backed currency; deposit ya gold na baadhi yamadini nchini mwetu yanaweza kutumika ku-fundinfrastructure katika nchi yetu. Naomba wataalam wa nchiyetu watazame suala la gold backed currency ili kuwezakujenga taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napongeza watendaji wa Serikali,nampongeza Waziri, naipongeza Wizara hii kwa kazi nzuriwanayoifanya. Mchango wangu ulikuwa ni huo tu, Bungelipate nafasi kukaa na team inayo-negotiate Bandari yaBagamoyo ili tupeane taarifa mbalimbali na tu-move thiscountry forward. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naunga mkonohoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana kwa kuchangia kwa kifupi kabisa,ni mchango mzuri sana.

Tunaendelea na Mheshimiwa MohamedMchengerwa, dakika saba, ajiandae Mheshimiwa CharlesMwijage.

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaSpika, ni aibu kubwa sana kwa taifa hili kuwa na wanasheriaambao wanafanya negotiation kwa miaka saba. Hiiinadhalilisha sana wanasheria hapa nchini au wale woteambao wapo katika tume ya kufanya negotiation kuhusuujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wewe ni shahidi, uliunda Kamatiya Tanzanite hapa pamoja na Kamati ya Almasi. Wabungewalitumia miezi mitatu tu kuishauri Serikali na kufanyamarekebisho katika mikataba ambayo ilikuwa ni mibovu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kupitia matakwa ya Ibara ya63 ya Katiba na marekebisho ya sheria tuliyoyafanya mwakajana ambayo yanalipa mamlaka Bunge kupitia mikatabambalimbali, nikuombe unda Kamati. Kama tatizo ni mkatabakwenye suala zima la Bandari ya Bagamoyo, unda Kamati,Wabunge wako vizuri, hatutatumia miaka saba. Tunahitajimiezi miwili, miezi mitatu na tutaishauri Serikali na penginetutawaita wahusika. Kama mkandarasi anayejenga hanauwezo, basi tutafute mkandarasi mwingine ambayeatahusika na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ikizingatiwakwamba bandari hii ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, anguko kubwa la kiuchumi la watuwa Pwani limetokana na ubovu wa miundombinu. Wewe nishahidi, Pwani ya Kusini, kuanzia Mkuranga, Kibiti, Rufiji naKilwa miaka 700 iliyopita walikuwa na uwezo wa kutengenezacoin yao. Juzi katika Pwani ya Australia wameokota coinambayo ilitengenezwa Kilwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wewe ni shahidi, tumekwendapamoja Russia, tumekutana na wananchi wa Fiji, waowanasema walitokea Rufiji, Pwani ya Tanganyika ambakondiko kunatokea Nyamisati na maeneo mengine. Wewe nishahidi tulikuwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Pwani siyo goigoibali tatizo kubwa tulilonalo ni miundombinu mibovu. Iwapo

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

miundombinu itaboreshwa, Pwani ya Kusini tutaweza kulishaTanzania hii.

Mheshimiwa Spika, wewe ni shahidi ulikuwa Kingupilana Ngarambe, Rufiji kuna viwanja vya ndege vitatu, ndiyowilaya pekee hapa nchini ambayo ina viwanja vya ndegevya kutosha. Mkoloni asingejenga viwanja vya ndege kamaeneo hili lilikuwa halifai kiuchumi. Kule Ngarambe kunavipepeo mamilioni ambavyo duniani hakuna lakini wataliiwatafikaje Ngarambe, ubovu wa miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hali ya miundombinu imefanyaWarufiji washindwe kuzalisha. Tunaona ni bora tulime vyakulavitakavyotufaa wenyewe kuliko kulima vyakula vingiambavyo inatugharimu kusafirisha kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, tarehe 4 Machi, 2017, MheshimiwaRais aliahidi ujenzi wa barabara ya Nyamwage – Utete.Sitakuwa na mchango wowote iwapo nitashindwa kutajabarabara ya Nyamwage – Utete ambayo Mheshimiwa Raisaliahidi.

Mheshimiwa Spika, sisi wanasheria tunatambua, zipoahadi wakati wa kampeni, ahadi hizi wakati mwinginezinaweza zisitekelezeke kwa sababu ni ahadi ambayo mtuanaahidi ili aweze kupata. Mheshimiwa Rais aliahidi 4 Machi2017 kwamba barabara hii itajengwa. Mimi nimpongeze sanaMheshimiwa Rais, anakuwa Rais wa kwanza kujengabarabara hii. Nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzikwa kuridhia barabara hii ijengwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Warufiji wamechoka na maneno,tumebadilisha Wabunge zaidi ya tisa, mimi ni Mbunge watisa ukianzia Bibi Titi Mohamed, kule ni miaka mitano mitanona Wabunge wamehukumiwa kwa sababu ya barabara hiiya Nyamwage – Utete. Unaweza ukawa ni Mbunge mzurisana, ukawa na mchango mzuri sana kama mimi lakini kamatutashindwa kujenga barabara ya Nyamwage – Utete,hatutoki. Katika sehemu ambayo kuna siasa, kule mtu

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

hajasoma darasa hata moja lakini ni profesa kwenye siasa,anayajua tusiyoyajua. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nimpongeze Wazirikwa kuridhia lakini kusema peke yake Warufiji wamechokana maneno. Nimesema sana, Waziri anajua, nimekwendasana ofisini kwake na yeye ameridhia barabara hii sasainakwenda kujengwa, Warufiji wanaomba kuona vitendo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Raisameridhia sasa kufungua Pwani ya Kusini, tunakwendakwenye utalii wa picha, tunakwenda kwenye mradi waumeme wa Stiegler’s lakini huko kote hatuwezi kufika kamabarabara zetu hazitaboreshwa. Barabara ya kutoka Kibiti –Mloka kama haitajengwa kiwango cha lami mradi waStiegler’s utachelewa sana, pengine utachukua miaka kumikukamilika. Kwa sababu ukarabati uliofanywa ambaoMheshimiwa Waziri ameuzungumzia kwenye kitabu chakehiki, ukurasa wa 15, ukarabati ule sasa hivi kutoka Kibiti -Mkongo unatumia saa nne, kilometa 15, niombe Serikalikukarabati barabara hii.

Mheshimiwa Spika, zipo barabara ambazo iwapozitafunguliwa Pwani kutakuwa kuchele kwelikweli. Nikuombebarabara ya Kisiju – Mkuranga; Vikindu – Vianzi; Nyamwage– Utete nimeshaisema; Ikwiriri – Mloka, Mloka – Kisarawe,Mloka – Kisaki, Utete – Ngarambe, Kibiti - Mloka pamoja naBungu – Nyamisati. Barabara hizi zikifunguliwa Pwanitutazalisha na tutailisha nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna bonde kubwa lenye ekarizaidi ya laki tano ambazo hazijalimwa; watalimaje? Kutoamazao kutoka shambani kupeleka sokoni tunatumia saanane au kumi. Niiombe Serikali, kwa kuwa Mheshimiwa Raisamedhamiria kuifungua pwani, tuifungue pwani kwakuboresha miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimkumbushe Mheshimiwa Waziri,katika ukurasa wa 15 amezungumzia barabara ya Chalinze,

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

express way. Mheshimiwa ndugu yangu, MheshimiwaSerukamba, amesema sana, nimuombe Mheshimiwa Waziri…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mchengerwa.Nakushukuru sana kwa mchango wako, umenikumbushambali, kweli nayaelewa maeneo haya.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

Waheshimiwa Wabunge, nikiwa kijana mdogo nikohuko, asubuhi unafungua mlango saa 11.00, 12.00, unakutamama mjamzito amewekwa hapo nje kwa sababu hawanausafiri wamehangaika naye tangu juzi, imeshindikanakujifungua na mimi peke yangu ndio niliyekuwa na Defender.(Makofi/Kicheko)

Kwa hiyo, unachukua watu wako mnaanzakumsafirisha yule mama kutoka Ngarambe kwenda Utete,mnatembea mnachimbua, hiyo gari inakwama kila mahali,mna sepetu, sululu, majembe mpaka mkimfikisha huyu mamabasi Mungu amependa. Kwa hiyo, barabara ya Nyamwagekwenda Utete ukivuka Ikwiriri tu pale inakwenda parallel naMto Rufiji, hiyo kweli ndiyo inang’oa Wabunge. Hii ya Mlokawala huna haja ya kuhangaika nayo maana lazimaitawekwa lami tu kwa sababu ndiyo inayoelekea Stiegler’s,kwa hiyo, tuombe Mungu, yote yanawezekana. (Makofi)

Nilishakutaja Mheshimiwa Charles Mwijage dakikatano, Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu dakika tano.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika,nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia kidogo Wizarahii.

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nikushukuru nakumpongeza Mheshimiwa Waziri na wasaidizi wake. Kipekeeniwapongeze Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenuya Ijumaa na leo.

Mheshimiwa Spika, itoshe mimi leo kuchangiakwamba safari yetu ni kwenda kwenye uchumi wa kati, uliojumuishi na ili kufika hapo lazima tujenge uchumi wa viwanda,siyo viwanda. Kuweza kujenga uchumi wa viwanda ni lazimatuwe na miundombinu wezeshi na saidizi. Kwa hiyo, Wizarahii ndiyo inayojenga miundombinu wezeshi na saidizi.Twaweza tusione leo hayo tunayoyataka lakinitunapokwenda kwenye uchumi wa kati nina imani hayotutayaona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo nalotaka kuzungumzia nibandari. Watu wa bandari, sitazungumzia suala la Bagamoyoila Mheshimiwa Ally Saleh, nikukosoe kidogo au nikupe taarifa,Bagamoyo Special Economic Zone itazalisha viwanda 1,000na watu laki tano watapata ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wa bandari, kuna kiwandacha Hengia cha Tanga kinachotaka kuzalisha tani milionisaba, nawaomba tukubaliane na wazo la kiwanda kile chakupata access. Alipokuja Dangote akazalisha tani milioni tatunchi nzima bei ilishuka, akiingia wa tani milioni saba mamboyatakuwa mazuri. Kama walivyosema wenzangu, twende kasikwenye maamuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wa TPA niwaeleze kuhusu kitukinaitwa Port Community. Tunafanya vizuri sana ndani yabandari lakini wale wanaotusaidia, kwa mfano TRA,TANROADS, hawafanyi kazi vizuri.

Mheshimiwa Spika, nimewaeleza kwa maandishikwamba ya nini kuweka mzani wa TANROADS Kurasini wakatiunaweza kuweka mzani huohuo bandarini na wote wakochini ya Wizara moja? Ndiyo maana kunakuwa na foleni.Niwaombe watu wa bandari tuongeze kasi, tunafanya vizuri.(Makofi)

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Mheshimiwa Spika, napenda nirudie tena; sisi Nacalana Beira si washindani wetu katika bandari, Durban simshindani, tunatengeneza washindani sisi wenyewe. Yaanini kama mtu unatengeneza mke mwenza, unashindwakumhudumia uliyenaye mpaka analazimika kwenda njekutafuta ushindani. Wanaokwenda Beira na Durbanwamelazimika kwenda kule. Tukisawazisha ease of doingbusiness, Nchi za Maziwa Makuu wanapenda kuja hapa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa na rafiki yangu mmojakwenye Serikali ya Kongo iliyomaliza muda, aliniambiawanaweza kutupa robo ya shehena waliyonayo, Bandari yaDar es Salaam haitapokea mzigo wa Tanzania au nchinyingine. Kama walivyozungumza tuitumie njia ya Kigomatuweze kuvuta huu mzigo wa Mashariki ili uweze kuja lakinina Kigoma iweze kuchangamka ili hawa ndugu zanguwaache mambo ya kulalamika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie ATCL, niwashauriwatu wa Wizara hii tafadhali Uwanja wa Ndege wa Bukobauangaliwe. Bukoba tunahitaji uwanja mkubwa, hatuhitajindege nyingi, sisi shida yetu ni kupakia bidhaa za kwendakwenye masoko makubwa. Mkoa wa Kagera unamilikisehemu kubwa ya Ziwa Victoria lakini viwanda vya samakihaviwezi kwenda pale kwa sababu ndege za mizigo haziwezikuja pale Bukoba.

Mheshimiwa Spika, lakini niwapongeze ATCL hapomlipofikia, mnachopaswa kufikia sasa ni kutengeneza sokokubwa, kuchangamsha soko na mimi nawaona Watanzaniawanakwenda kule. Mnakumbuka kuanzia tarehe 19Desemba mpaka Januari Bukoba mlikuwa mnapiga trip mbilikwa siku na ilikuwa inajaa.

Sasa ninachowashauri ATCL, nimekuwa nikiwaambiamuende kwenye utamaduni, mtu akipanda ndegeunamkaribisha kwamba karibu kahawa, unampa kahawa,unampa senene ili watu wapande ndege waweze kuzoeandege. (Makofi)

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

Mheshimiwa Spika, sisi hatufanyi mambo ya profit andloss, hii siyo biashara ya maandazi, wazoeshe Watanzaniandege hata kwa kuwapa free ride, wapande ndege nawazipende ili tutengeneze soko kubwa. Haya mambo yakuongeza destination watu wakishapanda ndegewakazizoea watapanda ndege.

Mheshimiwa Spika, kama alivyozungumzaMheshimiwa Kepteni Abbas, sitaki kuchangia, competitiveadvantage ya Air Tanzania ni soko la ndani.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa muda huo, mengine ntaleta kwa maandishi.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Dkt. MaryNagu, dakika tano.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Spika, bila kupoteza muda, dakika tanoni chache sana, naomba nianze na suala la barabara yaMogitu – Haydom – Sibiti. Mheshimiwa Rais aliahidi kwambaitaiwekwa barabara hii lami kwa sababu tuna Hospitali yaRufaa kule na watu wengi wa maeneo ya Hanang, Mkalamana hata Sibiti yenyewe wanakuja pale Haydom kupatahuduma ya afya.

Mheshimiwa Spika, suala la pili, kuna maeneoambayo wakati mvua ya El-Nino iliponyesha, makorongomakubwa yalitokea na yakitenganisha shule na watoto auzahanati na wagonjwa. Kwa hiyo, naomba wasiiachieHalmashauri tu, Wizara hii ya Ujezi nayo isaidie na namwambiaWaziri kila siku.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, naomba ni-declareinterest kwamba aliyesaini mkataba ule kuhusu Bandari yaBagamoyo ni mimi wakati nikiwa Waziri wa Uwekezaji. Natakaniwaambie tulifanya hivyo kwa sababu ilionekana Afrikanzima Ukanda wa Pwani the best place ya kuweka bandarini Bagamoyo lakini Bagamoyo si bandari tu, Bagamoyo niEconomic Special Zone ambapo kutakuwa na viwanda namiradi mingine mingi ambayo itainua uchumi wa Tanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaomba sana na miminisingesemea, mimi natoka Hanang huko hakuna bandari,lakini naisemea Bagamoyo kwa sababu kwa kweli ni mahaliambapo itasaidia sana na hii SGR itumike vizuri kuletaeconomic change kwenye Tanzania yetu na kwa kwelinaombeni sana muangalie hilo na sisi Wabunge nimeshukurusana Spika mwenyewe alivyosema na sisi wote tuwe pamoja,lakini sidhani kama hii Serikali wala inakataa, ina sababulabda kuchelewesha, lakini wajuwe ya kwamba kwa kwelihapa ni mahali ambapo tukipapuuza tunapuuza kukuzauchumi wa nchi hii ulingane na tunachotaka baadaye.

Mheshimiwa Spika, ya mwisho Rufiji si mahali padogoni mahali pa kubwa, babu yangu mimi alikuwa akipinganasana na wakoloni wakampeleka Rufiji wakamzika hukoalipokufa, sasa na mimi nashindwa kwenda kuona lile kaburila babu yangu, kwa hiyo tumsaidie Mchengerwa na yeyetuone umuhimu wa kuona eneo ambalo ni muhimu sana.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru na ninaunga bajetihii mkono na nina imani na Serikali hii kwamba wala hainashida na Bagamoyo, lakini wataona umuhimu wake na kutoakipaumbele, ahsante sana, sana na Mungu akubariki.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mary Nagu kwakweli ukweli ni huo Bagamoyo is the grand, grand project, sirahisi kupata project kama hiyo kirahisi. Mheshimiwa ElibarikiKingu kwa dakika tano, Mheshimiwa Hawa Ghasia tafadhali.

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa dakika hizo tano, lakini mimipia ninaona tu kwamba ninamshukuru Mungu kwa sababuili la Bagamoyo miongoni mwa nondo ambazo pia ambazonilikuwa nimeziandaa nilikuwa nimejiandaa sana kujakuchangia katika hii project ya Bagamoyo kwanzanikushukuru wewe binafsi kwa uzalendo mkubwa ambaoumeuonyesha kulizungumzia hilo, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, mimi nakumbuka mwaka 2012alipokuja Rais wa China kabla ya hapo Serikali hii ya Chamacha chetu cha Mapinduzi mwaka 2008 ili hire consultantambaye alifanya kazi ya kufanya feasibility study wakaja narecommendation za ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, lakinikama alivyosema mama yangu Nagu kipindi hicho miminilikuwa chini ya Wizara ya Viwanda nilikuwa nikifanya faircompetition, Mama Nagu alikuwa bosi wangu, natakanikuambie kitu kimoja not only kwamba hii Bandari yaBagamoyo tunaizungumza hapa kwamba ilikuwa inamuhimu, lakini ilikuwa inakwenda kuwa the biggest port inAfrica.

Mheshimiwa Spika, namba mbili Bandari hii yaBagamoyo ilikuwa inakwenda kufanya circulation ya kuingizamakontena zaidi ya milioni 22 kwa mwaka ukilinganisha naBandari ya Dar es Salaam, kwa wachumi waliokuwawamefanya feasibility study pamoja na consultant, bandarihii ilikuwa inakwenda kuwa hub ya kuzifungua nchi ambazoni land locked na mradi huu, nataka nikwambie ulikuwaunakwenda kuongezwa, wawekezaji hawa walikuwawanakwenda kujenga Standard Railway Gauge ambayoilikuwa inakwenda ku-connect kutoka Bagamoyo mpakakwenye Reli ya TAZARA.

Mheshimiwa Spika, mimi nataka nikwambie nduguzangu wa Serikali mimi ninawaomba hapa sisi kamaWabunge ni wawakilishi wa wananchi kwa maslahi ya hiliTaifa, hatuwezi tukaja hapa Bungeni tukazungumza kwalengo la kuikwamisha Serikali, nimesoma kitabu hichi,kinachozungumzwa ni kwamba inaonekana kwamba

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

mkandarasi sijui kuna mambo hayako kwa maslahi ya nchi,hatuwezi tukaishia hapo tu, tuangalie vipengele ambavyovinakwamisha tuviondoe, mradi huu ukatekelezwe kwamaslahi ya hili Taifa.

Mheshimiwa Spika, leo Rais tayari Serikali yetu imeanzakujenga Standard Gauge Railway kutoka Morogoro - Dar esSalam kuja Dodoma, kama tutafanikisha mradi huu tayari hiiReli ya Standard Gauge itaweza kupata access ya kuwa fadena mizigo ambayo tutaichukuwa kutoka Bandari yaBagamoyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mimi kwa unyenyekevumkubwa ninaungana na Wabunge wengine kuisisitiza Serikalithis is the grand project kama Spika ulivyosema, tunaishauriSerikali ikakae iangalie wapi tumekwama mradi huu uwezekutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, la pili naomba niende jimboni.Katika jimbo langu la Singida Magharibi na Mheshimiwa Wazirinimeshakuona zaidi ya mara tatu mwaka jana watu wanguwa Kata ya Iyumbu walivamiwa na majambazi saa tisamchana, maduka yakaporwa kila kitu, watu wakakosaaccess ya kufanya mawasiliano hata polisi kuja kuwasaidia,hakuna minara ya mawasiliano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka jana tumeletewa kitabuhapa na hili lazima tuliseme, Serikali Watanzania piawanaona, msiwe manakuja hapa jamani wakati mwinginemnatupiga longolongo tunapata shida huko, tuliletewavitabu hapa vinavyoonesha takwimu za minaraitakayokwenda kujengwa na makampuni ikiwemo TTCL,mpaka leo tunapozungumza, wale wananchi wangu mimikutoka makao makuu ya Wilaya mpaka ufike Kiyumbu ni zaidiya kilometa 190 hawana minara ya mawasiliano, makampuniya private mmeyazuia, sasa tunataka TTCL ikuwe lakini it mustbe competitive ili tuweze kuwasaidia watu wetu.

Mheshimiwa Spika, la pili kwenye kitabu nimeangaliabarabara inayojengwa kutoka Sepuka - Mlandala kwenda

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Mgugila, ninaomba nimalizie hili kwa uchache sana,barabara hii nimeanza kuiona toka nikiwa Mkuu wa Wilayaya Igunga mwaka 2012/2013; imejengwa madarajayasiyopungua 40, ni mwaka wa kumi hii barabara Serikaliwameshindwa kuipandisha/kuijengea tuta la moramu, leonaangalia kwenye kitabu imeombewa milioni 90.

Mheshimiwa Spika, mimi naiomba Serikali wananchihawa wa Iyumbu, Mheshimiwa Waziri nimeshakufuata zaidiya mara mbili.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ikungi asilimia 90 yarevenue inapata revenue kutokana na wakulima wanaotokakwenye Jimbo langu Singida Magharibi kwa sababutunazalisha mpunga na mchele kwa kiwango kikubwa, lakiniwananchi hawa tumeshindwa kuwakamilishia ujenzi wa hiibarabara for ten years madaraja yamejengwa. Mimi nasemasafari hii sitaingua mkono bajeti ya Wizara hii kama sita patamajibu ya ujenzi wa barabara ya watu wangu kwa sababuwatu hawa wamekuwa wakipata shida, nimekwendapersonal kulizungumza nimefanya njuhudi na sijapata majibuyoyote nashukuru sana.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Kingu, ahsantesana, nakushukuru sana na mimi sikusema yote kuhusu Chinamerchants, lakini tutaendelea kuwasiliana na MheshimiwaWaziri na na kadhalika, hilo likampuni kwanza ni likampuni laSerikali wala siyo private company sorry to say, ni Serikali yaChina inaunda mashirika na hili ni shirika mojawapo na zilebandari kubwa tatu duniani ambazo zote ziko, China wananne; tatu Mainland China na Hongkong; hizi tatu hizi ni ChinaMerchants plus the other zinazoendelea.

Kwa hiyo, kupata uwekezaji wa bandari wa trilioni 23iko maneno, hapa negotiation team yetu inabidi kwa kwelikama watakuwa hawa hawa kwenye miradi mingine haya.Mama Hawa Ghasia please atafuatiwa na MheshimiwaVenance Mwamoto, Mheshimiwa Engineer Christopher Chizaajiandae.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana na mimi nashukuru.

SPIKA: Dakika tano tano.

MHE. HAWA A. GHASIA: ...kwa kunipa dakika tanonitajaribukukimbia kimbia.

Mheshimiwa Spika, ahsante niipongeze Wizara kwakazi kubwa wanaoifanya katika kuhakikisha kwambamiundombinu ya nchi yetu inaboreshwa.

Mheshimiwa Spika, naomba nianzie jimboni kwanguambako kwanza ningependa suala la barabara ya Mtwara- Msimbati - Madimba - Kilambo ambazo ni barabarazinazounganisha nchi yaani Tanzania na Mozambiqueambayo ni sera yetu kuhakikisha kwamba barabarazinazounganisha nchi zinajengwa kwa kiwango cha lami,Mheshimiwa Waziri naomba utakapokuja kunijibu basiuniambie imefikia wapi suala la kujenga barabara ya Mtwara- Msimbati - Madimba - Kilambo kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, pia kuna suala la barabara yakutoka Hiari -Nanguruwe ambayo ni mchepuko, sasa hivikutokana na kiwanda cha saruji ambacho ni kikubwa sanamagari yote yanayokwenda Newala hayapiti tena Mtwarayanatumia barabara hii tumeiomba Serikali, nimekuja kwakoMheshimiwa Waziri nimezungumza na Meneja wa TANROADSkuomba barabara hii ichukuliwe na Wizara kwa sababuinapitisha malori makubwa ambapo TARURA peke yakehawawezi kuijenga barabara hii ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, katika Halmashauri yangu tulikuwatunajenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kivukonipale Msemo kwenda Msanga Mkuu, lakini barabara hiiimekuwa na changamoto kubwa sana watu wa bandari waMtwara hawataki barabara ipite katika maeneo yao, sasamaeneo yote hata Dar es Salaam kuna barabara ambazozinapita ndani ya eneo ya bandari na kule Msanga Mkuu ni

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

lazima upite katika bandari ndipo uweze kufika katika vijijivyetu.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziriaingilie kati kwa sababu barabara hii ilikuwa inajengwa sasahivi imesimama kwa eti tu kwamba hatuwezi kujengabarabara ya lami kupita eneo la bandari eneo ambalo hatakuendelezwa bado alijaendelezwa. Kwa hiyo, MheshimiwaWaziri naomba uingilie kati suala hilo.

Mheshimiwa Spika, tunayo barabara yetu ya kutokaMpapura kwenda Kitere mpaka Mkwichi kule Mtama,naomba hii barabara inaunganisha mikoa, Mkoa wa Lindina Mkoa wa Mtwara kama kawaida tunaomba barabarahii ijengwe kwa kiwango cha lami kwa sababu ndiyo serakuziunganisha kwa kiwango cha lami barabara zote ambazozinaunganisha mikoa.

Mheshimiwa Spika, na mimi niungane na wenzangukuzungumzia suala la Bandari ya Bagamoyo, hata wenzetuChina walivyotaka kuendeleza nchi yao, walivyotakakuanzisha maeneo ya special economic zone walianzia naChina ya Mashariki ambako ndiko ambako wanapakanana bahari. Sasa kuanzia Djibouti mpaka tunafika kule SouthAfrica, sisi hapa tulikuwa na nafasi kubwa sana ya kuwa nabandari kubwa ambayo itachukuwa meli za four generationambazo zingeweza kuleta mizigo baada ya kufika pale ilemizigo sasa ndiyo ikawa inaenda kwenye bandari zingine zaBeira, Mombasa, Dar es Salaam na maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali yetu suala hiliwaliangalie kwa mtizamo mpana zaidi na hasa wakisikilizana Wabunge michango yao pamoja na mchango wako.

Mheshimiwa Spika, na suala la mwisho ni suala la Relikutoka Mtwara kwenda Mbambabay na matawi la kwendaLiganga na Mchuchuma. Tunategemea kuchimba chuma,kuchimba makaa ya mawe na alivyokuja Waziri wa Ujenzialisema kuna tender ya kupeleka...

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Hawa Ghasia.Nil ishakutaja Mheshimiwa Venance Mwamoto naMheshimiwa Christopher Chiza ajiandae, Mheshimiwa NuruBafadhili, kwa dakika tano tano.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa niunge mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, ndoto ya uchumi na viwandahaitawezekana bila kuwa na barabara, reli, mawasiliano,bandari na viwanja vya ndege na ndege zenyewe. Kwa hiyomimi nishukuru, Mheshimiwa Waziri ujue kwambaunadhamana kubwa ya kututoa tulipo ya kutupeleka kwenyenchi ya uchumi ya viwanda, kama hutofanya vizuri kwenyeWizara hii/hamtofanya vizuri mjue kwenye hiyo ndoto yakwenda kwenye uchumi wa viwanda itakuwa haiwezekani,kwahiyo mnatakiwa mfanye kazi kwa nguvu zote.

Mheshimiwa Spika, mimi niwapongeze baadhi yasekta ambazo zimekuwa zikifanya vizuri, lakini sitakikuchukuwa muda mwingi kuchanganua hii kwa sababumuda niliopewa ni mdogo.

Mheshimiwa Spika, nirudi j imboni kwangu,ninapozungumza sasa hivi mvua zinanyesha, barabara zotezote zinakufa. Kwa hiyo, mimi niombe kitu kimoja kwambakwa kuwa tunakubali na tumepitisha Sheria ya TAKUKURUwenyewe, sasa basi tuangalie uwezekano wa kutusaidia,kuna maeneo, kuna Wilaya na Mikoa ambayo ni ya kiuchumi,mikoa ambayo inachangia pato la Taifa kwenye nchimojawapo ikiwa ni Kilolo.

Mimi nishukuru sana Mheshimiwa Rais alifika Kilolomwaka jana, akaahidi kutujengea barabara na ninashukuruMheshimiwa Kamwelwe tumekuwa tukiongea kila siku naumenihakikishia kwamba barabara hiyo itajengwa ya kuanziaIringa Mjini kwenda Kilolo na bahati nzuri kwa heshima yapekee tumeipa jina la Engineer Mfugale kama vile ambavyo

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Mheshimiwa Rais ametoa daraja na sisi tumempa heshimandugu yetu Mfugale kwanza anatoka Kilolo, lakini pia huwezikuwa daraja bila kuwa na barabara, kwa hiyo, tumempa nabarabara, kwa hiyo najua itajengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo na MheshimiwaKamwelwe pia kuna barabara tunategemea kukupa, kwahiyo na wewe umeolea kule Iringa, kwa hiyo kwa heshimaya pekee lazima uhakikishe kwamba barabara ya Kilolozinapatikana.

Mheshimiwa Spika, barabara za kiuchumi ni pamojana Kongwa. Kongwa ni sehemu ambayo tumesematutaweka maazimisho yote kule, kwa hiyo lazima ijengwekama vile itajengwa Kilolo, kwa hiyo, nikuombe Mheshimiwaile ahadi ya Rais usimwangushe na barabara ambazo nibarabara ya Mkoa kutoka Iringa - Dabaga - Edeteinaunganika na barabara ya kwenda Mlimba; kwa kuwabarabara ile mmeipeleka TARURA, lakini TARURA awanafedha naomba hiyo barabara muikamilishe wenyewe kwasababu Wilaya ya Kilolo kama nilivyosema safari hii kitaifakuchangia pato tumekuwa watu wanne na kutokana nakuchangia vizuri tumeinua Mkoa wa Iringa umekuwa Mkoawa kwanza kuchangia pato la Taifa na Mkoa wa piliumekuwa Geita, kwa hiyo niombe msituangushe.

Mheshimiwa Spika, kuna barabara ya kuanzia Kitoo -Pomerini - Kihesa - Mgagao - Mwatasi sasa hivi haipitika, miminikuombe Mheshimiwa jungu kuu halikosi ukoko, toa fedhahizo za tahadhari au za emergence ziweze kwendakuwasaidia wananchi kule wanapata taabu. Wilaya ya Kilolondiko ambako nguzo za barabarani za umeme zinatoka,Wilaya ya Kilolo ndiko mbao nyingi zinatoka sasa hivizinazojenga Makao Makuu, Wilaya ya Kilolo ndiko ambakotunazalisha pareto kwa wingi, inakuwaje mnaisahau?

Mheshimiwa Spika, mimi niombe mfanye kila jitihadaili zile barabara zijengwe na niombe pia barabara ile ambayoinaunganisha kama nilivyosema mkoa kwa mkoa na ikokwenye ilani ijengwe, na nimshukuru sana Engineer wa Mkoa

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Bwana Kindole ni mtu ambaye anatupa ushirikiano mzuri, kwahiyo nishukuru sana.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna barabara yaBusega - Nyasuga - Ngasamo kwa ndugu yangu Chegeni,mimi naomba mumsaidie kwa sababu huyu ni mkongwemwenzangu, tulitoka kwa ajili ya kukosa hizo barabara, sasammetupa matumaini tumerudi, sasa msituondoe tena kwasababu bado tunapenda kuwatumikia Watanzania nawananchi wa majimbo yetu, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mwamoto sijuibarabara ya Busega itasafirisha nini maana hawana kituhawa jamaa. (Kicheko)

Hawa Wanyantuzu watasafirisha nini hawa! Ahsantesana bado natafakari mchango wa Mheshimiwa CharlesMwijage bado ndiyo unaongoza hapa anasema kunabaadhi ya matendo mtu ukiyafanya ni kama unatengenezamke mweza wewe mwenyewe. Nikawa nafikiria hivi kuna mtuanaweza kutengeneza mke mwenza yeye mwenyewekabisa kwa kukusudia. (Kicheko)

Mheshimiwa Nuru Bafadhili, Mheshimiwa EngineerChiza jiandae kwa dakika tano, tano.

MHE. NURU A. BAFADHILI: Mheshimiwa Spika, ahsantesana na napenda kuzungumzia kuhusu ujenzi wa barabarakama Serikali ilivyosema kupunguza msongamano katika jijila Dar es Salaam nimejaribu kujenga barabara, lakini sasabarabara hizo ambazo zinatokea Ardhi - Makongo - Goba,mpaka kufika Kimara na Mbezi kwa kweli kwenye kitabuimeeleza kwamba barabara ya kutoka Ardhi mpakaMakongo tayari imeshakamilika kwa kiwango cha lami.Napenda kuiarifu Serikali kwamba barabara hii badohaijakamilika kwa kiwango cha lami, bado barabara hii nichangarawe kutoka Ardhi hadi Makongo, kwa hiyo naiombaSerikali ihakikishe hizi kilometa nne zinazotoka Ardhi mpakaMakongo zijengwe katika kiwango cha lami ili kupunguzamsongamano kwa sababu eneo la kutoka Ardhi mpaka

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Makongo kuna kuwa na msongamano na magari kutokanana mashimo mashimo.

Mheshimiwa Spika, nikizungumzia kuhusu barabara yaTanga - Pangani, Tanga - Pangani siku zote tunaambiwaitajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hapa sioni, sasa hivininaona kwenye kitabu imeandikwa kwamba tutajengwakiwango cha changarawe kuanzia Mabanda ya Papa hadiBoza Buyuni, sasa Mabanda ya Papa pale ni katikati ya jijipale, kuna lami mpaka sehemu ya Mwang’ombe ambayoni kilometa nne kutoka Mabanda ya Papa, kwa hiyo, palepana lami, changarawe inaanzia pale Mabanda ya Papampaka inafika huko Boza Buyuni. Sasa Serikali iangalieuwezekano wa kuifanya barabara ile iwe katika kiwango chalami.

Mheshimiwa Mwenykiti, na kwa taarifa yenu nikwamba sasa hivi mvua zinazonyesha barabara kutokaPangani mpaka Tanga haipitiki tena, inabidi sasa hivi wapitieeneo jingine linaloitwa Tongoni, wapiti Tongoni waendeLumbwa waingie Kisima Tui - Pongwe ndiyo warudi tenaTanga kwa sababu kuna daraja linaitwa Neema limearibika,gari haziwezi kupita.

Kwa hiyo, tunaiomba Serikali iangalie uwezekano wahizi barabara ikamilike kwa kiwango cha lami badala yakutengeneza tena changarawe maana yake hapainaonesha kuwa barabara itawekwa changarawe kuanziaMabanda Papa hadi Buyuni Boza.

Mheshimiwa Spika, vilevile napenda kuzungumziakuhusu mabasi haya ya mwendokasi. Mabasi ya mwendokasiyametusaidia sana lakini yard ya mwendokasi kwa kweliinasikitisha. Imejengwa mahali ambapo mvua zikinyeshapanajaa maji kiasi cha kuharibu miundombinu yote. Kwa hiyo,Serikali iangalie uwezekano wa kujenga tena upya nakufanya drainage system ili maji yaweze kupita chini na ileyard ikaweza kutumika au vinginevyo ile yard ya mwendokasiihamishwe pale iwekwe mahali pengine, kwa sababu maji

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

pale jangwani yanajaa kiasi cha kuyafanya mabasi tenahayafanyi kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikizungumzia kuhusu reli ya Tangahadi Arusha, kwa kweli reli hiyo imeshaanzwa kutengenezwaTanga hadi Same. Cha kusikitisha ile reli pia inatakiwaifanyiwe usafi. Kwa sababu kuna nyasi zimeota. Sasa mtumwingine anaweza kung’oa reli, bila mtu kujua reli paleimeng’olewa. Kwa hiyo, Serikali ihakikishe kwamba maeneoyale ambayo tayari yameshatengenezwa na ile reli vile vileinakuwa safi, inalimiwa vizuri ili kama kutakuwa na uharibifuwowote utakaotokea inaweza ikajua.

Mheshimiwa Spika, mwisho, napenda kuzungumziakuhusu viwanja vya ndege. Kwa kweli Serikali inajitahidikujenga viwanja mbalimbali vya ndege lakini tatizo linakuja,kuna baadhi ya viwanja vya ndege vinakosa taa nakusababisha usiku ndege haziwezi kutua. Kwa hiyo,tunaiomba Serikali katika viwanja vyote vile ambavyo havinataa za ndege ihakikishe taa zinawekwa ili kuwezesha ndegekutua wakati wa usiku.

Mheshimiwa Spika, mwisho...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Nuru. Ahsante sana.Mheshimiwa Engineer Chiza, dakika tano.

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa nafasi hii. Nitaongelea mambo mawili tu.Kwanza nampongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri naviongozi wote wa Wizara hiyo kwa kuleta hotuba nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, nataka niongelee mambo mawilitu; moja ni Mfuko wa Barabara; la pili ni kasi ya ujenzi wabarabara za lami hususan katika Mkoa wa Kigoma.

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Mheshimiwa Spika, kabla hatujaingia kwenye uchumiwa kati na uchumi wa viwanda bado Watanzaniatunategemea kilimo na tutaendelea kutegemea kilimo kamandiyo mhimili wa uchumi wetu. Wataalam wanasema asilimia60 ya upotevu wa mazao hutokea katika level ile yapostharvest, yaani miundombinu hafifu ya kuhifadhi mazao,lakini pia miundombinu hafifu ya kusafirisha mazao kutokashambani kwenda sokoni (farm to market roads). Hapa ndiponinapotaka kusisitiza umuhimu wa Mfuko huu wa Barabara.Nikitazama kwa mfano mkoa wangu wa Kigoma wote kwapamoja tumetengewa shlingi milioni 694 ndizo ninazozionakwenye kitabu hiki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, barabara hizi ambazo ndizozinatarajiwa zinategemewa na wakulima watoe mazao yaowasafirishe sasa waje kwenye truck road tunazojinga,kupeleka sokoni, bado bado sana. Kwa kweli tunahitaji mfukohuu upate pesa, TARURA wapate pesa tuwajengee wakulimamiundombinu ya barabara waweze kutoa mazao yaokwenda shambani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niunganishe hapa hapakwamba katika Jimbo langu kule tumejenga soko la kisasa,la Kimataifa katika Kijij i cha Muhange, soko ambalolitatufanya sisi tuunganishe tufanye biashara na wenzetu waBurundi. Soko hili ili liweze kufanya kazi vizuri sasa, ni muhimubarabara ile inayojengwa kutoka Nyakanazi kwenda mpakaKigoma ipate barabara ya kiungo kutoka Kakonko kupitaKinonko, kwenda Gwarama, kwenda mpaka Muhangesokoni ili sasa wananchi wetu waweze kufanya biashara nandugu zao wa Burundi kwa kutumia barabara nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakwenda haraka kidogo.Miundombinu hii tunayoijenga sisi watu tunaotoka Kigoma;kuufungua Mkoa wa Kigoma tunahitaji sasa miundombinuhii ijengwe kwa kasi kubwa ili mkoa huu uweze kuwa hub yabiashara hususan katika baadhi ya nchi za maziwa makuu.Tatizo tulilonalo kama nilivyosema awali ni usimamizi auucheleweshaji wa ujenzi wa barabara hizi.

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Nyakanazi,mpaka Kabingo pale kij i j ini kwangu mpaka hivitunavyozungumza tangu mwaka 2014 ni asilimia 60 tuambazo zimetekelezwa tangu 2014. Tumeikagua tukiwa naMheshimiwa Waziri Mkuu tukakuta hata Mkandarasimwenyewe yuko nje ya mkataba (out of contract) kwa siku986. Naiomba Wizara isimamie kwa karibu Mkandarasianayejenga barabara hii Nyakanazi mpaka pale Kabingo iliaweze kuongeza kasi ya utekelezaji. 2014 - 2019 asilimia 60,kwa kweli tunaendelea kuchelewa sana.

Mheshimiwa Spika, naomba tu nimalizie kwakuishukuru Serikali. Nimeona katika kitabu sasa, mmesemakutoka Kabingo kwenda Kasulu kwenda Kibondo Kasulu hadiManyovu, Benki ya Maendeleo ya Afrika imetutengea shilingibilioni 15 ili tuweze kujenga kilomita hizi 260 za barabara hii.Huu ndiyo mwendo ambao kwa kweli kama tutatekeleza, hiiitapelekea kufungua…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Wa kutufungia mjadala wetuawe ni Mheshimiwa Engineer Edwin Ngonyani ndio atakuwamchangiaji wa mwisho. Mheshimiwa Ngonyani ndio atakuwamchangiaji wa mwisho. Kama hayupo nimtaje mwingine.Karibu Engineer, ooh nimekuona.

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa fursa. Kwa kweli nichukue fursahii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa hii ya kuwahai na kuchangia leo hii. Kwa sababu muda ni mfupi, naombasana nianze na suala moja la taasisi mbili za TARURA naTANROADS. Kwa hivi sasa kwa mfumo tulionao, TARURA ikochini ya TAMISEMI na TANROADS iko chini ya Wizara hiitunayoiongelea leo.

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

Mheshimiwa Spika, hawa wote wanapata fedhakutoka Mfuko wa Barabara unaosimamiwa na Bodi ambapomgawanyo wake TANROADS wanapata asilimia 62.46,TARURA wanapata asilimia 26.77, Ujenzi wanapata asilimia6.94, TAMISEMI wanapata asilimia 2.97 na mfuko wenyewewa barabara kwa maana ya taasisi inayosimamia inapataasilimia 0.86.

Mheshimiwa Spika, wajibu wa road fundboard nipamoja na kusimamia au kufuatilia utekelezaji au matumiziya fedha zinazokwenda katika taasisi ya TARURA, Ujenzi naTANROADS. Wakati huo huo TAMISEMI wanapata hiyo asilimia2.97 kwa ajili ya ufuatiliaji wa miradi hiyo hiyo na Ujenziwanapata asilimia 6.94 kwa ajili ya ufuatiliaji wa ujenzi wabarabara hizo hizo.

Mheshimiwa Spika, kwa maana nyingine Ujenzi,TAMISEMI na mfuko wa barabara wote wanasimamiabarabara zinazoshughulikiwa na TANROADS na TARURA.Naomba, ni mawazo yangu kwamba TANROADS na TARURAwawe chini ya Wizara moja na kwa sababu Wizarainayohusika na barabara ni Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasil iano, basi ningependa TARURA maadamimeshaundwa chombo kinachojitegemea, basi sasaisimamiwe na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilianobadala ya TAMISEMI. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii haina maana kwamba D by Ditakuwa imekufa, hapana. Bado watu wa TAMISEMI suala laeyes on, hands off litabakia pale pale, linaendelea. Ni kamailivyo katika barabara za TANROADS, nazo zinasimamiwa naTAMISEMI hata kama hawapati fedha na wala hawawajibiki,kuisimamia lakini wana eyes on katika shughuli zotezinazofanywa na TANROADS. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba vilevile eyes oniendelee na watu wa TAMISEMI kwa maana ya Wizaranipamoja na mkoani katika barabara za TANROADSwanavyofanya sasa na wafanye sasa na TARURA, lakini sualala usimamizi lirudishwe liwe chini ya Wizara moja, chini ya

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

Waziri mmoja ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano. Hii itasaidia mambo mengi. Kwanza hizi helazote za usimamizi asilimia 6.94, 2.97 na 0.86 zote zitaunganazitafanya kazi kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, halafu na mgawanyo wa bajetihiyo suala la asilimia 70 kwa 30 halitakuwa na mvutano tenana wala hatutakuwa na mvutano tena wa kusemakupandisha barabara hadhi lakini sababu tu ni kutaka hizobarabara zishughulikiwe na TANROADS. Mvutano huohautakuwa tena kama taasisi zote hizo mbili zitasimamiwana Wizara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuliongea hilo, naombatena upande wa mawasiliano TTCL, Mkongo wa Taifa, Tumeya TEHAMA, pamoja na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.Taasisi hizi nimeangalia kwenye vitabu vya Mheshimiwa Waziri,sijaona kama amezipa mtaji wowote. Tatizo la taasisi hizo nimtaji. mimi nina uhakika taasisi hizi zina wataalam wa kutosha,lakini hawafanyi kazi yoyote kwa sababu hawana mtaji.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimeona katika bajeti yaMheshimiwa Waziri, ni vizuri kutoa zile trilioni kwa upande wauchukuzi pamoja na ujenzi lakini upande wa mawasilianohajapewa fedha ya kutosha au hajaomba fedha ya kutosha.Ni fedha ndogo sana na kwa hiyo, haiwezi kufanya kazikubwa inayotakiwa katika kutuimarishia mawasiliano natunashida kubwa katika uimarishaji wa mawasiliano pandezote; mawasiliano ya simu pamoja na data. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sana taasisi hizo zipatefedha za kutosha, zipate mtaji ili ziweze kujiendesha nakushindana na taasisi nyingine.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Naunga mkono hoja kwa asilimia miamoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Nakushukuru sana.

Waheshimiwa Wabunge, tumejitahidi mno kujaribu ku-accommodate, lakini bado wengi hamkupata nafasi,tusameheane sana, wakati mwingine. Natumainimmechangia kwa maandishi, ilikuwa siyo rahisi kwamba kilamtu aweze kupata nafasi kwenye Wizara hii muhimu, lakiniwengi mmeweza kuongea. Tumejitahidi mpaka asilimia tisinina kitu hivi, katika waliojiandikisha mmepata nafasi. Kwa hiyo,kwa maana ya Serikali kupata ushauri, kwa kweli wamepataushauri wa kutosha kabisa.

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. ENG. GERSON H. LWENGE: Mheshimiwa Spika,awali ya yote, naunga mkono hoja ya Waziri na nampongezasana Waziri, Naibu Mawaziri na vviongozi wote wa Wizara hiikwa hotuba yenye kuleta mabadiliko makubwa katikakujenga miundombinu itakayotufikisha kwenye uchumi wakati.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizi, naombaWaziri arejee kwenye barabara ya Njombe (Ramadhani) –Igwachanya – Iyayi ambayo ni barabara muhimu kwaniinaunganisha Makao Makuu ya Mkoa na Makao Makuu yaWilaya ya Waging’ombe (Igwachanya). Pia inapita maeneomuhimu ya utalii ya msitu wa asili wa Nyumbanintu na Hifadhiya Pori la Akiba la Mpanga/Kipangele pale Ludunga nakuunganisha na TANZAM Highway pale Igando. Barabara hiiilishafanyiwa upembuzi na usanifu wa kina toka mwaka 2014ilipokamilika na ipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015.

Mheshimiwa Spika, naomba pia Wizara ioneuwezekano wa kuongeza kiwango cha lami paleIgwachanya ambapo ni Makao Makuu ya Wilaya. Nimeonaimepangwa kujengwa mita 100 tu kwa bajeti hii 2019/20.

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Kumleta mkandarasi kuja kujenga mita 100 itagharimu pesakubwa kwani kuleta mitambo ya kujenga mita 100 hainatofauti na ile ya kujenga kilomita 5. Naomba tupate angalaukilomita 2.

Mheshimiwa Spika, sijaona mpango mahsusi nakuboresha Uwanja wa Ndege wa Njombe. Mkoa wa Njombeunahitaji kupata uwanja mkubwa wa ndege. Huu ulipo nimdogo na pengine itakuwa vigumu kuupanua kwa kiwangokikubwa.

Mheshimiwa Spika, nashauri toka bajeti ya 2018/2019kuwa Wizara ijaribu kwenda pale Ilembula Hospitali tunaouwanja wa ndege na ardhi ya kutosha ambapo ingewezakujenga uwanja mkubwa wa ndege kwa kiwango chauwanja wa ndege wa mkoa. Hakutakuwa na gharamakubwa ya fidia kama kupanua ule Uwanja wa Njombe Mjiniambapo majengo mengi ya kudumu yamejengwa.

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika,Mji wa Geita ulipewa ahadi na Mheshimiwa Rais kujengewakilomita 10 za lami. Mwaka jana nilipoongea na Waziri aliahidikuziweka kwenye bajeti ya mwaka huu wa 2019/2020.Nimeangalia kwenye kitabu lakini hakuna barabara zangu.Namwomba sana Mheshimiwa Waziri anionee huruma hii niahadi ya Rais ambayo kwa miaka yote minne imekuwainaonyeshwa kwenye vitabu lakini barabara hazijengwi. Kwaheshima kubwa, naomba jambo hili Waziri alipe umuhimuwake.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. ALLY S. UNGANDO: Mheshimiwa Spika, naombakuchangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawawiliano.

Mheshimiwa Spika, kwanza, nashukuru kwa ujenzi waGati la Nyamisati lililogharimu shilingi bilioni 14 na kazi inaendavizuri sana. Nina kila sababu ya kujivunia Serikali yangu yaAwamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Pombe Joseph Magufuli kwa kazi yake nzuri. Kweli huyu nimzalendo namba moja kwa kujali wananchi wa hali ya chini,wanyonge, kwani gati hili likikamilika litatua changamoto zausafiri kwa wananchi wa Wilaya ya Mafia na Kibiti.

Mheshimiwa Spika, lakini kila penye mafanikiohapakosi kuwa na changamoto. Barabara yetu ya Bungu-Nyamisati, naomba ijengwe kwa kiwango cha lami kwanikipindi cha mvua huwa haipitiki kabisa kwa hiyo huwaleteausumbufu wananchi hasa wa Wilaya ya Mafia na Kibiti.Naiomba Serikali yangu sikivu ituangalie kwa jicho la huruma.Vilevile, barabara ya kutoka Muhoro - Mbwera nayo ifanyiweukarabati wa kiwango cha changarawe kwani ina manufaamakubwa ukizingatia sasa kuna ujenzi mkubwa wa Kituo chaAfya-Mbwera.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Kibiti lina jumla ya kata16, vijiji 58 na vitongoji 272. Kati ya hivyo, baadhi yake vipokwenye visima/delta au pembezoni mwa Bahari ya Hindiambavyo vina jumla ya kata 5, vijiji 17 na vitongoji 42. Mojaya changamoto ya maeneo hayo ni kutokufikika kwa urahisi,miundombinu yake ya barabara siyo mzuri kabisa kamamaeneo ya Kata za Msala, Mbuchi, Kiongoroni, Salale naMaparoni. Naiomba Serikali yangu sikivu ya Chama chaMapinduzi (CCM) ituangalie kwa jicho la pekee ili tupatemagati madogo madogo sambamba na barabara zake ilikufikike kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya jambo lenyemanufaa kwa wananchi waishio vijijini kwa kuunda chomboambacho kinakwenda kutatua kero za wananchi waishiovijijini cha TARURA. Naomba sasa chombo hiki kiongezewenguvu za kifedha na ikama ya watumishi ili wakatekelezewajibu wao bila ya kupata kikwazo cha aina yoyotesambamba na kuongezewa vitendea kazi kama magari namaboti ya kuendea site.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali yangu sikivuituongezee fedha katika Jimbo langu la Kibiti ili tuwezekukamilisha baadhi ya barabara zetu za lami kama kutoka

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

Kibiti kwenda Makao Makuu ya Wilaya. Kazi imeshaanza lakiniinasuasua kutokana na uhaba wa fedha.

Mheshimiwa Spika, naomba barabara za mitaazichongwe ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa mifereji. Mfanobarabara ya Kibiti Mjini, Bungu Mjini, Jaribu Mpakani Mjini,Nyamisati Mjini, barabara hizi za mitaa miundombinu yakesiyo rafiki kupitika wakati wote na ukizingatia miji hii inakuakwa kasi na ina wakazi wengi sana. Barabara ya kwendaMakima ambayo ina jumla ya kilomita 32 tayari kilomita 17zimeshachongwa bado kilomita 15. Tunaomba chombochetu cha TARURA kipewa fedha za kutosha ili kutatuachangamoto hizo.

Mheshimiwa Spika, yapo maeneo yenye mitoambayo kipindi cha mvua huwa hayapitiki kwa urahisi.Maeneo hayo ni kama Kibanga Hodi, Mkelele Mkumbwa,Kipoka, Nyafeda na Daraja la Mbwera Mjini. Naombamaeneo haya yaangaliwe kwa jicho la pekee.

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu la Kibiti hadileo kuna maeneo hayana mawasiliano ambapo ni jumla yavij i j i 24 kwenye maeneo ya nchi kavu. Vij i j i hivyo niNyambunda, Nyambili, Majawa, Nyamatanga, Mchukwi A&B,Ngondae, Machepe, Nyamwimbe, Nyakinyo, Tomoni,Kingunguri, Mkenda, Kivinja A&B, Msindaji, Muyuyu, Ruaruke,Mbawa na Kilolatambwe. Kwenye visiwa (Delta – Rufiji) vijijiambavyo havina mawasiliano ya simu ni Kiomboni, Mfisini,Salale, Mchinga, Ruma, Kiomboni, Pombwe, Jafa, Mbuchi,Mbwera Magharibi na Mbwera Mashariki, Maparoni, Kechulu,Msala, Tuwasalie na Kiasi. Upatikanaji wa mawasilianoutaongeza kipato kwa wanafamilia, kutoa taarifa kwa harakapindi majanga yanapotokea kama ya wahalifu na mauajiya watu wasiojulikana.

MHE. OMARI A. KIGODA: Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa niipongeze Wizara na Mawaziri wake kwa kazi bora.

Mheshimiwa Spika, kipande kilichobaki cha Mziha -Handeni kwenye majibu ya Waziri kilitengewa shilingi bilioni

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

2, katika kitabu cha hotuba ya Waziri ukurasa wa 29-30ameeleza Serikali bado inatafuta hela. Naomba kwenyemajumuisho nipate ufafanuzi wa suala hili hasa akizingatiawananchi wa Handeni na Tanga kwa ujumla wamepatafaraja baada ya kusikia imeshatengwa shilingi bilioni 2kutokana na majibu ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, barabara nyingine yenyeumuhimu mkubwa ni ile ya Handeni – Kiberashi. Hii barabarandiyo litakapopita bomba la mafuta. Naomba ufafanuzi waSerikali kuhusu barabara hii kujengwa kwa kiwango cha lamihata tukianza kwa vipande vipande itasaidia.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaSpika, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwakuniwezesha kuchangia kwa maandishi hotuba ya bajeti yaWizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi kwa MheshimiwaRais kwa ununuzi wa ndege sita, ujenzi wa reli ya mwendokasi na mambo mengi sana ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia kuhusubarabara ya Bigwa – Mvuha – Kisaki (Morogoro Vijijini) kwakiwango cha lami. Wabunge wa Morogoro tumekuwatunachangia mara kwa mara na kuambiwa kuwaitatengenezwa lakini kwenye hotuba ya Mheshimiwa Wazirisikuweza kuiona kama kweli imetengewa fedha. NaombaMheshimiwa Waziri atueleze wananchi wa Morogoro Vijijinini lini barabara hii ya Bigwa – Mvuha - Kisaki itajengwa kwakiwango cha lami na ikakamilika?

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi kwa kutengewafedha kiasi cha shilingi milioni 2,020.00 kwa ajili ya kuendeleana ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Dumila – Kilosa– Mikumi sehemu ya Rudewa – Kilosa (km 24). Barabara hiinimekuwa nikiizungumzia mara kwa mara na hasa kipandecha Kilosa – Mikumi. Kipande hiki wakati wa mvua kinakuwa

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

kibaya sana na kupitika kwa shida. Maelezo ya mara kwamara ni kuwa wafadhili hawajapatikana. Je, ni lini kipandehiki kitatengewa fedha na Serikali au kitapata wafadhili kwaujenzi wa kiwango cha lami?

Mheshimiwa Spika, napongeza kwa fedhazilizotengwa shilingi 12,135.00 kwa ajili ya kuendelea na ujenziwa sehemu ya Kidatu-Ifakara (Barabara ya Kidatu – Ifakara– Lupilo – Malinyi – Londo – Lumecha – Songea). Nashaurifedha zilizotengwa 2019/2020 zitolewe zote na kwa wakatikwani mpaka sasa ujenzi huu unafanyika polepole auunasuasua.

Mheshimiwa Spika, Serikali chini ya Mheshimiwa Raiswa Awamu ya Tano, imefanya mambo mengi mazuri. Hatahivyo, nakumbushia barabara muhimu sana ya Lupiro –Mahenge – Mwaya kwa ujenzi wa kiwango cha lami. Kwenyehotuba hii sijaona kuwa barabara hii imetengewa fedha.Barabara hii nimekuwa nikiisemea pamoja na Mbunge waJimbo la Ulanga kwani kuna faida zinazopatikana Ulangakama madini, utalii pamoja na mazao mbalimbali kamampunga. Naomba maelezo ni lini barabara hii itaanzakuongelewa, kutengewa na kupatiwa fedha na ujenzi walami kuanza?

Mheshimiwa Spika, barabara ya Magole – Turiani –Mziha – Handeni. Nianze kwa kutoa pongezi kwa barabarahii, ujenzi wake unaenda vizuri na wananchi wa Wilaya yaMvomero wanaipenda na kuishukuru Serikali yetuinayoongozwa na Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, nashukuru Serikali kwani mradi huuumetengewa shiling milioni 1,170.00 katika mwaka wa fedha2019/2020 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya barabara yaTuriani – Mziha – Handeni (km104). Naamini kuna wakatibarabara hii itakamilika na wananchi wa Mvomero naHandeni watafurahi zaidi kwani miundombinu itakuwa vizuri.

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi kwa ujenzi wa reliya mwendokasi. Wananchi wanaisubiri kwa hamu ikamilike,

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

hasa wa Mkoa wa Morogoro Vijijini, Morogoro Mjini, Kilosa naMkoa mzima wa Morogoro kwa ujumla. Wananchi waliopishaumeme wa reli hii ya mwendokasi wanaulizia ni lini watalipwafidia yao? Ni vyema wakaelezwa kwani ni muda sasaumepita tangu evaluation imefanyika.

Mheshimiwa Spika, natoa hongera kwa MheshimiwaRais kwa ununuzi wa ndege sita na ukarabati wa viwanjavya ndege unaoendelea. Tuliahidiwa ujenzi wa viwanja vyandege sehemu za utalii, Mkoa wa Morogoro ujenzi wa kiwanjacha watalii Selou Kisaki (Morogoro Vijijini). Kwa kushirikianana Wizara husika ya Utalii, nashauri uwanja huu ujengwe.

Mheshimiwa Spika, mawasiliano. Kuna orodha ya vijijina kata vya wilaya ya Mkoa wa Morogoro ambavyoamepewa Mheshimiwa Naibu Waziri. Naomba wakajengeweminara ili waweze kupata mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, usalama wa usafiri kwenyebarabara ya Dar es Salaam – Morogoro – Dodoma. Kunamagari makubwa/malori mengi na baadhi ya ajalihusababishwa na magari haya. Nashauri mwenendo waobarabarani udhibitiwe.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika,nianze na kuunga mkono hoja iliyopo mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, niipongeze Serikali kwa namnaambavyo imeimarisha mitandao ya kiuchumi katika ujenziwa barabara, madaraja, gati, reli, viwanja vya ndege nabandari. Uwekezaji huu kwenye miundombinu itafanyawawekezaji/uwekezaji kukua kwa kasi na kuongeza mapatoya nchi.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali kufuatil iaukarabati wa barabara za lami unaondelea. Wahandisiwahakikishe wanawashauri wakandarasi kuweka viraka vyalami vinavyofanana na uhalisia wa lami ya zamani. Sasa hivi

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

barabara zetu ziko kama zimechorwa rangi, viraka vyeusi nalami yenyewe nyeupe. Sura ya barabara inaonekana kamani michoro ya rangi. Taifa letu ni kubwa, nchi yetu tuipeheshima na kuiweka katika sura nzuri inayopendeza.

Mheshimiwa Spika, ahsante, naunga mkono hoja.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, Wizarahii ina umuhimu sana kwa uchumi wa Taifa letu. Hakuna nchiiliyoendelea duniani bila uwepo wa mawasiliano yabarabara, reli, anga na majini. Katika nchi inayoendeleakama Tanzania ambayo uchumi wake unategemea kilimokwa asilimia 75 ni muhimu sana usafiri wa reli na barabaraukawepo ili kufikisha mazao sokoni.

Mheshimiwa Spika, pamoja na ujenzi unaondelea nimuhimu sana barabara zijengwe kwa kiwango kinachostahili.Ikumbukwe kuwa zaidi ya 40% ya fedha za miradi yoteimewekezwa kwa Wizara hii, hivyo, ni muhimu sana fedhahizi zikatumika ipasavyo. Kibaya zaidi fedha hizi zinanunuamalighafi za ujenzi kutoka nje huku tukiwa na malighafi hizikutoka nchini kama vile chuma cha Liganga ambachokingesaidia mataruma ya reli na pia makaa ya mawe namadini mengineyo.

Mheshimiwa Spika, ni jambo la ajabu kuona kuwaATCL haina sera madhubuti na mpango mkakati, jambolinalosababisha shirika kuendelea kupata hasara kubwa.Pamoja na mpango wa biashara bado tumeshindwa kushikasoko la utalii kutoka nchi mbalimbali kutokana na kutokuwana uwanja wa ndege maeneo ya karibu na mbuga kamaSerengeti hivyo, watalii hao kwenda Kenya na baadayekusafirishwa na magari hadi mbugani, jambo linalotukoseshamapato mengi. Nashauri uwanja wa ndege wa Seroneraukarabatiwe ili watalii watue hapo na iwe rahisi kwendakutalii.

Mheshimiwa Spika, kuna kilio kikubwa cha wananchiwa Dar es Salaam, hasa Ubungo - Kibamba, waliovunjiwanyumba na cha ajabu tunaelezwa barabara ya Dar es

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

Salaam – Chalinze (Express Way), haitajengwa kwa sasa.Jambo hili limetonesha vidonda kwa wale waliovunjiwa.

Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu Uwanja waNdege wa Msalato umekuwa ukizungumziwa lakini cha ajabupamoja na Makao Makuu kuhamia Dodoma uwanjaumekuwa ni huu ulio katikati ya Jiji na ni mdogo. Mwanzonituliambiwa ni wa muda tu lakini tumeshuhudia ukiendeleakupanuliwa na watu wakivunjiwa nyumba zao. Hivyo, natakakujua ile ahadi ya Uwanja wa Msalato ni lini itatimia?

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Hali ya Hewa nayoimekuwa na shida kubwa sana. Sielewi ni vifaa vya kizamaniau ni utaalam hafifu. Inashangaza tunapopewa forecastsambazo haziendani na uhalisia. Mfano kile Kimbunga Kenethkilivyotangazwa na hali ilikuwa sivyo kabisa, matokeo yakemadhara yakawa mikoani na si kule Mtwara. Ni aibu kubwasana katika ulimwengu huu wa digitali bado forecastszinakuwa hazieleweki. Iko siku tutaambiwa kutakuwa na juakali ghafla mnapata mvua za mafuriko, hivyo inakuwa jangakubwa na vifo.

Mheshimiwa Spika, kule Marangu kuna barabarakutoka Mtoni – Kirua, ujenzi ni kama umesimama lakini chaajabu hata zile sehemu ambapo ujenzi umekamilikamadaraja hayajajengwa. Hali hii ni hatari sana kwa kuwabarabara ni pana lakini kwenye madaraja ni nyembambakuweza kupitisha gari moja tu, hivyo kwa madereva wagenikuna hatari ya kupata ajali. Mfano Mto Ghona/Wona, MtoMakoa, kwa kifupi mito yote toka Marangu Mtoni mpakaKilema madaraja yake ni tishio kwa watumiaji.

Mheshimiwa Spika, ni wazi kuwa Dar es Salaam ni jijikubwa kuliko majiji yote na lenye kuiingizia nchi pato kubwasana. Hali ya msongamano Dar-es-Salaam inapoteza kwakiasi kikubwa pato hilo. Haiwezekani gari kutoka Ubungo hadiKibaha kilometa 30 litumie saa 2 – 3 wakati kwa hali yakawaida ni dakika 30 – 45. Hali hii imekuwa mbaya zaidikutokana na ujenzi wa barabara unaoendelea. Hivyo basi,ni muhimu sana malori ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

foleni kutokana na ama kuharibika na ukubwa wakeyatafutiwe njia mbadala au dry port eneo la Mlandizi au Ruvukupunguza adha hii kubwa ili kuongeza pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, suala la mawasiliano ya simu nimuhimu sana. Hivyo ni muhimu miundombinu ya minaraiboreshwe ili kupata usikivu mzuri. Imekuwa ni kilio kikubwakwa tatizo la usikivu wa simu kutoka eneo moja kwendalingine.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika,napenda kuchangia hoja hii katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, mgawo wa bajeti ya maendeleokwa Wizara ya Ujenzi mwaka 2016/2017 ulikuwa shilingi trilioni4.8, mwaka 2017/2018 shilingi trilioni 4.9, mwaka 2018/2019shilingi trilioni 4.1 ambayo ni 34.5% ya bajeti yote yamaendeleo. Mpaka mwaka huu wa fedha unaisha Bungelitakuwa limeidhinisha jumla ya shilingi trilioni 13.8 kwa miakamitatu.

Mheshimiwa Spika, napenda kujua ni sekta zipinyingine za uchumi zimechochewa kutokana na uwekezajihuu kama viwanda, ni vingapi vimeanzishwa? Watanzaniawangapi wameondokana na umasikini? Pato la Taifalimeongezeka kwa kiasi gani kutokana na uwekezaji huu?

Mheshimiwa Spika, sekta ya ujenzi. Kumekuwa nachangamoto kwa wakandarasi Watanzania kutopata kaziza kufanya ndani hata nje ya nchi. Serikali ina mkakati ganiwa kufanya wakandarasi hawa waweze kupata angalauasilimia 50 ya kazi za ndani ya nchi na hata za nje ya nchi?

Mheshimiwa Spika, TBA wanapewa kandarasi zaSerikali na mara nyingi hawashindanishwi. Hii imefanya kazizao kuwa chini ya kiwango na malalamiko yamekuwa mengi,Serikali ifanyie kazi suala hili.

Mheshimiwa Spika, barabara nyingi zimekuwahazikamiliki kwa sababu fedha nyingi zinaenda kwenye

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ambao unachukuamuda mrefu sana. Wananchi wanaathirika kwa kutosafirishamazao yao kwa wakati na uchumi kusuasua.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, kuna ahadi zaMheshimiwa Rais kutekeleza ujenzi wa barabara za Mkoa waIringa, nikitaja chache barabara ya Rujewa – Madibira, IringaMjini – Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (kilometa 14) na Ipogolo -Kilolo (kilometa 133). Barabara zote hizi fedha za ujenzi badohazijafika, kinachofanyika ni usanifu tu. Pamoja na utengajihuu wa fedha mnaouainisha, naitaka Serikali hii itekelezeahadi hizi mapema ili wananchi wasipate adha.

Mheshimiwa Spika, bado nasisitiza uendeshaji waShirika la Ndege la ATCL ni wa hasara. Serikali iangalie sualahili kwa makini kwani kodi za wananchi zinazidi kuteketea.

Mheshimiwa Spika, mradi wa SGR vifaa vinavyotumikavinatoka nje ya nchi. Nashauri Serikali itumie malighafi kutokahapa nchini. Kwa mfano, makaa ya mawe ambayo yapoMchuchuma yangetumika katika mradi huu.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, kwanzanawapongeza Mheshimiwa Waziri Kamwelwe na NaibuMawaziri; Mheshimiwa Kwandikwa na Mheshimiwa Nditiyekwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, kuna shida kubwa ya kukosaminara ya mawasiliano Kata za Shitage, Igulungu na Makazi.Naomba minara katika kata hizo.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Tabora – Mrambali –Ishitimulwa - Mhulidede ni muhimu kuwa na lami. Barabarahii muhimu kwani inaunganisha Mikoa ya Shinyanga naTabora.

Mheshimiwa Spika, pongezi kwa Mamlaka yaMawasiliano TCRA. TCRA wamefanya kazi kubwa ya kubadilimawasiliano na matangazo ya TV kutoka analojia na kuwadigitali na kuwa moja ya nchi za kwanza Barani Afrika na ya

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

kwanza EAC. Vilevile wanasimamia mgawanyo wa masafa(frequency monitoring) na ugawaji bora wa leseni za rediona televisheni. TCRA wamefanya kazi kwa weledi sanakusimamia mashirika ya huduma za simu na kuhakikishawanalipa kodi za Serikali kwa kutumia mtambo wa TTMS.

Mheshimiwa Spika, natanguliza shukrani.

MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Waziri, tunaombasanasana tuanze kujenga kwa lami barabara ya Kongwa –Arusha kupitia Olkesmet (Simanjiro). Tuanze hata kama nikilometa 15 tu.

Mheshimiwa Waziri, Kongwa Mjini tunahitaji lamiangalau tupate hata kilometa 5 tu.

Mheshimiwa Waziri, Daraja kubwa la Njoge kwenyebarabara itokayo Pandambili ni muhimu mno kujengwa.TARURA wapewe bajeti.

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Spika,niipongeze sana Wizara hii na Mheshimiwa Waziri kipekee naNaibu Mawaziri wake kwa kazi nzuri wanayofanya ilikuunganisha nchi yetu kwa barabara, reli na kimawasiliano,hongereni sana.

Mheshimiwa Spika, barabara yangu ya Ikungu -Malampaka ilitengewa bajeti ya shilingi milioni 800 ili iwezekujengwa kwa kiwango cha lami mwaka wa fedha 2018/2019 lakini ujenzi huu haujaanza mpaka leo. Katika bajeti ya2019/2020, Wizara imetenga shilingi milioni 300 kwa ajili yabarabara hii. Je, ni lini sasa barabara hii itaanza kujengwaikiwa tumebakia na mwezi mmoja tu mwaka wa fedha 2018/2019 uishe? Barabara hii ni muhimu sana kwa ajili yakuunganisha na bandari kavu ya Malampaka ambayoitakuwa ni lango la bidhaa na biashara kwa Mikoa ya Simiyu,Mara na maeneo ya Kenya.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara kwa kiwangocha lami ulilenga kuboreshwa kwa barabara na kurahisisha

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

usafiri ili uwe wa haraka zaidi na kufanya watu na usafirishajimizigo ifike mapema zaidi na hatimaye kuchochea shughuliza uchumi ziende kwa kasi zaidi. Cha kushangaza muda wakusafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza umebaki kuwani uleule kama wakati ule ambapo barabara hazikuwa zalami. Mabasi yalikuwa yanatoka saa 11.00 alfajiri Dar esSalaam kabla ya lami na kufika Mwanza saa 5.00 au saa 6.00usiku. Sasa tuna barabara za lami lakini muda unaotumikakwa mabasi kusafiri bado ni uleule na wakati mwingine nizaidi.

Mheshimiwa Spika, sasa barabara za lamizimetusaidiaje ikiwa hazijapunguza muda tuliokuwatunapoteza barabarani? Ni shughuli ngapi za kiuchumizinachelewa? Ni fedha kiasi gani zinapotea kwa kupotezamuda barabarani? Wizara hii inafanya kazi nzuri lakini tafuteniufumbuzi wa tatizo hili.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na naunga mkonohoja.

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja hii kwa asilimia 100 na niombeyafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, mkongo wa Taifa. TTCL na Tumeya TEHAMA iimarishe kwa kuwekeza mtaji wa kutosha ili sektaya mawasiliano ichangie zaidi katika uchumi wa Taifa naukuaji wa sekta ya viwanda.

Mheshimiwa Spika, katika Wilaya yangu yaNamtumbo kuna maeneo yenye wakazi wengi lakini hayanamitandao ya mawasiliano ya simu. Ni maeneo yote ya Kataza Msindo, Mgombasi na Lisimonji.

Aidha, vijiji vya Mtewamwachi, Likusanguse, Limamuna Mtakuja navyo havina usikivu wa mawasiliano ya simu.Naomba Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote utusaidiekukamilisha na kufungua mawasiliano ya simu na data katikamaeneo hayo.

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa kuisemea barabara ya kuunganisha Mikoa yaRuvuma na Morogoro ya Lumecha - Kitanda-Londo - KilosaKwa Mpepo – Lupiro - Ifakara - Mikumi. Mheshimiwa Raisameliisemea barabara hii wakati akifungua Daraja laKilombero na Kituo cha Mabasi cha VETA cha Namtumboau tuseme alipokuwa kwenye ziara Mkoani Ruvuma kuanziatarehe 4 hadi 09 Aprili, 2019 lakini katika kitabu naona shilingimilioni 80 tu ambazo haziwezi kujenga barabara kati ya Lupilo-Kilosa Kwa Mpepo-Londo - Lumecha kupitia Kitanda. Hii nisawa kweli? Namwomba Mheshimiwa Waziri aliangalie sualahili.

Mheshimiwa Spika, kwa wana Ruvuma barabara yakuunganisha Mikoa hii inaanzia Kilosa Kwa Mpepo - Londo -Kitanda. Kipande hiki cha kilometa 121.5 hivi ndiyo inawezakuitwa kiungo cha mikoa hiyo miwili. Naomba fedhazilizotengwa zishughulikie kipande hiki cha barabaravinginevyo tafsiri ya bajeti hii ni kujenga barabara ya Mikumi- Ifakara - Mlimba na kuelekea Njombe badala ya barabarayetu wana Namtumbo.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Wazirikwa kutufikiria wana Namtumbo kwa barabara zetu za kutokaNaikesi - Mkonga na Namtumbo – Likuyu –Namabengo –Mbimbi - Libango - Namtumbo na nyinginezo kwa kuzitengeafedha za matengenezo hususani lami nyepesi ya mita 100katika barabara ya Naikesi - Mtonya.

Mheshimiwa Spika, aidha, kupitia Waziri, nimshukuruna kumpongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wetu mpendwa kwa kuitengea fedha yaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina barabara yaMtwarapachani - Likusanguse - Nalasi jumla ya shilingi milioni450 na hivyo kumfanya Mhandisi Mshauri aendeleze nakukamilisha kazi iliyoanza.

Mheshimiwa Spika, TARURA na TANROADS, taasisi hizimbili zinapata fedha kutoka Hazina na Road Fund Board (RFB)

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

kwa kuwa taasisi hizi ni za kushughulikia barabara. Naombataasisi zote za TANROADS, RFB na TARURA ziwe chini yausimamizi wa mamlaka moja ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzina Mawasiliano. Kuziweka taasisi hizo katika Wizara mbilitofauti inaongeza gharama za utawala na uendeshaji nakugawana wataalam hususani Wahandisi wa sekta yabarabara wachache tulionao nchini. Hoja za kupandishahadhi barabara pamoja na kuiongeza TARURA mgao wafedha za Mfuko wa Barabara zitaondoka ikiwa taasisi hizi zaTARURA na TANROADS zitawekwa chini ya Wizara moja yenyewajibu wa kujenga na kukarabati barabara.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kuendelea kunipa pumzi. Aidha,nimpongeze Waziri na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kwa kuiwezesha mihimili ya utawalana Bunge kufanyakazi kwa umakini na kwa umoja kwakiwango cha kutuwezesha wana Namtumbo kuanza kuonamaendeleo katika sekta mbalimbali hususani barabara,mawasiliano ya simu, umeme na kadhalika. Ahsanteni sana.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia100 na naomba kuwasilisha.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa nimpongeze Waziri pamoja na timu yake yotekwa kazi kubwa wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, ndani ya Wilaya ya Lushoto hasakatika Jimbo la Lushoto, barabara za Lushoto siyo siasa tu, nizaidi ya maisha ya watu hasa barabara ya Mlalo – Ngwelo –Mlola – Makanya - Mlingano - Mashewa yenye kilometa 57.Barabara hii nimeizungumzia kwa muda mrefu sana kuwa nibarabara ya kiuchumi yenye wakulima wengi wanaozalishamazao ya kibiashara.

Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa,barabara hii inapigwa danadana na TARURA wanasema ipoTANROADS nao TANROADS wanasema ipo TARURA. NaombaMheshimiwa Waziri barabara hii muichukue iwe ya TANROADS

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

ili wananchi wa maeneo hayo niliyotaja waweze kunufaika.Kama hili Mheshimiwa Waziri haliamini, atume timu yake iendeili ajue ukweli wa haya niliyoyaandika.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, kunabarabara ya kuanzia Dochi - Ngulwi – Mombo. Kamaunavyofahamu Lushoto kuna barabara moja kubwa tu nabarabara hii ni nyembamba na imejaa maweyanayoning’inia juu ya barabara na ndiyo sababu mvuaikinyesha mawe yanaporomoka na kuziba barabara.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2017, barabara hii ilizibakwa siku zaidi ya 21 (wiki tatu) hali iliyosababisha usumbufumkubwa sana na kupelekea wakulima wa mboga mbogana matunda kupata hasara kubwa sana pamoja na hudumaza jamii kukosekana. Niiombe Serikali yangu Tukufu, kwa kunakuna barabara hii ya Dochi - Mombo kilometa 16 tuitengenezwe ili iwe barabara mbadala lakini siyo kwa kupitikatu ila pia ni barabara yenye mazao mengi na pia kunawananchi wengi wanaoishi katika maeneo hayo na kwa sasawanakosa huduma za afya pamoja na za kijamii. Pamoja nahayo, barabara zote hizi mbili siyo lazima ziwe na lami.Wananchi wanataka zipitike tu kwa mwaka mzima yaani ziweza changarawe tu.

Mheshimiwa Spika, pia kuna barabara ya TANROADSinayoanzia Nyasa – Mshizi - Gare - Magamba. Barabara hiikwa kweli nimshukuru Meneja wa TANROADS NduguNdumbali kwa kazi kubwa. Barabara hii ina maeneo yakujenga madaraja mawili; Daraja la Mshizi na Daraja laKongei pamoja na kuweka zege maeneo hatarishi kama vileMlima wa Yamba. Hili nalo niiombe Serikali yangu itengefedha ili barabara hii iweze kurekebishwa na kujenga hayomadaraja mawili.

Mheshimiwa Spika, pia niendelee kuipongeza Serikaliyangu tukufu kwa kutupatia kilometa 1 kila mwaka kwabarabara iliyoanzia Magamba kwenda Mlola na Magambakwenda Mlalo. Niiombe Serikali yangu ituongezee angalau

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

kilometa 3 ili ziwe 4 ili kuharakisha maendeleo ya Wilaya yaLushoto na huduma kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, kama mnavyofahamu kuwaTanga ni Jiji lakini tunayo changamoto za uwanja wa ndege.Kwa hiyo, niiombe Serikali yangu iupanue Uwanja wa Ndegewa Tanga ili ndege kubwa ziweze kutua.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hayo, mwaka janatuliomba Bombardier iweze kutua Tanga na Waziri alikubalilakini mpaka leo ndege haijatua. Naomba nikumbushie tenakuwa Bombardier itue Tanga sasa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja kwaasilimia 100.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Spika,uendeshaji wa ndege nchini. Serikali iliagiza ndege kubwa(Dreamliner) iko wapi? Mbona hatuoni ikifanya kazi?Inanunuliwa ndege ya maonyesho kwa cash money, kodi zawananchi halafu hatuoni ikifanya kazi kwa kuinua uchumiwa nchi kama ilivyoelezwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, zipo taarifa kuwa ndege hiyoimekodishwa Kenya. Kama ndivyo, hayo ndiyotunayolalamikia kuwa Serikali ina tatizo katika kusimamia nakupanga priorities. Hivi kulikuwa na sababu gani kukimbiliaDreamliner, ku-invest kwenye ndege ambayo return zakehaziwezi kuonekana kwa haraka? Ni bora Serikali ingewekezakwenye project kama za afya, maji na kadhalika, ndege boraingetumia PPP.

Mheshimiwa Spika, matengenezo ya ndege ndogotatu (Bombardier) zaidi ya shilingi bilioni 14, hivi kweli ndegezinajiendesha kwa faida? Kwa nini Serikali isingeachia privatesector au nchi zenye uzoefu wa biashara za ndege mfanoEthiopia na kadhalika?

Mheshimiwa Spika, SGR, kwa sasa ajira kwaWatanzania ni asilimia 20 na asilimia 80 ni Waturuki. Hiyo siyo

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

sawa, Serikali ilipaswa kuandaa watu wetu kuingia kwenyeajira kabla ya kuanzisha mradi wa SGR. Kazi ambazo niprofessional/technical skills zingefanywa na Watanzaniakuliko hivi sasa Watanzania wanaishia kwenye kazi ndogondogo.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Spika, naanzakwa kumshukuru Mwenyezi Mungu na pia kuwatakiaWaislamu wote Tanzania na duniani kwa ujumla, Mfungomwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Pangani ni miongonimwa barabara za kimkakati na ni miongoni mwa barabarainayounganisha Mikoa na Wilaya. Pangani road inaanzaMkoa wa Tanga na kupitia Wilaya za Muheza, Pangani naChalinze Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Pia barabara hiiinaunganisha nchi za Afrika Mashariki kwa barabara kuuitokayo Mombasa - Kenya kupitia Tanzania na hadi Nchi zaKusini mwa Bara la Afrika.

Mheshimiwa Spika, barabara hii imewekewa ahadina Marais wanne ambao sasa ni wastaafu ambao Julius K.Nyerere, Mzee Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa naJakaya Kikwete. Pamoja na fedha kupatikana (bajeti)upumbuzi yakinifu tayari na mkandarasi ameshapatikana,naiomba Serikali itoe tamko ni lini barabara ya Panganiitaanza kujengwa rasmi?

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara kwachangarawe. Barabara zifuatazo katika kitabu cha bajeti nasijaziona, naomba zitengewe fedha:-(i) Barabara ya Mabokweni-Maramba-Daluni-Korogwe;

(ii) Barabara ya Kirare-Mapojoni-Mkembe;

(iii) Barabara ya Amboni-Mleni-Rubawa-Pangarawe;

(iv) Barabara ya Pongwe-Marungu-Geza; na

(v) Barabara ya Fuweni-Mondura-Mwarongo.

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali iongeze fedhakatika bajeti hii ili barabara hizi ziweze kupitikana wakati wotewa mwaka.

Mheshimiwa Spika, Bandari ya Tanga ni miongonimwa bandari za kihistoria duniani. Kama tunavyojua, bandarini lango kuu la biashara lakini haitumiki ipasavyo pamoja nakufanyiwa ukarabati wa shilingi bilioni 1.8 na crane ya 40Ftmpya bado kuna upungufu wa vifaa vingi.

Mheshimiwa Spika, nashauri bandari hii ipatiwe fedhaza kutosha kwa ajili ya vifaa bora na vya kisasa. Serikali naMamlaka ya TPA ifanye utaratibu wa kupanga aina za mizigo(categories) kwa kila mandarin. Bandari ya Tanga ichukuemizigo ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Musoma naBukoba bila kusahau mizigo ya Uganda, Rwanda na Burundi.Bandari ya Mtwara (Mtwara Corridor) ichukue mizigo yaMtwara, Mbeya, Sumbawanga, Katavi, Kigoma, Iringa bilakusahau mizigo ya Zambia, Malawi na Congo DRC. Bandariya Dar es Salaam ni kuipa mizigo mikubwa sana. Dar esSalaam Port kwa kuifanya ishughulikie mizigo yote inayotokanchi za nje matokeo yake meli zinasubiri muda mrefu sanana kuwa ni sababu ya baadhi ya makampuni ya melikuikimbia Bandari ya Dar es Salaam na kushushia mizigoMombasa port, Beira na Maputo. Hivyo, naiomba Serikaliifanye categories za mizigo na Bandari zote za Tanga,Zanzibar, Dar es Salaam na Mtwara zifanye kazi kwa faida.

Mheshimiwa Spika, Bandari Bubu ziboreshwe. BandariBubu Tanzania ni jambo lisiloepukika kwa kuwa Watanzaniawanafanya kazi za usafirishaji kupitia maji (bahari, mito,maziwa). Bila kuathiri huduma hii kwa wananchi ni vyemaBandari Bubu zikafanyiwa tathmini na zinazokidhi vigezozikarasimishwa (kuboreshwa) na kuwa chanzo cha mapatoya Serikali.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Tanga tunazo BandariBubu katika maeneo ya Moa, Jasini, Monga, Tongoni,Mwarongo, Marungu (Tanga Mjini), Kigombe (Muheza),Kipumbwi na Mkwaja. Nashauri Bandari Bubu za Kigombe

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

(Muheza) na Kipumbwi (Pangani) ziboreshwe kwa kujengewamajengo bora ya TRA, TPA kwa ajili ya kukusanya mapato yaSerikali ya forodha na kodi mbalimbali. Bandari hizizikiboreshwa zitaongeza mapato ya Serikali na pia itaongezaajira na kuongeza mzunguko wa fedha kwa wananchi(wafanyabiashara) wa maeneo husika.

Mheshimiwa Spika, minara ya simu/mawasiliano. Mojaya vigezo vya maendeleo ni mwasiliano ya uhakika. Yapomaeneo katika Jimbo/Jiji la Tanga hakuna mawasiliano yauhakika. Unapotaka kuongea na simu lazima upande ju yamti, kichuguu au katika maeneo maalum hali inayopelekeawananchi kupata shida ya mawasiliano hususani katikakipindi cha dharura yoyote inapotokea au hata katikashughuli za biashara. Maeneo hayo baadhi ni Kata zaMarungu, Tongoni, Mzizima, Mabokweni, Kiomoni na Maweni.Naishauri Serikali kwa kushirikiana na Makampuni ya simu(Tigo, Airtel, Zantel, TTCL na Vodacom) kuongeza minara.

MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Spika,naomba sana ahadi ya barabara ya kutoka Njombe –Makete - Mbeya ifanyike. Kutoka Makete ni barabara yakutoka Makete - Bulongwa – Mbeya na Makete- Ivalalila -Ujuni kuunganisha barabara ya kutoka Bulongwa.

Mheshimiwa Spika, pia kwa ajili ya kuwezesha Hifadhiya Kitulo ni muhimu barabara ya kutoka Chimale- Matembaau Mfumbi kuja Matamba ijengwe kwa lami. Pia ili kuboreshaujenzi wa barabara za Ludewa, Kipengele- Mbalache - Lupilakwenda Ludewa ijengwe kwa lami.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mawasiliano Kata zaMang’ota, Ikuwo, Kigala, Lupila na Ukwama zipewemawasiliano ya Voda, Airtel, Halotel na Tigo. Hili likifanyikalitasaidia sana kutupa mawasiliano.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja, nampongeza Mheshimiwa Waziri, NaibuMawaziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara.

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Mheshimiwa Spika, naomba kuzungumzia ujenzi wabarabara ya Kigoma – Nyakanazi. Barabara hii imechukuamuda mrefu sana lakini mpaka leo haijakamilika. NombaSerikali iweze kusimamia ili iweze kukamilika.

Mheshimiwa Spika, kipo kipande cha kutoka Uvinza –Malagalasi, nacho ni tatizo. Tunaomba kipande hiki nachokiweze kujengwa. Kipo kipande cha Chagu - Kazilamburanacho tunaomba kiweze kujengwa ili wananchi wawezekuondokana na adha ya usafiri.

Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba nishukuru Serikaliinayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John PombeMagufuli kwa kuweza kukubali barabara ya kutoka Kabingo-Kibundo- Kasulu - Bulingwe kujengwa kwa lami kupitia fedhaza AfDB.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,nashukuru sana na naunga mkono hoja.

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Spika, nichukuefursa hii kuishukuru Serikali kwa kutuongezea kilomita 50 zabarabara ya lami kutoka Mnivati – Tandahimba. Ombi langukwa Serikali ni kwamba kwa kuwa barabara hii ni muhimukwa uchumi wa Mkoa wa Mtwara ambao unategemea sanazao la korosho huku asilimia 47% ya korosho zote Tanzaniazikiwa zinatoka maeneo hayo, Serikali iwape wakandarasizaidi ya mmoja ili tupate matokeo ya haraka sana.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe tu kuwa tunazokilomita 50 za awali za kutokea Mtwara kuelekea Mnivati lakinibarabara hii ambayo mkataba wake il ikuwa uweumekamilika ndani ya miezi kumi na saba mpaka sasa nikilomita 8 tu ndiyo zimewekwa lami. Hii ndiyo kusema kwakusuasua huku tutahitaji miaka 10 kukamilisha barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, naomba maeneo yafuatayoyapate minara ya simu; Kata za Mdimiba, Michenjele,Nganja, Mkwiti, Mkoreha na Chaume. Kata hizi hazinamawasiliano ya simu, naomba suala hili lishughulikiwe.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mheshimiwa Spika, niombe kuzungumzia suala la reliya kutoka Mtwara – Mbambabay - Mchuchuma - Liganga.Reli hii kama itejengwa italeta fursa za kibiashara Kusini mwaTanzania na nchi za Malawi, Zambia na Msumbiji.

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Spika,naomba niwapongeze Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, NaibuMawaziri, Makatibu Wakuu, Watendaji na Taasisi zote zilizochini ya Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mawasiliano, katika Jiji laDodoma eneo la pembezoni Kata ya Mbalawala, Kijiji chaLugala – Matangizi hakuna mawasiliano ya simu hali ambayoinasababisha wagonjwa kutopata huduma kwa harakakutokana na umbali wa eneo hilo. Naomba wananchi hawawapatiwe mawasil iano ya simu il i waondokane nachangamoto hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Seminari,mnamo mwaka 2015 wakati Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli akiwa mgombea wa Urais aliwaahidi wananchi waJimbo la Segerea kuwa barabara ya Segerea - Seminari -Majumbasita (km 3) itajengwa kwa kiwango cha lami. Hatahivyo, barabara hiyo haina hata dalili ya kutengenezwa kwakiwango cha lami. Naomba Serikali itekeleze ahadi hiyo yaMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nirudie kuwashukuru sanawatendaji wote kwa kazi nzuri wanayoifanya.

MHE. WILLIAM T. OLENASHA: Mheshimiwa Spika,napenda kwanza kuwapongeza Mheshimiwa Waziri, NaibuMawaziri na watendaji wa Wizara kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, napendakuishukuru Wizara ya Ujenzi na Serikali ya Awamu ya Tanokwa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara katika jimbo laNgorongoro, hususani barabara ya Loliondo - Mto wa Mbuinayojengwa kwa kiwago cha lami.

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

Mheshimiwa Spika baada ya pongezi hizo, naombanieleze changamoto zilizopo katika Jimbo la Ngorongoro.Kwanza, ni kusimama kwa ujenzi wa barabara ya Loliondo –Mto wa Mbu. Ujenzi wa barabara hii unasuasua kutokana naukosefu wa fedha na uchelewashaji wa malipo kwamkandarasi. Kwa sasa mkandarasi anadai zaidi ya shilingibilioni 13. Kwa sababu cashflow isiyo nzuri, mkandarasiamelazimika kusimamisha ujenzi kwa kiasi kikubwa kuanziatarehe 19/4/2019. Mkandarasi amelazimika pia kupunguzawafanyakazi 300 kwa sababu ya kukosa fedha za kuendeleana ujenzi. Ucheleweshaji huu wa malipo utaendelea kufanyamradi kuchelewa kukamilika. Tunaomba Wizara ifanyemalipo mapema ili ujenzi uweze kuendelea.

Mheshimiwa Spika, pili, kukwama kwa miradi yamawasiliano ya simu za mkononi, Tarafa ya Ngorongoro.Tunashukuru sana Wizara kupitia Mpango wa Mawasilianokwa Wote kwa kutuletea miradi ya mawasiliano katika Wilayaya Ngorongoro ikiwemo ile inayotekelezwa ndani ya Hifadhiya Ngorongoro, eneo la matumizi mseto ya ardhi lenye vijiji25 na wakaazi wapatao 95,000.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kupatikana msaadahuu wa Serikali, ujenzi wa minara umekwama kwa mudamrefu kutokana na vikwazo vya Mamlaka ya Hifadhi yaNgorongoro, ikiwepo taratibu za Tahmini ya Mazingira (EIA)inayochukua muda mrefu kukamilika. Baadhi ya miradiambayo imeshindwa kuendelea kwa wakati ni pamoja naile ya Embakaay (Naiyobi), Sendui (Alaililai) na Nainokarokainayojengwa na kampuni ya Halotel.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara itupie jicho miradiya mawasiliano ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwaniwananchi wanakosa huduma muhimu inayotolewa naSerikali. Wizara iangalie usahihi wa miradi midogo kamamiradi kufanyiwa tathmini kubwa ya mazingira (EIA) na katikanjia inayochukua muda mrefu.

Mhe Naibu Spika, baada ya kusema hayo machache,naomba kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

MHE. HAMOUD A. JUMAA: Mheshimiwa Spika, awaliya yote, napenda kutumia nafasi hii kumshukuru MwenyeziMungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kufika mahalihapa nami niweze kuchangia hotuba hii ya bajeti ya Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, kama inavyojieleza, hotuba hiiinakwenda kutatua changamoto mbalimbali na kutekelezamiradi ya kimaendeleo inayogusa sekta husika za ujenzi,uchukuzi na mawasiliano. Aidha, inakwenda kutekeleza Ilaniya Chama cha Mapinduzi kama ilivyoainishwa. Pia nichukuefursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja nawatendaji wote wa Wizara kwa kuandaa hotuba nzuri yenyemalengo chanya.

Mheshimiwa Spika, napenda kuanza kuchangia kwakuipongeza Serikali katika jitihada zake za kuendeleakuhakikisha nchi yetu inakua na barabra nzuri zinazopitikawakati wote. Lengo kuu la Serikali ni kuunganisha mikoa yotekwa barabara za lami i l i kuimarisha na kurahisishamawasiliano ya usafiri na usafirishaji wa watu, bidhaa namazao mbalimbali. Ni jambo la kujivunia sana kwani hadikufikia Februari 2019, jumla ya kilomita 266.78 za barabarakuu za mikoa zimekamilika na kilomita 392.2 zinaendeleakujengwa kwa kiwango cha lami. Vilevile katika jitihada zilezileSerikali imekamilisha ujenzi wa madaraja matano katika MtoLukuledi (Lindi), Mara (Mara), Sibiti (Singida), Momba (Rukwana Songwe) na Mlalakuwa (Dar es Salaam) na ujenzi wamadaraja 8 unaendelea katika sehemu mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa miradi hii, utatoa fursambalimbali kwa wananchi kupata ajira pamoja na kupatasoko kwa bidhaa na mazao yao. Aidha, utasaidia sanakuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini ikizingatiwamiundombinu yetu ni mizuri.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, bado naendeleakuipongeza Serikali kwa kuendelea kutekeleza ujenzi wamiradi ya barabra inayolenga kufungua fursa za kiuchumikwa wananchi. Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa barabara

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

kuwezesha mradi wa kuzalisha umeme wa Stigler’s Gorge kwakiwango cha changarawe kutoka Ubena Zomozi mpakaSelous kilomita 177.6 na ukarabati wa barabara ya kutokaKibiti - Mloka – Selous – Mpenda (Km 370), Makutano – Natta– Magumu - Liliondo (Km 239) na Loliondo - Lumecha (Km464). Haya yote kwa ujumla yamefanywa na Serikali yaChama cha Mapinduzi yenye viongozi imara wenyekutekeleza yale yote yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi yaCCM, ikiongozwa na Rais wetu shupavu na mpendamaendeleo.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa ujenzi waawamu ya kwanza wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaamhadi Morogoro kwa asilimia 42.8 na unatarajiwa kukamilikaifikapo Novemba, 2019. Hali kadhalika, ujenzi wa awamu yapili wa reli hiyo ya kisasa kutoka Morogoro - Makutupora JijiniDodoma umefikia asilimia 6.07. Hadi sasa mradi kutoka Dares Salaam - Makutupora umeshaajiri wafanyakazi wazawawapatao 6,335 sawa na asilimia 90 ya wafanyakazi wote. Nijambo la kupongezwa kwani limezalisha ajira kwa watu wetuna kuna faida kubwa mradi husika utakapokamilika.

Mheshimiwa Spika, sambamba na ujenzi wa reli mpyaya kisasa, Serikali katika mwaka 2018/2019 imeendelea nakazi ya kuboresha, kujenga na kukarabati miundombinu yareli ya kati kwa kuondoa reli zote nyepesi na kuweka reli mpyazenye uzani wa paundi 80 kwa yadi kati ya stesheni ya Dares Salaam na Isaka. Aidha, kazi ya ukarabati wa reli ya Tanga-Arusha imekamilika kwa sehemu ya Tanga – Same (Km 199).Hata hivyo, katika mwaka 2019/2020, Serikali itaendelea nakazi ya ujenzi wa reli ya kisasa, ukarabati wa ujenzi wa reli yakati na nyingine ikiwemo ya Tanga – Arusha ili kuimarishahuduma za usafirishaji na biashara kwa ujumla. Miradi hiiinatekelezwa chini ya Serikali ya Chama cha Mapinduziikiongozwa na Rais wetu anayetekeleza Ilani ya Chama.

Mheshimiwa Spika, tumeendelea kuwa nachangamoto ya msongamano katika Jiji letu la Dar es Salaamna imejitokeza pia katika baadhi ya miji, lakini Serikaliimefanya na inaendelea kufanya jitihada kubwa kutekeleza

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

miradi ya kuondoa msongamano wa magari kwenye Jiji laDar es Salaam ili kurahisisha usafiri na usafirishaji na kuchocheashughuli za kiuchumi kwani Jiji hili lina bandari kuu ambayohuchangia pato la nchi kwa kiasi kikubwa. Hivyo, jitihada hizizinafanyika kulingana na hali halisi iliyopo.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwakukamilisha ujenzi wa mradi wa barabara ya juu ya Mfugalena miradi mingine inayoendelea. Miradi ambayo ipo katikahatua mbalimbali za utekelezaji ni ujenzi wa barabara za juukwenye makutano ya Ubungo (Ubungo Interchange),upanuzi wa barabara ya Kimara Mwisho - Kiluvya (Km 19.2)kutoka njia mbili kuwa nane. Katika mradi huu upanuzi wa hiibarabara ya njia nane, naishauri Serikali mradi huu uwezekuishia mizani ya Vigwaza. Kwa kufanya hivyo kutasaidia sanakupunguza msongamano ambao sasa pia umeanzakujitokeza katika Mkoa wetu wa Pwani hasa Kibaha.

Mheshimiwa Spika, aidha, pongezi hizi pia zinakwendakatika mradi mpya wa daraja jipya la Salender namiundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya II naIII. Hata hivyo, katika mradi wa mabasi yaendayo haraka kwaawamu ya kwanza kumejitokeza changamoto mbalimbalina za muda mrefu ambazo wananchi wamekuwawakizilalamikia za uhaba wa mabasi, abiria kujaa kwa wingina kwa muda mrefu kwenye vituo vya mabasi hayo. Piachangamoto ya uwepo wa baadhi ya mabasi ya express,mabasi haya ya express hayana tija kwa kuwa miundombinuya mabasi haya yenyewe yanajitosheleza kufika kwa haraka.Kero ya mabasi haya ni pale yanapoacha abiria vituoni ilihali kuna uhitaji, athari zake ni abiria kuzidi kuongezeka.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kama ifuatavyo,mabasi yote ya express yarudishwe katika hali ya kawaida ilikukidhi mahitaji kwa sababu hivi sasa mradi unakabiliwa nauhaba wa mabasi. Kufanya hivyo, kutasaidia kupunguzamlundikano wa abiria katika vituo vya mabasi. Aidha,naishauri Serikali katika mradi huu wa mabasi yaendayoharaka awamu ya pili ufike mpaka Kibaha. Kuleta mradimpaka Kibaha kutarahisisha usafiri kwa wananchi kwani

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

mkoa wetu sasa umekua hasa Kibaha tunaongezeko kubwala watu wanaokuja kuishi na kufanya shughuli zao mbalimbali,pia ni eneo ambalo linakua kwa kiwango kikubwa katikaukuaji wa viwanda.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali kuanzisha treni yamoja kwa moja kutoka Posta hadi Mlandizi. Uwepo wa trenihii utakuwa na tija kwani treni inabeba abiria wengi kwawakati mmoja ukilinganisha na usafiri mwingine. Mfanotumeona mabasi yetu yanayotumika katika mradi wa mabasiyaendayo haraka, mabasi haya ni ya gharama kubwa,utunzaji wake pia ni wa gharama pamoja na vipuri vyake.Hali hiyo inapelekea mabasi haya yanapoharibika kuchukuamuda mrefu kukarabatiwa na hivyo kupunguza ufanisi wamradi huu lakini tutakapokuja na treni itatusaidia sanakupunguza adha hii ya usafiri.

Mheshimiwa Spika, aidha katika mradi huo wa treni,naishauri Serikali kwenye kila kituo treni itakaposimamakujengwe maegesho ya magari ya kulipia ili wananchiwanapotoka katika maeneo yao wanaacha magari yaohapo na kupanda treni. Hii itasaidia kuingiza kipato katikamaeneo husika.

Mheshimiwa Spika, changamoto nyingineinayotukabili wana Kibaha Vijijini ni kukosekana kwamawasiliano ya uhakika. Kuna maeneo hakuna minara nahivyo kuifanya dhana nzima ya uchumi wa viwanda kuwangumu, kwani mawasiliano ya simu ni muhimu, yanakwendasawia na dhana nzima ya uchumi wa viwanda. Maeneo hayoni Ruvu Station, Ruvu kwa Dosa, Kipangege, Miande, Dutuni,Madege, Lukunga, Videte, Boko Mpiji, Kwala, MperamumbiMsua na Waya.

Mheshimiwa Spika, hapana shaka yoyote juu yautekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara kamanilivyokwishapongeza hapo awali. Katika mwaka 2019/2020,Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wabarabara kwa kiwango cha lami kwa mikoa ambayohaijaunganishwa na barabara kuu za lami. Kibaha Vijijini tuna

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara, tunabandari kavu Kwala ambayo kwa kiasi kikubwa inakwendakuleta mapinduzi makubwa sana lakini barabara zakehaziridhishi. Naiomba Serikali kujenga kwa kiwango cha lamibarabara ya Vigwaza- Kwala kwani ikiwa katika kiwango chalami itavutia wawekezaji kuja kuwekeza eneo hili nakurahisisha uchukuaji wa mizigo.

Mheshimiwa Spika, aidha, tuna changamoto yabarabara za Chalinze – Magindu, tunaomba ijengwe kwakiwango cha lami. Hata hivyo, kuna mradi mkubwa wa ujenziwa miundombinu ya reli ya kisasa SGR lakini barabara hiiinayoelekea katika mradi huo kuanzia Kongowe – Soga ilipokarakana tunaomba ijengwe kwa kiwango cha lami. Kwasasa maeneo yale kutokana na mradi huu shughuli zakiuchumi zimekua kwa kiasi kikubwa, kujengwa njia hii kwakiwango cha lami kutazidisha kasi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Makofia- Mlandizi -Mzenga ni ya muda mrefu. Barabara hii imeongelewa hapaBungeni tangu Mbunge wa kwanza hadi awamu yangunimekuwa nikiisema hapa Bungeni ijengwe kwa kiwango chalami lakini hadi leo hatujapata majibu ya kuridhisha amautekelezaji. Barabara hii ina umuhimu mkubwa kwaniinaunganisha Majimbo takribani manne ya Bagamoyo,Mkuranga, Kibaha Vijijini na Kibaha Mji. Kwa umuhimu wake,hakika barabara hii inahitaji ijengwe kwa kiwango cha lamihasa ikizingatiwa kila Mbunge aliyewahi kuongoza Jimbo hiliamewahi kuizungumzia.

Mheshimiwa Spika, wakati wa kipindi cha kampenimgombea wa nafasi ya Urais wakati huo ambaye hivi sasandio Rais wetu, alituahidi wana Kibaha Vijijini kujengewabarabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 10.Hii ni ahadi ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuliambapo mpaka leo hii tumebakiza takribani mwaka na nusuwa kumaliza kipindi cha miaka mitano haijatekelezwa. Ni aibukwa Chama kwani tukirudi tena kuomba ridhaa kwawananchi hawa tutawaambia nini? Ni vema ahadi zote zaMheshimiwa Rais alizoahidi kutekelezwa kwa wakati kabla

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

hajamaliza muda wake. Namuomba Mheshimiwa Waziriwakati wa majumuisho atupatie majibu ya hoja hizi ili nasiwana Kibaha Vijijini tuwe na matumaini.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika, naombanianze kwa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, hususanMheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwaya ujenzi wa miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini.Naomba kusema, naunga mkono bajeti hii kama sehemu yakuunga mkono juhudi hizi za Mheshimiwa Rais na Serikali.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizo, naombayafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, ujenzi wa barabara yaKahama - Geita uanze. Kwa miaka mitatu mfululizo tumekuwatunatenga bajeti lakini fedha hazitolewi na ujenzi hauanzi.Hii ni bajeti ya mwisho kabla ya uchaguzi mwakani, hatunacha kuwaambia wananchi. Mheshimiwa Rais pamoja na Ilanikuahidi, pia aliahidi wakati wa kampeni mwaka 2015 naalipofanya ziara Shinyanga mwaka 2017, bado ujenzi hauanzi.Naomba sana, tuanze ujenzi hata kidogo ili tupate chakusema mwakani.

Mheshimiwa Spika, pili, usanifu wa barabara zaKahama – Bulige – Solwe – Mwanangwa, Kahama -Nyang’hwale - Busisi, Kahama – Kaliua - Mpanda naKagongwa – Itobo – Bukene – Tabora. Ukamilishwe haraka iliujenzi uanze kama Ilani yetu ya CCM ya mwaka 2015/2020ilivyoahidi.

Mheshimiwa Spika, tatu, ujenzi wa reli kwa SGR katiya Dodoma – Tabora – Isaka - Mwanza utaanza lini?

Mheshimiwa Spika, nne, ujenzi wa reli ya kisasa Isaka- Kigali umefikia hatua gani?

Mheshimiwa Spika, nashukuru.

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

MHE. SONIA J. MAGOGO: Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa, nianze kwa kuipongeza Wizara kwa nia ya kifufua reliyetu ya Tanga Moshi ambayo ni mwokozi mkubwa sana kwawananchi wa kanda nzima ya Kaskazini, kwani kwenye sualala usafirishaji mizigo na imeepusha barabara yetu kuharibikamara kwa mara kutokana na mizigo mingi kupita kwa njia yabarabara. Tunaomba mradi huu uwekewe mkazo.

Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, naiombaWizara ione umuhimu wa kupanua barabara ya Dodomainayoenda Dar es Salaam, maana kwa sasa hasa wakazi wanjia hiyo wameshaanza kukumbana na tatizo la foleni hasakipindi cha jioni na asubuhi.

Mheshimiwa Spika, pia bado matumizi mabaya yamitandao yanaendelea. Watu wamekuwa wakitapeliwa nahata kutuma vitu visivyofaa kwa jamii yetu na hivyo kupelekeammomonyoko wa maadili kwa vitendo vya ukatili. NaiombaWizara itoe adhabu kali na ziwe hadharani ili watu waogopekutenda mambo yasiyofaa. Anayeadhibiwa itangazwe nawengine wasikie waogope na wao.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri tunaombaukarabati ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani kwakiwango cha lami. Barabara hii imekuwa ni kero ya mudamrefu sana.

Mheshimiwa Spika, pia barabara ya Bagamoyo –Msata, matuta yamezidi, yapunguzwe kama zilivyo barabaraza highway nyingine.

Mheshimiwa Spika, Bandari ya Tanga vitendea kazivyake ni chakavu sana na ni bandari muhimu sana kwaustawi wa uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, pia kuliko mizigo kulundikanabandari ya Dar es Salaam, Bandari za Tanga na Mtwaraziimarishwe na mizigo igawanywe kikanda ili kuzijengeauwezo Bandari za Tanga na Mtwara na kupunguzamlundikano sehemu moja.

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, tunaombamtujengee uwanja wa ndege Manyara Babati pale eneo laMagugu. Pia tunaomba mawasiliano ya simu Kijiji cha Himiti,Chemchem, Imbilili na Babati Mjini.

Mheshimiwa Spika, vile vile tunaomba mwalipe fidiawananchi walio pembezoni mwa barabara za lami mita 12.5zilizoongezeka. All the best.

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA: Mheshimiwa Spika,naipongeza Wizara kwa kuleta bajeti yenye vipaumbele vyamiundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, kwenye utekelezaji, kipande chabarabara ya Kidahwe – Kibondo - Nyakanazikinachotekelezwa kutoka Nyakanazi ni Nyakanazi - Kabingokilometa 50, siyo Nyakanazi - Kibondo. Nashauri Wizaraisahihishe kwa sababu kati ya Kabingo na Kibondo kunakilometa 50 ambazo hazina Mkandarasi, ndiyo maanakwenye mradi utakaofadhiliwa na AFDB zinaonekanakilometa 260 za Kabingo – Kibondo – Kasulu – Manyovu. (Istand to be corrected)

Mheshimiwa Spika, wakazi wa Mkoa wa Kigomakatika wilaya zote za Kigoma, Uvinza, Kasulu, Buhigwe,Kibondo na Kakonko wanafanyia biashara zao nyingi katikaKanda ya Ziwa, hususan Mwanza na Shinyanga. NaishukuruWizara kwa kuliona hili na kutenga fedha za kujengabarabara yote ya Nyakanazi – Kabingo – Kibondo – Kasulu -Manyovu ili kuunganisha Mkoa wa Kigoma na mikoa yaKanda ya Ziwa.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kama ufuatao:-

(i) Mkandarasi wa Nyakanazi - Kabingo asimamiwekwa ukaribu, he is very slow. Tulipokagua utekelezaji naMheshimiwa Waziri Mkuu, Mkandarasi alikuwa ametekelezaasilimia 60 tu na tayari alikuwa na siku 986 nje ya mkataba.

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

Mheshimiwa Spika, nashauri kwa kipande chaKabingo - Manyovu AFDB utaratibu wa fidia uanze mapema.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara itekeleze ahadiya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ya 2015 ya kujengakilometa tatu za barabara za lami Mjini Kakonko. Kwamaelekezo ya Mheshimiwa Waziri, RC wa Kigoma, kupitiaTANROADS ameshatuma Wizara ya Ujenzi makisio yagharama ya kujenga kilometa tatu za Mjini Kakonko. Chondechonde, hii ni ahadi ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika,napenda kuchangia hoja hii kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mkinga – Maramba– Mng’aro, Mlalo hadi Lushoto ipo chini ya Wakala waBarabara ya Mkoa. Barabara hii inaunganisha Wilaya zaMkinga na Lushoto, lakini pia na pacha ya kwenda Korogwena wilaya jirani ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Mheshimiwa Spika, mara zote kwa kipindi cha miakamitano mfululizo barabara hii tumekuwa tukiipitisha katikavikao vyetu vya RCC ili itengewe fedha kwa ajili ya upembuzina usanifu wa kina (detailed design) mara zote inapofikakatika ngazi ya Taifa, budgets inakatwa. Tunataka kujuakulikoni? Tanga - Lushoto tunakosea wapi? Barabara hiiLushoto - Mlalo yenye kilometa 45 ni muhimu sana na kiungokikubwa cha uchumi kwa wananchi wa Usambara. Tunatakakujua kwa nini?

Mheshimiwa Spika, sisi tunaipanga barabara hii katikamipango yetu kwa kuzingatia vipaumbele. Tunapendakupata taarifa rasmi kutoka Serikalini. Hivyo Serikali itoeumuhimu wa kipekee kwa barabara hii angalau hata ijengwekwa kiwango cha lami hata kwa awamu za kilomita 10 kwakila mwaka. Vinginevyo kutokana na jiografia ya Lushotoilivyo, ikibaki kwa kiwango cha changarawe, Serikaliinapoteza pesa nyingi sana katika periodic maintenance.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Mheshimiwa Spika, nchi yetu ina viwanda 14vinavyochakata samaki katika Mikoa ya Mara, Mwanza naKagera, lakini kwa bahati mbaya kutokana na kutokuwa nandege za mizigo, minofu hii inasafirishwa kwenda Nairobi naEntebe hata Kigali ambako wenzetu wanapata mapato yaexport.

Mheshimiwa Spika, hivyo, nashauri, pamoja na ndegeza abiria, Serikali iweke mkazo kuanzisha mchakato wakununua ndege za mizigo ili pia viwanja mbalimbalivinavyoboreshwa viweze kutumika kusafirisha mazaombalimbali kwenda nje ya nchi kwa masoko.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali itazame upyagharama zetu za viwanja vya ndege ili viweze kuvutia hatandege za mizigo kuweza kutua katika viwanja vyetu.

Mheshimiwa Spika, shirika letu la ndege ATCLlinafanya vizuri sana lakini bado linakumbana na ushindanimkubwa kutoka mashirika ya ndege ya Kimataifa.

Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya sana hatawenzetu katika Kanda ya Afrika Mashariki miradi hiiwanaichukulia kama miradi ya kimkakati, hivyo kusimamiwana Serikali nzima tofauti na hapa kwetu ambapo jukumu hiloimeachwa kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pekee.

Mheshimiwa Spika, Mashirika kama Emirates, Turkish,RwandAir ni sehemu ya kukuza utalii na biashara ya Kimataifakatika nchi zao. Mfano, RwandAir inatumika kuitangaza Kigalikuwa kituo cha utalii wa mikutano ya Kimataifa. EthiopianAirways inajulikana kwa kuchangia pato la nchi hiyo kupitiasekta hii ya usafirishaji. Turkish Airline inasifika kwa kuifanyaUturuki kuwa kituo kikubwa cha biashara katika Bara la Ulayana Bara la Asia. Qatar Airways imeubadili mji wa Doha nakuwa kituo kikubwa cha biashara cha Asia na kuhakikishakuwa mji wa Doha unakuwa kiunganishi muhimu cha ndegezote za Kimataifa kwenda maeneo tofauti duniani.

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

Mheshimiwa Spika, kwa mtazamo na mifano hiyo,ATCL inawezaje kuhimili ushindani na mashirika haya ikiwahuko kwao yana misamaha ya kodi, hayalipi gharama zakutua viwanjani na uongozaji wa ndege yanaendesha au nisehemu ya mfumo wa uendeshaji ya viwanja vikubwa vyandege (mfano, Dubai Kigali, Doha na Addis Ababa) yanamilikikampuni za kutoa huduma viwanjani (ground handlingcompany), yanamiliki kampuni za kutayarisha vyakulavinavyotumika ndani ya ndege (inflight catering) na hatakumiliki shule za kutayarisha wafanyakazi wa karakana zautengenezaji wa ndege kwa mashirika mengine ya ndege.Kwa bahati mbaya gharama zote hizi hapa kwetuzimeachwa chini ya Shirika la ATCL.

Mheshimiwa Spika, gharama za uendeshaji wa ATCLambazo zinatokana na utoaji wa huduma zinazotolewa namashirika ya Serikali ambazo zinaweza kutazamwa kamawalivyofanya wenzetu kwa mashirika yao.

Mheshimiwa Spika, tusipoitazama ATCL kamauwekezaji wa kimkakati wa Kitaifa wenye nia ya kuwezeshasekta nyingine, hapo baadaye tutakwama, suala linawezakuchukuliwa kwamba ni biashara ya muda mfupi, lakinitukilipa mtizamo wa Kitaifa litakuwa na tija ambayo ndiyodhumuni kubwa ya kulifufua Shirika hili.

Mheshimiwa Spika, hivyo, badala ya kung’ang’aniatozo la gharama za kutua uwanjani na uongozaji ndege(landing and air navigation charges) ni vyema kuitazamaATCL kama sehemu ya utoaji huduma hizo isiyohitaji kulipiwa.

Mheshimiwa Spika, mwisho, lakini siyo kwa umuhimu,uwanja wa ndege wa Tanga unapaswa kufanyiwa ukarabatiili nasi tuweze kusafiri na kusafirisha bidhaa zetu kwendakwenye masoko ya Kimataifa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. Aidha, nawapongeza Mheshimiwa

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

Waziri, Naibu Mawaziri na timu yote ya Wizara katikautekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi pamoja nachangamoto za ufinyu wa fedha (bajeti).

Mheshimiwa Spika, katika mradi na ujenzi na reli yaSGR ni muhimu katika vituo vikubwa kama vile Morogoro, Dares Salaam na Dodoma kungejengwa maeneo makubwa yakuegesha magari (car parking) i l i kuwezesha abiriawanaotoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa usafiribinafsi, wanapofika Morogoro wanaweza kuegesha magariyao kwenye maengesho hayo, kisha kupanda SGR kwa safariya Dar es Salaam na hivyo hivyo wanaporudi.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Kidatu – Ifakara –Lupiro – Malinyi – Londo – Lumecha – Songea inapitia katikamaeneo muhimu kwa uchumi wa nchi pamoja na mradiSAGCOT (kilimo cha biashara) lakini barabara hii badohaijapewa kipaumbele.

Mheshimiwa Spika, barabara kipande ya Kidatu –Ifakara, ujenzi wa kiwango cha lami unasuasua sana. Sababuni uzembe wa Mkandarasi. Tunaiomba Serikali itafakari kamakweli Mkandarasi anao uwezo wa kumaliza kazi katika mudamuafaka. Aidha, Serikali ilete taarifa ni mkakati gani utafanyakatika kumsukuma Mkandarasi kumaliza kazi ndani ya muda.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Ifakara – Lupiro –Malinyi – Londo –Lumecha – Songea imefunguka tokamwaka 2017, lakini haipitiki kabisa kipande cha Mpepo -Londo kutokana na milima haijachongwa. Tunaiomba Serikaliirekebishe maeneo korofi yote ili barabara hii itumike kwakuwaunganisha wakazi wa Mikoa ya Morogoro na Ruvuma.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Ifaka – Lupiro –Malinyi – Londo imetolewa ahadi na Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli katika kampeni zake za uchaguzi mwaka 2015, lakinipia alirudia ahadi hiyo katika ziara yake mkoani MorogoroMei, 2018 kuanza kujenga kwa kiwango cha lami.

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

Mheshimiwa Spika, Serikali katika majumuisho,naomba itoe maelezo katika kutekeleza ahadi hiyo yaMheshimiwa Rais kwa wakazi wa Morogoro/Ruvuma.Ahsante.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Spika,barabara ya Mafinga – Mgololo, barabara ya Mgololo –Mtwango, barabara ya Kasanga – Mtambula – Nyigo ni zamuhimu sana katika kuinua uchumi kwa wananchi waMufindi. Kuna viwanda vya Chai, Mbao na Karatasi (MPM).Naomba Serikali ianze kujenga kiwango cha lami ili ziwezekupitika kwa mwaka mzima.

Mheshimiwa Spika, pia Serikali isimamie ujenzi wabarabara za vijijini ambazo zinatengenezwa na Wakala waBarabara Vijijini na Mijini (TARURA). Barabara ya Maguvani,Mtambale, Kilolo imeharibika sana wananchi wanashindwakusafirisha mazao yao. Barabara ya Nyanyembe hadi Idunda,barabara ya Malangali hadi Idunda, barabara ya Sawalahadi Iyegeya, barabara ya Maduma hadi Makugali zipo chiniya TARURA, zimeharibika sana. Naomba Serikali itengenezebarabara hii ili wananchi waweze kusafirisha mizigo yao, piakurahisisha shughuli zao za kila siku.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali ijenge minarakatika Kata ya Idete, Ihowanza, Idunda na Kiyowela. Maeneohaya hakuna mawasiliano kabisa, wananchi wanashindwakupata mawasiliano kiurahisi.

Mhesimiwa Spika, ahsante. Naunga mkono hoja.

MHE. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. Mheshimiwa Waziri pamoja na ManaibuWaziri nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya. Nashukurukwa miradi inayoendelea kujengwa Airport ya Mwanza, ujenziwa jumba la wasafiri ufanyike haraka kuondoa adha yawasafiri iliyopo kwa sasa.

Mheshimiwa Spika, usafiri wa ndege Dodoma –Mwanza ni vyema ukaanza kutokana na ukweli usiofichika

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

kuwa Kanda ya Ziwa ina abiria wengi sana wanaotumia usafiriwa anga. Nashukuru nimeona fedha imetengwa kwa ajili yafidia kwa wananchi wanaotakiwa kuondolewa eneo laviwanja. Ombi langu ni kwamba zoezi lisichukue muda mrefuili kuondoa kero iliyopo kwa sasa.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri nimeona fedhakidogo zimetengwa katika baadhi ya barabara. Ombi languni kwamba barabara ya Nyakato Veta – Igombe TX kilomita18 ina miaka mitatu; inajengwa kila mwaka kilomita moja.Naomba angalau ikamilishwe ili kuondoa mgongamano.

Aidha, barabara ya Airport – Kayenze – NyangugeKilomita 45 ijengwe kwa kiwango cha lami ili kurahisishawasafiri wanaoshuka uwanja wa ndege waendao Musomawaweze kutumia barabara hii badala ya kupita mjini ambakomsongamano unakuwa mkubwa sana.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa kivuko cha Kayenze –Baze unaendelea vizuri isipokuwa wasiwasi wangu ujenzi wamaegesho ya kivuko bado hawajaanza kujenga. Naombaangalau kivuko kinapokamilika kujengwa kiende sambambana ujenzi na ukamilishaji wa maegesho hayo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri waUjenzi alitembelea Jimboni na kujionea adha kubwa yawananchi wa Kigala Kata ya Buswelu kuwa na korongokubwa ambalo limekuwa mto, limekosa daraja na tayariwatoto walishachukuliwa na maji eneo hilo. Naomba ujenziwa daraja hilo ufanyike.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri waMawasiliano alitembelea Jimboni tukampeleka maeneoyenye kero ya mawasiliano, hakuna mawasiliano kabisa.Orodha ya maeneo tayari nilishakabidhi. Naomba utekelezajiufanyike ili kuondoa adha ya mawasiliano. Ahsante.

MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja ya bajeti ya Wizara hii ya Ujenzi na Mawasiliano.

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

Nampongeza Mheshimiwa Waziri na Timu yake kwa hotubana ripoti nzuri.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Kongwa (Hogoro) –Kibaya – Orkesimet – Oljoro – Arusha, ina mpango gani?Tunaomba tujengewe kwa awamu, Kongwa – Kibaya.Sababu ya barabara hii ni kusafirisha mazao toka Chemba,Kiteto, Kilindi na Handeni kwenda Dodoma na Dar es Salaam.Kwa kurahisisha barabara ya Babati – Kibaya – Dar es Salaam,Kondoa – Kibaya – Dar es Salaam, Kilindi – Kibaya – Dar esSalaam, Kilindi – Kibaya – Dodoma, Chemba – Kibaya –Dodoma.

Mheshimiwa Spika, mizigo mingi toka Dar es Salaamkwenda Babati, Simanjiro, Chemba, Kiteto, Kilindi, Kondoayote inapita hapa. Tusaidieni kwa sababu hii ni tooeconomical.

Mheshimiwa Spika, pia tunaomba kujua barabara yaHandeni – Kiberashi – Kibaya – Chemba – Kondoa – Singidaitajengwa lini kwa kiwango cha lami? Umuhimu wa barabarahii ni bomba la mafuta, bandari ya Tanga kwenda Kanda yaZiwa, kuunganisha Mikoa ya Tanga, Manyara Dodoma naSingida.

Mheshimiwa Spika, naomba Mawasiliano, tupatiweminara katika Kijiji cha Raiseli, Songambele, Kijunge, Rengatei,Sunya, Dongo, Mangungu na Namelok. Shahidi niMheshimiwa Dkt. Kalemani.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, naombakuchangia hoja hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu, hasakwenye transport economy. Muda umefika sasa Serikalikuhakikisha inajenga ama kukarabati viwanja vya ndegekatika Wilaya zote nchini. Kama bajeti hairuhusu, lazimaihakikishe basi mikoa yote ya nchi yetu ina viwanja vya ndegeambavyo vina hadhi za kupokea ndege za abiria ili kuwezakuharakisha safari toka sehemu moja ya nchi kwendanyingine.

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

Mheshimiwa Spika, mfano, Mkoa wa Mara ni mkoawenye fursa nyingi za kibiashara kama vile samaki toka ZiwaVictoria, biashara ya utalii maana tuna mbuga pale, tunamigodi na zaidi tuna kumbukumbu ya Baba wa Taidaambapo Mataifa mbalimbali wangependa kutembelea nakuweza kuingiza fedha kwenye mkoa wetu pamoja na Taifakwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, imekuwa ni aibu kwa kweli kuonamkoa ambao ametoka Baba wa Taifa hili na Rais wa Kwanzahadi leo hatuna uwanja wa ndege wenye hadhi na ambaoungepitika kwa maana ya ndege kutua muda wote.Nakumbuka kuna mwaka tulishashindwa kutua pale sababuya mvua na uwanja ule runway yake siyo ya lami na ilikuwani Kumbukumbu ya Kifo cha Mwalimu Nyerere.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikiongelea huu uwanjatangu Bunge la Kumi. Tunaomba sasa fedha ziende ili walewananchi walipwe fidia na hatimaye uwanja ukarabatiwena kupanuliwa ili wananchi wa Mara waweze kurahisishiwausafiri wa kutoka sehemu mbalimbali za nchi kama ndegeza Precision Bombadier na hata Dream Liner kutua. Naombasana Mheshimiwa Waziri wakati wa majumuisho atuelezewananchi wa Mara juu ya hatua ya uwanja wa Mara,Musoma.

Mheshimiwa Spika, noamba pia kuzungumzia kuhusuusikivu hafifu wa mawasiliano kwenye baadhi ya maeneoWilaya ya Tanze na hasa Jimbo la Tarime Mjini maeneo yaMofabiri, Nkende ambapo Mheshimiwa Naibu Waziri alifikana kuahidi kushughulikia hasa Kata ya Ketave, Nbende,Ngendoto na Kuyananyori. Vilevile Jimbo la Tarime Vijijini hasamaeneo ya Mpabani, Sirari na kule Nyamundu, ni muhimusasa hili lishughulikiwe maana tunapata Safaricom ya Kenya.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusu roundabout iliyopo Tarime Mjini ambayo ni junction ya kwendaSirari, Nyamagana, Mwanza na Soko Kuu. Ile round aboutinasababisha ajali nyingi sana na hasa kwa wageni maanasehemu ni finyu sana kuweza kuruhusu mzunguko wa magari

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

hasa makubwa (kama lori na mabasi). Pia ukifika unashindwakujua unaanzia wapi wala unaelekea wapi.Tumeshazungumzia sana hili kwenye Road Boad tangumwaka 2017 na TANROADS Mara iliahidi kulishughulikia.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kuondolewa ileround about na kuwekwa taa za barabarani ili ziwezekuongoza magari pale kama ile ya Mwenge inavyoruhusumagari ya kutoka Kawe/Lugalo, Mikocheni kwenda Ubungona kwenda Posta (hii junction ndiyo mfano). Hizi taa zitasaidiakuondoa ajali nyingi sana zinazopoteza maisha yaWatanzania lakini pia zitasaidia kupandisha hadhi Mji waTarime ambao unakua kwa kasi sana na upo jirani na nchiya Kenya.

Mheshimiwa Spika, vilevile tunaendelea kupata adhaya mtaro hasa kwenye barabara ya Nyamwaga kujaa hasamvua inaponyesha, mitaro midogo haikidhi haja kabisa.Vilevile, maungio ya barabara za TANROADS kuingia kwenyemitaa zinaachwa bila maingilio kwa barabara nyingine,kukatika kwa mawasiliano kati ya barabara za TANROADSna zile za TARURA.

Mheshimiwa Spika, naomba sana kujengewa darajala Nyandogo linalounganisha watu wa Kata ya Nyandogona Bunera pamoja na ukarabati au upanuzi wa daraja laMovi linaloenda uwanja wa ndege wa Magena.

Mheshimiwa Spika, mwisho ni kuhusu ATCL. Kwanzakabisa ieleweke kuwa naunga mkono uboreshaji wa Shirikala Ndege, ambapo kimekuwa ni kilio changu cha muda mrefuna tunatumia fedha za walipa kodi kulifufua. Naishauri Serikalikuiacha Menejimenti ya ATCL iwe huru kujiendeshakibiashara.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani imeshaurivyema. Ili Shirika liwe na ufanisi, Serikali haina budi kuwaachamenejimenti waweze kupanga na kulisimamia Shirika, maanawao ndiyo wana utaalam wa biashara hii ya ndege kulikosasa wanavyoingiliwa kibiashara, hili Shirika kuendeshwa

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

kisiasa na siyo kibiashara. Ona wenzetu wa KQ, Ethiopia,Emirate, Shirika lolote la operation, mawasil iano namengineyo.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, nimesomahotuba yako vizuri sana, lakini nasikitika miradi ya Jimbo namkoa wangu hazipo. Mradi wa lami Makao Makuu ya Jimbola kisasa (Mwandoya); kufanya upembuzi yakinifu wa mradiwa barabara ya lami kutoka Bariadi – Kisesa Mwandoya –Mwanhunzi, Bukundi (Sibiti) - Egiguno.

Mheshimiwa Spika, mradi huu ni wa kimkakati hasabaada ya ujenzi wa daraja la Sibiti kukamilika. Mradi huuutafungua uchumi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa Mara, Kagera,Mwanza, Simiyu na Shinyanga pamoja na nchi jirani za Kenyana Uganda.

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika,naungana na wote waliotangulia kupongeza kazi nzuriinayofanywa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.Mimi ni shahidi wa kazi inayoendelea barabara ya Sanya Juu- Kamwanga.

Mheshimiwa Spika, naomba baada ya mkataba waUjenzi wa barabara ya Kiboriloni –Kikarara, Tsuduni – Kidiakusainiwa, tunaomba sasa ujenzi uanze kwa kasi kabisabaada ya subira ya miaka zaidi ya saba.

Mheshimiwa Spika, vile vile tunaomba sehemu yabarabara ya kutoka Chuo cha Wanyamapori – Mweka hadilango la Mlima Kilimanjaro ijengwe kwa kiwango cha lami ilikuondoa kero kwa watalii, kwani ni ya charangawe na ninyembamba sana. Bahati nzuri mvua nazo katika eneo hiloni nyingi, hivyo kupelekea watalii kusukuma magari badalaya ku-enjoy safari.

Mheshimiwa Spika, pongezi kwa kazi nzuri iliyofanywakujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Marangu naMachame kuelekea Mlima Kilimanjaro, imesaidia kuboreshamazingira ya utalii.

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Mheshimiwa Spika, ushirikishwaji wa wanawake katikakazi za barabara ni jambo kubwa na zuri. Ni vizuri ushirikishwajihuu ufanyike kwenye Wilaya zote nchini. Kuna kazi za ujenziwa barabara katika wilaya zetu zinazoweza kutekelezwa nawanawake. Nashauri mwongozo wa Wizara kuhusu suala hiliuelekeze kila Wilaya kutoa mafunzo kwa wanawake nakuweka asilimia ya kazi ambazo lazima zifanywe nawanawake.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziriatakapohitimisha agusie mafunzo ya utunzaji barabara kwajamii. TANROAD na TARURA watoe mafunzo hayo.

Mheshimiwa Spika, kero kwa wale waliopita barabaraya Arusha - Moshi siku za karibuni watakubaliana nami kuwahii ni moja ya barabara yenye msongamano mkubwa wamagari. Inachukua muda wa saa tatu kusafiri umbali wakilometa 85 Tengeru - Himo.

Mheshimiwa Spika, tunaomba mazungumzo kati yaSerikali na JICA yakamilike mapema ili hatimaye upanuzi wabarabara kutoka Tengeru hadi Himo ufanyike kamailivyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimiamia moja.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, nianze nakumpongeza Waziri Mheshimiwa Eng. Kamwelwe, ManaibuMawaziri Mheshimiwa Kwandikwa, Mheshimiwa Eng. Nditiye,Makatibu Wakuu na Watendaji wa taasisi zote kwa kazi nzurisana zilizofanywa na kwa kuwasilisha hotuba hii ya bajeti.

Mheshimiwa Spika, naomba nichangie yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kuhusu ujenzi waviwanja vya ndege. Naishukuru sana Serikali hii ya Awamuya Tano kwa ahadi ya ujenzi wa viwanja kikiwepo kiwanjacha Nduli Iringa. Nilikuwa naomba Serikali ijitahidi pia kutoa

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

fidia kwa wakati kwa wananchi walioguswa na upanuzi wakiwanja hicho.

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusu Shirika la NdegeATCL. Niungane na wote walioipongeza Serikali kwa ununuziwa ndege sita. Napongeza pia kwa kuanzisha mfuko wandege katika kiwanja chetu cha Iringa, tunaamini sasa hatauchumi wetu kupitia utalii utaongezeka.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iangalieuwezekano wa kuwa na connection ya kiwanja cha Dodomaangalau kuwa na miruko mfano Mwanza – Dodoma, Mbeya– Iringa, Dodoma – Songea, Dodoma – Dar es Salaam ili kuwena urahisi wa Makao Makuu kufikika kwa urahisi na abiria niwengi. Vilevile bei za nauli za ndege ziangaliwe ili abiriawapande wengi.

Mheshimiwa Spika, Sekta hii ya Ujenzi inafanya kazinzuri sana hapa nchini. Napongeza sana kazi nzuri ya ujenziwa barabara nchini ikiwepo na mkoa wetu wa Iringa. KatikaMkoa wa Iringa naomba Serikali iangalie na kujengabarabara ya mchepuo itakayosaidia kuchepusha magarimakubwa sana kupitia katikati ya mji.

Mheshimiwa Spika, changamoto ya magarimakubwa kupita katikati ya mji, kwanza yanawezakusababisha ajali na hatari kubwa mno. Barabara ni finyu nakuna maduka hoteli na biashara ambazo zinafanyawananchi kuegesha magari na vyombo vya moto katikabarabara hiyo. Pia changamoto ni kwambawafanyabiashara wanashindwa kufanya biashara. Ni lini sasabarabara hiyo ya mchepuo itajengwa ili kuchepusha hayomagari kupita katikati ya Mji wa Iringa?

Mheshimiwa Spika, barabara ya Dodoma – Iringa,ukipita katika kona za Nyangoro, kuna maporomoko yamawe na wakati wa mvua yanaongezeka. Nimeshaulizasana maswali kuhusiana na changamoto hiyo: Je, ni mkakatigani unawekwa ili kuondoa changamoto hiyo?

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Spika, l ingine ni ujenzi wa reli.Naipongeza sana Serikali kwa kazi kubwa inayofanywa yakwa ujenzi wa reli hiyo. Ukikamilika utasaidia hata uharibifuwa barabara zetu ambazo zinaharibika kwa kubeba mizigomizito. Ujenzi huo mpaka sasa umefikia asilimia 50 phase oneDar es Salaam – Morogoro. Mradi huu ukikamilika, utaletaajira 10,000,000. Ni kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, nawapongeza kwa maboreshomakubwa mbalimbali ya sheria na elimu kwa bodaboda nabajaji. Pongezi kwa mtambo wa VTS, umesaidia kupunguzaajali barabarani. Changamoto kubwa ni abiria, wakipata ajaliwanapata taabu sana. Ni lini Serikali italeta sheria ya kuwekamiundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu?

Mheshimiwa Spika, TTCL wanafanya kazi nzuri sana.Je, yale madeni wanayodai katika taasisi za Serikaliwatalipwa kwa utaratibu gani?

Mheshimiwa Spika, UCSAF inafanya kazi nzuri sana,maeneo mengi yameweza kupata mawasiliano, lakini kunamaeneo bado hayajapata mawasiliano. Kwa mfano,Mafinga ni Kata ya Ideta, Ihowanza – Ipimo – Ihowasa – Kilolo– Kata ya Ihimbo.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika,kupitia njia ya maandishi nichangie bajeti ya Wizara hiimuhimu katika ujenzi wa Taifa imara. Rejea ya hotuba yaMheshimiwa Waziri, kwa sekta zote inaonyesha dhahiri kuwaujenzi wa uchumi wa viwanda uko kwenye uelekeo sahihi nakasi inayotakiwa.

Mheshimiwa Spika, naomba na kushauri TPAwakamilishe ujenzi wa mradi wa gati la Kyamkwikwi.Ukamilishaji wa mradi huu utawezesha sekta binafsi kujuamipaka ya mradi na kuweza kuendeleza eneo lililobaki.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi kwa Serikaliya Awamu ya Tano, kupitia Wizara hii kwa uwekezaji katika

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

vivuko. Naomba Wizara ifikirie maombi ya kupatiwa vivuko(pantoni/ferry).

Mheshimiwa Spika, kuanzia mwaka 2012 nimekuwanikiomba kivuko kwa ajili ya visiwa vya Bumbiile, Kelebe naGoziba. Kutokana na jitihada na mafanikio ya TPA kukamilishaujenzi wa gati Kyamkwikwi, ni busara kijamii na kiuchumikuweka vivuko ili tusaidie na kuokoa wananchi wanaosafiriziwani.

Mheshimiwa Spika, Tanzania upande wa Mkoa waKagera tunayo mahitaji ya uwanja wa ndege mkubwa.Tunaomba na kushauri Serikali kwa njia zote isaidie uchumiwa mkoa huu kwa kuwekeza katika upanuzi wa uwanja wandege wa Bukoba au tujenge uwanja mpya sehemu yaOmukajunguti. Hoja hapa ni kuwa na uwanja wa ndegeambao utawezesha ndege za mizigo kutua. Kagera ina fursaya kuvutia; viwanda vya samaki na uzalishaji wa matundana mboga kiurahisi kipindi chote cha mwaka.

Mheshimiwa Spika, nitoe pongezi na maombi kwaTANROADS kupitia kwa Mheshimiwa Waziri na watendajiwake wote. Barabara ya Muhutwe – Kamachumu – Mulebaujenzi unaendelea, hasa sehemu hii ya Muhutwe –Kamachumu. Naomba sehemu hii ya Muhutwe mpakaKamachumu isimamiwe ili ikamilike kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Spika, vile vile kipande cha Kamachumu/Ibuga mpaka Rutenge tunaomba kipigwe lami hasa ilesehemu ya Kamachumu Islamic School ambacho ni eneokorofi.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuwaombaTANROADS kupitia Wizara kuboresha barabara za TANROADSza Rutenge – Bulyakashaju – Rubale – Izimbya – Kara.Barabara hii ni muhimu kwa kuwa inaunga Wilaya ya Muleba,Bukoba na Karagwe. Eneo ipitapo barabara hii ni mkandamuhimu kiuchumi kwani inalengwa kuwekeza ufugaji wang’ombe wa kisasa na kilimo.

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuipongeza TPAkwa utendaji wa bandari wa sasa. Bandari hii kwa sasainafanya kazi masaa 24 kwa siku, siku saba za juma. Ushaurini Serikali kuhakikisha jamii yote za bandari (Port Community)kushirikiana ili kuongeza ufanisi mkubwa. Eneo moja dogo lakutolea mfano ni ukosefu wa ushirikiano wa TPA na TANROADkatika kupima mizigo, hali inayopelekea foleni eneo laKurasini.

Mheshimiwa Spika, ni rahisi magari yanayotokabandarini yapimwe yote uzito ndani ya eneo la bandari. Kazihii inaweza kufanyika chini ya wadau wote wenye maslahiikiwemo TANROADS na baada ya hapo magari yasipimweau kusimamishwa mpaka yatoke eneo la jiji. Faida mojakubwa ni kuondoa foleni hali ambayo itaongeza kasi.

Mheshimiwa Spika, yapo madai kuwa bandari zaNakura, Beira, Durban na hata njia za Angola ni washindaniwa bandari za Tanzania hasa Dar es Salaam. Kimsingi watejawote wanaopita njia hizo wamelazimika kupitia huko baadaya njia ya Tanzania kuwa na vikwazo. Nashauri Serikaliziangalie maslahi mapana na kwa pamoja naomba vikwazohivyo ili kuchangamka kwa biashara ya TPA kulete neemakwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, kwa niniSerikali inachelewesha miradi ya maendeleo yamiundombinu ya Mkoa wa Kigoma?

Mheshimiwa Spika, kwanza nitoe shukrani zangu zadhati kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kuendeleakuamini katika maendeleo ya Mkoa wa Kigoma na hususanMji wa Kigoma kwa kuwekeza katika ujenzi wa Bandari Kavuya Katosho pamoja na ujenzi wa Bandari ndogo za Kibirizi naUjiji.

Mheshimiwa Spika, miradi hii mitatu ikikamilikaitawezesha uwepo wa gati katika eneo la mji wa asili wa

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

kibiashara wa Ujiji na kuwezesha ndoto yetu ya kurejeshahadhi ya Ujiji katika maendeleo ya nchi yetu. Mradi waBandari kavu ya Katosho utawezesha mizigo ya nchi za DRC,Zambia na Burundi inayopitia bandari ya Dar es Salaamkuchukuliwa Kigoma na hivyo kurahisisha biashara na hichihizo jirani. Mamlaka ya Bandari pia wanajenga jengo la OSBC(One Stop Center) ambayo itarahisisha shughuli za ukusanyajikodi, biashara na uhamiaji.

Mheshimiwa Spika, ni matarajio yetu kuwa TRCwanajiandaa nao il i ukamilikaji wa miradi hii uendesambamba na uwepo wa reli ya kusafirisha kwa urahisi mizigoya Zambia, DRC na Burundi. Mambo haya yataingiza fedhakwenye mzunguko wa uchumi wa Mkoa wa Kigoma na kutoaajira kwa wananchi wenzangu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mkurugenzi Mkuuwa TPA kwa kuendeleza miradi hii na hii ni ishara ya imaniyake kwa ukuaji na maendeleo ya mji wetu na mkoa wetuwa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, vilevile napenda kumpongezaMeneja wa TANROADS Kigoma kwa kuwezesha mikataba yaBarabara ya Manyovu - Kasulu - Kibondo (mpaka Nyakanazi)kupitia ufadhili wa AFDB na barabara ya Uvinza - Darajanikupitia Kuwait Fund. Miradi hii ni muhimu kwa Mkoa waKigoma kwa kuwa itauunganisha Mkoa wa Kigoma na Mikoamingine na kurahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na shukrani hizo kwa watuwa TPA na TANROADS bado watu wa Kigoma wanalia kwakuwa ipo miradi yao ya msingi inayokwamishwa na Serikali.Licha ya Jumuiya ya Kimataifa kuelewa umuhimu wa Mkoawa Kigoma kijiografia na kiuchumi na hivyo kutoa fedha zamiradi ya maendeleo itakayochochea shughuli za kiuchumi,Serikali ya CCM imekuwa inavuta miguu kutekeleza miradihiyo. Nitawapa mifano michache ya namna Serikali ya CCMinavyohujumu Mkoa wetu wa Kigoma.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Mheshimiwa Spika, moja, Serikali ya Japanimeidhinisha mradi mkubwa wa kuboresha Bandari yaKigoma wenye thamani ya dola za Marekani milioni 40 (karibushilingi za Kitanzania bilioni 100), lakini kwa mwaka mzima sasaWizara ya Fedha haitaki kusaini mkataba ili zabuni itangazwena kazi ianze. Fedha hizi ni msaada, siyo mkopo.

Mheshimiwa Spika, pili, hoja ya Serikali ni kuwa Serikaliya Japan inataka msamaha wa Kodi ya VAT kwenye mradihuu, nayo haitaki. Sasa tunapewa mradi wa shilingi bilioni100, bure, kisha tunataka na VAT kwenye vifaa vinavyofumikakwenye mradi huo huo kweli! Serikali inaweza kupata mapatomengi mno ya kodi ikiwa mradi huu wa upanuzi wa bandariya Kigoma utafanyika. Kwa nini waukwamishe kwa mapatokiduchu tu ya VAT ya sasa? Kwa nini Serikali haioni pichakubwa?

Mheshmiwa Spika, tatu, Jumuiya ya Ulaya (EU) kupitiaBenki yao ya Uwekezaji (European Investments Bank)wameidhinisha fedha, dola milioni 20 sawa na shilingi zaKitanzania bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria katikauwanja wa ndege wa Kigoma na kuupanua uwanja ili ndegekubwa zitue kwa ajili ya kuunganisha nchi za maziwa makuuna Mji wetu. Tangu mwaka 2018 Januari, zabuniimetangazwa, mpaka leo kazi haijaanza wakati uwanja wandege wa Chato ambao haukuwa kwenye Bajeti ya Serikaliwala mpango wa maendeleo umejengwa na kukamilika.Serikali inataka kuwaambia nini watu wa Kigoma? Wao sioWatanzania kuliko ndugu zao wa Tabora?

Mheshimiwa Spika, nne, hata miradi ambayo fedhatayari zipo, haifanywi. Kwa mfano, Manispaa ya Kigoma Ujijituna mradi mkubwa wa kuweka pavements kwenye mitaayetu ili kutoa maarifa ya ufundi na kisha ajira kwa vijana.Lengo la mradi huu ni kutumia shughuli za ujenzi wamiundombinu kwa ajili ya kuongeza ajira kwa vijana namzunguko wa fedha kwa wananchi kwa vijana nawanawake kupewa mafunzo ya ujenzi wa hizo barabara zamawe (pavements) na kisha kupitia vikundi vyao kupewa kazihizo za ujenzi.

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

Mheshimiwa Spika, Serikali imegoma kusaini mkatabawa Mkandarasi Mshauri kwa ajili ya kufanya upembuzi nausanifu wa mradi huu pamoja na kuwa mfadhili wa mradi,Serikali ya Ubelgiji iko tayari na fedha ziko tayari. Mradi huuambao ungehusu kata nane za Manispaa ya Kigoma Ujijiungekuwa ni ‘Game Changer’ kwa uchumi wa Kigoma. Naounakwamishwa. Kwa nini?

Mheshimiwa Spika, watu wa Kigoma ni wavumilivusana. Wamevumilia kwa zaidi ya miaka hii 58 ya Uhuru waTanganyika na 55 ya uwepo wa Tanzania bila kuunganishwana mkoa wowote, wakatengwa kiuchumi. Uvumilivu huo unakikomo, hasa ikiwa ni kwa miradi yao ya miundombinu nauchumi inahujumiwa namna hii. Serikali isiwafikishe huko.

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Wizara hii ilipaswaichochee ukuaji wa uchumi, kwa nini uchumi unadumaa?

Mheshimiwa Spika, mgawo wa bajeti ya maendeleokwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa miakaminne ya Serikali ya Awamu ya Tano ni ufuatao: 2016/2017shilingi trilioni 4.8 ambayo ilikuwa 40.3 % ya bajeti yote yamaendeleo ya shilingi trilioni 11.8. Mwaka 2017/2018 shilingitirilioni 4.9 ambayo ilikuwa 40.8 % ya bajeti yote ya maendeleoya shilingi trilioni 11.9. Mwaka 2018/2019 shilingi trilioni 4.1ambayo ilikuwa 34.5 % ya bajeti yote ya maendeleo ya shilingitrilioni 12.0.

Mheshimiwa Spika, mpaka mwaka huu wa fedhaunaoisha 2018/2019 Bunge litakuwa limeidhinisha kwa Wizarahii jumla ya shilingi trilioni 13.8 katika miaka mitatu ya bajeti.Ni wastani wa 38.5% ya bajeti yote ya maendeleo kwa miakahii mitatu. Tukipitisha bajeti ya 2019/2020 tutakuwatumewekeza jumla ya shilingi trilioni 40.6 na kati ya hizo shilingi18.7 zitakuwa zimekwenda Wizara hii ya Miundombinu. Hii nisawa na 46% ya Bajeti yote ya maendeleo kwa miaka minnekati ya mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, ni halali kabisa kwa Wabungekuhoji: ajira ngapi za kudumu zimetengenezwa kutokana na

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

uwekezaji huu? Sekta zipi nyingine za uchumi zimechochewa(multiplier effect) kutokana na uwekezaji huu? Kwa Mfano,viwanda vingapi vya chuma vimeanzishwa? Pato la Taifalimeongezeka kwa kiasi gani kutokana na uwekezaji huu?Watanzania wangapi wameondokana naumasikini? Mapato ya Serikali yameongezeka kwa kiasi gani?

Mheshimiwa Spika, kikawaida ni Bajeti ya Wizara hiindiyo ambayo matumizi/manunuzi yake hutumikakuchochea shughuli za kiuchumi na kupeleka fedha kwawananchi kupitia miradi mbalimbali ya ujenzi. Hali iko hivyoduniani kote, lakini hapa nchini kwetu hali ni tofauti, manunuzimengi ya ujenzi yanayofanywa kupitia Wizara hiihayajachochea ukuaji wa uchumi, bali namna yalivyofanyikayamekuwa ni sababu ya kudumaza uchumi.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii ilirithi Bajeti ya Serikaliya Awamu ya Nne ya Mwaka wa Fedha wa 2015/2016ilipoingia madarakani Novemba 5, 2015. Katika wakati husikakasi ya mzunguko wa fedha nchini (M3) ilikuwa ni 15%. Hivyokila shilingi nchini ilibadilisha na wastani wa mikono 15 kwenyematumizi ya kiuchumi. Ripoti ya BOT ya Mwezi Machi, 2019(inayoelezea hali ya Februari, 2019) inaonyesha kuwa M3 kwasasa ni 3% tu. Mzunguko wa fedha umepungua mno.

Mheshimiwa Spika, kwa miaka mitatu tumepitishaTanzania Shillings 1.5 trillion kununua ndege. Fedha zote hizozimekwenda nje ya nchi, hakuna hata shilingi moja kati yahizo ambayo imerudi nchini. Hiyo ni moja ya sababu yakupungua kwa mzunguko wa fedha nchini.

Mheshimiwa Spika, tuna ujenzi wa SGR. Mkataba waUbia Kati ya Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki na kampuniya Construção Africa SA ya Ureno, naambiwa Kampuni hiiimejitoa kwenye mkataba huu na kwamba kuna Kampuninyingine iko kwenye huu mradi. Ikumbukwe ni hiyo kampuniya Ureno ndiyo yenye uzoefu wa ujenzi wa reli. Je, mbia mpyawa Yapi Merkezi ni Nani? Uwezo wake ukoje? Tumefanya DueDiligence ili mambo ya Indo Power ya kwenye koroshoyasijirudie? Taifa linapata nini?

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

Mheshimiwa Spika, tumerudia makosa tuliyoyafanyawakati wa ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kuja Dares Salaam. Mwezi Septemba, 2012, Wizara ya Fedha kwaniaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naBenki ya Exim ya China walitiana saini makubaliano ya mkopowa miaka 33 yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni1.225 kwa riba ya 2% kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesilinalounganisha eneo la Msimbati na Mnazibay mpaka Dares Salaam.

Mheshimiwa Spika, Kampuni zilizoshinda zabuni yaujenzi huu ni China Petroleum Technology and DevelopmentCorporation (CPTDC) na China Petroleum PipelineEngineering Corporation (CPPEC), ambapo kila kitukilichotumika kwenye ujenzi wa bomba hili kilitoka China nahakuna ushahidi wa kitaalam wa ujenzi huo ulioachwa nchini.Ndicho tunachofanya kwenye SGR. Mbaya zaidi kwa sasatunatoa hela ndani kupeleka Uturuki na za nje tunazozikopani kutoka mabenki ya kibiashara yenye riba kubwa.

Mheshimiwa Spika, reli inahitaji chuma na chuma chapua (Iron and Steel), mbao ngumu, wahandisi na mafundimchundo wengi, vifaa vidogo kama screws na kadhalika.Je, Serikali imefungamanisha ajenda ya viwanda na ujenziwa reli? Serikali inaweza kutuambia viwanda vingapi vyaugavi kwenye bidhaa za ujenzi wa reli vimejengwa?

Mheshimiwa Spika, viwanda vingapi vya matarumavimejengwa nchini? Tunaagiza mataruma na hata screws zakufungia mataruma kutoka nje ya nchi. Ndiyo maana trilionizote hizi tunazoipa Wizara kwa miaka hii mitatu hazisaidiiukuaji wa uchumi.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika,naomba nianze mchango wangu kwa kumshukuru MwenyeziMungu kwa uhai na afya njema. Pia, nachukua fursa hiikuwapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri, KatibuMkuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wenyeviti wa Bodi zote zilizokokwenye Wizara hii na Wakurugenzi Watendaji wote wa Taasisizote zilizopo kwenye Wizara hii kwa kazi kubwa ya kumsaidia

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Mheshimiwa Rais katika kuwatumikia Watanzania.Nawaombea dua kwa Mwenyezi Mungu awape umri mrefuili waweze kutimiza ndoto ya Mheshimiwa Rais ya kuonaTanzania mpya. Mwenyezi Mungu awabariki sana.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Nachingwea – Liwaleni barabara muhimu sana kwa Wilaya ya Liwale, kwani ndiyobarabara pekee inayoiunganisha Wilaya ya Liwale na MakaoMakuu ya Mkoa wa Lindi. Naishukuru Serikali kwa kuanzaupembuzi na usanifu wa kina kwa barabara hii. Nashauri kazihii iambatane na utafutaji wa fedha ili kuweza kujengabarabara hii kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Nangurukuru – Liwaleni barabara ya kiuchumi kwa Wilaya ya Liwale. Usafirishajiwa mazao kutoka Liwale hadi Dar es Salaam kupitia Lindikuna kilometa zaidi ya 750 ukilinganisha na kilometa 500ukipitia barabara ya Liwale to Nangurukuru. Hivyo, utaonaumuhimu wa barabara hii ni mkubwa sana kwa uchumi waWana-Liwale na nchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, nashukuru tena kuonakwenye bajeti hii kumetengwa shilingi milioni 300 ili kuanzaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina kama ilivyo barabaraya Nachingwea – Liwale. Hii pia Wizara ianze kutafuta fedhaili hatimaye nayo pia iweze kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mawasiliano,nashukuru kwa kupatiwa mawasiliano kupitia kampuni yaHalotel kwa kutujengea minara kwenye kata tisa ambaposasa kwa kiwango kikubwa upo unafuu kidogo, lakini badokuna shida ya mawasiliano katika Vijiji vya Ndapata, Mkutano,Kikulyungu, Nahoro, Kipelele, Mtungunyu na Mtawatawa. Vijijihivi hali ni mbaya sana katika mawasiliano ya simu.

Mheshimiwa Spika, Reli ya TAZARA bado ni reli muhimusana kwa nchi yetu. Kwa upande wa Zambia wao kwa relihii siyo kipaumbele chao tena pamoja na kuwa uongozi wareli hii kwa kiasi kikubwa unamilikiwa na upande wa Zambia.Wazambia wamekuwa wakifanya vitendo vya kuhujumu reli

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

hii kwa makusudi. Hivyo basi, imefika wakati Serikali yetu ifanyemapitio ya Sheria ya Uendeshaji wa Reli ya TAZARA. Hatua hiini muhimu na iende sambamba na kuifutia madeni au kuipamtaji ili iweze kujiendesha.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Mabaharia (DMI) nichuo kilichosahauliwa kwa muda mrefu ndiyo maana uwepowa chuo hiki hata kwa jamii hautambuliwi pamoja na kuwanchi yetu imezungukwa na bahari na maziwa makuu. Sektaya Uvuvi na Usafiri wa Majini una mchango mdogo katikanchi yetu kutokana na kupuuza chuo hiki muhimu kwa uchumiwa nchi yetu. Nashauri Serikali ianze sasa kuimarisha chuohiki ikiwa ni pamoja na kukitangaza, kwani sasa chuo hikihakitambuliwi katika jamii ya Watanzania.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Usafirishaji (NIT) ni chuomuhimu sana kwa sasa, hasa kwa kuwa nchi yetu inakwendakuimarisha Sekta ya Uchukuzi kwa kujenga reli ya kisasa,ununuzi wa ndege na ujenzi wa meli kwenye maziwa makuu.Hivyo basi, Serikali ione umuhimu wa kuimarisha chuo hiki,kwani ndiyo chuo kinachokwenda kupika wataalam katikaSekta ya Uchukuzi. Chuo hiki ni lazima kipewe fedha zakutosha ili kiweze kujiimarisha kupata wataalam.

Mheshimiwa Spika, sera ya kuunganisha mikoa yetukwa barabara za lami ni jambo linalopaswa kupewakipaumbele kwa mikoa yote kwani bado kuna mikoaambayo hadi leo haijaunganishwa siyo tu kwa barabara zalami, hata kwa barabara za changarawe. Mfano, Mkoa waMorogoro na Mkoa wa Lindi, mikoa hii, pamoja na kuwamikoa jirani lakini pia ni mikoa muhimu sana kwa kukuzauchumi wa mikoa hiyo miwili. Hivyo, naiomba Serikali kufanyakila iwezavyo kutekeleza sera hii ya kuunganisha Mikoa yaLindi na Morogoro kwa barabara ya Liwale – Mahenge(Ulanga).

Mheshimiwa Spika, Uwanja wa Ndege wa Lindi,pamoja na kuwa moja ya viwanja vya zamani nchini,hakijapewa kipaumbele. Hii ni kudumaza maendeleo yaMkoa wa Lindi sambamba na Bandari ya Lindi. Nashauri

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Bandari ya Uvuvi ya Kanda ya Kusini ikajengwe Lindi ili kuinuauchumi wa Mkoa wa Lindi.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo yote hapo juu, naungamkono hoja hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu.

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kupata nafasi nami niweze kuchangia Wizara hii muhimukwa manufaa ya wananchi wa Mkoa wa Mara naWatanzania wote kwa ujumla. Tunaona bajeti kwa miakamitatu zimetengwa shilingi trilioni 13, nataka Serikali ituelezetunapata ajira kiasi gani na return yake ni nini? Fedha nyingizinaenda kwenye upembuzi yakinifu, sijui huu upembuziyakinifu utaisha lini ili ujenzi kamili uweze kuanza kwa sababuWilaya ya Rorya, TARURA haijapata fedha za maendeleo yabarabara kwa miaka miwili mfululizo sasa.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Musoma – Busekelani ya kilometa 42, lakini fedha zilizotolewa ni kilometa tanotu, bado kilometa 37. Zitaishaje bila fedha? Naishauri Serikaliipeleke fedha za kumalizia hizo kilometa 37 zilizobakia.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Wanyere – Kitaryoimekatika, hakuna mawasiliano sababu ya daraja. Kwasababu Wizara hii imetengewa fedha nyingi, naishauri Serikaliifanye jitihada za haraka kuhakikisha inatengeneza barabarahii na daraja ambalo limeshaua watoto zaidi ya 20 ili kunusurumaafa mengine yasitokee.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Mara una miradi viporovingi sana kama vile Bunda – Kisorya, Makutano – Sanzate,Mugumu – Tabora B zinazohitajika fedha ili kuweza kukamilishamiradi hii viporo.

Mheshimiwa Spika, kuna round about ya Tarimeinasababisha ajali za mara kwa mara. Naishauri Serikaliiondoe hiyo round about badala yake ziwekwe taa zakuongozea kama vile Barabara ya Mwenge kwendaMikocheni, Kawe, Mjini, Ubungo ili kuepusha ajali zinazotokeamara kwa mara.

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Mara una uwanja wandege ambao unapanuliwa (unaongezwa), kitu ambachokinaathiri wananchi wanaozunguka (waliopakana) nauwanja huo kwani wananchi hawa walishafanyiwa tathminitakribani mwaka na miezi minne, lakini wananchi hawa hadisasa hawajui hatma yao kwani tathmini imefanyika bila waokujua nyumba zao zimefanyiwa tathmini ya shilingi ngapi.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali ikarudie kufanyatathmini na suala hili liwe shirikishi kwa wananchi wenyewena Serikali iwatengee (iwape) eneo lingine la kwendakujenga nyumba nyingine pale ambapo watakuwawameshalipwa fedha za kupisha uwanja wa ndege.

Mheshimiwa Spika, TBA hawafanyiwi ushindani namakampuni binafsi ndiyo maana kazi za TBA ni substandard(kazi nyingi za Serikali zinafanywa na TBA matokeo yakemajengo mengi hayakidhi viwango). Mfano mradi wanyumba Bunju zinazojengwa na TBA haziko competitive hatakidogo kwani haziwezi kuingia kwenye ushindani kwa vilehazina viwango. Kwanza hazina (hakuna) social serviceskama vile zahanati, shule, barabara na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kwa nini nyumba hizi hazinunuliwi?Ni kwa sababu bei iko juu sana kulinganisha na ubora wanyumba zenyewe, kwani hadi sasa nyumba zilizonunuliwa nichache sana, nyingi hazijanunuliwa, zimekaa tu nakuendelea kuharibika. Naishauri Serikali, hizi nyumbazipangishwe badala ya zinavyokaa zenyewe bila watu.

Mheshimiwa Spika, lingine katika Sekta ya Ujenzi; katiya wakandarasi Watanzania asilimia 80, ni wakandarasiasilimia 20 tu ndiyo wanaopata kazi. Ni aibu kwa nchi yetuya Tanzania. Ushauri wangu ni kwamba Serikali itoe ujuzi kwaWakandarasi wetu ili tuweze kuwatumia kuokoa pesazinazokwenda nje.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja kwa mchango ufuatao:-

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Mheshimiwa Spika, naomba barabara ya Kitosi –Mwampembe yenye urefu wa kilometa 67 ambayo nimkombozi kwa Tarafa ya Wampembe ichukuliwe na Serikaliau la, iwe inapewa fedha ya kutosha toka TANROADS. Wizarainatoa shilingi 90,000/=, inatosha nini? Tafadhali naomba tuwetunaipa fedha zaidi.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Nkara – Kala ni yaHalmashauri/TARURA lakini haipewi fedha. Adhazinazowapata wananchi wa Kata ya Kala inatakiwaiondolewe na Serikali. Tafadhali ongezeni fedha TARURA iliiwe na uwezo wa kusaidia wananchi vijijini.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Katongoro kwendaNinde haipitiki kabisa, kisa hakuna fedha ya kuhudumiabarabara hiyo ya kwenda Ninde na kata yote isifikiwe.Tafuteni fedha kuimarisha TARURA.

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusu mitandao ya simu.Naomba vijiji vifuatavyo vipate mawasiliano ya simu: Kijiji chaKasapa, Kata ya Sintali, Kijiji cha Msamba Kata ya Ninde, Kijijicha Kisambara Kata ya Ninde, Kijiji cha Lupata Kata yaWampembe, Kijiji cha Izinga Kata ya Wampembe na Kijiji chaMlalambo Kata ya Kizumbi.

Mheshimiwa Spika, Serikali ijenge magati ya melikatika vituo vya Namansi (Kijiji), Kijiji cha Ninde, Kijiji chaMsamba na bandari katika Mji mdogo wa Wampembe. Mjihuu una biashara za kutosha na wasafiri wengi. Hali ilivyoinapokuja meli ni hatari kwa wasafiri na matukio kadhaayanatokea.

Mheshimiwa Spika, nashauri Bandari ya Wampembena barabara toka Sumbawanga hadi Wampembe ikijengwani rahisi kupata soko la nafaka ya mahindi Kongo Kusini.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika,nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri,

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

Katibu Mkuu na wafanyakazi wote wa Wizara kwa kazi kubwana ngumu wanayoifanya. Hongereni sana.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wananchi waUrambo, tunashukuru sana barabara iliyokamilika katikati yaMji wa Urambo. Ahsanteni sana kwa kuongeza uzuri wa mji.Barabara hii nzuri ni muhimu sana ikaunganishwa vizuri paleinapoungana/kuchepuka kutoka barabara inayoendeleaKigoma.

Mheshimiwa Spika, tunaomba round about kwanzakwa usalama wa magari na waenda kwa miguu na pili kwamwonekano mzuri wa barabara inayoingia mjini.

Mheshimiwa Spika, tunaomba minara ya simu katikamaeneo ambayo hayana mtandao wa simu; na orodha yakata na vijiji imeletwa Wizarani.

Mheshimiwa Spika, tunaomba maombi mawili yaround about na minara yafikiriwe kwa manufaa ya wananchina Taifa kwa ujumla. Ahsante sana.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, napendakuchangia Wizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilianoambayo ni Wizara muhimu sana kwa maendeleo ya Taifaletu kwenye maeneo tofauti ili kuinua uchumi kama ifutavyo:-

Mheshimiwa Spika, TARURA waongezewe fedha.Suala hili limekuwa na changamoto kubwa sana, kwaniTARURA wana barabara nyingi za mitaa na vijiji lakiniwanashindwa kumaliza kazi hizi kwa muda muafaka kwasababu ya fedha kidogo.

Mheshimiwa Spika, lingine ni usafiri wa meli kwa ZiwaTanganyika. Kumekuwa na changamoto kubwa ya usafiri wamajini kwa wananchi wanaotumia Ziwa Tanganyika kwausafiri na biashara. Naomba kujua Serikali imefikia wapi katikasuala la Meli ya MV Liemba?

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko yaWakandarasi wengi kutokulipwa fedha zao kwa wakati. Kwanini Serikali isiwalipe Wakandarasi ili kuleta ufanisi kwa kazina miradi wanayopewa ili kuinua uchumi wa nchi?

Mheshimiwa Spika, ni vyema kufuatilia na kujua uwezohalisi wa Wakandarasi kabla ya kupewa tenda ili kuepushahasara zinazoweza kujitokeza kwa Taifa, kwani kumekuwana malalamiko mengi sana na kupelekea vitendo vya rushwana kupelekea hasara kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, suala la ujenzi wa viwanja vyandege ni vyema liangaliwe kwa umakini kwa kuangalia ainaya watu kwa maeneo ambayo wana uhitaji wa viwanja vyandege ili kuweza kukuza uchumi kwa eneo husika na Taifakwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, suala la TBA bado kunachangamoto; miradi mingi wanayopewa haikamiliki kwawakati. Pia napenda kuishauri Serikali ipunguze miradi kwaTBA na badala yake wapewe watu wengine ambapo kukiwana ushindani huleta ufanisi mzuri wa kazi na uharaka.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la watu kuwekewaX za kijani na nyekundu: kumekuwa na mkanganyiko katikautekelezaji wa suala hili pale inapotokea nyumba moja inaalama mbili ya kulipwa na kubomolewa, wanawaambiawananchi wabomoe. Je, suala hili likoje? Tunaombaufafanuzi.

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika,pongezi kwa Serikali kwa upana wake na Wizara kwa namnaya pekee kwa kazi kubwa na ya mfano wanayoifanya,hongera sana.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Tunduru Kaskazini nabajeti ya mwaka 2019/2020; nashukuru kwa miradi ifuatayoambayo imetengewa fedha. Ukurasa wa 348, daraja F/Mbanga – shilingi milioni 20 (ukamilishaji). Nina mashaka na

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

utoshelevu wa fedha hizi kukamilisha kazi iliyobaki kwani badokazi ni kubwa.

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 348 - matengenezoya barabara Mjimwema – Ngapa - Tunduru/NachingweaBoarder – shilingi milioni 60. Barabara hii ni muhimu sabakuunganisha Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Lindi. Tunaombaijengwe kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 348 - ujenzi wa Darajala Ngapa katika barabara ya Mindu – Ngapa - Nachingwea/Tunduru Boarder – shilingi milioni 60. Jumla ya fedha zote nishilingi milioni 140. Kwa kulinganisha na mahitaji katika Jimbolangu, pamoja na kushukuru kwa tulichopata tunaombayafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, mahitaji ya miradi muhimu sana.Barabara ya Mkoa – Mjimwema - Nachingwea Boarder.Tunaomba ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami,likiwemo Daraja la mto Lumesule.

Mheshimiwa Spika, barabara ya mchepuo (Tunduru-By-Pass), ni bahati mbaya haikupata umuhimu katika bajeti,tunaomba izingatiwe.

Mheshimiwa Spika, Tunduru Round about; hapa kunabarabara inayokwenda Songea, Mtwara na Msumbiji.Makutano ya barabara katika eneo hili, wakati wa ujenzi wabarabara za Tunduru – Matenanga – Namtumbo – NA –Tunduru – Nakapanya – Mangaka - Taaluma na umuhimu,ikiwemo usalama. Tunaomba yafanyike marekebisho yakitaalam.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mironde – Kalulu -Selous Game Reserve, ni barabara ya kimkakati; katika ziarayake Waziri Mkuu akiwa Kalulu alielezea umuhimu wake nakusisitiza kwamba Serikali itaijenga.

Mheshimia Spika, nashukuru sana.

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, Wizara yaujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ina majukumu yanayogusasekta kama tatu zenye kuwezesha maendeleo ya nchi nawananchi. Katika aya ya 26 ukurasa wa 15, Waziri ameelezaujenzi wa barabara ya Dar es Salaam – Chalinze, kilomita144 haujaanza kutokana na maamuzi ya Serikali kusogezambele utelekezaji wa mradi huu ili kukamilisha kwanza miradihii inayoendelea, ni vyema katika majumuisho Serikali ikaelezaimesogeza mbele mradi huu mpaka lini.

Mheshimiwa Spika, aidha, ni kwa nini Serikali imeamuakusogeza mbele wakati ambapo imesema mara kadhaakwamba mwaka 2011 kwamba mradi huu ungetekelezwakwa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP) na ungekuwana barabara za kulipia ili kurejesha gharama za ujenzi ambazozingeingiwa na sekta binafsi katika ujenzi.

Mheshimiwa Spika, katika aya ya 44, ukurasa wa 24,Serikali ieleze sababu ya barabaa za Kimara - Korogwe MajiChumvi (kilomita tatu) na sehemu ya Goba - Madale (kilomitatano), ujenzi wake kwenda taratibu. Aidha, ni kwa nini Serikaliimechukua kipande kidogo tu cha Mloganzila – Kisopwa(kilomita moja) kati ya kilomita 14.66 za barabara ya Kibamba– Kisopwa – Kwembe - Makondeko. Kwa kasi hii ndogoitachukua miaka takribani 14 kwa barabara hiyo kukamilika.

Mheshimiwa Spika, katika aya ya 54, ukurasa wa 30,imeelezwa kuwa ujenzi wa barabara ya juu (interchange)katika barabara ya Ubungo umefika asilimia 28. Hii inaoneshakwamba kasi ya ujenzi ni ndogo sana. Wizara ikumbukekwamba mwezi Machi, 2017 wakati na uzinduzi wa ujenziMheshimiwa Rais aliagiza kwamba ujenzi wa barabara yajuu ya Ubungo ukamilike ndani ya miezi 30. Kwa agizo hiloujenzi unapaswa kukamilika mwezi Agosti, 2019, hivyo kwaasilimia 28 mwezi Mei ni kiwango cha chini sana chautekelezaji. Hivyo Wizara itoe maelezo ni mikakati ganiimewekwa kuharakisha ujenzi ili ukamilike kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, kwenye aya ya 60, ukurasa wa 33,Waziri ameeleza kuwa upanuzi wa barabara kwa njia nane

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

kwa sehemu ya Kimara - Kiluvya (kilomita 19.2) unaendeleaambao utarahisisha pia upanuzi wa Madaraja ya Kibamba,Kiluvya na Mpiji. Hata hivyo, Waziri hajaeleza ujenzi wabarabara umefikia hatua gani, eneo ambalo ni vyemaakalieleza katika majumuisho. Katika kipindi cha uzinduziuliofanywa na Rais ambapo walishiriki, kasi ya ujenzi kablana baada ilikuwa kubwa. Hata hivyo, kwa sasa kasiimepungua, hivyo ni vyema Wizara ikafuatilia kwa karibukuwezesha ujenzi kufanywa kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, aidha, naomba mkandarasi kamaalivyofanya kwa eneo la Kibamba CCM kusawazisha eneokwa ajili ya kituo cha muda cha daladala afanye hivyo katikaeneo la Kiluvya. Eneo la kusimama daladala lilishawekwa,Wizara ihakikishe SUMATRA inasimamia daladala zifike Kiluvyabadala ya kuishia Kibamba CCM na kufanya wananchi waKiluvya waingie gharama kubwa za kupanda mabasiyanayokwenda Kibaha, Mkoani Pwani.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Rais kuhusufidia ya wananchi kupisha ujenzi wa barabara hii, naombaWizara irejee hukumu ya kesi ya wananchi wa Mbezi ambaowalifungua kesi Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ambapomahakama ilitamka wananchi wanastahili fidia.

Mheshimiwa Spika, katika aya ya 73, ukurasa wa 40,kwenye hotuba ya Waziri amezungumzia kuhusumiundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pilihadi ya tano. Naomba majibu ya Serikali katika majumuishoni awamu ipi hasa ya ujenzi itahusisha ujenzi wa miundombinuya mabasi yaendayo haraka kwa kipande cha kutoka Kimarampaka Kiluvya?

Mheshimiwa Spika, il i kutoiingiza nchi kwenyegharama kama iliyotokea katika maeneo mengine ambapolami na miundombinu mingine imelazimika kuvunjwakuwezesha kujengwa kwa miundombinu ya mabasiyaendayo haraka, ni vyema upanuzi wa sasa wa barabaraya Morogoro kutoka Kimara mpaka Kiluvya ukahusisha piaujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka.

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umekuwaukikabidhiwa ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali. Katiya kazi ambazo TBA imefanya hivi sasa ni pamoja na ujenziwa Makao Makuu ya Wilaya Mpya ya Ubungo. Naomba TBAiharakishe kukamilisha ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya.Aidha, naomba TBA izishauri mamlaka zinazohusika ili ujenzihuo unaofanyika katika Kata ya Kwembe, Mtaa wa Luguruniuhusishe pia ujenzi wa Ofisi ya Mbunge ambayo katikamichoro ya sasa haijawekwa.

Mheshimiwa Spika, TBA pia ikutanishwe na Shirikia laNyumba (NHC) kujadiliana kuhusu uendelezaji wa Mji waViungani (Satellite Town) wa Luguruni ili majengo ya Serikalina nyumba za viongozi katika eneo hilo TBA ifuatilie kwakaribu ujenzi uanze. Serikali ililipa muda mrefu fidia katika eneohilo lakini shughuli za uendelezaji zimesimama.

Mheshimiwa Spika, juu ya kasma 4138 ya kupunguzamsongamano katika Jiji la Dar es Salaam (De-congestion ofDar es Salaam Roads) kipande cha Goba - Makongo kilomitanne kimetengewa milioni 310 tu ilihali kuna kipande chabarabara ambacho kwa muda mrefu hakijawekewa lami.Naomba kiwango cha fedha kiongezwe kuwezesha eneolote lililobaki kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, kwenye kasma 4161 kuhusuMadaraja ya Juu (Dar es Salaam Road Flyovers) kwa upandewa Ubungo Interchange zimetengwa milioni 145 tu kwaupande wa fedha za ndani. Napendekeza kiwangokiongezwe kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo kwenyemkataba.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kasma 4132 juu ya fedhaza Mfuko Mkuu wa Serikali katika kutekeleza miradi ya mkoabarabara ya Kimara – Bonyokwa – Kinyerezi yenye kilomitambili umetengewa katika bajeti milioni 60 peke yake wakatibarabara hii ina hali mbaya. Naomba TANROADSwatembelee barabara hii na kufanya matengenezo

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

yanayostahili. Hali iko hivyo pia kwa barabara ya Goba –Matosa - Temboni.

Mheshimiwa Spika, katika kasma 2326 kumetengwamilioni 150 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina(feasibility study and design) kwa ajili ya ujenzi wa barabaraya juu (interchange) Mbezi mwisho kuelekea eneokutakapojengwa kituo cha mabasi ya mikoani. Naombamchakato huu uharakishwe ili uende sanjari na ujenzi wa kituounaoendelea pamoja na upanuzi wa barabara kuwa njianane.

Mheshimiwa Spika, fedha za Mfuko wa Barabarazitatumika pia kuboresha kwenda DSD barabara ya Kunguru- TATEDO (kilomita tano) ambapo kumetengwa milioni 120.Naomba hatua hiyo iende mbele zaidi kwa kujenga darajakatika eneo la Muungano, Kata ya Goba katika sehemuinayounganisha na Salasala.

Mheshimiwa Spika, katika kiambatisho namba 5(B-2),ukurasa 381, Waziri ameeleza barabara ambazo zitafanyiwamarekebisho ya muda maalum (period maintenance) kwakutumia fedha za Mfuko wa Barabara. Hata hivyo, katikaorodha hiyo hakuna hata barabara moja ya Jimbo laKibamba kwenye Kata sita za Kwembe, Msigani, Mbezi Luis,Goba, Saranga na Kibamba. Hivyo ni vyema Wizaraikaongeza katika orodha hiyo barabara muhimu za Jimbo laKibamba zenye kuunganisha Mkoa wa Dar es Salaam naMkoa wa Pwani na zenye kuunganisha Wilaya ya Ubungona Wilaya za Kinondoni na Ilala katika Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, kati ya barabara ambazo nimuhimu TANROADS ikazichukua na kuzifanyia matengenezoya haraka ni Temboni kwa Msuguri – Msingwa ambayoinaunganisha mpaka Wilaya ya Ilala. Kihistoria, barabara hiiTANROADS iliwahi kuitengeneza lakini baadhi ya wananchiwakaenda mahakamani miaka mingi nyuma hali iliyofanyaTANROADS kuacha kuihudumia kwa muda mrefu. Mgogorohuo umemalizika lakini TANROADS na TARURA badowanarushiana mpira mpaka sasa kuhusu kuihudumia. Pamoja

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

na kuwa TARURA wameanza matengenezo madogo,naomba barabara hii ichukuliwe na TARURA ili ifanyiwematengenezo makubwa na hatimaye ijengwe kwa kiwangocha lami.

Mheshimiwa Spika, kwenye sehemu (b) juu yabarabara za mikoa za changarawe/udongo. Matengenezoya barabara zilizopo kwenye Jimbo la Kibamba yamekuwayakifanyika lakini sio kwenye kiwango cha kuridhisha.Barabara hizo baadhi zimetajwa kwenye ukurasa wa 39o zaKibamba Shule – Magoe Mpiji na Makabe Junction – MbeziMsakuzi. Naomba katika majumuisho, Serikali ieleze ni liniitafanya matengenezo yenye kiwango. Pia kwa barabarakutoka Mbezi kupitia Mpiji Magoe – Mabwepande mpakaBunju. Barabara ina vipande kadhaa ambavyo viko kwenyehali mbaya ikiwemo kipande cha barabara kilichomo ndaniya Pori la Akiba la Pande.

Mheshimiwa Spika, Wakaguzi watembelee barabarahii na matengenezo yafanywe. Kwa upande mwingine,Serikali ieleze ni lini barabara hii itajengwa kwa kiwango chalami kama ambavyo Serikali iliahidi miaka ya nyuma.

Mheshimiwa Spika, kwenye kiambatisho namba 5(D-2) juu ya matengenezo makubwa ya madaraja namakalavati (bridge major repair) kwa kutumia fedha za Mfukowa Barabara. Nashukuru kwa kalavati (box culvert) la Msakuzikatika barabara ya Kibamba Shule – Mpiji Magohelimejumuishwa na kutengewa milioni 340. Naomba ujenzi wabox culvert hilo ufanyike kwa haraka. Aidha, naombamaelezo ya Serikali ya sababu za Kibwegere box culvertkutengewa shilingi milioni 10 tu.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Sekta yauchukuzi, Serikali ihakikishe ujenzi wa reli kwa kiwango chakisasa (SGR) unatumia kwa kiasi kikubwa malighafi kutokandani ikiwemo matumizi ya chuma kutoka Mchuchuma naLiganga ili kuhakikisha sehemu kubwa ya fedha zinabakikatika mzunguko wa ndani. Kamati za Kisekta zinazohusikazipewe nafasi ya kuangalia Mikataba mikubwa ya Ujenzi na

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

Uchukuzi il i kuhakikisha maslahi ya kiuchumi ya nchiyanalindwa kikamilifu.

MHE. ZAINABU M. AMIRI: Mheshimiwa Spika, awali yayote nampongeza Mheshimiwa Isack Kamwelwe, Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Pamoja na Naibu WaziriMheshimiwa Atashasta Nditiye kwa juhudi kubwawanazozifanya katika kusimamia miradi mbalimbali katikaWizara hii.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali iweke vifaa vyauokoaji maeneo ya barabara kuu, mfano, gari la zimamoto,winchi, magari ya breakdown ili kuweza kusaidia uokoaji pindiajali itokeapo na pia kuondoa msongamano barabarani wamagari endapo gari litapinduka na kuzuia magari, itachukuamuda mfupi kushughulikia zoezi la kutoa gari hilo na magarikuendelea na safari.

Mheshimiwa Spika, pia naishauri Serikali ifanye ukaguziwa mara kwa mara hususan SUMATRA katika magari yamizigo (maroli) ili kuona ubora wake maana mengi nimachakavu pia ubebaji mzigo mara nyingi ni hatarishi kwavyombo vingine vya usafiri. Mara nyingi magari hayahutazamwa uzito wa mzigo uliobeba katika mizani tu,ukilinganisha na magari ya abiria ambapo kila kituo kikubwacha mabasi, hufanyiwa ukaguzi.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali itoe elimu yakutosha hasa katika magari makubwa ya mizigo kwamadereva wake, kuacha tabia ya kupaki maroli pembezonimwa barabara mahala pasipostahiki, mfano Kibaigwa,Chalinze na kadhalika (double parking) na kupelekeausumbufu kwa magari yanayopita maana barabara inakuwafinyu na mara nyingine hupelekea ajali kutokea.

Mheshimiwa Spika, vile vile naishauri Serikali iwekevidhibiti mwendo katika magari ya mizigo maana yanaendakwa mwendo wa kasi wa kupelekea kusababisha ajari kwamagari mengine, mfano mabasi ya abiria ambayo

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

wamewekwa vidhibiti mwendo na hatimaye kupelekea vifokwa wananchi wasio na hatia.

Mheshimiwa Spika, naishauri pia Serikali iboresheviwanja vyote vya ndege nchini ili viweze kufanya kazi kwamasaa 24, yaani usiku na mchana. Viwanja vingi vya ndegemfano, Kiwanja cha Ndege Dodoma wakati wa usiku ndegehaiwezi kutua kutokana na ukosefu wa taa za kuongozeandege.

Mheshimiwa Spika, naishauri vile vile Serikali iboreshemizani iliyopo maeneo ya Mikese, Morogoro, maanakumekuwa na msongamano mkubwa wa magari naukizingatia eneo la mizani lipo karibu kabisa na barabara kuuna hii ndiyo sababu, kumekuwa na msongamano hivyonashauri Serikali iboreshe.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nawaombeaMheshimiwa Waziri na Naibu wake afya njema na maishamarefu ili wazidi kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Spika, awali yayote naomba niipongeze Serikali ya Awamu ya Tano chiniya Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe J. Magufuli, Wazirimwenye dhamana Mheshimiwa Mhandisi Isack Kamwelwe,Naibu Waziri Mheshimiwa Kwandikwa, Naibu WaziriMheshimiwa Mhandisi Nditiye, Katibu Mkuu na Watendajiwote wa Wizara husika. Mheshimiwa Waziri ameacha historiaPwani kwenye maji, nina hakika na barabara atazitendeahaki, hongera sana.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Wazirikwa usimamizi mzuri na kufuata ilani kwani miradi mingiimeweza kuvuka na kupiga hatua na kuleta sura nyinginenchini. Hii ni kwa sababu Mheshimiwa Rais Magufuliameamua kuleta maendeleo nchini. Kwani tumeona ununuziwa ndege, ukarabati vya viwanja vya ndege na hata Wilayayetu ya Mafia imepata fedha kwa ajili ya matengenezo yaMafia.

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Spika, sambamba na ukarabati waBandari ya Dar es Salaam, Mtwara, Tanga pia tunaishukuruSerikali kwa ujenzi wa Bandari ya Nyamisati na ukarabati,tunaomba ukarabati Gati la Kil indoni, Mafia uendesambamba kwani ndiyo itakuwa mwanzo/mwisho wa safarizote za wananchi wa Mafia na kuinua uchumi na kuendelezaKisiwa cha Mafia na hata idadi ya watalii itaongezeka.Naomba kupata maelezo lini kazi hiyo itaanza.

Mheshimiwa Spika, jiografia ya Mkoa wa Pwani ikokatika hali ya kutegemeana na mikoa mingine nchini na piakiungo cha safari zote za mikoani. Napenda kujua ujenzi wabarabara ambazo ni kiungo kikuu kwa wilaya nyingine nahata mikoa utaanza lini. Mfano, barabara ya Kisarawe –Maneromango – Vikumburu - Mloka, hii barabara ni muhimusana na hasa kwa sasa ambapo kuna ujenzi wa mradi waumeme Rufiji.

Mheshimiwa Spika, mkoa una visiwa vidogo vidogovingi katika Wilaya ya Kibiti, Mafia, Mkuranga na Rufiji,tunaomba bajeti zinazokuja wafikirie kupeleka boti za uhakikaili wananchi wa maeneo hayo nao wawe na uhakika wasafari na kupata huduma muhimu.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo kubwa la mawasilianokwenye Mkoa wa Pwani kwenye baadhi ya maeneo,kwingine mawasiliano ya simu na maeneo menginemawasiliano ya redia hasa Radio TBC. Mfano, Wilaya yaKisarawe ambako kuna minara yote/baadhi ya TV/Radiolakini bado kuna maeneo hawapati/kusikia chombo hichocha Taifa, ikiwemo Wilaya ya Mafia na baadhi ya maeneona hata mawasiliano ya simu. Hili suala linaeleweka kwenyeofisi ya Mheshimiwa Waziri, hivyo napenda kupata majibu yaufumbuzi wa matatizo hayo.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kupata taarifa rasmiya lini Kisiwa cha Mafia kitapata chombo/meli/boti/feri yauhakika kwa ajili ya wananchi wa Mafia.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa fursa ya kuchangia hoja hii muhimu sana kwamaendeleo ya nchi yetu. Namshukuru Mungu kwa rehemana neema yake kwa Bunge letu na uongozi mzima. Pianampongeza Mheshimiwa Waziri Kamwelwe na Manaibuwake wote na watendaji kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, Wilaya yangu ya Ileje imepatafedha za kujenga barabara kuu ya Mpemba - Isonpole kwakiwango cha lami na tayari kazi imeanza. Tunamshukuru sanaMheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwabarabara hii ambayo ilikuwa ni ahadi yake na vile vile ikokwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015. Ahsante sanaMheshimiwa Rais, wana Ileje wana deni kubwa kwake,wameingoja barabara hii miaka 42.

Mheshimiwa Spika, ziko barabara za TARURA WilayaniIleje ambazo kwa ugumu wake hazitaweza kujengwa naTARURA. Tulipeleka maombi ili zifikiriwe kujengwa na Wizaraya Ujenzi. Aidha, kuna barabara ambazo madaraja yalikatwana mvua tangu 2016 na kwa hivyo wananchi wa Chitete naMlale hawana mawasil iano kupitia Ilanga kitongojikinachopakana na Wilaya ya Vwawa. Tunaomba sanawatufikirie wana Ileje watupatie fedha za kujengamiundombinu ya Ileje, kwani ni migumu sana na hii imekuwakikwazo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi kwa Wilayaya Ileje.

Mheshimiwa Spika, naambatanisha kwa barua husikamaombi yetu kwa maandishi ili watufikirie.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. BALOZI. DKT. DIODORUS B. KAMALA: MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. KatikaJimbo la Nkenge, Wilaya ya Misenyi tuna ahadi tano muhimuza viongozi wetu ambazo zilitolewa wakati wa kampeni zauchaguzi mkuu uliopita. Naomba nimkumbushe MheshimiwaWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano achukue hatua zaharaka kutekeleza ahadi hizo. Ahadi hizo ni pamoja na:-

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

Mheshimiwa Spika, kwanza, kuongeza kasi ya ujenzikwa kiwango cha lami barabara ya Katoma hadi Bukwali.Barabara hii ni muhimu sana na inaunganisha Tanzania naUganda. Ni ahadi ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, pili, kujenga kwa kiwango cha lamibarabara ya Kajai hadi Hospitali Teule ya Wilaya ya Mugane.Ni ahadi ya Mheshimiwa Makamu wa Rais.

Mheshimiwa Spika, tatu, barabara ya Mutukula hadiMinziro, kujengwa kwa kiwango cha lami. Ahadi hii ilitolewana Mheshimiwa Rais alipozindua one boarder post yaMutukula.

Mheshimiwa Spika, nne, barabara ya kutoka Kituo chaAfya cha Kabyaile hadi Gera. Ahadi hii ilitolewa naMheshimiwa Rais alipotembelea Kituo cha Afya cha Kabyaile.

Mheshimiwa Spika, tano, ujenzi wa kiwango cha lamiwa kilometa tatu za lami Makao Makuu ya Wilaya (Kyaka –Bunazi). Ahadi ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, kivukokipya kati ya Bugorola – Ukara. Pamoja na jitihada za Serikalikuanza mchakato wa utengenezaji wa kivuko kipya baadaya ajali ya MV Nyerere, mchakato huu unaenda taratibu.Kivuko kilichopo sasa cha MV Saba Saba kina matatizo mengihali inayoendeleza hofu kwa watumiaji wa kivuko hiki. Ombi,kivuko hiki kikikamilika mapema ili kinusuru maisha ya watuwetu. Pia uangaliwe uwezekano wa kuweka usafiri wauhakika kwenye maeneo ya Kitale – Irugwa na Kakukuru –Gana.

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa kifusi kwa ajili yautengenezaji wa barabara. TANROADS wamekuwa nakawaida ya kuchimba kifusi/changarawe pembezoni mwabarabara jambo ambalo limekuwa linaacha mashimomakubwa sana na kusababisha vifo. Mfano, wiki iliyopita

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

tarehe 9 Mei, 2019 shimo lililochimbwa kwa ajili ya kifusi eneola Kijiji cha Nakamwa, Kata ya Namilembe, Wilaya yaUkerewe limesababisha vifo vya watu wawili baada ya garikutumbukia katika shimo hilo. Hii ni moja ya matukio ya kifona majeruhi ambayo yamekuwa yanatokea mara kwa maraWilayani Ukerewe. Ushauri, baada ya shughuli za ujenzi wabarabara mashimo haya yamekuwa yanafukiwa.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya lami; kwakuwa barabara ya Bukindo – Murutunguru – Bukonyo nimuhimu sana kwa uchumi wa ukerewe na sehemu yabarabara hii ilishafanyiwa upembuzi yakinifu, michoro namakadirio tayari yalishaandaliwa tayari yakisubiri upatikanajiwa fedha ili ijengwe. Naomba Wizara isaidie upatikanaji wafedha ili barabara hii iweze kujengwa kwani ni kilometa sabatu.

Mheshimiwa Spika, wakati wa ujio wa MheshimiwaRais Visiwani Ukerewe tarehe 5 Septemba, 2018 aliahidi ujenziwa barabara kilometa 14 kutoka Lugezi – Nansio kwa kiwangocha lami. Naomba Serikali itekeleze ahadi hii.

MHE. SUZANA C. MGONOKULIMA: Mheshimiwa Spika,miradi mbalimbali ya ujenzi wa viwanja vya ndegeinaendelea katika Mikoa mbalimbali kama vile Msalato,Tabora, Kigoma, Mpanda, Mtwara, Shinyanga, Kilimanjaro,Sumbawanga, Arusha, Songwe na Mwanza. Kazi kubwazinazofanyika katika miradi hiyo zinajumuisha ujenzi wabarabara za ndege, upanuzi na ukarabati wa maegesho yandege, ujenzi wa vituo vya waangalizi wa hali ya hewa, ujenziwa barabara za kuingilia viwanja vya ndege, uboreshaji waviwanja hivyo pamoja na ujenzi wa majengo ya abiria namizigo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi zote hizozinazoendelea bado kuna matatizo makubwa ya viwanjavingi kukosa uzio, tumeshuhudia Kiwanja cha Ndege chaMwanza mtu aliyekatisha ndani ya kiwanja wakati ndegeinaruka na kusababisha ajali. Lazima Serikali ihakikishe kilakiwanja cha ndege kinachojengwa na uzio unajengwa

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

kuepusha madhara yanayoweza kutokea kwa wanyama nabinadamu wanakatisha ndani ya kiwanja hata Kamatiilipotembelea Kiwanja cha Dodoma mbwa alikatisha.

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Mawasiliano kwa WoteUCSAF ulianzishwa na Serikali kwa Sheria Na. 11 ya mwaka2006 ukiwa na lengo la kupeleka huduma ya mawasilianomaeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara. Mfuko huoumejitahidi kupeleka huduma hiyo lakini bado maeneomengine yasiyo na mvuto wa kibiashara hayajapata hudumahiyo. Tunaiomba Serikali ifanye kama kusudio la sheriailiyoanzisha Mfuko huo lilivyo ili Watanzania wote huduma hiyokwa ajili ya kuleta maendeleo.

MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Spika,nampongeza sana Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Serikali nzima ya Awamu ya Tano na Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasil iano kwa kazi kubwainayoendelea kwenye WIzara hii. Naipongeza sana Serikaliya Awamu ya Tano kwa kutoa pesa za kutosha kwa Wizarahii kulingana na bajeti ya 2018/2019 (page 10 and 11).Matumizi ya kawaida fedha iliyotoka ni asilimia 72.66 Vsasilimia 75. Miradi ya maendeleo fedha iliyotoka ni asilimia60.98 Vs asilimia 75.

Mheshimiwa Spika, naipongeza sana miradi mikubwaya Kitaifa kama ilivyoorodheshwa kitabuni ukurasa 53, 61, 117,192 na kadhalika. Vile vile naipongeza sana Serikali kwamiradi mikubwa hapa Jijini na Mikoani Dodoma. Miradi hiyoni Dodoma outer ring roads pages 47,176 and 271. Ujenzi waIkulu ya Chamwino zikiwemo na barabara za kwenye Mji waChamwino. Ujenzi wa Miji ya Kiserikali pale Mtumba. Lamibarabara ya Kongwa Junction – Mpwapwa – Gulwe –Kibakwe.

Mheshimiwa Spika, nina ombi mahsusi; daraja kati yaChilonwa na Nzali ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Makamuwa Rais, mama Samia Suluhu Hassan. Barabara ya ChalinzeNyama – Chilonwa – Dabalo – Itiso – Chenene. Mawasilianoya simu za mkononi katika Kata zifuatazo: Zajilwa (ina vijiji

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

vitatu) Segola (ina vijiji vitano) Haneti (ina vijiji vinne) Itiso (inavijiji vinne) Dabalo (ina vijiji vitano) pia kwa sasa kuna Dabaloni Mji mdogo na Membe (ina vijiji vitatu). Kata hizi tano zinamawasiliano hafifu tena kwa wakati fulani.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi katikakuchangia mchango wangu na ushauri kwa Serikali katikaWizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, katika Ilani ya Uchaguzi ya CCMSerikali iliahidi kutekeleza ujenzi kwa kiwango cha lami katikabarabara ya Singida – Sepuka – Ndago – Kizaga yenye urefuwa takriban kilometa 92. Barabara hii imekuwa barabaramuhimu sana kwa sababu ya uzalishaji mkubwa wa mazaoya biashara kama vile alizeti, mahindi na kadhalika. Wakatiwa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 Mheshimiwa Raisalipita barabara hii na kuwaahidi wananchi kuwa barabarahii itajengwa kama ambavyo Ilani ya Uchaguzi wa CCMilielekeza, lakini mpaka hapa tunapoongea utekelezaji waIlani katika ujenzi wa barabara hii bado unasuasua na hivyokuwafanya wananchi kuendelea kupata adha katikakusafirisha mazao na hata mafuta yanayozalishwa katikaviwanda ambavyo vimejengwa maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, Serikali yetu imekuwa ikitumia sanafedha nyingi katika matengenezo ya muda mfupi na mrefuya barabara hii, jambo ambalo kama Serikali itawekadhamira ya dhati katika kujenga barabara hii kwa Mwakawa fedha 2018/19 Serikali ilitenga fedha za upembuzi yakinifuwa barabara hii lakini mpaka leo hatua za utekelzahihaueleweki.

Mheshimiwa Spika, katika Sekta hii hii ya barabara,Serikali tangu mwaka 2010 imejenga madaraja katikabarabara ya Sepuka – Mkandala – Mgungira tangu madarajayakamilike leo miaka 9 ujenzi wa tuta la barabaraumeshindikana, hivi tumetumiaje pesa za umma kwa

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

mamilioni na kushindwa kukamilisha ujenzi wa tuta tu?Barabara hii ni muhimu sana katika kusafirisha mazao yachakula na biashara kama vile mchele, alizeti na barabarahii ambayo inaungana na barabara ya Magereza –Mtuduru– Iyumbu imekuwa ya muda mrefu sana mvua zimenyeshawatu hawa wanakosa mawasiliano. Ni muda muafaka sasakwa Serikali kutekeleza ujenzi wa barabara hii muhimu kwawapiga kura wa Jimbo la Singida Magharibi.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, mawasiliano yaminara ya simu; jiografia ya Jimbo la Singida Magharibi ikovery complicated. Toka nimekuja Bungeni tumekuwatukipewa vitabu vinavyoonesha distribution ya minara yasimu, lakini hakuna utekelezaji wa mnara hata mmoja ambaouliahidiwa na Serikali ambao umejengwa.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2018 wananchi wa Kataya Iyumbu walivamiwa na majambazi mchana na madukayote kuporwa pesa, watu wetu hawakuweza kupata msaadasababu ya ubovu wa barabara na ukosefu wa minara yasimu, hakuna mawasiliano ya barabara wala ya simu na katahizo ndizo zinaendesha halmashauri ya Wilaya ya Ikungiambapo asilimia 90 ya mapato yanatoka kule kutokana nakiwango kikubwa cha uzalishaji wa mchele ambao unauzwaUganda, Rwanda na Burundi na kuliletea Taifa mapato yandani.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana vilitolewa vitabuhapa ambavyo TTCL wamepewa market share ili kufungwaminara katika maeneo hayo, lakini hakuna lolote lililofanyikakatika kuwasaidia Watanzania hawa.

Mheshimiwa Spika, haya mambo yanatuweka mahalipagumu sana. Naomba minara ya mawasiliano ikafungweIkungi, Igholwe na maeneo yote ambayo wananchiwanapata matatizo katika Jimbo la Singida Magharibi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, napendakutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali ya CCM kwakutumia zaidi ya bilioni mia mbili kwa ajili ya kukamilisha ujenziwa Daraja la Mto Sibiti ambalo litaunganisha Mkoa wa Simiyuna Singida na kunufaisha kiuchumi na kijamii wananchi waMkoa wa Simiyu hususan Wilaya ya Meatu. Naombakusaidiwa yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kujenga kwa kiwangocha lami kilomita 25, ahadi iliyotolewa na Mheshimiwa Raiswakati wa uzinduzi wa daraja. Pili, Daraja la Mto Sibitihalitakuwa na tija wakati mvua kubwa itakaponyeshamfululizo kama makorongo ya Itembe na Chombe yaliyopobarabara ya kutoka Sibiti hadi Mji wa Mwanhunzihayatajengewa madaraja ya juu. Naomba makorongo hayoyajengewe daraja ili kuwepo na thamani ya pesa kwa darajahilo kupitika kwa uhakika na magari ya aina zote.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE: MheshimiwaSpika, nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa WaziriKamwelwe, kwa kazi nzuri sana anayoifanya kuiongozaWizara hii. Niwapongeze sana Manaibu Waziri MheshimiwaJohn Kwandikwa na Mheshimiwa Engineer Atashasta Nditiyena Makatibu Wakuu wote kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Raiswetu kwa kutujengea barabara ya Mwanga – Kikweni –Vuchama – Ngofi – Kiriche - Lomwe kwa kiwango cha lami.Sisi Wanamwanga tunamshukuru sana. Pia tunawashukurusana kwa kuzipandisha barabara za Lembeni – Kilomeni -Ndorwe na barabara ya Kirya - Lang’ata Bora - Kifaru kuwabarabara za TANROADS.

Mheshimiwa Spika, suala langu la tatu ni mawasiliano,tunaishukuru sana Serikali kwa kulea uwekezaji katikamawasiliano. Hakika karibu nusu ya Watanzania wanamilikisimu ya mkononi, aidha, bei za kutumia mitandao ya simuzimeendelea kushuka. Hata hivyo, makampuni ya simu

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

yanatumia ujanja na control ya system nzima kuwaonea nahata kuwaibia wananchi wanaotumia mitandao yao.Unanunua kifurushi cha GB 15 kwa Sh.20,000/=, kwa siku saba,unatumia GB 3 kwa siku zote saba, halafu GB 12 zinamezwakwa kuwa siku saba zimekwisha. Huu ni wizi, mtumiaji wa simuakinunua kifurushi ni chake, lazima atumie mpaka kiishie ndiyoanunue kipya. Huu ndiyo utaratibu wa kununua na kuuza mali.

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa fursa.

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: MheshimiwaSpika, pamoja na mchango wangu niliochangia katika Bungelako Tukufu leo; nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwakumteua Waziri wa Ujenzi Engineer Kamwelwe ambayenatambua uchapa kazi wake, akiwa Naibu Waziri wa Mjialifanya kazi kubwa sana na kuwasaidia sana wananchi waJimbo langu. Pamoja na kazi kubwa aliyoifanya, pamoja namchango wangu wa kuongea Bungeni, nimwombe Waziriazingatie yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri kwa kukubaliujenzi wa barabara ya Nyamwage – Utete kilomita 33,barabara hii ni ahadi ya Rais Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli ya tarehe 4/3/2017 kuwa itakamilika kabla ya 2020.Nimwombe Mheshimiwa Waziri sasa kwa kuwa upembuziyakinifu umekamilika, aje sasa kuweka jiwe la msingi mweziJuni ili wananchi wapate imani kwani barabara hii imeondoaWabunge wengi.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali inisaidie ili niwezekurudi 2020 – 2025. Nyamwage-Utete ni kiini cha anguko lakiuchumi Rufiji, ubovu wa miundombinu ni kero kubwa kwawananchi, Mheshimiwa Waziri afike sasa Rufiji ili kuanza ujenziwa barabara hii, pamoja na barabara ya Nyamwage Utete.Niombe Serikali ikubali ujenzi wa barabara ya Kibiti - Mlokaambayo inasaidia wakandarasi wanaojenga mradi waumeme wa Rufiji (Stiegler’s). Barabara hii ni chafu sana nahaifai. Mradi huu wa umeme utachelewa sana iwapobarabara hii haitajengwa kwa kiwango cha lami. Ipobarabara ya Ikwiriri – Mloka ambayo ni kioo cha uchumi wa

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

Rufiji, tunaomba Serikali kuiweka katika mpango wa ujenziwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, ipo barabara ya Utete –Ngarambe, hii ni muhimu sana kufungua utalii wa Pwani yaKusini. Ngarambe kuna Selou na pia kuna vipepeovinavyoweza kuvutia watalii.

Mheshimiwa Spika, nyingine ni barabara ya Mloka -Kisarawe, Mloka - Kisaki, Bungu – Nyamisati – Kisiju - Mkuranga,Vikindu – Vianzi. Hizi ni barabara muhimu kwa kufunguauchumi wa Mkoa wa Pwani, ubovu wa miundombinu hiikumepelekea kudumaa kwa uchumi na ndiyo sababukumekuwepo na wimbi kubwa la umaskini katika eneo laPwani ya Kusini.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa fursa hii. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa WaziriKamwelwe, Manaibu Waziri Mheshimiwa Kwandikwa naMheshimiwa Nditiye. Naishukuru Serikali kwa utekelezaji waujenzi wa Gati la Nyamisati. Gati hili ujenzi wake unakaribiakwisha na matarajio ni kufikia mwezi Juni mwaka huu.Tunashukuru sana Serikali.

Mheshimiwa Spika, pia naishukuru Serikali kwakutenga fedha za kujenga kivuko kipya kati ya Nyamisati naKilindoni pamoja na ukweli kuwa kivuko hiki kilishatengewafedha katika mwaka wa fedha 2018/2019 na mchakato wakumpata mkandarasi ukaanza, lakini kwa masikitiko,kandarasi hii imefutwa kutokana na matatizo ya kisheria.Nimwombe Mheshimiwa Waziri atupie macho utendaji waWakala wa Ufundi Umeme na Mitambo (TEMESA),wahakikishe mchakato wa ujenzi wa kivuko hiki cha Nyamisatina Kilindoni.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni kivuko cha mudatulichopewa na Serikali kivuko kinachomilikiwa na Chuo chaMabaharia (DMI), mpaka ninapoandika hapa bado

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

hakijaanza kazi. Naomba sana Mheshimiwa Waziri atiemsukumo wa kuhakikisha boti hii inaanza kazi mara moja nahasa ukizingatia Gati la Nyamisati linakaribia kumalizika.

Mheshimiwa Spika, Gati la Kilindoni lipo katika halimbaya sana, mbao zimechoka na ngazi ya kupanda nakushuka inakatikakatika mara kwa mara na kuhatarishausalama wa abiria na mali zao. Mamlaka ya Usimamizi waBandari (TPA) walishaahidi kufanya matengenezo makubwaya gati hili. Kukamilika kwa Gati la Nyamisati itakuwa hakunamaana kama Gati la Kilindoni litakuwa bado bovu.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Kilindoni mpaka RasiMkumbi kilomita 45 ni ahadi ya Mheshimiwa Rais Mstaafu waAwamu ya Nne na imo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM yamwaka 2015 - 2020. Mpaka sasa upembuzi wa kina na usanifuumeshakamilika, bado kutengewa fedha za ujenzi.Nimwombe Mheshimiwa Waziri chonde chonde ujenzi wamatengenezo ya muda wa (periodical) maintenance)unakuwa mgumu kwani udongo wa kufanyia matengenezounakaribia kwisha. Hivyo ni bora barabara hii ikajengwa kwakiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, Uwanja wa Ndege wa Mafia;tunaomba uongezwe urefu sambamba na kuwekwa taa ilikuwezesha ndege kubwa za Kimataifa kutua moja kwa mojana kukuza utalii sambamba na ujenzi wa jengo la abiria(Terminal building)

Mheshimiwa Spika, suala la mawasiliano katika Kisiwacha Mafia bado ni changamoto katika Vijiji vya Miburani,Banja, Kitohi na Chemchemi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kutoa mchango wangukatika hoja hii muhimu ya Wizara ya Ujenzi inayosimamiamiundombinu ya barabara na mawasiliano nchini.

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru MwenyeziMungu kwa kutupa afya na uzima na kupata nafasi ya kuwammojawapo wa Waheshimiwa Wabunge kutoa mchangowa kuboresha kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya hii ya CCMya Awamu ya Tatu kupitia Wizara hii ya Ujenzi. Nachukuanafasi hii kuipongeza Serikali kwa utekelezaji wa miradimikubwa ya miundombinu ya usafiri nchini. NaipongezaSerikali kwa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ya reli ya kati tokaDar es Salam mpaka Kigoma.

Mheshimiwa Spika, nashukuru Serikali kwa sababu relihii ujenzi wa Awamu ya Kwanza toka Dar es Salam mpakaMorogoro unakamilika mwaka huu Desemba, 2019 na kwakiasi kikubwa barabara hii inapita katika Jimbo la MorogoroKusini Mashariki, Jimbo ambalo naliongoza mimi. Reli itakuwana msaada mkubwa wa kuinua hali ya vipato na uchumi wawananchi wa Morogoro Kusini Mashariki na Morogoro kwaujumla kwa kuwa itapunguza gharama ya usafiri wa mazaoya wakulima wa Ngerengere, Mikese, Kinole, Tegetero,Tununguo, Mkuyuni, Kiroka, Tomondo, Mkulazi na Vijiji vya Katazote za Morogoro kwa ujumla na kupunguza gharama zausafiri na kuongeza vipato vya wananchi wa Morogoro.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo yaSerikali ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. JohnJoseph Magufuli kwa kuweka katika bajeti barabara yaBingwa - Kisaki kuanza kwa ujenzi na kuanza kilometa 50 kwakiwango cha lami. Naipongeza Serikali kwa sababu ni sikivu,baada ya kusikiliza maombi yangu ya ujenzi wa barabarakuanza ujenzi kila Bunge la bajeti tangu kuingia katika Bungehili.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi na shukranihizo kwa Serikali kuiweka katika bajeti barabara ya Bingwa -Kisaki lakini kiasi kilichotengwa ni kidogo sana cha shilingimilioni mia moja arobaini na tano (145,000, 000) kwa kujengabarabara ya kilometa hamsini ni kiasi kidogo sana ambachohakiwezi kutosha kulipa hata fidia tu kwa wananchiwaliopisha ujenzi wa barabara hii ya Bingwa Kisaki. Ushauriwangu kwa Serikali kuongeza kiwango cha fedha katika

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

bajeti ya ujenzi wa barabara hii ya Bingwa - Kisaki ili ujenziwake uanze mwaka ujao wa fedha unaanza mwezi Julaibaada ya bajeti hii kupita.

Mheshimiwa Spika, kiasi hiki ni kidogo ambacho piahakiwezi kutosha kulipa mkandarasi malipo ya awali yaasilimia 15 kwa mujibu wa sheria. Naomba Serikali iongezefedha ili ujenzi uanze.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili naomba Serikalikutupatia minara ya mawasiliano katika Kata ya Tegetero,Rudewa, Seregete, Mkulazi, Tununguo, Kidugalo na Matuli naVijiji vyote vya Kata hiyo pamoja na Vijiji vya Luholole, Mwarazina Kibuko Kata ya Kibuko. Pia mnara katika Vijiji vya NewlandLubungo, Mhunga Mkola katika Kata ya Mikese.

Pia naomba ujenzi wa madaraja katika Mto Ruvukuunganisha Tarafa ya Mvuha na Tununguo kupitiaMbarangwe, Tununguo mpaka Kisanga Stendi. Pia naombadaraja la kuunganisha kati ya Kata ya Matuli na Kidugalokwenye Mto Ngerengere.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja,ahsante sana.

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Spika,napenda nianze kuzungumzia barabara ya Amani – Muheza,zaidi ya kilometa 20 ambayo Serikali iliahidi kuiweka lamikwani Tarafa ya Amani yenye kata sita inategemea barabarahiyo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, kilimo, utalii nakadhalika, je, ni lini barabara ya Amani – Muheza itajengwakwa kiwango cha lami?

Mheshimiwa Spika, barabara ya Muheza kwendaMagoroto inahitaji kuwekwa lami kwani ni barabarainayoenda kwenye mashamba ya michikichi ambayo nimaeneo yanayozalisha lakini pia Magoroto kiutalii (MagorotoCamp) ambayo inaingiza pato la halmashauri na nchi kwaujumla. Je, ni lini barabara hii itajengwa kwa lami ikizingatiwani muhimu kwa ukuaji wa uchumi.

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

Mheshimiwa Spika, Bandari Kavu Pangani naKigombe. Kumekuwa na kuzuka kwa bandari kavu (bandaribubu), naomba kufahamu Wizara ina utaratibu gani wakurasimisha bandari hizi ili ziweze kuwa chachu ya maendeleokwa Wilaya za Muheza na Pangani.

Mheshimiwa Spika, minara ya simu; kuna tatizo kubwala mawasiliano ya simu Tarafa ya Amani, Kata za Zirai, Misalaina Bwiti.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Spika, naombanichangie katika hoja hii kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, uwanja wa ndege; kwa kuwaKiwanja cha Ndege Njombe kiko katika hali mbaya, niombeSerikali ikarabati kiwanja hicho. Serikali imekuwa ikisema ikokwenye mchakato lakini sasa ni miaka minne Wananjombewanajibiwa kuwa kiko kwenye mchakato.

Mheshimiwa Spika, Barabara za Itoni – Ludewa(Njombe) – Njombe – Makete. Hali ya barabara zile sio nzuri,hasa kipindi hiki wakati wa mvua. Naomba wakandarasiwalipwe kwa wakati ili waweze kuharakisha ujenzi wabarabara hizo.

Mheshimiwa Spika, mawasiliano ya simu; maeneomengi ya Jimbo la Lupembe hakuna mawasiliano ya simumfano Madeke, Kanikerere na maeneo mengine. NaombaSerikali iwasaidie wananchi kupata mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, miradi kushirikisha Sekta Binafsi;kwa kuwa miradi mingi inasuasua kwa sababu Serikali pekeyake inagharamia. Ili kuharakisha maendeleo, nashauri miradihiyo washirikishwe sekta binafsi kwani sekta hiyo wakipewamiradi hiyo wataharakisha kumaliza miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika,naomba kumpongeza sana Mheshimiwa Engineer.

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

Kamwelwe, Waziri na Naibu Mawaziri kwa kazi nzuriwanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao. Serikalikupitia ahadi ya Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Magufuli aliahidi kutengenezwa kwa Barabara yaNyashumo – Ngasamo – Dutwa, kilomita 45 kwa kiwango chalami. Huu ni mwaka wa nne, ningependa kujua ni lini ujenziwa kiwango cha lami utaanza ili kuwezesha usafirishaji wabidhaa za kilimo pamoja na usafiri wa wananchi uwezekutekelezwa? Aidha, kumekuwepo na uimarishaji wamadaraja na baadhi ya sehemu korofi kwa kiwango si chakuridhisha. Hivyo naomba kupata majibu ni lini sasa ujenzihuu wa barabara utaanza.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika,barabara, maeneo ya uzalishaji. Pamoja na jitihada zakuunganisha mikoa kwa mikoa, nashauri na kupendekezaSerikali iongeze nguvu kwenye maeneo ya uzalishaji kiuchumiili kuchochea shughuli za uzalishaji na hivyo kuongeza Patola Taifa. Mfano, Wilaya ya Mufindi, Barabara ya Mafingakwenda Mgololo ni uti wa mgongo wa uchumi kuelekeakwenye Viwanda vya Chai, Karatasi na Mazao ya Misitu.Wakati wa mvua unakuta malori yamekwama kwa wikinzima, hii maana yake ni ku-slow down speed ya uzalishajina hasa usafirishaji.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Mufindi inachangia Patola Taifa kwa kuwa miongoni mwa wilaya tano bora kimapato.Pamoja na hali hii, bado inaweza kuchangia zaidi ikiwabarabara hii itapitika mwaka mzima. Hivyo, nia yangu hapani kuishauri Serikali kuwa itazame maeneo ya kimkakatikiuchumi hata kama maeneo haya hayaunganishi mkoa kwamkoa.

Mheshimiwa Spika, mawasiliano; Mji wa Mafinga nimji wa kibiashara na unakuwa kwa kasi sana kutokana nauwepo wa shughuli za viwanda vya mazao ya misitu. Hatahivyo, kuna maeneo ambayo ni just about or less than 15kilometres from Mafinga Town, hakuna mawasiliano.

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

Mawasiliano ni component muhimu kwenye shughuli zakiuchumi na purchasing power iko juu, wakipata mawasilianoyatachangia uchumi kwa kununua data na muda wamaongezi. Hivyo naomba mawasiliano katika Vijiji vya Kisada,Bumilayinga, Ulole, Kikombo, Maduma na Itimbo.

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Spika, nipendekuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Jangwani; nipendekujua nini sababu ya ujaaji wa maji, baada ya matengenezoya mwendokasi ndiyo imekuwa mbaya kuliko. Swali; je,upembuzi yakinifu haukufanyika au ilikuwaje, kila ikinyeshamvua lazima watu washindwe kupita barabara hii? Leo hiitunavyoongea Jangwani hakupitiki; je, hivi kweli wananchiwanazunguka na kupoteza muda mwingi kutafuta jinsi yakufika kazini kwao?

Mheshimiwa Spika, barabara na fidia kwa wananchiwa Kibaha wanaopisha upanuzi wa barabara TAMCO –Mapinga. Wananchi wanashindwa kujua hatma ya maishayao kufuatia tathmini iliyofanywa na malipo kukwama, hivyokusababisha wananchi kuwa na umaskini uliokithiri. Serikaliirudi kwa wananchi iwaambie wamekwama wapi kulipa fidiailiyowaahidi miaka minne iliyopita.

Mheshimiwa Spika, magari ya mwendokasi; najuakuwa SUMATRA ambao wanatetea pia wasafiri ambao niidara katika Wizara hii. Usafiri wa mwendokasi ni shida sana,magari ni machache sana na wasafiri ni wengi, hivyokupelekea wasafiri kujazana sana mpaka kukosa hewa nakusababisha wengine ku-faint kwa kukosa hewa. Nini maanaya kugharamia mradi huu na kuondoa mabasi ya kawaida,wananchi hawaielewi nia ya Serikali kuondoa magari yakawaida, Serikali imewapa mateso makubwa kwa kuletamradi huu.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa majengo kwa ajili yakuuza. Ujenzi unaojengwa na TBA usiangalie upana waviwanja na ubora wa majengo wanayoyajenga ambayo

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

inapelekea wananchi kushindwa kununua kutokana naudhaifu unaopelekea wanunuzi kuona nyumba hizi sio rafikikwa maisha yao.

Mheshimiwa Spika, TEMESA; matengenezoyanayotokana na TEMESA ukipeleka gari kutengenezwainatengenezwa kwa muda mrefu kuliko yanayotengenezwakwa watu binafsi. Hata barabarani taa zote zinapoharibikaurekebishaji ni shida.

Mheshimiwa Spika, bandari; nishauri Serikali kujifunzautoaji huduma wa Bandari za Durban, Beira na Mombasa,vinginevyo wateja watatukimbia iwapo urasimu wetu na tozonyingi utaendelea katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, TTCL; tumeimba mara nyingi sanakuwa Serikali ilipe madeni inayodaiwa pia itoe uhuru wauendeshaji ili ijiendeshe kibiashara, iwe na uwezo wa kukopana kukopesha.

MHE. MUHAMMED AMOUR MUHAMMED: MheshimiwaSpika, awali ya yote naomba nimshukuru Mwenyezi Munguwa rehema kwa kunipa uhai na uzima na pia kuniwezeshakuchangia mada iliyopo hewani kwa lengo la kulipaisha Taifaletu.

Mheshimiwa Spika, nianze na Bandari ya Bagamoyo.Ni vyema Serikali ingefikiria zaidi kujenga Bandari yaBagamoyo. Hii itasaidia kuimarisha uchumi wa maeneo hayona pia kuongeza Pato la Taifa. Bandari ya Bagamoyo kamaitajengwa, hata hii Reli ya Kati nayo ndiyo itaweza kufanyakazi vizuri, mizigo itapatikana kutoka nchi tofauti kuletwahapa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, usajili wa simu; kwa masikitikomakubwa sana, TCRA haionekani kutoa mashirikiano mazurina Zanzibar (SMZ). Kwa upande wa Zanzibar ZAN – ID ndiyokila kitu, ndimo yalimo maisha ya Wazanzibari. Ni vyema basikama ZAN – ID nayo ikatumika katika usajili wa simu.

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa bandari ni masuala yaMuungano, kule Zanzibar bandari zake zimekuwa hovyo sanana zimeachwa kama hazina mwenyewe, je, Serikali yaMuungano ina mpango gani kuhusiana na maboresho yabandari za Zanzibar?

Mheshimiwa Spika, wizi wa mitandaoni; kumekuwa nawizi mkubwa wa wananchi katika miamala ya fedha. Kwamfano kama utamtumia fedha mdogo wako na kwa bahatimbaya usipate wakati wa kumuarifu, baada ya muda basianapigiwa simu na mtu mwingine kama yeye ndiyealiyemtumia fedha na azirejeshe na namba ya kurejeshaanatoa na hii inarudi kwa mwizi. Zikitakiwa namba zilizotumikaninazo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, nimejiwana wazo ambalo ni kuona uwepo wa haja ya kumwenzi DktSalim Ahmed Salim kwa kupewa heshima ya jina laMheshimiwa kuingia kwenye kumbukumbu ya milele nako nikumuenzi akiwa hai na kusikia kiwa duniani kuwa Uwanja waNdege wa Songwe unapewa jina lake.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe Dkt. Salim ameshikanyadhifa nyingi ambazo ni: Balozi wa Zanzibar , Gairo; Baloziwa Tanzania, Cairo; Balozi wa Tanzania UN, New York; Katibuwa OAU; Waziri wa Nje, Ulinzi; na Waziri Mkuu, naomba hilolizingatiwe.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, kwanzanachukua fursa hii kukushkuru wewe kwa kunipa nafasi hii yakuchangia katika hotuba hii. Pili nachukua nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wakewote kwa kuandaa na kuwakilisha hotuba hii kwa umakinimkubwa sana. Katika kuchangia hotuba hii napendakuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Shirika la Posta (TPC) napendakuipongeza Serikali yetu kwa kuendeleza juhudi kubwa za

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

kuendeleza na kuiimarisha Shirika hili, shirika hili ni miongonimwa mashirika makongwe sana katika nchi hii. Shirika hililinajishughulisha na kazi ambazo ni lazima zifuatiliwe ilikufanikisha kazi hizi mfano, kazi ya posta mlangoni hii kaziinahitaji vitendea kazi vya usafiri ili kufika kwenye eneo husika.Ushauri wangu katika jambo hili ni Wizara kuzidisha juhudi yakuwatafutia usafiri wa uhakika ili kuweza kukabiliana naushindani mkubwa uliopo nchini.

Mheshimiwa Spika, Shirika la Mawasiliano Tanzania;shirika hili ni miongoni mwa mashirika muhimu sana katikauchumi wa nchi yetu. Nachukua nafasi hii kuipongeza idadiya wateja (Active customer) wa huduma mbalimbali, hili nijambo jema kwa sababu wateja ndio watakaowezeshaupatikanaji wa faida katika shirika hili.

Mheshimiwa Spika, kazi za mawasiliano kwa sasa zinaushindani mkubwa sana, mashirika mengi ya binafsiyamejitokeza na yanaendelea kujitokeza, hivyo ni vyemashirika likajipanga ili kukabiliana na ushindani huu.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali iliwezeshe shirikahili ili liweze kukabiliana na mashirika binafsi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Spika, nianze kwakumshukuru Mungu mwingi wa rehema kwa kunipa akili nabusara ili kuweza kutoa mchango wangu wa maandishikatika hoja hii muhimu kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)imeamua na kupitisha usajili wa line za simu kwa njia ya kidole(finger) kuanzia 1/5/2019 jambo ambalo ni jema, Zanzibar naWazanzibari kutoka ilipoanza kusajili simu za mkononi,Wazanzibar tulikuwa tukisajili line za simu kwa kupitiakitambulisho cha ZEN ID na hakukuwa na shida wala matatizoyoyote. Ni hivi karibuni tu mwezi Septemba, 2018 Serikali ya

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilitumia mabilioni kubadilisha nakuboresha kitambulisho cha ZEN ID.

Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya sana tunaonawakati zoezi hili likiendelea Wazanzibari ambao tulisajili linezetu kwa kitambulisho cha ZEN ID sasa kitambulisho hichokinakataliwa na kimeondolewa kabisa, kama nilivyosema sisiWazanzibari tulisajili kutumia ZEN ID bila shida yoyote na vilevile SMZ kutumia mabilioni kuboresha kitambulisho hicho nikwa nini sisi Wazanzibari ambao tulitumia kitambulisho chaSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tusiachiwe kuendelea nausajili wa kitambulisho hicho?

Mheshimiwa Spika, vile vile kuondolewa kwenye usajilikitambulisho cha ZEN ID si wazi kwamba kitambulisho hikiSerikali ya Muungano inaenda kukiondoa kabisa. Hivyo hivyowapo Wazanzibari ambao hawana kitambulisho cha NIDAlakini wana kitambulisho cha ZEN ID.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nimwombe MheshimiwaWaziri atueleze kwa kutumia kusajili line za simu kwaWazanzibari kwa kutumia ZEN ID tatizo ni nini? Suala hili nimuhimu wakati Mheshimiwa Waziri anafanya majumuisho nivyema akalitolea ufafanuzi kwani Zanzibar hasa wananchiwa Zanzibar wamekuwa wakijiuliza na kutoafautiana sana.Ahsante sana.

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Spika, napendakutoa pongezi za dhati kwa Wizara hii kwa ujumla wao kwamaslahi ya wananchi wetu, ni wizara pana ndani yautekelezaji wake, hivyo nasisitiza na kukubaliana na Kamatina kupongeza kwa kuongezewa bajeti, lakini ni bora zaidiikiwa Hazina watazitoa zote au kwa asilimia zaidi ya 85.

Mheshimiwa Spika, kwani tunatarajia kuinua utaliiambao unatupatia mgawo wa zaidi ya asilimia tano ya patola Taifa, pia kurahisisha mawasiliano ya barabara kwa uchumiwa nchi yetu. Tunashukuru jit ihada ya Serikali yakutuunganisha na nchi jirani kwa barabara ya kiwango chalami, Sumbawanga – Matai – Kassanga (DRC CONGO), Matai

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

– Kasesya (Zambia). Ombi, tunaomba kasi kuongezwa kwaukamilifu wa barabara hizi pamoja na kuwemo kwenye bajetiiliyobainishwa ukurasa wa 257, tunasisitiza fedha za miradiya maendeleo kutolewa zote na kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, hali ya barabara ya bonde laRukwa kutoka Kibaoni hadi Kilyamatunda ina hali ngumukutokana na maji yanayoporomoka kutoka mlimani nakuelekea Ziwa Rukwa, yanakuwa na nguvu na kukokota mitimikubwa na kuhatarisha madaraja katika barabara hiyo yotena yote yameharibika na kupelekea kila mwakakurekebishwa maeneo korofi na kuendelea kutumia pesanyingi za walipa kodi.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo na ushauri,barabara hii ni kutengenezwa kwa kiwango cha lami naujenzi wa madaraja makubwa na madhubuti, ndiyo suluhisholake. Pamoja na Bajeti iliyopendekezwa kwa baadhi yamaeneo katika ukurasa 302, Ntendo – Muze, Ilamba – Kaoze,Kasansa – Kilyamatundu, Mtowisa – Ilemba, ni matumainiyangu, ushauri wa muda mrefu wa ujenzi wa barabara hiikuliko ilivyo sasa.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Rukwa, tuna Kiwanjacha Ndege, Sumbawanga ambacho kinafanyiwa ukarabatina kuongezwa urefu wa uwanja huo, kwa kiwango cha lami,ili nasi tupate usafiri wa Anga. Ombi, tunaomba kasikuongezwa katika kuendeleza ukarabati huo, ambaohaujaonekana ipasavyo, kwani tuna kiu kubwa nakukamilishwa mradi huo kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, bado nasisitiza Wizara kuangaliauwezekano wa kuweka utaratibu wa kuzijenga barabara zamabonde ya Rukwa na Tanganyika kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, mwisho, naunga mkono hoja.

SPIKA: Sasa tuanze kupata feedback ya upande waSerikali. Tunaomba tuanze na Wizara ya Fedha, halafu naMheshimiwa Naibu Waziri Kwandikwa ajiandae robo saa.

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

Wizara ya Fedha dakika 10, Mheshimiwa Waziri wa Fedha,tafadhali.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,kwanza nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niwezekuchangia kwenye mjadala huu wa bajeti ya Wizara hiimuhimu sana ambayo inachukua sehemu kubwa ya keki yabajeti ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea, naombamuungane nami kumpa pole Secretary wangu ambayealfajiri hii amepotea mume wake, Mama Dionisia Mkoma,ndiyo maana sijakaa vizuri hata mimi mwenyewe.

MBUNGE FULANI: Pole sana.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Ahsante.

Mheshimiwa Spika, pia naomba nitoe pongezimahsusi kwa Mheshimiwa Rais ambaye ameendelea kutoakipaumbele cha juu kwenye ukarabati na ujenzi wamiundombinu msingi, yaani basic infrastructure na hiiamefanya kwa umahiri mkubwa tangu alipokuwa Waziri waUjenzi; na kwa kweli alitambua mapema sana kwambamiundombinu ni kichocheo na mhimili mkuu wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, pia nitumie nafasi hii kumpongezaMheshimiwa Waziri mwenye dhamana Mhandisi Kamwelwena Naibu Mawaziri Mhandisi Elias Kwandikwa, MhandisiAtashasta Nditiye. Kwa kweli wanatekeleza majukumu yaovizuri pamoja na watendaji wao ambao wamekaa kulenyuma ya kioo wakiongozwa na Makatibu Wakuu husika.Niseme mapema kabisa kwamba naunga mkono hojaambayo iko mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kusema,ninaunga mkono kwa sababu kwa kweli uwekezaji katikaujenzi wa miundombinu ya kisasa inachochea uchumi namaendeleo ya nchi na watu wake kwa namna nyingiambazo Waheshimiwa Wabunge wanazifahamu. Ujenzi wa

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

miundombinu unatengeneza fursa nyingi sana za ajira, lakinipia kipato kwa wananchi wetu. Ujenzi na ukarabati wamiundombinu unatumia nguvu kazi yenye ujuzi na ndiyomaana bench pale tunaona ni Wahandisi watupu auwaliowatangulia ni wanasayansi na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, pia miundombinu borainapunguza sana gharama za uwekezaji na uzalishaji nainaongeza uwezo wa kusafirisha watu, malighafi, bidhaa nakadhalika na kufanya biashara iende kwa haraka zaidi. Kwakweli moja ya tofauti kubwa ya nchi zetu masikini na nchizilizoendelea ni ubora wa miundombinu. Kila unaposafiriukaenda nchi yoyote il iyoendelea, kitu cha kwanzaunachoona ni tofauti ya miundombinu. Ndiyo maana katikamwaka ujao wa fedha kwa makusudi kabisa Serikaliimeitengea Wizara hii shilingi bilioni 606 zaidi ya bajeti yamwaka huu wa fedha tuliyonayo ambayo ni takribani asilimia12.8 ya ongezeko.

Mheshimiwa Spika, mgawanyiko wa fedha kwenyeWizara hii, umezingatia maoni ya wadau mbalimbali naWaheshimiwa Wabunge na hasa kwamba tujielekeze kamaSerikali kwenye ujenzi wa reli mpya ya kisasa ili barabara zetunazo ziweze kudumu lakini pia ili tuweze kupata manufaamakubwa ya kuwa na hiyo miundombinu ya kisasa.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasanaomba nichangie baadhi ya hoja ambazo zilijitokeza.Kwanza tulishauriwa kwamba Serikali katika ujenzi wa reli yakati iufanye kwa kuzingatia faida za kiuchumi. Napendanilihakikishie Bunge lako Mheshimiwa Spika na Watanzaniakwa ujumla kwamba kazi hii ya kujenga reli imezingatia fursambalimbali za kiuchumi na kijamii ambazo zinapatikanakatika ukanda mzima wa reli, fursa za kilimo, madini, mifugona uvuvi pamoja na biashara miongoni mwa mikoa yetu,lakini pia katika nchi jirani.

Mheshimiwa Spika, lilisemwa sana lile la kipande chaTabora – Kigoma ambacho inajulikana, nami ni mmoja wawadau wakubwa, nisisitize tu kwamba hili ni muhimu, halina

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

mjadala, lakini kikubwa ni kwamba tunajenga reli hii awamukwa awamu na changamoto kubwa tuliyonayo ni upatikanajiwa fedha na tunaangalia options zote ikiwemo na kiasiambacho kinaweza kugharamiwa na Serikali peke yake aukwa kushirikiana na wabia wengine na pia upande wamikopo. Punde tutakapomaliza upande huu wa financinghakuna mashaka kabisa. Napenda tujenge hata vipandevyote kwa mara moja. Kwa hiyo, hili tunalifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, tuliambiwa pia tuangalieuwezekano wa kupata mkopo wenye gharama nafuukuharakisha ujenzi wa reli nchini. Niseme tu kamanilivyotangulia kusema kwamba hili tunalifanya Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Shirika letu la Reli,wameanza upembuzi yakinifu kwa miradi ya reli ambayoitatekelezwa kwa utaratibu wa PPP na hususan ile ya Mtwara,Mbamba Bay kupitia Mchuchuma na Liganga na pia ile reliyetu ya Tanga - Arusha – Musoma.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa reli ya kati,naomba niliarifu Bunge lako kwamba Serikali iko katikamazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika ili watusaidieku-leverage private sector investment na PPP na nilipokuwaAbidjan nilikuwa na mazungumzo na Dkt. Adesina kwa ajiliya hii na siyo kwa kipande tu cha kuelekea Kigali, lakini kwavipande vingine vyote ambavyo bado tunatafuta fedha.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na swali kuhusu deni laTAZARA ambalo uhakiki wake umekamilika na kwambaSerikali ilipe hilo deni lililopo upande wa nchi yetu. Tulipokeamadai ya TAZARA bilioni 59.6 kwa ajili ya kulipa madeni yamishahara na michango kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.Kama inavyojulikana madeni hayana yanatokana nachangamoto mbalimbali ambazo zilikabili TAZARA kuanziamiaka ya 1990 ikiwemo na kushindwa kabisa kujendesha,lakini pia malimbikizo ya wastaafu. Sasa tumefanya nini kamaSerikali, kuanzia 2015 tulianza kusaidia ulipaji wa mishaharaya watumishi wa TAZARA na tunalipa takribani shilingi bilioni1.25 kwa mwezi na tumefanya hivyo hadi Aprili, 2019 natumekwishalipa jumla ya bilioni 67.44.

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

Mheshimiwa Spika, lakini mwaka uliopita 2017/2018,tuliongeza pia mtaji wa TAZARA tukalipa bilioni 10 kwa ajili yakukarabati vichwa na engine za treni za TAZARA. Kuhusumadai ya TAZARA ambayo yamepokelewa karibuni,tunayafanyia uchambuzi wa kina ili tuweze kupata namnabora ya kuyalipa na kuwezesha shirika kujiendesha kwa lengokudhibiti uzalishaji wa madeni mapya.

Mheshimiwa Spika, tuliambiwa pia hapa kwambaSerikali iharakishe kulipa madeni ya pension kwa wafanyakaziwaliokuwa Posta chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikulipunguzia mzigo shirika. Serikali ilikwishafanya malipo kwawastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na zoezimaalum la kuwalipa wastaafu li l ishafungwa natulishawaandika hivyo toka Disemba, 2016.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, tunashughulikia hojazinazowasilishwa na wastaafu kwa kulingana na maombi aumalalamiko yanayohusika na malalamiko hayo huwayanawasilishwa kupitia taasisi ambazo walizifanyia kazi haowastaafu.

Mheshimiwa Spika, kwa wafanyakazi wa Posta waJumuiya ya Afrika Mashariki, maombi ya madai yenye jumlaya shilingi bilioni sita yalikwishapokelewa na tumekwishalipabilioni 2.7 kufikia Februari, 2017 na kiasi kilichosalia ambaponyaraka zilikuwa zina utata kiliwasilishwa kwenye Ofisi yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mweziFebruari, 2019 kwa ajili ya uhakiki malipo yaweze kufanyika.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba mradiwa kuboresha Bandari ya Dar es Salaam...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana bahati mbaya muda umekwisha.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha.Sasa naomba nimwite Naibu Waziri, Mheshimiwa EliasKwandikwa, dakika 15.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, nikushukurusana kunipa nafasi nami niweze kuchangia kwenye hoja hiimuhimu. Kwanza nianze kwa kuunga mkono hoja hii muhimuiliyopo mbele yetu kwa asilimia mia moja. Pia nimshukuru sanaMwenyenzi Mungu kwa kuniwezesha kusimama hapa leo.Nimshukuru sana Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli kwa utashi na dhamira yake ya kweli yakuwajali wanyonge hususan kwa kutengeneza miundombinubora. Hii miundo mbinu itachangia kukuza uchumi nakupunguza umaskini kwa sababu huduma itakwenda kwawafanyabiasha, wakulima, huduma za kijamii wafanyakazina kadhalika.

Mheshimiwa Spika nimshukuru na kumpongezaMheshimiwa Waziri Mkuu wetu kwa namna anavyosimamiashughuli za Bunge, lakini niruhusu nimshukuru na kumpongezasana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe,kwa ushirikiano na miongozo anayonipa ili kutimiza majukumuyangu. Aidha, namshukuru pacha wangu MheshimiwaNditiye kwa namna tunavyoshirikiana katika kufanya kazi. Vilevile niwashukuru watendaji, Katibu Mkuu Arch. EliasMwakalinga na Makatibu Wakuu wengine wote LeonardChamuriho, Dkt. Maria Sasabo, Naibu Katibu Mawasiliano,Jim Yonaz na watendaji wengine wa Wizara nawashukurusana.

Mheshimiwa Spika, nikushukuru wewe mwenyewe,Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wenyeviti namnamnavyotupa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yetu yaWizara hii ya ujenzi. Pia inaishukuru Kamati yetu yaMiundombinu na Wabunge wote kwa ushirikiano wanaotupandani ya Bunge na hata nje ya Bunge. Tunaendelea kupokeamaoni na ushauri wa Wabunge na sisi pia inatuboresheakufanya kazi zetu. Vile vile niwashukuru wapiga kura waUshetu. Leo Madiwani wa Ushetu wapo hapa ni mashahidi,

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

Madiwani wote hawa wa Chama cha Mapinduzitunashirikiana vizuri na mimi kwa u-busy wangu Madiwanihawa kazi nyingi wanazifanya, Ushetu inakimbia kwa speedkubwa. Mwisho, niishukuru familia yangu Dkt. Macelina yupohapa mke wangu, namshukuru sana kwa ushirikianoanaonipa katika shughuli zangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja zilikuwa nyingi lakini ni uhakikakwamba sio rahisi kuzungumza mambo mengi sana hapa,lakini niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge ushauri waotumeupokea na yote waliyozungumza tutayajibu nakuyawasilisha kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, nizungumze mambo machache;kwanza kwa upande wa barabara; niseme tu kazi kubwaimefanyika, mtandao wa barabara nchi nzima barabara kuuza Kitaifa tuna kilometa 36,258. Kati ya hizo barabara kuu nikilometa 12,176, barabara za mkoa ni kilometa 24,082, lakinikati ya barabara hizo kilometa 10,061 zipo sasa kwenyematandao wa lami kwa maana barabara kuu kilometa 8,870na barabara za mkoa ni kilometa 1,756. Niseme tu kwa miradiinayoendelea hadi Aprili ni miradi 34 ambayo itakuwa naurefu wa kilometa 1,505 na hii miradi yote ikikamika ina-commit fedha nyingi kama Wabunge walivyosema trilioni7.799, ni fedha nyingi, lakini katika bajeti hii tuliyowasilishakutakuwa na ongezeko, tutakuwa na miradi kama 37 kwamaana tutakwenda kuhudumia barabara kwa ujenzi wa lamikilometa 1,961 na madaraja sita, hii ni achievement kubwa.Nitumie nafasi hii pia kumshukuru Mheshimiwa Rais zaidi nakumshukuru Waziri wa Fedha kwa sababu waanaendeleakutuwezesha na kazi kubwa inaendelea kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumze juu ya ujenzi waviwanja vya ndege kwa ufupi. Waheshimiwa Wabungewengi walivyokuwa wakichangia wamezungumza juu yamiradi ya fidia, lakini niseme kwamba, mwaka 2018 tulifanyauhuishaji wa uthamini ambao awali ulikuwa umefanyikamwaka 2007. Kwa hiyo, niwahakikishie tu Watanzania kwaujumla kwamba kwenye maeneo ambayo kwamba tunacompensation kwa mujibu wa sharia, tunahuisha ili kuona

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

tunakwenda kulipa compensation na wananchi wanapatahaki yao.

Mheshimiwa Spika, kwa wachangiaji tulikuwa naUwanja pia huu wa Ndege wa Msalato ambapo wapowaathirika ambao wanapisha ujenzi wa uwanja 1,926.Niwahakikishie kwamba takribani bil ioni 14 ambazotunazifanyia kazi ili waweze kulipwa hawa na kwa vile uelekeowa kupata fedha ili kujenga uwanja huu upo, kwa hiyowananchi hawa wa Dodoma husasan eneo la Msalato naotumejipanga pia pamoja na wengine wa maeneo menginewatapata fidia zao.

Mheshimiwa Spika, yapo maeneo mengi ambaouthamini wa mali umeendelea; Lake Manyara, kule Simiyu,kule uwanja wa ndege wa Nyerere, Musoma na Songea.Katika maeneo haya yote Waheshimiwa Wabungewalichangia, lakini tumejipanga vizuri kuendelea kufanyamalipo ya fidia, kwa sababu yapo maeneo mengi piaambapo malipo yameshafanyika, kwa hiyo, tunaendeleakufanya uhakiki tukipata fedha tuanendea kulipa.

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba WaheshimiwaWabunge pia wameuliza kwamba ni lini Serikali itaweka taaza kuongozea ndege. Kwa ufupi niseme kuwa, maeneo yoteambayo tunafanya maboresho ya viwanja vya ndegetutazingatia hili suala la kuweka taa za kuongozea ndege.Kwa hiyo katika maeneo mbalimbali ambayo tuna mradi kwamfano kule Mafia na kule Songwe, taratibu za manunuzizinakamilika mwezi wa tarehe 30 Aprili kwa hiyo tunaendeleakuharakisha ili tuende kufanya maboresho lakini katikamaboresho tutazingatia mahitaji na vipaumbele ili viwanjahivi viweze kuwa bora na bora zaidi.

Mheshimiwa Spika, nizungumze pia kwamba uwanjawetu wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere unatarajiakukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa Mei, 2019 na miradiya ujenzi wa viwanja vya ndege vingine katika maeneomengine tuko kwenye harakati ya kufanya maboresho;Uwanja wa Ndege wa Songea, Uwanja wa Ndege wa

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

Mtwara, ujenzi unaendelea kule Geita, Mwanza Nachingweana kama nilivyosema pia na upande wa Uwanja wa Songwetufanya maboresho makubwa ya jengo la abiria. NaonaMheshimiwa Mwakajoka ananiangalia hapa, kwa hiyotunakwenda vizuri katika uwanja huu ili tuweze kuufanyiamaboresho makubwa.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge piawameuliza kuhusu suala la ujenzi na ukarabati wa Viwanjavya Ndege vya Haydom, Kilwa Masoko, Lindi, Mafia,Manyara, Musoma, Mwanza na Tanga. Serikali inaendeleakutafuta fedha na pia inafanya mazungumzo na washirikambalimbali wa maendeleo ikiwa ni pamoja na Benki yaDunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika Serikali ya Jamhuri yaWatu wa China na kadhalika kwa ajili ya ujenzi na ukarabariwa viwanja vyote vya ndege hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, nizungumze kidogo juu ya vivuko;ujenzi wa vivuko vipya viwili katika mwaka 2018/2019umekamilika kwa maana ya Kivuko cha Kigongo- Busisi, MVMwanza imekamilika na Magogoni - Kigamboni MV Kazi napia tunaendelea kujenga vivuko vingine, kwa mfanoukarabati wa vivuko vitatu MV Sengerema, MV Kigamboni,MV Utete, lakini pia tunajenga kivuko kipya kitakachofanyahuduma kati ya Kayenze na Benzi. Tumepanga vivuko hiviviweze pia ku-move kwenda pande nyingine, kivuko hikikikikamilika ni cha kisasa, kitaweza kwenda maeneo ya Ukarakule Nansio kitatoa huduma katika maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, miradi mingine ya ujenzi wamaegesho ya Bwina kule Mkoani Geita maegesho ya kivukokati Lindi na Kitunda, Mkoani Lindi, upanuzi wa maegeshoKigamboni pamoja na upanuzi wa jengo la kupumzika abiria.Kule ng’ambo Kigamboni tunaendelea kufanya maboresho,kuna mchangiaji mmoja hapa Mheshimiwa Mbungealizungumza kwamba hakuna kinachoendelea, lakinitunaendelea kufanya maboresho, nafikiri labda hakuwepomuda mrefu, anaweza akajionea yeye mwenye kwambatumejipanga vizuri ili huduma hii iweze kuboreka.

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

Mheshimiwa Spika, ndugu yangu Mheshimiwa Tizebaamezungumza juu ya Kivuko cha Kome – Nyakalilo, tutafanyaitakavyokuwa imewezekana kwa sababu tuna harakati zakujenga vivuko vingi, tunaona namna nzuri ili wananchiwapate huduma ya vivuko kulingana na mahitaji. Kwa hiyo,nimtoe hofu Mheshimiwa Tizeba kwa sababu tulipata ajaliya kivuko wakati tulikuwa tumelenga tumpelekee kivuko kwasababu ya matatizo yaliyotokea, hivyo avumilie kidogo,tutaona namna nzuri ya ku-reallocate ili tuweze kupatahuduma nzuri katika eneo hili la Kome kwenda Nyakalilo.

Mheshimiwa Spika, nizungumze juu ya maboreshomakubwa na taasisi yetu ya TEMESA, Wabunge wengiwamezungumza, tunaendelea kuboresha, kumekuwa nachangamoto na huduma za TEMESA, nakubaliana nao, lakinikama Wizara tumejipanga kuboresha karakana hii kwamaana ya kuongeza vitendea kazi na kuweka vifaa stahiki.Hata hivyo, kuna baadhi ya maeneo kwenye Wilaya kamakule Ifakara tumepeleka huduma na maeneo menginetunaendelea kuwasogezea huduma wananchi ambaowanapata huduma hizi hususan taasisi za Serikali ili wawezekuzipata kwa ukaribu zaidi. Tunalenga kwenda kupelekahuduma hii katika Wilaya 25.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie juu ya huduma yamajengo na nyumba za Serikali. Imetolewa hoja kwambagharama ni kubwa katika ujenzi, lakini nilikuwa nimejaribukufanya mapitio kwamba pamoja na changamoto nyingiambazo zipo kwenye TBA, Wizara inaendelea kushughulikiaikiwepo tatizo la wafanyakazi, tunaendelea kuongezawafanyakazi ili tuweze kuboresha huduma hizi. Tulifanyautafiti kuona kwamba zile huduma za ujenzi bado zipo chinikwa miradi kadhaa, mfano, ujenzi wa mabweni Chuo Kikuucha Dar es Salaam tulijenga kwa bilioni 10, lakini wenginewaliwasilisha gharama za ujenzi kwa bilioni 90. Pia gharamaza ujenzi wa shule ya sekondari Ihungo wengine walituleteakwa bilioni 60 hadi 200, lakini Wakala walijenga kwa bilioni12. Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita bilioni 17 ndio TBAwanajenga, lakini wengine walituwekea bilioni 67. Sasautaona gharama zipo chini kati ya wastani wa 30% hadi 40%.

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

Mheshimiwa Spika, niseme jambo moja hapa ambaloWaheshimiwa Wabunge walizungumza juu ya kufanyauchunguzi kuhusu baadhi mikataba ambayo imehusikakwenye ujenzi wa shule kongwe, sisi Wizara tupo tayaritutaunda timu ambayo itahusisha wafanyakazi wa AQRB,CRB na ERB ili kupitia upya mikataba yote na tuweze kupataushauri kupata ushauri ili tuweze kuchukua hatua stahiki.

Mheshimiwa Spika, nimalizie tu kusema MheshimiwaKingu alizungumza kwa uchungu hapa kuhusu barabara zaSingida. Kwanza Mheshimiwa Kingu nimpe faraja kwambakatika bajeti hii tutatengezea barabara za mzunguko kwenyeMkoa Singida, kilometa 46 kwa mapendekezo ambayo yapombele ya meza. Hata hivyo, nimhakishie kwamba kwenyeeneo la kutoka Singida kwenda Mgungila kwamba katikabajeti ya mwaka huu inayoendelea 2018/2019, tulikuwatumetenga zaidi ya milioni 150 kwa ajili ya kuboresha, kujengamadaraja katika maeneo ambayo ni korofi na kuwezakuanza kunyanyua tuta. Kiasi cha fedha ambachokinaonekana hapa ni kwa ajili ya kuendelea kufanyamaboresho katika eneo hili na maeneo mengine, mudahautoshi, nafahamu kwamba yapo maeneo mengi ambayokwenye Mkoa wa Singida kama alivyosema MheshimiwaKingu tunaendelea kufanya maboresho mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, ningezungumza kidogo kwakumalizia kuhusu ule mgawanyo wa fedha wa Mfuko waBarabara. Niseme tu kwamba mgawanyo wa fedha upokisheria, ni suala la kuangalia sheria lakini kwa upande waWizara kupitia, Bodi Mfuko wa Barabara tumeweka mshauriili aweze kufanya mapitio tuone namna nzuri wa kufanyamgao huu wa fedha za TARURA na upande wa TANROADS.Hili zoezi linafanyika kwa sababu pale awali mgawo ulikuwa80% kwa 20% kabla haujaenda 70% kwa 30% kwa mujibu washeria ilivyokuwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunaendelea kukamilishiahili zoezi ili tuone urefu wa barabara, network nzima ili tuwezekuona matumizi ya barabara kwa sababu ndio baseskwamba ni vyombo vingapi, uzito upi unapita kwenye

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

barabara zetu ili sasa tuweze kuona namna nzuri namna nzuriya kufanya mgawanyo wa barabara hizi, pia tutazingatiahali ya jiografia. Ili twende vizuri wenzetu Wizara ya Fedhapia wanalifanyia kazi jambo hili na tukiweza kuongea fedhaza ujenzi wa barabara tutaendelea kuziboresha barabarazetu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,nikushukuru sana kwa nafasi hii na nimalizie kwa kusemakwamba, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri,Mheshimiwa Elias Kwandikwa, tunakushukuru sana kwakupitia hoja za Waheshimiwa Wabunge vizuri. NawaonaWaheshimiwa Madiwani wa Ushetu wapo hapa na leo poshozao zimezungumziwa hapa asubuhi, kwa hiyo hapa Dodomatunasema mambo mswanu, mambo mazuri.

Waheshimiwa Wabunge, basi kwa hatua hii,tutakaporudi jioni ataanza Mheshimiwa Nditiye kwa robo saa,halafu atafutiwa Mheshimwa Waziri, by saa kumi na mojakamili tutaanza kupitia mafungu kwa sababu ni mengi ilituone tutakimbia kiasi gani. Naomba wale ambaowamejiandaa kwa ajili ya mambo hayo, basi waweze kuwahina wengine wote tuwahi kufika ili tuimalize kazi hii mapemakwa pamoja.

Kwa hatua hii basi, naomba nisitishe shughuli za Bungehadi saa kumi kamili jioni ya leo.

(Saa 6.58 Mchana Bunge lilisitishwa mpaka Saa 10.00 Jioni)

(Saa 10.00 Jioni Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabuunge, tukae. Tunaendeleana Kikao chetu cha Ishirini na Sita na majadilianoyanaendelea.

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na upandewa Serikali, sasa namuita Mheshimiwa Naibu Waziri, Ujenzi naMawasiliano, Mheshimiwa Engineer Atashasta Nditiye. Karibusana, una robo saa. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa, naomba nichukue nafasi hii kumshukuru sanaMwenyezi Mungu kwa nafasi aliyotupatia kukutana mahalihapa kwa ajili ya kujadili mambo muhimu yanahusu nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, pili, nichukue nafasi hii kumshukurusana Mheshimiwa Rais kwa majukumu mengi sanaanayofanya kwa ajili ya nchi yetu. Nimpongeze vilevile kwamajukumu mengi anayoendelea nayo na nashukuru kwakuniamini niweze kumsaidia.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee kabisa,nichukue nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Mhandisi IsackAloyce Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilianokwa support kubwa anayonipatia katika kutekelezamajukumu yangu.

Nichukue nafasi hii vilevile kumpongeza sana nakumshukuru pacha wangu Naibu Waziri wa Wizara hii yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayehusika na Ujenzi,Mheshimiwa Eliasi John Kwandikwa bila kuwasahauwatendaji wote nikianza na Mhandisi Dkt. Chamuriho (KatibuMkuu wa Uchukuzi), Mhandisi Dkt. Maria Sasabo (Katibu Mkuuwa Mawasiliano) na Arch. Mwakalinga (Katibu Mkuu waUjenzi).

Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru sana Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa maelekezo namisaada mbalimbali wanayoipatia Wizara yetu katikakutekeleza majukumu yake. Nichukue nafasi hii niwashukuruWabunge wote kwa ushirikiano, urafiki na ukarimu ambaowanaitendea Wizara yetu katika kutekeleza majukumu yake.(Makofi)

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

Mheshimiwa Spika, nawashukuru sana wapiga kurawangu wa Jimbo la Muhambwe lililoko Mkoa wa Kigoma,Wilaya ya Kibondo. Vilevile naishukuru familia yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipatianafasi hii na mimi niweze kuchangia hoja iliyo mbele yetu.Kwa sababu ya muda nitajaribu kujieleza kwa baadhi ya hojachache tu, kwa upande wa uchukuzi nitagusia masuala yahali ya hewa lakini nitagusia miradi miwili mikubwa yakimkakati ya reli ya kutoka Tanga - Musoma na Mtwara -Mbambabay. Nikipata nafasi nzuri nitagusia masuala mazimaya ATCL lakini kwenye mawasiliano nitazungumzia suala lausajili wa laini za simu pamoja na utendaji wa UCSAF.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee, kwanza,nitoe pole kwa Watanzania wenzetu ambao wamepatamadhara sehemu mbalimbali kutokana na mvua nyingi nakubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchiyetu. Sasa hivi Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo kadhaaya Pwani yame-experience mafuriko ambayo yanaendelea,tunaona kwenye mitandao ya kijamii na sehemu mbalimbalina tunapigiwa simu hata na ndugu zetu kwamba hali si nzurisana kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, niipongeze Mamlaka ya Hali yaHewa imekuwa ikifanya kazi nzuri sana ya kuwaelimishaWatanzania juu ya athari ambazo zitatokea kwa siku zijazokutokana na vifaa vya kisasa wanavyovitumia. Itakumbukwakwamba tarehe 21 Aprili, 2019, Mamlaka ya Hali ya Hewawalitoa tahadhari kwamba Mikoa ya Kusini Lindi na Mtwaraingekumbwa na kimbunga cha Kenneth. Bahati nzurituliendelea sana kuhakikisha kwamba tunatoa tahadharikwa wananchi lakini Mungu akatuepushia mbali kilekimbunga hakikuweza kutoa athari kubwa. Ilipofika tarehe24 tuliwatahadharisha tena hata wenzetu wa Mikoa ya Simiyuna Shinyanga kwamba kuna kimbunga ambacho kingetokeakutokea misitu ya Congo kingeweza kuathiri maeneo yaKahama na tulishuhudia kwamba kulikuwa na mafurikoyaliyotokea.

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

Mheshimiwa Spika, hili najaribu kuwaelezea baadhiya Wabunge ambao walithubutu kusema kwamba Mamlakaya Hali ya Hewa inafanya utabiri kama waganga wa kienyeji,hiyo sio kweli. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania sasa hiviinafanya utabiri wake kwa asilimia 87.8. Katika hali yakawaida tungepaswa hata kuondoa lile neno utabiri tuwetunasema tu hali ya hewa kama mataifa yaliyoendeleayanavyofanya. Wakisema kitu kinatokea na sisi kupitiaMamlaka ya Hali ya Hewa tukisema kitu kinatokea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mvua kubwa zinazoendeleakunyesha Mkoani Dar es Salaam na maeneo ya Pwani nisehemu ya mvua za masika. Nitoe wito kwa Watanzaniawenzetu kwamba mvua hizi ni kubwa na zitaendelea kuwepokwa kipindi chote mpaka mwisho wa mwezi huu. Tunaombawachukue tahadhari na waendelee kufuatilia taarifa zaMamlaka ya Hali ya Hewa. Tumejipanga kuhakikisha kwambatunawahabarisha Watanzania ili wachukue tahadharimbalimbali kujiepusha na uharibifu wa mali zao lakini pia namaisha yao.

Mheshimiwa Spika, ili kuwezesha Mamlaka ya Hali yaHewa kutoa utabiri wa viwango vya kimataifa, Serikaliimeendelea kuhakikisha kwamba mamlaka ina wataalamwaliobobea katika masuala ya Hali ya Hewa. Aidha, Serikaliimeendelea kuhakikisha kuwa Mamlaka inakuwa na vifaavya kisasa vya kufanya uangazi (observation) na utabiri.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni Serikali imeingiamkataba wa ununuzi wa rada tatu za kisasa za hali ya hewaambazo zitafungwa katika Mikoa ya Mtwara, Mbeya naKigoma. Rada itakayofungwa Mtwara itasaidia kufuatiliavimbunga katika bahari ya Hindi, rada itakayofungwa Mbeyaitasaidia kuhudumia wakulima kwenye mikoa inayozalishachakula kwa wingi lakini na rada itakayofungwa Kigomaitasaidia katika kufuatilia na kutoa tahadhari ya matukio yaradi na taarifa muhimu kwa wananchi wanaofanya shughulizao katika Kanda ya Ziwa Tanganyika na mwambao wa ziwahilo. Ununuzi wa rada hizo tatu utaifanya Tanzania kuwa na

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

jumla ya rada tano ikijumuisha na rada zilizofungwa Dar esSalaam na Mwanza.

Mheshimiwa Spika, nitaongelea kiasi fulani suala laujenzi wa reli kati ya Tanga - Musoma. Hatua tuliyofika mpakasasa hivi kwa upande wa Serikali ni kufanya upembuzi yakinifulakini tumekwishafanya usanifu wa awali na wa kina,tumekwishajua gharama zinazopaswa. Hatua iliyoko sasa hivini kutafuta mwekezaji ambaye ataingia mkataba na Serikalikufanya mradi huo kwa njia ya PPP.

Mheshimiwa Spika, katika kufikia hatua hiyo kunakitengo ambacho kiko Wizara ya Fedha ambacho ndiyokinashughulika na mikataba hiyo. Watu wa Wizara ya Fedhawanatusaidia katika kuhakikisha kwamba mikatabaitakayoingia na mwekezaji mbia inakuwa na tija kwa nchiyetu. Hatuko tayari kuona kwamba nchi yetu inaingia kwenyemikataba ambayo haina tija kwa wananchi. Sisi tumejipangakuhakikisha kwamba mikataba yote tutakayoingia inakuwana tija lakini inawasaidia wananchi kwa kizazi cha sasa, chakesho na kinachokuja.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kuna wabiawamekuwa wakijitokeza mara kwa mara kupitia Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutaka kuwekeza kwa njiaya PPP kwa reli ya Tanga – Musoma lakini pia kwa reli yaMtwara - Mbambabay. Hata hivyo, masharti yao wakatimwingine yanakuwa ni magumu sana kutekelezeka natumekuwa tukiendelea na mazungumzo nao kuhakikishakwamba mkataba kati yetu sisi Serikali na wao basi unakuwana tija kwa nchi yetu. Tusiumie lakini na wao wasiumie wapatefaida kwa sababu tunategemea waingize hela zao katikashughuli hizo.

Mheshimiwa Spika, vipande vya reli kutoka Tanga -Musoma na kipande cha reli kutoka Mtwara - Mbambabayna matawi yake ya Mchuchuma na Liganga bado yakokwenye mazungumzo na yako mahali pazuri. Itakapofikiamahali muafaka tutawaelewesha Watanzania kwamba sasatunaingia mkataba kwa ajili kutengeneza reli hizo.

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kidogo suala landege zetu za ATCL. Serikali imenunua ndege hizo nakuwapatia ATCL ili wazifanyie biashara warudishe pesa kwaSerikali. Hivi karibuni kumetokea maneno ya manung’unikokidogo kutoka kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabungekwamba nauli za ATCL zimekuwa kubwa. Ukweli ni kwambasi sahihi, nauli za ATCL bado zimeendelea kuwa ni nafuukabisa na ndiyo maana Waheshimiwa Wabunge wengi huwawanakuwa na option namba mbili baada kukosa tiketi zaATCL, ni kwa sababu huduma ni nzuri na nauli zao ni nyepesi.

Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida tunakubalikuwa na ushindani, kuna ndege nyingine za Precision, zikondege za aina mbalimbali na zenyewe zinatoa hudumakwenye njia ambazo ATCL wanafanya kazi. Huwa wanaanzakwa bei nafuu lakini mwisho wa siku wanaenda kuwa nagharama kubwa sana ambazo wateja wao huwawanakimbilia ATCL. Nakuomba sana tuwashawishi Wabungewaiunge mkono ATCL, ni shirika letu la ndege ili liwezekuendelea kutoa huduma nzuri na za uhakika na ndege zetuni za uhakika.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo nikiri changamoto yakuwepo kwa delay za ndege zetu. Nikiri changamoto ya kuwana cancellation kwenye baadhi ya route. Hilo ni la kwelitumekwishalishuhudia na sisi kama Serikali tumeshatoamaelekezo kwa ATCL kwamba kuanzia sasa hivi ndegeyoyote ambayo itakuwa na delay zaidi ya nusu saa tunahitajitupate maelezo ya maandishi yakiambatana na vielelezo.Kama ni hali ya hewa basi tupate na taarifa ya hali ya hewaambayo imeambatanishwa ku-justify maelezo ya delay yasafari husika. Hilo tumekwishaongea na watu wa ATCL nawanafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba safarizote za ndege haziwi na changamoto mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, niongelee kwa harakaharakamasuala ya mawasiliano, kuna suala la usajili wa laini za simu.Ni kweli kuanzia tarehe 1 Mei, Serikali kupitia TCRA imeamuaWatanzania wasajili laini zao za simu kupitia alama za vidolezikiambatana na kitambulisho cha NIDA.

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

Mheshimiwa Spika, kwanza nifafanue ni laini moja kwakila mtandao. Kama una mitandao ya Tigo, Voda, Halotel,Airtel na TTCL unaruhusiwa kuwa na laini moja moja. Endapoutahitaji laini ya pili eleza tutakusajili.

Mheshimiwa Spika, nia ya kufanya hivyo ni kuhakikishakwamba kwa kiasi kikubwa tunayadhibiti matumizi mabayaya mtandao. Ukisajili laini zako tatu za Voda tukajua kabisani wewe umesajili maana yake ikitumika vibaya basitutakuchukua halafu tutakupeleka kwa upole kabisa ili uwezekwenda kuwasaidia Polisi kutoa maelezo ya hichokilichokufanya utumie mtandao vibaya, hatuna lengo baya.

Mheshimiwa Spika, suala la vitambulisho tumeamuakuchagua kitambulisho cha NIDA kwa sababu moja tukwamba ni kitambulisho ambacho kinavuka mipaka yoteTanzania Bara na Tanzania Visiwani. Kitambulisho cha Mkaziwa Zanzibar tunakikubali, ni halali na kizuri na hakina tatizolakini tunachokiona ni kwamba kile kinatumika kwaMzanzibar, kikija huku Bara hakitumiki, kwa hiyo, hakiwezikutumika kwa Bara lakini mitandao ya simu kama Halotel,Tigo na kadhalika inatumika Bara na Visiwani. Tukichukuakitambulisho cha kule peke yake hakitatusaidia kudhibitiuhalifu.

Mheshimiwa Spika, pia leseni za magari siyo kilaMtanzania aliyetimiza miaka 18 ni lazima awe na leseni yagari. Kuna wengine hawana leseni ya gari, wale ambaohawana leseni ya gari wanahitaji kuwa na mawasiliano yasimu. Kwa hiyo, tumeona kwamba kitambulisho cha NIDAkitawasaidia kwa sababu kile ni kitambulisho ambachokinamhusu Mtanzania yeyote aliyetimiza miaka 18.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa hivi nipende kutoataarifa kwamba kwa Zanzibar taarifa za NIDA zinasema zaidiya asil imia 90 wameshapewa namba ya usaji l i wavitambulisho vya NIDA. Masuala ya kupata kitambulishoyanaendelea taratibu lakini namba za usaji l iwamekwishapata. Kwa hiyo, tuna uhakika kwambawataweza kusajili bila tatizo lolote.

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Tanzania Baratuko kwenye Watanzania milioni 16. Kwa hiyo, ukichanganyatuko mahali pazuri na bado tunaamini kwamba kwa miezinane tuliyoitoa, Watanzania wengi watakuwa wameshasajilina wataweza kutumia huduma vizuri kwa usalama wao lakinikwa uchumi vilevile kuona kwamba zile message za tafadhalinitumie pesa kwa namba hii zinadhibitiwa kwa kiwangokikubwa.

Mheshimiwa Spika, Kuna Mheshimiwa Mbungealizungumza kuhusu masuala ya picha za ajabu ajabu. Ningumu sana kama Serikali kumdhibiti mtu yuko chumbanikwake akaamua kujipiga hizo picha akaangalia mwenyewe.Huwezi kumzuia mtu kama huyo apige picha aangaliechumbani kwake afurahi kama inaweza ikamsaidia lakinianapoitoa nje ya chumba chake ikaanza kusambaatutamkamata yule wa mwisho mpaka yule wa kwanzaaliyejipiga zile picha akazituma kule. Nia na madhumuni nikwamba mitandao ya mawasiliano itumike kwa faida kwaWatanzania wote bila kuathiri mtu mwingine yeyote ambayehataki taarifa ambazo wewe unazo. Tumejipanga kuhakikishakwamba tunadhibiti uhalifu wa kimtandao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa kuna suala laUCSAF na minara ya mawasiliano. Niliwahi kuzungumzakwamba tunafahamu changamoto ya minara yamawasiliano kwa Waheshimiwa Wabunge na tumeendeleakufanya kazi kwa bidii sana kuhakikisha kwamba eneo kubwasana la nchi yetu linapata mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa hivi asilimia 94 yaWatanzania wanawasiliana. Tunachokiangalia ni kwambakuna mawasiliano eneo fulani. Changamoto ndogo sanatunayoipata sasa hivi ni kwamba kama kuna mawasilianoya Halotel kuna Watanzania wanataka Voda au Tigo lakinisisi Kiserikali tunasema eneo fulani Kongwa wana mawasilianokwa sababu wana mtandao wa Halotel labda na TTCL.Wakipata dharura watapiga simu, wakitaka kuuza mazaowatapiga simu, wakitaka kufanya miamala kutoka Benkikwenda mitandao hiyo au kutoka mtandao kwa mtandao

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

watafanya miamala. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kwambakila watu wanawasil iana na kwa hilo asil imia 94 yaWatanzania wanawasiliana na hizi asilimia 6 zilizobakiampaka inapofika katikati ya mwaka ujao tunakwendakutangaza mwezi huu vijiji 689 tutakavyovipelekea minara yamawasil iano il i kuhakikisha kwamba Watanzaniawanaendelea kuwasiliana.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuzungumza hayo,naunga mkono hoja asilimia 100, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri, Eng.Atashasta Nditiye. Tunakushukuru sana kwa kupitia hoja zaWaheshimiwa Wabunge kama ulivyofanya na umetumiamuda wako exactly, ahsante sana.

Sasa naomba nimwite mtoa hoja Mheshimiwa Waziriwa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Eng. IsackKamwelwe ili aweze kupitia michango yenu na kutoa majibuya Serikali. Mheshimiwa Waziri, karibu tafadhali.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu ambaye kwa rehema zake nyingi ametujaliafya njema na kutuwezesha kukutana katika Bunge hili Tukufula Bajeti ili kuweza kukamilisha kazi tuliyoianza tarehe 9 Mei2019 ambapo niliwasilisha hoja hii.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kutoa shukranizangu za dhati kwako wewe binafsi, Mheshimiwa Naibu Spika,Wenyeviti wa Bunge na Katibu wa Bunge kwa kusimamia kwaufanisi mkubwa majadiliano yote kwenye Mkutano huu waKumi na Tano wa Bunge hili tukufu.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee napendapia kumpongeza Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni,Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge), WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongoziwake anaoendelea kutuonyesha wasaidizi wake katikamajukumu yetu ya kila siku Bungeni.

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii piakuwashukuru Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati zote zaBunge kwa kufanya kazi kwa karibu na Wizara yangu. Kipekeenimshukuru Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumuya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso,pamoja na Wajumbe wake ambao wameiongoza Wizaravizuri katika utekelezaji wa miradi ambayo imeainishwakwenye Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Ninaahidikwamba Wizara ninayoiongoza itafayafanyia kazi masualayote yaliyoshauriwa na Kamati hizo.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kumshukuruMsemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasil iano kwa maoni, ushauri namapendekezo yake kuhusu bajeti ya Wizara yangu.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikuwatambua Waheshimiwa Wabunge wote waliochangiakatika bajeti yangu. Waheshimiwa Wabunge 18 walichangiawakati wa majadiliano ya hoja ya Waziri Mkuu, WaheshimiwaWabunge 91 wamechangia kwa kuzungumza katika bajetihii inayoendelea na Waheshimiwa Wabunge 66wamechangia kwa maandishi wakati wa majadiliano ya hojaya Wizara yangu. Nawashukuru sana kwa michango yao.

Mheshimiwa Spika, hivi punde Waheshimiwa NaibuMawaziri wa Wizara yangu wameanza kujibu baadhi ya hojaza Waheshimiwa Wabunge kwa kuzingatia maeneo yakisekta (sekta ya ujenzi na sekta ya mawasiliano na uchukuzi).Niwashukuru sana kwa jinsi ambavyo wamejibu baadhi yahoja za Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, naomba nihitimishe kwa kujibuhoja za kisera pamoja na kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hojazilizojitokeza. Naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufukwamba Wizara itajibu hoja zote za Wabunge kwa maandishina kuwapatia Waheshimiwa Wabunge wote majibu ya hojahizo kwa njia ya kitabu kitakachoandaliwa kabla ya hitimishola Mkutano huu wa Bunge la Bajeti.

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo wotetunafahamu, mkataba wa miaka mitano kati ya wananchina Serikali waliyoichagua ni kusimamia utekelezaji wa Ilaniya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015ambayo itahitimishwa mwaka 2020. Baadhi ya ahadi zilizomokwenye Ilani ya Uchaguzi ni pamoja na ujenzi wa reli ya SGR,ukarabati wa reli ya kati, ukarabati wa bandari za Dar esSalaam, Mtwara na Tanga, ufufuaji wa Kampuni ya NdegeTanzania (ATCL), ukamilishwaji wa barabara zinazounganishamikoa, uboreshaji wa mawasiliano nchini na ufufuaji waKampuni ya Meli. Ahadi hizi zinatokana na kilio cha mudamrefu cha Waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili tukufuambao wamekuwa wakiishauri na kuitaka Serikali kuwa namiradi ya vipaumbele na kuitekeleza ili nchi iweze kupigahatua za haraka kuelekea kwenye uchumi wa kati.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hayo, ndiyo maanasehemu kubwa ya bajeti ya maendeleo imeelekezwakwenye Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasil iano.Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na hata leoameongeza zaidi ya shilingi bilioni 90 kwenye Wizara hii. Hii nikutokana na majukumu makubwa ambayo Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imeyabeba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano chiniya usimamizi wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasasa inakaribia kukamilisha ahadi ilizozitoa kupitia Ilani yakeya Uchaguzi. Napenda kulihakikishia Bunge lako tukufukwamba, nikiwa mwakilishi wa Mheshimiwa Rais kwenye eneola Sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kushirikianana Naibu Mawaziri pamoja na Wataalam wa Wizaratutaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi naahadi alizozitoa Mheshimiwa Rais zinazohusu Sekta hii ili kufikiamwisho wa mwaka 2020 ziwe zimekamilika.

Mheshimiwa Spika, aidha, tutaendelea kupambanana kuzitatua kero za wananchi zitakazojitokeza wakatitukiendelea na utekelezaji wa Ilani hii.

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

Mheshimiwa Spika, kuhusu deni la makandarasi, hadikufikia tarehe 30 Juni, 2018 madeni ya makandarasi naWahandisi Washauri yalikuwa shilingi bilioni 833 ambayoyalivuka na kuingia mwaka wa fedha 2018/2019. Katikamwaka wa fedha 2018/2019 makandarasi waliendeleakutekeleza miradi na kuzalisha hati za madai mpya, Serikaliimekuwa ikiendelea kulipa madeni ya makandarasi nawahandisi elekezi ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2019deni lilikuwa shilingi bilioni 962.

Mheshimiwa Spika, naomba kulitaarifu Bunge lakotukufu kwamba Wizara ya Fedha na Mipango hadi mwezihuu Mei itakuwa imelipa shilingi bilioni 609. Namshukuru sanaMheshimiwa Waziri wa Fedha kwa jinsi ambavyo ameitikiautekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kuhakikishakwamba katika mwaka huu wa fedha, tutakapoingia mwakampya wa fedha tena hatutavuka na deni kubwa, na kwajinsi hiyo basi miradi yote ambayo tumeiainisha kuanza katikamwaka ujao wa fedha tutaanza kuitekeleza bila wasiwasiwowote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewamezungumzia sana kuhusu deni la TAZARA, lakini piakwenye Taarifa ya Kambi ya Upinzani walizungumzia deni laTAZARA ambalo linaonekana kufikia shilingi bilioni 434.Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha amejaribukulifafanua deni hili, lakini moja tu nizungumzie kwamba,Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge deni hiliunapolizungumzia ni deni la nchi mbili, ni deni la Tanzaniapamoja na Zambia. Katika deni hili ukiliangalia shilingi bilioni237 ni deni ambalo limetokana na Itifaki ya Serikali ya China,kwa hiyo, itifaki hii inahusisha pia upande wa Zambia, lakininishukuru kwa madeni ambayo yanatuhusu sisi hukuyakiwepo malipo ya wastaafu Mheshimiwa Waziri wa Fedhaameyaelezea vizuri.

Mheshimiwa Spika, katika michango ya Wabunge,wamezungumzia kwa uchungu sana kuhusiana na utaratibuwa majadiliano yanayoendelea kati ya Serikali na Mwekezajiwa Bandari ya Bagamoyo. Nilichojifunza kwa Waheshimiwa

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

Wabunge ni kwamba Serikali ifanye haraka kuhakikishakwamba majadiliano hayo yanakamilika.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa taarifa kwambamajadiliano yangali yanaendelea, lakini kuna baadhi yaWaheshimiwa Wabunge walisema kwamba Serikaliimekataa, sina taarifa ya hilo. Na baada ya kumaliza Bungenilijaribu kuwasiliana na Mamlaka kuulizia kama majadilianoyameshafikia ukomo lakini ni kwamba majadilianoyanaendelea. Ila ni kweli kwamba yamechelewa kutokanana masharti ambayo yanaonekana hayana manufaa kwaupande wa Serikai ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba WaheshimiwaWabunge waridhie kwamba Serikali bado inaendelea namajadiliano na Bunge lako tukufu limekuwa muda mrefulinaishauri Serikali isije ikaingia mikataba ambayo hainamaslahi kwa umma. Kwa hiyo, Serikali inaendelea na paleitakapokuwa imefikia ukomo wa yale majadiliano, nikuahiditu kwamba Serikali itatoa taarifa kwa WaheshimiwaWabunge ili na wao waweze kutoa mawazo yako. Kwa hiyo,niseme tu kwamba bado tunaendelea na majadilianokuhusiana na uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 15 wa kitabu chabajeti ulizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara (express way)ya Dar es Salaam – Chalinze. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano kupitia TANROADS ilimwajiri Mhandisi Mwelekezi(Transaction Adviser) kutoka Korea. Transaction Adviser huyualiajiri makampuni mengine 11 yenye uzoefu na utaalam namiradi ya PPP kutoka duniani kote ili kuishauri Serikali namnabora ya kutekeleza mradi wa Dar es Salaam – Chalinze(express way) kwa utaratibu wa Public Private Partnership,alimaliza kazi hiyo mwezi Desemba, 2016.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya PPPWizara ya Fedha na Mipango ilitoa idhini tuendelee na hatuazingine za utekelezaji tarehe 22 Mei, 2017. Aidha, wakati idhiniya Wizara ya Fedha na Mpango inatolewa tayari Serikaliilishaanza juhudi za kupunguza msongamano katika bandari

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

ya Dar es Salaam, ambazo ni ujenzi wa bandari kavu ya Ruvu,ukarabati wa reli ya meter gauge na ujenzi wa reli ya SGR.Hivyo, busara ya Serikali zilipelekea kuamua kufanya mapitioupya ya taarifa ya upembezi yakinifu ili kupunguza madhara(risk) ambayo yangehamia upande wa Serikali kumlipamwelekezi ambaye angejitokeza kuwekeza katika mradi huukwa kuwa magari ya kubeba mizigo yangeanzia Ruvu badalaya kuanzia bandari ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa usanifu wa mradihuu wa express way ilikuwa ni kwamba barabara inakwendakuanzia bandari ya Dar es Salaam na kwamba ilikuwainategemea tozo sasa za magari ambayo yatakuwayanabeba mzigo kuanzia bandari ya Dar es Salaam. Lakinisasa hapa katika kwa sababu study zote zil ikuwazinaendelea, SGR na baada ya kuonekana kwamba bandariya Dar es Salaam sasa imekuwa na mizigo mingi uwezo wakeutapungua ndiyo tukaamua kujenga bandari ya Kwara.Ukiangalia study hiyo sasa inabidi irudiwe kwa sababu kamamwekezaji alikuwa anategemea tozo zake azipate kutokakwenye magari ni lazima hiyo iweze kurudiwa ili kuona kamabado tunaweza tukachukua mkopo kwa mwekezaji nakwamba mkopo huu utalipwa katika muda unaostahiki.

Mheshimiwa Spika, hilo ndiyo ambalo limefanyakwamba, kwa sababu tunaendelea na ujenzi wa SGR naambao tunategemea itabeba zaidi ya tani milioni 17 kwamwaka, wakati huo huo tumejenga dry port ya Kwara nakwamba SGR ikishafika Morogoro tunatarajia kujenga tenadry port nyingine Morogoro kwa hiyo, ikiwa kwamba zileparameters ambazo zilikuwa zimetumika, wakati wa kusanifuhuo mradi wa express way ziweze kurejewa tena ili tuwezekupata mradi ambao utakuwa na manufaa. Sambamba nahilo, Serikali imefanya maamuzi inajenge Kilometa 19.2barabara nane ambao na tayari mradi umeshaanza, kwahiyo, yote hayo inabidi yarejewe ili kuona kwamba kamamradi huo tutautekeleza utaendelea kuwa na manufaa.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewamezungumzia pia kuhusu ujenzi wa viwanja wa ndege vya

Page 215: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

Kigoma, Sumbawanga, Tabora na Shinyanga. Mikataba yaujenzi wa viwanja vya ndege vya Sumbawanga, Tabora,Shinyanga na Kigoma ilisainiwa tarehe 30 Juni, 2017 kati yaMamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na wakandarasi waujenzi chini ya ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya.Utekelezaji wa miradi hii umechelewa kuanza kwa kuwabaada ya Serikali kuhamisha miradi ya ujenzi wa viwanja vyandege kupeleka Wakala wa Barabara, mambo yafuatayoyalijitokeza na ambayo yamechelewesha utekelezaji wamradi huu.

Mheshimiwa Spika, moja, mfadhili ambaye ni Benkiya Uwekezaji ya Ulaya alitaka kujua taarifa juu ya mtekelezajimpya wa mradi huu yaani TANROADS. Serikali ilielekeza kuwaTANROADS ni Idara ya Serikali inayoaminika Serikali naimetekeleza miradi mbalimbali ya wafadhili, pia imepata Hatisafi za ukaguzi kwa miaka saba mfululizo. TANROADS imekuwaikifanya manunuzi makubwa ya Taasisi nyingine kama vileTACAIDS na ujenzi wa zahanati zinazofadhiliwa na washirikambalimbali wa maendeleo. Baada ya maelezo hayo yaSerikali, mfadhili alielewa na kukubali kwamba kazi ile sasaisimamiwe na Wakala wa Barabara.

Mheshimiwa Spika, kinachoendelea sasa hivi imebidiku-review sasa ile Financing Agreement ili kuondoa TAA nakuweka TANROADS ili sasa no objection iweze kutoka. Sasahivi kwa mujibu wa taarifa za Hazina ni kwamba shughuli hiiya ku-draft hiyo document ya Financial Agreement kwakuweka TANROADS na kuondoa TAA iko kwenye hatua zamwisho kwa sababu taratibu hizi za mikopo zina taasisi nyingiza kupitia ndiyo maana uchelewaji umekuwa mkubwa.Niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge hasa kwenye hayamaeneo ambayo yamekuwa earmarked Shinyanga, Tabora,Kigoma, Sumbawanga kwamba miradi hii WaheshimiwaWabunge itatekelezwa tuko kwenye hatua ya mwisho.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewamezungumzia kwamba katika miaka mitatu Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga fedha nyingi

Page 216: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu ya kimkakati.Wakataka kujua sasa kwanza impact ya utekelezaji huo,nishukuru kwamba jibu hilo amelijibu Mheshimiwa Waziri waFedha alipopewa zile dakika zake 10. Ziko faida nyingi siwezikuzirudia lakini Mheshimiwa Waziri wa Fedhaameshazizungumzia.

Mheshimiwa Spika, nitaomba nizungumzie kidogokuhusu local content. Katika mradi wa SGR makubaliano katiya Serikali na mkandarasi kuhusu ujenzi wa mradi huu, nikwamba asilimia 35 ya malipo yanayolipwa kwa mkandarasiyafanyike kwa fedha za ndani. Lengo ni kuhakikisha kwamba,mkandarasi anatumia siyo chini ya asilimia 35 ya fedha zoteza mradi katika matumizi ya rasilimali za ndani.

Mheshimiwa Spika, malighafi kama kokoto, mchanga,nondo na saruji anavyovitumia mkandarasi vyote ni vya ndaniya nchi. Aidha, matengenezo na uzalishaji wa mataruma yazege unaofanyika hapa nchini katika Kambi za Soga na Kilosaunatumia malighafi za humu nchini. Kiasi cha sarujikinachotarajiwa kutumika katika kipande cha Dar es Salaamhadi Makutopora kwa mujibu wa mkataba ni mifuko yacement au ya saruji 9,200,000 sawa na tani 460,000 za saruji.Kwa upande wa chuma, kiasi tani 115,000 zitatumika kutokaviwanda vya ndani. Chuma cha reli kinachotoka Japan niasilimia 5.2 tu ya thamani ya mradi na hii ndiyo fedha ambayotunaitoa kwenda kupeleka nje kwa hiyo ni asilimia 5.2, kwahiyo asilimia kubwa inabaki hapa ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, mradi utatumia mataruma1,204,000 ambayo ni asilimia 5.6 ya thamani ya mradi wotewa malighafi zake zote zinatoka hapa nchini na zinazalishwahapa nchini maana yake zinatumia nondo za hapa nchini,zinatumia mchanga hapa nchini, cement hapa nchinipamoja na kokoto ni hapa hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kamati kadhaa za Bunge lakotukufu zimetembelea maeneo haya na kujionea uzalishajiunavyofanyika kwa kutumia malighafi zinazozalishwa ndaniya nchi. Licha ya malighafi karibu zote zinazotumika katika

Page 217: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

mradi huu kuwa za ndani ya nchi ukitoa reli yenyewe ambayoinaagizwa kutoka Japan kwenye kiwanda pekee kinachotoareli za viwango vya juu, asilimia 20 ya wataalam wabobezikatika mradi huu ni wazawa, na kwamba asilimia 80 yawataalam wa kati na nguvu kazi ni Watanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa jumla ya wazawa 14,140wamepatiwa ajira katika mradi huu ambapo asilimia 90 niWatanzania. Ukiacha wananchi wengine wanaojihusisha nashughuli zisizo rasmi katika maeneo ya mradi, hii ina maanakwamba malipo ya watumishi hawa kiasi cha shilingi bilioni5.2 kwa mwezi, sawa na shilingi bilioni 62 kwa mwaka ni fedhazinazotumika ndani ya nchi moja kwa moja kutoka kwa watuambao wameajiriwa kwenye mradi. Aidha, wakandarasi zaidiya 500 wadogo wadogo wa ndani wamepewa kazi katikamradi huu, baadhi ya kazi hizo ni pamoja na za ujenzi, ugavina utoaji wa huduma mbalimbali ambapo wote hawawanalipwa na fedha za mradi huo.

Mheshimiwa Spika, mbali ya faida zil izoanzakuonekana katika hatua ya ujenzi, manufaa makubwa yamradi yataanza kupatikana baada ya ujenzi kukamilika.Mradi wa SGR unatarajiwa kuhudumia tani milioni 17 za mizigokwa mwaka, mizigo hii ni pamoja na ile ya nchi za jirani zisizona bandari za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri yaKidemokrasia ya Congo. Kwa upande wa miradi yabarabara, viwanja vya ndege, majengo na vivuko katikamwaka wa fedha 2015/2016 hadi mwaka 2017/2018 jumlaya miradi 4,816 imetekelezwa na makandarasi wazawa namiradi 116 imetekelezwa na makandarasi wa nje. Aidha,jumla ya ajira 362,854 zilizalishwa katika sekta ya ujenzi katikamiaka hiyo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017 jumla ya ajira109,846, mwaka 2017/2018 jumla ya ajira 116,864 na mwaka2018/2019 jumla ya ajira 136,144 zimezalishwa katika maeneombalimbali ya ujenzi ikiwemo miradi ya barabara, miradi yaviwanja vya ndege, miradi ya vivuko na miradi ya ujenzi wamajengo ya Serikali.

Page 218: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

Mheshimiwa Spika, naomba sasa nizungumzie kuhusuKampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), mpaka sasa Serikaliinatoa huduma kwa kutumia ndege mpya sita (6)zilizonunuliwa na Serikali kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika, ndege tatu aina ya BombadierQ4100-8 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, ndegembili (2) aina ya Air Bus A2200-300 zenye uwezo wa kubebaabiria 132 kila moja na ndege moja aina ya Boing 787-8Dream Liner yenye uwezo wa kubeba abiria 262. Aidha, ATCLimekabidhiwa na Mheshimiwa Rais ndege mbili zifuatazo;moja aina ya Foker 50 yenye uwezo wa kubeba abiria 44 naya pili aina Foker 28 yenye uwezo wa kubeba abiria 70.

Mheshimiwa Spika, pia ATCL inatarajia kupokeandege aina ya Bombader–8 mwezi Novemba mwaka huu2019 na Boeing 787 Dream liner ambayo inatarajiwakupokelewa Januari, 2020. Ili kuendelea kuiongezea uwezoATCL, Serikali imetenga fedha katika bajeti yake ya mwakawa fedha 2019/2020 kununua ndege nyingine moja aina yaBombardier Q4100-8 na ndege mbili aina ya Airbus. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ATCL kwa kutumia ndege sitazinazotoa huduma kutoka Dar es Salaam kwenda katika vituo10 ndani ya nchi vikiwemo Bukoba, Dodoma, Iringa,Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Tabora,Zanzibar na vituo vitano nje ya nchi ambavyo ni Bujumbura,Entebbe, ….Harare na Lusaka. Aidha, ATCL inatarajiakufungua kituo cha Johannesburg mwezi Juni, 2019, Mumbaimwezi Julai, 2019 na Kituo cha Guangzhou kabla ya mwishowa mwaka wa 2019. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa kuwana safari zinazounganisha Mji wa Dodoma na sehemunyingine za nchi, ATCL kufuatia maombi ya WaheshimiwaWabunge imeamua kuifanya Dodoma kuwa sub-hub. Aidha,ATCL inaangalia sasa uwezekano wa kuanzisha safari zakutoka Dodoma kwenda KIA, kutoka Dodoma kwendaMbeya, kutoka Dodoma kwenda Mwanza na kutokaDodoma kwenda Zanzibar. Sambamba na vituo hivyo, ATCL

Page 219: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

ipo kwenye maandalizi ya mwisho ya safari za kwenda Mkoawa Katavi Mji wa Mpanda na kuangalia uwezekano wakuanzisha safari kati ya Dar es Salaam na Tanga kupitiaPemba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamekuwepo na dhana kwambaununuzi wa ndege na gharama za awali na uwekezaji katikamifumo, mitambo na miundombinu zimehamishiwa kwenyeFungu 20, yaani Ikulu. Suala hili siyo la kweli kwa sababugharama hizo zimetengewa fedha katika Fungu 62 ambaloni la Sekta ya Uchukuzi. Aidha, gharama za uendeshaji waATCL zinatokana na mapato ya ndani ya kampuni kamainavyooneshwa katika hesabu za ATCL zinazokaguliwa naMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, ununuzi wote wa ndegeunafanywa na Wizara yangu ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano na ni Fungu 62 ambalo linapitishwa na Bungelako Tukufu; na hata katika bajeti hii tunaomba mpitisheshilingi bilioni 500 ili tuweze kununua ndege nyingine tatuambapo moja itakuwa ni Bombardier na mbili ni Airbus.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa wataalammarubani, ni kweli kwamba uwiano wa marubani wenyeleseni katika nchi yetu kwa sasa ni asilimia 49:51 ambapowazawa ni asilimia 49 na wageni ni asilimia 51. Hata hivyo,Serikali ina mikakati ya kuongeza marubani wazawa kwakuwasomesha hapa nchini katika Chuo cha Taifa chaUsafirishaji kupitia Mradi wa East African Skil ls forTransformation and Regional Integration Program. Mradi huuutatekelezwa kwa mkopo wa dola za Marekani milioni 21.5kutoka Benki ya Dunia na utaanza kutekelezwa rasmi mweziJuni, 2019. Nitoe tu taarifa kwamba fedha hizi, financialagreement imeshasainiwa, tayari tunazo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kupitia mradi huu, chuo hichokitakuwa na uwezo wa kusomesha marubani 10 kwa mwaka.Aidha, Wizara yangu inafanya mawasiliano na Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia ili Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi

Page 220: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

wa Elimu ya Juu iweze kuwakopesha wanafunzi wa kozi yaUrubani. Kwa sasa ili rubani aweze kuingia katika soko la ajiraatatakiwa kusoma na kupata leseni ya biashara kwagharama ya shilingi milioni 132.6.

Mheshimiwa Spika, Serikali pia ina Mfuko waKusomesha Marubani ambao unasimamiwa na Mamlaka yaUsafiri wa Anga TCAA ambao una uwezo wa kusomeshatakriban marubani watano hadi 10 kwa mwaka kulinganana makusanyo katika mwaka husika. Mfuko huu mpaka sasaumesomesha wanafunzi watano ambao wameshahitimu nakuajiriwa kwenye sekta. Aidha, wanafunzi 10 wataanzamasomo mwezi Oktoba, 2019. Serikali itaendelea kuhakikishainaongeza idadi ya marubani na wahandisi wazawa katikakipindi kijacho.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewamezungumzia Bandari ya Mtwara na hasa Kamati yanguya Miundombinu. Serikali ilibuni mradi wa kuboresha Bandariya Mtwara kwa lengo la kuboresha huduma zake za sasa nawakati ujao na baadaye katika ukanda wa Mtwara. Katikakutekeleza hili, kumekuwepo na hoja ya kujengwa nakuchimbwa kwa urefu wa kina cha mita 13 badala ya 15 naurefu kati ya maji yanapojaa na sakafu ya gati ya mita tanobadala ya mita 5.5.

Mheshimiwa Spika, vipimo vilivyozingatiwa wakati wakujenga na kuchimba Bandari ya Mtwara vilitokana naushauri wa awali uliotolewa na Mtaalam Mshauri MSURSkutoka Uingereza ambao ni urefu wa kina wa mita 13 na urefukati ya maji yanapojaa na sakafu ya gati ya mita tano. Aidha,uchambuzi wa kina wa kitaalam unaonesha kuwa vipimohivyo vinavyotumika ni sahihi kwa meli na shehena tarajiwakatika bandari hiyo.

Mheshimiwa Spika, Bandari ya Mtwara kutoka kwenyekina ambacho ni low tide inajaa mpaka mita nne. Kwa hiyo,ukichimba draft ya mita 13 wakati maji yamejaa, yatafikampaka mita 17. Kwa hiyo, meli ya aina yoyote ni lazima ita-dock kwenye Bandari ya Mtwara. (Makofi)

Page 221: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana MheshimiwaNaibu Waziri Nditiye amezungumzia suala la usajili wa laini zasimu, lakini naomba nitoe taarifa kwamba takwimuzinaonesha kuwa mwaka 2018 idadi ya wananchi nchiniilikadiriwa kuwa milioni 54.2 ambapo watu 52.6 wanaishiTanzania Bara na wananchi milioni 1.6 wanaishi TanzaniaVisiwani.

Aidha, asilimia 50 ya Watanzania wana umri chini yamiaka 18. Kwa kuwa zoezi la usajili wa laini za simu linamalizikamwezi Desemba, 2019 Serikali itahakikisha wananchi wenyekustahili kusajiliwa na NIDA wanasajiliwa ili kuwezeshawananchi kuendelea kupata huduma za mawasiliano zilizosalama. Kuna Waheshimiwa Wabunge walionesha kwambapengine kuna baadhi ya vitambulisho ambavyo havitumiki,lakini nashukuru kwamba Mheshimiwa Eng. Nditiyeamelizungumzia vizuri.

Mheshimiwa Spika, tunatambua uwepo wa uhitaji wavitambulisho vingine vyenye biometria vinavyotumika kwasasa kusajili laini za simu ikiwa ni pamoja na pasi za kusafiria,leseni za udereva, kitambulisho cha Mpiga Kura pamoja naZan ID. Hivi vyote vinatumika katika kusajili laini za simu. Sasahivi kuna kamati maalum ambayo inafanyia kazi. Kitukinachotakiwa ni kwamba laini zote kwa kutumia vitambulishovyote vinavyosajiliwa lazima visomane na lazima visomanepamoja na kitambulisho cha Taifa na hili litatusaidia kukwepamadhara tunayoyapata ya wananchi kuibiwa.

Mheshimiwa Spika, lengo letu tunataka kila laini yasimu, kila mtumiaji awe anafahamika. Kwa hiyo, kwa sasa nivitambulisho vyote vinatumika na wataalam wapowanaendelea na kuhakikisha kwamba wanafanya utafiti ilikwamba vitambulisho vyote hivi viweze kusomana pamojana kitambulisho cha Taifa.

Mheshimiwa Spika, hatua zilizochukuliwa na Serikalikuiongezea mtaji TTCL. Naomba pia kutoa kutoa ufafanuzikuhusu jitihada zilizochukuliwa na Serikali katika kutoa mtajikwa Shirika la Mawasiliano Tanzania. Serikali inaendelea

Page 222: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

kutekeleza mikakati yake madhubuti ya kuboresha mashirikayaliyokuwa yamebinafsishwa lakini yakashindwa kujiendeshakwa ufanisi. Kwa msingi huo, imetunga Sheria Na. 12 yamwaka 2017 ya kuanzisha Shirika la TTCL likiwa linamilikiwana Serikali kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali imeendelea najuhudi za kuhakikisha kwamba TTCL sasa inapewa mtaji. TTCLilipewa kibali cha kukopa jumla ya shilingi bilioni 96 nailishakopa shilingi bilioni 66. Sasa hivi iko kwenye process yakumalizia kukopa shilingi bilioni 30 ili iweze kuwekeza na TTCLiwe ni Taasisi ambayo inaweza ikajitegemea. Nashukurukwamba kwa muda mchache mwaka 2019 iliweza kutoagawio na mwaka huu tayari imeshajipanga kutoa gawio.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania imetengeneza corridor tatu; ya kwanza ni yakutoka Dar es Salaam kupitia Tanzam highway kwendampaka Zambia, corridor ya pili ni ile ambayo inakwendaCentral Corridor na ndiyo maana tunajenga SGR, lakinitunayo corridor ya tatu ambayo inatoka Mtwara kwendampaka Mbambabay na ninashukuru kwamba Serikali tayariimeshakamilisha barabara ya lami kutoka Mtwara kwendampaka Songea na kwenda mpaka Mbinga na sasa hivitunajenga kilometa 66 zilizobaki.

Mheshimiwa Spika, corridor hii ikishakamilika na kwasababu sasa hivi tunanunua flow meter ili ziweze kufungwaBandari ya Mtwara na flow meter zifungwe Bandari ya Dares Salaam pamoja na Bandari ya Tanga, tunataka tuwezeshecorridor zote hizi ili ziweze kuhudumia nchi jirani na kujiongezeamapato.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Bandari ya Tangatayari muda wowote mkataba utasainiwa. NilitembeleaTanga, Tanga ilikuwa imeshakwenda chini sana, lakinitunahakikisha sasa kwamba Tanga inaamka. Kwa sababuyale magati mawili yaliyojengwa yamejengwa kwenye draftambayo ni ndogo, maji ya kina cha mita tatu mpaka nne.Mikataba tutakayosaini tunataka tufanye dredging ili

Page 223: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

kuongeza kina kwa sababu kwa Tanga sasa hivi meli ilikuwaikifika inakwenda kupaki mita 1,400 halafu mizigo sasainapakiwa na matishari kuleta kwenye magati huku ambayoyanaweza yakatembea kwenye kina kidogo. Matokeo yakeilikuwa ina-discourage wenye meli kuja kuleta meli zao Tanga.

Mheshimiwa Spika, hilo tunaliondoa na hiyo ndiyoambayo Waheshimiwa Wabunge mlikuwa mnaizungumzia.Tunapambana na Bandari majirani. Tunataka tufanyedredging na kwa mujibu wa taarifa ambayo ninayo, TPAmmeipongeza, wanatarajia mpaka itakapofika mwezi waTatu mwakani dredging itakuwa imekamilika. Ikishafika mweziwa tisa wataongeza tena magati mawili yenye ukubwa wamita 300, 300. Hii itawezesha sasa Bandari ya Tanga iwezeku-compete na bandari nyingine za jirani.

Mheshimiwa Spika, tukiwa na Bandari ya Tanga nawakati huo huo tunaendelea kukarabati Bandari ya Dar esSalaam ambayo tunafanya dredging kwenda mita 15 na gatiNa.1 limeshakamilika, utaona kwa wale wanaopita Dar esSalaam sasa hivi hata kule meli zinaanza kupungua, lakinikwa ujumla, meli zinaongezeka kwa Bandari ya Dar esSalaam.

Mheshimiwa Spika, malengo yetu ni kwambatunataka tuboreshe bandari zetu na tunajenga gati linginela shilingi bilioni 137 kwa upande wa Mtwara. Tunatakatuhakikishe kwamba meli nyingi sasa zinakuja kupaki katikaBandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Tanga pamoja naBandari ya Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza kutekelezakuhakikisha kwamba inafufua usafiri kwenye maziwa. Upandewa Ziwa Nyasa tayari kuna meli tatu na zinafanya kazi.Upande wa Ziwa Victoria tumeshasaini mkataba wa melimoja kubwa itakayobeba abiria 1,200 na tani 400 pamojana ujenzi wa chelezo, tunakarabati na zile meli za zamani;Mv Victoria na Mv Butiama. Kwa upande wa Kigomatunatarajia kusaini tena meli moja mpya ambayo itakuwa

Page 224: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

inabeba abiria pamoja na mizigo na kukarabati meli ya MVLiemba. Taratibu za manunuzi zimekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunachotarajia sasa hivi ni mudawowote tutasaini mkataba kabla ya mwisho wa mwezi Juni,2019. Malengo yetu ni kuhakikisha kwamba maziwa yote sasayanatumika kiuchumi. Niseme tu kwamba Mkoa wa Katavitayari tumeshapata mfanyabiashara mmoja ambayeananunua tani 1,200 kila mwezi tutakuwa tunampelekeaCongo.

Mheshimiwa Spika, pia kuna madini ambayoyamepatikana upande wa Kongo ambayo yatakuwayanapitisha tani 2,000,000 kwa mwaka. Ndiyo maana tayaritunaendelea na mazungumzo ya pamoja na Benki yaMaendeleo ya Afrika ili tuwe na matishari ya kutosha piakatika Bandari ya Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu muda naonaunanitupa mkono, nimalizie kwa kutoa taarifa pia kwaWaheshimiwa Wabunge kwamba meter gauge kutoka Dares Salaam kwenda Isaka inaendelea na ukarabati,inafufuliwa. Meli yetu hii ya meter gauge kwenye usanifu wakeilikuwa imesanifiwa kubeba tani milioni tano kwa mwaka,lakini ilikuwa imeshuka mpaka inabeba tani 300,000. Baadaya ukarabati huo, tutarudisha sasa kwenda kwenye hizo tanizinazotakiwa.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa ushauriambao umetolewa na Waheshimiwa Wabunge kwambatuangalie namna ya kuikodisha TRC ili iweze kuhudumiapamoja na reli ya TAZARA. Nimshukuru sana na MheshimiwaTurky, leo kazungumza kitu ambacho nimewahi kukisikia maraya mwisho wakati alipotembelea yule Waziri wa Ethiopiaaliyejiuzulu. Nao nchi yao waliipeleka vizuri kutokana na hizibond. Kwa hiyo, ushauri wako Mheshimiwa Turky nimeupokea.

Mheshimiwa Spika, baada ya haya machache,naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako lipitishe kifungu

Page 225: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

kwa kifungu na lipitishe bajeti ya Wizara ya Ujenzi Uchukuzina Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, naomba kuta hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, naafiki.

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkono.Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzina Mawasil iano, Mheshimiwa Eng. Kamwelwe kwakuhitimisha hoja yako vizuri sana na imeungwa mkono.

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 68 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MWENYEKITI: Hili ndilo Fungu lile la mshahara wa Waziri,kuna majina kadhaa hapa, tuanze na Mheshimiwa SaadaMkuya...

NDG. ATHUMANI HUSSEIN - KATIBU MEZANI:Mheshimiwa Mwenyekiti, bado sijasoma.

MWENYEKITI: Ngoja kwanza, Mheshimiwa, mpakaKatibu asome kwanza.

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management………Sh.1,450,664,265/=

MWENYEKITI: Mheshimiwa Saada Mkuya, swali laufafanuzi la kisera!

MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Katika mchango wangu nilizungumzia zoezilinaloendelea la usajili wa laini za simu kwa kutumiavitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho yaTanzania (NIDA), lakini sasa kwa upande wa Zanzibar, kuna

Page 226: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

vitambulisho hivyo, maarufu ni kama ZAN ID, na kwambaTCRA wanakataa kusajili kwa kutumia ile ZAN ID, lazimawapate vitambulisho vya NIDA na kwetu kule Zanzibar,takriban Wazanzibari laki saba tayari wanavyo vitambulishovya ZAN ID na tunatumia kwa mahitaji mbalimbali, almostmahitaji yote kwa upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika majibu yaMheshimiwa Waziri sikupata ufafanuzi vizuri na naombaatakapojibu hili, kama hatujaridhika nitawaomba wenzagutusimame ili tuweze kulijadili kwa kina, nitakamata shilingi yaMheshimiwa Waziri ili tulijadili kwa kina, ni kwa sababu ganihasa za msingi vitambulisho vinavyotolewa na ZAN IDhavitumiki katika usajili wa laini za simu!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Kamwelwe, ufafanuzitafadhali!

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mtandao ni suala ambalokiasi fulani limekuwa ni hatari kwa sababu wizi ni mkubwa,kweli huko tulikotoka il if ikia mahali fulani kwambavitambulisho visitumike vyote. Tumeshaiagiza TCRA kwambasasa hivi wataalam wakae, wajaribu kuainisha vitambulishovya ZAN ID na nimevisoma kwenye taarifa yangu, kwambanavyo pia lazima vitumike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, TCRA wanafanyiakazi, Tanzania Zanzibar, Tanzania Bara, wote ni Watanzania,lazima wawasiliane, lazima watumiane fedha na kwambavile ni vitambulisho vya makazi kwa upande wa Zanzibar nahuku tuna hivi vitambulisho vya taifa ambavyovita-covermaeneo yote. Kama mnayo taarifa hata juzi Mheshimiwa Raisalisema, jamani msisimamishe, endeleeni kusajili. Kwa hiyosasa ni kazi ya watalamu kuhakikisha kwamba ZAN ID na hivyovilivyoko huko vya wapiga kura, leseni, passport, kwambavyote viwe vinaweza vikasomwa na kitambulisho cha Taifa.Kwa hiyo, Mheshimiwa Saada Mkuya naomba uache shilingiyangu tu kwamba, Serikali inalifanyia kazi na kwambavitambulisho vyote ni lazima vitumike.

Page 227: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

MWENYEKITI: Mheshimiwa Saada bado unasimamajambo lako limekubalika.

MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ndiyo, leo mimi nimekwenda kusajili pale na nilijaribu tu,ninacho kitambulisho cha NIDA, nilijaribu tu, nikawaambiamimi sina kitambulisho cha NIDA nataka kusajili kwa kutumiaZAN ID, wamekataa moja kwa moja. Kwa hiyo, naombakuondoa shilingi ya Mheshimiwa Waziri ili sasa tupate firmcommitment, lini TCRA kwa kuainisha Makampuni ya Simuwataanza kutumia ZAN ID katika usajili wa laini za simu.Naomba wenzangu mniunge mkono, kwa sababu hii hatuani hatua muhimu na ZAN ID ni kitambulisho ambachokinajulikana na kimepata certificate za quality pamoja nasecurity of information. Naomba wenzangu waniunge mkonoili tulijadili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.

MWENYEKITI: Hasa ninyi mliosimama mmesimamakuunga mkono nini. (Kicheko)

MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimetoa hoja.

MWENYEKITI: Hpana wewe mtoa hoja sikushangai,nawashangaa wanaounga mkono. Kwa sababu Waziriamesema, sasa hivi TCRA wameagizwa na Waziri, wakaewaangalie vitambulisho zaidi ya kitambulisho cha Taifa, ZANID itaingia, passport itaingia, leseni ya dereva itaingia.

Kwa hiyo, leo ukienda na leseni ya dereva kwa leohutaandikishwa lakini hivyo vinaingia katika utaratibu. Jambolikiagizwa si linachukua muda kunanii, ameshakubali kwambasiyo tu ZAN ID, kama alivyotoa mtoa hoja lakini, labda hilo laWaziri la lini, lakini vimekubalika zaidi ya hicho. Tukijadili sanaZAN ID sijui kama tunafanya sawa.

Mheshimiwa Waziri labda la lini hilo, hiyo processmnadhani lini labda vitaanza kusoma vyote hivyo ulivyovitaja.

Page 228: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru pamoja naWaheshimiwa Wabunge, kwa sababu hili ni suala la kitamam,tumeshawaagiza tayari waweze kulifanyia kazi, labda nisemesasa sijui nifanyeje maana yake mpaka niwasiliane nawataalam. Haya ni masuala ya kitaaalam, lakini niwekecommitment ya mwezi mmoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea, MheshimiwaGood luck Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Naomba maelezo ya Serikali, katikahitimisho lake Mheshimiwa Waziri hajaongelea miradi mingimikubwa ya ujenzi ambayo imekwama kwa sababu ya huumkanganyiko wa VAT. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri asiponipamajibu ya kuridhisha nitashika shilingi.

MWENYEKITI: Labda chukua kama dakika mbili elezakidogo, Waheshimiwa Wabunge wengine hawaelewimkanganyiko huu wa VAT unahusu nini.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Mwaka jana katika Finance Billtuliondoa VAT katika miradi mikubwa ya ujenzi ili kurahisishamiradi hiyo ambayo inafadhiliwa na nchi marafiki, nchiwashirika, wadau wa maendeleo, lakini sasa, miradi hiyoimekuwa na ucheleweshwaji mkubwa kwa wakandarasihawa kusamehewa VAT. Kwa hiyo, imesababisha hii miradiisifanyike, mingine isimame kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, mradi wa Nyakanaziwa Mizani, wa Manyoni, wa Kidatu Ifakara, barabara yoteimesimama. Kwa hiyo, ukimuuliza Waziri wa Fedha,anamtupia Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Ujenzi anasemakikwazo Waziri wa Fedha, kwa hiyo, wamekuwa wakirushianamipira na siku zinakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Page 229: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ni kwelimiradi hii imesimama kwa sababu ya hiyo?

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza nisemekwamba pengine hapo nyuma kidogo tulikuwa tunachangamoto ambazo zilikwamisha baadhi ya miradi ambayoilitakiwa ipate msamaha wa VAT, lakini nilihakikishie Bungelako kwamba hivi sasa tumerahisisha sana naninavyozungumza hivi sasa kwa mara mbili mfululizo, tumetoaGN ambayo kila mojawapo imesamehe zaidi ya miradi 380,kila moja ya hiyo Global GN.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nilieleze tu, zamaniilikuwa kwamba, ilitakiwa kila mradi utolewe msamaha pekeyake na kwa miradi ya nchi nzima kuwa scrutinized ilikuwa nichangamoto kubwa kweli, ile ofisi inayochambua ile miradiilikuwa imeelemewa. Kwa hiyo, tulichofanya ni kwambatumemtaka kila Waziri mwenye sekta, anapowasilisha ombila msamaha wa kodi kwa miradi yake, athibitishe kwambamaombi hayo yamezingatia matakwa ya sheria ya VAT. Kwasababu kabla ya hapo, tulikuta kwamba kuna vitu vingiambavyo havistahili kabisa msamaha. Sasa huo mzigoanabeba Waziri mwenye dhamana ya sekta, sisi Wizara yaFedha tutakwenda kukagua baadaye kama kweli matakwaya sheria yamekidhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia labda niseme tukwamba, Sheria ya VAT, kifungu cha 6 na cha 7, pamoja naaya ya 9 ya ile sehemu ya pili ya Jedwali la Sheria ya VAT,ndiyo inayotoa msamaha ili kupunguza gharama zautekelezaji wa miradi ya maendeleo na miradiinayogharamiwa na fedha za Serikali inahusu miradi yamiundombinu ya maji, usafirishaji, gesi, nishati, majengo yautoaji wa huduma za elimu na afya na kadhalika na hapondiyo tunatakiwa tutoe ile hati ya msamaha wa ile miradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 7(b) cha Sheriaya VAT kinatoa msamaha kwa kodi katika mikataba ambayoimesainiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Page 230: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

Sasa hiyo, ndiyo ilikuwa inataka kwamba, kila anayetekelezamradi alipe VAT kwa wale wenye mikataba yenye misamahaya kodi, halafu aje kurejesha baada ya kuzalisha aukutekeleza mradi husika na hiki kama WaheshimiwaWabunge mnatukumbuka, ndiyo kipengele tulichofuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko miradi ambayoimekuwa na changamoto na labda niitolee mfano, kunamradi wa kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, na hapa nikuwa mradi huu haukukidhi kigezo cha kupata msamaha waVAT na ni kwa mujibu wa kifungu cha 6(2), ambacho kwenyemkataba hakukuwa na kipengele cha msamaha wa kodi,kwa mujibu wa Sheria ya VAT. Kwa hiyo, tulichofanyamtekelezaji wa huu mradi amefanya marekebisho kwenyemkataba na hicho ndiyo kilichelewesha, alikwenda kufanyamarekebisho kwenye mkataba ili kuingiza kipengeleambacho kinatoa msamaha wa VAT. Kwa hiyo, ni kwa miradiya namna hiyo ambayo kumekuwa na ucheleweshaji, lakinihili sasa tumeshalimaliza na kama tulivyoeleza kwenyemaelezo ya Mheshimiwa Waziri, Serikali iliruhusu kutolewavifaa vya huo mradi vilivyokuwa vimekwama bandarini ilimradi uendelee kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kiasi kikubwasana suala la uchelewaji wa kutekeleza miradi kwa sababuya VAT limeondoka. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mlinga, swali lakoumeridhika.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante, Waziri anavyoviongea sasa hivi nitheory, lakini siyo practically, ukienda hata kwenye kitabuhiki cha Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, ameandika kuwaimekwama kutokana ucheleweshaji wa hiyo misamaha!(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya majibu anayotoa kilasiku ndiyo anayatoa hayo hayo. Ukimuuliza Waziri wa Ujenzi,atakwambia huyu ndiye anayechelewesha, yeye

Page 231: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

anakwambia tatizo liko kule, kwa hiyo, miradi imesimama,lakini ukiwauliza hivyohivyo wanatoa hizo sababu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi naombanitoe hoja ili Bunge lijadili, Serikali itoe commitments zakehapa, lini, kwa sababu ni mwaka mmoja tangu tupitishe hiyosheria. Naomba kutoa hoja.

MWENYEKITI: Nilikuwa naangalia kama mmefika kumi,lakini naona kama mmeshafika kumi. Haya, Mheshimiwa,simameni tena, Mheshimiwa Mary Nagu, Mheshimiwa, Katibuniandikie..

MBUNGE FULANI: Mtuka.

MWENYEKITI: Ahsante, mnaweza kukaa, nachukua tubaadhi, tuanze na Mheshimiwa Mary Nagu! Dakika mbilimbili.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa kweli Serikali imefanya jambo zuri kutoa VAT kwenyemiradi ambayo inaongeza maendeleo yetu, lakini ilekutolewa tu haitoshi, ni pale ambapo inaponufaisha kampunizile kubwa ambazo zinafanya miradi hiyo mikubwa, ndiyotutakuwa na faraja. Sasa kama watu wanakaa wanashindwakutekeleza kwa sababu ile VAT haitolewi kwa mudaunaotakiwa. Serikali naomba ione ni kitu gani ambachokinafanya basi practically, hil i jambo ambalo Waziriameonesha kwamba ameisamehe, ametoa, lakini haisaidii,kama vile VAT bado ipo. Kwa hiyo, tunaomba tupatemaelezo hayo, nina hakika tutaharakisha utekelezaji wamiradi ya maendeleo.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa YussufuHussein!

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Shida iliyopo katika Serikali yetu na tunapatamakubwa ni kwamba tunapokuwa hapa, WaheshimiwaMawaziri wanajibu maswali vizuri ili bajeti yao ipite au sualalile lionekane limepita, lakini ukiondoka hapa sasa, ukirudi

Page 232: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

kwenye utekelezaji, hakuna utekelezaji, miradi inakwama,shughuli zinakwama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tukikaa hapatukazungumza suala la pale Bandarini tu Dar es Salaam mizigoinayotoka Zanzibar, unapata majibu mazuri, ukirudi pale tatizolilelile, wapiga kura wetu wanatusakama, kwa hiyo, tunatakaSerikali tunaposema, ielewe kwamba tuna nia safi ya kwendambele kwenye nchi yetu na siyo hivyo wanavyotufanyiakwamba wanajibu ili funika kombe mwana haramu apite.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwakasaka!

MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Naomba tu Mheshimiwa Mlinga aachieshil ingi, kwa sababu kitu kinachoonekana hapa nimiscommunication tu kati ya Wizara ya Fedha na Ujenzi nakwa sababu tayari kwenye kitabu hiki cha Mheshimiwa Waziriwa Ujenzi kuna hilo suala la ku-mention hilo suala laucheleweshaji wa msamaha wa VAT, basi Serikali ingeji-commit tu kwamba hizi Wizara mbili ziweze kushirikiana vizuriili kuondoa huu ucheleweshaji. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Maghembe, profesa!

MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi. Kwenye Muswadawa Fedha mwaka jana, jambo hili lilitokea na tulidhanitumelitatua na tuliondoa VAT kwenye miradi ya ujenzi namiradi ya maji, lakini ukaenda Arusha sasa, tumepewamsaada na ADB kujenga mradi wa maji, lakini mkandarasiamechimba visima, visima vinatoa maji, tangu mwaka jana,mabomba yako bandarini yamenyimwa exemption ya VAT.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unajiuliza, fedhatumepewa na Waziri amesema vizuri kwamba kama mradiunatokana na mradi wenye makubaliano kati ya Donor na

Page 233: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

Serikali ya Tanzania, unasamehewa VAT, lakini tangu mwakajana, mabomba yako bandarini, yamenyimwa VAT,wananchi wanahitaji maji, na watu wanalaumiana tu,hakuna sababu yoyote ya jambo hili kutusumbua hapa!Hakuna complication yoyote kwa sababu miradi hii mikubwaama inatekelezwa na fedha za ndani za Serikali, au na donorambaye ana mkataba na Serikali, kigugumizi kinatoka wapi?Waziri atupe maelezo mazuri zaidi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Tizeba!

MHE. DKT. CHARLES J. TIZEBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri uwe na subirawamalize kwanza.

MHE. DKT. CHARLES J. TIZEBA: Alichokisema Waziri waFedha, theoretically ni sahihi kabisa, kwamba hapapaswikuwa na sababu, kwa sababu Bunge lil ikwisharidhialikamwondolea ile burden ambayo otherwise alikuwaanaibeba peke yake, lakini kinachositkisha ni pale ambapo,hata lililo obvious kabisa, kama anavyosema ProfesaMaghembe, jambo liko wazi! Grant, msaada, fedha yamsaada havipaswi kulipiwa kodi. Hata hivyo, utakuta mradiumesimama mwaka mzima, miezi nane, miezi mitano, miezimingapi exemption haipatikani, kuna nini? Kama liko tatizo,Wizara inaliona lipo tatizo iliweke wazi ili tulijadili tuliondoe,lakini kutujibu yaliyo kwenye sheria na maandishi, halafuutekelezaji haufanani, sidhani kama ni sahihi, tunatengenezamambo halafu tunapiga risasi miguuni mwetu sisi wenyewe.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsate sana Mheshimiwa Dkt. Tizeba.Mheshimiwa Chenge.

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Nimemuelewa Mheshimiwa Waziri waFedha, ana nia njema katika kulipeleka taifa mbele lakiniMheshimiwa Mlinga hoja yake ni ya msingi. Hili nataka

Page 234: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

niliseme, tulipofanya yale marekebisho ya sheria kumrejesheaWaziri wa Fedha mamlaka ya kusamehe kwa miradi ambayoilikuwa imeshakwama ili tuweze kuikwamua, wanasheriawatasema sheria unapoitunga inaanza kutumika kwendambele siyo kurudi nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tatizo tumelijenga sisiwenyewe. Lengo ilikuwa ni kukwamua miradi yote hii navigezo ambavyo vimo kwenye GN ile pamoja na Warakaambao umetolewa na Wizara ya Fedha unakaa vizuri tu,hakuna ubabaishaji kwamba utaleta vitu ambavyohaviruhusiwi kusamahewa VAT. Changamoto iliyopo ni ndogosana, ni hiyo sheria kuangalia kwenda mbele, haibebi miradiambayo ilianza kutekelezwa siku za nyuma kabla yamarekebisho hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachotakiwa kufanya nikesho kutwa kwenye Finance Bill, Serikali ifanye commitmenttu kwamba watakuja na mapendekezo ya kufanyamarekebisho ili tuibebe miradi yote ile ambayo imekwama.Tukifanya hivyo ni rahisi sana. Juzi kwenye Kamati ya Bajetiniliwaambia kama wanashindwa kuiandika hiyo mimi nawezanikajitolea kuandika amendment hiyo. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya, Mheshimiwa Waziri wa Majinilikuona ulisimama.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kumpa taarifa tu MheshimiwaMaghembe kwamba Wizara ya Maji tulikuwa na VATexemption, tulifanya maombi kwa ajili ya mradi wa Same,Mwanga na miradi ya ADB ya Arusha ambayo yote VATexemption tumeshazipata kwa upande wetu.

MWENYEKITI: Mmezipata lini Mheshimwia Waziri?

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, tumepata zaidi ya mwezi mmoja kwa sababumimi mwenyewe nilikuwa nafuatilia kila siku na tayaritumeshazipata.

Page 235: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

MWENYEKITI: Kwa hiyo, kumbe Mheshimiwa Waziri naMheshimiwa Maghembe mnaongea lugha moja. Kama nimwezi mmoja tu mmepata juzi maana yake mnaongeapamoja, kwamba imechelewa sana hadi kutoka. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri wa Fedha halafu anafuata mtoahoja nafikiri, kama una lolote kabla sijamrudishia Mlinga.

MHE. KABWE Z.R. ZITTO: Senator Chenge amemaliza.

MWENYEKITI: Hapana, lazima Serikali ipate nafasilabda kama hawataki. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi hii. Kamaalivyoanza kusema Mheshimiwa Waziri wa Fedha kulikuwana kutokuelewana nini kilitakiwa kifanyike kabla.

Hata hivyo, kwa sasa hivi imeshawekwa vizuri kwambakila Waziri wa sekta husika yeye anatakiwa ajiridhishekulingana na Sheria ya VAT kile anachokiomba kwa sababuyeye ndiyo kinamhusu. Tayari Mawaziri wote wa sektawameshaandika barua za commitment ya kwambawatakuwa wanajiridhisha wao ili inapofika Wizara ya Fedhatimu ile ya Wizara ya Fedha isianze kupitia tena ombi mojabaada ya lingine baada ya Waziri mwenye sekta kujiridhishakulingana na Sheria ya VAT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hiyocommitment, ndiyo hata hiyo aliyoisema Mheshimiwa Waziriwa Maji kwamba tayari miradi yake yote imeshapata VATexemption. Hakuna mradi hata mmoja ambao huna shidaya VAT exemption.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya mwezi huo mmojatayari tumeshatoa Global GN mara mbili. Katika kila GNtumetoa miradi 380, mara mbili ni zaidi ya 700 ambapotumeshatoa miradi hii na tutaendelea kufanya hivyo kwasababu sasa kumekuwa na uelewa wa pamoja ndani yaSerikali ya nini tunatakiwa kufanya.

Page 236: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe sanaMheshimiwa Mlinga rafiki yangu aachie shil ingi yaMheshimiwa Waziri wa Ujenzi ili tuende sasa kutekeleza miradiyote ambayo ina maombi haya ya kuombewa msamahawa VAT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Kwandikwa.

NAIBU WAZIRI, UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza, nimwombe Mheshimiwa Mlinga aweze kuachiashilingi ya Mheshimiwa Waziri i l i tukafanye kazi. Pianilifahamishe Bunge lako kwamba tatizo lilikuwepo pale awalilakini kuwa na changamoto ni jambo moja bali kushughulikiakwa usahihi ni jambo nyingine. Kazi imefanyika kuhusishaMaafisa wa TRA na Maafisa wa kwetu upande waTANROADS, tumekuwa na namba ya vikao vya kutoshaangalau kuweza kupata ufafanuzi ili tuweze kwendasambamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu baada ya kuwatumefika pazuri jumla ya miradi ambayo imesamehewa ni1,019 kwa muda huu mfupi. Wakati tunaandaa taarifa hiikulikuwa na changamoto lakini sasa tunaenda vizuri naMaafisa wa TRA walioko wenye ngazi ya Mkoa wakatimwanzo walikuwa hawahusishwi kwenye zoezi la exemptionnao sasa wanahusishwa ili kurahisisha zoezi la hii misamaha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombe tuMheshimiwa Mlinga aachie shil ingi sisi tunaendeleakulisimamia jambo hili ili miradi yetu isiendelee kukwama.Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Mlingatufungie hoja yako.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa michango ya Wabunge na

Page 237: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

commitment ya Serikali. Hata hivyo, naiomba Wizara yaFedha ipunguze urasimu isitake kula visivyoliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, narudisha shilingi.(Makofi)

MWENYEKITI: Sasa visivyoliwa sijui vitu gani tena?Mlinga bwana!

Haya tuendelee na Mheshimiwa Dkt. ShukuruKawambwa.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa hii ya kuchangiahoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangunilionesha mfadhaiko wa Watanzania wakiwemo wananchiwa Jimbo la Bagamoyo kuhusiana na kusitishwa mradimaalum wa uwekezaji Bagamoyo. Mradi huu kama vile miradimingine ya uwekezaji una mchango mkubwa sana katikakutufikisha katika uchumi wa kati kama ambavyo Vision 2025imetuelekeza. Jambo hilo tuna kwikwi nalo sana kwa sababunchi hii tunahitaji kufikia kiwango cha maendeleo ambachokinawatoa wananchi katika hali duni ya maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikiliza MheshimiwaWaziri katika maelezo yake na amesema kwambamajadiliano ya uwekezaji huu bado yanaendelea. Sasa miminimepata mfadhaiko, nimesoma ukurasa wa 99 wa kitabuchake aya ya 136 na naomba kunukuu, anasema:“Majadiliano na wawekezaji waliokuwepo yaani Kampuni yaChina Merchant Holding International Limited na StateGeneral Reserve Fund ya Serikali ya Oman yamesitishwa”.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndiyo ambayoMheshimiwa Waziri ameyaandika ndani ya kitabu chake.Sasa nataka kujua ukweli, nipokee yaliyokuwa kwenye kitabuhiki cha Waziri au kauli ambayo ameisema kwamba

Page 238: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

majadiliano bado yanaendelea? Nadhani Waziri kwa sektahii ndiyo mwenye mamlaka na kama majadilianoyamesitishwa yeye ndiyo mtu wa kwanza anayajua naameyaweka kwenye kitabu, hii kauli nyingine iliyokuja inanitiawasiwasi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda Waziri atupe kaulimuafaka ama firm commitment ya kwamba mradi huuunaendelea au mradi huu sasa haupo? Kama maelezo hayahayakunitosheleza, nina nia ya kukamata shilingi nakuwaomba Wabunge wenzangu waniunge mkono tulijadilijambo hili lenye manufaa kwa taifa letu. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano, Engineer Kamwelwe ufafanuzi tafadhali.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu hoja ya MheshimiwaDkt. Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Bagamoyo kuhusianana ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyozungumza nikwamba majadiliano (negotiation committee) kuhusiana naujenzi wa bandari yamechukua muda mrefu sana. Tulifikamahali tukaandikiana barua na huyo mwekezaji, wakatitunaandika hotuba hii mwekezaji alikuwa ameandikiwabarua muda mrefu sana na hakuweza kuijibu. Kwa hiyo,wakati tunaandika hii speech, hizi speech zinaanzakuandikwa mwezi Machi, alikuwa haja-respond kwamba sasaanarudi kwenye mazungumzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana kwenye kitabuikaonekana kwamba tumesitisha baada ya kuona kwambamuda ni mrefu sana. Kwa sasa ametuandikia kwamba yukotayari kuendelea na mazungumzo. Tulimwandikia barua yakwanza akachukua muda mrefu sana kuijibu sasa amejibukwamba tunaendelea na mazungumzo, ndiyo maanakwenye kitabu ikawa imeonekana kwamba tumesitisha lakinimazungumzo yanaendelea ili tuweze kufikia muafaka.

Page 239: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

KUHUSU UTARATIBU

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Utaratibu wa nini tena?

MHE. KABWE Z.R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataratibu za Kibunge kama kuja jambo jipya ambalo limetokeaambalo halikuwemo kwenye hotuba, Serikali au hataMbunge analeta amendment ya kurekebisha eneo lile. Kwahiyo, naomba uwape muda Serikali walete correction yahicho kifungu ukurasa wa 99 ili tuweze kuwa on recordkwamba neno yamesitishwa limefutwa. Wanaweza kuandikahata kwa mkono tu wakaweka saini hapa kwenye record zaBunge ikaingia kwamba neno limesitishwa limeondolewa.(Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Hilo halikubaliki, neno jipya lipi, hii ajendaimekuwepo muda wote, imekuwa mpya mpya tangu linitena?

Mheshimiwa Shukuru Kawambwa, wewe ndiyemwenye hoja.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaMwenyekiti, suala hili lina umuhimu mkubwa kwa wawekezajikwa maana ya nchi ya China na China Merchant Holding niShirika la Serikali ya China, Serikali yetu rafiki kwa miaka mingina pia Serikali ya Oman. Sijaafiki maelezo ya MheshimiwaWaziri kwa sababu nikisoma katika kitabu chake categoricallyimesema kwamba majadiliano haya hayatafanyika mpakawawekezaji wameondosha masharti na sasa hivi hajasemakwamba masharti yameondoka, kwa maana kwamba hiliambalo analisema ni jipya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi naondoshashilingi, naomba kutoa hoja ili Wabunge wenzangu waniungemkono tulijadili jambo hili. Naomba kutoa hoja.

Page 240: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,naafiki.

MWENYEKITI: Hamjafikia idadi ya kumi.

WABUNGE FULANI: Aaaaa. (Kicheko)

MWENYEKITI: Haya, Katibu niandie wako wengi mno,nikiandika mimi watasema nimependelea. Haya tukae basi,majina nil iyoandikiwa na Katibu, kwanza ataanzaMheshimiwa Mussa Mbarouk, dakika mbilimbili.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza niunge mkono hoja ya Mheshimiwa Dkt. Kawambwalakini labda mimi nitoe masikitiko yangu tu kwamba mamboyetu haya ya kuchelewachelewa na kutafuta sababu navisingizio wakati mwingine tunapoteza fursa wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ya Bandari yaBagamoyo, kwanza ilianza Bandari ya Tanga (Bandari mpyaya Mwambani) wakaja wawekezaji kutoka Kuwait pamojana Serikali ya Uganda yakaja maneno maneno hivi hiviikaenda mpaka Uganda na Rwanda wakaenda kushirikianakujenga Gati Na. 9 katika Bandari ya Kilindini, MombasaKenya. Bandari ni lango kuu la biashara duniani kwa nini sisitunatafuta sababu sababu. Kumbe kama ni VAT watuwalikwishazungumza kwamba iachwe. Kama ni suala labandari kwamba inatakiwa ijengwe tungefanya harakatukaiwahi hiyo fursa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sasa hivi kwa taarifaKenya wanajenga Bandari mpya ya Lamu, kuna hatari ikajaikawa Bandari yetu hiyo ya Bagamoyo ikajengwa kwakuchelewe kwetu ikawa haina maana. Mimi naishauri Serikaliufanyike mpango wa haraka haya mambo na visingizio nasababu zisizokuwa na msingi viishe.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Viwanda naBiashara.

Page 241: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Niseme tu kwamba mradi waKanda Maalum ya Uchumi ya Bagamoyo ni mradi mkubwana wa kimkakati lakini kumekuwa na upotoshaji mkubwasana tangu jana jioni kupitia kwenye mitandao ambapoimesababisha sintofahamu kwa wananchi na hata kwabaadhi ya viongozi. Ukweli ni kwamba mazungumzo ambayoyalikuwa yanafanyika kati ya Government Negotiation Teamna hawa wawekezaji yalikuwa yanakwenda vizuri mpakaOktoba, 2018 walipokutana kwenye kikao cha mwisho hawandugu zetu wakaja na madai tisa. Kati ya madai tisa, madaisaba hayakuwa na matatizo makubwa isipokuwa madaimawili ambayo yalikuwa yanaingilia uhuru wa nchi na hayaameeleza vizuri sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mwezi Desemba,Government Negotiation Team iliwaandikia barua ikielezakwamba tumezungumza lakini haya hayawezi kuzungumzwa,kwa hiyo, warudi mezani watueleze kama wako tayari.Mpaka sasa hivi hatujapata majibu kwamba wako tayarikutekeleza yale ambayo yanahusu uhuru wa nchi.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo, kwa sababu jana wame-indicate sasawako tayari kuja kuendelea na mazungumzo, sisi tunaiagizaGovernment Negotiation Team watakapokuwa tayari wakijahapa nchini wataendelea na mazungumzo. Hili ambalolimeandikwa hapa kwenye hotuba liko sawasawa, tulisitishakwa muda mpaka wawe tayari kuzungumza kama ambavyosisi tunataka. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Jamani, kelele ya nini Mheshimiwa Wazirianafafanua vizuri?

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

Page 242: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

MWENYEKITI: Tunaendelea Waheshimiwa,Mheshimiwa Zitto.

MHE. KABWE Z.R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kusimama kuunga mkono hoja ya Mbunge waBagamoyo, Mheshimiwa Dkt. Kawambwa kuhusiana namaelezo ambayo Serikali imeyatoa kuhusu mradi waBagamoyo Special Economic Zone. Ni dhahiri Wabungewenyewe wameona hapa kwamba maelezo ambayo Waziriwa Uchukuzi ameyatoa na maelezo ambayo Waziri waViwanda na Biashara ambaye Special Economic Zone ikochini yake ameyatoa yanaonesha kuna total confusion withinSerikalini. Ndiyo maana nilikuwa nimetoa ushauri kwambabaada ya maelezo ya Waziri wa Uchukuzi kwamba hotubayake iliandikwa mapema kabla ya taarifa mpya kutokailikuwa ni kiasi cha Waziri kuleta addendum ya hotuba ilikurekebisha hilo tuweze kuwa na official communicationkwamba majadiliano yanaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asubuhi leo umeliongeavizuri sana kwamba tunaendelea kujadiliana kwa miaka sabakwa mradi mkubwa kama huu, mradi ambao unaendakuipaisha nchi yetu na kuiweka kwenye ramani ya dunia sisini watu wa namna gani? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Dakika haziko kwako, MheshimiwaChumi.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi na kimsingi naweza kuelewaMheshimiwa Dkt. Kawambwa kama kila mmoja akijiwekakwenye position yake kama mtu ambaye pamoja na kuwani mradi wa Kitaifa utanufaisha Taifa zima lakini kwa wananchiwake ndani ya miaka saba bila shaka amewaeleza mambomengi na neema nyingi mabazo mradi huo wataupata.(Makofi)

Page 243: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, I can understandkama ni frustration ambazo Mheshimiwa Kawambwa anazo.Lakini pamoja na hayo ningemuomba na kumsihiMheshimiwa Dkt. Kawambwa arejeshe shilingi on the pointkwamba Mheshimiwa Waziri amesema kitabu kilipokuwakinaandaliwa walikuwa katika huo mtanzuko waliokuwepona nitumie fursa hii kuiomba na kuishauri Serikali, tuwe naspeed katika kufanya negotiation lakini pia tuwe natahadhari kwamba tusiwe na speed ambayo baadayetukaingia katika mradi ambao tukaja kukaushwa damu kwahiyo tuwe na speed lakini tuwe na umakini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa HawaGhasia.

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, napenda nimuunge mkono Mheshimiwakawambwa na hasa tukizingatia suala la majadilianokuchukua muda mrefu. Hapa tunazungumzia Bandari yaBagamoyo lakini tunalo tatizo jingine la Liganga naMchuchuma. Majadiliano chini ya NDC kuhusu chuma badoyanaendelea hatukuwa na sababu sisi ya kujenga SGR kwakutumia chuma kutoka Japan. Tungeweza kujenga reli kwakutumia chuma ya kutoka Liganga na Mchuchuma, ni kwasababu ya majadiliano kuchukua miaka chungu nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na namuunga mkono zaidihasa ukizingatia mgongano wa kauli za Mawaziri. Niliridhikazaidi na kauli ya Mheshimiwa Eng. Kamwelewe lakinialivyokuja Waziri wa Viwanda na Biashara nikachanganyikiwakabisa hawakuzungumza kabla ya kuja hapa? Ile kauli yaWaziri wa Uchukuzi ilikaa vizuri zaidi kwamba wakatianaandika hiyo taarifa walikuwa bado hawajajibu nakwamba wamejibu wataendelea na majadiliano lakiniMheshimiwa Waziri wa Viwanda anasema kauli sahihi ni ileiliyoko kwenye kitabu cha hotuba, sasa tumsikilize nani?

MWENYEKITI: Ahsante.

Page 244: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naungana na Mheshimiwa Kawambwa.

MWENYEKITI: Dakika mbili zimekwisha tumalizie naMawaziri wawili. Mhehsimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani naWaziri wa Fedha. Mheshimiwa Kango Lugola tafadhali.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, ni miongoni mwa Wabunge ambaotuliambatana na wewe kwenda China na tukapata fursa yakupata wasilisho la wale China Merchants kwa hiyo leo nikoupande wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajua umuhimu wa mradihuu lakini majibu ambayo Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi ameyasema na hata yale ambayoyako kwenye ukurasa wa 99 siyo majibu hata kidogoyanayojichanganya. Yote yamejengwa kwenye msingi wamakubaliano, yote yamejengwa kwenye msingi wa maslahimapana ya nchi. Majadiliaono ambayo Serikali inaendeleani kwasababu ya ukubwa wa mradi na changamoto.Makubaliano haya siyo ya ununuzi wa Bajaji wa Toyo ni mradimkubwa ambao unahitaji Serikali iwe katika hali ya utulivu.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaombawaelewe kwamba mradi huu makubaliano yetuyatakapokuwa yameleta muafaka mradi huu Serikaliitautekeleza pale ambapo masharti yale ambayo yanaminyamaslahi mapana ya Taifa yataondolewa ya kujipangia tozo…

MWENYEKITI: Ahsante sana.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: …mashartiya kuzuia Wawekezaji wengine…

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri ahsante.

Page 245: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante sana, naomba pana keleletuendelee. Mheshimiwa Waziri wa Fedha dakika mbili.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa fursa. Kwanza namuomba sanaNdugu yangu Mheshimiwa Dkt.Kawambwa muachie Wazirishilingi ili aweze kuendelea na hatua ambayo ameielezavizuri.

Waheshimiwa Wabunge mradi huu ni kweli kabisa unafursa kubwa hili halina ubishi lakini ni lazima tuwe waangalifuna masharti yale ambayo tulikuwa tunajadiliana naMuwekezaji na hususani kuhakikisha kwamba maslahi ya Taifayanazingatiwa. Hata kama tungefanya kwa miezi miwili, hatawiki moja kama hatukuzingatia maslahi ya Taifa Bunge hililitahukumiwa, Serikali itahukumiwa ni muhimu sana sanatuhakikishe kwamba maslahi ya Taifa yanazingatiwa,chelewa ufike. (Makofi)

Mheshimiwa Dkt. Kawambwa unaua pia kwambaSerikali kwa sasa inatekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwani pamoja na barabara ya kutoka Bagamoyo kwenda Tangampaka mpakani mwa Kenya ambayo nayo itakuwa ni fursakwa wananchi wako. Mheshimiwa Kawambwa nakusihi sanamuachie Waziri shilingi yake…

MWENYEKITI: Ahsante sana

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: …ili awezekutekeleza, kuendeleza

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Dkt.Kawambwa na Mwenyekiti nakuomba shilingi hiyo tafadhaliirudishe Bwana tuendelee lakini nakupa nafasi ueleze kidogo.Karibu sana Mheshimiwa Kawambwa.

Page 246: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii nilikuwa katikaSerikali na sina nia na makusudio yoyote ya kuivuruga Serikaliyangu. Na nina imani kubwa na Wataalam wetu wa Tanzaniakwa sababu kila siku wamekuwa makini na wamekuwamakini sana katika kazi. Nilikuwa katika Wizara hii kablanimefanya nao kazi successful katika miradi kadhaa kwahivyo nina imani kwamba tunauwezo wa kusonga mbelekama tutasimamiwa kuweza kusonga mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna walivyoniomba,kwangu, ombi lako ni amri lazima nitekeleze amri ya Spika.Shilingi ya Waziri nairudisha lakini nikitaka ile kauli yakeaisimamie iliyosema kwamba “majadiliano yataendelea aumajadiliano yanaendelea na kwa majadiliaono haya yazaematunda ili Taifa hili liondokane na umasikini”

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, nakushukuru sana.Mheshimiwa Ally Saleh.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu ni kuhusiana nakubadilisha muelekeo wa namna ya kuendesha miradi yetu.Hivi sasa tumekuwa tunaona fahari kama Taifa kusematunatoa pesa mifukoni mwetu kununua ndege, kujenga reli,kujenga vitu vingine vitu ambavyo vina gharama kubwasana. Hii ina gharama kubwa kwa sababu kama tunanunuakwa fedha zetu ina maana tunalipa fedha za kigeni nje lakinipia zinabakia huku ndani, tunalipa huku ndani. Maana yakeni nini? Maana yake tunapata matatizo kwenye kuhudumiavitu vingine kwa sababu fedha zinahama katika njia ambayohatuwezi kutumia vitu vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa rai yangu, nilikuwanataka nilichukue wazo ambalo alilileta Mheshimiwa Turkyasubuhi kwamba tutengeneze miradi yetu sasa nataka

Page 247: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

mabadiliko ya Kisera tutengeneze miradi yetu kwakutegemea zaidi private public partnership iende kwavitendo ili tupunguze na tuweze kuifanyia kazi kwa sababusasa hivi tumeunda Wizara maalum kwa ajili ya kusimamiajambo hilo. Kwa hivyo, nataka kujua Serikali iko tayari namnagani kutekeleza miradi hiyo kwa njia ya PPP hasa miradiambayo ni grand kama ulivyosema wewe asubuhi. Kamahatukuridhika nitaomba tujadiliane namna ambavyotuendeshe nchi yetu kiuchumi kusogea mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

MWENYEKITI: Ufafanuzi Mheshimiwa Waziri tafadhali.Mheshimiwa Waziri wa Fedha.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, ninasikia hoja inayojengwa na Mheshimiwa AllySaleh ni hoja nzuri kwa sababu kwa uhalisia kutekeleza miradiye Serikali peke yake kwa Fedha za Serikali peke yakehaiwezekani. Kwa hiyo, pale ambapo pana fursa yakutegemea PPP ni sahihi lakini kilicho cha msingi hebu turudikwenye uhalisia. Tukirudi kwenye uhalisia, miradi hii lazima uwena uwezo kwanza wa ku-solicit good PPP’s, lazima uwe nauwezo wa ku-negotiate good PPP’s vinginevyo huko nyumatulishaingia mkenge mara nyingi na ndiyo maana tumeundakitengo mahususi kabisa cha kusimamia miradi hii ya PPP siyokwamba tunaiweka pembeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana pia katikamaelezo yangu nilieleza hata baadhi ya miradi ambayotunai-fast truck iende kwa utaratibu huo wa PPP ikiwemo reliambayo tunakusudia kujenga kwenda all the way kupitiaLake Nyasa mpaka Mchuchuma na Liganga. Kwa hiyo, hilisidhani kama tunahitaji kubadilisha sera yoyote iko pale tayarina tunayo Sheria ya PPP kwahiyo suala ni kuitaayarisha nakuandaa watalaam wa kutosha kuweza kuihakikishiakwamba nchi inaingia kwenye miradi thabiti ya PPP.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ally Saleh dakika moja tunakupa maana yake tunaingia kwenye upande mwingine.

Page 248: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ok.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli sijaridhika na yeyeWaziri atakuwa shahidi, nilipeleka mradi wa PPP wa 1000megawatts au zaidi Serikali full funded bila senti moja yaSerikali na au pia uwezekano wa PPP na jibu la frustrationniliyoipata kutoka Wizara ya Nishati na Wizara yake yeyeWaziri hatukufika popote hata yule mtu hakuitwa kufanyamjadala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama upo muda naombakutoa hoja tujadili jambo hili.

MWENYEKITI: Bahati mbaya muda hakuna tunaingiakwenye guillotine sasa. Katibu tuendelee na tumekosa watuwawili, Mheshimiwa Chegeni na Mheshimiwa Cecil Mwambenext time.

NDG. ATHUMAN HUSSEIN -KATIBU MEZANI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 68 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Kif. 1001- Administration and Human Resources Management………...Sh.1,450,664,265/=

Kif. 1002 - Finance and Accounts Unit……….Sh.328,238,000/=Kif. 1003 - Policy and Planning Unit…………...Sh.334,487,031/=Kif. 1004 - Internal Audit Unit……….......………Sh.113,008,000/=Kif. 1005 - Legal Service Unit………………..….Sh.130,642,704/=Kif. 1006 - Government Communication

Unit......................................................Sh.232,667,000/=Kif. 1007 - Procurement Management Unit…Sh.188,338,000/=Kif. 1008 - Management Information System

Unit........................................................Sh.11,628,000/=Kif. 2001 - Communication Division……...…...Sh.595,530,000/=Kif. 2002 - Information, Communication

and Technology Unit……….………..Sh.587,994,000/=(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya

Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 249: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

Fungu 62 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Kif. 1001 - Administration and Human Resources Management….……. Sh.3,430,964,570/=

Kif. 1002 - Finance and Accounts Unit………..Sh.763,659,000/=Kif. 1003 - Policy and Planning Unit……...... Sh.1,875,489,150/=Kif. 1006 - Government Communication

Unit…..................................................Sh.285,396,000/=Kif. 1005 - Procurement Management

Unit….........................………………… Sh.473,751,000/=Kif. 1006 - Internal Audit Unit………...………... Sh.392,053,000/=Kif. 1007 – Legal Services Unit……….......……..Sh.416,502,000/=Kif. 1008 - Information, Communication

and Technology Unit………….…….Sh.441,048,000/=Kif. 2005 - Transport Infrastructure Division...Sh.1,479,261,150/=Kif. 2006 - Transport Service Division……... Sh.74,884,579,470/=Kif. 5002 - Transport Safety and Environment

Division…..................................……. Sh.965,427,660/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 98 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Kif. 1001 - Administration and Human Resources Management……...…Sh.1,785,684,970/=

Kif. 1002 - Finance and Accounts Unit………. Sh.647,465,900/=Kif. 1003 - Policy and Planning Division……... Sh.407,162,600/=Kif. 1004 - Government Communication

Unit………............................………… Sh.144,413,600/=Kif. 1005 - Procurement Management

Unit……………........................……… Sh.144,109,806/=Kif. 1006 – Internal Audit Unit………..………... Sh.147,732,500/=Kif. 1007 - Legal Service Unit………………..…. Sh.124,722,500/=Kif. 1008 - Information, Communication

and Technology Unit………...….… Sh.137,824,500/=Kif. 2002 - Technical Service Division……. Sh.14,224,090,800/=Kif. 2005 – Roads Division……………………Sh.17,924,624,300/=

Page 250: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

Kif. 5002 - Safety and Environment Unit……. Sh.331,040,300/=Kif. 6001 - Airport Construction Unit.……....… Sh.123,792,404/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO WA MAENDELEO

Fungu 62 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Kif. 1003 – Policy and Planning Unit……….Sh.26,000,000,000/=Kif. 2005 - Transport Infrastructure

Division……..............................Sh.2,947,722,242,895/=Kif. 2006 - Transport Service Division…… Sh.570,000,000,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 68 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Kif. 1003 – Policy and Planning Unit………………....……….Sh. 0Kif. 2001 – Communication Division……………...………….Sh. 0Kif. 2002 – Information, Communication and Technology…Sh.0

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 98-Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Kif. 1003 - Policy and Planning Division……....Sh.275,000,000/=Kif. 2002 - Technical Service Division……...Sh.53,117,000,000/=Kif. 2005 - Road Division………..……….. Sh.1,136,667,229,268/=Kif. 5002 - Safety and Environment Unit……Sh.1,800,000,000/=Kif. 6001 - Airport Construction Unit.……..Sh.102,192,375,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa naKamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

Page 251: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. MheshimiwaWaziri taarifa tafadhali.

T A A R I F A

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Spika, naomba kutoa taarifa kwamba Kamatiya Matumizi imepitia Makadirio ya Matumizi ya Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 Kifungu kwa Kifungu na kuyapitisha bila Marekebishohivyo basi naomba Makadirio haya yakubaliwe na Bungelako tukufu.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Mheshimiwa Spika, naafiki.

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkono.Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi hiyo, ahsantesana.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na kukubaliwa)

(Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka wa Fedhakwa 2019/2020 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

yalipitishwa na Bunge)

SPIKA: Naomba niwashukuru sana Mheshimiwa Waziri,Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi n.k wotekatika Wizara hii na Serikali kwa ujumla kwa kazi nzuri ambayommekuwa mkiendelea kufanya na mnayoendelea kufanya,kwa niaba ya Bunge hili niwapongezeni sana, mnafanyakazinzuri, Wizara hii ni kubwa, ni nzito, mambo yote ya ujenzi nanchi hii inejenga kila mahali, shughuli za uchukuzi ni nyingiuchukuzi wa ardhini, uchukuzi wa majini, uchukuzi wa anganina mawasiliano ndiyo kabisa, mnafanyakazi kubwa sanatunajua, tumejitahidi kama Taifa kuwapa bajeti kadritulivyoweza. Tunajua pamoja na bajeti hii bado siyo kwamba

Page 252: BUNGE LA TANZANIA MEI 2019.pdf · Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Mgante Sannda, Mbunge

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

inatosha kihivyo lakini mtajitahidi basi kwa kutumia bajeti hiikufika mbali kadri mtakavyoweza na kama mlivyoliahidiBunge hili sisi tunawatakia kila la heri.

Mheshimiwa Waziri Mkuu tunawatakia kila la heriSerikalini huko katika utekelezaji wa Bajeti hii ya 2019/2020katika kiwango hiki ambacho tulikubaliana. Kwa maranyingine tunawapongezeni sana kwa kweli kazi inaonekana,viwango vya majengo yetu, barabara zetu na kadhalikavinazidi kupanda kila kukicha, tuko pamoja na ninyi. (Makofi)

Basi baada ya pongezi hizo naomba sasa kwa kuwamuda wenyewe unakaribia karibia. Safari hii nashangaakidogo Waheshimiwa Wabunge futari ya safari hiihatukaribishani!! Mambo yamebana kidogo? Hata kwenyefutari jamani? Ukaribu wa futari si bado uko pale pale? Maanayake Spika hajapata card hata mwaliko mmoja tangu hiishughuli ianze sasa nikajiuliza mimi tu au na wenzangu pia!!Basi tukaribishane au labda bado kidogo siku zikisogeasogeakidogo? Nawatakia kila la heri ndugu zangu. (Kicheko)

Tunaahirisha shughuli za Bunge hadi kesho Saa TatuAsubuhi.

(Saa 12.00 Jioni Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Jumanne,Tarehe 14 Mei, 2019 Saa Tatu Asubuhi)