biashara inayokua ya ngozi za punda na matokeo …...faida nzuri katika majarida yaliyopitiwa na...

17
NGOZI Biashara inayokua ya ngozi za punda na matokeo yake kwa ustawi na maisha ya punda. JANUARI 2017

Upload: others

Post on 03-Feb-2020

34 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

NGOZI Biashara inayokua ya ngozi za punda na matokeo yake kwa ustawi na maisha ya punda.JANUARI 2017

3The Donkey Sanctuary | Ngozi2 www.thedonkeysanctuary.org.uk

YALIYOMO

Unaweza kufikiria itakuwa aje ukiamka asubuhi na kupata kuwa kila gari katika jiji au mji wako limetolewa injini na magurudumu yake? Hakuna magari – hakuna njia za wewe au mtu yeyote katika jamii yako kusafiri. Safari hizi zote ambazo tunaziona kuwa za kawaida – kwenda shuleni, kufika kazini kila siku, kwenda kwa duka la chakula – ghafla zinakuwa ngumu au kazi zisizowezekana.

Hivi majuzi, katika jamii ya mashinani nchini Tanzania, hivi ndivyo ilivyofanyika kabisa – isipokuwa magari hayo ya thamani hayakuwa motokaa, yalikuwa punda. Wanakijiji waliamka na kupata wanyama wao 24 wenye bidii wameibiwa, wameuwawa na kutolewa ngozi usiku. Pigo kubwa kwa jamii hii na njia ya kutisha kwa wanyama hawa wanaofanya kazi kwa bidii kuaga dunia.

Huu ni mfano mmoja tu wa athari ambayo biashara ya kimataifa ya ngozi za punda inavyoathiri ustawi wa punda na maisha ya watu duniani kote. Mahitaji ya sasa ya ngozi hayaonekani kupungua, na kwa kuwa ni kiungo muhimu katika dawa za kitamaduni za Kichina zinazoitwa ejiao, bei ya ngozi hizi zimepanda sana. Jamii duniani nzima ziko kwenye hatari ya kuwa masikini na kupoteza uhuru wao.

Rekodi yetu inaonyesha ukubwa unaotisha wa biashara hii ya kimataifa inapokuwa ikijaribu kutimiza mahitaji yanayoongezeka ya bidhaa hii. Idadi ya punda haiwezi kuendelea kuangamizwa na lazima jamii zisinyimwe njia yao ya kipekee ya kujikimu. Lazima hatua ichukuliwe ili kukabiliana na biashara hii kwa ajili ya maslahi ya wanyama na ustawi wa wanadamu.

DIBAJI NA MIKE BAKER

Mike BakerMtendaji Mkuu

DIBAJI NA MIKE BAKER

UTANGULIZI

PUNDA KAMA MNYAMA WA UZALISHAJI

BIASHARA INAYOKUA YA NGOZI ZA PUNDA

Soko la Ejiao

Uzalishaji wa Ejiao

Idadi ya Punda Uchina

ATHARI KWA PUNDA BARANI AFRIKA

MUHTASARI WA BIASHARA YA NGOZI: TISHIO LA KIMATAIFA LA USTAWI WA PUNDA

ATHARI KWA PUNDA BARANI ASIA

ATHARI KWA PUNDA BARANI AMERIKA

ATHARI KWA PUNDA KOKO

CHANGAMOTO ZA BIASHARA HII

HATARI KWA USTAWI WA PUNDA

Ununuzi wa Punda

Usafirishaji

Uchinjaji (Kihalali au Kinyume cha sheria)

Matokeo kwa punda wanaosalia na Wamiliki wake

Kuongeza Uzalishaji wa Punda

Mashtaka yanayohusu Ustawi wa Wanyama

HATARI KWA MAISHA NA MAZINGIRA

Athari kwa mazingira

Kuonekana kwa Punda katika Sheria

HITIMISHO NA NJIA YETU YA KUENDELEA MBELE

MAREJELEO

3

4

6

8

8

8

8

10

16

18

20

21

21

22

22

22

24

24

25

25

26

26

26

28

30

4 www.thedonkeysanctuary.org.uk

Idadi ya kimataifa ya punda inakadirikiwa kuwa milioni 44(1) na inahusishwa pakubwa na mataifa yanayokua kiuchumi ambapo punda ndio wanyama wanaofanya kazi. Jukumu la punda katika jamii, kitamaduni na kiuchumi ni tofauti kulingana na jamii punda hizo zinazoishi na kufanya kazi. Majukumu yake ya kawaida na ya kinyumbani ni pamoja na kubeba mizigo, kuendeshwa, kulima na kuvuta rukwama, na majukumu mengine madogo ya burudani na uzalishaji wa chakula.

Ijapokuwa jukumu la punda kama mnyama wa uzalishaji limedhihirishwa katika historia, rekodi za nyama na maziwa ya punda zikithaminiwa na Wamisri wa zamani(2), matumizi ya bidhaa za punda hayakuwa sana katika karne ya 20, lakini yameibuka tena katika karne ya 21.

Katika miaka mitatu iliyopita, The Donkey Sanctuary imegundua nia inayoibuka ya matumizi ya punda kama wanyama wa uzalishaji, bidhaa inayothaminiwa sana ikiwa ngozi, nyama na maziwa. Mahitaji ya kimataifa ya bidhaa hizi mbalimbali za punda zimekuwa kwa upana zaidi, nia kuu ikiwa bidhaa za thamani zinazotokana na ngozi za punda.

UTANGULIZI

Uzito wa biashara hii umesababisha wasiwasi katika sekta nyingi za jamii duniani. Ripoti zinazoenea katika vyombo vya habari vya kimataifa zinaelezea ustawi duni wa wanyama, vitisho vya usalama wa riziki na chakula mashinani. Hadi sasa, kumekuwa na maelezo machache, kumekuwa na ushahidi usiotosha kuhusu masuala muhimu kama vile idadi ya punda zilizochinjwa, njia za biashara, bei za bidhaa na hali za ustawi wa punda kabla na wakati wa kuchinja.

Ripoti hii inatoa muhtasari wa hali ya sasa inayohusiana na biashara ya ngozi ya punda na biashara husika ya nyama. (Maelezo ya kando yanapatikana kuhusu tasnia inayoibuka ya maziwa ya punda kutoka kwa The Donkey Sanctuary.) Ripoti yenyewe imetokana na ripoti za habari katika vyombo vya kindani na vya kitaifa kutoka nchi zinazohusika katika biashara ya bidhaa za punda, na kupitia mtandao wa kimataifa wa washirika wa The Donkey Sanctuary. Kwa kuwa hakuna sheria mwafaka iliyoko ya kulinda punda, wamiliki wa punda, wafanyabiashara wakuu na watumiaji wa bidhaa hizi, maelezo machache yanayopatikana tu kwa mashirika ya nje ambayo hutathmini na kufuatilia ukubwa na usito wa biashara hii.

SHUKRANIThe Donkey Sanctuary ingependa kuwashukuru sana mtandao wake wa marafiki, wenzi na washiriki duniani kote ambao wamechangia maelezo ya ripoti hii na waliotetea ustawi wa punda kila siku. Hali nyeti ya maelezo yao humaanisha tumeweka siri baadhi ya michango ya ripoti hii lakini hii haimaanishi kuwa michango yao si ya thamani. Tutaendelea kuunga mkono na kufanya kazi pamoja na washirika ili kukabiliana na changamato hizi za ustawi wa punda duniani kote.

Kaskazini mwa Tanzania wanawake wa Kimaasai pamoja na watoto wao mara

kwa mara huteka maji kila siku, na hao hutegemea punda wao kubeba mizigo

yao mizito kwa umbali mrefu sana.

6 www.thedonkeysanctuary.org.uk

Kama mnyama wa kubeba mizigo, jukumu la punda limebadilika kidogo sana katika karne zilizopita. Punda huendelea kutimiza kazi yake ya zamani ya kubeba bidhaa hadi sokoni, kulima shamba, kuchota maji na kubeba bidhaa muhimu za nyumbani au kusukuma rukwama(3, 4). Hata hivyo, katika historia yote kama mnyama wa nyumbani, punda imetumika pia kuzalisha bidhaa kwa matumizi ya mwanadamu. Bidhaa za punda zimetafutwa sana katika karne nyingi, Wamisri wa zamani walithamini maziwa ya punda na kula nyama ya punda(2). Katika vipindi vya hivi majuzi matumizi ya nyama ya punda yametekelezwa na baadhi ya makundi Afrika, ambayo inathaminiwa kama chanzo bei nafuu na kinachofikiwa kwa urahisi cha proteni ya wanyama(5). Hadi hivi majuzi nyama nyingi za punda zilizotumika Afrika zilitokana na kuchinjwa kwa punda ambazo zilikuwa zimezeeka sana au ambazo zilikiwa zimeishiwa na nguvu sana kuendelea kufanya kazi. Matumizi ya nyama ya punda katika baadhi ya maeneo ya Uchina yanaendelea kuwa utamaduni maarufu, ambapo nyama ya punda inathaminiwa sana na kugharimu sana(6). Vivyo hivyo, katika jamii nyingi duniani kote matumizi ya nyama au bidhaa za punda ni haramu. Mtazamo huu unaweza kuwa kwa sababu ya utamaduni wa ndani au mafunzo ya kidini kama vile katika imani ya Kiislamu ambapo nyama ya punda inachukuliwa kuwa 'haram' (imekatazwa)(5).

Kinachoonekana sana katika miaka miwili iliyopita imekuwa kuibuka kwa biashara kuu ya kimataifa ya ngozi za punda, ikikadiriwa kuwa angalau ngozi milioni 1.8 za punda zinauzwa kila mwaka. Kwa hivyo, mahitaji ya kimataifa yamekadiriwa kuwa yameongezeka hadi milioni nne(7), vyanzo vingine vikiripoti viwango vya juu Uchina kuwa ngozi milioni 10 kila mwaka(8). Ngozi za punda hutumika kutengeneza dawa za kitamaduni za Kichina (TCM) zinazoitwa ejiao, zinazojulikana pia kama Colla corii asini au 'gluu ya ngozi ya punda', ambayo inatolewa kwenye gelatini ya punda kwenye ngozi na kuchanganywa na mimea na viambatano vingine, ili kuunda kipande, tembe, au toniki ya rojorojo(9). Ejiao ni dawa yenye mizizi ya kale na imetangazwa kama bidhaa ya wafalme. Kumedaiwa kuwa na manufaa mengi ya afya ya bidhaa hizi, ikiwa ni pamoja na kuzuia kuzeeka, kuongeza ashiki na kupunguza magonjwa ya ogani ya uzazi katika wanawake. Tafiti nyingi za kisayansi

PUNDA KAMA MNYAMA WA UZALISHAJI

katika mamali zimetekelezwa, wanasayansi wakidai kuna faidi muhimu za kiafya(9 – 11). Kwa mfano, Wang et al.(9) iliripoti kuwa “Colla corii asini (ejiao) inaweza kuwa na uwezo wa kupunguza mchakato wa kuzeeka kupitia kuboresha michakato ya kuzuia oksaidi, kuokoteza viini huru, na kudhibiti jeni zinazohusia na kuzeeka ”. Vivyo hivyo, baada ya kutambua msingi wa virutubishi vya ejiao, Wu et al.(10) walihitimisha kuwa ejiao “inaweza kuwa na uwezo wa kuwafaidi wagonjwa wa saratani wanaogua kutokana na upungufu wa damu unaotokana na tibaredi au tibakemili”. Nia ya Wachina ya kuthibitisha hali ya hatua na kutoa ushahidi wa ufanisi wa TCM imesababisha tafiti nyingine kuhusu Colla corii asini, na maoni yake yanapatikana kila mahali. Ijapokuwa baadhi ya data huenda ikawa na utata, wengine wameonyesha faida nzuri katika majarida yaliyopitiwa na wenzi(12). Utajiri unaoongezeka na kutawanyika kwa matajiri wa Uchina, pamoja na kuaminika kwa bidhaa za ejiao, kunaonekana kumesababisha kiwango cha juu sana cha mahitaji ya ngozi za punda hadi ugavi wa kimataifa unashindwa kumudu, na kusababisha bei za juu na madai yanayoenea ya ulaghai(7, 13). Viwango kama hivyo vya mahitaji ya juu kutoka kwa soko la Kichina kunachangia pakubwa ripoti za ustawi duni wa punda, wizi na kuongezeka kwa ghafla kwa bei za kununua punda. Bidhaa za punda zinatafutwa sana hadi ejiao inaweza kuuzwa hadi $375/kg.

© H

akim

iliki

Geo

rge

Kno

wle

s H

ong

Kong

geo

rgee

know

les@

yaho

o.co

m

© H

akim

iliki

Geo

rge

Know

les

Hon

g Ko

ng g

eorg

eekn

owle

s@ya

hoo.

com

Mamia ya ngozi za punda zinakauka

kwenye jua kama sehemu ya mchakato

wa uzalishaji wa ejiao. Mahitaji

ya kimataifa yanakadiriwa

kuwa kati ya ngozi milioni nne na

milioni kumikila mwaka.

8 www.thedonkeysanctuary.org.uk

SOKO LA EJIAOIjapokuwa matumizi ya nyama na maziwa ya punda yanapungua, inaonekana ni mahitaji ya ngozi ya punda ambayo yanasababisha kuongezeka kwa punda kuchinjwa duniani. Zamani nchini Uchina, ejiao ilikuwa ya wafalme na ilikuwa maarufu hadi mapema karne ya 20. Baadaye majaribio ya serikali ya kupunguza upatikanaji wa ejioa kulimaanisha kuwa sheria zilianzishwa na serikali katika mwaka wa 1994 za kuweka bei za bidhaa za ejiao, ambayo ilisababisha kupungua kwa upatikanaji(14). Kukua kwa haraka kwa watu matajiri nchini Uchina kuliongeza mahitaji ya bidhaa za kipekee au za anasa za TCM kama vile ejiao, pembe za vifaru na sehemu za chui ambazo zina mizizi ya kale na zinaweza kufuatiliwa hadi karne nyingi za zamani. Kutangazwa kwa ejiao kupitia runinga na intaneti, hasa tangu mwaka wa 2010(14), kumeongeza mvuto kwa vijana, ambao ndio hadhira inayopenda kununua. Ijapokuwa soko kuu la ejiao liko Uchina, kunaonekana kuwa na mvuto ulioongezeka wa bidhaa za ejiao kimataifa. Ripoti za habari zimeangazia upatikanaji wa bidhaa zenye ejiao katika maduka ya TCM jijini London(15) na kuuzwa hadharani kupitia majukwaa ya kimataifa ya uuzaji kama vile eBay na Amazon.

BIASHARA INAYOKUA YA NGOZI ZA PUNDA

UZALISHAJI WA EJIAOUzalishaji na utangazaji wa bidhaa za ejiao umetekelezwa na makampuni kadhaa ya Uchina, kampuni kubwa ikiwa Don'ge Ejiao ambayo ilianzishwa mwaka wa 1952. Kwa sasa ina zaidi ya wafanyakazi 10,000, ambao wanachakata zaidi ya ngozi milioni moja kwa mwaka na imeorodheshwa kwenye soko la hisa la Uchina(3). Makampuni mengine madogo na ya jumla ya watengeneza TCM wameingia katika soko hili lenye faida kubwa, bila shaka wanaongezea ushindani wa nyenzo ghafi na kuongeza hatari ya ulaghai wa chakula na bidhaa. Uzalishaji wa ejiao unaonyesha kuongezeka kwa matumizi ya mashine, katika hali zote za uzalishaji kuanzia kuchinja na kutoa ngozi hadi uzalishaji wa miti ya ejiao kwa kutumia teknolojia za kisasa. Kwa mfano, katika maonyesho ya hivi karibuni kule Beijing mfumo wa uzalishaji ejiao kwa kutumia roboti ulionyeshwa ambao unadai kupunguza gharama za uzalishaji kupitia mbinu za kupunguza kazi(16).

IDADI YA PUNDA UCHINAIjapokuwa mahitaji ya ejiao nchini Uchina yameongezeka, mamlaka ya kilimo ya Uchina imeripoti kuwa idadi ya punda imepungua pakubwa, kuanzia karibu milioni 11 mwaka wa 1990 hadi karibu milioni 6 mwaka wa 2014(1, 17). Ijapokuwa baadhi ya wakulima wamejaribu kunufaika na mahitaji yaliyoongezeka ya bidhaa za punda kupitia 'kufuga' punda, wengi wametatizika kutoa idadi ya kutosha ya punda kwa sababu ya uzaaji wa chini, hasa wakati zinafugwa kwa makini au wakati teknolojia kama ya upandikizaji inapotumika(18). Hakika, inajulikana kuwa wazalishaji wa ejiao wametafuta usaidizi na kuendelea kushawishi serikali kugharimia na kuhimiza wafugaji punda nchini Uchina kukimu soko la ejiao na kupunguza upungufu wa ugavi(3). Vivyo hivyo inaeleweka kuwa majaribio yanatekelezwa ya kuboresha uzazi na ubora wa uzalishaji kupitia matumizi ya upandikizaji na uzazi wa kuchagua(19).

Kukua kwa utofauti huo mkubwa katika ugavi na mahitaji ya ngozi za punda kunaonekana kuchangia biashara inayoibuka ya kimataifa katika ngozi ya punda ambayo inaripotiwa katika maeneo yote duniani yenye idadi kubwa ya punda. Na baadhi ya makadirio ya mahitaji ya ngozi Uchina yakiongezeka kuwa hadi milioni 10 kwa mwaka(8) na ugavi unaoripotiwa wa kimataifa wa milioni 1.8 kila mwaka, ni dhahiri kuwa idadi ya punda kimataifa inaathirika pakubwa na soko hili.

© H

akim

iliki

Geo

rge

Kno

wle

s H

ong

Kong

geo

rgee

know

les@

yaho

o.co

m

Uzalishaji wa ejiao unaonyesha kuongezeka kwa matumizi ya mashine, katika hali zote za uzalishaji kuanzia kuchinja na kutoa ngozi hadi uzalishaji wa miti ya ejiao kwa kutumia teknolojia za kisasa.

© H

akim

iliki

Geo

rge

Know

les

Hon

g Ko

ng g

eorg

eekn

owle

s@ya

hoo.

com

Idadi kuu ya punda barani Afrika ndio lengo kuu la biashara ya ngozi. Historia ya hivi majuzi ya ushirikiano kati ya serikali za Afrika na Uchina – Uchina ilifadhili jengo la Muungano wa Afrika(21) na kuna mifano mbalimbali ya makubaliano ya biashara za kitaifa – imechangia katika kufanya Uchina na Afrika Kusini mwa Sahara msafirishaji mkubwa Afrika na mshirika wa maendeleo(22). Mnamo mwaka wa 2016 biashara hadi Uchina kutoka Afrika Kusini mwa Sahara ziliwasilisha takriban asilimia 25 ya biashara zote, ikilinganishwa na asilimia 2.3 katika mwaka

ATHARI KWA PUNDA BARANI AFRIKA

wa 1985. Ripoti za biashara ya ngozi za punda kuelekea soko la Uchina ili kutengeneza ejiao zimeenea sana na ni nyingi. Karibu nchi zote zenye idadi kubwa ya punda zimeripoti ongezeko la kuchinjwa kwa punda kwa ajili ya soko hili. Kunaonekana kuwa kuna michakato miwili ya uchinjaji: vichinjio halali vinavyoongozwa na serikali au vichinjio vinavyodhibitiwa na serikali(23); au mchinjaji mdogo wa 'mashinani', ambayo mara kwa mara uhusisha punda zilizoibiwa(24). Ijapokuwa ngozi za punda zinaonekana kuwa bidhaa msingi zinazolengwa wakati wa uchinjaji, imeripotiwa

pia kuwa nyama ya punda inaweza kuwa bidhaa yenye faida kivyake(25). Inayotatiza zaidi ufahamu wowote wa biashara barani Afrika ni imani za kidini ambazo zinazunguka matumizi ya nyama ya punda – inazingatiwa kuwa ni 'haram' (imekatazwa) katika imani ya Kiislamu(5). Ijapokuwa majimbo yenye Waisilamu wengi kama vile Mali yanaonekana kukataza uchinjaji wa punda na uuzaji wa nyama na bidhaa za punda(26), pia wanakumbana na shinikizo sawa na nchi nyingine ili kunufaika kiuchumi na soko la biashara linaloibuka la ngozi.

12 www.thedonkeysanctuary.org.uk

KICHINJIO HARAMU

MISRIUchinjaji haramu wa punda katika maeneo ya mashinani umeripotiwa kila mahali Afrika. Taarifa ya majuzi ya ugunduzi wa mizoga ya punda 250 zilizotolewa ngozi nchini Misri(27) zinaonyesha uzito wa tatizo hili katika nchi ambapo uchinjaji wa punda kwa ajili ya chakula kwa kawaida huchukuliwa kama jambo lisilokubalika kitamaduni. Ripoti nchini Misri zinaelezea bei za juu zilizolipwa kwa ajili ya punda na ongezeko kubwa katika bei zake, na hata pia faida ya soko la 'ngozi' nchini Uchina(28). Serikali ya Misri hivi majuzi iliamua kuruhusu ngozi ya punda kusafirishwa Uchini kwa matumizi ya 'dawa’(28).

TANZANIATanzania imeripoti pia uchinjaji mkubwa wa punda zilizoibiwa usiku katika vijiji vya mashinani(24). Wanajamii wanafunzwa kuhusu kulinda punda na wanajenga maboma yenye ua salama. mpango unaofadhiliwa na The Donkey Sanctuary, ili kulinda punda usiku. Mizoga iliyopatikana ya punda inaonyesha kuwa ni ngozi tu zilizochukuliwa na kutupa mwili wote. Pia kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa kuwa punda kaskazini mwa Tanzania wanapelekwa katika Hifadhi ya Wanyama

ATHARI KWA PUNDA BARANI AFRIKA

ya Kitaifa ya Kigosi ili kuchinjwa na kutolewa ngozi kwa kuwa ni vigumu kwa watekelezaji kupatikana ndani ya hifadhi (Mawasiliano ya Kibinafsi ya Siri)

Tabia kama hizo zinaweza kuashiria jinsi ngozi za punda zinavyotafutwa sana nchini Tanzania. Hata hivyo, hii ni nchi ambayo nyama ya punda tayari inaliwa na makundi fulani (Mawasiliano ya Kibinafsi ya Siri) na vituo vyenye mashine za kuchinja punda vinafanya kazi na vimepokea usaidizi kutoka kwa serikali za ndani na za kitaifa.

AFRIKA KUSINIMashirika ya ustawi wa wanyama nchini Afrika Kusini yanapokea ripoti mara kwa mara kuhusu punda waliochinjwa katika maeneo ya mashinani kwa ajili ya ngozi zao. Baraza la Kitaifa la Mashirika ya Kuzuia Ukatili kwa Wanyama limesema kuwa "punda wanasakwa / kuibiwa, kisha kusafirisha na kuchinjwa kwa ukatili kwa ajili ya ngozi zao”(29). Tafiti za majuzi kuhusu hali za kuogofya za punda wanaosubiri kusafirishwa na wanaosafirishwa kichinjioni kwa ajili ya soko la ngozi la Uchina zimesababisha kushtakiwa kwa watu kuhusiana na ukiukaji wa Sheria za Kulinda Wanyama. Kesi ya hivi majuzi ilizingatia wanyama 70 wagonjwa na waliodhoofika na kuachwa bila chakulia katika Bloemfontein, ambapo mwenyewe alisema kuwa "alikuwa akitaka tu ngozi za kusafirisha Uchina”(29).

© P

icha

kw

a hi

sani

ya

MAW

O, T

anza

nia

© P

icha

kw

a hi

sani

ya

MAW

O, T

anza

nia

Punda wote 24 katika kijiji cha Tanzania waliibiwa, kuuwawa na kutolewa ngozi usiku, na kuacha jamii ikiwa imetamaushwa. Kwa sababu hiyo, The Donkey Sanctuary imesaidia kufadhili utengenezaji wa maboma yenye ua salama ili kulinda punda usiku.

14 www.thedonkeysanctuary.org.uk

KICHINJIO CHA PUNDAKILICHOIDHIINISHWA NA SERIKALIBiashara zinazokubaliwa na serikali kushiriki katika bidhaa za punda zimeonekana nchini Namibia(30), Botswana(31), Tanzania(32) na Kenya(23), na ripoti zaidi za vichinjio vya punda vinavyoidhinishwa serikali katika maeneo ya Bishoftu and Asela.

ETHIOPIAEthiopia ina idadi kubwa zaidi ya punda barani Afrika, inakadiriwa kuwa na takriban punda milioni 7.4. Vichinjio viwili vikubwa vya punda vinavyomilikiwa na Wachina vimeundwa katika Debre Zeit (Bishoftu) na Asela, ijapokuwa bado havijaanza kufanya kazi. Kuanzishwa kwa vichinjio hivyo kunahusisha ushirikiano wa serikali ya Ethiopia. Serikali ilitoa taarifa kwa umma kuhusu uwezo wa biashara ya ngozi ya punda hadi Uchina lakini bado kuna maoni tofauti na mazungumzo yanayoendelea kati ya umma kuhusu kama ni nafasi ya biashara au tishio kwa jamii masikini ambazo zinategemea punda. Kuna uwezekano kuwa baada ya muda mrefu biashara hii itatatiza jamii na uchumi katika nchi ambayo asilimia 83 ya watu wanaishi mashinani na usafirishaji wa bidhaa unategemea punda (Mawasiliano ya Kibinafsi ya Siri).

KENYAVichinjio vikubwa vya punda vimeanzishwa pia nchini Kenya, na zaidi ya milioni KSh350 ($3.4 million) zikiwa zimetumiwa katika kichinjio cha Mogotio na wawekezaji wa Uchina(23), na kichinjio kingine cha punda cha Naivasha na mwekezaji wa ndani. Kupata leseni ya vichinjio vya punda nchini Kenya imesababisha mgawanyiko kwa sababu ya tamaduni za nchini kuhusu matumizi ya nyama ya punda. Matatizo kama hayo yanaonekana yametatuliwa kupitia matoleo ya leseni ya 'usafirishaji pekee'(23). Ni wazi kuwa ijapokuwa serikali za ndani na za kitaifa za Kenya zinaweza kuwa na matatizo na maoni ya umma kuhusu biashara ya punda, zinavutiwa na matokeo ya mamia ya kazi na mapato kutokana na ushuru wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja kama vile ushuru unaotozwa wa KSh200 hadi KSh300 ($1.90 hadi $2.90) kwa kila punda na serikali ya mitaa ya Nakuru punda zikichinjwa(33). Kutokana na mtazamo wa uchumi, serikali ya Kenya imeripoti pia ushuru ulioongezeka kwa usafirishaji wa ngozi ghafi kutoka 40% hadi 80% katika mwaka wa 2016(34).

ATHARI KWA PUNDA BARANI AFRIKA

BUKINAFASORipoti zinaashiria ukiukaji mkubwa na vichinjio vya punda kuhusiana na masuala ya ustawi na ya kimazingira(35, 36). Ripoti za serikali nchini zinakadiria kuwa, katika kipindi cha miezi sita, karibu punda 45,000 kutoka idadi ya karibu milioni 1.5 zimechinjwa tayari(4). Viwango kama hivyo vya uchinjaji, vinavyosababishwa na ukiukaji wa mazingira na ustawi na kuongezeka marudufu kwa bei ya punda ($75 katika mwaka wa 2014 hadi $135 katika mwaka wa 2016) kumesababisha majadiliano kuhusu sheria za uchinjaji katika ngazi za serikali na mnamo Agosti 2016 'Baraza la Mawaziri" lilipiga marufuku usafirishaji wa punda na bidhaa zake(37).

NIJERINijeri imepitia magumu kama hayo na biashara hii, zaidi ya punda 80,000 wakisafirishwa katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka wa 2016 ikilinganishwa na 27,000 katika mwaka wote wa 2015(21). Ongezeko hili la mahitaji limesababisha ongezeko mara tatu hadi nne la gharama ya punda. Serikali ya Nijeri imechukua hatua ya ziada na kutangaza kupigwa marufuku kwa uchinjaji wa punda zote(38).

GHANAIjapokuwa biashara ya ngozi za punda inakosa uwazi katika baadhi ya nchi, ni wazi katika nchi nyingine. Ripoti kuhusu siku za soko nchini Ghana zimeashiria kuwa ngozi zinanunuliwa na wanabiashara kwa $122 kila moja (Mawasiliano ya Kibinafsi ya Siri). Ripoti kutoka ndani ya Ghana zinapendekeza kuwa wanabiashara wa kati wanachinja hadi punda 200 kila siku na kwamba nyama na ngozi za punda ni mali ya thamani, kukiwa na soko la ndani la nyama(39). Licha ya haya, imetangazwa hivi majuzi na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ya Wanyama kuwa hakuna "kichinjio chochote kilichoidhinishwa cha punda kwa matumizi ya umma” na "kuna kichinjio kimoja tu kilichoidhinishwa kusafirisha ngozi"(40).

NCHI ZINGINEBiashara ya bidhaa za punda inaonekana kuwa imeenea sana katika nchi zingine nyingi barani Afrika, kukiwa na ripoti za uchinjaji kwa ajili ya ngozi na nyama nchini Botswana, Namibia(41) na Nijeria(42), na kuna tuhuma ya biashara hii nchini Zimbabwe na Zambia. Biashara ya nyama na bidhaa za ngozi za punda inaonekana kuwa imeenea zaidi katika Nijeria, ambapo kwa kawaida nyama ya punda huliwa na inauzwa kwa bei ya juu (c. $88 kwa kila mzoga) na ngozi zinauzwa zaidi ya $125(42).

Uchomaji wa mizoga ya punda katika kichinjio cha punda

kilichoidhinishwa na serikali.

16 www.thedonkeysanctuary.org.uk 17The Donkey Sanctuary | Ngozi

Biasharanje za punda zimepigwa marufuku

Biasharanje imethibitishwa

Biasharanje inazingatizwa

Waagizaji wakuu

Nchini Brazili punda wanasafirishwa

zaidi ya km 1,000 ili kuchinjwa, hii

inaonyesha biashara yenye faida

Kupungua kwa idadi ya punda nchini Uchina tangu 1991

Idadi ya jumla ya punda

Mahitaji yanayokaridiwa ya kila mwaka ya ngozi

Ugavi unaokadiriwa wa kila mwaka

Bei ya punda nchini Bukinafaso

imeongezeka kutoka $75 hadi $135 kati ya mwaka wa 2014

na 2016

Biashara ya jumla hadi Uchina kutoka Afrika Kusini mwa Sahari

1980

1985 2016

1990 2000 2010

2.3% 25%

46%

MUHTASARI WA BIASHARA YA NGOZI: TISHIO LA KIMATAIFA LA USTAWI WA PUNDA

Marekani ya Kaskazini

Marekani ya Kusini

Bahari la Pasifiki

Bahari la Atlantiki

Ulaya

Afrika

Mashariki ya Kati

Asia

Australia

Katika mwaka wa 2015 Pakistani ilikuwa nchi ya kwanza ya Asia kupiga marufuku biasharanje

ya ngozi za punda

18 www.thedonkeysanctuary.org.uk

UCHINARipoti zinaashiria kuwa idadi ya punda za Uchina zimepungua kwa karibu asilimia 50. Upungufu kama huo unawezekana kwa sababu ya uchinjaji mkubwa wa idadi hiyo kwa sababu ya ngozi na nyama. Inaonekana pia kuwa kuna nia mpya ya kufuga punda, mara kwa mara katika mifumo ya hali ya juu. Inaripotiwa kuwa mzalishaji mkuu wa ejiao, Dong'e Ejiao mwenyewe, ana shamba yenye zaidi ya punda 10,000 wanaofugwa kwa ajili ya ngozi zao. Katika kituo hicho kuna majaribio ya kuzalisha wanyama wakubwa na wanaokua kwa haraka ili kutoa bidhaa iliyo tayari zaidi(3). Bado Uchina inaripotiwa kuwa na idadi ya punda milioni sita(1) na, ijapokuwa punda wengi bado wanatumika katika kazi za kawaida za mashambani, kuna uwezekano mkubwa kuwa idadi hiyo haitatumiwa tena kwa soko lenye faida la ngozi na nyama.

MONGOLIAUchina inajulikana pia kwa kuhimiza nchi nyingine katika maeneo yake, kama vile Mongolia, kuzingatia kufuga punda kwa ajili ya uzalishaji(19). Mongolia ni nchi yenye historia ndogo ya kufanya kazi na punda au kufuga punda, inapendelea mifugo au farasi badala yake. Hata hivyo, uzalishaji wa punda unaendelea kuonekana kuwa sawa kama masoko yanayokua ya mifugo yanayokimu tamaa ya Wachina

ATHARI KWA PUNDA BARANI ASIA

ya nyama, na faida zinanakiliwa kuwa karibu maradufu ikilinganishwa na kufuga mifugo(19).

PAKISTANIPakistani ni nchi inayokadiriwa kuwa na punda milioni 4.9. Hadi hivi majuzi ilikiwa msafirishaji muhimu wa ngozi za punda, ikisafirisha 200,000 kati ya 2014 na 2016. Hata hivyo, matatizo makubwa yaliibuliwa kuhusu kuchinjwa kwa punda kuliosababisha nyama ya punda kuuzwa kama nyama ya ngombe kwa matumizi ya umma. Masuala kama hayo ya ulaghai yalikuwa mabaya sana katika nchi hii yenye Waisilamu wengi ambapo ulaji wa nyama ya punda ni haramu. Katika kushughulikia matatizo haya yaliyoenea, Pakistani ilikuwa nchi ya kwanza Asia kupiga marufuku biasharanje ya ngozi za punda(43), ili kupunguza matokeo ya nyama ya punda kuingia katika mzunguko wa chakula wa wanadamu. Hata hivyo, uchinjaji haramu bado huendelea(56).

KIRIGIZISTANIMalori ya punda hai huripotiwa kusafirishwa kutoka Kirigizistani hadi Uchina. Uchinjaji haramu umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa lakini biashara hii imeidhinishwa kupitia mkataba wa kusafirisha punda 4,000 hadi Uchina. Wafanyabiashara wasiojulikana wanasemekana kulipa 10,000 soms ($147) ikiliganishwa na thamani ya soko la ndani ya 3,000–4,000 soms ($44–$59)(62).

© H

akim

iliki

Geo

rge

Know

les

Hon

g Ko

ng g

eorg

eekn

owle

s@ya

hoo.

com

20 www.thedonkeysanctuary.org.uk 21The Donkey Sanctuary | Ngozi

MEKSIKOIjapokuwa inashukiwa kwamba Marekani hutoa kiwango kikubwa cha ngozi kwa soko la Uchina kila mwaka, kuna maelezo au ushahidi mdogo kwa usafirishaji halali wa ngozi za punda kutoka eneo hili. Hata hivyo, idadi kubwa ya punda wanachinjwa nchini Meksiko (walionunuliwa ndani ya Meksiko na mpaka wa Marekani)(44); nyama ya punda inapendwa na soko hili ambapo huchukuliwa kama lishe(5). Ngozi za punda huonekana zikitangazwa zinauzwa na makampuni ya Meksiko(45) lakini kunaonekana hakuna athari kubwa kwa idadi ya punda wa humu au idadi ya punda wanaoagizwa wakati huu(44).

KOLOMBIARipoti nchini Kolombia zinaonyesha uchinjaji haramu wa punda(46) kwa ajili ya ngozi zao, kukiwa na zaidi ya punda 50 wanaojulikana kuwa wamelengwa hivi karibuni. Ugunduaji wa mizoga iliyotolewa ngozi na miili yao ikawachwa bila kuguzwa umechangia wasiwasi wa wakazi kuwa ngozi zinasafirishwa nje. Polisi wa ndani wamekuwa na wasiwasi sana hadi wameanzisha kampeni katika eneo la Sucre inaoitwa 'Linda punda wako’.

ATHARI KWA PUNDA BARANI AMERIKA

Biashara ya ngozi na nyama ya punda ni tatizo linalokua kimataifa kuhusiana na ustawi wa wanyama, afya ya umma na uthabiti wa kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Matatizo haya yamekithiri sana katika nchi zinazokua ambapo jamii zinategemea punda sana kama wanyama wa kufanya kazi. Kwa bahati mbaya matatizo haya yanachangiwa na utegemezi wa kimataifa, hasa ule wa masoko yanayoibuka kama ya mataifa ya kusini na unachangiwa zaidi na uchumi wa Uchina (49). Mazungumzo ya kibiashara ya Uchina, hasa katika nchi za Afrika, yametoa njia halali na za kuvutia kifedha za biashara ya bidhaa za punda, ambapo huletea serikali, wafanyabiashara wa kati na tabaka aali la watu wenye uwezo kipato kikubwa. Ijapokuwa watu wachache wanaweza kuwa matajiri kutokana na biashara hii ya bidhaa za punda, kuna wasiwasi mkubwa wa ustawi kwa punda wengi wanaochinjwa kama matokeo ya biashara hii, na kwa jamii zinazofanywa kuwa masikini ambazo hutegemea punda hawa kama wanyama wa kufanyia kazi.

ATHARI KWA PUNDA KOKO

IDADI YA PUNDA KOKOMwanzoni, punda koko walionekana kuwa wanaolengwa na wanabiashara wa ngozi za punda, ikiripotiwa kuwa serikali nchini Australia(20) na Marekani ya Kusini waliombwa ili 'kuchukua' punda wa mwituni kwa ajili ya ngozi zao Pengine hii ni kwa sababu idadi kama hiyo ilichukuliwa kama rasilimali inayoweza kutumiwa kwa urahisi ambayo haina wamiliki halisi. Punda koko wanaonekana na wengi, pamoja na baadhi ya serikali, kuwa ni spishi 'geni' inayokera na hawaathiri mazingira ya ndani vizuri, kwa hivyo kufanya kufaidika kutokana na biashara ya ngozi (ambayo pia hupunguza idadi ya punda koko) kuwa pendekezo la kuvutia. Ijapokuwa kumekuwa na ripoti ambazo hazijadhibitishwa kutoka Brazili kuhusu biasharanje ya punda na idadi kubwa ya ngozi za punda, ushahidi wazi zaidi

BRAZILIBrazili inaweza kuonekana kama chanzo kikuu cha ngozi za punda kwa sababu ya vituo vilivyopo vya biasharanje ya mifugo na nyama ya ngombe na idadi ya punda milioni moja, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya uzaaji kaskazini mashariki mwa nchi hiyo(47). Mzigo mmoja uliokuwa na shaka sana wa punda 137 uligunduliwa kuwa umesafiri zaidi ya km 1,000 ili kuchinjwa, ikiripotiwa kuwa punda 14 kati ya hawa walikufa wakisafirishwa. Hii iliibua maswali kuhusu punda hao walikuwa wakipelekwa wapi: isipokuwa kama walikuwa sehemu ya biashara ya ngozi, usafiri kama huo wa muda mrefu hauwezekani kwa sababu nyama ya punda haitumiwi sana au kuthaminiwa nchini Brazili(48). Maelezo zaidi kutoka kwa wataalamu wa masuala ya wanyama nchini Brazili wanaweza kusema kuwa, ijapokuwa haijulikani vizuri, usafirishaji nje wa ngozi za punda hadi Uchina hufanyika mara kwa mara na ni sehemu kubwa (Mawasiliano ya Kibinafsi ya Siri).

unapatikana nchini Australia ambapo inaeleweka kuwa serikali inaonelea biasharanje ya bidhaa za punda hadi Uchina inahitaji uchunguzi zaidi(20). Ripoti za hivi majuzi kutoka Serikali ya Himaya ya Kaskazini nchini Australia inaonekana kuunga mkono ufugaji wa punda kwa ajili ya soko la TCM badala ya kulenga idadi ya punda koko, ikisema kuwa "ufugaji wa punda unawezekana kama biashara ya kipekee au kama bishara ya kando pamoja na uzalishaji wa mifugo". Bado tunasubiri kuona iwapo ufugaji punda kwa kiasi kikubwa utaendelea wakati idadi ya punda koko ni kubwa katika eneo hili. Maelezo zaidi kuhusu idadi ya punda koko na changamoto punda hao wanapitia kimataifa inapatikana katika ripoti ya The Donkey Sanctuary inayoitwa 'Feral Donkey Heards'.

CHANGAMOTO ZA BIASHARA HII

© H

akim

iliki

Geo

rge

Kno

wle

s H

ong

Kong

geo

rgee

know

les@

yaho

o.co

m

22 www.thedonkeysanctuary.org.uk

Ustawi wa punda wowote wakati wa maisha yake na mwisho wa maisha yake ni muhimu na unastahili kuwa jambo la msingi kwa mnyama yeyote anayezalisha chakula5). Cha kusikitisha ni kuwa ustawi wa punda wanaotumiwa kuzalisha ngozi na nyama unaripotiwa kuwa umehatarishwa sana(3, 24, 29) wakati wa ununuzi, kusafirisha na/au kuchinja.

KUNUNUA PUNDAPunda wanaolengwa kutoa nyama au ngozi za kusafirishwa Uchina wananunuliwa kwa njia nyingi. Punda wanaweza kuibiwa kutoka kwa wamiliki ambao wanawatunza vizuri, baada ya kugundua thamani yao ya kijamii na kiuchumi. Punda koko wengine au wanaomilikiwa kibinafsi wanaweza kununuliwa masokoni na wafanyabiashara wa kati wanaotafuta kufaidika na kuwakusanya punda kabla ya kuwauza kihalali au kuwachinja kiharamu. Punda hawa hupitia dhiki kwa sababu ya kutenganishwa na wengine ambao wamezoeana, na hata pia wamiliki wao wanaowajali, kukusanywa katika vikundi wasivyozoea, kushughulikiwa na wageni, na kuwekwa katika hali ambazo hazifai, ambapo hali hizi zote husababisha kuhatarishwa kwa ustawi wao.

Changamoto maalum zipo pia wakati punda wanachinjwa kwa sababu ya ngozi zao, bila kuthamini nyama yao. Hii husaidia kuendeleza faida zaidi ambayo inaweza kupatikana kutokana na kununua punda wagonjwa au dhahifu kwa bei ya chini kabla ya kuuzwa ili kuchinjwa, kwa kuwa ngozi itagharimu sawa ikilinganishwa na mnyama mwenye afya anayegharimu zaidi. Ununuzi wa punda kama hao wasiofaa husababisha kuongezeka kwa mateso na vifo. Huwahimiza pia wamiliki na wauzaji dhidi ya kupata punda wenye afya na ustawi unaofaa kwa kuwa kuna faida kidogo sana ya kiuchumi katika kufuga punda walio katika hali nzuri ya kimwili na wasio na magonjwa. Hali kama hizo zimeripotiwa Afrika Kusini(29), ambapo punda waliwachwa bila chakula kabla ya kuchinjwa kwa kuwa ngozi zao ndio zilionekana kuwa za thamani na ngozi zinapatikana haijalishi hali ya punda.

HATARI KWA USTAWI WA PUNDA

USAFIRIUsafirishaji hadi kichinjioni ni sehemu muhimu ya wasiwasi, kukiwa na visa vingi vilivyoripotiwa vya mizigo ya punda nchini Brazili (Mawasiliano ya Kibinafsi ya Siri), Tanzania(50) na Afrika Kusini(29) ikisimamishwa na kupatikana na punda wengi waliokufanya au wanaokufa wakisafirishwa; katika visa hivi vyote punda hawa walishukiwa kuwa wanapelekwa kuchinjwa kwa ajili ya biashara ya ngozi na hawakuzingatia ustawi wa punda hawa. Kukiwa na 'wafanyabiashara wengi wa kati' wanaoripotiwa kununua punda kwa idadi kubwa Afrika nzima na maeneo mengine, wamiliki wa punda wanaweza kubadilika mara nyingi sana, na kuuzwa kupitia masoko ya kati na kusafirishwa kwa muda mrefu (kama vile punda 137 walioripotiwa kusafirishwa kwa zaidi ya km 1,000 nchini Brazili). Hali wakati wa usafirishaji hazipatii punda nafasi ya kupumzika, kula au kunywa maji. Hii ni kweli kabisa wakati ngozi ndio bidhaa ya thamani tu. Sheria dhidi ya kuchinja punda katika maeneo mengine ni hatua nzuri kwa ujumla lakini serikali lazima zikumbuke kuwa hii inaweza kusababisha ukiukaji wa ustawi na maambukizi ya magonjwa kupitia usafirishaji kati ya mipaka na safari za muda mrefu ili wanabiashara waweze kufika katika masoko halali.

Ijapokuwa haijadhibitishwa, kumekuwa na ripoti za biasharanje ya punda hai hadi Uchina kupitia bahari(57). Ikiwa usafirishaji wa punda hai kutoka Misri hadi Uchina utaendelea, hii inaweza kuwakilisha zaidi ya siku 20 majini na safari ya ziada barabarani kwenda na kutoka bandarini. Punda ni spishi ya wanyama werevu na uhisi madhara ya dhiki. Kuna hatari kubwa ya idadi kubwa ya vifo kwa sababu ya kuwaweka wanyama wengi katika hali za dhidi ya kimwili na kihisia kwa sababu ya usafiri. Shirika la Afya ya Wanyama Duniani limechapisha maelekezo ya kusafirisha wanyama baharini(58) kama mojawapo ya vipaumbele vinne vya ustawi wa wanyama kimataifa. Ijapokuwa maelekezo haya ni wazi kuhusu vipengele vya kiufundi kama vile vifaa vya chombo, kuweka rekodi na kupakia, hayashughulikii punda kikamilifu na kwa hivyo hayashughulikii matatizo ya kitabia na kihisia ambayo punda wanaweza kupitia.

© H

akim

iliki

Geo

rge

Know

les

Hon

g Ko

ng g

eorg

eekn

owle

s@ya

hoo.

com

Hali wakati wa usafirishaji hazipatii punda nafasi ya kupumzika, kula au kunywa maji.

24 www.thedonkeysanctuary.org.uk 25The Donkey Sanctuary | Ngozi

UCHINJAJI (KIHALALI NA KINYUME CHA SHERIA)Uchinjaji wa punda kwa ajili ya ngozi na nyama yao hufanyika katika mazingira mengi, kuanzia punda mmoja kuchinjwa nyumbani hadi kuchinja katika kiwanda kikubwa kwa njia zote halali na zisizo halali. Maelezo kuhusu wizi na punda kuchinjwa msituni ni jambo la kawaida(24, 27, 46). Ijapokuwa baadhi ya uchinjaji unaweza kutekelezwa bila kumtesa punda, kuna uwezekano mkubwa kuwa nyingi kati ya vifo hivi huwa vimeharakishwa, na kutekeleza katika mazingira ambayo hayafai na watu wasiokuwa na uzoefu wakati punda wengine wakiona au kusikia. Visa vya hivi majuzi nchini Tanzania vimewahusisha punda kusafirishwa zaidi ya km 30 hadi msituni ambapo wanashukiwa kuwa waliuwawa kwa kudungwa sindano ya sumu kabla ya kutolewa ngozi; mizoga iliyosalia iliwachwa msituni(50).

Ijapokuwa vinasimamiwa, vichinjio vilivyoidhinishwa na serikali vinaonekana kuwajali zaidi punda katika kuwatoa uhai, lakini vituo kama hivyo pamoja na taratibu zao bado zina nafasi nyingi kwa ustawi wa punda kuhatarishwa(5). Video ya hivi majuzi iliyokuwa ikitangaza kichinjio kipya kilichofunguliwa cha Goldox kule Chemongoch nchini Kenya(51)

inaonyesha kituo kipya kinachosemekana kuweza kuwashughulikia punda 100 kila siku. Ijapokuwa kituo hiki kinaonekana kuwa na vifaa vya kisasa, wasiwasi kuhusu ustawi ni dhahiri katika video hiyo inayoonyesha punda wakikokotwa kichinjioni kwa kutumia minyororo kabla ya kufanywa kupoteza ufahamu. Wakati tabia duni kama hizo zinaonekana hadharani, zinaibua wasiwasi kuwa huenda kuna viwango vingine duni kama hivyo vya ustawi vinavyoendelea kichinichini. Vichinjio vipya vya punda vinaendelea kujengwa na kutumika hasa Afrika Mashariki. Ijapokuwa vituo hivyo vinaonekana kuwa 'vya kisasa', hali za kuwaweka punda kabla ya kuwachinja na kuwahamisha zinaoneka kuwa haziridhishi. Kwa mfano, The Donkey Sanctuary imefahamishwa na maafisa katika kichinjio kinachomilikiwa na Wachina kuwa punda 'huoshwa kwa maji baridi' kabla ya kuchinjwa ili kupunguza kupoteza damu (Mawasiliano ya Kibinafsi ya siri). Taratibu kama hizo zinaweza kusababisha dhiki kwa punda, ijapokuwa inasemekana kuboresha ubora wa ngozi, sababu msingi ya kuzuia kupoteza damu inatiliwa shaka. Kwa ufupi, ustawi kabla na baada ya kuchinja ndio

sehemu muhimu ya wasiwasi katika biashara hii inayoibuka ya ngozi na nyama ya punda. Maeneo maalumu ambayo wasiwasi wa ustawi unaweza kuibuka ni pamoja na:

• Kununua sokoni kutoka kwa mmiliki 'wa kwanza', hasa katika kununua punda wagonjwa au wenye maradhi ambao hawafaii kusafirishwa au ambao mateso yao yanastahili kukatishwa kupitia kifo cha huruma cha moja kwa moja.

• Kuwachanganya na punda wengine wanaoenda kuchinjwa katika vituo duni vyenye uwezekano mkubwa wa vita, majeraha, dhiki na magonjwa.

• Usafiri wa barabarani hadi vichinjio halali au visivyo halali katika magari yaliyoundwa vibaya ambayo yamejaa kupita kiasi, ambayo hayana chakula au maji.

• Mkusanyiko wa punda katika vituo vya kuchinja mara kwa mara bila chakula, maji au maficho.

• Punda wanavyoghulikiwa na wanavyopelekwa kichinjioni kwa njia za kinyama kama vile kwa michokoo na kuwakokota.

• Kuwatoa ufahamu kwa njia isiyofaa au hata kukosa kufanya hivyo kabla ya kuwachinja.

• Uchinjaji usiofaa unaosababisha hofu na uchungu kabla ya kifo.

MATOKEO KWA PUNDA WANAOSALIA NA WAMILIKI WAKEIjapokuwa matokeo ya ustawi wa punda wanaochinjwa kwa ajili ya ngozi na nyama huwa wazi kuona, kuna matokeo mengine zaidi ya ustawi kwa wanyama wanaofanya kazi. Kwa kila punda anayefanya kazi ambaye anauzwa katika biashara ya nyama na ngozi kuna matokeo mabaya kwa wanyama wengine wanaofanya kazi waliowekwa ili 'kujaza pengo'. wakati punda anapotokomea katika jamii, kuna uwezekano kuwa punda waliosalia (au wanyama wengine wanaofanya kazi kama farasi, nyumbu na ngombe) watalazimika kutekeleza kazi ambazo hawafai kufanya (k.m. ni wachanga mno, wajawazito, wazee au wagonjwa). Iwapo hakuna wanyama wengine wa ziada wa kuwatumia, inakuwa kazi ya akina mama na watoto katika jamii nyingi ya kufanya kazi hiyo ya punda. Kuna msemo wa Ethiopia unaosema "Mwanamke bila punda ni punda" unatoa muhtasari wa hali hii.

KUZIDISHA UZALISHAJI WA PUNDAMtindo mwingine unaosababisha wasiwasi zaidi katika ufugaji makini wa punda unaoonekana kukua zaidi, hasa nchini Uchina. Pamoja na majaribio ya kuzidisha ufugaji makini wa punda kuna ripoti za juhudi za kufuga jeni kubwa zaidi za punda, ambazo zina komaa kwa haraka zaidi(3). Mazao ya ukulima yakiendelea kuongezeka, ustawi wa wanyama wanaofugwa chini ya hali hizi huwa hauimariki. Wasiwasi kuhusu ustawi wa punda wanaofugwa kwa makini lazima uchukuliwe kuwa tishio(52) hasa kwa punda hawa wanaodhaminiwa sana kwa sababu ya ngozi zao bila kujali nyama yao.

MASHTAKA YANAYOHUSU USTAWI WA WANYAMAIjapokuwa ripoti zipo zinazohusu mashtaka yaliyofanikiwa dhidi ya kudhulumiwa kwa punda wanaolengwa kusafirishwa nje kwa sababu ya biashara ya ngozi nchini Afrika Kusini(53), kuna chunguzi au mashtaka mengine machache yaliyorekodiwa licha ya ukiukaji wa hali ya juu wa ustawi wa wanyama unaoripotiwa na vyombo vya habari duniani. Kuna viwango vya kutamausha katika ngazi za kimaeneo na kitaifa vya kutozingatia ustawi wa punda na familia na jamii ambazo punda hizo zinasaidia. Hii ni licha ya juhudi zinazoendelezwa na mashirika mengi za kuboresha ufahamu wa wanyama na umuhimu wa ustawi mwema.

26 www.thedonkeysanctuary.org.uk

Soko hili linalokua kwa haraka la punda wa uzalishaji limewafanya watu wengi kunufaika kutokana na mauzo au wizi wa punda. Baadhi ya wamiliki wa punda huenda kwa kweli walifaidika kutokana na soko hili jipya kwa 'bidhaa' zao, lakini kuna wengine wengi ambao huenda hawafahamu madhara mabaya ya muda mrefu ya soko hili kwa bei za punda na uendelezaji wa idadi ya punda.

Kumekuwa na upanuzi mkubwa hadi familia nyingi hazifahamu athari kubwa ya upungufu wa punda kindani, kitaifa na kimataifa. Jamii kutegemea punda kwa riziki kunaweza kusababisha kupoteza uwezo wa uzalishaji riziki kupitia chaguo lao la kuuza punda wao, il hali wengine wanapoteza kipato chao usiku kupitia wizi wa punda, ambapo kulingana na nguvu za soko; ni vigumu kuwanunua tena kwa sababu ya bei kuongezeka.

Utafiti umekadiria thamani halisi ya uchumi kwa mnyama anayefanya kazi kuwa hadi $2,272 kwa mwaka nchini Kenya, na kipato taslimu kikiwa cha wastani wa $330 kwa punda anayefanya kazi nchini Ethiopia(54). Takwimu hizi, zinazotokana na uwezo wa maisha ya kufanya kazi wa miaka 20 kwa punda, zinaonyesha kutolingana kati ya faida yoyote ya muda mfupi katika kuuza mnyama anayefanya kazi, na uwezo wa thamani ya kiuchumi wa mnyama huyo akifanya kazi kwa mwaka mmoja.

Inastahili pia kukumbukwa kuwa thamani ya punda anayefanya kazi haiwezi tu kuangaziwa katika thamani yake ya kifedha; punda huwa na jukumu muhimu katika jamii zao kwa kuwawezesha wanawake, kuwapa watoto uhuru wa kusoma na kukua, na kama mbinu ya jamii masikini kuokoa pesa na hao wenyewe kudhibiti hatari.

Umuhimu wa punda anayefanya kazi hauwezi kupuuzwa. Mchango wao wa thamani katika maisha ya mashambani unaendelea kutambuliwa na mashirika ya kimataifa kama vile UN(1) na OIE(55).

HATARI KWA MAISHA NA MAZINGIRA

ATHARI KWA MAZINGIRAWasiwasi wa kimazingira unaozunguka vichinjio vinavyotumia mashine na vile ambavyo si halali unaendelea kukua katika nchi kadhaa, na visa vya machafuko yanayohusishwa na uchafuzi wa mazingira na vichinjio vikiripotiwa nchini Bukinafaso, Tanzania na Ethiopia. Nchini Tanzania na Bukinafaso kunaonekana kuwa na wasiwasi unaohusiana na uchafuzi wa mazingira(32, 35) badala ya ustawi wa wanyama ambao ulisababisha kufungwa kwa vichinjio vya punda na kuzingatiwa kupigwa marufuku kwa vichinjio vikubwa. Cha ajabu ni malalamiko kama hayo ya umma kuhusu uchafuzi unaowezekana wa mazingira umekuwa suala kuu la kushughulikiwa kabla ya serikali kutoa kibali cha vichinjio vya punda nchini Namibia. Wakazi wa Okohandja wanaombwa kuchangia Utathmini wa Athari kwa Mazingira unaohusiana na kichinjio kinachopendekezwa pamoja na kituo cha uchakataji ambacho kinataka kuhudumia soko la biasharanje hadi Uchina(30).

KUZINGATIWA KWA PUNDA KISHERIAKutoonekana kwa punda kama spishi katika mpangilio wa kisheria wa serikali nyingi unasababisha ukosefu wa uwezo wa kusimamia biashara hii inayoibuka ya uchinjaji. Pamoja na vikwazo hivi vya kitaifa na kimaeneo kuna vikwazo vya wamiliki wenyewe wa punda; kwa kawaida punda humilikiwa na jamii ambazo hazina rasilimali na zilizo katika mazingira magumu ambazo hazina sauti au uwezo wa kuwafikia watoa maamuzi katika ngazi za juu. Ubaguzi kama huo hufanya jamii hizi kuweza kuathirika na maadili mabaya ya biashara, wizi na bei za juu zaidi za soko.

Thamani ya punda anayefanya kazi haiwezi kuangaziwa tu katika thamani yake ya kifedha. Punda wana jukumu muhimu katika jamii zao kwa kuwawezesha wanawake, kuwapa watoto uhuru wa kusoma na kukua, na kama mbinu kwa jamii masikini.

HITIMISHOBidhaa ambayo zamani ilikuwa ya wafalme sasa imekuwa bidhaa ya anasa katika karne ya 21, inatangazwa, kuuzwa na kuwasilishwa katika kiwango cha kimataifa.

Kama matokeo yake, kati ya punda milioni nne na kumi watahitajika kufa kila mwaka ili kutimiza mahitaji ya ejiao – mahitaji ambayo hayawezi kuendelezwa, na kwa wakati huo inasababisha kuteseka kwa punda kwa kiwango kikubwa na kuhatarisha riziki ya mamilioni ya watu wanaowategemea.

Vijiji vya mashambani kuanzia Afrika hadi Amerika Kusini vimeibiwa punda wao, wakachinjwa na kutolewa ngozi usiku - hivyo basi kuwafanya kuwa masikini papo hapo na kubadilisha maisha yao milele.

HITIMISHO NA NJIA YETU YA KUENDELEA MBELE

MAPENDEKEZO• The Donkey Sanctuary inatoa mwito wa

kukomeshwa kwa biashara ya ngozi za punda ili kutengeneza ejiao hadi athari ya biashara hii iweze kutathminiwa na kuonyesha kuwa inawafaa punda na inaweza kuendelezwa kwa jamii ambazo wanawategemea punda.

• Cha muhimu, The Donkey Sanctuary inahimiza nchi zilizoathiriwa na biashara hii kufuata hatua zilizochukuliwa na Bukinafaso na Nijeri na kupiga marufuku uchinjaji na biasharanje ya punda kwa ajili ya ngozi zao.

Mahitaji haya yanayokua yamesababisha kupanda kwa bei ya punda, kwa hivyo kuwafanya wasiweze kumudika kwa familia na jamii ambazo wanawahitaji zaidi. Hatua zilizochukuliwa na nchini kama vile Bukinafaso na Nijeri za kupiga marufuku uchinjaji na biasharanje ya punda zinasisitiza utambuaji wao wa jinsi biashara hii inatishia watu na uchumi wao.

Na biashara hii, kwa njia yake halali au ya haramu, inasababisha matatizo mengi ya ustawi wa punda katika kila hatua, kuanzia ununuzi hadi usafirishaji na mwishowe uchinjaji. Masuala haya hayawezi kupuuzwa – ustawi wa punda na thamani yao ya kweli ya kuunga mkono riziki ya watu iko hatarini.

© H

akim

iliki

Geo

rge

Know

les

Hon

g Ko

ng g

eorg

eekn

owle

s@ya

hoo.

com

• The Donkey Sanctuary inahimiza serikali na tasnia hii kujiunga na sisi katika kuhamasisha umma kuhusu athari ya biashara hii ili wateja wa ejiao waweze kufanya maamuzi ya busara.

• The Donkey Sanctuary inatoa mwito kwa serikali na serikali za mitaa kujiunga na juhudi za kusaidia jamii zilizoathirika, na kuzilinda dhidi ya biashara hii haramu na kuzuia kuangamizwa kwa punda kupitia biashara halali.

30 www.thedonkeysanctuary.org.uk 31The Donkey Sanctuary | Ngozi

1. The Food and Agriculture Organization [Intaneti]. 2016. Inapatikana kutoka: http://www.fao.org/faostat/en/#home

2. Blench R. The history and spread of donkeys in Africa. Donkeys, people and development. 1997;22–30.

3. Knowles G, Gallagher I. Decimation of the donkeys: How 4MILLION animals are slaughtered every year to make Chinese “miracle” youth serum [Internet]. Daily Mail Online. 2016 [cited 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.dailymail.co.uk/news/article-3930644/ Decimation-donkeys-4MILLION-animals-slaughtered-year-make- Chinese-miracle-youth-serum.html

4. Monks K. China banned from buying donkeys [Intaneti]. CNN. 2016 [ilinukuliwa 016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://edition.cnn. com/2016/09/29/africa/china-african-donkeys

5. Gregory NG, Grandin T. Animal Welfare and Meat Production. Grandin T, editor. CABI; 2007. 400 p.

6. Miao Q, Wang X, She L-N, Fan Y-T, Yuan F-Z, Yang J-F, Zhu X-Q, Zou F-C. Seroprevalence of Toxoplasma gondii in horses and donkeys in Yunnan Province, Southwestern China. Parasites & vectors. 2013 Jun 6;6(1):168.

7. Shortage of donkey skin breeds TCM fakes [Intaneti]. China Daily. 2016 [cited 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.chinadaily. com.cn/china/2016-01/28/content_23287841.htm

8. Wenqian Z. Dongeejiao Pharmaceutical to launch donkey food brands [Intaneti]. China Daily. 2015 [cited 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.chinadaily.com.cn/business/2015-12/17/ content_22734077.htm

9. Wang D, Ru W, Xu Y, Zhang J, He X, Fan G, Mao B, Zhou X, Qin Y. Chemical constituents and bioactivities of Colla corii asini. Drug Discoveries & Therapeutics. 2014 Oct 31;8(5):201–7.

10. Wu H, Ren C, Yang F, Qin Y, Zhang Y, Liu J. Extraction and identification of collagen-derived peptides with hematopoietic activity from Colla Corii Asini. Journal of ethnopharmacology. 2016 Apr 22;182:129–36.

11. Wu H, Yang F, Cui S, Qin Y, Liu J, Zhang Y. Hematopoietic effect of fractions from the enzyme-digested colla corii asini on mice with 5-fluorouracil induced anemia. The American journal of Chinese medicine. 2007 Jan 5;35(5):853–66.

12. Li Y, He H, Yang L, Li X, Li D, Luo S. Therapeutic effect of Colla corii asini on improving anemia and hemoglobin compositions in pregnant women with thalassemia. International journal of hematology. 2016 Nov;104(5):559–65.

13. Lv P, Zhao Y, Qi F, Zhou X, You J, Qin Y, Zhang Y. Authentication of Equine DNA from Highly Processed Donkey-Hide Glue (Colla Corii Asini) Using SINE Element. Journal of Food and Drug Analysis. 2011;19(2).

14. Mingrui H. Shanghai traditional medicines making a return [Internet]. ECNS. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.ecns. cn/2016/11-11/233597_2.shtml

15. “Youth serum” from donkey skins found in UK food: Ejiao discovered in dried dates in London shop [Intanetit]. Daily Mail Online. 2016 ] [ilinukuliwa 016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.dailymail. co.uk/news/article-3953644/Youth-serum-donkey-skins-UK-food- Ejiao-discovered-dried-dates-London-shop.html

16. Mullin K. Tech Check: Donkey Gelatin Devices and Westworld-Esque Droids at Beijing’s World Robot Conference [Internet]. The Beijinger. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www. thebeijinger.com/blog/2016/11/01/tech-check-donkey-gelatin- spewing-devices-westworld-esque-droids-and-finding-nimo

MAREJELEO

17. Starkey P, Starkey M. Regional and world trends in donkey populations. Starkey P, Fielding D, editors. Donkeys, People and Development. ATNESA; 2000. 10 – 21 p.

18. Oliveira JV de, Oliveira PV de LF, Melo e Oña CM, Guasti PN, Monteiro GA, Sancler da Silva YFR, Papa P de M, Alvarenga MA, Dell’Aqua Junior JA, Papa FO. Strategies to improve the fertility of fresh and frozen donkey semen. Theriogenology. 2016 Apr 15;85(7):1267–73.

19. Ruixue Z, Hui Y. Donkeys offer new source of wealth [Internet]. China Daily USA. 2015 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http:// usa.chinadaily.com.cn/epaper/2015-05/18/content_20749866.htm

20. Corrowa L. Donkey Business Potential of the donkey industry in the Northern Territory. 2016.

21. African Union opens Chinese-funded HQ in Ethiopia [Intaneti]. BBC News. 2012 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www. bbc.co.uk/news/world-africa-16770932

22. Pigato M, Tang W. China and Africa: Expanding economic ties in an evolving global context. World Bank; 2015.

23. Chege N. Government Approves Sh300 Million Donkey Slaughterhouse [Internet]. Kenyans.co.ke. 2016 [ilinukuliwa 2016

Nov 30]. Inapatikana kutoka: https://www.kenyans.co.ke/news/government-approves-sh300-million-donkey-slaughterhouse

24. Crisis as donkeys killed for skins in Tanzania [Intaneti]. The Donkey Sanctuary. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: https:// www.thedonkeysanctuary.org.uk/communities-face-crisis

25. Botswana govt issues permits for donkey meat export [Internet]. The Chronicle. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.chronicle.co.zw/botswana-govt-issues-permits-for- donkey-meat-export/

26. Malkom S. Kolongo: A slaughterhouse in donkeys opencast [Intaneti]. Mali’s News. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://malisnews.com/en/kolongo-abattoir-danes-a-ciel-ouvert-2/

27. 250 donkeys “found flayed” in Sohag [Internet]. Al-Dostor. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.dostor. org/1142470

28. Donkey leather to be exported to China: official [Internet]. Egypt Independent. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.egyptindependent.com/news/donkey-leather-be- exported-china-official

29. Massacre of Donkeys – latest victims of cruel trade in animal parts [Intaneti]. NSPCA SA. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana

kutoka: http://nspca.co.za/massacre-donkeys-latest-victims-cruel-trade-animal-parts/

30. Heita D. Namibia: Donkey Exports Planned for China [Internet]. allAfrica.com. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://allafrica.com/stories/201610050939.html

31. Pheage T. Govt issues permits for donkey meat export [Internet]. Mmegi Online. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka:

http://www.mmegi.bw/index.php?aid=62949&dir=2016/september/08

32. Welfare team helps to close down donkey abattoir in Tanzania [Intaneti]. The Donkey Sanctuary. [ilinukuliwa 016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: https://www.thedonkeysanctuary.org.uk/blog/donkey- abattoir-closed-down

33. County Government of Nakuru draft finance bill. 2016.

34. Kenya’s Hides, Skins fetch higher export tax [IIntaneti]. Kenya Leather Development Council. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.leathercouncil.go.ke/?p=564

35. Hien R. Where have all the donkeys gone? Burkina Faso’s export dilemma [Intaneti]. Phys.org. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://phys.org/news/2016-07-donkeys-burkina-faso- export-dilemma.html

36. Burkina Faso bans donkey skin exports, affecting Asian trade [Intaneti]. BBC News. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-37035229

37. Olusayo B. Burkina Faso Bans Export of Donkey Meat [Internet]. How Africa News. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://howafrica.com/burkina-faso-bans-export-donkey-meat/

38. Dunlop F. Niger bans the export of donkeys after Asian demand [Intaneti]. BBC News. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-37286811

39. Canacoo EA. Utilisation of donkeys in southern Ghana. Starkey P, Fieilding D, editors. ATNESA; 1994.

40. Public advised not to eat donkey meat [Intaneti]. The Ghanaian Times. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www. ghanaiantimes.com.gh/public-advised-not-to-eat-donkey-meat

41. Namibia: Chinese Businesses Want Namibian Donkeys [Internet]. allAfrica.com. 2014 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://allafrica.com/stories/201411030332.html

42. Yusuf VA, Ibrahim YA, Hamagam AM, Onuchukwu B. Chinese are going gaga for Nigerian donkeys [Intaneti]. Daily Trust. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.dailytrust.com.ng/news/ general/chinese-are-going-gaga-for-nigerian-donkeys/ 130348.html

43. Rana S. Government bans export of donkey meat, hides [Internet]. Tribune. 2015 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://tribune.com.pk/story/950242/government-bans-export- of-donkey-meat-hides/

44. Langenegger J. US to Mexico Weekly Livestock Export Summary [Intaneti]. East Central Iowa Cooperative. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov

30]. Inapatikana kutoka: http://www.ecicoop.com/news/story.php?id=2306423

45. Global Trading Ventures, Medical Implements, Mexico [Internet]. List of companies world wide. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.listofcompaniesin.com/Global_Trading_Ventures_ Company_1010219.html

46. They report slaughter of donkeys in Sucre to steal their skins [Internet]. Primero Noticias. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://primeronoticias.com.co/2016/04/20/denuncian-matanza-de- burros-en-sucre-para-robarse-sus-pieles/

47. Blakeway S. The Multi-dimensional Donkey in Landscapes of Donkey- Human Interaction. Relations. 2014 Jun 16;2(2.1):59–77.

48. Brazilian Northeastern Donkey: From “Best Friend” To Plague [Intaneti]. plus55. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http:// plus55.com/culture/2016/10/brazilian-northeastern-donkey

49. Biswas R, Mendez A. The Long Crisis Facing Emerging Markets : A Roadmap for Policy Reforms. 2016.

50. Tanzania: Transport Permits Banned As Donkey Meat Trade Soars [Intaneti]. allAfrica.com. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://allafrica.com/stories/201611100088.html

51. Ngugi A. Kenya’s first donkey slaughterhouse [Intaneti]. Africanews. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www. africanews.com/2016/11/07/kenya-s-first-donkey-slaughterhouse/

52. Baker M. A new farm animal? [Intaneti]. Write You. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.writeyou.co.uk/a-new-farm-animal

53. Guilty! Four sentenced in donkey horror case [Intaneti]. NSPCA SA. [ilinukuliwa 016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://nspca.co.za/guilty- four-sentenced-donkey-horror-case/

54. Valette D. Invisible Workers: The Economic Contributions of Working Donkeys, Horses and Mules to Livelihoods. 2015.

55. World Organisation for Animal Health (OIE) [Intaneti]. 2016 [ilinukuliwa 016 Nov 30]. Inapatikana kutoka: http://www.oie.int/index. php?id=169&L=0&htmfile=chapitre_aw_working_equids.htm

56. Thefts and smuggling of donkey hides persists in Pakistan [Intaneti]. International Leather Maker. 2016 [ilinukuliwa 2016 Nov 15]. Inapatikana kutoka: http://internationalleathermaker.com/news/fullstory.php/ aid/3416/Thefts_and_smuggling_of_donkey_hides_persists_in_ Pakistan.html

57 Agricultural Ministry mulls exporting 10,000 live donkeys to China [Intaneti}. Egypt Independent. 2016 [cited 2016 Dec 14]. Inapatikana kutoka: http://www.egyptindependent.com/news/agriculture- ministry-mulls-exporting-10000-live-donkeys-china

58 Transport of Animals by Sea [Intaneti]. World Organisation for Animal Health. 2005 [cited 2016 Dec 14]. Inapatikana kutoka: www.oie.int/ index.php?id=169&L=0&htmfile=chapitre_aw_sea_transpt.htm

59 Chinese businessman receives permit to export 4,000 donkeys from Kyrgyzstan to China [Internet] AKIpress. 2016 [ilinukuliwa 2016

Dec 16]. Inapatikana kutoka: http://akipress/news:586463/

60 Losing their asses: China trade deals deplete global donkey population [Intaneti] Animals 24 – 7. 2016 [ilinukuliwa 23 December 2016]. Inapatikana kutoka: http://www.animals24-7.org/2016/12/23/losing- their-asses-china-trade-deals-deplete-global-donkey-population/

61 Les Chinois veulent la peau de l’âne africain [Internet] L’édition du soir. 2016 [ilinukuliwa 20 December 2016]. Inapatikana kutoka: http://www. ouest-france.fr/leditiondusoir/data/894/reader/reader. html#!preferred/1/package/894/pub/895/page/6

62 Kyrgyz concerns about donkey exports to China [Internet] BBC News. 2016 [ilinukuliwa 16 December 2016]. Inapatikana kutoka: http://www. bbc.co.uk/news/blogs-news-from-elsewhere-38347330

63 Contrabando piel burro terroristas ocultar minas [Intaneti]. HispanTV. 2017 [cited 09 January 2017]. Inapatikana kutoka: http://www.hispantv. com/noticias/afganistan/329616/contrabando-piel-burro- terroristas-ocultar-minas

64 The mass slaughter of donkeys in Sogd. For what? [Intaneti] Avesta Information Agency. 2017 [cited 16 January 2017]. Inapatikana kutoka: http://avesta.tj/2017/01/13/massovyj-zaboj-oslov-v-sogde- dlya-chego/

65 From donkeys to dried scorpions [Internet] Al Arabiya. 2017 [ilinukuliwa 25 January 2017] Available from: http://english.alarabiya.net/en/ variety/2017/01/24/From-donkeys-to-dried-scorpions-the-tale- of-Chinese-imports-from-Africa.html

Kiwango cha ubadilishanaji kinachotumiwa kubadilisha fedha ni sahihi hadi Januari 2017

0046

3_16

_DS

THE DONKEY SANCTUARYSlade House Farm, Sidmouth, Devon EX10 0NU, United KingdomSimu [44] (0)1395 578222 Faksi [44] (0)1395 579266Barua pepe enquiries@thedonkeysanctuary.org.ukwww.thedonkeysanctuary.org.ukThe Donkey Sanctuary ilianzishwa na Dkt. Elisabeth Svendsen MBE mwaka wa 1969. The Donkey Sanctuary (nambari ya usajili ya ufadhili 264818) na wathamini wake wa kipekee wa shirika, The Donkey Sanctuary Trustee Limited (Nambari ya kampuni 07328588), waana ofisi yao iliyosajiliwa Slade House Farm, Sidmouth, EX10 0NU, United Kingdom.Wafadhili husika: The Elisabeth Svendsen Trust for Children and Donkeys (EST);The International Donkey Protection Trust (IDPT).