baraza la habari tanzania toleo la julai, 2019 issn sheria ya … · 2019. 11. 21. · sheria ya...

21
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 143, Julai, 2019 ISSN 0856-874X MCT yataka Polisi imwachie Kabendera CoRI yakubali pendekezo la Serikali Mahakama yaamuru kesi ya waandishi isikilizwe upya Uk5 Uk 21 Uk 7 Sheria ya Habari Z’bar yaiva

Upload: others

Post on 06-Mar-2021

4 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 143, Julai, 2019ISSN 0856-874X

MCT yataka Polisi imwachie Kabendera

CoRI yakubali pendekezo la Serikali

Mahakama yaamuru kesi ya waandishi isikilizwe upya

Uk5 Uk 21Uk 7

Sheria ya Habari Z’bar yaiva

Page 2: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Washiriki wa mkutano uliojadili kwa kina suala la kuwa na sheria mpya ya habari Zanzibar uliofanyika Julai 14, katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar.Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Habari Tanzania ofisi ya Zanzibar, Kituo cha Sheria na Chama cha Waandishi Habari Wanawake (TAMWA).

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Magazeti haya yaruhusiweMwanaHALISI, Mseto na Mawio ni

magazeti maarufu yenye wasomaji wake.

Ghafla… serikali imechukua hatua kali ya kuyafungia kwa kipindi kirefu sasa, na hayachapishwi na hayaonekani tena.

Serikali inaelekea imeyasahau kama Waziri mmoja alivyosema katika mahojiaano ya karibuni kwamba hakuna gazeti lililofungiwa akikumbuka tu gazeti la The Citizen lililofungiwa kwa siku saba.

Inealekea magazeti hayo maarufu kwa mtazamo wa watawala hayapo tena!

Yalifungiwa kwa sababu tofauti ikiwa pamoja na dai la uandishi mbaya kwa mtazamo wa dola.

Ukweli kwamba yalienda mahakamani na uamuzi wa serikali wa kuyafungia ulitupiliwa mbali na kuamuru yaendelee kuchapishwa kama kawaida, inaelekea wenye mamlaka wanajifanya hawatambui uamuzi wa mahakama.

Wachapishaji wa magazeti hayo wameona wasikae kimya. Wameamua kuwakumbusha watawala kuhusu kadhia yao ambayo licha ya kuwanyima wasomaji wao fursa ya kusoma magazeti yao pia wafanyakazi wao wanateseka tangu magazeti hayo yalipofungiwa.

Suala la magazeti haya matatu linatoa picha mbaya kwa wenye mamlaka hasa uamuzi wao wa kutotekeleza uamuzi wa mahakama kuwa unawafanya wanapuuza utawala wa sheria jambo ambalo linakinzana na utawala bora.

Awali ya yote, wenye mamlaka watambue kuwa kwa kuendelea kuyafungia magazeti , wanakandamiza uhuru wa kujieleza pamoja na uhuru wa habari.

Uhuru huu ni haki ya msingi ya binadamu na kwa serikali inayojinasibu kuwa na utawala bora, uwazi, uwajibikaji na zaidi ya hapo kuwa ya Kidemokrasia, kufungia magazeti , kudharau uamuzi wa mahakama ni mambo ya kinyume kabisa na usatarabu.

Ni muhimu wenye mamlaka wakabadilika, wakaondoa vikwazo na kuruhusu magazeti haya yachapishwe tena.

Wafanyie marekebisho sheria ya Huduma ya Vyombo vya habari ya 2016 kama ilivyoamriwa na hukumu ya Mahakama ya Afrika Mashariki katika kesi iliyowasilishwa na Baraza la Habari Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu na kuifanya kuwa sheria rafiki.

Tunasisitiza wenye mamlaka wabadilike. Kusimamisha ama kufungia magazeti yawe mambo ya historia.

Page 3: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

3

Habari

Toleo la 143, Julai, 2019

Na Mwandishi wa Barazani

Hatimaye matumaini yamei-buka kuwa sheria mpya ya habari karibu itapitishwa. Muswada wa sheria hiyo

unatarajiwa kufikishwa kwenye Baraza la Wawakilishi Septemba, mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa ushauri uliofanyika karibuni ambao ulihudhuriwa na wadau wa habari, ofisa wa sheria wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mustafa Omar Abdalla, alizungumzia Muswada wa

Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019.

Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele ya kamati ya utendaji ya wizara.

Alisema rasimu hiyo baadaye itawasilishwa mbele ya kamati ya Makatibu wakuu wa Wizara na Mwanasheria Mkuu kwa maboresho kabla ya kufikishwa kwenye Baraza.

‘’Tunatarajia muswada wa Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2019 kuwasilishwa kwenye Baraza la Wawakilishi kupata maoni yao kabla ya kupitishwa”, alifafanua.

Zanzibar inapanga kufuta sheria mbili

, Sheria ya Tume ya Utangazaji Na. 7 ya 1997 na ya Usajili wa Magazeti na Vitabu, Namba 5 ya 1988 kusafisha njia kwa sheria mpya ya Huduma ya Vyombo vya habari ya 2019.

Maelezo hayo ya ofisa mtendaji yanadhihirisha kwamba mchakato wa sheria hiyo mpya unapamba moto huku wadau wakihimiza kushirikishwa zaidi.

Katika mkutano huo wadau walihimiza pia kuwe na uwazi katika mchakato wa kupata sheria mpya isije ikatokea hatimaye kuwa na sheria mbaya. “Maoni ya wadau ni muhimu na ni muhimu yajumuishwe kwenye sheria,” walisiistiza.

Wadau walieleza licha kuwa wamekuwa wakishirikishwa katika hatua mbalimbali, ni muhimu wakashiriki pia kikamilifu hatua hii ya mwisho.

Ofisa Programu wa Baraza la Habari ofisi ya Zanzibar, Shifaa Hassan alisema Baraza limechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kukusanya maoni kutoka kwa wadau kuhakikisha kuwa sheria hiyo mpya inakidhi mahitaji ya wanahabari.

“Kutoka mwaka 2010, Baraza limechukua hatua kadhaa kuhakikisha inapatikana sheria nzuri” alisema.

Maoni yaliyokusanywa yalijumuisha ya taasisi zisizo za kiserikali na pia kuwasilishwa serikalini katika maandalizi ya kuwa na sheria rafiki itakayokuza uhuru wa habari na demokrasia.

Sheria mpya ya habari Zanzibar yatarajiwa Septemba

Wadau wa habari wa Zanzibar wakiwa katika mkutano uliojadili sheria mpya ya habari Visiwani.

Page 4: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Serikali imetakiwa ku-ruhusu kuchapishwa kwa magazeti matatu - MwanaHALISI,

MSETO na MAWIO na kusambazwa kufuatia hu-kumu ya makahama kufuta uamuzi wa serikali kuya-fungia.

Serikali iliyafungia magazeti hayo kwa sababu mbalimbali ikiwa pamoja na ukiukaji wa maadili ya uandishi lakini yakafungua kesi mahakamani na kushinda.

Wachapishaji wa magazeti hayo, Hali Halisi Publishers Ltd. (HHPL), katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Julai 12,

imeitaka serikali kuheshimu maamuzi ya mahakama na kuruhusu MwanaHALISI, MSETO na MAWIO kuendelea na shughuli yao ya kuchapisha na kusambaza magazeti hayo, kunusuru wafanyakazi wao ambao wamepata shida kwa muda mrefu.

Wachapishaji hao waliibuka na taarifa hiyo kutokana na kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Serikali iruhusu kuchapishwa MwanaHALISI, Mseto na Mawio

4

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Endelea Ukurasa wa 6

Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HaliHalisi.

Page 5: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeliomba Jeshi la Polisi kumwachia huru mara moja Mwandishi wa Habari za

Uchunguzi, Erick Kabendera, wanay-emshikilia kuanzia Julai 29, 2019.

Baraza katika tamko lake kuhusu kukamatwa kwa mwandishi huyo lililotolewa Julai 31,2019 na kusainiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga limeeleza kuwa kosa analotuhumiwa mwandishi huyo lina haki kisheria ya kupata dhamana.

Kuhusu suala la uraia wa mwandishi huyo, tamko hilo limeeleza kuwa ni la tangu 2013, ambapo Idara ya Uhamiaji ililishughulikia na kuthibitisha uraia wake.

Kabendera ni mwandishi anayejulikana kitaifa na kimataifa, kuendelea kumshikilia kwa sababu zilizotolewa kunaleta picha isiyo nzuri kwa Tanzania, lakini pia kunaleta hofu kwa waandishi wa habari, wanataaluma na wananchi kwa ujumla. Katika tamko hilo, Baraza limehoji Mwandishi huyo kushikiliwa na polisi badala ya Idara ya Uhamiaji ambayo ndio yenye jukumu la kufuatilia masuala ya uraia.

Baraza limesema kuwa jambo hili linaleta utata, hasa ukitilia maanani kuwa awali polisi ilikana kabla ya kubadili kauli na kukiri kuwa inamshikilia.

“Tunahimiza haja ya kufuatwa kwa sheria za nchi hasa pale raia au mwanataaluma anapokamatwa apewe stahiki zake kisheria kama kupewa dhamana na mwanasheria wa kumsimamia”, tamko hilo limesema.

Baraza limevisihi vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi kwa kushirikiana na vyombo vya habari kwani waandishi wa habari siyo maadui bali ni wadau wakubwa ambao wanaweza kulisaidia jeshi la polisi, katika kutekeleza majukumu yake.

Pia limetoa wito kwa wanahabari na wote wanaojali haki za raia kupaza sauti kupinga ukiukwaji wowote wa haki za raia, sharia na taratibu za nchi.

Kabendera alikamatwa Julai

29,2019 akiwa nyumbani kwake maeneo ya Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Taarifa kutoka kwa familia, majirani na vyombo vya habari zinaeleza kuwa siku ya tukio watu wanaodaiwa kuwa polisi wakiwa wamevalia kiraia walifika nyumbani kwa Kabendera na kumchukua kwa nguvu na wakidaiwa kugoma kuonyesha vitambulisho vyao.

Mwandishi huyo alikamatwa kwa namna inayofanana na mtuhumiwa wa ujambazi au mtu mwingine hatari kwa usalama. Katika tamko lake, Baraza limesisiyiza kuwa moja ya wajibu wa wake ni kusimamia uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari wenyewe wawapo katika majukumu yao ya kazi.

Baraza linao wajibu wa kuhakikisha mwanahabari anafanya kazi zake kwa uhuru na kwa kufuata misingi ya taaluma za uandishi wa habari.

MCT haifurahishwi na utaratibu uliotumika kumkamata Bw.

Kabendera nyumbani kwake, mbele ya wanafamilia wa karibu pamoja na majirani.

Katika Mkutano wake na waandishi wa habari Julai 30, 2019, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Lazaro Mambosasa alikiri kuwa jeshi la polisi linamshikilia mwandishi huyo kwa mahojiano kuhusu uraia wake, ikiwa ni siku ya pili tangu kukamatwa kwa mwandishi huyo. Wakati huo huo taasisi za habari za kimataifa, Kamati ya Kutetea Waandishi(CPJ) na Chombo wahariri na wanahabari waandamizi IPI, vimelaani kukamatwa Kabendera na vimetaka aachiwe mara moja.

Vimesema katika taarifa zao walizotoa kufuatia kukamatwa kwa Kibendera kuwa madai ya serikali hayana msingi na ni muendelezo wa kubinya uhuru wa habari.

Kwa mtazamo wao, Tanzania chini ya uongozi wa Rais Joseph Pombe Magufulu uhuru wa habari unazidi kudidimia.

5

Habari

Toleo la 143, Julai, 2019

MCT yataka Polisi imwachiemara moja Kabendera

Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera.

l CPJ, IPI waunga mkono

Page 6: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Akihojiwa na BBC mjini London, Uingereza , katika matangazo yaliyorushwa Julai 10, 2019, Prof. Kabudi, alikanusha kujua habari za magazeti mengine yoyote ambayo yamefungiwa na serikali isipokuwa gazeti la The Citizen ambalo lilifungiwa kwa siku saba.

Kwa faida ya Waziri Kabudi na umma kwa jumla ambao wanaweza kupotoshwa kutokana na mahojiano ya Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa HHPL, Saed Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chadema, katika taarifa aliyoisaini alisema hadi sasa magazeti ya MSETO lililofungwa 2016 bado liko hivyo, MwanaHALISI na MAWIO ambayo yalisimamishwa mwaka 2017 yako hivyo hadi leo.

Katika mahojiano hayo Waziri pia alisema magazeti yaliyosimamishwa yanaweza kuomba kusikilizwa na waziri.

Kulingana na taarifa ya Kubenea, hii haiwezekani kabisa kwa kuwa Waziri aliyehusika alifunga gazeti bila kutoa nafasi ya kujitetea.

“ Kampuni ya HHPL ilijaribu kupata haki katika mahakama kama inavyotakiwa na Katiba yetu lakini hadi sasa hatujaweza kuchapisha magazeti yetu na kuyasambaza licha ya amri ya mahakama”, taarifa hiyo imeeleza.

Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Serikali iruhusu kuchapishwa MwanaHALISI, Mseto na Mawio

6

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Inatoka Ukurasa wa 4

Page 7: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Umoja wa Kupata Habari (CoRI) umeamua kukub-ali pendekezo la serikali la kuwa na mahusiano ende-

levu ya kikazi kati ya vyombo vya habari na serikali.

Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, , Dr. Harrison Mwakyembe, ilitoa pendekezo hilo

wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Mei 3, 2019.

Barua ya kukubali pendekezo hilo la Serikali itawasilishwa kwa Waziri.

Uamuzi huo wa CoRI ulifanyika katika mkutano wake wa Julai 16, uliofanyika katika chumba cha mikutano cha Baraza la Habari Tanzania (MCT) chini ya Mwenyekiti wake , Kajubi Mukajanga ambaye pia ni Katibu

Mtendaji wa Baraza.Mkutano uliamua kwanza

kukubali pendekezo la Serikali na kuendelea na hatua zingine, kama kuteua timu itakayokuwa katika kamati ya pamoja ya vyombo vya habari na serikali itakayoshughulikia masuala kuhusu vyombo vya habari, baadaye.

Mwenyekiti wa CoRI hata hivyo alisema kuwa kamati kama hiyo kati ya Serikali na Vyombo vya habari iliundwa huko nyuma lakini haikuweza kufanyakazi kutokana na sababu mbalimbali.

Safari hii , Mukajanga alikuwa na matumaini kwamba chini ya utaratibu huu mpya mambo yatakwenda vizuri.

Ushirikiano unaolengwa unatarajiwa kukuza uelewano endelevu kati ya pande hizi mbili.

7

Habari

Toleo la 143, Julai, 2019

CoRI yakubali pendekezo la Serikali

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe

Page 8: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

8

Utaratibu

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

16

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Baraza la Habari Tanzania ni chombo huru kilichoundwa na wadau wa vyombo vya habari kusimamia weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Je! Una malalamiko juu ya habari au makala iliyotoka gazetini au kipindi chochote kilichorushwa hewani na radio au luninga?

Kama una malalamiko, basi wasiliana na mhariri wa gazeti au chombo husika cha habari. Ikiwa hutaridhika na hatua za chombo hicho cha habari, basi peleka malalamiko yako Baraza la Habari Tanzania. Baraza litashughulikia shauri lako haraka kwa misingi ya maridhiano na uungwana.

Jinsi ya kupeleka shauri katika Baraza• Kabla ya kuleta shauri katika Baraza dhidi ya chombo cha habari chochote au

mwandishi wa habari yeyote, mlalamikaji ajiridhishe kuwa juhudi za kuleta maelewano na kupata upatanishi kati yake na walalamikiwa zimeshindikana.

• Mlalamikaji anapaswa kuhakikisha kwamba wakati malalamiko yanaletwa kwenye Baraza habari zinazolalamikiwa hazikuchapishwa au kutangazwa zaidi ya wiki 12 zilizopita.

• Malalamiko yoyote yaletwayo kwenye Baraza sharti yawe katika maandishi na yaonyeshe tarehe, jina la chombo cha habari kilichochapisha au kutangaza habari zinazolalamikiwa. Baraza linaweza kukiamuru chombo cha habari au gazeti kumuomba radhi mlalamikaji na, au kumpa nafasi ya kujibu, au kutoa amri yoyote itakayoona inafaa na ambayo ipo ndani ya mamlaka yake.

• Iwapo mlalamikaji hataridhika na uamuzi wa Baraza anaweza kutafuta njia nyingine za kutatua shauri lake ikiwemo kulipeleka mahakamani. Hata hivyo, hatatumia uamuzi wa Baraza kama ushahidi Mahakamani. Hata hivyo, Mahakama inaweza kulialika Baraza wakati wowote kama “rafiki wa mahakama” (Amicus Curiae’) pale itakapohitaji ushauri wa kitaalamu kuhusu mambo ya habari.

Kwa mawasiliano na Baraza:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzania,Josam House, Kitalu B, Ghorofa ya Kwanza, Upande B, S.L.P 10160, Simu+255 22 2775728/ +255 22 2771947,Nukushi +255 22 2700370, Simu ya Kiganjani +255 732 998310Barua Pepe: [email protected]: mct.or.tz

BARAZA LA HABARI TANZANIA

Page 9: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani,

Maxence Melo Mubyazi mwanzili-shi mwenza na Mkurugenzi wa Jamii Forum amekuwa Mtanza-nia wa kwanza na mwafrika wa

23 kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Habari na Kamati ya Kutetea Waandishi (CPJ) tangu zilipoanzishwa mwaka 1991.

Kwa waendesha mtandao wa Afrika Zone 9 bloggers wa Ethiopia wameingia katika rekodi kama wa kwanza kupata Tuzo za CPJ katika miaka 28 iliyopita.

Akizungumzia kuteuliwa kwake kwa Tuzo hiyo, Melo alisema amefurahi na kufarijika kwa kutambuliwa kimataifa.

Amesema kuwa amepita kipindi kigumu cha uzoefu hasi na wakati mmoja kutokana na msimamo wake wa kulinda vyanzo vya habari alionekana kuwa anatumiwa.

Wachunguzi wanaona kuwa kwa mwelekeo wa mambo nchini Tanzania, kutatokea washindi wengi wa Tuzo za uandishi na za uhuru wa kujieleza.

Kulingana na CPJ, Maxence Melo Mubyazi, ni mtetezi wa uhuru wa kujieleza mtandaoni nchini Tanzania kwa kutoa fursa za majadiliano na kutoa habari katika mtandao wa Jamii Forum.

Melo amefunguliwa mashtaka chini ya sheria ya makosa mtandaoni na mwaka 2017 amefikishwa mahakamani mara 81. Melo na washindi wengine wanne wa Tuzo hizo za CPJ watatunukiwa tuzo zao katika sherehe itakayofanyika kwenye hoteli ya Grand Hyatt New York mjini New York Novemba 21, 2019

Taarifa ya CPJ iliyotolewa Juni 26, 2019 imeeleza Kamati ya Kutetea Waandishi wa habari itawatunza wanahabari kutoka Brazil, India, Nicaragua, na Tanzania Tuzo ya Kimataifa ya

Uhuru wa Habari.

Waandishi hao walikabiliwa na unyanyasaji mtandaoni na kupata vitisho vya kisheria na kimwili na hata kufungwa katika utafutaji wa habari.

CPJ itamtuza Mhariri wa Gazeti la Dawn, Zaffar Abbas, Tuzo ya Uhuru wa Habari ya Gwen Ifill.

Mwanahabari wa Brazil, Patrícia Campos Mello, ambaye pia ni mwanasafu wa gazeti la Folha de S. Paulo, ambaye alishambuliwa mtandaoni wakati wa kampeni za uchaguzi wa Urais nchini humo na wafuasi wa aliyekuwa mgombea urais, Jair Bolsonaro kwa kutuma ujumbe mwingi katika WhatsApp.

Neha Dixit, mwanahabari wa uchunguzi anayeandika habari za haki

za binadamu alikabiliwa na unyanyasaji

mtandaoni baada ya kuripoti matendo

ovu ya makundi ya kizalendo ya kupitiliza na polisi.

Lucía Pineda Ubau, Mkurugenzi wa habari na

Miguel Mora, mwanzilishi

na Mkurugenzi wa Shirila la utangazaji la 100% Noticias. Waandishi hao wawili walifungwa kutokana na kuandika habari za machafuko ya kisiasa. Waliachiwa June 11, baada ya kuwekwa ndani kwa miezi sita chini ya uangalizi mkali na kutengwa wakati wote.

"Washindi wa Tuzo ya CPJ kwa mwaka 2019 wanawakilisha utendaji mzuri katika uandishi wa habari na watu waliohatarisha maisha na uhuru wao kuweza kuandika habari. Wakati tunafurahia ujasiri wao, tunasisitiza kuwa hiyo ndiyo inayotakiwa," amesema Joel Simon, Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ.

"Ukweli mchungu ni kwamba duniani kote uandishi huru wa habari unatishiwa na watawala wapenda sifa ambao hupuuza kazi za vyombo vya habari. Hii ni kweli kabisa kwa nchi wanazotoka wapewa Tuzo wa safari hii na nchi nyingine nyingi”.

Waafrika wengine waliowahi kupewa Tuzo hiyo ya Uhuru wa Habari ya Kimataifa na nchi zao na mwaka kwenye mabano ni kama ifuatavyo: Pius Njawe (1991- Cameroon), Omar Belhouchet (1992- Algeria), Fred Membe (1995-Zambia), Christina Anyanwu (1996 – Nigeria), Gremah Boucar (1997 – Niger), Ruth Simon (1998 – Eritrea), Modeste Mutinga (1999 – D.R. Congo), Geofrey Nyarota (2000-

Zimbabwe), Fesshaya Yohannes (2002 – Eritrea), Aboubakar Jamal ( 2003 – Morocco), Alexius Sinduhije (2004 – Burundi), Beatrice Mtetwa (2004 –Zimbabwe), Madi Cessay (2006 – Gambia) na Andrew Mwenda ( 2008- Uganda).

Wengine ni Naziha Rajiba (Tunisia) , Dewit Kabede (2010 – Ethiopia), Mae Azango (2012 – Liberia), Bassem Yousef (2013- Egypt), Teriel Haffajee (2012 – South Africa), Zone 9 bloggers (2015 –

Ethiopia), Mohamed Abou Ziad (2015 – Egypt), Ahmad

Abba (2016 – Ethiopia) na Amal Habani (2017-

Sudan).

9

Toleo la 143, Julai, 2019

Melo awa Mtanzania wa kwanza kushinda Tuzo ya CPJ

Habari

Maxence Melo Mubyazi

Page 10: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Siku, miezi na sasa mwaka mmoja na miezi sita, haijulikani mahali alipo mwanahabari Azory Gwanda .

Gwanda alitoweka Novemba 21, 2017 katika kituo chake cha kazi Utete Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Juhudi za kushinikiza wenye mamlaka kumtafuta hazijazaa matunda hadi sasa.

Umoja wa Haki ya Kupata Habari (CoRI) umeamua kuongeza muda wa kampeni yake ya kukusanya saini kuhusu mwanahabari huyo aliyetoweka.

Uamuzi wa kuongeza muda huo ulifikiwa katika kikao cha CoRI kilichofanyika Julai 16, 2019 chini ya Mwenyekiti wake , Kajubi Mukajanga.

Wanachama wa CoRi walikubaliana kwa pamoja kuongeza muda kuhakikisha kwamba watu wengi zaidi wanatia saini kampeni hiyo kabla hazijapelekwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Kiongozi wa Mabalozi waliopo hapa nchini.

Waliamua kuhimiza watu zaidi na hasa wadau wa habari na wanahabari kusaini kampeni hiyo.

Mitandao ya habari yenye ushawishi pia itatumiwa kuhakikisha kampeni hiyo inavutia saini nyingi zaidi.

Kampeni hiyo ya CoRI kuhusu Azory Gwanda ina matakwa saba kama ifuatavyo:

• Wizara ya Mambo ya Ndani itangaze wazi kwa umma kwamba Azory Gwanda ametoweka;

• Serikali iviwezeshe vyombo vya usalama kufanya uchunguzi kuhusu kupotea kwa Gwanda kulingana na kanuni za Polisi Na. 232 kuhusu uchunguzi wa watu waliotoweka;

• Vyombo vya usalama, hasa jeshi la polisi, vitoe taarifa za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya uchunguzi;

• Vyombo vya habari vichapishe mara kwa mara taarifa za kupotea kwa Gwanda;

• Wamiliki wa vyombo vya habari kwa pamoja wawe na mkataba wa makubaliano kuhusu wanahabari wanaotoweka ikiwa pamoja na taratibu za kupata taarifa za uchunguzi kutoka kwa mamlaka husika kwa ajili ya kutangaza kwa umma. ;

• Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) itekeleze wajibu wake wa kufuatilia kutoweka kwa Gwanda na vyombo husika;

• Mkuu wa Mabalozi nchini awe tayari kutoa uwezo kwa serikali katika uchunguzi wa kutoweka kwa Gwanda.

Unaweza kuingia kwenye kampeni hiyo kwa kubofya http://bit.ly/AzoryPetition

Wakati huo huo Kamati ya Kimataifa ya Kutetea Wanahabari (CPJ) imeitaka serikali ya Tanzania kutoa maelezo ya kina kuhusu hatma ya mwanahabari Azory Gwanda baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania,, Palamagamba Kabudi, kueleza katika mahojiano kuwa mwanahabari huyo amekufa.

Katika mahojiano ya kipindi cha habari za Afrika cha BBC mjini London, Uingereza Kabudi alisema kwamba Gwanda "ametoweka na

amekufa" katika eneo la mashariki la Rufiji na kwamba serikali imeweza kuzima ghasia za mauaji katika eneo hilo. Kulingana na CPJ, serikali ya Tanzania haijatoa taarifa yoyote kuhusu uchunguzi wa Gwanda tangu alivyotoweka Novemba 21,2017.

"Kwa mwaka na nusu, familia ya Azory Gwanda na vyombo vya habari vya Tanzania vimehimiza serikali kufafanua nini kilichomsibu mpendwa wao," amesema Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Robert Mahoney kutoka New York.

"Ghafla anaibuka Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na kusema kama kupita tu mwanahabari yule amekufa.Hii haitoshi na inakera zaidi. Serikai ni muhimu itoe taarifa ilizo nazo kwa umma kuhusu kilichomsibu Gwanda. ."

Waziri amekanusha maelezo hayo kuhusu Gwanda na kudai kuwa ametafsiriwa vibaya.

10

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

CoRI yaongeza muda wa kampeni ya Azory Gwanda

Azory Gwanda.

Page 11: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Na Mwandishi wa Barazani

Kwa Azam Media na wanahabari nchini kwa jumla, Jumatatu Julai 8, 2019 ilikuwa siku ya

huzuni na simanzi kubwa.

Ilikuwa siku ambayo ajali mbaya ya barabarani ilipokatisha

maisha ya wanahabari vijana watano wa kampuni hiyo ambao walikuwa wametumwa kikazi kwenda Burigi Chato, katika wilaya ya nyumbani ya Rais John Pombe Magufuli kuandika habari za uzinduzi wa Hifadhi ya

wanyama ya Bugiri.

Waliofariki katika ajali hiyo wakati gari lao lilipogongana na lori katika eneo la mbali kuelekea Igunga ni Charles Wandi, Saidi Haji, Salim Mhando, Florence Ndibalema na Sylvanus Kasongo.

11

Habari

Toleo la 143, Julai, 2019

Huzuni, majonzi yatanda Azam kufuatia kufariki wafanyakazi watano katika ajali

Caption

Endelea Ukurasa wa 12

Page 12: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

12

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Habari

Salim Mhando wa Azam TV ( kulia ) akipokea Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2018 katika kundi la Utalii na Uhifadhi kutoka kwa Dk. Severin Kalongo,mwakilishi wa Mwakilishi Mkazi waMfuko wa Wanyamapori Duniani (WWF). Salim alifariki katika ajali hiyo na wafanyakazi wenzake wanne wa Azam Media.

Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwemo mawaziri, viongozi wa siasa, wawakilishi wa vyombo vya habari na wanahabari walifurika katika kampuni ya Azam Media kutoa heshima za mwisho kwa wanahabari hao waliofariki.

Simanzi kubwa ilitanda, ndugu za waliofariki, wafanyakazi wenzao na marafiki baadhi yao wakishindwa kujizuia kuangua kilio wakati miili ya wapiga picha Said Haji na Charles Wandwi , mchanganyapicha Salim Mhando, mtaalamu wa sauti Florence Ndibalema na mhandisi Sylvanus Kasongo ilipofikishwa kwenye makao ya kampuni hiyo Barabara ya Mandela.

Hayati Mhando alikuwa

mshindi wa mwaka huu wa Tuzo za Umahiri ya Uandishi wa Habari (EJAT) katika kundi la Utalii na Uhifadhi. Alikabidhiwa Tuzo hiyo katika kilele cha EJAT Juni 29, 2019.

Wafanyakazi hao watano pamoja na wengine watatu walikuwa wakienda Chato, ambapo Rais John Pombe Magufuli alipangiwa kuzindua hifadhi ya Bugiri Julai 9, 2019. Waliojeruhiwa ni pamoja na mpiga picha Said Mwinshehe na mhandisi Artus Masawe – ambao taarifa zinasema hali zao zinaendelea vizuri hospitalini.

Wawakilishi wa taasisi za vyombo vya habari – Baraza la Habari Tanzania, Jukwaa la Wahariri Tanzania, Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania na Chama cha wamiliki wa Vyombo

vya habari walitoa salamu za rambirambi kwa Azam Media kufuatia vifo vya wafanyakazi hao watano.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliyetumia fursa hiyo kutoa onyo kwa watu wanaopiga picha za wahanga wa ajali wakiwa katika hali mbaya na kuzituma mitandaoni.

Alisema si sahihi kwa wahanga hao na kuwa picha hizo ni mbaya. Aliwauliza wanaopiga picha kama hizo na kuzituma katika mitandao ya kijamii kujiuliza watajisikiaje kama picha kama hizo za jamaa zao zikitumwa kwenye mitandao?

Alisema anatoa onyo la mwisho na kwamba kuanzia sasa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.

Huzuni, majonzi yatanda AzamInatoka Ukurasa wa 11

Page 13: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Tumbi Kiganja

Ubora wa kazi zilizowasilishwa kuwania Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2018

uliwapa wakati mgumu majaji waliokuwa katika mchakato wa kupata washindi. Hii imetokana na mwamko mkubwa wa baadhi ya waandishi wa habari waliowasilisha kazi zao kwa lengo la kushindanisha.

Jumla ya majaji saba wakiongozwa

na Kiondo Mshana, Mhariri Mtendaji kutoka Uhuru Media Group (UMG), walikutana Bagamoyo kupitia kazi za Waandishi wa habari walizoleta kuzishindanisha katika mashindano ya umahiri wa uandishi wa habari kwa mwaka 2018.

Majaji wengine ni Dk. Joyce Bazira, mtaalamu wa masuala ya mawasiliano na pia mhariri wa muda mrefu, Aisha Dachi Mkurugenzi wa redio kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Hassan Mhelela mhariri wa vipindi vya mtandaoni-Azam, James Gayo Mkurugenzi wa kampuni ya GABA AFRICA, Pudenciana Temba-Mhariri magazeti ya Serikali (TSN) na Selemani Mpochi - Mhariri wa picha kampuni ya magazeti ya The Guardian Limited.

Jumla ya kazi 644 ziliwasilishwa katika mashindano ya EJAT mwaka 2018 na kufanya majaji kutumia muda mwingi zaidi na umakini wa hali ya juu kuzisoma, kuchambua, kuziangalia na hata kuzisikiliza na baadhi ya nyakati kutofautiana lakini

13

Toleo la 143, Julai, 2019

Habari

Majaji EJAT 2018 walivyokabiliwa na ugumu kuamua wateule, washindi

Majaji wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2018, wakipitia kazi mbalimbali zilizowasilishwa kuwania Tuzo hizo.

Endelea Ukurasa wa 18

Page 14: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

14

Maoni

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Musiba mchafuzi ama mwanaharakati?

Na Gervas Moshiro

Ni muda mrefu umepita sasa tangu nimsikie mtu aitwaye Cyprian Musiba akitema sumu kwa watu

anaowatuhumu kuwa ni wapinga utawala. Musiba amekuwa mashuhuri au mchafuzi, kutegemea ni upande gani upo na anajiita kuwa yeye ni raia huru, mzalendo na mwa-naharakati. Anajiita kuwa yeye ni mwandishi wa habari (japo kengeuki ) na anamiliki gazeti la Tanzanite na runinga ya mtandaoni.

Mambo yalifikia kilele mwanzoni mwa Julai wakati makatibu wakuu wastaafu wa CCM walipomwandikia barua mkuu wa nchi wakimlalamikia kuhusu Musiba. Barua au hati ya malalamiko hayo ilisambazwa pia kwenye vyombo vya habari.

Mrejesho wa barua hiyo umekuwa wa haraka na ghadhabu, sio kutoka kwa aliyeandikiwa, bali kutoka kwa Musiba akiungwa mkono na wengine wanaolaani barua hiyo, wakiwemo wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya, maafisa wa serikali na wanaojiita makada wa chama. Runinga za mtandaoni zimekuwa ndio makimbilio yao wakijisikia kuwa huru kusema lolote ili mradi linakandamiza mahasimu wao.

Katika kutupiana lawama, imekuwa pia ni fursa ya kubainisha wananchi ambao walikuwa wanangojelewa waangamizwe, ikibidi kama baadhi yao wanavyoapa, watawapoteza. Hii ni hatari kwani baadhi ya vyombo vya mtandao vimeanza kuwa wenzi katika kusambaza propaganda za kihasimu kana kwamba ni jambo jema.

Linalonichukiza zaidi ni kuona chombo cha habari, kilichopewa leseni na serikali, kikitumiwa

kuchochea uhasama baina ya watu, jambo ambalo ni kinyume kabisa na dhima ya vyombo hivyo na huku mamlaka za udhibiti zikikaa kimya.

Kwa ghafla, neno clip (vipande vya sauti, video au maelezo mafupi mafupi ya mtawanyiko) limekuwa sawa na kontena la maajabu lenye soga za wahaini wenye njama za kuiangusha serikali. Wanaharakati hao, licha ya kufichua maovu ya zamani ya mahasimu wao, wanajaribu pia kuwahusisha na vyama vya upinzani na kujenga taswira ya kuwafanya waonekana ni wapenda madaraka wanaotaka

kuleta vurugu nchini. Hivi karibuni kuna mtu alinipigia

simu kuniuliza kama nimeona clip inayotajwa sana mtandaoni ya Bernard Membe au Nape Mnauye au Zito Kabwe au January Makamba au Abdulrahman Kinana. Baadhi ya clip hizo ni mazungumzo binafsi baina ya watu wawili ambao bila shaka hawakujua walikuwa wanarekediwa. Katika nyingine ni hao wanaojiita wanaharakati wakizungumza na waandishi wa habari na sikuona la ajabu la kuzihusisha na njama yoyote dhidi ya Jamhuri.

l Chombo cha habari kutumiwa kukuza uhasama ni kinyume kabisa na dhima ya vyombo hivyolInashangaza mamlaka za udhibiti kukaa kimya

Endelea Ukurasa wa 16

Cyprian Musiba

Page 15: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

15

Habari

Toleo la 143, Julai, 2019

Na Mwandishi wa Barazani

Kikao cha karibuni cha Umoja wa Haki ya Kupata Habari (CoRI) kiligubikwa na hali ya kukatisha tamaa baada ya ku-

fahamika kuwa ripoti kuhusu utafiti mbalimbali ambao haujachapishwa haijatayarishwa.

Mwenyekiti wa CoRI , Kajubi Mukajanga, alihimiza timu iliyopewa jukumu hilo kuharakisha kukamilisha kazi hiyo kwa kuwa baadhi ya utafiti utakuwa umepitwa na wakati kabla haujachapishwa.

Chini ya Sheria ya Takwimu, utafiti hauwezi kuchapishwa mpaka upatiwe ruhusa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Karibu wanachama wengi wa CoRI wana utafiti ambao haujachapishwa kwa miaka kadhaa ukisubiri ruhusa.

Mukajanga alitolea mfano wa

Utafiti wa Ufuatiliaji wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOM) uliofanywa na Waandishi Wasio na Mipaka kutoka Ujerumani kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania.

Ingawa ripoti ya utafiti huo ilizinduliwa Novemba mwaka jana, utafiti kamili haujatolewa kwa sababu takwimu zake zinasubiri kupitishwa na NBS.

Alisema wakati utafiti huo utakapopata ridhaa ya NBS baadhi ya taarifa zake zitakuwa zimepitwa na wakati akitolea mfano wa mmiliko wa vyombo vya habari Reginald Mengi ambaye amefariki baada ya kufanyika utafiti huo. .

“Hii nchi inafungwa na kufungwa… tuatfika mahala kabla hujao, utatakiwa kuwa na kibali”, Mukajanga alisema.

Katika kikao hicho cha CoRI kilichofanyika Julai 16 baada ya Bunge kufanya marekebisho baadhi ya

vipengele vya sheria ya Takwimu, baadhi ya wajumbe walisema bado kuna chjangamoto kwa kuwa mambo mapya yanaibuliwa kuhusu kuchapisha kwa tafiti.

Baadhi walisema baadhi ya vyombo vya kisekta huhoji kama baadhi ya tafiti zina tija licha ya kuondolewa vikwazo vya kisheria.

Wajumbe wengine walipinga umuhimu wa kuhitajika vibali kabla ya kufanya tafiti.

Ingawa hili ni hitaji la kisheria, baadhi ya wajumbe walisema kuwa “linafanyika kisiasa”.

Mukajanga alihimiza waliopewa jukumu la kuandaa ripoti kuhusu tafiti zinazohitaji vibali na changamoto zinazokabiliwa na taasisi mbalaimbali wanachama wa CoRI kulingana na Sheria ya Takwimu kuharakisha utayarishaji huo ili ripoti iwasilishwe kwenye vyombo mbalimbali vilikusudiwa kupelekewa kama Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na vyombo vingine kama Benki ya Dunia, IMF na Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja Mataifa.

Twaweza – mwanacha wa CoRI ambayo kimsingi ni chombo cha utafiti ina tafiti zaidi ya 14 ambazo bado hazipitishwa na NBS.

CoRI inaundwa na Baraza la Habari Tanzania, Sikika, Twaweza, Chama cha Wanasheria Tanganyika Law , Jamii Forum, Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Jukwaa la Wahariri(TEF), Policy Forum,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika- kwa Tanzania ( MISA-Tan).

Wajumbe wa Umoja wa Haki ya Kupata Habari (CoRI) wakiwa katika kikao hivi karibuni.

CoRI kuharakisha kuandaa Ripoti kuhusu tafiti zisizochapishwa

Page 16: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

16

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Maoni

Katika kutazama clip hizo zilizozagaa kwenye runinga nyingi za mtandao, ndipo nilipogundua kuwa kuna jambo baya sana linalohitaji kushughulikiwa mapema na vyombo vya habari pamoja na vya udhibiti wa mawasiliano. Ninahofia kuwazia matokeo yake ikiwa halitashughulikiwa.

Kwa kutumia vigezo vya chombo cha habari, ninachoona kwenye runinga za mtandaoni kuhusiana na matokeo ya waraka ule wa Makamba na Kinana ni kwamba kuna hitilafu nyingi, kubwa ikiwa ni kupuuzwa kwa sheria. Kuhusu haki za habari, katiba ya nchi iko wazi kabisa. Katika Kifungu cha 16(1) haki ya faragha ya mawasiliano ya mtu imehakikishwa.

Kanuni za Sheria ya Posta na Mawasiliano Mtandaoni – EPOCA ya mwaka 2018 kifungu cha 16 kinataka mtangazaji kupata ruhusa ya mhusika kabla ya kutoa taarifa binafsi hadharani. Kwa mujibu wa kanuni hizo, ni wajibu wa mtoa huduma za mawasiliano ya kielektroni kulinda usiri wa taarifa binafsi.

Ndani ya katiba ya nchi Kifungu 18, mwananchi ana haki ya kufanya mawasiliano na mtu yeyote na mahali popote bila ya mawasiliano hayo kuingiliwa na yeyote.

Mawasiliano binafsi pia yanalindwa na kanuni za sheria ya EPOCA kifungu 6(1) kinachokataza mtu yeyote kuingilia mawasiliano ya mwingine mahali popote katika Jamhuri ya Muungano.

Kuingilia mawasiliano baina ya watu kunaruhusiwa tu pale sheria inapoagiza. Katika kusikiliza clip zile za maongezi baina yao sikuona uhalali wowote wa kuyaingilia kisheria, licha ya kuwa hayana uhusiano na maslahi ya wananchi kwani mazungumzo hayo ni ya kawaida katika jamii, na hasa pale ambapo watu wanaogopa kuyasema hadharani.

Ndani ya tasnia ya habari, sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016 imeweka bayana kuhusu mambo ya faragha na ukweli. Sehemu ya 7, Kifungu 47(1)(a)(ii) kinakataza uchapishaji wa taarifa za uongo zinazochafua heshima, haki na uhuru wa wengine, na ni kosa kuweka hadharani taarifa zao, kitu

ambacho hakipo katika nyingi ya clip nilizoona. Ni muhimu vile vile kufahamu kuwa wenye leseni za utangazaji mtandaoni, chini ya sheria ya EPOCA, kanuni za Maudhui Mtandaoni, GN. No.133, 8(b) wanatakiwa kuzingatia uandishi wa habari na uweledi.

Kanuni za maudhui za utangazaji wa redio na runinga za sheria ya EPOCA pia zinakataza mambo yahusuyo faragha au yanayoondoa faragha za wengine. Hata kwa viongozi wa umma, la maana ni kuhakikisha kuna ushahidi wa kweli na kwamba taarifa hizo ni kwa maslahi mapana ya nchi.

Maudhui ya habari mtandaoni yanatakiwa, kwa mujibu wa sheria, kutokuwa ya maudhi, tishio la kuumiza, ovu, kuchochea au kuhamasisha chuki au maangamizi ya kimbari dhidi ya kikundi cha jamii kinachofahamika.

Sheria zote zinazotawala vyombo vya habari ikiwemo katiba ya nchi, sheria ya huduma ya vyombo vya habari, sheria ya mamlaka ya mawasiliano TCRA na sheria ya mawasiliano ya kielektroni na posta – zote zinataka uzingatiaji wa taaluma na zinajali jinsi taarifa binafsi zinavyotakiwa kutunzwa. Clip hizo zinaonesha kupuuza matakwa hayo.

Kigezo namba mbili nilichotumia katika kutathmini clip hizo, ni kuona kama zinazingatia maadili ya jamii na ya taaluma. Katika Kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari zilizotolewa kwa niaba ya tasnia na Baraza la Habari, ukweli, uhakika/usahihi na faragha ni kanuni muhimu zinazoongoza maudhui ya chombo cha habari. Bila kujali kisingizio cha aina yoyote, ni muhimu kuelewa mipaka iliyopo kati ya maisha binafsi na ya umma, na hapa ndipo penye kutoelewana na mvutano mwingi. Kuna kesi mahakamani kuhusiana na sakata hili la Musiba na viongozi wa nchi na huenda Mahakama ikasaidia kufafanua vizuri dhana hizi.

Kinachonistaajabisha zaidi ni ushujaa walio nao watengenezaji wa clip ambao yaonekana kutofahamu maana ya utangazaji. Kuonesha na kuchapisha matukio ya siku pamoja na maoni kuhusu taarifa hizo ni uandishi wa habari bila kujali chombo kinachotumiwa. Uandishi wa

habari una kanuni na taratibu zake na kubwa kuliko yote ni ukweli.

Katika moja ya clip, mtu anayehutubia waandishi aliulizwa kuthibitisha aliyokuwa anasema, na jibu lake likawa ni kwamba hawezi kutaja ukweli kwani utaangamiza watuhumiwa. Mwandishi wa kweli angedai athibitishiwe, la sivyo apate pia upande unaotuhumiwa kabla ya kuchapisha taarifa hiyo.

Mamlaka za udhibiti zimekuwa kimya kwa sababu wanazozijua, lakini kinachostaajabisha ni huku kutoa leseni kwa mtu ili akachapishe vipande vya picha, sauti na taarifa na kuziita utangazaji – Tv au redio mtandaoni. Vipande hivi wanavyoitwa clip hutokea mara moja moja na vingine havina viwango vya taarifa ya umma, vikihatarisha utulivu wa nchi.

Vyombo ya habari mtandaoni pamoja na mitandao ya kijamii vinaanza kupendwa sana kwani inakuwa rahisi kufunua vitendo vya ufisadi bila hofu ya kujulikana mara moja na kuwezesha uchangiaji wa hoja papo kwa hapo. Hata hivyo sifa hii haina maana kama hakuna uwajibikaji kwa jamii.

Linakuwa jambo la kichekesho kuwa na mifumo miwili ya mawasiliano inayodhibitiwa tofauti, moja kwa mkono mzito wa sheria (ukali na ukatili) na mwingine kwa wepesi wa kubembelezwa. Kama nilichoona kwenye runinga za mtandao kingeoneshwa kwenye runinga za kawaida, mfano TBC au ITV, ungekuta zimekwisha fungiwa. Chombo cha mawasiliano hakitakiwi kutendewa tofauti na kingine inapokuwa maudhui yake yanafanana. Sheria, kanuni au utawala unaobagua bila ruhusa maalum, unafanya jambo hilo kuwa batili kama kinavyotamka Kifungu cha 13 cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bila kujali kisingizio cha aina yoyote, hakuna nafasi kwenye chombo cha habari ya kutukana, kutisha na kukashifu wengine kwa sababu huu ndio mwanzo wa chuki na usipodhibitiwa vizuri huwa mgogoro wa kijamii unaoweza kuhatarisha usalama. Kuna haja ya huduma ya vyombo vya habari mtandaoni kutii sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza taaluma hiyo, la sivyo tutaishi kujuta.

Musiba mchafuzi ama mwanaharakati?Inatoka Ukurasa wa 14

Page 17: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

17

Uchambuzi

Toleo la 143, Julai, 2019

Na Gervas Moshiro

Mjadala mkali unaende-lea baina ya wahariri waandamizi kufuatia viashirio vya upungufu

wa wajibu wa dhima ya tasnia ya habari kwa wananchi, ambao ndio wanaohalalisha kuwepo kwake na pia kwa wamiliki ambao wali-wekeza kwa matarajio ya kunu-faika.

Sababu nyingi zinatajwa – usimamizi na menejimenti dhaifu, kushindwa kuzingatia kwa wakati mabadiliko ya sayansi na teknolojia, kupungua uweledi, mgongano wa malengo, hofu na vitisho, sheria kandamizi, hujuma, umiliki wa serikali na nyinginezo. Kwa vyovyote ukweli utajulikana kama utafiti utafanywa kama yalivyo maoni yaliyotolewa kwenye ripoti ya hali ya vyombo vya habari - 2017/2018 State of the Media report.

Licha ya maoni hayo, kwa sasa tunaweza kutoa mawazo kutegemea na hali tunavyoiona, kuisikia na kuiwazia. Mtazamo ufuatao ni mchango wangu wa maoni kwenye malumbano hayo ya kama vyumba vya habari vinadidimia au la.

Hali kwenye vyumba vya habari sio shwari tena, inavyosemwa. Uchunguzi na utafiti uliofanywa na wanataaluma na matokeo yake kuchapishwa kwenye gazeti hili katika matoleo matatu yaliyotangulia, yanaashiria hali mbaya: baadhi ya vyombo vya habari vinakwepa wajibu wake wa kuchunguza mwenendo wa jamii – ambao ndio unaohalalisha uwepo wake kwenye mfumo mkuu wa taasisi za jamii. Uandishi wa uchunguzi – uliokuwa fahari ya taaluma, umetoweka. Maudhui ya ‘kitoto’ na rahisi yamekuwa ndiyo kawaida. Malipo ya ujira yaliyokuwa yanatolewa kwa wakati kila mwezi sasa ni nadra, wengine wakisubiri hadi miezi mitatu kabla ya kulipwa.

Mwandishi veterani Attilio Tagalile kwenye chapisho la Barazani mwezi wa Mei,

ameorodhesha upungufu mwingi wa kitaaluma unaoangusha tasnia mbele ya umma. Kwa jumla, kama walivyobainisha watafiti Christoph Spurk kutoka Uswisi na Abdallah Katunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye chapisho la 2018 Media Yearbook, uandishi wa habari unasikitisha.

Wala uandishi wa habari haujawa wa faraja kwani dalili za hofu zimejitokeza kufuatia matukio ya vitisho, unyanyasaji, mateso na kupoteza maisha. Hakuna uongozi wa serikali unaoonesha kusikitishwa, huku wakionekana kufurahia madhila yanayowasibu wanahabari. Wengine katika mikoa na wilaya wangefarijika kuona wanahabari wanaswekwa jela kuwa chakula cha mbu. Wangependa wanahabari wasiwepo kwani kwao “kutokutangazwa habari zao ni habari njema”. Tafsiri ya dhamiri yao ni kwamba kuna maovu wanayotenda na wasingependa yajulikane kwa wananchi wala viongozi wa juu.

Kufanya kazi kwenye mazingira ambayo viongozi wana shaka na waandishi na hawavumilii kukosolewa au kuwekwa hadharani vitendo vyao vibaya, hufanya maisha kitaaluma kuwa magumu na ni changamoto kubwa. Jinsi vyumba vya habari vinavyokabili changamoto hizi ndiko kunakotofautisha ufanisi au kushindwa kwa vyumba hivyo. Washindi ni wale wanaoweza kugeuza changamoto hizo kuwa ni fursa.

Ripoti ya hali ya vyombo vya habari kwa mwaka 2017/18 (State of Media Report 2017/18 ) iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) mwezi Aprili inaonesha mazingira magumu na ya kukatisha tamaa ambayo vyombo vya habari vinafanyia kazi lakini hata hivyo kukiwa na tumaini kuwa njia zitapatikana za kuyakwepa. Ripoti hizo zipo kwenye tovuti ya Baraza la Habari Tanzania.

Kwa ajili hiyo, ni dhahiri vyumba vya habari vina dhiki.

Matokeo yake ni mashaka makubwa - wengine wakipoteza wanataaluma wao mahiri waliochepukia kwenye vyombo vinavyolipa vizuri zaidi, wakati wengine wakiwa wameachana na sekta kujiunga wanakodhani kuna usalama wa maisha zaidi.

Nini kilichoharibika, waweza kuuliza. Ni bahati mbaya kuwa Rais John Magufuli alipokutana na wafanyabiashara kutoka wilaya za Tanzania bara Juni 7, 2019 hakuna aliyezungumzia masuala ya utendaji wa tasnia ya habari, japo mengi yaliyosemwa ya tasnia nyingine, pia yanahusu habari.

Rais angeelezwa kuwa vyombo vya habari vinakufa kwa sababu ya kukandamizwa na vyombo vya dola na utawala kwa kuvinyima uwezo wa kujiendesha, hasa matangazo na ufadhili wa taasisi za umma. Wangemtanabahisha mbinu mpya ya kupoteza kazi kwa kufungia vyombo vya habari, hasa magazeti ambayo matokeo ni serikali kupoteza mapato. Angearifiwa jinsi waandishi wa habari wanavyowindwa na kutimuliwa kutoka matukio ya habari. Rais angesikia kuhusu sheria dhalimu zinavyowapa nguvu wizara kufanya kazi ya mahakama. Hayo ni malalamiko machache, yako mengi.

Kwa robo karne tuliyokuwa na vyombo huru na anuwai vya habari, hapajawahi kuwepo waziri ambaye katika utumishi wake hakufungia vyombo vya habari. Imekuwa ni kama tambiko : huwezi kujidai kuwa umekuwa waziri wa habari kama hakuna gazeti lililofungiwa wakati wa utawala wako.

Pengine ni kipimo cha uwaziri! Nadra kusikia hospitali, shule, barabara, bandari na nyingine zimefungwa, kisa mtumishi wake katenda kazi ya kutowapendeza wakubwa zake kwenye utawala wa nchi, lakini kwenye habari haya hutokea!

Katika habari nchi hii, stori ndogo inayogusa ubinafsi wa kiongozi, hugeuka na kufanya mamia ya watu kukosa kazi na serikali kupoteza kipato. Hadi hii

Udhoofikaji vyumba vya habari

Endelea Ukurasa wa 19

Page 18: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

18

Washindi wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2018 wakiwa katika picha ya pamoja.

yote kwa lengo la kuhakikisha wanatenda haki na kupata washindi.

Kwa kawaida mchakato mzima huanza mara baada tu ya uzinduzi na kisha waandishi kuanza kuwasilisha kazi zao Barazani. Wafanyakazi wa MCT huanza kwa kuzipanga kazi katika makundi, kuzirudufu na kuziingiza katika mafaili tayari kwa ajili ya majaji kufanyia kazi.

Wakati wa uchambuzi wa kazi hizi, majaji huzisoma kazi za magazeti katika kundi fulani kisha kuanza kusikiliza kazi za redio na mwisho runinga, japo awali majaji walivutana juu ya mtindo upi wautumie lakini walikubaliana ni vema kuanza kundi moja hatua kwa hatua.

Washiriki wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuleta kazi zenye ubora hasa katika magazeti na baadhi kutoka katika runinga na redio.

Majaji walionyesha umahiri wao wa kujua vitu kutokana na uzoefu wao wa kufanya kazi kwa muda mrefu katika tasnia ya habari na wengi wao wakiwa katika nafasi za uhariri au ukurugenzi wa taasisi mbalimbali za

habari.Maamuzi waliyokuwa wakiyafanya

yalizingatia vigezo vyote vilivyowekwa na kamati ya maandalizi ya Tuzo za Ejat. Baadhi ya vigezo hivyo ni idadi ya wahusika waliotumika katika habari, utafiti uliofanywa na mwandishi husika kuhusiana na mada yake, athari ya habari au makala husika kwa jamii na pia ni jinsi gani mwandishi alivyoweza kutumia kalamu au ufundi wa kuelezea ili kuwavuta wasikilizaji/watazamaji au wasomaji.

Aidha, panapo jambo zuri basi na kasoro huwa hazikosekani. Baadhi ya kazi zilizowasilishwa zilikuwa chini ya kiwango. Mfano baadhi ya waandishi walikuwa na mawazo mazuri lakini walikosa vyanzo vya kutosha kuweza kuwathibitishia juu ya mada wanayoichunguza hivyo kujikuta wakiweka zaidi mawazo yao binafsi kitu ambacho si sahihi katika habari.

Pia, baadhi ya waandishi walishindwa kuzichakata na kuzitumia vizuri takwimu walizokuwa nazo na kujikuta wakiwa wamezirundika bila mpangilio na

kutoleta maana iliyokusudiwa.Kwa upande mwingine, kuna

habari ambazo zililetwa katika mashindano lakini hazikuwa na mwelekeo kabisa.

Mwandishi hakuweza kujikita katika mada husika hivyo hazikupewa nafasi maana hata msomaji asingeweza kuelewa mwelekeo wa mwandishi.

Tatizo jingine kubwa lililoonekana ni ukiukwaji wa maadili ya uandishi. Baadhi ya habari au makala za magazeti zilichapishwa zikiwa na vichwa vya habari vyenye kubeba tuhuma na hukumu, kuchukua upande mmoja kati ya zile zinazopingana.

Baadhi ya waandishi pia walisahau wajibu wao kama wanahabari na kujivika uanaharakati.

Zoezi la uchakataji wa kazi za waandishi wa habari lilifanyika Bagamoyo tarehe 13 – 19 Juni mwaka huu. Jumla wateule 83 walipatikana na kutunukiwa vyeti, zawadi na tuzo katika kilele cha EJAT ya kumi kilichofanyika Juni 29 katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Majaji EJAT 2018 walivyokabiliwa na ugumu kuamua wateule, washindiInatoka Ukurasa wa 13

Page 19: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

Uchambuzi

Toleo la 143, Julai, 2019

19

leo, kuna magazeti yamefungiwa ambayo yalinyimwa haki ya kupelekwa mahakamani, na hata baada ya kustaki serikali na kushinda, bado yamekataliwa kufunguliwa, mfano hai ni magazeti ya MwanaHALISI na Mawio. Sheria zinampa waziri uwezo wa kuhukumu bila kupitia mchakato wa mahakamani.

Kwa upande mwingine, inapohusu masuala ya falsafa na maendeleo ya miundombinu yanayogusa uadilifu wa chumba cha habari, sababu nyingine zinahusika kudhoofisha tasnia, hivyo kupunguza manufaa yake.

La kwanza kuchunguza ni kama vyombo vya habari vimejikita kwenye falsafa inayozingatiwa na nchi kwani vyombo hivyo huakisi tunu za jamii husika. Kama nchi ni ya kidemokrasia, vyombo vya habari huwa huru, vinavyojitegemea na anuwai.

Kunakuweko na vyombo vinavyomilikiwa na umma, serikali, watu binafsi na jamii, vyote vikihudumia jamii kwa kuongozwa na tunu za taifa kama zinavyotamkwa kwenye katiba ya nchi.

Vivyo hivyo, kama nchi ni ya kiimla, vyombo vya habari hutumiwa kutawala, vikieneza na kutetea matakwa ya viongozi. Miliki huwa ni ya serikali na taasisi zake au watu vibaraka wanaoaminika.

Viongozi wengi wa nchi, akiwemo Rais, wamekuwa wakilaumu vyombo vya habari kutokuunga mkono serikali wakati wote. Hawaelewi kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuacha dhima yake ya kuilinda jamii ambayo ndio wajibu unaotambuliwa rasmi.

Kadri vyombo vingi zaidi vinavyokubali shinikizo hilo la serikali la kuwa chombo cha kuitetea, ndivyo hivyo vinapokuwa vimeshindwa kuhudumia jamii.

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inavyotamkwa kwenye katiba ya nchi Ibara ya 3(1). Inatarajiwa, kwa hiyo, vyombo vya habari viakisi tunu za kidemokrasia zinazothaminiwa na

taasisi za kidemokrasia, kama vile uhuru, kujitegemea kimawazo, uanuwai wa maoni, utawala wa sheria na uadilifu.

Vyombo vyetu vya habari vikoje katika kanuni hizi? Viongozi wanajisifu kuwa vyombo vya habari kuongezeka ni ishara kuwa nchi ina demokrasia, lakini kisichosemwa ni kwamba kuongezeka idadi bila kuongezeka maoni anuwai, ni sawa na kuwa na chombo kimoja tu cha habari. Utangazaji wa runinga ni mfano mzuri ambapo kati ya vituo 26 vilivosajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano – TCRA, 12 vinamilikiwa na serikali kuu na tawala za mikoa, vingine viwili na taasisi za serikali, taasisi za dini vituo viwili, vituo sita na watu binafsi – mmoja akiwa na vituo vitatu na chama tawala vituo vinne. Hii ina maana kuwa ni vituo vinne tu vinavyoweza kujidai kuwa viko huru kati ya 26.

Kuna suala la ufikiwaji. Wananchi wote wanastahili maudhui ya habari yawafikie kama inavyotamkwa kwenye katiba ya nchi – Ibara ya 18(d). Kama hili haliwezekani kutokana na kukwazwa na hali iliyoibuka hivi karibuni ya kiuchumi, kiusafirishaji, kiuchumi na vikwazo kiteknolojia, basi ni dhahiri vyombo vya habari haviwahudumii wananchi ipasavyo.

Uangaliaji runinga una matatizo katika maeneo ya vijijini na yaliyo mbali na vituo vya kurushia matangazo kutokana na kukosekana umeme, mawimbi ya runinga kutokufika huko, kukosa uwezo wa kumiliki runinga na fedha za kulipia kila mwezi kupitia makampuni kama Startimes, Zuku, Azam, Continental na nyinginezo na kutokuwa na uwezo wa kumiliki simu za kisasa kwa kupokelea matangazo ya redio na runinga.

Licha ya vikwazo hivyo, hadi kufikia Oktoba 2018 – tarehe ambayo data za mwisho zimerekodiwa na mamlaka ya mawasiliano TCRA, leseni 180 za redio na runinga za mtandao zilikwisha tolewa. Leseni hizo ni nyingi na kwa kuwa chombo kimoja hutumiwa na watu wengi, ni dhahiri watumiaji ni wengi

wanaotumia njia hiyo ya mawasiliano ya mtandaoni.

Tangu zamani redio ndicho chombo kilichokuwa kinatumiwa na watu wengi zaidi kuliko vingine vyote. Kati ya vituo 135 vilivyoorodheshwa na TCRA kwenye tovuti yake, 90 viko mijini – Dar es Salaam 26, Mwanza 16, Iringa 11, Dodoma na Mbeya 9 kila mmoja, Arusha 8, Tanga 7, Morogoro 5 na Moshi 4. Vituo vilivyobaki 28 ama vina redio moja au mbili kila kimoja. Kutokana na ukumbwa wa nchi, ni dhahiri wananchi wengi nje ya mazingira ya miji hawafikiwi na matangazo ya redio.

Simu za mkononi na kompyuta zinazidi kuchukua nafasi ya vyombo vya zamani lakini bado ni adimu maeneo ya vijijini kutokana na sababu za kukosa umeme na ughali wa simu ambazo zinahitajika ili kuweza kumudu mawasiliano hayo kwani ni ghali kwa watu wengi.

Magazeti hayaonekani sehemu kubwa ya nchi, achilia mbali kuwa usambazaji umepungua sana, kutokana na ujio wa simu. Vyumba vingi vya habari havikuweza kwenda na wakati kwa kutumia fursa iliyoletwa na simu za mkononi ili magazeti yao yaweze kusomwa kupitia mitandao.

Kwa mwananchi inalipa zaidi akitumia sh. 1,000 kununua kadi ya muda wa simu itakayomwezesha kusoma mitandao na vitu vingi mtandaoni kwa siku nzima kuliko kutumia elfu hiyo kununua gazeti moja tu. Usomaji simu muda mwingi wa siku umekuwa ni tabia na itakuwa ni muhali kupata muda wa kusoma magazeti.

Kwa upande mwingine, vyombo vya kidijiti vimekuwa vingi mijini na kukumbatiwa sana na madaraja yote ya jamii na huenda vikachukua nafasi ya redio na runinga asilia. Blogu na mitandao ya kijamii vinawezesha kusikia na kuona matukio ya kihabari kiuhalisia na kutokana na asili yake huwezesha ushirikishwaji wa mtumiaji kwa kutoa maoni papo kwa hapo. Hii ndiyo inayofanya teknolojia hii kukumbatiwa na vyumba vya habari kuendana na

Udhoofikaji vyumba vya habariInatoka Ukurasa wa 17

Endelea Ukurasa wa 20

Page 20: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

20

Uchambuzi

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

utamaduni mpya wa watumiaji wa kupenda kusoma simu muda mwingi.

Kadri vyumba vya habari vinavyokumbatia muundo wa mtandaoni ndivyo yabidi kufanya marekebisho katika mafunzo na kupata teknolojia husika. Kwa chombo ambacho kinatumia uendeshaji wa zamani na huu mpya kwa pamoja, hatutarajii upungufu wa wafanyakazi, ila kinyume chake, na hii ni kama wanaweza kujirekebisha kupata stadi zinazohusika, la sivyo itabidi kustaafisha wasioweza kumudu matumizi ya teknolojia mpya. Ni fursa ya kujiongeza, kukuza ustadi na ubunifu katika kujiendesha.

Watangazaji biashara wameanza kutumia kwa wingi zaidi vyombo vya kidijiti na kusababisha uchapishaji magazeti kuzidi kupungua. Kila gazeti linalalamika kupungua kwa matangazo na mauzo ya nakala. Katika hali hii, waweza kusema kwa uhakika kuwa ni kweli vyumba vya habari vinadhoofika kwa kupoteza wafanyakazi na kushindwa kuuza magazeti.

Hii inathibitisha ile nadharia inayosema kuwa chombo cha mawasiliano kinapobadilika, na ndivyo tabia ya matumizi na matendo. Mfano ni unachosoma sasa – Barazani – jarida lililokuwa linachapishwa na kusambazwa nakala, sasa linapatikana kupitia mtandao tu.

Kudumaa kwa vyumba vya habari pia ni pale vyombo vya habari vinaposhindwa kwenda sambamba na demokrasia na badala yake vikasimama au hata kurudi nyuma kama tulivyokuwa kabla ya mageuzi ya 1992. Vitendo vya kurudi nyuma vinajumuisha vile vinavyotajwa kwenye Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari 2016 inayoanzisha mabaraza ya habari ya kisheria ya kutoa leseni kwa waandishi wa habari, kupiga faini wakosaji, kufanya makosa ya kashfa kuwa jinai, serikali kuamua nini cha kuchapisha na kutangaza, na haki ya kukamata mitambo na mali. Kwa kifupi sheria hiyo inaweka vyombo vya habari mikononi mwa serikali, hasa kwa kutumia lugha

isiyo dhahiri inayoweza kutafsiriwa kunufaisha zaidi serikali.

Katika mazingira ya sheria za aina hiyo, dhima ya vyombo vya habari ya kulinda wananchi inakuwa imesalitiwa. Kwa umma, vyombo vya habari vinakuwa vimewasaliti, na ndicho ninachoona kuwa ni udhaifu wa vyumba vya habari.

Tanzania hatuna vyombo vya habari vya huduma kwa umma, japo redio na runinga za taifa pamoja na magazeti ya serikali vinavyomilikiwa na serikali vinajinasibu hivyo. Hivyo sio vyombo vya huduma kwa umma kama ilivyo dhana ya umiliki wa umma kwenye vyombo vya habari. Chini ya sera na sheria zinazotawala vyombo hivyo haviwezi kuwa vya huduma kwa umma, ni vya serikali kutetea na kuendeleza maslahi ya serikali iliyo madarakani kwa kile inachodhani kuwa kina manufaa kwa umma. Wananchi hawawezi kudhibiti utawala wake wala kutumia vyombo hivyo wapendavyo kuhoji serikali kuhusu utendaji wake.

Mifumo mingine ya umiliki nayo ni ya mashaka. Umiliki binafsi ni kwa ajili ya kupata faida hivyo unalenga maeneo yanayovutia kupata fedha. Matokeo ni dhahiri : maudhui mepesi na ya juu juu yanayofikia zaidi watu wa mijini. Maeneo yaliyo na uchumi dhaifu hayapati wawekezaji wa vyombo vya habari.

Kadri uchumi unavyodidimia, maudhui bora ya gharama hukwepwa, hasa yale ya uchunguzi na yanayohitaji ubunifu mkubwa, ukweli ambao umeelezwa kwenye Ripoti ya hali ya Vyombo vya Habari 2017/18. Maudhui yanakuwa ya hovyo na hivyo kupunguza ufanisi wa vyombo vya habari.

Vyombo vya habari kwenye demokrasia humilikiwa pia na vikundi vya jamii katika mfumo unaoruhusu vyombo hivyo kuwa vya huduma kwa umma. Mfumo huu uliletwa na UNESCO miaka ya 1990 lakini bado haujastawi sana nchini. TCRA imetoa leseni kwa redio 27 za jamii kwa mujibu wa tovuti yao hadi Oktoba 2018.

Kati ya vituo hivyo, 16 ni vya biashara. Inawezekana redio ya jamii ikamilikiwa binafsi na kuendeshwa kibiashara na bado ikabaki kuwa ya huduma kwa jamii? Hili ni jambo la kutafiti zaidi kuona jinsi mifumo hii miwili inavyoweza kufanya kazi na kwa matokeo gani.

Hitimisho langu ni kuwa vyumba vya habari havijadhoofu kwa idadi kwani vingine vinaanzishwa kupitia mfumo mpya wa kidijiti na isitoshe sasa uwanda wa masafa ya kutangazia redio na runinga umekuwa mpana zaidi, hivyo kuna nafasi ya kuanzisha vituo vingi vya utangazaji na usambazaji wa habari.

Magazeti ya mtandaoni hayatakuwa mbadala wa magazeti ya sasa, bali mifumo hiyo miwili itakuwa sambamba kutimiza mahitaji ya soko. Inahitaji ubunifu katika kutayarisha maudhui ili kuvutia wasomaji, wasikilizaji na watazamaji.

Vyombo vipya vya kidijiti huhitaji stadi zile zile –kusoma, kusikiliza na kuangalia.

Kwa maoni yangu kudhoofika kwa vyumba vya habari ni pale wanahabari wanapokataa kukubali kuwa wanaharakati wa taaluma. Tunaamini kwenye kitu gani? Mwandishi mwanataaluma thabiti anafanyia kazi njonzi fulani – ile bora kuliko zote ambayo jamii ingependa kuwa, ikiwemo uendelezaji wa tunu za taifa.

Kanuni kuu za taaluma ndiyo itikadi inayomwongoza mwanataaluma kamili na ambayo lazima ilindwe kwa gharama yoyote : ukweli na uhakika, uhuru, haki na kutopendelea, utu na uwajibikaji. Kanuni hizi pia zinahusu maudhui ya kwenda kwa umma kupitia intaneti, mitandao ya kijamii, blogu na majukwaa.

Bado unaweza kushangaa : inakuwaje baadhi ya vyombo vya habari mtandaoni vinavyokiuka kanuni hizi havikemewi? Maudhui yake si ya kihabari na yanatakiwa yaeleweke hivyo. Wadhibiti na mamlaka za vyombo vya habari wanatakiwa kuwalinda wananchi kutokana na matumizi haya mabaya.

Udhoofikaji vyumba vya habariInatoka Ukurasa wa 19

Page 21: Baraza la Habari Tanzania Toleo la Julai, 2019 ISSN Sheria ya … · 2019. 11. 21. · Sheria ya Huduma ya Habari Zanzibar ya 2019. Alisema rasimu ya muswada huo itawasilishwa mbele

21

Habari

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Mwandishi Christopher Ga-maina

Mahakama Kuu ime-futa hukumu dhidi ya wanahabari watatu waliofungwa

kwa tuhuma za unyang’anyi na kuamuru kesi yao isikilizwe upya.

Waandishi hao Christopher Gamaina wa Raia Mema, Zephania Mandia wa Chanel Ten na Manga Masabala wa Mzawa walitiwa hatiani na kufungwa na Mahakama ya Wilaya ya Magu.

Akitoa uamuzi kwa rufani dhidi ya kifungo na kutiwa hatiani, Jaji wa Mahakama Kuu Siyani Julai 24 alifuta hukumu hiyo ya Mahakama ya Magu kwa kesi ya uhalifu namba 11/2018.

Katika uamuzi wake Jaji Siyani pia alifuta ushahidi wote uliowasilishwa na upande wa mashitaka na kuamuru kesi hiyo isikilizwe na hakimu mwingine.

Alisema kuwa kwa kuamuru kesi hiyo kusikilizwa upya analenga kulinda maslahi ya sheria kwa pande zote mbili.

Alisema iwapo baada ya kesi kusikilizwa upya na watuhumiwa watapatikana na hatia tena, basi katika kuwahukumu izingatiwe muda waliokwisha tumikia gerezani.

Watuhumiwa wameshauriwa kuomba dhamana tena.

Gamaina na watu wengine wawili walifungwa jela miaka 30 na mtu mmoja alifungwa miaka minne.

Katika rufani yao waliwakilishwa na mawakili Constantine Mutalemwa na Amri Linus.

Wanahabari hao ambao wanapewa msaada wa sheria na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wanadai kuwa wamebambikiwa kesi hiyo. Mwandishi Christopher Gamaina

Mahakama yaamuru kesi ya waandishi isikilizwe upya