aokolewa na punda - bible stories for kids: stories, …€œningelikuwa na upanga ningelikukata.”...

6

Click here to load reader

Upload: vuongmien

Post on 27-May-2018

282 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Aokolewa na Punda - Bible stories for Kids: Stories, …€œNingelikuwa na upanga ningelikukata.” Punda alimtazama Balaamu. “Je, si mimi ni punda wako ambaye umenipanda siku zote?

1

1 Mfalme Balaki wa Moabu aliwatazama Waisraeli waliokita kambi karibu na nchi yake na akawa na wasiwasi. Alikuwa amesha sikia sifa za wana wa Israeli walioitwa Waebrania na safari yao ndefu kupitia jangwani. Walikuwa wameshinda vita vingi na kuwashinda adui wengi. Sasa, makabila kumi na mawili pamoja na kiongozi wao Musa walikuwa hapa.

Mfalme alizitazama kambi za Waisraeli katika tambarare ya Moabu. “Tazama!” aliwaambia wakuu wa Midiani waliokuwa wamesimama kando yake. “Watu hawa wamefikisha idadi zaidi ya mamilioni. Ndio sababu walimshinda Ogu, Mfalme wa Bashani. Kama wanaweza kuyauwa majitu yanayoogofya basi wanaweza kunyakua nchi yetu.”

Wakuu wa Midiani walikubaliana naye. Waliogopa kuwa wana wa Israeli wangenyakua ardhi yao. “Tunajua kuwa BWANA ni mwenye hekima tena mwenye nguvu na kuwa jeshi letu ni ndogo sana.” Walisema. “Sharti tutafute njia za kuwang’atua watu hawa kabla ya kutuvamia!” Hawakujua kuwa Mungu alikuwa amemwambia Musa asiwavamie watu wa Moabu na Wamidiani.

2 Kwa pamoja, mataifa hayo mawili yalipanga mpango wa kijinga wa kuwaondoa Waisraeli. “Kuna nabii mashuhuri sana aitwaye Balaamu anayeishi kule Mesopotamia,” Walimwambia mfalme. “Tukimlipa pesa nyingi anaweza kulaani mtu yeyote.” Wakuu wa Midiani walitabasamu.”Naam, hebu tumlipe ili aweze kuwalaani Waisraeli nao watatoroka.”

Mfalme Balaki alilipenda wazo lile. Aliwakusanya wajumbe wake. “Nendeni mkamlete Balaamu.” Alisema. “Nitamlipa fedha nyingi ili aje na kuwalaani Waisraeli. Sharti tuwaondoe hawa Waebrania haraka iwezekananvyo!”

Huku wakiwa na mfuko uliojaa ada ya uaguzi, wajumbe walipanda ngamia zao na kung’oa nanga kuelekea Mesopotamia. Baada ya safari ndefu jangwani, walifika katika kijiji cha Pethori karibu na Mto Eufrati alikoishi Balaamu.

Upepo mwanana ulivuma juu ya nyumba. Miti mirefu ya minazi iliyumbishwa na upepo. Kila mtu alichungulia dirishani na kushangaa kuwaona wageni waliokuwa na ngamia. Je, wajumbe hawa wa kutoka Moabu ni akina nani?

Aokolewa na Punda“BWANA akamwambia Balaamu, “Usiende pamoja nao. Hupaswi kulaani watu hao kwa kuwa wamebarikiwa.”

(Hesabu 22:12)

Hesabu 22-24

Picha katika hadithi hii ya Biblia inaweza kupakuliwa bure kutoka www.freebibleimages.org katika PowerPoint, Keynote, JPEG au muundo wa PDF. Mpangaji wa Hadithi hii inaonyesha kinachotokea katika kila eneo. Soma akaunti kutoka kwa Biblia kisha ueleke jinsi utakavyosema hadithi hiyo. Vyanzo zaidi vya kufundisha bure vinaweza kupatikana kwenye www.biblepathwayadventures.com ikiwa ni pamoja na toleo la video la hadithi hii, karatasi za kazi, ebook na pakiti ya mwalimu.

Page 2: Aokolewa na Punda - Bible stories for Kids: Stories, …€œNingelikuwa na upanga ningelikukata.” Punda alimtazama Balaamu. “Je, si mimi ni punda wako ambaye umenipanda siku zote?

2

3 Wajumbe walifika katika makao ya Balaamu na kuingia ndani. “Tuna habari maalum kutoka kwa Mfalme wa Moabu.” Walisema. “Tunafahamu wazi kuwa yeyote umbarikie hupata baraka na yeyote umlaaniye hupata laana. Wana wa Israeli wamepiga kambi karibu na nchi yetu. Njoo uwalaani ndipo watuache.”

Mmoja wa wajumbe alichukua mfuko uliojaa pesa na kumkabithi Balaamu. ”Mfalme atakulipa fedha nyingi endapo utakubali kufanya hivyo,”alisema.

Balaamu aliutazama mfuko kwa ulafi. Alipenda sana lile wazo la kuwa tajiri na kuwa na mamlaka. Aliwaza kisha akasema, “Basi kaeni huku usiku kucha. Nitazungumza na Mungu kisha nitawajulisha nitakavyofanya.” Balaamu alifahamu kuwa angewalaani wana wa Israeli iwapo Mungu angeidhinisha jambo lile.

Usiku huo Balaamu alipokuwa usingizini, Mungu alinena naye, akisema, “Usiende pamoja nao. Hupaswi kulaani watu hao kwa kuwa wamebarikiwa.”

4 Asubuhi iliyofuata, Balaamu aliwaita wajumbe, “Rudini nyumbani,” alisema. “Mungu hataniruhusu niwalaani Waisraeli.” Wajumbe walipigwa na butwaa. “Mfalme atakulipa pesa chungu nzima. Utakuwa tajiri mkubwa!” lakini Balaamu alitikisa kichwa. “La,” alisema. “Nitakwenda tu kwa ruhusa ya Mungu.”

Baada ya kujaribu, hawakuweza kumshawishi Balaamu ili abadilishe wazo. Moja baada ya mwingine, walirudi Moabu bila nabii Balaamu.

Mfalme Balaki alipigwa na butwaa aliposikia kuwa Balamu hakuwa amerejea na wajumbe. Alifikiri kuwa nabii angependa kuwa tajiri na mwenye heshima. “BWANA hakumruhusu kuwalaani Waisraeli,” wajumbe walisema. “Hatukuweza kumshawishi Balaamu.”

Mfalme alihangaika huku na kule. Alihitaji msaada wa Balaamu haraka sana! “Sikiza,” alisema. “Nina wazo jingine. Tumpe fedha mara dufu ili awalaani Waisraeli.” Wakati huu aliwatuma wajumbe tofauti, waliokuwa na vyeo zaidi kuwaliko wa kwanza.

5 “Njoo uwalaani wana wa Israeli,” wajumbe walimwambia Balaamu walipokutana huko Pethori. “Mfalme wa Moabu atakupa kiwango kikuu cha fedha na atafanya lolote utakalo.”

Balaamu alitabasamu na kuvuta pumzi. Alipendezwa na jinsi Mfalme wa Moabu alivyomfanya kuwa wa muhimu. “Hata mkinipa kasri la mflame, fedha na dhahabu, katu siwezi kumwasi Mungu na kwenda nanyi. Lakini pia nanyi kaeni hapa usiku wote kama walivyofanya wenzenu. Nitazungumza na Mungu kisha nitawarejelea.”

Mungu alijua wazi kilichokuwa rohoni mwa Balaamu. Alijua kuwa nabii alipenda pesa kuliko kumtii Mungu. Usiku huo kila mtu alipokuwa amelala, Mungu akanena na Balaamu na kusema, “Watu hawa watakapokwambia mwende nao, jitayarishe kisha nenda nao. Utakapofika nchini Moabu, tahadhari, sema nitakachokwambia.” Licha ya hayo, Balaamu alikuwa na mpango mwingine.

Page 3: Aokolewa na Punda - Bible stories for Kids: Stories, …€œNingelikuwa na upanga ningelikukata.” Punda alimtazama Balaamu. “Je, si mimi ni punda wako ambaye umenipanda siku zote?

3

6 Asubuhi iliyofuata, Balaamu alishuka kitandani. Alipakia mizigo kwa punda wake na kung’oa nanga kuelekea nchini Moabu. Alipokua akisafiri, aliwaza na kuwazua kuhusu mpango wake wa kufurahisha Mungu na mfalme. “Pengine naweza kusema alichoniagiza Mungu na kumfurahisha mfalme pia,” aliwaza.

Nabii mlafi alipokuwa akielekea Moabu, Mungu akaamua kusimamisha mpango wake. Ghafla, malaika wa Mungu alisimama mbele ya Balaamu na punda wake ikawa hawawezi kupita.

Hee-haw, hee-haw. Punda alijawa na kiwewe si haba hivi kwambamiguu yake yalitetemeka. Punda alikimbia palipokuwa na uwanja kando ya barabara. Masikio yake makubwa yalipeperuka kama matawi. “Simama!” Balaamu alisema. “Unafanya nini?” Balaamu hakumwona malaika kama vile punda wake alivyomwona. Alimpiga punda wake kwa fimbo mpaka yule punda akarejea barabarani.

7 Balaamu na punda wake waliendelea na safari kuelekea Moabu. Punde si punde, walipita katikati ya shamba la mizabibu yaliyokuwa na nyua ndefu. Malaika akatokea kwa mara ya pili. Hawakuweza kupita.

Punda alikodoa macho kwa hofu. Huku akiegemea upande moja, punda aliupigisha mguu wa Balaamu kwenye ukuta. “Ole wangu! Mbona unafanya hivi?” Balaamu alisema kwa sauti. “Mguu wangu umeumia.” Balaamu alimpiga punda kwa hasira.

Walipoendelea na safari, malaika alisimama mbele yao katika barabara nyebamba. Punda alipomwona malaika kwa mara ya tatu, alijawa na hofu hata zaidi. Punda alilala njiani katikati ya barabara. Alikataa kata kata kutembea.

Balaamu alichemka nyongo. “Nini kinachokusumbua,” alifoka. Alichoshwa na tabia ya ajabu ya punda wake. Katu hakuwa ameshuhudia punda wake akifanya vile.

8 Hata ingawa wanyama hawawezi kuzungumza kama mimi na wewe, Mungu alimpa punda wa Balaamu uwezo wa kuongea. Alifungua kinywa chake na kusema, “Hee-haaw… Bwana wangu, mbona unanitendea haya?”

Balaamu alikuwa mwenye hasira. Alikuwa tayari kumpiga punda wake. “Mbona wanifanya mjinga,” alifoka. “Ningelikuwa na upanga ningelikukata.” Punda alimtazama Balaamu. “Je, si mimi ni punda wako ambaye umenipanda siku zote? Je, nimekuwa na tabia ya kufanya hivi siku zote?”

Wakati huo huo, Mungu akayafungua macho ya Balaamu. Alitazama juu na kushangaa. Malaika mwenye uadhama alikuwa amesimama kidete njiani. Hakuwa malaika wa kawaida. Malaika Yule alikuwa Yeshua, mwana wa Mungu.

Balaamu alijawa na hofu. Hakuwa na njia ya kutorokea. Alianguka mbele ya Yeshua huku moyo wake ukimpapa. Alijawa na hofu kiasi cha kutoweza kuzungumza.

Page 4: Aokolewa na Punda - Bible stories for Kids: Stories, …€œNingelikuwa na upanga ningelikukata.” Punda alimtazama Balaamu. “Je, si mimi ni punda wako ambaye umenipanda siku zote?

4

9 “Je, mbona ulimpiga punda wako mara tatu?” Yeshua alumuuliza Balaamu. “Nilikuja ili nikupinge kwa maana njia zako zimepotoka mbele yangu. Punda wako alinitambua na alisimama mara tatu. Iwapo hangesimama, ningechukua uhai wako na kumwokoa punda wako!”

Balaamu alilala mbele ya Yeshua na kumsihi amhurumie. “Kwa kweli nimetenda dhambi. Sikujua kwamba ulikuwa umesimama barabarani. Iwapo hutaki nielekee nchini Moabu basi nitarudi nyumbani.”

“Nenda Moabu,” Yeshua alisema. “Lakini uyaseme nitakayokwambia.” Balaamu alijizoazoa kutoka mchangani na kumpanda punda wake na kukimbia kuelekea Moabu.

Mfalme wa Moabu alipomuona Balaamu kwa umbali, alikimbia kumsalimu. “Mbona hukuja mara ya kwanza nilipoagiza uje?” aliuliza. “Je, sikuwapa wajumbe pesa za kutosha kwamba wakuletee?”

“Nipo hapa sasa,” Balaamu alisema. “Lakini nitazungumza niliyoagizwa na Mungu.” Mfalme alikuwa na matumaini. “Njoo haraka ukanilaanie Waisraeli,” alisema. Lakini Mungu alikuwa na mpango mwingine.

10 Asubuhi iliyofuata, Mfalme Balaki alimpeleka Balaamu mahali palipokuwa juu, ambapo watu wa Moabu waliabudu miungu ya uongo. Mahali pale palikuwa na madhabahu yaliyojengwa juu ya milima. Hapo ndipo walipotolea miungu ya uongo kama vile Baali dhabihu ya wanyama

Kutoka kileleni cha mlima, Balaamu aliweza kuyaona makabila kumi na mawili ya Israeli yaliyokita kambi chini ya mlima. Balaamu alimwambia mfalme, “Nijengee madhabahu saba. Kisha teketeza fahali saba na kondoo saba.” Mfalme alifanya madhabahu saba ya mawe na kuteketeza fahali na kondoo saba.

Dhabihu ilipokamilika, Balaamu akamwambia mfalme, “Kaa ange karibu na dhabihu yako. Nitasubiri maagizo ya Mungu.” Mfalme alifurahia huku akipiga makofi. “Hivi punde, Waisraeli watatoweka!” alisema kwa furaha.

Moabu alipiga magoti na kumwomba Mungu. “Nimefanya madhabahu saba na kuteketeza fahali saba na kondoo saba kwa kila dhabahu. Je, una ujumbe wa kumpa mfalme?” Mungu alimjibu, akisema, “Naam, nenda ukamwambie mambo haya nitakayokwambia.”

11 Balaamu aliamka na kusimama kisha akamjia mflame aliyekuwa amesimama kando ya dhabihu yake. Balaamu alisema, “BWANA asema, ‘Siwezi kulaani nilichobariki. Watu wa Israeli wamebarikiwa kushinda mataifa mengine.”

Mfalme Balaki aliduwazwa. Ujumbe huu haukuwa ule alioutarajia. “Wasemaje?” alilia. Aliupigisha mguu wake sakafuni na kumrushia Balaamu jicho kali. “Nilikuleta hapa ili uwalaani adui zangu lakini sasa umewabariki.”

“Sikiza!” Balaamu alisema. “Siwezi kufanya lolote. Nilikufahamisha kuwa ninaweza kusema tu nililoambiwa na Mungu.” Mfalme alipandwa na mori. Hakuwa tayari kukata tamaa. “Njoo nami mahali utakapo waona Waisraeli,” alisema. “Pengine waweza kuwalaani utakapowaona.”

Page 5: Aokolewa na Punda - Bible stories for Kids: Stories, …€œNingelikuwa na upanga ningelikukata.” Punda alimtazama Balaamu. “Je, si mimi ni punda wako ambaye umenipanda siku zote?

5

12 Mfalme Balaki alimpeleka Balaamu juu ya mlima. Kwa mara nyingine, aliyafanya madhabahu saba ya mawe na kutekeza fahali na kondoo saba kwa kila dhabahu.

Mfalme alipomaliza kuteketeza dhabihu, Balaamu akamwambia, “Simama kando ya dhabihu yako nami nitakwenda kuzungumza na Mungu.” Mfalme alikubali lakini baada ya muda mfupi akaanza kukerwa. Aliwataka wana wa Israeli watoweke mara moja.

Mungu alizungumza na Balaamu kwa mara nyingine. “Rudi kwa Balaki na umwambie Nitakayokwambia.” Balaamu alimtazama mfalme huku akiwa na hofu. Alichelea kuwa habari zile zingemkera mfalme hata zaidi.

Lakini Balaamu alimtii Mungu. Alimsogea mfalme na kusema, “BWANA asema, ‘Mimi sio kama mwanadamu. Sibadili nia yangu. Katu sitobadili baraka Zangu kwa watu wangu wa Israeli. Ninapoahidi jambo, hutimia. Niliwatoa Waisraeli kutoka Misri na kuwafanya wenye nguvu. Siwezi kuwalaani.’”

13 “Eti nini?!” Mfalme alimkodolea macho Balaamu. Hakuyaamini masikio yake. “Kama huwezi kuwalaani Waisraeli, ni heri usiwabariki!” Balaamu alishusha pumzi na kusema, “Nina uwezo wa kusema nilichoagizwa na Mungu.”

Mfalme Balaki alipandwa na mori. Asubuhi iliyofuata, alimpeleka Balaamu kwenye kilele cha mlima juu ya mawingu. “Pengine mungu wako anaweza kukuruhusu uwalaani waisraeli ukiwa hapa.” Alisema. Kwa mara nyingine mfalme aliyafanya madhabahu saba na kuteketeza fahali saba na kondoo saba katika kila dhabahu.

Balaamu aligundua kuwa Mungu alipendezwa na Waisraeli walipobarikiwa,alitazama tambarare ya Moabu walipokuwa wamekita kambi Waisraeli na kusema, “Kambi za Waisraeli zapendeza kweli. Watawashinda adui zao. Amebarikiwa anayewabariki Waisraeli. Amelaaniwa anayewalaani Waisraeli!”

14 Mfalme Balaki alichemka nyongo. Alipigisha mguu wake sakafuni. “Nilikwambia kinaga ubaga uwalaani Waisraeli, lakini umewabariki mara tatu! Nilikuwa nimeahidi utajiri mkubwa, lakini Mungu amekuzuia kupata zawadi yako. Basi nenda nyumbani sasa hivi!”

Balaamu alivuta pumzi. “Sikiza,” alisema. “Nilikwisha waambia wajumbe wako kuwa hata ukinipa utajiri mkuu kamwe siwezi kumwasi Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitakwenda nyumbani, lakini kwanza nina ujumbe kutoka kwa Mungu.”

Mfalme hakujua kama angependa kusikiza alichotaka kusema Balaamu. Alichelea kuwa nabii alikuwa na habari za kuhuzunisha. Lakini alikuwa amechelewa. “Masihi atatokea miongoni mwa wana wa Israeli na kuangamiza adui Zake,” Balaamu aliendelea, “Pamoja na watu wako wa Moabu.”

Moyo wa mfalme ulidunda. Aliyafunga masikio yake. Ujumbe huu ulikuwa mgumu zaidi. “Wasemaje?!” alifoka kwa hasira. ”Nyamaza! sitaki kuyasikia hayo. Nenda nyumbani!”

Page 6: Aokolewa na Punda - Bible stories for Kids: Stories, …€œNingelikuwa na upanga ningelikukata.” Punda alimtazama Balaamu. “Je, si mimi ni punda wako ambaye umenipanda siku zote?

6

15 Balaamu alitamani mali aliyoahidiwa na mfalme. Kabla ya kuondoka, alipanga mpango wa kuwadhuru wana wa Israeli. Alijua wazi kuwa Waisraeli walikuwa wamebarikiwa kwa sababu ya utiifu wao. Iwapo wangeasi amri za Mungu, basi wangeleta laana juu ya maisha yao wenyewe.

“Kama wataka kuwashinda Waisraeli,” Balaamu alisema. “Waalike wananaume ili kwamba wawe na uhusiano na wanawake wa Moabu na Midiani. Wanawake wale watawajulisha kuhusu miungu yao nao watasahau kuhusu maagizo ya BWANA.” Mfalme alichangamka. Alilipenda wazo lile. Alijua wazi kuwa wanaume wa Israeli wangewapenda wanawake wa Kanaani.

Hakika, wanaume wa Israeli walianza kushawishiwa na wale wanawake. Wanawake hawa walikuwa na itikadi na miungu yao. Punde, Waisraeli walisahau maagizo ya BWANA na wengi wao waliwaoa wanawake na wengine kuiga tabia na desturi zao.

16 Mungu hakufurahishwa na Waisraeli. “Watu wangu wametenda kinyume nami kwa kuabudu sanamu!” alisema. Mungu alituma mapigo kwa wale waliotenda hayo ili kuwapa funzo na wengi wakafa.

Mungu hakuwa amewasahau Wamidiani. Alichemka nyongo kwa kuwa walikuwa wamewalaghai watu Wake kwamba wamuasi. Alimwambia Musa, “Nenda ukakabiliane na Wamidiani kwani ni adui zenu.” Musa alichagua wanaume elfu moja kutoka katika makabila kumi na mawili ya Israeli kisha akawaongoza vitani. Walikuwa wamebeba sanduku la agano, ambalo lilikuwa sanduku la dhahabu lilokuwa hifadhi ya mawe yaliyochongwa ya Amri za Mungu.

Baraghumu na ngoma zilipigwa. Hata ingawa Wamidiani walikuwa wengi kuliko Waisraeli, haikuchukua muda mrefu kabla ya Waisraeli kuwaangamiza adui zao na kushinda vita. BWANA ni Yule jana, leo na milele. Anaahidi kubariki wana Wake wanaoyatii maagizo Yake na kufuata njia Zake. Mungu hutimiza ahadi zake.

17 ©Bible Pathway Adventures