ahadi za serikali kwenye sekta ya elimu 2012/2013 khakielimu.org/files/publications/govt promises...

4
Kila mwaka, katika mikutano ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge, ambao ni wawakilishi wa wananchi, huiuliza Seri- kali maswali mbalimbali kuhusu mipango iliyopo kwenye sekta mbalim- bali, ikiwemo elimu. Mawaziri husika au wawakilishi wao hutoa majibu ambayo mara nyingi huambatana na ahadi. Je, baada ya hapo, nani ana jukumu la kufuatilia utekelezaji wa hizi ahadi? Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muun- gano (1977), wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi. Pia, lengo kuu la Serikali ni ustawi wa wananchi na itawajibika kwao. Hii ina maana mwananchi yuko ndani ya wajibu na mamlaka yake akihoji na kufuatilia ahadi za seri- kali, kwani zinatolewa na viongozi wanaopaswa kuwajibika kwake. Ndi- yo maana, tangu 2006, Shirika la HakiElimu limekuwa likikusanya na kuchapisha ahadi za serikali na kusambaza machapisho haya kwa wananchi ili waweze kutimiza wajibu wao. Toleo hili, la kwanza la 2013, ni mkusanyiko wa ahadi zilizotolewa mwishoni mwa 2012 na mwanzoni mwa 2013. Ahadi za Serikali kwenye Sekta ya Elimu 2012/2013 Ahadi za Serikali kwenye Sekta ya Elimu 2012/2013 HakE kijarida Na 4K, 2013

Upload: others

Post on 30-Dec-2019

14 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Kila mwaka, katika mikutano ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge, ambao ni wawakilishi wa wananchi, huiuliza Seri-kali maswali mbalimbali kuhusu mipango iliyopo kwenye sekta mbalim-bali, ikiwemo elimu.

Mawaziri husika au wawakilishi wao hutoa majibu ambayo mara nyingi huambatana na ahadi. Je, baada ya hapo, nani ana jukumu la kufuatilia utekelezaji wa hizi ahadi?

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muun-gano (1977), wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi.

Pia, lengo kuu la Serikali ni ustawi wa wananchi na itawajibika kwao. Hii ina maana mwananchi yuko ndani ya wajibu na mamlaka yake akihoji na kufuatilia ahadi za seri-kali, kwani zinatolewa na viongozi wanaopaswa kuwajibika kwake. Ndi-yo maana, tangu 2006,

Shirika la HakiElimu limekuwa likikusanya na kuchapisha ahadi za serikali na kusambaza machapisho haya kwa wananchi ili waweze kutimiza wajibu wao.

Toleo hili, la kwanza la 2013, ni mkusanyiko wa ahadi zilizotolewa mwishoni mwa 2012 na mwanzoni mwa 2013.

Ahadi za Serikali kwenye Sekta ya

Elimu 2012/2013

Ahadi za Serikali kwenye Sekta ya

Elimu 2012/2013

HakE kijarida

Na 4K, 2013

Kwa mujibu wa taarifa za Bunge, ahadi zifuatazo zilizotolewa Bungeni na Ummy A. Mwalimu, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (4 Februari 2013), Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (10 Aprili 2013) na Aggrey Mwanri, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (10, 19 na 23 Aprili 2013): • Serikali itaanza rasmi kujenga shule ya wasicha-

na Borega (Halmashauri ya Wilaya ya Tarime) mwezi June, 2013. Ujenzi huu utakamilika ifikapo Novemba, 2014. Halmashauri kupitia mapato ya ndani imechangia shilingi milioni 28 na eneo la ujenzi limeshapimwa. Kwa sasa utara-tibu wa kutangaza zabuni unaendelea.

• Serikali imepanga kuviboresha vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDCs) kwa kuvikara-bati, kuvipatia watumishi na vyombo vya usafiri.

• Serikali itatumia fedha za malipo ya fidia ya rada kwa ununuzi wa vitabu na madawati katika

shule za msingi Tanzania Bara. Fedha itakayo-tumika kwa ajili ya ununuzi wa vitabu ni karibia shilingi bilioni 59 na fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati ni karibia shilingi bilioni 20. Mchakato wa ununuzi wa vitabu umekami-lika ambapo Serikali imeingia mikataba yenye thamani ya shilingi bilioni 57 na wachapishaji wa vitabu. Kulingana na mikataba, kazi hii inategemewa kukamilika ndani ya miezi sita tangu tarehe ya kuweka saini mikataba tarehe 18 Machi, 2013. Kwa upande wa ununuzi wa madawati, mchakato umeanza ambapo ka-tika Kikao cha Bunge la Bajeti ya mwaka wa fedha 2012/2013 iliazimiwa kuwa madawati yanunuliwe na kusambazwa katika halmashauri zote kwa usawa.

• Katika juhudi za kutatua tatizo la madawati nchini, Serikali imekuwa ikipeleka fedha katika halmashauri kwa ajili ya ununuzi na utengenezaji wa madawati. Mwaka 2010/2011 shilingi bilioni tatu zilipelekwa katika halmashauri zote kwa ajili ya madawati ambapo Mkoa wa Mara ulipata shilingi milioni 197 na mwaka 2012/2013 shilingi bilioni moja zilipelekwa katika halmashauri zote kwa ajili ya madawati na Mkoa wa Mara ukapata shilingi milioni 68.

• Kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi Serikali imekuwa ikitoa fedha za uendeshaji wa shule (ruzuku) kwa kiwango cha shilingi 10,000 kwa kila mwanafunzi. Hadi kufikia mwezi Machi, 2013 Serikali imeshatoa jumla ya shilingi bilioni 60 za ruzuku kwa shule za msingi nchini kote. Kiasi hiki ni sawa na shilingi 7,565 kwa mwanafunzi ambayo ni sawa na asilimia 75.

Kwa mujibu wa taarifa zilizo-tolewa Bungeni na Philipo A. Mulugo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi (7 Februari 2013) na Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (10 Aprili 2013):

• Katika mwaka wa fedha

2012/13, Serikali inata-rajia kupata fedha kiasi cha shilingi bilioni sita kutoka Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (UK-Department for International Development, DFID) ambazo zitatumika kukarabati majengo ma-pya katika vyuo saba vya

ualimu, Chuo cha Ualimu Kitangali kikiwa ni kimo-jawapo.

• Mwaka 2013 Serikali ime-fanikiwa kuajiri walimu wapatao 26,537. Kati ya hao, 13,568 ni wa shule za msingi na 12,969 ni wa shule za sekondari.

Ual

imu

Elimu kwa wasichana, ufundi stadi, vifaa vya shule n.k

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Bungeni na Philipo A. Mulugo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi (29 Januari 2013) na Mizengo Pinda, Waziri Mkuu (10 Aprili 2013):

• Kitengo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mnya-ki (Wilaya ya Mpanda) hakijafungwa na kitaendelea kuandikisha wanafunzi kadiri ya upatikanaji wao. Pia, Serikali, itaendelea kuajiri walimu wenye ujuzi wa kufundisha watoto wenye mahitaji maalum kila mwaka, ili kukidhi mahitaji ya shule katika halmashauri husika.

• Serikali inaendelea kuweka msukumo wa kipekee katika kutoa elimu maalum kwa watu wenye ulemavu wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi, uoni hafifu na usikivu. Katika mwaka 2012/2013, Serikali imeandaa mwongozo wa kufundishia wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi na uoni hafifu. Aidha, Serikali imenunua na kusambaza vifaa maalum na visaidizi vya kufundishia na kujifun-zia kuanzia ngazi ya Elimu ya Awali hadi Chuo Kikuu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Bungeni na Philipo A. Mulugo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafun-zo ya Ufundi (9 Novemba 2012), na Aggrey Mwanri, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (10 na 23 Aprili 2013):

•Katika mwaka wa fedha 2012/2013, Serikali ina mpango wa kuboresha miundombinu ya shule 264 nchi nzima au shule mbili kwa kila halmashauri. Ujenzi wa maabara na nyumba za walimu ume-fikia hatua ya kutangaza zabuni. Kwenye Hal-mashauri ya Rombo, ujenzi wa nyumba za walimu na maabara utafanyika ka-tika shule za sekondari za Mawanda na Maki. Mwaka 2012/2013, kila mwana-funzi wa shule ya sekond-ari ya Serikali, ametengewa kiasi cha 25,000/= kwa mwaka na katika fungu hili kuna fedha za kununua vitendea kazi.

•Shilingi bilioni 56.3 zita-tumika kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu

ya Sekondari (MMES II) kukamilisha hizi shule za sekondari 264. Hal-mashauri ya Wilaya ya Tarime inakamilisha tara-tibu za zabuni za shilingi milioni 484 kutekeleza mradi huu katika shule za sekondari Nyamwaga na Kurumwa. Aidha, kwa kushirikiana na sekta bi-nafsi, serikali imeongeza udahili wa walimu katika vyuo na walimu wanao-hitimu wataendelea kua-jiriwa na kupangwa katika halmashauri ili kuwa na walimu wa kutosha ka-tika shule zote ifikapo 2014. Mwezi Februari 2013, Serikali imewapanga walimu 12,973 katika shule za sekondari nchini na Wilaya ya Tarime ilipangi-wa walimu 184.

•Serikali ilitenga shilingi bilioni 74 kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ya shule za sekondari ikiwemo nyumba, maktaba, maabara

Elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu

Elimu ya sekondari

na vyoo. Serikali imeshatu-mia jumla ya shilingi bilioni 9.3 kukarabati shule kongwe za sekondari nchini ikiwemo shule ya sekondari ya Tarime, iliyopatiwa shilingi milioni 100. Vilevile shilingi bilioni 3.6 zimetolewa katika hal-mashauri kwa ajili ya ununuzi wa maabara hamishika. Hal-mashauri ya Wilaya ya Tarime ilipatiwa shilingi milioni 24.

•Kupitia Mpango wa Maende-leo ya Elimu ya Sekondari, awamu ya pili (MMES II), Serikali itakamilisha ujenzi wa shule za sekondari 1,200 kwa kuweka miundombinu muhimu ikiwemo umeme. Awamu ya kwanza, ambayo

imeanza ndiyo inalenga shule 264 kwa thamani ya shilingi bilioni 56.3 ambapo suala la umeme wa gridi ya Taifa au umeme wa jua limepewakipaumbele. Kuanzia mwezi Machi 2011 shule ya sekond-ari Kikombo (Dodoma)ilianza kutumia mfumo wa umeme wa jua kupitia mradi wa TASAF. Aidha, kuanzia mwezi Februari 2013, shule za sekondari Mpunguzi na Mbambala (Dodoma)zilianza kutumia umeme wa gridi ya Taifa baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha kuweka nguzo za umemekatika maeneo ya shule.

• Katika mwaka wa fedha 2010/11, Serikali katika kuun-ga mkono jitihada za wanan-chi kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ilitoa jumla ya shilingi milioni 625 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya elimu katika shule zote 41 za Serikali kwenye wilaya hii. Kwa kuzingatia gharama za ujenzi wa ghorofa shule tatu zilipata mgao ufuatao:- shule ya sekondari Bustani ilipewa shilingi milioni 57.6, shule ya sekondari Keni ilipewashilingi milioni 53.9 na shule ya sekondari Shimbi ilipewa shilingi milioni 53.9.

HakiElimu inawezesha wananchi kuleta mabadiliko katika elimu nademokrasia

SLP 79401 • Dar es Salaam • Tanzania. Simu (255 22) 2151852 • Faksi (25522) [email protected] • www.hakielimu.org