web viewhistoria yangu. jina langu ni paulina shirima.nimezaliwa katika kijiji cha ushiri wilaya ya...
TRANSCRIPT
HISTORIA YANGU
Jina langu ni Paulina Shirima.Nimezaliwa katika kijiji cha Ushiri wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na nina
umri wa miaka 40.Baba yangu anaitwa Michael na mama yangu anaitwa Selestina.Katika uzao wetu tumezaliwa
watoto saba,watatu wa kiume na wanne wa kike.Mimi nikiwa mtoto wa mwisho kuzaliwa.
Wazazi wangu ni wakulima na hupenda kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali pamoja na bustani za mboga ambazo hutumika kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani.
Kielelezo no 1 P Shirima
Mimi nilianza elimu ya msingi mwaka 1983 katika shule ya msingi Ushiri,chini ya uongozi wa mwalimu mkuu
ambaye jina lake ni Mrs Mtenga.Hatimaye nilimaliza elimu yangu ya msingi mwaka 1989,ila kwa bahati mbaya
sikuweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.Hivyo ilinibidi nikae nyumbani na wazazi wangu na
kuwasaidia kazi mbalimbali zikiwemo za ufugaji na kilimo.
Kutokana na nia yangu ya kutaka kuendelea na masomo,nilikuwa nikimsumbua mama mara kwa mara kuhusu
suala la shule.Baada ya mwaka mmoja kuisha mwaka uliofuata mzazi wangu alinichukulia fomu ya kujiunga na elimu
ya sekondari.Jambo ambalo lilinifanya nijisikie furaha moyoni mwangu. Baada ya siku si nyingi tarehe ya kufanya
mtihani wa usaili iliwadia na siku hiyo niliwahi mapema sana kwenye kituo cha mtihani.Baada ya siku kama kumi
kupita matokeo yalitoka na nikajikuta nimechaguliwa na kuanza kidato cha kwanza.
Maandalizi ya kuandaa mahitaji ya shule yalianza rasmi huku nikiwa na furaha sana na kuahidi kuwa
nitajitahidi sana katika masomo yangu yote.Mwaka 1991 nilijiunga na elimu ya sekondari ya katika shule ya Ugwasi
sekondari iliyoko wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.Shule hiyo ilikuwa ni ya kutwa,pia ilikuwa ya mchanganyiko wa
wasichana na wavulana. Ilikuwa chini ya uongozi wa mwalimu mkuu Mr Leina. Vilevile ilikuwa na mchepuo wa
masomo ya sayansi na art.
Nilipofika kidato cha pili wazazi wangu walishindwa kuendelea kunilipia ada jambo ambalo lilinisononesha
sana nafsini mwangu. Nikawa naenda shule na kufukuzwa kutokana na kushindwa kulipa ada. Hali hiyo ilinifanya
nikae nyumbani na kulima vibarua ili niweze kulipa ada ya shule. Mungu si athumani kwani ni mkubwa na hamtupi
mja wake,nilibahatika kupata mfadhili ambaye alinilipia ada na nikaendelea na masomo. Nilipofika kidato cha pili
nilifanya mtihani na nikafaulu nikaendelea na kidato cha tatu.Mwaka 1994 nilifanikiwa kumaliza elimu ya sekondari
na kubahatika kuchaguliwa kujiunga na chuo cha ualimu Korogwe,mwaka 1995 hadi 1997 nilihitimu mafunzo yangu
ya ualimu.Kwa bahati mbaya wakati huo ajira zilisitishwa.Hivyo sikuajiriwa kwa miaka minne ila nikaamua kujitolea
ili nipate mahitaji yangu.
Mwaka 2002 nafasi za kazi zilitangazwa katika mkoa wa Tanga.Hivyo ilinilazimu kwenda kwenye
usaili.Nikafanikiwa kuingia kwenye ajira mpya na kuajiriwa kama mwalimu wa daraja la III A kwa masharti ya
kudumu.Nilifanya kazi Tanga kwa muda wa miaka mitatu.Hatimaye nilihamia mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya
Moshi mwaka 2005 na kuendelea na kazi yangu ya ualimu.
Kwa sasa nina mume na watoto watatu.Mwaka 2014 niliamua kujiendeleza na masomo ya diploma ya shule
ya msingi katika chuo cha ualimu Marangu,ambapo hadi sasa bado nipo masomoni kwa muda wa miaka miwili.
Mwisho napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wazazi wangu,mfadhili wangu ambaye ameniwezesha
kuwa kama nilivyo sasa na bila kumsahau mume wangu mpendwa kwa kuniruhusu kuja chuoni.