mtihani wa pamoja sub-kaunti ya kakamega kusini · e-resources available online at / email:...

12
E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748 Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...……… Shule : …………………………………………………………………………………………………… Sahihi .................................... ……………………………………… Tarehe: ……………..................... 102/2 KISWAHILI LUGHA KARATASI YA 2 MACHI/APRIL 2014 MUDA: 2 ½ MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E) 102/2 KISWAHILI LUGHA KARATASI YA 2 MACHI/APRIL 2014 MUDA: 2 ½ MAAGIZO Jibu maswali yote. Karatasi hii ina sehemu nne, 1,2,34. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali. KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE. SEHEMU ALAMA TUZO 1 15 2 15 3 40 4 10 JUMLA 80

Upload: truongthuan

Post on 13-Feb-2019

299 views

Category:

Documents

0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………

Shule : ……………………………………………………………………………………………………

Sahihi .................................... ……………………………………… Tarehe: …………….....................

102/2

KISWAHILI LUGHA

KARATASI YA 2 MACHI/APRIL 2014

MUDA: 2 ½

MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

102/2

KISWAHILI LUGHA

KARATASI YA 2

MACHI/APRIL 2014 MUDA: 2 ½

MAAGIZO ➢ Jibu maswali yote. ➢ Karatasi hii ina sehemu nne, 1,2,34.

➢ Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE.

SEHEMU ALAMA TUZO

1 15

2 15

3 40

4 10

JUMLA 80

Page 2: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

Karatasi hii ina kurasa 11 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa

chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo. 1. UFAHAMU (ALAMA 15)

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

Utandawazi

Kufikia miongo michache iliyopita, ujumbe ulisafirishwa kwa njia zilizochukua muda mrefu sana

kufika. Kwa mfano, mtu alipotaka kupiga simu katika nchi jirani barani Afrika, ilimbidi kupitia kwa

opareta katika nchi za Ulaya ndipo aunganishwe. Kupigia simu kutoka Gambia kwenda Senegal ilibidi

kutumia opareta wa Kule London na wa Paris, Ufaransa, na wa Senegal.

Leo hii kuna njia nyingi za mawasiliano zilizo bora, za kutegemewa na zinazofikisha ujumbe kwa kasi

sana. Ujumbe ambao ungechukua muda mrefu kuufikisha, sasa unapelekwa kwa sekunde moja.

Miongoni mwa njia hizi ni mdahilishi, simu tamba na tuama, faksi, satelaiti, mitandao ya wavuti, n.k.

Hamna eneo sasa hivi hata liwe mbali vipi lisilofikika na aina hizi za mawasiliano.

Maendeleo haya ya mawasiliano yamechangia pakubwa sana kuufanya ulimwengu kuwa kijiji kimoja.

Sasa kuna uhusiano wa karibu sana miongoni mwa mataifa duniani katika Nyanja zote za maisha. Hali

hii ndiyo inayoitwa utandawazi au utandaridhi. Utandawazi umeleta mabadiliko mengi maishani.

Mojawapo ni utoaji na uzalishaji wa mali. Mabadiliko ya mawasiliano yameruhusu mashirika ya

kimataifa kusambaza utoaji na uzalishaji wa bidhaa zao katika maeneo mbalimbali duniani. Hali hii

ndiyo inayoitwa utandawazi au utandaridhi. Utandawazi umeleta mabadiliko mengi maishani.

Mojawapo ni utoaji na uzalishaji wa mali. Mabadiliko ya mawasiliano yameruhusu mashirika ya

kimataifa kusambaza utoaji na uzalishaji wa bidhaa zao katika maeneo mbalimbali duniani. Hali hii

imepunguza gharama za usafirishaji sana. Bidhaa inayoundwa na kiwanda chenye hakimiliki kilichoko

kule New York masafa ya mbali, inaweza kuzalishwa na kiwanda kilicho hapa Nairobi. Bila shaka

umesikia kuhusu madawa ya kurefusha maisha ya wahasiriwa wa UKIMWI ambayo yanazalishwa na

baadhi ya viwanda vya kutengeneza madawa humu nchini. Kiwanda chenye hakimiliki kipo jijini

London.

Viwanda ambavyo vilikuwa katika mataifa tajiri kama vile Uingereza, Ufaransa, Marekani, Ujerumani

na Japani sasa vimeweza kutandaza vitandabui vyake kote duniani. Utandazaji huu hufanywa kwa njia

kadhaa. Kwanza, viwanda hivi huvinunua viwanda vilivyoko katika mataifa yanayostawi. Vinaweza

kuingia katika ubia na viwanda vya mataifa wanakotaka kuhamia. Viwanda hivi vya mataifa

yanayoendelea hupatana kuwa watasimamia utoaji na uzalishaji wa bidhaa Fulani na kukubaliana

namna ya kugawa mapato.

Utandawazi katika sekta ya uzalishaji na utoaji bidhaa umeleta manufaa kadhaa katika nchi

zinazoendelea. Mojawapo ya haya ni kupatikana kwa nafasi za kazi. Pili, bidhaa za nchi zinazoendelea

ambazo hazingeshindana na zile za mataifa yalioendelea sasa zimepata nafasi ya kushindana.

Halikadhalika, wateja wana nafasi ya kupata bidhaa watakayo bila kuvunjwa moyo. Iwapo bidhaa

anayohitaji mteja haipatikani katika nchi, inaweza kuagizwa moja kwa moja kutoka kwa kiwanda

kingine chenye uhusiano nacho. Uagizaji hauchukui muda kutokana na hali ya mawasiliano inayoweza

Page 3: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza wakati. Fauka ya haya, wateja hupata uwanja mpana

wa kuchagua wanachokihitaji.

Utandawazi umehimiza kustawi kwa mazingira ya mashindano katika utoaji na uzalishaji mali

viwandani. Sasa hivi hamna nchi yenye uwezo wa kufungia bidhaa za nchi nyingine katika mipaka

yake. Kufanya hivi ni kujitia kitanzi kiuchumi. Lazima nchi zifungue masoko yao. Navyo viwanda vya

kimataifa huweza kuwania masoko haya. Matokeo yake ni wateja kufaidika kwa kupata uwanja mpana

wa bidhaa za kuchagua. Wateja pia hupata bidhaa za hali ya juu na kwa bei isiyo ghali kutokana na

mashindano haya. Mashindano ya kimataifa ni kama ya paka na panya na kiwanda kisichojifunga

nira vizuri, huwa kinajihatarisha. Kinaweza kujipata kimetupwa nje ya soko na kuangamia.

Manufaa mengine ya utandawazi ni kuwa watu sasa hivi wanaweza kuwasiliana kwa urahisi na wepesi.

Kwa kutumia simu, au mdahilishi, mtu anaweza kuwasiliana na mwenzake popote alipo licha ya

masafa. Zaidi ya haya, utandawazi umewawezesha watu kutoka asili mbalimbali kuingiliana na

kutangamana. Utangamano huu umeweza kuleta umoja baina ya watu kwa kutohoa hisia za ubaguzi.

Hata hivyo utandawazi umetokeza kuwa na madhara. Kwanza, uchumi wanchi nyingi umeibukia

kutawaliwa na matukio ambayo hayazihusu nchi hizo moja kwa moja. Uvamizi wa kijambazi wa

Septemba 11,2000 kule Marekani uliathiri uchumi wan chi nyingi sana. Matukio ya vita katika

Mashariki ya kati nayo yamechangia kuzorotesha uchumi wa nchi nyingi hasa zile maskini ambazo

zinategemea mafuta kutoka huko ilhali vita hivyo haviwahusu sikio wala ndewe.

Athari kubwa ya utandawazi yaonekana katika sekta ya kijamii. Tamaduni nyingi za jamii katika nchi

maskini zinaendelea kuvurugwa na maadili kuporomoka kutokana na ustawi wa kimawasiliano. Vijana

wanaiga kutoka mataifa ya kimagharibi bila kuchuja. Si ajabu kuwa vijana wetu wanavaa mavazi

yasiyositiri uchi wao vizuri na yasiyostahiki kwa jina la ustaarabu. Wavulana nao huzidisha kwa

kutoga masikio na kusuka nywele usiweze kuwatofautisha na dada zao.

Maswali

(a) Utandawazi ni nini? (alama 1½ )

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(b) Ni mambo yapi yanayosababisha kutokea kwa utandawazi? (alama 2)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(c) Mashirika ya mataifa yaliyostawi yanatumia mikakati ipi kutandaza vitandabui vyao kote duniani?

(alama 3)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Page 4: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(d) Fafanua:

(i) Manufaa matatu ya utandawazi. (alama 3)

(ii) Hasara tatu za utandawazi. (alama 3)

(e) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa. ( alama 2 ½ )

(i) Ubia

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(ii) Mashindano ya paka na panya

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(iii) Kutoga

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(iv) Vitandabui

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(v) Kujifunga nira

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

2. UFUPISHO (ALAMA 15)

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

Page 5: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

Ponografia ni tendo, maandishi, picha au mchoro unaoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya

ngono kwa ajili ya kuchochea ashiki ya kuifanya. Mambo haya machafu huwasilishwa ana kwa ana

kupitia sinema, video, magazeti, vitabu, muziki, televisheni, DVD, n.k.

Ponografia imekuwepo tangu jadi, hasa katika nchi za magharibi. Lakini sasa limekuwa tatizo sugu. Hii

ni kwa sababu imeenea ulimwenguni kote mithili ya moto katika mbuga wakati wa kiangazi. Uenezi

umechangiwa na mambo kadha wa kadha. Mchango mkubwa zaidi umetokana na kuimarika kwa

vyombo vya teknolojia ya habari na mawasiliano. Matumizi ya tarakilishi, mdahilishi na viungambali

vya picha yamesambaza ponografia ilivyoanza. Hata hivyo, hubuniwa au kutengenezwa na makundi

mbali mbali ya watu. Miongoni mwa hawa ni watu wasiojali maadili. Pili, kuna wale wenye matatizo

ya kisaikolojia na kijamii. Wao hutengeneza na kueneza uchafu huu kwa lengo la ama kuvuruga

maadili katika jamii au kuchukiza wanajamii waadilifu. Kundi linguine ni lile la wanaoichukulia

ponografia kama nyenzo ya kutosheleza ashiki zao. Hivi sasa, kundi kubwa ni lile la wanotumia matusi

haya kama njia ya kuchuma. Kwa mfano, wanamziki ambao hutumia ponografia kuvutia wateja na

hivyo kuzidisha mauzo yao.

Kushamiri kwa wimbi na uonyeshaji ponografia kuna athari kubwa kwa jamii na hasa watoto. Ingawa

watu wengine hudai picha hizi haziwaathiri, upo ushahidi kuonyesha kuwa wanaotazama picha za

ngono hupata matatizo. Lazima ieleweke kuwa kinachoonekana na jicho au kusikika kwa sikio huathiri

fikira au hisia. Picha za matusi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu akili. Badala ya kuzingatia

mambo muhimu kama masomo watu huanza kutafakari mambo machafu.

Vijana wengi ni kama bendera. Hivyo basi huanza kuiga wanayoyaona na kusikia. Hili ni tatizo

linalowafanya kuacha mkondo wa maadili. Kutokana na uchafu huu, watu wengi hushawishiwa

kuingilia shughuli za ngono mapema kabla hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia. Matokeo yake ni

mengi. Haya ni pamoja na ukahaba, utendaji mbaya shuleni, mahudhurio mabaya darasani na mimba

zisizotarajiwa. Vijana wengi huacha shule kabisa. Wengine nao huambukizwa magonjwa ya zinaa

ambayo huwaletea mauti.

Inasemekana kuwa akili za binadamu hunata zaidi mambo yanayowasilishwa kwa picha. Si ajabu

vijana huyadumisha matusi haya katika kumbukumbu zao na kuyasanya sehemu ya maisha yao. Wengi

huanza kuandama tabia mbovu kama ushoga, ubasha na usagaji. Kuna wale ambao huanza kujichua.

Kujichua ni hali ya mwanamke au mwanaume kumaliza haja za kimaumbile bila kufanya mapenzi na

mtu mwingine. Ponografia imechangia pakubwa kuenea kwa haya.

Jambo hili limegeuza mielekeo ya vijana. Wanaiga mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao.

Hali kadhalika, huiga lugha, ishara na miondoko inayohusiana na ngono. Yote haya yanapingana na

desturi za Mwafrika. Si ajabu visa vya ubakaji vinaongezeka kila kukuchapo.

Utazamaji wa picha chafu aghalabu huandamana na maovu mengine kama unywaji wa pombe,

matumizi ya dawa za kulevya, uvutaji sigara na utumiaji wa dawa za kuchochea uchu wa ngono.

Mambo haya huwapa vijana kutazama tabia za unyama.

Jambo hatari ni kuwa kuendelea kutazama picha hizi huzifanya nishai na hisia za watu kuwa butu,

yaani huondoa makali. Hata katika utu uzima, mtu atapoteza mhemko wa kawaida na kugeuzwa kuwa

mtegemezi wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na vijijini. Ipo haja ya dharura

kuikinga jamii kutokana na maenezi haya yasio na kizuizi.

Page 6: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

Jambo la kwanza ni kuongeza ufahamu wa umma wote kuhusu uovu wa picha hizi. Kwa namna hii

itawezekana kupunguza mahitaji na uuzaji wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na

vijijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na maenezi haya yasio na kizuizi.

Tatizo la kuenea kwa ponografia limeendelea kuwepo kwa sababu ya udhaifu wa sheria. Kilichoko basi

ni kuweka sheria za kuzuia utengenezaji wa upujufu huu. Kuambatana na haya, hatua kali zichukuliwe

kwa wanaovunja sheria hizi. Hali kadhalika, ushirikiano wa karibu baina ya wadau uimarishwe katika

ulimwengu mzima. Serikali na wanaohusika wakabiliwe ipasavyo. Jamii ingependa kuona michakato

ya kuharamisha utengenezaji, usambazaji na utangazaji wa ponografia ikiwekwa.

Wazazi nao wasijipweteke tu bali nao wasaidie. Ni muhimu washikilie kwa shati juhudi zao za

kuwaelekeza na kuwashauri watoto kuzingatia uongofu na kukwepa picha hizi najisi. Watoto lazima

waeleweshwe kuwa haifai kutazama picha au michoro michafu. Itikadi na imani za kidini na utamaduni

wa Kiafrika unakataza vikali mtu kuona uchi wa mtu mwingine. Matokeo ya kuasi makatazo haya yana

madhara makubwa kwa watu na jamii.

Maswali

(a) Fupisha ujumbe wa aya ya pili na ya tatu kwa maneno 20 – 25. (alama 6, 1 ya mtiririko)

Matayarisho

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Nakala safi

(b) Kwa kutumia maneno 55 – 60, dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya ya nne hadi ya tisa.

(alama 9, 1 ya mtiririko)

Matayarisho

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Page 7: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

(a) (i) Eleza maana ya silabi funge. (alama 1)

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(ii) Andika na uonyeshe silabi funge kwenye neno. (alama 2)

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(b) Tumia neno Uganda na nomino zilizotajwa kwenye mabano katika sentensi kama;

(i) Kivumishi (nomino ya pekee). (alama 2)

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(ii) Kielezi (Nomino ya ngeli ya A – WA). (alama 2)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(c) Tunga sentensi ukitumia:

(i) Kielezi namna kiigizi (alama 1)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Page 8: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

(ii) Kivumishi cha pekee chenye maana ya “zaidi ya’’ pamoja na ngeli ya LI – YA. (alama 2)

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(d) Yakinisha katika nafsi ya pili umoja. (alama 2)

Tusipoelewana na walimu hatutapata amani siku zote shuleni.

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(e) Bainisha mofimu katika neno: (alama 3)

Tukutiliaye

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------ ----

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(f) Geuza katika hali ya udogo wingi. (alama 3)

Jumba liliingiwa na jigombe ambalo lilikatwa kia.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(g) Ashiria vishazi katika sentensi: (alama 2)

Alikuja shuleni ingawa ni mgonjwa

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(h) Tunga sentensi ukitumia kihusishi “katika” kutoa dhana ya hali. (alama 1)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(i) Eleza tofauti ya kimaana katika sentensi hizi. (alama 2)

(i) Nilapo hushiba

Page 9: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

(ii) Ninapokula hushiba

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(j) Tunga sentensi inayoonyesha –ki- ya masharti kujumuisha. (alama 1)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(k) Tunga sentensi yenye yambwa tendwa na yambwa tendewa. (alama 2)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(l) Matumizi mawili tofauti ya nukta pacha. (alama 2)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(m) Eleza maana ya sentensi hizi kwa kuzingatia sehemu zilizopigiwa mstari. (alama 2)

(i) Maziwa yamegandama

(ii) Mama amepakata mtoto

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(n) Bainisha jinsi maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo yalivyotumika. (alama 2)

(i) Ni muhimu kudumisha lugha asili.

(ii) Mpaka sasa asili yake haijulikani.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Page 10: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(o) Tofautisha maneno yafuatayo kwa kuyatungia sentensi. (alama 2)

(i) Okoa (ii) Ongoa

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(p) Tunga sentensi kwa kutumia neno walakini kuleta maana ya: (alama 2)

(i) Kiunganishi

(ii) Kasoro

(q) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia mchoro wa matawi. (alama 4)

Ingawa Musa alikuwa amepona, aliaga dunia leo.

4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)

(a) Tofautisha kati ya kuhamisha msimbo na kuchanganya msimbo. (alama 2)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(b) Taja mambo mawili yanayoonyesha udhaifu katika mazungumzo na huchangia katika uhamishaji wa msimbo. (alama 2)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Page 11: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(c) Taja kaida mbili zinazotawala matumizi ya maamkizi katika jamii huku ukitoa mifano mwafaka.

(alama 2)

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

(d) Fananisha sifa zozote nne za sajili za maabadini na mahakamani. (alama 4)

Page 12: MTIHANI WA PAMOJA SUB-KAUNTI YA KAKAMEGA KUSINI · E-resources available online at / Email: infosnkenya@gmail.com / Tel.: +254202319748 kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza

E-resources available online at www.schoolsnetkenya.com / Email: [email protected] / Tel.: +254202319748

ANSWERS:

Order a copy of answers from www.schoolsnetkenya.com/order-e-copy

NB> We charge Kshs. 100 ONLY to meet website, e-resource compilation and provision costs