1 jina la yesu jina la yesu gordon h. richards kiswahili

25
Jina La Yesu 1 JINA LA YESU 1

Upload: buihanh

Post on 07-Feb-2017

338 views

Category:

Documents


21 download

TRANSCRIPT

Page 1: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

1

JINALA YESU

Gordon H. Richards

1

Page 2: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

KISWAHILI TRANSLATION

Copyright © 2011

Yesu anasema katika Mathayo 10:8, “Kwa kuwa mmepokea bure, toeni bure”. Pamoja na kuwa kitabu hiki kina hati miliki, unaruhusiwa kuna kiri bure ili uweze kusambaza nakala.

Kama kitabu hiki kitata fsiriwa katika lugha nyingine mwandishi wa kitabu hiki angependa nakala iliyotafsiriwa itumwe kwake kwa kutumia anwani ifuatayo:

Love Without Borders317 Sidney Baker So., # 127

Kerrville, TX 78028United States of America

E-mail: [email protected]: www.jesus4you.com

NGUVU (UWEZO)KATIKA JINA LA YESU

Waumini wengi wanaonyesha maisha mazuri ya kikristu katika sehemu nyingi za matembezi yao na Bwana. Tatizo moja walilonalo ni katika kuelewa na kutumia uwezo wa jina la Yesu.

SIRI ILIYOKO KATIKAJINA LA YESU

Wakristo duniani kote wanakumbwa na mazingira magumu (hali ngumu). Matatizo ya kiafya, kifedha au hali za kisiasa zinabadilika mara kwa mara na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa binadamu na Wakristo wengi hawajui la kufanya. Wazo la kukosa matumaini linajaribu kuwafanya watu waache kuitegemea imani tuliyopewa na Mungu. Tunapaswa kukumbuka kwamba tuko katika vita ya kiroho. Shetani anataka waumini wengi iwezekanavyo

2

Page 3: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

kushindwa kimaisha, na hataki nguvu ya Mungu ionekane ndani yetu. Shetani hataki walimwengu waone tofauti yoyote kati yao na Wakristo. Wazo la shetani ni kuwafanya watu wengi iwezekanavyo kutomtumikia Bwana.

Roho isiyo na matumaini inatoka kwa shetani, lakini KWA JINA LA YESU tuna uwezo wa kuikwepa roho hii. Vita kubwa inapewa uzito katika dunia ya leo, ambayo si ya kisiasa, bali ya kiroho. Makundi mengi yanajaribu kutothamini umungu wa Bwana Yesu, na wengine wanafikiri kwamba Yesu ni binadamu wa kawaida tu. Aya zifuatazo zitatuonyesha kwamba Yesu ni muumba, na siyo muumbwa:

Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2. Huyo MWANZO ALIKUWAKO KWA MUNGU. 3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 9. Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. 12. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 14. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Ufunuo 19:13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU. 16. Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Yohana Mbatizaji alimfahamu Yesu vyema. Roho Mtakatifu ali-mwambia Yohana kwamba Yesu angekuja, naye Yohana alikuwa na haya ya kusema kuhusu Yesu:

Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu akija kwake, akasema, tazama mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 34. Nami nimeona na nimeshuhudia kuwa HUYU NI MWANA WA MUNGU.

Yesu alimwambia Mwanamke msamaria kwamba alikuwa Mwana wa Mungu. Hakumlaumu Petro kwa kusema kitu kile kile. Angalia Mathayo 16:13-17. Vile vile aliwaambia viongozi wa dini ya Waisraeli kwamba yeye ni masiha.

Yohana 4:25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote. 26. Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.

Marko 14:61 Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu? 62. Yesu akasema, Mimi ndiye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni.

3

Page 4: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Mnyang’anyi pale msalabani pia alimtambua Yesu kama mwana wa Mungu.

Mathayo 27:54 Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

Roho zenye pepo zilikuwa na haya ya kusema, kwa sababu walimfahamu vyema Yesu, uwezo wake na nguvu alizokuwa nazo.

Luka 4:41 Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo.

Watu wanaofikiri kwamba Yesu alikuwa mwanadamu wa kawaida tu, mwalimu mzuri tu, au kitu kilichoumbwa, WANAMTUKANA muumba wa dunia. Kushindana na Muumba kunamweka mtu katika mazingira magumu. Wanashindwa kutambua kuwa ni kwa huruma yake tu hawahukumiwi Naye kwa sasa, kwa sababu wamekwisha laumiwa.

Yohana 3:15 Ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. 16. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 18. Amwaminiye yeye hahukumiwi; ASIYEAMINI AMEKWISHA KUHUKUMIWA; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 36. Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

VISHAWISHI VYASHETANI VINALIOGOPA

JINA LA YESUKila roho ya kishetani INALIOGOPA jina la Yesu. Sehemu nyingi katika Biblia tunaona kwamba roho za mapepo zinaonyesha uwoga wao kwenye uwepo wa Yesu. Ziliogopa sana uwezo na nguvu zilizofichika ndani ya maneno aliyoongea Yesu.

Mathayo 8:28 Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. 29. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? 30. Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. 31.Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile

4

Page 5: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

kundi la nguruwe. 32. Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.

Vishawishi vya shetani bado vinaogopa sana JINA LA YESU. Havina uwezo wa kushindana na nguvu lilizonazo jina la Yesu. Tunaweza tukaipinga hali yoyote ya kimapepo na kusababisha irudi nyuma tunapokuja na uwezo wa jina la Yesu. Ulinzi wa nguvu wa jina la Yesu pia utatulinda wakati mtu mwingine akituombea. Roho za kimapepo zinatambua uwezo huu na hazitaki kujaribu nguvu zao kupinga uwezo wa jina la Yesu. Sheria hii haiwezekani endapo mtu hajajikabidhi kwenye uwezo na amri za Bwana. Vishawishi vya shetani sasa vinaweza kuuteka ulinzi tulionao, kwa sababu tumeondoa sehemu ya uwezo wetu wa kiroho. Hivyo tunahitaji kutubu na kurudi chini ya ulinzi. Angalia Yakobo 4:7 na Waefeso 6:10-18

Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu, Mpingeni shetani, naye atawakimbia.

Ni kwa nini waumini wengi wanakuwa goigoi katika mwenendo wao wa Kikristo? Hawaonekani kuwa na nguvu za kushinda shambulizi za vishawishi vya shetani. Waumini hawa wanashindwa kuona uhusiano kati ya matatizo na matendo yao kuhusu kujitoa kikamilifu kwa Mungu. Hatutaweza kamwe kuwa na uwezo wa kushinda vishawishi vya shetani endapo hatuko tayari kufuata maelekezo ya Bwana. Hataruhusu uwezo wake kutujilia sisi ili kulishinda tatizo, wakati hatuishi kwa kujitoa kikamilifu kwake.

Katika 1 Petro 3:7-12 tutaona kwamba wakati hatupo katika umoja na Bwana wetu, sala zetu zitazuiliwa. Vile vile tunajiweka wenyewe katika nafasi ya kushindwa kuhimili mashambulizi ya vishawishi vya shetani.

1 Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, KUSUDI KUOMBA KWENU KUSIZUILIWE.

Kujaribu kutenda kiimani bila kuishi kiimani ni sawa na bure. Ni muhimu kwetu kuanzia pale tulipo; hatuwezi kurukia mara moja kwenye hali ya juu ya imani, ikiwa tumekuwa tukiishi katika mashaka kwa muda mrefu. Tunapaswa kuanza na kukua kutoka pale tulipoanzia. Marko ana haya ya kusema:

Marko 4:28 Maana nchi huzaa yenyewe; KWANZA jani, TENA suke, KISHA ngano pevu katika suke.

Imani itakuwa na maendeleo. Tusome neno kwa undani (kwa kina), kwa sababu hii ni njia ambayo Mungu ameichagua kwa ajili yetu ili kujenga imani yetu. Warumi 10:17 inatuambia: “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Kujaribu kutenda kiimani bila kuishi maisha yafananayo na utakatifu pia ni sawa na bure. Mtume Yohana

5

Page 6: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

anatuonyesha kuwa matumaini ya kupokea kutoka kwa Mungu yanategemea jinsi tunavyomtumikia Bwana.

1 Yohana 3:21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; 22. na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

Waumini wengi wanafungamanishwa na roho ya ukosefu na hawapati mahitaji yao. Wengine wanafikiri kwamba hawawezi kujibidisha lakini wanashindwa kuelewa kwamba juhudi si hiyari, bali imeamriwa. Machoni pa Bwana juhudi haisaidii. Angalia Mathayo 6:1-4. Wakristo wasiojibidisha wanafungua mlango kwenye mashambulizi ya adui, ambayo vile vile yataruhusu vishawishi vya shetani kushinda katika maeneo mengine ya maisha yao.

Asili ya ulinzi hairuhusu roho ya mtu kujitoa kikamilifu kwa Bwana. Hii itavifanya vishawishi vya shetani kuachana nasi tunapojaribu kupingana navyo. Mara nyingi asili ya ulinzi itataka kuongozwa na roho ya mtu. Haitaki Bwana awe na mamlaka kamili. Mchungaji wa kanisa ni mfano. Asili ya ulinzi wa mtu itasema kwamba hahitaji kujikabidhi kwa mchungaji, au kufuata maongozi ya kiongozi wa wimbo, na mitazamo hii itakomesha ghafla nguvu ya Mungu kufanya kazi.

MATUMIZI YA JINA LA YESUYohana 14:12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Yesu ametupa uwezo (mamlaka) au “nguvu ya uwakili” kutumia jina Lake wakati wowote linapohitajika. Kila mara tunapokutana na hali iliyo juu ya uwezo wetu tuna nafasi nzuri ya kutumia uwezo (nguvu) ulio katika jina Lake. Yohana 14:13 inatuaonyesha kwamba Baba anapata utukufu kwa sababu nguvu (uwezo) yake inatumika.

Wakristo wachache wanaelewa ni kwa nini sehemu inayofuata ya Yohana 14:13 ipo katika Biblia. Shetani anataka muda wote kuleta matatizo kwa watu wanaomtumikia Mungu. Anataka kuonyesha uwezo wake na, kuuonyesha ulimwengu kuwa Mungu hana uwezo (mamlaka). Mungu anataka mkristu kupinga vishawishi vya shetani kwa kutumia jina la Yesu. Hii inampa Mungu Baba utukufu haraka., kwa sababu inauonyesha ulimwengu kuwa Mungu ana nguvu na mamlaka zaidi kuliko shetani. Wakristo wengi wanaupokonya utukufu wa Mungu kwa sababu wanategemea uwezo wao na njia zao, badala ya nguvu (uwezo) ya Mungu. Wakristo wengine wanadhani kwamba wakati huu si wa miujiza. Wanafikiri kwamba miujiza ilihitajika ili

6

Page 7: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

kuanzisha kanisa, lakini baada ya siku za manabii, miujiza ilikwisha. Wazo hili limetoka kwa shetani mwenyewe, kwa sababu anachukia pale Mungu anapopata sifa ya aina yoyote ile.

Hatujapewa mamlaka ya kutumia jina la Yesu kama mazi-ngaombwe (uchawi). Tulipewa haya mamlaka ili kutumia tulipokutana na hali ambayo tusingeimudu. Mtu anapokuwa na pancha kwenye tairi la gari lake, ataweka tairi la akiba. Mungu hategemei mtu huyo vutandaza mikono yake juu ya tairi na kusema “kwa jina la Yesu, jazwa na upepo.” Mungu anategemea mtu huyo kufanya kile anachoweza. Tunaposhindwa ndipo tunaweza kumtegemea Mungu kutuongezea nguvu au uwezo unaohitajika.

Bibi yangu alitumia zaidi ya miaka sitini kama mmisionari katika Afrika. Wakati huo Mungu alinya kazi kwa njia yake kwa namna ya ajabu. Kabla, bibi na babu yangu walikwenda Afrika. Mwaka 1912 paa (dari) la nyumba yao lilishika moto. Wazo lake la haraka lilikuwa “Ni andiko gani la kutatulia tatizo hili.” Roho mtakatifu mara moja akamkumbusha aya zifuatazo.

Waebrania 11:33 Ambao KWA IMANI walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba. 34. WALIZIMA NGUVU ZA MOTO, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.

Baada ya hapo aliuelekea (aliugeukia) moto na kusema: “Kwa jina la Yesu isiwe hivi.” Mara moto ukazima, na paa halikuharibiwa hata kidogo. Ni nguzo tu chini ya paa zilizoungua. Miaka ya 1950 wazazi wangu waliporudi nchini, baba yangu alikwenda kuingalia nyumba. Ilikuwa imehamishiwa umbali wa maili sita toka pale ilipokuwepo mwanzo. Mmiliki mpya aliwapa ruhusa kwenda kwenye nafasi ndani ya paa na kuangalia nguzo, na walikuta bado ziko katika hali ya kuungua. Huu ulikuwa ni uthibitisho wa kimya wa imani ya bibi yangu.

KUZIKUBALI HAKI ZETUHatutumii imani ya Kimungu kuandika “cheki” (hati ya kuchukulia pesa benki) ya kiasi cha shilingi elfu ishirini na mbili kama tuna shilingi elfu arobaini na nne benki. Tungekuwa tunatumia uwezo wetu kuandika cheki. Sisi kama waumini, tunapaswa kutambua kuwa Yesu amekwishatupa uwezo wa kutumia jina Lake.

Warumi 8:16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17. na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

7

Page 8: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Waebrania 1:1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2. mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

Je, wewe ni mwana wa Mungu? U mwana wa Mungu endapo umempokea Yesu kama mwokozi wako na unaishi kwa ajili yake. Kama mwana wa Mungu, u kiungo kirithi na Kristo kwa sababu ya nafasi yako katika familia ya Mungu. Waumini wengi wako tayari kupokea hili KWA MASHARTI. Masharti waliyonayo akilini ni kwamba utimilifu hautakuwepo mpaka tutakapofika mbinguni au kuanza utawala wa kimi-lenia pamoja na Yesu. Itakuwa ni wakati ambapo tutaongoza na kutawala pamoja naye kwa miaka elfu moja. Aina hii ya muumini inashindwa kuelewa kwamba Bwana ana uwezo wa kuvishinda vishawishi vya shetani, na vile vile kuomba vitu vingi kwa njia ya uwezo wa ajabu wa jina la Yesu.

Wakristo wengi wanajaribu kuamini kwamba Yesu alimaanisha kile alicho-ongea. Mara chache panapokuwa na tukio kubwa la ghafla watarukia katika sehemu ya imani. Ndipo watakapoona nguvu ya Mungu ikionekana kwa njia ya maneno waliyotumia. Mpango wa Mungu kwetu sisi ni kuishi kiimani siku zote. Waumini wengi wanasikiliza tu mahubiri lakini hawatendi mambo yanayofundishwa na Biblia. Yesu aliwaita watu hawa “Wasikilizaji wa Neno, na sio watendaji,” Yakobo 1:22-25. Wasikilizaji wa Neno wanaona kina-chotokea, wakati mtendaji wa Neno anafungua mlango ili nguvu ya Mungu ifanye kazi kwa njia yake, Mathayo 7:24-27.

Yakobo 1:22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikilizaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.

Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27. mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

TUMIA AHADI ZA MUNGU

8

Page 9: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Zaburi 138:2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nita-lishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako LOTE.

Mungu amelikuza Neno lake kuliko jina lake, ametupa haki (uhuru) ya kunukuu na kutumia JINA LAKE. Yesu anatarajia sisi KUTUMIA JINA LAKE kwa sababu atayaimarisha maneno yetu kwa Neno Lake. Tunaweza tukasimama imara kwa Neno Lake yanapotokea mahitaji, tunajiwekea wenyewe mipaka, badala ya kutafuta Neno la Mungu na kuliruhusu lifanye kazi kwa ndani yetu.

Wakristo wengi wanaruhusu wazo la unyonge liingie katika maisha yao, wanatathimini ni jinsi gani walivyo katika Kristo, na jinsi ambavyo wange-paswa kuwa. Hili litakuwa na matokeo yasiyofaa kwa wale wanaotuzunguka. Tunapaswa kutambua kwamba Roho ya Bwana ndiyo yenye uwezo wa kufanya vitu vyote kwa njia yetu (ndani yetu), tunapokubali mafundisho ya ya ahadi za Mungu na kuyatumia.

Waefeso 3:20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.

1 Yohana 4:4 Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu; nanyi mmewa-shinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.

Majibu ya sala kwa njia ya imani ya Kimungu hayatakuja kwa sababu ya uwezo wetu, bali kwa sababu ya uwepo wa Mungu. Pia tunapaswa kuwepo ili kuruhusu nguvu yake ifanye kazi kwa njia yetu. Hili linatokea pale tunapotumia imani ya kimungu na kuongea maneno yafananayo na mafundisho ya ahadi za Mungu. Kwanza imani, halafu Mungu anafuata KATIKA JIBU LA MATUMIZI YA IMANI YETU. Mungu hawezi kufanya miujiza yoyote ile anapokumbana na imani haba.

Kuna masharti mawili yanayosababisha ahadi za Mungu kutimizwa katika maisha yetu. Sharti la kwanza daima litakuwa ni usafi wa moyo. Sharti la pili ni Imani ya kimungu (imani takatifu). Wakristo wengi wanakosa nafasi nzuri ajabu kwa sababu wanahitaji wanataka kutumia muda katika kusali KWA AJILI YA MAELEKEZO kabla ya kutenda. Nafasi nzuri inawapita wanapokuwa katika sala. Tunahitaji kufanya sala zetu mapema ili kwamba pindi nafasi nzuri zinapotufikia, tunaweza kulindwa na Roho Mtakatifu ili kuongea maneno yatakayofanya nguvu ya Mungu ifanikiwe.

Zaburi 138:8 Bwana ATANITIMILIZIA MAMBO YANGU; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.

9

Page 10: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Kuna ahadi nyingine nyingi zilizopo kwa ajili yetu. Je unaziamini? Wakristo wengi wanatenda kama vile hawatendi. Mungu anatutaka sisi:

1. Kuamini Neno Lake

2. Kuwa watendaji wa Neno

3. kutenda kufuatana na ahadi zilizo katika Neno.

2

UWEZO (MAMLAKA)

10

Page 11: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

WA JINA LA YESULeo hii Wakristo wengi wamepoteza mwelekeo wa uwezo wa jina la Yesu. Wanafahamu kwamba Yesu ni kiongozi wa kanisa; hata hivyo wanaishi maisha yasiyo na nguvu. Wanatenda kama vile Yesu ana mipaka sana na wao, na watapata nguvu yake baada ya shetani kutupwa ndani ya shimo refu lisilo na mwisho.

WAZO LA KUKOSA MATUMAINIWaumini wengi wanakumbana na hali ngumu. Hili linawezekana kwa sababu ya matatizo ya kiafya au hali ya kifedha, zinazoweza kumfanya mtu akose matumaini. Shetani anataka kuharibu imani yetu kwa Mungu na kutufanya tukate tamaa kabisa, ili tupoteze kabisa matumaini.

Kutokuwa na matumaini ni roho ya kishetani ambayo itajaribu kutukanda-miza ili tushindwe kuwajibika kwa ajili ya Bwana. Ayubu anatupa picha hii katika Ayubu 7:1-6.

Ayubu 7:4 Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. 5. Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kasha ikatumbuka tena. 6. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.

Kumbukumbu la Torati 28:67 asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.

Ukosefu wa matumaini unasababisha mkandamizo na uzito na uwezo ukaishia katika kukata tamaa. Ukosefu wa matumaini utaharibu mtazamo wa watu, na kusababisha vitu vitakavyosemwa kwamba vitaisimamisha imani kufanya kazi. Watu hawatambui kuwa Mungu yuko tayari kumsaidia kila mmoja wetu wakati wowote anapohitaji. Watu wengi wanaruhu adui awajaribu mara kwa mara kuacha kuzitegemea ahadi za Biblia au kuacha kumtu-mikia Bwana. Himili vishawishi hivi vya adui katika jina la ajabu la Yesu, na vitakimbia.Zaburi 37:39 Na wokovu wa wenye haki una BWANA; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu. 40. Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; Huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa; Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.

SILAHA YENYE NGUVU ZAIDI

11

Page 12: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Jina la Yesu ni silaha yenye nguvu zaidi aliyonayo Mkristo. Moja kati ya majini ya Yesu ni Neno la Mungu. Hii ina maana kwamba, ahadi zote za Biblia zimeunganishwa na kusimamiwa na jina la Yesu.

Ufunuo 19:13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2. Huyo MWANZO ALIKUWAKO KWA MUNGU. 3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 14. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Kanisa la mwanzo lilitegemea kabisa nguvu ya jina la Yesu. Kila kitu kanisa lilichokuwanacho na kusimamia kiliwezekana kwa sababu ya jina la Yesu. Kanisa la leo linapaswa kuamka kwa ukweli kwamba tunapigana vita vya kiroho, na ni lazima litegemee jina la Yesu kikamilifu.

WOKOVUWokovu unawezekana kwa sababu ya jina la Yesu. Watu wanaotegemea kazi zao nzuri, watakuta kwamba hawana kitu chochote cha kuwaokoa.

Yohana 14:6 Yesu akamwambia, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

Matendo ya Mitume 16:30 Kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? 31. Waka-mwambia, “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.”

Waefeso 2:8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9. wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

TIBA YA KIMUNGU Tiba ya kimungu inawezekana kwa njia ya nguvu ya jina la Yesu. Isaya aliona mbele kwenye tukio hili, na Petro aliona nyuma yake.

Isaya 53:4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. 5.

12

Page 13: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

1 Petro 2:24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

AMANI YETUMalipo ya amani yetu yalilindwa na Yesu pale msalabani. Wakristo wengi wanashindwa kutumia mwanya uliopo wa amani, na huwa wanachanga-nyikiwa mara kwa mara. Wanahisi kukandamizwa na kujawa na woga. Wanashindwa kutambua kwamba jina la Yesu litawafanya huru kutoka katika utumwa huu ikiwa watalitegemea Neno lake.

Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi, sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

Kanisa la mwanzo lilitegemea kikamilifu jina la Yesu kwa sababu lilikuwa ni kigezo cha kumwangusha na kumshinda shetani. Walijua kwamba shetani alikuwa na sheria pembe zote za dunia zilokuwa zikiziongoza serikali, mabenki, biashara na watu. Wakristo wa mwanzo walizipinga katika jina la Yesu na kusababisha zianze kudidimia. Wakati wowote shetani anaanza kutunga sheria kinyume na maisha yetu ya leo, nasi tuna uwezo wa kuziangusha kwa kutumia nguvu ya ajabu ya jina la Yesu.

Jina la Yesu lina nguvu mno kiasi kwamba hakuna kitu kiwezacho kushi-ndana nalo. Vishawishi vya shetani vinatetemeka mbele ya jina la Yesu. Shetani aligundua ni nini kinachomfanya ashindwe. Baadaye alianzisha mpango kabambe wa kulipinga kanisa, kusababisha lipoteze mwelekeo na maono ya nguvu za jina la Yesu. Alitaka kanisa lihisi kwamba jina la Yesu halikuwa na nguvu zaidi ya jina lingine lolote. Katika sehemu nyingi za dunia watu wanawapa watoto wao jina la “Yesu.” Mwishowe jina la Yesu likaonekana kuwa la kawaida na kupoteza umaana wake. Kitu kingine alichokifanya shetani ni kulishushia hadhi jina la Yesu kwa kulifanya kuwa msemo wa kawaida tu, au kwa watu wengine, neno la kulaani. Watu hawa wanashindwa kutambua kuwa kila wafanyapo hivi wanavunja amri moja kati ya zile kumi.

Kutoka 20:7 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, Maana Bwana, hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. - The Amplified Bible.

Watu wengine wanahisi kuwa kutumia moja ya herufi ya majina ya Mungu inakubalika. “Gee” linapotumika kama “Gee Whiz,” ni badala ya jina Yesu. “By Jove” ni kifupi cha “by Jehovah.” Mifano mingine mingi inaweza

13

Page 14: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

kutolewa. Watu wanashindwa kutambua kuwa sisi sote tutatoa maelezo kwa kila neon la uzembe tunalosema.

Mathayo 12:36 Basi, nawaambia, kila neno lisilo maana watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. 37. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

UWEZO TULIONAOKUTUMIA JINA LAKE

Yesu ametupatia jina la kutumia kwamba ambalo li juu ya kila jina na kila mamlaka yote ulimwenguni. Kila kitu kinapaswa kuli-inamia au kujikabidhi kwa jina la Yesu.

Wafilipi 2:9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10. Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11. na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Hatutakiwi kuongozwa na mawazo ya kidunia, kama vile mawazo ya hasira, kukata tamaa, kuanguka, na mawazo kwamba hatutafanikiwa. Hili linawezekana endapo akili yetu inaegemea kwenye mawazo yatokayo kwa Roho Mtakatifu. Kila mara wazo mojawapo ya haya linapotujia, tulitawale kwa jina la Yesu. Kila kimoja cha vitu hivi kinatakiwa kulipigia magoti jina la Yesu.

Shetani ni jina. Jina la Yesu liko juu sana ya jina hilo. Roho za uhalifu, ugonjwa, madawa ya kulevya, isiyo na kitu, umasikini n.k, zinajaribu kuja ndani na kutawala mazingira yatuzungukayo. Tuna uwezo wa kuhimili na kuziacha roho zote hizi au majina KWA JINA LA YESU.

Kansa ni jina, umasikini ni jina, kuanguka ni jina, ugonjwa wa moyo ni jina n.k, yote ni majina. Tunapaswa kutambuwa kwamba kila kimoja cha vitu hivi kinatakiwa kupiga magoti na kuwa mfuasi wa jina la Yesu. Kila mara wanajaribu kutupinga. Malaika wanatenda kwa jina la Yesu. Tunaponukuu Maandiko yanayoshinda tatizo tulilonalo, tunaweza kupoteza nguvu za kimalaika za kulishu-ghulikia tatizo, kwa sababu ya jina la Yesu. Hivyo wanatakiwa kutii maneno ya Mungu tunayoyanukuu. Haya yataleta majibu kwa matatizo yetu.

MPAKA WA MAMLAKA (UWEZO)

14

Page 15: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Yohana 15:4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

Wakati sisi si tena sehemu ya Mungu, hatuwi tena na mamlaka. Tuna-ondolewa kwenye ulinzi wa Bwana, na tunaweza kuharibiwa kiroho. Aya ya sita inaeleza kwamba tumechomwa na kuunguzwa.

Wakristo wengi wanaishi maisha duni kwa sababu hawamruhusu Roho Mtakatifu awalinde. Nguvu ya jina la Yesu haitafanya kazi kwa mtu wa namna hii.

ADHABU KWA KUTUMIAVIBAYA MAMLAKA (UWEZO)

Ushindi juu ya vishawishi vya shetani unawezekana endapo tunamtumikia Mungu. Watu wanaomtumikia Mungu katika sehemu tu ya muda, watakuta kwamba hawamtumikii shetani. Wahubiri saba watoto walidhani kwamba eti kwa sababu baba yao alikuwa mhubiri wangeweza kuwa na mamlaka juu ya roho chafu. Waliiambia roho chafu kutoka nje kwa jina la Yesu kama Paulo alivyohubiri. Roho chafu ilisema kuwa ilikuwa inajua Yesu ni nani, na vile vile Paulo ni nani. Sasa ilitaka kujua hao watoto ni akina nani. Walikimbia baada ya kucharazwa na mijeledi iliyosikika kwa sauti ya juu.

Matendo ya Mitume 19:13 Baadhi ya wayahudi wenye ku-tanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. 14. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. 15. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? 16. Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa. 17. Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.

YESU NI MFANO WETU

15

Page 16: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Yohana 14:12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Sasa inakuwa muhimu kwetu kusoma Injili mara kadhaa ili kujua aliyo-yafanya Yesu. Katika aya za hapo juu anatuambia kwamba si tu tunaweza kuiga yale aliyoyafanya, bali vile vile tunaweza kufanya MAMBO MAKUBWA.Hili halitakuwa kweli kwa Wakristo wote kwa sababu wengine hawaamini kwamba itawatokea. Wamezijaza roho zao na wazo kwamba Mungu hatendi miujiza sasa kama alivyokuwa akifanya enzi za manabii.

Sehemu ya mwisho ya sura ya 13 inatuambia nini? Tunaona kwamba Baba anataka kutukuzwa. Kadiri tunavyoyapinga mashambulizi ya adui na tunapokuwa washindi kwa sababu ya jina la Yesu, kwa kadiri hiyo hiyo Mungu anapata utukufu. Watu wanaobaki na mtazamo wa kutoamini wanamdanganya Mungu kutokana na utukufu ambao angependa kuupata. Huu ni mpango wa shetani, ambaye anataka kuonekana kuwa mwenye nguvu kuliko Mungu. Anataka kuwa na ushindi na kutufanya tushindwe kimaisha.

Wakati wa maisha ya Yesu tunaona kwamba alikuwa na nguvu juu ya ugonjwa, mapepo, kifo na maisha. Yesu hakuhitaji kujadiliana na matatizo au mapepo, bali alivitawala. Roho ya ugonjwa ilibidi itoke kwa sababu ya nguvu ya jina la Yesu. Uwezo kama huu tumepewa sisi! Tuna haki zote kuutumia na tunapaswa kuanza kuutumia kwa namna ya ajabu ili kuleta utukufu zaidi kwa Baba.

Matendo ya Mitume 3:6 Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende. 7. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. 8. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akimsifu Mungu.Mara mtu alipoliacha kanisa lake na kuongea yale aliyosema Petro katika aya za hapo juu, sasa alieleza kuwa walikuwa wamegeuza maelezo. Walifurahishwa sana kwa kuwa sasa walikuwa na shaba na dhahabu nyingi, lakini walishindwa kutambua kwamba walifanya biashara ya shaba na dhahabu kwa nguvu ya Mungu. Petro alijua kwamba jina la Yesu lilikuwa muhimu zaidi kuliko shaba au dhahabu, kwa sababu lingetoa uponyaji na vile vile shaba na dhahabu. Lile kanisa sasa lilikuwa na shaba na dhahabu lakini halikuwa na uwezo wa kusaidia watu kupata nguvu ya Mungu.

Maisha yetu si tu yafanane na yale ya Kristo, bali pia yanapaswa kuonyesha nguvu ya Mungu kama ilivyoonekana katika maisha ya Kristo. Tunapaswa kutambua kwamba jina la Yesu lina nguvu, na hakuna kitu kinachoweza

16

Page 17: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

kushindana nalo. Tuutumie uwezo tuliopewa na Yesu na kushinda matatizo yatokanayo na maisha au ugonjwa n.k.

Kwenye tukio moja nilikuwa nikiendesha gari kupandisha mlima wakati wa upepo mkali sana. Nilipofika kwenye mteremko mmoja, upepo ulinipuliza kwa nguvu ya ajabu na kutingisha gari. Niliushikilia usukani kwa makini ili kuuongoza na wakati huo huo nilisema: “Kwa jina la Yesu, tulia.” Mara upepo ukatulia. Mara nne zaidi wakati wa maisha yangu niliongea na upepo kwa jina la Yesu, na ulikuwa ukinitii. Mimi si mtu wa pekee, bali ni kwa sababu Mungu anataka kufanya kazi kwa njia ya kila muumini kwa namna ile ile. Sharti ni kwamba tuamini Neno lake. Tuanze kutenda kwa kutumia uwezo aliotupatia, na kuvishinda vishawishi hivi kwa jina Yesu.

Mara mvua ilipoanza kunyesha tulipokuwa tukihudhuria mkutano sehemu ya wazi pamoja na karibu watu elfu thelathini na tano kule Afrika Kusini, wengi wetu walianza kusali ili mvua itulie. Niliyaambia mawingu: “Kwa jina la Yesu, acha kunyesha.” Matone yaliyoachana na mawingu yalianguka ardhini, lakini mvua ikaacha kunyesha. Karibu nusu saa baada ya mawingu ya kwanza kutokomea mbali na wingu jingine jipya lenye maji mengi kutengenezwa juu yetu, ilipoanza kunyesha, mtangazaji alieleza kuwa tungeendelea kusali hata kama ingenyesha. Watu kadhaa walishindwa kuvumilia na kuondoka, lakini wengi wao waliamua kulivumilia tatizo. Niliruka na kulinyooshea mkono wangu lile wingu na kusema: “Labda mara ya mwisho hukunisikia, lakini nilisema, kwa jina la Yesu, acha kunyesha.” Mara mvua ikaacha na kusubiri mpaka mkutano ulipokwisha. Baada ya mkutano ikaanza kumwagika.

KINGA YA MATATIZOJina la Yesu lina nguvu zote. Hakuna kilicho na nguvu kuliko jina hili la ajabu. Hakuna kitu kisichozitii amri zitolewazo kwa jina la Yesu, pale maelezo yanaposimamiwa na uwezo utolewao na Yesu. Anatupa haki ya kulitumia jina lake. Vile vile ana haki ya kutuvua uwezo wa kutumia jina lake endapo hatuishi tena kwa ajili yake, au endapo tunalitumia vibaya jina hilo. Watu wengi wanaogopa kuacha kuwasaidia watu wasiokuwa na msaada kwenye barabara kuu. Sisi wote tunaoutegemea ulinzi wa Bwana nyumbani au kazini, vile vile tunaweza kuutegemea ulinzi wake kila mahali duniani. Nimeacha kuwasaidia watu barabarani Afrika, Mexico na Marekani, na nimekuwa na uwezo wa kutegemea ulinzi wa Bwana. Nimechukua idadi kubwa ya watu waliohitaji usafiri na wengi wao kwa wakati huo kama hawakuokoka, walimpokea na kumkubali Bwana walipokuwa nami. Nategemea ulinzi wa Bwana kila mahali.

17

Page 18: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Usiku mmoja wa manane nilikuwa nikiendesha gari huko Mexico na ndipo nilipomwona mtu amesimama katikati ya barabara akipunga mkono ili nisimame. Gari lake aina ya “pickup” lilikuwa limesimamishwa kando ya barabara. Nilidhani alikuwa akihitaji msaada, kwa hiyo nikasimama nyuma ya “Pickup.” Bwana akanifunulia kuwa huu ulikuwa ni mtego. Ghafla nikasema: “Kwa jina la Yesu hutanigusa.” Roho ya woga ikamjia, na akarukia kwenye gari lake na kufunga dirisha kwa sababu aliogopa kwamba huenda ningemfuata. Nilijivuta pembeni yake na kumuuliza alitaka nini. Niliuona woga machoni pake aliponiambia hakuhitaji chochote, kwa sababu alitaka niachane naye. Ni lazima aliwaona malaika wakinilinda kama ilivyoandikwa katika Zaburi 91:11

Katika tukio lingine, binti alikuwa akijaribu kulipita gari lingine na alikadiria vibaya umbali wake. Matokeo yake akawa anakuja kwetu uso kwa uso. Alichanganyikiwa kwa sababu hakujua la kufanya. Nikasema mara moja “Kwa jina la Yesu nipishe kwenye njia yangu” mara aligeuka na kutupisha. Niliwaambia marafiki zangu kwenye gari kwamba watu wengi wangedhani kwamba huu uli-kuwa ni muda wa kusali, lakini nilisali asubuhi hii, na kwamba huu ulikuwa ni muda wa kutenda. Sasa ilikuwa ni wakati wa kutenda na kumwambia mtu unataka afanye kitu gani. Wakristo wengi wanatenda kama vipima joto na kuruhusu matukio kutukia. Wengine wanatenda kama vifaa vinavyorekebisha joto kwa kukata na kuhifadhi mgao wa moto, na kudhibiti hali iliyopo.

MATAKWA YA MUNGUKutakuwa na nyakati ambapo tutakuwa na uwepo wa kutumia jina la Yesu kupinga vishawishi vilivyo kinyume nasi, lakini haitakuwa matakwa ya Mungu kwa tukio hilo.

Katika tukio moja nilihitaji kutumia simu kwenye mji mdogo katika Afrika, na simu mbili za kulipia zilikaribina. Moja ilikuwa na mlolongo mrefu wa watu wakisubiri kupiga simu. Nyingine haikuwa na mtu hata mmoja. Kwa hiyo nikauliza kama kulikuwa na tatizo lolote kwenye simu hiyo. Mtu mmoja akaniambia kuwa ilikuwa mbovu. Niliiendea na kutumbukiza pesa zangu na kusema: “Kwa jina la Yesu anza kufanya kazi.” Ghafla simu ikaanza kufanya kazi. Wakati mwingine nilikuwa katika mji ule ule nikiwa na tatizo lile lile. Nikaenda kwenye simu isiyofanya kazi, na nikaanza kusema kitu kile kile. Bwana akaniambia kwamba wakati huu haukuwa wa matakwa yake. Niliitundika simu na kuchukua pesa zangu. Niliweza kutumia simu nyingine katika shughuli moja. Kulikuwa na ajali mbaya sana kwenye barabara kuu nilipokuwa nikisubiria simu. Mmoja wa wanaume kwenye ajali alikatika miguu yote. Hatukuwa na usumbufu wowote kwa sababu nilicheleweshwa na simu

18

Page 19: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

ambayo isingefanya kazi. Mwishoni mwa wiki nilirudi Marekani, na mke wangu pamoja na mabinti zetu wawili walikuwa wakinisubiri kwenye uwanja wa ndege. Mabinti wote waliniuliza swali la aina moja. Je, nilikumbuka kitu kilichotokea siku ile? Bwana alikwishawaambia wote kuniombea kwa sababu ningekuwa katika hatari kubwa. Sasa nilielewa ni kwa nini Bwana hakutaka simu ifanye kazi siku ile. Ningeweza kusisitiza simu ifanye kazi endapo ningetaka, na Mungu angeiruhusu ifanye kazi, ili kulitukuza jina Lake, lakini hayakuwa matakwa yake.

SHUKRANIShukrani za pekee ziwaendee wanawake na wanaume wa imani walioni-tangulia. Tuna mifano mingi katika Biblia, na vile vile idadi kubwa ya watu waliokwishaishi, au ambao bado wanaishi katika karne hii. Sisi wote tunaweza kujifunza kutokana na mifano yao ya ajabu.

Kwa mke wangu mpendwa, Ethlyn, kwa uhamasisho na msaada wake katika kuandaa maandiko.

Kwa wanawake na wanaume wote wa ajabu walionisimamia na kunisaidia kifedha.

Kwa: Bwana Samuel Tayali, Bwana Robert Masunya, Bwana Deus Mkwanu kwa kutafsiiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili

Maandiko katika kijitabu hiki yamechukuliwa kutoka kwenye sura ya tisa na ya kumi za “Spiritual Warfare” (vita ya kiroho) na mwandishi yule yule.

Unless otherwise indicated,Scriptures taken from

Swahili Bible - Union Version

19

Page 20: 1 Jina La Yesu JINA LA YESU Gordon H. Richards KISWAHILI

Jina La Yesu

Copyright © 1994The Bible Societies of Tanzania and Kenya

Dodoma, Nairobi

Scripture quotation marked Amplified Bible.are taken fromThe Amplified Bible

Copyright © 1958, 1962, 1964Used by permission of Zondervan Bible Publishers

Ifuatayo ni orodha ya vitabu vilivyo andikwa kwa lugha ya Kiingereza na mwandishi yule yule:

Building Our Faith 14 chaptersLiving By Faith 14 chapters

Our Christian Privileges 14 chaptersFaith for Answered Prayer

The Holy Spirit 26 chaptersPrayer14 chaptersDaniel12 chapters

Daniel’s Vision Of Things To Come13 chaptersPhilippians 4 chapters

Divine HopeThe Name of Jesus

Can We Lose Our Salvation?Spiritual Warfare 10 chaptersGod Wants To Meet Our Needs

Overcoming DepressionA Successful Marriage

The Gifts Of The Holy SpiritVictory Through PrayerPower Of The Tongue

Promises For Victorious LivingEnd Time Victories

Daily Devotional: Increasing Your Divine Hope - January thru MarchDaily Devotional: Prayer - Talking With God - April thru June.

Daily Devotional: Restoration - God’s Plan For You - July thru SeptemberDaily Devotional: Holiness, a Lifestyle - October thru December

20